Ramadhan Special Thread
Kumlipia Gharama Za Hijjah Mwanamke Aliyekuwa Na Mahusiano Naye Yasiyo Halali



Alhidaaya.com





Swali:



Kuna mwanamke ambaye aliwahi kuwa rafiki yangu wa kimapenzi zaidi ya miaka 20 iliyopita ambaye nimeonana nae hivi karibuni. Mwanamke huyu kwa sasa ameolewa na msalihina (saalihiina) na khamsa salawatu. Kwa sasa hatuna mahusiano yoyote zaidi ya yaliyopita na wala hatuna nia ya kuanzisha mengine kwani sote sasa ni watu wazima na tunafata maaelekezo ya dini na tumetubia kwa yaliyotokea hapo nyuma. Shida yake ni kwenda Hija atimize.



Nguzo hii muhim ya dini. Mimi kwa nia moja na bila ya tarajio lolote zaidi ya thawabu kutoka kwa Allah nimeweka nia ya kumlipia gharama za kwenda Hija. Jee nikimlipia hija yake itasihi? Jee mimi sitokuwa nimetenda dhambi nikifanya hivyo?



Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Tunamshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kuwapa uongofu ndugu zetu walioingia katika makosa Akawaajalia ni wenye kupenda kutenda mema badala yake kama ndugu yetu muulizaji. Na kutukabili kuuliza jambo lenye utata ni ishara kuwa mna khofu kubwa ya kuingia katika makosa mara nyingine. Hii ni Neema kwenu hivyo inapasa kumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kukuonyesheni njia ya kuzidi kupata uongofu ili msiwe mnafanya yale yasiyomridhisha.



Swala lako ni lenye utata kwa sababu kadhaa zifuatazo ambazo nyingine tunaziweka kwa mfumo wa maswali.



Kwanza: Msaada wenyewe una uhusiano wa historia yenu ya urafiki wa kimapenzi ambao sio urafiki wa halali kwani bila ya shaka utakuwa ulihusiana na maasi. Na kama tunavyojua kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Hapokei jambo ila lililo zuri kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

((إنَ الله تعالى طَيِّبٌ لا يَقْبَلُ إلا طَيِّباً)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ

((Allaah ni Mwema na Hakubali ila kilicho chema tu)) [Muslim]



Pili:



Japokuwa mmeshaacha urafiki huo na wote mmeshatubu, lakini kuwasiliana naye kwa njia yeyote ile bila ya kujua mumewe na kuwa naye faraagha ni makosa makubwa:



قال صلى الله عليه سلم : ((لا يخلوّنّ أحدكم بامرأة إلا مع ذى محرم )) متفق عليه

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hawi faraagha mmoja wenu pamoja na mwanamke ila awepo Mahram wake)) [Al-Bukhaariy Na Muslim]





Hivyo haitokuwa ni kutubu kikweli ipasavyo, kwani uhusiano baina yako na huyo mwanamke unaendelea japokuwa unahisi kuwa hakuna chochote lakini uhusiano huo unaweza kurudisha ushetani uliokuweko kabla. Tambueni kwamba hizo ni hila na njia za Shaytwaan kukuvutieni katika maasi:



Ametuonya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ وَمَن يَتَّبِعْ خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ فَإِنَّهُ يَأْمُرُ بِالْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ ۚ

Enyi walioamini! Msifuate nyayo za shaytwaan; na yeyote yule atakayefuata nyao za shaytwaan basi hakika yeye anaamrisha machafu na munkari. [An-Nuwr: 21]



Tatu:



Je, umemjulisha mumewe kwamba unataka kumfanyia jambo la kheri mkewe? Na je, mumewe anajua kuwa nyinyi mlikuwa marafiki wa kimapenzi kabla ya kumuoa yeye huyo mke? Tuna shaka kama anajua hivyo kwani hatudhani kama atakubali baada ya kujua historia yenu. Kwa hivyo, hapo hapo utakuwa umepata jibu kuwa mnayofanya ni ya siri kwa sababu si sahihi na si halali. Hilo tu latosha kukuonyesha kuwa hamjaelewa maana halisi ya tawbah.



Nne:



Kwanini asiende na mumewe? Atakwendaje Hijjah bila ya Mahram wake? Ikiwa mume wake haendi kwani kama angekuwa anakwenda basi angemlipia na mkewe, na ikiwa ni mke pekee anataka kwenda na hana uwezo basi fahamuni kuwa mume anastahiki kujua njia za kumwezesha mkewe kwenda huko, na pia rukhusa ya mume ni muhimu, na kwenda mwanamke peke yake bila Maharimu ni makosa, na kuwa na Maharimu ni uwezo wa kwenda Hijjah, na akikosa Maharimu wa kusafiri naye, basi mjue kuwa haikumpasa bado nguzo ya Hijjah kwake kwani kuwa na Maharimu (Mahram) ni sharti mojawapo ya kuwa uwezo wa njia ya kwenda kutekeleza fardhi hiyo kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ

Na kwa ajili ya Allaah imewajibika watu watekeleze Hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo. [Al-'Imraan: 96]



Na pia makatazo ya mwanamke kusafiri peke yake bila Mahram wake yameshawekwa wazi kwenye Sunnah kama anavyotujulisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



((لا يحل لامرأة مسلمة تسافر مسيرة اليوم وليلة إلا مع ذي حرمة منها))

((Haimpasi mwanamke Muislamu kusafiri msafara wa mchana na usiku ila awe na Mahram)) [Al-Bukhaariy na Muslim]



Naye huyo mwanamke, madamu hana uwezo wa njia basi asitake kushikilia sana kutekeleza ibada kwa kuasi amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Nabiy Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), bali nia yake inamtosheleza kulipwa na Rabb Mtukufu. Tunafahamu kuwa bila ya shaka atakuwa na hamu kubwa ya kutaka kutekeleza ibada hiyo labda awe na matumaini kuwa atafutiwa madhambi yake yote. Lakini itambulike kuwa mja hufutiwa madhambi yake yote ya maasi anapotubu na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) hata kama hakwenda Hajj.



Kwa hiyo mas-alah haya sio ya kwamba utapata dhambi kumlipia gharama za Hajj, bali ni mashaka ya kutokukubaliwa Hijjah yake kutokana na sababu hizo. Na kuacha yale yenye mashaka ni bora kuliko kufanya yenye mashaka kama ambayo wewe unataka kuyafanya.



Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anatuonya hayo:



عَنْ أَبي مُحمَّدٍ الحسَنِ بْنِ عليّ بْنِ أبي طَالِب، سِبْطِ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم وَرَيْحَانَتِهِ رضيَ اللهُ عنهُما، قالَ: حَفِظْتُ مِنْ رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم: ((دَعْ ما يَرِيبُكَ إلى مَا لاَ يَرِيُبكَ )) رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَالنَّسَائِيُّ وَقَالَ التِّرْمِذِيُّ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.

Kutoka kwa Abu Muhammad Al-Hasan bin ‘Aliy bin Abi Twaalib mjukuu wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kipenzi chake (Radhwiya Allaahu ‘anhuma) alisema: ((Nilihifadhi kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) maneno haya: ((Acha kile kinachokutia shaka ufuate kile kisichokutia shaka)) [At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy, At-Tirmidhiy akisema kuwa ni Hadiyth Hasan na Swahiyh]



Tunakunasihi ukate mawasiliano na mahusiano yote baina yako wewe na huyo mwanamke ambaye si Mahram yako na haipasi kisheria kuwasiliana na mke wa mtu. Lazima ujue kuwa Tawbah ya kweli ni kujuta kikamilifu kwa yale uliyoyatenda na kutolirejea tendo hilo kwa njia yoyote ile hata kama ni kwa fikra njema ya kutaka kumlipia gharama za Hajj.



Tunakushauri kuwa ikiwa wewe bado hukutekeleza nguzo hiyo, basi utumie gharama hizo kwenda kuifanya Hajj. Na ikiwa umeshafanya Hajj, basi nenda kamhijie mzazi wako ikiwa ameshafariki. Na kama bado wazazi wako wangali hai, basi msaidie ndugu yako ambaye hajakwenda. Au vilevile unaweza kuwasaidia mayatima kwa gharama hizo. Na mengi yako ya kufanya yatakayokuingizia thawabu au Sadaka yenye kuendelea kuliko kumlipia mke wa mtu kwenda Hajj.



Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Azidi kuwaonyesha uongofu, Awazdishie taqwa, Awaghufurie nyinyi na sisi na Waislam wote na Atuongoze sote kwenye njia ya sawa; njia iliyonyooka; njia ya Rusuli, Mashahidi, wema waliopita na wasema kweli. Aamiyn





Na Allaah Anajua zaidi
 
Kumpeleka Hajj Mzazi Kwa Pesa Za Hawara



Alhidaaya.com



Swali:



Mimi nina mwanaume ambaye anapesa sana sasa nilitaka kumwambia anipe pesa nimpeleke mama yangu hajj ila nikasita nikaona bora niulize kwanza je inafaa? mana siendi mimi nampeleka mama yangu jekwa sababu ni mama inafaa? mana sio muhusika wa yule bwana ntakaeenda ni mama yangu? naomba ufumbuzi wa swala hili ndugu zangu ili tuelimishane.





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Kabla ya kujibu Swali lenyewe khaswa, inapasa utambue kwamba kuwa na mahusiano na mwanamume asiye Mahram (maharimu) wako ni maasi na jambo ambalo halimpasi mwanamke Muislamu kufanya. Umeeleza katika swali lako kwa kauli: “mimi nna mwanamume anapesa sana….” Je dada yetu hutambui kama jambo hilo ni la aibu na ovu kabisa wewe kuwa na mahusiano na mwanamume asiyekuwa mume wako? Ingawa umefanya vizuri kutukabili kuuliza kabla ya kupokea hizo pesa, lakini hakika inasikitisha sana kuona dada zetu mko katika maasi kama hayo na hali ni wazi kabisa kuwa ni jambo la haraam. Je, unafahamu kuwa hizo pesa atakazokupa wewe kwa matumizi yoyote ya kwako itakuwa ni haraam? Chakula chako, mavazi yako na mengineyo yote yatakuwa ni haraam kwako kwani hilo ni chumo la haraam. Kisha unapopokea pesa kutoka kwa mwanaume uliye na mahusiano naye ya haraam, huoni kwamba unajiweka katika fungu la wanawake wanaojiuza miili yao? Umefikiria yote hayo? Umeyaridhia?



Inapasa tutambue kwamba maamrisho ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anaposema:



يَا أَيُّهَا النَّاسُ كُلُوا مِمَّا فِي الْأَرْضِ حَلَالًا طَيِّبًا وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿١٦٨﴾إِنَّمَا يَأْمُرُكُم بِالسُّوءِ وَالْفَحْشَاءِ وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿١٦٩﴾

Enyi watu! Kuleni katika vilivyomo ardhini vya halali, vizuri; na wala msifuate hatua za shaytwaan. Hakika yeye kwenu ni adui wa wazi. Hakika hakuna isipokuwa anakuamrisheni maovu na machafu (na ubakhili) na mseme dhidi ya Allaah msiyoyajua. [Al-Baqarah: 168-169]





Halaal Inamaanisha:



1) Nyama iliyochinjwa kihalali

2) Rizki anayopata mtu kutoka njia ya halaal





Twayyiban Inaamanisha:



Vyakula vilivyo vizuri vya siha, ladha, vilivyomea vizuri n.k.



Tunaona kwamba Aayah ya pili yake inayotaja kuhusu su-u (maovu) wal-fahshaa (machafu) ina maana kila aina ya uovu na uchafu uliokatazwa katika dini yetu. Na ndio maana Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akaunganisha Aayah hiyo baada ya maamrisho Ya kula vya halaal na twayyib, kwani mtu anapokula vya haraam ikiwa ni chakula au pesa kuzitumia kwa mahitajio yoyote, humfanya mtu asiweze kumuabudu Rabb wake ipasavyo kwa sababu Shaytwaan atakuwa anaandamana naye wakati wote na popote. Hivyo basi kwanza tahadhari na ukate kabisa mahusiano na huyo mwanamume haraka yasije kukupelekea katika moto wa jahannam.



Ikiwa huyo mwanamume anakupenda kikweli naye ana uwezo kwanini basi asikuoe ukawa mke wake wa halaal? Huoni basi kuwa anataka kukuchezea tu kwa kutumia neema aliyojaaliwa na Rabb wake katika maovu?



Vile vile mwenye kula chumo la haraam asitegemee kabisa kutakabaliwa du’aa zake na Rabb kwani hazikubaliki du’aa zake wala amali zake zozote azitendazo kutokana na chumo hilo la haraam kama tulivyopata mafunzo kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



عن أبي هُرَيْرَةَ رَضي اللهُ عنه قال: قاَل رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : ((إنَ الله تعالى طَيِّبٌ لا يَقْبَلُ إلا طَيِّباً، وإنَّ الله أَمَرَ المُؤمِنينَ بِمَا أَمَرَ بِهِ المُرْسَلينَ فقال تعالى: ((يا أَيُّها الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيَّباتِ واعمَلُوا صالحاً)) [المؤمنون: 51] وقال تعالى: ((يا أَيُّها الَّذِينَ آمَنُوا كلُوا مِنْ طَيِّباتِ ما رَزَقْناكُمْ)) [البقرة: 172] ثُمَّ ذَكَرَ الرَّجُلَ يُطِيلُ السَّفَرَ أشْعَثَ أَغْبَرَ يَمُدُّ يَدَيْهِ إلى السَّماءِ يا رَبُّ يا رَبُّ، ومَطْعَمُهُ حَرَامٌ، ومَشْربُهُ حَرَامٌ، وَمَلْبَسُهُ حَرَامٌ وغُذِّيَ بالحَرَامِ، فأَنَّى يُسْتَجَابُ لهُ!)). رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye alisema: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: ((Allaah ni Mwema na Hakubali ila kilicho chema tu, Allaah Ameamrisha Waislamu kufanya yale aliyowaamrisha Rusuli, na Yeye (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Kasema: ((Enyi Rusuli! Kuleni katika vizuri na tendeni mema)) [Al-Mu’minuwn: 51]. Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa): ((Enyi walioamini! Kuleni vizuri Tulivyokuruzukuni)) [Al-Baqarah: 172] Kisha akataja (kisa cha yule) mtu aliyesafiri safari ndefu, kachafuka na kajaa mavumbi na huku anayanyua mikono yake mbinguni akisema “Ee Rabb! Ee Rabb! Nipe kadhaa, nikinge na kadhaa wakati chakula chake cha haraam, na kinywaji chake ni cha haraam, na kivazi chake ni cha haraam, na anashibishwa na haraam, je, vipi atajibiwa ([du’aa zake?])) [Imesimuliwa na Al-Bukhaariy na Muslim]



Tunshukuru kuwa umetukabili kutuuliza kabla ya kuamua kufanya jambo hilo, na hii ni dalili kwamba ni mtu mwenye kutaka kutambua haki ili ufuate. Hivyo tunatumai kuwa utapokea nasaha zetu za dhati kuhusu kujiepusha na huyo mwanamume na utajirudi haraka na kuachana naye na kufanya Tawbah ya kweli. Maelezo kuhusu Tawbah utayapata hapa:



Tawbah



Tukirudi katika swali lako utakuwa tayari umeshapata jibu kutokana na dalili zote tulizozinukuu hapo juu kwamba haipasi kabisa kupokea pesa za haraam na kuzifanyia jambo lolote la kheri hata kama kuwafanyia wazazi, ndugu au yeyote mwengine.



Maelezo zaidi utapata katika Swali na Jibu kwenye kiungo kifuatacho:



Kumlipia Gharama Za Hajj Mwanamke Aliyekuwa Na Mahusiano Naye Yasiyo Halali





Na Allaah Anajua zaidi
 
Kutumia Dawa Za Kuzuia Hedhi Wakati Wa Hijjah



Alhidaaya.com





Swali:



Kuna uhalali gani kwa wanawake kuchelewesha au kusogeza mbele siku zao za hedhi kwa kutumia dawa wakati wa hija? Hii inafanyika ili kutimiza ibada nzima ya hija.





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



'Ulamaa wengi wametoa ruhusa mwanamke kutumia dawa za kuzuia hedhi ikiwa anakwenda kutimiza nguzo ya Fardhi ya Hajj, na hoja zao ni zifuatazo:



Inafaa kutumia dawa kuzuia hedhi ili mwanamke aweze kukamilisha nguzo yake ya tano ya Kiislamu ikiwa atakhofu kupatwa hedhi wakati yuko katika taratibu za Hajj, kwa sababu ya kutokana na umbali wa masafa wa kusafiri na gharama zake nyingi ambazo pengine atashindwa tena kurudia kuitimiza nguzo yake miaka mingine.



Hapa inafaa tutaje kuhusu wale wanaotaka kutumia dawa hizo kwa kuwawezesha kufunga mwezi mzima wa Ramadhaan.



Rai za Maulamaa kuhusu jambo hili zime ikhtilafiana, kuna wachache waliokubali na wengi wamepinga mwanamke kutumia dawa hizo katika mwezi wa Ramadhwaan.



Wale waliokubali wamesema kwamba shuruti za kutumia dawa hizo ni kwamba mwanamke apate ruhusa kwa Daktari kuwa akitumia dawa hizo hazitomfanyia madhara yoyote kwani sheria ya dini yetu haipendi madhara kwa mtu.

لا ضرر ولا ضرار

"Hakuna kuleta madhara wala kudhurian "



Wale waliopinga kabisa kwa kusema kwamba hii na amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) aliyowaandikia binaadamu, kwa hiyo sio sawa kubadilisha maumbile ya mwanamke kama alivyoambiwa Mama wa Waumini 'Aaishah (Radhwiya Allahu 'anhaa) ilipomjia hedhi wakati wa Hajj kama ilivyo katika Hadiyth hii:



Imetoka kwa Mama wa Waumini 'Aaishah na Jaabir bin 'Abdillaah kuwa katika tarehe nane ya mwezi wa Dhul Hijjah siku ijulikanayo kuwa ni ya 'Tarwiyah' walipokuwa wakielekea Minaa na Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakaleta talbiya ya Hijja, kisha Nabiy akaenda kwa Bi 'Aishah (Radhwiya Allahu 'anhaa) akamkuta analia, akamuuliza: ((una nini?)) akajibu (Mama wa Waumini 'Aaishah Radhwiya Allahu 'anhaa) ''Nimepatwa na hedhi na watu wamehirimia na wamefanya twawaaf nami sijafanya vyote hivyo! Na sasa watu wanaelekea kuhiji hivi sasa!!'' Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia:



فإن ذلك شيء كتبه الله على بنات آدم، فافعلي ما يفعل الحاج غير أن لا تطوفي بالبيت حتى تطهري

Hili ni jambo Aliloliandika Allaah kwa wanawake (mabint Adam), basi nenda kaoge halafu kahirimie kisha Hiji na fanya yale anayofanya Mwenye kuhiji isipokuwa kutufu na kuswali)). Mama wa Waumini 'Aaishah akafanya matendo yote ya Hajj isipokuwa kufanya Twawaaf na Swalaah.



Vile vile kwa Rahma ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ametusahilishia dini yetu kwa kuturuhusu kuweza kulipa siku za Ramadhwaan ambazo mtu akishindwa kufunga ikiwa yuko safarini au ni mgonjwa na hali kama hii ya hedhi ya wanawake kwamba walipe siku zao miezi mingine baada ya kumalizika Ramadhwaan. Kwa hiyo ni bora zaidi mwanamke kukubali amri ya Allaah Aliyowaandikia kupata hedhi kwani kila majaaliwa ya Allaah juu ya binaadamu bila shaka yana hikma na manufaa makubwa kwetu.



فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ يُرِيدُ اللَّـهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّـهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿١٨٥﴾

Na atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi (inapaswa kulipa) idadi sawa katika masiku mengineyo. Allaah Anakutakieni mepesi na wala Hakutakieni magumu; na ili mkamilishe idadi na ili mumkabbir Allaah kwa kuwa Amekuongozeni na ili mpate kushukuru. [Al-Baqarah: 185]



Na Allaah Anajua Zaidi
 
Screenshot_20250531_083618_Google.jpg


Mawaidha ya Kumcha Allah (Taqwa):

Kumcha Allah ni msingi wa maisha ya Muislamu. Ni hali ya kumuogopa na kumtii Allah kwa kufanya yaliyo mema na kuacha maovu. Allah (S.W.) anasema:

"Enyi mlioamini! Mcheni Allah kwa kumcha kweli, wala msife ila hali ya kuwa Waislamu." (Qur'an 3:102)

🕌 Umuhimu wa Taqwa:
1. Ni ngao dhidi ya madhambi – Huongoza moyo kujiepusha na haramu hata akiwa peke yako.
2. Huleta msaada wa Allah – "…Na anayemcha Allah, atamtengea njia ya kutokea…" (Qur’an 65:2)
3. Huleta heshima ya kweli mbele ya Allah – "…Mbora wenu mbele ya Allah ni yule mwenye taqwa zaidi…" (Qur’an 49:13)

🛡️ Njia za Kuijenga Taqwa:
  • Kuswali kwa unyenyekevu na kwa wakati
  • Kukumbuka Allah kila wakati (dhikr)
  • Kuacha dhambi hata ndogo
  • Kusoma Qur’an na kutafakari maana yake
  • Kukaa na watu wema na wenye kumcha Allah

💡 Mawaidha kwa Moyo:
Taqwa si mavazi au maneno, bali ni hali ya moyo inayojidhihirisha kwa matendo. Iwe unapoonekana au hupo, Allah anajua hali yako.

Dua: "Ya Allah, tujaalie moyo wa kukucha, maneno ya kweli, na matendo yanayokuridhisha. Ameen."
 
Au Kwa Mtu Mmoja Anayechinja Au Kugharamia Uchinjaji?



Alhidaaya.com





Swali:



Maelezo mliyotoa kuwa mwenye kutia nia ya kuchinja azuwiye kukata nywele na makucha. Swali langu, je ni watu wote katika nyumba wajizuie au ni mtu anayelipia tu kuchinja? Mfano baba ndiye mwenye kulipa, je mkewe naye azuie kukata nywele na makucha na watoto pia? Nitashukuru kupata jibu haraka hali tumeshaingia katika siku kumi na hatuna hakika nalo jambo hili.

Wa Billah tawfik.





Jibu:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Mwenye kupasa kuzuia kukata nywele na kucha ni mtu mmoja katika nyumba, aghlabu ni baba mwenye kulipia kuchinja, yaani mwenye kumiliki uchinjaji. Hii ni kutokana na kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

عن أم سلمة رضي الله عنها، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((إذا رأيتم هلال ذي الحجة وأراد أحدكـم أن يضحّي فليمسك عــن شعره وأظفاره) وفي راوية: ((فلا يأخذ من شعره ولا من أظفـاره حتى يضحّي)) مسلم

Imetoka kwa Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mkiuona (Utakapoandama) mwezi wa Dhul-Hijjah na ikiwa yuko anayetaka kuchinja basi azuie (asikate) nywele zake na kucha zake)

Na katika riwaya nyingine ((Asikate nywele wala kucha mpaka akimaliza kuchinja)) [Muslim na wengineo]



Amri hiyo inampasa kutekeleza mwenye kuchinja ikiwa atachinja mwenyewe au hata kama anawakilisha mtu kumchinjia. Ama wale ambao kwa ajili yao wanachinjiwa yaani watu aliowajibika nao kuwachinjia, wao haiwahusu amri hiyo kwani kauli imetaja ((ikiwa yuko anayetaka kuchinja)), hivyo haikutajwa kwa ujumla na kama ingeliwajibika watu wote katika nyumba basi kungebainishwa.



Vile vile Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akichinja kwa ajili ya familia yake na hakuna mapokezi yoyote yanayoonyesha kuwa aliwaamrisha ahli yake wazuie kukata nywele na kucha.



Kadhaalika, kuna maswali mengi yanaulizwa kuhusiana na kucha kukatika yenyewe au kucha kutokezea kumuumiza, anaweza kuiondosha kwani hiyo ni dharura na ni kuondosha dhara. Wanachuoni wanaona hakuna ubaya katika hilo, na hata zile nywele zenye kutoka wakati wa kuzichana au ndevu zinapochanwa zikatoka moja moja; yote hayo hakuna ubaya, isipokuwa mtu anatakiwa ajitahidi asitumie nguvu na alainishe nywele zake kwa maji au mafuta ili zisiwe ngumu wakati wa kuzichana, kuepusha kukatika.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Kwenda Hajj Na Wazazi Ikiwa Mume Hataki Inafaa?



Alhidaaya.com







Swali:



Assalam Allaykum;



Mimi Mwanamke Mwenye Mume Na Nina Ya Kwenda Hijja Lakini Kila Nikimshauri Mume Wangu Kuhusu Hilo Anaonekana Ni Mzito Na Uwezo Anao. Sasa Itakuwa Vibaya Kama Nitakwenda Mimi Na Wazazi Wangu?





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Hakuna ubaya kabisa kwenda kutekeleza nguzo yako ukifuatana na wazazi wako. Bila shaka utakuwa umekusudia baba na mama yako, hivyo baba yako anakutosheleza kuwa ni mahram wako na ni jambo jema kabisa.



Kilichokuwa muhimu ni upate ruhusa ya mume vilevile jitahidi kumpa makala za Hajj zilizokuwemo Alhidaaya apate kusoma atambue umuhimu wa kutekeleza ibada hiyo na atambue kuwa kudharau amri za Rabb wake na hali anao uwezo ni maasi makubwa ya kupelekea ukafiri, kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ ﴿٩٧﴾

Na kwa ajili ya Allaah ni wajibu kwa watu watekeleze Hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo. Na atakayekufuru, basi hakika Allaah ni Mkwasi kwa walimwengu. [Aal-‘Imraan 96-97]



Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allahu 'anhu), Mujaahid na wengineo wamesema kuhusu Aayah hiyo kwamba: "Yeyote mwenye kukanusha umuhimu wa Hajj anakuwa ni kafiri na Allaah yuko mbali naye kabisa (Hamuhitajii kwa chochote)" [Tafsiyr Ibn Kathiyr].



Muislamu asitegemee kupewa umri zaidi, hakuna ajuaye lini ataondoka duniani na kama alivyosema 'Umar ibn Khatwtwwaab (Radhwiya Allahu 'anhu) "Yeyote mwenye uwezo wa kutekeleza Hajj kisha asitekeleze, atakapofariki hatokuwa na tofauti baina yake na Yahudi au Naswara" [Hii ina isnaad sahihi inayofika kwa 'Umar – Al-Hilya 9:252 – imenukuliwa katika Tafsiyr ya Ibn Kathiry]



Kwa hiyo tunaona hatari ya kudharau kutekeleza nguzo hii kwa mwenye uwezo kuwa atakapofariki hatokuwa katika Dini ya Uislamu, bila shaka hakuna mmoja wetu atakayependa kuwa na hatima mbaya kama hiyo.



Utakapojaaliwa kufika huko umuombee sana mumeo Allaah ('Azza wa Jalla) Ampe imani ya kupenda kutekeleza tuliyoamrishwa katika Dini yetu.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Kuna Ushahidi Aliyerudi Hajj Asomewe Maulidi



Alhidaaya.com
Swali:



Namshukuru Allaah Subhana Wataala kunipa fersa hii ya kuuliza.Jamaa yangu amerudi Hijja hivi watu wa nyumbani wanataka kumsomea Maulidi jee inafaa? Kama haifai kuna Adhabu kwa kufanya Maulidi ua kumsomea dua huyo hujaj,na imetokea wapi?kuna uthibitisho gani katika Qur an na hadithi? Nitafurahi kwa kupata jibu lenu kwani bado tupo nyuma.




Jibu:


AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Hakika Maulidi ni dhahiri kabisa kwamba ni bid'ah (uzushi) uliozushwa miaka baina 400 na 600 baada ya kufariki Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kundi potofu la Mashia Ismailiya (Aga Khan) walipokuwa wakitawala Misr. Kisha yakasambaa na kuenea kufikia pande mbali mbali za dunia hadi kufika kwetu Afrika Mashariki.



Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Ametuonya mara nyingi kujiepusha na uzushi na alikuwa akitanguliza khutba zake kwa kutoa maonyo hayo:



((إن خير الكلام كلام الله وخير الهدي هدي محمد صلى الله علي وسلم وشر الأمور محدثاتها وكل محدثة بدعة وكل بدعة ضلالة وكل ضلالة في النار)) أخرجه مسلم في صحيحه

((Maneno bora ni kitabu cha Allah (Qur-aan) na uongofu bora kabisa ni uongofu wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na jambo la shari kabisa ni uzushi, na kila jambo jipya (katika dini) ni bid'ah (uzushi) na kila bid'ah ni motoni)) [Muslim katika Swahiyh yake]


Maudhui haya yameelezewa kwa upana ndani ya tovuti, ni vizuri kuyasoma ili Muislamu atambue ubaya wake na aweze kuusalimisha Uislamu wake kwani hakika uzushi ni ufisadi mkuu wa Dini yetu ya Kiislamu. Hivyo bila ya shaka mwenye kutaka kubakia katika usalama wa Dini yake ni lazima ajifunze kujua yepi ni ya uzushi na yepi ni ya Sunnah ili asalimike na abakie katika radhi za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).


Juu ya hivyo, mwenye kutenda uzushi hana ila kupoteza muda wake kwa kutenda amali ambazo hazina thamani mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na zaidi ni kutumbukia katika madhambi na kujitayarishia makazi mabaya. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَقَدِمْنَا إِلَىٰ مَا عَمِلُوا مِنْ عَمَلٍ فَجَعَلْنَاهُ هَبَاءً مَّنثُورًا ﴿٢٣﴾

Na Tutayaendea yale waliyoyatenda ya ‘amali yoyote ile, Tutayafanya chembechembe za vumbi zinazoelea hewani zinazotawanyika. [Al-Furqaan: 23]



Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:


(( من عمل عملاً ليس عليه أمرنا فهو رد)) البخاري

((Atakayetenda kitendo kisichokuwa chetu (katika dini yetu) basi kitarudishwa)) [Al-Bukhaariy]



Bonyeza viungo vifuatavyo upate makala muhimu kuhusu mas-ala haya ya Maulidi

Sababu 35 Muislam Asisherehekee Maulid
Mawlid – Mtazamo Wa Kisheria

Hoja Za Wanaosherehekea Maulid Na Majibu Yake



Muislamu anayerudi kutoka Hajj hahitaji kufanyiwa lolote, kwani ikiwa ametimiza Hijjah yake basi atakuwa amerudi akiwa amefutiwa dhambi zake zote kwa dalili:



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: "سَمِعْتُ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((مَنْ حَجَّ لِلَّهِ فَلَمْ يَرْفُثْ وَلَمْ يَفْسُقْ رَجَعَ كَيَوْمِ وَلَدَتْهُ أُمُّهُ)) متفق عليه

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kasema: “Nilimsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Atakayefanya Hajj, kisha asiseme maneno machafu wala asitende vitendo vichafu atarudi akiwa kama siku aliyozaliwa na mama yake)) [Al-Bukhaariy, Muslim]



Watu wake wanaweza kumuombea du'aa kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amthibitishie Iymaan yake, Azidi kumuongoza na Amtakabalie hijjah yake. Kumuombea huko kuwe ni kila mtu binafsi katika Swalaah zake au nyakati nyinginezo na sio kwa kukusanyika pamoja kumuombea kwani hilo pia ni jambo lisilofaa na kukubalika katika Dini yetu kwa vile hatukupata mafunzo hayo katika Sunnah. Na juu ya hivyo kukusanyika watu kwa ajili ya kuwaombea au kuwapongeza mahujaji ni jambo linalopeleka katika Riyaa (kujionyesha) na hivyo huenda wakapoteza amali zao na wakakosa thawabu zake.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Mume Anaweza Kumlipia Mke Kufanya Hijjah. Kuna Sharti Zozote Zinazopaswa Kutimizwa?



Alhidaaya.com





Swali:



AAWW!



Nauliza:



Mume kumtolea nauli ya matumizi mke kwenda Hijjah inasihi? Kama jibu ni ndiyo, kuna pre-requisites e.g. Jee kama yeye mwenyewe an uwezo? Si Hijjah inamjuzu mwenye uwezo tu.





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Kwanza tunapenda kukumbusha ndugu muulizaji kuacha kufupisha salaam unapoandika, unapoteza fadhila na ujira kwa kufanya hivyo.



Kama tunavyoelewa kuwa Hijjah ni nguzo ya tano kwa Waislamu nayo ni Faradhi kwa waume na wake. Hiyo ni kuwa taklifu zote za amali katika Uislamu ni faradhi kwa wote. Allaah Anasema:



مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً ۖ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩٧﴾

Mwenye kutenda mema miongoni mwa wanamume au wanawake naye ni Muumin, Tutamhuisha uhai mzuri, na bila shaka Tutawalipa ujira wao kwa mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wakitenda. [An-Nahl: 97].



Na Hijjah imefaradhishwa kwa wote pindi yanapopatikana masharti Fulani. Allaah Anasema:



فِيهِ آيَاتٌ بَيِّنَاتٌ مَّقَامُ إِبْرَاهِيمَ ۖ وَمَن دَخَلَهُ كَانَ آمِنًا ۗ وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ ﴿٩٧﴾

Ndani yake kuna Aayaat (ishara, dalili) zilizo wazi; mahali pa kisimamo cha Ibraahiym. Na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Allaah imewajibika watu watekeleze Hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo. Na atakayekufuru, basi hakika Allaah ni Mkwasi kwa walimwengu. [Al-'Imraan: 97].



Na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "…Na kwenda Hijjah ukiweza kufanya hivyo" [Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na an-Nasaaiy kutoka kwa ‘Umar bin al-Khatwaab (Radhwiya-Allaahu ‘anhu)].



Ibara hii ya Aayah na Hadiyth ina maana ya kuwa kila Muislamu ni lazima ahiji mara moja katika maisha yake akiweza kufanya hivyo. Uwezo una tafswili nyingi na yaliyo muhimu ni: -

Awe na afya nzuri ya kuweza kustahamili mazito ya safari.



Kuwe na usalama njiani – kwenda na kurudi



Awe na uwezo wa kutoa gharama za safari na kuacha masurufu yote ya wale wanaomtegemea.

Ikiwa sharti moja katika hayo limekosekana basi Hijjah haijamlazimu mtu huyo. Hivyo, jibu ni kwamba inafaa kwa mume kumpeleka mkewe Hijjah ikiwa atakuwa ana uwezo huo. Na inapendeza zaidi ikiwa watakwenda pamoja kwani hilo litaongeza mahaba baina yao. Na kwa ajili hiyo alipokuja mtu kwa Nabiy (Swalla-Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).) akamwambia kuwa mkewe anakwenda Hijjah naye amejiandikisha kwenda katika Jihadi, Nabiy (Swalla-Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia aende na mkewe kuhiji.



Na ni msingi wa Uislamu kuwa ((Yeyote mwenye kumuelekeza mtu mwengine katika kheri atapata thawabu sawa na mwenye kufanya hiyo amali)) [Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na Ibn Maajah kutoka kwa Ibn Mas‘uud na Abu Hurayrah (Radhwiya-Allaahu ‘anhumaa)]



Na hivyo hivyo ikiwa mke ni muweza kuliko mumewe anaweza kumsaidia mumewe kumpeleka Hijjah na pia atapata ujira mkubwa. Ikiwa mke ana uwezo anaweza kujipeleka mwenyewe baada ya kupata mahri wa kusafiri naye. Na wakati huo inakuwa ni lazima kwake kwa sababu masharti yote yametimia. Ikiwa hana uwezo haiwi ni lazima kwake lakini ikiwa atasaidiwa kutekeleza Faradhi hiyo basi hakuna tatizo lolote. Na hii ni ‘Ibadah ambayo ni tofauti na ‘Ibadah nyingine ambazo mtu hata akiwa mgonjwa anatakiwa afanye mwenyewe kama Swalaah, lakini Hijjah ikiwa mgonjwa huwezi kwenda mwenyewe unaweza kumpatia mtu hela zinazohitajika akaenda kukuhijia.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Mwanafunzi Anasoma Kwa Mkopo Wa Serikali; Je,

Anaweza Kwenda Hajj Na Hali Ana Deni Hilo?



Alhidaaya.com






Swali:



Assalaam aleykum,



Mimi ni mwanafunzi niliepewa mkopo na serikali. Mkataba wangu na serikali ni kurudi nikawatumikie na niwalipe pesa waliyonipa. Niko nje ya nyumbani; na huku Alhamdulillah kuna waislam hutokezea wakanigiya pesa au kuninunulia vitu ambavo nahitaji alhmadulillah. Likizo hii nimebahatika kupata kazi ya halali na nahisi nitabarruk kwa kuwaangalia wazee kidogo, nitoe sadaka na nijaribu kumsaidia mwanafunzi mmoja ambae ni yatima huko nyumbani. Suala langu ni: je natakiwa nisitoe pesa nilionayo mpaka nimalize deni? Na hata nikitaka kuhijji baadae hili deni litanizuia? Nasikia uchungu kua deni si dogo na mimi nataka kusaidia na nikipata nafasi nikahiji kwa pesa za halali nitazopata.



Natanguliza shukrani,





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Hakika ni kuwa pindi unapokopeshwa na taasisi au mtu binafsi huwa mnaandikiana au mnakubaliana jinsi ya kulipa deni hilo. Baada ya makubaliano hayo inabidi ufanye juhudi ya kuweza kutimiza ahadi hiyo kila mwaka au mwezi au kama mlivyoagana na kukubaliana.



Ikiwa baada ya kulipa hilo deni utaweza kuwa na akiba ambayo itakuwa ni halali yako unaweza kufanya lolote. Kwa akiba hiyo unaweza ukawa unaweka kila mwezi kwa ajili ya kwenda Hijjah, kuwasaidia wazazi au yatima au kufanya shughuli yoyote nyingine ya halali bila tatizo lolote.



Jambo ambalo lililokatazwa ni wewe kuchukua mkopo kwa ajili ya kwenda Hijjah.



Ama ikiwa yule anayekudai deni lake akakubali kuwa ulicheleweshe kwa sababu kama hizo na akaridhia wewe badala ya kumlipa deni lake, uende kufanya Hijjah kwanza, basi kwa makubaliano hayo hakuna neno kufanya hivyo.



Na kwa faida yako, mikopo mingi wanayopewa wanafunzi na serikali mbalimbali huwa ina ribaa, na kwa hali hiyo ni haraam mtu kujiingiza kwenye mikopo ya namna hiyo.





Na Allaah Anajua zaidi
 
UJUMBE WA LEO:

Uzuri wa Uislamu wa mtu ni kutoingilia au kufuata yasiyo mhusu
 
Mwanamke Anaweza Kwenda Hijjah Bila Ya Mume Ikiwa Mumewe Haswali Na Analewa



Alhidaaya.com





Swali:



Asalaam Alaykum Warahmaturullah Taala Wabarakatuh.



Mimi nina mme. mme huyo anakunywa pombe na haswali. Nimejaribu kumlingania kwa hilo bila mafanikio. Mimi Maa Shaa Allaah naswali. Swali langu ni je! naweza kwenda hajj nikijaaliwa? Allaah awajaarie kheri kwa kuunda chombo hiki na kutuelimisha. In Shaa Allaah amiin.





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Nabiy, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.) kama ilivyozoelekea na wengi, bali andika kwa kirefu maneno hayo bila ya kuyafupisha. Andika (Subhaanahu wa Ta’aalaa) baada ya kumtaja Allaah, na andika Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) au (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kumtaja Nabiy. Hivyo ndivyo inavyopaswa, na ndio heshima zaidi na utukufu na ndivyo inavyotamkwa na si kama inavyofupishwa na wengi kimazoea na kivivu.



Mwanamke hawezi kwenda Hajj pasi na maharimu wake. Maharimu wake ni yule ambaye kisheria hawezi kumuoa kama baba, ndugu yake wa kiume, ami yake, mjombake au mtoto wake wa kiume ambaye tayari amebaleghe.



Ikiwa hutapata maharimu wa kwenda naye basi Hajj haijakupasa wewe na In shaa Allaah Atakufanyia sahali na wepesi upate wa kwenda naye.



Soma katika viungo vifuatavyo upate ufafanuzi kwa upana:



Mwanamke Asiye Na Mahram Hawajibiki Kufanya Hajj



Hijja Yake Imekubaliwa Ikiwa Amekwenda Bila Mahram?



Mwanamke Kumfanyia Hijja Mtu bila Mahram Haifai



Kulingana na maelezo yako ni kuwa wewe uko katika matatizo makubwa ambayo yanafaa yapatiwe ufumbuzi. Shida uliyo nayo ni ile ya unyumba na ikiwa hutachukuwa tahadhari za Kidini basi huenda na Imani yako ikafifia. Hukutueleza kama mumeo alikuwa akifanya hayo kabla ya kukuoa au vipi. Kwa hali yoyote inatakiwa uchukue hatua za haraka na dharura ili upate ufumbuzi.



Umetuelezea kuwa umejaribu kiasi cha uwezo wako bila mafanikio yoyote. Kwa ajili unatakiwa ufanye yafuatayo:

Itisha kikao baina yako, mumeo, wawakilishi wa mumeo na wako kwa ajili ya kukaa pamoja ili kutafuta ufumbuzi. Ajenda iwe ni tabia za mumeo wala usifiche. Ikiwa hakutakuwa na muafaka wowote basi,
Nenda kwa Qaadhi au muhusika yeyote mkubwa wa dini kama Shaykh ambaye ni muadilifu kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo. Ikiwa atajirekebisha utaendelea kukaa naye kama mumeo, na lau hatajirekebisha basi Qaadhi huyo atoe uamuzi wa kukuachisha.
Muislamu hafai kukaa na mume ambaye haswali, kwani Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



"Baina ya mtu na ushirikina na ukafiri ni kuacha Swalah" [Muslim] na baya zaidi kwa mume huyo wako ni kazidisha madhambi zaidi kwa kunywa na pombe.



Tunakutakia kila la kheri na tawfiki katika mambo yako yote mawili.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Hijja Yake Imekubaliwa Ikiwa Amekwenda Bila Mahram?



Alhidaaya.com







Swali:



Assalaamu Alaykum,



Ndugu Zangu, Naomba Kukuliza Haba Ri Ya Mwanamke Kwenda Hajj Peke Yake. Mimi Nimeenda Mwaka Jana.



Sikufuatana Na Muhreem Kwani Nimefiliwa Na Mume Wangu.,Wala Ndugu Wala Mtoto.....Etc Yaani Nimetia Niya Tangu 1984 Pamoja Na Mume Wangu Lakini Sikuitika Labbaika Wana Vyosema Watu. Na Mtoto Wangu Wa Kiume Anaeishi Nje Tangu Kufa Mume Wangu 2000 Anani Himiza Kwenda Hija Na Mimi Siku Zote Namkatalia Kwa Kujua Kwamba Mwanamke Hawezi Kwenda Hija Pekeyake. Nimejaribu Kuwauliza Wasomi Wa Dini Yetu Na Nime Jibiwa Kuwa Mpaka Lini Hata Niwapate Hao Ninaeweza.



Kufuatana Nao Na Umri Ni Huu Unakwisha Uwezo Nnao Kwa Fedha Na Siha. And So Nime Tawwakkal Na Nime Fuzu. Sasa Suali Langu Ni Hivi Hija Yangu Imekubaliwa?





Jibu:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Shukran kwa swali lako hilo na ni maarufu kwa kila mmoja kuwa nguzo ya Hijjah ina masharti yake ambayo yanafaa yatimizwe kabla ya kukubaliwa amali hiyo. Masharti ni kama yafuatayo:



Muislamu.
Aliyebaleghe.
Mwenye akili timamu.
Aliye huru (si mtumwa).
Mwenye uwezo wa kwenda katika safari.
Afuatane na mahram ikiwa ni mwanamke (hili ni sharti).


Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhuma) amesema amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Asikae faragha mwanamme na mwanamke isipokuwa awe na mahram yake wala asisafiri mwanamke ila awe na mahram wake pia”. Akasimama mtu mmoja na kuuliza: “Ee Rasuli wa Allaah! Mke wangu ametoka kwenda kuhiji nami nimejiandika kwenda jihadi kadhaa”. Alasema: “Nenda ukahiji pamoja na mke wako” [Al-Bukhaariy na Muslim].



Baadhi ya Wanachuoni wameweka kuwa mwanamke kufuatana na mahram ni sharti na ndio kuweza kwake. Miongoni mwao ni Abu Haniyfah na wanafunzi wake, an-Nakha‘iy, al-Hasan, ath-Thawriy, Ahmad na Is-haaq.



Na mashuhuri kwa Imaam Shafi‘iy kuwa ameweka sharti ya kuwa mwanamke ni lazima aende Hijjah pamoja na mume au mahram au wanawake wengine waaminifu. Na kauli nyengine ni kuwa mwanamke mwaminifu anaweza kwenda peke yake. Na mwenye Subulus Salaam amesema kuwa kipote cha 'Imamu wamesema inafaa kwa mwanamke mkongwe kwenda safari hiyo bila ya mahram.



Na rai ya kamati ya wanachuoni iliyopo Saudia wamesema: Mwanamke ambaye hana mahram hana lazima kufanya Hajj kwa sababu kuwa na mahram ni mojawapo ya uwezo wa kwenda kutimiza nayo ni sharti ya ambayo Hajj huwa imewajibika kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

((وَلِلّهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلاً))

((Na kwa ajili ya Allah imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezaye njia ya kwendea.)) [Al-Imraan: 3:97]



Wenye kuruhusu mwanamke kwenda peke yake ni ile Hadiyth ya ‘Adiy ibn Haatim (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia kuwa ukiishi muda mrefu utamuona mwanamke kwenye hawdaj akisafiri kutoka Hirah mpaka kutufu Ka‘bah hamuogopi yeyote ila Allaah [Al-Bukhaariy].



Imaam Ibn Taymiyah amesema kuwa Hijjah ya mwanamke bila ya mahram inasihi. Hao wanaonelea kuwa inawezekana mwanamke kusafiri na kundi kufanya Hajj, na wengine wamesema kuwa ikiwa mwanamke ni mwenye umri mkubwa pia anaweza kwenda na kundi la wenzake.



Kwa kulinganisha hoja zote mbili na dalili zao, tunashauri ni bora kuwa na mahram ili uweze kwenda kufanya Hajj, na kama huna mahram, basi hupaswi kufanya Hajj na utalipwa kwa nia yako kama ya yule aliyefanya Hajj inshaAllaah.





Mwanamke Kumfanyia Hijja Mtu Bila Ya Mahram





Na Allaah Anajua zaidi
 
Mwanamke Kumfanyia Hijjah Mtu Mwengine Bila Yeye Kuwa Na Mahram Haifai



Alhidaaya.com





Swali:



Assalam Aleikum,



Nina suali moja ntafurahi sana mukinijibu haraha kabla sijachukua hatua zangu. Mimi ni Mwanamke ambae nimeshafanya hajj mara kadha sasa ninataka kwenda kumfania mtu Hajj na huyo mtu hajawahi kwenda na mimi sina mahrim wangu kufuatana nae jee hi hajj itafaa? Na nitaweza kwenda bila ya mahrim.



Shukran Jazakalahu Kheri.





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Mwanamke haimpasi kusafiri bila ya Mahram wake, na hata katika kutekeleza ibada ya Hijjah, baadhi ya Maulamaa wameweka sharti kuwa lazima mwanamke awe ana Mahram wake ndio aweze kwenda kutekeleza fardhi hii. Kwa hiyo ikiwa kuna sharti ya kuwa na mahram katika ibada ya fardhi anayojitendea binafsi mwanamke, seuze iwe ni ibada kwa ajili ya kumfanyia mtu mwingine. Hadiyth ifuatayo imeelezea kuhusu makatazo hayo:



قالَ صلى الله عليه وسلم : (( لا تُسافِرِ المرأةُ إلاَّ معَ ذي مَحْرَمٍ)) رواه البخاري ومسلم

Amesema Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mwanamke asisafiri ila awe na mahram wake)) [Al-Bukhaariy na Muslim]



Kutokana na Hadiyth hiyo ambayo inaonyesha kuwa ni haraam kwa mwanamke kusafiri bila ya mahram, Maulamaa wengi wametoa rai kuwa kuwa na mahram ni moja ya sharti ya kuifanya Hajj kuwa imewajibika kwa mwanamke. Na mwanamke mwenye nia ya kutekeleza Hajj lakini ameshindwa kwa sababu hiyo hupata thawabu kutokana na nia yake In shaa Allaah.



Vile vile:



Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhuma) amesema amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Asikae faragha mwanamme na mwanamke isipokuwa awe na mahram yake wala asisafiri mwanamke ila awe na mahram wake pia”. Akasimama mtu mmoja na kuuliza: “Ee Rasuli wa Allaah! Mke wangu ametoka kwenda kuhiji nami nimejiandikisha kwenda kwenye vita vya Jihaad kadhaa”. Akajibu: “Nenda ukahiji pamoja na mke wako” [Al-Bukhaariy na Muslim].



Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) Aliulizwa kama iliwajibika Hajj kwa mwanamke aliyekuwa tajiri ambaye hakuwa na mahram. Alijibu: "Hapana". [Al-Mughniy 3/97]



Kwa hiyo haifai kwenda kufanya kwa ajili ya mtu mwingine ila kama utakwenda na mahram wako. Ukitaka kupata thawabu sawa na hizo madam unao uwezo, basi ni vizuri kumlipia gharama hizo Muislamu mwanaume aliyekwishafanya Hajj kabla ili akamtimizie fardhi hiyo ya huyo unayetaka kumfanyia, na hilo ni jambo jema litakalokupatia thawabu vilevile In shaa Allaah.



Bonyeza hapa kusoma jibu la maudhui kama hiyo:



Hijja Yake Imekubaliwa Ikiwa Amekwenda Bila Ya Mahram?





Na Allaah Anajua zaidi
 
Mwanamke Mwenye Kupata Hedhi Akiwa Katika Hajj Afanye Nini?



Alhidaaya.com





Swali:



Assallam allaikum warahmatullah wabarakatuh,



Ndungu wahusika, sina shaka email hii itawafika katika hali nzuri na afya njema. Baada ya salam ningeomba . kuuliza swali juu ya ibada ya Hijja.





1. Je Mwanamke anapokuwa katika ibada ya hijja kwa bahati nzuri au mbaya mwanamke huyu akapata period yake wakati akitekeleza ibada hii



(a) Je anatakiwa aendelee na ibada hii au akatishe? kwani tunavyofahamu ndungu zetu hawa wanapokuwa kwenye hali hii hawaruhusiwi kusali bali wanaweza kufanya ibada nyenginezo kama kumtaka Allaah na ibada nyenginezo! please nifafanulize saidi...





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Mwanamke mwenye kwenda Makkah kwa nia ya kutimiza fardhi ya Hijja, akapata hedhi yake, anatakiwa aendelee na ibada zote nyingine wanazofanya mahujaji isipokuwa kutufu Ka’abah ambayo ni sawa na Swalaah. Kwa hiyo ataacha pia kuswali kama ilivyo kawaida ya wanawake wanaopata hedhi kuwa wamezuilika kuswali na kufunga.



Dalili ni kutoka Hadiyth ifuatayo:



عن عائشة -رضي الله عنها- أن رسول الله -صلى الله عليه وسلم- دخل عليها وهي تبكي، فقال ((أنفست؟))" (يعني: هل جاءتك الحيضة؟) فقالت: نعم، قال: ((إن هذا شيء كتبه الله على بنات آدم، فاقضي ما يقضي الحاج، غير ألا تطوفي بالبيت حتى تغتسل))" رواه البخاري ومسلم

Kutoka kwa bibi 'Aishah (Radhwiya Allahu 'anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia (katika hema lake) akamkuta analia akasema: ((Je umepata hedhi?)) akasema: "Ndio". Akasema: ((Hii ni amri Allah Aliyowaandikia wasichana wa Adam, fanya yote wanayofanya mahujaji isipokuwa kutufu Ka’abah hadi utoharike)) [Al-Bukhaariy na Muslim]



Ibada nyingine zote zinazofanyika katika msimu wa Hajj ni zifuatazo:



- Kufanya Sa'ay (Kutembea Asw-Swafaa na Al-Marwa) mara saba.

- Kwenda Minaa kulala huko kwa ajili ya kutimiza nguzo nyingine.

- Kusimama 'Arafah

- Kulala Muzdalifah

- Kufanya jamaraat (kupiga mawe nguzo)

- Kuchinja



Na katika nyakati hizo zote anaruhusiwa kufanya dhikr za aina yoyote kama kuomba du'aa, kusoma Qur-aan, kusoma vitabu vya Dini, kufanya dhikr za tasbiyh (Subhaana Allaah) tahliyl (Laa ilaah Illa Allaah) tahmiyd (AlhamduliLLaah, takbiyr (Allaahu Akbar) na aina yoyote nyingine zilizothibitika katika Sunnah.



Atakapomaliza hedhi yake akakoga josho (ghuslu) atakwenda kufanya Twawaaf alizoshindwa kuzifanya, ikiwa ni Twawaaf ya 'Umrah au Twawaaf ya Ifaadhwah.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Nguo Za Rangi Ya Kijani Zina Maana Gani?



Alhidaaya.com





Swali La Kwanza:



Rangi ya kijani in Islam ina maana gani?





Swali La Pili:



Imekuwa ni kawaida yetu biharusi kuvaa kanzu ya kijani katika akdi. je, hii ni katika mafunzo yetu? Je, walivaa hivo wanawake wa zama mtume?





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Rangi ya kijani imetajwa katika Qur-aan kuwa ni nguo ambazo watakazozivaa watu wa peponi:



عَالِيَهُمْ ثِيَابُ سُندُسٍ خُضْرٌ وَإِسْتَبْرَقٌ ۖ وَحُلُّوا أَسَاوِرَ مِن فِضَّةٍ وَسَقَاهُمْ رَبُّهُمْ شَرَابًا طَهُورًا﴿٢١﴾

Juu yao wana nguo za hariri nyororo za kijani na za hariri nyororo za makhmel na watapambwa vikuku vya fedha; na Rabb wao Atawanywesha kinywaji cha kitwaharifu. Al-Insaan: 21]



Na Anasema Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa:



إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجْرَ مَنْ أَحْسَنَ عَمَلًا ﴿٣٠﴾أُولَـٰئِكَ لَهُمْ جَنَّاتُ عَدْنٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ يُحَلَّوْنَ فِيهَا مِنْ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٍ وَيَلْبَسُونَ ثِيَابًا خُضْرًا مِّن سُندُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُّتَّكِئِينَ فِيهَا عَلَى الْأَرَائِكِ ۚ نِعْمَ الثَّوَابُ وَحَسُنَتْ مُرْتَفَقًا ﴿٣١﴾

Hakika wale walioamini na wakatenda mema, hakika Sisi Hatupotezi ujira wa anayetenda ‘amali nzuri kabisa. Hao watapata Jannaat za kudumu milele zipitazo chini yao mito, watapambwa humo vikuku vya dhahabu, na watavaa nguo za kijani za hariri laini na hariri nzito nyororo; wakiegemea humo kwenye makochi ya fakhari. Uzuri ulioje wa thawabu na mahali pazuri palioje pa kupumzikia. [ Al-Kahf: 30-31]





Bila ya shaka kuna uzuri wake hiyo rangi hata ipewe sifa ya nguo za watu wa Peponi. Lakini isiwe ndio itikadi ya watu kuvaa nguo hizo kama ni hasa kwa ajili ya Hajj au 'Umrah, kama wanavyofanya baadhi ya watu.



Ama kumvalisha biharusi kanzu ya kijani pia hakuna dalili katika mafunzo ya dini yetu. Biharusi anaweza kuvaa nguo ya rangi yoyote.



Hiyo ni itikadi tu ya watu wa zamani na jambo lililoanzishwa bila ya dalili na linaendelea kutendeka. Inatupasa sote tuache kushikilia mila na itikadi zisizokuwa katika sheria ya Dini yetu.



Kuweka itikadi hizo ni kama kuwafuata wengine wanaovaa nguo hasa kwa sherehe fulani, mfano; Mabaniani wanavaa nguo nyekundu, na hata baadhi ya ndugu zetu wengine wa Kiislamu kama Wahindi wameiga nao mila hiyo. Au Wakristo wanawavalisha mabiharusi nguo nyeupe. Jambo hili pia tunaliona katika sherehe zetu za ndoa.



Waislamu tunapaswa tukate kabisa mizizi hiyo yenye itikadi na kufanya hivyo tutakuwa tumetekeleza mambo yafuatayo muhimu:



1. Tutazuia itikadi, uzushi na mila zisizokuwa na dalili kuendelea kwa vizazi vyetu vinavyokuja, na hii itakuwa ni moja wa njia ya kuinusuru dini yetu na kuibakiza iwe safi bila ya mambo ya itikadi na uzushi.



2. Tutapata thawabu kufanya hivyo.



3. Tutajiondoshea taklifu kulazimika kutafuta nguo za rangi hizo kwa kuvaa nguo ya rangi yeyote.



4. Tutajiokoa na kufuata mila za makafiri na dini nyingine, jambo linalomchukiza Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala na sisi wenyewe tutakuwa na hisia ya fakhari katika nyoyo zetu kuwa hatufati mila za dini nyingine na pia tutaridhisha nafsi zetu kwa kufuata amri za Mola wetu na kuacha makatazo Yake.





Na Allaah Anajua zaidi
 
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!



16- Kuweka Nadhiri Kwa Asiyekuwa Allaah



Alhidaaya.com





Kuweka nadhiri ni mtu kuilazimisha nafsi yake kwa kitu ambacho hajalazimishwa na Shariy’ah. Amesema Al-Isfhaan (Rahimahu Allaah) katika Mufradaat Alfaadhw Al-Qur-aan (uk. 797): “Nadhiri ni unapojishurutisha kutenda jambo lisilokuwa wajibu kwa sababu ya kutaka jambo fulani likutokee. Anasema Allaah:



إِنِّي نَذَرْتُ لِلرَّحْمَـٰنِ صَوْمًا

Hakika mimi nimeweka nadhiri ya swawm kwa Ar-Rahmaan [Maryam: 26]



Baadhi ya ‘Ulamaa wameharamisha kwa dalili ya Hadiyth ifuatayo:



عن النبيَّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ ؛ أنه نهى عن النذر وقال: إنه لا يأتي بخير. وإنما يستخرج من البخيل

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza nadhiri akasema: ((Haileti khayr bali inatolewa kutoka kwa bakhili)) [Muslim (1639)]



Na katika riwaayah nyingine:



نَهَى النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ النَّذْرِ وَقَالَ: إِنَّهُ لَا يَرُدُّ شَيْئًا وَلَكِنَّهُ يُسْتَخْرَجُ بِهِ مِنْ الْبَخِيلِ

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza nadhiri akasema: ((Hakika hairudishi chochote, bali inatolewa kutoka kwa bakhili)) [Al-Bukhaariy (6693)]



Na Hadiyth ya Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba amesema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



من نذر أن يُطِيعَ اللهَ فلْيُطِعْهُ ، ومن نذرَ أن يعصِيَه فلا يَعْصِه

((Aliyeweka nadhiri kumtii Allaah amtii, na aliyeweka nadhiri kumuasi Allaah, basi asimuasi))[Al-Bukhaariy (6696)]





Kutokana na Hadiyth hii, inadhihirisha kukubaliwa kwake nadhiri pindi mtu akiazimia, kwa dalili pia za Qur-aan:

وَمَا أَنفَقْتُم مِّن نَّفَقَةٍ أَوْ نَذَرْتُم مِّن نَّذْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُهُ

Na chochote mtoacho au mkiwekacho nadhiri, basi Allaah Anakijua. [Al-Baqarah: 270]



Na pia kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا﴿٧﴾

Wanatimiza nadhiri na wanaiogopa siku ambayo shari yake ni yenye kuenea kwa upana. [Al-Insaan: 7]



Na pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



ثُمَّ لْيَقْضُوا تَفَثَهُمْ وَلْيُوفُوا نُذُورَهُمْ

Kisha wamalize ‘ibaadah zao; wajisafishe taka zao na watimize nadhiri zao, [Al-Hajj: 29]





Na kwa vile nadhiri ni aina ya ‘Ibaadah, haifai kuielekeza kwa asiyekuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) mfano kuifanya kwa ajili ya Nabiy, au Walii, au Shaykh, au kaburi na kadhaalika. Kufanya hivyo ni shirki kubwa inayomtoa mtu nje ya Uislamu.



Fataawa za ‘Ulaama kuhusu kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):





Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)



Swali:



Je, ikiwa mtu ameweka nadhiri mfano akasema: “Allaah Akinipa shifaa kwa magonjwa yangu, nitachinja kwa ajili ya Allaah katika kaburi la fulani ili kujikurubisha kwa Allaah. Je, inajuzu mfano wa ‘amali kama hii? Na je, kuna sehemu zilizoharamishwa kuchinja?



Jibu:



Ikiwa ameweka nadhiri kuchinja kwa ajili ya Allaah katika kaburi, basi nadhiri hii ni ya maasi, haijuzu kuitimiza. Na kuchinja katika kaburi ikiwa imekusudiwa kujikurubisha kwa mwenye kaburi, hiyo ni shirki kubwa inayomtoa mtu katika Dini hata kama ataja Jina la Allaah wakati anachinja.



Na ikiwa kujikurubisha kwa Allaah basi hayo ni maasi makubwa na wasiylah (njia ya kujikurubisha) za shirki kwa sababu haijuzu kuswali kaburini wala kuomba wala kuchinja kaburini hata kama tunakusudia Allaah kwani hivyo ni kujifananisha na washirikina na wasiyla za shirki.



Abuu Daawuwd amepokea kutoka kwa Thaabit bin Adhw-Dhwahaak (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba mtu mmoja aliweka nadhiri kuchinja ngamia katika Buwaanah. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akauliza: ((Je, kuliweko masanamu ya kijaahiliyyah (kabla Uislamu) yakiabudiwa?”

Wakasema: “Hapana” Akasema: ((Je, kuliweko sherehe za kijaahiliyyah zikifanywa hapo?)) Wakasema: “Hapana” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Timiza nadhiri yako, kwani hakuna kutimiza nadhiri katika kumuasi Allaah, wala katika ambayo hayamiliki bin Aadam)). [Abuu Daawuwd na ameisahihisha Al-Albaaniy]







Imaam bin Baaz (Rahimahu Allaah)



Swali:



Imenitokea mushkila nikaweka nadhiri kwa ajili ya mmojawapo wa ma-Imaam, kisha nikaja kutambua kuwa haifai kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah. Tambua kuwa sehemu aliyoko huyo Imaam iko mbali, je, inajuzu nilipize nadhiri hii kwa mafakiri au niifanyie kafara?



Jibu:



Nadhiri hiyo ni baatwil, kwa sababu ni ‘ibaadah kwa asiyekuwa Allaah. Inakupasa utubie kwa Allaah kwayo na urudi Kwake kwa kutubia na kuomba maghfirah na kujuta kwani nadhiri ni ‘ibaadah, Anasema Allaah Ta’aalaa:



وَمَا أَنفَقْتُم مِّن نَّفَقَةٍ أَوْ نَذَرْتُم مِّن نَّذْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُهُ

Na chochote mtoacho au mkiwekacho nadhiri, basi Allaah Anakijua. [Al-Baqarah: 270]



Yaani: Atakulipeni kwayo. Na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



من نذر أن يُطِيعَ اللهَ فلْيُطِعْهُ، ومن نذرَ أن يعصِيَه فلا يَعْصِه

((Aliyeweka nadhiri kumtii Allaah amtii, na aliyeweka nadhiri kumuasi Allaah, basi asimuasi))



Kwa hiyo nadhiri hiyo ni baatwil, na ni kumshirikisha Allaah (‘Azza wa Jalla) kama vile nadhiri kwa ajili ya ma-Imaam na waliokufa ni nadhiri baatwil na ni kumshirkisha Allaah, basi nadhiri haijuzu isipokuwa kwa ajili ya Allaah Pekee, kwa sababu ni ‘ibaadah kama vile Swalaah, na kuchinja na nadhiri, na kufunga Swiyaam na du’aa zote ni kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kama Anavyosema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):



إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ﴿٥﴾

Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada. [Al-Faatihah: 5]





Na Anasema (Subhaanahu):

وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ

Na Rabb wako Amehukumu kwamba: “Msiabudu isipokuwa Yeye Pekee [Al-Israa: 23]





Na Anasema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



فَادْعُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ﴿١٤﴾

Basi mwombeni Allaah wenye kumtakasia Dini japokuwa wanachukia makafiri. [Ghaafir: 14]







Na Anasema (‘Azza wa Jalla):

وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا﴿١٨﴾

Na kwamba Misikiti ni kwa ajili ya Allaah, basi msiombe yeyote pamoja na Allaah. [Al-Jinn: 18]





Basi ‘ibaadah ni haki ya Allaah, na nadhiri ni ‘ibaadah, na Swawmi ni ‘ibaadah, na Swalaah ni ‘ibaadah, na du’aa ni ‘ibaadah basi inawajibika kuisafisha kwa ajili ya Allaah Pekee. Kwa hiyo nadhiri hiyo ni baatwil, na haikupasi kufanya chochote, si kwa mafukara wala wengineo, bali inakupasa utubie tu na huna haja ya kuilipizia nadhiri hiyo kwa vile ni baatwil na ni shirki, ila tu utubie tawbah ya kikweli na kufanya matendo mema, Allaah Akuwafikie na Akuongoze katika yanayomridhisha na Akujalie ufanye tawbah ya kikweli.
 
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم



Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!



17 -Kutabarruk (Kutafuta Kupata Baraka)


Alhidaaya.com







Maana ya barakah ni wingi wa khayr na kuthibitika kwake.





Tabarruk ni aina mbili; iliyothibiti ki-shariy’ah kwa kutajwa kitu fulani kina baraka kama Anavyosema Allaah (Subahaanahu wa Ta’aalaa) kuhusu Qur-aan:



كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ مُبَارَكٌ لِّيَدَّبَّرُوا آيَاتِهِ وَلِيَتَذَكَّرَ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٢٩﴾

Kitabu Tumekiteremsha kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) chenye Baraka, ili wapate kuzingatia kwa makini Aayaat zake, na ili wapate kukumbuka wenye akili. [Swaad: 29]





Mfano wa kutaka baraka za Kitabu hiki (Qur-aan) ni kama vile alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ الله عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَنْ قَرَأَ حَرْفًا مِنْ كِتَابِ اللَّهِ فَلَهُ بِهِ حَسَنَةٌ وَالْحَسَنَةُ بِعَشْرِ أَمْثَالِهَا لَا أَقُولُ الم حَرْفٌ وَلَكِنْ أَلِفٌ حَرْفٌ وَلَامٌ حَرْفٌ وَمِيمٌ حَرْفٌ))

Imetoka kwa 'Abdullaahi bin Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, ((Atakayesoma herufi moja katika Kitabu cha Allaah atapata hasanah (jema) moja, na kila hasanah moja ni sawa na thawabu kumi, wala sisemi 'Alif-Laam-Miym' ni herufi moja, bali Alif ni herufi moja na Laam ni herufi moja na Miymni herufi moja)) [At-Tirmidhiy (2910) na ameisahihisha Shaykh Al-Albaaniy katika As-Silsilah Asw-Swahiyhah (3327), Swahiyh Al-Jaami’ (6469)]





Tabarruk inagawanyika sehemu mbili:





1-Iliyothibiti katika Shariy’ah ambayo inatokana na Muislamu kufanya juhudi katika ‘amali fulani ili achume thawabu nyingi na apate khayr nyingi kabisa. Mifano ni michache ni:



i) Kusoma Qur-aan na kufuata hukumu na maamrisho yake kama ilivyothibiti katika Qur-aan na Sunnah (Aayah na Hadiyth zilizotangulia kutajwa juu). Na pia Anasema Allaah (Subhanaahu wa Ta’aalaa):



إنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّـهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ تِجَارَةً لَّن تَبُورَ ﴿٢٩﴾

Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Allaah na wakasimamisha Swalaah, na wakatoa kutokana na yale Tuliyowaruzuku kwa siri na dhahiri wanataraji tijara isiyoteketea.





لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ ۚ إِنَّهُ غَفُورٌ شَكُورٌ ﴿٣٠﴾

Ili (Allaah) Awalipe ujira wao timilifu, na Awazidishie kutokana na fadhila Zake, hakika Yeye ni Mwingi wa kughufuria, Mwingi wa kupokea shukurani. [Faatwir: 29-30]







ii) Kuomba maghfirah kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) ambayo matokeo yake ni kujipatia khayr nyingi kama ilivyo tajwa kuhusu kauli ya Nabiy Nuwh (عليه السلام) alipowalingania watu wake:





اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ إِنَّهُ كَانَ غَفَّارًا﴿١٠﴾

Nikasema: “Ombeni maghfirah kwa Rabb wenu; hakika Yeye ni Mwingi mno wa kughufuria.



يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا﴿١١﴾

“Atakutumieni mvua tele ya kuendelea.”

وَيُمْدِدْكُم بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَيَجْعَل لَّكُمْ جَنَّاتٍ وَيَجْعَل لَّكُمْ أَنْهَارًا﴿١٢﴾

“Na Atakuongezeeni mali na wana, na Atakupeni mabustani na Atakupeni mito.” [Nuwh: 10-12]







Na mifano michache miongoni mwa mingineyo katika Sunnah:





i) Kuswali katika Masjid Al-Haraam, Makkah ambayo Swalaah humo thawabu zake ni maradufu.



عَنْ جَابِرٍ (رضي الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((صَلَاةٌ فِي مَسْجِدِي أَفْضَلُ مِنْ أَلْفِ صَلَاةٍ فِيمَا سِوَاهُ إِلَّا الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ، وَصَلَاةٌ فِي الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ أَفْضَلُ مِنْ مِائَةِ أَلْفِ صَلَاةٍ فِيمَا سِوَاهُ)) رواه أحمد وابن ماجه

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swalaah katika Msikiti wangu ni bora kuliko Swalaah elfu kwengineko isipokuwa Al-Masjid Al-Haraam. Na Swalaah katika Al-Masjid Al-Haraam ni bora kuliko Swalaah elfu mia (laki moja) kwengineko)) [Ahmad, Ibn Maajah na imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy; Swahiyh Ibn Maajah (1163), Swahiyh Al-Jaami’ (3838)]



Pia:



عن أبي هريرة رضي الله عنه ان رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((من قال : لا إلهَ إلَّا اللهُ وحدَه لا شريكَ له، له المُلْكُ وله الحمْدُ، وهو على كلِّ شيءٍ قديرٌ . في يومٍ مائةَ مرَّةٍ ، كانت له عِدلُ عشرِ رِقابٍ ، وكُتِبت له مائةُ حسنةٍ، ومُحِيَتْ عنه مائةُ سيِّئةٍ ، وكانت له حِرزًا من الشَّيطانِ يومَه ذلك حتَّى يُمسيَ ، ولم يأتِ أحدٌ بأفضلَ ممَّا جاء به إلَّا رجلٌ عمِل أكثرَ منه))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ’anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayesema: Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku walahul-Hamdu wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr [Hapana muabudiwa wa haki ila ni Allaah Peke Yake, hana mshirika, ni Wake Ufalme, na ni Zake Himdi na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza], mara mia kwa siku, basi atapata sawa na thawabu za kuwaacha huru watumwa kumi na ataandikiwa mema mia moja na atafutiwa makosa mia moja, na atakuwa na kinga ya shaytwaan kwa siku hiyo yote hadi jioni na hatakuwa mtu yeyote mbora kumshinda ila yule aliyefanya zaidi yake)) [Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h, (4/95) [3293], Muslim (4/2071) [2691].



Na pia:



عن عقبة بن عامر رضي الله عنه أن خرج رسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليهِ وسلَّمَ ونحنُ في الصُفَّةِ. فقال: ((أيكم يحبُّ أن يغدو كلَّ يومٍ إلى بطحانَ أو إلى العقيقِ فيأتي منهُ بناقتيْنِ كوماويْنِ، في غيرِ إثمٍ ولا قطعِ رحمٍ؟)) فقلنا: يا رسولَ اللهِ نحبُّ ذلك. قال: ((أفلا يغدو أحدكم إلى المسجدِ فيُعَلِّمَ أو يقرأَ آيتيْنِ من كتابِ اللهِ عزَّ وجلَّ خيرٌ لهُ من ناقتيْنِ. وثلاثٌ خيرٌ لهُ من ثلاثٍ وأربعٌ خيرٌ لهُ من أربعٍ. ومن أعدادهنَّ من الإبلِ))



Imetoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir (Radhwiya Allahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitujia wakati tulikuwa katika Swuffah akauliza, kuna yeyote miongoni mwenu anayependa kwenda soko la Butw-haan au Al-'Aqiyq na akapata humo ngamia wawili (wa thamani kabisa wa kike) bila ya kutenda dhambi au kukata undugu? Tukajibu: “Ee Rasuli wa Allaah! Tunapenda hivyo.” Akasema: ((Basi aende mmoja wenu Msikitini akajifunze au asome Aayah mbili katika Kitabu cha Allaah basi akifanya hivyo ni bora kuliko ngamia (wa thamani kabisa wa kike). Na Aayah tatu ni bora kuliko ngamia watatu, na Aayah nne ni bora kuliko ngamia wanne, na mfano wa hivyo hivyo wa Aayah kwa ngamia)) [Muslim]





2- Tabarruk iliyoharamishwa ambayo huwa shirki au bid’ah



Kuitakidi kwamba kiumbe fulani ana baraka na kumuomba kiumbe huyo khayr ambazo hana uwezo nazo isipokuwa Allaah, huwa ni shirki kwa sababu ni Allaah (Subhaanahu Ta’aalaa) Pekee Mwenye kutoka baraka kama alivyothibitisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



عن جابر بن عبد الله رضي الله عنه: رأيْتُني مع النبيِّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم وقدْ حَضَرَتِ العَصْرُ، وليس معَنا ماءٌ غيرَ فَضلَةٍ، فجُعِلَ في إناءٍ فأُتيَ النبيُّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم بهِ، فأدْخَلَ يدَهُ فيه وفَرَّجَ أصابِعَهُ، ثم قال: ((حيَّ علَى أهلِ الوضوءِ، البَرَكَةُ مِن اللَّهِ)) فلقدْ رأيتُ الماءَ يَتَفَجَّرُ مِن بينِ أصابعِهِ، فتَوَضَّأ الناسُ وشَرِبوا، فجَعَلْتُ لا آلُو ما جَعَلتُ في بطْني منه، فعَلِمتُ أنَّه بَرَكَةٌ . قلتُ لجابرٍ :كَم كُنتُم يومَئِذٍ ؟ قال: ألْفًا وأربَعمِائةٍ

Imepokewa kutoka kwa Jaabir bin Abdillaah akisema: “Nilikuwa na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na muda wa kuswali Swalaah ya Al-‘Aswr ukafika. Tulikuwa hatuna maji isipokuwa maji kidogo tu ambayo yalikuwa ndani ya chombo ambayo yaliletwa kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Basi aliweka mkono wake ndani ya maji hayo na kutandaza vidole vyake na huku akisema: ((Njooni Haraka watu wote ambao wanataka kutawadha Hii ni baraka kutoka kwa Allaah)). Nikaona maji yakibubujika kutoka katika vidole vyake. Hivyo watu walitawadha na wengine wakawa wanakunywa maji hayo na mie nilitaka kunywa maji mengi kupita kiasi (kwa sababu nilijua kuwa ilikuwa ni baraka). Mpokeaji wa Hadiyth hii kutoka kwa Jaabir alisema kuwa nilimuuliza Jaabir Je, mlikuwa watu wangapi wakati huo? Akajibu, “Tulikuwa watu elfu moja na mia nne.” [Swahiyh Al-Bukhaariy(7/543) Swahiyh Muslim (4/779)]





Aghlabu shirki na bid’ah zinazotendwa katika kutabarruk:





i-Kufanya ‘ibaadah kadhaa kama kuomba du’aa na kuswali kuelekea kaburi la Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kuitakidi kuwa du’aa na Swalaah hiyo ni ya kutakabaliwa au inamridhisha Allaah (Subhanaahu wa Ta’aalaa):



Amesema Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: “‘Ulamaa wengi wamewafikiana kwamba huu ni munkar uliozushwa na ni haraam, wala ma-Imaam wa Dini hawakutofautiana kwa hili.” [Ar-Radd ‘Alal-Bakriy, uk. 56]



Na akasema kuhusu du’aa mbele ya kaburi la Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Wala asisimame mtu kujiombea kwani hiyo ni bid’ah, wala hakutokea Swahaabah akisimama kaburini kujiombea bali walikuwa wakielekea Qiblah na wakiomba katika Masjid yake.” [Majmuw’ah Ar-Rasaail Al-Kubraa li Ibn Taymiyyah (2/408)], na Iqtidhwaa Swiraatw Al-Mustaqiym (2/681)]





ii- Kugusa kaburi na kuta za kaburi la Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) au Al-Ka’bah na kujipangusia mwilini, au kubusu kwa kutegemea kupata khayr na barakah.

Lililothibiti kubusiwa ni Al-Hajar Al-Aswad pekee lilioko katika Al-Ka’bah kwa dalili:

((إِنَّ مَسْحَ الْحَجَرِ الأَسْوَدِ ، والركنَ اليمانيِّ، يَحُطَّانِ الخطايا حطًّا))

((Kugusa Al-Hajar Al-As-wad na Ar-Rukn al-Yamaaniy ni kufutiwa madhambi)) [Hadiyth ya Ibn ‘Umar; Swahiyh Al-Jaami’ (2194)]



Na ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alipolibusu alisema:



"إني أَعْلَمُ أَنَّكَ حَجَرٌ لا تَضُرُّ ولا تَنْفَعُ، وَلَوْلا أَنِّي رأيت النبي صلى الله عليه وسلم يُقَبِّلُكَ ما قَبَّلْتُكَ" - البخاري و مسلم

“Hakika mimi najua kwamba wewe ni jiwe usiloweza kudhuru wala kunufaisha, na ingelikuwa sikumuona Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anakubusu basi nami nisingelikubsu.” [Al-Bukhaariy, Muslim]





iii-Kutabarruk sehemu sehemu ambazo zimetajwa katika Siyrah ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Imedhihirika watu wengi kukosea wanapofika Makkah au Madiynah kutekeleza ‘Umrah kupendelea kutembelea sehemu hizo wakiitakidi kuwa zina baraka na wengine hufika kujikalifisha kupanda majabali kama Jabal Ath-Thawr, Ghaar Hiraa, Jabali la ‘Arafah na sehemu nyinginezo.

Haikuthibiti kuwa Swahaabah (Radhwiya Allaahu ‘anhum) walitabarruk na chochote au popote alipopita au alipokaa kitako Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya kuwa wao walikuwa na mapenzi makubwa kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na wenye kutilia hima zaidi ya kutekeleza Sunnah.



Shaykh Al-Islaam amesema: “Kina Abu Bakr na ‘Umar na ‘Uthmaan na wengineo miongoni mwa Al-Muhaajiriyn na Answaar walikuwa wakisafiri kutoka Madiynah mpaka Makkah kutekeleza Hajj na ‘Umrah wala haikupokelewa kutoka kwao kuwa mmoja wao alikuwa akitafuta sehemu alizokuwa akiswali Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa salalm). Basi ni dhahiri kwamba ingekuwa ni jambo la kupendekezwa wangekuwa wao ni wa kwanza kutangulia kufanya, kwani wao ni wajuzi zaidi wa Sunnah zake na wenye kufuata mno kuliko wengineo.” [Iqtidhwaa Swiraatw Al-Mustaqiym (2/748)]



Katika moja ya msafara wake kwenda vitani Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na Swahaba zake walipitia sehemu wakataka kutafuta baraka kwa kuweka silaha zao katika mti, lakini aliwakataza. Na hii ni dalili pia haipasi kutabarruk kwa miti na vitu kama hivyo.



عن أَبِي وَاقٍد اللَّيْثِيِّ (رضي الله عنه) قَالَ: خَرَجْنَا مَعَ النَّبِيِّ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وآله وَسَلَّمَ) إِلَى حُنَيْنٍ وَنَحْنُ حُدَثَاءُ عَهْدٍ بِكُفْرٍ، وَلِلِمُشْرِكِينَ سِدْرَةٌ، يَعْكُفُونَ عِنْدَهَا وَيُنَوِّطُونَ بِهَا أَسْلِحَتَهُمْ، يُقَالَ لَهَا ذَاتُ أَنْوَاطٍ، فَمَرَرْنَا بِسِدْرَةٍ فَقُلْنَا: يَا رَسُولَ اللهِ اجْعَلْ لَنَا ذَاتَ أَنْوَاطٍ كَمَا لَهُمْ ذَاتُ أَنْوَاط. فَقَالَ النَّبِيُّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم):َ((الله أكبر! هَذَا كَمَا قَالَ قَوْمُ مُوسَى "اجْعَلْ لَنَا إِلَهًا كَمَا لَهُمْ آلِهَةٌ" وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَتَرْكَبُنَّ سُنَّةَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ))

Imepokewa kutoka kwa Abuu Waaqid Al-Laythiyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Tulitoka pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwenda (vitani) Hunayn nasi ndio kwanza tumetoka katika ukafiri, na washirikina walikuwa na mkunazi wanaufanyia ‘ibaadah na walikuwa wakitundika silaha zao (kupata baraka). Wakiuita ‘Dhaatu Anwaatw’. Tukapita mbele ya mkunazi tukasema: “Ee Rasuli wa Allaah, tufanyie nasi Dhaata Anwaatw kama walivyokuwa nao (makafiri) Dhaatu Anwaatw.” Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Allaahu Akbar! (Allaah ni Mkubwa!) Hivi ni kama walivyosema watu wa Muwsa “Tufanyie nasi muabudiwa kama walivyokuwa nao muabudiwa.” Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, mtafuata nyendo za walio kabla yenu [za ujahili na kufru].)) [At-Tirmidhiy; Swahiyh At-Tirmidhiy (2180)]



iv- Kutabarruk kwa Msahafu:



Shaykh Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amejibu Swali: “Kuweka Msahafu katika gari kwa ajili ya kujikinga na khatari au kujikinga na jicho ni bid’ah, kwani Swahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum) hawakuwa wakibeba Misahafu walipokuwa wakipanda ngamia wao kwa ajili ya kujikinga na khatari au jicho baya.” [Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb (2/4)]





v-Kutabarruk kwa watu kama mashekhe na wanaoitwa masharifu, kwa kuwagusa au kupangusa nguo zao au kuvaa nguzo zao au kunywa kinywaji walichoanza kunywa, au maji waliyoyatemea mate n.k. kwa kutegemea au kuitakidi vitu hivyo vina baraka.



Haikuthibiti kutoka kwa Swahaba kwamba walitabarruk kwa Swahaabah watukufu, kama Abu Bakr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) wala wengineo waliobashiriwa Jannah wala watu wa nyumba ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kwa hiyo kufanya hivyo si jambo lenye kukubalika katika Shariy’ah.
 
Back
Top Bottom