Masomo ya hisabati na computer/coding yafundishwe kwa kiingereza shule za msingi

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
5,466
Reaction score
15,685
kuna haja ya kuanza kufikiria mfumo ambao Hisabati na Computer Science/Coding vinafundishwa kwa kutumia Kiingereza kwa kiwango kikubwa zaidi kuanzia shule za msingi.

Sababu kubwa ni kwamba dunia ya sayansi na teknolojia inatumia sana lugha ya Kiingereza. Istilahi nyingi ambazo mwanafunzi atakutana nazo baadaye katika programming, computer science, engineering na masomo mengine ya STEM tayari ziko kwa Kiingereza.
Kwa mfano, kwenye Hisabati mwanafunzi anaweza kuanza kuzoea maneno kama:
  • Addition
  • Subtraction
  • Multiplication
  • Division
  • Fraction
  • Percentage
  • Equation
  • Geometry
Na kwenye Coding:
  • Variable
  • Function
  • Loop
  • Condition
  • If
  • Else
  • Algorithm
  • Program
Hii inaweza kumsaidia mwanafunzi asifikie sekondari au chuo akiwa analazimika kujifunza dhana na lugha ya kitaaluma kwa wakati mmoja.

Lakini sidhani kama tunapaswa kumlazimisha mtoto mdogo kuelewa kila kitu kwa Kiingereza pekee. Uelewa wa dhana ndio jambo la kwanza. Mwalimu anaweza kutumia Kiswahili pale inapohitajika, huku istilahi na maelekezo muhimu yakianza kujengwa kwa Kiingereza.

Mfano wa swali la Hisabati:

"A farmer has 12 cows and buys 8 more. How many cows does he have altogether?"

Mtoto anajifunza Kiingereza huku akitatua:

12 + 8 = 20
Kwenye Coding:
"If the score is greater than 50, display 'Pass'."
Mtoto anaanza kuelewa lugha inayotumika kwenye programming pamoja na mantiki ya computer.

Tunaweza kutumia lugha zote mbili kwa mkakati unaomjengea mtoto uwezo wa kuelewa dhana, kutumia teknolojia na baadaye kusoma sayansi na computer science kwa ufanisi.
Tanzania inahitaji kizazi kinachoweza kutumia teknolojia, kutengeneza software na kushindana katika uchumi wa kidijitali. Msingi huo unaweza kuanza kujengwa mapema kabisa shule ya msingi.
Wakusoma 12
 
Hisabati na Computer Science/Coding vinafundishwa kwa kutumia Kiingereza kwa kiwango kikubwa zaidi kuanzia shule za msingi.
Kukwepa Computer Engineering ni kujikabidhi kwa "super intelligence slavely". Computer science/coding without mastering the technology of producing your own motherboard and all those chips that help coding ni utumwa. Ona wanachowafanyia programmers wetu. Wanawayumbisha balaa ili waendee kuwa watumwa.

Sijiui naekeweka.!? Au ndiyo naonekana pure insane.
 
Kukwepa Computer Engineering ni kujikabidhi kwa "super intelligence slavely". Computer science/coding without mastering the technology of producing your motherboard and all those chips that help coding ni utumwa. Ona wanachowafanyia programmers wetu. Wanawayumbisha balaa ili waendee kuwa watumwa.

Sijiui naekeweka.!? Au ndiyo naonekana pure insane.
hujaeleweka, ongeza minyama!
 
Kukwepa Computer Engineering ni kujikabidhi kwa "super intelligence slavely". Computer science/coding without mastering the technology of producing your motherboard and all those chips that help coding ni utumwa. Ona wanachowafanyia programmers wetu. Wanawayumbisha balaa ili waendee kuwa watumwa.

Sijiui naekeweka.!? Au ndiyo naonekana pure insane.
hapa unaeleweka
 
Back
Top Bottom