Ewaaa..mzigo uko kama kwenye web nimeuelewa..! Ile ya mwanzo binafsi nilikua napata shida kutumia..nilikua nafurahia sana nikitumia goole chrome kuliko app but now safi..
 
Kwangu siioni hiyo uption ya kuinstall nametumia brower ya chrome,google na opera mini zote zime fail,Max ikoje hii???
Screenshot_2021-05-20-06-20-49-50.jpg
 
Great work Melo...

Nimeisoma thread yako kwenye app ya awali na sasa nareply kupitia hii mpya...

A lot of changes aisee, ni kama nipo kwa browser tu...

Naona hata app size ni ndogo, few kb's compared to around 50MBs kwa ile app ya awali...

Screenshot_20210520-064152~2.png
 
Naam wakuu,

Kwa mara nyingine tumeona tuboreshe huduma ya JF ili izidi kuwa rahisi kutumia.

Kwa sasa unaweza ku-Install JF App kwa PC au Tablet (iPad zikiwemo) na Simu za Mkononi (Android na iPhones).

FAIDA:

1) Ni rahisi kutumia na haina tofauti yoyote na main site, hakutakuwa na malalamiko tena kuwa kuna kukosa notifications au kushindwa kufanya actions kadhaa

2) Ni rahisi kufunguka kuliko unavyodhania. Installation yake inachukua sekunde moja au pungufu. Haichukui space kwenye simu yako au kifaa chako

3) Ukiwa offline, bado kuna content utakuwa na access nayo kwa urahisi zaidi. Hulazimiki kuwa mtandaoni

4) na mengine mengi

Hatua za kufuata:

Kwa wanaotumia PC:

Tembelea JF kwa kutumia Google Chrome Browser, kisha utaona sehemu kama hii kwenye browser yako:

View attachment 1791283

View attachment 1791292

Kisha bonyeza Install kama inavyoonekana hapa chini:

View attachment 1791284

Utaona tayari unayo App kwenye PC yako. Kuanzia hapo hutokuwa ukilazimika kutembelea tovuti kwa njia ya browsing ya kawaida.

Mfano, mwenye Macbkook ataona icon ya App ya JF ikiwa hivi:

View attachment 1791290

Kwa wanaotumia Android Devices:

Tumia Google Chrome (au native browser ya simu yako):

Bonyeza mistari mitatu iliyo kushoto mwa LOGO ya JamiiForums, utaona kitu kama hiki chini:

View attachment 1791285

View attachment 1791286

Bonyeza INSTALL kisha utaona hivi (itachukua sekunde 1 ku-Install)

View attachment 1791287

Kwa wanaotumia iPhone au iOS devices:

Tumia Safari Browser, bonyeza sehemu hizi zilizozungushiwa na fuata maelekezo kwenye simu... Just add to your device's home screen.

View attachment 1791288
View attachment 1791289

Ukikwama usisite kuuliza, tupo kwa ajili yako.

TAKE NOTE: Siku zijazo tutaondoa App zilizopo kwenye Google na Apple stores!

Karibuni
It works! Great look n’ feel!
 
Tunashukuru kwa maboresho mkuu Ila

1. Ni lazima mtu utumie Google chrome at least ianzie version gani?

2. Vipi kuhusu watumiaji wa opera Mimi,Uc broswer, brave broswer n.k?
 
Back
Top Bottom