Status
Not open for further replies.
Kitendo Cha Magufuli Kuangalia Makabila Ndio Ukabila Wenyewe Atakua Ana U-practice, Vilevile Dini. Kitu Cha Msingi Ni Kua Na Fursa Nyingi Za Ajira, Ili Wenye Sifa Waajirike, Waache Kulalama Mitaani Na Kuzusha Hofu Na Distrust. Funny How! Wabongo Wanatabia Ya Kuipondea Kenya Sana Kua Ina Ukabila Kumbe Hapa Bongo Ndio Cancer Yenyewe, Ukiwa Kabila Fulani Hutakiwi Kua Prezidaa, Ukiwa Dini Fulani Usubiri Mpaka Zamu Yako Ije, Manake Ni Wazamu Kwa Zamu. Ukiwa Nje Ya Chamadola Hupewi Hata Ukuu Wa Chuo, Tuache Unafiki.

Kuongeza wigo Wa ajira ni sawa lkn siyo ufumbuzi. Wale waliyohodhi ajira wataendelea kuvuta /kuwapa watu wao kazi. Swali langu n kwamba huu mdudu Wa ajira kukaa kidini, kikabila na kikanda utauawa lini? Hiyo ndiyo hoja yangu.

Usizunguuke mbuyu. Pasua jipu
 
Kuna Wizara inaitwa Wizara ya Elimu, ilihamisha Watumishi pale Makao Makuu mwishoni mwa mwaka Jana. Mpaka sasa hivi hawajapewa pesa zao za Usumbufu(Disturbance Allowance). Hongera Prof. Sifuni Mchome kwa kupunguza watumishi pale Makao Makuu mkabala na Ofisi Kuu ya Nchi, ila hukufanya jambo jema kutowalipa Disturbance Allowance mpaka leo.
 
Ni kweli kabisa. Tumuombee raisi wetu aendelee kuwa na afya na kasi isiyoyakifani.. afikie hyo stage ya kushughulikia hilo tatizo kweny ajira.. mm binafsi natamani kweli liishe, watu tuanze kuajiriwa kulingana na qualifications
 
Kwa staili ya uandishi umelenga vitu viwili TRA na NSSF,
Kuwa Muwazi Unataka wafanyakazi wa TRA wafanyweje?
Je NSSF wafanyweje?
Majipu, majipu!!!!!!!!!!!!!
Me nimechoka na style hii ya majipu, Tunataka kuishi maisha ya amani na upendo.
Nijuavyo mimi hakuna mfanyakazi wa TRA au NSSF anayefanya kazi bila kutimiza vigezo. Swala la ukabaila na udini halijaanza leo, Lipo toka Enzi za Mwalimu Julius Nyerere(sikiliza hotuba yake ya 1995 yote), Hata wakati anaanzisha jumuiya ya afrika mashariki lengo ilikuwa kupunguza ukabaila na udini kenya na uganda... Mambo ya ukabaila yamekaa hivi:
KILIMANJARO, ARUSHA, MBEYA, IRINGA, KAGERA ni mikoa yenye wasomi wengi sana. Maprofessa wengi wanatoka kanda ya Ziwa,
Utasikia Professa Tibaijuka, Professa Kamuzora, Utasikia Professor Kuzilwa, Utasikia Professor.......
For your information: Hii mikoa imepeleka shule WATOTO wengi sana, kwa hiyo ukiona wapo wamejaa ofisini ujue wamekwenda shule.

Me nakumbuka kozi niliyoisomea chuo, ktk darasa langu kati ya wanafunzi 120 mkoa wangu nilikuwa mimi tu. wengine wote walikuwa Iringa, kilimanjaro, mbeya, kagera.....n.k

Swala la Dini: liliibuka waziwazi June 30,2009. Sitaki kuongea sana, kwa maslahi ya amani ya nchi. lakini wote tunajua kilichotokea. Kwa hiyo aliyelala usimwamshe, ukimwamsha unalala wewe. Hivyo tu.

Nadhani nchi hii ina mengi ya kufanyiwa, Tujitahidi kuangalia tufanye nini ili tupige hatua...kwa sababu huwezi kuwafanya wanyonge kupata nguvu kwa kuwadhoofisha wenye nguvu.

KIJANA WA KITANZANIA, whatever you do, DO AT BEST.
 
Tunaomba mwenye data za waajiriwa wa NSSF atuwekee hapa. Ikiwezekana na majina kabisa maana hao ni waajira wa mashirika ya umma yanayoendeshwa kwa kodi zetu. Tumechoka na hizi ngojera.

Tunaomba mwenye data za waajiriwa wa TRA, CRDB & BOT atuwekee hapa. Ikiwezekana na majina kabisa maana hao ni waajira wa mashirika ya umma yanayoendeshwa kwa kodi zetu. Tumechoka na hizi ngojera.
 
Huo wimbo wa UKABILA na UDINI kaimbe na familia yako. Kama hukidhi vigezo usitake ubebwe kwa ajili ya dini ama kabila lako.

Wewe ni mmoja wa waalibikiwa ktk nyumba unayoiongoza na usione tatizo. in fact si wewe tu, wapo wengi wanaogopa kuyaongelea haya kisa tu Tanzania haina udini au ukabila...
 
Tena mimi naanza na watumishi wa wilaya ya mkuranga mkoa wa pwani,hasa walimu wa shule za msingi na sekondari hado leo naandika ujumbe huu hatujalipwa areas zetu,tangu tupande daraja 2011 hatujalipwa areas zetu na mimi nikiwa mmoja wao.Tena mimi naanza na watumishi wa wilaya ya mkuranga mkoa wa pwani,hasa walimu wa shule za msingi na sekondari hado leo naandika ujumbe huu hatujalipwa areas zetu,tangu tupande daraja 2011 hatujalipwa areas zetu na mimi nikiwa mmoja wao.

Yaani wewe Mkuu unadai ulipwe areas tu mambo yanakwisha? Unataka upewe areas uanze KILIMO cha mananasi? Sasa hiyo halmashauri imeshindwa nini kuwapeni hayo maeneo ya kulima?
 
Rais magufuli amwagiza balozi mahiga kutatua mzozo wa Burundi.huu ni mthn wa kwanza kwa waziri huyo.chanzo mwananchi.
 
Burundi inahitaji "Military diplomacy" sio hadithi na ngonjere; AU iunde kikosi maalumu cha jeshi kiingie Burundi mara moja na kumuadabisha yule kichwa maji Nkurunzinza mithili ya operesheni ya Comoro.



Rais magufuli amwagiza balozi mahiga kutatua mzozo wa Burundi.huu ni mthn wa kwanza kwa waziri huyo.chanzo mwananchi.
 
Hakuna mtihani hapo Balozi mahiga ana uzoefu wa kutosha katika masuala ya kidiplomasia.kama utakumbuka mara ya mwisho alikuwa mjumbe maalum wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa kushughulikia matatizo ya Somalia.
 
wanajamvi;
Nakubali wote waliojenga maeneo yasiyofaa wabomolewe.

Ila hoja yangu ni tusiishie hapo tu, twende hata ktk nyanja nyingine tofauti. Magufuli awafikie watumishi.
Kama mtumishi uliwahi kula 10% yoyote ktk utumishi wako, yaani uliwahi kufanya ubadhirifu wa mali ya umma, ulikuwa mpokea rushwa, ulifisadi kwa namna yeyote huko nyuma iwe enzi za Mwinyi, Mkapa na Kikwete, wewe na waliokuwa wanajenga kiholela kuvunja kwenu sheria ni sawa. Mali zote walizo nazo tutapenda zithamanishwe na zilinganishwe na kipato chao halali vinginevyo zitaifishwe tu. Kwa hapa naomba ng'ombe, ardhi, mbuga nk navyo vizingatiwe please. Kama umewahi kutumia muda wa kazi vibaya kwa kuchelewa, hata kwa kuchat we jipeleke kwa mkuu wako tu uwajibishwe, ikiwa una ndugu alitumia cheti kisicho chake toa taarifa nk nk maana hakuna namna nyingine. Tanzania tumeamua kuwa watakatifu.
 
Sijui kama kuna mdau kesha weka humu? Mimi naomba atengue ule uteuzi wa balozi wa heshima wa ufisadi wa Guangzou. Halafu afuatilie unyayo kwa unyayo shughuli za makampuni yake huyo Balozi na washirika wake. HAPA KAZI TU.
 
naomba nitumie uhuru wangu wa kujieleza kuwasilisha maoni yangu kuhusu njia madhubuti za kudhibiti wizi wa fedha na mali za umma 1 kukwepa kodi kodi liwe kosa lisilo na dhamana wala msamaha 2 mtumishi atakaesaidia upotevu wa kodi afutwe kazi na kufungwa si chini ya miaka 30 jela 3 lianzishwe dirisha la hamasa ya kulipa kodi ambapo serikali itatoa motisha kwa wanunuaji wenye risiti halali 4 mtu aliepewa kusimamia shirika la umma asipotengeneza faida ajira yake isitishwa
 
Rais Magufuli nabaki nikisubiri kwa hamu zote kuvunja bodi ya kahawa nchini.

Nasikitika sana kahawa yetu kule kiraracha na kibosho zikielekea ukingoni na kubaki historia naamini zao hili lilikuwa muhimu mpaka kufanya mwananchi kujikwamua kwa umaskini nashangaa bei ya kahawa inabaki 2000@ kg wakati kahawa yetu ni moja ya brand nzuri ya kahawa katika soko la dunia hivi kuwepo kwa mashirika kama TACRI niulize huu utafiti wao ni wa kuua zao hili la kahawa cha kushangaza kuna ufisadi wa hali ya juu pale KNCU wananchi wamekata tamaa kahawa inakufa taratibu majengo ya KNCU yamebaki ni ya vikao na vilabu vya mbege.

Ewe Rais nusuru zao hili mikononi mwa hawa walanguzi na mafisadi.

Kahawa 2000 kwa kg? Halafu nje inauzwa zaidi ya elfu kumi

Cc waziri kilimo Mwigulu Nchemba.

By gilbert massawe
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom