App Mpya ya JamiiForums: Fuata hatua hizi

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
3,960
2,000
Naam wakuu,

Kwa mara nyingine tumeona tuboreshe huduma ya JF ili izidi kuwa rahisi kutumia.

Kwa sasa unaweza ku-Install JF App kwa PC au Tablet (iPad zikiwemo) na Simu za Mkononi (Android na iPhones).

FAIDA:

1) Ni rahisi kutumia na haina tofauti yoyote na main site, hakutakuwa na malalamiko tena kuwa kuna kukosa notifications au kushindwa kufanya actions kadhaa

2) Ni rahisi kufunguka kuliko unavyodhania. Installation yake inachukua sekunde moja au pungufu. Haichukui space kwenye simu yako au kifaa chako

3) Ukiwa offline, bado kuna content utakuwa na access nayo kwa urahisi zaidi. Hulazimiki kuwa mtandaoni

4) na mengine mengi

Hatua za kufuata:

Kwa wanaotumia PC:

Tembelea JF kwa kutumia Google Chrome Browser, kisha utaona sehemu kama hii kwenye browser yako:

HomepageChrome.jpg


the-button.jpg


Kisha bonyeza Install kama inavyoonekana hapa chini:

Install.png


Utaona tayari unayo App kwenye PC yako. Kuanzia hapo hutokuwa ukilazimika kutembelea tovuti kwa njia ya browsing ya kawaida.

Mfano, mwenye Macbkook ataona icon ya App ya JF ikiwa hivi:

Screenshot 2021-05-20 at 02.25.42.png


Kwa wanaotumia Android Devices:

Tumia Google Chrome (au native browser ya simu yako):

Bonyeza mistari mitatu iliyo kushoto mwa LOGO ya JamiiForums, utaona kitu kama hiki chini:

Screenshot 2021-05-20 at 02.14.18.png


Android-0.jpg


Bonyeza INSTALL kisha utaona hivi (itachukua sekunde 1 ku-Install)

Android_1.jpg


Kwa wanaotumia iPhone au iOS devices:

Tumia Safari Browser, bonyeza sehemu hizi zilizozungushiwa na fuata maelekezo kwenye simu... Just add to your device's home screen.

iPhoneORiPad_1.jpg

iPhoneORiPad2.jpg


Ukikwama usisite kuuliza, tupo kwa ajili yako.

TAKE NOTE: Siku zijazo (sio karibuni) tutaondoa App zilizopo kwenye Google na Apple stores. Kuna mabadiliko zaidi yanakuja kwenye mwonekano na user experience katika kutumia huduma ya JF.

PS: Kuna watu wanataka kujua kuhusu kupata notifications. Tafadhali enable push notifications kwenye settings na utazipata bila shaka.

Karibuni
 

kinjekitile70

JF-Expert Member
Oct 11, 2017
1,032
2,000
Mkuu Max ,nashukuru sana kwa features mpya!

Kwangu imefanya kazi

Japo nimeshazoea ile app ya play store ila najua una nia njema kuhamia huku!

Chini kabisa kwenye browser kuna Add inaelekeza kwenye group la Telegram.

Naomba kujua kama hyo add Siyo SCAM

Nimeweka attachment hapo chini

20210520_025447.jpg
 

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
3,960
2,000
Mkuu Max ,nashukuru sana kwa features mpya!

Kwangu imefanya kazi

Japo nimeshazoea ile app ya play store ila najua una nia njema kuhamia huku!

Chini kabisa kwenye browser kuna Add inaelekeza kwenye group la Telegram.

Naomba kujua kama hyo add Siyo SCAM

Nimeweka attachment hapo chini
Hili ni tangazo letu JF na ni Channel yetu. Itembelee JamiiForums
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom