Shaka apiga kombora ofisi za Wakuu wa Wilaya na Mikoa

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
SHAKA H SHAKA, KATIBU KATIBU WA ITIKADI AMEZUNGUMZA HOJA NZURI SANA.

Na Elius Ndabila
0768239284

Leo nikiwa nimekaa mahali ninapumzika lilinijia wazo moja. Wazo langu lilifanana Kwa kiasi na wazo la Shaka, lakini Mimi nilienda Mbali zaidi.

Nilijiuliza hivi, kazi ya Viongozi wa CCM ngazi za Mkoa na Matawi ni kuisimamia Serikali tu na kupongeza? Nilienda mbali nikajiuliza siku hizi hata kuisimamia serikali ni maeneo machache sana, wengi wanatumia muda kupongeza.

Niliendelea kujiuliza, hivi viongozi wa mikoa mpaka matawi wangekuwa wanatumia muda mwingi kuwaelimisha Wananchi namna serikali ya CCM inavyofanya kazi, je Viongozi wa juu wasingepumua? Nilijiuliza kwa nini Chama kinaajiri watu Bubu na Wanachama kuchagua watu Bubu wasioweza kusema mazuri yanayofanywa?

Uhalisia ni kuwa binadamu ana hulka ya kusahau. Hata tunaposoma darasani unatakiwa kusoma kitu hata mara kumi ili kikae kichwani. Ukisoma mara Moja kinapotea. Hivyo hivyo Kwa mafanikio ya CCM na Serikali yake, hupaswi kuwaambia Wananchi mara Moja. Ukiwaambia mara Moja akaja mtu mwingine akawapotosha wanasahau ulichowaambia wanakumbuka kipya.

Leo Katibu Shaka amesikitishwa na MaDC na MaRC,s Kwa kushindwa kuzungumza mema yanahofanywa na serikali ya CCM. Kama ni bakora amewachapa kwenye wakiwa wamelowa na kumwagiwa pilipili na chumvi mwilini.

Haiwezekani kila jambo wanatakiwa kulisemea tu viongozi wa Kitaifa na Viongozi wengine kuishia kwa kibwagizo Cha ANAUPIGA MWINGI. Huu ni uvivu! Akisema Rais, Waziri au Viongozi wa juu wa Chama basi viongozi mnaobaki mnatakiwa kushuka chini kwenye kaya kuzungumza na kutoa Elimu.

Wananchi zaidi ya 60% hawasomi Twitter, hawasimi Instagram, hawasomi Facebook wala JF. Wanahitaji kwenda kuzungumza nao na kuwaambia kinachofanyika.

Ukifanya research, hata viongozi wachache wanaojaribu kufanya utakuta kama wanaigiza. Wengi wanatunia vyombo vya habari kufubaza ukweli aliozungumza Shaka. Mtu anajaza camera kuliko KAZI.

Kule vijijini Wananchi hawajui kama Serikali ilitoa milioni 500 kila Wilaya. Wananchi hawajui vyumba vya madarasa vimetoka wapi. Wananchi hawajui vituo vya afya pesa imetoka wapi? Wananchi hawajui mkopo wa riba nafuu tulipata shilingi ngapi na zimefanya nini? Wananchi hawajui ni Wafanya KAZI wangapi wamepandishwa madaraja? Wananchi hawajui Kwa nini mradi wa umeme wa Nyerere utakamilika mwaka 2024? Wananchi hawajui tozo ya miamala inaenda wapi? Bado Wananchi wanashangaa, kwa nini umeme unakatakata? Kwa nini maji yanakata kata? Je, mwaka mmoja wa Rais Samia amefanikiwa kwa kiasi gani? Hawaishii hapo, Mimi kuna siku nimeulizwa Mbona kuna watu wanapita huku Nsalala Mbalizi na wanasema wanapima ardhi na kuweka jiwe moja( tunashare) watu wawili? Nilikosa majibu.

Ukweli tunatakiwa kusema mara Kwa mara kazi zinazofanyika. Na tunatakiwa kwenda zaidi vijijini kuliko mjini ambako wanataza TV wanasoma na mitandaoni.

Tunaposema Mama anaupiga mwingi, Wananchi wanataka kujua huo mwingi ni upi?

Ninawapongeza Wafanyakazi leo habari yenu imefika Dunia yote kwa muda mfupi kwa kuwa jambo lenu hamjasubiria kusemewa. Hongera Katibu wetu Shaka Kwa Uwazi, Uzalendo na Ujasiri. Inawezekana mshangao wako utakutengenezea maadui, lakini umetimiza wajibu wa Uongozi na utasubiria matokeo.
 
Back
Top Bottom