Yaliyojiri JamiiForums Space kuhusu Maambukizi ya COVID-19 na Utoaji Chanjo Tanzania

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
Jamii Forums inakukaribisha kushiriki kwenye Mjadala kuhusu Maambukizi ya #COVID19 pamoja na Utoaji wa Chanjo nchini Tanzania

Mjadala huu unafanyika Agosti 6, 2021 kupitia Twitter Spaces (JamiiForums) kuanzia Saa 12 jioni na utahusisha Wataalamu wa Afya watakaozungumzia Masuala anuani kuhusu Janga hili

====

UPDATES;1800hrs

======

Kufuatilia mjadala huu, fungua hii link.

#UVIKO3
IMG_20210806_071308_690.png

Je, ni lazima Mtu avae Gloves wakati wa kuchanja mtu?

Dr. Francis& Dr. Mariam: Kuvaa Gloves unatakiwa kila Gloves moja mtu mmoja, kwahiyo kwa siku mtu anayetoa chanjo anatakiwa avae Gloves 400. Hivyo kutokuvaa gloves ni rahisi hata kusafisha mikono kila baada ya kuchanja kuliko kuvua na kuvaa gloves. Pia muongozo wa Kuchanja unaruhusu kuchanja bila gloves.

Je, ni asilimia ngapi ya Watanzania Wachanje tuseme watu wengi wana kinga?

Dr. Mariam: Asilimia 70 hadi 80 ndo inashauriwa.

Dkt. Maryam: Watu wengi wanapokuwa hawana Chanjo ndivyo ambavyo Kirusi kinavyopata nafasi zaidi ya kuweza kubadilika

Hadi tutakapofikia 70% - 80% ya Watu waliopata Chanjo ndipo tunaweza kusema tumefanikiwa katika kupunguza Maambukizi

Dkt. Francis: Tunapozungumzia UVIKO19 kuna athari kubwa kwa Mtu na inaongeza mzigo kwenye utoaji huduma za Kiafya ikiwemo ICU na Oksijeni

Kwa hiyo wote tunaingia gharama kwasababu kuna Mtu atakosa Oksijeni akiwa na Magonjwa mengine sababu ya Mtu mwenye COVID19

Dkt. Maryam: Watu wengi wanapokuwa hawana Chanjo ndivyo Kirusi kinavyopata nafasi zaidi ya kuweza kubadilika

Hadi tutakapofikia 70% - 80% ya Watu kuwa wamepata Chanjo ndipo tunaweza kusema tumefanikiwa katika kupunguza Maambukizi

Dkt. Elisha: Nimeridhika na mwamko wa Watanzania kwenda kuchanjwa na naweza kusema mpaka hapa tulipofika ni 'success'

Tulipotoka Watu hata walikuwa hawaruhusiwi kuongelea #COVID19 huku wengine wakiwa kwenye Lockdown

Dkt. Francis: Watu wengi wanaogopa kwenda kuchanjwa kwasababu ya Uoga. Mitandao ya kijamii ina taarifa nyingi ambazo zimepotosha Watu

Mbele ni kuzuri ila cha msingi tuendelee kuwapa Watu taarifa sahihi. Mtu akiona mwenzie hajapata tatizo naye atakwenda kuchanjwa

Dkt. Norman: Ni ngumu kusema tumeridhika na mwamko wa Watanzania kwasababu hatuna Data za Dawa ngapi zilikuwepo na ngapi zimetoka

Ni matarajio yangu mpaka mwisho wa Mwaka Watu wote kwenye makundi Maalum watakuwa wamekuwa 'Covered'

Dkt. Norman: Kwa Dunia kasi ya uchanjaji inaendelea vizuri ambapo Mpaka Machi zilikuwa zimeshatoka dozi takriban bilioni 1.3

Kwetu tujitahidi ku-cover makundi Maalum. Afrika bado hakuna Nchi ambayo imeshafikia 5% ya Uchanjaji kwasababu Kampuni nyingi wanahodhi Chanjo

Dkt. Sajjad: Nimeridhika kwa kiasi fulani lakini bado tuna safari ndefu. Nimeridhika kwasababu kulikuwa a upotishaji. Baadhi ya Viongoxi walikuwa wanapotosha Jamii

Kuna mwamko sasa hivi, angalau tumefika sehemu nzuri. Ni jukumu letu sote kuelimisha jamii

Dkt. Maryam: Mtu ambaye ni Mgonjwa na yupo hoi Hospital hatakiwi kupata chanjo wakati huo bali asubiri mpaka Wiki 4 ndio apate Chanjo

Mtu anapokuwa anaumwa Mwili wake unakuwa unapambana na Maambukizi, akipewa Chanjo inakuwa inazidisha hali yake kuwa mbaya

Dkt. @amour_maryam: Mgonjwa mwenye maambukizi hai (active) yaani ana dalili za wazi hatakiwi kupata chanjo wakati huo bali asubiri mpaka Wiki 4

Kwa wakati huo mwili unakuwa unapambana na Maambukizi, akipewa Chanjo inakuwa inazidisha hali yake kuwa mbaya

Dkt. @furia_francis: Watu wanaopewa chanjo ni ambao hawana dalili, ukiwa mgonjwa huwezi kupata chanjo

Hakuna utaratibu kwamba tunawapima watu kabla ya kuwapa chanjo. Tunachoangalia ni dalili za ugonjwa, na tunauliza. Kama hauna dalili unaweza kupewa chanjo

Dkt. Maryam: Ukishapata Chanjo hakikisha unaendelea na taratibu zote za kujilinda ikiwemo kuvaa Barakoa

Kupata Chanjo haimaanishi uanze kujiachia. Ukikuta foleni kwenye Chanjo jitahidi kukaa mbali kidogo na Watu unapoendelea kusubiri

Dkt. @amour_maryam: Ukishapata Chanjo hakikisha unaendelea na taratibu zote za kujilinda ikiwemo kuvaa #Barakoa

Kupata Chanjo haimaanishi uanze kujiachia. Ukikuta foleni kwenye Chanjo jitahidi kukaa mbali kidogo na Watu unapoendelea kusubiri

Dkt. @SajjadFazel: Chanjo ya Johnson & Johnson ilisitishwa Marekani kwa muda ili kuangalia madhara waliyopata Watu ni kiasi gani

Baada ya utafiti waliridhika iko salama na imeendelea kutumika. Kusema tumeletea Chanjo iliyokataliwa sio sawa. WHO pia imeikubali ni salama

Dkt. Maryam: Ukishapata Chanjo hakikisha unaendelea na taratibu zote za kujilinda ikiwemo kuvaa Barakoa

Kupata Chanjo haimaanishi uanze kujiachia. Ukikuta foleni kwenye Chanjo jitahidi kukaa mbali kidogo na Watu unapoendelea kusubiri

Dkt. @amour_maryam: Ukishapata Chanjo hakikisha unaendelea na taratibu zote za kujilinda ikiwemo kuvaa #Barakoa

Kupata Chanjo haimaanishi uanze kujiachia. Ukikuta foleni kwenye Chanjo jitahidi kukaa mbali kidogo na Watu unapoendelea kusubiri

Dkt. Sajjad: Chanjo ya Johnson & Johnson ilisitishwa Marekani kwa muda ili kuangalia madhara waliyopata Watu ni kwa kiasi gani

Baada ya utafiti waliridhika iko salama na imeendelea kutumika. Kusema tumeletea Chanjo iliyokataliwa sio sawa. WHO pia imeikubali ni salama

Dkt. Norman: Chanjo inaenda kusisimua mwili, mara nyingi side effects zinaweza kutokea. Kuna baadhi ya watu kichwa kitauma, watasijikia kuchoka

Dalili hizi mara nyingi zinaisha ndani ya siku chache, zikiendelea ni vyema mtu akarudi kituo alichopata chanjo

Dkt. Sajjad: Sio kila anayepata Chanjo ya Coronavirus atapata tatizo la kuganda. Kuna sababu nyingi za Damu kuganda

Ukishapata Chanjo ikafika siku 6 - 15 tangu uchanjwe ukianza kuona dalili za kutokuona vizuri na maumivu kwenye Kifua ni vizuri kwenda Hospital haraka

Dkt. @SajjadFazel: Utafiti mbalimbali unafanyika duniani kuangalia hizi chanjo zinatoa kinga kwa kiasi gani dhidi ya Kirusi cha Corona aina ya Delta

Baadhi ya Chanjo mfano Johnson & Johnson inaweza kukupa kinga asilimia 60-70

Dkt. Maryam: Utafiti wa hivi karibuni unaonesha Effectiveness ya Chanjo ya Johnson&Johnson unaweza kufikia mpaka asilimia 80

Kuwepo kwa Kirusi Delta hakumaanishi vile Virusi vingine havipo
 
Nafikiri ni muda muafaka kwa serikali kuzingatia wananchi wake wanakula nini na wanakunywa nini!

Hili jambo ni moja ya kitu muhimu sana kama serikali inajali afya za watu wao.

Chakula kitaimarisha Kinga za watu hata Kama tutakuwa katika janga Kama hili wakati wa kusubiri dawa ama Kinga tukute hata miili yetu ikiwa imara.

Huu ni ushauri mdogo tu kwa serikali na kwa mtu mmoja mmoja afya ni ya kwako na hiyo ndio afya ya taifa.

Samahani Kama nimeandika kinyume na uzi.
 
Karibu sana Mkuu.
 
Jamii Forums inakukaribisha kushiriki kwenye Mjadala kuhusu Maambukizi ya #COVID19 pamoja na Utoaji wa Chanjo nchini Tanzania

Mjadala huu unafanyika Agosti 6, 2021 kupitia Twitter Spaces (JamiiForums) kuanzia Saa 12 jioni na utahusisha Wataalamu wa Afya watakaozungumzia Masuala anuani kuhusu Janga hili

#UVIKO3
View attachment 1882254
Naona siasa za Corona zimekuja kwa kasi kubwa

USSR
 
Jamii Forums inakukaribisha kushiriki kwenye Mjadala kuhusu Maambukizi ya #COVID19 pamoja na Utoaji wa Chanjo nchini Tanzania

Mjadala huu unafanyika Agosti 6, 2021 kupitia Twitter Spaces (JamiiForums) kuanzia Saa 12 jioni na utahusisha Wataalamu wa Afya watakaozungumzia Masuala anuani kuhusu Janga hili

#UVIKO3
View attachment 1882254
Hivi huwezi kuweka link ikawa rahisi kufuatilia kule? Nimesha-subscribe na nikipata muda nitaeleza lile tukio la kunusurika kushambuliwa na Wanakijiji wakidhani nimeenda kuwachanja watoto wao
 
Hii siyo kinda bado
Ungechanja na hakuna tena
Mambo ya kuvaa barakoa hapo
Sawa...
Mbona kuna watu wamechanja na wamekufa

Ova
Sijasikia. Kwahiyo unataka ukichanja uishi milele? Ni wakati wa kutambua mchangi wa Wataalamu.
 
Back
Top Bottom