Status
Not open for further replies.
Aachane na mambo ya kikosi kazi maalumu tofauti na vile vilivyo katika katiba aache kufuatilia maneno ya watu wanaomkosoa kwani maneno hayaui.Bashite anamharibia serikali yake
 
- Aache kuua watu
- Atoe ajira
- Aheshimu bunge na mahakama
- Aheshimu watumishi wa umma na awape haki zao
- Afuate sheria zilizopo na katiba hii hii kama mpya anaona haimfai
- Aache kutumia pesa za walipa kodi masikini kuhonga kina MTULIA badala yake atengeneze MFUKO wa kukopesha GRADUATES Wajasiriamali vijana na kina mama
- Awape uhuru mawaziri wake na aache kupenda kuabudiwa, na kuwafokea na kuwatukana hadharani
- Aache UBAGUZI
- Aache kuchukua wake za watu na aheshimu familia yake
- Aheshimu viongozi wa dini na wafanyabiashara
- Mwisho kama analipenda taifa hili ni bora AJIUZULU kwa kuwa kazi aliyoiomba kiukweli HAIWEZI. Uwezo wake ni mdogo, analazimisha tu

NI HAYO TU !
.
 
Wizara zote aondoe wazee wanaofanyakazi kwa mazoea aweke VIJANA WACHAPAKAZI

Asiwategemee maprofesa katika kazi zake maana niwasahaulifu,leo wakisema hivi kesho wanabadilika.Arejee maneno ya Mkumbo na Kabudi

Miaka ya kustaafu iwe 55 ili ajira zipatikane kwani kundi la vijana ndio nguvukazi kuu zaidi

Azingatie ushauri wa viongozi wa dini,ajue wanaona mbali pia ajue wapo karibu zaidi na wanajamii kuliko anavyodhani.Hii nikwasababu wanasiasa wanaenda kwa wananchi kwa majira na matukio maalum ila viongozi wa dini wanayajua maisha ya waumini wao kila siku

HERI YA PASAKA MH.RAISI TUNAKUTEGEMEA KWA MUSTAKABALI WA TAIFA
 
- Aache kuua watu
- Atoe ajira
- Aheshimu bunge na mahakama
- Aheshimu watumishi wa umma na awape haki zao
- Afuate sheria zilizopo na katiba hii hii kama mpya anaona haimfai
- Aache kutumia pesa za walipa kodi masikini kuhonga kina MTULIA badala yake atengeneze MFUKO wa kukopesha GRADUATES Wajasiriamali vijana na kina mama
- Awape uhuru mawaziri wake na aache kupenda kuabudiwa, na kuwafokea na kuwatukana hadharani
- Aache UBAGUZI
- Aache kuchukua wake za watu na aheshimu familia yake
- Aheshimu viongozi wa dini na wafanyabiashara
- Mwisho kama analipenda taifa hili ni bora AJIUZULU kwa kuwa kazi aliyoiomba kiukweli HAIWEZI. Uwezo wake ni mdogo, analazimisha tu

NI HAYO TU !
.
Avunje baraza la mawaziri na awachague wachaga wote kuwa mawaziri
Afute teuzi zote za makatibu wakuu, wakurugenzi na awachague wacha kujaza nafasi hizo
Wenyeviti wote wa bodi na wajumbe wake 2/3 wawe wachaga
Kama ilivyokuwa zamani awajaze TRA na babdari wachaga watupu
Alifute ATC na ndege zote awape Precision Air
Ajenge Bullet train kwenda Moshi..
Alifanye kabila la kichaga kuwa kabila bora Tanzania na Chief Mariale kuwa shujaa wa taifa hili na siyo msaliti....
 
Hilo hutu mwishowe litakuoa kabisa unakoelekea
 
Ninamtazama Mkuu wetu wa nchi na jinsi anavyosisitiza kuwa anatekeleza na namna ambavyo anaonesha bidii na juhudi katika kuitumikia Tanzania na watanzania.Kwa muda wote alokaa madarakani amejitahidi sana kufanya mambo mengi kwa wakti mmoja ila mimi binafsi bado naona kuna mambo inabidi ayafanyie kazi mapema sana.Mambo hayo ni pamoja na:
  1. Katiba Mpya:Huu mchakato ulikula pesa zetu,zaidi ulitatua kero nyingi sana.Nafikiri niwakati sasa wa kuileta katiba ya Warioba ama la basi waanze kuchukua vipengele vidogo vidogo vidogo waingize kwenye katiba ya sasa ili kuihuisha
  2. Jeshi la polisi:Ni wakati sasa kwa rais kuhakikisha kuwa Jeshi la polisi halitumiki vibaya kuwanyanyasa wale wanaomkosoa.Afahamu kuwa unyanyasaji unaofanyika unajenga chuki kisasi na zaidi inajinga hisia mbaya za matumizi mabaya ya madaraka
  3. Aandike kitabu:Kwa mwenendo wa uongozi wake na namna anavyfanya kazi nafikiri ni wakati sasa kwa mheshimiwa rais kutuandikia kitabu hata kama atatoa chapter 1ila wiki.Awaeleze watanzania kinaga kwamba nini maono yake kwa taifa ili historia imhukumu kwa usahihi
Nawakilisha
 
Katiba Mpya sio kipaumbele cha serikali yetu. Viwanda kwanza.
Sio kipaumbele cha serikali ila ni kipaumbele cha wananchi ambao hata hivo viwanda bado hawavioni vikiwatatulia kero zao na hata ukiwatazama kadiri siku zinavyokwenda wanazidi kukunja ndita na kuwa na sura ya ulizo na mashaka.Mkiwapa wananchi katiba mtaepusha hivo viwanda kuja kuharibiwa wakati wananchi wakidai katiba mpya kwa fujo.H
 
Maisha yakiboreshwa hakuna mwananchi atakuwa na hasira na serikali, na ndicho serikali ya JPM inafanya kuboresha maisha ya wananchi kwa kujenga barabara, reli, vyanzo vya umeme na viwanda.
 
kwani hujui yapi maono ya magufuli mkuu?,maono yake ni sawa na ya chama chake cha CCM kuona mafisadi kama akina LUGUMI wanaishi maisha ya kishetani.
 
Rais Magufuli kila siku unazindua vitu, ni sawa lakini unasahau kuwa vitu havijawahi kuleta furaha ya mtu.

Ili Watanzania wawe na furaha wanahitaji utu. Wape uhuru wa kukosoa, kupata habari, kujieleza na kutoa maoni bila hofu.

Wape uongozi wa kidemokrasia na diplomasia ukifahamu kuwa Tanzania ni nchi ya vyama vingi vya siasa. Hivyo uhuru wa mikutano ya siasa na maandamano ya amani ni haki ya wananchi kama ilivyoainishwa kwenye Katiba ya Tanzania.

Hata familia tajiri yenye baba dikteta haiwezi kuwa na furaha. Mwisho wa siku familia hiyo husambaratika na kupotea kabisa.
 
Msingi wa maendeleo ya mwanadamu yeyote unaanzia kwenye uhuru wake, ndio maana wakoloni weupe walitolewa siyo kwamba walikuwa hawaleti maendeleo la hasha! Bali walitolewa ili kuleta heshima na utu wa mwanadamu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom