Ramadhan Special Thread
Siku Kumi Bora Kabisa Za Allaah: 1 - 10 Dhul-Hijjah



Alhidaaya.com



Inatupasa tumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa neema Aliyotujaalia ya kutuwekea miezi mitukufu, au siku tukufu au nyakati tukufu ambazo ‘amali njema huwa na thawabu nyingi mno. Na hivi tunakaribia kabisa kuingia katika mwezi mwingine mtukufu wa Dhul-Hijjah. Katika mwezi huu, siku kumi za mwanzo ni siku bora kabisa mbele ya Allaah ambazo 'amali yoyote inayotendwa humo ni yenye kupendwa mno na Allaah:



عن ابن عباس رضي الله عنهما، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((مَا مِنْ أَيَّامٍ الْعَمَلُ الصَّالِحُ فِيهَا أَحَبُّ إِلَى اللَّهِ مِنْ هَذِهِ الْأَيَّامِ)) يَعْنِي أَيَّامَ الْعَشْرِ قَاُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ وَلَا الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ؟ قَالَ: ((وَلَا الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ إِلَّا رَجُلٌ خَرَجَ بِنَفْسِهِ وَمَالِهِ فَلَمْ يَرْجِعْ مِنْ ذَلِكَ بِشَيْ)) البخاري

Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ameahadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakuna siku ambazo ‘amali njema zinazotendwa humo, zinapendwa mno na Allaah kama (‘amali zinazotendwa katika) siku kumi hizi.” Yaani: Siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Dhul-Hijjah. Wakauliza: Ee Rasuli wa Allaah! Je, hata kuliko jihaad katika njia ya Allaah? Akajibu: “Hata Jihaad katika njia ya Allaah isipokuwa mtu aliyetoka (kwenda kupigana jihaad) mwenyewe na mali yake kisha kisirudi chochote katika hivyo.” [Al-Bukhaariy]





Ee ndugu Muislamu! Usiache fursa hii kukupita kujichumia thawabu tele kutokana na uzito wa malipo katika masiku haya. Hivyo basi tunawanasihi kusoma yafuatayo kuhusu fadhila za masiku haya kumi ya Dhul-Hijjah pamoja na amali za kutenda katika masiku haya matukufu kabisa mbele ya Allaah ('Azza wa Jalla).





I-Allaah Ameziapia Siku Kumi Hizi:



Kwa jinsi zilivyokuwa na umuhimu mkubwa siku hizo kumi, hadi kwamba Allaah (Subhaanah wa Ta'aalaa) Ameziapia katika Qur-aan Anaposema:

بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ((وَالْفَجْرِ)) ((وَلَيَالٍ عَشْرٍ))

Kwa Jina la Allaah, Mwingi wa rahmah, Mwenye kurehemu. ((Naapa kwa Alfajiri)) ((Na kwa masiku kumi)) [Al-Fajr: 1-2]



Wanachuoni wafasiri wa Qur-aan wamekubaliana kwamba zilokusudiwa hapo ni siku kumi za Dhul-Hijjah.



II-Siku Za Manufaa Na Kumdhukuru Allaah:



Inapasa kumdhukuru mno Allaah (Subhaanah wa Ta’alaa) kwa kukumbuka neema Zake zisizohesabika kama Anavyosema:



((لِيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ وَيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ فِي أَيَّامٍ مَّعْلُومَاتٍ))

((Ili washuhudie manufaa yao na kulitaja Jina la Allaah katika siku zinazojulikana)) [Al-Hajj: 28]



Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kasema: “Hizo ni siku kumi za Dhul-Hijjah.” Na Amesema: “Manufaa ya dunia hii na ya Aakhirah.” Manufaa ya Aakhirah yanajumuisha kupata radhi za Allaah. Manufaa ya vitu vya dunia inajumuisha wanyama wa kuchinjwa na biashara. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]





III-'Amali Zake Ni Bora Kuliko Kwenda Katika Jihaad Fiy SabiliLLaah:



Kutokana na ilivyotajwa katika usimulizi wa Hadiyth ifuatayo, kwamba amali yoyote utendayo katika masiku kumi hayo, ni bora kuliko kwenda kupigana jihaad vitani. Ukizingatia kwenda kupigana jihaad ni jambo zito mtu kuliitikia, kwani huko kuna mashaka mbali mbali, ikiwemo kupoteza mali, khofu ya kujeruhiwa na kupoteza viungo vya mwili, kufariki, n.k. Ila hilo si zito kwa mwenye iymaan ya hali ya juu kabisa kutaka kuyakabili mashaka hayo na kutamani kufa shahidi. Kwa hiyo usidharau ‘amali yoyote hata iwe ndogo vipi itekeleze kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni Al-Jawwaad (Mwingi wa Ukarimu), Al-Kariym (Mkarimu), Al-Wahhaab (Mwingi wa kutunuku, Mpaji wa yote), Al-Majiyd (Mwingi mno wa vipawa na ukarimu).



عن ابن عباس رضي الله عنهما، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((مَا مِنْ أَيَّامٍ الْعَمَلُ الصَّالِحُ فِيهَا أَحَبُّ إِلَى اللَّهِ مِنْ هَذِهِ الْأَيَّامِ)) يَعْنِي أَيَّامَ الْعَشْرِ قَاُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ وَلَا الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ؟ قَالَ: ((وَلَا الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ إِلَّا رَجُلٌ خَرَجَ بِنَفْسِهِ وَمَالِهِ فَلَمْ يَرْجِعْ مِنْ ذَلِكَ بِشَيْ)) البخاري

Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ameahadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakuna siku ambazo ‘amali njema zinazotendwa humo, zinapendwa mno na Allaah kama (‘amali zinazotendwa katika) siku kumi hizi.” Yaani: Siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Dhul-Hijjah. Wakauliza: Yaa Rasula-Allaah! Je hata kuliko jihaad katika njia ya Allaah? Akajibu: “Hata Jihaad katika njia ya Allaah isipokuwa mtu aliyetoka (kwenda kupigana jihaad) mwenyewe na mali yake kisha kisirudi chochote katika hivyo.” [Al-Bukhaariy]





IV-'Ibaadah Zote Zimejumuika Katika Siku Hizi



'Ibaadah zote zimejumuika katika siku kumi hizi nazo ni Swalaah, kufunga Swiyaam, Swadaqah, Hajj, wala hazijumuiki pamoja wakati mwingine.







V-‘Amali Za Kutenda Katika Siku Kumi Hizi:







1- Kutekeleza Hajj na 'Umrah (kwa mwenye uwezo):



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((العُمْرَةُ إِلَى العُمْرَةِ كَفَّارَةٌ لِمَا بَيْنَهُمَا، وَالحَجُّ الـمَبْرُورُ لَيْسَ لَهُ جَزَاءٌ إِلَّا الجَنَّةُ))

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: “'Umrah hadi 'Umrah hufuta (madhambi) baina yake, na Hajjum-Mabruwr haina jazaa ila Jannah) [Al-Bukhaariy na Muslim]



عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: "سئل رسول الله صلى الله عليه وسلم: أي الأعمال أفضل؟ قال: ((إيمان بالله ورسـوله)). قيل: ثم مـاذا؟ قال: ((الجهاد في سبيل الله)) قيل: ثم ماذا؟ قال: ((حج مبـرور)) متفق علية

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba aliulizwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ‘Amali gani ni bora kabisa? Akasema: “Kumuamini Allaah na Rasuli Wake.” Akaulizwa: Kisha nini? Akasema: “Jihaad katika njia ya Allaah.” Akaulizwa: Kisha nini? Akasema: “Hajj Mabruwr.” [Al-Bukhaariy na Muslim]



Bonyeza viungo vifuatavyo upate faida ziyada:



Umuhimu Wa Kukimbilia Kutekeleza Nguzo Ya Hajj



Fadhila Za ‘Umrah Na Hajj - Kutoka Kitabu: Alhidaaya Katika Manaasik Za Hajj Na 'Umrah







2- Kuomba Tawbah ya kweli na kujiepusha na maasi:



Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

(( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا))

((Enyi walioamini! Tubuni kwa Allaah tawbah iliyo ya kweli!)) [At-Tahriym: 8]



Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametupa matumaini makubwa ya kufutiwa madhambi na makosa yetu katika usimulizi ufuatao:



عن أَنَسُ بْنُ مَالِكٍ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((قَالَ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى يَا ابْنَ آدَمَ، إِنَّكَ مَا دَعَوْتَنِي وَرَجَوْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ عَلَى مَا كَانَ فِيكَ وَلَا أُبَالِي، يَا ابْنَ آدَمَ لَوْ بَلَغَتْ ذُنُوبُكَ عَنَانَ السَّمَاءِ ثُمَّ اسْتَغْفَرْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ وَلَا أُبَالِي، يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ لَوْ أَتَيْتَنِي بِقُرَابِ الْأَرْضِ خَطَايَا ثُمَّ لَقِيتَنِي لَا تُشْرِكُ بِي شَيْئًا لَأَتَيْتُكَ بِقُرَابِهَا مَغْفِرَةً))

Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Allaah (Tabaaraka wa Ta’aalaa) Amesema: Ee bin-Aadam! Hakika ukiniomba na ukanitaraji (kwa malipo) Nitakughufuria yale yote uliyonayo na wala Sijali, Ee bin-Aadam! Lau zingefikia dhambi zako ukubwa wa mbingu, kisha ukaniomba maghfirah, Ningekughufuria bila ya kujali (kiasi cha madhambi uliyoyafanya). Ee bin-Aadam! Hakika ungenijia na madhambi yakaribiayo ukubwa wa ardhi, kisha ukakutana nami na hali hukunishirikisha chochote, basi Nami Nitakujia na maghfirah yanayolinga nayo.” [At-Tirmidhiy na Shaykh Al-Albaaniy kaipa daraja ya Hasan]



Bonyeza kiungo kifuatacho upate faida ziyada:



Tawbah: Hukmu Na Fadhila Zake





3-Kumdhukuru Mno Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



Kwa kuleta Takbiyrah kuanzia unapoandama mwezi wa dhul-Hijjah mpaka mwisho wa Ayyaamut-Tashriyq (Yaani tarehe 13 Dhul-Hijjah) baada ya Swalaatul-'Asr ndio kumalizika kwake. Dalili ni zifuatazo: Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



لِّيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ وَيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ فِي أَيَّامٍ مَّعْلُومَاتٍ عَلَىٰ مَا رَزَقَهُم مِّن بَهِيمَةِ الْأَنْعَامِ ۖ

((Ili washuhudie manufaa yao; na walitaje Jina la Allaah katika siku maalumu kwa yale Aliyowaruzuku kati ya wanyama wenye miguu minne wa mifugo. [Al-Hajj 28]



Na pia Hadiyth:



كَانَ إبْن عَمَر وَأبُو هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّه عَنْهُما يَخْرُجَانِ إِلَى السُّوقِ فِي أَيَّامِ العَشْرِ يُكَبِّرَانِ، وَيُكَبِّرُ النَّاسُ بِتَكْبِيرِهِمَا

Ibn 'Umar na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) walikuwa wakienda sokoni katika siku kumi (za Dhul-Hijjah) na kutamka Takbiyr kwa sauti na watu wakiwaigiza. [Al-Bukhaariy]



Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَاذْكُرُوا اللَّـهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ ۚ

Na mdhukuruni Allaah katika siku za kuhesabika. [Al-Baqarah: 203]



Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: "Siku za kuhesabika ni siku za tashriyq (11, 12, 13 Dhul-Hijjah) na siku maalumu ni siku za kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah." [Al-Qurtwubiy: 3.3]



Mdhukuru Allaah Ta'aalaa zaidi kwa Tasbiyh, Tahmiyd, Tahliyl, Takbiyr: Maana yake ni: kusema: Subhaana Allaah, AlhamduliLLaah, laa Ilaaha illa Allaah, Allaahu Akbar.



Takbiyr katika masiku haya matukufu ni aina mbili:[1]





A) Takbiyr Al-Mutwlaq: Za Nyakati Zote:



Takbiyr wakati wote mchana na usiku, mahali popote ulipo, tokea unapoingia mwezi wa Dhul-Hijjah na inaendelea mpaka siku ya mwisho ya Tashriyq (tarehe 13 Dhul-Hijjah) na kumalizika baada ya kuingia Magharibi.



B) Takbiyr Al-Muqayyad: Za Kuthibitika Mahali Maalumu Na Nyakati Maalumu, Za Kukadirika:



Takbiyr baada ya kila Swalaah za fardhi na huanza baada ya Swalaah ya Alfajiri Siku ya 'Arafah mpaka mpaka baada ya Swalaah ya Alasiri siku ya mwisho ya Tashriyq (tarehe 13 Dhul-Hijjah).





Inavyopasa kufanya Takbiyr:



اللَّهُ أَكْبَرُ، اللَّهُ أَكْبَرُ، لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، اللَّهُ أَكْبَرُ، اللَّهُ أَكْبَرُ، وَلِلَّهِ الْحَمْد

Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, laa Ilaaha illa Allaah, Allaahu Akbar Allaahu Akbar WaliLLaahil-Hamd





Bonyeza Upate Takbiyrah Ya Sauti:







4- Kufufua Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



Wanaume wanatakiwa waseme kwa sauti ili kuwakumbusha wengine na wanawake waseme kimya kimya isipokuwa wakiwa na mahaarim wao. Kufufua Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni muhimu kwa sababu bila ya kufanya hivyo ni kukosa fadhila zake, na pia ni kupoteza Sunnah za kipenzi chetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).



مَنْ سَنَّ فِي الْإِسْلَامِ سُنَّةً حَسَنَةً فَعُمِلَ بِهَا بَعْدَهُ كُتِبَ لَهُ مِثْلُ أَجْرِ مَنْ عَمِلَ بِهَا ، وَلَا يَنْقُصُ مِنْ أُجُورِهِمْ شَيْءٌ .

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: “Atakayefufua tendo jema katika Uislaam na watu wakalitenda baada yake, basi ataandikiwa ujira sawa na yule atakayelitenda, na hakipungui chochote katika ujira wao. [Muslim]







5- Kufunga Swiyaam siku hizi khaswa siku ya 'Arafah:



Kufunga Swiyaam siku hii ni kufutiwa madhambi ya miaka miwili:



عَنْ أَبِي قَتَادَةَ رضي الله عنه أن النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((صِيَامُ يَوْمِ عَرَفَةَ أَحْتَسِبُ عَلَى اللَّهِ أَنْ يُكَفِّرَ السَّنَةَ الَّتِي قَبْلَهُ وَالسَّنَةَ الَّتِي بَعْدَهُ )) أخرجه مسلم

Abuu Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: “Swawm ya 'Arafah nataraji (kwa Allaah) kufuta madhambi ya mwaka uliopita na wa baada yake.” [Muslim]



Swawm inamweka mtu mbali na Moto.

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رَسُو

لُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم : مَنْ صَامَ يَوْماً فِي سَبِيلِ اللَّهِ بَعَّدَ اللَّهُ وَجْهَهُ عَنْ النَّارِ سَبْعِينَ خَرِيفًا.

Abuu Sa'iyd Al-Khudhwriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayefunga Swiyaam siku moja kwa ajili ya Allaah, Allaah Atauweka uso wake mbali na moto masafa ya miaka sabiini.” [Al-Bukhaariy na Muslim]





Na Swawm ina thawabu maradufu.



عنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((كُلُّ عَمَلِ ابْنِ آدَمَ يُضَاعَفُ الْحَسَنَةُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا إِلَى سَبْعمِائَة ضِعْفٍ قَالَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ إِلَّا الصَّوْمَ فَإِنَّهُ لِي وَأَنَا أَجْزِي بِهِ يَدَعُ شَهْوَتَهُ وَطَعَامَهُ مِنْ أَجْلِي لِلصَّائِمِ فَرْحَتَانِ فَرْحَةٌ عِنْدَ فِطْرِهِ وَفَرْحَةٌ عِنْدَ لِقَاءِ رَبِّهِ وَلَخُلُوفُ فِيهِ أَطْيَبُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ رِيحِ الْمِسْكِ))

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Kila 'amali njema ya mwanaadamu inalipwa mara kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi mia saba, na Allaah (‘Azza wa Jalla) Anasema: Isipokuwa Swawm, kwani hiyo ni kwa ajili Yangu na Mimi Ndiye Nitakayemlipa. Ameacha matamanio yake na chakula chake kwa ajili Yangu. Kwa aliyefunga Swawm atapata furaha mbili; furaha anapofuturu na furaha atakapoonana na Rabb wake, harufu inayotoka kinywani mwa aliyefunga ni nzuri mbele ya Allaah kuliko harufu ya misk.” [Muslim na Ahmad]



Bonyeza kiungo kifuatacho upate fadhila za Swiyaam:



Fadhila Za Swiyaam Za Fardhi Na Za Sunnah





6- Kuzidisha ‘amali njema mbali mbali:



Kuanzia kuswali Swalaah za fardhi kwa wakati wake kisha kuswali Swalaah za Sunnah, kusoma Qur-aan, kutoa swadaqah, kuomba du’aa kwa wingi, kutii wazazi na kuwafanyia wema, kuwasiliana na jamaa (kuunga undugu), kuwafanyia wema jirani, kuamrishana mema na kukatazana maovu, kufanyiana wema na ihsani na kadhalika.







7- Kuchinja baada ya Swalaah ya 'Iyd:



Anasema Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa):

((فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ))

((Basi Swali kwa ajili ya Rabb wako na uchinje)) [Al-Kawthar: 2]





Na usimulizi ufuatao tunapata maelezo ya aina ya mnyama wa kuchinja na uchinjaji wake.





فعَنْ أَنَسٍ رضي الله عنه قَالَ: ضَحَّى النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِكَبْشَيْنِ أَمْلَحَيْنِ أَقْرَنَيْنِ ذَبَحَهُمَا بِيَدِهِ وَسَمَّى وَكَبَّرَ وَوَضَعَ رِجْلَهُ عَلَى صِفَاحِهِمَا متفق عليه

Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alichinja kondoo wawili weupe* wenye pembe, amewachinja kwa mikono yake, akasema BismiLLaah na Allaahu Akbar na akaweka mguu wake upande wa nyuma yao. [Al-Bukhaariy na Muslim]



*Baadhi ya Wanachuoni wamesema kuwa ni weupe ulio na alama nyeusi, wengine wamesema uliochanganyika na wekundu.



‘Amali hii ya kuchinja ni 'ibaadah tukufu na ni Sunnah iliyosisitizwa hata wanachuoni wameona kuwa ni waajib kwa kila aliyekuwa na uwezo wa kuchinja.





Yanayompasa kufanya mwenye kutaka kuchinja:



Baada ya kutia niyyah ya kuchinja, asikate mtu nywele wala kucha mpaka amalize kuchinja kama tulivyoamrishwa katika Hadiyth ifuatayo:





عن أم سلمة رضي الله عنها، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: (((ِذَا رَأَيْتُمْ هِلَالَ ذِي الْحِجَّةِ وَأَرَادَ أَحَدُكُمْ أَنْ يُضَحِّيَ ، فَلْيُمْسِكْ عَنْ شَعْرِهِ وَأَظْفَارِهِ))) وفي راوية: ((فَلَا يَأْخُذْ مِنْ شَعْرِهِ وَلَا مِنْ أَظْفَارِهِ شَيْئًا، حَتَّى يُضَحِّيَ)) مسلم

Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mtakapoona mwezi umeandama wa Dhul-Hijjah na ikiwa yuko anayetaka kuchinja basi azuie (asikate) nywele zake na kucha zake).” [Muslim na wengineo] Na katika riwaayah nyengine: "Asikate nywele wala kucha mpaka akimaliza kuchinja."



Hii ni fadhila na neema kwetu maana tunakuwa kama vile tumo katika ihraam ndogo kama vile wanavyokuwa Mahujaji katika ihraam zao, ingawa ihraam zao zimeshurutishwa kwa kuharamishwa mambo mengineyo. Ikiwa amesahau mtu, mfano akakata kucha basi aendelee tu na niyyah yake mpaka amalize kuchinja.



Bonyeza kiungo kifuatacho upate faida ziyada:



Kuchinja - Fadhila, Hikmah Na Hukmu Zake





8- Kuhudhuria Swalaah ya 'Iyd:



Kwenda kuswali Swalaah ya ‘Iyd ni jambo lilosisitizwa mno na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Lakini Waislaam wengi wamepuuza ‘amali hii na hali Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amehimiza mpaka wanawake walio katika hedhi na wazee waende kusikiliza khutbah ya Swalaah. Wakati wa Swalah ukifika, wanawake hao wenye hedhi wajitenge kando hadi itakapomalizika Swalaah na kisha wajiunge na wenzao kusikiliza khutbah.







9-‘Amali za Kutenda Siku Ya ‘Arafah Ambayo Ni Siku Ya Tisa Dhul-Hijjah



a) Mwenye kufunga Swawm, atafutiwa madhambi ya miaka miwili!



Siku hii tukufu ni siku iliyokamilika Dini yetu. Thawabu za kufunga siku hii ni kufutiwa madhambi ya miaka miwili.

عَنْ أَبِي قَتَادَةَ رضي الله عنه أن النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((صِيَامُ يَوْمِ عَرَفَةَ أَحْتَسِبُ عَلَى اللَّهِ أَنْ يُكَفِّرَ السَّنَةَ الَّتِي قَبْلَهُ وَالسَّنَةَ الَّتِي بَعْدَهُ )) أخرجه مسلم

Abuu Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Swawm ya 'Arafah, nataraji kwa Allaah kuwa afute madhambi ya mwaka uliopita na wa baada yake.” [Muslim]



b) Siku ambayo huachiliwa watu wengi huru kutokana na moto



عَنْ عَائِشَةَ (رضي الله عنها) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَا عَمِلَ آدَمِيٌّ مِنْ عَمَلٍ يَوْمَ النَّحْرِ أَحَبَّ إِلَى اللَّهِ مِنْ إِهْرَاقِ الدَّمِ, إِنَّهَا لَتَأْتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ بِقُرُونِهَا, وَأَشْعَارِهَا, وَأَظْلَافِهَا وَأَنَّ الدَّمَ لَيَقَعُ مِنْ اللَّهِ بِمَكَانٍ قَبْلَ أَنْ يَقَعَ مِنْ الْأَرْضِ فَطِيبُوا بِهَا نَفْسًا))

Mama wa Waumini, 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakuna kitendo cha bin Aadam kilichokuwa ni kipenzi kabisa kwa Allaah siku ya kuchinja kama kumwaga damu. Atakuja (huyo mnyama) siku ya Qiyaamah na pembe zake, kucha zake na nywele zake. Damu yake itamwagika mahali fulani Allaah Anapajua kabla ya kumwagika katika ardhi. Hivyo zipendezesheni nafsi kwayo.” [At-Tirmidhiy, Sunan Ibn Maajah]



Na alipoulizwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



مَا هَذِهِ الْأَضَاحِيُّ؟ قَالَ: ((سُنَّةُ أَبِيكُمْ إِبْرَاهِيمَ)) قَالُوا: فَمَا لَنَا فِيهَا يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: ((بِكُلِّ شَعَرَةٍ حَسَنَةٌ)) قَالُوا: فَالصُّوفُ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: ((بِكُلِّ شَعَرَةٍ مِنْ الصُّوفِ حَسَنَةٌ))

Nini hivi vichinjo? Akajibu: “Ni Sunnah ya baba yenu Ibraahiym.”. Wakasema, "Nini umuhimu wake kwetu?” Akasema: “Katika kila unywele kuna jema moja.” Wakasema: Na sufi? Akasema: “Katika kila unywele wa sufi kuna jema moja.” [Ahmad, Ibn Maajah]





c) Du'aa bora kabisa ni Du'aa katika siku ya 'Arafah





Inapasa kumdhukuru mno Allaah siku hii kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa:



((خَيْرُ الدُّعَاءِ دُعَاءُ يَوْمِ عَرَفَةَ، وخَيْرُ مَا قُلْتُ أنَا وَالنَّبيُّونَ مِنْ قَبْـلِي: لَا إِلَهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيْكَ لَهُ، لَهُ الـمُلْكُ، ولَهُ الـحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيءٍ قَدِير)) روى الترمذي

“Du’aa bora kabisa ni du’aa katika siku ya 'Arafah, na yaliyo bora kabisa niliyosema mimi na Manabii kabla yangu ni:





Laa Ilaaha illa Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku Walahul-Hamdu wa Huwa 'alaa kulli shay-in Qadiyr. [At-Tirmidhiy]



Bonyeza kiungo kifuatacho upate faida ziyada:



Fadhila Za Siku Ya 'Arafah Na Yawmun-Nahr (Siku Ya Kuchinja)





10-Amali Za Kutenda Siku Ya Kuchinja Ambayo Ni Sikukuu Ya ‘Iyd



Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



((إِنَّ أعظمَ الأيامِ عندَ اللهِ تباركَ وتعالى يومُ النَّحْرِ ، ثمَّ يَومُ القَّرِّ)) سنن أبي داود

“Siku iliyo tukufu kabisa kwa Allaah ni siku ya kuchinja, kisha siku ya kutulia.” (yaani siku ya kukaa Minaa) [Sunan Abi Daawuwd]



Kadhalika hii ni Sikukuu ya pili ya Waislamu, inapaswa siku hii kwenda kuswali Swalaah ya 'Iyd, kuamkiana na Waislamu, kuunga undugu kwa kuwatembelea na kuwasiliana nao kwa njia mbalimbali, kupeana zawadi khasa kuwapa watoto, kula na kunywa na kufurahi kwa kila aina za starehe zinazoruhusika kishariy'ah.





Pia bonyeza viungo vifuatavyo upate faida nyenginezo za 'amali za kutenda katika Siku hii tukufu ya 'Iydul-Adhwhaa na mambo ya kujiepusha nayo:



'Iyd Al-Fitwr: Yaliyo Sunnah Kutekelezwa





'Iyd - Yaliyo Ya Sunnah Na Yaliyo Bid'ah Katika Sherehe Za 'Iyd







Wa biLLaahi At-Tawfiyq




[1] Takbiyr hizo za masiku haya matukufu zimetekelezwa na baadhi ya Maswahaba watukufu na ni Mustahabb (imependekezwa) na wengi katika Salaf wa madhehebu ya Hanbaliy, Ash-Shaafi’iyy, Hanafiy na wengineo kama ifuatavyo:

Imaam An-Nawawiy - Al-Majmuw’ (5/32).

Ibn Rajab - Fat-hul-Baariy (6/125, 130).

Ibn Taymiyyah - Majmuw’ Al-Fataawaa (24/220. 222).

Imaam Ibn Baaz - Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb (13/355).

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn - Ash-Sharh Al-Mumti’ (5/166), Majmuw’ Fataawaa wa Rasaail Al-‘Uthyamiyn (16/262, 265).
 
Hajj
Fadhila Za Siku Ya 'Arafah Na Yawmun-Nahr (Siku Ya Kuchinja)



Alhidaaya.com





‘Arafah ni jabali ambalo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisimama katikati ya bonde lake kuhutubia Maswahaba katika Hajjatul-widaa’i. (hajj ya kuaga), na hapo ndipo wanaposimama Mahujaji kutimiza fardhi ya Hajj. Kusimama hapo ndio nguzo mojawapo kuu ya Hajj. Bila ya kusimama ‘Arafah hijjah ya mtu itakuwa haikutimia kwa dalili ifuatayo:



عن عبد الرحمن بن يعمر قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((الْحَجُّ عَرَفَة، مَنْ جَاءَ قَبْلَ طُلُوعِ الْفَجْرِ مِنْ لَيْلَةِ جَمْعٍ فَقَدْ أَدْرَكَ الْحَجّ)) صحيح الجامع

‘Abdur-Rahmaan bin Ya’mur (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Al-Hajj ni ‘Arafah, atakayekuja kabla kutoka Alfajiri usiku wa kujumuika atakuwa ameipata Hajj)) [Swahiyh Al-Jaami’].







A-Fadhila Za Siku ya ‘Arafah:



1-Ni Siku Iliyokamilika Dini Yetu



عَنْ طَارِقِ بْنِ شِهَابٍ قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ مِنَ الْيَهُودِ إِلَى عُمَرَ، فَقَالَ: يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ، آيَةٌ فِي كِتَابِكُمْ تَقْرَؤُونَهَا، لَوْ عَلَيْنَا نَزَلَتْ مَعْشَرَ الْيَهُودِ، لَاتَّخَذْنَا ذَلِكَ الْيَوْمَ عِيدًا. قَالَ: وَأَيُّ آيَةٍ؟ قَالَ: ((الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمْ الْإِسْلَامَ دِينًا)) فَقَالَ عُمَرُ: إِنِّي لَأَعْلَمُ الْيَوْمَ الَّذِي نَزَلَتْ فِيهِ، وَالْمَكَانَ الَّذِي نَزَلَتْ فِيهِ، نَزَلَتْ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ، بِعَرَفَاتٍ، فِي يَوْمِ جُمُعَةٍ.

Twaariq bin Shihaab (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba alikuja Myahudi mmoja kwa ‘Umar akasema: Ee Amiri wa Waumini! Aayah katika Kitabu chenu mnaisoma, kama ingeteremkwa kwetu hadhara ya Mayahudi, basi bila shaka tungeifanya siku hiyo kuwa ni siku ya kusherehekea. Akasema (‘Umar): Aayah ipi? Akasema: ((Leo Nimekukamilishieni Dini yenu na Nimekutimzieni Neema Zangu kwenu na Nimekuridhieni Uislamu kuwa ni Diyn yenu)) [Al-Maaidah (5: 3] ‘Umar akasema: Hakika naijua siku gani imeteremka Aayah hii, na sehemuu iliyoteremkia, imeteremka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa ‘Arafah, siku ya Ijumaa. [Muslim]



Ilikuwa ni mara ya kwanza Waislamu kutekeleza Hajj, kwa hiyo imemaanishwa kukamilika dini yao baada ya kukamilisha kutumiza nguzo za Kiislamu zote.





2-Kufunga Swawm ni kufutiwa madhambi ya miaka miwili:



Ni fadhila kubwa kwa Waislamu kufutiwa madhambi yao.



عَنْ أَبِي قَتَادَةَ رضي الله عنه أن النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ : ((صِيَامُ يَوْمِ عَرَفَةَ أَحْتَسِبُ عَلَى اللَّهِ أَنْ يُكَفِّرَ السَّنَةَ الَّتِي قَبْلَهُ وَالسَّنَةَ الَّتِي بَعْدَهُ )) أخرجه مسلم

Abuu Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swawm ya 'Arafah nataraji (kwa Allaah) kufuta madhambi ya mwaka uliopita na wa baada yake)) [Muslim]



Kufunga Swawm siku ya ‘Arafah ni makhsusi kwa wasiokuweko huko ‘Arafah siku hiyo. Ama mahujaji hawatakiwi kufunga Swawm siku hiyo kwa dalili:



عنْ مَيْمُونَةَ زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، أَنَّهَا قَالَتْ: إِنَّ النَّاسَ شَكُّوا فِي صِيَامِ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَوْمَ عَرَفَةَ، فَأَرْسَلَتْ إِلَيْهِ مَيْمُونَةُ بِحِلَابِ اللَّبَنِ، وَهُوَ وَاقِفٌ فِي الْمَوْقِفِ، فَشَرِبَ مِنْهُ وَالنَّاسُ يَنْظُرُونَ إِلَيْهِ

Mama wa Waumini Maymuwnah bint Al-Haarith (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amehadithia kwamba watu walitia shaka kuhusu Swawm ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) [kama alifunga] Siku ya ‘Arafah, nikampelekea maziwa, naye akiwa amesimama akayanywa na huku watu wanamtazama. [Al-Bukhaariy]





3-Siku Ambayo Wataokolewa Waja Kutokana Na Moto; Wataghufuriwa Madhambi Yao



عن جابر رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((مَا مِنْ يَوْمٍ أَفْضَلُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ يَوْمِ عَرَفَةَ، يَنْزِلُ اللَّهُ تَعَالَى إلَى سَمَاءِ الدُّنْيَا فَيُبَاهِي بِأَهْلِ الْأَرْضِ أَهْلَ السَّمَاءِ)) وروى ابن حبان

وفي رواية: ((إنَّ اللَّهَ يُبَاهِي بِأَهْلِ عَرَفَةَ مَلَائِكَتَهُ، فَيَقُولُ: يَا مَلَائِكَتِي، اُنْظُرُوا إلَى عِبَادِي، قَدْ أَتَوْنِي شُعْثا غُبْرا ضَاحِينَ))

Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna siku iliyo bora kabisa mbele ya Allaah kama siku ya ‘Arafah. Anateremka Allaah Ta’ala mbingu ya dunia (ya kwanza) kisha Anawafakhiri watu ardhi kwa watu wa mbingu))



Na pia:



عن عبدالله بن عمرو إنَّ اللهَ عزَ وجلَّ يباهي ملائكتَهُ عشيةَ عرفةَ بأهلِ عرفةَ فيقولُ : انظروا إلى عبادي أتوني شُعثا غُبرا

((Hakika Allaah (‘Azza wa Jalla) Huwafakharisha watu ‘Arafah kwa Malaika Wake jioni ya ‘Arafah na Husema: “Watazameni waja Wangu wamenijia wakiwa timtimu wamejaa vumbi.”)) [Musnad Ahmad (12/42) na ameisahihisha Imaam Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Targhiyb (1153), Swahiyh Al-Jaami’ (1868), Taz pia As-Silsilah Asw-Swahiyhah (1503)




Pia,

قَالَتْ عَائِشَةُ إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ مَا مِنْ يَوْمٍ أَكْثَرَ مِنْ أَنْ يُعْتِقَ اللَّهُ فِيهِ عَبْدًا مِنْ النَّارِ مِنْ يَوْمِ عَرَفَةَ وَإِنَّهُ لَيَدْنُو ثُمَّ يُبَاهِي بِهِمْ الْمَلَائِكَةَ فَيَقُولُ مَا أَرَادَ هَؤُلَاءِ. اشْهَدُوا مَلاَئِكَتِي أَنِّي قَدْ غَفَرْتُ لَهُمْ. صحيح الترغيب

‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakuna siku Anayoacha Allaah kwa wingi huru waja kutokana na moto kama siku ya ‘Arafah. Na huwa karibu kisha Anajigamba kwao kwa Malaika na Husema: Wametaka nini hawa? Shuhudieni Malaika wangu kwamba hakika Mimi Nimewaghufuria)) [Swahiyh At-Targhiyb]



Pia:

عن جابر قال: قال رَسُوْلُ الله صلى الله عليه وسلم : (( ما مِنْ أيامٍ عِنْدَ الله أَفْضَل مِنْ عَشْرِ ذِي الحِجَة)) قَال: فَقَالَ رَجُلٌ: يا رَسُولُ الله هُنُّ أَفْضَلُ أمْ عَدَدَهُنَّ جِهَادًا في سَبِيلِ الله؟ قال: ((هُنَّ أَفْضَل مِنْ عَدَدُهْنَّ جِهادًا في سَبِيلِ الله، ومَاَ مِنْ يَوْم أفْضَلُ عِنْد الله مِنْ يَوم عَرَفةَ: يَنْزِلُ الله تَبَارْكَ وتَعَالى إلى السْمَاءِ الدُّنيا فَيُباهي بِأهْلِ الأرض أهَلْ السْمَاءِ، فيقول: انْظُروا إلى عِبَادِي جَاءوا شُعْثًا غُبْرًا حَاجِين جَاءْوا مِنْ كُلِ فجٍّ عَمِيقْ يَرجُونَ رَحْمَتي ولم يَروا عَذَابي، فَلَم يُرَ يومٌ أكثر عتيقًا مِنْ النَّار مِنْ يَوم عَرَفْة))

Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna Siku iliyo bora kabisa kama siku kumi za Dhul-Hijjah, akasema mtu: “Ee Rasuli wa Allaah, hizo ni bora au jihaadi katika njia ya Allaah? Akasema: ((Hizo ni bora kuliko jihaad katika njia ya Allaah, na hakuna siku bora kabisa mbele ya Allaah, kama siku ya ‘Arafah, Anateremka Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa katika mbingu ya dunia kisha Anawafakhiri watu wa ardhini kwa watu wa mbinguni kisha Anasema: Tazameni waja Wangu wamenijia timtimu wamejaa vumbi wamekuja kutoka kila pembe ya mbali wanataraji rahmah Yangu na wala hawajaona adhabu Yangu. Na wala hakuona siku inayoachwa huru shingo kutokana na moto kama siku ya ‘Arafah)) [At-Targhiyb wat-Tarhiyb – Isnaad yake Swahiyh au Hasan]



4-Siku Ya Kutakabaliwa Du’aa



Amesema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



((خَيْرُ الدُّعَاءِ دُعَاءُ يَوْمِ عَرَفَةَ، وخَيْرُ مَا قُلْتُ أنَا وَالنَّبيُّونَ مِنْ قَبْـلِي: لَا إِلَهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيْكَ لَهُ، لَهُ الـمُلْكُ، ولَهُ الـحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيءٍ قَدِير)) روى الترمذي

((Du’aa bora kabisa ni du’aa katika siku ya 'Arafah, na yaliyo bora kabisa niliyosema mimi na Manabii kabla yangu ni:



لَا إِلَهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيْكَ لَهُ، لَهُ الـمُلْكُ، ولَهُ الـحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيءٍ قَدِير



'Laa Ilaaha illa Allaah Wah-dahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku wa-Lahul-hamdu wa Huwa 'alaa kulli shay-in Qadiyr



Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Hana mshirika, ufalme wote ni Wake, na Himdi zote ni Zake, Naye ni Mweza wa kila kitu daima)) [Swahiyh At-Tirmidhiy (3/184), Silsilatu Al-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah (4/6)]





5-Siku Ambayo Allaah Ameiapia



Allaah Ameiapia siku hii ya ‘Arafah ambayo inajulikana kwa ‘Siku ya Kushuhudiwa’. Hii kutokana na kauli Yake Subhaanahu wa Ta’ala:

وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الْبُرُوجِ ﴿١﴾

Naapa kwa mbingu zenye sayari kubwa zilizodhahiri.

وَالْيَوْمِ الْمَوْعُودِ ﴿٢﴾

Na (Naapa kwa) Siku iliyoahidiwa (ya Qiyaamah).



وَشَاهِدٍ وَمَشْهُودٍ ﴿٣﴾

Na (Naapa kwa) shahidi na kinachoshuhudiwa. [Al-Buruwj 85: 1-3]



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللّهِ صَلّى اللّه عَلَيْهِ وَسَلّمَ: ((الْيَوْمُ الْمَوْعُودُ يَوْمُ الْقِيَامَةِ وَالْيَوْمُ الْمَشْهُودُ هُوَ يَوْمُ عَرَفَةَ وَالشّاهِدُ يَوْمُ الْجُمُعَةِ))

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa alihi wa sallam) amesema: ((Siku ya kuahidiwa ni siku ya kufufuliwa. Siku ya kushuhudiwa ni siku ya ‘Arafah, na Siku ya kinachoshuhudiwa ni Siku ya Ijumaa)) [At-Tirmidhiy, Swahiyh Al-Jaami’ (8201)]





6-Siku Ambayo Allaah Amechukua Fungamano (ahadi) Kutoka Kizazi Cha Aadam



عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ( أَخَذَ اللهُ الْمِيثَاقَ مِنْ ظَهْرِ آدَمَ، فَأَخْرَجَ مِنْ صُلْبِهِ كُلَّ ذُرِّيَّةٍ ذَرَأَهَا، فَنَثَرَهُمْ بَيْنَ يَدَيْهِ كَالذَّرِّ ، ثُمَّ كَلَّمَهُمْ قِبَلًا، قَالَ🙁( أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ ؟ قَالُوا بَلَى شَهِدْنَا أَنْ تَقُولُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَذَا غَافِلِينَ، أَوْ تَقُولُوا إِنَّمَا أَشْرَكَ آبَاؤُنَا مِنْ قَبْلُ وَكُنَّا ذُرِّيَّةً مِنْ بَعْدِهِمْ أَفَتُهْلِكُنَا بِمَا فَعَلَ الْمُبْطِلُونَ))

Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah Amechukua fungamano kutoka mgongo wa Aadam katika Na’maan yaani ‘Arafah. Akalete mbele mgongo wake kizazi chake chote na akawatandaza mbele Yake, kisha Akawakabali kuwauliza: “Je, Mimi siye Rabb wenu?” Wakasema: “Ndiye, tunashuhudia!” (Allaah Akawaambia): “Msije kusema Siku ya Qiyaamah: hakika sisi tulikuwa tumeghafilika nayo haya. Au mkasema: “Hakika baba zetu ndio walioshirikisha kabla, nasi tulikuwa kizazi baada yao. Basi Utatuangamiza kwa yale waliyoyafanya wabatilifu?” (Al-A’raaf 7: 172-173) [Ameipokea Ahmad na imepewa daraja ya Swahiyh na Shaykh Al-Albaaniy]



B-Fadhila Za Yawmun-Nahr – Siku ya Kuchinja:



Siku kuu ya ‘Iydul-Adhw-haa na ndio inajulikana pia kwa Yawmun-Nahr. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



((إنَّ أَعْظَمَ اْلأيَّامِ عِنْدَ الله تبارك وتعالى يَوْمُ النَّحْرِ ثُمَّ يَوْمُ الْقَرِّ)) رواه أبو داود والنسائي وصححه الألباني

((Siku iliyo tukufu kabisa kwa Allaah ni siku ya kuchinja, kisha siku ya kutulia (siku ya Minaa)) [Abuu Daawuwd]



Sababu ya kuchinja ni kufuata Sunnah ya baba yetu Nabiy ‘Ibraahiym (‘Alayhis-Salaam) alipotaka kumchinja mwanawe Ismaa’iyl na Allaah Akamteremshia badala yake kafara ya mnyama.



Bonyeza kiungo kifuatacho upate faida ziyada:



Kuchinja - Fadhila, Hikmah Na Hukmu Zake
 
Maswali: Hajj


Aliyefariki Akihijiwa, Dhambi Zake Zitafutika Japo Hakuwahi Kutubia Alipokuwa Hai?



Alhidaaya.com



Swali:



Asalaam Alaykum Warahma tullah taala Wabarakatu



Nilikua nauliza kuwa nimewahi kusikia kuwa mtu ambaye anayekwenda Makka kuhiji na Hijjah yake ikakubalika akirudi huwa amefutiwa zambi zake zote na huwa kama mtoto mchanga (yaani hana zambi) sasa swali langu ni hivi:- Je? Mtu ambaye aliasi sana kwa kufanya dhambi nyingi hapa duniani na akafa wakati hakuwahi kutubia zambi zake hizo. Je, mtu kama huyu akienda kuhijiwa makka na mtoto wake hizo zambi zake atafutiwa zote na atakuwa hana zambi?Naomba ufafanuzi juu ya hili wabillah tawfiq.



Asalaam Alaykumu Warahma tullahi Wabarakatu





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Hakika hili ni swali zuri na maelezo uliyoyaeleza kuhusu kufutiwa dhambi kwa anayehiji Hijjah ni ya sawa kabisa, inatokana na Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) iliyo sahihi kabisa. Hata hivyo, ni sikitiko kubwa sana kuwa zipo baadhi ya Hadiyth ambazo zimekosa kueleweka inavyostahiki.





Ukiacha aliyekufa ambaye anahijiwa, hata aliyehai anatakiwa baada ya Hijjah hiyo iliyokubaliwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) awe atajikita katika Uislamu wa sawa, awe na msimamo katika hilo mpaka aage dunia katika njia hiyo ya Uislamu. Mara nyingi watu huenda wakafanya Hijjah au hufanya kila mwaka kwa kumchezea shere Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Wanafanya vipi hilo? Wanafanya kwa kurudi katika maasiya baada ya Hijjah hivyo Hijjah zao hutuyakinishia kuwa hazikukubaliwa kabisa, kwani Ibadah inayokubaliwa inatakiwa imuweke mtendaji katika ‘amali njema daima dawamu.





Sasa ikiwa anayefanyiwa Hijjah alifanya madhambi makubwa au matendo ya kumtoa katika Uislamu, Hijjah hiyo haitamsaidia lolote wala chochote. Msingi mkubwa wa Uislamu ni kuwa lazima mwanaadamu atubie kwa madhambi yake kabla hajaaga dunia pamoja na kujirekebisha na kufanya mema na mazuri. Ikiwa hakufanya hivyo, Ibadah anazofanyiwa na wengine (jamaa zake) hazitomsaidia na chochote





Hivyo, tuswali wenyewe kabla ya kuswaliwa na tutubie wenyewe tusitarajie kufanyiwa toba na wengine.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Hajj


Amekufa Hajafanya Hajj Na Alikuwa Na Uwezo Wa Kufanya Lakini Akapuuzia’ Je, Anaweza Kulipiwa Hiyo Hajj Na Jamaa Zake?



Alhidaaya.com





Swali:



Mtu ana uwezo wa kwenda hajj, na ameshapeleka watu kadhaa kwenda Hajj ilhali yeye binafsi akiambiwa kwenda, anasema wanaye watamhijia. Ikatokea kweli akafa hajenda hajj, itafaa kumhijia mtu huyu?



Ni ipi kauli ya ulamaa juu ya mtu alokuwa na uwezo wa kwenda hajj, lakini akafa hajafanya hajj,yafaa kumhijia?



Baaraka Allaahu fiyk





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.




Mtu ambaye hajakwenda Hajj akafariki na alikuwa na uwezo wa kwenda Hajj na akaacha kwa makusudi au kwa kuzembea; wote hao kwa mujibu wa Aqwaal za Ahlul-'Ilm hawahitajii kufanyiwa Hajj hata kama kuna mali zao wameacha zinazotesheleza kufanyiwa Hajj.



Japo kuna Wanachuoni wengijne wanaoona kuwa kama kaacha mali anaweza kufanyiwa Hajj kwa mali yake aliyoacha. lakini kauli yenye nguvu ni kutofanyiwa Hajj ya badali (Hajj Al-Badal) kwa sababu kama alikuwa na uwezo na nafasi ya kwenda Hajj na akapuuzia, vipi afanyiwe Hajj na hali mwenyewe hakujali!



Huu ni msimamo wa Imaam Ibn Al-Qayyim (Rahimahu Allaah) na kaenda nao Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) ambaye amesema kuwa, kama alikuwa na uwezo wa kufanya Hajj na akapuuzia, basi hakuna Hajj itakayohesabiwa kwake hata kama watu watamfanyia Hajj mara elfu moja.



Akaendelea kusema kuwa, hilo linamhusu hata aliyeacha Swawm kwa kupuuzia na hali alikuwa anaweza kufunga, huyo hawezi kulipiwa akifariki kwa sababu aliacha kwa uzembe na kupuuzia. Ama ile Hadiyth ya Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) isemayo, "Yeyote aliyefariki hali ya kuwa anadaiwa Swawm, basi Warithi wake wanapaswa kumfungia." Hadiyth hiyo inamhusu yule ambaye alikuwa hajaacha kufunga kwa kupuuzia.

[Fataawa Ibn 'Uthaymiyn (21/226)]





Na Allaah ni Mjuzi zaidi
 
Anataka Kuhiji Lakini Ana Deni La Nyumba Benki



Alhidaaya.com





Swali:



Assalam Alekum,



Swali langu ni: - Mimi nina deni la nyumba bank, hali ninaweza kwenda kuhiji? Ninaomba msaada wenu kwani mimi sina elimu ya kutosaha. Waasalam





AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Ieleweke kuwa Hijjah ni nguzo ambayo inampasa kuitekeleza yule Muislamu mwanamume au mwanamke aliye na uwezo wa kuiendea njia hiyo – kwa kuwa na hela za kutosha kwa safari hiyo, kuwa na usalama katika safari, kuacha masrufu kwa wale wanaokutegemea huku nyuma unapoondoka.





Katika hilo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ

Na kwa ajili ya Allaah imewajibika watu watekeleze Hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo. [Al-'Imraan: 97].





Na katika Hadiyth ndefu ya ‘Umar bin al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuhusu Jibriyl (‘Alayhis-salaam) aliyekuja kumuuliza maswali Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Alipoulizwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu Uislamu alisema, "…na kwenda Hijjah ukiweza kufanya hivyo" (Muslim, At-Tirmidhiy na Abu Daawuud).





Kawaida ya mkopo wowote inakuwa mkopesha na mkopeshwa na hasa ikiwa ni kutoka Benki wanaandikia kuhusu malipo hayo. Kwa mfano, ikiwa kila mwezi mdaiwa anatakiwa kulipa shilingi 100,000 kwa muda wa miaka kumi. Ikiwa mdaiwa ana pato zaidi ya hilo analolipa akaweza kuweka akiba ya hela kwa kiasi ambacho kinatimiza masharti ya kwenda Hijjah kama tulivyotaja hapo juu kutakuwa hakuna shida yoyote kwake kwenda Hijjah, japokuwa kimsingi ana deni.





Ikiwa kwenda kwake Hijjah kutamfanya asilipe deni lake analodaiwa au aruke kwa miezi kadhaa itakuwa bado hajakamilisha masharti kwa yeye kufunga safari hiyo ya mara moja katika uhai wake.





Tanbihi: Tunawapatia nasaha dada na ndugu zetu kuwa mikopo ya Benki za kawaida ina riba ambayo mdaiwa anaipatia banki. Hivyo, kuifanya mikopo aina hiyo kuwa haramu. Mara nyingi watu wamefilisika kwa kukiuka agizo la Muumba, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Tuwe na tahadhari sana katika mas-ala hayo.





Na Allaah Anajua zaidi.
 
Anaweza Kumfanyia Mzazi Aliyefariki Hajj?



Alhidaaya.com





Swali:



Aww, ninaulizo kuhusu hija, sheriya inakubali mtoto kumfanyiya hija mzazi wake kama alifariki?





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Kwanza tunakukumbusha ndugu muulizaji, kutokufupisha salaam unaposalimia. Iandike kikamilifu upate ujira kamili In shaa Allaah.



Tukirudi kwenye swali, Shari’ah hakika inaruhusu mtoto (kijana) kumfanyia Hijjah mzazi na Hijjah hiyo itahesabiwa ni ya mzazi. Hata hivyo, inatakiwa awe mtoto mwenyewe ashafanya Hijjah. Mtoto hawezi kumhijia mzazi ikiwa yeye mwenyewe hajahiji.



Mtoto akishahiji na akawa na uwezo wa kumfanyia mzazi wake Hijjah itakuwa vyema.



Zaidi pia unaweza kusoma katika viungo vifuatavyo:



Kumhijia asiyehiji



Kumgharimia Mtu Hijjah Kabla Ya Kufanya Mwenyewe Inafaa?





Na Allaah Anajua zaidi
 
Kumgharimia Mtu Hijjah Kabla Ya Kufanya Mwenyewe Inafaa?



Alhidaaya.com





Swali:



Assalam alaykum warahmattullah wabarakatuh.



Mimi ni mwanamke nilioolewa, ninahamu ya kwenda kumhijia bibi yangu ambae amefariki, swali langu je hajj itakubaliwa wakati mimi mwenyewe sijwahi kwenda hajj, nategemea kutoa gharama ya nauli ya hajj kwa mjomba wangu ambae na yeye hajawahi kuhiji ili akamuhije huyo bibi yangu ambae yeye atakuwa mama yake, mama yangu ameshaenda hajj ikiwa huyo mjomba wangu hawezi kwenda je mama yangu anaweza kwenda. Matumaini yangu mtaelewa hayo mazingira ili mnijibu swali kwa ufasaha zaidi. Assalam alaykum





Jibu:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Inatakiwa tufahamu kuwa Hijjah imewekewa Waislamu wenye uwezo wa kwenda kwa kutoa gharama. Kama machimbuko ya Uislamu yanavyo tueleza. Kuhusu hilo Allaah Aliyetukuka Anasema:

فِيهِ آيَاتٌ بَيِّنَاتٌ مَّقَامُ إِبْرَاهِيمَ ۖ وَمَن دَخَلَهُ كَانَ آمِنًا ۗ وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ

Ndani yake kuna Aayaat (ishara, dalili) zilizo wazi; mahali pa kisimamo cha Ibraahiym. Na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Allaah imewajibika watu watekeleze Hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo. [Al-'Imraan: : 97].



Na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) naye ametuambia hayo hayo: "Na kuhiji katika Nyumba kwa mwenye uwezo" [Muslim].



Ikiwa bibi yako hakuhiji kwa kutokuwa na uwezo basi ilikuwa si faradhi kwake. Lau angekuwa na mali na hakuhiji basi mgetenga katika mali yake ya kutumwa mtu kumhijia kabla kugawa urathi.



Ama mas-alah ya Hijjah mtu hawezi kumhijia mwenziwe hata akiwa ni mzazi wake kabla ya yeye mwenyewe kutekeleza faradhi hiyo. Hivyo, kwako imekuwa ni faradhi kuhiji si bibi yako wala mjomba wako. Na wewe au mjombako hamuwezi kumhijia bibi kwa kuwa nyinyi wewe hamjatekeleza hilo. Na ikiwa wewe una uwezo wa kuhiji basi inatakiwa mwanzo utumie pesa hizo kwenda wewe, na baada ya kwenda wewe kuhiji ukapata pesa nyingine unaweza kumpatia mamako akamhijie bibi yako, au wewe mwenyewe kufanya hivyo wakati huo.



Na suala hilo ni sahali wala lisikukere, bibi yako kwa kutokwenda hana madhambi mbali na kwamba niyyah yako ni nzuri Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atakulipa kwa niyyah yako. Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Akusahilishie uende ukahiji na pia Akufanyie wepesi wa kumhijia bibi yako.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Anaweza Kumlipia Mumewe Gharama Za Kwenda Hijjah?



Alhidaaya.com





Swali:



Assalaam Alaykum Warahmaturllaah Taallah wabarakatu.



Namshukuru Allaah mtukufu aliyewapa uwezo wa kutuelimisha. Ninamuomba Rabb wetu mtukufu awajaalie kila la kheri. Nashukuru jibu lenu mlilonijibu limezaa matunda mema Allaah mtukufu awatilie wepesi. kwani kutokana na ushauli wenu nikaenda kumlingania mme wangu.alhamdu lillaah rabbi l'alamiina sasa ameacha pombe na anaswali swala tano. Allaah mtukufu awabarikiinshaallah amiin!.



Sasa swali langu naweza kwenda naye hijja kwa gharama zangu?.





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Tunashukuru kujua kwamba nasaha zetu zimekusaidia na umeweza kuwa sababu ya kuongoka mumeo kwa idhini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Inapasa umshukuru Rabb Mtukufu kwani Yeye Ndiye Mwenye kuwahidi waja Wake, sisi ni njia tu za kupitia kupata uongofu kama huo.





Ama kuhusu kumlipia kwenda Hajj, na kwenda naye pamoja, inafaa ikiwa unao uwezo na umependa mwenyewe. Hili ni jambo jema kabisa khaswa kwa vile mumeo alitoka kwenye maasi na kuingia katika twaa'a (Uchaji Allaah). Kwa hiyo ni vizuri kukimbilia kutekeleza ibada/fardhi hiyo muhimu ili Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Azidi kumuongoza katika njia iliyonyooka.





Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Awazidishie iymaan ya dini Yenu na mzidi kubakia katika ridhaa Yake Rabb Mtukufu.





Na Allaah Anajua
 
Anaweza Kwenda Hajj Ikiwa Ana Deni La Swawm Za Ramadhwaan?



Alhidaaya.com





Swali:



Ukiwa na deni la saumu ya Ramadhaan halafu Allaah akajalia deni lile hukuwahi kulipa mpaka imefikia wakti umeenda zako hijja jee inakuwaje?juu ya hijja yako?





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Deni la Ramadhwaan lina wasaa na muda wa kulipa japokuwa ni vyema zaidi kulipa haraka iwezekanavyo na kutegemea kama udhuru uliokufanya usifunge siku kadhaa za Ramadhaan umeondoka. Siku ulizokosa kufunga unaweza kulipa baada ya ‘Iydul Fitwr (1 Shawwal) hado kabla ya Ramadhwaan ya mwaka unaofuata (yaani mwezi wa Sha‘baan).



Swawm na Hijjah ni ‘Ibaadah mbili ambazo haziingiliani wala kupingana. Ikiwa umetimiza masharti ya kwenda Hijjah nawe unadaiwa Swawm unaweza kwenda Hijjah na utakaporudi nyumbani utaanza kulipa deni la funga kwa siku unazodaiwa za Ramadhwaan bila mushkila wala tatizo lolote.



Bonyeza kiungo kifuatacho kupata maelezo ziada:



Fataawaa: Kulipa Swawm Na Kafara





Na Allaah Anajua zaidi
 
Atekeleze Fardhi Ya Hajj Kwanza Au Aoe?



Alhidaaya.com





Swali:



Kwanza sina budi kumshukuru Allaah ambae ameumba mbingu na arthi, na yeye ni mjuzi wa kila kiu. Vile vile natuma salamu zangu kwako kwa kusema Assalam alaykum.



Mwalimu naomba kuuliza swali langu kama ifuatavyo;



Kwa mujibu wa dini ya Kiislamu neno Ndowa ni sunna, na vile vile ukitizama neno hijja ni nguzo ya tano ya Uislam na pia ni Fardhi. Sasa je mwalimu mimi nnapesa taslimu za kunitoshelezea kwenda kuhiji, lakini mimi ni kijana ambaye sina mke, sasa je nnaweza kuhijji kwa kuwa Hijja ni fardhi au kwanza nifunge ndowa? Natumai swali langu litajibiwa vizuri na kwa ufasaha zaidi.





Jibu:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Mara nyingi huchanganyikiwa kuhusu mas-ala ya ndoa kwani wengi wetu huchukua kuwa ni Sunnah tu, hivyo mtu aweza kuoa au kuacha kufanya hivyo. Uhakika wa mambo sivyo kabisa kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ametoa amri kwetu tuoe na Akaileta kwa njia ya lazima. Hiyo ni:



وَأَنكِحُوا الْأَيَامَىٰ مِنكُمْ وَالصَّالِحِينَ مِنْ عِبَادِكُمْ وَإِمَائِكُمْ ۚ إِن يَكُونُوا فُقَرَاءَ يُغْنِهِمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٣٢﴾

Na waozesheni wajane miongoni mwenu na walio Swalihina kati ya watumwa wenu wanaume na wajakazi wenu. Wakiwa mafakiri Allaah Atawatajirisha katika fadhila Zake. Na Allaah Mwenye Wasaa, Mjuzi wa yote. [An-Nuwr: 32]



Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



"Yeyote mwenye kukengeuka na Sunnah yangu si katika mimi [Al-Bukhaariy na Muslim] Ndoa ikiwa ndani yake.





Kwa minajili hiyo, ‘Ulamaa wamegawanya ndoa katika sehemu tatu:



Faradhi kwa yule asiyeweza kujizuia.


Sunnah iliyohimizwa kwa Muislamu anayejiweza.


Haraam kwa asiyeweza kumuweka mke ima kwa kutoweza kumtimizia tendo la ndoa na kadhalika.


Kuhusu kadhiya yako inategemea uko katika kundi gani. Ikiwa uko katika kundi la mwanzo itakuwa ni aula mwanzo uoe ili usiingie katika zinaa baadaye utakwenda Hijjah. Ama ukiwa katika aina ya pili au ya tatu, utahitajika mwanzo kwenda Hijjah, kisha uoe.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Du'aa Gani Kuomba Unapokunywa Maji Ya Zamzam?



Alhidaaya.com



Swali:



Asalam Aleikum wa Rahmatullah wa Barakat

Fadhli ni ya Subhanahu wa Ta'aalaa alojalia Ahli Alhidaaya ujuzi wa ku elimisha Umati Muhammad Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa salam.

Maombi yangu, ni ilimishwe "DUA" ya kuomba kabla ya kunywa maji ya zamzam wakati mtu yupo Hajj?

Jazakum Allaahu Kul Khair wa Asalam Aleikum wa Rahmatullah wa Barakatuh.


Jibu:

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.




Hakuna du'aa maalumu iliyopatikana kutoka katika Hadiyth Sahihi ya kuomba wakati wa kunywa maji ya zamzam. Baadhi ya du'aa zilizonukuliwa zimechambuliwa kwa dalili kuwa ni kutoka katika zile Hadiyth dhaifu. Iliyopatikana kuwa ni Swahiyh ni kwamba unaomba chochote utakacho mwenyewe wakati kunywa. Hii ni kutokana na dalili ifuatayo:



(( ماء زمزم لما شرب له)) صحيح ابن ماجه

((Maji ya zamzam kwa (jambo liloombewa) wakati wa kunywa)) [Swahiyh Ibn Maajah na imepewa daraja ya Swahiyh na Shaykh Al-Albaaniy]


Na Allaah Anajua zaidi
 
Fadhila Za Siku Ya ‘Arafah, Sababu Zake Na Tofauti Ya Nyakati Baina Ya Nchi



Alhidaaya.com





Swali La Kwanza:





Assalam Alaykum,



Alhamdulillah leo nimemtumia msg swahiba wang kuhusu Arafah kwamba afunge siku ya Alhamis sawa na mwezi9 wa saudia,akanjib kua Nabiy amefunga mwez 9 wala si siku ya Arafah nkamuliza nini lengo la kufunga si kuungana na mahujaji? akanjib Nabiy amefunga Arafah kwa lengo la kukutana Adam na Hawaa na kuchinja mwezi 10 kwa lengo la Nabiy Ibrahim kabla ya kufaradhishwa Hijjah, akasema amemskia shekh maneno ayo huku shekh amestadil hadiyth ya bi Aisha swahiba wng akaniuliza je kama lengo la Arafah ni kungana na waislam makkah kuna mchi kama marekan hadi linazama jua la mchana wa Arafah wao markan ni usiku au Australia ni sa5 za usiku je enyi mashekh zang wana Alhidaaya haya nikweli?mm nkafanya bahthi kwenye alhidaaya sjaona sehem inayosema kua Nabiy amesema watu wafunge mwez9 au siku ya Arafah?nime search kwenye Arafah nkaona fadhila za siku ya arafah sio lini wafunge arafah je ni siku au kisimamo? nimeonelea ntumie email hii ili npate majibu haraka kwan siku ya alhamis haiko mbali ningetumia email ya masuala nngechelewa kujibiwa labda kwa kutoliona hili mapema. Rabb awazidishien kwa kuwaelimisha Ummah





Swali La Pili:



Katika hii dunia tumetofautiana kimasaa utakuta nchi moja hadi nyingine wametofautiana masaa 8 hadi 12. Je inakuwaje pale watu wanakuwa kwenye viwanja vya arafa na wao unakuta wapo nyuma kimasaa?





Jibu:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Maana ya ‘Arafah ni jina la Jabali lilioko mji wa Makkah ambalo alisimama Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwahutubia Maswahaba alipotekeleza Hajj yake ya mwisho. Na hiyo ndio nguzo mojawapo kuu ya Hijjah bila ya kuweko hapo mwenye kuhiji atakuwa hakutimiza hijja yake kama tunavyopata dalili katika Hadiyth ifuatayo:



عن عبد الرحمن بن يعمر قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((الحج عرفة ، من جاء قبل طلوع الفجر من ليلة جمع فقد أدرك الحج)) صحيح الجامع

Kutoka kwa ‘Abdur-Rahmaan bin Ya’mur ambaye amesema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam: ((Al-Hajj ni ‘Arafah, atakayekuja kabla kutoka Alfajiri usiku wa kujumuika atakuwa ameipata Hajj)) [Swahiyh Al-Jaami’]



Mwezi wa tisa katika kalenda ya Kiislamu ni mwezi wa Ramadhwaan ambao umefaridhiswa Swawm kama tunavyojua sote. Sasa hatuelewi muulizaji amekusudia nini. Ama ikiwa ni tarehe 9 ya Dhul-Hijjah, basi hiyo ndiyo siku ya ‘Arafah na ni siku ambayo mahujaji wanakusanyika wote hapo kutimiza nguzo hii kuu ya Hijjah. Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakufunga Swawm siku hiyo kwa dalili iliyo wazi kabisa.



عن ميمونة بنت الحارث: أن الناس شكوا في صيام النبي صلى الله عليه وسلم يوم عرفة ، فأرسلت إليه بحلاب ، وهو واقف في الموقف ، فشرب منه والناس ينظرون" البخاري

Kutoka kwa Maymuunah bint Al-Haarith (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba watu walitia shaka na Swawm ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) [kama alifunga] Siku ya ‘Arafah, nikampelekea maziwa, naye akiwa amesimama akayanywa na huku watu wanamtazama” [Al-Bukhaariy]





Kwa hiyo hakuna hukmu ya Swawm siku ya ‘Arafah kwa mahujaji. Bali Swawm ya siku hiyo ni kwa Waislamu wasiojaaliwa kuweko siku hiyo ‘Arafah kwa ajili nao wapate fadhila za siku hiyo tukufutu ambayo Swawm yake ni kufutiwa madhambi ya miaka miwili kama tunavyopata dalili katika Hadiyth ifuatayo:



عَنْ أَبِي قَتَادَةَ رضي الله عنه أن النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ : ((صِيَامُ يَوْمِ عَرَفَةَ أَحْتَسِبُ عَلَى اللَّهِ أَنْ يُكَفِّرَ السَّنَةَ الَّتِي قَبْلَهُ وَالسَّنَةَ الَّتِي بَعْدَهُ )) أخرجه مسلم

Imetoka kwa Abu Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: "Swawm ya 'Arafah nataraji (kwa Allaah) kufuta madhambi ya mwaka uliopita na wa baada yake." [Muslim]





Fadhila nyinginezo zinapatikana katika kiungo kifuatacho:





Fadhila Za Siku Ya 'Arafah Na Yawmun-Nahr (Siku Ya Kuchinja)



Ama kuhusu tofauti ya masaa baina ya nchi na nchi, inampasa Muislamu aamini Aayah na Hadiyth zinazoeleza mas-alah haya bila ya kutilia shaka au kujaribu kuzipinda. Hii ndio ‘Aqiydah sahihi ya Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah.





Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):



إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٠﴾

Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na mabadiliko ya mfuatano wa usiku na mchana; bila shaka ni Aayaat (ishara, zingatio) kwa wenye akil [Aal-‘Imraan: 190]



Bila shaka kuna hikma yake ya kuwa nchi zote ulimwenguni zikhitilafiane kwa wakati. Ikiwa Kusini au Magharibi mwa dunia ni asubuhi, Kaskazini au Mashariki ya dunia kuwe ni usiku. Hii inaonyesha pia Rehma za Allaah kwa waja Wake kutokuwatia katika mashaka, Naye Ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi kwa namna yake ya mzunguko wa ardhi, jua na mwezi. Na Ndiye Mwenye kudhibiti mizunguko hiyo. Hivyo Aliyoyaumba yote ni kwa ajili ya manufaa ya binaadamu wote ulimwenguni. Na Anapotoa hukmu fulani basi tutambue kwamba ina hikma yake na tuwe wenye kusikia na kutii bila ya kutilia shaka.



Na kuamini huku ni sawa na kuamini kuteremka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) thuluthi ya mwisho ya usiku katika mbingu ya kwanza:





عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((يَنْزِلُ رَبُّنَا تَبَارَكَ وَتَعَالَى كُلَّ لَيْلَةٍ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا حِينَ يَبْقَى ثُلُثُ اللَّيْلِ الْآخِرُ يَقُولُ: مَنْ يَدْعُونِي فَأَسْتَجِيبَ لَهُ مَنْ يَسْأَلُنِي فَأُعْطِيَهُ مَنْ يَسْتَغْفِرُنِي فَأَغْفِرَ لَهُ)) البخاري و مسلم

Imetoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa Huteremka (kwa namna inavyolingana na utukufu Wake) kila siku katika mbingu ya dunia (mbingu ya kwanza) inapobakia thuluthi ya mwisho ya usiku na Husema: Nani ananiomba Nimtakabalie? Nani Ana shida Nimtekelezee? Nani ananiomba maghfirah Nimghufurie?” [Al-Bukhaariy, Muslim]



Na hivyo kila Muislamu popote alipo ulimwenguni anaweza kupata fadhila zilotajwa katika Hadiyth hiyo ya kuamka thuluthi ya mwisho ya usiku kwa wakati wa nchi aliyoko. Haiingii akilini kwamba Mahujaji wasimame ‘Arafah Makkah wakati ni machana, na watu walioko nchi za mbali ambako kwao ni wakati wa usiku huko, nao wafunge Swawm zao usiku na hali kufunga Swawm ni kuanzia Alfajiri hadi jua kuzama kwa jua.





Na Allaah Anajua zaidi
 
UJUMBE WA LEO

Tumeingia mwezi wa Dhul Hijja miongoni mwa miezi mitukufu,hivyo tusizidhulumu nafsi zetu kwa kutenda maovu

Hakika ukitenda mema mwezi huu unalipwa maradufu,hivyo tushikamane na kusoma sana qur'an,kumtaja Allah azza wa jalla kwa wingi, kwakuleta adhakar mbali mbali

Kusoma mambo ya elimu kama ambavyo tunafanya katika uzi huu na kusikiliza mawaidha

Swala tano pamoja swala za sunna kwa wingi

Bila kusahau kufunga swaumu katika haya masiku kumi,usipoweza kufunga zote basi walau chache utakazo jaaliwa
 
NIA MAHALA PAKE NI MOYONI

Najua tumesoma makala kuhusiana na mambo ya nia kwamba niya hasa haitamkwi bali mahala pake ni moyoni

Nimeamua kujadili kidogo kwasababu ni somo ambalo bado ni changamoto kwa wengi wetu kwakuwa huko nyuma tulikaririshwa kutamka maneno fulani fulani ya nia nikiwemo mimi

Lakini tunaambiwa Nabii swalla aallahu alaiyhi wa aliih wa sallamu hakuwahi kufundisha au kuelekeza maneno yoyote ya nia,na lau yangekuwepo basi lazima maswahaba wangetufahamisha

Sasa najua mazoea yanaleta shida lakini tupambane tufanye lile lililo sahihi baada ya mda tutazoea,binafsi bado sometime mazoea yanakuja kichwani mfano ninapo tia udhu ,unapoanza kuosha uso huwa tunasema Nawaitu faradhi wudhui,basi saa nyingine najikuta hiyo kauli inakuja

Lakini katika hali halisi inasemekana Mtume swalla aallahu alaiyhi wa aliih wa sallam alisema Bismillah wakati wa kuanza kuosha viganja vya mikono,na vile vile kuna mashaka hiyo hadith ni dhaifu,lakini walio wengi wamekubaliana kwamba kwakuwa kwa jambo lolote la kheri katika dini tunapaswa kuanza na Bismillah,basi wakaona ni sahihi unapanza kutia udhu basi uanze na Bismillah

Kwahiyo hata kwenye swala haikuwahi kufundishwa nia ya swala yoyote ile,bali Mtume alisikika akifungua swalla kwa takbira Allaahu Akbar

Kwa kila ibada yoyote lazima iwe na nia,na mahala pa nia ni moyoni,na ndio penye ikhlaaswi

Ndio maana Allah huwa haangalii sura zetu na viwiliwili vyetu ila nyoyo zetu

Tusome hadith zifuatazo:

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صلى الله عليه وآله وسلم): ((إِنَّ اللَّهَ لاَ يَنْظُرُ إِلى أجْسمِكُمْ وَلاَ إِلَى صُوَرِكُمْ وَلَكِنْ يَنْظُرُ إِلَى قُلُوبِكُمْ)) رواه مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Allaah Hatazami viwiliwili vyenu wala sura zenu, lakini Anatazama nyoyo zenu)). [Muslim]



Nyoyo ndizo zitakazodhihirisha ikhlaasw ya mtu kwani humo ndipo kunapofichika shirki kama ilivyobainishwa katika Hadiyth ifauatayo:



عَنْ أَبِي سَعِيدٍ، قَالَ: خَرَجَ عَلَيْنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَنَحْنُ نَتَذَاكَرُ الْمَسِيحَ الدَّجَّالَ، فَقَالَ: ((أَلا أُخْبِرُكُمْ بِمَا هُوَ أَخْوَفُ عَلَيْكُمْ عِنْدِي مِنَ الْمَسِيحِ الدَّجَّالِ؟)) قَالَ: قُلْنَا: بَلَى! فَقَالَ: ((الشِّرْكُ الْخَفِيُّ، أَنْ يَقُومَ الرَّجُلُ يُصَلِّي، فَيُزَيِّنُ صَلاتَهُ، لِمَا يَرَى مِنْ نَظَرِ رَجُلٍ)) سنن ابن ماجه (4204).

Imepokelewa kutoka kwa Abu Sa’iyd (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja kwetu wakati tulikuwa tukijadiliana kuhusu Dajjaal, akasema: ((Je, niwajulisheni kile nikikhofiacho zaidi kwenu kuliko hata (hatari za) Dajjaal?)) Tukasema: Ndio. Akasema: ((Basi ni shirki iliyojificha. Mtu anasimama kuswali, anaipamba na kuiremba Swalaah yake kwa kujua kuwa kuna watu wanamtazama)) [Sunan Ibn Maajah (4204)]

Nadhani mpaka hapo tumeona hasa moyo ndio sehemu halisi ya kutakasa ibada ya mtu

Tuje kwenye hadith nyingine,Nabii swalla aallahu alayhi wa sallam alisema hakika kila mtu atalipwa kutokana na nia yake,yule ambaye kuama kwake kwa ajili ya Allah na Mtume wake watalipwa kutokana na kile walichonuia na waliohama ili wapate wanawake wa kuoa watapata kwa kile walichonuia

Sasa tuje kwenye mfano hapo juu,je hao waliohama kwa nia ya kumpata mke,je walisema "sasa nanui kwenda madina kupata mke"? Au ilipita katika nyoyo zao tu wanahama kwa ajili ya kutafuta mke

Kama kulikuwa kuna maneno maalumu ya nia yao basi wasingelipwa kwa nia yao hiyo kwakuwa walikuwa hawajafundishwa na Nabii swalla aallahu alayhi wa sallamu nini cha kusema,na hao walihama kwa ajili ya Allah na Mtume nao hatusikia kwamba kuna maneno maalumu walifundishwa ya kusema

Nimeyasema haya ili akili yako itafakari na kuona kwa mapana na marefu

Kwahiyo nia ni kusudio la kufanya jambo fulani ambalo lipo moyoni mwako,mfano mwingine je mathalani unataka kulog in jf, je huwa unajitamkisha maneno maalumu kuwa "sasa naweka nia ya kulog in jf" AU huwa inapita tu moyoni kwako tu kuwa uingie jf

Jibu ni kwamba huwa inapita tu moyoni kwako uingie jf,hiyo ndio nia yako au kusudio
lako kwa wakati huo

Je unaposikia adhana inalingania kwenda kuswali, je huwa unasema kwa maneno '"sasa nanuia kwenda kuswali" au tu inapita moyoni kwako huu ni mda wa swala

Kile kitendo cha kujua huu ni mda wa swala na kuelekea kuswali tayar umeweka kusudio au nia ya kwenda kuswali

Kile kitendo cha kujua swala haiswihi bila udhu na ukaelekea kwenye bomba la maji au ukachota maji ya kutia udhu tayar moyoni mwako lilipita kusudio au azimia la kutia udhu na hiyo ndio nia yako

Kwahiyo nia siku zote iko moyoni mwa mtu kwa kila kitendo,hata ukitaka kumtukana mtu huwa kuna kusudio linatangulia kwamba huyu fulani leo lazima nimpe makavu yake

Natumaini walau tutakuwa tumepata picha kuhusiana na nia kwenye ibada zetu

Subhaanaka allahuma wabihamdika ashahadu anlaa ilaaha ila anta astaghfiruka waatubu ilaik
 
Khutuba ya Ijumaa kuhusu Hajj (Hijja):

Khatibu:

Alhamdulillahi, tunamshukuru Allah (S.W.) kwa kutujaalia uhai na Imani hadi tukafika Ijumaa hii tukufu. Rehma na amani zimshukie Mtume Muhammad (S.A.W.), maswahaba wake, na wote wanaomfuata kwa wema hadi siku ya mwisho.

Kipengele Kikuu: Hajj – Safari ya Kiimani

Ewe Muislamu! Hajj ni nguzo ya tano ya Uislamu, na ni ibada ya kipekee yenye mafunzo makubwa ya kiroho, kijamii, na kibinadamu. Allah amesema:

"Na kwa ajili ya Allah, watu wanawajibika kuhiji Nyumba hiyo – mwenye uwezo wa kuifikia..." (Qur'an 3:97)

Faida za Hajj:

1. Huondoa madhambi – Mtume (S.A.W.) amesema:
"Aliyefanya Hajj bila kusema ovyo au kufanya mambo machafu, atarudi kama siku alipozaliwa (bila dhambi)." (Bukhari, Muslim)

2. Huunganisha Umma – Hajj hukusanya Waislamu wa rangi, lugha na mataifa mbalimbali. Inatufundisha umoja na usawa mbele ya Allah.

3. Huimarisha subira na ibada – Kupitia vizingiti vya safari, ibada nyingi, na kujizuia na makatazo, muumini hujifunza kujitawala.

Wito kwa Waislamu:

  • Wenye uwezo wajitahidi kuhiji mapema wasisubiri uzee au matatizo.
  • Waliokwisha hajj, watumie mfano wa ibada hiyo kuimarisha maisha yao ya kila siku.
  • Tuwaombee Waislamu wote walioko Hijja watekeleze kwa ikhlasi na salama.
 
UJUMBE WA LEO

Ndugu zangu katika imani,tunafahamu wote kwamba huu ni msimu wa Hijja,hakika huu ni mwezi mtukufu,ndani yake kuna haya masiku kumi ambayo ni matukufu sana

Na mwezi tisa kuna funga ya arafa ambayo ni muhimu sana,mja wa Allah akifunga swaumu hiyo basi hufutiwa madhambi ya miaka miwili subhaanallah,ya mwaka uliopita na mwaka ujao

Je tunataka nini tena ndugu zangu katika imani? Wallah huu ni mwezi wa kuchuma lau tungejua

Kwa wanaofuta mwezi wa kimataifa arafa itakuwa siku ya alhamis na eid siku ya ijumaa,na wanaofuta muandamo wa mwezi wa zone yao arafa itakuwa ijumaa na eid jumamosi

Lakini fursa ya kuchuma thawabu zaidi ipo kwa kufunga swaumu katika hizi siku nyingine ambazo tayar tupo ndani yake

Huu ni mwezi wa kufanya adhkar kwa wingi,kithirisha kusema "subhanallah,alhamdulillah,allahu akbar, laa ilaaha illallah,subhaanallah wabihamdih subhaanallah liadhwiim,lahaula wala qwata illa billah

Na nyiradi nyengine unazo zijua,zitaje kadri ya uwezo wako,uwe kazini,uwe unadrive mtaje Allah

Mswalie Nabii swalla aallahu alayhi wa sallamu kwa wingi

Soma qur'an na tafsir yake na zingatia ujumbe wake

Hakuna mda wa kupoteza kwani hakika masiku yenyewe ni machache

Swali swala za faradhi,pamoja na sunna,jipinde uamke usiku uswali tahajjud

Amali zozote utakazo zifanya hulipwa maradufu ndani ya masiku kumi haya matukufu
 
Maswali: Hajj
SWALI:

ASALAMA ALAYKUM

mimi suala langu kuwa hija yangu itaswihi ikiwa sisemeshani na familiya ya mume wangu, lkn mimi nipo tayari kwa kusemesha nao lkn wao hapo tayari tena hata kwa kuisogelea ile nyumba yao. Naomba nifahamishe uzuri kuhusu hili suala langu.

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu uhasama na jamaa za mumeo.

Hakika ni kuwa uhasama ni sifa ambayo haifai kuwepo baina ya Waislamu licha jamaa wanaohusiana kwa kuoana.

Ikiwa utahiji ukiwa na uhasama na jamaa za mumeo, Hija yako itaswihi bila ya wasiwasi wowote. Hata hivyo, ikiwa wewe ndiye uliyeanza uhasama thawabu za ‘amali zako nyingi zitapungua kwa ajili ya kuwa na sifa mbaya kama hiyo. Jambo ambalo unafaa ufanye ni kujaribu njia zote za kuweza kurudisha hali ya awali na kuondosha utesi na uhasama. Tufahamu kuwa Muislamu ni ndugu ya Muislamu, hivyo Waislamu hawafai kuhusudiana wala kuwa na uhasama.

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Wala si halali kwa Muislamu kumhama nduguye Muislamu zaidi ya siku tatu” (al-Bukhaariy na Muslim).

Na pia amesema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Hufunguliwa milango ya Pepo siku ya Jumatatu na Alkhamisi, akasemehewa kila mja asiyemshirikisha Allaah na chochote, ila mtu ambaye ana uhasama na nduguye. Husemwa: Waongozeni hawa wawili mpaka wapatane, Waongozeni hawa wawili mpaka wapatane” (Muslim).

Wa kwanza ambaye anaondoka katika uhasama huo ni yule anayemsalimia mwenziwe. Ikiwa utakuwa umejaribu kuwatolea salamu wakakataa basi makosa yote yatawarudia wao nawe hutakuwa na makosa aina yoyote ile.

Na Allaah Anajua zaidi
 
Hijja Wanayopelekwa Watu Na Serikali Au Mialiko Ya Nje Inafaa?



Alhidaaya.com





Swali:



AAWW!



Nauliza:


Hizi Hijja wanzokwenda viongozi kwa gharama za serikali au mialiko ya mfalme wa Saudia zinasihi?



Wabillahi Taufiq,





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Kwanza tunapenda kukumbusha ndugu muulizaji kuacha kufupisha salaam unapoandika, unapoteza fadhila na ujira kwa kufanya hivyo.



Kwa hakika usaidizi unatakiwa upewe Waislamu wanaostahiki ambao ni hohehahe. Mara nyingi fursa hizi huwa zinatumiwa vibaya kwa kupewa watu ambao ni viongozi wenye uwezo au ambao tayari wameshakwenda kufanya Hijjah kama ambavyo tunaona wanavyofanya baadhi ya viongozi wa taasisi za Kiislamu. Na jambo lenye kusikitisha zaidi, kuna baadhi ya viongozi wa Taasisi fulani za Kiislamu huuza hizo tiketi za bure wanazopewa na serikali ya Saudia Arabia ambayo inafanya juhudi kubwa sana za kusaidia nchi nyingi duniani kila mwaka ili wale wasio na uwezo wapate nao fursa ya kutekeleza nguzo hiyo tukufu.



Na haitokuwa vyema ikiwa mtu ana uwezo kukubali mwaliko kama huo na vizuri akatae ili fusra hiyo wapewe wale wasio na uwezo na hususan wale wenye umri mkubwa.



Hata hivyo, wakati mwengine serikali ya Saudia huwa inataka viongozi wa nchi tofauti kwa ajili ya makongamano na mikutano na ikiwa ni msimu wa Hijjah basi hutaka waalikwa wao wafanye Hijjah kabisa na katika hilo hakuna tatizo. Hijjah aina hizi hazina tatizo lolote na ni thawabu kwa wenye kujitolea kwa hilo. Hata hivyo kujitolea huko kungekuwa natija nzuri zaidi lau wangepatiwa:



Waislamu wasiokuwa na uwezo (masikini na mafakiri) ambao hawajawahi kwenda.
Wengine wasio na uwezo kama madu'aat (walinganiaji) ambao hawajawahi kwenda.
Wenye uwezo kukataa kuchukua fursa hizo na badala yake kupendekeza watu wengine.
Kina mama pia nao wapatiwe fursa hizo (Wakiwa wana mahaarim zao)
Kusiwe na ubaguzi katika kuchagua watu.


Na Allaah Anajua zaidi
 
Kuchukua Mkopo Wa Ribaa Kwa Ajili Kwenda Hijjah Inafaa?



Alhidaaya.com





Swali:



Asaalam Alykum,



Mimi nna nia ya kwenda hija, lakini hizi pesa nnazotaka kwendea Hijja ninataka kukopa kwenye chama chetu cha kuweka na kukopa. Mimi nimechangia sh.1,000,0000 na nna uwezo wa kukopa sh.3,000,000 lakini wanakata na intrest. Je pesa hizi zitafaa kuwendea hijja?





Jibu:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Fardhi ya kutekeleza Hijjah ni fardhi inayompsa mtu kutekeleza akiwa na uwezo kama Anvyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ

Na kwa ajili ya Allaah imewajibika watu watekeleze Hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo. [Al-'Imraan: 96]



Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kutokana na Hadiyth iliyopokelewa kutoka na 'Umar bin Khatwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu):

((Na kwenda Hijjah ukiweza kufanya hivyo)) [Muslim, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy]



Ibara hii ya Aayah na Hadiyth yana maana ya kuwa kila Muislamu ni lazima ahiji mara moja katika maisha yake akiweza kufanya hivyo. Uwezo una tafswili nyingi na yaliyo muhimu ni: -



Awe na afya nzuri ya kuweza kustahamili mazito ya safari.



Kuwe na usalama njiani, kwenda na kurudi.

Awe na uwezo wa kutoa gharama za safari na kuacha masurufu yote ya wale wanaomtegemea.



Ikiwa sharti moja katika hayo imekosekana basi Hijjah haijamlazimu mtu huyo.



Fardhi hii ni sawa tu na fardhi ya kutoa Zakaah kwani maskini hana waajib wa kutoa Zakaah pamoja na kuwa Zakaah ni nguzo ya Uislam, na hata mwenye uwezo pia kuna masharti yake mfano, awe na kiasi maalum cha mali na pia sharti ya mali yenyewe iwe imetimia kwa mwaka mzima bila ya kutumiwa. Muislamu anaposhindwa kutimiza sharti hizo, waajib wa kutekeleza fardhi hizo huwa umemuondokea. Na hata atakapofariki akiwa katika hali ya kukosa uwezo basi hana jukumu wala dhambi mbele ya Allaah.



Ikiwa hali ni hiyo basi, kuchukua mkopo kwa ajili ya kutekeleza Hajj haifai, kwani ni jambo la kujikalifisha ambalo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ametuondoshea.



Juu ya hivyo ni kwamba mkopo wenyewe una riba jambo ambalo ni haraam kwani haruhusiwi kula na kufaidika nayo wala kufanyia Hajj. Maonyo kadhaa yamethibiti kuhusu ribaa yakiwemo Hadiyth:



"Dirhamu ya ribaa anayokula mtu na huku anajua ni mbaya zaidi kuliko kuzini mara thelathini na sita." [Ahmad]



"Ribaa ina milango 73 iliyo nyepesi na sahali ni mtu kumuoa mamake." [Al-Haakim]



"Jiepusheni na mambo saba yenye kuangamiza… kula ribaa." [Al-Bukhaariy na Muslim]



Hivyo kufanya Hajj kunahitaji kipato kilichokuwa safi kutoka katika chanzo cha halaal.



Vile vile deni ni jambo zito katika Uislamu kwani ni haki ya mtu, hivyo ni jambo la kwanza la kutekelezwa kabla ya ‘ibaadah yoyote. Atakapofariki Muislamu mwenye deni, akasubiri kwanza alipe deni lake, kisha akafariki akiwa hakutimiza Hijjah, basi ataonana na Rabb wake akiwa amekamilisha Uislamu wake kwa sababu Hijjah haikuwa ni waajib kwake. Lakini akitekeleza Hijjah kabla ya kulipa deni kisha akafariki, atakuwa katika hatari kwa sababu hata wanaofariki wakiwa Mashahidi wanasamehewa kila kitu isipokuwa deni. Sasa vipi basi iwe wengine?



Hitmisho ni kwamba haikupasi kuchukua mkopo kwa ajili ya kutekeleza Hijjah ikiwa ni mkopo wenye riba au hata bila ya riba.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Kufanya Hajj Na Huku Familia Yake Inalishwa Na Serikali Ulaya; Hawakusema Serikalini Kuwa Wameoana



Alhidaaya.com





Swali:



Assalam Alaykum Warahmatullah



Mimi Naomba Niulizie Kuhusu Mtu Ambae Anataka Kwenda Kutekeleza Ibada Ya Hajj Na Anouwezo Wa Kiafya Na Kifedha Za Kuachia Mke Wake Na Watoto Wake Kwa Ajili Ya Matumizi Yao, Lakini Nyumba Wanayokaa Wanalipiwa Na Serikali Kwa Sababu Hawakusema Kwamba Wameoana Jee Inafaa Au Akiilipia Kwa Muda Mfupi Tu Ili Katika Kile Kipindi Cha Kua Yeye Yuko Katika Ibada Hio Ya Hajj Awe Amejilipia Mwenyewe Jee Inafaa?





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Kuiambia serikali kuwa hajaona na mkewe au kuiambia kuwa wametengena na mkewe na hali hawajatengana; hayo ni makosa na ni mambo ambayo yanaweza hata kumtenganisha mtu na mkewe kutegemea na makusudio yake.



Hivyo, atakuwa amefanya makosa kwa udanganyifu wake ambao umesababishwa na maslahi madogo tu ya kidunia ya kubana pesa za kulipia nyumba kwa ajili ya kujilimbikizia mali ili ima ajenge kwao alipotoka au aanzishe biashara n.k.



Mtu huyo atakuwa na madhambi mbele ya Allaah Aliyetukuka kwa kuongopa kwake. Hakika huko ni kuudhalilisha Uislamu wake kwa Makafiri na hata kumtukunisha mkewe ambaye pindi atakapoonekama amebeba mimba italeta picha ya kuwa Muislamu huyo ni malaya.



Tafadhali soma zaidi yaliyomo kwenye viungo vifuatavyo:



Nasaha Kwa Wakimbizi Wanaoishi Kusema Hawajaoana Ili Wapate Ruzuku Ya Serikali



Anapewa Pesa Na Serikali, Je, Mume Hapasi Kumhudumia Ikiwa Ni Hivyo?



Hata hivyo, ‘Ibaadah yake ya Hijjah ikiwa chumo lake ni la halali itakuwa ni sawa na itabidi aombe msamaha kwa Allaah Aliyetukuka na atoke katika nyumba ambayo ameipata kwa udanganyifu.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Back
Top Bottom