Nuzulati Scott junior magnifico Jerusalem2006 Aizat
Tulipoingia kwenye kikao, wakasema wale wote mliowakamata hawajui lolote katika tukio la kulipua Ubalozi. Wakatuuliza tunaweza kupata askari anayelifahamu vizuri Jiji la Dar es Salaam? Tukawaambia ndiyo. Wakasema mleteni. Akaletwa (jina linahifadhiwa) kutoka makao makuu. Wakamuuliza unafahamu eneo linaloitwa Kimara? Akasema ndiyo. Wakasema tupeleke.....
Inaendelea......
“Aliwapeleka hadi Kimara. Wakamuuliza unaifahamu gereji ya (jina linahifadhiwa), akasema ndiyo. Wakamwambia tuonyeshe. Aakawapeleka hadi gereji. Pale gereji wakasema fundi anayeitwa (jina linahifadhiwa) yuko wapi? Akaitwa huyo fundi akaja. Wakajitambulisha kwake na kumweleza kuwa wao ni FBI kutoka Marekani na wanafuatilia ulipuaji wa Ubalozi wa Marekani. Wakamsihi asiwe na wasiwasi hawatamkamata, bali awape ushirikiano na taarifa watakazomwomba, ikiwa anazo.
“Wakamuuliza. Wiki mbili zilizopita ulitengeneza boksi la chuma hapa gereji? Akasema ndiyo. Wakamuuliza huyo mteja mlikuwa mnafahamiana? Akasema hapana, ila alikuja hapa alikuwa na kanzu nyeupe na ndefu nyingi, akanielekeza nimtengenezee boksi la aina hiyo.
Wakamuliza kama anajua anapoishi huyo mtu, akasema hajui. Wakamwambia alipigiwa simu na huyo mtu siku… baada ya hapo huyo fundi gereji waliongozana naye kwenda maeneo ya Ilala na kwingine ambapo walikamatwa watu wawili waliosaidia Ahmed Khalfan Ghailani kukamatwa nchini Pakistan na akawataja wenzake. Watu 14 dunia nzima walikamatwa na kuwekwa katika Gereza la Guantanamo Bay, Marekani.