Swali kwa Kinana, lini Rais Samia alipigiwa Kura na wajumbe au amerithi kiti hicho cha urais?

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,615
3,909
NI wazi kwamba Samia Suluhu Hassan alirithi kiti cha urais baada ya Hayati Magufuli kufariki dunia huyu ndiye aliyepitishwa na wajumbe wa mkutano mkuu na vikao vya chama hadi akawa rais.

Kinana asipotishe umma kwamba desturi ya CCM NI kumwachia rais aliyepo sasa kuendelea na mhula mwingine bila kushindanishwa lini Samiah alipigiwa Kura ya vikao vya CCM na kupitishwa kuwa mgombea wa uraisi hajui kama mama amerithi kupitia kwa mwenzake?

Kinana ujuwe kuwa nchi hii ina watu wenye akili timamu kauli kama hizo ni kauli zinazoleta mtafaruku ndani ya nchi kwani ni vizuri demokrasia ikatawala na watu wachukue form wapate. raisi wanaoona anafaa kuwaongoza hivyo mama ashindanishwe kwani hata akishindanishwa akashinda basi atakuwa ametetea kiti chake na ndiyo maana ya demokrasia.

Hakuna mtu anayesema wala kubisha mama hafai isipokuwa ashindanishwe na wagombea wengine ndani ya CCM hiyo ndoo demokrasia tunayoijuwa.

Kauli hizo tunaomba makamu mwenyekiti wa chama ysiendelee kuzisema kwani zinaibua maswali mengi ndani ya chama na nchi kwa ujumla.

Mama mwenyewe tayari anawasili wake alishawatonya anahitaji kujipumzikia iweje Leo mumlazimishe.
 
Kiswahili sasa!
Wasomaji tunapata taabu sanaa au wewe ni Mkenya?
...kuridhi..... kurithi
...anawasili... ana wasiri
 
Kumbe Demokrasia ipo kwenye Chaguzi zetu zote ??!!
 
🤣🤣🤣nimemkumbuka Joyce Banda ghafla,hivi alihudumu kama raisi wa Malawi kwa muda gani vile?
Wadau naombeni majibu manake Nina amnesia,70 years siyo mchezo🤣
 
Je kuna aliekua raisi kwenye muhula wa kwanza akazuiwa kugombea uraisi sababu mwingine kachaguliwa kuwa mwenyekiti ?
 
CCM haijawahi kufiwa na Rais aliyepo madarakani Hadi useme ni Utaratibu wa CCM.

BUSARA na taratibu ziheshimiwe!!
Samia ni raisi aliyepo madarakani. Alivyoupata uraisi si muhimu. Kwa hivyo kama utaratibu wao CCM ni kwamba aliyepo madarakani amalize kipindi cha pili cha miaka 5 wako sahihi. Utaratibu huu haukuanza na Samia.

Hata hivyo ni utaratibu mbovu uliochochewa na ulafi wa madaraka.
 
Back
Top Bottom