Waziri January Makamba, ateua Wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa TPDC

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,877
TAARIFA KWA UMMA

Kufuatia uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kumteua Balozi Ombeni Sefue kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), leo nimewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Shirika hilo:

1. Ruth Zaipuna — Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB. Aliwahi kuwa Mkaguzi wa Mahesabu ya PriceWaterhouseCoopers na Afisa Mkuu wa Fedha Standard Chartered.

2. Dkt. Natu Mwamba - Mhadhiri Mwandamizi katika Shule Kuu ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Aliwahi kuwa Naibu Gavana Benki Kuu ya Tanzania.

3. Musa Makame — Mshauri Mwelekezi katika sekta ya mafuta na gesi. Aliwahi kuwa Afisa Mwandamizi wa Biashara katika kampuni ya Equinor (zamani Statoil) na kabla ya hapo Makamu wa Rais (Fedha na Utawala) katika kampuni ya Wentworth (zamani Artumas).

4. Mpambika William Chiume — Mshauri Mwelekezi kwenye sekta ya mafuta na gesi. Aliwahi kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya PanAfrican Energy na Mkuu wa Masuala ya Biashara wa Kampuni ya Ophir Energy na pia kama Msimamizi wa Miradi Kenya na Seychelles.

5. Protase Ishengoma - Mwanasheria Mbobezi wa Sekta ya Mafuta na Gesi.

6. Paul Makanza ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC), Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) na Makamu Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF).

7. Dismas Fuko ni Mshauri Mwelekezi wa Miradi ya Nishati hasa kwenye uchambuzi wa kifedha (Project Financial Modelling). Aliyekuwa Mkurugenzi wa Masoko na Uwekezaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)

8. Balozi Peter Kallaghe — Mkufunzi wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa (National Defense College). Aliwahi kuwa Msaidizi wa Rais Ikulu na kwa nyakati tofauti alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Canada na Cuba.

Uteuzi huu unaanza mara moja.

January Makamba (Mb.) Waziri wa Nishati
10 Juni 2022

IMG-20220610-WA0005.jpg
 
Posho ndefubtu wanSaini hata milion Mia Tisa huwenda wakatengewa wanabodo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom