Chama cha walimu Tanzania ni cha walimu wenyewe

HaMachiach

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
3,399
6,077
Kuna mengi yanasemwa kuhusu chama cha walimu na isivyo bahati kati ya hayo mengine ni hasi. Siku ya mei mosi 2023 katika uwanja wa Jamhuri Morogoro wale wenye hasi wangeweza kujibiwa na wimbo wa Dar es salaam Jazz Band uliorekodiwa tarehe 8 Oktoba 1965 RTD ukisema We mtoto acha kupiga mayowe, acha watu waone wenyewe. Kabla ya mei mosi mengi yalisemwa kuhusiana na Tshirts na mengi yakazushwa kwamba hizo Tshirts fedha zake zimeliwa kwa sababu ya uzoefu mdogo walionao viongozi walioko madarakani na ufisadi na kwamba hazitokuwepo wakati wa meimosi. Wale mliofanikiwa kuangalia runinga na mliosikiliza redio ulikuwepo ushahidi dhahiri kwamba walimu ndio waliopendezesha ile siku kwa sababu kwanza ndicho chama kikubwa cha wafanyakazi chenye wanachama wengi lakini pia ni moja ya vyama vya wafanyakazi kwa sasa chenye uadilifu mkubwa. Mei Mosi iliyopita wakati wa uongozi wa Deus Seif na Abubakari Alawi zilitengenezwa Tshirts bila kofia 106,012 kati ya 285,000 ambapo zilitumika takribani shilingi Bilioni 5, wanachama wengi hawakupata Tshirt wala kofia. Mwaka huu zimechapishwa zaidi ya Tshirt 285,000 ili wapatiwe wanachama walioongezeka na wadau mbalimbali kwa chini ya shilingi Bilioni 4. Nikweli kwamba siku ya mei mosi mikoa michache ilipata upungufu mdogo wa Tshirt. Vyanzo vetu vilibaini kwamba tarehe 29 isivyo bahati mtandao wa TRA ulikua chini ilipofika jumanne tarehe 3 kila mwanachama wa CWT nchini pamoja na wadau walikua wamepata Tshirts, kofia na kwa mara ya kwanza walipata skafu. Isisahaulike pia kwamba Tshirts za mwaka jana zilikua na skendo ya ubadhirifu, kwanza zilikuwa chache sana, hazikuwa za kiwango na zilipatikana kwa mkopo wa shilingi Bilioni 5 bila kuhesabu riba uliokiumiza sana chama. Inapaswa kuupongeza Uongozi wa sasa kwa kufanya yafuatayo.

Uongozi umenunua Tshirts zilizojitosheleza bila mkopo, wameendesha mikutano mikuu miwili ya lazima kwa mujibu wa katiba kila mkutano ukiwa na wajumbe zaidi ya 1,000, mwezi disemba 2022 jijini Dodoma na mwezi februari 2023 jijini Tanga bila mkopo ambapo kwa wakati wa Deus na Alawi mishahara ya wafanyakazi ilikuwa inalipwa kwa overdraft na riba ilikuwa ni milioni 20 kila mwezi hivyo kwa miezi 12 chama kilikuwa kinapoteza shilingi milioni 240. Leo hii uongozi uliopo unaweza kulipa mishahara na ziada inabaki kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli nyingine za chama bila kukopa. Hivi fedha kiasi hiki ambazo zilikuwa ni faida ya benki zingeweza kununua madawati mangapi kwa wanafunzi au kujenga madarasa mangapi? Kama MCB kufaidika na chama cha walimu inafaidika na mengi.

  1. Hundi ya makato ya asilimia 2 ya kila mwalimu kutoka hazina kwenda kwa chama cha walimu kiwango tunakihifadhi inapitia MCB
  2. Mishahara yote ya wafanyakazi wa chama cha walimu zaidi ya 600 hupitia MCB
  3. Posho zote za viongozi wa chama ngazi ya wilaya, mikoa na taifa hupitia MCB
  4. Ruzuku zote za chama(15% wilayani na 8% mikoani) kwa wilaya zote na mikoa yote hupitia MCB
  5. Mikopo mingi ya walimu iko MCB
  6. kiwango cha shilingi bilioni 3 cha mishahara ya walimu wanaoghilibiwa na MCB kupitia kwa Jackson Joseph Gahima (ambaye ameshastaafu CWT mwenye lugha ya kitapeli kwa walimu) zinapitia MCB
Huko kote chama kinapata riba ndio maana Deus Gracewell Seif hata baada ya kufungwa alibaki kuwa mmoja ya wakurugenzi wa benki hii hadi leo huku Mtendaji Mkuu wa MCB hajathubutu kumtoa hapo ambapo kwenye congress ya MCB mwaka jana 2022 jijini Mbeya alisema ni wajibu wa BOT kufanya hivyo. Deus Gracewell Seif anapata posho ya ukurugenzi mpaka leo hata wakati akiwa mfungwa.

Hivi sasa kuna baadhi ya watu ambao wanaendelea kuihujumu CWT na ni jukumu letu kuwabainisha.
  1. Evod Kanyayangio. Kwa sasa ni Katibu wa CWT Bukoba Manispaa aliyeandika demand note ya kumtaka ndugu Japhet Maganga Katibu mkuu CWT aondoke ofisini kabla hajampeleka Mahakamani cha kujiuliza ni kwamba amepata wapi ujasiri wa kuandika demand note hiyo wakati ambpo chama kiko vizuri? Jambo la kwanza, wakati wa kesi ya Deus Seif na Abubakari Alawi fedha za rushwa zilipitishiwa kwenye mikoa na wilaya ambazo mafisadi hao walikuwa na ushawishi, na makatibu walilazimika kuzichukua fedha hizo bila proper documentation na kumkabidhi Deus. Jane Shoo Katibu wa Ubungo alitoa kwenye akaunti ya chama shilingi milioni 6 akamkabidhi Deus na baadae akazilipa kwa kutumia fedha zake mwenyewe. Mwingira katibu wa ilala alitoa shilingi milioni 25 na kumkabidhi Deus, haijulikani kama amekwishazirejesha ama hapana na baadae mwekahazina wa CWT ilala Masoli alitoa milioni 20 na sakata lake liko TAKUKURU ambao hadi leo wamelinyamazia. Wilaya ya Kinondoni katibu Evod Kanyayangio alitoa shilingi milioni 6 ambapo baada ya kuhamishiwa Bukoba alipobanwa na TAKUKURU alichukua mkopo wa Milioni 6 MCB ili kufidia fedha alizowapa Deus seif na Abubakari Alawi. Kwa Mujibu wa Salary Slip ya mshahara wa Evod uliotoka tarehe 29 Aprili 2023 Evodi alipata shilingi 270,000 na ndio maana kule wilayani kwake amekuwa akifanya ziara peke yake katika shule mbalimbali na kujilipa posho kutoka kwenye fungu la OC huku wanachama wake wakiendelea kupungua ili aweze kuishi na amepanga nyumba kwa mjumbe wa kamati ya CWT mkoa wa Kagera ambaye sasa ndiye anayemtetea na kuivuruga kamati ya utendaji ya CWT manispaa ya Bukoba.
Je wanaompa ujasiri wa kupambana na uongozi wa CWT ni nani? Na kwa nini? Ninaomba hapa niwabainishie mmoja baada ya mwingine nikibainisha kwamba Evod ni Scapegoat (Mbuzi wa zazeli) Lengo ni kuutikisa uongozi wa taifa uliopo madarakani ambao kwa sasa umeleta matumaini mapya kwa walimu.

  1. Alhaj Mohamed Utaly aliwahi kuwa mwekahazina wa taifa wakati huo kulitokea ajira CWT akaighilibu kamati ya utendaji ya taifa ikaajiri michepuko yake yote miwili wa kwanza Irene Mrabu na Christina Francis Mwezi. Irene Urabu aliajiriwa kama afisa ugavi na manunuzi wakati Christina Mwezi aliajiriwa kama msaidizi wa mkaguzi wa hesabu za ndani (Assistant Internal Auditor). Utaly ilibidi kufunga ndoa na Christina Mwezi kwa sababu yeye alimpiku Irene kukubali kubadili dini ili apate mume na akaitwa Balkis. Hatua ya kumpata Balkis ilimsaidia sana kwa sababu kwa mbinu zake alimpandisha kuwa mhasibu mkuu wa chama wakafanikiwa kumsaidia Utaly kifedha kugombea ubunge jimbo la Lindi Mjini, kujenga jumba la kifahari eneo la Kifuru Dar es salaam, Kujenga Jumba la kifahari Dodoma, na kupitia Deus familia ilipata fedha za kwenda kumpandikiza Balkis mimba ya mapacha nchini Uganda kwa gharama ya shilingi Milioni 300 tunamshukuru Mungu mapacha wapo mpaka leona Mungu aendelee kuwalinda, Christina kwa ushirikiano na Deus alikuwa na fedha za kutosha kabla Utaly hajapata huruma ya Mama ya kumpatia ajira ya uhasibu idara ya uhasibu wizara ya elimu makao makuu. Utaly amekuwa akikipiga vita chama cha walimu, hapa kuna mifano mitatu. i) Siku ya kufariki kwa Batholomeo Chilwa, Chilwa alikwenda baa ya carnival Dodoma kuchukua fedha kwa Deus ambazo aliwatumia waandishi mbalimbali wa habari waliofanikisha kuripoti kwamba uongozi wa CWT ulikiuka zuio la mahakama. Baada ya kuwatumia waandishi wa habari fedha kwa simu alikwenda kwa Utaly ili yeye na mke wa Utaly wampe mbinu za mapambano katika kuuchafua uongozi na chama. Baada ya kutoka hapo kumbe mwenyezi Mungu kapanga lake Chilwa aliigonga treni akafariki (ii)Wakati wa Mazishi walikuwepo Leah Ulaya rais wa CWT na Japhet Maganga katibu mkuu CWT. Cha kushangaza Utaly alimtambulisha Deus Gracewell Seif kama katibu mkuu wa CWT (iii) Utaly katika taarifa yake kanisani aliushutumu uongozi wa CWT kuwa chanzo cha kifo cha Chilwa kwa sababu eti kabla ya kifo cha Chilwa katibu mkuu Maganga alimuandikia Chilwa barua ya kujieleza ni kwa nini aliitisha mkutano wa vyombo vya habari kwenye ukumbi ghorofa ya pili kwenye ukumbi wa CWT Dodoma bila taarifa yake, kwa mujibu wa Utaly barua hiyo ilimpatia Chilwa wendawazimu wa muda (insanity) uliosababisha kifo chake.
  2. Christina Francis Mwezi aliyeajiriwa kama mkaguzi wa hesabu wa ndani msaidizi akamahamishiwa kampuni tanzu ya chama (Teachers Development Company Limited na baadae akahamishiwa CWT makao makuu kama mhasibu mkuu. Alifanya yafuatayo (i) Baada ya TAKUKURU kunusa ufisadi mwingi CWT ikiwemo safari ya Deus Seif na Abubakari Alawi kutumia fedha za walimu kwenda kuangalia mechi ya mpira kati ya Taifa Stars na Cape Verde nchini Cape Verde, Christina Francis Mwezi aliwanyima TAKUKURU vielelezo vyote kwa ajili ya safari hiyo na akatamba kwamba hawana nakala halisi na huwa TAKUKURU huwa hawashindi kesi. (ii) Katika wizi wao alipewa kinyemela milioni 270 ili kuwezesha jambo lililokwisha kubainishwa hapo awali (iii) aliandikiwa barua na katibu mkuu Japhet Maganga kuhamia kwenye kampuni ya maendeleo ya walimu akakataa uhamisho huo kwa barua kinyume na Kanuni za CWT ambapo Katibu Mkuu anayo mamlaka ya kumhamisha mtumishi yeyote wa chama kadiri anavyoona inafaa. Christina alikataa uhamisho huo kwa barua hadi sasa ni miezi 5 analipwa mshahara bila ya kuwa kazini. Alhaji Utaly anatambua kwamba ni marufuku kwa Muislamu kula fedha ya haramu. Yeye anaishi kwa fedha ya haramu, Mungu wake anajua pepo yake itakavyokuwa ila lazima ajue kesho kuna moto kwa kula vya haramu vikiwepo zizi la ng’ombe alilopewa na wamasai wa Mvomero alipokuwa mkuu wa Wilaya ili awakandamize wakulima na alifanya hivyo.
  3. Queen Augustino Luvanda, huyu pia anamdanganya Evod kwa sababu yeye alikuwa mwanasheria wa Geita, Deus akampatia ajira CWT akawa na mkataba wa likizo bila malipo na Deus akampa mkataba wa ajira ya kudumu CWT. Hivi kwa nini mkurugenzi wa Geita halioni hili na Queen anamshauri vibaya Evod kwa sababu yeye mwenyewe baada ya kupata changamoto ya uzazi wa pili ajira yake iko kwenye utata, Mkurugenzi wa Geita analijua hili alishamuandikia barua ya kurudi kazini japo wanajaribu kulizima kwa hila.
  4. Stella Kiabo na Stella Mamoto hawa wanamshauri vibaya Evod, hawa wana janga lao, kwa kuwa hawakuingia CWT kihalali wao walikuwa wajumbe wa kamati ya utendaji ya taifa ambao kwa mujibu wa katiba ya CWT kamati hiyo ndio mwajiri; katika kikao chao cha Mwanza cha 2018 kamati iliamua yafuatayo (1) Kuwashusha madaraka maafisa waandamizi wa CWT makao makuu Prosper Lubuva, Mwandile Kiguhe, Simon Keha na Dagobath Deogratius Tigalioma(marehemu). Kamati hiyo hiyo iliwateua wajumbe wa kamati hiyo hiyo Stella Kiabo kuwa mkuu wa idara ya elimu na mafunzo nafasi iliyokuwa ya Prosper Lubuva na Stella Obeid Mamoto kuwa mkuu wa idara ya wanawake na jinsia iliyokuwa ya Mwandile Kiguhe. Hawa hawawezi kuwa washauri wazuri wa Evod kwa sababu hawapo kihalali ni hii ni dhambi ya kamati ya utendaji ya taifa kwa sababu wanajua ili mtumishi kuajiriwa makao makuu kuna utaratibu gani.

CWT kwa sasa imekaa vizuri, ingefanya vibaya ukweli ungedhihiri wangechemka na hata wakichemka tutawasema waziwazi. Tunaomba siasa za majitaka ziishe, Ni vizuri kubainisha ni nani marafiki wa chama na ni nani sio marafiki wa chama wa nje na ndani. Tunafahamu viongozi wa juu wa kisiasa na wale wa serikali kupitia Deus Seif na Abubakari Alawi wamekuwa wakifaidika na fedha za walimu. Tafakarini Chukueni Hatua.
 
CWT pumbavu nyie mnatuibia sana ila basi mnatukandamiza walimu benki mmeanzisha hata haitusaidii hata hamfikiri endeleeni Kula vya sisi wajinga ila KISUKARI inawasubili
 
CWT sio Mali ya walimu,ni mali ya viongozi WA Cwt na CCM.CWT inafanya kazi kwa manufaa ya viongozi wake,na kwa manufaa ya ccm.Hiki chama Kiko compromised na ccm na mifumo yake na hakifurukuti tena.
Kwa sasa kimepoteza hadhi ya chama cha wafanyakazi.Hata baadhi ya viongozi wa chama hiki ni makada na Wana uongozi tena ndani ya ccm.HUU NI UKWELI MCHUNGU AMBAO CWT HAMTAKI KUUSIKIA.Uwezo wenu wa kutetea masilahi ya walimu umepotea,mmebaki kutetea matumbo yenu tu.
 
Walimu waishukuru serikali kwa kuruhusu kuwepo chama kingine cha chakuhawata ambacho kinakata ada ya uanachama kwa kiwango cha aina moja tsh 5000 pasipo kujali mshahara wako basic ni shilingi ngapi.Hao siwitiii wanakata mishahara ya walimu wetu kwa asilimia 2 ya basic hali iliyosababisha variation isiyo na sababu.Huyo anayekatwa hela nyingi anapata nini cha ziada kutoka kwenye chama ukilinganisha na yule anayekatwa kidogo?Cwt msipobadilika miaka miwili ijayo mtabaki historia

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna chama chochote cha wafanyakazi nchini chenye kubeba maslahi ya wafanyakazi - sio CWT, TPAWU.

Ila walimu wetu ni wa kuonea huruma kweli, unyonge, woga na ujinga wao unasikitisha mno.
 
CWT sio Mali ya walimu,ni mali ya viongozi WA Cwt na CCM.CWT inafanya kazi kwa manufaa ya viongozi wake,na kwa manufaa ya ccm.Hiki chama Kiko compromised na ccm na mifumo yake na hakifurukuti tena.
Kwa sasa kimepoteza hadhi ya chama cha wafanyakazi.Hata baadhi ya viongozi wa chama hiki ni makada na Wana uongozi tena ndani ya ccm.HUU NI UKWELI MCHUNGU AMBAO CWT HAMTAKI KUUSIKIA.Uwezo wenu wa kutetea masilahi ya walimu umepotea,mmebaki kutetea matumbo yenu tu.
Hao Tucta nao watu wa ovyo sana siku ya mei mosi juzi walishindwa hata kutanua mdomo kuwasemea wazee wetu kuhusu machungu ya kikokotoo .Hizi lawama siwitiii hamzikwepi kwa sababu nyie ndio wenye wanachama wengi zaidi kwenye shirikisho ila mnashindwa kuwasilisha hiyo hoja Tucta kwa sababu waanzilishi wa kwamba watumishi walipwe mafao kiduchu ya asilimia 25 ni nyie mpaka serikali ikawashangaa na kuwaonea huruma watumishi kwa kuongeza 8.3% ikawa 33.3

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Kuna mengi yanasemwa kuhusu chama cha walimu na isivyo bahati kati ya hayo mengine ni hasi. Siku ya mei mosi 2023 katika uwanja wa Jamhuri Morogoro wale wenye hasi wangeweza kujibiwa na wimbo wa Dar es salaam Jazz Band uliorekodiwa tarehe 8 Oktoba 1965 RTD ukisema We mtoto acha kupiga mayowe, acha watu waone wenyewe. Kabla ya mei mosi mengi yalisemwa kuhusiana na Tshirts na mengi yakazushwa kwamba hizo Tshirts fedha zake zimeliwa kwa sababu ya uzoefu mdogo walionao viongozi walioko madarakani na ufisadi na kwamba hazitokuwepo wakati wa meimosi. Wale mliofanikiwa kuangalia runinga na mliosikiliza redio ulikuwepo ushahidi dhahiri kwamba walimu ndio waliopendezesha ile siku kwa sababu kwanza ndicho chama kikubwa cha wafanyakazi chenye wanachama wengi lakini pia ni moja ya vyama vya wafanyakazi kwa sasa chenye uadilifu mkubwa. Mei Mosi iliyopita wakati wa uongozi wa Deus Seif na Abubakari Alawi zilitengenezwa Tshirts bila kofia 106,012 kati ya 285,000 ambapo zilitumika takribani shilingi Bilioni 5, wanachama wengi hawakupata Tshirt wala kofia. Mwaka huu zimechapishwa zaidi ya Tshirt 285,000 ili wapatiwe wanachama walioongezeka na wadau mbalimbali kwa chini ya shilingi Bilioni 4. Nikweli kwamba siku ya mei mosi mikoa michache ilipata upungufu mdogo wa Tshirt. Vyanzo vetu vilibaini kwamba tarehe 29 isivyo bahati mtandao wa TRA ulikua chini ilipofika jumanne tarehe 3 kila mwanachama wa CWT nchini pamoja na wadau walikua wamepata Tshirts, kofia na kwa mara ya kwanza walipata skafu. Isisahaulike pia kwamba Tshirts za mwaka jana zilikua na skendo ya ubadhirifu, kwanza zilikuwa chache sana, hazikuwa za kiwango na zilipatikana kwa mkopo wa shilingi Bilioni 5 bila kuhesabu riba uliokiumiza sana chama. Inapaswa kuupongeza Uongozi wa sasa kwa kufanya yafuatayo.

Uongozi umenunua Tshirts zilizojitosheleza bila mkopo, wameendesha mikutano mikuu miwili ya lazima kwa mujibu wa katiba kila mkutano ukiwa na wajumbe zaidi ya 1,000, mwezi disemba 2022 jijini Dodoma na mwezi februari 2023 jijini Tanga bila mkopo ambapo kwa wakati wa Deus na Alawi mishahara ya wafanyakazi ilikuwa inalipwa kwa overdraft na riba ilikuwa ni milioni 20 kila mwezi hivyo kwa miezi 12 chama kilikuwa kinapoteza shilingi milioni 240. Leo hii uongozi uliopo unaweza kulipa mishahara na ziada inabaki kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli nyingine za chama bila kukopa. Hivi fedha kiasi hiki ambazo zilikuwa ni faida ya benki zingeweza kununua madawati mangapi kwa wanafunzi au kujenga madarasa mangapi? Kama MCB kufaidika na chama cha walimu inafaidika na mengi.

  1. Hundi ya makato ya asilimia 2 ya kila mwalimu kutoka hazina kwenda kwa chama cha walimu kiwango tunakihifadhi inapitia MCB
  2. Mishahara yote ya wafanyakazi wa chama cha walimu zaidi ya 600 hupitia MCB
  3. Posho zote za viongozi wa chama ngazi ya wilaya, mikoa na taifa hupitia MCB
  4. Ruzuku zote za chama(15% wilayani na 8% mikoani) kwa wilaya zote na mikoa yote hupitia MCB
  5. Mikopo mingi ya walimu iko MCB
  6. kiwango cha shilingi bilioni 3 cha mishahara ya walimu wanaoghilibiwa na MCB kupitia kwa Jackson Joseph Gahima (ambaye ameshastaafu CWT mwenye lugha ya kitapeli kwa walimu) zinapitia MCB
Huko kote chama kinapata riba ndio maana Deus Gracewell Seif hata baada ya kufungwa alibaki kuwa mmoja ya wakurugenzi wa benki hii hadi leo huku Mtendaji Mkuu wa MCB hajathubutu kumtoa hapo ambapo kwenye congress ya MCB mwaka jana 2022 jijini Mbeya alisema ni wajibu wa BOT kufanya hivyo. Deus Gracewell Seif anapata posho ya ukurugenzi mpaka leo hata wakati akiwa mfungwa.

Hivi sasa kuna baadhi ya watu ambao wanaendelea kuihujumu CWT na ni jukumu letu kuwabainisha.
  1. Evod Kanyayangio. Kwa sasa ni Katibu wa CWT Bukoba Manispaa aliyeandika demand note ya kumtaka ndugu Japhet Maganga Katibu mkuu CWT aondoke ofisini kabla hajampeleka Mahakamani cha kujiuliza ni kwamba amepata wapi ujasiri wa kuandika demand note hiyo wakati ambpo chama kiko vizuri? Jambo la kwanza, wakati wa kesi ya Deus Seif na Abubakari Alawi fedha za rushwa zilipitishiwa kwenye mikoa na wilaya ambazo mafisadi hao walikuwa na ushawishi, na makatibu walilazimika kuzichukua fedha hizo bila proper documentation na kumkabidhi Deus. Jane Shoo Katibu wa Ubungo alitoa kwenye akaunti ya chama shilingi milioni 6 akamkabidhi Deus na baadae akazilipa kwa kutumia fedha zake mwenyewe. Mwingira katibu wa ilala alitoa shilingi milioni 25 na kumkabidhi Deus, haijulikani kama amekwishazirejesha ama hapana na baadae mwekahazina wa CWT ilala Masoli alitoa milioni 20 na sakata lake liko TAKUKURU ambao hadi leo wamelinyamazia. Wilaya ya Kinondoni katibu Evod Kanyayangio alitoa shilingi milioni 6 ambapo baada ya kuhamishiwa Bukoba alipobanwa na TAKUKURU alichukua mkopo wa Milioni 6 MCB ili kufidia fedha alizowapa Deus seif na Abubakari Alawi. Kwa Mujibu wa Salary Slip ya mshahara wa Evod uliotoka tarehe 29 Aprili 2023 Evodi alipata shilingi 270,000 na ndio maana kule wilayani kwake amekuwa akifanya ziara peke yake katika shule mbalimbali na kujilipa posho kutoka kwenye fungu la OC huku wanachama wake wakiendelea kupungua ili aweze kuishi na amepanga nyumba kwa mjumbe wa kamati ya CWT mkoa wa Kagera ambaye sasa ndiye anayemtetea na kuivuruga kamati ya utendaji ya CWT manispaa ya Bukoba.
Je wanaompa ujasiri wa kupambana na uongozi wa CWT ni nani? Na kwa nini? Ninaomba hapa niwabainishie mmoja baada ya mwingine nikibainisha kwamba Evod ni Scapegoat (Mbuzi wa zazeli) Lengo ni kuutikisa uongozi wa taifa uliopo madarakani ambao kwa sasa umeleta matumaini mapya kwa walimu.

  1. Alhaj Mohamed Utaly aliwahi kuwa mwekahazina wa taifa wakati huo kulitokea ajira CWT akaighilibu kamati ya utendaji ya taifa ikaajiri michepuko yake yote miwili wa kwanza Irene Mrabu na Christina Francis Mwezi. Irene Urabu aliajiriwa kama afisa ugavi na manunuzi wakati Christina Mwezi aliajiriwa kama msaidizi wa mkaguzi wa hesabu za ndani (Assistant Internal Auditor). Utaly ilibidi kufunga ndoa na Christina Mwezi kwa sababu yeye alimpiku Irene kukubali kubadili dini ili apate mume na akaitwa Balkis. Hatua ya kumpata Balkis ilimsaidia sana kwa sababu kwa mbinu zake alimpandisha kuwa mhasibu mkuu wa chama wakafanikiwa kumsaidia Utaly kifedha kugombea ubunge jimbo la Lindi Mjini, kujenga jumba la kifahari eneo la Kifuru Dar es salaam, Kujenga Jumba la kifahari Dodoma, na kupitia Deus familia ilipata fedha za kwenda kumpandikiza Balkis mimba ya mapacha nchini Uganda kwa gharama ya shilingi Milioni 300 tunamshukuru Mungu mapacha wapo mpaka leona Mungu aendelee kuwalinda, Christina kwa ushirikiano na Deus alikuwa na fedha za kutosha kabla Utaly hajapata huruma ya Mama ya kumpatia ajira ya uhasibu idara ya uhasibu wizara ya elimu makao makuu. Utaly amekuwa akikipiga vita chama cha walimu, hapa kuna mifano mitatu. i) Siku ya kufariki kwa Batholomeo Chilwa, Chilwa alikwenda baa ya carnival Dodoma kuchukua fedha kwa Deus ambazo aliwatumia waandishi mbalimbali wa habari waliofanikisha kuripoti kwamba uongozi wa CWT ulikiuka zuio la mahakama. Baada ya kuwatumia waandishi wa habari fedha kwa simu alikwenda kwa Utaly ili yeye na mke wa Utaly wampe mbinu za mapambano katika kuuchafua uongozi na chama. Baada ya kutoka hapo kumbe mwenyezi Mungu kapanga lake Chilwa aliigonga treni akafariki (ii)Wakati wa Mazishi walikuwepo Leah Ulaya rais wa CWT na Japhet Maganga katibu mkuu CWT. Cha kushangaza Utaly alimtambulisha Deus Gracewell Seif kama katibu mkuu wa CWT (iii) Utaly katika taarifa yake kanisani aliushutumu uongozi wa CWT kuwa chanzo cha kifo cha Chilwa kwa sababu eti kabla ya kifo cha Chilwa katibu mkuu Maganga alimuandikia Chilwa barua ya kujieleza ni kwa nini aliitisha mkutano wa vyombo vya habari kwenye ukumbi ghorofa ya pili kwenye ukumbi wa CWT Dodoma bila taarifa yake, kwa mujibu wa Utaly barua hiyo ilimpatia Chilwa wendawazimu wa muda (insanity) uliosababisha kifo chake.
  2. Christina Francis Mwezi aliyeajiriwa kama mkaguzi wa hesabu wa ndani msaidizi akamahamishiwa kampuni tanzu ya chama (Teachers Development Company Limited na baadae akahamishiwa CWT makao makuu kama mhasibu mkuu. Alifanya yafuatayo (i) Baada ya TAKUKURU kunusa ufisadi mwingi CWT ikiwemo safari ya Deus Seif na Abubakari Alawi kutumia fedha za walimu kwenda kuangalia mechi ya mpira kati ya Taifa Stars na Cape Verde nchini Cape Verde, Christina Francis Mwezi aliwanyima TAKUKURU vielelezo vyote kwa ajili ya safari hiyo na akatamba kwamba hawana nakala halisi na huwa TAKUKURU huwa hawashindi kesi. (ii) Katika wizi wao alipewa kinyemela milioni 270 ili kuwezesha jambo lililokwisha kubainishwa hapo awali (iii) aliandikiwa barua na katibu mkuu Japhet Maganga kuhamia kwenye kampuni ya maendeleo ya walimu akakataa uhamisho huo kwa barua kinyume na Kanuni za CWT ambapo Katibu Mkuu anayo mamlaka ya kumhamisha mtumishi yeyote wa chama kadiri anavyoona inafaa. Christina alikataa uhamisho huo kwa barua hadi sasa ni miezi 5 analipwa mshahara bila ya kuwa kazini. Alhaji Utaly anatambua kwamba ni marufuku kwa Muislamu kula fedha ya haramu. Yeye anaishi kwa fedha ya haramu, Mungu wake anajua pepo yake itakavyokuwa ila lazima ajue kesho kuna moto kwa kula vya haramu vikiwepo zizi la ng’ombe alilopewa na wamasai wa Mvomero alipokuwa mkuu wa Wilaya ili awakandamize wakulima na alifanya hivyo.
  3. Queen Augustino Luvanda, huyu pia anamdanganya Evod kwa sababu yeye alikuwa mwanasheria wa Geita, Deus akampatia ajira CWT akawa na mkataba wa likizo bila malipo na Deus akampa mkataba wa ajira ya kudumu CWT. Hivi kwa nini mkurugenzi wa Geita halioni hili na Queen anamshauri vibaya Evod kwa sababu yeye mwenyewe baada ya kupata changamoto ya uzazi wa pili ajira yake iko kwenye utata, Mkurugenzi wa Geita analijua hili alishamuandikia barua ya kurudi kazini japo wanajaribu kulizima kwa hila.
  4. Stella Kiabo na Stella Mamoto hawa wanamshauri vibaya Evod, hawa wana janga lao, kwa kuwa hawakuingia CWT kihalali wao walikuwa wajumbe wa kamati ya utendaji ya taifa ambao kwa mujibu wa katiba ya CWT kamati hiyo ndio mwajiri; katika kikao chao cha Mwanza cha 2018 kamati iliamua yafuatayo (1) Kuwashusha madaraka maafisa waandamizi wa CWT makao makuu Prosper Lubuva, Mwandile Kiguhe, Simon Keha na Dagobath Deogratius Tigalioma(marehemu). Kamati hiyo hiyo iliwateua wajumbe wa kamati hiyo hiyo Stella Kiabo kuwa mkuu wa idara ya elimu na mafunzo nafasi iliyokuwa ya Prosper Lubuva na Stella Obeid Mamoto kuwa mkuu wa idara ya wanawake na jinsia iliyokuwa ya Mwandile Kiguhe. Hawa hawawezi kuwa washauri wazuri wa Evod kwa sababu hawapo kihalali ni hii ni dhambi ya kamati ya utendaji ya taifa kwa sababu wanajua ili mtumishi kuajiriwa makao makuu kuna utaratibu gani.

CWT kwa sasa imekaa vizuri, ingefanya vibaya ukweli ungedhihiri wangechemka na hata wakichemka tutawasema waziwazi. Tunaomba siasa za majitaka ziishe, Ni vizuri kubainisha ni nani marafiki wa chama na ni nani sio marafiki wa chama wa nje na ndani. Tunafahamu viongozi wa juu wa kisiasa na wale wa serikali kupitia Deus Seif na Abubakari Alawi wamekuwa wakifaidika na fedha za walimu. Tafakarini Chukueni Hatua.
Acha bhangi,bhangi ni mbaya sana.
 
CWT sio Mali ya walimu,ni mali ya viongozi WA Cwt na CCM.CWT inafanya kazi kwa manufaa ya viongozi wake,na kwa manufaa ya ccm.Hiki chama Kiko compromised na ccm na mifumo yake na hakifurukuti tena.
Kwa sasa kimepoteza hadhi ya chama cha wafanyakazi.Hata baadhi ya viongozi wa chama hiki ni makada na Wana uongozi tena ndani ya ccm.HUU NI UKWELI MCHUNGU AMBAO CWT HAMTAKI KUUSIKIA.Uwezo wenu wa kutetea masilahi ya walimu umepotea,mmebaki kutetea matumbo yenu tu.
You are extremely wrong
 
You are extremely wrong
Mkoani kwangu, Mwenyekiti wa CWT Mkoa alikuwa anagombea ubunge kwenye jumbo mojawapo katika mkoa huu kwa tiketi ya CCM. Mtu huyu ni kada mtiifu. Je, anaweza kusimama kidete pale masilahi ya walimu yanapokuwa hatarini? Je, huyu anaweza kuishinikiza serikali itekeleze kilio chetu cha siku nyingi cha teaching allowance?

Huu ni mfano mmoja tu. Wapo wengi ndani ya CWT. Wanachofanya tu ni kuitikia mashinikizo kutoka CCM na kuignore masilahi ya walimu. Kama wewe sio mwalimu, huwezi kuelewa jinsi huu ubia usio rasmi kati ya CCM na CWT unavyoumiza walimu.

Kingine kibaya ni kwamba tabia na mienendo ya viongozi wa CWT haina tofauti na ile ya ndani ya CCM. Rushwa wakati wa uchaguzi, upendeleo, na maovu mengine ndio zao.
 
Maelezo yote hayo ni kuhusu T-Shirt TU? Mbona mnatia aibu hayo ndiyo mahitaji ya mwalimu wa Tanzania. Kweli adui wa mwalimu ni mwalimu.
 
Mkuu Umesema ukweli jamaa Ametoa maelezo mengi ya T-shirt hivi ni kweli walimu wanahitaji sana hizo T-shirt.Kwaio CWT ipo kwa ajili ya kuhakikisha walimu nchi nzima wanapata t-shirt za mei mosi
Tusiendelee kuleta huu ujinga Aisee na hizi ni dharau kubwa sana kwa walimu wetu.Hao viongozi uliokuja hapa kuwasagia kunguni na hao unawataka kwa maslahi ya tumbo lako walitakiwa tuwaone waki address changamoto za walimu na kuzitolea solution kwa mwajiri ambae ni Serikali zifanyiwe Kazi kwa wakati ili mwalimu aboreshewe maslahi na mazingira ya Kazi.
Take Note
Uache huu ujinga T-shirt haiwezi kumkomboa mwalimu atoke kwenye maslahi duni na mazingira mabovu ya kufanyia kazi.
 
Hivi walimu wanaona huduma kubwa kupewa na chama chao ni kununuliwa t shirt, kapelo na scarf Mei mosi tuu.
Endeleeni kulea ujinga huku viongozi wezi wanakula kwa raha zao michango yenu.
 
Ni kweli ndio maana barua za siwitii kila mwisho lazima ziandikwe ndugu mwakilishi mahala pa kazi waambie walimu wafunge Mikanda kwa mwaka huu hela ya mahala pa kazi haitarudi kwa sababu tumenunulia t-shirt

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom