Larson
JF-Expert Member
- Dec 9, 2015
- 206
- 148
Yuko vizuri, Sera zake zinaeleweka kamanda, sio lazima kila mgombea aongee kama Lissu. CCM mbele kwa mbele, CCM tano tena.Mh sana Rais na Mgombea Urais wa CCM ndugu John Magufuli pokea ushauri wangu huu wa bure kabisa.
Mosi, nakushauri sana tena sana. Usimjibu Tundu Lissu maana kwa kufanya hivyo utaendelea kutapata aibu kubwa.
Level za Lissu ni za juu sana sioni mwanaccm wa sasa wa kuweza kushindana nae kwa hoja kwahiyo kwa heshima yako na ya chama chako jikite tu kwenye sera zenu. Hilo la kwanza.
La pili nakushauri usipende kuiga na kutaka kutembelea nyota ya Lissu. Usidandie treni kwa mbele hasa ahadi ambazo chama chako haijazifanyia utafiti hivyo kutoka na uwezo wa kuzitekeleza km mlivocopy sera ya Chadema ya elimu bora na bure. Hili pia litakufedhehesha ww binafsi na chama chako iwapo utaendelea.
Ni hayo tu kutoka kwangu, kukubali au kukataa ni uamuzi wako. Ushauri kama huu huwezi kupewa na mwanaccm wao kazi yao kubwa ni kujipendekeza ili wapate vyeo kwa kukudanganga kua unakubalika unapendwa wkt hali halisi mtaani wewe mwenyewe umeshaiona.
Nukuu ya kwenye katiba: "Rais hatawajibika kufuata ushauri wa mtu yeyote"