Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,310
2,000
Hii thread iwe Maalum kwa Maoni, Ushauri na Mapendekezo mbalimbali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Mimi namuomba, Mheshimiwa Rais mteuliwa, kwa heshima na taadhima hili ni ombi binafsi kwako.

Nnaomba uhakikishe huyu mrembo wa ACT Bi Anna Mghwira unamuingiza bungeni na unampa wadhifa anaostahiki, huyu mama ni kichwa adhyim na adim kabisa.

Nimemfatilia mikutano yake mingi sana ya kampeni, anatoa vitu kichwani utafikiri ana word processor inayopanga na kuchuja anachokizungumza kutoka kichwani bila kusoma.

Halikadhalika leo kanifurahisha sana alipostukizwa na kutoa hotuba pale Diamond, ilikuwa fupi na imelenga points zote nzuri na ameeleweka vyema kabisa.

Anna heko sana na nitakuunga mkono katika siasa zako.
Ili kuipa hadhi na kuitangaza lugha yetu ya taifa, nashauri rais wetu mpya atumie Kiswahili katika shughuli zote rasmi za kitaifa na kimataifa. Cha msingi ni kuwa na wakalimani mahiri katika shughuli za kimataifa. Hii itainua hadhi na heshima ya nchi yetu badala ya kuendelea kuthamini lugha za kigeni. Tumekuwa watumwa mno wa lugha ya kiingereza mpaka kufikia hatua kudhani kuwa mtu anayeongea kiingereza vizuri ndiye aliye elimika wakati si kweli. Elimu ni uwezo siyo kuongea kiingereza. Hiki kiingereza cha "izi, wozi, wea, kongrugesheni, ameizingi, wati?, yu no, no problemu hakitusaidii kitu. Na kwa ujinga wetu tunafundishana kwa lugha tusiyoijua vizuri matokeo yake watoto wanafeli halafu tunawaona wajinga kumbe sera zetu ndio mbovu. Wachina, wakorea, wajerumani, wareno, wafaransa mbona wanatumia lugha zao na wanapiga hatua kubwa sana katika uchumi na sayansi. Sisi na kiingereza chetu cha kuombea maji tumefika wapi zaidi ya kutudhalilisha?

Maoni yangu haya hayana maana kuwa sitambui uwezo mkubwa wa kiingereza alio nao dr. Nataka aendeleze pale mwenzake alipoachia mwenzake, kwani alianza kwa kuhutubia kwa kiswahili kwenye mkutano wa AU lakini baadaye akaacha. Mimi nashauri Dr. sasa ajikite pamoja na mambo mengi kuitangaza lugha ya kiswahili kimataifa kwa yeye mwenyewe kuitumia badala ya kiingereza. Huwa naona viongozi wa nchi nyingine kama za kiarabu pamoja na kuwa wanajua kiingereza lakini utakuta wanazaunguza kiarabu na kisha wasiojua kutafsiriwa. Wakalimani sasa hivi tunao wengi, ni vizuri wakatumika vizuri kuikuza lugha yetu ya taifa. Ukweli ni kuwa unapotumia lugha mama au lugha ya taifa una kuwa na uhuru na uwezo mkubwa sana wa kujieleza na kuelezea kuliko unapotumia lugha za kigeni. Kwa watanzania wengi lugha yetu ya mama ni kiswahili.
Jambo moja ambalo Magufuli aliliona wazi katika kampeni zake ni kwamba Watanzania wanataka mabadiliko, na kwamba wengi walihisi mabadiliko haya yangeletwa na UKAWA. Magufuli akaahidi kwamba yeye ataleta madadiliko Watanzania wanayotaka.

Ushauri wangu kwa Magufuli ni kwamba kama kweli kweli anataka kuwaletea Watanzania mabadiliko - basi asiwe mtu wa kutafuta ushari kwa Kikwete na Mkapa. Wao walikuwa na nafasi ya kuletea Watanzania mabadiliko, na wengi waliona kuwa kwa sehemu kubwa walishindwa kuleta mabadiliko yaliyotakiwa, japo kulikuwa a mafanikio kataka sehemu chache.

Magufuli be your own man and master - Personality yako, kufikiri kwako na kule kwa kwa Kikwete na Mkapa ni tofauti kabisa na Watanzania wanategemea hilo litaleta mabadiliko wanayotarajia. Kuendelea kupokea ushauri toka kwa Kikwete na Mkapa ni kuwapa Watanzania mvinyo ule ule wa zamani katika glasi mpya; hilo ni hatari sana, na linaweza kukufanya uongoze kwa miaka mitano tu na kushindwa uchaguzi ujao.

Tunajua Kikwete a Mkapa walikuwa na mchango kukufanya uwe Raisi wa Tanzania - washukuru yaishie hapo. Waambie wakapumzike sasa, kazi yao imekwisha. Kuendelea kupokea ushauri wao kila wakati utajikuta unafanya kazi ili kuwaridhisha wao na sio Watanzania waliokuchagua. Pia epuka sana kupokea ushauri wao kwa mambo ambayo hujawaomba ushauri.

Lakini kuwa na washauri ni jambo nzuri tu - ila sasa tafuta washauri wako mwenyewe, watu wasio rafiki zako ambao wanaeleweka kuwa na busara na uzoefu katika uongozi, bila kuwa na haja ya kukufurahisha wewe kibinafsi, kutafuta urafiki na wewe au kujipendekeza kwako
Uchaguzi ulisha kwisha good enough tuna katiba ambayo inasema mtu akishatangazwa basi ndiyo rais na huna uwezo wa kupinga matokeo hayo popote its good when it is your turn but mind you atakuja tokea chizi mmoja me or ke ambaye ataamua kumuingiza mkewe au mmewe kwa kujua siku ya siku yeye ndiye mwenye mamlaka ya kutangaza matokeo ya urais atamtangaza spouse wake kutakucha, tuyaache hayo.

Binafsi kama ningepata wasaa wa kuongea na Magufuli ningemshauri haya yafuatayo

1. Hali ya hudumu ya afya ya Tanzania ni mbaya mbaya mbaya hakuna daktari aliye na moyo wa kufanya kazi kwa moyo ule uliokuwapo mwanzo. Mfano, hospitali yetu ya taifa ambayo ni tegemeo ya maskini wote wa Tanzania na daraja la viongozi kupita kwenda India huduma ni hovyo hovyo.

Hivi unajua kuwa huduma za CT Scan na MRI Muhimbili zimesimama Zaidi ya miezi minne na hakuna anayejali. Watu wa wizara ya afya naona hawajali kabisa.

Mimi nashauri wizara ya afya isihusike moja kwa moja na Muhimbili kama mtafuta habari nilienda pale, hakuna mwenye nia za dhati wa kuikomboa sekta ya afya.Wao wanachotaka serikali iendelee kupeleka watu India ili waendelee kupata pesa wanazopata wanajua namna wanavyopata, si watu hawa tunakufaa maskini.

2.Taasisi ya mifupa MOI tunaomba ijipambanue kama ni taasisi ya umma au ni kama Agha Khan kwani huduma zinazotolewa hapa afadhali malipo yake yangekuwa na risiti basi ni ujanja ujanja tu.

Heri na feri kwenye soko la samaki kuliko hapo, elimu yao haifanani na huduma wanazotoa.

Mimi naomba kama kama una power hiyo hizi taasisi ziwe chini yako kwani afya ya watu unaowaongoza ni muhimu saaana tena sana elimu ifuate.

Tanzania sasa tumempata Rais mpya wa awamu ya 5, ambaye watanzania wengi tuna matumaini atatekeleza ahadi zake kwa asimilia zaidi ya 90, katika ahadi zake aliahidi kufufua viwanda , katika kufufua viwanda asisahau zao la mkonge , zao hili kwa sasa limekuwa na soko kubwa sana ukilinganisha na kipindi cha nyuma mkonge kwa sasa grade ya SS kwa tani 1 ni takribani US dollar 2500- 3000 katika soko la dunia na local market ni makadirio ya Tsh 2,500,000 kwa tani , na SSUG ni takribani US dollar 1900-2200 kwa tani

Hivyo basi katika mashamba ya mkonge ajira nyingi zinaweza zalishwa na vijana wengi kuajiriwa wasomi na wasio wasomi na kulipwa vizuri , mashamba mengi yamebinafsishwa kwa wawekezaji ambao wanapunja maslahi ya wafanyakazi hasa unskilled labor kwa kuwapa ujira wa 4950 kwa siku ambayo ni ndogo kulinganisha na kinachozalishwa pia chama cha wafanyakazi mashambani TPAWU wakupe ushirikiano kurekebisha mishahara ya mashambani itakayokidhi maisha ya sasa

Mashamba mengi yamekufa na machache yanauhai , hivyo juhudi zifanyike kurudisha zao la mkonge katika ubora na kupunguza tatizo la ajira kwani mahitaji kwa mkonge duniani ni makubwa sana kulipo hapo awali

Nawasilisha, nikiwa nimefanya research ya kutosha kuhusu zao la mkonge Tanzania
Pamoja na kwamba sina imani na chama chako, ila naomba unishawishi wewe binafsi katika serikali yako.
Kama ulivyojinaji kuwa serikali yako, yani Tanzania ya Magufuli itakuwa KAZI TU, basi naomba udhihirishe hivyo katika baraza lako la mawaziri.

Kabla hata sijataka kujua waziri mkuu ambaye ataendana na sura ya kauli mbiu yako, lakini nataka usituletee watu hawa ambao walikuwa mzigo kwa taifa na waliolifikisha nchi hapa ilipo chini ya aliyekutangulia pamoja na waziri mkuu wake.

1. Sopteter Muhongo.
Huyu pamoja na kwamba tunaambiwa hakuhusika moja kwa moja kwenye kashfa xa escrow lakini alikuwa kinara wa utetezi katika sakata hili. Pia ni miongoni mwa waziri wenye elimu kubwa lkn hakuwa na mkakati bunifu wa kutatua tatizo la umeme nchini zaidi ya kuiacha tanesco kwenye deni kubwa. Pia ni miongoni mwa viongozi ambao hawathamini wawekezaji wa ndani, anaamini nchi itajengwa na wazungu au wachina.

2. Lazaro Nyalandu.
Huyu ni miongoni mwa mawaziri ambao tumeshuhudia tembo wakiuliwa kwa wingi, na twiga wetu wakisafirishwa kwenda nje, hafai katika serikali yako, kwani atafanya kazi ya mazoeaa ya serikali ya awamu ya 4.

3. Mwigulu Nchemba.
Pamoja na kwamba hakukaa kwenye wizara ya fedha kwa mda mrefu, lkn ni miongoni mwa vijana ambao hawana adabu katika taifa hili. Ni mmoja wa wanasiasa wachanga ambao hajali matamshi yake mbele ya umma, haangalii baada ya hapa athari zake zitanipeleka wapi, sio mstaarabu.

4. Willium Lukuvi.
Huyu kwa mwendo wa kasi inayohitajika nchini hatufai, utendaji wake hauto tofautiana na wa awamu ya 4, hana jipya ndani ya serikali yako.

5. Shukuru Kawambwa
Huyu ni moja ya mawaziri walioshusha thamani ya elimu yetu. Sio mbunifu. Fedha za fidia za rada mpaka leo hatujui matumizi yake yalienda wapi, hatufai kabisaa.

6.Hawa Ghasia.
Huyu mama bado uchama umemkaa kichwani kuliko maslai ya taifa. Hayupo active katika utendaji wake.

7. Jumanne Maghembe.
Huyu ni moja ya mawaziri ambao ndio chanzo cha huduma mbovu za elimu na maji. Elimu yake ni kubwa lkn haina msaada kwetu.

8.Harrison Mwakyembe.
Huyu kinachompa sifa ni lile sakata la richmond ambalo tunamwona kama shujaa. Lakini kiukweli hafai hata kuwa mwenyekiti wa kijiji. Sijaona mafanikio yake katika wizara alizozisimamia, ni mzigo ana asili ya mtandao ambao ni chanzo cha utendaji mbovu nchini. Ni mafya wa kisiasa

9. Magreth Sitta
Mama huyu tangu zamani ni outdated, haendani na kasi ya dunia, yupo nyuma na mda, hafai katika serikali yako.

10. Sofia Simba
Hana tofauti na Mama sitta, tena huyu uchama na mtandao wa uongozi umemjaa kichwani, hafai katika serikali yako.

11. Andwer Chenge
Najua huyu unamfahamu vema

12. Anna Tibaijuka
Najua unamfahamu vizur

13. Willium Ngeleja
Najua wamfahamu vzr

NB.
1. Mheshimiwa Rais kuna vijana wengi ambao naamini katika utendaji wao lkn siamini kundi lake, na mmoja wao ni Januari Makamba. Huyu binafsi namwamini kiutendaji, ubunifu lakini kinachomsumbua ni kutaka madaraka makubwa, kundi lake lililo nyuma yake, Huyu badala ya kuchapa kazi atakuwa anawaza urais baada yako kustaafu. Kwa mtazamo wangu ungemweka kando kwa mda baada ya miaka miwili ndo uumpe majukumu.

2. Kwa kukusaidia mh Rais ni vema ukachagua mawaziri wachache ambao wengi wao hawakuwa mawaziri, sio viongozi katika chama, vijana, wenye elimu isiyo na shaka. Hawa ndio wataileta tanzania mpya ya HAPA KAZI TU.

Mh Rais ukikosea kwenye baraza la mawaziri basi jua umeuwa nchi, na hapo tutadhibitisha kuwa hakuna cha Magufuli 4 change itakuwa ccm ni ile ile.

Asantee.
Hali ya Kisiasa
Mgogoro wa Zanzibar ni jukumu lako kwa sasa halikwepeki. Tafuta wasuluhishi wawili (kutoka Bara na Visiwani) wakusaidie kulishughulikia hili
2. Katiba mpya ya JMT ? pengine si ajenda ya chama chako kwa sasa lakini linahitaji dhamira yako? chonde chonde litendee haki taifa hili.

Mfumo na Uendeshaji wa Serikali
Uza mashangingi ya Serikali na ubakize machache tu kwa shughuli muhimu. Watumishi wa Serikali wakopeshwe magari na wapewe mafuta ili kuokoa fedha nyingi mno zinazopotea kiholela.[/FONT]

Rejesha nyumba za Serikali kwani wananchi wengi hatuna imani kuhusu dhamira, mantiki na umuhimu wa kuziuza nyumba za Serikali

Punguza sana idadi ya Wizara na Mawaziri ili kupunguza gharama

Boresha kipato cha Watumishi serikalini ili kuwaongezea morali

Toa fursa katika vipindi tofauti mikoani ukutane na wananchi wenye matatizo uwasikilize ana kwa ana, mmoja mmoja (uwe rais wa wananchi)

Misamaha ya kodi ni donda ndugu linalohujumu Taifa mapato, dhibiti hili kwa nguvu zako zote.

Panua wigo wa vyanzo vya mapato ya Serikali ? hili ni muhimu sana

Dhibiti safari za nje zisizo za lazima kwa Viongozi waandamizi wa Serikali

Rushwa na Ufisadi

Mahakama ya Rushwa na Ufisadi ianzishwe kama ulivyoahidi

TAKUKURU ipewe mamlaka ya kuwafikisha watuhumiwa mahakamani bila kibali cha DPP

Afya, Maji na Mazingira

Karabati hospitali za umma (Taifa, Mikoa, Wilaya) ziko katika hali mbaya (Zahanati kwa kila kijiji inawezekana!)

Imarisha Hospitali ya Muhimbili ikidhi viwango vya kimataifa ili kupunguza gharama za matibabu nje ya nchi

Panua wigo wa Mfuko wa Bima ya Afya ili ijumuishe wananchi wote (Rwanda wameweza hili) watakaochangia kiwango nafuu

Miji na Majiji ni machafu mno (taka ngumu na maji taka), imeshindikana kubadili hali na inaelekea hakuna suluhisho, inabidi tuzoe uchafu ? tunaomba wahusika wageukie taka

Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto iboreshwe kwa nguvu zote

Serikal igharimie magonjwa hatarishi ikiwemo saratani na UKIMWI

Matumizi ya mifuko ya plastiki yapigwe marufuku (Rwanda, Zanzibar imewezekana)

Anzisha Mfuko wa Maji Vijijini ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa maji katika maeneo yote

Elimu
Wanafuzi wengi wa elimu ya juu hawakupata mikopo kwa mwaka2015/2016? litatue hili kwani ni aibu

Elimu ya bure hadi kidato cha nne iwe kweli na yenye ubora

Shule ziimarishwe kwa kupatiwa madarasa, maabara, vitabu, walimu na lishe muafaka?
One Computer, One Pupil? ? tujenge taifa la kisasa na linaloendana na mabadiliko ya nyakati kimaendeleo
Anzisha Kamisheni ya Taifa ya Ushauri kuhusu elimu

Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Viwanda

Fufua kilimo cha mazao asilia (mkonge, kahawa)

Anzisha Mfuko wa Taifa wa Kilimona Mifugo utakaotoa mikopo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi

Imarisha na jenga miradi ya umwagiliaji na majosho ya mifugo

Imarisha vyama vya ushirika na viwezeshe kujitafutia masoko

Futa kodi zote kandamizi kwa wakulima, wafugaji na wavuvi

Anzisha viwanda vya kusindika mazao ya kilimo, ufugaji na uvuvi

Weka kodi nafuu na shindani kuhamasisha wawekezaji

Miundombinu na Uchukuzi

Punguza gharama za vifaa vya ujenzi ili wananchi wengi wamudu kujenga nyumba bora

Fufua Shirika la Ndege la Taifa (ATC)

Imarisha miundombinu ili kuondosha misongamano katika majiji na miji mikubwa (Dar, Mwanza, Mbeya, Arusha)
  1. Usikubali kofia mbili; wewe ni Raisi, uenyekiti wa CCM muachie mwingine ili chama kibaki chama na serikali ibaki serikali.
  2. Washauri Wabunge wa CCM, watangulize maslahi ya taifa mbele ya maslahi ya chama.
  3. Washauri Wabunge wa CCM kama itawezekana wamchague Spika wa Bunge asiyeegemea upande wowote.
  4. Pokea ushauri kutoka kwa vyama vya siasa lakini uwe huru kufanya maamuzi kulingana na matakwa ya Katiba ukizingatia maslahi ya wananchi.
  5. Usiruhusu Ikulu kutumika kwa maslahi ya CCM, vikao vya chama vifanyike nje ya Ikulu.
  6. Washauri CCM waachie mali za wananchi kwa kuzirudisha mikononi mwa wananchi kupitia serikali.
  7. Agiza vyombo vya dola vitoe haki sawa kwa wananchi bila upendeleo.
  8. Futa sheria zote kandamizi zinazozuia uhuru wa kutafuta, kupokea na kutoa habari. Vyombo vyote vya habari viwe huru.
  9. Hakikisha mikataba yote tunayoingia inawekwa wazi ili vijadiliwe na kupitishwa na Bunge.
  10. Vikumbushe vyombo vya dola kwamba jukumu lao la kwanza ni kuwalinda Watanzania na mali zao na si kupambana nao.

Watu wengi wanaishi wilayani na mahitaji yao mengi yanatatuliwa wilayani hukohuko, hivyo kuweka watendaji mahili na wabunifu kwenye ngazi ya wilaya ndio mtihani wa kwanza wa rais Magufuli. Wakuu wa wilaya na watendaji wengine wa JK sio kabisa, na huwenda ndio chanzo cha migogoro mingi ya wananchi dhidi ya serikali yao. JPM hana namna nyingine zaidi ya kuwaweka pembeni watendaji wote wavivu na wabadhilifu wilayani na mikoani ambao wengi wao wameshachukiwa tayari na wananchi wao.

Mtihani wa pili ni namna atakavyo atakavyotumia uwezo wake kupambana wa watu wajanjawajanja kama vile akina Lyatonga, Chenge, Tibaijuka, Manji, Aziz, Nazir, Harison, Samuel na wengine. Kwa muonekano wao ni wapenda sifa binafsi na kujali maslahi yao tu.

Mtihani wa tatu ni namna atakavyoweza kukaa mbali na kundi la mzee Mkapa waliohusika na kuuza viwanda, migodi, mabenki, mashamba, nyumba za serikali na hata waliotajwa kwenye kashifa ya EPA, meremeta, rada, ndege ya rais, n.k, ambao ni chanzo kikubwa leo cha ukosefu wa ajira kwa vijana na ongezeko kubwa la deni la taifa.

Mtihani wa Nne ni namna ya atakavyopambana na wimbi la watoto na wajukuu wa viongozi wa wakuu wa CCM wanaotaka kupewa nafasi serikalini kwa upendeleo kutumia nafasi za wazazi wao.

Mtihani wa Tano ni namna atakavyoweza kupambana na udini, ukabila, na ukanda katika kutoa nafasi za ajira nchini. Hali ilivyo hivi sasa ni mbaya sana, ajira wizarani, kwenye vitengo mbalimbali, mialiko kwenye mikutano, semina na nafasi za mafunzo inatolewa kwa ukanda, ukabila, udugu na udini.

Asipozingatia haya atahesabika kuwa ameanza na mguu mbaya sana utakaomgarimu sana uchaguzi wa 2020.
Secta ya bunge kitengo cha huduma na haki za mbunge kilichokuwa chini ya Chenge kilipangia bunge masulufu makubwa mno na bado wabunge kwa makusudi au kwa utovu wa adabu walikuwa wanaona haziwatoshi.

Mfano posho za kuhudhuria bunge ni shs 300.000 bado wabunge walikuwa wanaona hazitoshi ziongezwe chini ya Chenge

Mh. Rais kubana matumizi ya serikali iangalie sana secta hii ya bunge

Pia ninakuomba usitishe mikopo ya mashangingi, waheshimiwa wabunge wanunue RAV 4 au NOA kwa hela zao kwa sababu majimbo yamegawanywa na kuwa madogo yanayoweza kufikika kilaisi na usafiri huo.

Mh Rais fanya kazi ya ubunge iwe ngumu lli uchaguzi ujao wanachi wasiikimbilie

Ushauri huu pia nimekutumia kwa e.mail tafadhari naomba unijibu kama kutakuwa na ugumu katika utekelezaji wake

KIFUPI: Bunge linamega sehemu kubwa sana ya keki ya Taifa, serikali ya awamu ya tano liipunguze keki hiyo.
"Hapa Kazi tu", ndio msemo unaotawala sasa katika eneo la siasa. Siku chache zilizopita msemo wa 'mabadilikooo' Lowasaaa, Lowassaa mabadilikoo' ndio ulitamba. Wakati huo vijana, wazee na watoto walitamani mabadiliko aliyotangaza Mh. Edward Ngoyai Lowassa. Lowassa aliwajengea wafuasi wake Imani kubwa hasa pale alipowaambia wampigie kura kwa wingi na suala la kumtangaza mshindi tumuachie yeye. Wananchi wakampigia kura kwa wingi na hadi leo, suala la kutangaza mshindi wamemuachia Lowassa.

Vyovyote vile, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni John Pombe Magufuli. Anaweza asiwe mioyoni mwa raia wengi zaidi, nikiwemo mimi, lakini ndio Rais. Tukitaka kujadili mambo Makubwa ya Taifa letu, hakuna budi kumtambua Magufuli kwamba ndiye Rais, kwa sasa.

Rais Magufuli ameanza kazi kwa staili ya JK alipoingia mwaka 2005. Magufuli amekuwa akivamia taisisi nyeti za umma, kukagua, kujionea hali halisi, kutoa maagizo na pengine kujifunza. Ni vema na haki kuona tuna Kiongozi anayeonesha kuyajali majukumu ya wengine kiasi cha kufanya ziara za kustukiza kwa lengo la kuona uhalisia wa mambo. Kama Magufuli angekuwa anatoa taarifa za ziara zake, labda pangefanyika maandalizi yanayoweza kuziba sura halisi ya utoaji huduma katika taasisi husika.

Wapo wanaobeza, kukejeli na kupuuza na hata kuita ziara hizi kuwa ni maigizo tu au Nguvu ya soda tu. Wengine wanasema hayo kwa sababu wao wannamini hivyo kutokana na sababu zao wanazoona kuwa ni za msingi, na wengine wanatamani iwe hivyo ili Magufuli akishindwa wajigambe mbele ya 'wapinzani' wao wa kisiasa. Watu hawa hawajui kuwa kushindwa kwa Magufuli ni kushindwa kwa Taifa. Na Taifa ni letu wote, kwa hiyo na sisi sote tutakuwa tumeshindwa.

Mimi binafsi naziona ziara za ghafla za Magufuli kama michezo ya mtoto mdogo anayejifunza kutembea. Mtoto mdogo anapocheza ni ishara ya maendeleo mazuri kiafya. Ni ishara kuwa mtoto hana tatizo. Ni matumaini. Hutokea hata mzazi kushikwa na wasiwasi mtoto wake anapoacha kucheza na wenzake, na hali ilkizidi humpeleka kituo cha afya.

Magufuli anacheza, na hiyo ni ishara nzuri kwa mtoto. Na hapo ndipo inapokuja hamu ya kutaka kuona maendeleo chanya ya Rais wangu Magufuli. Atakapoanza kutembea, atembelee maeneo haya.

1. MADAWA YA KULEVYA
Jeshi la wananchi la Tanzania JWTZ, lina wanajeshi wapatao 30,000 na kuongeza au kupunguza kidogo (around 30,000). Takwimu za vijana walioathirika kwa madawa ya kulevya ni around 700,000 (laki saba) kwa mwaka 2013. Kwa hiyo ukichukua 700,000 ? 30,000 = 23 (aprox).

Hii ni sawa na kusema ukichukua vijana waliathiriwa na madawa ya kulevya unapata ndani yake majeshi 23 ya Tanzania (kwa idadi ya watu). Hili ni kundi ambalo kwa kiasi kikubwa halizalishi, halilipi kodi, ni tegemezi na wengi wao ni wahalifu ingawa uhalifu zaidi ni matokeo ya uathirika wao.

Vijana ni nguvu kazi ya taifa, ndio nguzo ya taifa. Nguzo hii ikiliwa na mchwa taifa litaanguka.

Kwa hiyo kila mtanzania atapenda zaidi kuona Mh. Magufuli anapigana vita kufa kupona dhidi ya madawa ya kulevya ili kuokoa afya za vijana wetu kabla hajawatembelea kwa kushtukiza huko mahospitalini.

Wananchi wangependa kuona madawa ya kulevya yanakamatwa, na kuchomwa moto ili kudiscourage biashara hii ya kuhuisha. Na zaidi amuombe JK majina aliyodai kuwa nayo (kama haukuwa mkwara) ili aanze nayo.

Angalizo: Kila mtu anaweza kuwa mwathirika wa madawa ya kulevya.

2. UJANGILI
Sasa hivi Kilo moja ya meno ya Tembo ina thamani ya Tsh. 200,000. Siku chache zilizopita tumeambiwa Tanzania iliizuia Malawi kuteketeza Meno na pembe za Ndovu zilizokamatwa nchini huko zikitokea Tz. Ripoti zaidi kuhusu ujangili huo hazileti furaha kwa wazalendo.

Al Jazeera wameiita Tanzania 'Point of extinction'. Kwa maana eneo la kuondoa uhai Duniani, au eneo la maangamizi, wakiakisi hali ya ujangili katika Tanzania inayoonesha kuwa Tembo wamepungua kutoka 109,051 mwaka 2009 na kufikia 43,330 mwaka 2014.

Tembo 85181 wameuawa kwa kipindi cha miaka 5. Sawa na tembo 17,016 kila mwaka. Maana yake kwa tembo 43,330 waliobaki ukigawa kwa 17,016 ni sawa na miaka chini ya mi3, tembo watakuwa wamekwisha ikiwa hali haitadhibitiwa. Hiyo ni kwa Tembo tu. Magufuli aguse na hapo.

3. UFISADI
Escrow, Epa, Richmond, Meremeta, Mabilioni ya Uswis, Ufisadi katika uchaguzi, na madudu mengine kibao. Magufuli akitaka kujenga imani kwa wananchi asiache kushughulikia mafisadi kama alivyoahidi. Lakini akiendelea ku'deal' na wanataaluma (mf. Madaktari Muhimbili) lakini akaacha wanasiasa wafanye wanavyotaka, wafanyakazi watapoteza imani naye. Na hapo kazi zitafanyika siku akivamia maofisini na siku mbili tatu baadae halafu 'business as usual'. Itapendeza kama atagusa na Mafisadi.

4. MIKATABA YA MADINI, MAFUTA NA GESI
Tumeshuhudia ugeni mkubwa nchini petu mara baada ya ugunduzi wa mafuta na gesi. Lakini hata sasa watanzania wana wasiwasi kuhusu mikataba 35 ya siri iliyofanywa na Rais wa awamu ya nne na wageni wake Rais Obama wa Marekani na Xi Ji Ping wa China.

Magufuli atakapoacha michezo ya ziara za kustukiza, tungependa aweke mikataba hii wazi, kisha wananchi washuhudie, na kama kuna harufu ya maslahi binafsi ya viongozi waliotia saini mikataba hiyo kwa siri, hatua mahususi zichukuliwe.

Tumeonewa sana kwenye Madini. Wamiliki wa migodi hii sio tu ni watu Matajiri bali pia ni watu wenye ushawishi mkubwa kwenye serikali za mataifa yalipoasisiwa makampuni hayo. Magufuli atapata sifa akituokoa na dhuluma hii iliyofanywa kwa miaka mingi. Haina maana 'neno hapa kazi tu' halafu rasilimali zetu zinakombwa kwa ridhaa yetu wenyewe. Badala ya hapa kazi tu inakuwa 'Hapa ubwege tu'.

5. KATIBA MPYA
Katiba yenye tija, tumaini jipya na mwanzo mpya wa Utanzania tunaotamani. Inafahamika wazi kuwa Magufuli ni miongoni mwa wanaCCM waliouteka na kuubaka mchakato wa katiba mpya. Mh. Sitta akajiandikia kijitabu chake akakiita 'katiba pendekezwa' huku akishadidiwa na wanaCCM, wakapiga makelele ndani ya bunge letu 'tukufu' kama mazuzu waliokosa kunywa dawa siku hiyo. Magufuli alikuwa miongoni mwao.

Sasa Mh. Rais Magufuli ana nafasi ya kuwa huru na kuacha kufuata mihemko ya siasa za vyama kwenye jambo la msingi ka Katiba. Pindi apatapo wasaa, aurejeshe mchakato wa katiba mpya ili kurudisha matumaini yaliyopotezwa. Na hili halihitaji kuvamia wizara ya katiba na sheria.

Maeneo ya msingi ni mengi na muda wa miaka mitano ni mchache sana. Naomba itokee kuwa 'drama' hizi za Mh. Rais iwe mwanzo wa safari ya kuelekea huko nilipoeleza. Haitapendeza kama lengo la hizi 'drama' ni kutafuta kukubalika tu halafu business as usual (cheap popularity).

Pia, ifahamike kuwa kutekeleza mambo hayo ni kama kuingia vitani. Kwa hiyo Mh. Rais Magufuli anapaswa kuwa mtu anayehitaji msaada katika vita hii kuliko mtu mwengine yeyote. Kwa hiyo itakuwa vizuri zaidi endapo 'drama' hizi za ziara za kustukiza zikawa mbinu za kutafuta 'kupendwa na wananchi' na hivyo kupata support kubwa pale atakapoanzisha hiyo vita.

Au kama sivyo, basi ni vema Mh. Rais Magufuri akawa na malengo ya msingi kuliko maeneo niliyogusia. Kumbe sasa endapo hatagusia hayo atagusa wapi? Mh. Rais Utakapomaliza Michezo yako, Naomba uguse na hayo.

Asante.

0713933736

Rais magufuli komesha tatizo la watu kukaimu nafasi kwa mida mrefu

Nafahamu Rais JPM anafahamu kuwa serikalini kuna tatizo la baadhi ya watu kukaimu nafasi za madaraka kwa muda mrefu bila huku wakiwa hawana sifa za kushika madaraka hayo. Wenye sifa wamekuwa wakinyimwa gursa hiyo na hivyo kuwakatisha tamaa na kuzorotesha utendaji kazini.

Watu hao mara nyingi wamekuwa wakisaidiwa na baadhi ya wakubwa walioko wizarani kwa kile kinachoonekana ni ukabila, undugu na urafiki.

Nimetembelea maeneo mengi mfano Singida, Bunda, Shinyanga manispaa na kukuta tatizo hilo hasa kwenye idara za afya, manunuzi na uhasibu.

Naomba serikali hii ishughulikie hili ili wenye sifa wapewe nafasi hizo na hii itaongeza tija ya utendaji serikalini.
Mimi miongoni mwa watanzania zaidi ya milioni hamsini natumia fursa hii kutuma hoja tano kwend kwa JPM kama sehemu yangu ya kumshauri kiongozi wangu wa nchi tuweze kufikia kile wengi tunachokitamani.

1. Nguvu kazi iliyopo utumiwe ipasavyo na kuwa na mkakati kfanikisha wazalishaji mali (producers) wazidi walaji(consumers). Hapa serikali ufungue kilimo na shughuli zingine asilia ambazo ndiyo zinabeba idadi kubwa ya watu. Serikali na secta binafsi nunueni tractors na kutenga maeneo kwa ajili ya kilimo cha mazao mbalimbali na vijina wawekwe ktk mashamba hayo kwa ajili ya kuzalisha. Irrigation schemes ziwepo kwa wingi na serikali iweke utaratibu wa upatikanaji masoko.

2. Tuwe na viwanda vinavyoa aksi malighafi yetu tunayoizalisha sisi ili tukuze hizo shughuli zinazotoa malighafi. Si lazima kuwa na viwanda vikubwa sasa hivi bali tuanze na viwanda vyetu vidogovidogo vinavyoaksi uchumi wetu badala ya kupokea viwanda toka nje hii hataisaidia kwa mda mrefu kwani badae tutajikuta hatumiliki uchumi sisi.

3. Fedha inayopatikana asilimia kubwa yake ifanye maendeleo ya jamii kkt huduma za jamii km afya na miradi ya maendeleo kuliko kuendesha serikali kwani ni wazi kuna bilioni nyingi zinatumika kuendesha serikali pasipo na ulazima . Mfano idadi kubwa ya magari ya kifahari kutokana na vyeo vvyingi km vile idadi kubwa ya wabunge,wakuuu wa mikoa na wilaya,RPCs,wakurugenzi,mawaziri na utitili mwingi ambao wote wanatumia pesa nyingi.

4. Mabadiliko na utungaji wa sheria mpya na hata katiba mpya ili kuiweka Tanzania ktk nafasi salama zaidi yenye maslahi mapana ya nchi.

5. Yapo mambo makubwa yanalitafuna taifa na bado hayajaguswa wala kuzungumziwa mfano mikataba mibovu ya madini. Rais sasa ahame toka kwenye kupapasa ili akajikite na mambo hayo mazito ambayo ni shida kwa taifa.

Asante
By GGM.
 

gkileo

JF-Expert Member
Apr 16, 2010
1,064
1,500
Mh. Rais wa jamhuri ya Muungano-Tanzania ,
Salaam!

HONGERA KWA KAZI.

MAPENDEKEZO KUHUSU GESI ASILIA kutoka MTWARA.
-serekali iweke mkakati mkubwa kuwezesha gasi hii ITUMIKE kwenye MAGARI-

-Hii itainua sana uchumi wetu kwani licha ya gharama za gesi asili
kua ndogo (kama 1/2) lkn pia pesa itabakia nyumbani!
-Inaweza kuimarisha thamani ya shilingi yetu.
-itaongeza ajira
-serekali haina gharama kwani ikishaweka sera na sheria utekekezaji unabakia kwenye sekta binafsi.
-serekali itoe ELIMU , ihamasishe , iondoe kodi ktk vifaa vya kubadili magari yaweze kutumia gesi.
-ipunguze kodi kwa magari yanayoagizwa yanayotumia gesi
- mapato ya serekali yatakua makubwa sana kwani serekali ndio inamiliki gesi
(Angalia mawazo ya wataalam wa DIT)
https://www.dailynews.co.tz/news/vehicle-conversion-to-natural-gas-cuts-expenditure.aspx Nitabaki kua mzalendo daima.
Asante!
 

gunga yenna

Member
Apr 11, 2019
90
95
Maoni ushauri kwa Dr. Magufuli inaonesha jinsi gani baadhi yetu Watanzania tunavyofikiri kwamba Rais ndiye kila kitu katika nchi hii, inasemekana Muhimbili kumeoza pamoja na juhudi zote za Rais hakuna mafanikio, mashine zimehujumiwa za kupimia wagonjwa, hiyo ni kazi ya Rais, haya kuna ujangili ni kazi ya Rais? mwandishi hakuna mahali popote anapopongeza juhudi za Rais wa awamu ya tano alizotekeleza kwa kipindi kifupi alichokaa madarakani, ana mlolongo wa mahitaji ambayo ikibidi Rais Magufuli ayatatue anahitaji kukaa madarakani zaidi ya miaka ishirini, kumbuka matatizo hayo ni malimbikizo ya miongo minne kwa awamu nne zilizopita, huenda ikahitajika miongo minne kuondokana na changamoto zote hizo za mwandishi wa makala ya ushauri kwa Rais Dr. Magufuli, pia ni muhimu Watanzania wote kuwa pamoja wakaungana kutatua hizo changamoto badala ya kumlenga Rais peke yake. Zanzibar kuna tatizo lakini linakuzwa sana kisiasa, kumekuwa na maridhiano na yalifanya kazi lakini humo ndani katika utekelezaji kunatokea mkanganyo kwa sababu ya kukiuka makubaliano ya awali upande mmoja kutaka zaidi kinyume Cha makubaliano ni shida za Kiafrika. Ni vema kwa Watanzania wote tunapochangia mawazo kuhusu mstakabali wa nchi yetu tujifunze kuzungumzia hoja zinazojenga mawazo yetu kama raia ili tushiriki katika kutatua mlolongo wa changamoto alizoainisha mshauri kwa Dr. Magufuli namna ya kuendesha nchi, badala ya kumlenga Rais peke yake. Tuna utamaduni uliojengeka miongoni mwa Watanzania kutothamini nchi yetu ndiyo sababu kuna uhamasishaji wa uzalendo na kuipenda nchi yetu, lakini bado kuna baadhi yetu hatuamini kama Tanzania ni kwetu na tunapaswa kuilinda bila kujali itikadi ya mtu.
Tubadilike.
 

lloydsam

Member
Nov 8, 2015
41
125
Tujiulize kama wewe ungekuwa Raisi leo ungefanya nini kama nchi ilivyo leo. Mimi ningefanya hivi kwa uzoefu wangu na nina Imani kabisa nchi ingebadilika na maendeleo ya kiuchumi yangeonekana. Hivi vitu nitavitaja kwa umuhimu kwamba ninaanza na nini. Hivyo namba hapo chini ni kama hatua moja moja • Kwa kutumia ofisi ya CAG na kampuni za consulting za kimataifa kama (Deloitte, Ernst & Young (EY), KPMG and Pricewaterhouse) wafanye uchunguzi kwenye idara zote za serikali na watoe report ya kuongeza ufanisi mfano kuunganisha idara, kuongeza technologia na kuangalia idadi ya wafanyakazi. Lengo ni kupunguza gharama, kuongeza ufanisi na kutoa maelezo ya kila mfanyakazi anatakiwa kufanya nini na malengo yake ni yapi. Hivyo kila mtu kuanzia katibu mkuu anakuwa na malengo ya mwaka. Hii itasaidia kila mtu kuamka na kuafanya kazi bila mpangilio maalumu na kuongeza ufanisi kazini. Vilevile nitajua serikali ikoje kwa urahisi na mapungufu. Kwenye hili hakuna siasa.
 • Nitatoa uhuru kwa vyombo vya habari na wanasiasa wawe na uwezo wa kufanya mikutano wakati wowote bila kujali. Maendeleo hayajali maneno. Lakini demokrasia inaleta maendeleo. Kutakuwa na demokrasia ya ukweli
 • Mfumo wa shule kuanzia msingi mpaka form six kubadilika. Nitabadilisha mfumo wa sasa wa elimu wote. Lengo kubwa ikiwa kushindanisha watoto wetu hasa kwenye technologia. Hivyo nitahimiza technoologia iweze kutumiaka zaidi kwenye mashule na tutaongeza walimu wa technologia ngazi zote. Vilevile nitaomba misaada kutoka kwa waziri mkuu wa India, US na kwenye foundation kama Bill gate foundation kuweza kusaidia kuweka technologia kwenye madarasa. Lakini sio hilo tu nitaomba watuwekee utaratibu ili wahitimu wetu waweze kujifunza software mbalimbali ili waweze kufanya kazi kimataifa hata wakiwa Tanzania. Vilevile nitaongea na kampuni za software mbalimbali kama SAP ya German, Oracle na Cisco za USA kutusaidia kwenye hili. Kuna vitu virahisi sana mfano simu nyingi ni computer tayari ina maana kukiwa na data free basi unaweza kutafuta simu za bei rahisi zigawe kwa kila mtoto na kuweka vitabu, lecture za vyuo na kuunganisha n ahata na vyuo na shule mbalimbali duniani. Mtoto wa Tanzania anaweza kufanya homework yake akaipiga picha na mwalimu wa kujitolea ambaye yuko India anaweza kusahihisha hii inawezekana kama tunafikiria vizuri. Haya ni mambo ya kuongeza tu haina maana tusiwe na walimu lakini ni mfano tu.
 • Nitawekeza kwenye kilimo. Tukasome sera za kilimo kwanza na tufanye kama sera ilivyo
 • Mapendekezo ya kubadilisha katiba hasa kwenye mambo ya kiuchumi. Nita ruhusu watu zaidi kuja Tanzania wenye vipaji kwenye technologia, diaspora wa Tanzania na NGO za maendeleo. Mimi siamini kama tuna matatizo ya kuwa wengi au tutapoteza mashamba yetu nchi yetu ni kubwa na tunahitaji watu productive. Mimi mwenyewe niko nchi ya watu kwa sasa!. Sera za kijinga za uraia nitazitoa kwa manufaa makubwa ya nchi mfano mzuri ni katiba ya Kenya. Tofauti ni kwamba kwenye katiba hii hakutakuwa na kuongeza ukubwa wa serikali kama ilivyo Kenya. Nitabadilisha mfumo wa Ardhi ili iongeze uwekezaji lakini kutakuwa na sehemu maalumu ambazo huta ruhusu uwekezaji ni za makazi tu.
 • Bodi maalumu za ushauri. Kutakuwa na bodi za ushauri kila wizara. Hizi board ni za wasomi mbali mbali na watu wenye nia nzuri na Tanzania wanashauri kwenye sera. Hakuna kulipwa ukiwa mwana bodi wala posho ni kujitolea. Diaspora wa watu wanje wenye nia nzuri wanakaribishwa.
 • Mahakama nitaiacha huru na kuwapa watakalo kuongeza ufanisi.
 • Tutatoa elimu ya Afya kwa vijana hasa chini ya miaka 30 ya mazoezi na lishe na itaingiza kwenye elimu yetu
 • Tutakuwa na Parks za kupumzikia, kukimbia, kutembea ,kucheza watoto, na kuendesha baiskeli na kila wilaya ni lazima iwe na sehemu za wazi za hivi.
 • Nitakuwa nahutubia Taifa kila mwezi
 • Nitakuwa nafanya debate na kupokea maswali kutoka kwa wananchi kila miezi mitatu. Debate wapinzania wanaruhusiwa na itakuwa kwenye TV kwenye chuo kimojawapo live. Debate za maendeleo tu.
 • Nitaanzisha mfumo wa mobile Hospital. Yaani hospitali za magari ziende kila kijiji na Dr wa meno, kisukari, watoto nk kupunguza watu kusubiri kuzidiwan na kuja hospitali za rufaa ambazo ni chache. Yaani hii itakuwa kama kinga.
 • Ningewapa bank kuu kazi ya kuhakikisha lengo lao ni pamoja na kuongeza ajira kama ilivyo USA. Hii itasaidia Bank kuweka sera za kusaidia biashara ndogondogo ambazo ndiyo waajiri
Nitatoa mengine baadae nipe yako
Safi sana
 

gunga yenna

Member
Apr 11, 2019
90
95
Kamundu hakika una maono makubwa na mapenzi makubwa kwa nchi yako, mafanikio katika nchi yoyote hutokana na mageuzi ya kifikra ya wananchi wake, sijaona popote unapoeleza ni jinsi gani utaandaa fikra geuzi kwa wananchi hawa ili wakabiliane na maendeleo stahiki yanayotarajiwa kutoka kwako kama Rais ajaye.
Mfano rahisi tu hapa kwetu Tanzania awamu zote zilizopita za uongozi, Halimashauri zilikusanya mapato na kuyatumia kwa maendeleo ya maeneo yao, ikabuniwa miradi hewa watu wakajinufaisha sana, pesa ikaonekana pia mtaani, awamu ya sasa iliona huo udhaifu ikabadilisha utaratibu ili kudhibiti mapato na matumizi hivyo pesa yote inakwenda moja kwa moja Serikali kuu, mtaani kumekauka hakuna pesa watu watakwambia hii Serikali ni mbaya Sana watu hawana pesa, lakini Serikali imedhibiti mapato yake yasichezewe na watu,haijamnyang'anya mtu biashara yake.
Wananchi hapa wanatakiwa wabadilike kifikra kwa sababu uchumi wao wa awali ulikuwa ni wa bandia.
Kamundu ndugu yangu, kila kiongozi wa nchi katika dunia hii mwenye maono huwa ana mikakati mikubwa ya kuiletea nchi yake uchumi na heshima, Donald Trump alisema America First kwa maana kila Mmarekani aiweke nchi hiyo kwanza kabla ya kitu kingine, Wachina wana ajenda ya kutaka kuwa matajiri zaidi duniani kushinda Marekani hayo ni maono kila mtu anayetaka kukamata nafasi kubwa kabisa katika nchi yake.
Tanzania tuliambiwa wakati kampeni za uchaguzi kwamba kipaumbele ni Elimu, Afya, Miundombinu, na kupambana na rushwa na ufisadi yote yanakwenda sawia.
Nafikiri kila mtu akileta mipango yake hapa patakuwa hapatoshi,isipokuwa tusaidie Serikali itimize malengo yake iliyojiwekea ya maendeleo bila ya kuibeza bila sababu, ikiwa kuna mapungufu katika utekelezaji basi eneo hilo husika likosolewe, sio kazi yote ionekane kama haifai au Rais na mawaziri hawafai sio sahihi.
Tuipende nchi yetu na tuwe wazalendo kweli kweli.
 

Kamundu

JF-Expert Member
Nov 22, 2006
3,329
2,000
Kamundu hakika una maono makubwa na mapenzi makubwa kwa nchi yako, mafanikio katika nchi yoyote hutokana na mageuzi ya kifikra ya wananchi wake, sijaona popote unapoeleza ni jinsi gani utaandaa fikra geuzi kwa wananchi hawa ili wakabiliane na maendeleo stahiki yanayotarajiwa kutoka kwako kama Rais ajaye.
Mfano rahisi tu hapa kwetu Tanzania awamu zote zilizopita za uongozi, Halimashauri zilikusanya mapato na kuyatumia kwa maendeleo ya maeneo yao, ikabuniwa miradi hewa watu wakajinufaisha sana, pesa ikaonekana pia mtaani, awamu ya sasa iliona huo udhaifu ikabadilisha utaratibu ili kudhibiti mapato na matumizi hivyo pesa yote inakwenda moja kwa moja Serikali kuu, mtaani kumekauka hakuna pesa watu watakwambia hii Serikali ni mbaya Sana watu hawana pesa, lakini Serikali imedhibiti mapato yake yasichezewe na watu,haijamnyang'anya mtu biashara yake.
Wananchi hapa wanatakiwa wabadilike kifikra kwa sababu uchumi wao wa awali ulikuwa ni wa bandia.
Kamundu ndugu yangu, kila kiongozi wa nchi katika dunia hii mwenye maono huwa ana mikakati mikubwa ya kuiletea nchi yake uchumi na heshima, Donald Trump alisema America First kwa maana kila Mmarekani aiweke nchi hiyo kwanza kabla ya kitu kingine, Wachina wana ajenda ya kutaka kuwa matajiri zaidi duniani kushinda Marekani hayo ni maono kila mtu anayetaka kukamata nafasi kubwa kabisa katika nchi yake.
Tanzania tuliambiwa wakati kampeni za uchaguzi kwamba kipaumbele ni Elimu, Afya, Miundombinu, na kupambana na rushwa na ufisadi yote yanakwenda sawia.
Nafikiri kila mtu akileta mipango yake hapa patakuwa hapatoshi,isipokuwa tusaidie Serikali itimize malengo yake iliyojiwekea ya maendeleo bila ya kuibeza bila sababu, ikiwa kuna mapungufu katika utekelezaji basi eneo hilo husika likosolewe, sio kazi yote ionekane kama haifai au Rais na mawaziri hawafai sio sahihi.
Tuipende nchi yetu na tuwe wazalendo kweli kweli.
Gunga, ukisoma vizuri utagundua mipango yangu hapo haipishani na mipangilio yeyote ya serikali bali ni kuongeza ufanisi. Sababu mojawapo inayopunguza ufanisi serikalini ni kwamba viongozi hawajui vizuri wanatakiwa kufanya nini kama wewe ni kiongozi leo au mfanyakazi wa serikali unatakiwa kujua malengo yako kikazi. Kuwe na Lengo la mwaka halafu kwenye hilo kunakuwa na malengo wa mwezi na kila mfanyakazi anajua anatakiwa kufanya nini. Kweye kampuni binafsi ndiyo wanavyofanya 'goals" Na ndiyo maana nilisema cha kwanza

"
 • Kwa kutumia ofisi ya CAG na kampuni za consulting za kimataifa kama (Deloitte, Ernst & Young (EY), KPMG and Pricewaterhouse) wafanye uchunguzi kwenye idara zote za serikali na watoe report ya kuongeza ufanisi mfano kuunganisha idara, kuongeza technologia na kuangalia idadi ya wafanyakazi. Lengo ni kupunguza gharama, kuongeza ufanisi na kutoa maelezo ya kila mfanyakazi anatakiwa kufanya nini na malengo yake ni yapi. Hivyo kila mtu kuanzia katibu mkuu anakuwa na malengo ya mwaka. Hii itasaidia kila mtu kuamka na kuafanya kazi bila mpangilio maalumu na kuongeza ufanisi kazini. Vilevile nitajua serikali ikoje kwa urahisi na mapungufu. Kwenye hili hakuna siasa. "
 

gunga yenna

Member
Apr 11, 2019
90
95
Gunga, ukisoma vizuri utagundua mipango yangu hapo haipishani na mipangilio yeyote ya serikali bali ni kuongeza ufanisi. Sababu mojawapo inayopunguza ufanisi serikalini ni kwamba viongozi hawajui vizuri wanatakiwa kufanya nini kama wewe ni kiongozi leo au mfanyakazi wa serikali unatakiwa kujua malengo yako kikazi. Kuwe na Lengo la mwaka halafu kwenye hilo kunakuwa na malengo wa mwezi na kila mfanyakazi anajua anatakiwa kufanya nini. Kweye kampuni binafsi ndiyo wanavyofanya 'goals" Na ndiyo maana nilisema cha kwanza

"
 • Kwa kutumia ofisi ya CAG na kampuni za consulting za kimataifa kama (Deloitte, Ernst & Young (EY), KPMG and Pricewaterhouse) wafanye uchunguzi kwenye idara zote za serikali na watoe report ya kuongeza ufanisi mfano kuunganisha idara, kuongeza technologia na kuangalia idadi ya wafanyakazi. Lengo ni kupunguza gharama, kuongeza ufanisi na kutoa maelezo ya kila mfanyakazi anatakiwa kufanya nini na malengo yake ni yapi. Hivyo kila mtu kuanzia katibu mkuu anakuwa na malengo ya mwaka. Hii itasaidia kila mtu kuamka na kuafanya kazi bila mpangilio maalumu na kuongeza ufanisi kazini. Vilevile nitajua serikali ikoje kwa urahisi na mapungufu. Kwenye hili hakuna siasa. "
Kamundu sijakupinga kabisa ila tu kuamusha fikra za maendeleo ni shida Sana, huko Ulaya na Marekani kuna maendeleo miaka 200 iliyopita hapa ndiyo kwanza tunaanza, tunaitwa nchi zinazoendelea, walimu wa sayansi Marekani wa high school hapa wanafundisha chuo kikuu ona tofauti hiyo, mipango yako ni mizuri angalia jinsi ya kuindaa jamii utakayokuwa nayo wakati wa utawala wako ndiyo hoja yangu, Dr. Magufuli anayo mengi sana kichwani ya kuisaidia nchi hii lakini ona katika mitandao kejeli zinazoandikwa hakika zinakatisha tamaa, lakini yeye ni shujaa anaendelea na mipango yake. Hata wewe ujifunze utamaduni wa Kiafrika katika siasa.
 

Kamundu

JF-Expert Member
Nov 22, 2006
3,329
2,000
Kamundu sijakupinga kabisa ila tu kuamusha fikra za maendeleo ni shida Sana, huko Ulaya na Marekani kuna maendeleo miaka 200 iliyopita hapa ndiyo kwanza tunaanza, tunaitwa nchi zinazoendelea, walimu wa sayansi Marekani wa high school hapa wanafundisha chuo kikuu ona tofauti hiyo, mipango yako ni mizuri angalia jinsi ya kuindaa jamii utakayokuwa nayo wakati wa utawala wako ndiyo hoja yangu, Dr. Magufuli anayo mengi sana kichwani ya kuisaidia nchi hii lakini ona katika mitandao kejeli zinazoandikwa hakika zinakatisha tamaa, lakini yeye ni shujaa anaendelea na mipango yake. Hata wewe ujifunze utamaduni wa Kiafrika katika siasa.
Gunga haya si mambo ya Ulaya wala USA vitu vyote nilivyosema hakuna ugumu wowote wa kufanya ukisoma vizuri. Mfamo kuruhusu uhuru ni jambo la Ulaya na USA? kuwekeza kwenye kilimo?, afya ni vitu ambayo vinafanyika. Ujue nchi nyingi za ASIA zilikuwa kama sisi miaka 35 iliyopita hizi nchi si za Ulaya. Mambo mengi magumu tunajitakiwa au hatuna tu mpangilio mzuri. Sasa Raisi kwanini ujali mitandao kama kweli unafanya kazi vizuri! huwezi kuwa unajali maneno. Maneno yanakuwa na tija pale tu ambako ni ya kweli
 

gunga yenna

Member
Apr 11, 2019
90
95
Gunga haya si mambo ya Ulaya wala USA vitu vyote nilivyosema hakuna ugumu wowote wa kufanya ukisoma vizuri. Mfamo kuruhusu uhuru ni jambo la Ulaya na USA? kuwekeza kwenye kilimo?, afya ni vitu ambayo vinafanyika. Ujue nchi nyingi za ASIA zilikuwa kama sisi miaka 35 iliyopita hizi nchi si za Ulaya. Mambo mengi magumu tunajitakiwa au hatuna tu mpangilio mzuri. Sasa Raisi kwanini ujali mitandao kama kweli unafanya kazi vizuri! huwezi kuwa unajali maneno. Maneno yanakuwa na tija pale tu ambako ni ya kweli
Inawezekana Uhuru unaozungumzwa tunatofautiana tafsiri, mtu akishindwa jambo lake hapa hatua ya kwanza anatua kuishambulia Serikali na Rais wake, kiongozi wa Chama Cha upinzani akisimama jukwaani ni kuishambulia Serikali bila hata sababu, nikafikiri anazungumzia Sera nzuri kama ulivyoainisha wewe ulipoingiza mada ya jinsi ungefanya ungepata nafasi, hayo ndiyo mazungumzo chanya, lakini mtu anaanza kuhutubia oohh Serikali hii blabla akiacha Serikali anamvaa Rais, January hadi December ni kuponda kila kitu anachokitekeleza Rais ni shida sana, unajua huko majuu mambo hayo yalifanyika toka zamani watu wameyazoea, huku kwetu kumtukana Rais au kumdhihaki ni issue inawezekana katiba ikawekwa pembeni ili kukabiliana na hali hiyo, ili kuiondoa contempt isijengeke miongoni mwa raia dhidi ya Rais. Hakika
Kamundu umenipa changamoto za kuibua hoja mbalimbali kwa faida ya nchi yetu.
Endelea na mikakati yako siku moja ukifanikiwa tukumbukane.
 

gunga yenna

Member
Apr 11, 2019
90
95
Gunga haya si mambo ya Ulaya wala USA vitu vyote nilivyosema hakuna ugumu wowote wa kufanya ukisoma vizuri. Mfamo kuruhusu uhuru ni jambo la Ulaya na USA? kuwekeza kwenye kilimo?, afya ni vitu ambayo vinafanyika. Ujue nchi nyingi za ASIA zilikuwa kama sisi miaka 35 iliyopita hizi nchi si za Ulaya. Mambo mengi magumu tunajitakiwa au hatuna tu mpangilio mzuri. Sasa Raisi kwanini ujali mitandao kama kweli unafanya kazi vizuri! huwezi kuwa unajali maneno. Maneno yanakuwa na tija pale tu ambako ni ya kweli
Watakao kupinga wapo wengi, Libya ilikuwa paradise leo nini kinatokea, nchi zetu hizi zinataka utawala wa mkono wa chuma kama China au Urusi ili watu wawe na akili, nikiangalia sana kuongoza hapa siasa iwe kidogo utendaji ufanyike kwa vitendo sio kwa maneno.
 

Kamundu

JF-Expert Member
Nov 22, 2006
3,329
2,000
Watakao kupinga wapo wengi, Libya ilikuwa paradise leo nini kinatokea, nchi zetu hizi zinataka utawala wa mkono wa chuma kama China au Urusi ili watu wawe na akili, nikiangalia sana kuongoza hapa siasa iwe kidogo utendaji ufanyike kwa vitendo sio kwa maneno.
Kwa mfano wako jiulize Ghadafi yuko wapi? Sudan vipi, Tunisia hakuna mtu asiyependa freedom na ujamaa umsshidwa tayari toka 1984 Nyerere alipoondoka
 

Nzengatumbi

Member
Jul 28, 2018
13
45
Mh. Rais nakusifu kwa kazi nzuri unayoifanya ya kuinua uchumi ni mzalendo no mmoja pamoja na kuwabana mafisadi na wahujumu uchumi vizuri natoa ushauri ili mizania ya uchmi ikae vizuri na haraka zaidi ili iwiane na kipato cha mwananchi basi liangazie wilayani kuja vijijini kwani huku hakujaguswa kiupotefu wa fedha kwani miradi mingi haina ukaguzi wa utekelezaji na ukaguzi wa fedha mtandao unamwaga fedha ambazo zinapigwa na viongozi wa vijiji kata na wilaya na hilo likiachiwa mizani ya uchumi haitafikia badala yake wanchi watalalama hali ngumu na kuongezewa mshahara kitu ambacho sio kizuri kimapato ushauri wangu ukaguzi wa fedha kila kijiji na miradi yote ilioko vijijini kama mfuko wa maji mfuko wa umwagiliaji n.k ili kuzuia fedha zinazotumi na wachache na kuyumbisha sarikali kwa kuhitaji ruzuku wakati miradi hiyo ingejiendesha yenyewe na kutoa gawio. Napongeza mashirika yanayotoa gawio ndio maana halisi ya miradi ya serikali ili kuinua kipato selikalini. Usiwashangae wanaobeza Reli au kununua ndege. Hawaelewi gawio au faida kupata serikali ilitokea bank ya taifa ilitoa gawio ikaleta mzozo na wengine walishanga na wengine waliwaona wafanyakazi wa Bank majuha hivo haikutoke tena kwa miradi ya selikali kuingiza faida bali kuomba fedha serikalini hadi awamu yako nakupongeza sana sana umenifanya nijisikie raha tuliyojifunza ueneshaji serkal kwa kodi na vyanzo vya mapato kwa miradi ya serikali wakati wa ujana wangu leo inafanyika asante mungu akupe maisha marefu na ukamilishe kazi ngumu amin
 

Nzengatumbi

Member
Jul 28, 2018
13
45
Nimeandika ushauri hu kwa rais ili aufanyie kazi husasan ukaguzi wa mapato kwa vijiji vyote na miradi iliyomo ukaguzi wa ndani . na ukaguzi wa nje ambao unafanywa na COASCO. Hakuna aliounga hoja lmani yangu kwamba wengi wetu uzalendo hatuna au sijaeleweka.
 
 • Thanks
Reactions: VMD

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
844
1,000
Tutateua sana...
Tutatengua sana...

Kwa mfano, kuna waziri aliteuliwa wakati wa sakata la korosho akiaminika kuwa atafanya vizuri, leo katenguliwa kwa sakata la wafanyabiashara hata kabla ya kufikisha miezi nane.

Mwishowe tutaona wote hawafai.
Suluhisho ni kuwa na Taasisi Imara na siyo Mtu Imara.

Na hii itapatikana kupitia KATIBA MPYA ya Watanzania. Serikali iliyo madarakani pia inahitaji katiba mpya, tukiendelea na katiba hii, tutateua sana, tutatengua sana lakini good achievement nduhu.
 

Gellangi

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
775
1,000
Tutateua sana...
Tutatengua sana...

Mwishowe tutaona wote hawafai.
Suluhisho ni kuwa na Taasisi Imara na siyo Mtu Imara.

Na hii itapatikana kupitia KATIBA MPYA. Serikali iliyo madarakani pia inahitaji katiba mpya, tukiendelea na katiba hii, tutateua sana, tutatengua sana lakini good achievement nduhu.
Suluhusho pekee Ni Katiba ya Watanzania,hizi teua/tengua hazisaidii na siyo sahihi.Kila ajaye atumie utashi wake kuendesha ofisi ya umma!
Lazima tutengeneze mfumo wa utawala unaowajibika kwa wananchi.Vinginevyo tusitegemee maendeleo kwa mfumo huu.
 

comred

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
1,875
2,000
Tutateua sana...
Tutatengua sana...

Mwishowe tutaona wote hawafai.
Suluhisho ni kuwa na Taasisi Imara na siyo Mtu Imara.

Na hii itapatikana kupitia KATIBA MPYA. Serikali iliyo madarakani pia inahitaji katiba mpya, tukiendelea na katiba hii, tutateua sana, tutatengua sana lakini good achievement nduhu.
Katiba mpya kwa watanzania wazamani au na wao wapya..Hizo tahasisi imara zitaundwa na watanzania gani kama sio hawa hawa..

Hatuitaji katiba mpya kwa sasa, iliyopo inatosha. Kiongozi mwenye maono ndie tunaitaji kwa sasa ndizo hizo taasisi zitapata watu wenyeweledi wakuzisuka..
 

comred

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
1,875
2,000
Tutateua sana...
Tutatengua sana...

Mwishowe tutaona wote hawafai.
Suluhisho ni kuwa na Taasisi Imara na siyo Mtu Imara.

Na hii itapatikana kupitia KATIBA MPYA. Serikali iliyo madarakani pia inahitaji katiba mpya, tukiendelea na katiba hii, tutateua sana, tutatengua sana lakini good achievement nduhu.
Katiba mpya kwa watanzania wazamani au na wao wapya..Hizo tahasisi imara zitaundwa na watanzania gani kama sio hawa hawa..

Hatuitaji katiba mpya kwa sasa, iliyopo inatosha. Kiongozi mwenye maono ndie tunaitajika kwa sasa ndizo hizo taasisi zitapata watu wenyeweledi wakuzisuka..
 
 • Thanks
Reactions: VMD
Top Bottom