utekaji tanzania

No Wikipedia entry exists for this tag
  1. mwanamwana

    JamiiForums Tanzania Azim Dewji: Siamini serikali inaweza kuwa na sababu ya kumpoteza mtu; anaweza kufungwa au kutafutiwa kesi ili kumuondoa kwenye reli

    Mhoji (Charles William): Mara nyingi unapotoka kuzungumzia kuhusu masuala ya amani, utulivu na jinsi ambavyo watu hawatakiwi kuendeshwa na propaganda, kuna watu wamekuwa wakisema mzee Azim Dewji anatakiwa kuungana na Watanzania ambao wanalaani baadhi ya vitu vinavyotokea hapa Tanzania, matukio...
  2. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania Wachokonozi: Kwa sheria za nchi yetu, lile halikuwa zoezi la ukamataji, niliona ni weledi mdogo katika utendaji kazi

    Joseph Mrindoko wa Wachokonozi amesema hakushangazwa na tukio lililomhusisha, akieleza kuwa alilitarajia kutokana na mazingira na upeo wa watu wanaohusika. Amesisitiza kuwa, kwa uelewa wake wa mifumo ya kisheria, kilichotokea hakikuwa zoezi halali la ukamataji kwa kuwa hakikufuata taratibu...
  3. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania Godfrey Mosha: Watanzania wanadanganywa eti kuna utekaji ni uongo mtupu

    Mwenyekiti wa Mufindi Environmental Transformation, Godfrey Mosha, amesema madai kuhusu kuwepo kwa matukio ya utekaji nchini ni ya uongo, akidai yanalenga kueneza hofu na kuidhoofisha Tanzania. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mosha alisema kwa sasa wananchi wana uhuru wa...
  4. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania Mchungaji Kimondo: Tulidhani yaliyotokea Oktoba 29, yangekuwa mwisho, lakini baada ya hapo vitendo vya utekaji vinaendelea

    Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Steven Kimondo, amesema matukio ya utekaji nchini yameanza kuwa jambo la kawaida, akieleza kuwa yanapaswa kukemewa kwa nguvu zote. Amesema ingawa waathirika wa matukio hayo pamoja na familia, marafiki na majirani zao huumia, bado...
  5. Papaa Mobimba

    JamiiForums Tanzania Mchungaji Kimondo: Utekaji unaendelea ili kunyamazisha sauti za watu wasidai haki

    Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Steven Kimondo, amefichua kuwa kuendelea kwa matukio ya utekaji wa raia nchini ni mkakati wa makusudi unaoratibiwa ili kuwatia hofu wananchi na kunyamazisha sauti zote zinazojitokeza kudai haki, utulivu, na usawa. Pia soma >...
  6. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania Prof. Tibaijuka: Watu waliopotea ni doa kubwa kwa taifa hili, Polisi wana wajibu wa kuwatafuta

    Waziri mstaafu na Mchumi, Profesa Anna Tibaijuka, ameeleza kusikitishwa kwake na wimbi la watu kupotea nchini na kulani vitendo hivyo akivitaja kama doa kubwa kwa taifa. "Kazi ya kwanza ya serikali—na mimi nazungumza kama profesa wa uchumi hapa—kazi ya kwanza ya serikali wala sio kuleta...
  7. W

    JamiiForums Tanzania Msanii Hakeem 5: Wanataka kumteka Mama yangu naomba ulinzi wa Serikali

    Msanii Mkongwe wa Bongo Fleva, Hakeem 5 ametoa taarifa kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa kuna watu walienda kwa mama yake usiku majira ya saa sita wakimtaka afungue atoke nje wakidai wao wametumwa na wakubwa na wakijitambulisha kuwa ni polisi hali ilifanya wapate hofu kwanini waende usiku...
  8. Idugunde

    JamiiForums Tanzania Heche ana hoja ya msingi juu ya Polisi. Kwa intelijensia yao iwe inabaini taarifa za mikutano ya Chadema na sio utekaji?

    Hili ni suala la msingi sana ambalo linatakiwa kupatiwa majibu. Wamepotea watu ambao kama taifa watu wanahuzuni kubwa sana. Humphrey Poleole, Azory Gwanda na wengine wengi wanahuzunisha taifa kwa kupotea kwao. Lakini hadi leo hii Polisi wapo kimya. Jambo la ajabu kila siku wanataarifa za...
  9. Chachu Ombara

    JamiiForums Tanzania Heche: Familia mnasema Anthony na wenzake walienda kituo cha polisi, wanapoteaje wakiwa kituoni? Polisi wawarudishe kwenye mikono ya familia zao

    Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, ametembelea familia ya Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Iringa, Ibrahimu Myovela, ambaye kwa mujibu wa familia na chama hicho hajulikani alipo tangu alipopotea mwezi Februari mwaka huน. Kwa hiyo sisi tumekuja ku-sympathize na nyie lakini pia kuwapa...
  10. M

    JamiiForums Tanzania Mwambigija: Askari mnapoambiwa maelezo ya juu kwani lazima ufanikishe dili ya utekaji?

    Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAZECHA) Mkoa wa Mbeya, David Mwambigija, ametoa wito mzito kwa askari wa jeshi la polisi nchini kutojihusisha na matukio ya utekaji wa raia, akisisitiza kuwa wanapaswa kulinda haki badala ya kutekeleza maagizo haramu. Namnukuu...
  11. Q

    JamiiForums Tanzania Godfrey Polepole: Ndani ya siku 4 nitaweka wazi ufisadi wa ndege ya Rais

    Godfrey Polepole ambaye ni mdogo wa Humphrey Polepole ametishia kuweka wazi ufisadi unaofanywa na ndege za rais Gulf Stream 550 na Gulf Stream 700 kama wasipo muachia Balozi Humphrey Polepole. Yetu masikio.
  12. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania Mwigulu: Kutekwa kwa Djumbe ni Michezo na haijaanza Jana

    Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema hayo Mei 23, 2026 wakati akizungumza na wananchi katika Viwanja vya Kichangani kwenye ziara yake ya kikazi ya siku mbili. "Tunagombanishwa mno. Watu wanapoteza muda hata wa kutafakari kila jambo, kwamba hili limetokeaje. Unakaa hivi, unasikia sister...
  13. Cute Wife

    JamiiForums Tanzania Marekani ikitumia Section 7031(c) ina maana wana taarifa za UHAKIKA, mbali na Mafwele kuna majina mangapi mengine kwenye Faili?

    Wakuu, Kama wamechomoa jina la Mafwele wakiwa na data zote hizo, unadhani faili lina majina mangapi? Je, wanasubiri nini kuyachomoa? ====== Kuna tofauti kubwa kati ya kelele za kisiasa na hatua rasmi ya dola. Kwa miaka mingi, Watanzania wamekuwa wakisikia majina ya watu wanaotajwa kwenye...
  14. Cute Wife

    JamiiForums Tanzania Jeshi la Polisi fungueni "comment section" tumsifie Mafwele

    Wakuu, Nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa Jeshi la Polisi kwenye mitandao yao ya kijamii. Naomba kujikita katika post yao ya jana tarehe 2 Machi 2026 ikimhusu Faustine Mafwele kama kiongozi (Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya Jinai Polisi Kanda maalum Dar es Salaam)🌚🌚 Sote tunajua kuwa mtu huyu...
  15. McLaren

    JamiiForums Tanzania Nini kimemkuta yule Mtendaji aliyesema kuwa anahofia maisha yake mbele ya Waziri Mkuu? Mwigulu anajali? Serikali imempatia ulinzi?

    Wakuu, Kama mnakumbuka siku kadhaa nyuma kulikuwa na stori ya Mwenyekiti wa Kitongoji (CCM), aliposema mbele ya Waziri Mkuu kuwa anahofia kutekwa na Kuuwawa baada ya kuzuia miti kukatwa kinyemela huko Machemba, Muheza. Sasa ni kama siku 3 zimepita tangu hiyo ishu kutokea. Nyie wenzangu mna...
  16. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Askofu Gwajima: Magumu yaliyokupata wewe ni kwasababu mimi nilikataa 'Utekaji', mpaka leo nakataa vilevile

    Wakuu, Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Dkt. Josephat Gwajima, ameonekana mara ya kwanza kwenye madhabahu ya kanisa hilo lililopo Ubungo Kibo, Dar es Salaam, katika ibada ya mkesha wa mwaka mpya tangu lilipofungwa Juni 2, 2025. Katika mahubiri yake, amegusia changamoto walizokabiliana...
  17. Cute Wife

    JamiiForums Tanzania Thadei Kweka achukuliwa na watu wanaodaiwa kuwa Polisi baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Moshi

    Wakuu, Kutoka Kisiwa cha Amani mpaka Kisiwa cha Utekaji! Mpaka lini Watanzania tutaacha kuishi wa hofu?! ==== Ameandika Liberatus mtandaoni; "Diaspora mwenzetu mkazi wa USA— Thadei Kweka ametekwa na vikosi vya Samia usiku huu. Polis na watu wasiojulikana wamevamia nyumbani kwake Moshi...
  18. B

    JamiiForums Tanzania Nini kimempata Nicodemus Julius Loyore baada ya kukamatwa na watu waliojitambulisha kuwa Polisi? Yupo wapi?

    Salam Wakuu, Taarifa zilizombaa ni kuwa toka Nicodemus Julius Loyore akamatwe Disemba 19 akiwa ofisini na watu waliojitambulisha kuwa Polisi, mpaka leo hajulikani yupo kituo gani! Toka siku hiyo ndugu zake wanamtafuta katika vituo vya polisi bila mafanikio yoyote! Kama alikuwa na kosa...
  19. Mshana Jr

    JamiiForums Tanzania Askofu Rweyongeza: Kuna watu na makundi yanayotumia nguvu, risasi na mabomu ya machozi kwa sababu ya kushindwa hoja

    Askofu wa Jimbo Katoliki la Kayanga mkoani Kagera, Mhashamu Almachius Vincent Rweyongeza, amesema kuna watu na makundi katika jamii ya leo yanayotumia nguvu, risasi na mabomu ya machozi kwa sababu ya kushindwa hoja, akifananisha tabia hiyo na akina Herode waliokataa kumpokea Yesu Kristo, Mfalme...
  20. Cute Wife

    JamiiForums Tanzania Polisi kuendelea na ukamataji usiozingatia taratibu: Hawajasikia maagizo ya Simbachawene? Wanafuata maagizo ya nani?

    Majuzi Waziri Simbachawene alitoa maagizo akiwataka Jeshi la Polisi kukamata raia kwa kufuata taratibu na sheria, kwa kutokamata raia kihuni. Wawe wanavaa sare, na waache kuvaa kininja. Itakuwa Simbachawene si lolote si chochote, maana toka atoe maagizo hayo bado watu wanakamatwa kihuni, mara...
Back
Top Bottom