Ramadhan Special Thread
Dhambi Za Kutowahudumia Wazazi Na Kuwafanyia Ihsaan
Maswali: familia-Jamii
SWALI:



Asalam Aleikum



Nini hukmu ya mtoto ambaye ana nafasi katika maisha lakini hamuangalii kimaslahi mzazi wake wakati uwezo anao.



Kwa maana ingine hana CONTINUITY ya kumsaidia mzazi wake. Anamsaidia siku akipenda. Na wala hana kawaida ya kumjulia HALI hata kwenye simu. Vile vile naomba munipe ile hadithi ya sahaba wa mtume ambaye alishindwa kutoa shahada mpaka ilipodhihiri kuwa alimuudhi mama yake.



Wabillahi Taufiq



JIBU:





Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukran zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuwatendea wema wazazi. Ni utovu wa nidhamu na adabu kwa mtoto kutowatazama wala kuwatendea wema wazazi wake. Allaah Aliyetukuka Ameonyesha kuwa kuwatendea wema wazazi ni jambo kubwa sana hata Akalitaja baada tu ya kutomshirikisha Yeye, Anasema:



“Na Mola wako Ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu! Warehemu kama walivyonilea utotoni” (17: 23 – 24).



Mtu ambaye atawakuta wazazi wake katika uzee kisha asiingie Peponi basi huyo amekhasirika vibaya sana. Watoto hata wakifanya nini hawawezi kulipa fadhila walizofanyiwa na wazazi wao ila wawakute kuwa ni watumwa wawanunue kisha wawaache huru. Ikiwa si hivyo basi hata ukafanya nini huwezi kurudisha ihsani uliyofanyiwa na mzazi, baba na mama. Na mama ana daraja kubwa zaidi. Faida ni kubwa kwa mtu kuwafanyia ihsani wazazi wake kama ilivyokuja katika Hadiyth ndefu ya wale watu watatu waliofungiwa katika pango na kila mmoja akataka msaada wa Allaah Aliyetukuka kwa kuomba kupitia kwa 'amali njema alizofanya. Na kwa wema aliowafanyia wazazi wake Allaah Aliyetukuka Akakubali na kuwapatia takhfifu na kuwafungulia pango hilo. [Al-Bukhaariy na Muslim].



Na pia khasara ni kubwa maradufu kwa mtu kutowafanyia wema wazazi wake hapa duniani kabla ya Aakhirah.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Du’aa ya Kuwaombea Watoto Ili Wawe Wanaswali Daima
Maswali: familia-Jamii
SWALI:



Asalam alaikum warhmatullahi wabarakat naomba dua lolote zuri sana na mjarab niombee wanangu wasali bila ya kuhimizwa.



JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani kwa swali lako kuhusu du’aa ya kuwaombea watoto wawe ni wenye kuswali.

Hakika mwanzo kabla ya kuwaombea du’aa inatakiwa uwape watoto wako malezi mazuri, nawe pia uwe mfano mwema kwa kuswali pamoja nao, kuwapeleka Madrasah kufundishwa Diyn na kuwasuhubisha na watoto wenye marika yao walio wema.

Baada ya hapo muombe Allaah Aliyetukuka kwa du’aa yoyote ile inayolingana na matakwa yako. Na miongoni mwa du’aa nzuri ni ile aliyoomba Nabii Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) inayoesema: “Rabbij’alniy Muqiymasw Swalaati wa min Dhurriyyatiy Rabbaana wa Taqabbal Du’aa’ - Mola wangu Mlezi! Nijaalie niwe mwenye kusimamisha Swaalah, na katika dhuriya zangu pia. Ee Mola wetu, na ipokee du’aa yangu” (Ibraahiym [14]: 40).



Na Allaah Anajua zaidi
 
Husda Inayofaa Na Isiyofaa
Maswali: familia-Jamii


SWALI:



assalam aaleykum wa rahmatulalla wa barakatuh

napenda kuuliza kama binaadam umepatwa na husda dawa yake kitu gani au kuna duaa yoyote



waaleykumsalaam wa rahmatualla wa barakatuh.









JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Ingelikuwa ni vizuri kama muulizaji angelieleza hali yake ilivyo hata akahukumu kwamba amepatwa na husda. Kwa sababu maneno haya mara kwa mara tunayasikia, ni wepesi mtu kuhukumu kuwa kapatwa na husda anapofikwa na mtihani ukiwa ni mkubwa au mdogo.



Husda (al-hiqd) ziko aina mbili; husda nzuri na mbaya; nzuri ni ile ambayo umemuona mwenzio amejaaliwa neema ya mali na elimu ukatamani nawe uwe kama yeye. Haya ni mambo ya kupendekezeka kwani ni kujitamania mazuri ya Aakhirah. Hadiyth ifuatayo inaelezea aina hii ya husda:

عن أبي سعيد قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((لا حسد إلا في اثنتين : رجل آتاه الله القرآن فهو يتلوه آناء الليل وآناء النهار , فيقول الرجل : لو آتاني الله مثل ما آتى فلانا فعلت مثل ما يفعل , ورجل آتاه الله مالا فهو ينفقه في حقه فيقول الرجل : لو آتاني الله مثل ما آتى فلانا فعلت مثل ما يفعل)). أحمد

Kutoka kwa Abu Sa'iyd ambaye amesema: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna husda isipokuwa kwa mawili; mtu aliyepewa na Allaah Qur-aan akawa anaisoma nyakati za usiku na nyakati za mchana akasema [huyo mtu anayemhusudu] “Allaah Angelinipa na mimi mfano alivyopewa fulani ningelifanya kama anavyofanya”. Na mtu aliyepewa mali na Allaah akawa anaipa haki yake kwa kuitoa akasema huyo mtu, “Allaah Angelinipa kama alivyopewa fulani ningelifanya kama anavyofanya”)) [Ahmad na wengineo kwa usimulizi mwengine]





Hivyo husda kama hii haimdhuru mtu na wala mtu mwenye kuhusudu kwa kutamani kupata neema kisha afanye mema hapati dhambi kuwa na husda kama hiyo. Ama husda isiyopasa mtu kuwa nayo kwa nduguye Muislamu ni ile iitwayo 'al-hiqdil-haqiyqiy' (husda ya kweli) nayo ni kuwa na chuki na kutamani neema aliyonayo mwenzio imuondoke na makatazo hayo tumepata mafunzo yake kama ifuatavyo:



(( وَلاَ تَتَمَنَّوْاْ مَا فَضَّلَ اللّهُ بِهِ بَعْضَكُمْ عَلَى بَعْضٍ لِّلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِّمَّا اكْتَسَبُواْ وَلِلنِّسَاء نَصِيبٌ مِّمَّا اكْتَسَبْنَ وَاسْأَلُواْ اللّهَ مِن فَضْلِهِ إِنَّ اللّهَ كَانَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا))



((Wala msitamani alichowafadhili Allaah baadhi yenu kuliko wengine. Wanaume wana fungu katika waliovichuma, na wanawake wana fungu katika waliovichuma. Na muombeni Allaah fadhila Zake. Hakika Allaah ni Mjuzi wa kila kitu)) [An-Nisaa: 32]



Kwa hiyo aliyekosa neema fulani inampasa aridhike na alivyojaaliwa na akipenda amuombe Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ambaye Ndiye mtoaji rizki na neema zote Naye ni Rahiymun-Kariym (Mwenye kurehemu na Mkarimu).







Na kutoka katika Sunnah:

عن أبي هُريرةَ رضي اللهُ عنه قال: قال رسوُل الله صلى الله عليه وسلم : ((لا تَحَاسَدُوا، ولا تَنَاجَشُوا، ولا تَباغَضُوا، ولا تَدَابَرُوا، ولا يَبعْ بَعْضُكُمْ على بَيْعِ بَعْضٍ، وكُونُوا عِبادَ اللهِ إخْوَاناً، المُسْلمُ أَخُو المُسْلمِ: لا يَظْلِمُهُ، ولا يَكْذِبُهُ، ولا يَحْقِرُهُ، التَّقْوَى هاهُنا – (ويُشِيرُ إلى صَدْرِه ثَلاثَ مَرَّاتٍ ) بِحَسْبِ امْرِىءٍ مِنَ الشَّرِّ أن يَحْقِرَ أخاهُ المُسْلِمِ، كُلُّ المُسْلِمِ على الْمسْلِم حَرَامٌ: دَمُهُ ومالُهُ وعِرْضُهُ)) مسلم

Kutoka kwa Abu Hurayra (Radhiya Allaahu 'anhum) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: ((Msioneane choyo, wala msizidishiane bei (za vitu), wala msichukiane, wala msipigane mapande (msitengane), wala msishindane kwa kupunguza bei. Lakini kuweni ndugu, enyi waja wa Mwenyeezi Mungu, Muislamu ni ndugu wa Muislamu mwenzake, hamdhulumu wala hamvunji, hamwambii uongo wala hamdharau. Ucha Mungu uko hapa (huku akiashiria kifuani kwake kwa vidole vyake) mara tatu. Ni uovu wa kutosha kwa mtu kumdharau ndugu yake Muislamu. Muislamu ameharamishiwa kwa Muislamu mwenzake; damu yake, mali yake na heshima yake (Yaani haramu kuchukua mali ya mwenzako, kumuua na kumdhalilisha) [Imesimuliwa na Muslim]





Husda hiyo huenda imamdhuru mtu akafikwa na maovu, kama kupungukiwa na hizo neema, au kupata maafa au kuumwa au aina yoyote ya mashaka. Ndio maana tumefunzwa adhkaar za kila aina ambazo zina kinga ya kutuhifadhi na kila aina ya maovu pamoja na husda. Inapomfika mtu hali hiyo inampasa ajitibu kwa Ruqyah (kinga) zenye mafunzo kutoka Qur-aan na Sunnah kama ifutavyo:



Kusoma Qur-aan kwa wingi kwani Qur-aan ni uongofu, nuru, poza na tiba ya nyoyo na mwili.


Aayah tano za mwanzo katika Suratul-Baqarah.


Aayatul-Kursiy na Aayah mbili zinazofuatia.


Aayah mbili za mwisho katika Suratul-Baqarah.


Kusoma Suratul-Ikhlaasw (Qul-Huwa Allaahu Ahad) na Al-Ma'udhaataan (Qul-A'uudhu Birbbil-Falaq na Qul-A'uudhu Birabbin-Naas) mara tatu kila asubuhi na jioni.




Nyiradi za asubuhi na jioni zilioko katika kitabu cha


Hiswnul-Muslim: Du’aa Na Adhkaar Kusoma Na Kwa Kusikiliza (Toleo Lilohaririwa)





027-Hiswnul-Muslim: Nyiradi Za Asubuhi Na Jioni



Hizi pekee zinamtosheleza mtu kumkinga na kumtoa katika husda na kila aina ya shari ikiwa atazidumisha kila siku ipasavyo. Lakini wengi hawalitii manani hili jambo muhimu la kujikinga na pia kujipatia neema nyingi, na jambo ambalo hata halimchukui mtu zaidi ya dakika kumi. Wanasubiri hadi mtu yamfike maovu ndipo anapoanza kuhangaika.



Bonyeza upate du'aa pia:



035-Hiswnul-Muslim: Du’aa Unapopatwa Janga Au Balaa





Na Allaah Anajua zaidi
 
Itakuwa Ni Nadhiri Akisema Moyoni Kuwa Atampa Mtoto Jina La Aliyefariki Kisha Asimpe?
Maswali: familia-Jamii
SWALI:



Assalamu alaikum, nina suali langu ambalo nataka kuliza, hivi karibuni tulitoewa na msiba wa mtoto mdogo wa miaka sita. baada ya siku mbili tatu hivi, nikafikiria tu mimi mwenyewe kuwa nikipata mtoto nitamwita jina lake, ikiwa mpaka hapo hakuna yeyote ambaye ashalita jina hilo. lakini sikumwambiya mtu yoyote. je, kwa mfano ikiwa nimepata mtoto na mimi nataka kuita jina lengine inafaa? tafadhali ni jibu. Ahsantum.









JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako la kumpatia mtoto wako jina.

Hakika suala la kufikiria kitu au kukipanga ni suala la kawaida kabisa ambalo humtokea kila mmoja wetu.







Hiyo si nadhiri, kwani nadhiri unaielekeza kwa Allaah Aliyetukuka kwa kumwambia nikipata mtoto, nitafanya jambo kadhaa. Ikiwa hukuweka Niyah hiyo kutakuwa hakuna tatizo la kubadilisha jina lake atakapo zaliwa au kumuita jina hilo hilo.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Jirani Kafiri Anatubughudhi Sana Tumuombee Du’aa Gani?
Maswali: familia-Jamii
SWALI:



Assalaam alaykum,



Nina jirani ambae anatubughudhi

sana (SI MUISLAMU) mimi na aila yangu kwa muda mrefu sasa. tumejaribu kila mbinu kuzungumza nae aachane na maovu na pia kutubughudhi lakini nimeshindwa. Anaonekana kushinda kila wakati tukitaka kimshitaki mbele ya serekali. Tumekosa raha, tunapata maradhi kwa ajili yake.

Kuna dua ya kumuomba Allaah atusaidie, mtume (saw) najuwa alibughudhiwa sana, alikuwa na dua maalum akisoma??? hili ni tatizo kubwa sana ambalo linaharibu familia yetu kiasi kikubwa sana. Tafadhali tupe mawazo





JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Mtume, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.) kama ilivyozoelekea na wengi, bali andika kwa kirefu maneno hayo bila ya kuyafupisha. Andika (Subhaanahu wa Ta’ala) baada ya kumtaja Allaah, na andika Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) au (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kumtaja Mtume. Hivyo ndivyo inavyopaswa, na ndio heshima zaidi na utukufu na ndivyo inavyotamkwa na si kama inavyofupishwa na wengi kimazoea na kivivu.





Shukrani zetu kwako ewe ndugu yetu kwa swali lako. Hakika ni kuwa mitihani ni jambo la kawaida kwa mwanaadamu na hasa Waislamu. Hili ni jambo ambalo haliwezi kukosekana katika maisha ya mwanaadamu katika dunia hii. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anatuelezea: “Hakika jazaa kubwa ni pamoja na mtihani na misukosuko, na hakika Allaah Aliyetukuka Anapoipenda kaumu huipatia mtihani” [At-Tirmidhiy, aliyesema kuwa ni Hadiyth nzuri (Hasan)].



Na Allaah Aliyetukuka Anasema:



((أَحَسِبَ النَّاسُ أَن يُتْرَكُوا أَن يَقُولُوا آمَنَّا وَهُمْ لَا يُفْتَنُونَ))

((وَلَقَدْ فَتَنَّا الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَلَيَعْلَمَنَّ اللَّهُ الَّذِينَ صَدَقُوا وَلَيَعْلَمَنَّ الْكَاذِبِينَ))



((Je, mwanaadamu anadhani ataachwa tu kwa kusema kuwa nimeamini naye hajapatiwa mtihani?))



(Hakika Tumewapatia mitihani na kuwatia katika taabu waliokuwa kabla yenu, na kwa yakini Allaah Atawatambulisha wale walio wakweli na wale walio waongo)) [Ar-Ruum: 29: 2 – 3].





Vilevile Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ametuhimiza tumfanyie wema jirani katika Aayah kadhaa, Anasema:



((وَاعْبُدُواْ اللّهَ وَلاَ تُشْرِكُواْ بِهِ شَيْئًا وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَبِذِي الْقُرْبَى وَالْيَتَامَى وَالْمَسَاكِينِ وَالْجَارِ ذِي الْقُرْبَى وَالْجَارِ الْجُنُبِ وَالصَّاحِبِ بِالجَنبِ وَابْنِ السَّبِيلِ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ إِنَّ اللّهَ لاَ يُحِبُّ مَن كَانَ مُخْتَالاً ))



((Muabuduni Allaah wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Hakika Allaah Hawapendi wenye kiburi wanao jifakhiri)) [An-Nisaa: 36]



Tunaona kwamba kumfanyia wema khaswa jirani aliye karibu na ndipo Mama wa Waumini 'Aishah (Radhiya Allaahu 'anha) alipomuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kutaka kujua yupi jirani mwenye haki zaidi naye:



عن عائشة رضي الله عنها وقالت له: ((يا رسول الله! إن لي جارين فإلى أيهما أهدي؟ قال: إلى أقربهما منك باباً)) رواه البخاري



Kutoka kwa Mama wa waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anhaa) aliuliza: "Ee Mjumbe wa Allaah, nnao jirani wawili, yupi miongoni mwao nimpe zawadi" Akanijibu: ((Aliye karibu na mlango wako [aliye karibu zaidi])) [Al-Bukhaariy]



Kuwa na jirani muovu ni mojawapo ya mitihani migumu. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akahimiza sana mtu kumtendea wema jirani yake kwani kutendana maovu kutaleta vurugu na ukosefu wa amani. Wema huu Muislamu anatakiwa amtendee kila jirani ikiwa ni Muislamu au si Muislamu. Miongoni mwa kauli yake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni:



((من كان يؤمن بالله واليوم الآخر فليحسن إلى جاره)) البخاري و مسلم



((Yeyote mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho basi amkirimu jirani yake)) [Al-Bukhaariy na Muslim].



Miongoni mwa njia bora za kuweza kuvunja makali ya adui ni kusuburi, kutenda mema, kutekeleza 'Ibaadah, na kumtendea wema huyo adui mbali na yale maovu anayokufanyia. Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Anasema:



((وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِّمَّن دَعَا إِلَى اللَّهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِينَ))

(( وَلَا تَسْتَوِي الْحَسَنَةُ وَلَا السَّيِّئَةُ ادْفَعْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ فَإِذَا الَّذِي بَيْنَكَ وَبَيْنَهُ عَدَاوَةٌ كَأَنَّهُ وَلِيٌّ حَمِيمٌ))

((وَمَا يُلَقَّاهَا إِلَّا الَّذِينَ صَبَرُوا وَمَا يُلَقَّاهَا إِلَّا ذُو حَظٍّ عَظِيمٍ))



((Na ni nani asemaye kauli bora zaidi kuliko aitaye kwa Allaah na mwenyewe kafanya vitendo vizuri na akasema: ‘Hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu’.))



((Mambo mazuri na mabaya hayawi sawa. Ondosha ubaya unaofanyiwa kwa mema, tahamaki yule ambaye baina yako na yake kuna uadui atakuwa kama ni jamaa yako mwenye kukufia uchungu))



((Lakini jambo hili hawatopewa ila wale wanaosubiri, wala hawatapewa ile wenye hadhi kubwa)) [Fusw-swilat 41: 33 – 35].



Anasema tena Aliyetukuka:



((وَاسْتَعِينُواْ بِالصَّبْرِ وَالصَّلاَةِ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلاَّ عَلَى الْخَاشِعِينَ))



((Na jisaidieni katika mambo yenu kwa kusubiri na kwa kuswali, na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu)) [Al-Baqarah 2: 45).



Kama ulivyotaja kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alibughudhiwa na kuteswa kwa kiasi kikubwa kuliko mtu mwengine yeyote lakini alivumilia na mwishowe aliweza kuwateka mahasimu wake wakubwa kama kina Abuu Sufyaan, Hind bint 'Utbah na wengineo na baada ya hapo wakawa wafuasi wake wakuu. Usikate tamaa kabisa kwani ushindi itakuwa ni wako dhidi yake leo au kesho.



Msijitie maradhi kabisa kuhusu suala hilo bali mfanyieni wema na mpuuze maudhi yake kwa kuyafanya si lolote si chochote. Jaribuni tena kumfanyia wema kwa kumpelekea hadiya, mzuruni akiwa na msiba au mgonjwa na kadhalika. lakini kwa sharti la kumlingania aingie kwenye Dini ya Haki, kama alivyofanya Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokwenda kumzuru yule mtoto wa Kiyahudi aliyekuwa akimbughudhi kila mara, na alipomzuru alimlingania aingie kwenye Uislamu.



Ikiwa yote hayo hayakufaa kitu basi someni du’aa zifuatazo aliyotufundisha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



1-Du'aa ifuatayo aliyokuwa akijinga na jirani muovu kama alivyokuwa akiomba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

((اللهم إني أعوذ بك من جار السوء في دار المقامة، فإن جار البادية يتحول)) حديث صحيح، رواه ابن حبان، والحاكم وصححه الذهبي والألباي

((Allaahumma Inniy audhu Bika min jaaris-suu fiy daaril-muqaamah, fainna jaaral-baadiyah yatahawwal

[Ee Allaah, najikinga Kwako na jirani muovu katika makazi ya kudumu kwani jirani wa jangwani hubadilika badilika kuhama)) [Hadiyth Swahiyh aliyosimulia Ibn Maajah, Al-Haakim na akaipa daraja ya Swahiyh Shaykh al-Albaaniy]





2- Vile vile alikuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiomba:



اللهم إني أعوذ بك من يوم السوء، ومن ليلة السوء، ومن ساعة السوء، ومن صاحب السوء، ومن جار السوء في دار المقامة .

((Allaahumma Inniy audhu Bika min yawmis-suu, wa min laylatis-suu, wa min saa'atis-suu, wa min swaahibis-suu, wa min jaaris-suu fiy daaril-muqaamah

Ee Allaah najikinga Kwako na siku ovu, na usiku muovu, na saa ovu, na rafiki muovu, na jirani muovu katika makazi ya kudumu))



3- Na du'aa ifutayo (japo Wanachuoni wametofautiana usahihi wake) ambayo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliisoma aliporudi kutoka Twaaif baada ya kupata maudhi na watu wa mji huo, kwa kumpiga mawe, kumtukana na kumfukuza:



اَلَّلهُمَّ إِنِّي أَشْكُو إِلَيْكَ ضَعْفَ قُوَّتِي, وَقِلَّةَ حِيْلَتِي, وَهَوَانِي عَلَى النَّاسِ, يَا أَرْحَمَ الرَّاحِمِين, أَنْتَ رَبُّ الْمُسْتَضْعَفِينَ وَاَنْتَ رَبّي إِلَى مَنْ تَكِلْنِي؟ إِلَى بَعِيدٍ يَتَجَهَّمُنِي أَمٍ إِلَى عَدُوٍ مَلَّكْتَهُ أَمْرِي؟ إِنْ لَمْ يَكُنْ بِكَ غَضَبٌ عَلَىَّ فَلاَ أُبَاِلي، وَلَكِنَّ عَافِيَتَكَ أَوْسَعُ لِي مِنْ ذُنُوبِي, أَسْأَلُكَ بِنُورِ وَجْهِكَ الَّذِي أَشْرَقَتْ لَهُ الظُّلُمَاتُ، وَصَلَحَ عَلَيْهِ أَمْرُ الدُّنْيَا وَالأَخِرَةِ مِنْ أَنْ يُنْزِلَ عَلَيَّ غَضَبُكَ أَوْ يَحِلُّ عَلَىَّ سَخَطُُكَ وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِكَ

((Allaahumma Inniy Ashkuu Ilayka Dhwa'fa Quwwatiy, Wa Qillata Hiylatiy, Wa Hawaaniy 'Alan-Naas. Yaa Arhamar-Raahimiyn. Anta Rabbul-Mustadhw'afiyn, Wa Anta Rabbiy Ilaa Man Takilniy? Ilaa Ba'iydin Yatajahhamuniy? Am Ilaa 'Aduwwim-Mallaktahu Amriy? In-lam Yakun Bika Ghadhwabun 'Alayya Falaa Ubaaliy, Wa Laakin 'Aafiyataka Awsa'u Liy Min Dhunuubiy. As-aluka Binuuri Wajhika-lladhiy Ashraqat Lahudh-Dhwulumaat, Wa Swalaha 'Alayhi Amrud-Duniyaa Wal-Aakhiratiy Min Ay-yunzila 'Alayya Ghadhwabuka Aw Yahillu 'Alayya Sakhatwuka, Wa Laa Hawlaa Walaa Quwwata Illaa Bik.

Ya Allaah, Kwako peke Yako nalalamika udhaifu wa nguvu zangu, na uchache wa uwezo wangu na unyonge wangu (wa kukabili adha) za watu. Wewe Ndiye Mwenye wingi wa Rehma na wingi wa Huruma na Upole.

Wewe ni Mola wa wasiojiweza na wadhaifu. Nawe ni Mola Wangu. Unanitupa kwenye mikono ya nani (atakayenisaidia)? Kwenye mikono ya jamaa yangu aliye mbali na asiye na huruma na mimi? Ambaye ananihamakia kwa chuki na kunidharau? Au kwenye adui aliyepewa utawala juu ya mambo yangu? Lakini kama ghadhabu Yako haitoanguka kwangu au haitonifikia basi hakuna kitu nitakachojali. Na hakika msamaha Wako ni mkubwa kuliko dhambi zangu.

Nakuomba kutokana na Nuru ya Wajihi Wako, ambayo inaangazia mbingu na inaondoa kiza na kutawala mambo yote ya dunia na akhera ili hasira Yako isinifikie au ghadhabu Yako isiniangukie. Na hakuna mamlaka wala nguvu na uwezo ila Wako peke Yako.))



Pia omba usaidizi kwa kukithirisha du’aa baada ya kila Swalah, unapoinuka usiku kwa Tahajjud na katika mwezi huu wa Ramadhwaan unapokuwa katika Swawm.



Ikiwa hukupata afueni lakini kwa njia hizo za kumtegemea Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) bila shaka utapata nafuu kubwa. Lakini ikiwa kinyume utambue kuwa huo ni mtihani mwingine kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala), hivyo itabidi labda uamue kuhama sehemu hiyo.

Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Akusahilishie tatizo hilo na Akutolee njia muafaka, Aamiyn.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Kadi Za Michango Na Kadi Za Mialiko Katika Ndoa Za Kiislam
Maswali: familia-Jamii


SWALI:

Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakaatuh.
ndugu mpendwa katika imani naomba nipatiwe ufumbuzi wa kina wa kisheria juu ya suala la kutoa kadi kwa ajili ya michango au mualiko katikandoa za kiiislam. Je suala hili lina nafasi gani kwa mujibu wa kitabu na sunnah


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu kwa swali lako hili zuri kuhusu mambo hayo mawili. Hili ni suala ambalo limezua tatizo kwa sababu limekosa ule msingi kuwa jambo hilo halikuwepo wakati wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake baada yake.

Huenda wengine wakapinga mambo ya kuchapisha kadi za michango au harusi kwa kutoa dalili ifuatayo. Imepokewa kwa Mama wa Waumini, Ummu 'Abdillaah 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

"Mwenye kuzua katika hili jambo (Dini) letu lisikuwamo humo litakataliwa" (al-Bukhaariy na Muslim). Katika riwaya nyengine ya Muslim: "Mwenye kufanya amali isiyokuwa na hukumu yetu, itakataliwa".

Hivyo, hizi riwaya mbili zinaonyesha kuwa kuzua amali au kuzua maneno katika Dini, ni mambo yasiyokubalika.

Hadiyth hii ieleweke inabidi tueleze baadhi ya ibara ili ifahamike vyema. ‘Kuzua’ ni kuanzisha kitu kwa mtu kupenda mwenyewe na kufuata hawaa yake tu. ‘Katika jambo hili letu’ ina maana katika Dini na Shari 'ah yetu aliyotuchagulia Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala). ‘Lisilokuwamo humo’ ina maana lenye kupingana na kutokubaliana na Shari'ah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) na jambo ambalo halina ushahidi wala dalili yoyote ya kuafikiana na misingi ya Dini. Mwenye kufanya hivyo jambo hilo litakataliwa na halitakubaliwa kabisa. Haya ni mambo ambayo yanafungamana moja kwa moja na Dini na Shari'ah.

Ama mambo ambayo yanahusiana na dunia yetu hayo ni mambo yanayopendeza katika Dini yakiwa mazuri na kuweka nidhamu muruwa na barabara. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipofika Madiynah aliwakuta watu wake wakichavusha mitende yao kwa kutumia chembe za chavua. Akawauliza kwanini wanafanya hivyo? Mwaka huo mazao yakawa kidogo sana, naye (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akawauliza sababu ya hilo. Wao wakamjibu kwa kumwambia: "Sisi tulikuwa tunachavusha mitende nawe ukatukataza, na hii ndio natija". Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akawaambia: "Nyinyi mnajua vyema mambo ya dunia yenu".

Tukiyapigia darubini mas-ala haya ya kadi utaona kwamba yana uzuri wake na ubaya wake:

Kuhusu Kadi za Michango

Ni kupatikana maslahi kwa jamii yetu baada ya kuvurugika katika ufisadi na ulaji wa pesa kwa njia za haramu. Maslahi kwa jamii ni jambo muhimu sana ikiwa haitakwenda kinyume na Shari’ah na Dini. Mara nyingi watu wanaokusanya pesa kwa njia isiyokuwa ya kadi labda wawe waaminifu sana lakini huwa hawapeleki pesa zote kwa mradi wanaoukusanyia pesa. Nyingine wanakula na nyingine wanapeleka, lakini kwa sababu ya kutoa kadi imeondoa ufisadi mwingi sana hivyo kuwa ni maslahi kwa miradi na jamii.

Kuhusu kadi za Mwaliko wa Ndoa

Kadi katika harusi zimekuja kwa kutokea vurugu kwa watu ambao hawakualikwa au kuleta aibu kwa chakula kutotosha kwa sababu ya watu ambao wamekwenda bila kualikwa. Kwa hiyo, wenye harusi wanatoa kadi ili kudhibiti wasioalikwa kuingia katika Waliymah (Karamu ya Ndoa).
Imepokewa na Ibn ‘Umar kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Yeyote asiyekubali mwaliko amemuasi Allaah na Mtume Wake, na mwenye kuingia bila kualikwa anaingia kama mwizi na kutoka katika sehemu hiyo kama mvamizi” (Abu Daawuud).
Pia waalikwa wengi wanakiuka agizo la Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambalo ni mtu akialikwa basi ajibu mwito kama tunavyozinukuu hapa dalili kutoka katika Sunnah:


Kwanza:

((فُكُّوا الْعَانِيَ، وَأَجِيبُوا الدَّاعِيَ، وَعُودُوا الْمَرِيضَ))

((Acheni huru wafungwa, itikieni (kubalini) mwaliko na tembeleeni wagonjwa)) [AL-Bukhaariy]

Pili:

((إِذَا دُعِيَ أَحَدُكُمْ إِلَى الْوَلِيمَةِ فَلْيَأْتِهَا عَرْساً كَان أَوْ نَحْوه وَمَنْ لَمْ يُجِبِ الدَّعْوَةَ، فَقَدْ عَصَى اللّهَ وَرَسُولَهُ))

((Anapoalikwa mmoja wenu katika karamu, basi ahudhurie, ikiwa ni karamu ya harusi au nyingineyo. Na yeyote asiyeitikia (asiyekubali) mwaliko basi atakuwa amemuasi Allaah na Mtume Wake)) [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]
lakini kwa sababu ya vurugu au maasi yanayokuwemo katika baadhi ya sherehe za Ndoa ndizo zinasababisha mtu asiitikie mwaliko, na anapofanya hivyo mtu katika hali hiyo, huwa hatumbukii katika hukumu za Hadiyth hizo hapo juu kwa sababu Muislam haruhusiwi kushiriki shughuli zozote zenye maasi.

Ubaya wake:

Baadhi ya watu hufanya israaf katika kutengeneza hizo kadi. Wengine huwa ni kutaka kushindana kutengeneza kadi iliyokuwa nzuri kabisa na yenye gharama ya juu, wakati hiyo gharama ya hizo kadi angeliweza mwenye Waliymah kuwaalika watu wengine ambao ni masikini. Aghlabu wanaoalika kwa kadi hupendelea kualika matajiri na kuwasahau masikini jambo ambalo linakwenda kinyume na maagizo ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokataza kualika matajiri pekee na kupendelea masikini pia waalikwe:

((شَرُّ الطَّعَامِ طَعَامُ الْوَلِيمَةِ يُدْعَىٰ لَهَا الأَغْنِيَاءُ وَيُتْرَكُ الْمَسَاكِينُ، وَمَنْ لَمْ يَجِبْ الدَّعْوَةَ فَقَدْ عَصَىٰ اللَّهَ وَرَسُولَهُ)).

((Chakula kiovu kibaya kabisa ni chakula cha karamu ya harusi ambayo wamealikwa matajiri na kutengwa kando masikini. Yeyote atakayekataa mualiko atakuwa amemuasi Allaah na Mtume Wake))[Muslim na Al-Bayhaqiy]

Ubaya mwingine ni kuwa hizo kadi nyingine huwa za kuchorwa picha za viumbe mfano bwana harusi na bibi harusi. Dini yetu imetukataza kuchora picha za viumbe wenye roho.

Pamoja na kuwa kuwepo na nidhamu ya kualika watu kwa kadi kumekuwa na maslahi pamoja na nidhamu kwa karamu hizo, lakini wengi hawatumii njia hizo vizuri na huchukua fursa hiyo ya kualika watu kwa kadi ili waweze kualika tu wale wanaowataka wao ima kwa ujamaa, ukabila, uhali wa kijamii kama ni wafanyabiashara wenzake, au wafanyakazi wenzake tu, au wanaofanana naye kihali ya kijamii n.k. na kuacha kualika maskini na mafakiri kama alivyohimiza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Wanaofanya hivyo wanapaswa wamche Allaah na waache tabia hizo ambazo haziendani na uzuri wa Uislam.
Kwa hivyo, kisheria, hakuna tatizo lolote kwa watu kutoa kadi kwa ajili ya michango au Waliymah (karamu) maadam kutafuatwa taratibu za kisheria na hakutakiukwa ndani yake mafunzo ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

Na Allaah Anajua zaidi
 
Kaka Amempiga Dada Yake, Nini Hukmu Yake?
Maswali: familia-Jamii
SWALI:



Assalaam aleykum

Kaka kampiga dada yake (wote wawili ni watu wazima). Mama ana uchungu sana kwa hicho kitendo. Je kisheria hili tatizo litatuliwe vipi? Tafadhali nipe dalili kutoka Quran na sunnah





JIBU:





Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kaka kumpiga dadake.

Inatakiwa tufahamu kuwa yule anayefaa kupigwa ni mtoto mdogo kabla hajafika umri wa miaka kumi kwa mujibu wa wanachuoni kuichukua Hadiyth ifuatayo.

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameusia:

“Wafundisheni watoto wenu Swalah wakiwa na miaka saba na wapigeni wakiacha kuswali wakiwa na miaka kumi” (Abu Daawuud).

Hivyo, mtu akishapita miaka kumi haifai kupigwa ila awe ni mke wa mtu aliyekengeuka na maamrisho ya Uislamu. Hata hivyo, haifai kumpiga hata mtumwa kipigo cha kumuumiza wala kulenga uso.



Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametabiri kuwa kutakuja wakati ambapo wanaume watakuwa wanawapiga wanawake, nao watakuwa ni watu wa Motoni. Akasema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

“Watu aina mbili ni katika wakaazi wa Motoni ambao sijawaona: Watu wenye viboko kama mikia ya ng’ombe nao watakuwa wanawapigia watu…” (Muslim).



Jambo ambalo linatakiwa lifanywe na familia sasa, baba akiwepo achukue jukumu la kuwakutanisha wahusika ili kufanywe suluhu ili jambo hilo lisitokee tena. Na katika suluhu lazima kupatikane chanzo cha tatizo lenyewe, na kutoka hapo upatikane ufumbuzi. Hata ikiwa dada ni mkosa inatakiwa huyo kaka aelezwe kuwa hatua ya kupiga imepita mipaka ya kishari’ah. Na Allaah Aliyetukuka Anasema:

“Na suluhu ni bora”.

Pia,

“Hakika Waumini wote ni ndugu, suluhisheni baina ya ndugu zenu na mcheni Allaah ili mpate kurehemewa” (al-Hujuraat [49]: 10).



Na Allaah Anajua zaidi
 
Skip to main content

Ukurasa Wa Kwanza
Search form
Tafuta
Submit
Ukurasa



Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno



04- Shirki Inabatilisha ‘Amali




Alhidaaya.com





‘Amali za Muislamu bila ya kuwa na niyyah safi kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) au ikhlaasw, huwa hazina thamani mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa dalili zifuatazo:



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



وَقَدِمْنَا إِلَىٰ مَا عَمِلُوا مِنْ عَمَلٍ فَجَعَلْنَاهُ هَبَاءً مَّنثُورًا ﴿٢٣﴾

Na Tutayaendea yale waliyoyatenda ya ‘amali yoyote ile, Tutayafanya chembechembe za vumbi zinazoelea hewani zinazotawanyika. [Al-Furqaan: 23]



Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَلَقَدْ أُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ﴿٦٥﴾

Kwa yakini umefunuliwa Wahy na kwa wale walio kabla yako kwamba: “Ukifanya shirki bila shaka zitaporomoka ‘amali zako na bila shaka utakuwa miongoni mwa waliokhasirika.” [Az-Zumar: 65]



Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٨٨﴾

Na kama wangemshirikisha bila shaka yangeporomoka yale waliyokuwa wakitenda. [Al-An’aam: 88]







Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametaja katika Hadiyth Al-Qudsiy:





عنْ ابي هريرة رضي الله عنه أنَّه صلَّى الله عليه وسلَّم قال: ((قال الله تعالى: أنا أغْنى الشُّركاء عن الشِّرْك، فمَن عمل عملاً أشْرَك فيه معي غيري تركتُه وشِرْكه))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Allaah Ta’aalaa Anasema: ‘‘‘‘Mimi Ni Mwenye kujitosheleza kabisa, Sihitaji msaada wala mshirika. Kwa hiyo, yule afanyaye amali kwa kunishirikisha na mtu, Nitaikanusha pamoja na mshirika wake.” Yaani: hatopata ujira wowote kwa amali hiyo. [Muslim (2985), Ibn Maajah (4202)]





Mfano bayana wa kubatilika ‘amali za mtu kwa anayetoa swadaqah kwa riyaa ni kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُم بِالْمَنِّ وَالْأَذَىٰ كَالَّذِي يُنفِقُ مَالَهُ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ صَفْوَانٍ عَلَيْهِ تُرَابٌ فَأَصَابَهُ وَابِلٌ فَتَرَكَهُ صَلْدًا ۖ لَّا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَيْءٍ مِّمَّا كَسَبُوا ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٢٦٤﴾

Enyi walioamini! Msibatilishe swadaqah zenu kwa masimbulizi na udhia kama yule ambaye anatoa mali yake kwa kujionyesha kwa watu wala hamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Basi mfano wake ni kama jabali juu yake pana udongo, kisha likapigwa na mvua kubwa ikaliacha tupu. Hawana uwezo juu ya lolote katika waliyoyachuma. Na Allaah Haongoi watu makafiri. [Al-Baqarah: 264]
 
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ



Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!



05-Hatima Ya Mwenye Riyaa (Kujionyesha)




Alhidaaya.com







Juu ya kuwa ‘amali za mtu zinabatilika kwa sababu ya riyaa, vile vile hatima ya mwenye riyaa ni mbaya mno!



Mwenye kudhihirisha ‘amali zake kwa riyaa atafedheheshwa Siku ya Qiyaamah kwa dalili Hadiyth ifuatayo:



عَنْ جُنْدَبِ بْنِ عَبْدُ الله بْنِ سُفْيانَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَنْ سَمَّعَ سَمَّعَ اللَّهُ بِهِ وَمَنْ رَاءَى رَاءَى اللَّهُ بِهِ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Jundab bin ‘Abdillaah bin Sufyaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: “Nabiy Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema:

“Mwenye kuzungumza (au kusoma) ili watu wamsifu, Allaah Atamfedhehesha Siku ya Qiyaamah, na mwenye kuwafanyia watu riyaa (kwa amali njema ili aonekane ni mtukufu), Allaah Atazidhihirisha siri zake (Siku ya Qiyaamah).” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Mtu huyo mwenye riyaa hatosikia harufu ya Jannah:



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَنْ تَعَلَّمَ عِلْمًا مِمَّا يُبْتَغَى بِهِ وَجْهُ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ لَا يَتَعلَّمُهُ إِلَّا لِيُصِيبَ بِهِ عَرَضًا مِنْ الدُّنْيَا لَمْ يَجِدْ عَرْفَ الْجَنَّةِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يَعْنِي رِيحَهَا.

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) amesema: ((Yeyote anayejifundisha elimu ambayo anapaswa kuitumia kwa ajili ya Allaah, (kisha akaitumia) kwa ya kupata manufaa ya kidunia hatonusa harufu ya Jannah Siku ya Qiyaamah)) [Abu Daawuwd (3656), Ibn Maajah (255) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Abiy Daawuwd (3664)]





Mwenye kuswali kwa riyaa atapata maangamizi. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



فَوَيْلٌ لِّلْمُصَلِّينَ ﴿٤﴾

Basi Ole kwa wanaoswali ...





الَّذِينَ هُمْ عَن صَلَاتِهِمْ سَاهُونَ ﴿٥﴾

Ambao wanapuuza Swalaah zao.



الَّذِينَ هُمْ يُرَاءُونَ ﴿٦﴾

Ambao wanajionyesha (riyaa). [Al-Maa’uwn: 4-6]





Watu watatu wa kwanza kuhesabiwa Siku ya Qiyaamah ni: aliyekufa Shahidi, ‘Aalim (aliyejifunza Dini na Qur-aan) aliyetoa mali yake katika njia ya Allaah. Lakini ambaye ameingiza riyaa katika ‘amali hizi basi ataingizwa Motoni:



عَنْ أبي هريرة رضي الله عنه قال: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهم عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ ((إِنَّ أَوَّلَ النَّاسِ يُقْضَى يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَيْهِ رَجُلٌ اسْتُشْهِدَ فَأُتِيَ بِهِ فَعَرَّفَهُ نِعَمَهُ فَعَرَفَهَا قَالَ: فَمَا عَمِلْتَ فِيهَا؟ قَالَ: قَاتَلْتُ فِيكَ حَتَّى اسْتُشْهِدْتُ، قَالَ: كَذَبْتَ وَلَكِنَّكَ قَاتَلْتَ لِأَنْ يُقَالَ جَرِيءٌ فَقَدْ قِيلَ ثُمَّ أُمِرَ بِهِ فَسُحِبَ عَلَى وَجْهِهِ حَتَّى أُلْقِيَ فِي النَّارِ، وَرَجُلٌ تَعَلَّمَ الْعِلْمَ وَعَلَّمَهُ وَقَرَأَ الْقُرْآنَ فَأُتِيَ بِهِ فَعَرَّفَهُ نِعَمَهُ فَعَرَفَهَا قَالَ: فَمَا عَمِلْتَ فِيهَا؟ قَالَ: تَعَلَّمْتُ الْعِلْمَ وَعَلَّمْتُهُ وَقَرَأْتُ فِيكَ الْقُرْآنَ، قَالَ: كَذَبْتَ وَلَكِنَّكَ تَعَلَّمْتَ الْعِلْمَ لِيُقَالَ عَالِمٌ وَقَرَأْتَ الْقُرْآنَ لِيُقَالَ هُوَ قَارِئٌ فَقَدْ قِيلَ ثُمَّ أُمِرَ بِهِ فَسُحِبَ عَلَى وَجْهِهِ حَتَّى أُلْقِيَ فِي النَّارِ، وَرَجُلٌ وَسَّعَ اللَّهُ عَلَيْهِ وَأَعْطَاهُ مِنْ أَصْنَافِ الْمَالِ كُلِّهِ فَأُتِيَ بِهِ فَعَرَّفَهُ نِعَمَهُ فَعَرَفَهَا قَالَ: فَمَا عَمِلْتَ فِيهَا؟ قَالَ: مَا تَرَكْتُ مِنْ سَبِيلٍ تُحِبُّ أَنْ يُنْفَقَ فِيهَا إِلَّا أَنْفَقْتُ فِيهَا لَكَ قَالَ كَذَبْتَ وَلَكِنَّكَ فَعَلْتَ لِيُقَالَ هُوَ جَوَادٌ فَقَدْ قِيلَ ثُمَّ أُمِرَ بِهِ فَـسُحِبَ عَـلَى وَجْهِهِ ثُمَّ أُلْقِيَ فِي النَّارِ ))

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi sallam) akisema: ((Wa mwanzo kuhesabiwa Siku ya Qiyaamah ni mtu aliyekufa shahidi katika vita, ataletwa na kujulishwa neema alizoneemeshwa na baada ya kuzijua ataulizwa (na Allaah): “Umezifanyia kazi gani neema hizi?” Atasema: “Nimepigana jihaad kwa ajili Yako mpaka nikafa shahidi.” Ataambiwa: “Umesema uongo, bali ulipigana ili isemwe kuwa wewe ni jasiri na imeshasemwa.” Kisha itaamrishwa abururwe kwa uso wake na kuingizwa Motoni. Na mtu (mwengine) 'Aalim aliyejifundisha Dini akaijua vizuri, akasoma na Qur-aan, ataletwa na kujulishwa neema alizoneemeshwa, kisha ataulizwa; “Umezifanyia kazi gani neema hizi?” Atasema: “Nimejifunza elimu nikafundisha na kwa ajili Yako nikasoma Qur-aan.” Ataambiwa: “Umesema uongo, bali ulijifunza elimu ili isemwe kuwa wewe ni ‘Aalim. Ukasoma Qur-aan ili isemwe kuwa wewe ni msomaji (mzuri), na imeshasemwa.” Kisha itaamrishwa abururwe kwa uso wake na kuingizwa Motoni. Na mtu (mwengine) Allaah Amempa wasaa, akampa kila aina ya mali, ataletwa na kujulishwa juu ya neema alizoneemeshwa, kisha ataulizwa: “Umezifanyia kazi gani neema hizi?” Atasema: “Sijaacha njia Unayopenda mtu atoe katika mali yake ila mimi nimetoa kwa ajili Yako.” Ataambiwa: “Umesema uongo, bali umetoa ili isemwe kuwa wewe ni mkarimu na imeshasemwa. Kisha itaamrishwa abururwe kwa uso wake na kuingizwa Motoni”. [Muslim]
 
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ



Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!



06- Shirki Ni Miongoni Mwa Al-Kabaair (Madhambi Makubwa)







Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا ﴿٤٨﴾

Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa; lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amezua dhambi kuu. [An-Nisaa: 48]



Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا﴿١١٦﴾

Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa; lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amepotoka upotofu wa mbali. [An-Nisaa: 116]





Na Hadiyth za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam):



((ألاَ أُنبِّئكم بأكبرِ الكبائر؟ الإشراك بالله)) متفق عليه.

((Je, hivi nikujulisheni madhambi makubwa kabisa? Ni kumshirikisha Allaah)) [Al-Bukhaariy, Muslim]



Na pia Hadiyth:



عَنْ أبي أيوب الأنصاري رضي الله عنه انَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((مَنْ جَاءَ يَعْبُدُ اللَّهَ وَلاَ يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا وَيُقِيمُ الصَّلاَةَ وَيُؤْتِي الزَّكَاةَ وَيَجْتَنِبُ الْكَبَائِرَ كَانَ لَهُ الْجَنَّةُ)).‏ فَسَأَلُوهُ عَنِ الْكَبَائِرِ فَقَالَ‏: ((الإِشْرَاكُ بِاللَّهِ وَقَتْلُ النَّفْسِ الْمُسْلِمَةِ وَالْفِرَارُ يَوْمَ الزَّحْفِ)).‏

Imepokelekewa kutoka kwa Abuu Ayyuwb Al-Answaariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayekuja akiwa anamwambudu Allaah wala hamshirikishi na chochote, na anasimamisha Swalaah, na anatoa Zakaah, na anajiepusha na Al-Kabaair (madhambi makubwa) atapata Al-Jannah)) Wakamuuliza kuhusu Al-Kabaair akasema: ((Kumshirkisha Allaah na kumuua Muislamu, na kukimbia (vita) siku ya mapambano (vita).)) [An-Nasaaiy (4009) na ameisahihisha Al-Albaaniy]



Na shirki ni katika mambo saba yanayoangamiza:



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه (عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((اجْتَنِبُوا السَّبْعَ الْمُوبِقَاتِ)) قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ وَمَا هُنَّ؟ قَالَ: ((الشِّرْكُ بِاللَّهِ وَالسِّحْرُ وَقَتْلُ النَّفْسِ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلاَّ بِالْحَقِّ وَأَكْلُ الرِّبَا وَأَكْلُ مَالِ الْيَتِيمِ وَالتَّوَلِّي يَوْمَ الزَّحْفِ وَقَذْفُ الْمُحْصَنَاتِ الْمُؤْمِنَاتِ الْغَافلاَتِ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Jiepusheni na mambo saba yanayoangamiza!)) Wakauliza: Ni yepi hayo ee Rasuli wa Allaah? Akawaambia: ((Ni kumshirikisha Allaah, sihri [uchawi], kuua nafsi Aliyoiharamisha Allaah isipokuwa kwa haki, kula ribaa, kula mali ya yatima, kukimbia wakati wa vita na kuwatuhumu uzinifu wanawake Waumini waliohifadhika walioghafilika.)) [Al-Bukhaariy, Muslim]
 
Skip to


إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ



Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!



07-Shirki Ni Kuharamishwa Kuingia Jannah Na Badala Yake Kuingizwa Motoni




Alhidaaya.com







Mwenye kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) atakosa kuingia Jannah bali makazi yake yatakuwa ni ya kudumu Motoni kwa dalili zifuatazo:

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ﴿٧٢﴾

Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni motoni. Na madhalimu hawatopata yeyote mwenye kunusuru.” [Al-Maaidah: 72]



Na Hadiyth zifuatazo:



عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال: قال النبي صلى الله عليه وسلم: (( مَنْ مَاتَ وَهُوَ يَدْعُو مِنْ دُونِ اللهِ نِدَّاً دَخَلَ النَّارَ )) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaahi bin Mas-‘uwd (Radhwiya Alaahu ‘anhu) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayekufa akiwa katika hali ya kumuomba asiyekuwa Allaah kumfanyia mlinganishi (mshirika) ataingia Motoni)) [Al-Bukhaariy na Muslim]



Na pia:



عن ابن مسعود رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَنْ مَاتَ يُشْرِكُ بِاللَّهِ شَيْئًا دَخَلَ النَّارَ))

Kutoka kwa Ibn Mas‘uwd pia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayefariki akiwa katika hali ya kumshirikisha Allaah kwa chochote ataingia Motoni)) [Al-Bukhaariy 1238, Muslim 92]



Pia:



عن جابر رضي الله عنه: أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((مَنْ لَقِي اللهَ لاَ يُشْرِك بِهِ شَيْئاً دَخَلَ الْجَنَّة، وَمَنْ لَقِيَه يُشْرِك بِهِ شَيْئاً دَخَلَ النَّار))

Imetoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (Atakayekutana na Allaah akiwa hamshirikishi na chochote Ataingia Jannah, na atakayekutana Naye akiwa anamshirikisha na chochote ataingia Motoni)) [Muslim 94.]



Na pia:



عَن أَبي ذَرٍّ رضي الله عنه عنِ النَّبيِّ صلَّى اللَّهُ عليهِ وسلَّمَ؛ أنَّهُ قالَ: ((أتاني جبريلُ عليهِ السَّلامُ فبشَّرَني أنَّهُ من ماتَ من أمَّتِكَ لا يشرِكُ باللَّهِ شيئًا دخلَ الجنَّةَ)) قلتُ: وإن زنَى وإن سرقَ؟ قالَ: ((وإن زنَى وإن سرقَ))

Kutoka kwa Abuu Dharr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Amenijia Jibriyl ‘alayhis-salaam akanibashiria kwamba atakayefariki katika Ummah wangu akiwa hamshirikishi Allaah kwa chochote ataingia Jannah)). Nikasema: “Je hata akizini au akiiba?” Akasema: ((Hata akizini au akiiba)) [Al-Bukhaariy 1237, Muslim 94]



Na Hadiyth ya Abuu Huraryah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ لاَ يَسْمَعُ بِي أَحَدٌ مِنْ هَذِهِ الأُمَّةِ يَهُودِيٌّ وَلاَ نَصْرَانِيٌّ ثُمَّ يَمُوتُ وَلَمْ يُؤْمِنْ بِالَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ إِلاَّ كَانَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ

((Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, hasikii yeyote kuhusu mimi (kutumwa kwangu ujumbe) katika Ummah wa (Da’wah) Myahudi au Mnaswaara kisha afariki akiwa hayamini yale niliyotumwa nayo, isipokuwa atakuwa miongoni kwa watu wa Motoni)) [Muslim (1/80) Mlango wa Iymaan – Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu)]



Pia:



عَن عبدالله بن عمر جاءَ أعرابيٌّ إلى النَّبيِّ صلَّى اللَّهُ عليْهِ وسلَّمَ فقالَ: يا رسولَ اللَّهِ إنَّ أبي كانَ يصِلُ الرَّحمَ وَكانَ وَكانَ فأينَ هوَ؟ قالَ: ((في النَّارِ)) قالَ فَكأنَّهُ وجدَ من ذلِكَ فقالَ: يا رسولَ اللَّهِ فأينَ أبوكَ قالَ رسولُ اللَّهِ صلَّى اللَّهُ عليْهِ وسلَّمَ: ((حيثُما مررتَ بقبرِ مشرِكٍ فبشِّرْهُ بالنَّارِ)) قالَ: فأسلمَ الأعرابيُّ بعدُ وقالَ: لقد كلَّفني رسولُ اللَّهِ صلَّى اللَّهُ عليْهِ وسلَّمَ تعبًا ما مررتُ بقبرِ كافرٍ إلَّا بشَّرتُهُ بالنَّارِ

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Bedui mmoja alikuwa kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Baba yangu alikuwa akiunga undugu na alikuwa akifanya kadhaa wa kadhaa, je yuko wapi?” Akasema: (Motoni)). Ikawa kama kwamba lilikuwa jambo zito kwake. Akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Je, baba yako yuko wapi?” Akasema: ((Utakapopita kaburi la Mushrik yeyote mbashirie Moto)). Bedui akasilimu baada ya hapo kisha akasema: “Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): amenitwika jukumu gumu kwamba kila nikipata kaburi la kafiri nimbashirie Moto.” [Swahiyh Ibn Maajah 1288]



Wala haifai kuwaombea wazazi makafiri wakafariki wakiwa katika hali ya ukafiri kwa kuwa imeshabainika kuwa ni watu wa Motoni, tena hata kama ni wazazi, ndugu au jamaa wa karibu. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ﴿١١٣﴾

Haimpasi Nabiy na wale walioamini kuwaombea maghfirah washirikina japokuwa ni jamaa zao wa karibu baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa moto uwakao vikali mno. [At-Tawbah: 113]
 
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ



Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!



08- Sifa Mbaya Za Washirikina




Alhidaaya.com





1- Washirikina ni viumbe waovu kabisa kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَاۚ أُولَـٰئِكَ هُمْ شَرُّ الْبَرِيَّةِ ﴿٦﴾

Hakika wale waliokufuru miongoni mwa watu wa kitabu na washirikina watakuwa katika moto wa Jahannam, ni wenye kudumu humo; hao ndio waovu kabisa wa viumbe. [Al-Bayyinah: 6]





2-Washirikina ni wapotofu hawana akili kama vile wanyama walivyokuwa hawana akili, bali wapotofu zaidi kuliko wanyama!



Kwa sababu wana Aadam wamefadhilishwa kupewa akili kinyume na wanyama, lakini wana Aadam hao wanaomkufuru na kumshirkisha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) ni wenye kufuata hawaa zao, hawatumii akili zao! Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



أَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَـٰهَهُ هَوَاهُ أَفَأَنتَ تَكُونُ عَلَيْهِ وَكِيلًا ﴿٤٣﴾

Je, umemuona yule aliyefanya hawaa yake kuwa ndio mwabudiwa wake? Je, basi utaweza wewe kuwa ni mdhamini wake?





أَمْ تَحْسَبُ أَنَّ أَكْثَرَهُمْ يَسْمَعُونَ أَوْ يَعْقِلُونَ ۚ إِنْ هُمْ إِلَّا كَالْأَنْعَامِ ۖ بَلْ هُمْ أَضَلُّ سَبِيلًا ﴿٤٤﴾

Je, unadhania kwamba wengi wao wanasikia au wanatia akilini? Wao si chochote isipokuwa kama wanyama, bali wao wamepotea zaidi njia. [Al-Furqaan: 43-44]





3- Washirikina, kwa shirki na kufru zao, wamekuwa ni wenye kula na kustarehe kama wanyama. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَالَّذِينَ كَفَرُوا يَتَمَتَّعُونَ وَيَأْكُلُونَ كَمَا تَأْكُلُ الْأَنْعَامُ وَالنَّارُ مَثْوًى لَّهُمْ﴿١٢﴾

Na wale waliokufuru wanastarehe na wanakula kama walavyo wanyama wa mifugo na moto ndio makazi yao. [Muhammad: 12]







4- Washirikina ni vipofu, viziwi, mabubu, hawatumii akili!



Washirikina walipokuwa wakiitwa kufuata Uongofu wa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kufuata Tawhiyd na kuacha kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) walikanusha, wakapigiwa mfano kama viziwi, mabubu, vipofu, hawana akili! Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):





وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اتَّبِعُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ قَالُوا بَلْ نَتَّبِعُ مَا أَلْفَيْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا ۗ أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ﴿١٧٠﴾

Na wanapoambiwa: “Fuateni Aliyoyateremsha Allaah” Husema: “Bali tunafuata tuliyowakuta nayo baba zetu.” Je, japokuwa baba zao walikuwa hawaelewi kitu chochote na wala hawakuongoka?





وَمَثَلُ الَّذِينَ كَفَرُوا كَمَثَلِ الَّذِي يَنْعِقُ بِمَا لَا يَسْمَعُ إِلَّا دُعَاءً وَنِدَاءً ۚ صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿١٧١﴾

Na mfano wa wale waliokufuru ni kama mfano wa yule ambaye anapiga kelele kwa ambaye hasikii ila sauti na mwito. Viziwi, mabubu, vipofu kwa hiyo hawatii akilini. [Al-Baqarah: 170-171]





Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَلَقَدْ ذَرَأْنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيرًا مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ ۖ لَهُمْ قُلُوبٌ لَّا يَفْقَهُونَ بِهَا وَلَهُمْ أَعْيُنٌ لَّا يُبْصِرُونَ بِهَا وَلَهُمْ آذَانٌ لَّا يَسْمَعُونَ بِهَا ۚ أُولَـٰئِكَ كَالْأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ﴿١٧٩﴾

Kwa yakini Tumeumba Jahannam kwa ajili ya wengi katika majini na wana Adam. Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama, bali wao ni wapotovu zaidi. Hao ndio walioghafilika. [Al-A’raaf: 179]





Na ndio maana wakawa viumbe waovu kabisa kwa kuwa hawakutaka kumtii Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipowalingania. Wakabakia katia shirki na kufru zao. Basi hawana kheri yoyote ile mbele ya Allaah. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ قَالُوا سَمِعْنَا وَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ﴿٢١﴾

Na wala msiwe kama wale waliosema: “Tumesikia”; na hali wao hawasikii.





إِنَّ شَرَّ الدَّوَابِّ عِندَ اللَّـهِ الصُّمُّ الْبُكْمُ الَّذِينَ لَا يَعْقِلُونَ﴿٢٢﴾

Hakika viumbe viovu kabisa mbele ya Allaah ni viziwi, mabubu ambao hawatumii akili.





وَلَوْ عَلِمَ اللَّـهُ فِيهِمْ خَيْرًا لَّأَسْمَعَهُمْ ۖ وَلَوْ أَسْمَعَهُمْ لَتَوَلَّوا وَّهُم مُّعْرِضُونَ﴿٢٣﴾

Na kama Allaah Angelijua kuwa wana kheri yoyote ile, basi Angeliwasikilizisha; na kama Angeliwasikilizisha, wangeligeuka nao huku wakipuuza. [Al-Anfaal: 21-23]







5- Washirikina ni watu wa najisi!



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْمُشْرِكُونَ نَجَسٌ فَلَا يَقْرَبُوا الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ بَعْدَ عَامِهِمْ هَـٰذَا

Enyi walioamini! Hakika washirikiana ni najisi, basi wasikaribie Al-Masjid Al-Haraam baada ya mwaka wao huu. [At-Tawbah: 28]







6-Imeharamishwa kufunga ndoa na washirikina! Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anaamrisha:



وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ ۗ وَلَا تُنكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤْمِنُوا ۚ وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ ۗ أُولَـٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ ۖوَيُبَيِّنُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٢٢١﴾

Na wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni. Na wala msiwaozeshe (wanawake wa Kiislamu) wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni. Hao wanaitia katika moto na Allaah Anaitia katika Al-Jannah na maghfirah kwa idhini Yake. Na Anabainisha Aayaat (na shariy’ah) Zake ili wapate kukumbuka. [Al-Baqarah: 221]
 
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ



Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!



09 Kusujudu Na Kuinamia Kwa Asiyekuwa Allaah







Washirikina wa kale walimshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa namna mbali mbali; kuna walioabudu masanamu wakiyasujudia na kurukuu mbele yao. Wengine walirukuu na kusujudia mwezi, nyota na jua, jambo ambalo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ameliharamisha katika kauli Yake:



وَمِنْ آيَاتِهِ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ ۚ لَا تَسْجُدُوا لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَاسْجُدُوا لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ﴿٣٧﴾

Na katika Aayaat (ishara, dalili) Zake, ni usiku na mchana, na jua na mwezi. Msisujudie jua wala mwezi; bali msujudieni Allaah Ambaye Aliyeviumba ikiwa Yeye Pekee mnawambudu. [Fusw-swilat: 37]





Hali kama hii inatendwa na baadhi ya Waislamu kuinamia binaadamu wenzao katika maamkizi n.k. kwa kudhihirisha mapenzi, takrima na heshima. Baadhi ya mila zinaamrisha watoto kuwainamia wazazi wao, au waalimu na watu wakubwa katika maamkizi. Kadhaalika, hata baadhi ya watu wa itikadi mbalimbali wenye vyeo wanapenda kusalimiwa kwa kuinamiwa! Kitendo hiki kinaingia katika kumshikirisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).





Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaahu) amesema: “Sujudu ni kwa ajili ya Allaah Pekee na shariy’ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni shariy’ah kamilifu kabisa, basi haijuzu kumsujudia yeyote asiyekuwa Allaah, ikiwa ni katika maamkizi wala katika ‘ibaadah. Ama katika shariy’ah zote, sujudu ya ‘ibaadah ndio haijuzu kabisa isipokuwa kwa Allaah. Isipokuwa ilikuwa zamani (kabla ya Uislamu) sujudu ilikuwa ikitumika kama maamkizi ya kudhihirisha heshima kama alivyofanya (Nabiy Ya’quwb) baba yake Nabiy Yuwsuf na ndugu zake na kama walivyofanya Malaika kumsujudia Aadam. Hii ni katika maamkizi ya takrima wala si kusudio la ‘ibaadah. Ama katika shariy’ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Allaah (‘Azza wa Jalla) Amekataza hivyo Akaifanya sujudu ni kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Pekee wala haijuzu kumsujudia yeyote; si Manabiy wala wengineo, hata Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza asisujudiwe na yeyote na akajulisha kwamba sujudu ni kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Pekee.” [Fataawaa Nuwr ‘Alaa Ad-Darb (4/112-113)]



Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah amenukuu katazo kama hilo katika Majmuw’ Al-Fataawaa (1/377) .



Na Al-Lajnah Ad-Daaimah lil-buhuwthil-‘ilmiyyah wal-Iftaa katika Fatwa namba (4400) wamefutu ifuatavyo:



“Yeyote aliyeamini Risala ya Nabiy wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na yale yote aliyokuja nayo katika shariy’ah, kisha baada ya hapo akamsujudia yeyote asiyekuwa Allaah; ikiwa ni walii wake au mtu kaburini, au shekhe wa Twariyqah (Masufi) basi yeye anahesabika kuwa ni kafiri aliyeritadi kutoka katika Uislamu, ni mshirikina akimshirikisha Allaah na wengineo katika ‘ibaadah hata kama atakuwa anatamka Shahada mbili wakati wa kusujudu kwake, kwa kuleta jambo lenye kupinga kauli yake kwa kumsujudia asiyekuwa Allaah.”



Katazo hilo limethibiti katika Qur-aan na Sunnah:



عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي أَوْفَى، قَالَ: "لَمَّا قَدِمَ مُعَاذٌ مِنَ الشَّامِ سَجَدَ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: ((مَا هَذَا يَا مُعَاذُ ؟)) قَالَ: أَتَيْتُ الشَّامَ فَوَافَقْتُهُمْ يَسْجُدُونَ لِأَسَاقِفَتِهِمْ وَبَطَارِقَتِهِمْ، فَوَدِدْتُ فِي نَفْسِي أَنْ نَفْعَلَ ذَلِكَ بِكَ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((فَلَا تَفْعَلُوا، فَإِنِّي لَوْ كُنْتُ آمِرًا أَحَدًا أَنْ يَسْجُدَ لِغَيْرِ اللَّهِ، لَأَمَرْتُ الْمَرْأَةَ أَنْ تَسْجدَ لِزَوْجِهَا، وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ، لَا تُؤَدِّي الْمَرْأَةُ حَقَّ رَبِّهَا حَتَّى تُؤَدِّيَ حَقَّ زَوْجِهَا، وَلَوْ سَأَلَهَا نَفْسَهَا وَهِيَ عَلَى قَتَبٍ لَمْ تَمْنَعْه))

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Abiy Awfaa (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Muaadh aliporudi kutoka Shaam alimsujudia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Ee Mu’aadh! Nini hivyo?)) Akasema: “Nimekuja kutoka Shaam nikawakuta wanawasujudia Maaskofu na Mapadri wao nafsi yangu ikapenda nikufanyie hivyo.” Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Usifanye hivyo! Kwani hakika ingekuwa ni kumuamrisha mtu amsujudie asiyekuwa Allaah, basi ningeliamrisha mke amsujudie mumewe. Naapa kwa Ambaye nafsi ya Muhammad ipo Mikononi Mwake; Mke hatoweza kutimiza haki za Mola Wake mpaka atimize haki za mumewe, na hata kama atamtaka hali akiwa katika nundu la ngamia basi asimnyime)) [Riwaayah mbali mbali kama hiyo na hii ni lafdhw ya Ibn Maajah (1853) na ameisahihisha Al-Albaaniy]



Na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:



مَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُؤْتِيَهُ اللَّـهُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ ثُمَّ يَقُولَ لِلنَّاسِ كُونُوا عِبَادًا لِّي مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَـٰكِن كُونُوا رَبَّانِيِّينَ بِمَا كُنتُمْ تُعَلِّمُونَ الْكِتَابَ وَبِمَا كُنتُمْ تَدْرُسُونَ ﴿٧٩﴾

Ni mustahili kwa mtu kwamba Allaah Amempa Kitabu na Al-Hukma na Unabii kisha awaambie watu: “Kuweni wenye kuniabudu mimi badala ya Allaah” Bali (atawaambia): “Kuweni Wanachuoni waswalihina kwa yale mliyokuwa mkiyafundisha ya Kitabu na kwa yale mliyokuwa mkiyasoma.”





وَلَا يَأْمُرَكُمْ أَن تَتَّخِذُوا الْمَلَائِكَةَ وَالنَّبِيِّينَ أَرْبَابًا ۗ أَيَأْمُرُكُم بِالْكُفْرِ بَعْدَ إِذْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿٨٠﴾

Na wala hakuamuruni kuwachukua Malaika na Manabii kuwafanya miola. Je, anakuamrisheni ukafiri baada ya nyinyi kuwa mmejisalimisha kwa Allaah? [Aal-‘Imraan: 79-80]
 
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!



10-Kumhusisha Rasuli wa Allaah Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam

Katika Kumshirikisha Allaah.



Alhidaaya.com







Baadhi ya Waislamu wanamhusisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa namna mbali mbali. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na Rasuli wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wamekemea mno kwa dalili kadhaa miongoni mwazo ni:



Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba ilipoteremshwa kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ ﴿٢١٤﴾

Na onya (ee Muhammad Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) jamaa zako wa karibu. [Ash-Shu’araa: 214]





Alisimama Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:



((يَا مَعْشَرَ قُرَيْشٍ!)) أَوْ كَلِمَةً نَحْوَهَا ((اشْتَرُوا أَنْفُسَكُمْ، لاَ أُغْنِي عَنْكُمْ مِنَ اللَّهِ شَيْئًا، يَا بَنِي عَبْدِ مَنَافٍ لاَ أُغْنِي عَنْكُمْ مِنَ اللَّهِ شَيْئًا، يَا عَبَّاسُ بْنَ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ لاَ أُغْنِي عَنْكَ مِنَ اللَّهِ شَيْئًا، وَيَا صَفِيَّةُ عَمَّةَ رَسُولِ اللَّهِ لاَ أُغْنِي عَنْكِ مِنَ اللَّهِ شَيْئًا ، وَيَا فَاطِمَةُ بِنْتَ مُحَمَّدٍ سَلِينِي مَا شِئْتِ مِنْ مَالِي لاَ أُغْنِي عَنْكِ مِنَ اللَّهِ شَيْئًا))

((Enyi maashara Quraysh!)) Au mfano wa maneno hayo ((Okoeni nafsi zenu, mimi sitowafaa kwa chochote mbele ya Allaah! Enyi Baniy ‘Abdi Manaaf! Mimi sitowafaa kwa chochote mbele ya Allaah! Ee ‘Abbaas bin ‘Abdil-Mutwalib! Sitokufaa kwa chochote mbele ya Allaah! Na ee Faatwimah bint Muhammad! Niombe utakacho katika mali, lakini sitokufaa kwa chochote mbele ya Allaah)) [Al-Bukhaariy (2753), Muslim (206)].





Amesema Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) katika Majmuw’ Fataawa wa Rasaail (9/285- 288):



“Ikiwa ujamaa wa karibu na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hautowafaa chochote jamaa zake, ni dalili hiyo kukatazwa tawassul kwa jaha ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kuwa jaha ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hainufaishi kwayo isipokuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na ndivyo ikawa kauli sahihi kabisa ya Wanachuoni ni uharamu wa tawassul kwa jaha ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).”





Na Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema katika Majmuw’ Fataawaa (3/98):



“Mwongozo na kipimo cha hakika ni kufuata yaliyokuja katika Qur-aan Al-Kariym na Sunnah Al-Mutwaharrah kwa kauli na na vitendo na kuitakidi. Ama unasaba, hakika hautofaa (mtu) wala hauna umuhimu kama alivyosema Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam:



وَمَنْ بَطَّأَ بِهِ عَمَلُهُ لَمْ يُسْرِعْ بِهِ نَسَبُهُ

((…na ambaye kazorotesha ‘amali zake, haitomharakisha nasaba yake)). [Muslim]



Akasema: ((Enyi maashara Quraysh! Okoeni nafsi zenu, mimi sitowafaa kwa chochote mbele ya Allaah!)). Hivyo ndivyo alivyomwambia ‘Ammi yake na ‘Ammat (shangazi) yake, na binti yake Faatwimah. Basi ingekuwa unasaba utamfaa mtu, ungewafaa hao.”





Baadhi ya vitendo vinavyomhusisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni kama ifuatavyo:





1-Kumtukuza mno Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka kumfikisha daraja ya Allaah!



Amekemea Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

لا تُطْرُونِي كَمَا أَطْرَتْ النَّصَارَى ابْنَ مَرْيَمَ فَإِنَّمَا أَنَا عَبْدُهُ فَقُولُوا عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ) رواه البخاري

Msinitukuze Kama Manaswara [Wakristo] walivyomtukuza Masiyh mwana wa Maryam, hakika mimi na mja kwa hiyo semeni, ‘mja wa Allaah na Mjumbe Wake’)). [Al-Bukhaariy na Muslim.]



Na pia Hadiyth:



عَنْ أَنَسٍ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) أَنَّ نَاسًا قَالُوا: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! يَا خَيْرَنَا وَابْنَ خَيْرِنَا, وَسَيِّدَنَا وَابْنَ سَيِّدِنَا! فَقَالَ: ((يَا أَيُّهَا اَلنَّاسُ! قُولُوا بِقَوْلِكُمْ، وَلاَ يَسْتَهْوِيَنَّكُمْ اَلشَّيْطَانُ، أَنَا مُحَمَّدٌ عَبْدُ اَللَّهِ وَرَسُولُهُ، مَا أُحِبُّ أَنْ تَرْفَعُونِي فَوْقَ مَنْزِلَتِي اَلَّتِي أَنْزَلَنِي اَللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ)) رَوَاهُ النَّسَائِيُّ بِسَنَدٍ جَيِّدٍ

Imepokelewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: kwamba watu walisema: “Ee Rasuli wa Allaah! Ee mbora wetu na mwana wa mbora wetu, na bwana wetu, na mwana wa bwana wetu!.” Akasema: ((Enyi watu! Semeni msemayo, asikupambieni shaytwaan hawaa zenu. Mimi ni Muhammad mja wa Allaah na Rasuli Wake. Sipendi mnipandishe cheo kuliko cheo changu ambacho Ameniteremshia Allaah Ázza wa Jalla)). [An-Nasaaiy kwa isnaad nzuri]



Na kutukuzwa kwengine ni vile kusifiwa mno kwa uzushi na pia kutajwa kwa sifa ambazo ni Sifa za Allaah Pekee. Mfano katika Mawlid mbalimbali kama Barzanjiy, Nuwn, Al-Hibshiy (Sumtud-Durar), Burdah n.k. Vilevile kwenye nyiradi mbalimbali miongoni mwa nyiradi za Kisufi kama, Swalaatun-Naariyah, Wasiylatush-Shaafi’, Dalaail Al-Khayraat, n.k.



i) Maneno ya shirki yaliyomo katika Swalaatun-Naariyah:



للهم صلي صلاةً كاملة وسلم سلاما تاما على سيدنا محمد الذي تنحل به العقد، وتتفرج به الكرب، وتقضى به الحوائج ، وتنال به الرغائب، وحسن الخواتيم ويستسقى الغمام بوجهه الكريم وعلى آله وصحبه في كل لمحة ونفس بعدد معلوم لك



Ee Allaah, Mswalie Swalaah iliyotimu bwana wetu Muhammad ambayo kwa fadhila zake, vizuizi vyote vinaondoka, mazonge (misukosuko) yanapoa, shida zote zinafarijika, na mahitaji yanakidhika, na inafikisha kwa yanayotamaniwa, na mwisho mwema wapatikana, na kwa fadhila zake yule mwenye uso mtukufu mawingu (mvua) huombwa kunyesha, na Swalah na Salaam ziwe juu ahli zake na Maswahaba wake kwa kila muda na kila pumzi kwa idadi ya kadiri ya Ujuzi Wako)





ii) Baadhi ya sifa za kumtukuza mno katika Mawlid ya Barzanjiy:



“Katika saa ya kuzaliwa Mtume alihudhuria Aasiyah na Maryam kutoka Mbinguni.”



“Wanyama walitamka kwa Kiarabu kuwa leo imechukuliwa mimba ya Mtume.”



“Wanyama wakapeana khabari ya kuchukuliwa mimba ya Mtume.”



“Majini wakatoa khabari kwa watu kuwa imechukuliwa mimba ya Mtume.”



“Katika saa ya kuzaliwa Mtume alihudhuria Aasiyah na Maryam kutoka Mbinguni.”



“Wanavyuoni wameona ni jambo zuri watu kusimama wakati inapotajwa kuzaliwa Mtume.”



“Akamwona Allaah kwa macho yake.”





iii) Baadhi ya maneno ya shirki kwenye Mawlid Ya Nuwn



“Lau kuwa si Mtume asingepatikana Aadam wala Ibraahiym….. na ufalme wa Nabii Sulaymaan…”



“Manabii wote ni manaibu wa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakimwendeshea kazi yake.”





iv) Baadhi ya maneno ya shirki katika uradi wa Nabhaaniy:



“Lau kuwa si Nabii Muhammad tusingekuja ulimwenguni wala tusingeishi!”







2-Kumuomba du’aa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) badala ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):





Du’aa huelekezwa kwake kama kusema: “Ee Rasuli nisaidie”, “Ee Rasuli niondoshee dhiki, shida zangu”. Hakuna kiumbe yeyote mwenye uwezo wa hayo isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Angekuwa na uwezo huo basi yasingemfika madhara, mateso, maudhi mbali mbali yaliyomsibu kutoka kwa makafiri. Allaah Alimuamrisha awaambie washirikina:



قُل لَّا أَمْلِكُ لِنَفْسِي نَفْعًا وَلَا ضَرًّا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۚ وَلَوْ كُنتُ أَعْلَمُ الْغَيْبَ لَاسْتَكْثَرْتُ مِنَ الْخَيْرِ وَمَا مَسَّنِيَ السُّوءُ ۚ إِنْ أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ﴿١٨٨﴾

Sema: “Siimilikii nafsi yangu manufaa yoyote wala dhara yoyote isipokuwa Apendavyo Allaah. Na lau ningekuwa najua ya ghayb, bila shaka ningelijikithirishia ya kheri, na wala lisingelinigusa ovu. Mimi si chochote isipokuwa ni mwonyaji na mbashiriaji kwa watu wanaoamini.” [Al-A’raaf: 188]





Na Akamwambia tena aseme:

قُلْ إِنَّمَا أَدْعُو رَبِّي وَلَا أُشْرِكُ بِهِ أَحَدًا﴿٢٠﴾

Sema: (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi namuomba Rabb wangu na wala simshirikishi na yeyote.”



قُلْ إِنِّي لَا أَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا رَشَدًا﴿٢١﴾

Sema: “Hakika mimi sikumilikieni dhara na wala uongofu.”



قُلْ إِنِّي لَن يُجِيرَنِي مِنَ اللَّـهِ أَحَدٌ وَلَنْ أَجِدَ مِن دُونِهِ مُلْتَحَدًا﴿٢٢﴾

Sema: “Hakika hakuna yeyote awezaye kunilinda na Allaah na wala sitoweza kupata mahali pa kukimbilia. [Al-Jinn: 20-22]





Na pia Akamuamrisha Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) :



قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا ﴿١١٠﴾

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi ni mtu kama nyinyi, nafunuliwa Wahy kwamba: Hakika Muabudiwa wa haki wenu ni Ilaah Mmoja Pekee. Hivyo anayetaraji kukutana na Rabb wake, basi na atende ‘amali njema na wala asimshirikishe yeyote katika ‘ibaadah za Rabb wake.” [Al-Kahf: 110]





3-Kumuomba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mbele ya kaburi lake:



Kuna wanaoelekea kaburi lake wanapofika Masjid Nabawiy Madiynah na kumuomba. Inavyopasa ni kuelekea Qiblah. Allaah Anakataza wazi kumshirikisha Yeye ndani ya Misikiti na hata penginepo, pale Anaposema:



وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا﴿١٨﴾

Na kwamba Misikiti ni kwa ajili ya Allaah, basi msiombe yeyote pamoja na Allaah. [Al-Jinn: 18]



Naye Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amekataza:

((لا تجعلوا قبري عيدًا))

((Msifanye kaburi langu ni sehemu ya kurudiwa rudiwa [kuendewa kila mara])). [Musnad Ahmad, Muswannaf 'Abdur-Razzaaq]



Na akasema:



لعنة الله على اليهود والنصارى اتخذوا قبور أنبيائهم مساجد

((Allaah Amewalaani Mayahudi na Manaswara, wamefanya makaburi ya Manabii wao kuwa misikiti)). [Al-Bukhaariy (425) Muslim (531)]





4-Kutawassul (kujikurubisha) kwa du’aa kupitia kwake:



Mfano kusema: “Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kwa jaha ya Rasuli Wako Unikidhie haja zangu kadhaa, au Uniokoe na janga au balaa fulani, Unighufurie dhambi zangu n.k.”



Baada yakufariki Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) haipasi kutawassal kwake. Maswahaba waliacha kutawassal kwake bali walitawassal kwa ami yake ‘Abbaas kwa kuwa alikuwa hai wakati huo kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:



عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ (رضي الله عنه) أَنَّ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) كَانَ إِذَا قَحَطُوا اسْتَسْقَى بِالْعَبَّاسِ بْنِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ فَقَالَ: "اللَّهُمَّ إِنَّا كُنَّا نَتَوَسَّلُ إِلَيْكَ بِنَبِيِّنَا فَتَسْقِينَا وَإِنَّا نَتَوَسَّلُ إِلَيْكَ بِعَمِّ نَبِيِّنَا فَاسْقِنَا" قَالَ" فَيُسْقَوْنَ

Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba ‘Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) aliomba mvua kulipokuwa na ukame kwa kutawassal kwa ‘Abbaas bin ‘Abdil-Muttwalib akisema: “Ee Allaah, tulikuwa tunatawassal Kwako kupitia Nabiy wako, Ukatunyeshea mvua, na sasa tunatawassal Kwako kupitia ‘ami wa Nabiy Wako basi tunyweshee mvua”. Akasema: Wakanyweshewa mvua. [Al-Bukhaariy]
 
UJUMBE WA LEO :
Maneno ya Luqman kwa mwanae

Screenshot_20250527_080517_Quran Swahili.jpg
 
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!

11- Kutufu Makaburi Kuwaomba Waliomo Kaburini


Alhidaaya.com





Miongoni mwa shirki kubwa ni kutufu makaburini, kuwaomba au kutawassal kwa walio makaburini. Maiti hawasikii du’aa wala hawaitikii, bali hawana uwezo wa kumnufaisha mtu wala kumdhuru! Dalili ni kauli za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) zifuatazo:



إِنَّ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ عِبَادٌ أَمْثَالُكُمْ ۖ فَادْعُوهُمْ فَلْيَسْتَجِيبُوا لَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿١٩٤﴾

Hakika wale mnaowaomba badala ya Allaah ni waja kama nyinyi. Hebu waiteni wakuitikieni ikiwa nyinyi ni wakweli. [Al-A’raaf: 194]



Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَلَا تَدْعُ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَ ۖ فَإِن فَعَلْتَ فَإِنَّكَ إِذًا مِّنَ الظَّالِمِينَ﴿١٠٦﴾

Na wala usiombe badala ya Allaah visivyokufaa wala visivyokudhuru. Na ukifanya, basi hakika utakuwa miongoni mwa madhalimu. [Yuwnus: 106]



Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَالَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ لَا يَسْتَجِيبُونَ لَهُم بِشَيْءٍ إِلَّا كَبَاسِطِ كَفَّيْهِ إِلَى الْمَاءِ لِيَبْلُغَ فَاهُ وَمَا هُوَ بِبَالِغِهِ ۚ وَمَا دُعَاءُ الْكَافِرِينَ إِلَّا فِي ضَلَالٍ ﴿١٤﴾

Na wale wanaowaomba badala Yake, hawawaitikii kwa chochote isipokuwa kama anayenyosha viganja vyake viwili vya mikono kwenye maji ili yafikie kinywani mwake, na wala hayafikii hata kidogo. Na du’aa za makafiri hazipo ila katika upotofu. [Ar-Ra’d: 14]



Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



قُلْ مَن رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ قُلِ اللَّـهُ ۚ قُلْ أَفَاتَّخَذْتُم مِّن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ لَا يَمْلِكُونَ لِأَنفُسِهِمْ نَفْعًا وَلَا ضَرًّا ۚ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ أَمْ هَلْ تَسْتَوِي الظُّلُمَاتُ وَالنُّورُ ۗ أَمْ جَعَلُوا لِلَّـهِ شُرَكَاءَ خَلَقُوا كَخَلْقِهِ فَتَشَابَهَ الْخَلْقُ عَلَيْهِمْۚ قُلِ اللَّـهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ وَهُوَ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ ﴿١٦﴾

Sema: “Ni nani Rabb wa mbingu na ardhi?” Sema: “Ni Allaah.” Sema: “Je, mnawafanya wengineo badala Yake kuwa walinzi na hali hawamiliki kwa ajili ya nafsi zao manufaa wala dhara?” Sema: “Je, kipofu analingana sawa na mwenye kuona, au je, viza vinalingana sawa na nuru?” Au wamemfanyia Allaah washirika walioumba kama uumbaji Wake, kisha yakafanana maumbile kwao? Sema: “Allaah ni Muumbaji wa kila kitu, Naye ni Mmoja Pekee, Mwenye kudhibiti na kudhalilisha, Mshindi, Asiyepingika.” [Ar-Ra’d: 16]





Nukuu kutoka Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah (1/206) inasema:

“…wala haijuzu kuomba du’aa kwa Mawalii au wengineo baada ya kufa kwao, bali inajuzu kuwaomba waja wema wakuombee. Wala haijuzu kutufu makaburi, kwani kutufu ni makhsusi kwa Ka’bah tukufu pekee. Atakayetufu makaburini kwa ajili ya kujikurubisha na watu wake humo ni shirki kubwa, japokuwa akiwa anakusudia kujikurubisha kwa Allaah tu! Hivyo ni bid’ah inayochukiza kabisa kwani haipasi kutufu makaburi wala kuswali kuyaelekea hata kama itakuwa ni kwa makusudio ya kutaka radhi za Allaah.”



Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ مَا يَمْلِكُونَ مِن قِطْمِيرٍ ﴿١٣﴾

Na wale mnaowaomba badala Yake hawamiliki hata kijiwavu cha kokwa ya tende.





إِن تَدْعُوهُمْ لَا يَسْمَعُوا دُعَاءَكُمْ وَلَوْ سَمِعُوا مَا اسْتَجَابُوا لَكُمْ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُونَ بِشِرْكِكُمْ ۚ وَلَا يُنَبِّئُكَ مِثْلُ خَبِيرٍ ﴿١٤﴾

Mkiwaomba, hawasikii maombi yenu, na hata wakisikia, hawatakuitikieni. Na Siku ya Qiyaamah watakanusha ushirikina wenu, na wala hakuna atakayekujulisha vilivyo kamaMwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Faatwir: 13-14]





Bali Siku ya Qiyaamah utadhihirika uadui baina yao na watawakanusha kabisa kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)!



وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّن يَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَن لَّا يَسْتَجِيبُ لَهُ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ وَهُمْ عَن دُعَائِهِمْ غَافِلُونَ﴿٥﴾



“Na nani aliyepotoka zaidi kuliko ambaye anayeomba asiyekuwa Allaah ambaye hamuitikii mpaka Siku ya Qiyaamah; nao wala hawatambui maombi yao.”





وَإِذَا حُشِرَ النَّاسُ كَانُوا لَهُمْ أَعْدَاءً وَكَانُوا بِعِبَادَتِهِمْ كَافِرِينَ﴿٦﴾

Na pale watakapokusanywa watu, (miungu ya uongo) watakuwa ni maadui wao, na watakuwa wenye kuzikanusha ‘ibaadah zao. [Al-Ahqaaf: 5- 6]







Washirikina kabla ya Uislamu walikuwa wakiomba masanamu ya Al-Laata, ‘Al-‘Uzza na wengineo, na hawakuwa wakiitakidi kuwa wana uwezo wa kuumba au kuteremsha mvua bali walidai kuwa yanawakurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na kwamba masanamu hayo ni kama viombezi kwao. Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ إِنَّ اللَّـهَ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ فِي مَا هُمْ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي مَنْ هُوَ كَاذِبٌ كَفَّارٌ ﴿٣﴾

na wale waliojichukulia badala Yake walinzi (wakisema): “Hatuwaabudu isipokuwa ili wapate kutukurubisha kwa Allaah tumkaribie” Hakika Allaah Atahukumu baina yao katika yale waliyokhitilafiana nayo. Hakika Allaah Hamwongoi aliye muongo, kafiri. [Az-Zumar: 3]



Basi hakuna tofauti na wanaoomba wakaazi wa makaburi kwani sanamu, makaburi, matwaghuti… yote yana maana moja ya kuabudu au kuomba asiyekuwa Allaah; ikiwa ni maiti au hai, na sababu za kuomba ni kama hizo. Anakanusha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) hayo Anaposema:



قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِهِ فَلَا يَمْلِكُونَ كَشْفَ الضُّرِّ عَنكُمْ وَلَا تَحْوِيلًا ﴿٥٦﴾

Sema: “Iteni wale ambao mnadai (ni waabudiwa) pasi Naye, basi hawamiliki kukuondesheeni dhara na wala kuihamisha (kwa mwengine).” [Al-Israa: 56]





Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anamwambia Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) awajibu washirikina:



قُلْ أَفَرَأَيْتُم مَّا تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ إِنْ أَرَادَنِيَ اللَّـهُ بِضُرٍّ هَلْ هُنَّ كَاشِفَاتُ ضُرِّهِ أَوْ أَرَادَنِي بِرَحْمَةٍ هَلْ هُنَّ مُمْسِكَاتُ رَحْمَتِهِ ۚ قُلْ حَسْبِيَ اللَّـهُ ۖ عَلَيْهِ يَتَوَكَّلُ الْمُتَوَكِّلُونَ﴿٣٨﴾

Sema: “Je, mnaonaje wale mnaowaomba badala ya Allaah; ikiwa Allaah Atanikusudia dhara; je, wao wataweza kuondosha dhara Yake? Au Akinikusudia rahmah; je wao wataweza kuizuia rahmah Yake?” Sema: “Ananitosheleza Allaah”, Kwake watawakali wenye kutawakali. [Az-Zumar: 38]



Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



قُل لَّا أَمْلِكُ لِنَفْسِي نَفْعًا وَلَا ضَرًّا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۚ وَلَوْ كُنتُ أَعْلَمُ الْغَيْبَ لَاسْتَكْثَرْتُ مِنَ الْخَيْرِ وَمَا مَسَّنِيَ السُّوءُ ۚ إِنْ أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ﴿١٨٨﴾

Sema: “Siimilikii nafsi yangu manufaa yoyote wala dhara yoyote isipokuwa Apendavyo Allaah. Na lau ningekuwa najua ya ghayb, bila shaka ningelijikithirishia ya kheri, na wala lisingelinigusa ovu. Mimi si chochote isipokuwa ni mwonyaji na mbashiriaji kwa watu wanaoamini.” [Al-A’raaf: 188]



Na pia Anasema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ ۖ لَا يَمْلِكُونَ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَمَا لَهُمْ فِيهِمَا مِن شِرْكٍ وَمَا لَهُ مِنْهُم مِّن ظَهِيرٍ ﴿٢٢﴾

Sema: “Ombeni wale mnaodai kwa dhana (ni waabudiwa) badala ya Allaah, hawamiliki hata uzito wa sisimizi mbinguni wala ardhini, na wala hawana humo ushirika Naye, na wala Yeye (Allaah) Hana msaidizi miongoni mwao.” [Sabaa: 22]



Tahadhari Muislamu kuingia katika shirki kubwa juu ya kuwa hao wanaoombwa hawawezi kukuitikia du’aa zako bali elekea kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ambaye Ndiye Mwenye uwezo wa kukunufaisha au kukuondoshea madhara kama Anavyosema:



أَمَّن يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ وَيَجْعَلُكُمْ خُلَفَاءَ الْأَرْضِ ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ ﴿٦٢﴾

Au nani Anayemuitika mwenye dhiki mno anapomwomba, na Akamuondoshea ouvu na Akakufanyeni makhalifa wa ardhi? Je, yuko mwabudiwa pamoja na Allaah? Ni machache mno mnayokumbuka. [An-Naml: 62]





Aayah hiyo aliisoma mtu alipofikwa na balaa la kukaribia kuuliwa, alipoisoma Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Alimuokoa. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]



Tena Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Yuko karibu mno nawe na Mwenye kuitikia du’aa za kila anayemuomba, Anasema:



وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ﴿١٨٦﴾

Na watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi ni Niko karibu (kwa ujuzi); Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba. Basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi, wapate kuongoka. [Al-Baqarah: 186]





Na fuata mafunzo Swahiyh kama alivyofundisha Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba unapozuru au kupitia makaburi usome du’aa:



السَّلامُ عَلَـيْكُمْ أَهْلَ الدِّيارِ مِنَ المؤْمِنيـنَ وَالْمُسْلِمينَ، وَإِنّا إِنْ شاءَ اللهُ بِكُـمْ لاحِقُـونَ، (وَيَرْحَمُ اللَّهُ الْمُسْتَقْدِمِينَ مِنَّا وَالْمُسْتَأْخِرِينَ) أَسْـاَلُ اللهَ لَنَـا وَلَكُـمْ العَـافِيَةَ.

Assalaamu ’Alaykum ahlad-diyaar minal Mu-uminiyna wal Muslimiyn, wainnaa In Shaa Allaahu bikum laahiquwn. (Wa yarhamu-Allaahu al-mustaqdimiyna minnaa wal musta-akhiriyna). As-alu-Allaaha lanaa walakumul-’aafiyah.



Amani ishuke juu yenu watu wa nyumba za Waumini na Waislamu, nasi apendapo Allaah tutakutana nanyi (Na Allaah Awarehemu wa mwanzo na wa mwisho). Namuomba Allaah Atupe sisi nanyi afya njema. [Hadiyth ya Buraydah bin Al-Huswayb (Radhwiya Allaahu ‘anhu) - Muslim (2/671) [975], Ibn Maajah na tamshi lake (1/494) [1547] kutoka kwa Buraydah (Radhwiya Allaahu ‘anhu). Yaliyo katika mabano ni Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) iliyopokelewa na Muslim (2/671) [974].]
 
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ



Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!



12 -Kuchinja Kwa Niyyah Ya Asiyekuwa Allaah




Alhidaaya.com









Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anaharamisha:





حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ وَالْمُنْخَنِقَةُ وَالْمَوْقُوذَةُ وَالْمُتَرَدِّيَةُ وَالنَّطِيحَةُ وَمَا أَكَلَ السَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيْتُمْ وَمَا ذُبِحَ عَلَى النُّصُبِ وَأَن تَسْتَقْسِمُوا بِالْأَزْلَامِ ۚ ذَٰلِكُمْ فِسْقٌ



Mmeharamishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na kilichotajiwa asiyekuwa Allaah katika kuchinjwa kwake, na aliyenyongwa au aliyepigwa akafa, au aliyeporomoka, au aliyepigwa pembe, na aliyeliwa na mnyama mwitu, isipokuwa mliyewahi kumchinja kihalali (kabla ya kufa); na waliochinjwa kwa ajili ya ‘ibaadah ya waabudiwa, na kupiga ramli kwa mishale. Hayo kwenu ni ufasiki. [Al-Maaidah: 3]





Sababu kuchinja ni ‘ibaadah tukufu kabisa Ameamrisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ichinjwe kwa ajili Yake Pekee.

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ ﴿٢﴾

Basi swali kwa ajili ya Rabb wako na chinja kwa ajili Yake. [Al-Kawthar: 2]



Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦٢﴾

Sema: “Hakika Swalaah yangu, na kuchinja kafaara na ‘ibaadah zangu na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah Pekee Rabb wa walimwengu.” [Al-An’aam: 162]





Na Rasuli wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) amelaani mwenye kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Hadiyth ya ‘Aliy bin Abiy Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu):



عَنْ عَلِيِّ بن أبي طالب (رضي الله عنه) قَالَ: حَدَّثَنِي رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) بأرْبَعِ كَلِمَاتٍ: ((لَعَنَ اللَّهُ مَنْ ذَبَحَ لِغَيْرِ اللَّهِ, وَلَعَنَ اللَّهُ مَنْ لَعَنَ وَالِدَيْهِ, وَلَعَنَ اللَّهُ مَنْ آوَى مُحْدِثًا, وَلَعَنَ اللَّهُ مَنح مَنَارَ الأَرْضِ ))

Imepokewa kutoka kwa ‘Aliy bin Abiy Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alinihadithia maneno manne: ((Allaah Amemlaani anayechinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, na Allaah Amemlaani anayewalaani wazazi wake, na Allaah Amelaani anayemkaribisha na kumhami mhalifu, na Allaah Amelaani anayemlaani mzazi wake, na Allaah Amelaani anayebadilisha mipaka ya ardhi [anayomiliki])) [Muslim]





Pia:



‏حديث ثَابِتُ بْنُ الضَّحَّاكِ قَالَ : نَذَرَ رَجُلٌ عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنْ يَنْحَرَ إِبِلاً بِبُوَانَةَ فَأَتَى النَّبِىَّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ: ‏إِنِّى نَذَرْتُ أَنْ أَنْحَرَ إِبِلاً بِبُوَانَةَ. فَقَالَ النَّبِىُّ -صلى الله عليه وسلم : ((هَلْ كَانَ فِيهَا ‏وَثَنٌ مِنْ أَوْثَانِ الْجَاهِلِيَّةِ يُعْبَدُ)) قَالُوا: لاَ. قَالَ: ((هَلْ كَانَ فِيهَا عِيدٌ مِنْ أَعْيَادِهِمْ )) ‏قَالُوا : لاَ. قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((أَوْفِ بِنَذْرِكَ فَإِنَّهُ لاَ وَفَاءَ لِنَذْرٍ ‏فِى مَعْصِيَةِ اللَّهِ وَلاَ فِيمَا لاَ يَمْلِكُ ابْنُ آدَمَ )). وصححه الألباني

Imepokelewa kutoka kwa Thaabit ibn Adhw-Dhwahhaak (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba: “Mtu mmoja aliweka nadhiri kuchinja ngamia sehemu ya Buwaanah. Akaja kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Nimeweka nadhiri kuchinja ngamia Buwaanah”. Akasema Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Je kuliweko masanamu ya kijaahiliyyah (kabla Uislamu) yakiabudiwa?”. Wakasema: “Hapana” Akasema: ((Je kuliweko sherehe za kijaahiliyyah zikifanywa hapo?)). Wakasema: “Hapana” Rasuli wa Allaahh (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Timiza nadhiri yako, kwani hakuna kutimiza nadhiri katika kumuasi Allaah, wala katika ambayo hayamiliki bin Aadam)). [Abuu Daawuwd na ameisahihisha Al-Albaaniy]



Al-Lajnah Ad-Daaimah (1/226) wamefutu: “Kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah ni shirki na hukmu ya kichinjo ni hukmu ya nyamafu (mzoga) haijuzu kuliwa nyama yake hata kama imetajwa Jina la Allaah ikiwa imehakiki kuwa imechinjwa ghairi ya Allaah.”





Na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema katika Majmuw' Fataawa Ibn ‘Uthaymiyn (2/148): “Kuchinja kwa ajili kwa ajili ya aisyekuwa Allaah ni shirki kubwa kwa sababu kuchinja ni ‘ibaadah, kwa hiyo anayechinja kwa ajili (niyyah) asiyekuwa Allaah ni mshirikina ambaye shirki yake inamtoa nje ya Uislamu – tunajikinga na Allaah – ikiwa amechinja kwa ajili ya Malaika au kwa ajili ya Nabiy yeyote au kwa ajili ya Khaliyfah yeyote au kwa ajili ya awliyaa (waja wema) au kwa ajili ya Mwanachuoni yeyote. Yote ni kumshirikisha Allaah (Subhanaahu wa Ta’aalaa) na inamtoa nje ya Uislamu. Na kuhusu kula nyama ya vichinjo hivyo ni haraam kwa sababu amechinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Allaah na kila kinachochinjwa kwa ajili ya chochote ghairi ya Allaah au amechinjwa juu ya jiwe la madhabahu (mazimwi) ni haraam.”





Hadiyth ifuatayo inadhihirisha kwamba hata ikiwa ni kiasi kidogo vipi kitu kinachokurubishwa pasi na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa kuchinja, huwa ni shirki na hatari yake humuingiza mtu Motoni:



((دَخَلَ الْجَنَّةَ رَجُلٌ فِي ذُبَاب، وَدَخَلَ النَّار رَجُلٌ فِي ذُبَاب)): قَالُوا: وَكَيْفَ ذَلِكَ يَا رَسُولَ الله؟ قَالَ: ((مَرَّ رَجُلانِ علَى قَوْمٍ لَهُمْ صَنَمٌ لاَ يَجُوزُهُ أحَدٌ حَتَّى يُقَرِّبَ لَهُ شَيْئاً، فَقَالُوا لإَحَدِهِمَا: قَرِّبْ، قَالَ: لَيْسَ عِنْدِي شَيْءٌ أُقَرِّبَهُ، قَالُوا بِه: قَرِّبْ وَلَوْ ذُباَبًا، فَقَرَّبَ ذُبَاباً، فَخَلُّوا سَبِيْلَهُ، فَدَخَلَ النَّارَ، وَقَالُوا لِلآخر: قَرِّبْ، فَقَالَ: مَا كُنْتُ لأُقَرِّبَ لأحَدٍ شَيْئًا دُونَ الله عَزَّ وَجَلَّ. فَضَرَبُوا عُنقَهُ، فَدَخَلَ الْجَنَّةَ))

((Mtu mmoja ameingia Jannah kwa nzi, na ameingia Motoni mtu kwa ajili ya nzi)). Wakasema: Vipi hivyo ee Rasuli wa Allaah? Akasema: ((Watu wawili walipitia mbele ya watu walikuwa na sanamu lao, hapiti mtu hadi ajikurubishe kwa kuchinja. Wakamwambia mmoja wao: Jikurubishe! [Chinja!] Akasema: Sina kitu cha kujikurubisha. Wakasema: Jikurubishe japo kwa nzi. Akajikurubisha kwa nzi. Wakamwachia apite njia akaingia Motoni. Wakawambia mwengine: Jikurubishe! Akasema: Sikuwa najikurubisha [nachinja] kwa yeyote pasi na Allaah ‘Azza wa Jalla. Wakampiga shingo [wakamuua] akaingia Jannah)). [Ahmad, Fataawaa Shaykh Ibn Baaz]





Shaykh Fawzaan bin Fawzaan akifafanua Hadiyth hiyo anasema:

“[Mtu wa kwanza] Ametoa udhuru kutokuwa na kitu. Hakusema “hakika kuchinja pasi na Allaah haijuzu au ni munkari” – Tunajikinga kwa Allaah. Na hii inafahamika kwamba lau angelikuwa ana mnyama wa kuchinja angelichinja. Wakamwambia: “Jikurubishe walau kwa nzi!” Akajikurubisha kwa nzi, yaani akafanya hivyo kwa ajili ya sanamu wakamwachia apite njia, akaingia Motoni kwa sababu ya shirki. Amejikurubisha pasi na Allaah, na 'ibra (zingatio) hapa ni niyyah na kusudio wala sio kuhusu kinachochinjwa. Na kwamba hakuchukia jambo hili wala hakujiepusha nalo, bali ametoa udhuru kutokuwa na kitu na kwa hivyo amengia Motoni – Tunajikinga kwa Allaah.



Na wakamwambia mwengine: “Jikurubishe!” Akasema: “Sikuwa ni mwenye kuchinja chochote kwa ajili ya asiyekuwa Allaah ‘Azza wa Jalla.” Amejiepusha na amechukia shirki. Wakampiga shingo yake, kwa maana wamemuua akaingia Jannah kwa sababu ya Tawhiyd.



Hivyo basi katika Hadiyth hii tukufu kuna mafunzo muhimu:





Kwanza: Hadiyth inaruhusu kuelezea habari za ummah zilizopita na kuelezea ilivyothibiti kwa ajili ya kuwaidhi na zingatio.





Pili: Katika Hadiyth kuna dalili ya kuharamishwa kujikurubisha kwa kuchinja pasi na Allaah, na mwenye kujikurubisha pasi na Allaah, atakuwa ametenda shirki kwa sababu mtu aliyeua nzi ameingia Motoni hata ikiwa ni kitu kichafu cha kutemwa (kidogo, duni mno). Na mtu wa pili amechukia shirki na amejiepusha japokuwa ilikuwa ni kitu cha kuchukizwa (duni) akaingia Jannah.





Tatu: Kama alivyosema Shaykh (Rahimahu Allaah) kuhusu mas-alah ya niyyah ya 'amali za moyo, japokuwa ni kitu kichafu cha kutemwa (kidogo, duni mno) lakini itambulike kuwa niyyah ni 'amali ya moyo.





Nne: Kama alivyosema Shaykh (Rahimahu Allaah) kuhusu wepesi wa bin Aadam kukaribia Jannah na Moto ni kama alivyosema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Jannah iko karibu zaidi kwa mmoja wenu kuliko nyuzi za viatu vyake, na Moto kama hivyo)). [Al-Bukhaariy]



Huyu amepigwa shingo yake (ameuliwa) akaingia Jannah. Na yule wamemwachia njia akaingia Motoni.



Tano: Kwamba mtu aliyeua nzi alikuwa Muumini, akaingia Motoni kwa sababu ya kujikurubisha kwake kwa nzi, kwa sababu angelikua kafiri, angeliingia Motoni kwa kufru yake si kwa kujikurubisha kwa nzi. Akadhihirisha kwamba alikuwa Muumini, na mas-alah haya ni khatari sana!



Basi wako wapi wanaochinja kwa ajili ya makaburi, na majini, na mashaytwaan, na kwa ajili ya ardhi, na wachawi?



Akaonyesha kwamba shirki kubwa kabisa inamtoa mtu nje ya Dini japokuwa ikiwa ni kitu chepesi. Hivyo basi, suala la Tahwiyd na ‘Aqiydah hayasamehe hayo.” [Sharh Kitaab At-Tawhiyd – Baab maa jaa-a fiy adhdhab-h li-ghayri-LLaah]
 
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!



13- Kutundika Kitu Kwa Ajili Ya Kinga Na Kumlinganisha Allaah


Alhidaaya.com





Katika kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni kutundika vitu ukatani au milangoni n.k. Itikadi ya kitendo hiki ni aina mbili;



Kwanza: kutundika kwa kuitakidi kwamba hicho kitu kilichotundikwa ni kinga ya jicho au husda n.k. Vinavyotundikwa huenda ikawa ni fremu za Aayah katika Qur-aan, au du’aa au Majina ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Au wengine hutundika vitu kama pilipili na ndimu, aina ya vijiwe vya buluu vyenye jicho n.k. Yote haya ni shirki kwa hiyo haijuzu abadani kwa sababu hakuna baya lolote la kumdhuru mtu isipokuwa kama Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amelikidhia kama Anavyosema:



مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۗ وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ يَهْدِ قَلْبَهُ ۚ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴿١١﴾

Hausibu msiba wowote isipokuwa kwa idhini ya Allaah. Na yeyote anayemuamini Allaah, (Allaah) Huuongoza moyo wake. Na Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi. [At-Taghaabun: 11]



Na kinyume chake ni kukosa kutawakali Kwake Subhaanahu wa Ta’aalaa na kukosa kufuata kinga iliyothibiti. Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Hukaym ifuatayo imethibitisha katazo hilo:



((مَنْ تَعَلَّقَ شَيْئًا؛ وُكِّلَ إِلَيْهِ)) رَوَاهُ أَحْمَدُ وَالتِّرْمِذِيُّ

((Atakayetundika kitu (kuitakidi ni kinga) basi amejiweka katika ulinzi wa hicho kitu alichokivaa)) [na kitamdhalilisha]. [Ahmad na At-Tirmidhiy. Hadiyth Marfu’w]



Tanbihi: Mifano ya vitu vinavyotundikwa kuitakidi kuwa kitamfaa au kumzuia shari ni: talasimu, hirizi, zindiko na vinginveyo kama ilivyobainishwa katika makala hizi.



Haijuzu kabisa kutundikia kitu kuitakidi ni kinga, bali inatosha kabisa kutawakali kwa Allaah kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema :



وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ فَهُوَ حَسْبُهُ

Na yeyote anayetawakali kwa Allaah, basi Yeye Humtosheleza. [Atw-Twalaaq: 3]



Na mafunzo Swahiyh ya kujikinga ni kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:





عن خَوْلَةَ بِنْتَ حَكِيمٍ (رضي الله عنها) قالت: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((مَنْ نَزَلَ مَنْزلاَ ثُمَّ قَالَ: "أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللَّهِ التَّامَّاتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ" لَمْ يَضُرَّهُ شَيْءٌ حَتَّى يَرْتَحِلَ مِنْ مَنْزِلِهِ ذَلِكَ)) رواه مسلم

Imepokelewa toka kwa Khawlat bint Hakiym (Radhiwa Allaahuu ‘anhaa) kwamba kamsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Atakayefikia mahali kisha akasema:

أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللَّهِ التَّامَّاتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ



A’uwdhu bikalimati-LLaahit-taammati min sharri maa Khalaq' (Najilinda kwa maneno ya Allaah yaliyotimia na shari ya Alichokiumba), hakuna kitakachomdhuru hadi atakapoondoka mahali pake hapo)). [Muslim]





Mafunzo mengine sahihi ni kusoma Adhkaar na nyiradi za asubuhi na jioni zilizothibiti.



Ama kuhusu kutundika Qur-aan, baadhi ya watu wanaona ni jambo la kupendeza lakini hakika haijuzu kwa sababu Qur-aan imeteremshwa kwa ajili ya Mwongozo, mawaidha, ukumbusho, na kusomwa na kufanyia kazi maamrisho yake na kuacha makatazo yake, na wala si kwa ajili ya kutundikwa.



Ibnul-‘Arabiyy Al-Maalikiyy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kutundika Qur-aan si katika Sunnah, bali Sunnah ni kuisoma bila ya kuitundika.”





Aghlabu ya watu hutundika Aayatul-Kursiyy au Al-Maw’idhataan na Suwratul-Ikhlaasw ambazo ni nyepesi kabisa kuzihifadhi na kuzisoma na ndizo zilizothibiti katika mafunzo Swahiyh kwamba ni kinga ya Muislamu. Basi kwanini mtu atundike badala ya kuzisoma na kuzihifadhi?



Picha za baadhi ya vitu ambavyo baadhi ya watu wanavitundika wakiamini ni kinga:

















Pia kutundika vitu madukani au majumbani kama pilipili, ndimu n.k.

















Pili: Kutundika Jina la Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ukutani mifano kama ifuatavyo:



























Haijuzu kutundika picha kama hizo, kwani haiwezekani kuwa Muumba na aliyeumbwa wawe katika daraja moja, hata kama niyyah ni kupamba nyumba au kudhihirisha mapenzi yao, kwa sababu wengi hudai kuwa hawakusudii kumlinganisha sawa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Basi kujiepusha na hilo ni bora hata kama mtu haitakidi hilo, kwani kukaa mbali na utata ndio njia ya salama katika Dini ya mtu.



Kadhaalika, Wanachuoni wamekemea jambo hili kama ifutavyo:



Fatwa ya 1 - Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah Lil-Buhuwth Al-'Ilmiyyah Wal-Iftaa imepitia yaliyofikishwa kwa Mufti Mkuu kutoka kwa muulizaji Humuwd ‘Abdul-Aziyz As-Saayigh kwa marejeo Nambari 6860 9/11/1421H.



Muulizaji ameuliza swali na haya hapa maelezo yake:

“Allaah Akuhifadhini, na kukhofia yanayojiri katika Dini hii na kutilia mkazo yanayofisidi ‘Aqiydah na ambayo yanaenea kwa Ummah huu kutoka kwa maadui wa Allaah na wa Dini Yake na wepesi wa watu kufuata mambo wanayodhania ni madogo mno lakini kumbe ni makubwa mno na ikawa kuondosha madhara yake ni vigumu. Kama ilivyokuwa hali katika watu wa Nuwh na masanamu yao; walivyoanza kuweka picha za waja wema wakaanza kuziabudu wakidhania ni jambo jema kumbe ni shirki iliyowasababisha watu waliofuata kuabudu masanamu.



Tunadhihirisha mbele yenu aina mbali mbali za picha zilizotayarishwa kuwekwa pande mbili; upande kuna Jina la Allaah (’Azza wa Jalla) na upande wa jina la Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Wala sijui lipi bado litakalojiri baada ya haya! Na baadhi ya ndugu wamewaandikia Baraza la Fatwa maombi haya ili kufuatilia maovu ya ‘Aqiydah wakitaraji mtoe maoni yenu ambayo huenda ikiwa ni sababu ya ufumbuzi na tiba ya kuondosha uovu huu, Allaah Awathibitishieni na Akulipeni kwa kuwanufaisha waja Wake Katika utiifu Wake.”



Jibu la Baraza la Fatwa:



Haijuzu kuandika Jina la Allaah Aliyetukuka [Allaah] pamoja na [Muhammad] jina la Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) sambaba katika karatasi au kwenye ubao [au vitambaa], au kutundika ukutani [kwa hali yoyote]. Huko ni kupindukia mipaka kwa haki yake Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na kumlinganisha yeye sawa na Allaah. Haya ni mas-alah miongoni mwa masuala ya shirki na hali yeye mwenyewe amekataza katika kauli yake, aliposema:

“Msinitukuze kama Manaswara walivyomtukuza Masiyh mwana wa Maryam, hakika mimi ni mja kwa hiyo semeni mja wa Allaah na Rasuli Wake.”



Na hivyo ni wajibu kuondosha picha hizo au karatasi na kufutilia mbali maandishi kama hayo katika kuta au popote penye aina hizo za picha, ili tuilinde ‘Aqiydah na kufuata wasia wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

Wa biLLaahi At-tawfiyq. Wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyinaa wa ‘alaa aalihi wa swahbihi wa sallam.



[Fataawa Al-Lajnah Ad-Daaimah Lil-Buhuwth Al-'Ilmiyyah Wal-Iftaa]





Fatwa ya 2: Fatwa ya Shaykh Ibn ‘Uthaymin (Rahimahu Allaah):

Hakika kuandikwa Jina la Allaah (الله) upande mmoja na jina la (محمد) upande wa pili, yakiwa majina hayo yako sambamba na kama hivi:

الله *** محمد yanamfanya anayetazama kuona kwamba wako katika cheo kimoja na hali Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimjibu mtu mmoja aliyemwambia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) “Atakavyotaka (au Akipenda) Allaah [In Shaa Allaah) na ukataka wewe.” Akamjibu: ((Je umenilinganisha mimi kuwa sawa Allaah? Bali sema: Akipenda Allaah [In Shaa Allaah] pekee)).



Na ikiwa maandishi kama hayo yamewekwa hivyo mbele ya wanaoswali, yatakuwa ni sababu ya kuwashughulisha watu na Swalaah zao. Pia ‘Ulamaa wakubwa wamechukizwa [na kukataza] kuandikwa kitu mbele ya Qiblah kwa sababu kitamshughulisha na kumshawishi mwenye kuswali. Hivyo, haipasi kuandikwa hivyo; namaanisha الله *** محمد Na popote palipoandikwa hivyo panapaswa kufutiliwa mbali!

Na katika sharh yake ya Kitabu cha Buluwghul-Maraam, Kitabu cha Swalaah, Mlango wa Misikiti, Mkanda namba 16 upande wa pili, anasema Shaykh kuwa, kwa uchache maandishi kama haya ni shirk ndogo.”

Ameandika: Muhammad Bin Swaalih Al-‘Uthaymiyn 9/1/1420H.





Basi ndugu Waislamu tutahadhari kutundika vitu kama hivyo au chochote kile mfano wa hivyo kwa kuitakidi ni kinga au baraka.
 
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!

14 -Kuvaa Kitu Kwa Ajili Ya Kinga


Alhidaaya.com





Itikadi za watu kuvaa vitu au kujifunga navyo mwilini kwa kuepusha au kujikinga na kijicho, husda na madhara mengineyo. Jambo hili halijuzu kwa sababu hivyo vitu havina uwezo wa hayo wala hakuna atakayeweza kumuondoshea mtu madhara isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Anasema:



وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يَمْسَسْكَ بِخَيْرٍ فَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٧﴾

Na Allaah Akikugusisha kwa dhara, basi hakuna yeyote wa kukuondolea hiyo isipokuwa Yeye; na Akikugusisha khayr, basi Yeye juu ya kila kitu ni Muweza. [Al-An’aam: 17]





Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameharamisha hayo katika Hadiyth mbali mbali:



عَنْ قَيْسِ بْنِ السَّكَنِ الأَسَدِيِّ قَالَ: دَخَلَ عَبْدُ اللهِ بْنُ مَسْعُودٍ رضي الله عنه عَلَى امْرَأَةٍ، فَرَأَى عَلَيْهَا خَرَزًا مِنَ الحُمْرَةِ، فَقَطَعَهُ قَطْعًا عَنِيفًا، ثُمَّ قَالَ: إِنَّ آلَ عَبْدِ اللهِ عَنِ الشِّرْكِ أَغْنِيَاءُ، كَانَ مِمَّا حَفِظْنَا عَنِ النَّبِيِّ صلّى الله عليه وسلّم: ((إِنَّ الرُّقَى وَالتَّمَائِمَ وَالتِّوَلَةَ شِرْكٌ)) رواه الحاكم وقال: " صحيح الإسناد "، ووافقه الذّهبي والألبانيّ في "الصّحيحة" (برقم 331).

Imepokelewa kutoka kwa Qays bin As-Sakan Al-Asadiyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Abdullaah bin Mas‘uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) aliingia kwa mwanamke ambaye alivaa shanga nyekundu, akazikatilia mbali kisha akasema: “Hakika ahli ya ‘Abdullaah hawahitaji shirki!”. Akasema pia: “Katika ambayo amehifadhi kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni: ((Hakika Ar-Ruqaa (zisizothibiti), At-Tamaaim, At-Tiwaalah ni shirki).)) [Al-Haakim amesema Isnaad Swahiyh na ameikubali Adh-Dhahabiy na Al-Albaaniy katika Asw-Swahiyhah (331)]



At-Tamaaim: Wanachofungwa watoto (kama kitambaa cheusi au nyuzi n.k.) shingoni (au mkononi) kukinga jicho baya.





Ar-Ruqaa au Al-‘Azaaim: Ni tabano au azima inayosomwa. Imeruhusiwa tu inapokuwa haina shirki. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameiruhusu inapokuwa hali ya kudonelewa na mdudu sumu au anapopatwa mtu na jicho baya (au husda) au homa.





At-Tiwaalah (mvuto wa ndere): Kinachodaiwa kuwa kinasababisha mwanamke apendwe zaidi na mumeme au mume apendwe zaidi na mkewe.





Hadiyth nyenginezo zinazoharamisha kuvaa vitu kwa ajili ya kinga ni zifuatazo:



عَنْ أَبِي بَشِيرٍ الأَنْصَارِيِّ (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) أَنَّهُ كَانَ مَعَ رَسُولِ اللهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فِي بَعْضِ أَسْفَارِهِ، فَأَرْسَلَ رَسُولاً, أَنْ ((لاَ يَبْقَيَنَّ فِي رَقَبَةِ بَعِيرٍ قِلادَةٌ مِنْ وَتَرٍ أَوْ قِلادَةٌ إِلاَّ قُطِعَتْ)).

Imepokewa kutoka kwa Abu Bashiyr Al-Answaariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba alikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika safari mojawapo. Akamtuma mjumbe kuamrisha kwamba: ((Kusiachwe kidani cha uzi au kidani chochote katika shingo za ngamia isipokuwa kikatwe)). [Al-Bukhaariy na Muslim]



Pia:



رَوَى أَحْمَدُ عَنْ رُوَيْفِعٍ قَالَ؛ قَالَ لِي رَسُولُ اللهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((يَا رُوَيْفِعُ، لَعَلَّ الْحَيَاةَ سَتَطُولُ بِكَ؛ فَأَخْبِرِ النَّاسَ أَنَّ مَنْ عَقَدَ لِحْيَتَهُ، أَوْ تَقَلَّدَ وَتَرًا، أَوِ اسْتَنْجَى بِرَجِيعِ دَابَّةٍ أَوْ عَظْمٍ؛ فَإِنَّ مُحَمَّدًا بَرِيءٌ مِنْهُ))

Ahmad amepokea kutoka kwa Ruwayfi’ ambaye amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameniambia: ((Ee Ruwayfi’! Huenda ukaishi zaidi baada yangu. Kwa hiyo wajulishe watu kwamba: Yeyote atakayefunga fundo ndevu zake, au akaweka nyuzi au mshipi shingoni mwake [kuwa ni talasimu] au akastanji na mkojo wa mnyama au mfupa, basi Muhammad amejitenga naye)). [Ahmad, Abuu Daawuwd]





Vitu ambavyo aghlabu hutumiwa na watu kuvivaa au kujifunga wakiamini vinawakinga:





a) Hirizi za vitambaa vyenye maandishi ndani ikiwa ya Quraan au mengineyo.























b) Mtoto mchanga kupakwa masinzi au wanja usoni au kuandikwa Jina la Allaah!





c) Kuwapaka watoto wachanga wanja usoni na nakshi za nyota na mwezi, kwa kuamini ule wanja unazuia 'ayn (kijicho).





d) Anapolazwa mtoto mchanga kukiwa chini ya mto wake vitu kama kisu, ndimu n.k.





e) Kuvalishwa vyuma mkononi.



f) Kuvalishwa mtoto mchanga au hata wakubwa, kidani chenye lakti ya Aayatul-Kursiy au Jina la Allaah! Ni jambo linalotendwa na wengi! Hakika ni kosa kubwa kwani ni kudhihirisha kutokumadhimisha Allaah kwa sababu kidani hicho anaingia nacho mtu chooni. Juu ya hivyo ni kuitakidi kuwa kinamkinga mtu na shari, uhasidi, jicho n.k. Imeshatangulia Hadiyth mbali mbali na Fataawa za ‘Ulamaa kukataza haya, na rejea mlango wa “Kutundika vitu”.



g) Kuvalishwa kitambaa cheusi mkononi wengine wanatia mvuje ndani yake yenye harufu mbaya kuepusha majini.



h) Mapambo yenye kuandikwa Aayah za Qur-aan:









i) Mapambo ya vijiwe vya rangi ya buluu, vinginevyo vina jicho.





































j) Kuvaa pete au mapambo yenye vito rangi kadhaa kwa kuitakidi rangi hizo zina maana ya wanachoita ‘bahati nzuri’ au kuleta hali fulani njema kutokana na tarehe au miezi ya kuzaliwa:
 
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!

15- Kuapa Kwa Asiyekuwa Allaah


Alhidaaya.com







Haijuzu Muislamu kuapa isipokuwa kwa Jina la Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa sababu kuapia kwa yeyote au chochote ni kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Inavyopasa kuapa ni ima kusema: “Wa-Allaahi”, au “BiLLaahi” au “Ta-Allaahi” kama ilivyothibiti katika Qur-aan. Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kuapia chochote isipokuwa kwa Jina la Allaah akasema:



مَنْ حَلَفَ بِغَيْرِ اللَّهِ فَقَدْ كَفَرَ أَوْ أَشْرَكَ

((Atakayeapa pasi na Allaah, atakuwa amekufuru na amemshirikisha Allaah) [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Hibbaan, Al-Haakim na wengineo na ameipa daraja ya Swahiyh Al-Albaaniy]



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Pekee Ndiye Mwenye haki kuapia Atakacho kwani Yeye ni Muumba wa kila kitu. Ndio maana Anaapia katika Qur-aan vitu vingi; Wa-Tiyni waz-Zaytuni, Wal-‘Aswr, Wadh-Dhwuhaa, Wash-Shamsi, Wal-Layli, Wal-Fajr, Wal-‘Aadiyaat n.k.



Hata Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) haikumpasa kuapia chochote, na ndio maana tunaona anapotaka kuapa, mara nyingi husema:



وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ

Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake… [Akimkusudia Allaah]





Na akakataza katika Hadiyth mbali mbali zifuatazo kuapia kwa yeyote au kwa chochote isipokuwa kuapia kwa Allaah pekee:



عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ رَضِي اللَّه عَنْهمَا أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَدْرَكَ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ وَهُوَ يَسِيرُ فِي رَكْبٍ يَحْلِفُ بِأَبِيهِ فَقَالَ : أَلَا إِنَّ اللَّهَ يَنْهَاكُمْ أَنْ تَحْلِفُوا بِآبَائِكُمْ مَنْ كَانَ حَالِفًا فَلْيَحْلِفْ بِاللَّهِ أَوْ لِيَصْمُتْ

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaahi bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikutana na ‘Umar bin Al-Khattwaab akiwa katika msafara wa ngamia akawa ameapia kwa baba yake. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Tanabahi Allaah Anawakatezeni kuapia kwa baba zenu. Anayetaka kuapa basi aapie kwa Allaah au anyamaze kimya)) [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]



Pia:



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ - رضي الله عنه: لَا تَحْلِفُوا بِآبَائِكُمْ, وَلَا بِأُمَّهَاتِكُمْ, وَلَا بِالْأَنْدَادِ, وَلَا تَحْلِفُوا إِلَّا بِاللَّهِ, وَلَا تَحْلِفُوا بِاللَّهِ إِلَّا وَأَنْتُمْ صَادِقُونَ

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Msiapie kwa baba zenu wala mama zenu, wala kwa mnaowalinganisha na Allaah. Na wala msiape isipokuwa kwa Allaah, wala msiape kwa Allaah isipokuwa mnapokuwa mnasema ukweli)) [Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy]



Amekataza pia kuapia kwa uaminifu akasema Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam:



عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ بُرَيْدَةَ عَنْ أَبِيهِ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: (لَيْسَ مِنَّا مَنْ حَلَفَ بِالأَمَانَةِ

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Buraydah kutoka kwa baba yake kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Si miongoni mwetu anayeapia kwa amana)) [Ahmad (5/325) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika As-Silsilah Al-Hadiyth Asw-Swahiyhah (1/325)]





Na Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



مَن حلَف فقال في حَلِفه: باللات والعُزَّى، فليقل: لا إله إلا الله

((Yeyote atakayeapa akasema katika kiapo chake: “Naapa kwa Al-Laata, na Al-’Uzzaa” basi aseme: “Laa ilaaha illa-Allaah”)) [Al-Bukhaariy na Muslim]





Na Ibn Mas-‘uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema:



لأَنْ أَحْلِفَ بِاللَّهِ كَاذِبًا أَحَبُّ إِلَيَّ مِنْ أَنْ أَحْلِفَ بِغَيْرِهِ صَادِقًا

“Ni bora kwangu kuapa kwa Jina la Allaah wakati naongopa kuliko kuapa kwa asiyekuwa Allaah kwa jambo la kweli.” [Majm’a Az-Zawaaid (4/180), na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Targhiyb (2953)]







Aina za viapo ni vitatu:





1- Al-Yamiyn Al-Ghamuws (Kiapo cha uongo):



Ni kula kiapo huku kukusudia kuongopa, kama vile kusema: “Wa-Allaahi nimenunua kitu kadhaa kwa gharama ya fedha kadhaa”, na hali si kweli kuwa umenunua bei hiyo. Au kusema: “Wa-Allaahi nimefanya kadhaa”, na hali hakufanya. Kuapa hivi ni miongoni mwa madhambi makubwa kama alivyosema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو بْن الْعاص (رضي الله عنهما) عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ َقَالَ: ((الْكَبَائِرُ الإِشْرَاكُ بِاللَّهِ وَعُقُوقُ الْوَالِدَيْنِ وَقَتْلُ النَّفْسِ وَالْيَمِينُ الْغَمُوسُ)) البخاري

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amri bin Al-‘Aasw (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Al-Kabaair [Madhambi makubwa] ni kumshirikisha Allaah, kuwaasi wazazi wawili, kuua nafsi na yamini [kiapo] ya uongo)) [Al-Bukhaariy]



Na katika riwaya nyingine:



أنَّ أَعْرَابِياً جَاءَ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّه,ِ مَا الْكَبَائِر؟ ُ قَالَ: ((الإشْرَاكُ بِاللَّهِ)) قَالَ: ثُمَّ مَاذَا؟ قَالَ: ((الْيَمِينُ الْغَمُوسُ)) قُلْتُ: وَمَا الْيَمِينُ الْغَمُوسُ؟ قَالَ: ((الَّذِي يَقْتَطِعُ مَالَ امْرِئٍ مُسْلِمٍ!)) يَعْنِ: بِيَمِينٍ هُوَ فِيهَا كَاذِبٌ

Alikuja Bedui mmoja kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza: Ee Rasuli wa Allaah! Ni yepi Al-Kabaair [madhambi makubwa]?” Akasema: ((Kumshirikisha Allaah)) Akasema: Kisha yepi? Akasema: ((Yamini ya uongo)). Nikauliza: Ni ipi yamini ya uongo? Akasema: ((Ni ambayo mtu hujichukulia mali ya Muislamu!)) yaani akaapa kwa uongo. [Al-Bukhaariy]



Imeitwa Yamiyn Al-Ghamuws (kiapo cha uongo) kwa sababu yamzamisha mwenye yamini hiyo ndani ya dhambi na yamini hii ndiyo iliyokusudiwa katika kauli ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



مَنْ حَلَفَ يَمينٍ صَبْرٍ لِيَقْتَطِعَ بِها مَالَ امْرِىءٍ مُسْلِمٍ، لَقِيَ اللهَ وَهُوَ عَلَيْهِ غَضْبانُ

((Atakayekula yamini hali yeye katika yamini hiyo anaongopa ili apate kwa yamini hiyo kumega mali ya mtu mwengine Muislamu basi mtu huyo atakutana na Allaah hali Amemghadhibikia)). [Al-Bukhaariy na Muslim]



Hukmu yake: Kuna kauli mbili,



i) Yamiyn Al-Ghamuws haina kafara bali mtu atubie tawbah ya kwelikweli. Ni rai ya Imaam Abiy Haniyfah, Imaam Maalik na Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahumu-Allaah). Pia Fatwa ya Al-Lajnatud-Daaimah (23/133) wamefutu: ”Al-Yamiyn Al-Ghamuws ni katika madhambi makubwa na haihitaji kafara kwa sababu ya ukubwa wa dhambi yake, bali inahitaji tawbah na kuomba maghfirah na ndio ilivyo sahihi kutokana na kauli za ‘Ulamaa.”



Na Shaykh Al-Islaamiy Ibn Taymiyyah amesema katika Majmuw’ Al-Fataawaa (34/139) baada ya kutaja ikhtilafu kuhusu kiapo cha Ghamuws….

“Wameafikiana kwamba dhambi haianguki kwa ajili ya kufanya kafara”.

Amesema pia:

Ikiwa amemdhulumu mja mwenziwe basi amrudishie haki yake pamoja na kumuomba msamaha.



ii) Ama Imaam Ash-Shaafi’iy ameona inapasa kafara.





2-Al-Yamiyn Al-Laghw (Kiapo cha upuuzi):



Hiki ni kile kiapo kipitacho katika ulimi wa Muislamu bila kukusudia, kama yule ambaye katika mazungumzo yake hujitokeza kwa wingi mno wa neno: “Wa-Allaahi hapana”. Hii ni kufuatia kauli ya Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa):

لغو اليمين كقول الرجل لا والله وبلى والله،

“Upuuzi katika yamini ni maneno anayozungumza mtu, “Hapana Wa-Allaahi, Ndio Wa-Allaahi.” [Al-Bukhaariy]



Hukumu ya yamini aina hii ni kuwa haina dhambi wala kafara kwa mhusika, kwa kauli yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika Suwrah Al-Maaidah (5: 89):



لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ

Allaah Hatokuchukulieni kwa viapo vyenu vya upuuzi, [Al-Maaidah: 89]







3-Al-Yamiyn Al-Mun’aqidah (Kiapo cha kufungika):



Ni kukusudia jambo la baadae. Kama vile Muislamu kusema: “Wa-Allaahi nitalifanya jambo kadhaa” Au “Wa-Allaahi sitolifanya…” kisha akafanya kinyume chake.



Hukmu yake ni katika Suwrat Al-Maaidah (5: 89):



وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا عَقَّدتُّمُ الْأَيْمَانَ

lakini Atakuchukulieni kwa (kuvunja) viapo mlivyoapa kwa niyyah mlioifunga thabiti. [Al-Maaidah: 89]



ambayo inampasa afanye kafara:



فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚوَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٨٩﴾

Basi kafara yake ni kulisha maskini kumi chakula cha wastani mnachowalisha ahli zenu, au kuwavisha nguo, au kuacha huru mtumwa. Lakini asiyeweza kupata (katika hayo), basi afunge Swiyaam siku tatu. Hiyo ndio kafara ya viapo vyenu mnapoapa. Na hifadhini yamini zenu. Hivyo ndivyo Allaah Anavokubainishieni Aayaat (na hukmu) Zake ili mpate kushukuru. [Al-Maaidah: 89]





Vinavyoapiwa kimakosa:



1- Kuapia vitu kadhaa:



Unapoapa kimakosa kwa kutumia vitu kuapia huhitaji kafara bali inakupasa urudi kutubia kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). ‘Ulamaa wamekubaliana hivyo kama alivyosema Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah katika Al-Fataawa Al-Kubraa (3/222):

“Kuapia vitu viliyvoumbwa kama Al-Ka’bah, Malaika, mashekhe, wafalme, wazazi, makaburi ya wazazi n.k haihitajiki kafara kama ilivyokuwa ni rai ya Wanavyuoni. Bali imeharamishwa na Wanavyuoni na haramisho hili ni haraam kutokana na rai iliyo na nguvu kabisa”.





2- Kuapia kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



Baadhi ya watu huapa kwa tamshi la: “Wan-Nabiy!”, “Haki ya Mtume!” n.k.





3- Kuapia kwa Msahafu:



Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) aliulizwa kuhusu hukmu ya kuapia Msahafu alijibu:

"Hairuhusiwi kuweka nadhiri au kuapa isipokuwa kwa Allaah au moja ya Sifa Zake. Ikiwa mtu ataapa kwa jina la Allaah, basi hakuna haja tena kuleta Msahafu kwa ajili ya kuapa kwa sababu kuapa kwa Msahafu haikufanyika zama za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba. Hata baada ya Qur-aan kukusanywa katika Kitabu kimoja hawakuwa wakiapia Msahafu bali mtu alikuwa akiapa kwa Allaah bila ya kushika Msahafu."

[Fataawaa Nuwr 'Alaa Ad-Darb]





4- Kuapia kwa Al-Ka’bah:



Baadhi ya Waislamu hufikishana Makkah kuapizana kwa Al-Ka’bah jambo ambalo halijuzu bali ni kuvuka mipaka ya ‘Ibaadah, na kupoteza muda na mali ya kuwapeleka huko.





5- Kuapia wazazi, watoto:



Makatazo katika Hadiyth zilotanguliwa kutajwa juu.





6- Kuapia ‘amali njema kama Swiyaam (funga), Swadaqah n.k.
 
Back
Top Bottom