Shalom,

Toka ameingia madarakani kwa bahati ya umauti wa Magufuli kuna vitu hayuko sawa kuongoza na kusimamia watendaji.

Yafuatayo ayatibu

1. Anafanya usanii kuhusu haki za wafanyakazi mishshara hajaboresha, kuhusu malimbikizo ni usanii hajalipa.
2. Wafanyakazi wanaonewa sana na mabosi wao hasa kutopewa haki zao mfano kuna taasisi nyingi mabosi hawatekelezi viwango vipya vya posho za usafiri na vikao.
3. Halindi wakulima hasa bei ya pembejeo na pembejeo nyingi ni fake.
4. Masomo ya mazao ya wakulima hakuna jitahada.
5. Kero za Halmashauri kwa wakulima zimerudi.
6. Kero za maji, umeme, mfumuko wa bei.
7. Uhaba wa Dollar, kupanda kwa nauli Tena bila huruma na hakuna unsfuu wa maisha,
8. Analea kauli zenye dharau hana machungu (Mwigulu na Nape, January), anaongea kiulaini sana na yupo kinyumbani zaidi kauli zake na sio kama Rais wa nchi.
9. Toka ameingia ikulu hajawahi kutoa kauli thabiti za kukemea.
10. Wanaomsifia wanamdanganya wanaonufaika ni wafanyabiashara wanaokula na TRA, viongozi wenye mafungu ya kuiba na safari nyingi.
11. Kuna rushwa kithiri za pesa na ngono kwenye kupata kazi.
12. Bodi ya mikopo elimu ya juu inawatesa sana wanafunzi wa vyuo imefika wakati wanafunzi wanatoa rushwa za ngono na pesa ili mambo yao ya mikopo ifa ikiwe. Hii ni kero kubwa hadi aibu.
13. Watu wanakwepa kutoa receipts za EFD hapa ni kilio kikubwa TRA wamekaa ofisni inatia hasira sana.
14. Uanzishwaji wa biashara lessen na vibali ni jini la umaskini TRA ni nyoka mwenye sumu biashara zinakufa viwango vikubwa vya makadirio ya Kodi, wivu, ukiritimba.
15. Kodi ya mapato kwa wanaopangisha nyumba haikusanywi TRA wamekaa ofisni kimya, wenye nyumba wanaokula bata hawalipi Kodi ya mapato.
16. Anasafiri sana kuliko kutenga muda wa kushughulikia kero za wananchi, Hana muda wa kuhamasisha kufanya kazi kwa bidii na kulipa Kodi.
17. Hajui kama raia wanamchukia, wanahasira nae kwa kukosa ukali kwa watendaji wake.
18. CCM wanamchora tu ila yeye hajui wanampaka mafuta kwa gongo la chupa.
19. Mzunguko wa pesa ni aibu maisha magumu, mtu kupata chenji ya elfu10 na elfu5 ni kero kero kubwa.
20. Watumishi wengi wamekata tamaa wanafuraha nyumbani kuliko kazini, extra duty na overtime sifuri.

Rais shtuka kidogo kula na kipofu. Maisha ni ubinadamu ongeza furaha kwa wananchi na watumishi.

Ni hayo tu

Wadiz
Mkuu kwanza nikuombe hiyo notion ya kutumia neno USANII katika kunasibisha tabia ama mwenendo wenye longolongo ndani yake ni kutudhalilisha wasanii ambao tunafanya kazi kubwa kwenye jamii. Tunaelimisha, Tunaburudisha, Tunatibu kupitia sanaa zetu.

Tukirejea kwenye hoja.
Pale juu pameshakosa umakini, ndo maana KR yupo karibu isivyo kawaida ya status yake kujaribu kuokoa baadhi ya yanayookoleka.

Pili. Mimi simuoni kama SSH anakosea, bali tunasahau shina na mzizi wa fitina ni CCM. Tudeal nayo badala ya kuchambua watu wa kushughulika nao ndani humo
 
Ukweli uwekwe wazi.
Samia sio kiongozi mzuri bado anahitaji kuongozwa.
Ccm kwa ajili ya kupenda rushwa, dhuruma na ufisadi wameshindwa kabisa kumuongoza Rais. Wanaona hiki ndio kipindi chao cha mavuno.
Hali si shwari ktk nyanja nyingi.
 
Ifike muda tuambizane ukweli hata kama hatupo tayari kwa hilo.

Samia Urais hauwezi na sio Urais hata uwaziri na cheo cha kuongoza watu kwake ni mzigo mzito.

Kama atapata bahati ya kusoma huu ujumbe au kufikishiwa huu ujumbe atambue fika kuwa Urais kwake ni zigo zito.

Sio kila mtu anaweza kuwa kiongozi wa umma, siongei haya kwa sababu ya chuki yoyote bali kwa mengi nayo fahamu kuhusu viongozi wa taifa namna wanavyopaswa kuwa.

Taifa letu sasa lilipo fika sio taifa la majaribio tena limekwisha kua lina umri mkubwa halina uchanga wowote tena ni vyema viongozi wachaguliwao wakaenenda na ukubwa wa taifa letu.

Kwa wale watakaoweza kumuambia ukweli wamwambie nafasi aliyonayo ni kubwa kwake pasipo kujali maneno ya wanafiki wanaompamba.

Kwa mataifa yaliyo makini Samia alipaswa aziishi ndoto zake za kuwa muhudumu wa ndege basi ila kwenye uongozi hapana anapwaya sana.

Ni vyema ukweli kutamkwa.
 
Usipende kuropoka ropoka tu ilimradi uonekane umezungumza. Kwanza uwe na adabu na heshima kwa Rais Wetu.

Rais Samia Ni Kiongozi ambaye kama Afrika ingekuwa ni nchi moja basi Rais Samia angechaguliwa kwa kishindo kuwa Rais wake.anao uwezo wa kuongoza Taifa lolote lile na likapata maendeleo makubwa kama tuliyoyapata.

Ndio maana ni katika uongozi wake tumeshuhudia ukamilishwaji wa miradi mikubwa mikubwa katika Historia ya Taifa letu ,miradi hiyo ni pamoja na bwawa la mwalimu Nyerere ambalo litatupatia megawati 2115 sawa na megawati zinazozalishwa katika mabwawa mawili ya kidatu megawati 204 pamoja na mtera megawati 80.

Ni Rais Samia ameweka historia katika macho ya watanzania kushuhudia treni ya umeme ikitembea katika ardhi ya Taifa lao.

Ni Rais Samia ameweka rekodi ya kutoa Elimu bure mpaka kidato cha sita kwa kutoa billion 33 kila mwezi,huku mikopo ya elimu ya juu ikitolewa kwa kila mwanafunzi mwenye sifa.ni Rais samia amekifanya kilimo kuwa kimbilio la watu baada ya kukipa thamani na kuja na kauli mbili ya kilimo ni biashara.pamoja na kupandisha bajeti kufikia Billion mia tisa 70.
Ni Rais Samia amewafanya watumishi wa umma kufurahia utumishi wao wa umma badala ya kuona kama ni kazi ya kitumwa.hii ni baada ya kuwapandisha madaraja kwa mserereko pamoja na kuwalipa malimbikizo ya madai yao.kutoa ajira kwa maelfu ya vijana.

Kujenga vyumba vya madarasa zaidi ya elfu 30 na hivyo kufanya katika Historia wanafunzi wote kuripoti shuleni kwa wakati mmoja.kujenga vituo vya afya kila kona ya nchi yetu .kutiririsha zaidi ya trilioni sita katika Secta ya Afya na hivyo kufanya huduma mbalimbali kupatikana hapa hapa nchini badala ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi ambako wanyonge walikuwa hawawezi kumudu gharama zake.

Kutoa zaidi ya Billion 250 kama Ruzuku katika kilimo kila mwaka na hivyo kupungua kwa bei ya pembejeo hususani mbolea.,kuongeza mapato kwa mwezi bila kukimbizana wala kufungia biashara za watu.kuimarisha uchumi na kujenga uchumi shirikishi ambao unawagusa watu moja kwa moja.

Kujenga miundombinu mbalimbali ya barabara katika kufungua fursa za kiuchumi.mfano kunakwenda kujengwa barabara ya njia nne kutoka igawa mkoani Mbeya mpaka Tunduma mkoani Songwe yenye urefu wa 237.9KM ambazo zitaongeza kasi usafirishaji,kuondoa foleni pamoja na kupunguza ajali za barabarani hasa za malori kufeli breki na kwenda kugonga magari ya abiria na madogo na kusababisha ajali na vifo,maana sasa kila magari yatakuwa yanapita njia yake.

Miradi ya maji Inaendelea kutekelezwa maeneo mbalimbali nchini.

Naomba niishie hapa. Nitarejea muda siyo mrefu
 
Ifike muda tuambizane ukweli hata kama hatupo tayari kwa hilo.

Samia Urais hauwezi na sio Urais hata uwaziri na cheo cha kuongoza watu kwake ni mzigo mzito.

Kama atapata bahati ya kusoma huu ujumbe au kufikishiwa huu ujumbe atambue fika kuwa Urais kwake ni zigo zito.

Sio kila mtu anaweza kuwa kiongozi wa umma, siongei haya kwa sababu ya chuki yoyote bali kwa mengi nayo fahamu kuhusu viongozi wa taifa namna wanavyopaswa kuwa.

Taifa letu sasa lilipo fika sio taifa la majaribio tena limekwisha kua lina umri mkubwa halina uchanga wowote tena ni vyema viongozi wachaguliwao wakaenenda na ukubwa wa taifa letu.

Kwa wale watakaoweza kumuambia ukweli wamwambie nafasi aliyonayo ni kubwa kwake pasipo kujali maneno ya wanafiki wanaompamba.

Kwa mataifa yaliyo makini Samia alipaswa aziishi ndoto zake za kuwa muhudumu wa ndege basi ila kwenye uongozi hapana anapwaya sana.

Ni vyema ukweli kutamkwa.
Ni kweli, rais anayeuweza urais ni yule anayekuwa na vikundi vya kuteka wasiomsujudia.
 
Usi laumu
Juzi kasem alitamani kiwa air hostess.
Na ndilo zilipo ndoto zake.
Na ukiangalia anavyo safiri ni kwamba N timiza ndoto zaks.
 
Ni kweli, rais anayeuweza urais ni yule anayekuwa na vikundi vya kuteka wasiomsujudia.

..Samia ni laghai.

..anadai analeta Reconciliation halafu anapandisha vyeo waliohusika na utesaji wakati wa Magufuli.
 
Back
Top Bottom