Rais Samia afupisha ziara yake Dubai kurejea nchini haraka iwezekanavyo, Serikali kugharamia mazishi na matibabu ya majeruhi wa mafuriko ya Hanang

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuwa serikali igharamie mazishi ya wote waliopoteza maisha kutokana na mvua kubwa iliyotokea na mafuriko katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang.

Rais Samia pia ametaka majeruhi wote ambao wapo kwenye hospitali mbalimbali wapate matibabu yote yanayostahili kwa gharama za Serikali, huku vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea kutoa msaada wa dharura na uokoaji.

Aidha Rais Samia ameelekeza Serikali ya Mkoa na Kitengo cha Maafa cha Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha wananchi wote ambao makazi yao yamesombwa na maji wapate makazi ya muda kwa ajili ya kuwastiri wananchi hao.

Maafa haya yameathiri mji wa Katesh hususan vijiji vya Jorodom, Ganana, Katesh na Dumbeta na pia vijiji vya Gendabi, Sarijandu, Arukushay, na Sebasi.

Kwa taarifa za awali nyumba na mifugo imeathirika sana huku idadi za kaya zilizoathirika ni 1,150, idadi ya watu walioathirika hadi sasa ni 5,600 na pia ikikadiriwa takriban ekari 750 za mashamba zimeharibika.

Licha ya changamoto kadhaa zilizokuwepo uokoaji unavyoendelea ikiwemo barabara kuharibika huku tope na magogo kujaa barabara kuu na mitaani na kusababisha mawasiliano kukatika, serikali inajitahidi kukabiliana nazo.

Idadi ya vifo hadi sasa ni zaidi ya watu 50 huku majeruhi waliopelekewa katika hospitali mbalimbali za wilaya, mkoa na vituo vya afya ni zaidi ya 80.

Wakati huo huo Rais Samia ameelekeza tathmini ya kina ifanyike juu ya maafa hayo na vitengo na taasisi zote za Serikali zinazohusika kuwepo eneo la tukio na kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha hali inarejea kawaida.

Rais Samia anatoa pole kwa wafiwa wote kutokana na msiba mkubwa uliowakumba na pia anawahakikishia wananchi walioathirika kuwa serikali iko pamoja nao na itahakikisha inashughulikia masuala yote yaliotokana na janga hili.

Rais Samia ambaye amekuwepo Dubai kwa ajili ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) ameamua kufupisha safari hiyo na kurejea nchini haraka iwezekanavyo ili kushughulikia kwa karibu janga hilo.

WhatsApp Image 2023-12-04 at 13.48.07.jpeg

WhatsApp Image 2023-12-04 at 13.48.08.jpeg

Pia soma; Manyara UPDATE: Waliofariki kwa Mafuriko Wilayani Hanang wafikia 63
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuwa serikali igharamie mazishi ya wote waliopoteza maisha kutokana na mvua kubwa iliyotokea na mafuriko katika

Halmashauri ya Wilaya ya Hanang.

Rais Samia pia ametaka majeruhi wote ambao wapo kwenye hospitali mbalimbali wapate matibabu yote yanayostahili kwa gharama za Serikali, huku vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea kutoa msaada wa dharura na uokoaji.

Aidha Rais Samia ameelekeza Serikali ya Mkoa na Kitengo cha Maafa cha Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha wananchi wote ambao makazi yao yamesombwa na maji wapate makazi ya muda kwa ajili ya kuwastiri wananchi hao.

Maafa haya yameathiri mji wa Katesh hususan vijiji vya Jorodom, Ganana, Katesh na Dumbeta na pia vijiji vya Gendabi, Sarijandu, Arukushay, na Sebasi.

Kwa taarifa za awali nyumba na mifugo imeathirika sana huku idadi za kaya zilizoathirika ni 1,150, idadi ya watu walioathirika hadi sasa ni 5,600 na pia ikikadiriwa takriban ekari 750 za mashamba zimeharibika.

Licha ya changamoto kadhaa zilizokuwepo uokoaji unavyoendelea ikiwemo barabara

kuharibika huku tope na magogo kujaa barabara kuu na mitaani na kusababisha mawasiliano kukatika, serikali inajitahidi kukabiliana nazo.

Idadi ya vifo hadi sasa ni zaidi ya watu 50 huku majeruhi waliopelekewa katika hospitali mbalimbali za wilaya, mkoa na vituo vya afya ni zaidi ya 80.

Wakati huo huo Rais Samia ameelekeza tathmini ya kina ifanyike juu ya maafa hayo na vitengo na taasisi zote za Serikali zinazohusika kuwepo eneo la tukio na kufanya

kazi usiku na mchana ili kuhakikisha hali inarejea kawaida.
Utuambie pia serikali ilichukua hatua gani kabla ya mafuriko hayajatokea maana TMA walitoa angalizo mda mrefu serikali ikaweka pamba masikioni.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuwa serikali igharamie mazishi ya wote waliopoteza maisha kutokana na mvua kubwa iliyotokea na mafuriko katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang.

Rais Samia pia ametaka majeruhi wote ambao wapo kwenye hospitali mbalimbali wapate matibabu yote yanayostahili kwa gharama za Serikali, huku vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea kutoa msaada wa dharura na uokoaji.

Aidha Rais Samia ameelekeza Serikali ya Mkoa na Kitengo cha Maafa cha Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha wananchi wote ambao makazi yao yamesombwa na maji wapate makazi ya muda kwa ajili ya kuwastiri wananchi hao.

Maafa haya yameathiri mji wa Katesh hususan vijiji vya Jorodom, Ganana, Katesh na Dumbeta na pia vijiji vya Gendabi, Sarijandu, Arukushay, na Sebasi.

Kwa taarifa za awali nyumba na mifugo imeathirika sana huku idadi za kaya zilizoathirika ni 1,150, idadi ya watu walioathirika hadi sasa ni 5,600 na pia ikikadiriwa takriban ekari 750 za mashamba zimeharibika.

Licha ya changamoto kadhaa zilizokuwepo uokoaji unavyoendelea ikiwemo barabara kuharibika huku tope na magogo kujaa barabara kuu na mitaani na kusababisha mawasiliano kukatika, serikali inajitahidi kukabiliana nazo.

Idadi ya vifo hadi sasa ni zaidi ya watu 50 huku majeruhi waliopelekewa katika hospitali mbalimbali za wilaya, mkoa na vituo vya afya ni zaidi ya 80.

Wakati huo huo Rais Samia ameelekeza tathmini ya kina ifanyike juu ya maafa hayo na vitengo na taasisi zote za Serikali zinazohusika kuwepo eneo la tukio na kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha hali inarejea kawaida.

Rais Samia anatoa pole kwa wafiwa wote kutokana na msiba mkubwa uliowakumba na pia anawahakikishia wananchi walioathirika kuwa serikali iko pamoja nao na itahakikisha inashughulikia masuala yote yaliotokana na janga hili.

Rais Samia ambaye amekuwepo Dubai kwa ajili ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) ameamua kufupisha safari hiyo na kurejea nchini haraka iwezekanavyo ili kushughulikia kwa karibu janga hilo.
View attachment 2832970
View attachment 2832974
Mkutano wa Cop28 ulinalizika 2/12/2023, hiyo ziara aliyokatisha Leo ni ipi?
 
Utuambie pia serikali ilichukua hatua gani kabla ya mafuriko hayajatokea maana TMA walitoa angalizo mda mrefu serikali ikaweka pamba masikioni.
Uzuri wa Serikali ya CCM ikipewa ushauri na vyombo vinavyo husika vya maafa kabla ya tukio halija tokea. Inaweka pamba masikioni mpaka kukitokea majangaa ndio inakuwa mstari wa mbele katika kushughulikia waliopatwa na hayo majangaa hiyo ndio Serikali ya CCM inavyofanya kazi.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuwa serikali igharamie mazishi ya wote waliopoteza maisha kutokana na mvua kubwa iliyotokea na mafuriko katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang.

Rais Samia pia ametaka majeruhi wote ambao wapo kwenye hospitali mbalimbali wapate matibabu yote yanayostahili kwa gharama za Serikali, huku vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea kutoa msaada wa dharura na uokoaji.

Aidha Rais Samia ameelekeza Serikali ya Mkoa na Kitengo cha Maafa cha Ofisi ya Waziri Mkuu kuhakikisha wananchi wote ambao makazi yao yamesombwa na maji wapate makazi ya muda kwa ajili ya kuwastiri wananchi hao.

Maafa haya yameathiri mji wa Katesh hususan vijiji vya Jorodom, Ganana, Katesh na Dumbeta na pia vijiji vya Gendabi, Sarijandu, Arukushay, na Sebasi.

Kwa taarifa za awali nyumba na mifugo imeathirika sana huku idadi za kaya zilizoathirika ni 1,150, idadi ya watu walioathirika hadi sasa ni 5,600 na pia ikikadiriwa takriban ekari 750 za mashamba zimeharibika.

Licha ya changamoto kadhaa zilizokuwepo uokoaji unavyoendelea ikiwemo barabara kuharibika huku tope na magogo kujaa barabara kuu na mitaani na kusababisha mawasiliano kukatika, serikali inajitahidi kukabiliana nazo.

Idadi ya vifo hadi sasa ni zaidi ya watu 50 huku majeruhi waliopelekewa katika hospitali mbalimbali za wilaya, mkoa na vituo vya afya ni zaidi ya 80.

Wakati huo huo Rais Samia ameelekeza tathmini ya kina ifanyike juu ya maafa hayo na vitengo na taasisi zote za Serikali zinazohusika kuwepo eneo la tukio na kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha hali inarejea kawaida.

Rais Samia anatoa pole kwa wafiwa wote kutokana na msiba mkubwa uliowakumba na pia anawahakikishia wananchi walioathirika kuwa serikali iko pamoja nao na itahakikisha inashughulikia masuala yote yaliotokana na janga hili.

Rais Samia ambaye amekuwepo Dubai kwa ajili ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) ameamua kufupisha safari hiyo na kurejea nchini haraka iwezekanavyo ili kushughulikia kwa karibu janga hilo.

View attachment 2832970
View attachment 2832974
Ikipendeza eneo hilo apewa mwekezaji ili aliboreshe.
 
Back
Top Bottom