Ufisadi wa Kutisha: Wanasiasa na Viongozi wa Umma kununua viwanja kwa Mabilioni ya Pesa huko Arusha! Watanzania tusiposimama imara, tumekwisha

Kuna tuhuma nzito zimetolewa zikiwa na ushahidi kuhusu Viongozi wa Kisiasa na Utumishi wa Umma kununua viwanja kwa mabilioni ya pesa huko Arusha.

Kwenye tuhuma hizo zilizotolewa usiku huu na Mtanzania Mange Kimambi kupitia Akaunti yake ya X zimeonesha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Paul Makonda kanunua viwanja viwili vyenye thamani ya Bilioni 1.

Pia kwenye Orodha hiyo ameonekana Katibu wa Rais Bwana Waziri Salum, Mpambe wa Rais Brig General Nyambura Mashauri, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka, Waziri wa Ardhi Deogratius Ndejembi, Mbunge Christopher Ole Sendeka pamoja na kampuni mbalimbali.

Baada ya kuona orodha hii nimejiuliza maswali yafuatayo;

1. Viongozi na Wanasiasa hawa wamepata wapi pesa za kununua viwanja hivi?

2. Mchakato wa kuomba na kuuziwa viwanja hivi ulikuwaje?

Mwisho nawaonea huruma sana askari polisi wanaotumika vibaya kuwapiga virungu na kuwatesa Chadema ambao kimsingi wanapigania kuondoa Ufisadi nchini ili Watanzaia wote waishi maisha mazuri.

Pili nawaonea huruma sana TISS ambao kutwa kazi yao ni kuwalinda Mafisadi ambao wanaliibia hili taifa na kujinufaisha binafsi huku Watanzania wengi wakiteseka kukosa huduma za msingi na kufia kwenye umasikini wa kutisha.

Tatu nawaonea huruma JWTZ ambao wanakula kiapo cha kuilinda Katiba inayoweka misingi ya utawala bora na uwajibikaji wakati Viongozi wa nchi hii wanakiuka hiyo misingi na kufanya ufisadi wa kutisha huku wao wakiwepo.

Watanzania tuna kila sababu kuwaunga mkono Chadema ili kuhitimisha huu ufisadi unaofanywa dhidi ya nchi yetu na Taifa letu.

Kuna kila sababu tuipambanie No Reform No Election ili tupate Viongozi wanaowajibika kweli kwetu na ambao tutaweza kuwawajibisha.
Kuleni urefu wa kamba zenu (Hangaya, 2022).
 
Viongozi karibu wote wana mabilioni wamejilimbikizia. Nilipoona yule waziri uso wake umemvimba kama kapigwa ngumi, anataka kununua eneo la biashara kwa 1.5 B sema wao wanataka 3 B.

Ndiyo tuone kwanini, kama nchi na wananchi wake hawapati huduma nzuri za kibinadamu. Sababu kuna kikundi cha watu wanagawana wao na watu wao. Nyinyi mtajijua wenyewe.
Wapi huko?
 
Tanzanians are too gullible.

Easily tossed to and fro by every wind of cheap gossip, human cunning, craftiness and deceitful schemes.

Where Bashite gets his money is none of my business, all I can say is that Mange's Report is all bonkers.

Unbelievable....​
None of your business? Really? Whose business is it?

In the grand scheme of things, Mange’s allegations aren’t unreasonable. You don’t need Mange’s report to conceive a suspicion that there’s widespread looting in the government. Samia’s wasteful spending, for example, is a trailing indicator of looting!
 
Kati ya siku nimetamani ningekuwa mwanajeshi ni leo baada ya kumsoma mange.

Juzi nimeenda Hospitali Chanika nimeambiwa dawa hamna nenda pharmacy ya nje ya hospitali alafu leo unaingia mtandaoni unakutana na hii habari.
Utapata pressure bure
Fanya mambo yako kalale
 
Viongozi karibu wote wana mabilioni wamejilimbikizia. Nilipoona yule waziri uso wake umemvimba kama kapigwa ngumi, anataka kununua eneo la biashara kwa 1.5 B sema wao wanataka 3 B.

Ndiyo tuone kwanini, kama nchi na wananchi wake hawapati huduma nzuri za kibinadamu. Sababu kuna kikundi cha watu wanagawana wao na watu wao. Nyinyi mtajijua wenyewe.
Acheni wivu
Tafuta chimbo ulambe asali
 
Kuna tuhuma nzito zimetolewa zikiwa na ushahidi kuhusu Viongozi wa Kisiasa na Utumishi wa Umma kununua viwanja kwa mabilioni ya pesa huko Arusha.

Kwenye tuhuma hizo zilizotolewa usiku huu na Mtanzania Mange Kimambi kupitia Akaunti yake ya X zimeonesha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Paul Makonda kanunua viwanja viwili vyenye thamani ya Bilioni 1.

Pia kwenye Orodha hiyo ameonekana Katibu wa Rais Bwana Waziri Salum, Mpambe wa Rais Brig General Nyambura Mashauri, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka, Waziri wa Ardhi Deogratius Ndejembi, Mbunge Christopher Ole Sendeka pamoja na kampuni mbalimbali.

Baada ya kuona orodha hii nimejiuliza maswali yafuatayo;

1. Viongozi na Wanasiasa hawa wamepata wapi pesa za kununua viwanja hivi?

2. Mchakato wa kuomba na kuuziwa viwanja hivi ulikuwaje?

Mwisho nawaonea huruma sana askari polisi wanaotumika vibaya kuwapiga virungu na kuwatesa Chadema ambao kimsingi wanapigania kuondoa Ufisadi nchini ili Watanzaia wote waishi maisha mazuri.

Pili nawaonea huruma sana TISS ambao kutwa kazi yao ni kuwalinda Mafisadi ambao wanaliibia hili taifa na kujinufaisha binafsi huku Watanzania wengi wakiteseka kukosa huduma za msingi na kufia kwenye umasikini wa kutisha.

Tatu nawaonea huruma JWTZ ambao wanakula kiapo cha kuilinda Katiba inayoweka misingi ya utawala bora na uwajibikaji wakati Viongozi wa nchi hii wanakiuka hiyo misingi na kufanya ufisadi wa kutisha huku wao wakiwepo.

Watanzania tuna kila sababu kuwaunga mkono Chadema ili kuhitimisha huu ufisadi unaofanywa dhidi ya nchi yetu na Taifa letu.

Kuna kila sababu tuipambanie No Reform No Election ili tupate Viongozi wanaowajibika kweli kwetu na ambao tutaweza kuwawajibisha.
Taarifa inayotolewa na Mange Pigia Mstari.

Niliwaambia mkija kupata akili mtamuelewa sana LISU kudai reform ya hakika bila ya ku compromise.

Hoja za CCM kwamba reform inalengo la kuiweka nchi kwenye machafuko ni hoja yenye Nia ya kulinda maslqhi ya wachache

Pia niliwaambia yule katibu yule muangalieni sana.Akija Rais mpya huyu jamaa apandishwe kizimbani. Afunguliwe mashtaka ya Ufisadi na kuhujumu Uchumi… kuna mengi ya kifisad nyuma yake

NYUma yake kuna Anafanya Ufisadi mkubwa sana kwa kushirikiana na boss wake

Samia hana control ya financial resources … she can’t change … yupo hivo kwa sababu ndio yupo hivyo.

Mnajiuliza deni lipo juu , serikali inakopa sana na kuuza resources but yet nchi haina maendeleo.

Kila kona barabara zinajengwa utasema ndio tumepata uhuru jana

4 years barabara za mjini tu hazijakamili na kila siku unawaona watu wapo busy …. Kuna shida mahali

Amueni watanzania, wengine tulishahamisha na familia zetu ….. no life in Tanzania … ni survival of the fittest… kumkoMa nyan giadi
 
Kati ya siku nimetamani ningekuwa mwanajeshi ni leo baada ya kumsoma mange.

Juzi nimeenda Hospitali Chanika nimeambiwa dawa hamna nenda pharmacy ya nje ya hospitali alafu leo unaingia mtandaoni unakutana na hii habari.
Usingeweza kufanya chochote hata ungekuwa mwanajeshi. Jeshi letu lilipewa nidham ya ajabu sana

Ili kufanya lolote…. Lazima kuwe na a very organized elite, few of them na wawe top management …. Hii ni ngumu cause top management wanalishwa neema sana

Wanaoumia na kuwa na life ngumu ni hao wanajeshi wa Lower level

Hivi unajua Brigedia General Salary yake haifiki 6M , ? Do you know that

Maafisa wajeshi wanna salary ndogo sana

Pesa ya nchi inaliwa na Politicians na familia zao
 
Kuna kila sababu tuipambanie No Reform No Election ili tupate Viongozi wanaowajibika kweli kwetu na ambao tutaweza kuwawajibisha.
Maneno hayo ndiyo yaliyobeba uzito wote wa mada.

Polisi; TISS; JWT,.'..rank and file' ni kuwaonea tu kuwaweka kwenye lawama hizi. Kukosekana kwa majina ya viongozi wa vikosi hivyo kwenye orodha ya Mange ndiko kukufanye kusahau ni nani anajibu lawama kwa vijana wa vikosi hivyo?

Watu kama huyo Nyambura kwenye orodha hiyo, naye utasema kachota mahali mali ya umma na kwenda kuimwaga kwenye ardhi ya Arusha?
Hii vita haitawezekana kwa kusambazia matope kila mtu bila ya kulenga wahusika wenyewe; kama huyo Bashite mwenye bilioni, sijui kaitoa wapi?
 
Kati ya siku nimetamani ningekuwa mwanajeshi ni leo baada ya kumsoma mange.

Juzi nimeenda Hospitali Chanika nimeambiwa dawa hamna nenda pharmacy ya nje ya hospitali alafu leo unaingia mtandaoni unakutana na hii habari.
Bado ninakushangaa sana ulivyo badilika nyuzi 360 kamili! Hii si kawaida kabisa. Sijui kulitokea kitu gani katika muda mfupi vile uliokufanya uwe tofauti kabisa na ulivyo sasa.
 
Tanzania is a bandit economy, no doubt about it. But I have been in real estate business for a while to understand that, this bizarre report is laced with exaggerations and financial ignorance.

Plots/Landed Properties are not always bought at a market price enunciated within the valuation report. The law mandates it, but things are different on the ground.

It's like the frenzied sale of plots at O'Bay and Masaki under Magufuli, where Government officials bought houses at a cheaper price only to later value them in billions.

Akili Kumkichwa Mwanangu...​
Shida siyo bei ya kiwanja, shida ni hao watumishi wa serikali wanapata wapi hayo Mabilioni ya ku nunua viwanja?
 
Maneno hayo ndiyo yaliyobeba uzito wote wa mada.

Polisi; TISS; JWT,.'..rank and file' ni kuwaonea tu kuwaweka kwenye lawama hizi. Kukosekana kwa majina ya viongozi wa vikosi hivyo kwenye orodha ya Mange ndiko kukufanye kusahau ni nani anajibu lawama kwa vijana wa vikosi hivyo?

Watu kama huyo Nyambura kwenye orodha hiyo, naye utasema kachota mahali mali ya umma na kwenda kuimwaga kwenye ardhi ya Arusha?
Hii vita haitawezekana kwa kusambazia matope kila mtu bila ya kulenga wahusika wenyewe; kama huyo Bashite mwenye bilioni, sijui kaitoa wapi?
Hao Polisi TISS na JWTZ hawana mpango chochote hawawezi fanya chochote . TISS kazi yao kubwa ni ipi? Zaidi ya kukimbizana na upinzani

JWTZ kuwatisha raia na magwanda

Pambanieni nchi yenu
 
Back
Top Bottom