Safari za Rais Samia nje ya nchi

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,250
113,634
Mjinga mimi nina swali. Ni swali kumhusu Rais Samia [baadhi yenu ni mama yenu].

Sina takwimu wala taarifa zingine zozote za kuufuta huu ujinga wangu.

Na hata sijui niende wapi ili kuzipata takwimu na taarifa hizo.

Hivyo basi, JamiiForums ndiyo kimbilio langu nitakapo kupata baadhi ya taarifa.

Kwa namna fulani, JF imekuwa ni injini ya utafutaji wa baadhi ya taarifa.

Sasa ni hivi; huyu Rais wetu tokea achukue madaraka, ameshakaa nchini kwa hata mwezi mzima [mmoja] bila kusafiri kwenda nje ya nchi?

Nauliza hivyo kwa sababu naona kama vile kila baada ya wiki mbili hivi huwa ni lazima asafiri kwenda nje ya nchi, jambo ambalo sidhani kama lina tija sana kitaifa.

Wajuzi nijuzeni, tafadhalini sana.
 
Sidhani kama Rais anajipangia safari. Ana timu ya wataalamu wabobezi; mabingwa wa nyanja zote ambao hupanga safari zake. All options, possibilities, pros and cons; advantages and disadvantages zinakuwa zimezingatiwa by the time Rais anapokuwa anaelekea airport. Take that!
 
Kwanza naona umeonyesha wasiwasi wako wa kuona kama ziara za Mheshimiwa Rais pengine hazina tija nje ya nchi.ningependa kukuhakikishia na kukuambia kuwa safari za Mheshimiwa Rais zimekuwa na tija kubwa sana kiuchumi , kibiashara.kuongeza watalii, wawekezaji na kujenga mahusiano mazuri na nchi mbalimbali, hasa kwa kuzingatia sera yetu ya mambo ya nje ambayo inahusu mambo ya uchumi.

Mfano ziara ya Mheshimiwa Rais ya hivi majuzi kule nchini Indonesia imepelekea na kusaidia kupata fursa ya uwekezaji utakao leta kicheko na tabasamu kwa mamilioni ya wakulima.kwa kuwa kuna kiwanda cha mbolea kinakuja kujengwa hapa nchini. Jambo litakalofanya mbolea kupatikana hapa hapa nchini na kwa bei nafuu zaidi itakayochochea uzalishaji kwa mkulima na hivyo kuongeza kipato na kuondoa umaskini wa kaya.

Ziara ya Mheshimiwa Rais kule china ilifungua ukurasa mpya katika mambo mbalimbali ya kiuwekezaji na kidiplomasia ,ambapo ni katika ziara hiyo tuliweza kusamehewa deni la takribani billion 31 fedha ambazo zinaweza kujenga zaidi ya km 30 za barabara au vituo vya afya takribani 61 vya millioni mia tano tano au kutoa Ruzuku katika mbolea au kununua vifaa tiba mahospitalini n.k.

Ziara ya Mheshimiwa Rais kule Marekani ilifungua pia fursa mbalimbali ambapo pia alipata kuonana na makampuni mbalimbali ya utalii akafanya nayo mazungumzo ,jambo ambalo kwa sasa limepelekea kupata mafuriko ya watalii wanaomiminika na kupishana angani kuja Tanzania kama mwewe na sasa tunapokea watalii zaidi ya milioni moja na laki nane..lakini pia ni katika ziara hizo na kujenga mahusiano mazuri tumeweza kurudishwa katika mpango wa mapesa ya millenium challenge.

Amekwendaa pia huko india ambako tumepata soko kwa ajili ya mbaazi na korosho zetu ambapo hapo awali bei ya mazao hayo ilikuwa imeporomoka kama jiwe lililodondoka toka darini.lakini pia hospitali ya Apollo itajenga hapa hospitali nyingine ambapo badala ya wagonjwa kusafirishwa kwenda india watakuwa wanapatiwa matibabu hapa hapa na hivyo kuokoa matumizi ya dollar ambayo itatumika katika manunuzi ya bidhaa zingine muhimu nje ya nchi.

Amekwenda kule Ufaransa nako tumeweza kusainiana mikataba yenye manufaa makubwa sana kiuchumi na kibiashara.

Kwa ufupi ni kuwa Rais samia Amekuwa ni Rais mwenye shabaha ambaye anafanya ziara kwa shabaha maalumu ya kupata na kulenga kitu fulani chenye manufaa kwa Taifa letu Rais Samia hasafiri tu ilimradi. Lakini pia Mheshimiwa Rais amekuwa akihudhuria vile vikao muhimu ambavyo huwakutanisha wakuu wa nchi na serikali mbalimbali hapa Duniani.mfano kama vikao vya umoja wa mataifa.vikao vilivyowakutanisha wakuu wa nchi na serikali katika kujadili matumizi ya nishati safi na salama badala ya matumizi ya kuni .vikao vilivyowakutanisha wakuu wa nchi na serikali pamoja na umoja wa falme za kiarabu kule Dubai n.k.

Usiangalie gharama linapokuja suala la kukutana na viongozi wenzako bali angalia tija ya vikao na ziara hizo itakayopatikana kwa Taifa lako. Ziara za Mh Rais zimeleta matokeo chanya sana kwa Taifa letu.imeifungua nchi yetu na sasa fursa za kiuchumi zinatiririka nchini kama maji ya mafuriko.

Tanzania siyo kisiwa na kama Taifa hatuwezi kujifungia ndani wenyewe na mambo yetu wenyewe utafikiri watu wenye ukoma au wagonjwa wa corona au kipindupindu .ni lazima mkuu wetu wa nchi afanye ziara za kuonana na wenzake katika kujadili masuala mbalimbali yatakayoleta na kuchochea fursa za biashara.hatuwezi tukasema tutalima sana kila aina ya zao wakati hujaweka mikakati ya wapi utauza bidhaa zako pamoja na wapi utapata mbolea au fedha za kuwekeza katika ujenzi wa viwanda au kuvutia watu wakija kujenga viwanda vya bidhaa fulani lakini ukitoka nje ya nchi au kualika wenzako basi utapata fursa mbalimbali zenye matokeo chanya kwa Taifa lako.

Tupo katika Dunia ya ushindani,Dunia ambayo kila mtu anatafuta fursa kwa ajili ya Taifa lake.ndio maana hakuna anayetulia na kujifungia ndani tu kama kipofu wakati wenzako wanakulika fursa hadi kwa tochi.
 
Mjinga mimi nina swali. Ni swali kumhusu Rais Samia [baadhi yenu ni mama yenu].

Sina takwimu wala taarifa zingine zozote za kuufuta huu ujinga wangu.

Na hata sijui niende wapi ili kuzipata takwimu na taarifa hizo.

Hivyo basi, JamiiForums ndiyo kimbilio langu nitakapo kupata baadhi ya taarifa.

Kwa namna fulani, JF imekuwa ni injini ya utafutaji wa baadhi ya taarifa.

Sasa ni hivi; huyu Rais wetu tokea achukue madaraka, ameshakaa nchini kwa hata mwezi mzima [mmoja] bila kusafiri kwenda nje ya nchi?

Nauliza hivyo kwa sababu naona kama vile kila baada ya wiki mbili hivi huwa ni lazima asafiri kwenda nje ya nchi, jambo ambalo sidhani kama lina tija sana kitaifa.

Wajuzi nijuzeni, tafadhalini sana.
Watakuja kujibu japo kwa majibu mepesi ila yasio na weledi!
 
kwenda nje sio shida, shida ni inaleta faida au hakuna kitu...??
Kwenda nje mara kwa mara siyo vizuri. Safari za rais ni gharama sana.

Kwa nchi maskini kama hii Tanzania yetu, siyo busara kutumia kodi za wananchi kwa safari zisizo na tija yoyote.

Rais anapaswa kuwa ndo mfano mzuri wa kubana matumizi.

Nchi ni maskini sana kwa Rais kuwa mzururaji wa dunia nzima.
 
Sidhani kama Rais anajipangia safari. Ana timu ya wataalamu wabobezi; mabingwa wa nyanja zote ambao hupanga safari zake. All options, possibilities, pros and cons; advantages and disadvantages zinakuwa zimezingatiwa by the time Rais anapokuwa anaelekea airport. Take that!
Hao hao unaowaita wabobezi ndio wanataka akae nje ya nchi muda mwingi ili wafanye yao! Sasa hivi naelewa kwa nini Magu aligoma kutoka nje ya nchi! Mama anapigwa kisawasawa! Nimemwambia na mimi aniteue japo kwa mwaka huu mmoja uliobaki kwenye utawala wake na sisi tule mema ya nchi!
 
kwenda nje sio shida, shida ni inaleta faida au hakuna kitu...??
Exactly, bottom line ni Mtanzania Afaidike, what's the point mtu akae ndani kama tupo kisiwani wakati anaweza kutengeneza Connection nyingi nje?

Mfano Kariakoo sasa hivi kuna ongezeko kubwa la wa Congo, Zambia, Wamalawi na Wacomoro, wengi walikimbia awamu iliopita wameanza kurudi kwa kasi Baada ya Raisi kupitia Nchi za jirani na kuwahimiza warudi.

Ndio maana hata wafanyabiashara walivyogoma Tra na Polisi kuharass hawa wageni na kudai Rushwa za Dola fasta fasta wakapigwa marufuku wasiwaguse.
 
Mjinga mimi nina swali. Ni swali kumhusu Rais Samia [baadhi yenu ni mama yenu].

Sina takwimu wala taarifa zingine zozote za kuufuta huu ujinga wangu.

Na hata sijui niende wapi ili kuzipata takwimu na taarifa hizo.

Hivyo basi, JamiiForums ndiyo kimbilio langu nitakapo kupata baadhi ya taarifa.

Kwa namna fulani, JF imekuwa ni injini ya utafutaji wa baadhi ya taarifa.

Sasa ni hivi; huyu Rais wetu tokea achukue madaraka, ameshakaa nchini kwa hata mwezi mzima [mmoja] bila kusafiri kwenda nje ya nchi?

Nauliza hivyo kwa sababu naona kama vile kila baada ya wiki mbili hivi huwa ni lazima asafiri kwenda nje ya nchi, jambo ambalo sidhani kama lina tija sana kitaifa.

Wajuzi nijuzeni, tafadhalini sana.
Ngoja mbunge wa zamani wa mbeya mzee sugu akusikie, maana ndie kuchakutwa alikuwa analazimisha na kuuliza maswali, kwa nini jpm haendi njeee??
 
Hao hao unaowaita wabobezi ndio wanataka akae nje ya nchi muda mwingi ili wafanye yao! Sasa hivi naelewa kwa nini Magu aligoma kutoka nje ya nchi! Mama anapigwa kisawasawa! Nimemwambia na mimi aniteue japo kwa mwaka huu mmoja uliobaki kwenye utawala wake na sisi tule mema ya nchi!
"Ili wanfanye yao"! That's very wrong kama kuna mteule anafanya hivyo yafaa afungwe jiwe la kusagia shingoni akatupwe kilindi kirefu!
 
Mjinga mimi nina swali. Ni swali kumhusu Rais Samia [baadhi yenu ni mama yenu].

Sina takwimu wala taarifa zingine zozote za kuufuta huu ujinga wangu.

Na hata sijui niende wapi ili kuzipata takwimu na taarifa hizo.

Hivyo basi, JamiiForums ndiyo kimbilio langu nitakapo kupata baadhi ya taarifa.

Kwa namna fulani, JF imekuwa ni injini ya utafutaji wa baadhi ya taarifa.

Sasa ni hivi; huyu Rais wetu tokea achukue madaraka, ameshakaa nchini kwa hata mwezi mzima [mmoja] bila kusafiri kwenda nje ya nchi?

Nauliza hivyo kwa sababu naona kama vile kila baada ya wiki mbili hivi huwa ni lazima asafiri kwenda nje ya nchi, jambo ambalo sidhani kama lina tija sana kitaifa.

Wajuzi nijuzeni, tafadhalini sana.
Naunga mkono hoja
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom