Mkurugenzi wa Bandari amesema kuwa DP World bado hawajaanza kazi na hakuna mfanyakazi aliyevunjiwa mkataba wake

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,262
9,714
Ndugu zangu Watanzania,

Mkurugenzi Mkuu wa bandari yetu ya Dar es salaam Ndugu Mrisho amekanusha taarifa za uzushi na uongo mkubwa ulioenezwa na watu kuwa wafanyakazi wa bandari ya Dar wamevunjiwa mkataba na DP World ambao wameleta wafanyakazi wao.amesema kuwa taarifa hizo ni za uongo na zenye kuleta taharuki tu katika jamii.

Amesema kuwa taarifa hizo ni za uongo kwa kuwa DP World bado hajaanza kazi au shughuli zake japo anatarajia kuanza kazi hivi karibuni na pia hakuna mfanyakazi ambaye atavunjiwa mkataba wake, ameeleza kuwa pia bandari inaendelea na kazi yake usiku na mchana huku wafanyakazi wakifanya kazi kwa shift na wala hakuna mgomo wa aina yoyote ile wa wafanyakazi wa bandari,Lakini pia amekanusha habari ya kuwa kuna upendeleo katika utoaji wa mizigo pale bandarini.amesema kuwa taarifa hizo nazo ni za uzushi na uongo kwa kuwa jambo hilo halipo hata kidogo na badala yake haki inatendeka vyema kwa watu wote..

Rai yangu ni kuwa serikali ianze kuwachukulia hatua kali sana vijana wa CHADEMA ambao wamekuwa mstari wa mbele kutoa na kuleta habari za uzushi ,uongo na uchonganishi kupitia mitandao ya kijamii.nasema hivi kwa kuwa hata habari hii imezushwa na vijana wa CHADEMA ambao wakati wote wamekuwa ni watu wenye kuleta habari za kuleta taharuki na sintofahamu katika jamii.

Tabia hii ikiachwa iendelee na kukomaa pasipo watu hawa kuchukuliwa hatua za kisheria italeta shida kubwa sana mbele ya safari,ipo siku watakuja wazue jambo litakalo tetemesha na kutikisa usalama wetu wa Taifa pamoja na utulivu katika Taifa hili .watafanya hivi kwa kujuwa kuwa hakuna hatua za aina zozote zile zitakazochukuliwa zidi yao ,mfano katika suala hilo walilozusha linaleta athari katika uchumi wetu kwa sababu linaleta taharuki na sintofahamu kwa Wafanyabiashara wanaotegemea na kuitumia bandari yetu.

Kutoa taarifa kuwa kuna upendeleo katika utoaji wa mizigo bandarini maana yake ni kuwapa hofu watumiaji wa bandari ambao wanaweza kuhama kuitumia bandari yetu katika kupitishia mizigo yao, na kuamua kutumia bandari za washindani wetu na hivyo kupunguza mapato yatokanayo na bandari na hivyo kupunguza mapato katika nchi. Jambo hili tunaweza kuliona dogo lakini katika jicho la tatu hili siyo la kulifumbia macho maana linauwezo wa kuathiri uchumi wetu.

Lakini pia watu hawa hasa vijana wa CHADEMA wanaweza kutumiwa na mahasimu wetu na washindani wetu kiuchumi au hata maadui zetu waliojificha kuwapa taarifa za uongo na uzushi ili wazitoe kupitia mitandao ya kijamii na hivyo kuleta taharuki,kuharibu mahusiano ya kidiplomasia,kuleta hali ya kutoaminiana,kuleta na kupandikiza chuki kwa watu,kuleta uhasama,visasi na vinyongo.

kwa hiyo ni muhimu sana serikali ianze kuwachukulia hatua kali sana za kisheria. uhuru una mipaka yake.uhuru pasipo mipaka ni fujo na hatari kwa usalama wa Taifa letu.ni lazima tufahamu upi ni uhuru wa mtu na wapi unaishia na upi ni wajibu wa mtu.ni lazima kila mtu ajuwe ana wajibu wa kuheshimu sheria zetu pasipo kutoa habari au taarifa zenye kuleta taharuki katika jamii pasipo ushahidi wa aina yoyote ile.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
 
Kuna hili la kuwa kutakuwa na watumishi watakaoamia DP WORLD na watakaobaki TPA. Je kama wafanyakazi wa TPA wote watagoma kwenda DP WORLD nini kitatokea kama DP WORLD akiajir watumishi wapya hawa waliobak TPA watakuwa watumishi hewa au watafanya kazi gani nyingine?
 
Sasa kilichopelekea taharuki kwa wafanyakazi jana na juzi ni nini? Na kwann huyu mkurugenzi alikuwa hapokei simu na akawa anawakimbia waandishi wa habari?

Hii ni janja janja tu ndugu zangu (in jiwe's voice) . Haya maneno amelishwa,. Yaani ni maelekezo maalumu toka kwa wateule wake kuwa aje atulize hali ya hewa.
 
Kuna hili la kuwa kutakuwa na watumishi watakaoamia DP WORLD na watakaobaki TPA. Je kama wafanyakazi wa TPA wote watagoma kwenda DP WORLD nini kitatokea kama DP WORLD akiajir watumishi wapya hawa waliobak TPA watakuwa watumishi hewa au watafanya kazi gani nyingine????
Nani kakuambia kuwa DP World ataajiri wafanyakazi wapya? Suala la mikataba ya wafanyakazi ni suala la ndani kwa hiyo hilo ondoeni shaka juu ya wafanyakazi wetu wa kitanzania kuendelea kuwepo bandarini maana ujio wa DP world haujaja kuuwa ajira za watanzania bali umekuja kuongeza ajira zaidi ,mapato zaidi pamoja na ufanisi zaidi katika kuhudumia utoaji wa mizigo pale bandarini.
 
Sasa kilichopelekea taharuki kwa wafanyakazi jana na juzi ni nini? Na kwann huyu mkurugenzi alikuwa hapokei simu na akawa anawakimbia waandishi wa habari...
Acha uzushi wako wewe ulimpigia simu ipo ambayo akawa hapokei.kwani ni lazima ukimpigia mtu simu apokee hapo hapo?

Hujuwi mwingine wakati unampigia simu anaweza akawa kwenye vikao ,au anaendesha chombo cha moto au yupo mbali na simu?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mkurugenzi Mkuu wa bandari yetu ya Dar es salaam Ndugu Mrisho amekanusha taarifa za uzushi na uongo mkubwa ulioenezwa na watu kuwa...
DP wafunge virago maana tanzania hawatakua na amani. Watanzania hawahitaji wezi hawa wala hawawekezi ila kula faida ya uwekezaji uliyofanywa na umma. Dubai washatuibia loliondo sasa wanatamani bandari zetu maana washatuona wajinga.
 
DP wafunge virago maana tanzania hawatakua na amani. Watanzania hawahitaji wezi hawa wala hawawekezi ila kula faida ya uwekezaji uliyofanywa na umma. Dubai washatuibia loliondo sasa wanatamani bandari zetu maana washatuona wajinga.
Acha mawazo ya kijima wewe.
 
Sasa kilichopelekea taharuki kwa wafanyakazi jana na juzi ni nini? Na kwann huyu mkurugenzi alikuwa hapokei simu na akawa anawakimbia waandishi wa habari??

Hii ni janja janja tu ndugu zangu (in jiwe's voice) . Haya maneno amelishwa,. Yaani ni maelekezo maalumu toka kwa wateule wake kuwa aje atulize hali ya hewa.
CEO ni mtu wa ijumaa ni kipenzi cha maza
 
Acha uzushi wako wewe.ulimpigia simu ipo ambayo akawa hapokei.kwani ni lazima ukimpigia mtu simu apokee hapo hapo? Hujuwi mwingine wakati unampigia simu anaweza akawa kwenye vikao ,au anaendesha chombo cha moto au yupo mbali na simu?
Umeisoma comment yangu yote na kukimaliza? Nimesema alikuwa mpk anawakimbia waandishi wa habari. It means alikuwa anaonekana.

DP World imeanza kung'ata , na huu ni mwanzo tu.
 
Back
Top Bottom