Status
Not open for further replies.

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,886
109,218
Hii thread iwe Maalum kwa Maoni, Ushauri na Mapendekezo mbalimbali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Mimi namuomba, Mheshimiwa Rais mteuliwa, kwa heshima na taadhima hili ni ombi binafsi kwako.

Nnaomba uhakikishe huyu mrembo wa ACT Bi Anna Mghwira unamuingiza bungeni na unampa wadhifa anaostahiki, huyu mama ni kichwa adhyim na adim kabisa.

Nimemfatilia mikutano yake mingi sana ya kampeni, anatoa vitu kichwani utafikiri ana word processor inayopanga na kuchuja anachokizungumza kutoka kichwani bila kusoma.

Halikadhalika leo kanifurahisha sana alipostukizwa na kutoa hotuba pale Diamond, ilikuwa fupi na imelenga points zote nzuri na ameeleweka vyema kabisa.

Anna heko sana na nitakuunga mkono katika siasa zako.

Hali ya Kisiasa
Mgogoro wa Zanzibar ni jukumu lako kwa sasa halikwepeki. Tafuta wasuluhishi wawili (kutoka Bara na Visiwani) wakusaidie kulishughulikia hili
 
Ungemuomba atumie nguvu yake kusimamia haki

Mbagala wameporwa mbunge wao.

Kuna uchaguzi wa mameya wa majiji, asimamie haki walioshinda ndo wapewe.

yasije rudia ya manispaa ya Arusha mjini kuhusu uchaguzi wa meya hasa hapa Dar.
 
FaizaFoxy,

Kitufe cha like hakipo, nalazimika nikunukuu.

Ukumbi wa diamond jubilee ulikuwa kimya pale mama Mghwira aliposema tunataka katiba mpya kama kichocheo halali cha kuleta mabadiliko.

Hakika zile ndio siasa, siasa mpya. Huyu mama ametokea kupendwa ghafla.
 
Kila chama kilikuwa na ilani yake, sasa kusema ampe ubunge then cheo anachostahili Serikalini una maana gani? Je akiwa serikalini atakuwa anatekeleza ilani ipi kati ya ile ya ACT ya kwake na hii yenu ya CCM?
 
Kama nilivyompenda ghafla FaizaFoxy !!
 
Last edited by a moderator:
Kila chama kilikuwa na ilani yake, sasa kusema ampe ubunge then cheo anachostahili Serikalini una maana gani? Je akiwa serikalini atakuwa anatekeleza ilani ipi kati ya ile ya ACT ya kwake na hii yenu ya CCM?

Mbatia alipewa ubunge na mwenyekiti wa CCM alikuwa anatekeleza ilani ipi?
 
Kila chama kilikuwa na ilani yake, sasa kusema ampe ubunge then cheo anachostahili Serikalini una maana gani? Je akiwa serikalini atakuwa anatekeleza ilani ipi kati ya ile ya ACT ya kwake na hii yenu ya CCM?
Ilani zote zipo kwa ajili ya kumletea mtanzania maendeleo, hakuna zaidi ya hilo.
 
Kila chama kilikuwa na ilani yake, sasa kusema ampe ubunge then cheo anachostahili Serikalini una maana gani? Je akiwa serikalini atakuwa anatekeleza ilani ipi kati ya ile ya ACT ya kwake na hii yenu ya CCM?

Kwani Maalim Seif anatekeleza ilani ipi kama Makamu wa Rais wa Zanzibar?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…