Elias Msuya
Platinum Member
- Dec 23, 2011
- 197
- 795
Wakati matukio ya miili kuokotwa yakizidi kuokotwa ndani ya mwaka huu, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetaka ufanyike uchunguzi wa kimahakama kubaini vyanzo vya baadhi ya vifo hivyo.
Miili hiyo imekuwa ikiokotwa kwenye mito, fukwe, barabarani na maeneo ya wazi katika mikoa mbalimbali nchini, hali iliyozua hofu kubwa miongoni mwa wananchi kuhusu usalama wa maisha na ongezeko la vifo vya mazingira ya kutatanisha.
Jijini Dar es Salaam, tukio lililotikisa wengi ni la James Rogers Temba, mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Institute of Finance Management (IFM), ambaye mwili wake uliokotwa Aprili 30, 2026 ukielea kwenye Mto Msimbazi eneo la Kipawa, Ilala ukiwa hauna kichwa.
Uchunguzi wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ulipelekea kukamatwa kwa watuhumiwa watano, huku Mei 13 kichwa chake kikidaiwa kupatikana kikiwa kimefukiwa Kitunda Kibeberu. Tukio hilo lilizua mjadala mkubwa kuhusu ukatili na usalama wa vijana mijini.
Katika jiji hilo hilo, Mei 11, 2026 mwili wa Aisha Miraji, mkazi wa Nzasa Temeke, uliokotwa ukielea karibu na Daraja la Salender. Aisha alikuwa ametoweka siku moja kabla akiwa Muhimbili National Hospital alipokuwa akipatiwa matibabu ya muda mrefu. Taarifa zilisema mwili wake haukuwa na majeraha ya nje, jambo lililoacha maswali mengi kuhusu mazingira ya kifo chake.
Kadhalika, kikosi cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kiliuopoa mwili wa mwanamke mwingine mwenye umri unaokadiriwa kuzidi miaka 60 uliokuwa ukielea kwenye mto eneo la Stakishari, Ukonga. Wakati huohuo, taarifa nyingine zilieleza kuhusu mwili wa mwanaume asiyejulikana uliokuwa ukielea karibu na Daraja la Salender huku polisi wakiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Katika Wilaya ya Ilala pia, wananchi walishuhudia mara kadhaa miili ikiokotwa kwenye mkondo wa Mto Msimbazi, huku baadhi ya miili hiyo ikiwa haijatambulika mara moja. Matukio hayo yameendelea kuongeza taharuki kuhusu usalama wa watu wanaopotea katika mazingira yasiyoeleweka.
Nje ya Dar es Salaam, matukio hayo pia yameripotiwa, ambapo mkoani Manyara, Machi 20, 2026 mwili wa mwanaume asiyejulikana uliokotwa eneo la Magugu wilayani Babati ukiwa na majeraha makubwa kichwani yanayoaminika kusababishwa na shoka.
Katika eneo la mpaka wa Manyara na Arusha, miili ya watu wawili wasiojulikana ilikutwa imetelekezwa pembezoni mwa barabara ya Babati–Arusha katika kijiji cha Olasiti ikiwa na majeraha, huku pikipiki na simu zao zikikutwa karibu na eneo hilo.
Mkoani Arusha, mwili mwingine wa mwanaume ambaye hakufahamika ulionekana pembezoni mwa barabara kuu ya kuelekea Dodoma karibu na Uwanja wa Ndege wa Kisongo. Mashuhuda walidai mtu huyo aligongwa na gari na baadaye kuvutwa pembeni ya barabara akiwa na majeraha makubwa kichwani pamoja na mkono uliovunjika.
Katika Wilaya ya Handeni, Mkoa wa Tanga, mwili wa dereva bodaboda Abdallah Ibrahim Chambo maarufu “Chame” uliokotwa Mei 5, 2026 katika Mtaa wa Kilole. Taarifa za awali zilieleza kuwa alikodiwa na watu wawili usiku kabla ya kuuawa kwa kukatwa shingo na kuporwa pikipiki yake.
Aidha, katika Wilaya ya Mkinga, Tanga, kijana Mohamed Mohamed Kisingwe alipoteza maisha Februari 7, 2026 katika mazingira yaliyohusishwa na operesheni ya Drug Control and Enforcement Authority (DCEA), baada ya kudaiwa kuanguka akiwa anakimbia maafisa hao huku akiendesha pikipiki iliyobeba mirungi.
Mfululizo wa matukio haya umeendelea kuibua maswali makubwa kuhusu ongezeko la mauaji, ukatili, watu kutoweka na usalama wa raia katika maeneo mbalimbali nchini
Wakili William Maduhu wa LHRC amesema wamekuwa wakifuatilia matukio hayo, lakini imeonekana bado yanahitaji uchunguzi wa kijinai.
“Sisi kama watetezi wa haki za binadamu tunafuatilia matukio haya, japo bado kuna maswali mengi, lakini tunasikiliza taarifa zinazotolewa na Jeshi la Polisi,” amesema.
Hata hivyo, Maduhu anasema wamepata changamoto ya kupata ushirikiano kutoka familia za marehemu hao.
“Kutokana na utata wa vifo vyeneywe tulijaribu kutafuta familia za wahusika, lakini hatukupata ushirikiano. Kwa mfano familia ya James Temba, hawakuwa tayari kutoa ushirikiano. Hata ule mwili wa pili hatukupata taarifa za undani,” amesema.
Anaendelea, “Kunahitajika uchunguzi wa kina kwa sababu haiingii akilini mtu atokeo huko alikotoka na mwili wa mtu kisha aje autupe pale Selander Bridge ambako kuna ulinzi mkali saa 24 na kuna kituo cha polisi.
“Hata hiyo iliyokutwa kwenye mito, mwaka huu hakujawa na mvua kubwa za kuweza kusukuma mwili kutoka labda mto Gide hadi zilete kwenye ufukwe wa bahari.
“Hata mwili wa James Temba ulikutwa Bonde la Mto Mzimbazi mahali ambapo hakuna pori, uliwekwa na nani?”
Maduhu ameshauri kufanyika uchunguzi wa kimahakama, huku akishauri wanafamilia jutoa ushirikiano.
“Kuna Mahakama ya Corona, ambayo huwa inayoa amri ya uchunguzi wa vifo vyenye utata, lakini ni mpaka mtu afungue kesi. Tatizo, huwezi kufungua kesi bila ridhaa ya wanafamilia.” Amesema.