Ni wazo zuri, make Tanesco wanajisahau sana mpaka kero.

Shirika lina watendaji wabovu kweli ambao hawawajibiki ipasavyo sijui hata waziri wa Nishati na Madini haoni akafanya afumue sehemu zenye kasoro na afanye reform.
 
Nunua kwa TIGOPESA App, watakata ela Ila baada ya 2-3 hrs watatuma umeme.
Nimenunua hivo jana mara 2 na leo asubuhi.
Ila wa leo asubuhi umekataa kuingia.
 
Ameshaweka waziri Nishati na madini basi ni vyema kushuka hadi meneja TANESCO, mabwawa ya umeme na vituo vya kupoza umeme. Hii nchi ni ngumu sana ina vikundi vya kukwamisha rais
 
Majuzi nilikutana na toyo imepakia magenereta kama vile mnunuzi alipewa tahadhari ya umeme kuwa shida hivi karibuni.

Hebu tuone kama mama ataliweza hili!
 
Siyo kweli, kaongeze na darasa la Cyber security alafu uje ulete mrejesho.
Yaaah upo sahihi pia , Tena sana tu, zote ni possibilities na hata kuchokonoa mfumo hata Kama ww ni developer ni sehemu ya cyber...yote hii ni katka kujisetia mazngra ya maintenance au namna yoyote ile ya kupiga hela
 
Hata Mimi juzi mimi niliweka wa elfu moja kwa airtel ukakubali, nikaweka elfu tano kwa Hallotel, ikakataa!
nahisi mtandao upo down hivyo tuendelee tu kujarijaribu maana hata mimi nilijaribu kununua zaidi ya mara nne ikagoma but baadae ilikubali hivyo tuendelee kujarijaribu but ukipata fursa nunua mwingi maana huwez jua tatizo hili litaisha lini
 
Mazingira ya upigaji yanaandaliwa hapo kuna kampuni itapewa tenda ya kurekebisha huo ufumo alafu baadae uliza wamelipwa shingapi

Utabaki kinywa wazi
 
nahisi mtandao upo down hivyo tuendelee tu kujarijaribu maana hata mimi nilijaribu kununua zaidi ya mara nne ikagoma but baadae ilikubali hivyo tuendelee kujarijaribu but ukipata fursa nunua mwingi maana huwez jua tatizo hili litaisha lini
Ni kweli, ndo maana nimemwambia Mpendwa asikimbilie kumwita jamaa mzushi, kwa kusema alifanikiwa kununua!
 
Mama anajihujumu mwenyewe anademka tu unategemea wenzake wasidemke ni kama third law of motion

#gogo gang
#sukuma gang
#chadema4revolution
 
Majuzi liripotiwa hapa JF mfumo wa TRA kuwa na dosari baada ya Uwepo wa moto HQ.
Jana na Leo TANESCO mfumo uko taabani.
Mifumo mingine muhimu pia imekuwa down wakati EGA wapo, Waziri Ndungulile, Katibu Mkuu wa Sayansi na Teknolojia yupo lkn hawana majibu yoyote kuhusu kadhia hii ya Mifumo ya TEHAMA
Mwisho tutaambiwa mifumo hiyo haifai, imeleta mfumo mpya. Hapo ndio upigaji wa mil 7 Kwa dk utakaporudi.
 
Kwanza nianze kwa kukiri kwamba mimi ni sio mwanasiasa ila kwa kipindi fulani nilikuwa shabiki mkubwa wa chadema.Kiukweli miongoni mwa wale waliokuwa wakimponda sana na hata kutokuhuzunishwa na kwenda kwa mwendazake na mimi nilikuwemo.Ninakiri wazi kuwa nilifanya makosa makubwa sana na sikujua kuwa nilikuwa nakataa almasi kwa kukusanya kokoto.

Ni miezi miwili sasa mzigo wangu umekwama bandarini kwa madai kuwa taratibu za ushuru kutokukamilika hali ya kuwa risiti zote halali ninazo.Mbaya zaidi ni mzigo wa biashara hivyo kadri muda unavyoenda nazidi kupata hasara.Sikujua kuwa ukali wa kiongozi mkuu unaweza kusaidia watendaji wa chini wakatimiza majukumu yao kwa weledi na uharaka kwa kumjali mwananchi.Pili hali ya umeme huku mtaani kwetu ni tete,Kila mara umeme unakatika,Na mita za luku system hazifanyi kazi mara kwa mara umeme haununuliki.Ninajiuliza mbona kipindi cha mwendazake haya mambo hayakuwepo? Ina maana utendaji wa hawa wafanyakazi unaangalia zaidi kiongozi mkuu aliyepo juu yao?

Kiukweli nimeshuhudia mambo mengi ya hovyo ndani ya muda huu mfupi,Tukiachilia mbali la kuahirishwa mechi ya Simba na Yanga bila kiongozi yoyote kuchukuliwa hatua,Madawa ya kulevya yameongezeka kwa kasi huku mitaani,wizi na ujambazi navyo vinashamiri ndani ya muda mfupi,Kwanini?

Kwakweli niseme tu kuwa ninajuta sana kumponda mwendazake popote alipo anisamehe na Mungu anisamehe.Na ninamuombea azidi kupumzika kwa amani.
 
Natumaini humu ndani kuna wajuvi wa mambo mengi sana.

Naombeni mnisaidie ni kwa namna gani naweza nunua umeme wa LUKU nje ya mfumo.

Kuna vijana 3 wananitegemea, posho yao inategemea uwepo wa umeme. Sasa wananililia hapa na mimi cha kuwasaidia nimeshindwa maana nategemea umeme ili nipate cha kuwapa.

Hivi generator nzuri ya umeme ina sh. ngapi kwa wastani?
 
Hii itakua hujuma aisee , maana haijawahi tokea huduma hii muhimu kuwa down siku tatu,
Kwa hili bila Shaka kuna watu wanatakiwa kuwajibishwa aisee
 
Back
Top Bottom