Mh. Rais,
Heshima yako kiongozi wangu..!
Mh. Kwanza nikupongeze kwa yale yote ambayo umekuwa ukiyafanya kukuza uchumi wa nchi,kuimarisha utendaji serikalini,kupambana na ufisadi pamoja rushwa.
Mh. Rais,nimeamua kutumia jukwaa hili kuleta ombi langu kwako mkuu. Nimefuatilia leo wakati ukiwapongeza mashujaa wetu na kwa furaha uliyoipata,ukaamua kuwazawadia viwanja wachezaji wote wa timu ya Taifa.
Mh. Rais,Mimi siyo mchezaji,lkn kutokana na mazingira ya kazi za ujasiriamali,nimeshindwa kabisa kuweka akiba na kuweza kujinunulia japo kiwanja. Tendo la leo ulilolifanya kwa wachezaji limenifanya nijitoe muhanga na mm niombe kwako kiongozi km itawezekana unisaidie kiwanja hapa dar.
Wewe ni Rais wa wanyonge,na naamini hapa unapita kila wakati kusoma. Me naomba unisaidie kiwanja tu,ntafanya juhudi za kila aina ili nikijenge kwa nguvu zangu.
Mh. Rais,kukuomba hapa haina maana kwamba me ni mzembe,lkn km nilivyoeleza hapo juu kipato changu nimeshindwa kabisa kuweza kupata pesa za kununua kiwanja.
Naamini hata wachezaji wetu umewapa viwanja si kwa sababu hawana uwezo bali mapenzi yako ya dhati kwa watanzania.
Mh. Rais naomba ombi langu ulipokee mkuu wangu,mm sitakuangusha kukijenga. Ntapiga vibarua mpaka nyumba isimame na ntakuwa natoa taarifa kwa wasaidizi wako.
Naamini ombi km langu ni la ajabu sana mh. Rais,lkn wewe ni baba wa wote. Nimeondoa uoga nikiamini taarifa zangu zitafika kwako na utanisaidia. Siamini kwamba ukinisaidia mimi kupata kiwanja kupitia jukwaa hili,basi kila mtu ataomba sidhani km itatokea!
Mwisho:
Nitashukuru sana iwapo ombi langu litapokelewa na kukubaliwa.
NB: wasaidizi wa Rais mlioko hapa jukwaani naomba mfikishe ombi langu kwa Rais. Hata km mnaona atalikataa lkn lifikisheni tu. Ahsante
Sent using
Jamii Forums mobile app