Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879

TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA MANUNUZI YA LUKU KWA BAADHI YA WATEJA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawaomba radhi wateja wake kutokana na hitilafu iliyotokea kwenye mfumo wa manunuzi ya umeme wa LUKU siku ya Jumatatu, Mei 17, 2021 na kusababisha baadhi ya wateja kushindwa kununua umeme.

Tunaomba uvumilivu wakati wataalamu wetu wanafanya kazi kuhakikisha tatizo hilo linatatuliwa haraka.

Tutaendelea kutoa taarifa kadri huduma itakavyo kuwa ikirejea.

Tunawaomba radhi kutokana na hitilafu iliyotokea kwenye mfumo wa manunuzi ya umeme wa LUKU siku ya Jumatatu, Mei 17, 2021 na kusababisha baadhi ya wateja kushindwa kununua umeme. Tunaomba uvumilivu wakati wataalamu wetu wanafanya kazi kuhakikisha tatizo hilo linatatuliwa haraka.

---
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA MANUNUZI YA LUKU KWA BAADHI YA WATEJA


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawaomba radhi wateja wake kutokana na hitilafu iliyotokea kwenye mfumo wa manunuzi ya umeme wa LUKU siku ya Jumatatu, Mei 17, 2021 na kusababisha baadhi ya wateja kushindwa kununua umeme.

Tunaomba uvumilivu wakati wataalamu wetu wanafanya kazi kuhakikisha tatizo hilo linatatuliwa haraka.

Tutaendelea kutoa taarifa kadri huduma itakavyo kuwa ikirejea.

Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza

Kituo cha miito ya simu makao makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya kijamii

Twitter: www.twitter.com/tanescoyetu

Facebook Tanesco Yetu

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
Mei 18, 2021.


MAJIBU YA NAIBU WAZIRI WA NISHATI, STEPHEN BYABATO

Tumepata shida kubwa sana kwenye mfumo wa kidigitali wa kununua na kuuza LUKU lakini tunalishughulikia, tunaahidiwa na wataalamu wetu kabla siku ya leo haijaisha tatizo la LUKU litakuwa limeisha, niwaambie Watanzania wote kama ukifika ofisi za TANESCO unaweza ukanunua umeme, shida iliyopo ni kwenye mifumo ya kibenki na simu. Ninaomba radhi kwa niaba ya wenzangu

Tunaahidiwa na wataalamu wetu kabla siku ya leo haijaisha tatizo la LUKU litakuwa limeisha, niwaambie Watanzania wote kama ukifika ofisi za TANESCO unaweza ukanunua umeme, shida iliyopo ni kwenye mifumo ya kibenki na simu. Ninaomba radhi
 
Ni siku ya pili leo ununuzi wa luku kupitia mitandao yote ni shida tupu, mamlaka husika zipo Taarifa hatupewi tupo tu gizani mimi naona viongozi wa TANESCO wameanza kuleta siasa na uhujumu aiingii akilini wataalamu mnao wanashindwa kurejesha mfumo kwa siku mbili no, huu ni uzembe.

Wiki mbili zilizopita walikuwa wanachezea tu umeme mara wawashe mara wanazima mara zaidi ya ishirini mpaka wakaunguza vitu kibao vya jirani yangu almanusura nyumba iungue moto,no tanesco mmechoka tunamuomba Mama awamulike huko mmezidi upuuzi.
 
Uvumilivu hadi lini? Boresheni mifumo I we na mmbadala Tanesco ni shirika kubwa sana ni aibu hii
Mkuu nasoma computer science....katika programming hakuna hitirafu ,na hata virus ni program ya computer inayofanya kazi kwa kuipa ubize computa au kupiga copy au kudelete files muhimu na ni mtu anaeza tengeneza virusi, hebu nirud kwenye point, program ikiandikwa haibadiliki, ni pure number ile, I mean automation is perfect, Kama ilivo 1*1=1 it can't change.

Changamoto huwa ni pale uneunda program kwa Kaz flan na ofisi ikaongeza matumizi au huduma ambazo hujaziprogram, yaan zifanyike manually.

Jawabu ni kwamba programmers huwa wanachokonoa system ili wapige pesa ya maintenance, Kwan huwa wanaacha backdoors za wao kuingia na kuedit mifumo, hvo program ni solution ya ku automate shughuli mbali mbali, hazibdiliki na ni lazma mumlipe programmer pesa nyingi Kwan inahtajika solution ya haraka ili Mambo yasisimame, believe me namuona mtu akipga pesa ndefu nyuma ya hil tatzo, labda Kama wameuzma ili kuboresha huduma
 
Wakuu toka jana tarehe 17/ May umeme was Tanesco kwa mfumo was Luku haupatikani kabisa. Tanesco wanachodai ni Kuwa mfumo upon down. Kwa zaidi ya Masaa 24 wateja wanakosa huduma ya umeme, serekali nayo inakosa mapato yake.

Najiuliza je hii inaweza kuwa ni hujuma kukwamisha juhudi za mama? Ingefaa wahusika wachunguze kulikoni Tanesco?
 
Ni siku ya pili leo ununuzi wa luku kupitia mitandao yote ni shida tupu,mamlaka usika zipo taharifa atupewi tupo tu gizani mi naona viongozi wa tanesco wameanza kuleta siasa na uhujumu aiingii akilini wataalamu mnao wanashindwa kurejesha mfumo kwa siku mbili no, huu ni uzembe.

Wiki mbili zilizopita walikuwa wanachezea tu umeme mara wawashe mara wanazima Mara zaidi ya ishirini mpaka wakaunguza vitu kibao vya jirani yangu almanusura nyumba iungue moto,no tanesco mmechoka tunamuomba Mama awamulike huko mmezidi upuuzi.
Haya ndo yatafanya akumbukwe
 
Mkuu nasoma computer science....katika programming hakuna hitirafu ,na hata virus ni program ya computer inayofanya kazi kwa kuipa ubize computa au kupiga copy au kudelete files muhimu na ni mtu anaeza tengeneza virusi, hebu nirud kwenye point, program ikiandikwa haibadiliki, ni pure number ile, I mean automation is perfect, Kama ilivo 1*1=1 it can't change.

Changamoto huwa ni pale uneunda program kwa Kaz flan na ofisi ikaongeza matumizi au huduma ambazo hujaziprogram, yaan zifanyike manually. Jawabu ni kwamba programmers huwa wanachokonoa system ili wapige pesa ya maintenance, Kwan huwa wanaacha backdoors za wao kuingia na kuedit mifumo, hvo program ni solution ya ku automate shughuli mbali mbali, hazibdiliki na ni lazma mumlipe programmer pesa nyingi Kwan inahtajika solution ya haraka ili Mambo yasisimame,,, believe me namuona mtu akipga pesa ndefu nyuma ya hil tatzo, labda Kama wameuzma ili kuboresha huduma
Naelewa unachokizungumzia pengine kuna ukweli ndani yake ila kwa shirika kubwa hivyo ni lazma wawe na mmbadala na usalama wa system yao kingine system lazma ziwe updated continuously kwa kuwa programmers wanakuwa na ile prototype hivyo swala La virus so kesi kubwa kama wanafanya kazi na watu kwenye ufanisi wakutosha, swala La kwamba system imezidiwa ni wao kutokuwa na mikakati ya muda mrefu maana kila siku wateja wanaongezeka ni swala la installation ya serves zenye uwezo wa kuwahudumia kwa pamoja
 
Leo Siku ya tatu, nyumbani umeme umekata, afu shida sielewi Ni nini?

Kama niluku sina uwakika kama imeisha Ila umeme ulikata ghafla tu, kwenye nyumba yetu, Na nyumba zingine upo mpka muda huu, lakini toka Jana naweka Luku inagoma, nikajua kwasababu kulikua Na shida ya mtandao.

Jana kila ukijalibu kununua umeme, wanakwambia huduma aipatikani kwa sasa jaribu tena, baadae, lakin usiku wa saa nne nikabahatika nikatumiwa tokeni, kila nikiingiza kwenye mashineni ya luku, inaandika reject hata sielewi, shida Ni nini? Kwa mwenye uelewa wa ilo tatizo, anisaidie hata ushauri
 
Haya ndo yatafanya akumbukwe
Mama kati ya Taasisi korofi na hatari kwako ni TANESCO wazingue mapema kama alivyofanya Hayati hawafai. Dr Kaleman tunakuomba utafune kichwa cha MD hawa wanafanya kazi kwa mazoea. Siku ya 3 bila mtandao wa Luku hasara kwa taifa na usumbufu kwa nchi.
 
Majuzi liripotiwa hapa JF mfumo wa TRA kuwa na dosari baada ya Uwepo wa moto HQ. Jana na Leo TANESCO mfumo uko taabani.

Mifumo mingine muhimu pia imekuwa down wakati EGA wapo, Waziri Ndungulile, Katibu Mkuu wa Sayansi na Teknolojia yupo lkn hawana majibu yoyote kuhusu kadhia hii ya Mifumo ya TEHAMA
 
Hapana inaweza kuwa kweli ni shida za kiufundi na zinaweza kutokea awamu yeyote tu!
Muda wa tatizo ni mrefu mno na haijawahi kutokea, majumuisho ya hasara yanotokana na hill tatizo ni makubwa sana kwa upande wa shirika la umeme na serekali kukosa mapato na adha kubwa kwa wananchi na wanaweza wakapoteza imani na utendaji wa serekali ambyo inaweza kuwa mtaji kwa wasiofurahia uongozi mzuri na wenye matumaini tele wa mama.
 
Majuzi liripotiwa hapa JF mfumo wa TRA kuwa na dosari baada ya Uwepo wa moto HQ.
Jana na Leo TANESCO mfumo uko taabani.
Mifumo mingine muhimu pia imekuwa down wakati EGA wapo, Waziri Ndungulile, Katibu Mkuu wa Sayansi na Teknolojia yupo lkn hawana majibu yoyote kuhusu kadhia hii ya Mifumo ya TEHAMA
EGA - (Kwa urefu)?
 
Back
Top Bottom