Rais Samia: Baada ya taarifa za maafa na kukatisha mkutano wa COP28 Dubai, marafiki zetu wametuchangia Bilioni 2.5

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,785
Safi sana mama Kwa kuwa unaheshimika na wenzako na wanaithamini Tanzania tunashukuru Kwa hayo mabilioni waliyotoa hao marafiki wa Tanzania.

Nimeona hapo mnasema mtawajengea makazi na mambo mengingineyo,nishauri pesa hizi wapewe Suma JKT wajenge makazi Kwa oparesheni kama wanavyofanha kule Msomela Kwa masai.

Usije thubutu kuwapa hao Tamisemi na watu wengine wa dizaini hiyo maana Watanzania sio watu ni majizi.
---
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa Dubai kwa ajili ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28), kabla ya kufupisha safari hiyo na kurejea nchini ili kushughulikia kwa karibu janga la mafuriko Wilayani Hanang amesema akiwa Dubai Mashirika mbalimbali yamechangia Tsh. bilioni 2.5 kwa ajili ya kusaidia Waathirika wa janga hilo.

Akiongea na Wananchi walioathirika na janga hilo katika Shule ya Msingi Katesh Wilayani Hanang leo December 07,2023, Rais Samia amesema “Nawashukuru Watanzania waliotoa msaada kwa njia moja au nyingine, huu ndio upendo tunaozungumza siku zote, janga lilipotokea nilikuwa safarini, taarifa zimetoka wenzetu kule wamesikia na kwahiyo wenzetu kule wengi tu Mashirika yaliyokuwepo kule wametuchangia kiasi cha Tsh. bilioni 2.5 na nimeelekeza waziingize benki”

“Mpango kamili ukitimia wa Waziri Mkuu basi fedha za matumizi zipo pale na tunategemea michango zaidi ili tutimize mpango wetu wa kukamilisha makazi kwa walioathirika, wito wangu kwa Kamati ni kufanya matumizi mazuri ya fedha zinazokusanywa, fedha za majanga sio za kumnufaisha Mtu binafsi kwahiyo tuwe Waadilifu”

My Take
Serikali haikuleta Mafuriko kama ambavyo haikuleta tetemeko in Magufuli 's Voice.

Serikali kuwajengea walioathirika
Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali imekusudia kuwajengea makazi waathirika wa maporomoko ya tope Hanang na kuagiza kukamilisha haraka uchunguzi wa kina chanzo kilichosababisha madhara hayo.

Ameyasema hayo leo Alhamis Desemba 7, 2023 katika viwanja vya Shule ya Msingi Katesh alipokwenda kutoa pole kwa waathirika wa maporomoko hayo yaliyotokea alfajiri ya Desemba 3,2023, ambapo hadi leo jioni vifo vimefikia 76 na majeruhi zaidi ya 110.
 
Hizo kama pesa za Gawio tu
Nitakuwa wa mwisho kuamini
mzikwibe tena kama za DUKOBA

Hela za wahanga zisinufaishe mtu binafsi

"Baada ya maafa yaliyochukua uhai wa baadhi ya ndugu zetu, kazi ya kuurudisha mji mdogo wa Katesh pamoja na vijiji jirani katika hali ya kawaida sasa inaendelea.

Waathirika wa maafa haya waliopo kwenye matibabu tutaendelea kuwahudumia mpaka pale watakaporejea katika hali ya kawaida. Wale walio kwenye kambi tutaendelea kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu. Nimeagiza pia uwepo wa huduma ya kisaikolojia kama sehemu ya tiba kwa madhila waliyopitia ndugu zetu hawa. Sambamba na hayo, nimewaeleza kwamba Serikali itashirikiana na wadau mbalimbali kuwapatia makazi.

Nawakumbusha wale tuliowapa jukumu la kuratibu misaada hii kwa ndugu zetu kuwa fedha za majanga si fedha za kumnufaisha mtu binafsi, hivyo basi, uadilifu uzingatiwe. Tutumie fedha hizi kwa lengo lililokusudiwa ambalo ni kuwahudumia waathirika, kufanya marekebisho na kuwafariji ili waweze kurejea katika maisha yao ya kawaida."- Imeeleza taarifa ya Rais Samia Suluhu Hassan.
 
Back
Top Bottom