Status
Not open for further replies.
Umshauri MTU anayejua kila kitu ,aliyesoma kombi zote ,jiniasi utamshauri vipi ?

Keshaanza kuona ukweli kwa vitendo. Sakata la korosho peke yake linatosha kumfanya ajue kuwa anadanganywa kila siku na pia si kila anachokifanya kina matokeo chanya. NHC sasa hivi ni disaster waiting to happen - well, alilikuta hilo la NHC lakini haonekani kuchukua hatua yeyote. NHC itaondoka na mabenki, watch this space.
 
Taifa : Kuwa Taifa tunahitaji umoja , upendo, amani na mshikamano. Tusikubali itikadi za kidini, kikabila au kichama kutugawa. Mh. Rais John Pombe Magufuli anatakiwa kurudisha uzalendo na mapenzi ya wananchi dhidi ya Nchi hii.
 
Namshairi aendelee kuchapa kazi #HapaKaziTu
Rais Dr. John Joseph Pombe Magufuli hakushuka Tanzania kama Malaika akawa muarobaini wa nchi hii, ni binadamu ambaye makosa ni sehemu ya utendaji, korosho ni jambo geni ambalo limeleta mkanganyo katika maamuzi yake, lakini Watanzania tushirikiane kutafuta jinsi ya kumaliza sakata hata kushauri Serikali iuze hata kwa nusu ya Bei iliyokusudiwa kwani ni afadhali nusu hasara kuliko hasara kamili, lakini Serikali imepata fundisho kuhusu korosho badala ya kumlenga na kumkejeli Dr. John Magufuli wakati anapambana ili kuokoa hali hiyo.
 
Ya kwangu naelekeza kwa idara ya uhamiaji. Naamini Serikali itakuwa imegharimia fedha za kutosha kuwa na mfumo uliopo wa maombi ya pasi za kusafiria.
Mtu anapotoa maombi anaweka namba zake za simu, na ukiangalia ule mfumo unatoa mwanya wa kufiluatilia hatua ya maombi ya pasi ilipofikia, lakini cha kusikitisha hicho kisehemu hakifanyi kazi.
Ukiamia upande mwingine, pamoja na mwanachi kutoa namba ya simu, inamlazimu kwenda kurundikana ofisi za uhamiaji kuulizia kama pasi yake ipo tayari.

Mapendekezo
Watu wa mifumo wa idara waweze sehemu ya ufuatiliaji wa hati ufanyike online. Ili baafa ya mwananchi kuwa amekwisha kamilisha maombi yake na kufanya malipo aweze kuona hatua iliyopo mpaka siku inapokuwa imekamilika

Simu za waananchi zinazowekwa kwenye maombi zitumike kuwajulisha siku ya kwenda kuchukua pasi na watengewe muda badala ya watu kwenda kukusanyika kwenye ofisi za uhamiaji. Manufaa ya hili pendekezo
a) Itapunguza misongomano isiyo ya lazima ktk ofisi za uhamiaji
b) Maofisa uhamiaji watakuwa na muda wa kutosheleza bila kuwa na mwingiliano kutimiza majukumi mengine
c) Wananchi watakuwa na muda mfupi wa kukaa ofisi za uhamiaji kwa ajili ya kuhudumiwa na hivyo muda mwingine watautumia katika shughuli zao za uzalishaji iwe ni ktk biashara, maofisini, hospitalini, viwandani, ktk kutoa ushauri nk.

Wanaomsaidia Rais ktk eneo hili walitupiye macho ili kuboresha kwa manufaa ya taifa.
 
YAH: kichwa cha habari tajwa hapo juu☝️
Wanasema samaki ana mengi na hata siri za kuteta ila......ndio tatizo.
Hebu turudi kwenye mada husika, hivi ikitokea siku ya leo ukakutana uso kwa uso na rais wa awamu ya tano wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshiwa J.P Magufuli je ni swali lipi ungependa kumuuliza!? Au ni jambo lipi ungependa kumwambia!?
#Amoun.
 
Nitamwambia tunataka serikali yake, ijenge barabara kwa ajili ya utalii ukanda wa bahari,hata km 50 tu
 
YAH: kichwa cha habari tajwa hapo juu☝
Wanasema samaki ana mengi na hata siri za kuteta ila......ndio tatizo.
Hebu turudi kwenye mada husika, hivi ikitokea siku ya leo ukakutana uso kwa uso na rais wa awamu ya tano wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshiwa J.P Magufuli je ni swali lipi ungependa kumuuliza!? Au ni jambo lipi ungependa kumwambia!?
#Amoun.
alipofanya hadi sasa panatosha - ampishe mwengine 2020.

hilo tu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom