tanesco

TANESCO
Shirika la umeme Tanzania(TANESCO) ni shirika la umma nchini Tanzania lililoanzishwa November 26, 1931 na liliitwa 'Tanganyika Electric Supply Company Limited' kazi yake kubwa ikiwa ni kuzalisha na kusambaza umeme nchini Tanzania.
  1. Suley2019

    Biteko: TANESCO inanunua umeme wa Megawati 31 kutoka Uganda na Zambia

    Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko bungeni jijini Dodoma, wakati akisoma hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2024/2025 amesema: Katika mwaka 2023/24 Serikali iliendelea kuchukua hatua za kuimarisha uzalishaji na upatikanaji wa umeme nchini ambapo hadi...
  2. C

    TANESCO: Umeme tunaozalisha ni mwingi mahitaji ni madogo nchi nzima, hakuna mgawo kwa sasa

    Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema limelazimika kuzima mitambo mitano kwakuwa majitaji ya umeme yapo chini huku uzalishaji wa umeme ukiwa ni mwingi. TANESCO imesema hayo wakati Afisa wa Shirika hilo akiongea mbele ya Waziri Mkuu kwenye Maonesho ya Wiki ya Nishati yaliyofanyika Viwanja...
  3. Petro E. Mselewa

    Ndugu zetu TANESCO, tatizo nini tena?

    Jana usiku, maeneo ya Kibaha mkoani Pwani, umeme ulikatika. Hata sasa, umeme umekatika tangu asubuhi. Ni hivi karibuni tu ndugu zetu TANESCO mmepongezwa kwa kuzalisha umeme mwingi kuliko matumizi yetu watanzania. Sasa haya ya kukatikakatika kwa umeme yanatokana na nini? Kama ni mgawo tena...
  4. P

    Waziri Mkuu Majaliwa: TANESCO imezalisha umeme zaidi ya mahitaji

    Waziri Mkuu majaliwa ameipongeza TANESCO kwa kuzalisja umeme zaidi ya mahitaji yaliyopo sasa, "Leo tarehe 19 April 2024 uzalishaji wa umeme ni mkubwa, shirika letu la TANESCO limemudu kuzalisha umeme zaidi ya mahitaji tuliyonayo na bwawa la Nyerere limeanza kazi, tayari Megawati 235 ziko kwenye...
  5. Jumanne Mwita

    Ilikuchukua muda gani mpaka kuunganishiwa Umeme na Tanesco?

    Mtaa ninamoishi una makazi mengi sana, tena watu hujenga kama vile wamavamia, ila ukweli ni kwamba watu wamejenga, siyo siri. Nikifikiria siku ninunua hapa, miji haikuwepo kabisa. Ilikuwa ni wazi, unaweza sema kwamba uwezekano wa watu kuja eneo lile haukuwepo, au isingechukua muda mfupi wawe...
  6. Shark

    Zoezi la TANESCO la kubadili Mita limejaa Usumbufu, Utapeli na Ubabaifu

    Kwema Wakuu, Mimi ni mkaazi wa Kitongoji Kimoja wilaya ya Kinondoni hapa Dar es Salaam. Jumatatu nilipigiwa simu na watu wa TANESCO kunifahamisha kua Kwa kua number ya mita yangu inaanzia na 24... basi nitabadilishiwa mita hiyo kesho yake yaani juzi. Juzi Jumanne kweli walikuja asubuhi...
  7. A

    TANESCO yakemea upotoshaji kuhusisha mafuriko Pwani na JNHPP

    TANESCO yakemea upotoshaji kuhusisha mafuriko Pwani na JNHPP DODOMA: SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limefafanua kuwa Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) limechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza athari za mafuriko katika maeneo ya Wilaya za Rufiji na Kibiti, tofauti na...
  8. M

    TANESCO na Serikali walipeni watu fidia wahamishwe Rufiji. Bwawa la Umeme ni muhimu. Kila Mtanzania achangie fidia kwa kuongezewa 1000 kwenye Luku

    Bwawa la umeme Rufiji ni muhimu sana kwa nchi nzima. hivyo tunapaswa wa Tanzania wote kulilinda bwawa lisibomoke kwa kuchangia pesa za fidia ya kuhamisha watu wote wa rufiji maana umeme tunautaka wote Tanzania nzima Hali ya rufiji ni mbaya. nawaza tu kwa nini serikali isiwahamishe wakazi...
  9. Roving Journalist

    Dkt. Biteko: Watendaji wazembe TANESCO kuanza kuchukuliwa hatua kila mwezi

    Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ameagiza ripoti ya taarifa kila wiki ya Kituo cha Huduma kwa Wateja ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ianze kutolewa kila mwezi ili kufahamu maeneo yenye changamoto ya umeme nchini na kurahisisha watendaji wazembe kuchukuliwa hatua...
  10. N

    TANESCO imetosha sasa, huu umeme wa kushituashitua namna hii bora usiwepo maana upo ila hatuwezi kuutumia

    TANESCO, Huu ndio umeme mmeona leo mtulee watu wa Mbezi mwisho kweli, hivi mna nini nyie? Hapo ukute kwenye ripoti zenu mmejaza Mbezi wana umeme ndio huu? Sisi tutaufanyia nini iwapo hata taa tu inasumbuka kiasi hiki? Au mnalengo la kutuunguzia vitu, maana ukitulia dk 5 unaaanza kwa spidi a...
  11. Jidu La Mabambasi

    Kukatika umeme Pasaka, TANESCO mnatupiga changa la macho, ni uzembe

    Jumapili saanane usiku na jumatatu ya Pasaka haikuwa njema. Umeme ulikatika karibia nchi nzima. Chanzo cha tatizo kilikuwa kujizima mitambo huko Kidatu Tumeelezwa na TANESCO kuwa , kujizima huko kunatokana na maji "kuzidi" na mitambo kujizima. Maelezo hayo kimsingi hayana maana kabisa...
  12. JanguKamaJangu

    Naibu Waziri Mkuu Dkt. Biteko afichua orodha ya matendo ya uhujumu wa miundombinu ya TANESCO

    Hizi hapa Nukuu za Dkt. Biteko akifichua Mtao wa uhujumu miundombinu 1. ’'Tarehe 13 mwezi wa pili mwaka 2024, BAGAMOYO alikamatwa mtu mmoja pale akiwa na Lita 80 za mafuta ya Transfoma, kesi imefunguliwa, maana yake ile Transfoma imekufa mafuta yamesha chukuliwa’’ 2. ‘’Mwezi wa tatu tarehe...
  13. Vichekesho

    TANESCO Hamko serious hata kidogo

    Nimegundua mita yangu haikati umeme hata unit zikiisha, ni mpya kabisa na imefungwa kwenye nguzo yao ya umeme. Wamefunga mita za nyumba kama 4 kwenye nguzo hiyo, kwahiyo tunatumia vile vi remote ku control. Sasa baada ya kubaini hitalafu hiyo jana nikaenda kwenye ofisi yao kuripoti, mhudumu...
  14. Replica

    Waandishi wetu bhana! Kapewa tip Tanesco vibarua wanalipwa 15,000 kwa mwezi kaileta redioni kama ilivyo

    Mwandishi wa Wasafi ambae jina sijalipata, kapata tip huko mtaani vibarua wa Tanesco wanalipwa elfu 15 kwa mwezi nae kaibeba kama ilivyo kaja nayo redioni bila hata kufanya kitafiti kidogo. Angejiuliza tu 15,000 ukiigawa kwa siku 30 unapata jero kila siku, tenahapo akadai na NSSF wanaikata...
  15. Pfizer

    Miaka Mitatu ya Samia Arusha: TANESCO Pekee ndio waliompunguzia 'point'

    Wananchi katika Mkoa Wa Arusha wameeleza kuridhishwa na kazi inayoendelea kufanya na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Nchini hususani katika kuwaleta wananchi pamoja na utekelezaji Mbalimbali Wa Miradi ya maendeleo na kutoa ahueni ya wafanyabiashara kufanya Biashara zao Kwa uhuru. Wameyasema hayo...
  16. U

    TANESCO watorosha Maji Bwawa la Nyerere, na kuharibu mazao Kwa mafuriko

    Licha ya TANESCO kutoa adhabu ya kugawa Umeme Kwa wananchi wa TANZANIA na kuendeleza mateso hawajaridhika na sasa wameamua kufungulia maji ya bwawa la nyerere na kusababisha mafuriko makubwa na uharibifu wa mazao katika vijiji vilivyopo mkondo wa chini wa bwawa hilo. Maji hayo ambayo...
  17. Inside10

    Naibu Waziri Mkuu Doto Biteko ateua Wajumbe wapya Bodi ya TANESCO

    Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amefanya uteuzi wa wajumbe wanane wa bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) watakaohudumu kwa miaka mitatu. Wajumbe hao ni Dk Lucy Mboma, Isaack Chanji, Boma Raballa, Grace Joachim, Profesa Hellen Bandiho, Balozi Zuhura...
  18. kichongeochuma

    USHAURI: TANESCO kutokana na ukubwa wa huduma yenu kuna ulazima kuanzisha TANESCO KATA

    Nashauri kuwe na TANESCO kwa kila kata hata kukiwa na fundi mmoja tuu akasaidiana na hawa mafundi wasaidizi waliopo ili kutatua changamoto za umeme ambazo zinatokea kwa sababu kuna wakati inaanguka nguzo tu ya umeme lakini inaweza kuchukua hadi wiki 2 bado hawaja badilisha wakati huduma yao...
Back
Top Bottom