Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,752
218,339
Miongoni mwa siri zilizofichuliwa leo kuhusu Mkataba wa kuiuzia kampuni ya Waarabu Bandari za Tanzania, imo habari kwamba Bandari zitakazohusika ni zile za Tanganyika Pekee, za Zanzibar hazitahusika.

Ikumbukwe kwamba Bandari ni miongoni mwa mambo ya Muungano, ikiwa kama jambo hili lina faida kwanini tunaitenga Zanzibar. Je, Wazanzibar hawataki faida?

Bali kitu pekee ambacho tumekiona ni kwamba Waziri Aliyesaini Mkataba huu anayeitwa Makame Mbarawa anatokea upande wa Zanzibar kama alivyo Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia soma > Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World

---
MAONI YA WADAU

Mapato yatakayotokana na bandari za Tanganyika ni ya muungano na Zanzibar inapata mgao wake achilia mbali mgao wa 4.5% BoT kwa pato linalotokana na rasilimali za Bara.

Sasa hivi Zanzibar wana mpango wa kulipa wajumbe wa nyumba kumi mishahara. Tayari wazee wanalipwa pensheni na waliobaki wanatumia umeme bure. Hapo hawajui gharama za ulinzi , mambo ya ndani na nje au taasisi zingine za muungano.

Huyu Mbarawa anakuwaje waziri wa jambo lisilo la muungano? Sasa Rais wa JMT ni Mzanzibar, Rais wa SMZ ni Mzanzibar na Waziri ni Mzanzibar. Nani anamtetea Mtanganyika kwa usawa huo.

Uuzwaji wa bandari hauna uchungu isipokuwa kwa Watanganyika.
Nyerere, Mkapa, Kikwete , JPM walijua hilo hawakuwahi kufikiria. Walijua ni rasilimali na hazina za Watanganyika
Mwinyi aliuza Loliondo ''ujombani'' akiwa na Waziri Diria. Historia bwana!

JokaKuu Pascal Mayalla
 
A huge miscalculation by SSH. Watanzania (watanganyika) wameibiwa sana kwa mgongo wa ubinafsishaji, yaani serikali inatumia matrilioni kuwekeza kwenye kitu alafu mwisho wa siku wahuni wachache wanapiga dili na kuuziwa kwa bei za kutupa.

Imetokea tena na tena na tena, ATCL, TTCL, TRC, NBC, mashamba ya serikali, nyumba za serikali, viwanda vya serikali na mengine mengi. Bado CCM haijifunzi tu??

Watu wanamlaumu JPM kuwa alikuwa katili lakini bwana yule alikuwa na akili za kutatua changamoto, akiona sehemu kuna mapungufu basi anaumiza kichwa kuona taitizo ni nini, watu? Mifumo? Sheria? Kisha anajaribu kutatua.
 
Sielewi viongozi wa sasa walilenga nini
 
Miongoni mwa siri zilizofichuliwa leo kuhusu Mkataba wa kuiuzia kampuni ya Waarabu Bandari za Tanzania , imo habari kwamba Bandari zitakazohusika ni zile za Tanganyika Pekee , za Zanzibar hazitahusika .

Ikumbukwe kwamba Bandari ni miongoni mwa mambo ya Muungano , ikiwa kama jambo hili lina faida kwanini tunaitenga Zanzibar , Je Wazanzibar hawataki faida ?

Bali kitu pekee ambacho tumekiona ni kwamba Waziri Aliyesaini Mkataba huu anayeitwa Makame Mbarawa anatokea upande wa Zanzibar kama alivyo Rais Samia Suluhu Hassan .
Mapato yatakayotokana na bandari za Tanganyika ni ya muungano na Zanzibar inapata mgao wake achilia mbali mgao wa 4.5% BoT kwa pato linalotokana na rasilimali za Bara.

Sasa hivi Zanzibar wana mpango wa kulipa wajumbe wa nyumba kumi mishahara. Tayari wazee wanalipwa pensheni na waliobaki wanatumia umeme bure. Hapo hawajui gharama za ulinzi , mambo ya ndani na nje au taasisi zingine za muungano.

Huyu Mbarawa anakuwaje waziri wa jambo lisilo la muungano? Sasa Rais wa JMT ni Mzanzibar, Rais wa SMZ ni Mzanzibar na Waziri ni Mzanzibar. Nani anamtetea Mtanganyika kwa usawa huo.

Uuzwaji wa bandari hauna uchungu isipokuwa kwa Watanganyika.
Nyerere, Mkapa, Kikwete , JPM walijua hilo hawakuwahi kufikiria. Walijua ni rasilimali na hazina za Watanganyika
Mwinyi aliuza Loliondo ''ujombani'' akiwa na Waziri Diria. Historia bwana!

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Mapato yatakayotokana na bandari za Tanganyika ni ya muungano na Zanzibar inapata mgao wake achilia mbali mgao wa 4.5% BoT kwa pato linalotokana na rasilimali za Bara.

Sasa hivi Zanzibar wanampango wa kulipa wajumbe wa nyumba kumi mishahara. Tayari wazee wanalipwa pensheni na waliobaki wanatumia umeme bure. Hapo hawajui gharama za ulinzi , mambo ya ndani na nje au taasisi zingine za muungano.

Huyu Mbarawa anakuwaje waziri wa jambo lisilo la muungano? Sasa Rais wa JMT ni Mzanzibar, Rais wa SMZ ni Mzanzibar na Waziri ni Mzanzibar. Nani anamtetea Mtanganyika kwa usawa huo.

Uuzwaji wa bandari hauna uchungu isipokuwa kwa Watanganyika.
Nyerere, Mkapa, Kikwete , JPM walijua hilo hawakuwahi kufikiria. Walijua ni rasilimali na hazina za Watanganyika
Mwinyi aliuza Loliondo ''ujombani'' akiwa na Waziri Diria. Historia bwana!

JokaKuu Pascal Mayalla
Daaaah
 
Miongoni mwa siri zilizofichuliwa leo kuhusu Mkataba wa kuiuzia kampuni ya Waarabu Bandari za Tanzania , imo habari kwamba Bandari zitakazohusika ni zile za Tanganyika Pekee, za Zanzibar hazitahusika .

Ikumbukwe kwamba Bandari ni miongoni mwa mambo ya Muungano, ikiwa kama jambo hili lina faida kwanini tunaitenga Zanzibar , Je Wazanzibar hawataki faida?

Bali kitu pekee ambacho tumekiona ni kwamba Waziri Aliyesaini Mkataba huu anayeitwa Makame Mbarawa anatokea upande wa Zanzibar kama alivyo Rais Samia Suluhu Hassan .
Bandari sio ishu ya Muungano ingawa DP World wamepewa kandarasinya kujenga Bandari Mpya ya Zanzibar na huenda ndio wakawa operator pia.
 
Ndugu yangu Nguruvi3, long time sana Mzee wangu..

Mmepotelea wapi na wenzio kama kina Mag3, Mchambuzi nk??

Ninayemwona na kumsoma mara Kwa mara humu ni ndugu yangu mmoja tu JokaKuu na jitegemee na Mwalimu

Hata kule Jukwaa la GT tulikokuwa tunafuatilia mijadala yenye hoja za nguvu kumepoa sana siku hizi...

Nikajiuliza hawa wazee na walimu wetu wa ujenzi wa hoja wamepatwa na mambo gani...

All in all, binafsi nafurahi sana kukuona na kukusoma tena....

NB: Ndugu Erythrocyte sikukusudia kukukwoti wewe. Nimekosea ila kwoti hii inamhusu ndugu Nguruvi3

Niwie radhi kama nimekukwaza kwa namna yoyote
 
Ndugu yangu Nguruvi3, long time sana Mzee wangu..

Mmepotelea wapi na wenzio kama kina Mag3, Mchambuzi nk??

Ninayemwona na kumsoma mara Kwa mara humu ni ndugu yangu mmoja tu JokaKuu na jitegemee na Mwalimu

Hata kule Jukwaa la GT tulikokuwa tunafuatilia mijadala yenye hoja za nguvu kumepoa sana siku hizi...

Nikajiuliza hawa wazee na walimu wetu wa ujenzi wa hoja wamepatwa na mambo gani...

All in all, binafsi nafurahi sana kukuona na kusoma tena....

NB: Ndugu Erythrocyte sikukusudia kukukwoti wewe. Nimekosea ila kwoti hii inamhusu ndugu Nguruvi3

Niwie radhi kama nimekukwaza kwa namna yoyote
Amina
 
Back
Top Bottom