Status
Not open for further replies.
Unaandika hutaji lolote.. huna la kuandika juu ya unachomuomba.. hata miaka mitano 5 unalalamika shwiiiiiiii

Unaonesha unauchungu na nchi hii unahitaji taifa lisonge mbele tunakupongeza kwa jitihada unazoendelea kuzichukua kuboresha miundombinu lakini kuna mambo madogo inabidi uyafanyie kazi ili wananchi waendelee kukuunga mkono juhudi zako kuna watu wanasema wanahitaji democrasia ni jambo zuri lakini kwa mawazo yangu mimi tanzania Tunahitaji rais mkweli na muwazi kama nyerere ambaye alikuwa anakubali kabisa kuna mambo amefanikiwa nakuna mengine amekosea kipindi cha uongozi wake tofaut na uongoz wa sasa kuna mambo mengi watu wanabolonga lakini wamekuwa wanataka sifa
 
Ningeanza kwa kumsalimia, "mzee mwangaluka? Mzee umefanya mengi sana ya kufurahisha na kukarahisha lakini ndio ubinadamu huo."
Nikaendelea, "sasa mzee nakushauri sana tuu, mwakani usichukue fomu za chama maana huyu Membe na wenzake watakuaibisha kabisa maana wamejipanga. Wewe singizia ugonjwa au vyovyote ili waachie kiti chao aibu ya nini?"
 
Nitamwambia "Shkamoo Mr Jiwe. Kwanini biashara zimekuwa doro sana mtaani?, na kwanini akina Membe, Nape, Makamba, wastaafu, nk hawatekwi kama wapinzani? Au CCM wana kinga dhidi ya kutekwa hata wakifanya uhaini?"
 
Aangalie mwenendo na maamuzi yake dhidi ya watumishi.

Asijidai anajenga sehemu huku upande mwingine kunabomolewa tena Kwa speed kubwa.

Tafakari
 
Hata Mimi nitamuunga mkono kama 2020 ataamua kupumzika siasa na kuwaachia wengine kwa moyo mweupe.
Kazi aliyoifanya inatosha, miaka 20 ya Ubunge na 5 ya Urais inatosha kabisa kwa vile hii minne ya mwisho taifa nimegubikwa na kukosa furaha na kujaa woga kama tuko Afghanistan kumbe tuko nchi aliyoikuta na amani.
Hicho kitakuwa kitendo cha kishujaa sana na heshima kuliko kusubiri kina Membe waje wamgaragaze pale Dodoma kwa aibu.
Umeanza vizuri kuchangia ila sijui umeishia wapi
 
Mkuu, rais nijuavyo ndie husimamia system yote, na kibongobongo anamamlaka hakuna mfano wake, sasa kama anajua yote hayo anashindwaje kusema iwe na ikawa?
je kuna mtu mwingine mwenye mamlaka makubwa zaidi nyuma ya raisi ambaye humpangia kipi afanye na lipi aache?
Au mioyo yao ni migumu kama jiwe,
isiyitaka mabadiliko mapya?
Tatizo unaloliongelea wewe hapo ni sawa na alivyofikiri huyo rafiki yangu.

Alifikiri ukimuonesha rais tu kitu sahihi cha kufanya, anaweza kuamrisha kila mtu afanye hivyo na mengine yote yakanyooka.

Watu wengi wana assumptions hizi chini, assumptions ambazo si lazima ziwe sahihi.

Assumptions hizo ni kwamba.

1. Assumption- Rais ana nia nzuri kwa maendeleo ya nchi.

Hili si lazima liwe kweli. Maendeleo ya nchi yanaweza kumaanisha watu wataelimika zaidi na watawala watashindwa kuwatawala watu kwa mtaji wa ujinga wao. Sasa hapo, rais akiwa na maamuzi ya ama awape watu uwezo wa kupata elimu na kujielewa, halafu watu hao wakipata kujielewa na elimu mara moja wamtoe madarakani (kwa sababu ya maovu mengi yanay na yaliyofanywa naye na chama chake) au awaache watu wasipate elimu na kujielewa kweli, lakini kuwaacha watu kwenye ujinga hivyo kutamsaidia kisiasa kwa kumpa nafasi ya kufanya mazingaombwe aonekane kama anajali watu, lakini kiukweli anawaacha kwenye ujinga, viongozi wetu wengi wameamua kufanya hilo la pili, kupata urahisi wa kisiasa zaidi ya kutatua matatizo ya wananchi.Kwa sababu historia imeonesha kila sehemu ambayo watu wameinuka kutoka umasikini, ujinga na maradhi, serikali na watawala wamepata tabu kuendelea kukaa madarakani kama hakuna performance inayopanda kila mwaka.

Yani ni kwamba, ukileta maendeleo sana, kiongozi wa siasa ujitayarishe kuona watu waliowezeshwa na maendeleo hayo wanakutoa madarakani kama hujaweza kuongeza sana maendeleo kila mwaka.

Kwa msingi huu, viongozi wengi wa siasa huamua kuleta maendeleo kidogo tu yatakayoonesha wanafanya kazi, wakiogopa kuleta maendeleo sana ambayo yanaweza kuwawezesha watu kuwa huru kiasi cha kuwaondoa watawala kwenye utawala.

Ndiyo maana kuna kampuni moja ya kuchimba dhahabu ilikuja Tanzania, ikataka kuwalipa Watanzania mishahara ambayo ni ya kawaida kimataifa, lakini kwa viwango vya Tanzania ni mikubwa, mawaziri wa Tanzania wakakataa hiyo mishahara na kusema ni mikubwa sana.

Yani Waziri wa nchi anakataa watu wa nchi yake wasilipwe mishahara mikubwa na wageni kutoka nje wanaowekeza kwenye kuchimba dhahabu!

Huo ni mfano mmoja mdogo tu unaoonesha kwamba hii dhana nzima kamba watawala wana nia nzuri ya kufanya maisha ya wananchi yawe bora kabisa, ni dhana iliyojaa propaganda za kisiasa kuliko vinginevyo.

2. Assumption - Rais ana uwezo wote.

Rais wa Tanzania ana nguvu sana, hili ni kweli. lakini hilo halimaanishi ana uwezo wote.Kuna watu wamefanya deal naye tangu hajawa rais wana faili lake, kuna wanaojua michepuko yake, kuna mambo mengi sana hatuyajui, especially kipindi cha Kikwete nilichokizungumzia, kujenga consensus ilikuwa kazi sana, na Kikwete alikuwa anafuatilia mambo, mengine anapotezea anasema mtajiju. Hata leo, rais ana amepewa nguvu sana, na kumpa nguvu sana kumefanya urais uwe na udhaifu.Rais huyo huyo ni Mwenyekiti wa CCM. Mambo mengine ukifanya vizuri serikalini yakaleta maendeleo yanahatarisha umaarufu wa CCM. Hapo kuna conflict. Tushaona rais hayuko popular miongoni mwa viongozi kama watu wengi walivyofikiri, na kuna watu wanapewa maagizo hawayatekelezi, na rais ana mambo kibao kufuatilia kila kitu vigumu.Maneno mengine anasema kwa ukali kisiasa tu aonekane mkali, lakini hata yeye mwenyewe ufuatiliaji hawezi, especially kwa sababu anataka kila kitu afanye mwenyewe.

Magufuli na ukali wake wote bado watu wanamchenga sana serikalini, wanakula rushwa, wanapiga hela, hawatekelezi maagizo, wanavuruga mipango yake, etc. Kwa hiyo ingawa kapewa nguvu sana katika mfumo rasmi, katika mfumo halisi anategemea sana watu wengine .

3. Assumption- Rais ana right views.

Rais mjuaji anaweza akawa ana contrarian views. Ana makabrasha yote, ana studies zote, lakini yeye anajiona anajua kuliko wasomi na anapingana nao na hataki kufanya walivyomuelekeza anafanya anavyotaka yeye. Mfano mzuri ni kesi ya mtu anaitwa Lawrence Mafuru. Jamaa ni well respected banker mpaka London Charter of Bankers wanamtambua. Alikuwa Msajili wa Hazina. Magufuli alimwambia atoe fedha zote za serikali benki za\ote azipeleke Benki Kuu, Mafuru akamwambia mheshimiwa naelewa unataka kubana ubadhirifu, lakini unachoshauri hapo ni sawa na kutaka lori kubwa ligeuke mara moja kwa kufunga breki kali.Unaweza kusababisha ajali. Tufanye hii kazi kwa polepole, kwa awamu.Tutafikia lengo lile lile, lakini hatutautikisa uchumi kwa mara moja, tufanye kama gari linapunguza mwendo taratibu, halafu linapinda kona na kurudi lilikotoka, unaepusha ajali.

Magufuli akakasirika sana kuambiwa vile, akaona kama jamaa kamsahihisha wakati yeye anajua kila kitu. Akamfukuza kazi Mafuru kwa style ya "atapangiwa kazi nyingine" (style inayoligharimu sana taifa, mtu analipwa mshahara bila kufanya kazi). Mafuru alishauri vizuri tu, kitaalamu, akasema Magufuli akifanya anavyotaka mzunguko wa fedha utaminywa sana na hali itakuwa ngumu sana mtaani. Magufuli hakumsikiliza, akafanya kivyake alichotaka. Matokeo yake mzunguko wa fedha umepata kudhoofika vibaya sana kama alivyotabiri Mafuru na biashara zinadorora.

Ukiangalia sakata la bei ya korosho lilivyoenda, utaona kwamba hata kama rais alikuwa na nia nzuri, hakuwa na mtazamo mzuri na execution plan yake imefail vibaya sana.

Yote haya yanaonesha nguvu za rais hazisaidii kitu kama.

1. Rais hana nia nzuri.
2. Rais hana ushirikiano wa wengine.
3. Rais hana execution plan nzuri.
 
1)Nitamuuliza snipers wa Kibongo wanapata wapi mafunzo? Je ni kawaida 38 kummiminia mtu mmoja na aka'survive? Au wale waliotuwakilisha Dodoma kwenye zoezi la kudili na Msingida walitokea kwa Mr Slim?
2)Zile trillion zetu kuna siku zitatolewa maelezo zilipoyeyukia?
3)Tumezoea kusikia serikali ya Kenya,serikali ya Marekani na kadhalika, inakuwaje hii yetu inatwa serikali yako kwa kukutaja jina? Je hii serikali ni private property yako?
4)Neno uhaini limebadilishwa maana mwaka gani? Inakuwaje siku hizi mtu akiwa na mawazo tofauti na ya kwako anaitwa mhaini? So uhaini ni kutofautiana mawazo na mitazamo?
 
Pamoja na kutambua kua una majukumu mengi sana kwa nafasi yako kama Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Mimi nikiwa kama mwananchi wako au mtanzania mwenzako. Napendekeza kufanyike review kwa Mashirika na taasisi zote za serikali zenye kutoa huduma katika jamii kama zinaenenda sawa sawa na kasi ya maono yako ya Tanzania ya viwanda!
Kwa maana taasisi nyingi za serikali zina ukakasi hata kama huduma itolewayo ni kwaajili ya kukuza pato la Taifa kwa maendeleo ya mtanzania. Kuna wengine wunatambua umuhimu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa lao. Lakini leo hii ukifika TRA utashangaa! Watu wana siku tatu hata wiki wanabembeleza NETWORK System inayosumbua ili tu walipie. Kumbuka wengine wanalazimika kufunga biashara zao kutokana na kwamba biashara ni changa bado haina uwezo wa kuajiri. Yote hii kwaajili ya ulipaji wa kodi tu.

Ukija kwa hawa jamaa TANESCO ndio tunashindwa kuelewa nini dhumuni la hili shirika. Kama kauli mbiu ni "TANESCO TUNAANGAZA MAISHA YAKO" wanaangaza maisha ya nani? Ikiwa watanzania wengi tunaishi gizani na si kwasababu ya kushindwa kulipia huduma zao lah! Bali kwa huduma mbovu na zisizo jali muda na nn kusudi au uwepo wa shirika lenyewe .. Mtu unajaza fomu ya maombi unakaa zaidi ya miezi mitatu hata savey hajafika. Ukifatilia unaambiwa gari haina mafuta! Sasa unajiuliza hili ni jukumu la nani kuhakikisha gari lina mafuta kwaajili ya kutoa huduma kwa wakati.. Yani bila rushwa hupati savey kwa wakati unaweza subiri hata mwaka usipate huduma. Ukilipia napo shida ipo pale pale utasikia nguzo chache mara nguzo zimeisha sasa tunajiuliza hizo nguzo ni za hisani au lah! Kumbuka katika malipo tunajumlishiwa na gharama za nguzo kama kuna ulazima wa kuwepo...
Mimi kama kijana,mtoto wako, au Mtanzania mwenzio. Pamoja na kuwa tuna utofauti wa kiitikadi wa chama bado natambua juhudi zako kama Raisi katika kuifikisha Tanzania katika uchumi wa viwanda..
Ila Tanzania ya viwanda inatakiwa ienende sawa sawa na maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Tanzania kwa ujumla.
Ila
Maendeleo bila ulipaji wa kodi wenye tija kwa taifa. Bado itakua ni ndoto

Na kodi yenye tija kwa taifa bila TRA kuleta utaratibu mzuri wa ulipaji na wenye kuzingatia viwango halisi vya kodi husika. Bado itakua ni ndoto

Na serikali bila kuangalia utaratibu mzuri wa kumaliza usumbufu wa NETWORK SYSTEM error katika taasisi zake zote. Bado itakua ni ndoto kufika uchumi wa kati

Viwanda bila umeme wa uhakika na wenye kupatikana kwa wakati bado itakua ndoto. Si kwako tu Muheshimiwa Bali kwa wote tunao amini Tanzania na viwanda inawezekana
 
Ahsante mkuu mkuu, umenena vyema,
siku moja nitakutafuta, shukurani.
Tatizo unaloliongelea wewe hapo ni sawa na alivyofikiri huyo rafiki yangu.
Alifikiri ukimuonesha rais tu kitu sahihi cha kufanya, anaweza kuamrisha kila mtu afanye hivyo na mengine yote yakanyooka.
Watu wengi wana assumptions hizi chini, assumptions ambazo si lazima ziwe sahihi.
Assumptions hizo ni kwamba.
1. Assumption- Rais ana nia nzuri kwa maendeleo ya nchi.
Hili si lazima liwe kweli. Maendeleo ya nchi yanaweza kumaanisha watu wataelimika zaidi na watawala watashindwa kuwatawala watu kwa mtaji wa ujinga wao. Sasa hapo, rais akiwa na maamuzi ya ama awape watu uwezo wa kupata elimu na kujielewa, halafu watu hao wakipata kujielewa na elimu mara moja wamtoe madarakani (kwa sababu ya maovu mengi yanay na yaliyofanywa naye na chama chake) au awaache watu wasipate elimu na kujielewa kweli, lakini kuwaacha watu kwenye ujinga hivyo kutamsaidia kisiasa kwa kumpa nafasi ya kufanya mazingaombwe aonekane kama anajali watu, lakini kiukweli anawaacha kwenye ujinga, viongozi wetu wengi wameamua kufanya hilo la pili, kupata urahisi wa kisiasa zaidi ya kutatua matatizo ya wananchi.Kwa sababu historia imeonesha kila sehemu ambayo watu wameinuka kutoka umasikini, ujinga na maradhi, serikali na watawala wamepata tabu kuendelea kukaa madarakani kama hakuna performance inayopanda kila mwaka.
Yani ni kwamba, ukileta maendeleo sana, kiongozi wa siasa ujitayarishe kuona watu waliowezeshwa na maendeleo hayo wanakutoa madarakani kama hujaweza kuongeza sana maendeleo kila mwaka.
Kwa msingi huu, viongozi wengi wa siasa huamua kuleta maendeleo kidogo tu yatakayoonesha wanafanya kazi, wakiogopa kuleta maendeleo sana ambayo yanaweza kuwawezesha watu kuwa huru kiasi cha kuwaondoa watawala kwenye utawala.
Ndiyo maana kuna kampuni moja ya kuchimba dhahabu ilikuja Tanzania, ikataka kuwalipa Watanzania mishahara ambayo ni ya kawaida kimataifa, lakini kwa viwango vya Tanzania ni mikubwa, mawaziri wa Tanzania wakakataa hiyo mishahara na kusema ni mikubwa sana.
Yani Waziri wa nchi anakataa watu wa nchi yake wasilipwe mishahara mikubwa na wageni kutoka nje wanaowekeza kwenye kuchimba dhahabu!
Huo ni mfano mmoja mdogo tu unaoonesha kwamba hii dhana nzima kamba watawala wana nia nzuri ya kufanya maisha ya wananchi yawe bora kabisa, ni dhana iliyojaa propaganda za kisiasa kuliko vinginevyo.
2. Assumption - Rais ana uwezo wote.
Rais wa Tanzania ana nguvu sana, hili ni kweli. lakini hilo halimaanishi ana uwezo wote.Kuna watu wamefanya deal naye tangu hajawa rais wana faili lake, kuna wanaojua michepuko yake, kuna mambo mengi sana hatuyajui, especially kipindi cha Kikwete nilichokizungumzia, kujenga consensus ilikuwa kazi sana, na Kikwete alikuwa anafuatilia mambo, mengine anapotezea anasema mtajiju. Hata leo, rais ana amepewa nguvu sana, na kumpa nguvu sana kumefanya urais uwe na udhaifu.Rais huyo huyo ni Mwenyekiti wa CCM. Mambo mengine ukifanya vizuri serikalini yakaleta maendeleo yanahatarisha umaarufu wa CCM. Hapo kuna conflict. Tushaona rais hayuko popular miongoni mwa viongozi kama watu wengi walivyofikiri, na kuna watu wanapewa maagizo hawayatekelezi, na rais ana mambo kibao kufuatilia kila kitu vigumu.Maneno mengine anasema kwa ukali kisiasa tu aonekane mkali, lakini hata yeye mwenyewe ufuatiliaji hawezi, especially kwa sababu anataka kila kitu afanye mwenyewe.
Magufuli na ukali wake wote bado watu wanamchenga sana serikalini, wanakula rushwa, wanapiga hela, hawatekelezi maagizo, wanavuruga mipango yake, etc. Kwa hiyo ingawa kapewa nguvu sana katika mfumo rasmi, katika mfumo halisi anategemea sana watu wengine .
3. Assumption- Rais ana right views.
Rais mjuaji anaweza akawa ana contrarian views. Ana makabrasha yote, ana studies zote, lakini yeye anajiona anajua kuliko wasomi na anapingana nao na hataki kufanya walivyomuelekeza anafanya anavyotaka yeye. Mfano mzuri ni kesi ya mtu anaitwa Lawrence Mafuru. Jamaa ni well respected banker mpaka London Charter of Bankers wanamtambua. Alikuwa Msajili wa Hazina. Magufuli alimwambia atoe fedha zote za serikali benki za\ote azipeleke Benki Kuu, Mafuru akamwambia mheshimiwa naelewa unataka kubana ubadhirifu, lakini unachoshauri hapo ni sawa na kutaka lori kubwa ligeuke mara moja kwa kufunga breki kali.Unaweza kusababisha ajali. Tufanye hii kazi kwa polepole, kwa awamu.Tutafikia lengo lile lile, lakini hatutautikisa uchumi kwa mara moja, tufanye kama gari linapunguza mwendo taratibu, halafu linapinda kona na kurudi lilikotoka, unaepusha ajali.
Magufuli akakasirika sana kuambiwa vile, akaona kama jamaa kamsahihisha wakati yeye anajua kila kitu. Akamfukuza kazi Mafuru kwa style ya "atapangiwa kazi nyingine" (style inayoligharimu sana taifa, mtu analipwa mshahara bila kufanya kazi). Mafuru alishauri vizuri tu, kitaalamu, akasema Magufuli akifanya anavyotaka mzunguko wa fedha utaminywa sana na hali itakuwa ngumu sana mtaani. Magufuli hakumsikiliza, akafanya kivyake alichotaka. Matokeo yake mzunguko wa fedha umepata kudhoofika vibaya sana kama alivyotabiri Mafuru na biashara zinadorora.
Ukiangalia sakata la bei ya korosho lilivyoenda, utaona kwamba hata kama rais alikuwa na nia nzuri, hakuwa na mtazamo mzuri na execution plan yake imefail vibaya sana.
Yote haya yanaonesha nguvu za rais hazisaidii kitu kama.
1. Rais hana nia nzuri.
2. Rais hana ushirikiano wa wengine.
3. Rais hana execution plan nzuri.
 
Binafsi nilitokea kukichukia Chama changu Cha Mapinduzi yaani CCM tangia nikiwa sekondari. Chuki zangu dhidi ya CCM sikupandikizwa na mtu bali uelewa na upeo wangu mkubwa wa masuala ya kitaifa.

Nakumbuka nikiwa kidato cha kwanza mpaka namaliza kidato cha Sita nilikuwa na ndoto ya kuwa Rais wa Tanzania siku moja.. najua wengi mnacheka ila nilikuwa serious kabisa, na bado nina ndoto ingawa inafifia ila ya Mungu mengi wenda akaiamsha upya.

Mwaka 2015, binafsi nilikuwa mpinzani mkubwa wa MAGUFURI sababu kubwa ilikuwa nampinga MAGUFURI zi yeye bali kuwa mgombea wa CCM iliyokuwa imechakaa sana na hiaijiwezi tena... Hivyo niliamini MAGUFURI atakuwa kama Marais waliomtangulia ukimuondoa mwl. NYERERE.

Msiojua Tanzania vyema na uelewa wa siasa za Tanzania yetu hamuwezi kujua kuwa tulikuwa tunatawaliwa KIFALME. Namanisha tabaka la watu/familia fulani zilijidhatiti kuhakikisha wanatutawala milele. Ila kwa kuwa MUNGU SI ATHUMANI WALA YOHANA siyo nilichokuwa nakiwaza kinafanywa na MH. RAIS MAGUFURI kwa asilimia kama 95% hivi, licha ya dosari ndogo dogo yeye si malaika.

Hivi Karibuni kulitokea udukuaji wa mawasiliano ya baadhi ya MAKADA WA CCM sitapenda kuzungumzia uhalali wa kudukua mawasiliano ya mtu, wanaojinasibu kuwa wao ndiyo CCM ASILIA, nisikitike kusema kuwa hili ni GENGE moja hatari kabisa lenye malengo mahususi ya kuitawala Tanzania kwa msingi ya koo na urafiki wa kifamilia.

Kama umefuatilia maongezi ya mzee YUSUFU MAKAMBA, JANUARY MAKAMBA NA NAPE NAUYE utakuwa ulionote kitu gani hawa jamaa wanapanga, moja kwanza no dhahiri kuwa wao waliamini Wana Hati na haki miliki ya kudumu na kuitawala Tanzania. Mzee MAKAMBA anasikika akimwelekeza NAPE kuwa baba yake NAPE mzee NAUYE na KINGUNGE NGOMBARE MWIRU eti hajawajatambuliwa mchango wao kwa kepewa majina ya mitaa. Hapo ndipo utajua kuwa kuna koo za kiutawala nchii hii.

Pia ndugu, KAMILIUS MEMBE ukimsikiliza hoja zake utagundua kauli zake anakerwa na kitendo cha MH. Rais MAGUFURI kuteuwa watu pasipo kujali hizo koo za kiutawala na hasa kitendo cha kuzibomoa hizo koo tawala.

Kimsingi naomba kumshukru na kumpongeza MH. Rais MAGUFURI kwa jinsi anavyofanya teuzi zake bila kujali hizi koo tawala. Enzi za NYUMA ilikuwa fhahiri kujua nani anaandaliwa kuwa Rais kitu ambacho ni ujinga kwa taifa la watu wapenda demokrasia ingawa Ina ukakadi bado.

Wapinzani niwashauri kitu, kwasasa hamna MTU MBADALA WA QUALITY ya MAGUFURI kusema mkampanishe, ata CCM hawana huyu MEMBE anashida na urais wala shida wala hashira na shida za watanzania. Mkenge wanaouvaa Wapinzani ni kuacha kuzima nyumba yao inayoungua na kujiunga na koo tawala eti lumpinga MAGUFURI.

Movie nyingine inayochezwa na Wapinzani ni UKANDA na UKABILA, hili nimeliona kanda ya kaskazini hasa ARUSHA na Kilimanjaro turufu ya kumpinga MAGUFURI Iliyobakia ni kupandiza UKABILA na UKANDA hii dhambi ya upanguzi inayofanywa na Wapinzani itawatafuna na imeisha anza uwezi amini Upinzani unakufa slowly kaskazini.

Mimi huwa ni mtafiti mzuri sana, vita dhidi ya MAGUFURI inaongozwa na wachaga ila mjue hizi cheap politics huwa hazidumu ni kama upepo zinapita fasta.

Kitendo cha MH. Rais MAGUFURI kuligeuka hili kunditawala/Kootawala Namuona shujaa na jasiri kabisa.

Nimalize na HEKIMA YA MZEE DR. SLAA" Vijana tunavyotaka mageuzi lazima tu tafakari juu ya AINA YA MAGEUZI TUNAYOTAKA na NJIA SAHIHIHI ZA KUYATAFUTA/KUYAPATA.

ViVa MAGUFURI...2020.
 
Nakumbuka nikiwa kidato cha kwanza mpaka namaliza kidato cha Sita nilikuwa na ndoto ya kuwa Rais wa Tanzania siku moja..
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
najua wengi mnacheka ila nilikuwa serious kabisa, na bado nina ndoto ingawa inafifia ila ya Mungu mengi wenda akaiamsha upya.

Endelea na ndoto yako usijirudishe nyuma.. jiongeze kimaarifa na kifikra utafika.

Magufuli 2020 hiyo haina ubishi.. oyeeeeee
 
Hawa ni wale vijana wa Chato walio letewa Containa la Computer na furniture toka United State of America. Kama hukuwa unafahamu Ukanda... fuata Twiga na Tembo.
 
Status
Not open for further replies.
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom