BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,410
- 8,191
Bunge limepitisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali namba 4 wa mwaka 2023 ambapo moja ya marekebisho katika sheria ya Mafao ya Kustaafu katika Utumishi wa kisiasa inapendekezwa Wenza (Mke/Mume) wa Marais Wastaafu, Wenza wa Makamu wa Rais Wastaafu na Wenza wa Mawaziri Wakuu Wastaafu walipwe kiinua mgongo kwa kipindi cha uongozi wa Wenza
wao.
Akiwasilisha marekebisho hayo leo Oktober 31,2023 wakati wa kikao cha Bunge Mjini Dodoma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dk. Eliezer Feleshi amesema kuwa vifungu vipya vya 9A, 12A na 14A vinapendekezwa kuongezwa katika Sheria ya Mafao ya Kustaafu katika Utumishi wa Kisiasa, Sura ya 225.
Sambamba na marekebisho hayo, vifungu vya 11, 13 na 15 vinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka utaratibu wa malipo ya fadhila kwa Wenza wa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu endapo watafariki wakiwa madarakani au baada ya kumaliza muda wao na kufariki kabla ya kulipwa mafao au stahiki zao.
Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kifungu cha 18 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka utaratibu wa wenza wa Spika Mstaafu aliyefariki kupokea mafao ya pensheni ya kila mwezi.
Muswada huo uliopitishwa utawasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aweze kuutazama muswada huo na akiuridhia atasaini ili iwe sheria.
#MillardAyoBUNGENI