Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akitembelea maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko katika Mji wa Katesh Wilaya ya Hanang Mkoa wa Manyara na Kuzungumza na Wananchi Katika Uwanja wa Shule ya Msingi Katesh.


Rais Samia amewapa Pole na kuwaasa kupokea hali hii na kushukuru kwa kuwa ni kazi ya Mungu. Ameahidi Serikali kuwa pamoja kwa kutoa misaada ya hali na mali kwa wananchi hao huku wakiangalia namna ya kuwaepusha wananchi wengine kuingia kwenye balaa kama hili.

IMG_9294.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waathirika wa Mafuriko waliopo kwenye kambi zao Katesh, Wilayani Hanang mkoani Manyara

Baadhi ya Nukuu za Rais Samia akizungumza na wakazi wa Hanang
Majanga kama haya yanapotokea huwa yanaleta mfadhaiko kwa wananchi. Hivyo basi, nimeitaka Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii na Makundi Maalum kuleta wataalam (wa saikolojia) hapa wazungumze na waathirika na waweze kuwarudisha katika hali ya kawaida kabisa.

Mimi nimekuja kama mkuu wa nchi kuja kuona kilichotokea, na nimekuja kuwaona kuwapa faraja kwamba sisi kama Serikali tuko nanyi toka jambo limetokea lakini tutakuwa nanyi mpaka tuhakikishe kila mmoja amekaa mahali anapostahili kukaa.

Wataalam wameweza kupata eneo ambalo tunahisi Serikali tutahamishia watu huko na tukawa nao bega kwa bega katika kukamilisha ujenzi wao na kuhakikisha wamepata makazi ambayo yatakuwa makazi yao ya kudumu na kuondoka kwenye makambi.

Huku haya yakijiri, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama amesema Madhara yaliyotokana na janga hilo hadi sasa yamesababisha vifo 76 mpaka leo, majeruhi 117 na kaya 1,150 zenye wakazi wapatao 5,600 zimeathirika. Ekari 750 za mashamba zimeharibika, na pia kuna vifo vya mifugo.
 
Vijana wa ufipa umekubali raisi ni mmoja tu nchi hii haya nendeni mkasalimie wagonjwa huko Bugando nao pia ni watanzania na wanawahusu!
 
Hili ndio jambo la Aibu la kufungia Mwaka 2023, lakini cha kushangaza ni kwamba Wananchi wa Hanang ni kama wamepuuza ujio huo huku wakionekana wazi kujitenga, pamoja na ukweli kwamba wana uhitaji sana , lakini hawana furaha na ugeni huo.

Nadhani shida kubwa ni kugeuza maafa haya kuwa shughuli ya ccm , Wanajeshi wanaofanya kazi kufa na kupona hawatambuliki tena!

Kiukweli Jambo hili ni Aibu kwa Taifa.
 
Hili ndio jambo la Aibu la kufungia Mwaka 2023 , lakini cha kushangaza ni kwamba Wananchi wa Hanang ni kama wamepuuza ujio huo huku wakionekana wazi kujitenga...
Ndio chama tawala kilichounda serikali wacha wajimwage nyinyi mlitaka kwenda kama nani?
 
Back
Top Bottom