Hivi vifaa vya kujengea nyumba za viongozi huwa vinanunuliwa wapi? Nyumba moja kugharimu milioni 838

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Sisi ghorofa zetu tunajenga kwa miliono 120-200 na zinapendeza na kukalika kwa kuji nafasi. Hawa viongozi hizi ghorofa zao huwa wananunulia vifaa wapi au gharama zinatokana na nini?
===

Mamilioni kujenga nyumba za wakuu wa wilaya na mikoa. Milioni 838 kumalizia nyumba ya mkuu wa mkoa Kagera, Milioni 170 kujenga uzio na nyumba ya mlinzi kwa mkuu wa wilaya Temeke. Milioni 555 kukarabati nyumba ya mkuu wa mkoa Ruvuma.


PIA SOMA:
-
Kakonko: Makusanyo kwa mwaka ni Tsh Milioni 539, lakini Ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya umetengewa Tsh milioni 700
 
Hapa kama ni sisi wananchi tungetumia laki tatu au nne.

IMG_20210328_095624.jpg
 
Sisi ghorofa zetu tunajenga kwa miliono 120-200 na zinapendeza na kukalika kwa kuji nafasi. Hawa viongozi hizi ghorofa zao huwa wananunulia vifaa wapi au gharama zinatokana na nini?

View attachment 1759477
Gharama zake zinatokana na manunuzi ya vifaa kwa kupitia channel ya manunuzi ya serikali! Pia consultants wana asilimia yao.

Hazijengwi kwa gharama kama ya nyumba zetu hizi tunazojenga kwa wajenzi wa kienyeji! Hivyo hata wewe ungejenga hilo ghorofa lako la mil.120-200 kwa taratibu za ujenzi wa nyumba za serikali ungechunwa kati ya mil. 300-500
 
Labda labda ipo hivi kwenye kila mfuko mmoja wa saruji wanafyatua tofari kumi na tano tu yaani ratio kali na udongo wa kujengea wanachanganya mfuko mmoja wa saruji kwa ndoo kumi ndogo za mchanga.

Materials ya kujengea hasa mchanga watakua wanatumia mchanga wa makinikia yale yaliokwama pale bandari. Mbao za kupaulia itakua wanatumia mvule au mninga au mkongo.

Bati nazo ukiachana na hizi Geji 32, 30 na 26 hawa watakua wanatumia bati za geji 16. Kuhusu finishing materials itakua wanainport kutoka kwa mabeberu.

Pumbavu sana hawa.
 
Ni mwanzo mzuri, ngoja tuone bajeti zijazo, nadhani ndio jinsi ya kuingiza pesa mtaani kama tulivyotaka. 838m kumalizia nyumba, 555m kukarabati na 170m kujenga uzio.

Nakumbuka nyumba ya Mhando wa Tanesco siku zile ilikarabatiwa kwa bilioni kadhaa.

Jumba la kifahari la Bakhresa limejengwa kwa USD 3m, kama bilioni 6 na pointi hivi, inawezekana hiyo inayomaliziwa kwa 838m itakuwa kama hiyo.

Kazi iendelee
 
Million 400 inatosha kujenga nyumba nzuri na ya kisasa (Kwa taifa ambalo halina uchumi thabiti), inakuwaje ukarabati utumie kiasi hiki? Ni wakati wa kuweka michoro na ramani rasmi ya miundombinu ya serikali hasa majengo.

Mahakama, ofisi za serikali, shule, nyumba za viongozi na watumishi, vituo vya polisi kila mkoa zinatakiwa kuwa sawa. Viongozi hawa wakumbuke ni watumishi wa wananchi kwa maana nyingine ni wawakilishi wa serikali.
 
Ni mwanzo mzuri, ngoja tuone bajeti zijazo, nadhani ndio jinsi ya kuingiza pesa mtaani kama tulivyotaka. 838m kumalizia nyumba, 555m kukarabati na 170m kujenga uzio....
Samahani! Hili jumba la Bakhresa limejengwa maeneo gani? Nisaidie picha kama zinapatikana.

Natarajia kujenga jengo na ukarabati wa mazingira at least kwa TZS Billioni 3 mambo yakikaa sawa.
 
Samahani! Hili jumba la Bakhresa limejengwa maeneo gani? Nisaidie picha kama zinapatikana.

Natarajia kujenga jengo na ukarabati wa mazingira at least kwa TZS Billioni 3 mambo yakikaa sawa.
Sikubahatika kupata picha, niliona video ya ndani na nje, parking ya magari na migari iliyopo, ni hatari na nusu, muhindi mmoja alishea.
 
Back
Top Bottom