Lubebenamawe
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 1,952
- 2,194
Kama meli inayoshusha diesel lita milion 60 na kufanya reserve ifikie lita milioni 150 zinazotosha kwa siku 24 tu sasa Mataragio alikosea nini kusema kuwa mafuta iliyopo inatosha kwa siku 15 tu iwapo hakuhusisha shehena ambayo kwa wakati haikuwa imefika?? Binafsi alikuwa sahihi. Hata kwa sasa waziri anajitapa eti tunashehena inayoweza kutupeleka mpaka siku 24. Aibu sana mi nilidhani angejivuna iwapo shehena iliyopo yaweza kutupeleka hadi miezi mitatu mpaka sita.Huenda Dk James Mataragio ambaye ni mkurugenzi mkuu wa TPDC akafutwa kazi kwa kile kilichosemwa na Makamba ni kuupotosha umma.
James, hivi karibuni alinukuliwa akisema endapo meli ya mafuta isipotia nanga ndani ya wiki mbili Nchi itashuhudia uhaba mkubwa wa mafuta jambo ambalo limeonekana kumkwaza Makamba.