Status
Not open for further replies.
Habari za jioni wanajukwaa la siasa.
Baada ya malalamiko mengi kuhusu serikali pendwa ya Raisi ,jemedari wa vita , mtu wa Mungu , na mpambanaji JPM.

Leo najibu maswali na kupokea changamoto za utawala wetu pendwa chini ya Raisi mpendwa JPM, kama una maoni , maswali na hasira zako nipo tayari kukujibia .
Karibuni kuijenga taifa letu , karibu kuinua Tanzania yetu.
 
Mheshimiwa Rais Magufuli, unaweza ukawa huambiwi na wasaidizi wako lakini amini usiamini; ukweli japo unaweza kuwa ni mchungu kwako ni kuwa HAUTAFANIKIWA kwenye yote uyafanyayo (japo mtu akikusikiliza anaweza kuona nia uliyonayo ya kuleta mabadiliko). Sababu kuu ni hii:

Mfumo wa elimu uliopo nchini hauzalishi aina ya wahitimu wanaohitajika ku-support unachotaka kukiona kikitendeka.

Rais Magufuli umezungukwa na wanafiki ambao lengo lao kuu ni maslahi yao binafsi. Wanajua kuwa unapenda kusifiwa na wakikusifia utawa-reward. Naomba utafakari wale uliowatumbua mwanzoni kabisa mwa utawala wako (kwa mfano mwalimu wangu Likwelile); utaona walikuwa na character ile ile MOJA tu. Walipata ujasiri wa kukuambia UKWELI waliokuwa wanauamini. Bado una nafasi (japo inazidi kupungua) ya kurekebisha mambo.
Mungu Jehovah aonae yaliyo sirini akuongoze.
 
Habari za jioni wanajukwaa la siasa.
Baada ya malalamiko mengi kuhusu serikali pendwa ya Raisi ,jemedari wa vita , mtu wa Mungu , na mpambanaji JPM.

Leo najibu maswali na kupokea changamoto za utawala wetu pendwa chini ya Raisi mpendwa JPM, kama una maoni , maswali na hasira zako nipo tayari kukujibia .
Karibuni kuijenga taifa letu , karibu kuinua Tanzania yetu.

Hayo mamlaka ya kujinasibu kufanya uliyoyaandika hapa umeyapata wapi?
 
I'd like start this short opinion piece by quoting the great Maya Angelou who once said "I did then what I knew how to do. Now that I know better, I do better".

In the last few years, we have witnessed some outstanding changes in the way the country is being run. These changes are still sending shockwaves and aftershocks to every corner of the country. But what I want to touch on today is the outlook or frame of mind that's driving these changes.

I am not going to say whether the President means well because at the end of the day that may not really matter. There is a proverb that says that "the road to hell is paved with good intentions" or that "hell is full of good meanings but heaven is full of good works." In other words, his so-called good intentions can be the very catalyst for evil to flourish in the land, and there are some indications that this has already taken root.

After carefully examining the recent deliberations about the order, presented as an advice, to release those who are behind bars for unbeilable economic sabotage and money laundering charges if they confess and also pay back what they are accused of owing the government, what I have concluded without any reasonable doubt is that unfortunately our President doesn't have even the elementary grasp of the rule of law. We might be blaming him for something that possibly he just doesn't get.

How would you describe his 'wish' to have a country without prisons or prisoners? We call that lawlessness, disorder and anarchy.

Now you mix that with some element of being a pathological liar, arrogance that's out of this world and a deep-seated and inborn habit of showing vengeance to his enemies, we could be having a much bigger problem than we initially thought.

What we have is a classic case of a clear and present danger. The former president of USA, John F. Kennedy said it best. In one of his speeches many years ago, he argued that:

"For we are opposed around the world by a monolithic and ruthless conspiracy that relies primarily on covert means for expanding its sphere of influence--on infiltration instead of invasion, on subversion instead of elections, on intimidation instead of free choice, on guerrillas by night instead of armies by day. It is a system which has conscripted vast human and material resources into the building of a tightly knit, highly efficient machine that combines military, diplomatic, intelligence, economic, scientific and political operations".

Substitute 'around the world' to 'around the country' and you will have a recap of what the country is facing at the moment.
 

Rais Magufuli waachie hawa watu. Watakufia katika uongozi wako. Itakuwa dosari kwako.

Maovu waliyo yafanya ni kwa sababu mfumo uliruhusu. Kama mfumo usingeruhusu wasingepata nafasi ya kutenda waliyo yatenda. Kama rushwa ndiyo tatizo, basi watanzania karibu wote tulihusika ikiwemo na wewe pia japo kuwa sio direct bali indirekt. Na wahusika wakubwa zaidi ni viongozi wa juu kama wewe na hao wanaendelea kula bata.

Sioni kama ni haki ya watu kama akina Kinana na Nape ambao, mbali na hujuma, walikusudia kukupindua wewe pia, lakini wao unawaacha free kwa kisingizio wametubu. Basi wape na wao nafasi ya kutubu.

Rais Magufuli wewe pia unamakosa, kwani kwa watu kama akina Kinana, Nape na Januari Makamba ulikuwa mnafiki. Ulijua maovu yao, lakini hata hivyo uliwang'ang'ania wawe madarakani kwa kujaribu kuwa protect. Jitihada zako zote Mungu wako naye kakusuta. Kila mmoja ana makosa.

Kama hii mijitu uliyo ikingia kifua iko free, kwa nini usiwaache na hawa wakawa free poa? Wote walikuwa kwenye meli moja.

Piga mstari na kusema mpaka hapa ni mwisho. Watakao endelea na uujumu uchumi hao sasa wapewe hadhabu kali.

Chukua mfano wa Nelson Mandela aliye wasamehe Makaburu walio msweka mpaka jela kwa kosa la kutetea haki zake!
 
Habari za mchana wana jukwaa!

Nikiri wazi tu,nimepokea kwa mashaka taarifa za watuhumiwa wanaoshtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi, kuwa tayari kulipa kiasi kinachofikia shilingi bilioni 107 za kitanzania. Kusema wanaotuhumiwa kuchukua pesa na wako tayari kuzirudisha upo tayari kuwasamehe ninajiuliza maswali kadhaa;

● Je, ni wote walioshtakiwa/kukamatwa kwa hilo kosa wana hatia?

● Je, kwa wale wasio na hatia na hawana cha kulipa wao wataendelea kusota rumande mpaka lini?

WanaJukwaa, ninayaandika haya kwa sababu siku hizi kumejengeka dhana kwamba hili kosa linatumika kuwakomoa wabaya wa serikali kwa kuwapachika kosa la uhujumu uchumi ili kuwafunga midomo, kwa kuwasweka rumande kwa sababu hilo kosa halina dhamana. Na tumeona ni jinsi gani upande wa jamhuri/ upelelezi wameshindwa kuwa na ushahidi wa moja kwa moja na wa haraka dhidi ya hao wanaotuhumiwa, matokeo yake wapo waliokaa rumande yapata mwaka wa pili au wa tatu sasa. Kwa upande wangu,hilo nalo naliona haliko sawa, kwani ni wazi hawa watuhumiwa wananyimwa haki yao ya kuwa uraiani na kuungana na familia zao, na marafiki wao.

■ KWANINI HILI KOSA LA UHUJUMU UCHUMI HALINA DHAMANA?

■KWANINI TENA HIZI KESI ZA UHUJUMU UCHUMI ZINACHUKUA MUDA MREFU SANA KUSIKILIZWA NA HATIMAYE KUTOLEWA HUKUMU?

Wana jukwaa,hayo hapo juu ni maswali yanayonipasua kichwa kila nikifikiria kuhusu hizi kesi, tujiulize, ni wangapi kati ya wote waliokamatwa kwa hilo kosa wameshahukumiwa, kulinganisha na wale ambao wanaendelea kusota magerezani hapa nchini kisa tu upelelezi wa kesi dhidi yao bado haujakamilika?

Naomba nieleweke wazi, siwatetei na wala sitaki huruma ya aina yoyote kwa wote walioliibia hili taifa wakati wa tawala zilizopita, na hii taarifa ya leo kwamba wapo tayari kurudisha Tshs bilioni 107 ni njema sana kwangu. Ninachotaka nieleweke vizuri hapa ni vipi kuhusu wale waliokamatwa miaka miwili mpaka mitatu iliyopita, wanaona wameonewa kwa kupewa hizo kesi, na kesi zao zinaendelea kuahirishwa kila siku mahakamani na hawana pesa za kulipa ili tu nao wawe huru, kwa sababu ninaamini hakuna anaependa kukaa gerezani, au ni kwamba wote walioko magerezani wakituhumiwa kwa hilo kosa wana hatia?!

HITIMISHO.

Mheshimiwa Rais, umekuwa ni muumini mkubwa sana wa kutaka haki itendeke kwa raia wako, hivyo basi, kwa nafasi yako nikuombe uziamuru idara zote zinazohusika na usikilizwaji wa hizi kesi, kuanzia upelelezi mpaka mahakamani, waharakishe ili kuwasaidia wale wote wanaoshtakiwa kwa hili kosa lisilo na dhamana. Hii itasaidia sana kuondoa dhana inayoanza kujengeka kwamba hili kosa lipo kwa ajili ya kuwakomoa wanaoonekana kuwa wabaya wa serikali yako, na hivyo kuzidisha imani ya serikali yako kwa watanzania.

Wasalaam!
 
Jamani tupunguze lawama maana yapo maamuzi Rais anafanya il nyuma yan siri nzito sana na hawez kuanza tusimulia. Hivyo tujifunze kufunga midomo tuache serikal ifanye kaz yake. Hiz kelele ni dalili ya taifa lililo jaa wanafiki na watu wasiofikiri.
Kama yapi?
 
Jamani tupunguze lawama maana yapo maamuzi Rais anafanya il nyuma yan siri nzito sana na hawez kuanza tusimulia. Hivyo tujifunze kufunga midomo tuache serikal ifanye kaz yake. Hiz kelele ni dalili ya taifa lililo jaa wanafiki na watu wasiofikiri.
Rubbish.
 
Jamani tupunguze lawama maana yapo maamuzi Rais anafanya il nyuma yan siri nzito sana na hawez kuanza tusimulia. Hivyo tujifunze kufunga midomo tuache serikal ifanye kaz yake. Hiz kelele ni dalili ya taifa lililo jaa wanafiki na watu wasiofikiri.
Labda kama hiyo siri ni wizi na dhuluma. Kila mwenye akili timamu atang'amua hilo, wala sio siri.
 
Jamani tupunguze lawama maana yapo maamuzi Rais anafanya il nyuma yan siri nzito sana na hawez kuanza tusimulia. Hivyo tujifunze kufunga midomo tuache serikal ifanye kaz yake. Hiz kelele ni dalili ya taifa lililo jaa wanafiki na watu wasiofikiri.

Sheria ziko wazi, azifuate maana yeye ni bingwa wa kusisitiza wengine wafuate. Hata sisi wengine tuna mambo mazuri tunataka kufanya lakini sheria ndio zinakuwa kikwazo. Isitoshe tulishatoka kwenye dunia ya uongozi mtu na tuko kwenye dunia ya uongozi taasisi, ambapo sheria ndio huongoza na sio hisia za kiongozi.
 
Jamani tupunguze lawama maana yapo maamuzi Rais anafanya il nyuma yan siri nzito sana na hawez kuanza tusimulia. Hivyo tujifunze kufunga midomo tuache serikal ifanye kaz yake. Hiz kelele ni dalili ya taifa lililo jaa wanafiki na watu wasiofikiri.
Mfano hili jambo la kutubu siri aliyokuwa nayo ilikuwa Rugemalira na Singasinga WATUBU..apige Bilioni zile..
Sasa ndio WAMEGOMA..!! Teh Teh Teh Kwi Kwi Kwi...
Rais wa ovyo haijapata kutokea.
 
Jamani tupunguze lawama maana yapo maamuzi Rais anafanya il nyuma yan siri nzito sana na hawez kuanza tusimulia. Hivyo tujifunze kufunga midomo tuache serikal ifanye kaz yake. Hiz kelele ni dalili ya taifa lililo jaa wanafiki na watu wasiofikiri.
Kama wewe umeyajua basi sio siri tena
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom