Wanging'ombe: Watumishi wa Umma Mbaroni Wakiwa Kwenye Mchakato wa Kuuza Ultra Sound ya Serikali

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
42,857
49,553
Watumishi wezi kiasi hiki Huwa mnawatoa wapi?

--
Tamisemi.png

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Deogratius J. Ndejembi (Mb) amezindua jengo la Wagongwa mahututi (ICU) katika hospitali ya Wilaya Mpwapwa mkoani Dodoma.

Pia ametoa tafadhali na onyo kali kwa watumishi na wananchi wanaojihisusisha na wizi wa vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya kote nchini.

Mheshimiwa Ndejembi ameyasema hay oleo tarehe 03 Mei mwaka 2023 wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma wakati akizindua wa jengo jipya la Wagonjwa mahututi pamoja na vifaa tiba ambalo ni matokeo ya jitihada za Serikali ya awamu ya sita za kuboresha utoaji wa huduma za afya.

“Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea na kuboreshaji utoaji wa huduma za afya nchini ikiwa ni pamoja na Wilaya Mpwapwa ambapo imejenga Majengo pamoja na ununuzi wa vifaa tiba vya kidigital.”

Amesema Mkoa wa Dodoma umepokea zaidi ya Sh bilioni 1.15 kwa ajili ya ujenzi wa majengo matatu ya huduma za dharura katika wilaya za Kongwa, Bahi na Kondoa, ujenzi unaoenda sambamba na ununuzi wa vifaa tiba vya thamani ya Sh bilioni 1.58.

Aidha, Ndejembi ametoa onyo na tahadhali kwa wizi wa vifaa tiba ambao umekuwa ukijitokeza katika vituo vya kutolea huduma za afya ikiwemo tukio la wiki iliyopita la watumishi wa kituo cha afya katika wilaya Wanging’ombe.

Katika tukio hilo, watumishi wamekamatwa kwa wizi wa “Ultraound” nyenye thamani ya milioni 75 wakiwa wanaiuza mkoani Dar es Salaam.

Ndejembi amewataka Watumishi na Wasimamizi wa huduma za afya kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa Wananchi ili kutimiza lengo la Serikali la kutoa fedha za kujenga majengo na kununua vifaa vya kisasa na kidigitali ili kuboresha utoaji wa huduma.

Kwa Upande wake, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI (Afya), Dkt. Wilson Mahera amewata watumishi na wasimamizi wa huduma za afya kuhakikisha wanatunza majengo na vifaa tiba ambayo vimenunuliwa kwa gharama kubwa ili kutoa huduma bora na nzuri kwa wananchi.

“Viongozi wa wilaya kuweni makini maana kuna baadhi watumishi wanachonga funguo na kuiba.

Chanzo: ORTAMISEMI
 
Watumishi wezi kama hawa ni wa kufukuzwa kazi na utumishi bila kulipwa senti hata moja japo watakuwa wanaangamiza familia zao kwa kukosa mishahara ya kuwahudumia kimaisha. Unaajiriwa halafu unakuwa mwizi bila haya hustahili kuendelea na ajira
 
Back
Top Bottom