Waziri Makamba: Hakuna uhaba wa mafuta nchini, amtaka Mkurugenzi wa TPDC akajieleze kabla hawajachukua hatua

Hii issue ya ukosefu wa mafuta wiki ijayo huenda ni kweli.

Jamaa yangu anayefanya kazi kwenye kampuni inayoagiza na kuuza mafuta kwa jumla amedai huenda wiki ijayo wakawa hawana mafuta na madereva wao wanaorejea kutoka safari za masafa wamejulishwa hilo kwamba wiki ijayo wakapumzike hadi meli itaposhusha mzigo.

Ikumbukwe James Mataragio alitoa onyo kuhusu hilo wiki jana.

34672B67-6E02-4320-906E-D7B1D9E3CA29.jpeg
 
January kasema yapo na yeye ndo Serikali.
Serikali hiyo hiyo ndio ilisema leo tarehe 15 november 2021 wataanza kujaza bwawa la maji la SG. Lakini kwa sasa kichekesho kiko kwenye hatua ya kuagiza winch! Serikali hii hii ndio ilisema Nov 2019 reli kipande cha Dar-Moro kitaanza kazi, badala yake tunaona kombati za jeshi tu kuvaliwa na mama wa kambo. 2014 Muhongo akiwa waziri alisema ikifika 2020 Tanzania itakuwa inauza umeme nje ya nchi, ajabu ni kuwa wauzaji umeme hata umeme hatuna hadi muda huu!
 
Ndio tuseme na usafiri wa umma na binafsi nao utasimama?

Wafanyakazi maofisini na wanafunzi mashuleni wataendaje?

Au serikali itoe likizo ya muda mfupi kwa wote mpaka pale mafuta yatakaporejea?

Haya mambo ya ajabu ajabu huanza pale ambapo taifa linakuwa na kiongozi toka ukanda wa Pwani, bahati mbaya na waziri husika nae ana tabia za kijanja janja tu.

Mafuta yakiwa machache maana yake kuna uwezekano mkubwa yakapanda bei, yakipanda bei na nauli zitaongezeka, gharama za maisha zinazidi kupanda kila siku mtanzania masikini anazidi kuisoma namba.

Magufuli alipokuwa akinyoosha mambo mlikuwa kutwa nzima mkimtukana

Leo mambo yameanza kwenda mrama mnaanza kulialia

Leo January Makamba anatwambia mgao wa umeme, Dawasa nao wanasema mgao wa maji, EWURA nao mafuta hakuna

Hapa kuna harufu ya hujuma kubwa tu

Tutamkumbuka sana Jemedari wetu Magufuli, chini yake kulikuwa hakuna hujuma wala mpuuzi atakayethubutu kuleta upuuzi wa hujuma
 
Hii issue ya ukosefu wa mafuta wiki ijayo huenda ni kweli.

Jamaa yangu anayefanya kazi kwenye kampuni inayoagiza na kuuza mafuta kwa jumla amedai huenda wiki ijayo wakawa hawana mafuta na madereva wao wanaorejea kutoka safari za masafa wamejulishwa hilo kwamba wiki ijayo wakapumzike hadi meli itaposhusha mzigo.

Ikumbukwe James Mataragio alitoa onyo kuhusu hilo wiki jana.
Weweeeee, sisi hatumuamini huyo jamaa yako. Tunamwamimi mteule tu! Akisema hakuna uhaba wa mafuta maana yake hakuna uhaba wa mafuta. Na asipoangalia huyo jamaa yako naye tutamwita ajieleze! Alaaaaa!?
 
Magufuli alipokuwa akinyoosha mambo mlikuwa kutwa nzima mkimtukana

Leo mambo yameanza kwenda mrama mnaanza kulialia

Leo January Makamba anatwambia mgao wa umeme, Dawasa nao wanasema mgao wa maji, EWURA nao mafuta hakuna

Hapa kuna harufu ya hujuma kubwa tu

Tutamkumbuka sana Jemedari wetu Magufuli, chini yake kulikuwa hakuna hujuma wala mpuuzi atakayethubutu kuleta upuuzi wa hujuma
Mbona alitwambia maji yanafunguliwa kwenye mabwawa ndo maana ulikuwa unakatika kipindi chake!!? Au umesahau
 
Site za kuweka "shell" zina mea kama uyoga kwa sasa. Labda yatabanwa mpaka zikamilike( jokes ha ha haaa!)
 
Ndio tuseme na usafiri wa umma na binafsi nao utasimama?

Wafanyakazi maofisini na wanafunzi mashuleni wataendaje?

Au serikali itoe likizo ya muda mfupi kwa wote mpaka pale mafuta yatakaporejea?

Haya mambo ya ajabu ajabu huanza pale ambapo taifa linakuwa na kiongozi toka ukanda wa Pwani, bahati mbaya na waziri husika nae ana tabia za kijanja janja tu.

Mafuta yakiwa machache maana yake kuna uwezekano mkubwa yakapanda bei, yakipanda bei na nauli zitaongezeka, gharama za maisha zinazidi kupanda kila siku mtanzania masikini anazidi kuisoma namba.
Wakati wa nyerere mafuta yalikua yanakosekana Sana,ni mwinyi toka pwani ndiye alyekomesha tatizo hilo
 
Rafiki yako ni muongo na mzushi kabisa, mdogo wangu yupo deep sea ndio wanadeal na meli za mafuta hakuna kitu kama hicho.
 
Ngoja tusubiri hiyo wiki ijayo.
Unaongelea wiki ijayo? Sasa hivi Kuna vituo kibao havina mafuta wafanyakazi wako nyumbani hawana kazi mleta mada muongo

Wiki ijayo kadanganya Sasa hivi Tayari wafanyakazi kibao wa vituo vya mafuta wako nyumbani hawana kipato kwani hulipwa kwa Lita wanayouza
 
Rafiki yako ni muongo na mzushi kabisa, mdogo wangu yupo deep sea ndio wanadeal na meli za mafuta hakuna kitu kama hicho.
Muongo wewe mafuta labda yako huko deep see vituo kibao Dar havina mafuta
 
Yawezekana uzushi huu ni mbinu ya wafanyabiashara wa mafuta ili wauze stock fasta maana wanajua bei ya mafuta kuanzia Dec itashuka Sana.
Sio uzushi wa wiki ijayo leo hii vituo kibao mitaani havina mafuta dar es salaam
 
Back
Top Bottom