Ramadhan Special Thread
Taratibu Za Hajj Na 'Umra





Imaam Muhammad Bin Swaalih Al-‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)





Imetarjumiwa na www.alhidaaya.com







AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Hajj ni aina mojawapo ya ‘ibaadah bora kabisa na ni amali tukufu kabisa kwani ni mojawapo ya fardhi za Kiislamu ambazo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amemtuma Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kutuongoza. Dini ya mja wa Kiislamu haikamiliki bila ya Hajj. Ni ‘ibaadah inayokubaliwa pindi yafuatayo yatahakikishwa:





Mtu ataifanyia bidii ya dhati kuwa ni kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Pekee na kwa kutamani Aakhirah na haitowezekana kufanyika kwa ajili ya kumuonyesha mtu au kwa ajili ya maslahi ya dunia.

Inampasa mtu anapotenda ‘ibaadah yake afuate mfano wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa maneno na vitendo na hii haiwezekani kutimia ila kwa kujifunza na kupata elimu ya mafundisho ya Sunnah.





Aina Za Hajj



Kuna aina tatu za Hajj; Tamattu'u, Ifraad na Qiraan.



Tamattu’



Hajji anavaa Ihraam ya 'Umrah tu wakati wa miezi ya Hajj (anapokwenda Makkah mapema) ambayo inamaanisha kwamba anapofika Makkah atafanya twawwaaf na Sa'yi ya 'Umrah. Kisha atanyoa au kukata nywele. Siku ya Tarwiyyah ambayo ni siku ya nane Dhul-Hijjah, atavaa nguo zake za Ihraam kwa ajili ya Hajj tu na atatekeleza yote yanayompasa kufanya.



Ifraad:



Hajji atavaa Ihraam kwa ajili ya Hajj pekee. Atakapofika Makkah atafanya twawwaaf pamoja na Sa'yi ya Hajj. Hana haja kunyoa au kukata nywele zake kwani hatoki kwenye Ihraam yake. Bali atabakia katika Ihraam mpaka amalize kurusha vijiwe katika Jamrah Al-'Aqabah siku ya 'Iyd. Anaruhusiwa kuchelewesha Sa'yi yake ya Hajj mpaka amalize twawwaaf ya Hajj.



Qiraan:



Hajji anavaa Ihraam ya zote mbili; 'Umrah na Hajj au anavaa kwanza Ihraam ya 'Umrah, kisha anatia niyyah ya Hajj kabla ya twawwaaf ya Hajj. Wajibu wa anayefanya Ifraad ni sawa sawa na anayefanya Qiraan, isipokuwa tu mwenye kufanya Qiraan inampasa achinje na mwenye kufanya Ifraad haimpasi kuchinja.





Aina ya Hajj iliyo bora kabisa katika hizi ni ya Tamattu'u ambayo ndio Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisisitiza ummah wake waitekeleze.



Hata kama Mweny kuhiji akitia niyyah ya kufanya Qiraan au Ifraad, anaruhusiwa kubadilisha niyyah yake kuingia katika Hajj ya Tamattu'u. Na anaweza kufanya hivi hata kama baada ya kufanya twawwaaf na Sa’yi kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipofanya Twawwaaf na Sa’yi mwaka wa Hijjah ya Widaa' (Hajj ya kuaga) pamoja na Maswahaba zake, aliamrisha wote ambao hawakuleta mnyama kwa ajili ya kuchinja, wabadilishe niyyah zao za Hajj na kutia niyyah ya 'Umrah, wakate nywele zao, na wavue Ihraam mpaka Hajj. Akasema:

(("لولا أني سقت الهدي لفعلت مثل الذي أمرتكم به)) البخاري

"Ingelikuwa sikuleta mnyama ningelifanya hivyo nilivyokuamrisheni mfanye" [Al-Bukhaariy]







'Umrah



Akipenda Hajji kuwa katika Twahaara ya 'Umrah, akoge kama josho la janaba. Mwanamume atie manukato mazuri kabisa na apake mafuta mazuri kichwani. Hakuna ubaya harufu ikibakia baada ya Ihraam.



Kukoga ili kuingia katika Ihraam ni Sunnah kwa mwanamume na mwanamke pamoja na wanawake wenye hedhi na wale wenye Nifaas (damu ya uzazi).



Baada ya kukoga na kujitayarisha, Mahujjaaj wote isipokuwa wanawake wenye hedhi au nifaas wataswali Swalaah za fardhi inapowadia wakati wake kama kawaida. Na ikiwa sio wakati wa Swalaah ya fardhi basi ataswali Raka'h mbili ambazo ni vizuri mtu kuswali kila anapotia wudhuu.



Atakapomaliza kuswali atasema Talbiyah hii:



لَبَّيْكَ اللَّهُمَّ عُمْرَة لَبَّيْكَ اللَّهُمَّ لَبَّيْكَ، لَبَّيْكَ لاَ شَرِيكَ لَكَ لَبَّيْكَ، إِنَّ الْحَمْدَ، وَالنِّعْمَةَ، لَكَ وَالْمُلْكَ،لاَ شَرِيكَ لَكَ

Labbayka-Allaahumma ‘Umrah, Labbayka-Allaahumma Labbayk. Labbayka laa shariyka Laka Labbayk. Innal-Hamda Wan-Ni'imata Laka wal-Mulk laa shariyka Lak.



"Nimekuitikia (Ee Allaah) 'Umrah, Nimekuitika (Ee Allaah) nimekuitika, nimekuitika (ee Allaah) Huna mshirika, nimekuitika (ee Allaah), hakika Himdi na Neema na Ufalme ni Vyako Huna mshrika"



Mwanamume atasema kwa sauti na mwanamke atasema kiasi cha kumsikia wa pembezoni mwake. (Wanawake wenzake).



Anatakiwa mtu kusema Talbiyah kila mara khaswa anapofika na kubadilisha kituo. Mfano anapopanda na kushuka kipando wakati wa safari au wakati wa usiku unapoingia na asubuhi kunapopambazuka. Pia Amuombe Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) radhi Zake za kupata Jannah na aombe kujikinga na moto kwa Rahmah Za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).



Anatakiwa mtu aseme Talbiyah wakati wa 'Umrah tokea anapovaa Ihraam yake hadi anapoanza Twawwaaf. Wakati wa Hajj aseme Talbiyah kutokea mwanzo wakati anapovaa Ihraam yake mpaka anapoanza kupiga mawe Jamarah ya 'Aqabah siku ya 'Iyd.



Hajji anapoingia msikitini atangulize mguu wake wa kulia na kusema:



أَعُوذُ بِاللَّهِ الْعَظِيمِ، وَبِوَجْهِهِ الْكَرِيمِ، وَسُلْطَانِهِ الْقَدِيمِ، مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ,، (بِسْـمِ الله، وَالصَّلاةُ) (وَالسَّلامُ عَلى رَسولِ الله)، اللّهُـمَّ افْتَـحْ لي أَبْوابَ رَحْمَتـِك

A’uwdhu biLlaahil-‘Adhwiym, wabi Wajhihil-Kariym wa-Sultwaanihil-qadiym, minash-shaytwaanir-rajiym (BismiLLaah was-swalaatu) (was-salaamu ‘alaa Rasuwli-Llaah) Allaahummaftah-liy abwaaba Rahmatika



“Najikinga na Allaah Mtukufu, na kwa Wajihi Wake Mkarimu, na kwa utawala Wake wa kale, dhidi ya shaytwaan aliyeepushwa na Rahmah za Allaah (Kwa jina la Allaah na Swalaah na salaam zimfikie Rasuli wa Allaah) Ee Allaah nifungulie milango ya Rahmah Yako.”



Anakaribia Hajar Al-Aswad (jiwe jeusi) na kuligusa kwa mkono wake wa kulia na kulibusu. Ikiwa hii haiwezekani, basi aelekeze tu uso wake kuelekea kwenye Hajar Al-Aswad na kuashiria kwa mkono wake. (Usibusu mkono wako!) Haifai kusukuma na kusababisha madhara kwake na kwa watu.



Anapoligusa au kuliashiria Hajar Al-Aswad anatakiwa aseme hivi:





بسم الله والله أكبر، اللهم إيماناً بك، وتصديقاً بكتابك، ووفاء بعهدك، واتباعاً لسنة نبيك محمد صلى الله عليه وآله وسلم

BismiLLaahi wa-Allaahu Akbar, Allaahumma Iymaanam-Bika, Wa taswdiyqam-bikitaabika, wa wafaa-aan bi'ahdiak, wat-tibaa'al-lisunnati Nabiyyika Muhammad Swalla Allaahu 'Alayhi wasallam.



Kwa jina la Allaah, na Allaah ni Mkubwa, Ee Allaah kwa iymani Kwako, na kwa kuamini kitabu Chako, na kwa kutekeleza ahadi yako, na kufuata Sunnah ya Nabii Wako Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).



(Tanbihi: Pamoja na Imaam kutaja ziada ya du'aa baada ya 'BismiLLaahi Wa-Allaahu Akbar' (Kwa jina la Allaah, na Allaah ni Mkubwa), maelezo yaliyofuatia pamoja na kwamba yananasibishwa na Maswahaba 'Aliy bin Abi Twaalib, Ibn 'Abbaas na Ibn 'Umar, lakini Wanachuoni wengi wa Hadiyth miongoni mwao Ibn Hajr na Al-Albaaniy wameeleza kuwa hazijathibiti kutoka kwao.)



Hajji lazima atembee huku Ka'bah liko kushotoni mwake. Anapofika Rukn Al-Yamani aiguse lakini asibusu bali atakapokuwa baina yake na Hajar Al-Aswad aseme:





رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الاَخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ



((Rabbanaa Aatinaa fid-duniyaa Hasanatan wafil Aakiharati Hasanatan waqinaa 'adhaaban-naar)).



"Rabb wetu, Tupe duniani mema, na Aakhirah mema, na Utulinde na adhabu ya moto"



((اللهم إني أسألك العفو والعافية في الدنيا والآخرة))



Allaahumma Inniy As-alukal-'afuw wal-'aafiyata fid-duniyaa wal-Aakhirah



"Ee Allaah Nakuomba msamaha na al-‘aafiyah (afya, salama amani kutokana na kila shari na ovu) duniani na Aakhirah"



Kila mara akilipita Hajar Al-Aswad anatakiwa aseme "Allaahu Akbar"



Katika kufanya Twawwaaf zilizobakia anaweza kusema anachopenda katika Du'aa, kumtaja Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kusoma Qur-aan. Hii kwa sababu twawwaaf, Sa’yi na kurusha vijiwe Jamrah imekhusiwa kwa ajili ya kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).



Katika Twawwaaf hii anahitajika mwanamume afanye vitu viwili:





Aweke Al-Idhwtwiba'a kutoka mwanzo wa Twawwaaf mpaka mwisho. Al-Idhwtwiba'a ina maana kwamba ni kuweka sehemu ya katikati ya vazi (ridaa) chini ya kwapa lake la kulia na kipande cha ridaa akipitishe juu ya bega la mkono wa kushoto. Anapomaliza kufanya Twawwaaf anaweza kurudisha ridaa yake katika hali yake ya mwanzo kwa sababu wakati wa Idhwtwiba'a ni wakati wa Twawwaaf tu.





Kufanya Ar-Raml katika Twawwaaf tatu za mwanzo. Ar-Raml ina maana kwamba kuzunguka kwa mwendo wa haraka kwa hatua ndogo ndogo. Kisha anatakiwa atembee mwendo wa kawaida katika Twawwaaf zake nne za mwisho.





Atakapomaliza mizunguko saba ya Twawwaaf, atakaribia Maqaam Ibraahiym na atasoma:



وَاتَّخِذُواْ مِن مَّقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى

fanyeni mahali pa kusimama Ibraahiym kuwa ni pahala pa kuswalia. [Al-Baqarah: 125]





Ataswali Raka'ah mbili fupi, akiwa karibu kiasi iwezekanavyo na nyuma ya Maqaam Ibraahiym. Katika Raka'ah ya mwanzo atasoma Swratul-Kaafiruwn na Raka'ah ya pili atasoma Suwratul-Ikhlaas. Atakapomaliza Raka'ah mbili atarudi kuligusa Hajar Al-Aswad kama itawezekana. Atakwenda Al-Mas-'aa, atakapofika karibu na As-Swafaa atasoma:



إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ ۖ

158. Hakika Asw-Swafaa na Al-Marwah ni katika alama za Allaah. [Al-Baqarah: 158]





Atapanda (kilima cha) Swafaa mpaka aweze kuona Ka'abah. Aelekee Ka'abah na anyanyue mikono yake, amtukuze Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na aombe Du'aa apendayo. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliomba:



لا إِلهَ إلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ وهُوَ عَلى كُلِّ شَيءٍ قَديرٌ، لا إِلَهَ إلا اللهُ وَحْدَهُ أَنْجَزَ وَعْدَهُ، وَنَصَرَ عَبْدَهُ وَهَزَمَ الأَحْزَابَ وَحْدَهُ



Laa iIlaaha illa-Allaah Wahdahu laa shariyka Lah, Lahul-Mulku Walahul-Hamd wa Huwa 'alaa kulli shay-in Qadiyr. Laa ilaaha illa-Allaah Wahdahu, Anjaza Wa'dahu Wanaswara 'Abdahu Wahazamal-Ahzaaba Wahdahu.



“Hapana muabudiwa wa haki ila Allaah, hali ya kuwa Peke Yake, wala Hana mshirika, Ufalme ni Wake na Himdi ni Zake, Naye juu ya kila kitu ni Muweza. Hapana muabudiwa wa hakii ila Allaah hali ya kuwa Peke Yake, Ametekeleza ahadi Yake, na Amemnusuru mja Wake, na Amevishinda vikosi Peke Yake”





Atasema mara tatu akiomba Du'aa baina yake.





Atateremeka As-Swafaa na kuelekea Al-Marwah kwa mwendo wa kawaida mpaka anapofika katika alama ya kijani, hapo atatembea kwa mwendo wa kukimbia mpaka alama ya kijani nyingine. Ataendelea kuelekea Al-Marwah kwa mwendo wa kawaida. Atakapofikia atapanda (kilima) na kuelekea Qiblah, atanyanyua mikono na kurudia kusema kama alivyosema alipokuwa As-Swafaa. Atateremka Al-Marwah kuelekea As-Swafaa, akihakikisha anatembea sehemu zinazohusika na kukimbia katika sehemu zinazohusika.





Ataendelea kufanya hivyo hivyo mpaka amalize mizunguko saba. Kutoka As-Swafaa kwenda Al-Marwah ni mzunguko mmoja na kurudi ni mzunguko mwingine. Wakati wa Sa’yi anaweza kusoma anachotaka kama Du'aa, Qur-aan na kumtaja Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).





Anapomaliza Sa’yi atanyoa nywele. Mwanamke atakata nywele kiasi cha urefu wa ncha ya kidole. Inapendekezeka kunyoa nywele zote, na kunyoa ni bora kuliko kukata kwani Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaombea du’aa walionyoa mara tatu na waliokata mara moja. Isipokuwa ikiwa Hajj iko karibu na hakuna wakati wa kutosha kwa nywele kurudi kukua, basi ni bora kukata ili nywele zibakie kwa ajili ya kunyoa wakati wa Hajj, kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaamrisha Maswahaba kukata nywele katika 'Umrah kwani walifanya asubuhi ya tarehe nne ya Dhul-Hijjah.



Baada ya hapo 'Umrah itakuwa imemalizika na Hajji atakuwa huru kuvaa nguo nyingine, kutia manukato (mwanamume) na kurudia hali ya ndoa (kujimai na mkewe) na kadhalika.









***************









Hajj:





Siku Ya Tarwiyyah, Tarehe 8 Dhul-Hijjah





Siku ya tarehe 8 Dhul-Hijjah, Hajji atajitoharisha tena kwa kukoga kama alivyofanya kabla ya 'Umrah mahali hapo anapokaa. Atavaa Ihraam yake na kusema:



لَبَّيْكَ حَجّاً لَبَّيْكَ اللَّهُمَّ لَبَّيْكَ ، لا شَرِيكَ لَكَ لَبَّيْكَ ،إنَّ الْحَمْدَ ،وَالنِّعْمَةَ ،لَكَ وَالْمُلْكُ ، لا شَرِيكَ لَكَ

Labbayka Hajja Labbayka-Allaahumma Labbayk, Labbayka, laa shariyka Laka Labbayk, innal-Hamda wan-Ni'mata Laka wal-Mulk, laa shariyka Lak



"Nimekuitikia (Ee Allaah) Hajj, Nimekuitika (Ee Allaah) nimekuitika, nimekuitika (ee Allaah) Huna mshirika, nimekuitika (ee Allaah), hakika Himdi na Neema na Ufalme ni Vyako Huna mshirika "





Ikiwa atakhofu kuwa jambo litamzuia kukamilisha Hajj yake basi atie niyyah kwa kusema:

وإن حبسني حابس فمحلي حيث حبستني

"Ikiwa nitazuiliwa na kizuizi chochote sehemu yangu ni popote nilipozuiliwa"



Ikiwa hana khofu kama hiyo basi hana haja kujishurutisha hivyo.



Kisha Hajji atakwenda Mina na huko ataswali Swalaah ya Adhuhuri, Alasiri, Magharibi, 'Ishaa na Al-Fajiri na kufupisha Swalaah za Raka'h nne kuwa mbili mbili kila moja bila ya kuziunganisha. (Yaani kuswali kila moja vile kwa wakati wake ila ziwe fupi tu) kwani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali Qaswran (kufupisha) na sio Jam'an (kujumuisha).







Tarehe 9 Dhul-Hijjah – Siku ya ‘Arafah



Jua litakapochomoza siku ya pili ambayo ni tarehe 9 Dhul-Hijjah, atakwenda 'Arafah na huko ataswali Adhuhuri na Alasiri kwa kuunganisha wakati wa Adhuhuri na kufupisha mbili mbili. Atabakia katika msikiti wa Namirah mpaka jua litakapokuchwa. Atamdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) hapo 'Arafah na kuomba Du'aa nyingi sana awezavyo huku akielekea Qiblah na sio kuelekea Mlima wa 'Arafah.



Ikiwa atakuwa hakujaaliwa kuweko katika Msikiti wa Namirah karibu na Jabali la 'Arafah basi popote alipokuweko kwani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisimama katika jabali la 'Arafah na akasema:



((وقفت هاهنا وعرفة كلها موقف، وارفعوا عن بطن عرنة))

((Nimesimama hapa na 'Arafah yote ni kisimamo (cha 'Arafah) na msisimame katika bonde la 'Uranah))



Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiomba:



لا إِلَهَ إلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَريكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ ولَهُ الحَمْدُ وهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَديرٌ.



Laa ilaaha iIlla-Allaah Wahdahu laa shariyka Lah, Lahul-Mulku Walahul-Hamd wa Huwa 'alaa kulli shay-in Qadiyr



“Hapana muabudiwa wa haki ila Allaah hali ya kuwa Peke Yake, Hana mshirika, ni Wake Ufalme na ni Zake Himdi, Naye juu ya kila kitu ni Muweza”



Atakapochoka anaruhusiwa kuzungumza na wenzake au kusoma vitabu vyenye faida khaswa vile kuhusu ukarimu, utukufu wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na neema kubwa za Allaah kwetu ili apate kuzidi kupata matumaini kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Kisha arudi kuendelea kuomba Du'aa na kuhakikisha kuwa anatumia wakati wake wa mwisho wa siku hiyo katika Du'aa nyingi na nzito kwa sababu Du'aa zilizo bora kabisa ni Du'aa za siku ya 'Arafah.





Muzdalifah:



Jua litakapozama ataondoka 'Arafah kwenda Muzdalifah na huko ataswali Magharibi, 'Ishaa na Al-Fajiri Ikiwa atachoka au ana uchache wa maji, anaruhusiwa kuunganisha Magharibi na 'Ishaa. Ikiwa atakhofu kuwa hatofika Muzdalifah mpaka baada ya usiku wa manane, basi aswali kabla ya kufika huko kwani hairuhusiwi kuchelewesha Swalaah mpaka usiku wa manane.



Atabakia huko Muzdalifah akiomba Du'aa na kumtaja Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) mpaka Alfajiri, ataswali Alfajiri mapema kwa adhaan na Iqaamah, kisha ataelekea Mash'aril-Haraam (sehemu tukufu) na atafanya tahliyl, yaani atasema "Laa ilaaha illa Allaah" pia "Allaahu Akbar" na ataomba Du'aa mpaka kupambazuke vizuri. Ikiwa hakujaaliwa kwenda Mash'aril-Haraam, ataomba hapo hapo alipo kutokana na kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

((وقفت هاهنا وجمع كلها موقف))

((Nimesimama hapa na kote hapa ni kisimamo (cha Muzdalifah)) [Muslim]



Na atakuwa akiomba Du'aa kwa kuelekea Qiblah na huku akinyanyua mikono.







Minaa – Ar-Ramiy (Krusha vijiwe) Katika Jamrah







Ikiwa ni mtu dhaifu na hawezi kustahamili zahma za watu wakati wa Ar-Ramiy (kurusha vijiwe), (kama mwanamke na mtu mzima), basi anaruhusiwa kwenda Minaa mwisho wa usiku huo kupiga Jamrah kabla ya zahma ya watu kuwa kubwa.







Tarehe 10 Dhul-Hijjah:





Karibu na jua kuchomoza Hujaji ataondoka Muzdalifah kuelekea Minaa. Atakapofika atafanya yafuatayo:







Atarusha vijiwe saba moja moja katika Jamrah ya 'Aqabah ambayo iko karibu na mnara wa Makkah na kusema :

الله أَكْبَر

Allaahu Akbar



Kwa kila kijiwe anachokirusha.





Atachinja mnyama, na kula baadhi ya nyama na atatoa nyingine kuwapa masikini. Kuchinja ni fardhi kwa wale wanaofanya Hajj ya Tamattu'u na Qiraan. (Kwa hali ilivyo sasa huwa haiwezekani kufanya hivi, hivyo anaweza kutekeleza kama anavyoamrishwa yaani kulipa na kuacha jukumu hili kwa serikali ifanye kazi ya kuchinja)







Atanyoa au kukata nywele. Inapendekezwa kunyoa kuliko kukata (kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika maelezo ya 'Umrah hapo juu). Mwanamke atakata nywele zake urefu wa ncha ya kidole.





Mambo matatu hayo yafanywe kama ilivyo taratibu yake ikiwezekana, lakini hakuna kikwazo au sharti ikiwa mtu atatanguliza kitendo chochote kabla ya chengine.



Akimaliza hayo mambo matatu anaruhusiwa kujitoa katika Ihraam. Na anaweza kuvaa nguo zake za kawaida na kufanya kila jambo la halaal ila kuingia katika kitendo cha ndoa.



Atakwenda Makkah kufanya Twawwaaful-Ifaadhwah na Sa’yi kwa ajili ya Hajj. Ni Sunnah kujitia manukato kabla ya kwenda Makkah (kwa wanaume) kutokana na kauli ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba:



((كنت أطيب النبي صلى الله عليه وسلم لإحرامه قبل أن يحرم، ولحله قبل أن يطوف بالبيت )) البخاري و مسلم

((Nilikuwa nikimpaka manukato Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kabla ya kuingia katika Ihraam na na baada ya kutoka katika Ihraam kabla ya kutufu Ka'aba)) [Al-Bukhaariy na Muslim]



Atakapomaliza Twawwaaf na Sa’yi, Hujaji anaruhusiwa kufanya kila kitu kilicho halali hata tendo la ndoa.







Tarehe 11 na 12 Dhul-Hijjah:





Baada ya kufanya Twawwaaf na Sa’yi atarudi Minaa kulala huko usiku wa tarehe kumi na moja na wa kumi na mbili Dhul-Hijjah.



Atarusha vijiwe Jamrah tatu jioni zote za siku ya tarehe kumi na moja na kumi na mbili Dhul-Hijjah. Ataanza kwanza Jamrah ya kwanza ambayo iko mbali na Makkah, kisha ya katikati, kisha ya mwisho Jamrah Al-Aqabah.



Katika kila moja ya Jamrah atarusha vijiwe saba moja moja na huku atasema Takbiyr kwa kila kijiwe anachokirusha.



Atasimama baada ya kurusha vijiwe Jamrah ya kwanza na ya katikati kufanya Du'aa akielekea Qiblah akiwa amenyanyua mikono na kuomba Du'aa ndefu akiweza kufanya hivyo, au asimame kadiri atakavyoweza. Wala haimpasi kuacha kuomba Du'aa kwani ni Sunnah na watu wengi sana hawatekelezi hivi aidha kwa kutokujua au kupuuza. Na kila inapokuwa Sunnah haitekelezwi huwa kutangazika kwake kwa watu na kutendeka huenda ikaachwa kabisa na kupotea.



Hairuhusiwi kurusha vijiwe kabla ya Adhuhuri katika siku mbili hizi.



Ni bora kabisa kutembea kwenda kurusha vijiwe, ingawa kipando kinaruhusiwa.



Ikiwa mtu ana haraka baada ya kurusha vijiwe siku ya kumi na mbili Dhul-Hijjah, anaweza kuondoka Minaa lakini iwe kabla ya jua kuzama. Lakini akipenda kuzidisha makazi yake, ambayo ni bora zaidi, basi alale Minaa usiku wa kumi na tatu na arushe mawe jioni kama alivyofanya siku ya kumi na mbili.







Twawaaful-Widaa’ (Twaaf Ya Kuaga):



Atakapokuwa tayari kurudi kwao, atafanya twawwaaful-Widaa' ambayo ni mizunguko saba katika Ka'abah kutokana na kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



((لا ينفر أحد حتى يكون آخر عهده بالبيت ((مسلم

((Asikimbie mtu (asiondoke zake) mpaka iwe shughuli yake (kitendo chake cha mwisho) katika Nyumba (Ka'abah)) [Muslim]



Wanawake wenye hedhi na nifaas hawana lazima kufanya Twawwaaful-Widaa'i kama ilivyo katika Hadiyth ifuatayo:



((أمر الناس أن يكون آخر عهدهم بالبيت إلا أنه خفف عن الحائض)) البخاري و مسلم

((Aliamrisha watu iwe shughuli zao za mwisho ni Ka'abah isipokuwa waliruhusiwa (wanawake) wenye hedhi)). [Al-Bukhaariy na Muslim]



Ikiwa baada ya twawwaaful-Widaa'i umebakia wakati wa kusubiri wenzake au kipando chake au kununua kitu njiani hakuna neno juu yake, wala hana haja ya kurudia kufanya Twawwaaful-Widaa'i isipokuwa akitia niyyah ya kuchelewesha safari yake, mfano akitaka kuondoka mwanzo wa siku akatufu Ka'abah, kisha akachelewesha safari yake hadi mwisho wa siku, basi itamlazimu arudie kufanya Twawwaaf ili kiwe kitendo chake cha mwisho ni Ka'abah.







****************









Kutemebele Msikiti Wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):







Hajji atakwenda Madiynah kabla au baada ya Hajj kwa niyyah ya kutembelea msikiti wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kuswali humo na sio kwa niyyah ya kutembelea kaburi kutokana na Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



((لا تشد الرحال إلا إلى ثلاثة مساجد: المسجد الحرام، ومسجدي هذا، والمسجد الأقصى)) البخاري ومسلم



((Msifanye ziara ila kwa misikiti mitatu; Masjidul-Haraam [wa Makkah], na Msikiti wangu [wa Madiynah], na Masjidul-Aqswaa [wa Palestina])) [Al-Bukhaariy na Muslim]



Swalaah moja humo ni bora kuliko Swalaah elfu mahali pengine isipokuwa msikiti wa Makkah.





Anapofika msikitini atatanguliza mguu wa kulia na kusema:



أعوذ بالله العَظيـم وَبِوَجْهِـهِ الكَرِيـمِ وَسُلْطـانِهِ القَدِيـمِ مِنَ الشّيْـطانِ الرَّجِـيمِ،[ بِسْـمِ الله، وَالصَّلاةُ] [وَالسَّلامُ عَلى رَسولِ الله]، اللّهُـمَّ افْتَـحْ لي أَبْوابَ رَحْمَتـِكَ



A'uwdhu BiLLaahil-'Adhwiym, wa Biwajhihil-Kariym wa Sultwaanihil-Qadiym minash-shaytwaanir-rajiym, BismiLLaahi wasw-Swalaatu was-Salaam 'alaa Rasuli-LLaah, Allaahuumaf-tah-liy abwaaba Rahmatik.



“Najilinda na Allaah Aliye Mtukufu, na kwa Wajihi Wake, mtakatifu, na kwa utawala Wake wa kale, kutokana na shatywaan aliyeepushwa na Rahma za Allaah, (kwa Jina la Allaah na Swalaah) (Na salaam zimfikie Rasuli wa Allaah) Ee Allaah nifungulie milango ya Rahmah Zako"



Anatakiwa aswali Raka'ah mbili za Sunnah ya kuamkia msikiti au aswali Swalaah za fardhi ikiwa ameingia katika wakati wake.



Atakwenda katika kaburi la Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na atasimama mbele yake, atamsalimia kwa kusema:



السَّلاَمُ عَلَيْكَ أَيُّها النَّبِيُّ وَرَحْمَةُ اللَّهِ وَبَرَكَاتُه



Amani zishuke juu yako ee Nabiy na rahmah za Allaah na baraka Zake



اللّهُـمَّ صَلِّ عَلـى مُحمَّـدٍ وَعَلـى آلِ مُحَمَّد كَمـا صَلَّيْـتَ عَلـى آلِ إبْراهـيم وَعَلـى آلِ إبْراهـيم إِنَّكَ حَمـيدٌ مَجـيد



اللّهُـمَّ بارِكْ عَلـى مُحمَّـدٍ وَعَلـى آلِ مُحَمَّد كَمـا بارِكْتَ عَلـى إبْراهـيم وَعَلـى آلِ إبْراهـيم إِنَّكَ حَمـيدٌ مَجـيد



Allaahumma Swalliy 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym Innaka Hamiydun-Majiyd.



Allaahumma Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiyma wa 'alaa aal Ibraahiym Innaka Hamiydun-Majiyd.



“Ee Allaah Mswalie Muhammad, na aila ya Muhammad kama Ulivyomswalia Ibraahiym na aila ya Ibraahiym hakika Wewe Umesifika na Umetukuka"



"Ee Allaah Mbariki Muhammad, na aila ya Muhammad, kama ulivyombariki Ibraahiym na aila ya Ibraahiym, hakika Wewe Umesifika na Umetukuka.



أشْهَد أنَّكَ رَسُولُ الله حَقاً، وَأنَّكَ قَدْ بَلَّغْتَ الرِّسَالَةَ، وَأدَّيْتَ الأَمَانَةَ، وَنَصَحْتَ الأُمَّةَ، وَجَاهَدْتَ فِي اللهِ حَقَّ جِهَادِه، فَجَزاكَ اللهُ عَنْ أُمَّتك أَفْضَل ما جَزَى نَبِيَّا عَنْ أُمَّتِه.



Ash-hadu Annaka Rasuwlu-Allaah haqqan, wa Annaka qad ballaghtar-Risaalah, wa addaytal-amaanah, wa naswahtal-Ummah, wa jaahadta fil-Llaahi haqqa jihaadih, fa-Jazaaka-Allaahu 'an Ummatika afdhwal Maa jazaa Nabiyyan 'an Ummatih



"Nashuhudia kwamba wewe hakika ni Rasuli wa Allaah, Na kwamba umefikisha ujumbe, na umefikisha amana. Na umenasihi Ummah, na umefanya jihaad kwa njia ya Allaah ipasavyo hakika, basi Allaah Akulipe kwa Ummah wako bora kuliko Alivyomlipa Nabiy (yeyote) kwa Ummah wake"



Kisha atasogea hatua moja au mbili upande wa kulia kujiweka mbele ya Abu Bakar na kumsalimia kwa kusema :

السَّلاَمُ عَلَيْكَ

Assalaamu 'alayka



"Amani zishuke juu yako"



Na akipenda amuombee Du'aa munaasib kama kusema:



رَضِيَ اللَّهُ عَنْكَ وَجَزَاكَ اللَّهُ عَنْ أُمَّة مُحَمَّد أَفْضَل جَزَاء



Radhiya-Allaahu 'anka wa Jazaaka-Allaahu 'an Ummati Muhammad afdhwal jazaa



"Allaah Aridhike na wewe na Akulipe malipo bora kwa niaba ya Ummah wa Muhammad"



Kisha asogee hatua moja au mbili upande wa kulia kidogo na kuelekea kwa 'Umar na kumsalimia kwa kusema:



السَّلاَمُ عَلَيْكَ

Assalaamu 'alayka



"Amani zishuke juu yako"



رَضِيَ اللَّهُ عَنْكَ وَجَزَاكَ اللَّهُ عَنْ أُمَّةَ مُحَمَّد أَفْضَل جَزَاء



Radhiya-Allaahu 'anka wa Jazaaka-Allaahu 'an Ummati Muhammad afdhwal jazaa



"Allaah Aridhike na wewe na Akulipe malipo bora kwa niaba ya Ummah Wa Muhammad"



Haifai mtu kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kugusa ukuta wa chumba cha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) au kufanya twawwaaf (kuzunguka). Pia haelekei mtu huko bali anaelekea Qiblah wakati wa kuomba Du'aa. Kwa sababu kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) haiwi ila kama Alivyotuwekea shariy’ah Yeye pamoja na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na ‘ibaadah zinatakiwa zifuatwe sio zianzishwe.



Na mwanamke haimpasi kuzuru kaburi la Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala kaburi la yeyote mwingine kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amelaani wanawake wanaozuru makaburi. Lakini aswali na kumsalimia mahali hapo hapo alipo kwani zinamfikia salamu kama alivyosema:



)) صلوا علي فإن صلاتكم تبلغني حيث كنتم" وقال: "إن لله ملائكة سياحين في الأرض يبلغوني من أمتي السلام(( النسائي و أحمد



((Niswalieni kwani Swalaah zenu zinanifikia popote mlipo. Na akasema: ''Hakika Allaah Anao Malaika wanazunguka katika ardhi na kunitumia salamu kutoka kwa ummah wangu'')) [An-Nasaaiy na Ahmad]





Akiwa Katika hali ya Twahaarah atakwenda kuswali katika Msikiti wa Qubaa.





Atakwenda Al-Baaqiy'i kutembelea kaburi la 'Uthmaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu) atasimama mbele yake na kumsalimia kwa kusema:



السَّلاَمُ عَلَيْكَ

Assalaamu 'alayka



"Amani zishuke juu yako"



رَضِيَ اللَّهُ عَنْكَ وَجَزَاكَ اللَّهُ عَنْ أُمَّةَ مُحَمَّد أَفْضَل جَزَاء



Radhiya-Allaahu 'anka wa Jazaaka-Allaahu 'an Ummati Muhammad afdhwal jazaa



"Allaah Aridhike na wewe na Akulipe malipo bora kwa niaba ya Ummah Wa Muhammad"



Kisha atawasalimia Waislamu wengine waliofariki waliopo hapo makaburini Al-Baaqiy'i kwa kusema:



السَّلامُ عَلَـيْكُمْ أَهْلَ الدِّيارِ مِنَ المؤْمِنيـنَ وَالْمُسْلِمينَ، وَإِنّا إِنْ شاءَ اللهُ بِكُـمْ لاحقون، ( وَ يَرْحَمُ اللَّهُ الْمُسْتَقْدِمِينَ مِنَّا وَالْمُسْتَأْخِرِينَ) نَسْـاَلُ اللهَ لَنَـا وَلَكُـمُ العَـافِيَةَ.



Assalaamu 'alaykum ahlad-diyaari minal-Muuminiyna wal-Muslimiyn, wa In Shaa-Allaah bikum laahiquwn, wayarhamu Allaahu ahul-mustaqdimiyna minnaa walmusta-akhiriyn) nas-alu-Allaaha lanaa wa lakumul-'aafiyah



“Amani ishuke juu yenu watu wa nyumba za Waumini na Waislamu, nasi Apendapo Allaah tutakutana nanyi, [Na Allaah Awarehemu wa mwanzo na wa mwisho] namuomba Allaah Atupe sisi nanyi Al-‘Aafiyah (afya, salama, amani kutokana na kila ovu na shari)”





Atakwenda Uhud na kutembelea kaburi la Hamza (Radhwiya Allaahu 'anhu), pamoja na Mashuhadaa waliozikwa hapo. Atawatolea salaam na kuwaombea hivyo hivyo Du'aa ya kuzuru makaburi.





Tanbihi Muhimu:





Zifuatazo ni Tanbihi muhimu kwa mwenye kufanya Hajj au 'Umrah





1

Ajishurutishe katika fardhi za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) za dini zinazompasa kama kuswali kwa wakati wake na kuswali Jama'ah



2

Ajiepusha na yote yaliyoharamishwa kama uchafu, dhulma, utovu wa adabu kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَّعْلُومَاتٌ ۚ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ ۗ

Hajj ni miezi maalumu. Na atakayekusudia kuhiji (akahirimia), basi asifanye tendo la ndoa wala ufasiki wala mabishano katika Hajj. [Al-Baqarah: 197]



3

Ajiepushe na kuwadhuru Waislamu wenziwe kwa maneno au vitendo katika sehemu tukufu na kwengine kote.





4

Ajiepushe na yote aliyozuiliwa kufanya katika Ihraam kama yafuatayo:





Kwa Hajji wa kiume na wa kike



a) Asikate nywele. Hapana ubaya kukuna kichwa au kuchana nywele na ikiwa zitatoka kwa ajili hiyo hakuna ubaya.



b) Asikate kucha. Ikikatika kucha na ikiwa inamuudhi hakuna ubaya kuikata.



c) Asijitie manukato mwilini, au katika nguo zake baada ya kuingia katika Ihraam. Ama kabla ya Ihraam inafaa (kama ilivyoelezwa mwanzo). Vile vile katika chakula kama kutia zaafarani kwani zaafarani ni katika harufu nzuri. Vilevile ajiepushe na kuoga sabuni iliyo na manukato. Hakuna ubaya ikiwa manukato aliyotia kabla ya Ihraam yamebakia katika nguo zake.



d) Asimguse na kumbusu mke/mume wake kwa hamu na baya zaidi asifanye naye jimai (kitendo cha ndoa).



e) Asifunge Nikaah (Ndoa) au kupeleka posa kwa mwanamke kwa ajili yake au mwenzake.



f) Asivae glavu, lakini hakuna ubaya kufunika mikono yake kwa nguo yake.





Tanbihi kwa Hajjah mwanamume pekee:







a) Asivae nguo zilizoshonwa kama fulana, shati, suruwali, soksi, viatu na kadhalika ila tu ikiwa hakuweza kupata Izaar na makubadhi au malapa ndio anaweza kuvaa suruwali na viatu. Anaruhusiwa kuvaa saa, miwani visaidizi vya kusikia au kuzungumzia.



b) Haifai kujifunika kichwa kama kuvaa kofia, kilemba, ghutra na kadhalika. Ama kujifunika mwavuli kwa ajili ya kujihifadhi jua hakuna ubaya. Pia hakuna ubaya akibeba begi lakekichwani.







Tanbihi kwa mwanamke pekee:







a) Asivae niqaab na glavu. Kuna ‘Ulamaa waliosema kuwa haifai kujifunika uso wake kwa niqaab au chochote kingine ila kama kuna wanaume karibu yake, basi inambidi ajifunike uso wake (kuepusha fitna) na hatakiwi kulipa fidia akifanya hivyo.







Wa Swalaatu was-Salaam ‘alaa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na ahli zake na Maswahaba zake.









Faharasa







Al-Baaqiy'i

Sehemu Madiynah ambako kuna makaburi ya Maswahaba



Al-Idhwtiba'a

Kuweka sehemu ya katikati ya shuka (Ridaa) Chini ya kwapa ya mkono wa kulia na ncha zake juu ya bega la mkono wa kushoto katika twawwaaf



Al-Ikhlaas

Suwrah Namba 112 katika Qur-aan.



Al-Kaafiruwn

Surah Namba 109 katika Qur-aan.



Al-Marwah



Jina la kilima ambako Muislamu anaanza Sa’yi.

Ar-Raml

Kwenda mwendo wa mbio mbio kwa hatua ndogo ndogo katika mizunguko mitatu ya mwanzo kwenye twawwaaf



'Arafah

Sehemu muhimu kabisa ya kusimama katika Hajj iliyoko baada ya Muzdalifah



Ar-Ramiy

Kurusha vijiwe



As-Swafaa

Jina la kilima ambako Muislamu anamalizia Sa’yi yake ya mwisho



Dhul-Hijjah

Mwezi wa kumi na mbili katika kalenda ya Kiislamu

Hajar Al-Aswad

Jiwe Jeusi lililoko pembeni mwa Ka'abah



Hajji

Mwanaume mwenye kutekeleza fardhi ya Hijjah huko Makkah



Hajjah

Mwanamke mwenye kutekeleza fardhi ya Hijjah huko Makkah



Hamzah

'Ami yake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam aliyekufa Shahiyd katika vita vya Uhud.



Hedhi

Damu anayopata mwanamke kila mwezi



Ifraad

Aina ya Hajj ya iliyo pekee



Ihraam

Hali ya kuingia katika tendo la kufanya ‘ibaadah ya Hajj, au pia nguo za Hajj zinaitwa hivyo.



Jamrah



Mnara katika Minaa

Jamrah Al-Aqabah

Mnara ulio karibu na Makkah



Ka'abah



Nyumba tukufu iliyoko katika msikiti mtukufu wa Makkah.

Maqaamu Ibrahiym

Jiwe alilokanyaga Nabiy Ibraahiym na kusimama kuomba Du'aa baada ya kujenga Ka'abah



Mas-'aa

Sehemu iliyonyooka baina ya Swafaa na Marwah



Minaa

Bonde karibu na Makkah na mahali patukufu wanapokwenda kulala wanaofanya Hijjah kutekeleza baadhi ya vitendo vya fardhi (za) Hijjah.



Muzadalifah

Sehemu tukufu wanapolala waislamu katika ’ibaadah ya Hajj, ipo baina ya 'Arafah na Minaa



Namirah

Msikiti uliopo 'Arafah.



Nifaas



Damu ya uzazi

Niqaab

Kifuniko cha uso wanachovaa wanawake waislamu



Qiraan



Aina ya Hajj ya kusindikizwa.



Qubaa

Msikiti wa mwanzo waliojenga waislamu pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walipoingia Madiynah kutoka Makkah pamoja na



Ridaa

Sehemu ya nguo (shuka) ya juu wanayovaa wanaume katika Ihraam





Rukn Al Yamaani

Pembe katika Ka'abah inayoelekea Yemen.



Sa’yi



Kutembea baina ya Swafaa na Marwah

Sunnah

Mwenendo wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika kauli na matendo, au pia Hadiyth za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).





Takbiyr



Kusema Allaahu Akbar (Allaah Mkubwa)

Talbiyah

Du'aa ya Muislamu anayosema anapoingia katika Ihraam baada ya kutia Nia.



Tamattu'

Aina ya Hajj ya kustarehe (mapumziko)



Tarwiyyah

Tarehe nane ya Dhul-Hijjah



Twawwaaf

Mzunguko katika Ka'abah



Twaaful-Ifaadhwah

Twawwaaf ya Hajj ambayo ni moja ya fardhi katika taratibu za Hijjah.



Twawwaaful-Widaa'

Twawwaaf ya kuaga



Uhud

Mlima ulioko Madiynah umeitwa hivyo kutokana na vita vilivyotokea hapo.



'Umrah

Hijjah ndogo inayofanywa kwa twawwaaf na Sa’yi pekee.
 
Wanawake Wanaweza Kungia Katika Ihraam Wakiwa Katika Hedhi?



Alhidaaya.com






Swali:



Assalam alaikum warahmatullahi wabarakatu,

I had a question. What if someone wants to slaughter but is on their period? Is she allowed to get into ihram?

wasalaaam alaikum warahmatullahi wabarakatu..





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Mwanamke mwenye hedhi anaweza kutia niyyah ya Ihraam kwa sababu Ihraam haimzuii mwanamke mwenye hedhi, ila tu hatoweza kufanya ‘ibaadah ambazo zinajulikana kuwa hazifai kutekelezwa na mwanamke akiwa katika hali hiyo kama Swalaah, kufunga, kutufu Ka’bah n.k kwa dalili zifuatazo:



عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا فِي حَدِيثِ أَسْمَاءَ بِنْتِ عُمَيْسٍ حِينَ نُفِسَتْ بِذِي الْحُلَيْفَةِ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَمَرَ أَبَا بَكْرٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ فَأَمَرَهَا أَنْ تَغْتَسِلَ وَتُهِلَّ - مسلم

Kutoka kwa Jaabir bin 'Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Asmaa bint 'Umays alizaa katika Dhul-Hulayfah, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamuamrisha Abu Bakar (Radhwiya Allaahu 'anhu) amwambie afanye ghuslu na aingie katika Ihraam)) [Muslim]



Pia:



عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَتْ خَرَجْنَا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي حَجَّةِ الْوَدَاعِ . . فَقَدِمْتُ مَكَّةَ وَأَنَا حَائِضٌ وَلَمْ أَطُفْ بِالْبَيْتِ وَلا بَيْنَ الصَّفَا وَالْمَرْوَةِ ، فَشَكَوْتُ ذَلِكَ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ : ((انْقُضِي رَأْسَكِ وَامْتَشِطِي وَأَهِلِّي بِالْحَجِّ )). . . الحديث . ورواه البخاري و مسلم

Kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) mke wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye amesema: Tulikwenda na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hijjatul-Widaa'(Hijjah ya kuaga). Nikaenda Makkah nikiwa katika hedhi na sikuzunguka Nyumba (Ka'bah) au kufanya Sa'y baina ya Asw-Swafaa na Al-Marwah. Nikalalamika kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia: ((Fungua msuko wa nywele zako na uchane nywele (yaani fanya ghuslu) na ingia katika Ihraam ya Hajj…." [Al-Bukhaariy na Muslim]



Vile vile:



عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ((الْحَائِضُ وَالنُّفَسَاءُ إِذَا أَتَتَا عَلَى الْوَقْتِ (أَيْ : الْمِيقَات) تَغْتَسِلانِ وَتُحْرِمَانِ وَتَقْضِيَانِ الْمَنَاسِكَ كُلَّهَا غَيْرَ الطَّوَافِ بِالْبَيْتِ)) رَوَاهُ أَبُو دَاوُد وصححه الألباني في سنن أبي داود

Na kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhuma) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Wanawake wenye hedhi na wanawake walio katika damu ya uzazi wakifika Miyqaat [sehemu ya kutilia Ihraam] wafanye ghuslu na waingie katika Ihraam na wafanye taratibu zote isipokuwa twawaaf ya Ka'bah)) [Abuu Daawuwd na imepewa daraja ya Swahiyh na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh Abiy Daawuwd (1774)]



Kwa hiyo hakuna shaka kuwa wanawake wanaweza kuingia katika Ihraam katika hali yoyote.





Na Allaah Anajua zaidi
 
UMUHIMU WA KUFANYA MATENDO MAZURI YA KIIBADA

Ndugu zangu katika imani,hatukuumbwa kwa lengo la kula,kulala,kucheza,kustarehe na mambo kama hayo,bali tumeumbwa hasa kwa lengo moja kuu la kumwabudu Allah

Allah anasema Sikuumba majini na watu isipokuwa ili waniabudu.

Roho bila mwili ni sawa na hakuna kitu,na mtu kusema kwamba yeye ana moyo mzuri wa wema bila kufanya aamali (vitendo) vyema napo hapo kunakuwa hakuna thamani yoyote ile

Ndugu zangu katika imani,tutambue kwamba vitendo vya kiibada ni kwa ajili yako wewe binafsi,yani vitakufaa wewe mwenyewe. Allah amejitosheleza na yeye si mhitaji,bali sisi ndio wahitaji

Kwahiyo isipite katika nafsi yako kwamba kutoswali kwako wewe eti Allah anapata hasara,kutofunga kwako,kutosoma kwako qur'an na kumdhukuru Allah pamoja na matendo mengine ya kiibada,hayo ni kwa faida yako mwenyewe

Unayahitaji yote hayo ili siku ya hukumu uwe na hoja kwa Mola wako kwamba ulifanya juhudi kwa ajili ya kutaka radhi za Allah azza wa jalla

Kumbuka hakuna atakaye ingia peponi kwa matendo yake mema,yani hakuna kiumbe ambacho kimefaulu kwa asilimia mia moja katika kutekeleza ibada za Allah,isipokuwa ni kwa rehema ya Allah,kwasababu mkamilifu pekee ni Allah

Atachofanya Allah ni kuangalia matendo yetu je tulifanya kwa ikhlaas? Kwa maana tuyalifanya kwa ajili yake tu!

Na kwa kiasi gani tulitekeleza maagizo yake na kuacha makatazo yake

Hapo ndio kwa huruma yake wale waliojitahidi kwa vipimo vyake atawaingiza katika rehema yake

Basi nasi tushikamane kwa nguvu zetu zote tufanye amali njema ili tupate rehema ya Allah
 
Hutuba Fupi ya Ijumaa: "Kumcha Allah na Kushikamana na Uislamu"

Khutuba ya Kwanza:

Alhamdulillahi Rabbil 'aalamiin. Tunamshukuru Allah, tunamuomba msaada na msamaha wake. Tunajilinda kwake dhidi ya shari za nafsi zetu na madhambi yetu.

Enyi Waumini! Nawasii kumcha Allah (taqwa) kwa moyo wa kweli, kwa maneno na vitendo. Allah anasema:
"Enyi mlioamini! Mcheni Allah kama inavyostahiki kumcha, wala msife ila mkiwa Waislamu." (Qur'an 3:102)

Taqwa ndiyo silaha ya Muislamu duniani na kesho akhera. Mtu mwenye taqwa hujihadhari na dhambi hata akiwa peke yake, hufanya mema hata bila kuonekana.

Khutuba ya Pili:

Enyi Waja wa Allah! Tukumbuke kuwa dunia ni ya muda, lakini malipo ya amali zetu ni ya milele.
Tushikamane na swala, tusameheane, tuepuke fitina, na tujenge umoja kama alivyoamrisha Allah na Mtume Wake ﷺ.

Hadith: Mtume ﷺ amesema:
“Mtu bora zaidi ni yule anayemcha Allah sana na kufanya mema kwa watu.”

Tuombe dua:
"Allahumma ij’alnaa min al-muttaqiin, wa thabbit quluubanaa ‘alaa diinika."
(Ya Allah, tufanye tuwe miongoni mwa wamchao na uthibitishe mioyo yetu katika dini yako.)

Wasalamu Alaikum Warahmatullah Wabarakatuh.
 
UJUMBE WA LEO

Kuchinja inafaa mpaka dhulhijja 13,kwahiyo kama kama hukufanikiwa kuchinja siku ya eid,basi waeza chinja eid pili mpaka mwisho ni tarehe 13 dhulhijja

Wenye uwezo basi muifanye ibada hii ili mpate fadhila kutoka kwa Allah
 
Siyrah Ya Nabiy


Hijrah: Chanzo Cha Mageuzi





Alhidaaya.com









Allaah Amejaalia njia ya haki kuwa na ishara za wazi. Na Akajaalia kufikiwa katika lengo linalohitajika kwa juhudi na kujitolea. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



إِنَّ اللَّـهَ اشْتَرَىٰ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ ۚ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ ۖ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ وَالْقُرْآنِ ۚ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ مِنَ اللَّـهِ ۚ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُم بِهِ ۚ وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿١١١﴾



Hakika Allaah Amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwamba watapata Jannah. Wanapigana katika njia ya Allaah, wanaua na wanauawa. Hii ni ahadi ya haki Aliyojiwekea katika Tawraat na Injiyl na Qur-aan. Na nani atimizae zaidi ahadi yake kuliko Allaah? Basi furahieni kwa biashara yenu mliyofungamana Naye. Na huko ndiko kufuzu adhimu. [At-Tawbah:111]



Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alibeba bendera ya ushujaa mpaka ikawa ni yenye kunyanyuka katika kila sehemu ya pembe ya ulimwengu. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikaa miaka 13 Makkah baada ya kupewa utume akiilingania kaumu yake katika Uislamu. Hakika alibughudhiwa, kuudhiwa na kukadhibishwa Da‘awah yake. Mbali na hayo walikuwa wanajua ukweli na uaminifu wake mpaka wakawa wanamuita As-Swaadiqul Amiyn (Mkweli Muaminifu).





Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake walivumilia maudhi yao yote, adhabu na mateso. Katika mwezi wa Muharram Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliashiria kwa Swahaba zake kuhamia Madinah. Wakatoka wote isipokuwa wale waliokuwa na haja zao katika mji wa Makkah au walioshikwa na kufungwa kwa nguvu na makafiri.





Sababu ya Hijrah, ni pale Ma-Quraysh waliposhindwa kumkinaisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuacha Da‘awah yake na kuendelea kwake kumuabudu Allaah tu. Hivyo, walifikiria ima kumfunga au kumuua au kumtoa katika mji lakini uamuzi uliochukuliwa ulikuwa ni kumuua kabisa. Walichagua vijana wenye nguvu kutoka kila ukoo ili kutekeleza mkakati wao huo. Vitimbi vyao hivyo vilifichuliwa na Mwenye habari na Mjuzi, naye alitoka mbele ya vijana bila kuonekana na hao vijana waliokuwa wamekaa nje ya nyumba yake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



وَإِذْ يَمْكُرُ بِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِيُثْبِتُوكَ أَوْ يَقْتُلُوكَ أَوْ يُخْرِجُوكَ ۚ وَيَمْكُرُونَ وَيَمْكُرُ اللَّـهُ ۖ وَاللَّـهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ﴿٣٠﴾



Na pindi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) walipokupangia makri wale waliokufuru ili wakufunge, au wakuue, au wakutoe (Makkah). Na wanapanga makri, na Allaah Anapanga makri (kupindua njama zao), na Allaah ni Mbora wa wenye kupanga makri.[Al-Anfaal: 30]





Walifika kwenye pango na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akawalinda na maadui hao ambao walikuja mpaka kwenye mdomo wa pango la Thawr. Abubakar (Radhwiya Allaahu 'anhu) alipowaona makafiri wakiwa nje ya pango alisema: “Lau mmoja wao ataangalia chini ya miguu yake basi atatuona”. Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa utulivu na bila wasiwasi alimwambia: “Ee Abu Bakr! Dhana yako ni ipi kwa wawili ambao watatu wao ni Allaah” [Al-Bukhaariy na Muslim]. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Analizungumzia tukio hilo kwa kusema:



إِلَّا تَنصُرُوهُ فَقَدْ نَصَرَهُ اللَّـهُ إِذْ أَخْرَجَهُ الَّذِينَ كَفَرُوا ثَانِيَ اثْنَيْنِ إِذْ هُمَا فِي الْغَارِ إِذْ يَقُولُ لِصَاحِبِهِ لَا تَحْزَنْ إِنَّ اللَّـهَ مَعَنَا ۖ فَأَنزَلَ اللَّـهُ سَكِينَتَهُ عَلَيْهِ وَأَيَّدَهُ بِجُنُودٍ لَّمْ تَرَوْهَا وَجَعَلَ كَلِمَةَ الَّذِينَ كَفَرُوا السُّفْلَىٰ ۗ وَكَلِمَةُ اللَّـهِ هِيَ الْعُلْيَا ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴿٤٠﴾



Msipomnusuru (Rasuli), basi Allaah Amekwishamnusuru, pale walipomtoa (Makkah) wale waliokufuru akiwa wa pili katika wawili; walipokuwa katika pango, alipomwambia swahibu yake: Usihuzunike, hakika Allaah Yu Pamoja nasi. Basi Allaah Akamteremshia utulivu Wake, na Akamsaidia kwa majeshi msiyoyaona, na Akajaalia neno la waliokufuru kuwa chini. Na Neno la Allaah kuwa ndilo lililo juu. Na Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [At-Tawbah: 40].





Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Aliwaokoa wao wawili na vitimbi vya mushrikina. Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ataendelea Kuwahami na Kuwalinda walinganiaji wa haki mpaka Siku ya Qiyaamah.





Na hapo makafiri wakatoa zawadi ya ngamia mia moja (100) kwa atakaye wapata hai au maiti. Na hii hii ndiyo mbinu ambayo inatumiwa na makafiri wa sasa wanavyofanya wakati wanawatafuta watu. Na ndio wanazuoni wetu wakasema: “Ukafiri mila yao ni moja”.





‘Umar ibn al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu) baada ya kushauriana na Swahaba waliokuwa hai wakati wa Ukhalifa wake waliamua kuanza tarehe ya Kiislamu kwa tukio hilo, kwani ndio ilokuwa chanzo cha ushindi na kubadilisha historia yote. Hapo wakawa Waislamu Mashariki ya ardhi na Magharibi yake wanafahamu kabisa kwa uhakika kuwa ni Hijrah ndiyo iliyoharakisha mapambano na kujitolea mhanga. Lakini ni masikitiko kuwa hatufahamu umuhimu wa tukio hilo isipokuwa ni msimu wa kidini ambapo tunakariri matukio ya kimada ya Hijrah na jinsi alivyohama Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake na walivyopokewa kwa ukarimu Madinah na kula pilau kumaliza kabisa shughuli yenyewe





Ama mazingatio, maana matukufu makuu huwa mara nyingi hatuyataji sana na tukiyataja basi hayafiki kooni. Hakika, Hijrah ina mambo mawili: Zingatio la kimada na la kiroho.





1. Zingatio la kimada: Hii inaanza wakati alipotoka Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Makkah na kurudi kwake akiwa mshindi, huku akinyanyua bendera ya Tawhiyd na kuvunja masanamu. Na faida hii tunaiona mpaka wakati wetu huu wa sasa ambapo watu wanaingia katika Uislamu bila hesabu.



2. Zingatio la kiroho: Hii ni matokeo ya mapinduzi makubwa katika nafsi ya Muislamu na Ummah kwa ujumla wake kwa kufanya Da‘awah, na kutoka katika giza la ujinga na shirki kuelekea katika nuru ya elimu na Imani. Hijra inatufundisha kuacha maovu na riyaa na kujitwika tabia ya ukweli na uwazi na kupeana nasaha na kuifanya ndio msingi wa mahusiano yetu na watu wote – viongozi na raia bila kuogopa. Aliingia wakati mmoja ‘Amr ibn ‘Ubaydah kwa Khaliyfah wa Bani ‘Abbaas, al-Mansuur na akamsomea aya ifuatayo:

إِنَّ رَبَّكَ لَبِالْمِرْصَادِ

Hakika Rabb wako bila shaka Yu tayari Awavizia. [Al-Fajr: 14].



Khaliyfah akasema: “Onyo hili ni kwa nani, ewe Abu ‘Ubaydah?





Akamjibu bila khofu: “Hakika ni kwa wale wanaofanya mfano unayofanya wewe. Mche Allaah, ewe Amiri wa Waumini! Hakika katika mlango wako upo moto unaowaka, haufuati Kitabu cha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) wala Sunnah ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nawe una jukumu na utaulizwa kwa unayoyafanya na wala sio wanayoyafanya. Hivyo, usitengeneze dunia yao kwa kuiharibu Akhera yako. Ama Wa-Allaahi lau wafanyakazi wako wangejua kuwa huridhiki ila uadilifu wangekuja karibu nawe. Ee Amiri wa Waumini! Hakika watu wamekuchukua kama ngazi, wewe ndiye mshikaji pembe na wengine ndio wenye kukama maziwa. Hawa hawatakunufaisha chochote kwa Allaah. nami nakunasihi ewe Amiri wa Waumini, hakika wamelaaniwa Bani Israili kwa ulimi wa Dawuud na ‘Iysa kwani wao walikuwa:



كَانُوا لَا يَتَنَاهَوْنَ عَن مُّنكَرٍ فَعَلُوهُ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿٧٩﴾



Walikuwa hawakatazani munkari waliyofanya. Uovu ulioje waliyokuwa wakiyafanya. [Al-Maaidah: 79]





Hijrah inatakiwa ibadilishe maadili yetu – ya mtu na jamaa, na inatakiwa itutoe katika usingizi na iwe nukta ya kuanzia, hapo ndio tutaanza ili kutengeneza jamii nzuri zaidi na yenye ufanisi wa nyumba zote mbili (duniani na Akhera). Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa anahama aliomba kwa kusema: “Ee Rabb wangu! Hakika Wewe Unajua kuwa wao (yaani makafiri) wamenitoa katika mji ninaoupenda zaidi, hivyo nipatie maskani katika mji Unaopendwa zaidi na Wewe”





Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atubariki, Aturehemu na Atupatie fanaka katika mwaka huu wa Hijri. Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atupatie hima ya kurudi katika misimamo ya sawa na njia ya sawa inayompendeza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) pamoja na kufuata mwenendo wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). In shaa Allaah sote tuwe na azma ya kikweli kweli ya kubadilika na tutie bidii katika hilo na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atatusaidia katika hilo. Kwani Amesema:



إِنَّ اللَّـهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا مَا بِأَنفُسِهِمْ

Hakika Allaah Habadilishi yale yaliyoko kwa watu mpaka wao wenyewe wabadilishe yale yaliyomo katika nafsi zao. [Ar-Ra’d: 11]
 
Siyrah Ya Nabiy


Historia Fupi Ya Al-Ka’abah





Muhammad Faraj Salim As-Sa’y (Rahimahu Allaah)





Alhidaaya.com





Yaliyomo



Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam) anawasili Misri



Anarudi kwao



Anawasili Makkah



Anaamrishwa amchinje mwanawe



Mama yake Ismaa’iyl na kisima cha Zamzam



Watu wa kabila la Jurhum



Mwambie abadilishe kizingiti



Wananyanyua nguzo za Msikiti



Kisa cha Watu wa ndovu (As habul fiyl)



Kuujenga upya Al-Ka’abah



Wanaishiwa na pesa za halali



Mara ngapi umebomolewa na kujengwa upya?



Inajengwa tena



Hitimisho





Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam) alizaliwa katika mji unaoitwa Aar uliopo kandokando ya mto wa Furaat (Euphrates) Al Kufa - Iraq.



Inajulikana kuwa Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam) aliuhama mji huo na kuishi sehemu iliyokuwa ikiitwa Haraan na hatimaye akahamia nchi ya Palestina na huko ndiko alikofanya makao yake ya kuufikisha ujumbe alopewa na Rabb wake.



Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam) Anawasili Misri



Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam) akifuatana na mkewe alikwenda kutembelea nchi ya Misri, na huko alipokelewa na mfalme wa Misri aliyewaweka ndani ya qasri yake, na usiku ulipoingia mfalme huyo alijaribu kumdhuru Bibi Sarah mke wa Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam), lakini Allaah alimkinga bibi huyo na shari hiyo kwa kuufanya mkono wa mfalme upooze kila anapojaribu kumsogelea.



Alipoona dalili za qudra ya Allaah zikimlinda bibi huyo, mfalme akaacha vitimbi vyake na kuamua kumpa Bibi Sarah zawadi, na zawadi hiyo ni binti yake aitwae Hajar, na Sarah akaikubali zawadi hiyo na akamuozesha binti huyo mumewe Ibraahiym (‘Alayhis-salaam).



Anarudi kwao



Ibraahiym (‘Alayhis-salaam) akarudi kwao akiwa amefuatana na wake zake wawili, Bibi Sarah na Bibi Hajar, na kutokana na mke mpya, Allaah alimruzuku mtoto wa kiume waliyempa jina la Ismaa’iyl, jambo lililomfanya Bibi Sarah awe na wivu mkubwa juu ya mke mwenzake, na baada ya kuamrishwa na Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa, Nabiy Ibraahiym akamchukuwa Bibi Hajar pamoja na mwanawe Ismaa’iyl aliyekuwa bado mchanga wakati huo, na kufunga nao safari ndefu kutoka Palestina hadi nchi ya Hijazi (Saudia hivi sasa).



Anawasili Makkah



Alipowasili Makkahh penye bonde baina ya Swafa na Marwa mahali kilipo kisima cha maji ya zamzam hivi sasa, na wakati huo nyumba ya Allaah (Al-Ka’abah) ilikuwa ni sehemu iliyonyanyuka tu juu ya ardhi, ikishambuliwa na upepo mkali pamoja na mikondo ya maji ya mvua iliyokuwa ikizikwanguwa pembe nne za nyumba hiyo.



Hapakuwa na mtu anayeishi mahali hapo wala nyumba wala maji isipokuwa mti mmoja alipowaacha mkewe na mwanawe chini yake, akawawekea birika la maji pamoja na chombo alichowatilia tende ndani yake, kisha akageuka na kuianza safari ndefu ya kurudi Palestina.



Mama yake Ismaa’iyl alipomuona mumewe akirudi na kuwaacha mahali hapo walipopafikia baada ya safari ndefu iliyowachukuwa siku nyingi njiani, mahali pasipo na mji wala kijiji. Hapakuwa na hata dalili ya kuwepo mtu mahali popote karibu na hapo, akamfuata mumewe na kumuuliza:



“Unatuachia nani mahali hapa pasipo na mtu yeyote?”



Akamuuliza hivyo mara nyingi lakini Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam) hakumjibu.



Mwisho Mama yake Ismaa’iyl akamuuliza:



“Allaah ndiye Aliyekuamrisha?”



Nabiy Ibraahiym akamjibu:



“Naam, ndiyo.”



Kwa imani iliyothibiti, kwa utiifu mkubwa na kwa moyo uliosalimu amri, Bibi Hajar akamwambia:



“Kwa hivyo Hatotupoteza”.



Hapo ndipo Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam) alipogeuka na kuianza safari ndefu ya kurudi Sham akimuacha nyuma mkewe na mwanawe wa mwanzo na wa pekee wakati ule, na baada ya kutembea muda kidogo mahali ambapo mkewe hakuweza kumuona, Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam) akageuka nyuma na kuomba dua ifuatayo:



رَّبَّنَا إِنِّي أَسْكَنتُ مِن ذُرِّيَّتِي بِوَادٍ غَيْرِ ذِي زَرْعٍ عِندَ بَيْتِكَ الْمُحَرَّمِ رَبَّنَا لِيُقِيمُواْ الصَّلاَةَ فَاجْعَلْ أَفْئِدَةً مِّنَ النَّاسِ تَهْوِي إِلَيْهِمْ وَارْزُقْهُم مِّنَ الثَّمَرَاتِ لَعَلَّهُمْ يَشْكُرُونَ

Rabb wetu! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuria wangu katika bonde lisilokuwa na mmea wowote, kwenye Nyumba Yako Tukufu. Rabb wetu, ili wasimamishe Swalaah na Ujaalie nyoyo za watu zielekee kwao na Uwaruzuku mazao ili wapate kushukuru. [Ibraahiym: 37]



Anaamrishwa Amchinje Mwanawe



Nabiy Ibraahiym alikuwa mara kwa mara akija Makkah kuwazuru mkewe na mwanawe na hapana anayejuwa uhakika wa idadi ya ziara hizo, isipokuwa wanahistoria wameelezea juu ya ziara nne maarufu.



Ya mwanzo ni pale alipooteshwa kumchinja mwanawe wa pekee Ismaa’iyl (‘Alayhis-salaam) na mwanawe akakubali kutii amri hiyo, na alipomlaza mwanawe kifudifudi ili asiuone uso wake asije akamuonea huruma, na baada ya Ismaa’iyl (‘Alayhis-salaam) kutoa shahada, na Ibraahiym kusalimu amri kwa Allaah huku akijitayarisha kumchinja mwanawe, Allaah akamfunulia Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam) kuwa asimchinje mwanawe na badala yake akamkomboa kwa kondoo.



Kisa hicho kimeelezwa ndani ya kitabu cha Allaah Aliposema:



فَلَمَّا أَسْلَمَا وَتَلَّهُ لِلْجَبِينِ. ﴿١٠٣﴾ وَنَادَيْنَاهُ أَنْ يَا إِبْرَاهِيمُ﴿١٠٤﴾ قَدْ صَدَّقْتَ الرُّؤْيَا إِنَّا كَذَلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ. إِنَّ هَذَا لَهُوَ الْبَلَاء الْمُبِينُ﴿١٠٥﴾ وَفَدَيْنَاهُ بِذِبْحٍ عَظِيمٍ﴿١٠٧﴾

Basi wote wawili walipojisalimisha, na akamlaza kifudifudi juu ya kipaji. Na tukamwita: ee Ibraahiym. Kwa yakini umesadikisha ndoto. Hakika Sisi hivyo ndivyo Tunavyolipa wafanyao ihsan. Hakika hili bila shaka ni jaribio bayana. Na Tukamtolea fidia kwa dhabihu adhimu. [Asw-Swaffaat: 103-107].



Mama Yake Ismaa’iyl Na Kisima Cha Zamzam



Bibi Hajar (Mama yake Ismaa’iyl) akawa anakula zile tende alizowekewa na mumewe huku akimnyonyesha mwanawe, lakini haukupita muda mrefu maji yakaanza kupunguwa na hatimaye kumalizika, na mwanawe alipoanza kuona kiu, Bibi Hajar akaanza kuhangaika huku na kule akimtafutia maji.



Akaliendea jabali lililokuwa karibu yake - ‘Jabal Swafa’ – na kulipanda, na alipofika kileleni akaanza kutizama huku na kule akitafuta maji au msafara wa watu watakaokuwa na maji, lakini hakuona kitu.



Akateremka na kuanza kutembea taratibu penye bonde lililopo baina ya jabali Swafa na jabali Marwa, na alipofika kati kati ya bonde akaanza kukazana huku akiliendea jabali Marwa na kulipanda, na alipofika kileleni akaanza kutizama huku na kule, lakini bila mafanikio yoyote.



Anasema Ibni ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



“Hiyo ndiyo Saayi mnayotembea baina ya Swafa na Marwa.”



Bibi Hajar aliendelea kufanya hivyo mara saba, na alipokuwa akiliendea jabali Marwa akasikia sauti ngeni ikimsemesha. Alinyamaza kimya ili aisikie vizuri huku akitazama mahali alipo mwanawe, akamuona Malaika amesimama mahali kilipo kisima cha Zamzam hivi sasa, huku akichimba kwa ubawa wake mpaka maji yalipofurika, ndipo mamake Ismaa’iyl alipoyaendea na kuanza kuyachota kwa mikono yake huku akimnywesha mwanawe na kunywa yeye mwenyewe.



Alipokuwa akinywa na kumnywesha mwanawe, Malaika akamwambia:



“Usiogope - hutopotea, kwani hapa ndipo ilipo nyumba ya Allaah itakayojengwa na mtoto huyu na baba yake."



Watu Wa Kabila La Jurhum



Hazikupita siku nyingi na mama yake Ismaa’iyl akajiwa na msafara wa watu wa kabila la Jurhum ambao asili yao ni kutoka Yemen waliokuwa wasafiri waliopiga kambi sehemu ya chini ya mji wa Makkah mbali na hapo, na walikuja baada ya kuwaona ndege wakiruka sehemu aliyopo mama yake Ismaa’iyl wakasema:



“Bila shaka ndege hawa wameona maji”, na kwa vile inajulikana kuwa sehemu zile si kawaida kupatikana maji, wakaamua kutuma watumishi wakachunguze sehemu walipoonekana ndege, na walipokiona kisima cha maji ya Zamzam wakarudi kuwajulisha wenzao walioamua kukiendea haraka sana, lakini walipomuona mama yake Ismaa’iyl na mwanawe wakamuomba wakae naye wakamwambia:



“Utaturuhusu tukae pamoja na wewe mahali hapa?”



Mama yake Ismaa’iyl akawaambia:



“Nitakuruhusuni, lakini maji haya ni yangu.”



Wakasema:



“Tumekubali.”



Anasema Ibni ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:





“Jambo hilo lilimfurahisha sana mama yake Ismaa’iyl, kwani alikuwa mwenye kupenda watu.”



Mwambie abadilishe kizingiti



Watu wa kabila la Jurhum wakateremka na kuazisha maisha mepya mahali hapo, na Nabiy Ismaa’iyl (‘Alayhis-salaam) akaishi pamoja nao, akajifundisha kwao lugha ya kiarabu, akajifundisha kuwinda, na alipokuwa mkubwa wakamuozesha mmoja katika binti zao.



Baada ya kuishi muda aloishi, mama yake Ismaa’iyl akafariki dunia na Ismaa’iyl akaendelea kuishi mahali hapo pamoja na watu wa kabila hilo la Jurhum.



Nabiy Ibraahiym alikuja kumtembelea mwanawe katika ziara yake ya pili lakini bahati mbaya hajamkuta nyumbani na badala yake alimkuta mkewe, na alipomuuliza mahali alipo Ismaa’iyl akamwambia:



“Ametoka kwenda kututafutia rizki.”



Nabiy Ibraahiym akamuuliza juu ya hali zao na mwanamke akamjibu:



“Sisi ni wanadamu na hali zetu ni za dhiki na shida.”



Akaendela kumshitakia hali zao, na Nabiy Ibraahiym alipoondoka kurudi nchi ya Palestina akamwambia:



“Akirudi mumeo msalimie kisha mwambie abadilishe kizingiti cha nyumba.”



Aliporudi Nabiy Ismaa’iyl (‘Alayhis-salaam) alihisi kuwa jambo fulani limetokea nyumbani kwake, akamuuliza mkewe:



“Alikuja mtu hapa?”



Mkewe akajibu:



“Ndiyo, alikuja mzee mmoja na wasfu wake ni hivi na hivi, akauliza juu yako na mimi nikamwambia ulipo, akaniuliza juu ya hali zetu, nikamwambia kuwa sisi ni wanadamu na kwamba hali zetu ni za dhiki na shida.”



Akamuuliza:



“Alikuusia jambo lolote?”



Akajibu:



“Ndiyo, alinambia ukija nikusalimie kisha nikwambie ubadilishe kizingiti cha nyumba.”



Akamwambia:



“Yule alikuwa baba yangu na ameniamrisha nifarikiane na wewe, kwa hivyo rudi kwa wazee wako.”



Baada ya kumtaliki mkewe wa mwanzo, Nabiy Ismaa’iyl (‘Alayhis-salaam) akaoa mke mwingine, na inasemekana kuwa alikuwa binti wa Mudhaadh bin Amru aliyekuwa Sheikh wa kabila la Jurhum.



Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam) akaja tena kumtembelea mwanawe katika ziara ya tatu, na safari hii hajamkuta pia, na alipomuuliza mkewe akamwambia:



“Amekwenda kutuletea mahitaji yetu.” Na Ismaa’iyl alikuwa mwindaji anayesafiri mara kwa mara sehemu za mbali kwa ajili ya kazi yake hiyo na huchukuwa muda mrefu Swafarini.



Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam) akamuuliza:



“Vipi hali zenu?”



Akajibu:



“Tumesitirika AlhamduliLlaah tumo katika kheri kubwa.”



Akawa anasema hivyo huku akimshukuru Allaah.



Nabiy Ibraahiym akamuuliza:



“Mnakula chakula gani?”



Akajibu:



“Nyama.”



Akamuuliza:



“Mnakunywa nini?”



Akajibu:



“Maji.”



Akamwambia:



“Allaah vibariki nyama na maji.”



Anasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Siku hiyo hawakuwa na chochote nyumbani kwao.”



Nabiy Ibraahiym akamwambia:



“Akirudi mumeo mpe salamu zangu na umwambie akidhibiti vizuri kizingiti cha nyumba yake.”



Aliporudi Ismaa’iyl akauliza:



“Alikuja mtu leo?”



Akajibu:



“Alikuja mzee mmoja mwenye umbo zuri, akataka kujuwa habari zako, nikamjulisha, akaniuliza juu ya hali zetu nikamwambia kuwa tupo katika kheri.”



Akamuuliza:



“Alikuusia jambo lolote?”



Akamwambia:



“Ndiyo, yeye anakupa salamu nyingi na anakwambia ukidhibiti vizuri kizingiti cha nyumba yako.”



Akamwambia:



“Yule alikuwa baba yangu na ananiamrisha nikamatane na wewe.”



Wananyanyua Nguzo za Msikiti



Nabiy Ibraahiym akaja tena katika ziara yake ya nne, na safari hii Ismaa’iyl alikuwepo nje ya nyumba yake chini ya mti karibu na kisima cha maji ya zamzam akichonga mshale wake, na alipomuona baba yake akamnyanyukia kwa heshima kubwa, akamwamkia kama mtoto anavyoamuamkia baba yake wakakumbatiana kisha Nabiy Ibraahiym akasema:



“Allaah amenipa amri.”



Ismaa’iyl akamwambia;



“Fanya kama ulivyoamrishwa na Rabb wako.”



Akamwambia:



“Na wewe unisaidie.”



Akamwambia:



“Nitakusaidia.”



Akamwambia:



“Allaah Ameniamrisha nijenge nyumba mahali hapa.”



Akamuonesha ile sehemu ya ardhi iliyoinuka karibu na kisima cha maji ya zamzam, kisha wote kwa pamoja wakaanza kufanya kazi ya kuzinyanyua nguzo za nyumba na kuijenga Al-Ka’abah, na Ismaa’iyl akawa anamsogezea baba yake mawe huku Ibraahiym akijenga, mpaka nyumba ilipokamilika. Walikuwa wakijenga huku wakiomba dua ifuatayo:



“Eee Rabb Wetu! Tutakabalie (tutakabalie amali yetu hii ya kujenga huu Msikiti.”



Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:



وَإِذْ يَرْفَعُ إِبْرَاهِيمُ الْقَوَاعِدَ مِنَ الْبَيْتِ وَإِسْمَاعِيلُ رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ

Na aliponyanyua Ibraahiym na Ismaa’ily msingi wa Nyumba (Al-Ka’abah): Rabb wetu, Tutakabalie, hakika Wewe ni Mwenye kusikia yote,Mjuzi wa yote. [Al-Baqrah:127]



Na Akasema (Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa):



رَبَّنَا وَابْعَثْ فِيهِمْ رَسُولاً مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِكَ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُزَكِّيهِمْ إِنَّكَ أَنتَ العَزِيزُ الحَكِيمُ

Rabb wetu, wapelekee Rasuli miongoni mwao atakayewasomea Aayaat Zako na atakayewafunza Kitabu na Hikmah na atakayewatakasa. Hakika Wewe ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Al Baqarah:129]



Na hii ndiyo tafsiri ya hadiyth ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipoulizwa juu ya mwanzo wa amri yake akasema:



“Mimi ni dua ya baba yangu Ibraahiym na bishara ya ndugu yangu ‘Iysa (‘Alayhis- salaam).”



Anasema Ibni ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhu) kuwa baada ya kukamilisha ujenzi wa Msikiti wa Al-Ka’abah, Allaah akamuamrisha Nabiy Ibraahiym awatangazie watu waje kuhiji, na Nabiy Ibraahiym akasema:



“Ewe Mola wangu vipi itawafikia sauti yangu.”



Akamwambia:



“Juu yako ni kutangaza tu, na ni juu Yangu kuifikisha,” ndipo Nabiy Ibraahiym alipopanda juu ya kilele cha mojawapo ya milima ya Makkah na kupaza sauti yake akisema:



“Enyi watu mumefaridhishiwa Hijah katika nyumba kongwe,” na tangazo hilo likamfikia kila kiumbe baina ya mbingu na ardhi.



“Hamuoni kuwa watu wanauitikia mwito huo kutoka katika kila pembe ya dunia? Na katika riwaya nyingine; “Na wa mwanzo kuuitikia mwito huo walikuwa watu wa Yemen."



Kisa cha Watu Wa Ndovu (Aswhaabul Fiyl)



Abraha Mhabeshi aliyekuwa gavana wa An-Najaashiy katika nchi ya Yemeni iliyokuwa ikitawaliwa na Ethiopia wakati huo alikuwa akiona wivu kila anapowaona waarabu wakifunga safari ndefu kwenda kuizuru Al-Ka’abah, na kwa ajili hiyo akaamua kujenga kanisa kubwa kati ya mji wa Sana-a (mji mkuu wa Yemen) kisha akawataka waarabu waache kwenda Makkah na badala yake wakahiji penye kanisa lake.



Habari hizo zilimfikia mmoja katika watu wa kabila la bani Kinanah, aliyeamua kuingia kanisani nyakati za usiku na kulipaka mavi, jambo lililomghadhibisha sana Abraha aliyekusanya jeshi kubwa lenye idadi ya askari wanaozidi elfu sitini pamoja na tembo ishirini na mbili na yeye mwenyewe akiwa juu ya tembo mkubwa sana, na kuelekea nalo Makkah kwa ajili ya kuibomoa Al-Ka’abah.



Alipokaribia Makkah, penye bonde la Muhsir baina ya Muzdalifa na Mina, tembo mkubwa akapiga magoti na kukataa kuendelea na safari. Ikawa kila wanapomuelekeza kusini au kaskazini anainuka na kutembea, lakini wanapomuelekeza upande wa Makkah anakataa na hupiga magoti.



Wakawa katika hali hiyo mpaka pale Allaah alipowapelekea ndege makundi kwa makundi, wakawapiga kwa mawe ya udongo unaounguza.



Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:



أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِأَصْحَابِ الْفِيلِ ﴿١﴾أَلَمْ يَجْعَلْ كَيْدَهُمْ فِي تَضْلِيلٍ ﴿٢﴾وَأَرْسَلَ عَلَيْهِمْ طَيْرًا أَبَابِيلَ ﴿٣﴾تَرْمِيهِم بِحِجَارَةٍ مِّن سِجِّيلٍ ﴿٤﴾فَجَعَلَهُمْ كَعَصْفٍ مَّأْكُولٍ ﴿٥﴾

Je, hukuona (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) jinsi Rabb wako Alivyowafanya watu wa tembo? Je, Hakujaalia hila zao katika maangamizi?. Na Akawatumia juu yao ndege makundi kwa makundi yafuatanayo? Wakiwarushia mawe ya udongo uliookwa motoni. Akawafanya kama nyasi kavu zilizoliwa. [Al-Fiyl: 1-5]



Ndege walikuwa wakiwajia kwa wingi makundi kwa makundi, mfano wa vijumba mshale au zuwarde, kila mmoja akiwa amebeba mawe matatu yenye ukubwa kiasi cha dengu, moja mdomoni na mawili ameyabana mguuni, na kila anayepigwa na jiwe mwili wake hukatika vipande vipande na kufa.



Si wote waliopigwa na mawe hayo, walikuwemo wachache walioachwa wakarudi mbio kuelekea makwao huku wakiangukiana. Ama Abraha, Allaah alimsalitishia maradhi yaliyosababisha makucha yake kukatika na kupukutika huku akirudi alikotoka, na alifariki alipowasili mji wa Sana-a mwili wake ukiwa mfano wa kuku aliyenyonyoka manyoa.



Makureshi, wao walikimbilia sehemu mbali mbali mbondeni na juu ya vilele vya majabali wakihofia maisha yao, na hawakurudi majumbani mwao mpaka baada ya kumalizika yaliyotokea.



Tukio hili lilitokea mwezi wa Muharram kabla ya kuzaliwa kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa siku hamsini au hamsini na tano takriban muwafaka wa mwisho wa mwezi February au mwanzo wa mwezi wa March mwaka 571 baada ya Nabiy ‘Iysa.



Katika tafsiri ya Suratul Fiyl anasema Ibni Kathiiyr;



“Hii ni mojawapo ya neema za Allaah walizopewa Makureshi baada ya kuwalinda na shari walهokuja nayo watu wa ndovu waliokuja wakiwa na azma ya kuibomoa Al-Ka’abah na kuiondoa ili isiwepo tena. Lakini Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) aliwaangamiza na kuwalazimisha waliobaki warudi wakiwa wameshindwa juu ya kuwa walikuwa watu wanaofuata dini ya Manasara na kwa wakati ule wao walikuwa bora kuliko Makureshi waliokuwa wakiabudu Masanamu, lakini haya yalikuwa ni matayarisho ya kuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwa sababu kauli nyingi zinasema kuwa katika mwaka ule alizaliwa.



Kama kwamba uhakika wa mambo unasema; ‘Enyi Makureshi hamkupata nusura hii juu ya Mahabeshi kutokana na ubora wenu, bali kwa ajili ya kuilinda nyumba kongwe itakayopata heshima kwa kuzaliwa hivi karibuni kwa Rasuli wa Allaah Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mwisho wa Rusuli."



Habari za tukio hili zilienea kila pembe ya ulimwengu wa wakati ule, na kwa vile Wahabeshi walikuwa na uhusiano mzuri na Warumi, Waajemi waliokuwa wakingoja fursa nzuri kama hii wakaingia na kuiteka nchi ya Yemen kwa haraka sana, na dola mbili hizi (Uajemi na Roma) ndizo zilizokuwa dola kubwa za wakati ule, na wakati huo huo tukio hili la kuangamizwa kwa watu wa ndovu liliujulisha ulimwengu juu ya utukufu wa nyumba ile ya Allaah na kwamba Allaah ndiye aliyeitukuza na kuiadhimisha, na kwa ajili hiyo atakapotokea yeyote katika watu wake akasema kuwa yeye ni Nabiy, basi tukio hilo linampa nguvu mtu huyo.



Kwa hivyo ndani ya tukio hili mna hekima iliyojificha ya Allaah ya kuwapa ushindi washirikina dhidi ya watu wa imani kwa njia ya kimiujiza.



Kuujenga Upya Al-Ka’abah



Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na umri wa miaka thelathini na tano wakati Makureshi walipoujenga upya Msikiti wa Al-Ka’abah, kwa sababu miaka mingi ilikwishapita tokea Nabiy Ismaa’iyl alipoujenga na hapakuwa na kilichobaki katika jengo hilo isipokuwa rundu la udongo lenye urefu wa kiasi cha dhiraa sita, bila ya kipaa, jambo lililowarahisishia wezi kuingia ndani na kuiba hazina zinazowekwa humo.



Na kwa vile miaka mingi ilikwishapita tokea kujengwa kwake, kanuni za maumbile zilikwishafanya kazi yake. Kuta zilikuwa na nyufa, na miaka mitano kabla ya kupewa utume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yalitokea mafuriko makubwa yaliyosababisha maji kuingia ndani ya Msikiti na kubomoa sehemu kubwa za Msikiti huo, na kwa ajili ya yote hayo Makureshi wakaamua kuujenga tena Msikiti huo.



Wakakubaliana kuwa zisiingizwe katika ujenzi wa jengo hilo pesa zozote za haramu. Zisiingizwe pesa za mahari ya mzinzi, wala pesa za riba, wala pesa alizodhulumiwa mtu n.k.



Walikuwa wakiogopa kuubomoa Msikiti na kuanza kuujenga upya wasije wakadhurika, mpaka alipotangulia Al Walid bin Mughiyrah na kuianza yeye kazi hiyo, na wenzake walipoona kuwa hapana kilichomsibu, ndipo nao wakaingia kazini. Wakawa wanaendelea kuubomoa mpaka walipozifikia nguzo zilizosimamishwa na Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam), kisha wakaanza kuujenga upya Msikiti huo, na kila kabila likapewa sehemu yake ya kujenga, na kila kabila lilikuwa likikusanya mawe yake ya ujenzi, na msimamiaji wa ujenzi alikuwa Mrumi aitwae Baqum.



Kazi ilikwenda vizuri mpaka ulipofika wakati wa kulirudisha jiwe jeusi mahali pake, ndipo mzozo ulipoanza kila kabila likataka kupewa heshima hiyo ya kulirudisha mahali pake.



Mgogoro uliendelea muda wa siku nne au tano na mambo yakawa magumu hata watu wakakaribia kutaka kupigana vita, panga mkononi mpaka pale Abu Umayyah bin Mughiyra Al Makhzumiy alipotoa rai kuwa; wa mwanzo kuingia Msikitini kupitia mlangoni ndiye atakayeamua baina yao, na wote wakaridhika na rai hiyo.



Allaah akataka Nabiy wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) awe mtu huyo, na walipomuona tu akiingia, wote kwa pamoja wakapiga ukelele wa kuridhika:



"Huyu Muaminifu! Sote tumeridhika naye, huyu Muhammad."



Alipojulishwa juu ya uamuzi huo, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) (hii ilikuwa kabla ya kupewa utume) alikubali, na kwa utulivu akaomba kiletwe kitambaa, akakitandaza na kuliweka jiwe jeusi juu yake, kisha akawataka viongozi wa makabila yote kila mmoja akamate upande wa kitambaa, kisha wanyanyuwe kwa pamoja. Wakalinyanyua na walipopafikia mahali pa kuliweka, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)) akalinyanyua yeye kwa mikono yake miwili na kulirudisha mahali pake.



Kwa njia hii Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliweza kulitatua tatizo lililokaribia kuleta umwagaji wa damu mkubwa baina ya Makabila ya Kikureshi, na kila mmoja aliondoka hapo akiwa ameridhika.



Wanaishiwa Na Pesa za Halali



Makureshi walishindwa kuukamilisha Msikiti baada ya kuishiwa na pesa za halali, wakaamua kupunguza kiasi cha dhiraa sita upande wa kaskazini mwa Al-Ka’abah na hii ni ile sehemu inayojulikana kwa jina la Al Hijr (Hijr Ismaa’iyl) wakashindwa kuunganisha Msikiti pamoja na Hijri Ismaa’iyl ambayo asili yake ilikuwa imekamatana na Msikiti. Wakaunyanyua mlango kiasi cha dhiraa mbili kutoka juu ya ardhi asiweze kuingia isipokuwa wanayemtaka wao tu, na urefu wa jengo ulipotimia kiasi cha dhiraa kumi na tano wakaezeka sakafu juu ya nguzo sita, na baada ya kumalizika kazi hiyo, Al-Ka’abah ikawa na umbo la mraba lenye urefu wa mita kumi na tano, na upande wa jiwe jeusi pamoja na upande wa pili yake (mkabala wake) pande zote mbili kila moja ilikuwa na urefu wa mita kumi.



Na jiwe jeusi liliwekwa juu kiasi cha urefu wa mita unusu kutoka juu ya ardhi, na upande wa mlango na upande wa mkabala wake ukawa na urefu wa mita kumi kila upande, na mlango ukanyanyuliwa kiasi cha mita mbili kutoka juu ya ardhi, na upande wa nje ya Al-Ka’abah ikaachwa ikiwa imezungukwa na msingi ulionyanyuka kutoka juu ya ardhi kiasi cha robo mita na upana wa kiasi cha nusu mita.



Na sehemu hii ilikuwa ikiitwa Ash Shadherwan, sehemu ambayo asili yake ilikuwa ndani ya jengo la Al-Ka’abah, lakini Makureshi iliwabidi waiache sehemu hii bila kuijenga, na kwa ajili hiyo Msikiti ukawa na umbo la mraba badala ya umbo lake la asili lililofanana na herufi D iwapo utaunganishwa na Hijr kama ulivyojengwa na Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis salaam).



Mara Ngapi Umebomolewa na Kujengwa Upya?



Inajulikana kuwa Msikiti wa Al-Ka’abah umejengwa kwa mara ya mwanzo na Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam).



Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:



وَإِذْ يَرْفَعُ إِبْرَاهِيمُ الْقَوَاعِدَ مِنَ الْبَيْتِ وَإِسْمَاعِيلُ رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ



Na aliponyanyua Ibraahiym na Ismaa’ily msingi wa Nyumba (Al-Ka’abah): Rabb wetu, Tutakabalie, hakika Wewe ni Mwenye kusikia yote,Mjuzi wa yote.[Al-Baqarah: 127]



Imesimuliwa na Imam Muslim katika Sahihi yake na pia ndani ya vitabu vyengine mbali mbali vya elimu ya hadiyth na vya Siyrah katika mlango ya 'Kubomolewa na kujengwa upya Msikiti wa Al-Ka’abah' kama ifuatavyo:



Sehemu kubwa ya Msikiti iliungua wakati Al Hajjaj alipoushambulia akitumia 'Manjaniq' (mtambo wa kutupa mawe uliokuwa ukitumika katika vitani vya zamani) akitaka kumuuwa ‘‘Abdullaah bin Az-Zubayr bin ‘Awaam (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na hii ilikuwa wakati wa utawala wa Yazid bin Mu’aawiyah.



Mwana wa Az-Zubayr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) aliuacha Msikiti kama ulivyo mpaka ulipoingia msimu wa Hijah wa mwaka ule na watu wakawa wengi, akawakusanya na kuwahutubia, akasema:



"Enyi watu! Nataka ushauri wenu juu ya Al-Ka’abah. Niuvunje Msikiti wote kisha niujenge upya au nitengeneze tu sehemu zilizoungua?"



Ibni ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akasema:



"Mimi ninayo rai, naona ni bora usiubomoe, bali utengeneze tu na uiache kama ilivyo nyumba waliosilimu watu juu yake, na mawe waliosilimu watu juu yake, na alitumwa kwa ajili yake nyumba hiyo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)."



Mwana wa Az-Zubayr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akasema:



"Mmoja wenu ikiungua nyumba yake hatoridhika kuiacha ilivyo (bila shaka atapenda kuijenga upya), vipi basi nyumba ya Rabb wenu? Mimi nitaswali Istikhaarah mara tatu kisha nitaamua."



Na baada ya kukamilisha tatu akaamua kuubomoa, lakini kila mmoja aliogopa kupanda na kuianza kazi hiyo asije akadhurika, mpaka alipopanda mtu mmoja na kunyanyua jiwe, akalitupa chini, na watu walipomuona hajadhurika wakaingia na wao kazini na kuianza kazi ya kuubomoa Msikiti mpaka walipozifikia nguzo, kisha mwana wa Az-Zubayr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akazinyanyua nguzo na kuujenga upya, na alipomaliza akaishonea Al-Ka’abah pazia, akaujenga Msikiti kama ulivyokuwa wakati wa Nabii Ibraahiym (‘Alayhis-salaam) kisha akasema:



"Nilimsikia khale yangu (Bibi ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) akisema kuwa amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)) akisema:



"Ingelikuwa watu hawakutoka hivi karibuni tu katika ujahilia na ningelikuwa na pesa za kutosha kuujenga vizuri Msikiti, ningeongeza dhiraa tano na kuuganisha na Hijri (Ismaa’iyl) kisha nikajaalia mlango kwa ajili ya watu kuingia ndani yake na mlango wa kutokea."



Na katika riwaya nyingine:



"Makureshi walipoijenga nyumba walishindwa kuikamilisha kwa sababu waliishiwa na pesa."



Na katika riwaya nyengine kupitia kwa ‘‘Abdullaah bin Abi Bakr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema:



"Na ningejenga milango miwili, mmoja mashariki na mmoja magharibi ikawa juu ya ardhi kisha ningeunganisha Msikiti na Hijri Ismaa’iyl."



Akasema ‘‘Abdullaah bin Zubair (Radhwiya Allaahu ‘anhu):



"Mimi leo ninazo pesa na siwaogopei watu."



Akaongeza dhiraa tano na akajenga milango miwili, mmoja kwa ajili ya watu kuingia na mwengine wa kutokea.



Inajengwa Tena



Alipouliwa ‘‘Abdullaah bin Az-Zubayr (Radhwiya Allaahu ‘anhu), Al Hajjaj akamuandikia ‘Abdul-Malik bin Marawan aliyekuwa Khalifa wa Waislamu wakati huo na kumjulisha juu ya mabadiliko aliyofanya mwana wa Az-Zubayr katika Msikiti, na ‘Abdul Malik akamjibu:



"Urefu alouongeza mwana wa Az-Zubayr uache na sehemu aloongeza katika Hijri ibomowe na milango aloiongeza izibe."



Al Hajjaj akafanya kama alivyoambiwa.



Hitimisho



Riwaya zinazokubalika zilizopokewa na 'Ulamaa zinasema kuwa Msikiti umejengwa mara nne.



Ya kwanza ulipojengwa na Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam).


Ya pili wakati wa ujahilia kabla ya Uislamu, na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)) alishiriki katika ujenzi huo na wakati huo alikuwa na umri wa miaka thelathini na tano na katika riwaya nyingine alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano.


Ya tatu ulipojengwa na mwana wa Az-Zubayr (Radhwiya Allaahu ‘anhu).


Ya nne ulipojengwa tena na Al Hajjaj baada ya kupewa amri na ‘Abdul Malik bin Marwaan ya kubomoa zile sehemu zilizoongezwa na mwana wa Az-Zubayr (Radhwiya Allaahu ‘anhu).


Imepokelewa pia kuwa Haaruun Ar-Rashiyd alitaka ushauri wa kuujenga upya Msikiti huo na kuzirudisha zile sehemu zilizojengwa na ‘‘Abdullaah mwana wa Zubayr (Radhwiya Allaahu ‘anhu), lakini Imam Maalik akamnasihi kwa kumwambia:



"Kwa ajili ya Allaah ewe Amiri wa Waislamu, tafadhali iache nyumba kama ilivyo, na usiifanye ikawa mchezo kwa wafalme, kila mmoja akaja kubomoa na kuujenga upya atakavyo, na mwisho wake haiba ya nyumba itaondoka ndani ya vifua vya watu."
 
Siyrah Ya Nabiy


Mafunzo Kutoka Katika Hijrah



Muhammad Faraj Saalim As-Sa’iy (Rahimahu Allaah)



Alhidaaya.com





Ndugu zangu Waislam, katika kalenda ya Hijri (Kalenda ya Kiislam) imeanza, na kwa ajili hiyo tutajikumbusha kidogo juu ya umuhimu wa siku hizi kwa ajili ya kuelewa umuhimu wake na kwa ajili ya kujifunza angalau machache juu ya Hijrah ya Nabiy wetu mtukufu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na Swahaba wake watukufu (Radhwiya Allaahu ‘anhum).



Mwaka jana katika mnasaba huu, tulisoma namna gani tukio la Hijrah lilivyokuwa muhimu kupita matukio yote yaliyopata kutokea katika historia ya Kiislam, na hii ni kwa sababu kutokana na Hijrah, taifa la mwanzo la Kiislam liliweza kuundwa, na Waislamu wakaweza kuweka miguu yao juu ya ardhi, madhubuti kwa ajili ya kuisimamisha dini yao, kuilinda itikadi yako, na kuweza kuieneza ulimwenguni kote.



Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na Waislamu wa mwanzo waliokuwa wachache sana, wakiongozwa na Abu Bakr na ‘Umar na ‘Uthmaan na ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhum), walihiari kuhatarisha maisha yao, kupoteza mali zao, milki zao pamoja na kila walichokuwa nacho kwa ajili ya kutaka radhi za Rabb wao Subhaanahu wa Ta’aalaa.



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖ تَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا ۖ

Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Rasuli wa Allaah. Na wale walio pamoja naye ni wakali zaidi dhidi ya makafiri; wanahurumiana baina yao. Utawaona wakirukuu na wakisujudu wakitafuta fadhila na radhi kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). [Al-Fath: 29]



Tukasema kuwa kwa ajili ya umuhimu wake, ndiyo maana Waislam walikubaliana kuianzisha Kalenda ya Hijrah ya Kiislam kuanzia mwaka huo.



Siku tukufu ambayo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akifuatana na Sahibu yake Abu Bakr Asw-Swiddiyq (Radhwiya Allaahu ‘anhu), walihama kutoka Makkah kwenda Madiynah, wakitanguliwa na kufuatiliwa na Swahaba watukufu (Radhwiya Allaahu ‘anhum).



Waislamu ambao wakati huo walikuwa wachache sana, walipata mtihani mkubwa kutokana na mateso waliyopata pamoja na kudharauliwa na kunyanyaswa na makafiri wa Makkah. Lakini mara baada ya kutakiwa na Nabiy wao (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuihama nchi yao hiyo na kwenda Madiynah, wakaanza kukumbana na mtihani mwingine. Mtihani wa kuiacha nchi yao, nchi waliyozaliwa na kulelewa na kucheza juu ya mchanga wake. Iliwabidi waiache nchi hiyo pamoja na kuacha nyuma mali zao, nyumba zao na kila walichomiliki isipokuwa vichache sana walivyoweza kuvibeba katika safari ndefu iliyojaa kila aina ya hatari na mashaka. Walikuwa tayari kupambana na yote hayo kwa ajili ya utiifu wao kwa Rabb wao na kwa ajili ya kuinusuru na kuiendeleza dini yao.



Kwa vile wengi wao walitoka nyakati za usiku kwa kujificha wakihofia maisha yao, iliwabidi waache vitu vyao vingi vilivyokuwa vizito na vengine vya thamani, ili waweze kukimbia kwa wepesi na haraka na ili wasalimike na mateso ya Maquraysh. Waliacha vyote hivyo nyuma yao na kuianza safari ndefu iliyowawezesha kufika kwa ndugu zao waliokuwa wakiwasubiri kwa hamu na shauku kubwa sana huko Madiynah ili washirikiane nao katika kuiendeleza mbele dini yao hii tukufu na mpya.



Anasema Ibn Kathiyr katika Al-Bidaayah wan Nihaayah kuwa:



"Katika mwaka wa kumi na sita na inasemekana katika mwaka wa kumi na saba wa Ukhalifa wa ‘Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu), Waislam walikubaliana kuianzisha Kalenda yao, kutokana na matatizo yaliyokuwa yakitokea mara kwa mara baina yao wakati watu wakiandikiana mikataba ya madeni au ya aina nyengine.



Waarabu walikuwa wanayohesabu ya miezi yao, lakini hawakuwa na hesabu ya miaka, na kwa ajili hiyo wengine walikuwa wakitumia kalenda za Kifursi na wengine za Kirumi na wengine wakitumia matukio ya wakati wa ujahilia.



‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alipowataka Waislam kutoa rai zao kuhusu jambo hilo, wengine wakapendekeza ianzie mwaka aliozaliwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na wengine wakapendekeza ianzie pale alipopewa Utume na wengine wakapendekeza siku aliyokufa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Lakini Khalifa wa Waislam ‘Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akapendelea rai zilizosema kuwa ianzie siku ile ya Hijrah na wengi wakakubaliana naye.



Kwa vile mwezi wa Al-Muharram ndio mwezi wa mwanzo wa Kiarabu, wakakubaliana kuhesabu kuanzia mwezi huo."



Ufuata ni mpangilio wa Miezi ya Kiislam:



Al-Muharram (Mfunguo nne)



Swafar



Rabiy’ul Awwal (Mfunguo sita)



Rabiy’uth Thaaniy



Jumaadal Awwal



Jumaadath Thaaniy



Rajab



Sha’abaan



Ramadhaan



Shawwaal



Dhul Qa'dah (Mfunguo pili)



Dhul Hijjah (Mfunguo tatu)



Baada ya kutoa dalili mbali mbali, Mwanachuoni Ibn Kathiyr katika kitabu chake hicho mashuhuri kiitwacho Al-Bidaayah wan Nihaayah akamaliza kwa kusema:



"Nimekuelezeeni kwa ushahidi wa kutosha ulioandamana na isnadi zake na njia zake kutoka katika Siyrah ya ‘Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na AlhamduliLlaah na kusudi langu ni kuwa wao (Swahaba) walikubaliana wote kwa Ijmai kuianzisha Kalenda ya Kiislam kuanzia Mwaka wa Hijrah na wakakubaliana kuufanya mwezi wa mwanzo uwe mwezi wa Al-Muharram na hii pia ni kauli za Maimaam wote waliobaki".



Ama kuhusu rai ya Imaam Maalik, Ibn Kathiyr ameandika yafuatayo:



"Amesema As-Suhayliy na wengineo kuwa Imaam Malik amesema kwamba mwanzo wa Mwaka wa Kiislam ungeanzia mwezi wa Rabiy’ul-Awwal (na si Al-Muharram), kwa sababu mwezi huo ndio aliohama ndani yake Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na akaegemea ushahidi wake katika kauli ya Allaah Subhanahu wa Ta’aalaa pale Aliposema:



لَا تَقُمْ فِيهِ أَبَدًا ۚ لَّمَسْجِدٌ أُسِّسَ عَلَى التَّقْوَىٰ مِنْ أَوَّلِ يَوْمٍ أَحَقُّ أَن تَقُومَ فِيهِ ۚ

Usisimame humo abadani. Bila shaka Msikiti ulioasisiwa juu ya taqwa tokea siku ya kwanza unastahiki zaidi usimame humo. [At-Tawbah: 108]



(Kusudi la 'Siku ya mwanzo' katika Aayah hii, ni siku ile Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alipowasili Madiynah).



"Bila shaka kauli ya Imaam Malik ndio inayonasibiana, lakini (Swahaba kabla yake) walikwishakubaliana kuwa Mwaka wa Kiislam uanzie Mwaka aliohama Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ndani yake (Mwaka wa Al-Hijrah), na wakakubaliana Mwezi wa mwanzo uwe mwezi wa Al-Muharram ili wasibabaike. Wa-AAllaahu Ta’aalaa A’alam”.



Hivi ndivyo alivyomaliza Imaam Al-Haafidh Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah).



Safari za jangwani zilikuwa zikiwatoa jasho majabari na mashujaa wakubwa wa wakati ule wanaosafiri wakiwa katika amani, kwa hivyo munaweza kukisia hatari za namna gani zilizokuwa zikimkabili Rasuli wa (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliyeondoka akiwa na sahibu yake Asw-Swiddiyq (Radhwiya Allaahu ‘anhu) huku wakiwa wanasakwa na makafiri waliokwishaamua kuwa lazima auliwe, wakatangaza zawadi ya ngamia mia moja kwa yeyote atakayeweza kumkamata Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa hai au amekwishakufa.



Hawezi kuyakisia haya ila yule aliyewahi kuuonja moto wake.



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwahi kulikata jangwa lile alipokuwa mdogo akiwa amefuatana na mama yake siku ile walipokwenda Madiynah kwa ajili ya kulizuru kaburi la baba yake, kisha akarudi Makkah peke yake kwa sababu mama yake alifariki dunia alipowasili Madiynah. Lakini safari hii Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) analikata tena jangwa hilo hilo akiwa na umri uliopindukia miaka hamsini pamoja na Sahibu yake Asw-Swiddiyq (Radhwiya Allaahu ‘anhu), si kwa ajili ya matembezi wala kwa ajili ya biashara, bali kwa ajili ya kuuendeleza ujumbe aliokuja nao.



Anasafiri ili aweze kuusimamisha ujumbe huo juu ya ardhi ya Yathrib (Madiynah), na kuiweka mizizi yake hapo baada ya kung'olewa katika mji wa Makkah.



Aliondoka Makkah kuelekea Madiynah akiwa na yakini kupita mtu yeyote yule kuwa Rabb wake Atamnusuru na kuidhihirisha dini Yake, na alikuwa na uhakika pia kuwa Rabb wake atamrudisha tena Makkah.



Allaah Alikwishamwambia:

فَإِنَّكَ بِأَعْيُنِنَا ۖ

Kwani hakika wewe uko chini ya Macho Yetu. [Atw-Twuwr: 48]



Na Akasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



إِنَّ الَّذِي فَرَضَ عَلَيْكَ الْقُرْآنَ لَرَادُّكَ إِلَىٰ مَعَادٍ ۚ

Hakika Yule Aliyekufaridhishia Qur-aan (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم,) bila shaka Atakurudisha mahali pa marejeo. [Al-Qaswasw: 85]



Mwenendo Wa Rusuli ('Alayhim-Salaam)



Kutokana na Hijrah hii Nabiy wetu mtukufu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) atakuwa ametimiza Sunnah ya Rusuli wenzake waliomtangulia, kwani Rusuli yote ('Alayhim-salaam) kuanzia Nabii Ibraahiym mpaka kufikia kwa ‘Iysa (‘Alayhis-salaam), wote waliihama miji yao waliyozaliwa, wakateswa na kusubiri ili wawe mfano mwema kwa watu wao.



Na hii ndiyo maana Waraqah bin Nawfal siku ile alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



"Yalaiti ningeliishi mpaka siku ile watu wako watakapokutowa katika nchi yako".



Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amesema:



وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِرُسُلِهِمْ لَنُخْرِجَنَّكُم مِّنْ أَرْضِنَا أَوْ لَتَعُودُنَّ فِي مِلَّتِنَا ۖ

Wakasema wale waliokufuru kuwaambia Rusuli wao: Bila shaka tutakutoeni katika ardhi yetu, au mtarudi kwa hakika katika mila zetu. [Ibraahiym: 13]



Tofauti Ya Kuhama Kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) Na Kuhama Kwa ‘Umar Bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘Anhu)



"Inaweza kumpitikia mtu kutaka kufananisha baina ya kuhama kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na kuhama kwa ‘Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu), akajiuliza:



"Kwa nini ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akahama mchana tena mbele ya watu bila kuogopa, huku akiwabishia makafiri pale alipowaendea na kuwaambia:



‘Zimedhalilika nyuso zenu, zimedhalilika nyuso zenu, yeyote kati yenu anayetaka mamake ampoteze na wanawe wawe mayatima na mkewe awe kizuka, basi na akutane nami nyuma ya bonde hili.’



Wakati Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alihama kwa kificho bila kumjuulisha mtu. Mtu anaweza kujiuliza:



"Hivyo ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) anaweza kuwa shujaa kuliko Nabiy?



Jibu lake litakuwa:



"Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) au Muislam yeyote yule, hukmu yao ni tofauti na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwani matendo ya mtu yeyote yule awe ‘Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) au mwengine yanahesabiwa katika dini kuwa ni matendo yake mwenyewe binafsi, na kwamba si hoja inayoweza kusimama katika dini kama yalivyo matendo ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kwani mtu mwingine asiyekuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anaweza kutumia njia zozote zile azitakazo anazoziona kuwa ni mnasaba kwake, ama Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yeye matendo yake ni Shari’ah, na hii maana yake ni kuwa matendo yake yote yanayohusiana na dini yanahesabiwa kuwa ni Shari’ah kwetu, na kwa ajili hiyo Mafundisho yake (Sunnah zake) yakawa ni asili ya pili ya Shari’ah, yakiwemo matendo yake, maneno yake, sifa zake na yale yaliyofanywa mbele yake na akayakubali.



Lau kama Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) angefanya kama alivyofanya ‘Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu), baadhi ya watu wangedhania kuwa hivyo ndivyo anavyowajibikiwa kila Muislam kufanya, na kwamba haina haja mtu kuchukua tahadhari wala kuogopa pale anapokuwa katika hatari.



Baada Ya Kuhamia Madiynah



Tuliona huko nyuma kuwa mara baada ya kuwasili mjini Madiynah, jambo la mwanzo alilofanya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ni kufungisha udugu baina ya watu wa Makkah na watu wa Madiynah, na jambo la pili ni kuujenga Msikiti uliokuwa mfano wa Chuo Kikuu kilichokuwa kikifundisha Imani, udugu, umoja, ushujaa, fiqhi pamoja na tabia na mwenendo mwema, na kutokana na hayo Chuo hicho kikaweza kutoa mashujaa walioweza kuzifungua nchi nyingi pamoja na nyoyo nyingi.



Nabiy (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) Akiwa Madiynah



Anasema Shaykh Abu Bakr Al-Jazairiy:



"Hakika ya miaka yote kumi na tatu aliloishi Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pale Makkah tokea alipopewa utume mpaka siku ile aliyohama kwenda Madiynah, yote ilikuwa ni maumivu na machozi na huzuni. Hakupata kufurahi hata kwa muda wa saa moja au kustarehe angalau kwa siku moja.



Ama miaka kumi aliloishi Madiynah, yote ilikuwa ni miaka ya Jihaad iliyokamatana. Hakupata hata siku moja kukaa bure wala kustarehe. Hata maisha; kwake yalikuwa magumu, hakupata hata siku moja kushiba mkate au tende wala hata kula vizuri mara mbili katika siku moja.



Naam, ingawaje kwa siku alizoishi Madiynah zilikuwa ni siku za kuchomoza, lakini siku nyingi katika hizo zilikuwa ni za kuunguza".



Kusilimu Kwa ‘Abdullaah Bin Salaam (Radhwiya Allaahu ‘Anhu)



Mara baada ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwasili mji wa Madiynah alikuja kwake ‘Abdullaah bin Salaam (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na kuzitamka shahada mbili.



Akasema:



"Nashuhudia kuwa hapana anayepaswa kuabudiwa isipokuwa Allaah na kwamba wewe ni Rasuli wa Allaah na kwamba uliyokuja nayo ni haki. Ee Rasuli wa Allaah, Mayahudi ni watu waongo, wanajua kuwa mimi ni bwana wao na mwana wa bwana wao na wanajuwa pia kuwa mimi ni ‘Aalim wao na mwana wa ‘Aalim wao, kwa hivyo nakuomba (uniache nijifiche, kisha) uwaite na uwaulize juu yangu kabla ya kuwajulisha juu ya kusilimu kwangu, kwani wakijua kuwa nimesilimu watasema juu yangu yale nisiyokuwa nayo".



Wakasema mara tatu:



"Sisi hatujui"



Kisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawauliza:



“Ana daraja gani kwenu ‘Abdullaah bin Salaam?”



Wakasema:



"Yule ni bwana wetu na mwana wa bwana wetu, na ‘Aalim kutupita sote na mwana wa ‘aalim kutupita sote".



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawauliza:



“Munaonaje akisilimu?”



Wakasema:



"Haiwezekani hata siku moja akasilimu"



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawauliza hivyo mara tatu, kisha akasema:



“Ee ‘Abdullaah bin Salaam, watokee.”



Akawatokea na kusema:



"Enyi Mayahudi, mcheni Allaah kwani naapa kwa yule ambaye hapana anayepaswa kuabudiwa isipokuwa Yeye, mnajua vizuri kuwa huyu ni Rasuli wa Allaah na kwamba amekuja na haki".



Wakasema:



"Muongo! wewe si bwana wetu wala si ‘Aalim wetu".



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaamrisha watolewe nje.



[Imepokewa na Al-Bukhaariy]



Mwenye Kumtii Nabiy (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) Atakuwa Pamoja Naye



Swahaba wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na hususan watu wa Madiynah walikuwa wakimpenda Nabiy wao (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kupita kiasi, na walikuwa tayari wakati wote kuzitanguliza roho zao na nafsi zao kwa ajili ya kumlinda Nabiy wao mtukufu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na yale aliyokuja nayo. Ni wao waliohatarisha maisha yao hapo mwanzo walipomfuata Nabiy wao mtukufu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) huko Makkah katika usiku ule wa hatari na kumpa ahadi ya kumnusuru na kumlinda ikiwa atahamia kwao Madiynah. Kisha wakafungamana naye kwa siri mahali panapoitwa Al-’Aqabah katika mafungamano yaliyokokuja kujulikana baadaye kama 'Fungamano la ‘Aqabah' (la mwanzo na la pili).



Watu wa Madiynah waliitimiza ahadi yao hiyo ya kumlinda Nabiy wao (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na kuwalinda Waislam wote waliohamia kwao na kuwasaidia kwa hali na mali. Na pale Allaah Subhaanahu Wa Ta’aalaa Alipoiteremsha kauli Yake:

أُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَاتَلُونَ بِأَنَّهُمْ ظُلِمُوا ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ نَصْرِهِمْ لَقَدِيرٌ ﴿٣٩﴾الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِم بِغَيْرِ حَقٍّ إِلَّا أَن يَقُولُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ۗ

Wameruhusiwa (kupigana) kwa wale wanaopigwa kwa kuwa wamedhulumiwa. Na kwamba Allaah bila shaka ni Muweza wa kuwanusuru. Ambao wametolewa majumbani mwao bila ya haki isipokuwa kwa kuwa wanasema: Rabb wetu ni Allaah. [Al-Hajj: 39-40]



Watu wa Madiynah wakaingia katika mapambano mbali mbali na majeshi ya makafiri mpaka pale Allaah alipowawezesha Waislamu kuuteka mji wa Makkah na kuyabomoa masanamu yaliyokuwepo ndani ya Al-Ka’abah na kuidhihirisha Haki na kuiangamiza Baatwil.



Hadiyth ifuatayo inatuwezesha kuihisi angalau kwa uhaba ladha ya namna Swahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum) na hasa watu wa Madiynah walivyokuwa wakimpenda na kumuenzi na kumthamini Nabiy wao mtukufu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na namna gani walivyokuwa tayari kujitolea kwa hali na mali kumtii Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).



Imetolewa na Imaam Al-Bukhaariy na Muslim na Atw-Twabaraaniy na wengineo kuwa mara baada ya kumalizika vita vya kuuteka mji wa Makkah, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aliwakusanya mateka na kuwauliza:



“Mnadhani nitakufanyeni nini?”



Wakajibu:



‘Utatufanyia kila la kheri, ewe ndugu mwema na mwana wa ndugu mwema.’



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawaambia:



“Nendeni, nyote nimekuacheni huru.”



Karibu mateka wote hao wakasilimu kwa hiari yao na kujiunga na jeshi la Kiislamu lililoondoka hapo Makkah kuelekea mji wa Hunayn kwa ajili ya kupambana na majeshi ya watu wa Huwzan waliokuwa njiani kuelekea Makkah kuwashambulia Waislam.



Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Zayd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa baada ya Waislam kushinda katika vita vya Hunayn, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwagawia ngawira iliyopatikana katika vita hivyo watu wa Makkah tu hasa wale waliosilimu hivi karibuni kwa ajili ya kuwalainisha nyoyo zao, na watu wa Madiynah hawakupewa chochote.



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alijuwa kuwa watu wa Madiynah hawakufurahi kwa sababu na wao pia walitegemea kupewa chochote katika ngawira ile kama walivyopewa wenzao watu wa Makkah.



Alipojulishwa juu ya hayo, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akawaita watu wa Madiynah na kuwahutubia, akasema:



“Nini haya maneno niliyosikia kuwa mlikuwa mkiyasema?”



Viongozi wao wakasema:



"Ama wakubwa wetu hawakusema lolote, isipokuwa watu wengine wanasema; "Allaah Amghufirie Nabiy wake, anawapa Maquraysh ngawira kwa mamia na sisi hatupi chochote wakati damu zao bado hata hazijakauka juu ya panga zetu?"



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:



“Mmekasirika kwa sababu ya faida ndogo tu ya kidunia enyi watu wa Madiynah? Mimi nimewapa hawa kwa sababu wao ndio kwanza wametoka katika ukafiri na kuingia katika Uislam ili niwalainishe nyoyo zao, nikakuacheni nyinyi kwa kuutegemea Uislam wenu. Enyi watu wa Madiynah! Si niliwakuta mmepotoka Allaah Akakuongozeni kupitia kwangu? Na nikawakuta masikini na Allaah Akakutajirisheni kupitia kwangu? Mmegawanyika na Allaah Akakuunganisheni kupitia kwangu? Mafakiri na Allaah Akakuneemesheni kupitia kwangu?”



Walikuwa kila wanapoulizwa wakijibu:



"Allaah Ametufanyia ihsani zaidi na Nabiy Wake ametufanyia Ihsani zaidi"



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawauliza:



“Mbona hamnijibu?”



Wakasema:



"Tukujibu nini ee Rasuli wa Allaah?"



Akasema:



“Kama mngenijibu kwa maneno mengine zaidi ya haya mngekuwa mnasema kweli. Mngetaka, mngeweza kusema; "Na wewe pia ulikuja kwetu ukiwa umefukuzwa na watu wako na sisi tukakupokea, umekadhibishwa na sisi tukakusadiki. Ulikuja peke yako umo hatarini na sisi tukakunusuru, na tukayakubali yale watu wako waliyoyakataa. Kisha mkawa mnanihesabia mema yote mliyonitendea.”



Kisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawaambia:



“Hamridhiki wakati wenzenu wanaondoka wakiwa na ngamia na kondoo na nyinyi mtaondoka mkiwa na Rasuli wa Allaah mpaka makwenu? Watu wa Madiynah (Al-Answaar) ni mfano wa nguo iliyokamatana na ngozi na waliobaki ni mfano wa guo la juu, Enyi watu wa Madiynah! Si Allaah Amekuiteni majina mazuri mazuri (kama vile) 'Answaar wa Allaah' na 'Answaar wa Nabiy Wake?' Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu imo mikononi Mwake, lau kama nisingehajiri basi ningelikuwa mmoja kati ya watu wa Madiynah, na lau kama watu wote watafuata njia zao katika mabonde na mitaa, na watu wa Madiynah watafuata njia nyingine, basi mimi ningefuata njia ya watu Madiynah. Allaah Warehemu ma-Answaar (watu wa Madiynah) na wana wa Answaar na wajukuu wa Answaar.”



Anasema Ibn Is-haaq aliyoisimulia sehemu ya mwisho ya Hadiyth hii kuwa:



"Waliohudhuria wakaanza kulia kwa kwikwi mpaka ndevu zao zikarowa, wakasema:



"Tumeridhika na Allaah kuwa Rabb wetu na Rasuli Wake kuwa sehemu yetu."



Kisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaondoka na wao wakatawanyika.



Sehemu ya mwisho ya Hadiyth hii imepokelewa kwa njia ya Imaam Ahmad peke yake na kusimuliwa na Ibn Is-haaq.



Ndugu zangu Waislam, anayetaka kuwa pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba wake watukufu (Radhwiya Allaahu ‘anhum) siku ya Qiyaamah, lazima awe mtiifu wa maamrisho aliyokuja nayo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).



Imepokelewa na Atw-Twabaraaniy na Ibn Mardawiya na Abu Na’iym kutoka kwa Mama wa Waumini ‘Aaishah bint Abi Bakr (Radhwiya Allaahu anhum) kuwa: Siku moja mtu mmoja alimwendea Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na kumwambia:



"Ee Rasuli wa Allaah, kwa hakika mimi nakupenda kuliko ninavyoipenda nafsi yangu na kuliko ninavyowapenda wanangu. Ninapokuwa nyumbani basi nikikukumbuka tu, siwezi kustahamili tena, lazima nije nikutazame. Lakini kila ninapokumbuka kuwa siku moja mimi nitakufa na wewe utakufa, kisha nikakumbuka kwamba wewe daraja yako itakuwa juu pamoja na Rusuli, na mimi nikiingia Jannah naogopa (daraja yangu haitokuwa ya juu kama yako) nisiweze kukuona tena huko".



Katika riwaya nyingine:



"Swahaba yule aliyekuwa katika watu wa Madiynah alilia sana, na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomuuliza:



“Nini kinachokuliza?”



Akamjibu:



"Kila ninapokumbuka kuwa wewe daraja yako itakuwa ya juu pamoja na Rusuli, na mimi nikiingia Jannah naogopa (daraja yangu haitokuwa ya juu kama yako) na sitoweza kukuona tena huko".



Kabla Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwahi kumjibu Swahaba yule (Radhwiya Allaahu ‘anhu), Jibriyl (‘Alayhis-salaam) aliteremka na kauli ya Allaah isemayo:



وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا ﴿٦٩﴾

Na atakayemtii Allaah na Rasuli, basi hao watakuwa pamoja na wale Allaah Aliowaneemesha miongoni mwa Manabii na Swiddiqiyna na Mashuhadaa na Swalihina, na uzuri ulioje kuwa pamoja na hao. [An-Nisaa: 69]



Yaani atakayefanya yale aliyoamrishwa na Rabb wake na Rasuli wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na akayaacha yale alokatazwa na Rabb wake na aliokatazwa na Rasuli wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), basi Allaah Atamuingiza katika Jannah yake na atakuwa pamoja na Rusuli na Swiddiqiyn na Mashahidi na Swaalihiyn (watu wema).
 
EID MUBARAK!

Assalaam alaikum warhamatullah wabarakatuh

Baada ya Swalaa natumaini wengine mnaelekea kwenye maandilizi ya kuchinja

Allah atufanyie wepesi sote kuiendea ibada hii,kwa wale wasio fanikiwa kuchinja basi tuweke nia panapo maajaliwa mwakani inshaAllah tutekeleze ibada hiyo

Kikubwa leo ni siku ya furaha,basi tujumuike na ndugu na jamaa na marafiki tufurahi pamoja

Tujiweke mbali kabisa na maasi ili tuwe salama mbele ya Allah azza wa jalla

Eid Mubarak!
 
Nasaha kwa Siku ya Eid:

🕌 “Eid ni siku ya furaha, lakini isiwe sababu ya kusahau ucha Mungu.”

Eid ni zawadi kutoka kwa Allah baada ya ibada kubwa — iwe Ramadhan au Hijja. Ni wakati wa kushukuru, kusameheana, kuungana, na kuwatembelea wengine kwa upendo na huruma.

Nasaha Muhimu:
1. Shukuru neema ya kufikia Eid kwa afya na imani.
2. Usifurahie kwa kupita mipaka — epuka dhambi, miziki haramu, au anasa zisizofaa.
3. Wakumbuke wasiokuwa na uwezo — kwa sadaka, chakula au tabasamu.
4. Samehe waliokukosea — kwa Eid, moyo uliojaa chuki hupoteza ladha ya sikukuu.
5. Shikamana na sala — hata baada ya Ramadhan, uislamu hauishi na mwezi.

"Mwenye furaha ya kweli ni yule anayerejea kwa Allah kwa moyo ulio safi, si tu mwenye mavazi mapya."
 
Siyrah Ya Nabiy




Muujiza Wa Al-Israa Wal-Mi'raaj Na Mafunzo Yake



Imekusanywa Na: Alhidaaya.com





بسم الله الرحمن الرحيم





Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَىٰ بِعَبْدِهِ لَيْلًا مِّنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ ﴿١﴾

Utakasifu ni wa Ambaye Amemsafirisha usiku mja Wake kutoka Al-Masjid Al-Haraam mpaka Al-Masjid Al-Aqswaa ambao Tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake; ili Tumuonyeshe baadhi ya Aayaat (miujiza, ishara, dalili) Zetu. Hakika Yeye (Allaah) ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote. [Al-Israa 17: 1]





Utangulizi:



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anaelezea Utukufu Wake, Ukubwa Wake na Uwezo Wake, kuwa Yeye ni Mweza wa kila kitu na Anafanya kila kitu Anachotaka kukifanya. Yeye pekee Ndiye Mwabudiwa wa kweli na Yeye pekee Yake Ndiye Rabb (Muumba, Mtoaji wa Riziki na Mwenye kutoa ukimu wa kila kiumbe). Alimchukua mja Wake Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kutoka Makkah na kumpeleka katika Masjid Al-Aqswaa (Msikiti wa mbali) huko Jerusalem katika usiku mmoja. [Tafsiyr ya Ibn Kathiyr].







Baadhi Ya Miujiza Ya Rasuli Wa Allaah (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam):





Qur-aan:



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipewa miujiza mingi na Rabb wake. Muujiza wake mkubwa ni Qur-aan; Kitabu ambacho kiliteremshwa miaka 1400 iliyopita na hakuna hata mtu mmoja ambaye ameweza kubadilisha hata herufi moja au kuleta kitabu cha mfano wake. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ ﴿٩﴾

Hakika Sisi Tumeteremsha Adh-Dhikra (Qur-aan) na hakika Sisi bila shaka ndio Wenye kuihifadhi. [Al-Hijr 15: 9]





Aayah hii ni changamoto dhidi kwa makafiri waliojaribu kuandaa mifano ya Qur-aan wakashindwa na kufedheheka.





Vitabu vingine vitokavyo kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni Tawraat na Injiyl ambavyo viliharibiwa ima kwa kuongeza maneno au kupunguzwa maneno. Ama Qur-aan Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ametoa ahadi kuwa “Atailinda” na kweli Ameilinda na Ataendelea Kuilinda.



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kila Nabiy aliyekuja kabla yangu alipewa muujiza na miujiza hiyo ilibakia kuwa miujiza wakati wa uhai wao hao Manabii: Mfano ‘Iysaa (‘Alayhis-Salaam) alikuwa na muujiza wa kutibu watu wagonjwa na kufufua wafu Muwsaa (‘Alayhis-Salaam) alipewa fimbo ya miujiza na mambo mengine, nami nimepewa muujiza wa milele, Qur-aan itabakia kuwa muujiza hadi kusimama Qiyaamah. Hivyo natarajia kuwa wafuasi wangu watakuwa ni wengi katika idadi zaidi ya wafuasi wa Manabii wengine kwa kuwa muujiza wangu utabakia na utakuwepo hadi Siku ya Qiyaamah ambao ni Qur-aan. Kila anayekisoma Kitabu hiki hata kama ni mpagani basi yeye huvutika na kuona ukweli uliomo ndani yake na kuona hakuna aliyekiandika isipokuwa Rabb wa Mbingu na Ardhi.” [Swahiyh Al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim].





Kupasuka Kwa Mwezi:



Muujiza mwingine wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ulikuwa ni kupasuka kwa mwezi. Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) anasema katika riwaayah yake, kuwa watu wa Makkah walimtaka Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) awaonyeshe muujiza na akawaonesha kupasuka kwa mwezi. [Swahiyh Al-Bukhaariy, Juzuu ya 4 Namba 831].





Kutoka Maji Kutoka Vidole Vya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)



Imepokewa kutoka kwa Jaabir ibn Abdillaah akisema: “Nilikuwa na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na muda wa kuswali Swalaah ya Al-‘Aswr ukafika. Tulikuwa hatuna maji isipokuwa maji kidogo tu ambayo yalikuwa ndani ya chombo ambayo yaliletwa kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) . Basi aliweka mkono wake ndani ya maji hayo na kutandaza vidole vyake na huku akisema, “Njooni Haraka watu wote ambao wanataka kutawadha Hii ni baraka kutoka kwa Allaah.” Nikaona maji yakibubujika kutoka katika vidole vyake. Hivyo watu walitawadha na wengine wakawa wanakunywa maji hayo na mie nilitaka kunywa maji mengi kupita kiasi (kwa sababu nilijua kuwa ilikuwa ni baraka). Mpokeaji wa Hadiyth hii kutoka kwa Jaabir alisema: “Nilimwuliza Jaabir Je, mlikuwa watu wangapi wakati huo?” Akajibu, “Tulikuwa watu elfu moja na mia nne.” [Swahiyh Al-Bukhaariy, Juzuu 7 namba 543 na Swahiyh Muslim, Juzuu 4 namba 779].





Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa amepewa miujiza mingine mingi. Muujiza mwingine mkuu ni ule wa Israa na Mi’raaj au “Safari ya Usiku.”



Makala hii ni kujaribu kuonesha faida zinazopatikana katika safari hii na mafunzo yanayopatikana katika muujiza huu mkubwa.





Tukio la Israa na Mi’raaj lina hekima na mafunzo makubwa mno. Funzo lake kubwa ni kuwa mja hapaswi kukata tamaa, lazima awe daima anamtegemea Rabb wake kuwa atamletea faraja hata kama kutakuwa na mambo mazito yanamkabili. Zaidi ya hapo mwana Aadam anapaswa kuwa daima karibu na Rabb wake hasa wakati anapokuwa anakabiliwa na mambo mazito na vitendo vya kuhuzunisha au mikasa mizito, kwani matatizo hayo hupotea kama vile yalikuwa hayajatokea.









Baadhi Ya Matukio Yaliyotokea:





1- Kifo cha Abuu Twaalib.





Abuu Twaalib alikuwa ni mlinzi na mlezi wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati Waislamu wakiwa Makkah na yeye alimkinga dhidi ya mashambulizi ya makafiri wa Makkah. Watu wa Makkah walipopinga kwa nguvu risala ya Muhammad na kuanza kumshambulia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na kuwashambulia Waislamu, Abuu Twaalib alikinga kifua chake na kumhami mtoto wa nduguye. Alisema, “Tunapenda kusaidia tunakubali ushauri wako na tunayakubali maneno yako. Hawa ni watu wa jamii yako ambao umewakusanya na mimi ni miongoni mwao, lakini mimi ni mwepesi kuliko wote kufanya kile ukitakacho. Fanya kila lile uliloamriwa kufanya. Nitakulinda na kukuhami, lakini siwezi kuiacha dini yangu.” Abuu Lahab akapayuka na kusema: “Wa-Allaahi jambo hili ni jambo ovu na wewe lazima umkataze hayo ayafanyayo kabla ya watu wengine hawajamkanya.” Abuu Twaalib akasema: “Naapa nitaendelea kumlinda na kumhami katika maisha yangu yote.” [Ar-Rahiyq Al-Makhtuwm].





Al-‘Abbaas bin Abdil-Mutwalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kuwa alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Hukuwa mwenye kumsaidia ‘Ami yako, Abuu Twaalib, japo kuwa yeye alikuwa ni mtu mwenye kukuhami sana na alikuwa anachukizwa sana kwa mambo uliyokuwa unatendewa na Makureshi.” Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Yuko katika moto mwepesi, kama si mimi angelikuwa kwenye moto wa tabaka la chini kabisa huko Jahanam.” [Swahiyh Al-Bukhaariy Juzuu 5 Namba 222].





Hivyo licha ya kuwa Abuu Twaalib ni kafiri, lakini alimuunga mkono Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa nguvu zake na mali yake dhidi ya makafiri. Wakati Abuu Twaalib alipokuwa hai makafiri walikuwa hawawezi kumdhuru Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hata hivyo, kifo cha Abuu Twaalib kilikuwa ni mwanya kwa makafiri wa kuendeleza vitimbi vyao dhidi ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na dhidi ya Waislamu kwa ujumla. Tabia yao ya ukatili ilimfanya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aone maisha mjini Makkah ni magumu. Kusilimu kwa Maswahaba mjini Makkah ilikuwa ni njia ya kujitangazia uadui wa wazi wazi na wakawa wanapata madhila na kuadhibiwa vibaya. Kila aliyesilimu aliambiwa afanye moja kati ya mambo mawili: aritadi au aondoke hapo nchini au sivyo basi roho yake itafariki dunia; makafiri hawakutaka njia nyingine zaidi ya hiyo. Lakini Maswahaba licha ya kuwa hiki kilikuwa ni kipindi kigumu sana na chenye taabu kubwa sana katika maisha yao kutokana na adhabu na madhila waliyoyapata, waliendelea kusimama imara juu ya imani ya Uislamu na walisonga mbele na Rasuli wao (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika msimamo huo.





Kupanuka kwa Uislamu kuliwaudhi sana makafiri na wakajaribu kila njia ili kuzuia na kukinga Uislamu usiwepo katika nchi yao. Ulinganiaji wa Dini hii ukawa mzito kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na hata kuishi mjini Makkah ikawa ni hali ngumu sana kwake na kwa Waislamu.





2- Kifo cha Khadiyjah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa):



Ni miezi miwili tu baada ya kifo cha Abuu Twaalib. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipata tatizo lingine zito lililomhusu yeye binafsi. Mke wake na Mama ya Waumini, Sayyidah Khadiyjah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) alifariki. Mama wa Waumini Khadiyjah, alikuwa ni rehma kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Alikuwa daima na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakati akipata madhila na maudhi ya Makureshi na alikuwa naye siku zote wakati wa mitihani mizito ilipokuwa inamfikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kutoka kwa mahasimu wake wa Kikureshi na walikuwa pamoja katika hali hiyo kwa muda wa miaka 25. Na kwa yote hayo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ukaribu huo aliokuwa nao Mama wa Waumini Khadiyjah alisikitika sana kwa kifo cha mkewe mpenzi na kuna wakati alisikika akisema juu ya Sayyidah Khadiyjah: “Aliniamini wakati wengine hawakufanya hivyo, Alijiunga na Uislamu wakati watu walikuwa hawataki kufanya hivyo. Pia alinisaida na kuniliwaza mwenyewe na na kwa mali zake wakati kulikuwa hakuna hata mtu wa kuniunga mkono. Pia nilipata watoto kutoka kwake.’’ [Musnad Ahmad 6/118].





Matukio haya mawili yalitokea mfululizo. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa amefikia hali ya kubabaika namna gani awaongoze Makureshi wa Makkah, basi aliangalia upande wa Twaaif mji ambao kwa wakati huo ulikuwa unahitajia msaada na uongozi. Lakini hata huko pia hakupokelewa na hali hiyo kuongeza machungu moyoni mwake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hata akaona kipindi hicho kuwa ni “Mwaka wa Huzuni”.





Baada ya mitihani hiyo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Alimchukua mja Wake katika muujiza mkubwa wa Israa na Mi’raaj ili amwoneshe Aayah Zake na kumpatia msaada na himaya. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا ۚ

Ili Tumuonyeshe baadhi ya Aayaat (miujiza, ishara, dalili) Zetu. [Al-Israa (17: 1)]





Kwa muujiza wa Israa na Mi’raaj, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Aliweka msingi kwa waja Wake kuwa hata kama makafiri wangelifunga mlango wa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Allaah Ndiye Mwenye Kumhami na ndio Mlezi Wake na milango ya Peponi iko wazi kwa ajili ya Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hakuna nguvu ambayo inaweza kumteza au kumdhuru yule ambaye yuko chini ya ulinzi wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).





Israa na Mi’raaj ilikuwa ni dalili ya kuonesha kufanikiwa kwa Da’wah ya Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na ushindi wake juu ya maadui zake pamoja na kuwepo kwa mitihani hiyo.





Safari ya Israa:



Lini kilikuwa kipindi cha Israa na Mi’raaj?



Tarehe hasa ya tukio la Israa na Mi’raaj haifahamiki kwa uhakika. Ibn Kathiyr amenukuu kutoka kwa ‘Ulamaa mbali mbali katika kitabu chake Al-Bidaayah wan-Nihaayah (3/108) juu ya terehe ya tukio hilo. ‘Ulamaa wengi wanaona kuwa tarehe hiyo ilikuwa kati ya miezi 12 na 16 kabla ya Hijrah yake kwenda Madiynah. Na wa zaidi ya hapo wamekhitilafiana juu ya siku na hata huo mwezi.



Kabla ya Safari:



Malaika Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) alifungua kifua cha Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), akatoa moyo wake na kuuosha kwa maji ya Zam Zam. Anasema Anas Bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu): “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alichukuliwa katika Israa na Mi’raaj kutoka Masjid Al-Haraam (Msikiti Mtukufu Makkah). Watu watatu walimjia (ndotoni) akiwa amelala ndani ya Masjid Al-Haraam kabla hakufunuliwa Wahyi kwake. Mmoja wao akasema: “Ni yupi kati ya hawa watu?” Malaika wa kati akasema: “Yule ambaye ni mbora kuliko wote.” Na Malaika wa Mwisho akasema: “Chukueni aliye mbora wao.” Mambo haya yalitokea katika usiku huo huo. Usiku huo hakuwaona, lakini aliwaona usiku mwingine ambapo tayari Wahyi ulikuwa umefunuliwa kwake na alikuwa macho amelala lakini alikuwa hadhiri (Ni kawaida ya Manabii wote kulala macho wakati wako hadhiri). Wale Malaika hawakumsemesha bali walimbeba hadi wakamfikisha katika kisima cha Zam Zam. Miongoni mwao ni Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) alikuwa akiongoza na kuelekeza kifanyike nini. Alipasua sehemu kati ya koo na kati ya kifua na akatoa vyote vilivyokuwemo kifuani na kuviosha kwa maji ya Zam Zam kwa mikono yake mwenyewe na pia kusuuza sehemu za ndani za mwili na kisha kikaletwa chano cha dhahabu kikiwa na bakuli la dhahabu kililetwa ndani ya bakuli mkiwa mkajazwa iymaan na busara. Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) akachukua vitu hivyo kutoka ndani ya bakuli na kuvijaza kifuani mwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kisha akachukua viungo vya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na mishipa ya damu akavijaza kifuani kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kukifunga kifua.” [Swahiyh Al-Bukhaariy, Juzuu 9 Namba 608, na Juzuu 5 Namba 227].





Israa maana yake ni safari ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yeye akiwa ni mwili wake na akili zake na roho yake kutoka Ka’bah huko Makkah mpaka Masjid Al-Aqswaa (Msikiti wa Mbali) huko Quds (Jerusalem) akiwa amebebwa na mnyama wa ajabu mwenye kuvutia umbo lake anayeitwa Buraaq na kisha safari ya kurejea kwake Makkah.





Al-Buraaq:





Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alichukuliwa kutoka Masjid Al-Haraam, Makkah mpaka Masjid Al-Aqswaa mjini Quds juu ya mnyama aitwaye Al-Buraaq akiwa ameambatana na Malaika Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwelezea Al-Buraaq kuwa: “Nililetewa Al-Buraaq, mnyama mrefu wa umbo na mweupe, ni mkubwa kiasi zaidi ya punda lakini ni mdogo kuliko nyumba, ambaye anapokwenda mbio hatua yake ni upeo wa macho yake. Nilimpanda mnyama huyo mpaka nikafika Masjid Al-Aqswaa huko Al-Quds (Jerusalem). Hapo nilimfunga pale mahali ambapo Manabii wengine walikuwa wakifunga wanyama wao.” [Swahiyh Al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim].





Anas Bin Maalik alisema: “Katika usiku ambao Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipelekwa mbinguni, Al-Buraaq aliletwa kwake akiwa amefungwa vikuku na ana matandiko, lakini alifanya ugumu kidogo, na ndipo Jibriyl alipomwambia Al-Buraaq: “Je unafanya haya kwa Muhammad? Hakuna mtu mtukufu aliyewahi kukupanda ambaye ni mtukufu zaidi ya huyu mbele ya Macho ya Allaah.” Kisha akatoa jasho.” [At- Tirmidhiy na Musnad Ahmad].





Maana Ya Al-Buraaq Kwa Kiarabu Ni Mwale Unaotoka Katika Mwanga:





Leo hii, Wanasayansi wanatuambia kuwa mwanga una mwendo kasi zaidi ya vitu vyote duniani. Huenda masafa ya maili 700 milioni kwa saa moja. Miaka 1400 iliyopita wakati ambapo kulikuwa hapajatokea utafiti na uvumbuzi palikuwa hakuna mtu ambaye aliweza hata kukisia mwendo kasi wa mwanga wala ukweli wake ukoje. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walimwita mnyama huyo kama Al-Buraaq kwa msingi wa mwendo wake ulivyo na kasi kali. Huu ni ukweli ambao unthibitisha ukweli wa Uislamu na ukweli wa Unabiy wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama Alivyosema Allaah ndani ya Qur-aan:



سَنُرِيهِمْ آيَاتِنَا فِي الْآفَاقِ وَفِي أَنفُسِهِمْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُ الْحَقُّ ۗ أَوَلَمْ يَكْفِ بِرَبِّكَ أَنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ﴿٥٣﴾

Tutawaonyesha Aayaat (ishara, dalili) Zetu katika peo za mbali na katika nafsi zao, mpaka iwabainike kwamba hiyo ni haki! Je, haitoshelezi Rabb wako kuwa Yeye ni Shahidi juu ya kila kitu? [Fusswilat 41: 53].







Hapo kale watu walipinga na kusema: “Mnyama huyo katokea wapi tena ambaye alimchukua Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kutoka sehemu moja ya dunia mpaka nyingine na kisha kapita naye katika anga za mbingu na tena katika usiku mmoja?”



Leo hii tunaona vipando ambavyo vimeundwa na wana Aadam; roketi na misali vikikata maelfu ya maili kwa muda dakika chache tu. Basi iweje Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ashindwe kuumba mnyama mwenye uwezo wa kukata masafa ya mamilioni ya maili kwa muda mfupi, ilhali Yeye Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ndiye Muumba wa ulimwengu na Wana Aadam hao na Ndiye Yeye Aliyewajaalia uwezo wa kuunda hivyo vitu?





Kituo cha kwanza cha Safari ni Al-Aqswaa:





Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: “Kisha niliingia Masjdi Al-Aqswaa, nikaswali Raka’ah mbili.” [Swahiyh Muslim].





Riwaayah nyingine ambazo zinaeleza kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali na Manabii wengine hapo Msikiti wa Al-Aqswaa na yeye akiwa Imaam.





Msikiti wa Al-Aqswaa umekuwa na sifa ya kuwa ni kituo cha Manabii wote, toka siku ya Al-Khaliyl Ibraahiym (‘Alayhis-Salaam). Hivyo Manabii wote walikusanyika hapo na Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawa Imaam wao. Hii ni dalili ya nafasi kubwa aliyo nayo Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye ni Nabiy wa mwisho miongoni mwa Manabii wengine (‘Alayhimus- Salaam). [Tafsiyr Ibn Kathiyr].





Kisa cha Israa na Mi’raaj kimeelezwa ndani ya Qur-aan [Al-Israa 17:1]





Aayah inayofuatia inaeleza matendo ya aibu na makosa ya Mayahudi na kufuatia juu ya hayo makemeo makali ya Qur-aan. Mpangilio huo si kwa bahati tu, Al-Quds ilikuwa ni kituo cha kwanza cha safari hii ya Usiku na hapa kuna ujumbe ambao unaelekezwa kwa Mayahudi na kupewa ujumbe kuwa hadhi waliyokuwa nayo ya kuongoza dunia na bin Aadam kwa ujumla imetanguliwa. Utenguzi wa uongozi kwa Mayahudi ulitokana na mabaya yao waliyokuwa wakiyafanya na yale ambayo wanaendelea kuyafanya.



Ujumbe huo unathibitisha wazi wazi kuwa uongozi huo umehamia kwa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) achukue uongozi wa makao makuu ya ‘Aqiydah ya Baba Ibraahiym na pia kuwa makao hayo sasa ni Makkah na Masjdi Al-Aqswaa (Msikiti wa mbali) huko Al-Quds. Hivyo mamlaka hayo yalihamishwa kwenda kwenye taifa ambalo ni la wenye taqwa na lenye utii kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) pamoja na Nabiy ambaye amependelewa kubeba Qur-aan ambayo inaongoza watu kuelekea kwenye ukweli. [Ar-Rahiyq Al-Makhtuwm].





Uchaguzi wa Asili (Fitwrah):





Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba:



“Vyombo viwili vya dhahabu vililetwa kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kimoja kikiwa kimejazwa maziwa na kingine kikiwa kimejazwa mvinyo (pombe). Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) achague kinywaji kati ya hivyo vinywaji viwili. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alichagua maziwa na akainua kile chombo na kuyanywa. Jibriyl alisema, “Umeongozwa katika fitwrah na umefikia daraja ya fitwrah. Kama ungelichagua mvinyo, watu wako wangelipotea.” [Swahiyh Al-Bukhaariy Juzuu 6 Namba 232].





Neno fitwrah lina maana ya silika asili ambayo imo kwa kila mtoto anapozaliwa. Silika hiyo inamtambua Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa); kama silika hiyo haikufisidiwa humpeleka mja katika iymaan ya Tawhiyd ya Allaah.



Imaam An-Nawawiy alisema kuwa kauli ya Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) kwa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Umechagua fitwrah” maana yake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa amechagua Dini ya Islaam, yaani: “Umechagua nembo ya Islaam na Istiqaamah (kuwa imara katika Njia Iliyonyooka). Maziwa yalikuwa ni alama tu kwa sababu ni rahisi kuyanywa wakati mvinyo ni “mama wa maasi na maovu” na chanzo cha matendo ya kikatili.”



Kwa lugha nyepesi ni kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliletewa vitu viwili; kimoja kinawakilisha matendo mema na kingine kinawakilisha matendo maovu na viliwekwa mbele ye Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kwa silika akachagua kile kilicho kizuri. Kwa leo hii mtu akiacha fitwrah na kuanza kutafuta vitu vinginevyo anaonekana jinsi anavyohangaika baada ya kuacha njia ambayo amewekewa na Rabb wake. Ni wajibu wa mwana Aadam kushikamana na Njia ambaye ameamrishwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa sababu Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَىٰ ﴿١٢٤﴾

“Na atakayejitenga na ukumbusho Wangu basi hakika atapata maisha ya dhiki, na Tutamfufua Siku ya Qiyaamah hali akiwa kipofu.”



قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَىٰ وَقَدْ كُنتُ بَصِيرًا ﴿١٢٥﴾

Atasema: “Rabb wangu! Kwa nini Umenifufua kipofu, na hali nilikuwa naona?”



قَالَ كَذَٰلِكَ أَتَتْكَ آيَاتُنَا فَنَسِيتَهَا ۖ وَكَذَٰلِكَ الْيَوْمَ تُنسَىٰ ﴿١٢٦﴾

(Allaah) Atasema: “Hivyo ndivyo, zilikufikia Aayaat Zetu ukazisahau na kadhaalika leo umesahauliwa.” [Twahaa 20: 124 - 126].





Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَمَن كَانَ فِي هَـٰذِهِ أَعْمَىٰ فَهُوَ فِي الْآخِرَةِ أَعْمَىٰ وَأَضَلُّ سَبِيلًا ﴿٧٢﴾

Na atakayekuwa kipofu katika hii (dunia) basi yeye Aakhirah atakuwa kipofu na atapotea zaidi njia. [Al-Israa 17: 72].











Mi’raaj ni hali iliyomfikia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ya kupaa mbinguni kutoka Masjid Al-Aqswaa na kwenda katika mbingu ya saba.



Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) alikuwa naye katika msafara huo wa kupaa. Ibn Kathiyr aliandika katika kitabu chake cha Al-Bidaayah wan-Nihaayah: “Safari ya kupaa haikuwa kwa kutumia Al-Buraaq kwa sababu alikuwa amefungiwa katika mlango wa Baytul-Maqdis, akisubiri Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akirejea kutoka mbinguni ili ampeleke Makkah.”





Baada ya ziara ya Masjid Al Al-Aqswaa, Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walianza safari ya kwenda mbinguni. Kila alipofika kwenye mbingu alibisha hodi na aliulizwa na walinzi wa mbingu hiyo, “Wewe nani?” na alipojibu kuwa ni “Jibriyl!” aliuliulizwa tena, “Nani umefuatana naye?” Alisema “Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)” Na aliulizwa tena, “Je ameitwa?” Na Jibriyl alijibu: “Naam, hakika ameitwa!” Na ndipo Malaika walisema: “Marhaba, anakaribishwa, safari yake ni njema kabisa.” Milango ilifunguliwa na wakamwona Aadam (‘Alayhis-Salaam). Jibriyl alisema akimwambia Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Huyu ni baba yako Aadam (‘Alayhis-Salaam). Mpe heshima zake kwa salaam.” Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimsalimu na Aadam aliitikia na akasema: “Unakaribishwa ee mwanangu Nabiy Mtukufu.” na akamwombea du’aa njema.



Kisha walipanda mbingu ya pili na sawa kama hapo awali Jibriyl alibisha hodi na kuwaomba walinzi kufungua milango ya mbingu na wakamuuliza maswali kama yale aliyoulizwa hapo mbingu ya kwanza. Hali ya namna hiyo iliendelea hadi kufika mbingu ya saba. Hatima milango ilifunguliwa na wakawa wamekaribishwa kwa kauli ya “Marhaba, anakaribishwa, safari yake ni njema kabisa.”



Katika mbingu ya pili Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimuona ‘Iysaa bin Maryam (‘Alayhimas-Salaam) na Yahyaa bin Zakariyyaa (‘Alayhimas-Salaam) mtu na binamu yake. Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: “Nilikutana na ‘Iysaa bin Maryam. Alikuwa na umbo la wastani na uso wake ni mwekundu kama vile katoka kuoga…” [Swahiyh Al-Bukhaariy Juzuu 4 Namba 647]





Jibriyl alisema: “Hawa ni Yahyaa bin Zakariyyaa na ‘Iysaa (‘Alayhimus Salaam) wasalimu.” Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwasalimu na wote wawili walijibu salamu zake na kusema: “Unakaribishwa Ee ndugu yetu Nabiy Mtukufu.” Na kisha wakamwombea dua njema.





Baada ya hapo walipanda mbingu ya tatu ambako walimkuta Yuwsuf (‘Alayhis-Salaam) ambaye amejaliwa uzuri wa sura wa nusu ya dunia. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimsalimu naye akajibu salamu hiyo na akamkaribisha na akaondoka nao wakaenda mbingu ya nne pamoja. Milango ya mbingu ya nne ilifunguliwa na Idriys (‘Alayhis-Salaam) alikuwa hapo. Qur-aan inasema juu yake:



وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِدْرِيسَ ۚ إِنَّهُ كَانَ صِدِّيقًا نَّبِيًّا ﴿٥٦﴾

Na mtaje katika Kitabu Idriys. Hakika yeye alikuwa mkweli wa dhati na Nabiy. [Maryam 19: 56-57].





Idriys (‘Alayhis-Salaam) alimkaribisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na wakasalimiana. Kisha Idriys (‘Alayhis-Salaam) aliondoka nao wakaenda mbingu ya tano ambako walimkuta Haaruwn (‘Alayhis-Salaam). Nabiy Haaruwn (‘Alayhis-Salaam) aliwapokea na akajibu salamu zao na kumwombea dua njema Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).



Kisha Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipelekwa mbingu ya sita ambako alimkuta Muwsaa (‘Alayhis-Salaam). Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Nilikutana na Muwsaa (‘Alayhis-Salaam) nilipokwenda Mi’raaj. Alikuwa ni mtu mrefu akiwa na nywele ndefu kama vile ni mtu wa kabila la Shamu. [Swahiyh Al-Bukhaariy, Juzuu 4 Namba 647].





Muwsaa (‘Alayhis-Salaam) alimkaribisha Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Jibriyl (‘Alayhis-Salaam), na wakasalimiana na walipoondoka kuendelea na safari yao, Muwsaa (‘Alayhis-Salaam) alilia. Aliulizwa kwa nini analia basi Muwsaa (‘Alayhis-Salaam) alijibu: “Nalia kwa sababu amepelekwa Nabiy duniani baada yangu, kijana ambaye wafuasi wake wataingia Peponi kwa makundi makundi zaidi ya watu wangu.”



Kisha waliendelea na safari yao kuelekea mbingu ya saba na huko wakamkuta Ibarahiym (‘Alayhis-Salaam) akiwa ameegemea Baytul-Ma’amuwr (Nyumba ambayo inatembelewa mara kwa mara). Ndani ya nyumba hii kila siku wanaingia Malaika 70,000 na wala hawarudi tena … na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: “Nilimwona Ibraahiym (‘Alayhis-Salaam) ambaye mimi nafanana naye sana kuliko watoto wake wote.” [Swahiyh Al-Bukhaariy, Juzuu 4 Namba 647].





Ibraahiym alimkaribisha Muhammad na wakasalimiana na Ibraahiym (‘Alayhis-Salaam) akamwombea dua njema Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). [Swahiyh Al-Bukhaariy, Juzuu 5 Namba 227 na Swahiyh Muslim]





Ameeleza ‘Abdullaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: “Ndani ya usiku wa Mi’raaj nilikutana na Ibraahiym (‘Alayhis-Salaam) ambaye aliniambia, “Muhammad wapelekee Salaam zangu watu wako na waambie kuwa Jannah ni uwanda mpana ambao umeenea udongo safi, maji safi na miti yake hutoa sauti; “Subhaana Allaah, AlhamduliLLaah, laa ilaha illa Allaah, Allaahu Akbar.” [At-Tirmidhiy namba 1445]





Kituo Cha Mwisho Cha Safari - Sidratul-Muntahaa





Amesema ‘Abdullaah bin Mas’uwd, “Wakati Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipochukuliwa safari yake kwenda mbinguni alifikishwa mpaka Sidratul-Muntahaa ambapo kila kitu kinachopanda kutoka ardhini hukomea na na kile kinachoshuka kutoka juu hukomea hapo…” [Muslim 329].



Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Kisha nilichukuliwa hadi Sidratul-Muntahaa mti ambao majani yake ni kama masikio ya tembo na matunda yake makubwa kama mitungi. Na mti huu ulipogubikwa na amri za Allaah, basi ulibadilika kuwa katika hali ambayo hakuna kiumbe ambaye anaweza kumsabihi Allaah kwa uzuri wake.” [Muslim].



Kisha katika riwaayah nyingine: “Kisha nilipandishwa mbinguni hadi kufikia Sidratul-Muntahaa. Matunda yake yalikuwa makubwa kama magudulia ya Hajr (sehemu ambayo ni karibu na Madiynah) na majani yake yalikuwa makubwa kama masikio ya tembo. Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) akasema: “Huu ni mkunazi wa mbali kabisa.” Kulikuwa na mito minne karibu yake miwili ikiwa haionekani na miwili ikiwa wazi inaonekana. Nikauliza: “Hii mito miwili ni mito gani ee Jibriyl?” Basi akajibu: “Ama kwa mito miwili isiyoonekana ni mito miwili ya Peponi na mito miwili inayoonekana ni mto wa Naili (Nile) na Furati (Euphrates).”





Hii hadiyth haina maana kuwa mito hiyo miwili inayoonekana kuwa asili yake ni Peponi, lakini ni kuonyesha tu mahali ambapo atakuwepo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na watu daima watabakia wenye kushikamana na Uislamu na kurithishana kizazi kimoja baada ya kingine. [Ar-Rahiyq Al- Makhtuwm].





Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pia alisema: “Jibriyl alinipandisha mbinguni hadi tukafika Sidratul-Muntahaa (mkunazi ambao una mpaka wa mwisho) ambao ulikuwa umepamba kwa rangi ambazo haziwezi kuelezeka. Kisha niliruhusiwa kuingia Peponi ambamo nilikuta mahema (madogo madogo) au kuta ambazo zimejengwa kwa lulu na ardhi yake ilikuwa ni ya miski.” [Al-Bukhaariy, Juzuu 1 Namba 345].





Wakati nilikuwa natembea humo Peponi (katika usiku wa Mi’raaj) niliona mto na katika kingo zake kulikuwa na vijihema ambavyo vimejengwa kwa kutumia lulu zenye uwazi katikati. Niliuliza: “Nini kile ee Jibriyl?” Akasema: “Huo ndio mto wa Al-Kawthar ambao Rabb wako Amekupa wewe.” Basi harufu iliyotoka humo au kwenye matope ilikuwa ni miski. (Mmoja wa wapokeaji wa riwaya hii, Hudba hana hakina ilikuwa imetumika ibara gani). [Swahiyh Al-Bukhaariy, Juzuu 8 Namba 583].





“Katika usiku wa Mi’raaj huko mbinguni pia nilimwona Maalik (Malaika) mlinzi wa Milango ya Motoni na Ad-Dajjaal; ni miongoni mwa miujiza ambayo Allaah Alinionesha huko.”



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kisha akasoma:



وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ فَلَا تَكُن فِي مِرْيَةٍ مِّن لِّقَائِهِ

Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Kitabu, basi usiwe na shaka katika kukutana naye. [As-Sajdah 32: 23)]



Hivyo usiwe na mashaka juu ya kukutana na Muwsaa (‘Alayhis-Salaam) huko mbinguni katika usiku wa Mi’raaj. [Al-Bukhaariy, Juzuu 4 Namba 462].





Na kwa riwaayah nyingine Anas bin Maalik amesema, “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema, “Katika usiku wa Mi’raaj nilipopandishwa kupelekwa mbinguni nilipita karibu na watu ambao walikuwa wana makucha ya shaba na walikuwa wakijiparura nyuso zao na vifua vyao. Nilisema: Hawa ni nani ee Jibriyl?” Alijibu na kusema kuwa: “Hawa ni wale watu waliokuwa na tabia ya kusengenya na kuwazulia watu maneno machafu na kuharibu heshima za watu.” [Sunan Abiy Daawuwd, namba 4860].





Na katika riwaayah nyingine: Abuu Hurayrah anasema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: “Katika usiku wa Mi’raaj nilipopelekwa mbinguni niliona watu ambao matumbo yao yalikuwa makubwa kama nyumba na ndani yake kuna majoka ambayo yalionekana nje ya matumbo yao. Niliuliza kuwa walikuwa kina nani, na Jibriyl alinijibu kuwa wao walikuwa wale watu waliokuwa wakila mali ya riba.” [Musnad Ahmad, Ibn Maajah na At-Tirmidhiy namba 2828].





Kasema Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu): “Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, “Usiku wa Mi’raaj nilipopelekwa mbinguni niliwakuta watu na midomo yao ikichanwa na mikasi ya moto. Nikamuliza Jibriyl ni nani hao na akasema walikuwa ni wahubiri miongoni mwa wafuasi wangu, ambao walisema ambayo wao hawakuyafanya.” [At-Tirmidhiy (ghariyb) Namba 4801].





Buraydah bin Al-Haasib (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alieleza jinsi siku moja asubuhi Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyomwita Bilaal na kusema: “Umefanya nini mpaka ukaingia Peponi kabla yangu? Sikupata kuingia Peponi pasina kusikia mchakacho wako ukiwa mbele yangu.” Bilaal akajibu: “Sijapata kuadhini ila baada yake kuswali rakaa mbili. Na sijapata kutenguka wudhuu ila nilitawadha papo hapo na kujiona kuwa nina deni kwa Allaah la rakaa mbili.” Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Ni kwa sababu hizo.” [At-Tirmidhiy namba 326].





Na Jaabir bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alisema: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema, “Nilijiona naingia Peponi na mara nikamwona bi Ar-Rumayswah, mke wa Abuu Twalhah. Nilisikia hatua za mtu. Nikauliza: “Wewe nani?” Mtu mmoja akajibu: “Ni Bilaal.” Kisha nikaona kasri na mwanamke akiwa amekaa katika ukumbi wake. Nikauliza: “Kasri la nani hili?” Basi kuna mtu alijibu: “Hilo ni la ‘Umar.” Nikatamani kuingia ili nione ndani kukoje, lakini nilikumbuka jinsi ‘Umar alivyo na wivu (ghiyrah) basi sikuingia.” Mara ‘Umar akadakiza “Fidaka Abiy wa Umiy, Yaa Rasula-Allaah! Nitathubutu namna gani mimi kudhania kuwa umenikosea wewe kwa kuingia kwangu?” [Al-Bukhaariy, Juzuu 5 Namba 28].





Kutokana na Hadiyth hizi tunaona jinsi Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyokuwa mtu mwenye kulea watu wake na kuwafundisha mambo kwa hekima. Alipowafundisha tabia njema haikuishia bali yeye aliyafanya hayo kwa mifano ya wazi wazi kabisa. Alipata kusema: “Kama mtu atachungulia katika nyumba ya mtu bila rukhsa ya mwenyewe na huyo mwenye nyumba akachokora jicho lake, kutakuwa hakuna tatizo wala hilo jicho halitalipwa fidia”. [Sunan Abiy Daawuwd, namba 5153].





Kwa sababu yule anayechungulia katika nyumba za watu amefanya wizi kwa kuingilia siri za watu na hifadhi zao na hivyo Allaah Ametoa hukumu kali kwa kosa wizi.



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, “Mkono wa mwizi unapaswa kukatwa hata kama kwa wizi wa robo dinar.” [Al-Bukhaariy, Juzuu 8 Namba 781].







Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Anakutana Na Allaah - Je, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alipata Kumuona Rabb Wake?





Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّىٰ ﴿٨﴾

Kisha akakurubia na akashuka.



فَكَانَ قَابَ قَوْسَيْنِ أَوْ أَدْنَىٰ ﴿٩﴾

Kisha akawa kiasi cha umbali wa mipinde miwili au karibu zaidi.



فَأَوْحَىٰ إِلَىٰ عَبْدِهِ مَا أَوْحَىٰ ﴿١٠﴾

(Allaah) Akamfunulia Wahy mja Wake yale Aliyomfunulia Wahy.





مَا كَذَبَ الْفُؤَادُ مَا رَأَىٰ ﴿١١﴾

Moyo haukukadhibisha yale aliyoyaona.



أَفَتُمَارُونَهُ عَلَىٰ مَا يَرَىٰ ﴿١٢﴾

Je, mnambishia kuhusu yale aliyoyaona?



وَلَقَدْ رَآهُ نَزْلَةً أُخْرَىٰ ﴿١٣﴾

Na kwa yakini amemuona (Jibriyl) katika uteremko mwingine.



عِندَ سِدْرَةِ الْمُنتَهَىٰ ﴿١٤﴾

Kwenye mkunazi wa mpaka wa mwisho kabisa.



عِندَهَا جَنَّةُ الْمَأْوَىٰ ﴿١٥﴾

Karibu yake kuna Jannah ya Al-Ma-waa.



إِذْ يَغْشَى السِّدْرَةَ مَا يَغْشَىٰ ﴿١٦﴾

Ulipoufunika mkunazi huo unachokifunika



مَا زَاغَ الْبَصَرُ وَمَا طَغَىٰ ﴿١٧﴾

Jicho lake halikukengeuka wala halikupinduka mipaka.



لَقَدْ رَأَىٰ مِنْ آيَاتِ رَبِّهِ الْكُبْرَىٰ ﴿١٨﴾

Kwa yakini aliona miongoni mwa Aayaat (ishara, dalili) za Rabb wake kubwa kabisa. [An-Najm (53: 8-18)]







Waislamu wa mwanzo walitofautiana juu ya swala la Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kama alimuona Rabb wake kwa jicho lake au hapana.





Mama wa Waumini ‘Aaishah, Abuu Hurayrah na Ibn Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhum) wanakataa kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuona Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa macho yake. Kuna riwaayah kupitia kwa Ibn Abiy Haatim kwamba Ibn Mas’uwd alieleza Aayah zilizotajwa hapo juu, kwamba, “Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimuona Jibriyl katika umbo lake halisi mara mbili. Na mara Jibriyl alipokuwa katika umbo lake halisi basi alifunika anga yote kwa mwili wake. Kwa mara ya pili Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipomwona katika umbo lake halisi ni wakati wa safari yao ya kwenda mbinguni. Na hiyo ndiyo maana ya maneno:

وَهُوَ بِالْأُفُقِ الْأَعْلَىٰ ﴿٧﴾

Naye yuko juu kabisa katika upeo wa macho. [An-Najm (53: 7)] [Tafsiyr Ibn Kathiyr].





Hivyo Aayah hii inaonyesha kuwa Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) alijongea na kuwa karibu na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). [Fat-hul-Baariy, ukurasa 263, 264 ya Juzuu 17].





Amesimulia Masruwq (Radhwiya Allaahu ‘anhu): “Nilimuuliza Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) “Ee mama wa Waumini, Je, Rasuli wa Allaah alipata kumwona Rabb wake? Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) akasema: “Hicho ulichokisema kinafanya mwili wangu kusisimka na nywele kujivuta. Jua kuwa iwapo mtu atakwambia kitu katika hivi vitatu vifuatavyo ni mwongo: “Mtu akikwambia kuwa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuona Rabb wake, ni mwongo huyo.” Kisha mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anha) akasoma:



لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ ﴿١٠٣﴾

Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yote; Naye ni Mwenye kudabiri mambo kwa ulatifu, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika [Al-An’aam (6: 103)]



وَمَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُكَلِّمَهُ اللَّـهُ إِلَّا وَحْيًا أَوْ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ أَوْ يُرْسِلَ رَسُولًا فَيُوحِيَ بِإِذْنِهِ مَا يَشَاءُ ۚ إِنَّهُ عَلِيٌّ حَكِيمٌ﴿٥١﴾

Na wala haikuwa kwa mtu yeyote kwamba Allaah Amsemeze isipokuwa kwa Wahy au kutoka nyuma ya kizuizi, au Hutuma Mjumbe, kisha Anamfunulia Wahy Ayatakayo kwa idhini Yake; hakika Yeye ni Mwenye ‘Uluwa, Ametukuka, Mwenye hikmah wa yote. [Ash-Shuwraa (42: 51)]





Jambo la pili kama mtu atakwambia nini kitatokea kesho, ni mwongo.” Kisha akasoma:



وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا ۖ

Na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho. [Luqmaan (31: 34)]



Na pia akaongezea jambo la tatu kwa kusema: “Yeyote atakayekuambia kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alificha baadhi ya Wahy alioletewa na Allaah kutangaza, ni mwongo na akasoma:



يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ وَاللَّـهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٦٧﴾

Ee Rasuli! Balighisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako. Na usipofanya, basi utakuwa hukubalighisha ujumbe Wake. Na Allaah Atakuhifadhi dhidi ya watu. Hakika Allaah Haongoi watu makafiri [Al-Maaidah (5: 67)]





Kisha Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) aliendelea kusema: “Lakini Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuona Jibriyl (Alayhis-Salaam) katika umbo lake halisi mara mbili.” [Al-Bukhaariy, Juzuu 6 Namba 378].



Kwa upande mwengine Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhuma) alisema kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuona Allaah, na akasema kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuona Rabb wake mara mbili. [Tafsiyr Ibn Kathiyr].



Al-Haafidhw Ibn Hajar alisema: “Maelezo ya Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhuma) yamekuja katika hali ya kutodhibitiwa (hayaelezi kama Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimuona Rabb wake kwa macho yake au vipi) wakati kauli za Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) na wenziwe zimedhibitiwa kwa kusema Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakumuona Allaah “Kwa macho yake”. Tunaweza kuunganisha kauli hizo mbili kwa kusema Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) alikataa muono “Kwa macho yake” na kauli ya Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhuma) kuwa ni kamuona kiroho.” [Fat-hul-Baariy, 8/608].





Pili, kauli hizo mbili, ya Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) na ya Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa), kwa njia nyingine kuwa kauli ya Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) alisema kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuona Rabb wake wakati akiwa katika usingizi, jambo ambalo ni ndoto ya kweli na isiyokuwa alimuona Siku ya Mi’raaj wakati kauli ya Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) inakataa kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakumuona Rabb wake wakati yeye akiwa macho, lakini kauli hiyo haikatazi kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuona Rabb wake akiwa usingizini. Alichokana hapa ni kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakumuona Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa macho yake meupe, akiwa macho.





Wale ambao wanao msimamo kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuona Rabb wake kwa macho yake meupe wanaleta Hadiyth Dhaifu. Hakuna Hadiyth Swahiyh ambayo inaeleza ya kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuona Rabb wake kwa macho yake akiwa macho. Wenye msimamo huo wanaleta Hadiyth ya At-Tirmidhiy ambayo Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) anasema kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuona Rabb wake. Ikrimah alimuuliza: “Vipi Aayah ambayo inasema:



لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ

Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yote. [Al-An’aam (6: 103)]



Alijibu: “Ni wakati tu Allaah amezungukwa na Nuru, lakini Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuona Rabb wake mara mbili. “Hadiyth hii ni dhaifu.”



Kwa hali hiyo kwa namna jinsi ilivyo hakuna mgongano wa kauli, na Allaah Anajua zaidi. [Sharh ya Uswuul Al-I’itiqaad cha Al-Laalika’iy, 93/512, As-Sunnah 1/181 na Swifat Al-Maqdisiy ukurasa 109-111].





Zawadi Ya Mi’raaj



‘Abdullaah bin Mas’uwd alisema, “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipewa vitu vitatu: alipewa Swalaah tano, alipewa Aayah mbili za kumalizia Suwrah ya Al-Baqarah na kusamehewa kwa madhambi ya wale watu ambao hawamshirikishi Allaah miongoni mwa ummah wake.” [Muslim Namba 329].





Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: “Allaah Alinipa ufunuo na Akasema kuwa Ummah wangu wanawajibika kuswali Swalaah khamsini (50) kila siku; usiku na mchana. Nilishuka kwenda kwenye mbingu ya Muwsaa (‘Alayhis-Salaam) akaniluza: “Lipi Rabb wako Amekupatia kwa ajili ya ummah wako?” Nikasema: “Swalaah Khamsini.” Akasema: “Rejea kwa Rabb wako na omba Akupunguzie katika idadi hiyo ya Swalaah, maana watu wako hawawezi kubeba mzigo huo mzito. Kama vile nilivyotiwa katika mtihani na wana wa Israaiyl na nikawajaribu nikawaona kuwa walikuwa dhaifu sana na hawawezi kubeba mzigo kama huo.” Hivyo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimgeukia Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) kama vile akitaka kupata ushauri wake juu ya hilo. Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) akasema: “Ndiyo, sawa, kama unataka hivyo.” Na wakarejea tena juu kwa Allaah.” [Al-Bukhaariy, Juzuu 9 Namba 608].





Kisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Nilirejea kwa Rabb wangu na kusema, “Ee Rabb wangu, Fanya vitu viwe vyepesi kwa ajili ya Ummah wangu. Allaah Alipunguza idadi ya Swalaah khamsini na kuwa tano kwa ajili yangu. Nilishuka chini nikaenda kwa Muwsaa (‘Alayhis-Salaam) ambaye alisema: “Hakika watu wako hawataweza kubeba mzigo huu mzito. Rejea kwa Rabb wako umwombe afanye wepesi wa hilo, Ee Muhammad! Mimi nilijaribu kuwalingania Ummah wangu wana Israaiyl ili wafanye kidogo zaidi ya hayo, lakini hawakuweza kuyafanya hayo bali waliishia kukata tamaa.” [Al-Bukhaariy, Juzuu 9 Namba 608].





Basi nikawa natangatanga kati ya mbingu ya Muwsaa na kwa Rabb wangu mwisho Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akasema: “Kuna Swalaah tano kila siku, usiku na mchana Ee Muhammad. Kila Swalaah imebeba uzito wa Swalaah kumi, na hivyo hizo ni khamsini vile vile. Mtu yeyote anayetia niyyah ya kufanya jambo zuri na asipolifanya basi atapata thawabu kwa hilo, na kama atalifanya hilo tendo, basi itaandikwa thawabu kumi kwa hilo. Wakati ambapo mtu aliyenuia kufanya uovu na akaacha kuufanya haitasajiliwa hiyo na kama atafanya uovu huo basi utasajiliwa uovu mmoja tu. Hapo nikashuka kwa Muwsaa (‘Alayhis-Salaam) na kumwambia hayo, Muwsaa akasema: “Nenda kwa Rabb wako ili afanye mambo yawe mepesi zaidi.” Juu ya kauli hiyo Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Nimekuwa nikienda kwa Rabb wangu mara kwa mara hadi naona aibu kusimama mbele yake. [Muslim].



Juu ya hilo Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) akasema: ”Kwa jina la Allaah! Shuka sasa!” Kisha Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaamka akiwa ndani ya Masjid Al-Haraam (Msikiti Mtukufu wa Makkah)” [Swahiyh Al-Bukhaariy, Juzuu 9 Namba 608]



Na pia ndani ya maelezo ya Al-Bukhaariy kuna maelezo zaidi kuwa: “…nilipoondoka nilisikia sauti: “Nimetoa amri Yangu na kisha nimewapunguzia uzito Waja Wangu.”





Utukufu Na Umihumu Wa Swalaah:



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ameitukuza Swalaah na kuipa daraja kubwa sana kwa kuifaradhisha katika usiku wa Mi’raaj. Amri zote zingine zililetwa na Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) ardhini kwa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Swalaah ilifaradhishwa baada ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuitwa kwenda mbinguni na mawasiliano yalikuwa ni moja kwa moja kutoka kwa Rabb hadi kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Aayah nyingi za Qur-aan na Hadiyth nyingi za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zinashuhudilia utukufu na umuhimu wa Swalaah.





Ibn Hajar anaandika katika sharh yake ya Al-Bukhaariy (1/460), “Hekima ya kufaradhishwa Swalaah wakati wa Mi’raaj ni kuwa hapo ndipo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipopata utukufu kamili kwa nje na ndani ya mwili wake. Alikoshwa kwa maji ya Zam Zam na kisha akanyunyuziwa na iymaan na hekima. Kwa kuwa Swalaah imetanguliwa na wudhuu, ilikuwa hasa mahali pake maamrisho ya Swalaah yaletwe akiwa katika hali hiyo yaani baada ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kutakaswa na kusafishwa.”



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

وَإِن تَعُدُّوا نِعْمَةَ اللَّـهِ لَا تُحْصُوهَا ۗ

Na mkihesabu neema za Allaah hamtoweza kuziorodhesha hesabuni. [An-Nahl (16: 18)]





Kupunguzwa kwa idadi ya Swalaah ni neema kutoka kwa Allaah na kisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

وَقَلِيلٌ مِّنْ عِبَادِيَ الشَّكُورُ ﴿١٣﴾

Na wachache miongoni mwa waja Wangu wenye kushukuru. [Sabaa (34: 13)]





Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



إِنَّ الْإِنسَانَ لِرَبِّهِ لَكَنُودٌ ﴿٦﴾

Hakika mwana Aadam kwa Rabb wake bila shaka ni mtovu wa shukurani. [Al-‘Aadiyaat (100: 6)].









Je, kuna neema gani tukufu ziaidi ya hii kuwa Swalaah ambazo zilikuwa ni khamsini zimepunguzwa na kuwa tano kwa siku, usiku na mchana na kisha malipo ya hizo Swalaah tano ni sawa na Swalaah khamsini zile za mwanzo?



Ibn Hibbaan anasema katika Swahiyh yake (1/133): “Kisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alifaradhishiwa Swalaah khamsini, amri hii ilikuwa ni mtihani mkubwa, mtihani ambao alitaka kumpima nao kipenzi Wake Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Wakati akimwambia kuwa Ummah wake wakaswali Swalaah khamsini alikuwa anajua fika kuwa wataswali Swalaah tano tu na amri ya kuswali Swalaah khamsini ilikuwa ni mtihani tu! Hii ni sawa na maneno yetu kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anaweza Akaamrisha kitu kwa mja Wake ambaye atapokea amri hiyo lakini si lazima aitekeleze kwa vitendo. Mfano mzuri wa hilo ni pale Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Alipomwamuru Ibraahiym (‘Alayhis-Salaam) kumchinja mwanae mpenzi. Utashi wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) wa amri hii ilikuwa ni kuwa Amri Yake ipokelewe na ikubaliwe kikamilifu. Na pindi wote mzazi na mtoto waliposalimu amri na kujisalimisha kwa Rabb wao, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Alitoa kafara ya mtoto huyo badala yake kwa kafara kubwa sana. Kama Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Angelikuwa Anataka yatekelezwe yale aliyoyaamuru basi Ibraahiym angelikuta mtoto wake kachinjwa kweli. Hali kadhalika kutoa amri ya kuswali Swalaah khamsini kwa kila siku ilikuwa ni amri ya kukubaliwa lakini kitu kingine ambacho ni chepesi kwa matendo chenye uzito sawa sawa ndiyo kifanyike ambazo ni Swalaah tano.”





Yeyote anayedharau Swalaah, siyo kwamba kakataa nguzo ya Uislamu bali pia kakataa zawadi kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Swalaah ni nguzo ya kwanza katika mpangilio aliowekewa mwana Aadam na ndio ‘ibaadah ya kwanza kuulizwa mja siku ya Qiyaamah na pia ilikuwa ni amri ya mwisho ambayo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiitamka mpaka mwisho. Wakati Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa katika maradhi yake ya mwisho alikuwa akisema: “Swalaah, Swalaah na vile ambavyo mikono yenu ya kuume inavimiliki.” [Hadiyth Swahiyh imesahihishwa na Imaam Al-Albaaniy, Ibn Maajah na Musnad ya Ahmad].





Mtu anapokufa hasemi ila maneno yale ambayo anayaona kuwa ni ya muhimu sana kwake na anapendelea watu wachukue ushauri wake wa mwisho. Hivyo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alituamuru kwa maneno hayo ambayo aliyaona kuwa ni ya muhimu sana. “Tuchunge Swalaah.”



‘Abdullaah bin Qart alisema kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: “Tendo la kwanza ambalo mja atawajibika nalo siku ya Qiyaamah ni Swalaah. Kama Swalaah yake itakuwa ni nzuri basi matendo mengine yote yatakuwa ni mazuri. Na kama Swalaah itakuwa ni mbaya basi matendo mengine nayo yatakuwa ni mabovu.” [At-Twabaraaniy].



Alisema Abuu Buraydah bn Al-Haasib: “Rasuli wa Allaah amesema: “Kitu ambacho kinatutofautisha Waumini na makafiri na wanafiki ni jinsi tulivyo karibu na Swalaah. Mtu asiyeswali anaangukia katika kundi la makafiri.” [At-Tirmidhiy Namba 1083]



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema kuwa watu wa motoni watatupwa katika moto wa Jahannam na wataulizwa: Kitu gani kimekusababisheni kuingia katika moto wa Jahannam? Nao watajibu:



كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ رَهِينَةٌ﴿٣٨﴾

Kila nafsi iko katika rehani kwa yale iliyoyachuma.

إِلَّا أَصْحَابَ الْيَمِينِ﴿٣٩﴾

Isipokuwa watu wa kuliani.

فِي جَنَّاتٍ يَتَسَاءَلُونَ﴿٤٠﴾

Katika Jannaat wanaulizana.

عَنِ الْمُجْرِمِينَ﴿٤١﴾

Kuhusu wahalifu.

مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ﴿٤٢﴾

(Watawauliza): “Nini kilichokuingizeni katika motoni?”



قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ﴿٤٣﴾

Watasema: “Hatukuwa miongoni mwa wanaoswali. [Al-Mudathir (74 :38-43)].







Hivyo jambo la kwanza ambalo wataungama itakuwa: “Walikuwa wameacha Swalaah.”



Umuhimu wa Swalaah unaonekana katika Msikiti wa Qubaa. Msikiti huu ulijengwa wakati Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipohama kutoka Makkah kwenda Madiynah. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikaa sehemu za Qubaa siku nne kabla hajaingia mjini Madiynah, hakupanga kukaa Qubaa wala hakujenga chochote hapa. Kitu alichofanya hapa alijenga Msikiti wa Qubaa. Kitendo cha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kujenga Msikiti hapa Qubaa kinaonesha umuhimu wa Msikiti katika Uislamu. Hivyo basi Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipeleka kikundi cha Maswahaba kwenda kupigana Jihaad. Aliwaambia waahirishe vita hivyo, waache kila kitu wakisubiri adhana. Anasema Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu): “Daima mtu alipotoka nasi kwenda kupigana Jihaad dhidi ya watu wowote wale, hakuturuhusu kupigana hadi asubuhi na atasubiri kusikiliza kama kutatokea adhana. Akisikia adhana basi ataahirisha vita hivyo na kama hakusikia adhana basi aliamuru vita hivyo viendelee…” [Al-Bukhaariy, Juzuu 1 Namba 584].





Ndugu Waislam, tusome tukio hili kwa mazingatio makubwa kwa kuyafanyia kazi mafunzo yanayopatikana ndani yake, na si kwa kusherehekea, kufunga na kutenga siku maalum ya kula, kuswali Swalaah za aina fulani na du’aa za namna fulani, kugawa vyakula na kufanya mikusanyiko ya masimulizi ya kuburudisha kama ambavyo imekuwa ni ada kwa baadhi ya watu, hayo yote hayajathibiti wala kufanywa na wema waliopita. Tuige matendo ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na watangu wema na tutafanikiwa In Shaa Allaah.





Vitabu vya Rejea:



Tafsiyr ya Ibn Kathiyr

Swahiyh Al-Bukhaariy

Swahiyh Muslim

Sunan Abiy Daawuwd

Kitabu cha Siyrah Ar-Rahiyq Al-Makhtuwm

Mihadhara juu ya Mi’raaj ya Ihsaan Ilaahi Dhwahiyr.





Wa biLLaahi At-Atawfiyq
 
Siyrah Ya Nabiy


Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Hatetewi Kwa Dhulma Na Ujinga



Imefasiriwa Na: Abuu Suhayl



Alhidaaya.com









Himdi Anastahiki Allaah, Rahmah na amani zimuendee Rasuli wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na aali zake na Swahaba zake na Waislamu wote. Ama baada ya hayo.





Hakuna Muislamu ambaye anaweza kukubaliana na kutukanwa, kudhalilishwa, kudhauruliwa na kusingiziwa mambo mabaya Rasuli wetu mpendwa (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Imaamu wa Ahlus-Sunnah kama Imam Maalik, Al-Layth, Ahmad, na Ash-Shaafi’iy, wamekubaliana kwa pamoja kwamba yeyote atakayemvunjia heshima, kumtukana au kumdhalilisha au kumtia ila Rasuli wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) atakuwa amekufuru, na adhabu inayomstahili kwa yule anayeishi katika dola ya Kiislamu na akafanya hivyo ni kifo, adhabu ambayo itakuwa katika mikono ya mtawala wa Kiislamu.





Hapana shaka kwamba mashambulizi ya aina hii kwa Rasuli wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yatasababisha hasira na kukata matumbo ya kila Muislamu kutokana na mapenzi yao kwa Allaah, Rasuli wake na Dini yake. Lakini Muislamu aliye mkweli, muadilifu na muaminifu hawezi kuruhusu kuchukuliwa na hasira na jazba na kujibu mashambulizi haya kwa matendo ya kihuni ambayo yanakusanya matendo ambayo Allaah na Nabiy wake wameyakataza. Zaidi atakuwa kama katika matendo mengine na subra, kisha anayarejesha mambo hayo katika Qur-aan na Sunnah na ufahamu wa Swahaba na ‘Ulamaa walioshikana barabara na elimu. Hivyo Muislamu anakuwa na subira na anaithibitisha miguu yake kwa elimu na anajisalimisha kwa hukumu za Allaah na Rasuli wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) anasema:



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا ﴿٥٩﴾

Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Rasuli na wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli mkiwa mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri zaidi. [An-Nisaa : 59].





Al-Haafidhw Ibin Kathiyr ametaja kuwa maana ya



وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ



“wenye madaraka katika nyinyi.”



kwa mujibu wa Ibn ‘Abbaas, Mujaahid na ‘Atwaa na wengine katika Salaf, inakusudiwa “ ‘Ulamaa”. Na Ibn Kathiyr amesema inakusudiwa ’Ulamaa na watawala na hapa inakusudiwa ’Ulamaa wa Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah.





Ambacho kimetokea siku chache zilizopita katika ardhi za Waislamu na sehemu nyingine kama hatua za kupinga filamu inayoshambulia Uislamu na kumtukana Rasuli wetu mpendwa (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yanapingana na muongozo wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Tunatakiwa tukumbuke kuwa mashambulizi haya si mapya. Allaah Ametaja katika Qur-aan kuwa Rusuli Wake (‘Alayhim-salaam) walishambuliwa na kutukanwa, watu wao waliwaita vichaaa, wendawazimu na hata kuwaita wachawi. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



كَذَٰلِكَ مَا أَتَى الَّذِينَ مِن قَبْلِهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا قَالُوا سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ ﴿٥٢﴾

Ndio kama hivyo, hawakuwafikia wale wa kabla yao Rasuli yeyote isipokuwa walisema: Mchawi au majnuni. [Adh-Dhaariyaat : 52].





Na haya yametokea kwa Rusuli kuanzia Nuwh (‘Alayhis-salaam) mpaka kwa Nabiy wa mwisho Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).





Katika kipindi cha maisha ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuna ambao walikuwa wakimtusi na kumkashfu hadharani. Ka’ab bin Ashraf Al-Yahuwdiy aliyekuwa Madiynah alikuwa akiimba mashairi ya kumkashifu Nabiy na kuimba mashairi mabaya kuhusu wanawake wa Kiislamu. Na Makkah alikuwepo ‘Abdullaah bin Khatal ambaye alikuwa na waimbaji wawili wa kike ambao walikuwa wakiimba mashairi ya kumkejeli Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).





Aliporudi toka safari ya Makkah kuja Madiynah Ka’ab bin Al-Ashraf akaanza kuimba mashairi ya kumtukana. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwauliza Swahaba zake, ‘Nani atakayemdhibiti Ka’ab bin Al-Ashraf? Kwani amemdhuru Allaah na Rasuli Wake.’ Na hapa ni pale Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa katika dola yake na yeye alikuwa ndiye kiongozi na Al-Ka’abah alikuwa akiishi chini ya mamlaka yake hapo Madiynah. Lakini Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwaambia Swahaba zake kwenda kuwaadhibu majirani zake, rafiki zake au familia yake kwa yale aliyokuwa akifanya Al-Ka’abah bin Al-Ashraf. Wala hakuuadhibu ukoo wake wa Banu Nadhwiyr au kuwaadhibu Mayahudi wengine wa Madiynah.





Yeyote mwenye akili iliyosalimika hawezi kukubaliana na hili kwani halikubaliani na mantiki achilia mbali maandiko ya Kitabu na Sunnah.





Alichofanya kama mtawala Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuadhibu Al-Ka’abah ambaye ndiye aliyekuwa anafanya kosa hilo.





‘Abdullaah bin Khatal alikuwa Makkah na alikuwa na waimbaji wawili wa kike aliowafundisha kuimba nyimbo za kumkejeli na kumkashifu Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na wakati huo Nabiy alikuwa ni kiongozi na hakuwahi kamwe kuwashambulia makafiri wa Madiynah au miji au vijijiji vingine kama malipo ya matusi ya ‘Abdullaah bin Khatal kwake yeye. Pia hakuwaamrisha Swahaba zake kuishambulia Makkah au watu wa Makkah kwa sababu ya ‘Abdullaah bin Khatal.





Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na subira na hakuwakandamiza watu au kuchupa mipaka. Alikuwa na subira na alikuwa muadilifu. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipoiteka Makkah na jeshi lake, akaamrisha asidhuriwe yeyote ambaye hatopigana nao, isipokuwa kikundi kidogo cha watu ambao aliwataja kwa majina.





Hapa Nabiy alikuwa na nguvu, ameiteka Makkah na alikuwa na nguvu na miongoni mwa aliowataja ni ‘Abdullaah bin Khatal na waimbaji wake wawili wa kike. Hakuamrisha majirani zake wala familia yake kuadhibiwa. Hakuamrisha mali za ukoo wake kuharibiwa. Alichoamrisha ni kuuawa ‘Abdullaah bin Khatal na waimbaji wake wawili wa kike.





Hii ni mifano miwili tu ya jinsi Nabiy alivyofanya na watu waliomtukana akiwa hai. Alikuwa ni muadilifu na subira. Hakumkandamiza mtu wala kumdhulumu na hawa watu walimlaani, wakamtukana, wakamdhalilisha na kumkashifu akiwa hai (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).





Sasa matendo haya ya haya makundi na wajinga wengine walioathiriwa na hayo makundi wameyapata wapi kwa kutazama mwenendo wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)?





Mmeona wapi kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake walikwenda katika miji mingine na kuandamana, na kuua watu wasiokuwa na hatia, kuharibu mali zao kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyafanya Ibn al-Ashraf na Ibn Al-Khatal wakiwa Makkah na Madiynah?





Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na subira na uadilifu. Na uadilifu ni kukiweka kila kitu mahali pake. Na haya tunayayona toka kwa watu Misr, Yemen, Libya na nchi zingine katika mashariki ya kati ni ukandamizaji, dhulma na kuvunja Sunnah. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



ۚ فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٦٣﴾

Basi watahadhari wale wanaokhalifu amri yake, isije kuwasibu fitnah au ikawasibu adhabu iumizayo. [An-Nuwr : 63].





Kinachofafanua zaidi tofauti katika muongozo wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na wale Waislamu ambao wanachukuliwa na jazba na upotevu ni Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) ambayo imesimuliwa na [Al-Bukhaariy, Muslim, Ahmad] na wengineo, walipokuja kundi la Mayahudi kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia “As-Saamu ‘Alaykum” (kifo kiwe juu yako). ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anha) alielewa walichosema hivyo akawajibu “Wa ‘alaykum As-Saam wa la‘ana.” (Na kifo na laana ziwe juu yenu). Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema, “Taratibu ee ‘Aaishah, bila shaka Allaah Anapenda upole katika mambo yote.” ‘Aaishah akasema “Ee Rasuli wa Allaah! Hukuwasikia waliyoyasema?” Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema, “Nimeshawajibu (kwa kusema) “Wa ‘Alaykum.”Na juu yenu pia.” Na Dini yetu haiendi kwa hisia na jazba. Muislamu ambaye anampenda kiukweli Allaah na Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) atafuata muongozo na Sunnah zake.



قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣١﴾

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-‘Imraan : 31].





Tuzizingatie Nukta Zifuatazo:





-Maandamano haya ambayo yameenea katika ardhi za Waislamu na yameeingia mpaka Kuwait ni bida’a kama walivyosema wanachuoni wa Ahlus Sunnah Waljama’a kama Shaykh Ibn Baaz, Shaykh Al-Albaani, Shaykh Ibn ‘Uthaymini na walivyoyafafanua. Ni matendo ya kuwapinga na kupambana na viongozi wa Kiislamu na ni katika njia za Makhawaariji. Makundi ya kisiasa wanayaruhusu na kuyatetea kwani ni njia ya kupambana na watawala wa Kiislamu na ndio njia ya kuchukua madaraka.



Tumeona jinsi vijana waliojawa na hamasa walivyochukua hatua kuingia mitaani katika maandamano haya na kupambana na polisi na kusababisha uharibifu kwa mali na si mali za balozi - ambacho pia kitendo hichi ni ukandamizaji lakini mali za Waislamu pia!! Na hii ndio inaitwa kumlinda Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)? Haiwezekani kwa Muislamu kumtetea Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ukandamizaji wakati Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ametuamrisha kuwa waadilifu:



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ لِلَّـهِ شُهَدَاءَ بِالْقِسْطِ ۖ وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ عَلَىٰ أَلَّا تَعْدِلُوا ۚ اعْدِلُوا هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿٨﴾

Enyi walioamini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Allaah mkitoa ushahidi kwa uadilifu. Na wala chuki ya watu isikuchocheeni kutokufanya uadilifu. Fanyeni uadilifu; hivyo ni karibu zaidi na taqwa. Na mcheni Allaah; hakika Allaah ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika kwa yale myatendayo. [Al-Maaidah : 8].



Al-Haafidhw Ibn Kathir amesema: “Usiache chuki zako kwa watu zikufanye ukaacha kuwafanyia uadilifu. Fanya uadilifu kwa kila mtu akiwa ni rafiki au adui.”



Shaykh Wa Uislamu Ibn Taymiyyah Amesema:



“Kwani watu hawakutofautiana kuhusiana na ukweli kwamba mwisho wa dhulma ni mbaya na una madhara na mwisho wa uadilifu ni mzuri wenye kupendeza.” Kwa ajili hiyo pamesemwa: Allaah atalisaidia taifa ambalo linafanya uadilifu hata kama watakuwa ni makafiri na hatolisaidia taifa litakalokuwa linafanya dhulma hata kama taifa hilo litakuwa limeamini.” [Majmu’u Al-Fataawaa 28/63].



Jua kwamba kuwaadhibu watu wengine kwa makosa ya mtu mwingine sio uadilifu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



قُلْ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْغِي رَبًّا وَهُوَ رَبُّ كُلِّ شَيْءٍ ۚ وَلَا تَكْسِبُ كُلُّ نَفْسٍ إِلَّا عَلَيْهَا ۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُم مَّرْجِعُكُمْ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ﴿١٦٤﴾

Sema Je, nitake ghairi ya Allaah kuwa ni Rabb na hali Yeye ni Rabb wa kila kitu? Na wala nafsi yoyote haitochuma (khayr au shari) ila ni juu yake. Na wala habebi mbebaji, mzigo (wa dhambi) wa mwengine. Kisha kwa Rabb wenu ndio marejeo enu, Atakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkikhitilafiana nayo. [Al-‘An’aam : 164].





Makundi ya kisiasa wanatumia maandamano haya na matukio kama haya kama jukwaa na mimbari za kuenezea mashaka na hila zao kwa watu ili watu wawageuke watawala.





- Maandamano haya ambayo ’Ulamaa wamesema ni bid’ah yametumika kama ngao kujificha kwa wale walio katika Manhaj ya Khawaarij kuua wasio na hatia. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



“Yeyote katika Waislamu atakayeua mtu ambaye anaishi kwa mkataba au makubaliano (na Waislamu) hatoonja harufu ya Jannah japokuwa harufu ya Jannah inasikika umbali wa mwendo wa miaka 40.” [Al-Bukhaariy].



Na katika Hadiyth nyingine amesema:



“Mkataba wa amani kwa Waislamu ni mmoja, yeyote atakayeuvunja mkataba wa amani na usalama kwa Muislamu mwengine ni juu yake laana ya Allaah, Malaika na watu wote.”



Al-Haafidhw Ibn Hajr (Rahimahu Allaah) amefafanua:





“Maneno mkataba wa amani kwa Waislamu ni mmoja’ ina maana kuwa kumpa mtu uhakika wa usalama wa amani ni sahihi (unakuwa mkataba umefungika). Kama mmoja wao atampa mkataba wa amani kafiri ni haramu kwa yeyote yule kuuvunja.”





Makafiri wanaoishi na kufanya kazi katika nchi za Waislamu wamepewa mkataba wa amani kwa hiyo kuwashambulia ni kupambana na kuwapinga watawala wa Kiislamu na kitendo cha usaliti na dhulma.





Shaykh Twaariq As-Subay’i amesema kwamba kama Muislamu atampa amani asiyekuwa Muislamu, hata kama huyo Muislamu atakuwa ni mwanamme au mwanamke, muungwana au mtumwa, na hata akiwa amepewa amani kwa ishara tu au kama amepewa amani kwa makubaliano ya kibalozi au kwa kumpa viza kuingia katika nchi -mtu huyo atakuwa amepewa mkataba wa amani na usalama wa maisha yake. Ni haramu kwa Waislamu kumdhuru. Na Muislamu atakayemdhuru ataangukia katika laana za Allaah, na Malaika na watu wote.





- Ukitazama wanaoongoza maandamano haya utawakuta wote ni katika viongozi wa vyama vya kisiasa. Na ushahidi kuwa hakuna katika Wanachuoni wa Ahlus-Sunnah ambaye amejihusisha na haya maandamano yatosha kuwa dalili kwa mtu mwenye akili, kama ambavyo Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alivyotumia hoja kama hii dhidi ya Makhawaarij kwamba hakuna hata Swahaba mmoja aliye pamoja nao aliposema:



“Bila shaka nimekuja kwenu kutoka katika Swahaba wa Rasuli wa Allaah na hakuna hata Swahaba mmoja aliye pamoja nanyi.”



Tunaona Waislamu wakiandamana, wakipambana na polisi wakiharibu mali na mambo mengine mabaya zaidi ya yote hayo yanafanyika kwa jina la kumtetea Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kutokana na filamu iliyotengenezwa na mtu mmoja anayeishi Marekani. La kusataajabisha hakuna hata mmoja anayechukizwa na Misikiti yenye makaburi ndani ambapo asiyekuwa Allaah anaabudiwa kama Msikiti wa Badawi, Zaynab na Al-Husayn?! Dhambi kubwa kabisa mtu anayoweza kuifanya inafanyika katika ardhi za Waislamu na watu wanashambulia mali na haki za watu kwa kitu ambacho hawana mamlaka nacho au uwezo wa kufanya chochote kukizuia!



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا ﴿٤٨﴾

Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa; lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amezua dhambi kuu. [An-Nisaa : 48].





Kwa hiyo Waislamu hawa na makundi haya wanataka kumtetea Nabiy kwa kufanya dhulma na na uonevu - lakini uko wapi utetezi wa Allaah na Tawhiyd yake kutokana na shirk zinazofanywa na Waislamu katik ardhi ya Waislamu wenyewe!





Jua kwamba Allaah Ametuamrisha kuwa na subira na uvumilivu na Ametukataza kufanya dhulma na uonevu. Na hakuna uadilifu katika matendo tunayoyaona toka kwa kaka zetu na dada zetu wa Misr, Yemen, Tunisia, Morocco, Sudan na nchi nyingine ambapo haya yanatokea. Matendo haya ni matendo ya ujinga, dhulma, upotevu na kuiacha Sunnah ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).





Aliyetengeneza filamu hii chafu anaishi Marekani na Marekani ni nchi ambayo ina kanuni zake inazotumia kutawala raia wake. Jambo hili halipo katika mikono ya sisi watu wa kawaida na hatuna uwezo wa kufanya lolote kulihusu. Jambo muhimu kwetu na subira na kushikamana na Sunnah za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na hii ni njia bora zaidi ya kumtetea Nabiy zaidi ya haya tunayoyaona yakifanywa na makundi haya na wafuasi wao.





Na ni muhimu kuzingatia kuwa subira yetu na uvumilivu wetu na kushikamana kwetu na Sunnah wakati wa hali kama hizi wakati hatuna uwezo wa kuzikabili si alama ya udhalili au unyonge. Makundi yaliyopotea ndiyo yamewaingiza vijana katika fikra hizi kuwa ukikosa uwezo wa kuchukua hatua ni sawa na kutochukua hatua, huu ni usaliti na upotevu.





Ibn Mas’uwd amesimulia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali katika Ka’abah na alipokuwa akisujudu mmoja kati ya wafuasi wa Abu Jahl alimuwekea matumbo ya ngamia mgongoni kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati Ibn Mas’uwd akiwa anamtazama. Ibn Mas’uwd amesema: “Nilikuwa natazama lakini sikuwa na cha kufanya. Laiti ningekuwa na nguvu na uwezo (wa kumzuia).” [Al-Bukhaariy].





Hili linatuonyesha kwamba wakati hatuna uwezo kutokana na kuwa na miili dhaifu, au kukosa uwezo au kuna kitu kinakuzuia hakuna aibu kwa hilo, kama ambavyo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyoshindwa kuwasaidia Yaasir, ‘Ammaar na mama yake ‘Ammaar (Radhwiya Allaahu ‘anhum) alipowaona wakiteswa kwa sababu ya kumuamini Allaah. Hivyo akawaambia: “Fanyeni subra enyi watu wa nyumba ya Yaasir, kwani mmeahidiwa Jannah.” [Al-Mastadrak Al-Haakim (3/383), Al-Hilyah (1/140), na vingine. Tazama vilevile Swahiyh Siyrat An-Nabawiyyah cha Shaykh Al-Albaanee (uk. 154-155)].





Haya tumayoyaandika hapa si kwa ajili ya kuitetea filamu hiyo. Hiyo filamu nasi tunaiona kuwa ni matusi yenye kuudhi kama watu wengine. Lakini tunafanya hivi kama njia ya kumtetea Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Dini yetu dhidi ya wale wenye kuchupa mipaka, na wale wanaocheza na hisia za Waislamu na vijana na kuwaita katika njia za upotevu. Huu ni wito wa kuwa na subra na kuwa na uadilifu na kushikama na Sunnah za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na haya ndiyo yaliyokuwa yanahitajika kuelezewa na kufafanuliwa. Allaah ni mjuzi zaidi.





Rahmah na amani zimuendee Rasuli wetu Muhammad na aali zake na Swahaba zake wote. Na shukrani njema zinamstahili Allaah.
 
Siyrah Ya Nabiy


Vita Vya Badr



Imekusanywa Na Muhammad Faraj Saalim As-Sa’iy (Rahimahu Allaah)



Alhidaaya.com





Badr ni jina la mji ulio kiasi cha kilomita mia na hamsini mbali na mji wa Madiynah, na mahali hapo hapakuwa na chochote isipokuwa bonde tu na kisima kilichokuwa milki ya mtu mmoja aitwae Badr, na kwa ajili hiyo mahala hapo pakaitwa ‘Badr’. Kwa vile vita hivyo vilipiganwa mahali hapo, ndiyo maana vikaitwa vita vya Badr.



Vita hivyo vilitokea asubuhi ya siku ya Ijumaa, Ramadhwaan ya kumi na saba mwaka wa pili baada ya Hijrah (baada ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhamia Madiynah).





Sababu Za Vita



Chanzo cha vita hivi kilikuwa ni msafara wa biashara wa makafiri ukiongozwa na Abu Sufyan uliokuwa ukitoka nchi ya Sham ukirudi Makkah ukiwa na watu wasiozidi arobaini. Msafara huu ulikuwa umebeba mali nyingi sana ya watu wa Makkah, na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaona hii ni fursa nzuri ya kuipiga dola hiyo ya kikafiri kiuchumi, kijeshi na kisiasa, na pia kulipiza kisasi. Hasa kwa vile Waislam walipohama Makkah kwenda Madiynah, Makafiri waliwalazimisha kuziacha mali zao zote huko, na kuondoka bila chochote isipokuwa nguo zao na mnyama wa kumpanda. Bali wengine walinyang’anywa hata wanyama wao, na ikawabidi kutembea kwa miguu mpaka Madiynah na wengine waliviziwa njiani na kuuliwa.



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawaambia Waislam:



“Msafara huu wa ma-Quraysh umejaa mali zao, uendeeni, huenda Allaah akatulipa (haki zetu walizotunyang’anya) kwa kutuwezesha kuuteka.”





Nguvu Za Jeshi La Waislam



Si watu wengi waliojitolea kwenda, na hii ni kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakutilia mkazo sana kutoka huko. Hakumlazimisha mtu kwenda naye na wala hakumlaumu yeyote yule asiyetoka pamoja naye. Bali alimwacha kila mmoja ajiamulie mwenyewe ikiwa anataka kwenda au hataki. Na kwa ajili hiyo Swahaba wachache tu walimfuata.



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaondoka akiwa na watu wapatao mia tatu na kidogo tu hivi. Inasemekana walikuwa mia tatu na kumi na tatu au kumi na nne na riwaya nyengine zinasema kuwa walikuwa mia tatu na kumi na saba. Themanini na sita kati yao ni Muhajiriyn (watu wa Makkah waliohamia Madiynah) na mia mbili thelathini na moja ni watu wa pale pale Madiynah.



Swahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhu) hawakujuwa kuwa msafara huu utakuja geuka kuwa ni moja katika mapambano makubwa baina ya Haki na Baatwil. Walidhania kuwa yatakuwa yale mapambano ya kawaida baina ya makundi ya wapiganaji wa Kiislam na misafara midogo midogo ya makafiri. Hawakujua kuwa Allaah amekwisha panga atimize jambo lililokuwa lazima litendeke.



Waliondoka wakiwa na farasi wawili tu, mmoja wa Zubair bin Awaam na mwengine wa Mikidaad bin Al-Aswad Al-Kindy (Radhwiya Allaahu ‘anhu). Walikuwa pia na ngamia sabiini wakipokezana katika kuwapanda.





Jeshi La Waislam Linaondoka Kuelekea Badr



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaondoka Madiynah pamoja na Swahaba zake hao (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuufuatia msafara huo wa Abu Sufyan. Akamchaguwa Ibni Ummi Makhtuum (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa ni mkuu wa Madiynah badala yake, lakini alipofika nje kidogo ya Madiynah, mahali panapoitwa Ar-Rawha, akamrudisha Swahaba mmoja anayeitwa Aba Lubaba (Radhwiya Allaahu ‘anhu), na kumtaka yeye awe khalifa wake pale Madiynah badala ya Ibni Ummi Makhtuum (Radhwiya Allaahu ‘anhu).



Katika msafara huo, Nabiya (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamchagua Mas-‘ab bin ‘Umair (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa ni mshika bendera, na bendera yenyewe ilikuwa ya rangi nyeupe.



Akaligawa jeshi makundi mawili:



1. Kikosi cha Muhajiriyn (watu wa Makkah) na akampa bendera yao ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu).

2. Kikosi cha watu wa Madiynah, na akampa bendera yao Sa’ad bin Mu’aadh (Radhwiya Allaahu ‘anhu).



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaondoka na jeshi lake hilo akiifuata njia ya Makkah, na alipofika mji uanoitwa Ar-Rawha akapumzika, na baada ya kupumzika mahala hapo akaondoka kuelekea mji wa Badr akiiacha njia ya Makkah kushotoni kwake na kuendelea na safari yake mpaka akalifikia bonde la Rahiyqan na baada ya kuendelea mbele kidogo, akawatuma Swahaba Basis bin ‘Umar na Uday bin Azzaghaabah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) watangulie na kupeleleza habari za msafara waliokusudia kuuteka.





Msafara Wa Abu Sufyan



Ama Abu Sufyan aliyekuwa kiongozi wa msafara wa biashara ya makafiri wa Makkah, alikuwa ni mtu mwenye kuchukua hadhari sana, alijuwa kuwa njia ya Makkah ina hatari nyingi, na kwa ajili hiyo, kila mara alikuwa akitanguliza wapelelezi ili wamletee habari za mbele ya safari, wakati huo huo alikuwa akimuuliza kila anayekutana naye, iwapo huko alikotoka ameona chochote kile kisichokuwa cha kawaida.



Katika kuuliza uliza kwake akamuuliza mtu mmoja anayeitwa Majdi bin ‘Amru iwapo ameona jeshi kutoka mji wa Madiynah, akasema:



“Mimi sikuona majeshi, lakini niliona kundi kubwa la watu waliopumzisha ngamia wao mahali hapa”.



Abu Sufyan akaenda kupafanyia uchunguzi mahali pale alipoambiwa kuwa watu walipumzisha ngamia wao. Baada ya kuchambua kinyesi cha ngamia waliopumzishwa mahali hapo na kuona kokwa za tende ndani yake, akasema:



“Madamu choo chao kimejaa kokwa za tende, hapana shaka yoyote kuwa hawa ni ngamia wa watu wa Madiynah”.



Alipotambua hayo, akajua kuwa anaviziwa, na hapo hapo akageuza njia yake na kumtuma mtu mmoja aitwae Dhamdham bin ‘Amru Al-Ghafaariy atangulie mbio sana. Aende kuwazindua watu wa Makkah juu ya hatari inayoukabili msafara wao wenye vitu vya thamani kubwa sana.



Watu wa Makkah waliposikia hayo, wakasema:



“Muhammad anadhania kuwa atauteka msafara huu kwa urahisi kama alivyouteka msafara wa ‘Amru bin Al-Hadhramiy?” (Kisa cha kutekwa kwa msafara wa ‘Amru nimekielezea katika makala ya ‘Miezi Mitukufu’).



Makafiri wakaendela kusema:



“Haitokuwa hivyo kabisa! Wa-Allaahi atakiona chake Muhammad safari hii”.





Jeshi La Makafiri Wa Makkah



Ma-Quraysh mara baada ya kujuulishwa juu ya hatari hiyo, wakakusanya jeshi la watu wapatao alfu moja na mia tatu, farasi wapatao mia moja na ngamia wengi sana. Wakaondoka hapo wakiongozwa na Abu Jahal bin Hishaam pamoja na vigogo vya ma-Quraysh.



Walisafiri kwa kasi kubwa sana kuelekea kaskazini mahali uliopo mji wa Badr. Walipoufikia mji uitwao Al-Juhufa, wakapata salamu kutoka kwa Abu Sufyan kuwa; msafara wake umekwishasalimika na hatari ya kutekwa, na akawataka warudi Makkah.



Kwa sababu mara Abu Sufyan alipotambua kuwa anafuatwa, akabadilisha njia na kupita njia ya pwani pwani badala ya kupitia njia ya mji wa Badr. Na kwa ajili hiyo akaokoka na kuwapelekea habari hizo wenzake.



Abu Jahal akasema:



“Wa-Allaahi haturudi, mpaka tufike Badr, tukae hapo siku tatu, tuchinje wanyama wetu, tunywe pombe yetu na waimbaji waimbe mpaka habari zetu ziwafikie Waarabu wote ili wapate kutujuwa ni nani sisi na ili watuogope”.





Tatizo La Jeshi La Waislam



Waislam walipata habari za kuwaponyoka kwa msafara wa Abu Sufyan na wakati huo huo wakapata habari za jeshi kubwa la watu wa Makkah lililowakabili lililoazimia kwenda mji wa Badr, na kwa ajili hiyo wakaingia katika tatizo kubwa sana.



Baadhi yao wakaingiwa na hofu, na wengine wakatoa wazo la kurudi Madiynah, na hii ni kwa sababu walikuwa wachache, hawana silaha za kutosha na hawakutoka kivita. Lakini ikawabidi kulikabili tatizo hilo kwa ushujaa mkubwa kabisa kwani iwapo watakimbia kupambana na jeshi la makafiri na kuliacha litambe hapo Badr, mji ulio katika eneo la karibu na mji wa Madiynah, huko kutawapa nguvu na kichwa kikubwa makafiri na watapata moyo zaidi, jambo ambalo halitakuwa na mwisho mwema. Wakati huo huo haiba ya jeshi la Waislam itaondoka.



Mwanachuoni mkubwa Al-Mubaarak Fury anasema katika kitabu chake Ar-Rahiyqul Makhtuum:



“Jeshi la Waislam lingekuwa mfano wa mwili bila ya roho, na makafiri wangepata moyo wa kujaribu kuushambulia mji wao wa Madiynah bila ya hofu yoyote ile”.



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



كَمَا أَخْرَجَكَ رَبُّكَ مِن بَيْتِكَ بِالْحَقِّ وَإِنَّ فَرِيقًا مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ لَكَارِهُونَ﴿٥﴾يُجَادِلُونَكَ فِي الْحَقِّ بَعْدَ مَا تَبَيَّنَ كَأَنَّمَا يُسَاقُونَ إِلَى الْمَوْتِ وَهُمْ يَنظُرُونَ﴿٦﴾وَإِذْ يَعِدُكُمُ اللَّـهُ إِحْدَى الطَّائِفَتَيْنِ أَنَّهَا لَكُمْ وَتَوَدُّونَ أَنَّ غَيْرَ ذَاتِ الشَّوْكَةِ تَكُونُ لَكُمْ وَيُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُحِقَّ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ وَيَقْطَعَ دَابِرَ الْكَافِرِينَ﴿٧﴾لِيُحِقَّ الْحَقَّ وَيُبْطِلَ الْبَاطِلَ وَلَوْ كَرِهَ الْمُجْرِمُونَ﴿٨﴾



Kama Alivyokutoa Rabb wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kutoka nyumbani kwako kwa haki, na hakika kundi miongoni mwa Waumini linachukia. Wanajadiliana nawe katika haki baada ya kubainika, kama kwamba wanasukumwa katika mauti nao huku wanatazama. Na pindi Allaah Alipokuahidini moja kati ya makundi mawili (la msafara au la jeshi) kwamba ni lenu; nanyi mkatamani kwamba lisilo na silaha liwe lenu, na Allaah Anataka Athibitishe haki kwa maneno Yake, na Akate mizizi ya makafiri. Ili Athibitishe haki na Abatilishe ubatilifu japokuwa wakhalifu wamekirihika. [Al-Anfaal: 5-8]





Nabiy (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) Anashauriana Na Sahaba Zake (Radhwiya Allaahu ‘Anhum)



Kutokana na mabadiliko haya ya ghafla na ya hatari, ilimbidi Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aitishe mkutano wa mashauriano na wakuu wa jeshi la Waislam ili kuwajuulisha juu ya hali ya mambo ilivyo na kutaka ushauri wao.



Ama wale aliowashauri katika wakubwa wa jeshi lake, kwanza aliinuka Abu Bakr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akatoa hutoba nzuri ya kumuunga mkono Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) juu kulazimika kwao kupigana na makafiri. Kisha akainuka ‘Umar bin Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na kutoa hotuba nzuri vile vile. Kisha akainuka Al-Mikdaad bin ‘Amru (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akasema:



“Ee Rasuli wa Allaah, nenda kama atakavyokuonyesha Allaah, na sisi tuko nyuma yako. Wa-Allaahi hatukuambii kama walivyomuambia wana wa Israili Nabiy wao Muwsaa:


فَاذْهَبْ أَنتَ وَرَبُّكَ فَقَاتِلَا إِنَّا هَاهُنَا قَاعِدُونَ ﴿٢٤﴾

Basi nenda wewe na Rabb wako mkapigane, hakika sisi tunakaa hapa hapa. [Al-Maaidah: 24]



Bali tunakwambia: “Nenda wewe na Rabb wako ukapigane na sisi pamoja nanyi tutapigana ” Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Vyema” Kisha akamuombea du’ah.



Hawa watatu wote walikuwa katika Muhajiriyn (Watu wa Makkah), ambao ni wachache katika jeshi hilo, na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akapenda kujua rai ya viongozi wa watu wa Madiynah waliokuwa wengi katika jeshi hilo, akasema: “Nipeni shauri lenu enyi watu”.



Akikusudia watu wa Madiynah. Sa’ad bin Mu’aadh (Radhwiya Allaahu ‘anhu) aliyekuwa mmoja wa viongozi wa watu wa Madiynah akatambua hayo, akasema: “Wa-Allaahi kama kwamba unatukusudia sisi ee Rasuli wa Allaah?”Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Ndiyo” Sa’ad (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akasema:



“Sisi tumekuamini na kukusadiki, na tukashuhudia kuwa uliyokuja nayo ndiyo haki, na tukakupa ahadi zetu na neno letu kuwa tutakusikiliza na kukutii, kwa hivyo endelea tu kama unavyotaka kwani Wa-Allaahi kama utatutaka tuivuke bahari hii, ukaivuka, basi tutaivuka pamoja nawe na hapana hata mmoja kati yetu atakayebaki nyuma, sisi hatuogopi kupambana na adui kesho, sisi ni watu wenye kusubiri katika vita na wakweli katika mapambano na In Sha Allaah Allaah atakuonyesha ndani yetu yale yatakayokufurahisha macho yako, kwa hivyo tuongoze kwa baraka za Allaah”.



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akafurahishwa sana na maneno ya Sa’ad (Radhwiya Allaahu ‘anhu), akasema:



“Nendeni na nakupeni bishara njema, Allaah ameniahidi moja wapo ya makundi mawili. Wa-Allaahi kama kwamba ninaona wapi wataanguka kila mmoja kati ya maadui.”





Majeshi Ya Kiislam Yanafanya Upelelezi



Walipowasili mahali panapoitwa Addiya, karibu na Badr, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na Sahibu yake wa pangoni Abu Bakr As-Swiddiyq (Radhwiya Allaahu ‘anhu), wakatoka na kuanza kufanya uchunguzi nje ya kambi yao, na katika kutembea kwao, wakakutana na mzee mmoja wa Kiarabu na kumuuliza juu ya habari za jeshi la ma-Quraysh na juu ya habari za jeshi la Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ili asiweze kutambua ni katika kundi gani wao.



Yule mtu akawaambia: “Kabla sijakujibuni, nambieni kwanza nyinyi mnatokea wapi?”

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia:

“Ukituambia na sisi tutakuambia…?”

Yule mtu akasema:

“Nimesikia kuwa jeshi la Muhammad na Sahibu zake lilitoka siku kadhaa wa kadhaa, ikiwa habari hizo ni sahihi, basi leo watakuwa washafika mahali kadhaa.”

Akapataja mahali lilipo jeshi la watu wa Madiynah.

“Na nimesikia kuwa ma-Quraysh wametoka siku kadhaa wa kadhaa, na ikiwa maneno niliyoambiwa ni kweli, basi leo watakuwa washafika mahali kadhaa wa kadhaa.”

Akapataja mahali lilipo jeshi la ma-Quraysh.

Baada ya kumaliza kusema, akawauliza:

“Nyinyi mnatokea wapi?”

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuambia:

“Sisi tunatokana na maji.”

Kisha akaondoka.

Yule mtu akawa anajiuliza:

“Hawa wanatoka katika maji ya Iraaq au maji gani?”



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakusema uongo, kwani viumbe vyote vinatokana na maji. Allaah anasema:

وَجَعَلْنَا مِنَ الْمَاءِ كُلَّ شَيْءٍ حَيٍّ



Na Tukajaalia kutokana na maji kila kitu kilicho hai. [Al-Anbiyaa: 30]





Waislam Wanapata Habari Muhimu Kuhusu Jeshi La Ma-Quraysh:



Mchana wake siku hiyo, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwatuma watu watatu kwenda kupeleleza juu ya habari za jeshi la ma-Quraysh, nao ni: ‘Aliy bin Abi Twaalib, Az-Zubayr bin ‘Awaam na Sa’ad bin Abi Waqaas (Radhwiya Allaahu ‘anhum). Walipokwenda penye kisima cha Badr wakawakuta watoto watatu wanachota maji kwa ajili ya kuwapelekea jeshi la ma-Quraysh, wakawateka na kwenda nao kambini ili kuwauliza masuali.



Walipofika nao kambini Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiswali, kwa hivyo wao wakaanza kuwauliza mateka wao.



Vijana hao wakasema kuwa wametumwa na ma-Quraysh ili kuwachotea maji. Swahaba walikasirishwa na jibu hilo, kwani walitamani wawe watu wa msafara wa Abu Sufyan. Wakawapiga sana mpaka wakasema kuwa wao ni watu wa Abu Sufyan na si watu wa jeshi la ma-Quraysh. Baada ya kutamka hayo, wakawaachilia.



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kumaliza kusali akawaambia:

“Waliposema kweli mliwapiga, na walipokudanganyeni mkawachilia. Walisema kweli Wa-Allaahi, kwani wao ni watu wa jeshi la ma-Quraysh”

Kisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawuliza wale vijana:

“Nipeni habari za ma-Quraysh.”

Wakasema:

“Wapo katika ng’ambo ya bonde lile la mbali”.

Akawauliza:

“Wako wangapi?”

Wakasema:

“Wengi”

Akawauliza:

“Idadi yao ngapi?”

Wakasema:

“Hatujuwi”

Akawauliza:

“Wanachinja wanyama wangapi kila siku?”

Wakasema:

“Siku nyingine wanachinja ngamia tisa na siku nyingine kumi”.

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema kuwaambia Swahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum):

“Idadi yao ni baina ya watu mia tisa na elfu.”

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawauliza tena wale vijana:

“Nani katika vigogo vya ma-Quraysh wamo miongoni mwao?”

Wakasema:

“Utbah na Shaiba watoto wa Rabia, Abu Al-Bakhtari bin Hishaam, Hakiym bin Hizaam, Naufil bin Khuwailid, Al-Haarith, Taimah, An-Nadhar bin Haarith, Zaamah bin Aswad, Abu Jahal bin Hishaam, na Umayyah bin Khalaf”.

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema kuwaambia Swahaba zake (Radhwiya Allaahu ‘anhum): “Makkah imekutupieni (imekuleteeni) vipande vya maini yao [vigogo vyao na vipenzi vyao].”





Kuteremka Kwa Mvua



Waislam wakasogea mbele kidogo mpaka wakakaribia bonde la karibu na mahali yalipopiga kambi majeshi ya ma-Quraysh.



Allaah aliwateremshia Waislam utulivu wakalala vizuri, hata wengine wakaota na kuamka wakiwa na janaba. Lakini mahali hapo hapakuwa na maji ya kuogea ili wapate kujitahirisha na wala ya kunywa, na Shaytwaan akaanza kuwatia wasi wasi: “Vipi mtapigana kesho wakati miili yenu haina tohara, vipi mtapigana kesho mkiwa na kiu…?”



Allaah akawateremshia mvua iliyowasaidia sana. Kwa sababu kutokana na mvua hiyo waliweza:



Kujitahirisha,
Kuondoa uchafu wa shetani, na
Kuzipa nguvu nyoyo zao.
Na maji ya mvua pia yakawasaidia kuufanya mchanga chini yao uwe mgumu ili waweze kutembea vizuri bila ya kuteleza wakati wa mapambano.



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



إِذْ يُغَشِّيكُمُ النُّعَاسَ أَمَنَةً مِّنْهُ وَيُنَزِّلُ عَلَيْكُم مِّنَ السَّمَاءِ مَاءً لِّيُطَهِّرَكُم بِهِ وَيُذْهِبَ عَنكُمْ رِجْزَ الشَّيْطَانِ وَلِيَرْبِطَ عَلَىٰ قُلُوبِكُمْ وَيُثَبِّتَ بِهِ الْأَقْدَامَ﴿١١﴾



Pindi Alipokufunikeni kwa usingizi kuwa ni amani kutoka Kwake, na Akakuteremshieni maji kutoka mbinguni, ili Akutwaharisheni kwayo, na Akuondosheeni wasiwasi na rai ovu za shaytwaan, na ili Atie nguvu nyoyo zenu, na Athibitishe kwayo miguu. [Al-Anfaal: 11]





Jeshi La Waislam Linatangulia Kukamata Sehemu Muhimu



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaliamrisha jeshi lake liondoke pale walipo haraka sana ili wawahi kusogea mbele karibu na mahali yalipo maji ya mji wa Badr. Wakasogea mpaka wakafika mwanzo wa visima vya maji ya Badr na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawaamrisha kupiga kambi hapo.



Mmoja katika Swahaba aitwaye Al-Khabaab bin Mundhir (Radhwiya Allaahu ‘anhu), akamuuliza Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



“Ee Rasuli wa Allaah, mahala hapa tuliposimama, Allaah amekuamrisha na hatuna haki ya kusonga mbele zaidi au ni katika hila za kivita tu na rai yako mwenyewe?”

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia:

“Bali ni hila za kivita na rai yangu mwenyewe.”

Akasema:

“Ee Rasuli wa Allaah, mimi naona kuwa hapa si makaazi mazuri, bora tusogee mbele mpaka mwisho wa visima vya maji ya Badr, tuvizunguke kisha tujenge mahodhi, tuyajaze maji, kisha tupambane nao, sisi tutakuwa tunakunywa na wao wasipate kunywa”.

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:

“Rai uliyotowa ni nzuri.”



Wakaondoka hapo na kusogea sehemu ya juu ya mahali yalipo maji, na usiku wakaanza kutengeneza mahodhi na kuyajaza maji.





Makao Makuu Ya Jeshi



Baada ya kumaliza kazi yao hiyo, Sa’ad bin Mu’aadh (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akatoa rai pajengwe mahali patakapokuwa makao makuu ya jeshi lao, ili waweze kujitayarisha na kuikabili hali ya hatari yoyote itakayotokea iwapo jeshi lao litashindwa katika vita hivyo.



Akasema:



“Ee Rasuli wa Allaah, unaonaje tukakujengea kipaa mfano wa hema (‘Ariish), kisha tukakuwekea tayari wanyama wa kupanda, kisha sisi tutapambana na adui, ikiwa Allaah atatujaalia tukawashinda, hayo ndiyo tunayoyapenda. Ama ikiwa kinyume na hivyo, basi wewe utapanda wanyama wako na utakwenda kujiunga na wenzetu tuliowaacha nyuma, kwani hao tuliowaacha nyuma mapenzi yao juu yako ni makubwa pia kama sisi. Wangelijuwa kuwa utapambana na adui, basi wasingerudi nyuma kabisa na wangepigana jihadi pamoja nawe.”



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuombea kila la khayr kwa rai yake hiyo, na Waislamu wakajenga mfano wa hema juu ya kilima, sehemu ya Kaskazini ya uwanja wa mapambano, sehemu ambayo mtu anaweza kuviona vita bila ya taabu huku vikipiganwa.





Usiku Kabla Ya Mapambano



Usiku kabla ya mapambano, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alilipanga vizuri jeshi lake. Kisha akawa anatembea huku akiwaonyesha Swahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum), mahali watakapokufa maadui mbali mbali, kabla hata vita havijaanza. Alikuwa akisema:



“Hapa ataanguka fulani, hapa atauliwa fulani …”



Alipokuwa akiwapanga watu wake, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipita mbele ya Sawaad bin Aziya (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akamgonga kwa nguvu tumboni pake kwa bapa la mkuki na kumwambia:



“Simama vizuri ee Sawaad.”



Sawaad (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akamwambia:



“Umeniumiza ee Rasuli wa Allaah na Rabb wako amekuleta kwa ajili ya kusimamisha haki na uadilifu, kwa hivyo uniache na mimi nikulipizie katika mwili wako”.



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akalifunua tumbo lake na kumwambia:

“Jilipie kisasi chako.”

Sawaad akalikumbatia tumbo la Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) huku akilibusu. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia:

“Kipi kilichokupeleka ukafanya hivi?”

Akasema:

“Ee Rasuli wa Allaah, mambo ndiyo kama unavyoyaona na mimi nilipenda tendo langu la mwisho kabla sijafa liwe kuugusa mwili wako”.

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuombea du’ah nzuri.



Baada ya kuwapanga watu wake sawa na kuwataka wasianze kupigana mpaka atowe amri yake, akawaambia:



“Wakianza kuja, anzeni kuwarushia mishale na msitoe panga zenu mpaka wawe karibu nanyi kabisa.”





Jeshi La Watu Wa Makkah



Usiku ule baadhi ya ma-Quraysh walijaribu kutaka kunywa maji penye mahodhi waliyoyajenga Waislam, lakini kila aliyejaribu kuyasogelea aliuliwa, isipokuwa mtu mmoja aitwae, Haakim bin Hizaam, huyu aliachwa na alisilimu baadaye na akawa Mwislam mwema.



Ma-Quraysh walimtuma ‘Umair bin Wahaab Al-Jahamiy aende kuchunguza nguvu za jeshi la Waislam. Akawa anazunguka mbali na jeshi hilo akiwa juu ya farasi wake, huku na kule, kisha akarudi kwa wenzake na kuwaambia:



“Jeshi lao ni kiasi cha watu mia tatu na zaidi kidogo, lakini naona kesho balaa litakuwa kubwa sana, maana watu hawa hawana pa kukimbilia, na hawana cha kupoteza, wanajuwa kuwa wao watauliwa tu. Hawana isipokuwa panga zao tu, na nyuma yao jangwa tupu, kwa hivyo inaelekea watapigana kwa ushujaa na hawatokubali mmoja wao auliwe bila ya yeye naye kuuwa mtu mmoja kati yenu, kwa hivyo tizameni wenyewe”.



Pakatokea mzozo mkubwa baina ya ma-Quraysh, wengi wao wakamtaka Abu Jahal arudi na jeshi lake Makkah, na kwamba hapakuwa na haja ya kupigana na jeshi la Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Lakini Abu Jahal kwa haraka akafanikiwa kuuzima moto huo na kumlaumu ‘Umair kwa kumwambia:



“Umeingiwa na hofu wewe ulipouona uso wa Muhammad, pale ulipokuwa ukiyachunguza majeshi yake ndiyo sababu ukaja na uwoga na unataka kututia na sisi uwoga huo.”



Akaweza kuwaingiza watu wake mori wa vita, kwa kuwakumbusha kuuliwa kwa ‘Amru bin Al-Hadhramiy na kwamba lazima walipe kisasi chake.





Majeshi Yanakabiliana



Asubuhi ya siku ya Ijumaa, tarehe kumi na saba, mwezi wa Ramadhwan, mwaka wa pili baada ya Hijrah, majeshi hayo mawili yakapambana. Allaah aliwafanya Waislam walione jeshi la makafiri kuwa ni wachache ili wasiwaogope na akawafanya makafiri wawaone Waislamu pia kuwa ni wachache ili wasiwaogope na kurudi nyuma, yote haya ili kitendeke kile anachokitaka Subhaanahu wa Ta’aalaa.



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) anasema:



وَإِذْ يُرِيكُمُوهُمْ إِذِ الْتَقَيْتُمْ فِي أَعْيُنِكُمْ قَلِيلًا وَيُقَلِّلُكُمْ فِي أَعْيُنِهِمْ لِيَقْضِيَ اللَّـهُ أَمْرًا كَانَ مَفْعُولًا ۗ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ﴿٤٤﴾يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا لَقِيتُمْ فِئَةً فَاثْبُتُوا وَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَثِيرًا لَّعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ﴿٤٥﴾



Na pindi (Allaah) Alipokuonyesheni machoni mwenu, pale mlipokutana, kuwa wao ni wachache na Akakufanyeni nyinyi kuwa wachache machoni mwao; ili Allaah Akidhie jambo lilokuwa lazima litendwe. Na kwa Allaah Pekee hurejeshwa mambo yote. Enyi walioamini! Mtapokutana na kikosi (cha makafiri), basi simameni imara, na mdhukuruni Allaah kwa wingi ili mpate kufaulu. [Anfaal: 44 - 45]



Majeshi yalipoanza kupambana, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaingia ndani ya lile hema, yeye na Abu Bakr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) peke yao, na hapana mwengine aliyeingia humo isipokuwa wao, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaanza kuomba du’ah huku akisema:



“Rabb wangu hawa ma-Quraysh wamekuja kwa jeuri na kiburi chao, wakikupinga na kumkadhibisha Nabiy wako. Rabb wangu nitimizie yale uliyoniahidi, Rabb wangu watu hawa wakishindwa leo, basi hutaabudiwa tena…”



Kila vita vikipamba moto, naye huongeza kuomba du’ah.



Akawa anaendelea kuomba mpaka nguo yake ya begani ikamwanguka, na As-Swiddiyq (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akaiokota na kumvisha tena huku akimwambia:



“Inatosha ee Rasuli wa Allaah, ushamuomba vya kutosha Rabb wako.”



Kisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasimama penye mlango wa ‘Ariish aliyojengewa akawa anaisoma aayah ya 45 ya Suwrah Al-Qamar:



سَيُهْزَمُ الْجَمْعُ وَيُوَلُّونَ الدُّبُرَ ﴿٤٥﴾

Na maana yake ni:



Utashindwa mjumuiko wao na watageuka nyuma. [Al-Qamar: 45]





Mubaraza (Mapigano) Kabla Ya Mapambano



Kwa kawaida kabla ya kuanza mapambano,



Waarabu walikuwa na tabia ya kuanzisha Mubaraza, na maana yake ni, mtu mmoja au wawili au watatu hutoka kutoka kila upande na kuanza kupambana wao kwanza kila mmoja na mwenzake mpaka wauwane, kisha vita ndiyo vinaanza. Mapigano haya kwa kawaida ndiyo yanayotowa picha ndogo ya mwisho wa vita.



Katika mapigano haya, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwatoa upande wa Waislam, ‘Aliy bin Abi Twaalib, Ubaidah bin Haarith na Hamzah (Radhwiya Allaahu ‘anhum). Kwa upande wa makafiri wakatoka, Utbah na ndugu yake Shaibah, na Al-Waliid mtoto wa Utbah – wote wakiwa watu wa aila moja. Katika mapigano hayo, Hamza (Radhwiya Allaahu ‘anhu), alimuuwa mpinzani wake Shaibah, na ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu), alimuuwa mpinzani wake Al-Waliid bila taabu na bila kuchukuwa muda mferu. Ama Ubaidah (Radhwiya Allaahu ‘anhu), yeye na mpinzani wake, wote wawili waliumizana wakaanguka chini, lakini ‘Aliy na Hamzah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) wakawahi kumrukia Al-Waliid na kumuuwa kisha wakamuokoa mwenzao na kumvuta nyuma na kumrudisha katika kambi ya Waislam. Lakini hatimaye kutokana na damu nyingi iliyomwagika alifariki dunia siku nne baada ya tukio la Badr kwa homa ya manjano.





Mashambulio



Mapigano haya yalimaanisha mwisho mbaya wa jeshi la washirikina. Kwa sababu wamepoteza watatu katika wapiganaji wao wakubwa kwa mpigo mmoja, na kwa kawaida Waarabu walikuwa na itikadi ya kuvipima vita kutokana na mapigano ya mwanzo (Mubaraza). Kwa ajili hiyo wakawavamia Wasilam kwa ghadhabu na kwa nguvu zao zote, na Waislam wakapambana nao kwa ujasiri mkubwa kabisa.



Wakati huo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawatokea Waislam na kuwaambia:



“Naapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhammad ipo mikononi pake, yeyote atakayepigana nao leo kisha akauliwa akiwa katika hali ya subra, bila ya kurudi nyuma, basi Allaah atamuingiza Jannah.”



‘Umair bin Al-Hamaam (Radhwiya Allaahu ‘anhu) aliyekuwa akila tende, mara baada ya kusikia maneno hayo akasema:



“Hivyo baina yangu na baina ya kuingia Jannah ni kupigana na kuuliwa na watu hawa na tende hii ndiyo inanichelewesha?”



Akazitupa tende zake, akaingia vitani, akapigana mpaka akauliwa.



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasogea mbele, akachota gao la mchanga, akawakabili ma-Quraysh kisha akasema:



“Zimeangamia nyuso zao.”



Kisha akawarushia nao.



Allaah Anasema:



فَلَمْ تَقْتُلُوهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ قَتَلَهُمْ ۚ وَمَا رَمَيْتَ إِذْ رَمَيْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ رَمَىٰ ۚ وَلِيُبْلِيَ الْمُؤْمِنِينَ مِنْهُ بَلَاءً حَسَنًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿١٧﴾ذَٰلِكُمْ وَأَنَّ اللَّـهَ مُوهِنُ كَيْدِ الْكَافِرِينَ﴿١٨﴾



Hamkuwaua nyinyi, lakini Allaah Ndiye Aliyewaua. Na wala hukurusha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم mchanga) pale uliporusha lakini Allaah Ndiye Aliyerusha; ili Awajaribu Waumini jaribio zuri kutoka Kwake. Hakika Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote. Ndivyo hivyo! Na hakika Allaah ni Mwenye kudhoofisha mbinu za makafiri. [Al-Anfaal: 17-18]



Kisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawaambia Swahaba zake (Radhwiya Allaahu ‘anhum):



“Wakazieni vizuri, inukeni muifuatilie Jannah ambayo upana wake tu ni sawa na mbingu na ardhi.”



Kisha akaondoka na kurudi penye ‘Ariish yake ile aliyojengewa.



Mapambano makali yakaanza baina ya makundi mawili hayo, na ushindi ukawa wa Waislam. Wakauliwa waliouliwa katika vigogo vya ma-Quraysh na wakatekwa waliotekwa.



Haya ni mapambano ya pekee ambayo Malaika walishiriki, akiwemo Jibriyl ('Alayhis-salaam). Baadhi ya Swahaba walisema:



“Siku hiyo tulikuwa tukiona vichwa vikikatika tu na kuruka huku na kule, hatujuwi nani anayevikata”.



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَاسْتَجَابَ لَكُمْ أَنِّي مُمِدُّكُم بِأَلْفٍ مِّنَ الْمَلَائِكَةِ مُرْدِفِينَ﴿٩﴾وَمَا جَعَلَهُ اللَّـهُ إِلَّا بُشْرَىٰ وَلِتَطْمَئِنَّ بِهِ قُلُوبُكُمْ ۚ وَمَا النَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِندِ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴿١٠﴾إِذْ يُغَشِّيكُمُ النُّعَاسَ أَمَنَةً مِّنْهُ وَيُنَزِّلُ عَلَيْكُم مِّنَ السَّمَاءِ مَاءً لِّيُطَهِّرَكُم بِهِ وَيُذْهِبَ عَنكُمْ رِجْزَ الشَّيْطَانِ وَلِيَرْبِطَ عَلَىٰ قُلُوبِكُمْ وَيُثَبِّتَ بِهِ الْأَقْدَامَ﴿١١﴾إِذْ يُوحِي رَبُّكَ إِلَى الْمَلَائِكَةِ أَنِّي مَعَكُمْ فَثَبِّتُوا الَّذِينَ آمَنُوا ۚ سَأُلْقِي فِي قُلُوبِ الَّذِينَ كَفَرُوا الرُّعْبَ فَاضْرِبُوا فَوْقَ الْأَعْنَاقِ وَاضْرِبُوا مِنْهُمْ كُلَّ بَنَانٍ﴿١٢﴾ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ شَاقُّوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ وَمَن يُشَاقِقِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَإِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ﴿١٣﴾ذَٰلِكُمْ فَذُوقُوهُ وَأَنَّ لِلْكَافِرِينَ عَذَابَ النَّارِ﴿١٤﴾



Na pindi mlipomuomba uokovu Rabb wenu Naye Akakuitikieni kuwa: Hakika Mimi Nitakusaidieni kwa Malaika elfu wafuatanao mfululizo. Na Allaah Hakujaalia haya isipokuwa ni bishara na ili zitumainike nyoyo zenu kwayo. Na hakuna nusura isipokuwa kutoka kwa Allaah. Hakika Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. Pindi Alipokufunikeni kwa usingizi kuwa ni amani kutoka Kwake, na Akakuteremshieni maji kutoka mbinguni, ili Akutwaharisheni kwayo, na Akuondosheeni wasiwasi na rai ovu za shaytwaan, na ili Atie nguvu nyoyo zenu, na Athibitishe kwayo miguu. Pindi Rabb wako Alipowatia ilhamu Malaika (kuwaambia): Hakika Mimi Niko pamoja nanyi; basi wathibitisheni wale walioamini. Nitavurumisha kizaazaa katika nyoyo za waliokufuru. Basi wapigeni juu ya shingo na wapigeni kila kiungo. Hivyo kwa kuwa wao wamempinga Allaah na Rasuli Wake. Na yeyote ampingae Allaah na Rasuli Wake basi hakika Allaah ni Mkali wa kuakibu. Ndivyo hivyo kwenu (jazaa), basi ionjeni, na kwamba makafiri wana adhabu ya moto. [Al-Anfaal: 9-14]





Kifo Cha Abu Jahal



Abu Jahal alipoona majeshi yake yanaanza kurudi nyuma akawa anapiga kelele huku akisema:

“Wasikutisheni hao, msiogope kwa kuwa ‘Utbah na Al-Waliid wameuliwa, leo hatuondoki hapa mpaka turudi nao Makkah tukiwa tumewafunga kamba wote hawa”.



Anasema ‘Abdur-Rahmaan bin Auf kuwa nilipokuwa nimesimama vitani nikageuka kutizama kuliani kwangi na kushotoni kwangu nikidhania watakuwepo watu wazima ili tusaidiane vita vikipamba moto. Lakini nikavunjika moyo nilipowaona watoto wadogo wawili wamesimama mmoja kushotoni pangu na mwengine kuliani pangu. Nikasema moyoni mwangu: “Leo sina pa kuegemea”. Yule mtoto aliye kuliani pangu akaniomba niiname apate kuniuliza ili yule mwenzake asisikie. Akaniuliza:



“Ami! Yupi kati yao Abu Jahal?”



Nikamuuliza:



“Ee mwana wa ndugu yangu, unamtakia nini Abu Jahal?”



Akanijibu:



“Nimesikia kuwa anamtukana Rasuli wa Allaah, Wa-Allaahi nikimuona basi sitomwacha, lazima nitamuuwa”



Yule mtoto aliye kushotoni pangu akaniuliza vile vile kama mwenzake, na nikamjibu kama mwenzake na akasema yale yale aliyosema mwenzake.



Nilipomuona Abu Jahal nikawaambia:



“Yule rafiki yenu mnayemtafuta”



Wakamkimbilia na panga zao, wakamvamia na kumpiga kwa mapanga mpaka wakamuuwa.



Mara baada ya kumuuwa wakakimbia mpaka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kumpa habari njema hizo. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawauliza:



“Yupi kati yenu aliyemuuwa?”

Kila mmoja akasema:

“Mimi ndiye niliyemuuwa”.

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawaambia:

“Hebu nione panga zenu.”

Baada ya kuzitizama akasema:

“Kweli, nyote mmeshirikiana katika kumuuwa.”

Kisha akasema:

“Allaahu laa ilaaha illa huwa” mara tatu.

Kisha akasema:

“Alhamdu lillaahi lladhiy swadaka wa’adahu, wa naswara ‘abdahu, wa hazama l-ahazaaba wah–dahu”.



Katika vita hivi waliuliwa ma-Quraysh sabiini, na wengine sabiini walitekwa, na katika waliouliwa alikuwemo Firauni wa Umma huu – Abu Jahal na ‘Utbah bin Rabia na mwanawe Al-Waliyd na nduguye Shaiba na wengi wengineo.



Na miongoni mwa mateka alikuwemo Al-‘Abbaas – Ami yake Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na ‘Aqiyl bin Abi Twaalib, na Nawfal bin Al-Haarith, na Umayya bin Khalaf na wengi wengineo.



Hawa wote walikuwa upande wa ma-Quraysh.





Mizoga Ya Makafiri



Baada ya vita kumalizika, Waislam wakawazika wenzao waliokufa Mashahid na idadi yao walikuwa kumi na nne. Kisha wakaichukua mizoga ya Mushrikina na kuitupa katika kisima kisichokuwa na maji kilicho karibu na mahali palipotokea mapambano hayo.





Nabiy (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) Anawafokea Maadui Wake



Usiku wa manane Waislam walimsikia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa amesimama penye kile kisima walichotupa mizoga ya Mushrikina akiwafokea huku akisema:



“Enyi mlio kisimani, ubaya ulioje mliokuwa nao jamaa zangu nyinyi kwa Nabiy wenu! Mlinikadhibisha wakanisadiki watu (kweli), mkanitoa katika mji wangu, wakanipokea watu (kweli), mkanipiga vita wakanisaidia watu (kweli). Je! Sasa nyinyi mmekwisha pata kweli yale aliyokuahidini Rabb wenu? Ama mimi nimepata kweli yale aliyoniahidi Rabb wangu.”



Swahaba wakamuuliza:



“Ee Nabiy wa Allaah unazungumza na watu washakuwa mizoga?”



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:

“Wao wanasikia kuliko nyinyi haya niliyowaambia isipokuwa hawawezi kujibu.”





Bishara Njema



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwatuma watu kwa haraka sana waende Madiynah ili kuwapa habari njema hizo za ushindi wao juu ya Makafiri.



Usaamah bin Zayd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) anasema:



“Zilitufikia habari tulipokuwa tukimzika Bibi Ruqayya (Radhwiya Allaahu ‘anha) binti wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), mke wa ‘Uthmaan bin ‘Affaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu).



Zayd bin Harithah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alipoingia msikitini, watu walimzunguka huku akisema kwa furaha:



“Amekwisha uliwa ‘Utbah bin Rabia na Shaibah bin Rabia na Abu Jahal.” Akawa anawataja mmoja mmoja katika vigogo vya ma-Quraysh waliouliwa Badr.



Zayd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) anasema:



“Nikamuuliza, Babangu unasema kweli?”



Akanijibu:



“Naam, kweli mwanangu”





Kuondoka Mji Wa Badr



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), akaondoka hapo Badr pamoja na mateka wao na ngawira zao na alipofika karibu na Madiynah alisimamisha msafara katika bonde la Safra akawagawia Waislam ngawira yao sawa sawa na kila anapoukaribia mji wa Madiynah, alikuta makundi kwa makundi ya watu waliosimama pembezoni mwa njia wakimpongeza.



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) anasema:



إِذْ أَنتُم بِالْعُدْوَةِ الدُّنْيَا وَهُم بِالْعُدْوَةِ الْقُصْوَىٰ وَالرَّكْبُ أَسْفَلَ مِنكُمْ ۚ وَلَوْ تَوَاعَدتُّمْ لَاخْتَلَفْتُمْ فِي الْمِيعَادِ ۙ وَلَـٰكِن لِّيَقْضِيَ اللَّـهُ أَمْرًا كَانَ مَفْعُولًا لِّيَهْلِكَ مَنْ هَلَكَ عَن بَيِّنَةٍ وَيَحْيَىٰ مَنْ حَيَّ عَن بَيِّنَةٍ ۗ وَإِنَّ اللَّـهَ لَسَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿٤٢﴾إِذْ يُرِيكَهُمُ اللَّـهُ فِي مَنَامِكَ قَلِيلًا ۖ وَلَوْ أَرَاكَهُمْ كَثِيرًا لَّفَشِلْتُمْ وَلَتَنَازَعْتُمْ فِي الْأَمْرِ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ سَلَّمَ ۗ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ﴿٤٣﴾



Pindi nyinyi mlipokuwa kando ya bonde la karibu na wao (Makafiri) walipokuwa kando ya bonde la mbali, na msafara (wa mali zao) ulikuwa uko chini yenu. Na lau mngeliahidiana basi mngelikhitalifiana katika miadi hiyo, lakini ili Allaah Akidhie jambo lilokuwa lazima litendwe; ili ahiliki (kwa ukafiri) yule wa kuhiliki kwa hoja bayana na ahuike (kwa iymaan) mwenye kuhuika kwa hoja bayana. Na kwamba Allaah bila shaka ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote. Pindi Allaah Alipokuonyesha usingizini mwako kwamba wao ni wachache. Na lau Angelikuonyesha kuwa wao ni wengi, bila shaka mngelivunjikwa moyo, na bila shaka mngelizozana katika jambo hilo (la kupigana), lakini Allaah Amesalimisha (hayo). Hakika Yeye ni Mjuzi kwa yaliyomo vifuani. [Al-Anfaal: 42–43]





Matukio Mbali Mbali



Baada ya kumalizika vita, Masa-‘ab bin ‘Umair (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alimuona ndugu yake Abu ‘Aziiz aliyekuwa upande wa makafiri akiwa ametekwa na amefungwa kamba.



Akamwambia yule aliyemfunga kamba:



“Mfunge vizuri huyo kwa sababu mamake ana mali nyingi, anaweza kumkomboa”



Ndugu yake akamwambia:



“Huko ndiko kuwapa usia mwema ndugu yangu?”



Mas-‘ab akamwambia:



“Huyu aliyekukamata ni ndugu yangu kuliko wewe”.



Baada ya kutupwa maiti za makafiri kisimani, Abu Hudhaifah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) mwana wa ‘Utbah bin Rabia alikuwa na huzuni sana. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza:



“Unaona vibaya juu ya babako, (kwa vile ni kafiri na ametupwa kisimani na wenzake)?”



Abu Hudhaifah akasema:



“Laa wa-Allaahi, ewe Rasuli wa Allaah, isipokuwa babangu alinifanyia fadhila nyingi sana na alikuwa akinipenda, nikadhani kwa ajili hiyo naye atasilimu, na nilipomuona kuwa amekufa kafiri, ndio nikahuzunika”.



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuombea du’ah kumtakia kila la khayr.



Wale watoto wawili waliomuuwa Abu Jahal nao wana kisa chao. Walipokuja kutaka kushiriki katika vita, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamkubali ndugu mkubwa na akamkataa yule mdogo.



Yule mdogo akasema:

“Ee Rasuli wa Allaah, kwa nini umemkubali kaka yangu na mimi hukunikubali?”

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia:

“Kwa sababu umri wako ni mdogo.”

Akasema:

“Lakini sisi siku zote tukipigana mieleka, mimi namshinda kaka yangu.”

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:

“Hebu piganeni mieleka nikuoneni.”



Wakapigana na yule mdogo akamshinda mkubwa wake, kisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamkubali.



‘Umar bin Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alimuuwa siku hiyo mjomba wake Al’Aas bin Hisham, aliyekuwa upande wa makafiri.





Hitimisho



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) anasema:



وَلَقَدْ نَصَرَكُمُ اللَّـهُ بِبَدْرٍ وَأَنتُمْ أَذِلَّةٌ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿١٢٣﴾



Kwa yakini Alikunusuruni Allaah katika Badr na hali nyinyi mlikuwa (kikosi) dhaifu. Basi mcheni Allaah mpate kushukuru. [Al-‘Imraan: 123]



Allaah, hapa anatujuulisha kuwa Yeye tu ndiye wa kutegemewa, na si viumbe vyake dhaifu. Yeye tu ndiye mwenye kuleta ushindi, na anayestahiki kukimbiliwa wakati wa dhiki, badala ya kuwakimbilia viumbe vyake dhaifu.



Na hili ni somo kwa wale ndugu zetu ambao mara wanapokumbwa na tatizo dogo, wanaikimbilia ile du’ah ya Hal-Badiri (Ahlul-Badr) ambayo ndani yake mna majina ya Swahaba walioshiriki katika vita hivyo, na kuomba msaada kutoka kwao.



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) anasema:



وَلَقَدْ نَصَرَكُمُ اللَّـهُ بِبَدْرٍ وَأَنتُمْ أَذِلَّةٌ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿١٢٣﴾



Kwa yakini Alikunusuruni Allaah katika Badr na hali nyinyi mlikuwa (kikosi) dhaifu. Basi mcheni Allaah mpate kushukuru. [Aal-‘Imraan: 123]



Allaah aliwapa ushindi Waislamu katika vita hivi juu ya uchache wao, wakati katika vita vya Hunain, kwa mara ya mwanzo Waislamu walipigana vita idadi yao ikiwa kubwa zaidi kuliko ya makafiri lakini waliendeshwa mbio na makafiri mpaka Allaah alipowateremshia utulivu wake. Hakupata Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kutoka na jeshi kubwa kuliko la siku hiyo, alitoka na watu elfu kumi na mbili, hata Waislamu wakawa wanasema:



“Hatutoshindwa leo kwa vile tuko wengi.”



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) anasema:



لَقَدْ نَصَرَكُمُ اللَّـهُ فِي مَوَاطِنَ كَثِيرَةٍ ۙ وَيَوْمَ حُنَيْنٍ ۙ إِذْ أَعْجَبَتْكُمْ كَثْرَتُكُمْ فَلَمْ تُغْنِ عَنكُمْ شَيْئًا وَضَاقَتْ عَلَيْكُمُ الْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ ثُمَّ وَلَّيْتُم مُّدْبِرِينَ﴿٢٥﴾



Kwa yakini Amekunusuruni Allaah katika maeneo mengi, na Siku ya (vita vya) Hunayn (pia); ulipokupendezeni wingi wenu (kwa kujigamba), lakini haukukufaeni chochote; na ardhi ikawa dhiki juu yenu juu ya upana wake, kisha mkageuka na kurudi nyuma kukimbia. [At-Tawbah: 25]



Anasema Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) kuwa:



“Katika vita vya Yarmuuk, ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) aliwaambia Waislamu:



“Mtakapotaka msaada katika vita hivi, basi muandikieni Abu ‘Ubaidah”.



Vita vilipoanza, wakamuandikia Abu ‘Ubaidah aje kuwasaidia, na kwamba wako katika hatari. Abu ‘Ubaidah akawaandikia hivi:



“Imenifikia barua yenu ikitaka msaada kutoka kwangu, lakini mimi nitakujulisheni yule atakayeweza kukusaidieni mkapata ushindi kuliko nitakavyoweza kukusaidieni mimi; - Allaahu ‘Azza wa Jallah – ombeni msaada kutoka kwake mkitaka kupata ushindi. Kwa sababu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipewa ushindi na Allaah siku ya Badr akiwa na watu wachache kuliko nyinyi. Itakapokufikieni barua yangu hii, piganeni nao na wala msiniandikie mimi.”



Anasema Iyaadh Al-‘Ash-ary (Radhwiya Allaahu ‘anhu), mwenye kuisimulia Hadiyth hii:



“Tukapambana nao na tukawashinda, na tukapata ngawira nyingi siku hiyo”.
 
Maswali: Bid'ah - Uzushi


Bin-Aadam Anatokana Na Kizazi Cha Nyani?



Alhidaaya.com





SWALI:



Pia ninahitaji kufahamu, tunasoma kuwa Binadamu ametokana na generation ya nyani? je Qur'aan inasemaje ya suala hili.





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho



Hakika nadharia hiyo haina ithbati yoyote kutoka hata kwa sayansi yenyewe. Bali nadharia hiyo ililetwa na Myahudi Darwin ili kumdhalilisha mwanaadamu. Nadharia hiyo ni potofu na ni kinyume na Qur-aan.



Hiyo ni kuwa Allaah Aliyetukuka Anatuambia:

لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ فِي أَحْسَنِ تَقْوِيمٍ ﴿٤﴾

Kwa yakini Tumemuumba mwana-Aadam katika umbile bora kabisa. [At-Twiyn 95: 4].



Na Akasema:

الَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّاكَ فَعَدَلَكَ ﴿٧﴾

Ambaye Amekuumba Akakusawazisha (umbo sura, viungo) na Akakupima na kukulinganisha sawa. [Al-Infitwaar: 7].



Na Aayah zinazotueleza kuwa mwanaadamu ameumbwa na Allaah Aliyetukuka ni nyingi sana.



Kadhalika hakuna Muislam asiyefahamu kuwa Aadam (‘Alayhis-salaam) ambaye ni mwanaadam wa kwanza, aliumbwa kwa udongo na akatokana naye mkewe Hawwaa na vizazi Haabiyl na Qaabiyl hadi kutufikia sisi leo hii. Sasa huyo nyani katokea wapi hapo?





Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Bid'ah - Uzushi


Kisomo Cha Arubaini Baada Ya Maiti Kufa Ni Sunnah Au Bid'ah?



Alhidaaya.com



SWALI:



Imezoeleka maiti anapozikwa baada ya siku tatu watu hufanya kisomo, wengine hufanya Arobaini je hiki kisomo haswa kinahitajika kifanyike lini? na hii Arobaini inabidi iwe imesomwa kabla au baada ya kupita siku Arobaini tangu kupita mazishi?



JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho



Hakika ni kuwa jambo hili la kufanya kisomo baada ya siku tatu au kufanya arobaini na watu kula mpunga kama katika karamu ni mambo yaliyozoeleka sana. Zipo sehemu nyingine wanakusanyikana Msikitini kwa ajili ya kisomo kwa siku tatu mfululizo. Lakini kwa kuwa uchumi umezorota huwa siku hizi inafanywa siku moja peke yake na thawabu ya kisomo wanaona zinamfikia maiti.



Hakika jambo hili halikuthubutu kabisa kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Swahaba zake (Radhwiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema. Hakika ni kuwa kisomo hicho thawabu zake hazimfikii maiti.



Ifahamike kuwa katika Uislamu hakuna kabisa mas-alah ya siku arobaini. Arobaini kimtazamo wa fiqhi ni zile siku za uwingi ambazo anakaa mwanamke aliyezaa akiwa anatokwa na damu ya Nifaas. Wakati huu mwanamke huyo huwa ana udhuru hivyo haruhusiwi kishari’ah kuswali wala kufunga.



Sasa na watu wenye kupenda mambo ya kuzua mambo katika Dini bila msingi wowote wamechukuwa kuwa baada ya mtu kufa watu wanakusanyikana katika nyumba ya aliyefariki wakifanya kisomo na du’aa na hapo kuandaliwa chakula aina kadhaa ili watu wale pamoja na kumkumbuka aliyefariki. Hakika jambo hili la arobaini halipo kabisa na hivyo ni uzushi.



Inabidi sisi tuachane na jambo hilo na tuangalie mambo ambayo yanaweza kumfaa maiti kaburini. Yapo mambo mengi lau yatafanywa na watu wa aliyefariki basi yeye anapata thawabu japokuwa keshafariki. Miongoni mwa mambo hayo ni:



1. Kuombewa Du’aa na mtoto wake mwema.



2. Kulipiwa madeni anayodaiwa.



3. Kufanyiwa Hajj ikiwa hakuwahi kufanya.



4. Kutolewa sadaka wakati wowote ule na sio baada ya siku arobaini au siku tatu.



5. Kumlipia nadhiri zake.



6. Waislamu kwa jumla kumuombea Du’aa.



Hayo ni mambo yatakayomsaidia sana kuliko mkusanyiko wa mara moja na watu kusoma, kula na kuondoka.



Kadhaalika soma makatazo ya jambo hilo kwenye kitabu cha ‘Bid-a’ cha Shaykh ‘Abdullaah Swaalih Farsiy, ambacho vilevile kinapatikana hapa:



Bid'ah - Shaykh 'Abdullaah Swaalih Faarsiy (Aliyekuwa Qaadhi Wa Zanzibar Na Kenya)







Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Bid'ah - Uzushi


Kuamkiana Kila Ijumaa Kwa Kutumiana Mashairi,

Du'aa, Kupitia Barua Pepe, Text Messages .n.k.



Alhidaaya.com



SWALI:



Asalam aleikum



Tunashukuru kupata mahali pa kuuliza maswali yetu yenye utata.



Swali langu ni kwamba kuna mtindo siku hizi watu kusalimiana kila Ijumaa kwa kupelekeana ima text message au e-mail na kuamkiana 'Ijumaa ya Baraka' wengine hutumiana mashairi, kuombeana dua etc. wanasema inadumisha mapenzi baina ya Waislamu na pia wanaadhimisha siku ya Ijumaa. Je ni hukmu yake?





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho





Ndugu katika Uislamu, kusalimiana ni jambo ambalo lipo katika kila jamii tena lilikuwepo kabla ya hata kuja Uislamu. Ulipokuja Uislamu haukuliondoa bali ulileta matamshi yake maalumu kwa Waislamu kusalimiana, matamshi ambayo kama yalivyothibiti katika Hadiyth ni yale yale waliyosalimiana baba yetu Aadam (‘Alayhis Salaam) na Malaika wa Ar-Rahmaan kama yalivyothibiti katika Hadiyth:





"Allaah Amemuumba Aadam kwa sura yake urefu wake alikuwa dhiraa sitini, Alipomuumba Alimwambia: Nenda ukawasalimie kikundi kile pale miongoni mwa Malaika waliokaa na usikilize watachokuitikia nacho; kwani hayo maamkizi watayokuitikia nayo ndio maamkizi yako na ya vizazi vyako; Aadam akawaamkia kwa kusema: Assalaamu ‘Alaykum; Malaika wakamuitikia: Assalaamu ‘Alaykum wa RahmatuLlaahi, Malaika waliongeza wa-Rahmatu Llaahi…" [Imepokewa na Al-Bukhaariy, kitabu cha Istiidhaan, mlango wa kuanza Salaam].





Ni vyema tuelewe kuwa dini yetu Anayoiridhia Allaah ilikamilika toka wakati wa uhai wa Mjumbe Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama inavyothibitisha Aayah iliyo wazi katika Suwrah Al-Maaidah; hivyo basi mitindo yote kama ulivyonukuu kauli yako; 'kuna mtindo siku hizi' iliyokuwa haipo wakati ule haitegemewi kuwa na faida kwa Waislamu hata wakitumia ndani yake Hadiyth au jambo lililokuwepo katika dini na lililokuwa likitekelezwa na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum) kama hili la 'watu kusalimiana kila Ijumaa kwa kupelekeana ima text message au e-mail na kuamkiana 'Ijumaa ya Baraka (Barakatul Jumu’ah)' au 'Jumaa Mubarak' wengine hutumiana mashairi, kuombeana dua'.





Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu ‘anhum) na Salafus Swaalih na Waislamu wenye kumpenda Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kumuomba Mola Awawafikishe kushikamana na Sunnah za Mjumbe Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) huwa wanasalimia kila wakati na kila siku na si kila Ijumaa; tena husalimia kwa kila mmoja kumsikia mwenzake huku akitabasamu au akiwa na uso mkunjufu.





Waislamu wenye kumpenda Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) humuomba Rabb Awawafikishe kushikamana na Sunnah za Mjumbe Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na katika kujaribu kwao kutekeleza na kushikamana na maaamrisho ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) huwa wanasalimiana kama alivyokuwa alikisalimiana Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu ‘anhum) kwa kusema 'Assalaamu 'Alaykum' na hakuna katika yaliyothibiti kuwa siku ya Ijumaa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu ‘anhum) ambao kwa kweli walikuwa wakiilewa vyema siku ya Ijumaa au hata Salafus Swaalih kwamba walikuwa wakisalimiana na kuamkiana kwa kusema: 'Ijumaa Kariym' au 'Ijumaa ya Baraka' (Jumu'ah Mubaarakah). Kwa hiyo haya mambo ambayo hivi sasa yanaenea kwa kasi kwenye barua pepe, text msgs za simu za mkononi n.k. ni mambo yanayopelekea kwenye uzushi na kupotosha mafundisho sahihi ya Uislam na siku za mbele vizazi vinavyokuja watakuja kuona haya ni sehemu katika Dini na mwisho itakuwa ni jambo litakaloonekana kama ni faradhi. Na tukiangalia historia ya mambo ya uzushi, tutaona yalianza kama hivi.





Waarabu walikuwa wakisifika sana kuwa ni mabingwa katika fani ya mashairi na Qur-aan katika baadhi ya Surah zake imekuja kama shairi kwa kumalizika kila Aayah kwa namna moja kama yanavyomalizika mashairi na ilikuwa katika kawaida yao kushindana kwa kuleta shairi na yalieleweka yale yaliyokuwa mazuri na bora katika hayo kwa jina la Mu’alaaqaat kumi ambayo ilitundikwa katika A-Kaabah. Ulipokuja Uislamu pia Swahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum) walitumia njia hiyo hiyo ya mashairi kuwalingania watu lakini hakuna katika yote yaliyopokewa kuwa yalikuwa yakitumiwa makhsusi kwa siku ya Ijumaa kama hivi ‘wengine hutumiana mashairi’ wala haikupokewa kuwa mshairi wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Hassaan bin Thaabit (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alikuwa akitunga mashairi na kumsalimia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) siku ya Ijumaa; bali alikuwa alitunga mashairi kushajiisha watu kupigania dini ya Allaah na kuinusuru sio kusalimiana.





Du'aa ni katika ‘Ibaadah kubwa ambayo alishikamana nayo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu ‘anhum) na Salafus Swaalih na mpaka leo Waislamu wenye kumpenda Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) huwa du'aa ndio silaha yao kubwa kila siku na kila wakati na huwa wanajitahidi kuomba katika nyakati ambazo kumethibiti uzuri wa kuomba du’aa katika nyakati hizo ambazo zimethibiti katika Sunnah za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama siku ya Ijumaa na kadhalika.





Kuhusu 'kuombeana dua n.k.' ni kwamba du'aa nzuri kumuombea Muislamu mwenzako kama ilivyothibiti katika Sunnah ni kumuombea bila ya yeye kuelewa kama unamuombea; kumuombea katika hali ya siri; hivyo kumpelekea du'aa kama hivi huwa mtu kisha kwenda kinyume na ushauri wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na pia huenda ikawa kuna aina fulani ya kujionyesha; kuwa unamuombea du'aa, hivvo kuna hatari fulani, hivyo basi la kufanya ni kuombeana du'aa kwa siri bila ya muombaji kumueleza au kumpa ishara yoyote kwa yule anayemuombea ishara itayompelekea kuelewa kuwa kuna anayemuombea du'aa; kinachotakiwa ni ikhlaasw; na ikhlaasw haihitaji hilo la kupelekea text wala shairi kwani mapenzi baina ya Waislamu hayahitaji mashairi wala tenzi.





Watu wana haki ya kusema wakitakacho na wote wanachokisema kinaweza kurejeshewa wenyewe lakini katika Uislamu, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema huwa akisemacho ni amri, hivyo Waislamu hutakiwa washikamane nacho na hawana khiari wakipenda wasipende; vinginevyo huwa imani zao hazijakamilika. Sasa basi kama kuna miongoni mwa wenye kudai kuwa wanampenda Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kumfuata kwa kuwa wanasema hizo ‘Ijumaa ya Baraka ‘barakatul Jum’ah’ zao 'wanasema inadumisha mapenzi baina ya Waislamu' waelewe kuwa alichosema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye hasemi kwa matamanio yake kuwa kinadumisha mapenzi baina yetu ni hiki na si chengine:



"Naapa kwa Yule ambae nafsi yangu iko Mikononi Mwake, hamtoingia peponi mpaka muamini na hamtoamini mpaka mpendane, Je nikuelezeni kuhusu jambo mkilifanya mtapendana?!: Toleaneni Salaam baina yenu" [Imepokewa na At-Tirmidhiy, kitabu cha Istiidhaan kutoka kwa Mjumbe wa Allaah, mlango "Yaliyokuja kuhusiana na kutoa Salaam" At-Tirmidhiy amesema :Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh].





Siku ya Ijumaa ni siku tukufu kama ilivyothibiti katika Hadiyth nyingi na utukufu wake umeipata kutoka kwa Mola si kwa mwengine; na kusema kwako kuwa 'pia wanaadhimisha siku ya Ijumaa'. Tufahamu kuadhimisha jambo lolote lile katika Uislamu lazima liwe na asili kama Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) au Makhalifa wake waongofu au Swahaba zake waliadhimisha jambo hilo; na katika yaliyopokewa kuhusiana na siku hii kama tutayapa jina kuwa ni maadhimisho ya siku ya Ijumaa ni kama haya:



Kukoga siku ya Ijumaa ni wajibu kwa kila aliye baleghe


Kujitia manukato (mwanaume)


Kwenda Msikitini mapema; mwenye kwenda saa za mwanzo huwa kama aliyetoa Sadaqah ya ngamia na mwenye kwenda saa za mwisho ni kama aliyetoa yai na kadhalika.


Bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:





Mambo Ya Kufanya Siku Ya Ijumaa



Kwa hiyo kama tunataka kuadhimisha Ijumaa basi hayo ndio baadhi ya maadhimisho ya kuadhimishwa na si vyenginevyo.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Kuchangia Na Kushiriki Shughuli Za Bidaa Ni Dhambi?



Alhidaaya.com



SWALI:



Assalaam Alaykum

Nimepatwa na mtihani, mzazi wangu kafariki na ndugu wanataka tusome dua ya hitima mwezi huu, Sasa nauliza je nitoe mchango katika hiyo shughuli?

Pili je kama sitatoa pesa nikahudhuria naweza kula nyama iliyochinjwa katika hitima hiyo, Naomba mnipatie jibu mapema ili niwape msimamo kwani nahofia wasione nimewasaliti ila nataka kama haiwezekaniki niwakatalia kwa points



Wabilah Tawfiq





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Katika Swali hilo kuna mas-ala mawili ambayo yote hayafai kutendeka; khitmah na kuchinja kwa ajili ya aliyefariki:



Khitmah ni bid'ah (uzushi) kwani halimo kabisa katika mafunzo ya Sunnah, kwa maana hakuna dalili yoyote kama Nabiy Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifanya khitmah au kukubali ifanywe. Na lau kama ni jambo sahihi basi tungelipata uthibitisho kuwa lilitendeka walipofariki watu wake au Maswahaba zake. Lakini hakuna hata usimulizi mmoja unaoelezea kuwa lilitendekea zama hizo wala zama za wema waliopita. Hivyo hatuna budi kujiepusha nalo kwani maonyo mengi tumepata kutoka kwa Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kujiepusha na mambo ya bid'ah.



Bid’ah kama hizo ambazo zimeanzishwa zamani bila ya dalili, imekuwa ni jambo sugu katika jamii.







Ni wajibu wetu kuendelea kuwafunza watu na kuwafahamisha mafunzo sahihi tusichoke, hata kama ni jamaa zetu tujitahidi kuwapa nasaha na kutowatenga.





Bonyeza viungo kifuatacho upate maelezo kamili kuhusu hukmu ya khitmah na ujaribu kuwafikishia ndugu zako ujumbe huo ili wajiepushe nalo.



Khitma: Kutokufaa Na Madhara Yake



Kuchinja pia kwa ajili ya aliyefariki, hakuna ushahidi kuwa Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifanya hivyo kwa ajili ya mtu aliyekufa. Alichinja kwa ajili ya Umma huu wa Kiislamu Yawmun-Nahr (siku ya kuchinja) ambayo ni tarehe 10 Dhul-Hijjah. Alichinja pia kwa ajili ya ‘Aqiyqah wanayofanyiwa watoto. Kama alivyowafanyia wajukuu zake kina Al-Hasan na Al-Husayn (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa).





Kuchangia katika mambo hayo haifasi kabisa kwani utahesabika kuwa ni mmojawapo wa mwenye kutenda bid’ah hiyo.





Hivyo inakupasa kwanza ujiepushe kabisa na mambo hayo. Kisha ujaribu kuzuia bid’ah hizo zisitendeke, na kufanya hivyo utakuwa umetimiza wajibu wako wa kuzuia maovu yasitendeke kama tulivyoamrishwa katika Hadiyth ifuatayo:



عن أَبي سعيدٍ الخُدْريِّ رضي اللَّه عنه قال : سمِعْتُ رسُولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقُولُ : ((مَنْ رَأَى مِنْكُم مُنْكراً فَلْيغيِّرْهُ بِيَدهِ ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطعْ فبِلِسَانِهِ ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبقَلبهِ وَذَلَكَ أَضْعَفُ الإِيمانِ)) رواه مسلم .

Kutoka kwa Abuu Sa'iyd Al-Khudhriy (Radhwiya Allahu 'anhu) ambaye amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Yeyote yule atakayeona kitendo kiovu akiondoe (abadilishe) kwa mkono wake, ikiwa hawezi basi kwa ulimi wake (alikemee au kukataza), na ikiwa hawezi basi kwa moyo wake (achukie) na huo (yaani kuona baya na kunyamaza) ni udhaifu wa Imani)) [Imesimuliwa na Muslim]





Yanayompasa kumfanyia aliyefariki kama yalivyokuja katika mafunzo ya Sunnah ni; kumuombea du'aa, kumtolea swadaqah, kumfanyia Hajj ikiwa hakuwahi kufanya. Kwa hiyo badala ya kufanya jambo lisilo na msingi ni bora kufanya yale ambayo hayana shaka yaliyopatikana dalili zake katika mafunzo sahihi. Hivyo vile vile utakuwa umetoa mafunzo sahihi ya Sunnah na utajichumia thawabu kwa hayo.





Bonyeza kiungo kifutacho upate maelezo zaidi kuhusu mas-ala haya:



Kumsomea Khitmah Maiti Kumchinjia Na Kumuombea D'uaa Kwa Pamoja





Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Azidi kutuongoza kufuata yaliyo haki na kuacha yaliyo batili.



Na Allah Anajua zaidi
 
Kufanya Adhkaar Kwa Pamoja Inajuzu?



Alhidaaya.com



SWALI:



Assalam aleykum.. kwanza napenda to pongezi kwa kuanzisha website hii, inatusaidia sana hasa kwa sie tulio ughaibuni, Allaah (Subhanahu wa Ta'aalaa) awajaze majazo mema.



Swali langu ni hili... nilipokua nyumbani (tanzania) chuo chetu kilikua cha dhikri nadhani nikisema hivo utakua umenielewa... Nachotaka Kujua Sasa Je Dhikri Ni Halal Au La? Na Je Kama Ni Halal Au Haram Kuna Ushahidi Wowote? A.aleykum warahma tullah wabarakat..





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho





Hakika dhikr (utajo wa Allaah) ni jambo ambalo limehimizwa sana na Allaah Aliyetukuka na Nabiy wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).





Hata hivyo, njia ya kuifanya ndio inafanya iwe halali au haramu. Allaah Aliyetukuka Anasema kuhusu kumdhukuru:

لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّـهَ كَثِيرًا ﴿٢١﴾

Kwa yakini mna kigezo kizuri kwa Rasuli wa Allaah kwa mwenye kumtaraji Allaah na Siku ya Mwisho na akamdhukuru Allaah kwa wingi. [Al-Ahzaab: 21].



Na Anasema pia:

...وَالذَّاكِرِينَ اللَّـهَ كَثِيرًا وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا ﴿٣٥﴾

Na wanaomdhukuru Allaah kwa wingi wanaume na wanawake; Allaah Amewaandalia maghfirah na ujira adhimu. [Al-Ahzaab: 35].



Sasa jinsi yakutekeleza dhikr ndio muhimu na kuhusu hilo tumepata maelekezo kutoka kwa Qur-aan yanayosema:

وَاذْكُر رَّبَّكَ فِي نَفْسِكَ تَضَرُّعًا وَخِيفَةً وَدُونَ الْجَهْرِ مِنَ الْقَوْلِ بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ وَلَا تَكُن مِّنَ الْغَافِلِينَ ﴿٢٠٥﴾

Na mdhukuru Rabb wako katika nafsi yako kwa unyenyekevu na kwa khofu na si kwa jahara katika kauli asubuhi na jioni; na wala usiwe miongoni mwa walioghafilika. [Al-A’raaf: 205].





Kwa minajili hiyo, dhikr za watu kukusanyikana na kukohoa hazipo katika shari’ah yetu na hiyo inakuwa haramu.





Ama mtu kukaa Msikitini au nyumbani kwake au sehemu yoyote ile na kuanza kumtaja Allaah Aliyetukuka kama alivyotufundisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni jambo zuri linalopendekezwa sana.





Na watu kupoteza wakati kwa kuwaingiza watoto wao au vijana wao kwenye vyuo kama hivyo vya kudhikiri kwa kupiga kelele na kukohoa na maneno ya ‘Huw’ ‘Huw’ au kufundishwa kupiga twari (dufu) ni mambo yasiyo na manufaa kwa Dini yao wala kuwaongezea Iymaan, isitoshe ni mambo yenye kuwapotezea wakati wao na miaka ambayo wangejifunza mambo muhimu kama Tawhiyd, ‘Aqiydah, Qur-aan, Hadiyth, Fiqh ambayo ndio mambo ya msingi Muislamu kuyafahamu na yenye kuweza kumsaidia kuongeza Iymaan yake na kumpeleka Peponi.





Kwa hiyo, ni muhimu sana wazazi na watu kuchagua vyuo vya kuaminika vya watu wa Ahlus Sunnah wal Jama’ah wenye kufundisha Uislamu kama ulivyokuwa ukifahamika na Salafus Swaalih (Wema waliotangulia; Swahaba, Tabiina na waliowafuata Tabiina).





Kwa maelezo na manufaa zaidi, bonyeza viungo vifuatavyo:



Kusoma Uradi Kwa Pamoja Kila Mwezi Kwa Kukusanyika Inafaa?



Kumuombea Du'aa Mgonjwa Kwa Mkusanyiko Inafaa?





Na Allaah Anajua zaidi
 
Kufanya Tasbiyhi Kutumia Mkono Wa Kushoto



Alhidaaya.com



SWALI:



Assalaam Alaykum.

Naomba nipatiwe ufafanuzi kuhusu kusoma nyiradi (Subhanallah, Alhamdulillah, Allahu Akbar) baada ya swalaah kwa kutumia vidole, iwapo utatumia mikono yote wa kulia na wakushoto haifai? kuna mtu ameniambia kuna hadithi inakataza kutumia mkono wa kushoto, unatakiwa utumie wa kulia pekee. Naomba uafanunuzi ndugu zangu.





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho





Katika Sunan ya Abu Daawuud kumeelezwa kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitumia mkono wa kuume pekee katika kuleta tasbiyh. Hivyo inatakiwa nasi tutumie mkono huo huo kwa kufanya hilo.





Pia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitukataza kutumia mkono wa kushoto ila kwa mambo machafu kama kujisafisha baada ya kwenda haja na akatuhimiza kutumia mkono wa kuume kwa mambo mazuri kama kula na kadhalika.





Hivyo tasbiyh zinatakiwa zitumie mkono wa kuume kuhesabiwa na sio mkono wa kushoto.



Kadhalika unaweza kusoma majibu mengine katika viungo vifuatavyo:





Kutumia Tasbihi Katika Kumdhukuru Allaah Inafaa?



Inafaa Kutumia Tasbiyh Kwa Khofu Ya Kupotewa Hesabu?





Na Allaah Anajua zaidi
 
Back
Top Bottom