BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,515
8,415
Bunge limepitisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali namba 4 wa mwaka 2023 ambapo moja ya marekebisho katika sheria ya Mafao ya Kustaafu katika Utumishi wa kisiasa inapendekezwa Wenza (Mke/Mume) wa Marais Wastaafu, Wenza wa Makamu wa Rais Wastaafu na Wenza wa Mawaziri Wakuu Wastaafu walipwe kiinua mgongo kwa kipindi cha uongozi wa Wenza
wao.

Akiwasilisha marekebisho hayo leo Oktober 31,2023 wakati wa kikao cha Bunge Mjini Dodoma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dk. Eliezer Feleshi amesema kuwa vifungu vipya vya 9A, 12A na 14A vinapendekezwa kuongezwa katika Sheria ya Mafao ya Kustaafu katika Utumishi wa Kisiasa, Sura ya 225.

Sambamba na marekebisho hayo, vifungu vya 11, 13 na 15 vinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka utaratibu wa malipo ya fadhila kwa Wenza wa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu endapo watafariki wakiwa madarakani au baada ya kumaliza muda wao na kufariki kabla ya kulipwa mafao au stahiki zao.

Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kifungu cha 18 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka utaratibu wa wenza wa Spika Mstaafu aliyefariki kupokea mafao ya pensheni ya kila mwezi.

Muswada huo uliopitishwa utawasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aweze kuutazama muswada huo na akiuridhia atasaini ili iwe sheria.

#MillardAyoBUNGENI
 
DODOMA; Bunge limepitisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali Namba 4 wa mwaka 2023 ambapo moja ya marekebisho katika sheria ya Mafao ya Kustaafu katika Utumishi wa kisiasa inapendekezwa wenza wa Rais Mstaafu, Makamu wa Rais Mstaafu na Waziri Mkuu Mstaafu kulipwa kiinua mgongo kwa kipindi cha uongozi wa wenza wao.

Muswada huo uliopitishwa utawasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ili aweze kuusaini na kufanya muswada huo kuwa Sheria.

Akiwasilisha marekebisho hayo leo Oktoba 31 wakati wa kikao cha Bunge Mjini Dodoma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dk. Eliezer Feleshi amesema kuwa vifungu vipya vya 9A, 12A na 14A vinapendekezwa kuongezwa katika Sheria ya Mafao ya Kustaafu katika Utumishi wa Kisiasa, Sura ya 225.

Sambamba na marekebisho hayo, vifungu vya 11, 13 na 15 vinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka utaratibu wa malipo ya fadhila kwa wenza wa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu endapo watafariki wakiwa madarakani au baada ya kumaliza muda wao na kufariki kabla ya kulipwa mafao au stahiki zao.

Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kifungu cha 18 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka utaratibu wa wenza wa Spika Mstaafu aliyefariki kupokea mafao ya pensheni ya kila mwezi.

Habarileo

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Daaah hiii nchi siasa inalipa sana
 
Waone namna ili mwenza (Kigongoni) akipoteza maisha wakati yupo madarakani, arithi cheo hicho

Ili hizi pensheni/mafao yatumike vizuri!

Pia nazani mafao yao hayana kikokotooo, kama ya watendaji wa umma!
 
1. Hawana PAYE
2. Hawachangii NHIF
3. Wanahudumiwa kila kitu
4. Wana diplomats priviledges
5. HAwakatwi pesa ya mafao
6. Wakistaafu, wanapewa 80% ya mshahara wa aliyeko madarakani.

Wakistaafu baada ya miaka 5, 10 wanachota mara 1,000 zaidi ya waliofanya miaka 36, kutoka kwenye hazina waliojitajirisha nayo wakiwa kwenye viti, jasho la aliyepigika kwa miaka 36.

Haitoshi?

Utashanga akina Fai..., Luc... wanaelewa!
 
Bunge limepitisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali namba 4 wa mwaka 2023 ambapo moja ya marekebisho katika sheria ya Mafao ya Kustaafu katika Utumishi wa kisiasa inapendekezwa Wenza (Mke/Mume) wa Marais Wastaafu, Wenza wa Makamu wa Rais Wastaafu na Wenza wa Mawaziri Wakuu Wastaafu walipwe kiinua mgongo kwa kipindi cha uongozi wa Wenza
wao.

Akiwasilisha marekebisho hayo leo Oktober 31,2023 wakati wa kikao cha Bunge Mjini Dodoma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dk. Eliezer Feleshi amesema kuwa vifungu vipya vya 9A, 12A na 14A vinapendekezwa kuongezwa katika Sheria ya Mafao ya Kustaafu katika Utumishi wa Kisiasa, Sura ya 225.

Sambamba na marekebisho hayo, vifungu vya 11, 13 na 15 vinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka utaratibu wa malipo ya fadhila kwa Wenza wa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu endapo watafariki wakiwa madarakani au baada ya kumaliza muda wao na kufariki kabla ya kulipwa mafao au stahiki zao.

Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kifungu cha 18 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka utaratibu wa wenza wa Spika Mstaafu aliyefariki kupokea mafao ya pensheni ya kila mwezi.

Muswada huo uliopitishwa utawasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aweze kuutazama muswada huo na akiuridhia atasaini ili iwe sheria.

Ikumbukwe mwaka mmoja uliopita aliyewasilisha Ombi hilo la wake wa marais walipwe, ni mke wa Kikwete Mama Salma Kikwete wakati akiwasilisha hoja hiyo Bungeni, ambapo tangu mwaka 2017 amekuwa akihudumu kama mbunge wa kuchaguliwa wa jimbo la Mchinga. Tizama video hii akiwasili hoja hiyo

View: https://youtu.be/pc9ZyIa6wkE?si=UwkRkNd9SoCT0jU5
 
Back
Top Bottom