BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,119
Licha ya Rais William Ruto kueleza manufaa ya ziara zake Nje ya Nchi, mapokeo yamekuwa tofauti kwa Wananchi wakiwemo Watumiaji wa Mitandao ambao wanakidai Rais hakai Ofisini ili kutatua changamoto za Gharama za Maisha. Katika kipindi cha miaka miwili, Ruto amefanya ziara 42 katika 26, Nchi 15 ni za Afrika na 11 ni za nje ya Bara la Afrika.
Nchi zote kwa ujumla ni Ubelgiji, China, Visiwa vya Comoro, DR-Congo, Djibouti, Misri, Eritrea, Ujerumani, Israel, Msumbiji, Netherlands, Rwanda, Senegal, Afrika Kusini, Korea Kusini, Switzerland, Zambia, Burundi, Jamhuri ya Congo, Saudi Arabia, Uingereza, Ethiopia, Ufaransa, Uganda, Marekani na Tanzania.
ZIARA ALIZOFANYA RAIS WILLIAM RUTO KWA MIAKA MIWILI
ZIARA ZILIZOFANYWA NA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KWA MIAKA MITATU
Kwa upande wa Rais Samia aliyeingia Madarakani Machi 19, 2021 akichukua nafasi ya Urais kwa mujibu wa Katiba baada ya Rais John Magufuli kufariki, amefanya ziara 46 katika Nchi 28, Nchi 17 kati ya hizo ni kutoka Afrika na 11 ni za Nje ya Bara la Afrika.
Angola, Ubelgiji, China, DR. Congo, Ethiopia, Ufaransa, Ghana, India, Morocco, Namibia, Nigeria, Oman, Saudi Arabia, Switzerland, Umoja wa Falme za Kiarabu, Burundi, Misri, Malawi, Qatar, Rwanda, Senegal, Afrika Kusini, Uingereza, Zambia, Kenya, Msumbiji, Marekani na Uganda.