Mkuu, rais nijuavyo ndie husimamia system yote, na kibongobongo anamamlaka hakuna mfano wake, sasa kama anajua yote hayo anashindwaje kusema iwe na ikawa?
je kuna mtu mwingine mwenye mamlaka makubwa zaidi nyuma ya raisi ambaye humpangia kipi afanye na lipi aache?
Au mioyo yao ni migumu kama jiwe,
isiyitaka mabadiliko mapya?
Tatizo unaloliongelea wewe hapo ni sawa na alivyofikiri huyo rafiki yangu.
Alifikiri ukimuonesha rais tu kitu sahihi cha kufanya, anaweza kuamrisha kila mtu afanye hivyo na mengine yote yakanyooka.
Watu wengi wana assumptions hizi chini, assumptions ambazo si lazima ziwe sahihi.
Assumptions hizo ni kwamba.
1. Assumption- Rais ana nia nzuri kwa maendeleo ya nchi.
Hili si lazima liwe kweli. Maendeleo ya nchi yanaweza kumaanisha watu wataelimika zaidi na watawala watashindwa kuwatawala watu kwa mtaji wa ujinga wao. Sasa hapo, rais akiwa na maamuzi ya ama awape watu uwezo wa kupata elimu na kujielewa, halafu watu hao wakipata kujielewa na elimu mara moja wamtoe madarakani (kwa sababu ya maovu mengi yanay na yaliyofanywa naye na chama chake) au awaache watu wasipate elimu na kujielewa kweli, lakini kuwaacha watu kwenye ujinga hivyo kutamsaidia kisiasa kwa kumpa nafasi ya kufanya mazingaombwe aonekane kama anajali watu, lakini kiukweli anawaacha kwenye ujinga, viongozi wetu wengi wameamua kufanya hilo la pili, kupata urahisi wa kisiasa zaidi ya kutatua matatizo ya wananchi.Kwa sababu historia imeonesha kila sehemu ambayo watu wameinuka kutoka umasikini, ujinga na maradhi, serikali na watawala wamepata tabu kuendelea kukaa madarakani kama hakuna performance inayopanda kila mwaka.
Yani ni kwamba, ukileta maendeleo sana, kiongozi wa siasa ujitayarishe kuona watu waliowezeshwa na maendeleo hayo wanakutoa madarakani kama hujaweza kuongeza sana maendeleo kila mwaka.
Kwa msingi huu, viongozi wengi wa siasa huamua kuleta maendeleo kidogo tu yatakayoonesha wanafanya kazi, wakiogopa kuleta maendeleo sana ambayo yanaweza kuwawezesha watu kuwa huru kiasi cha kuwaondoa watawala kwenye utawala.
Ndiyo maana kuna kampuni moja ya kuchimba dhahabu ilikuja Tanzania, ikataka kuwalipa Watanzania mishahara ambayo ni ya kawaida kimataifa, lakini kwa viwango vya Tanzania ni mikubwa, mawaziri wa Tanzania wakakataa hiyo mishahara na kusema ni mikubwa sana.
Yani Waziri wa nchi anakataa watu wa nchi yake wasilipwe mishahara mikubwa na wageni kutoka nje wanaowekeza kwenye kuchimba dhahabu!
Huo ni mfano mmoja mdogo tu unaoonesha kwamba hii dhana nzima kamba watawala wana nia nzuri ya kufanya maisha ya wananchi yawe bora kabisa, ni dhana iliyojaa propaganda za kisiasa kuliko vinginevyo.
2. Assumption - Rais ana uwezo wote.
Rais wa Tanzania ana nguvu sana, hili ni kweli. lakini hilo halimaanishi ana uwezo wote.Kuna watu wamefanya deal naye tangu hajawa rais wana faili lake, kuna wanaojua michepuko yake, kuna mambo mengi sana hatuyajui, especially kipindi cha Kikwete nilichokizungumzia, kujenga consensus ilikuwa kazi sana, na Kikwete alikuwa anafuatilia mambo, mengine anapotezea anasema mtajiju. Hata leo, rais ana amepewa nguvu sana, na kumpa nguvu sana kumefanya urais uwe na udhaifu.Rais huyo huyo ni Mwenyekiti wa CCM. Mambo mengine ukifanya vizuri serikalini yakaleta maendeleo yanahatarisha umaarufu wa CCM. Hapo kuna conflict. Tushaona rais hayuko popular miongoni mwa viongozi kama watu wengi walivyofikiri, na kuna watu wanapewa maagizo hawayatekelezi, na rais ana mambo kibao kufuatilia kila kitu vigumu.Maneno mengine anasema kwa ukali kisiasa tu aonekane mkali, lakini hata yeye mwenyewe ufuatiliaji hawezi, especially kwa sababu anataka kila kitu afanye mwenyewe.
Magufuli na ukali wake wote bado watu wanamchenga sana serikalini, wanakula rushwa, wanapiga hela, hawatekelezi maagizo, wanavuruga mipango yake, etc. Kwa hiyo ingawa kapewa nguvu sana katika mfumo rasmi, katika mfumo halisi anategemea sana watu wengine .
3. Assumption- Rais ana right views.
Rais mjuaji anaweza akawa ana contrarian views. Ana makabrasha yote, ana studies zote, lakini yeye anajiona anajua kuliko wasomi na anapingana nao na hataki kufanya walivyomuelekeza anafanya anavyotaka yeye. Mfano mzuri ni kesi ya mtu anaitwa Lawrence Mafuru. Jamaa ni well respected banker mpaka London Charter of Bankers wanamtambua. Alikuwa Msajili wa Hazina. Magufuli alimwambia atoe fedha zote za serikali benki za\ote azipeleke Benki Kuu, Mafuru akamwambia mheshimiwa naelewa unataka kubana ubadhirifu, lakini unachoshauri hapo ni sawa na kutaka lori kubwa ligeuke mara moja kwa kufunga breki kali.Unaweza kusababisha ajali. Tufanye hii kazi kwa polepole, kwa awamu.Tutafikia lengo lile lile, lakini hatutautikisa uchumi kwa mara moja, tufanye kama gari linapunguza mwendo taratibu, halafu linapinda kona na kurudi lilikotoka, unaepusha ajali.
Magufuli akakasirika sana kuambiwa vile, akaona kama jamaa kamsahihisha wakati yeye anajua kila kitu. Akamfukuza kazi Mafuru kwa style ya "atapangiwa kazi nyingine" (style inayoligharimu sana taifa, mtu analipwa mshahara bila kufanya kazi). Mafuru alishauri vizuri tu, kitaalamu, akasema Magufuli akifanya anavyotaka mzunguko wa fedha utaminywa sana na hali itakuwa ngumu sana mtaani. Magufuli hakumsikiliza, akafanya kivyake alichotaka. Matokeo yake mzunguko wa fedha umepata kudhoofika vibaya sana kama alivyotabiri Mafuru na biashara zinadorora.
Ukiangalia sakata la bei ya korosho lilivyoenda, utaona kwamba hata kama rais alikuwa na nia nzuri, hakuwa na mtazamo mzuri na execution plan yake imefail vibaya sana.
Yote haya yanaonesha nguvu za rais hazisaidii kitu kama.
1. Rais hana nia nzuri.
2. Rais hana ushirikiano wa wengine.
3. Rais hana execution plan nzuri.