Mtukufu Rais wa Nchi ya Maziwa na Asali, Ulipochukua madaraka, ulituonya kwamba utawashusha wanaoishi kama mailaika kuishi kama mashetani. Hakika utabiri wako umetimia.
Mr. Kamu.......Ni afisa wa kati wizara ya mifugo. Alipanga nyumba mbezi makonde ambako pia alipaki gari zake mbili za kifahari, Harrier na Mark X, Kila siku asubuhi alichukuliwa na pia kurudishwa jioni kifaharai na gari la walipa kodi almaarufu kama V8 mpya.
Bwana huyu alikuwa na safari nyingi sana ndani na nje ya nchi hadi sisi tukamuona kama kigogo mzito. Watoto wake watatu kati ya wanne walikuwa wakisoma shule za bweni. Ghafla bin vuu, bwana huyu maisha yamebadilika, tena kwa kasi ya ajabu.
Watoto wote watatu wamerudi nyumbani na sasa wanasoma St. Kayumba. Mbezi Makonde kapahama, amehamia kenye nyumba yake eneo la Madale. Nyumba yenyewe inatia huruma, kwani limeezekwa robo tu. Chumba kimoja, jiko na Sebule. Kwingine kote kuko wazi. Kwa hiyo watoto wote, mama mtu na dada wa kazi wanalala sebuleni. Mtu na mkewe na chumba chao. Magari yao mawili yote yameuzwa. Maisha yamekuwa ya kishetani.
Safari za nje, marupurupu, kwisha habari. Ni maisha ya kubanana. Gari la kifahari bado linakuja Madale kumchukua bosi mwenye msongo wa mawazo. Hatujui huko kazini kazi zinafanyikaje. Hatujui hawa ndio wale wanaosaidia maadui wa nchi kulihujumu taifa au la, maana wazi kabisa wanaonyesha kutokuridhika na maisha wanayoyaishi.
Hali imekuwa mbaya hasa ukiangalia watu wanavyoangukia kwenye maisha ya kishetani. Baba legezma