Ramadhan Special Thread
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم



Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!



18- Isti’aanah (Kuomba Msaada) Kwa Asiyekuwa Allaah


Alhidaaya.com









Maana Ya Isti’aanah (kuomba msaada) na dalili zake:



Isti’aanah ni kuomba msaada. Na Isti’aanah kwa Allaah ni kuomba katika mambo ya Dini na ya dunia na inajumuisha mja kujidhalilisha kwa Mola wake na kuwa na yakini na kumtegemea Yeye (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Pekee kama Anavyosema:

فَاعْبُدْهُ وَتَوَكَّلْ عَلَيْهِ

basi mwabudu Yeye na tawakali Kwake. [Huwd: 123]





Na katika Suwratul-Faatihah ambayo inajumuisha aina zote za Tawhiyd, Muislamu anakariri katika Swalaah zake zote:

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ﴿٥﴾

Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada. [Al-Faatihah: 5]





Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

إِيَّاكَ نَعْبُدُ

Inathibitisha Tawhiyd ya Uluwhiyyah (kumpwekesha Allaah katika kumwabudu); yaani aina zote za ‘ibaadah zinahitaji kuelekezwa Kwake Pekee Subhaanahu wa Ta’aala.



Na

وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

Inathibitisha Tawhiyd ya Ar-Rubuwbiyyah (kumpwekesha Allaah katika Uola) kwa sababu ni kuomba msaada kwa Ar-Rabb (Mola) Ambaye ni Al-Khaaliq (Muumbaji), Ar-Raaziq (Mtoaji rizki), Al-Mudabbir (Mwendeshaji mambo), Al-Maalik (Mwenye kumiliki) Ambaye mambo yote yamo Mikononi Mwake. Kwa hiyo anapaswa Yeye kuombwa mahitaji yetu kama vile Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alivyomuusia Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ambaye amehadithia:



كُنْتُ خَلْفَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم يًوْماً، فقال: ((يا غُلامُ، إنِّي أُعَلِّمُكَ كلِماتٍ: احْفَظِ اللهَ يَحْفَظْكَ، احْفَظِ اللهَ تَجِدْهُ تُجاهَك، إذا سأَلْتَ فاسْأَلِ اللهَ، وإذا اسْتَعنْتَ فاسْتَعِنْ باللهِ، واعْلَمْ أنَّ الأُمَّة لَوِ اجْتَمَعَتْ على أَنْ يَنْفَعُـوكَ بِشَيءٍ لَمْ يَنْفَعُوكَ إلا بِشَيْءٍ قدْ كَتَبَهُ اللهُ لَكَ، وإن اجْتَمَعُوا على أن يَضُرَّوكَ بِشيءٍ لَمْ يَضُروكَ إلا بِشَيءٍ قَدْ كَتَبهُ اللهُ عَلَيْكَ، رُفِعَتِ الأقْلامُ وَجَفَّتِ الصُّحُفُ))

Siku moja nilikuwa nyuma ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia: “Ee kijana! nitakufundisha maneno (ya kufaa); Mhifadhi Allaah (fuata maamrisho Yake na chunga mipaka Yake) Atakuhifadhi. Muhifadhi Allaah utamkuta mbele yako. Ukiomba, muombe Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), ukitafuta msaada tafuta kwa Allaah. Tambua kwamba ikiwa ummah mzima utaungana kukunufaisha wewe kwa kitu, basi hutonufaika ila tu kwa kile Alichokwishakuandikia Allaah. Na wakikusanyika kukudhuru kwa chochote, hutodhurika ila tu kwa kile Allaah Alichokwishakukuandikia (kuwa kitakudhuru), kwani kalamu zimeshanyanyuliwa (kila kitu kishaandikwa) na swahifa zimeshakauka.” [At-Tirmidhiy, na amesema Hadiyth Hasan Swahiyh]



Kumuomba bin-Aadam msaada wa jambo ambalo limo katika uwezo wake inafaa kwa dalili zifuatazo katika Qur-aan na Sunnah:



Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ

Na shirikianeni katika wema na taqwa, na wala msishirikiane katika dhambi na uadui. [Al-Maaidah: 2]



Na Hadiyth ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



عن أبي هُرَيْرَة رضي اللهُ عنه، عن النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قال: "مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ الدُّنْيا نَفَّسَ اللهُ عَنْهُ كُرْبَةً من كُرَبِ يوْمِ القيامَةِ، ومَنْ يَسَّرَ على مُعْسِرٍ يَسَّرَ اللهُ عليه في الدنْيا والآخِرَةِ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِماً سَتَرَهُ الله في الدُّنْيا والآخِرَةِ واللهُ في عَوْنِ الْعَبْدِ ما كانَ الْعَبْدُ في عَونِ أخيهِ"

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Yeyote atakayemuondoshea shida ya kidunia Muislamu mwenzake, Allaah Atamuondoshea moja katika shida za Siku ya Qiyaamah. Na yeyote yule atakayemsaidia muhitaji (maskini) Allaah Atamsaidia haja zake hapa duniani na Aakhirah. Na yeyote yule atakayemsitiri Muislamu, Allaah Atamsitiri hapa duniani na Aakhirah. Allaah Humsaidia mja wake wakati wote madamu mja (huyo) yungali anamsaidia nduguye (Muislamu).” [Muslim]



Pia,



عَنْ عَبْدِ الله بنِ عُمَرَ رَضِيَ الله عَنْهُما، أَنَّ النَّبِيَ صَلَّى الله عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "أَحَبُّ النَّاسِ إِلَى الله أَنْفَعُهُمْ لِلّنَاسِ، وَأَحَبُّ الأَعْمَالِ إِلَى الله سُرُورٌ تُدْخِلُهُ عَلَى مُسْلِمٍ أَوْ تَكْشِفُ عَنْهُ كُرْبَةً أَوْ تَقْضِيَ عَنْهُ دَيْناً أَوْ تَطْرُدُ عَنْهُ جُوعاً، وَلأَنْ أَمْشِيَ مَعَ أَخِي المُسْلِمِ فِي حَاجَةٍ أَحَبُّ إِلَيَّ مِنْ أَنْ أَعْتَكِفَ فِى هَذَا المَسْجِدِ يعني مسجدَ المدينةِ شهرًا، وَمَنْ كَفَّ غَضَبَهُ سَتَرَ اللهُ عَوْرَتَه وَمَنْ كَظَمَ غَيْظَهُ وَلَوْ شَاءَ أَنْ يُمْضِيَه أَمْضَاهُ مَلأَ اللهُ قَلْبَهُ رَجاءً يَوْمَ القِيَامَةِ وَمَنْ مَشَى مَعَ أَخِيهِ المُسْلِمِ فِى حَاجَةٍ حَتَّى تَتَهَيَّأَ لَهُ أَثْبَتَ اللهُ قَدَمَهُ يَوْمَ تَزِلُّ الأَقْدَامُ وَإِنَّ سُوءَ الخُلُقِ لَيُفْسِدُ العَمَلَ كَمَا يُفْسِدُ الخلُّ العَسَلَ"

‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Mtu ambaye ni kipenzi kabisa kwa Allaah ni yule ambaye ni mbora kabisa katika kunufaisha wenziwe. Na ‘amali zilizokuwa kipenzi kabisa kwa Allaah ('Azza wa Jalla) ni furaha aingizayo kwa Muislamu, au kumuondoshea shida, au kumtimizia deni lake, au kumuondoshea njaa. Na hakika mimi kwenda kumtimizia ndugu yangu haja yake, ni kipenzi kwangu kuliko nikae I’tikaaf (kijifunga katika ‘ibaadah Msikitini) mwezi mzima katika Masjid hii (Masjid Nabawiy). Na atakayeacha ghadhabu zake, basi Allaah Atamsitiri aibu zake. Na atakayezuia ghaydhi (ghadhabu na huzuni moyoni) zake japokuwa haogopi kuzionyesha, lakini anazuia, Allaah Atamjaza moyo wake kwa matumaini Siku ya Qiyaamah. Na atakayetembea na nduguye katika kumtimizia haja mpaka akamsaidia kikamlifu basi Allaah Atamthibitisha miguuu yake Siku ambayo miguu haitothibitika. Hakika khulqu (tabia) mbaya inaharibu ‘amali kama vile siki inavyoharibu asali.” [As-Silsilah Asw-Swahiyhah (906)]



Mifano ya mtu kumuomba bin-Aadam mwenziwe;



“Ee fulani! Nakuomba unisaidie kunilipia deni langu!”



“Ee fulani! Nakuomba unisaidie kunilipia gharama za matibabu ili nitibiwe!”



Au kuomba msaada wa mtu kumsimamia kazi yake, kumpatia anachohitaji katika matumizi, au kuomba kushirikiana katika ‘amali za khayr, au kuomba kusaidia jambo lolote la khayr ambalo litampatia thawabu kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa kumfanyia wema mwenziwe kama ilivyothibiti katika Hadiyth zilizotangulia.



Ama kuomba jambo ambalo halimo katika uwezo wa ki-bin-Aadam hapo huwa ni shirki. Mfano mtu kumuomba mtu amsaidie kupata kizazi, au kumwendea mtabiri amsaidie kumtazamia mambo ya ghayb, au mchawi kumuomba amfanye awe tajiri, au kuwaomba msaada wa riziki walio kaburini au kuwaomba wawaondoshee maradhi n.k.



Hizo ni aina za ‘ibaadah zipasazo kuelekezwa kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Pekee, kwa hiyo, 'Ibaadah kuielekeza kwa mwengine ni shirki kubwa kabisa kwa sababu ni kumshirikisha Allaah na viumbe Vyake katika mambo ambayo ni Allaah ('Azza wa Jalla) Pekee Mwenye uwezo nayo. Na shirki hii inamtoa mtu nje ya Uislamu kwa dalili kauli ya Allaah (Subahaanahu wa Ta’aalaa):



وَمَن يَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ فَإِنَّمَا حِسَابُهُ عِندَ رَبِّهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ ﴿١١٧﴾



Na yeyote yule anayeomba du’aa (au kuabudu) pamoja na Allaah muabudiwa mwengine hana ushahidi wa wazi wa hilo; basi hakika hesabu yake iko kwa Rabb wake. Hakika hawafaulu makafiri. [Al-Muuminuwn: 117]





Ilhali Allaah ('Azza wa Jalla) Ametuamrisha tumuombe Yeye Pekee kama Anavyosema:



وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ﴿١٨٦﴾

Na watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi ni Niko karibu (kwa ujuzi); Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba. Basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi, wapate kuongoka. [Al-Baqarah: 186]





Na Yeye Allaah ('Azza wa Jalla) Ndiye Mwenye kumuondoshea mtu dhiki zake Anapoombwa Yeye Pekee bila ya kumshirikisha, Anasema Allaah (Subahaanahu wa Ta’aalaa):



أَمَّن يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ وَيَجْعَلُكُمْ خُلَفَاءَ الْأَرْضِ ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ ﴿٦٢﴾

Au nani Anayemuitika mwenye dhiki mno anapomwomba, na Akamuondoshea ouvu na Akakufanyeni makhalifa wa ardhi? Je, yuko mwabudiwa pamoja na Allaah? Ni machache mno mnayokumbuka. [An-Naml: 62]



Na pia Akamuamrisha Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kumpwekesha na kutokumshirikisha na kwamba hata yeye Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hana uwezo wa kumnufaisha mtu wala kumdhuru wala kumjaalia hidaaya:



قُلْ إِنَّمَا أَدْعُو رَبِّي وَلَا أُشْرِكُ بِهِ أَحَدًا﴿٢٠﴾

Sema: (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi namuomba Rabb wangu na wala simshirikishi na yeyote.”





قُلْ إِنِّي لَا أَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا رَشَدًا﴿٢١﴾

Sema: “Hakika mimi sikumilikieni dhara na wala uongofu.” [Al-Jinn: 20-21]



Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَلَا تَدْعُ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَ ۖ فَإِن فَعَلْتَ فَإِنَّكَ إِذًا مِّنَ الظَّالِمِينَ﴿١٠٦﴾

Na wala usiombe badala ya Allaah visivyokufaa wala visivyokudhuru. Na ukifanya, basi hakika utakuwa miongoni mwa madhalimu.





وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يُرِدْكَ بِخَيْرٍ فَلَا رَادَّ لِفَضْلِهِ ۚ يُصِيبُ بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۚوَهُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿١٠٧﴾

Na Allaah Akikugusisha dhara, basi hakuna wa kuiondosha isipokuwa Yeye. Na Akikutakia kheri, basi hakuna wa kurudisha fadhila Zake, Anasababisha kumfikia kwayo (fadhila Yake) Amtakaye katika waja Wake. Naye ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Yuwnus: 106-107]





Na maharamsho mengineyo mengi yanapatikana katika Qur-aan:



إِنَّ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ عِبَادٌ أَمْثَالُكُمْ ۖ فَادْعُوهُمْ فَلْيَسْتَجِيبُوا لَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿١٩٤﴾

Hakika wale mnaowaomba badala ya Allaah ni waja kama nyinyi. Hebu waiteni wakuitikieni ikiwa nyinyi ni wakweli. [Al-A’raaf: 194]





Wale ambao wanaombwa, hawawezi kujiondoshea wenyewe madhara wala kujinufaisha Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِهِ فَلَا يَمْلِكُونَ كَشْفَ الضُّرِّ عَنكُمْ وَلَا تَحْوِيلًا ﴿٥٦﴾

Sema: “Iteni wale ambao mnadai (ni waabudiwa) pasi Naye, basi hawamiliki kukuondesheeni dhara na wala kuihamisha (kwa mwengine).” [Al-Israa: 56]





Na Anasema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ ۖ لَا يَمْلِكُونَ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَمَا لَهُمْ فِيهِمَا مِن شِرْكٍ وَمَا لَهُ مِنْهُم مِّن ظَهِيرٍ ﴿٢٢﴾

Sema: “Ombeni wale mnaodai kwa dhana (ni waabudiwa) badala ya Allaah, hawamiliki hata uzito wa sisimizi mbinguni wala ardhini, na wala hawana humo ushirika Naye, na wala Yeye (Allaah) Hana msaidizi miongoni mwao.” [Sabaa: 22]





Hakuna anachokipata yule ambaye anamshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) isipokuwa ni khasara duniani na Aakhirah na kujiweka katika upotofu:



وَمِنَ النَّاسِ مَن يَعْبُدُ اللَّـهَ عَلَىٰ حَرْفٍ ۖ فَإِنْ أَصَابَهُ خَيْرٌ اطْمَأَنَّ بِهِ ۖ وَإِنْ أَصَابَتْهُ فِتْنَةٌ انقَلَبَ عَلَىٰ وَجْهِهِ خَسِرَ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةَ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْخُسْرَانُ الْمُبِينُ ﴿١١﴾

Na miongoni mwa watu yuko anayemwabudu Allaah ukingoni. Inapompata kheri, hutumainika kwayo; Na inapompata mtihani hugeuka nyuma juu ya uso wake (kurudia kufru). Amekhasirika duniani na Aakhirah. Hiyo ndiyo khasara bayana.





يَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُ وَمَا لَا يَنفَعُهُ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الضَّلَالُ الْبَعِيدُ ﴿١٢﴾

Humwomba badala ya Allaah ambavyo visivyomdhuru na wala visivyomnufaisha. Huo ndio upotofu wa mbali.



يَدْعُو لَمَن ضَرُّهُ أَقْرَبُ مِن نَّفْعِهِ ۚ لَبِئْسَ الْمَوْلَىٰ وَلَبِئْسَ الْعَشِيرُ ﴿١٣﴾

Humwomba yule ambaye dhara yake iko karibu kuliko manufaa yake. Bila shaka ni mlinzi muovu kabisa, na bila shaka ni rafiki muovu kabisa. [Al-Hajj: 11-13]





Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّن يَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَن لَّا يَسْتَجِيبُ لَهُ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ وَهُمْ عَن دُعَائِهِمْ غَافِلُونَ﴿٥﴾

“Na nani aliyepotoka zaidi kuliko ambaye anayeomba asiyekuwa Allaah ambaye hamuitikii mpaka Siku ya Qiyaamah; nao wala hawatambui maombi yao.” [Al-Ahqaaf: 5]







Pia, maharamisho kadhaa katika Sunnah za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yameshatangulizwa katika silsilah za maudhui hii ya “Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!”
 
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم



Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!



19 - Istighaathah (Kuomba Uokozi) Kwa Asiyekuwa Allaah

Alhidaaya.com











Maana Ya Istighaathah na dalili zake:



Istighaathah maana yake ni kuomba uokozi kwa ambaye ataweza kuokoa kutokana na hali ya shida, dhiki na kukaribia kudhurika au kuangamia. Na istighaathah kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) inajumuisha kujidhalilisha Kwake na kuitakidi kwamba hakuna mwengine atakayeweza kuokoa isipokuwa Yeye, kama vile hali ilivyokuwa katika vita vya Badr, Ibn Kathiyr amesema:





"Ilipokuwa siku ya Badr na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaona uchache wa Maswahaba wake na wingi wa adui zake, wakawa katika shida na khofu, akaelekea Qiblah na kuomba uokovu na akaendelea kumuomba Mola wake mpaka joho lake likamuanguka begani mwake, Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Akateremsha:



إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَاسْتَجَابَ لَكُمْ

Na pindi mlipomuomba uokovu Rabb wenu Naye Akakuitikieni [Al-Anfaal: 9] [mpaka mwisho wa Aayah 13 Suwrat Al-Anfaal]





Kuomba uokovu kwa bin-Aadam kwa jambo ambalo limo katika uwezo wake inafaa kwa dalili kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuhusu kisa cha Nabiy Muwsaa (‘Alayhis-Salaam):



وَدَخَلَ الْمَدِينَةَ عَلَىٰ حِينِ غَفْلَةٍ مِّنْ أَهْلِهَا فَوَجَدَ فِيهَا رَجُلَيْنِ يَقْتَتِلَانِ هَـٰذَا مِن شِيعَتِهِ وَهَـٰذَا مِنْ عَدُوِّهِ ۖ فَاسْتَغَاثَهُ الَّذِي مِن شِيعَتِهِ عَلَى الَّذِي مِنْ عَدُوِّهِ

Na akaingia mjini wakati watu wake wako katika mighafiliko, akakuta humo watu wawili wanapigana; mmoja ni miongoni mwa kundi lake, na mwengine miongoni mwa adui wake. Akamsaidia kumuokoa yule ambaye katika kundi lake dhidi ya yule ambaye ni katika adui wake… [Al-Qaswasw: 15]



Pia, mtu anaweza kuomba uokovu kwa mwenziwe amuokoe kutokana na adui zake katika hali ya vita n.k. Au mfano mtu anapokuwa katika hali ya kukaribia kuzama baharini akaita: “Ee ndugu! Nazama niokoe!”



Ama kuomba uokovu kwa jambo ambalo halimo katika uwezo wa bin-Aadam, hapo huwa ni shirki. Mfano mtu kumuomba mwenziwe:



“Ee fulani! Nisaidie kuniokoa na Moto wa Jahannam na niingize Jannah!”



“Ee Fulani! Nisaidie kuniokoa katika upotofu unijaalie hidaaya!”



Au kuomba walio kaburini:



“Ee walii wangu, au shekhe wangu!



Au sharifu fulani! Nisaidie kuniokoka na adhabu za kaburi! Nisaidie kuniokoa katika maradhi niliyo nayo!”



Kadhaalika, kuomba uokovu kwa mazimwi, mashaytwaan n.k. kuitakidi kuwa wao wana uwezo wa kuokoa katika hali ambazo hakuna mwenye uwezo isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).



Vilevile kuomba uokovu kwa kumchanganya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihu wa sallam) kwa mfano: kusema "Ee Allaah niokoe mie katika hizi dhiki kwa baraka Zako na baraka za Rasuli Wako."



Hivyo ni shirki kubwa na inamtoa mtu nje ya Uislamu.



Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwamba hao wanaoombwa uokovu n.k. hawawezi wenyewe kujinusuru nafsi zao humo walimo makaburini wala Siku ya Qiyaamah hawatokuwa na uwezo wowote ule!

يَوْمَ لَا يُغْنِي مَوْلًى عَن مَّوْلًى شَيْئًا وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ﴿٤١﴾

Siku ambayo jamaa wa karibu hatomfaa jamaa wa karibu chochote, na wala wao hawatonusuriwa. [Ad-Dukhaan: 41]



Hata Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa na uwezo wa kumuokoa mtu kwa dalili kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema katika Aayah kadhaa kwamba yule Ambaye Ameshamhukumu kuwa ni mpotofu, basi hakuna wa kumhidi:



مَن يَهْدِ اللَّـهُ فَهُوَ الْمُهْتَدِ ۖ وَمَن يُضْلِلْ فَلَن تَجِدَ لَهُ وَلِيًّا مُّرْشِدًا ﴿١٧﴾

Ambaye Allaah Amemwongoza, basi yeye ndiye aliyehidika. Na Anayemwacha kupotoka basi hutompatia mlinzi wa kumuongoza. [Al-Kahf: 17]



Au ambaye Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amemhukumu kuwa ni mtu wa Motoni, basi hakuna wa kumuokoka, Akamwambia Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



أَفَمَنْ حَقَّ عَلَيْهِ كَلِمَةُ الْعَذَابِ أَفَأَنتَ تُنقِذُ مَن فِي النَّارِ ﴿١٩﴾

Je, yule iliyemthibitikia neno la adhabu je, basi wewe utaweza kumuokoa aliyemo katika moto? [Az-Zumar: 19]





Alikuweko mnafiki mmoja akiwaudhi Waumini ikahadithiwa:



عن عُبَادَةَ بْنَ الصَّامِتِ (رضي الله عنه) قال: خَرَجَ عَلَيْنَا رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَقَالَ أَبُو بَكْرٍ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ): قُومُوا نَسْتَغِيثُ بِرَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) مِنْ هَذَا الْمُنَافِقِ. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ: ((أنه لاَ يُسْتَغَاث بِي، وَإِنَّمَا يُسْتَغَاثُ باِلله))

Kutoka kwa ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitujia kisha Abu Bakr akasema: Simameni tutake msaada kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) atuokoe na mnafiki huyu. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Hakika haipasi kuombwa uokovu kwangu, bali inapaswa kuombwa uokovu kwa Allaah)) [At-Twabaraaniy fiy Mu’jamil–Kabiyr]



Pia Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba ilipoteremshwa kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ ﴿٢١٤﴾

Na onya (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) jamaa zako wa karibu. [Ash-Shu’araa: 214]





دَعَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قُرَيْشًا فَاجْتَمَعُوا فَعَمَّ وَخَصَّ فَقَالَ: ((يَا بَنِي كَعْبِ بْنِ لُؤَيٍّ، أَنْقِذُوا أَنْفُسَكُمْ مِنْ النَّارِ، يَا بَنِي مُرَّةَ بنِ كَعْبٍ أَنْقِذُوا أَنْفُسَكُمْ مِنْ النَّارِ، يَا بَنِي عَبْدِ شَمْسٍ أَنْقِذُوا أَنْفُسَكُمْ مِنْ النَّارِ،يَا بَنِي عَبْدِ مَنَافٍ أَنْقِذُوا أَنْفُسَكُمْ مِنْ النَّارِ، يَا بَنِي هَاشِمٍ أَنْقِذُوا أَنْفُسَكُمْ مِنْ النَّارِ ، يَا بَنِي عَبْدِ الْمُطَّلِبِ أَنْقِذُوا أَنْفُسَكُمْ مِنْ النَّارِ، يَا فَاطِمَةُ أَنْقِذِي نَفْسَكِ مِنْ النَّارِ، فَإِنِّي لَا أَمْلِكُ لَكُمْ مِنْ اللَّهِ شَيْئًا غَيْرَ أَنَّ لَكُمْ رَحِمًا سَأَبُلُّهَا بِبَلَالِهَا))

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaita Maquraysh akawaonya kwa ujumla kisha makhsusi (kwa kabila fulani) akasema: ((Ee Baniy Ka’ab bin Luayy, okoeni nafsi zenu kutokana na Moto! Ee Baniy Murrah bin Ka’b, okoeni nafsi zenu kutokana na Moto! Ee Baniy ‘Abdi Shams, okoeni nafsi zenu kutokana na Moto. Ee Baniy ‘Abdi Manaaf, okoeni nafsi zenu kutokana na Moto.” Ee Baniy Haashim, okoeni nafsi zenu kutokana na Moto.” Ee Baniy ‘Abdil-Muttwalib, okoeni nafsi zenu kutokana na Moto.” Yaa Faatwimah, okoa nafsi yako kutokana na Moto! Kwani hakika mimi similiki uwezo wowote kwenu isipokuwa nitaendelea kuweka uhusiano wetu wa damu.)) [Muslim]



Anatahadharisha pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika kauli Zake mbali mbali:



وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَكُمْ وَلَا أَنفُسَهُمْ يَنصُرُونَ﴿١٩٧﴾

Na wale mnaowaomba (na kuwaabudu) badala ya Allaah hawawezi kuwanusuru na wala hawawezi kujinusuru nafsi zao. [Al-A’raaf: 197]



Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



أَمْ لَهُمْ آلِهَةٌ تَمْنَعُهُم مِّن دُونِنَا ۚ لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَ أَنفُسِهِمْ وَلَا هُم مِّنَّا يُصْحَبُونَ ﴿٤٣﴾

Je, kwani wana waabudiwa wanaoweza kuwakinga Nasi? Hawawezi kujinusuru nafsi zao na wala hawatolindwa Nasi. [Al-Anbiyaa: 43]



Na pia Anasema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَاتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ آلِهَةً لَّعَلَّهُمْ يُنصَرُونَ ﴿٧٤﴾

Na wamejichukulia badala ya Allaah waabudiwa ili wakitumaini kuwa watawanusuru!



لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَهُمْ وَهُمْ لَهُمْ جُندٌ مُّحْضَرُونَ ﴿٧٥﴾

Hawawezi kuwanusuru, na watahudhurishwa (adhabuni) kama askari dhidi ya hao (waliowaabudu). [Yaasiyn: 74-75]
 
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم



Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!



20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah




Alhidaaya.com











Isti’aadhah maana yake ni kuomba kujikinga kuepukana na shari. Na Isti’aadhah kwa Allaah ni kuomba kujikinga Kwake (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na kuitakidi kuwa unabakia katika hifdhi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na inapasa kujidhalilisha Kwake na kumtegemea Yeye Pekee kuwa Ndiye Atakayekukinga na shari zinazokusudiwa kujikinga nazo.



Ibnul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Tambua kwamba tamshi la عاذ na yanayohusiana katika Swarf (sarufi) inamaanisha kujihifadhi na kinga na kuokoka. Na hakika maana yake ni kukimbia kitu unachokiogopa kwa ambaye atakayekuepusha nacho. Na ndio maana ikaitwa Isti’aadhah kwake kama ilivyo maana ya kimbilio.” [Badaa’i Al-Fawaaid (2426)].



Isti’aadhah inaweza kuwa kwa kutaja Jina Lake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kama Anavyosema:



وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ﴿٣٦﴾

Na utakapokuchochea uchochezi kutoka kwa shaytwaan, basi omba kinga kwa Allaah. Hakika Yeye Ndiye Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote. [Fusw-Swilat: 36]





Kujikinga na shaytwaan ni kwa sababu shaytwaan ni adui mkubwa kabisa kwa bin-Aadam, inahitajika kujikinga naye katika kila hali kwa sababu ya ahadi yake ya kuazimia kuwapotosha wanaadamu. Ndio maana Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anaamrisha kujikinga naye pale anapoanza kuchochea.



Na katika hali ya kusoma Qur-aan pia inahitajika zaidi kujikinga naye. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ameamrisha:



فَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ﴿٩٨﴾

Unaposoma kusoma Qur-aan basi (kwanza) omba kinga kwa Allaah dhidi ya shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa. [An-Nahl: 98]





Na katika Swalaah inatakiwa kuomba kinga kutokana na shaytwaan kwa pindi anaposhawishi katika Swalaah kwa kusema:

أَعُوذُ بِاللَّه مِنْ شَرِّ خَنْزَبْ

A’uwudhu biLLaahi min sharri khanzab



kama maelezo yalivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:



عن عُثْمَانَ بْن أَبِي الْعَاصِ رضي الله عنه أنه أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّ الشَّيْطَانَ قَدْ حَالَ بَيْنِي وَبَيْنَ صَلَاتِي وَقِرَاءَتِي يَلْبِسُهَا عَلَيَّ: فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((ذَاكَ شَيْطَانٌ يُقَالُ لَهُ خَنْزَبٌ، فَإِذَا أَحْسَسْتَهُ فَتَعَوَّذْ بِاللَّهِ مِنْهُ وَاتْفِلْ عَلَى يَسَارِكَ ثَلَاثًا)) قَالَ: فَفَعَلْتُ ذَلِكَ فَأَذْهَبَهُ اللَّهُ عَنِّي .

‘Uthmaan bin Abiy Al-‘Aasw (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba alikwenda kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Hakika shaytwaan kanijia baina yangu na Swalaah yangu na kisomo changu akinivaa. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema ((Huyo ni shaytwaan anayeitwa Khanzab, basi ukimhisi jikinge naye kwa Allaah, na tema mate upande wa kushoto kwako mara tatu)). Akasema: Nikafanya hivyo basi akaniondoka shaytwaan. [Muslim]



Isti’aadhah pia inawezekana kwa kutaja ‘Rabb’ kwa dalili ya Suwrah mbili katika Qur-aan zinajulikana kama ni Al-Mu‘awwidhataan (mbili za kujikinga)



قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ ﴿١﴾

Sema: “Najikinga na Rabb wa mapambazuko. [Al-Falaq: 1] mpaka mwisho wake na



قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ﴿١﴾

Sema: “Najikinga na Rabb wa watu. [An-Naas: 1] mpaka mwisho wake.



Na isti’aadhah inafaa pia kwa kutumia Sifa Zake na Utukufu Wake. Ilipoteremka Aayah:



قُلْ هُوَ الْقَادِرُ عَلَىٰ أَن يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عَذَابًا مِّن فَوْقِكُمْ أَوْ مِن تَحْتِ أَرْجُلِكُمْ

Sema: “Yeye ni Muweza wa kukuleteeni adhabu kutoka juu yenu, au kutoka chini ya miguu yenu, [Al-An’aam: 65]





Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliomba kinga akasema:



أَعُوذُ بِوَجْهِكُ

Najikinga kwa Wajihi Wako [Hadiyth kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesimulia Al-Bukhaariy]



Na pia kwa kuunganisha Jina Lake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) pamoja Sifa Zake kama ilivyothibiti katika kinga ya pale mtu anapopata maumivu akashika sehemu inayopatikana maumivu akasema:



أَعُوذُ بِاللَّهِ وَقُدْرَتِهِ مِنْ شَرِّ مَا أَجِدُ وَأُحَاذِرُ

A’uwdhu biLLaahi wa-Qudratihi min sharri maa ajidu wa uhaadhiru



Najikinga kwa Allaah na kwa Uwezo Wake kutokana na shari ya ninachokisikia na ninachokiogopa)) [Muslim, Ibn Maajah na wengineo kwa usimulizi tofauti kidogo]



Pia Isti’aadhah kwa kutumia Maneno Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa dalili:



أَعُوْذُ بِكَلِماتِ اللَّهِ التَّامَّتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ

A’uwdhu bi-Kalimaati-LLaahit-ttaammati min sharri maa khalaq (mara 3 jioni na asubuhi)



Najikinga kwa Maneno ya Allaah yaliyotimia kutokana na shari Aliyoiumba [Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ameisimulia Ahmad (2/290), An-Nasaaiy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah [590], Ibn As-Sunniy [68]. Taz. Swahiyh At-Tirmidhiy (3/187), Swahiyh Ibn Maajah (92/266), Tuhfat Al-Akhyaar (Uk. 45) katika Swahiyh Al-Jaami’ [6427] (Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayesema mara tatu jioni hatodhuriwa na mdudu wa sumu usiku huo”]



Pia; Dalili nyingi zipo katika Sunnah kuhusu kuomba kinga za kila aina;



-Kuomba kinga kutokana na adhabu za Allaah za duniani na Aakhirah.



-Kuomba kinga kutokana na adhabu za kaburi, fitnah za Masiyh Ad-Dajjaal na fitna za uhai na fitnah za mauti.



-Kuomba kinga kutokana na Moto wa Jahannam.



-Kuomba kinga kutokana na shari za mashaytwaan na majini.



-Kuomba kinga kutokana na shari za adui.



-Kuomba kinga kutokana na maradhi.



-Kuomba kinga kutokana na upotofu.



-Kuomba kinga kutokana na ufakiri na kufru,.



-Kuomba kinga kutokana na shari za viungo vya mwili, na vitu vinginevyo kadhaa.



-Pia kuomba kinga kutokana na hali kadhaa wa kadhaa. [Rejea Du’aa za Sunnah ya Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam]



Kujikinga kupitia kwa bin-Aadam inaruhusika pale inapokuwa jambo ambalo analoombwa kukinga ni katika uwezo wake kwa dalili:





عَنْ جَابِرٍ أَنَّ امْرَأَةً مِنْ بَنِي مَخْزُومٍ سَرَقَتْ فَأُتِيَ بِهَا النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَعَاذَتْ بِأُمِّ سَلَمَةَ زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((وَاللَّهِ لَوْ كَانَتْ فَاطِمَةُ لَقَطَعْتُ)) يَدَهَا فَقُطِعَتْ

Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba mwanamke mmoja katika Baniy Makhzuwm aliiba akaletwa kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akajikinga kwa Ummu Salamah ambaye ni mke wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Wa-Allaahi angekuwa ni Faatwimah (aliyeiba) ningelimkata mkono wake)) Ukakatwa mkono wake. [Muslim]



Pia kujikinga katika mahali kadhaa:



عَنْ أبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((سَتَكُونُ فِتَنٌ الْقَاعِدُ فِيهَا خَيْرٌ مِنَ الْقَائِمِ، وَالْقَائِمُ خَيْرٌ مِنَ الْمَاشِي، وَالْمَاشِي فِيهَا خَيْرٌ مِنَ السَّاعِي، مَنْ تَشَرَّفَ لَهَا تَسْتَشْرِفْهُ، فَمَنْ وَجَدَ مَلْجَأً أَوْ مَعَاذًا فَلْيَعُذْ بِهِ))‏.‏

Abuu Huraryah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kutatokea fitnah ambayo mtu aliyekaa kitako atakuwa bora kuliko yule aliyesimama, na aliyesimama atakuwa bora kuliko yule anayetembea, na anayetembea humo atakuwa bora kuliko anayekimbia. Atakayajitokeza kuingia katika fitnah hizi basi zitamuangamiza. Kwa hiyo yeyote atakayepata mahali pa kujikinga au kimbilio basi ajikinge kwayo)) [Al-Bukhaariy]



Na pia:



عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ ابْنِ الْقِبْطِيَّةِ، قَالَ دَخَلَ الْحَارِثُ بْنُ أَبِي رَبِيعَةَ وَعَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَفْوَانَ وَأَنَا مَعَهُمَا، عَلَى أُمِّ سَلَمَةَ أُمِّ الْمُؤْمِنِينَ فَسَأَلاَهَا عَنِ الْجَيْشِ الَّذِي يُخْسَفُ بِهِ وَكَانَ ذَلِكَ فِي أَيَّامِ ابْنِ الزُّبَيْرِ فَقَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((يَعُوذُ عَائِذٌ بِالْبَيْتِ فَيُبْعَثُ إِلَيْهِ بَعْثٌ فَإِذَا كَانُوا بِبَيْدَاءَ مِنَ الأَرْضِ خُسِفَ بِهِمْ))‏ ‏ فَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ فَكَيْفَ بِمَنْ كَانَ كَارِهًا؟ قَالَ: ((يُخْسَفُ بِهِ مَعَهُمْ وَلَكِنَّهُ يُبْعَثُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَى نِيَّتِهِ)) ‏ وَقَالَ أَبُو جَعْفَرٍ هِيَ بَيْدَاءُ الْمَدِينَةِ

‘Ubaydu-Allaah bin Al-Qitwbiyyah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Haarith bin Abiy Rabiy’ah na ‘Abdullaah bin Abiy Swafwaan pamoja nami tulikwenda kwa Mama wa Waumini Ummu Salamah wakamuuliza kuhusu jeshi ambalo litadidimizwa ardhini, na hii ni pale wakati ambapo Ibn Zubayr (alipokuwa gavana wa Makkah). Akahadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: ((Atatafuta mtu kinga katika Nyumba Tukufu kisha jeshi litatumwa kwake (ili wamuue) basi litakapoingia ardhi kame iliyohamwa (jangwa) litadidimizwa)) Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Je itakuwaje kwa ambaye amelazimishwa hayo? Akasema: ((Atatadimizwa nao lakini atafufuliwa Siku ya Qiyaamah katika hali ya niyyah yake)) Abu Ja’far amesema: Ardhi kame ni Madiynah. [Muslim]



Ama kujikinga kinyume na vile ilivyothibiti katika shariy’ah kwa kuomba kinga kwa mambo ambayo hakuna mwenye uwezo nayo isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) huwa ni shirki, kama vile walivyofanya washirikina walipokuwa wakijikinga kwa majini Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَأَنَّهُ كَانَ رِجَالٌ مِّنَ الْإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٍ مِّنَ الْجِنِّ فَزَادُوهُمْ رَهَقًا﴿٦﴾

“Na kwamba walikuwa wanaume miongoni mwa wana Aadam wanajikinga na wanaume miongoni mwa majini, basi wakawazidishia madhambi, uvukaji mipaka ya kuasi na khofu.” [Al-Jinn: 6]





Makosa yafanywayo na Waislamu wa sasa katika kujikinga kwa asiyekuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kufuata mila mfano;



-Baadhi ya watu wanaojikinga katika kufunga ndoa kwa kumwaga damu ya mbuzi na kuikanyaga.



-Kuna wanaojikinga dhidi ya jicho baya au husda kwa kuvunja mayai kwenye hicho kitu alichonunua mtu kama vile gari mpya.



-Kuna wanaojikinga kwa mayatima kwa kuwafadhili kwa chakula kuitakidi kuwa du’aa yao inawatosheleza kujikinga.



-Kuna wanaojikinga na mashaytwaan wanapohamia nyumba mpya kwa kuchinja mbuzi au mialiko ya watu kusoma kisomo.





Kinga hizo zote hazijuzu bali mtu Muislamu anapaswa kutumia kinga zilizothibiti katika mafundisho Swahiyh aliyokuja nayo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Mfano katika kuhamia nyumba mafunzo Swahiyh ni:



عن خَوْلَةَ بِنْت الحَكِيمِ قالت: سمعت رَسُولِ الله -صلى الله عليه وسلم -يقَولَ: ((مَنْ نَزَلَ مَنْزِلاً فقَالَ أَعُوذُ بِكلِمَاتِ الله التّامّاتِ مِن شَرّ مَا خَلَقَ لَمْ يَضُرّهُ شيءٌ حَتّى يَرْحَلَ مِنْ مَنْزِلِهِ ذَلِكَ))

Khawlat bint Hakiym amehadithia kwamba kamsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Atakayeteremka katika kituo (au makazi) kisha akasema: “A’uwdhu bi-Kalimaatil-LLaahit-taammati min sharri maa Khalaq - Najilinda kwa Maneno ya Allaah yaliyotimia na shari Alichokiumba” hakuna kitakachomdhuru hadi atakapoondoka katika kituo (au makazi) hicho)) [Muslim]
 
UJUMBE WA LEO

Ewe mja wa Allah tubu toba ya kweli na mrudie Allah ili uwe na mwisho mwema
 
Mawaidha ya Kumcha Allah (Taqwa):

Kumcha Allah ni msingi wa maisha ya Muislamu. Ni hali ya kumtii Allah kwa mapenzi na kumuogopa kwa heshima, kwa kutekeleza amri Zake na kuacha makatazo Yake.

📖 Aya za Qur’an:
"Enyi mlioamini! Mcheni Allah kama inavyostahili kumcha..." (Qur'an 3:102)
"Na atakayemcha Allah, Atamfungulia njia, na Atamruzuku kutoka asikotarajia..." (Qur'an 65:2-3)

🧠 Faida za Kumcha Allah:
1. Huongoza maamuzi bora.
2. Huleta rehema na msamaha wa Allah.
3. Huweka amani moyoni na hofu ya kweli kwa Mwenyezi Mungu.
4. Hulinda na dhambi, hata ukiwa peke yako.

🛡️ Namna ya Kuishi Kwa Taqwa:
  • Fanya ibada kwa ikhlasi (kuswali, kufunga, kutoa zakat).
  • Jizuie na maneno au vitendo vya dhambi.
  • Kusamehe, kuwa mnyenyekevu, na mkweli.
  • Kumbuka Allah mara kwa mara (dhikr na Qur’an).

Nukuu ya hekima:
"Mtu mwenye taqwa hata akiteleza, hurudi haraka kwa Allah kwa toba."

Dua:
“Ya Allah, tujaalie moyo wa kukucha, maneno ya haki, na maisha yanayokuridhisha. Ameen.”
 
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم



Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!



21-Kutabiria Ya Ghayb Ya Khayr Au Shari, Nuksi, Unajimu Na Kutazamia Kwa Mtabiri

Alhidaaya.com







Kubashiria mambo ya ghayb ni katika ujuzi wa ghayb ambayo hakuna mwenye ujuzi nayo isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kama Anavyosema Mwenyewe (‘Azza wa Jalla):





قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّـهُ ۚ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ ﴿٦٥﴾

Sema: “Hakuna aliyoko katika mbingu na ardhi ajuaye ghayb isipokuwa Allaah. Na wala hawatambui lini watafufuliwa.” [An-Naml: 65]





Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ

Na Kwake (Allaah) zipo funguo za ghayb; hakuna azijuaye ila Yeye tu [Al-An’aam: 59]



Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



إِنَّ اللَّـهَ عِندَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَيُنَزِّلُ الْغَيْثَ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْأَرْحَامِ ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ ﴿٣٤﴾

Hakika Allaah Ana elimu ya Saa (Qiyaamah), na Anateremsha mvua na Anajua yale yaliyomo katika tumbo la uzazi na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho, na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani, hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika [Luqmaan: 34]





Na kutabiria au kubashiria ya ghayb ni miongoni mwa shirki kubwa inayomtoa mtu nje ya Uislaam kwa dalili, kauli za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، عَنْ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((مَنْ أَتَى كَاهِنًا، أَوْ عَرَّافًا، فَصَدَّقَهُ بِمَا يَقُولُ، فَقَدْ كَفَرَ بِمَا أُنْزِلَ عَلَى مُحَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم ))

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayemwendea kahini au mpigaji ramli akamuamini asemayo, basi atakuwa ameshakufuru yale aliyoteremshiwa nayo Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).” [Ahmad, na Aswhaabus-Sunan wanne, na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Targhiyb wat-Tarhiyb (3047)]



Na kwa dalili pia kuwa Swalaah hazikubalikiwi siku arubaini!



مَنْ أَتَى عَرَّافًا فَسَأَلَهُ عَنْ شَيْءٍ لَمْ تُقْبَلْ لَهُ صَلَاةٌ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً

((Atakayekwenda kwa mtabiri akamuuliza kitu haitokubaliwa Swalaah yake siku arubaini)) [Muslim]



Basi jiulize ndugu Muislaam unayemshirikisha Allaah! Je, itakuwaje pindi akikufikia Malak-Al-Mawt (Malaika wa kufisha) akakutoa roho yako kipindi hicho wakati uko nje ya Uislaam?



Mifano ya njia zinazotabiriwa:



1- Kwenda kwa mtabiri:





Mtabiri hutazamia kwa mikono na kumbashiria mtu mazuri yatakayomfika siku za mbele au mabaya yatakayomsibu mtu. Hutazamia ima kwa vikombe baada ya huyo mtu anayetazamiwa kunywa chai au kahawa ikabakishwa kidogo, basi huzungushwa kikombe chake cha chai au kahawa kisha hutabiriwa ya khayr au shari kumfikia. Au hutabiri kwa kuandika nambari katika vikaratasi, kwa nyota, au kutazamwa viganja vya mikono n.k.



2- Kutazamia kwa unajimu na kutangazwa kwenye magazeti na majarida (horoscope):



Pia, kuna wanaotabiri kwa njia ya unajimu (kutazamia nyota) kuhusiana na mwezi aliozaliwa mtu inayojulikana kama 'horoscope'. Unajimu huu hutiwa magazetini na watu husoma kila mara kutabiri bahati zao au shari zitakazowasibu katika siku fulani. Wanadai kuwa sayari kama gemini, taurus, aries n.k. zinahusiana na mwezi wa mtu aliozaliwa na hivyo basi waliozaliwa katika sayari hizo siku hiyo kwao huwaathiri nafsi zao na kadhaa wa kadhaa.



Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameharamisha unajimu:



عن عبد الله بن عباس (رضي الله عنهما) عن النبي (صلى الله عليه وسلم): ((من اقتبس شعبةً من النجومِ فقد اقتبس شعبةً من السحرِ زاد ما زاد))

Amehadithia ‘Abdullaah bin ‘Abaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayejichumia tawi katika ujuzi wa unajimu, atakuwa amejichumia tawi katika sihri, na itaendelea kuzidi na kuzidi.” [Abuu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh]





3- Kutabiri khayr au shari au nuksi kutokana na matukio fulani:



Ni mambo yanayotabiriwa na watu katika jamii za Kiislamu na kuyaitakidi kwamba ni mambo yatakayomtokea mtu. Mambo hayo huwa ima ya khayr au shari, au nuksi, mkosi, ukorofi n.k. Na hakika itikadi hizi miongoni mwa Waislaam zimekuwa kama ni jambo la kawaida na ilhali ni jambo la khatari kabisa kwa kuwa ni miongoni mwa shirki kubwa ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Hamghufurii mtu asiporudi kutubia! Yanayotabiriwa yako mengi mno, ila haya yafuatayo ndio ambayo tumejaaliwa kuyajua na kuyanukuu:



a) Akitajwa mtu kisha hapo hapo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akajaalia huyo mtu atokee au asikike kwa simu n.k., basi hubashiriwa kuwa atakuwa na umri mrefu!



b) Jicho likimcheza mtu upande wa kushoto huamini kuwa itamfika shari na ikiwa upande wa kulia huamini kuwa itamfikia khayr! Na wengine husema: “Sharr ba’iyd na khayr qariyb”(shari iwe mbali na khayr iwe karibu).



c) Kusemwa: “Swallu ‘alan-Nabiy!” - inasemwa kwa ajili ya kuondosha jicho baya au husda! Na hutamkwa hivyo katika hali ya kuona jambo zuri, au katika sherehe za harusi kumkinga nayo bi harusi au wenye harusi. Pia kwa ajili ya kunyamazisha mzozano, au anapoona mtu jambo la ajabu n.k. Haya ni mambo ya bid’ah na inaingia katika shirki pia. Vile vile wanawake khaswa kusema kwao katika sherehe: “Aswalaatu was-salaamu ‘alaa habiybinaa Muhammad!” kisha hupigwa vigelegele! Haya pia ni katika bi’dah.



d) Pindi mtu akimuona paka mweusi basi inaitakidiwa kuwa siku hiyo itakuwa ni ya mkosi!



e) Mkono umkimuwasha mtu basi inabashiriwa kuwa kuna kupata pesa!



f) Akifagia mtu usiku basi inatabiriwa kuwa ni kuondosha baraka au kufukuza wageni!



g) Akipaliwa mtu hutabiriwa kuwa “anatajwa!”



h) Ukikata kucha zote pamoja (ya mikono na miguu) inatabiriwa kuwa shida zikija zitakuja zote pamoja!



i) Kushika mbao inaitakidiwa kuwa ni kuepusha hjicho baya na husda! Kwa hiyo unapotaja jambo zuri la kusifia jambo au mtu, itasemwa: “Shika mbao!”



j) Mtoto wa kike akivalishwa kofia ya mwanamume ni itikadi kuwa atakosa mahari!



k) Mtu akipatwa na mtihani basi huambiwa akaoge na avue ile nguo kwani ile nguo ina mkosi na ikitokea kuirejea kuvaa ile nguo basi mtu huyo huwa na mashaka kupata tatizo tena. Hali hiyo hupelekea mtu kutoivaa tena ile nguo kwa kuamini akiivaa tu atapata tena mkosi!



l) Unapofagia ukapitishia ufagio kama kumsogezea taka binti basi ni itikadi kuwa hatoolewa!



m) Mtoto akichetama na kujichungulia 'awrah (sehemu ya siri) yake, basi watu huamini kuwa mama yake atashika ujauzito!



Hizo ni baadhi ya itikadi potofu, za kishirikina na za kijaahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Uislaam) kwa sababu washirikina walikuwa wanapotaka kufanya jambo kama vile kusafiri, walikuwa wanatabiria kwa Tatwayyur; (kubashiria mkosi kwa kumrusha ndege). Hurushwa ndege, basi pindi akiruka kuelekea upande wa kulia basi hubashiria kuwa ni khayr na pindi akiruka ndege huyo kuelekea kushoto, basi hubashiria ya shari na hivyo safari huvunjwa!



Ukaja Uislaam na kuharamisha shirki hiyo katika Qur-aan na Sunnah. Miongoni mwa Hadiyth za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



عن عبد الله بن مسعود قال قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((الطِّيَرَةُ شِركٌ، الطِّيَرَةُ شِركٌ، الطِّيَرَةُ شِركٌ))

Ibn Mas’uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atw-Twiyarah (kutabiri nuksi, mikosi n.k) ni shirki, Atw-Twiyarah ni shirki, Atw-Twiyarah ni shirki.” [Swahiyh At-Targhiyb (3098)]



Atw-Twiyarah: Maana yake ni kutabiria khayr au kinga ya shari na zaidi inatumika kutabiria nuksi.



Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza katika Hadiyth nyengineyo:





عنْ عُرْوَةَ بْنِ عامِرِ (رضي الله عنه) قال: ذُكِرتِ الطَّيَرَةُ عِنْد رَسُولِ اللَّه صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فقَالَ: ((أحْسَنُهَا الْفَألُ، وَلا تَرُدُّ مُسْلِماً، فَإذا رأى أحَدُكُمْ ما يَكْرَه ، فَلْيقُلْ: اللَّهُمَّ لا يَأتى بالحَسَناتِ إلاَّ أنتَ، وَلا يَدْفَعُ السَّيِّئاتِ إلاَّ أنْتَ، وَلا حوْلَ وَلا قُوَّةَ إلاَّ بك))

‘Urwah bin ‘Aamir (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Ilitajwa habari ya kupiga fali mbaya (mkosi) mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Ilio bora zaidi ni kupiga fali nzuri, wala (kupiga fali mbaya) haimrudishi Muislaam (kutokutenda aliloazimia). Mmoja wenu atakapoona analolichukia, aseme: “Allaahumma laa yaa-tiy bil-hasanaat illa Anta, walaa yadfa’us-sayyiaat illa Anta, walaa hawla walaa quwwata illa Bika“ - Ee Allaah, hakuna anayeweza kuleta mambo mema isipokuwa ni Wewe, wala hakuna anayeweza kukinga mabaya isipokuwa ni Wewe. Hakuna uwezo (wa kuepuka kutenda mabaya) wala nguvu (ya kutenda mema) isipokuwa ni Kwako.) [Hadiyth Swahiyh ameipokea Abu Daawuwd kwa isnaad Swahiyh]



Akasema pia: “Hakuna mkosi, na ni bora tegemea khayr (matumaini mema).” Wakauliza nini matumaini mema (matarajio ya kufanikiwa) Yaa Rasuwla-Allaah? Akasema: “Ni neno jema alisikialo mmoja wenu.” [Al-Bukhaariy]



Mas-alah haya ya kubashiria ghayb yanapasa kuzingatiwa kwa kina na kuazimiwa kuwafundisha watu khatari zake, kwa sababu watu wengi hawana ujuzi kuwa ni katika mambo ya kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) wakidhania kuwa ni mambo ya kawaida. Kwa hiyo ni waajib wa kila Muislamu anayesoma makala hizi kufanya juhudi kuwafikisha Waislamu waepukane na shirki hizi.



Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amebainisha jinsi mambo kama haya yanavyomwepesisha mtu kuingia katika kufru:



عَنْ زَيْدِ بْنِ خَالِدٍ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: صَلَّى لَنَا رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) صَلاةَ الصُّبْحِ بِالْحُدَيْبِيَةِ عَلَى إِثْرِ سَمَاءٍ كَانَتْ مِنَ اللَّيْلِ، فَلَمَّا انْصَرَفَ أَقَبْلَ عَلَى النَّاسِ، فَقَالَ ((هَلْ تَدْرُونَ مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ؟)) قَالُوا: اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمَ. قَالَ: ((قَالَ أَصْبَحَ مِنْ عِبَادِي مُؤْمِنٌ بِي وَكَافِرٌ، فَأَمَّا مَنْ قَالَ مُطِرْنَا بِفَضْلِ اللَّهِ وَرَحْمَتِهِ، فَذَلِكَ مُؤْمِنٌ بِي كَافِرٌ بِالْكَوْكَبِ، وَأَمَّا مَنْ قَالَ مُطِرْنَا بِنَوْءِ كَذَا وَكَذَا، فَذَلِكَ كَافِرٌ بِي مُؤْمِنٌ بِالْكَوْكَبِ))

Zayd bin Khaalid (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alituswalisha Swalaah ya asubuhi Hudaybiyah baada ya usiku wa mvua. Alipomaliza akawakabili watu akasema: “Je, mnajua Rabb wenu Amesema nini?” Wakajibu: Allaah na Rasuli Wake ndio wajuao. Akasema: ‘Allaah Amesema: Baadhi ya waja Wangu wameamka leo wakiwa wenye kuniamini, na wengine wamekufuru. Aliyesema kuwa mvua ni kutokana na fadhila na Rahmah za Allaah, basi huyo ni mwenye kuniamini wala haamini nyota. Ama aliyesema: Tumenyeshewa mvua kutokana na nyota fulani, yeye ni mwenye kunikufuru na mwenye kuamini nyota.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
 
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!

22 -Kumtii Kiumbe Katika Kumuasi Allaah

Alhidaaya.com





Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza mtu kumtii kiumbe yeyote katika kumuasi Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa dalili ya Hadiyth ifuatayo:



لاَ طَاعَةَ في مَعْصِيَةِ الله ، إِنَّمَا الطَّاعَةُ فِي المَعْرُوفِ

Hakuna kutii katika kumuasi Allaah, bali utiifu ni katika yanayokubalika ki-shariy’ah katika mema.[Al-Bukhaariy na Muslim]



Muislamu anapaswa atii amri kwa anayepasa kumuamrisha hata kama ni jambo analolichukia madamu tu haliko katika kumuasi Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kama alivyoamrisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



عَلَى الْمَرْءِ الْمُسْلِمِ السَّمْعُ وَالطَّاعَةُ فِيمَا أَحَبَّ وَكَرِهَ إِلَّا أَنْ يُؤْمَرَ بِمَعْصِيَةٍ فَإِنْ أُمِرَ بِمَعْصِيَةٍ فَلَا سَمْعَ وَلَا طَاعَةَ

“Muislamu anapaswa kusikia na kutii kwa anayoyapenda na anayoyachukia, madhali hakuamrishwa kuasi. Na pindi akiamrishwa katika maasi, basi hakuna kusikia wala kutii.” [Al-Bukhaariy na Muslim





Mfano wa katika yasiyokubalika katika ki-shariy’ah ni kama usimulizi wa Hadiyth ifuatayo ambako kiongozi alitaka kuwaangamiza Waislamu katika moto:



عَنْ عَلِيٍّ، قَالَ: بَعَثَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سَرِيَّةً، وَاسْتَعْمَلَ عَلَيْهِمْ رَجُلًا مِنَ الْأَنْصَارِ وَأَمَرَهُمْ أَنْ يَسْمَعُوا لَهُ وَيُطِيعُوا، فَأَغْضَبُوهُ فِي شَيْءٍ، فَقَالَ: اجْمَعُوا لِي حَطَبًا، فَجَمَعُوا لَهُ، ثُمَّ قَالَ: أَوْقِدُوا نَارًا، فَأَوْقَدُوا، ثُمَّ قَالَ: أَلَمْ يَأْمُرْكُمْ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ تَسْمَعُوا لِي وَتُطِيعُوا؟ قَالُوا: بَلَى، قَالَ: فَادْخُلُوهَا، قَالَ: فَنَظَرَ بَعْضُهُمْ إِلَى بَعْضٍ، فَقَالُوا: إِنَّمَا فَرَرْنَا إِلَى رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنَ النَّارِ، فَكَانُوا كَذَلِكَ، وَسَكَنَ غَضَبُهُ، وَطُفِئَتِ النَّارُ، فَلَمَّا رَجَعُوا ذَكَرُوا ذَلِكَ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: ((لَوْ دَخَلُوهَا مَا خَرَجُوا مِنْهَا، إِنَّمَا الطَّاعَةُ فِي الْمَعْرُوفِ))

Kutoka kwa ‘Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alituma jeshi chini ya uongozi wa mtu mmoja wa Answaar. Wakamkasirisha kwa sababu ya jambo fulani akawaambia: Kusanyeni kuni. Wakamkusanyia akasema: Niwashieni moto! Wakamuashia. Akasema: Kwani Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakukuamrisheni mnitii? Wakasema: Ndio! Akasema. Basi uingieni! Wakatazamana kisha wakasema: Hakika sisi tumekimbilia kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kujiepusha na moto. Wakawa hivyo hivyo. Kisha ghadhabu zake zikatulia na moto ukazimwa. Waliporudi kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakamwelezea yalivyojiri, hapo yeye akasema: “Mngeliuingia, msingetoka kamwe humo. Hakika utiifu ni katika mema.” [Al-Bukhaariy na Muslim]



Katika ambayo hayapasi utiifu:





1. Kutii katika mambo ya haraam. Maswahaba walimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



عَنْ عَدِيّ بْنِ حَاتِمٍ: أَنَّهُ سَمِعَ اَلنَّبِيَّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقْرَأُ هَذِهِ الآيَةَ: اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ وَالْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا إِلَـٰهًا وَاحِدًا ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚسُبْحَانَهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٣١﴾ فَقُلْتُ لَهُ: إِنَّا لَسْنَا نَعْبُدُهُمْ. قَالَ: ((أَلَيْسَ يُحَرِّمُونَ مَا أَحَلَّ اَللَّهُ فَتُحَرِّمُونَهُ وَيُحِلُّونَ مَا حَرَّمَ اَللَّهُ فَتُحِلُّونَهُ؟)) فَقُلْتُ بَلَى. قَالَ🙁(فَتِلْكَ عِبَادَتُهُم))رَوَاهُ أَحْمَدُ وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَحَسَّنَهُ



Imepokewa toka kwa ‘Adiyy bin Haatim (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisoma Aayah: Wamewafanya Wanachuoni Marabai wao wa dini na Wamonaki wao kuwa ni miola badala ya Allaah, na (pia) Al-Masiyh mwana wa Maryam na hali hawakuamrishwa isipokuwa kumwabudu Ilaah Mmoja Pekee. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye. Utakasifu ni Wake kutokana na yale yote wanayomshirkisha nayo. [At-Tawbah: 31] Nikasema: Hakika sisi hatuwaabudu. Akasema: "Je, kwani hawaharamishi Aliyoyahalalisha Allaah nanyi mkayaharamisha? Na wanahalalisha Aliyoyaharamisha Allaah nanyi mnayahalalisha?" Nikasema: Ndio. Akasema: "Basi hivyo ndivyo kuwaabudu." [Ahmad na At-Tirmidhiy na ameipa daraja ya Hasan]





2. Kuwatii wazazi katika maasi na kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):





Mzazi anapaswa kupewa haki yake kumfanyia ihsaan na wema. Lakini pindi anapomuamrisha mwanawe katika kumshirkisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa njia yoyote ile, au kuamrisha kufuata bid’ah (uzushi) au maasi yoyote yale mengineyo ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wameyakataza, basi haipasi kabisa kumtii mzazi, hapo inapasa mtoto akatae kuwatii, na dalili ni kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حُسْنًا ۖ وَإِن جَاهَدَاكَ لِتُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۚ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٨﴾

Na Tumemuusia insani kuwafanyia wema wazazi wake wawili. Lakini wakikushikilia kuwa Unishirikishe na ambayo huna elimu nayo, basi usiwatii; Kwangu ni marejeo yenu, Nitakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda. [Al-‘Ankabuwt: 8]





Na mifano mingi tunayo katika Siyrah za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu Maswahaba waliokataa kuwatii wazazi wao, mmojawapo ni Sa’d bin Abiy Waqqaasw (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye mama yake alichukia mno yeye kuingia katika Dini ya Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Akamwambia mwanae: “Naapa ima uachane na Dini yako hii mpya au nitajifungia kula na kunywa mpaka nife.” Sa’ad akamwambia: “Ee mama yangu nina mapenzi makubwa kwako kama mama yangu uliyenizaa, lakini mapenzi yangu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na Rasuli Wake ni makubwa zaidi. Wa-Allaahi lau hata roho elfu moja na moja zitaondoka (kwa kunitaka nirudi dini yangu ya zamani) kamwe sitorudia dini yangu.”



3. Kumtii mume au mke katika maasi:



Mifano ya mke kumtii mumewe katika maasi ambayo yanajulikana katika jamii, ni mume kumtaka mke achonge nyusi zake na hali laana ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) inamfikia mwenye kunyofoa au kuchonga nyusi zake.



Pia kumtii mume kutokujistiri kwa vazi la Hijaab.



Pia kumtii mume katika yaliyoharamishwa kama kumtaka jimai mchana wa Swawm ya Ramadhwaan, au kumtaka afanye naye tendo la ndoa wakati wa hedhi, au kumtaka amuingilie katika utupu wake wa nyuma... na mifano iko mingi.



Mfano mzuri tunao katika Qur-aan wa Aasiyah ambaye alikuwa mke wa Fir’awn muasi aliyejifanya kuwa mungu. Aasiyah alikataa kumtii mumewe katika maasi ya kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa sababu alimuamini Allaah. Fir’awn akamuadhibu adhabu kali na kumuua lakini yeye alibakia katika iymaan yake na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anampigia mfano wa wenye kuamini:



وَضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا لِّلَّذِينَ آمَنُوا امْرَأَتَ فِرْعَوْنَ إِذْ قَالَتْ رَبِّ ابْنِ لِي عِندَكَ بَيْتًا فِي الْجَنَّةِ وَنَجِّنِي مِن فِرْعَوْنَ وَعَمَلِهِ وَنَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ﴿١١﴾

Na Allaah Amewapigia mfano wale walioamini; mke wa Fir’awn, aliposema: “Rabb wangu! Nijengee nyuma Kwako kwenye Jannah na niokoe na Fir’awn na vitendo vyake na niokoe na watu madhalimu.” [At-Tahriym: 11]





Siku ya Qiyaamah wanaofanyiana utiifu katika maasi hali itakuwa kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

يَوْمَ تُقَلَّبُ وُجُوهُهُمْ فِي النَّارِ يَقُولُونَ يَا لَيْتَنَا أَطَعْنَا اللَّـهَ وَأَطَعْنَا الرَّسُولَا ﴿٦٦﴾

Siku zitakapopinduliwa nyuso zao motoni, watasema: “Laiti tungelimtii Allaah, na tungelimtii Rasuli.”





وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءَنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا ﴿٦٧﴾

Na watasema: “Rabb wetu! Hakika sisi tumewatii mabwana zetu, na wakuu wetu, basi wametupoteza njia.”





رَبَّنَا آتِهِمْ ضِعْفَيْنِ مِنَ الْعَذَابِ وَالْعَنْهُمْ لَعْنًا كَبِيرًا ﴿٦٨﴾

“Rabb wetu! Wape adhabu maradufu, na walaani laana kubwa.” [Al-Ahzaab: 66-68]





4. Kumtii rafiki kuacha Swalaah na maasi mengineyo:



Kumtii rafiki anayemuamrisha mwenzie aache Swalaah ili wakimbilie katika michezo fulani, mechi za mpira n.k. Au kumtii rafiki katika kusililiza muziki na ngoma, kwenda sehemu zinazotendeka maasi n.k.



Siku ya Qiyaamah rafiki huyo atamkanusha mwenziwe kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَيَوْمَ يَعَضُّ الظَّالِمُ عَلَىٰ يَدَيْهِ يَقُولُ يَا لَيْتَنِي اتَّخَذْتُ مَعَ الرَّسُولِ سَبِيلًا ﴿٢٧﴾

Na siku dhalimu atakapotafuna mikono yake akisema: “Laiti ningeshika njia pamoja na Rasuli.



يَا وَيْلَتَىٰ لَيْتَنِي لَمْ أَتَّخِذْ فُلَانًا خَلِيلًا ﴿٢٨﴾

“Ee ole wangu! Laiti nisingelimfanya fulani kuwa rafiki mwandani.”





لَّقَدْ أَضَلَّنِي عَنِ الذِّكْرِ بَعْدَ إِذْ جَاءَنِي ۗ وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِلْإِنسَانِ خَذُولًا ﴿٢٩﴾

“Kwa yakini amenipoteza mbali na Ukumbusho baada ya kunijia.” Na shaytwaan kwa insani daima ni mwenye kutelekeza. [Al-Furqaan: 27- 29]





Ndugu Muislamu, inapokuwa ni amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ya kujiepusha na maasi basi usimtii yeyote isipokuwa Yeye (‘Azza wa Jalla) na hapo ndipo itakapohakiki iymaan ya mtu kwa dalili ifuatayo ya Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):





عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((ثَلاَثٌ مَنْ كُنَّ فِيهِ وَجَدَ حَلاَوَةَ الإِيمَانِ: أَنْ يَكُونَ اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِمَّا سِوَاهُمَا, وَأَنْ يُحِبَّ الْمَرْءَ لاَ يُحِبُّهُ إِلاَّ لِلَّهِ, وَأَنْ يَكْرَهَ أَنْ يَعُودَ فِي الْكُفْرِ كَمَا يَكْرَهُ أَنْ يُقْذَفَ فِي النَّارِ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mambo matatu atakayekuwa nayo, atapata utamu wa ‘iymaan: Allaah na Rasuli Wake wawe vipenzi zaidi kwake kuliko wengineo, ampende mtu na wala asimpende isipokuwa kwa ajili ya Allaah, na achukie kurudi katika ukafiri baada ya Allaah kumuokoa kutoka huko kama anavyochukia kuingizwa motoni." [Al-Bukhaariy na Muslim]



Hitimisho ni kwamba mtu anapochochewa kutenda maasi basi inamtosheleza kujibu kwa kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ifuatayo:



إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿١٣﴾

“Hakika nikimuasi Rabb wangu, nina khofu adhabu ya Siku adhimu.” [Az-Zumar: 13]
 
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!

23- Sihri (Uchawi) Na Michezo Ya Mazingaombwe

Alhidaaya.com





Neno “As-Sihr” (uchawi) maana yake ni kitendo cha kujikurubisha na shaytwaan na kwa msaada wake (shaytwaan) na uchawi ni kulibadilisha jambo mbali na uhakika wake, nako ni kuwadhihirishia watu jambo lisilo la kweli wakaliona kuwa ni la kweli.” [Lisaan Al-‘Arab]





Na Sihri ni tendo la kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kuwa linahusiana na shaytwaan 'aaswi mwenye kumkufuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Kauli Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَاتَّبَعُوا مَا تَتْلُو الشَّيَاطِينُ عَلَىٰ مُلْكِ سُلَيْمَانَ ۖ وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَانُ وَلَـٰكِنَّ الشَّيَاطِينَ كَفَرُوا يُعَلِّمُونَ النَّاسَ السِّحْرَ وَمَا أُنزِلَ عَلَى الْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَارُوتَ وَمَارُوتَ ۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ ۖفَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِ بَيْنَ الْمَرْءِ وَزَوْجِهِ ۚ وَمَا هُم بِضَارِّينَ بِهِ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ ۚ وَلَقَدْ عَلِمُوا لَمَنِ اشْتَرَاهُ مَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ ۚ وَلَبِئْسَ مَا شَرَوْا بِهِ أَنفُسَهُمْ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿١٠٢﴾

Na wakafuata yale waliyoyasoma mashaytwaan juu ya ufalme wa Sulaymaan; na Sulaymaan hakukufuru lakini mashaytwaan ndio waliokufuru; wanafundisha watu sihiri na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili katika (mji wa) Baabil; Haaruwt na Maaruwt. Nao wawili hawamfundishi yeyote mpaka waseme: “Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru.” Kisha wakajifunza kutoka kwa hao wawili yenye kupelekea kufarikisha kwayo baina ya mtu na mkewe. Na wao hawawezi kamwe kumdhuru yeyote kwayo isipokuwa kwa idhini ya Allaah; na wanajifunza yanayowadhuru na wala hayawanufaishi; na kwa yakini walijua kwamba atakayechuma haya hatopata katika Aakhirah fungu lolote, na ni ubaya ulioje walichojiuzia nafsi zao, lau wangelikuwa wanajua. [Al-Baqarah: 102]





Pia, sihri ni miongoni mwa Al-Kabaair (madhambi makubwa) na ni miongoni mwa ambayo yanamuangamiza mtu kwa dalili ya Hadiyth:



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((اجْتَنِبُوا السَّبْعَ الْمُوبِقَاتِ)) قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ وَمَا هُنَّ؟ قَالَ: ((الشِّرْكُ بِاللَّهِ وَالسِّحْرُ وَقَتْلُ النَّفْسِ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلاَّ بِالْحَقِّ وَأَكْلُ الرِّبَا وَأَكْلُ مَالِ الْيَتِيمِ وَالتَّوَلِّي يَوْمَ الزَّحْفِ وَقَذْفُ الْمُحْصَنَاتِ الْمُؤْمِنَاتِ الْغَافلاَتِ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Jiepusheni na mambo saba yanayoangamiza!)) Wakauliza: Ni yepi hayo yaa Rasuwla Allaah? Akawaambia: ((Ni kumshirikisha Allaah, sihri [uchawi], kuua nafsi Aliyoiharamisha Allaah isipokuwa kwa haki, kula ribaa, kula mali ya yatima, kukimbia wakati wa kupambana na adui na kuwatuhumu uzinifu wanawake Waumini waliohifadhika walioghafilika)). [Al-Bukhaariy na Muslim]





Na sihri ilikuwa ni miongoni mwa shirki za kaumu ya Fir’awn na ndio sababu mojawapo ya kutumwa Nabiy Muwsaa ('Alayhis-Salaam) kuwataka waache. Alipowaonesha miujiza ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) wachawi wa Fir’awn hapo hapo walisujudu kwa kuwa walitambua kuwa sihri ni batili na ni shirki, wakakubali haki na wakajiepusha nayo kama ilivyokuja katika Qur-aan:



قَالَ لَهُم مُّوسَىٰ أَلْقُوا مَا أَنتُم مُّلْقُونَ ﴿٤٣﴾

Muwsaa akawambia: “Tupeni vile mnavyotupa.”





فَأَلْقَوْا حِبَالَهُمْ وَعِصِيَّهُمْ وَقَالُوا بِعِزَّةِ فِرْعَوْنَ إِنَّا لَنَحْنُ الْغَالِبُونَ ﴿٤٤﴾

Wakatupa kamba zao na fimbo zao; na wakasema: “Kwa utukufu wa Fir’awn! Hakika sisi ni wenye kushinda.”





فَأَلْقَىٰ مُوسَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ تَلْقَفُ مَا يَأْفِكُونَ ﴿٤٥﴾

Basi Muwsaa akatupa fimbo yake, tahamaki inameza vyote walivyovizua.





فَأُلْقِيَ السَّحَرَةُ سَاجِدِينَ ﴿٤٦﴾

Basi wale wachawi wakaanguka wakisujudu.



قَالُوا آمَنَّا بِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٤٧﴾

Wakasema: “Tumemwamini Rabb wa walimwengu.



رَبِّ مُوسَىٰ وَهَارُونَ ﴿٤٨﴾

“Rabb wa Muwsaa na Haaruwn.” [Ash-Shu’araa: 43-48]





Na pia katika Suwrah nyengine baada ya wachawi kusujudu wakasilimu wakasema:



إِنَّا آمَنَّا بِرَبِّنَا لِيَغْفِرَ لَنَا خَطَايَانَا وَمَا أَكْرَهْتَنَا عَلَيْهِ مِنَ السِّحْرِ ۗ وَاللَّـهُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ ﴿٧٣﴾

“Hakika sisi tumemwamini Rabb wetu ili Atughufurie madhambi yetu, na yale uliyotushurutisha katika ya sihiri. Na Allaah ni Mbora Zaidi na Mwenye kudumu zaidi.” [Twaahaa: 73]





Fir’awn akatakabari na kukanusha haki akasema:



قَالَ آمَنتُمْ لَهُ قَبْلَ أَنْ آذَنَ لَكُمْ ۖ إِنَّهُ لَكَبِيرُكُمُ الَّذِي عَلَّمَكُمُ السِّحْرَ فَلَسَوْفَ تَعْلَمُونَ ۚ لَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُم مِّنْ خِلَافٍ وَلَأُصَلِّبَنَّكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٤٩﴾

(Fira’wn) Akasema: “Je, mmemwamini kabla sijakupeni idhini? Hakika bila shaka kubwa lenu ndiye amekufunzeni sihiri. Basi mtakuja kujua. Nitakukatenikateni mikono yenu na miguu yenu kinyume (kulia kwa kushoto), kisha nitakusulubuni nyote.” [Ash-Shu’araa: 49]





Lakini wachawi baada ya kuamini wakasema:



قَالُوا لَا ضَيْرَ ۖ إِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ ﴿٥٠﴾

Wakasema: “Hakuna dhara yoyote! Hakika sisi tunarudi kwa Rabb wetu.





إِنَّا نَطْمَعُ أَن يَغْفِرَ لَنَا رَبُّنَا خَطَايَانَا أَن كُنَّا أَوَّلَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٥١﴾

“Hakika sisi tunatumai kwamba Rabb wetu Atatughufuria madhambi yetu kwa vile tumekuwa wa kwanza wenye kuamini.” [Ash-Shu’araa: 49-51]





Kuna aina mbili za uchawi: Kufanya sihri kwa ajili ya kumuathiri mtu na kufanya micheo ya sihri (mazingaombwe).





1- Kufanya sihri kwa ajili ya kumuathiri mtu:





Wachawi hutumia mashaytwaan kushirikiana nao. Hufanya sihiri kwa malengo mbali mbali; kumroga mtu apatwe na masaibu, maafa, au amuue, au afarikiane mke na mume kama ilivyotajwa juu katika Suwratul-Baqarah, au aelekeze mapenzi ya mtu kwa mtu fulani na mengi mengineyo. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameonya:

عن ابي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم: مَنْ عَقَدَ عُقْدَةً ثُمَّ نَفَثَ فِيهَا, فَقَدْ سَحَرَ, وَمَن ْسَحَرَ فَقَدْ أَشْرَكَ, وَمَنْ تَعَلَّقَ شَيْئًا وُكِلَ إِلَيْهِ))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayefunga fundo kisha akalipuliza amefanya uchawi. Na atakayefanya uchawi amefanya shirki, na atakayetundika kitu [talasimu, au kuvaa hirizi, zindiko] basi amejiweka katika ulinzi wa hicho kitu alichokivaa)) [na itamdhalilisha])) [An-Nasaaiy]



Na pia:

مَنْ أَتَى كَاهِنًا أَوْ سَاحِرًا فَصَدَّقَهُ بِمَا يَقُولُ فَقَدْ كَفَر بِمَا أُنْزِلَ عَلى مُحَمَّدٍ صلى الله عليه وسلّم

Atakayemwendea kahini au mchawi akasadiki yale anayoyasema basi amekufuru ambayo Ameteremshiwa nayo Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) [Tafsiyr Ibn Kathiyr; Hadiyth ina isnaad ya upokezi Swahiyh na kuna Hadiyth zinazokubaliana na hii].





Aghlabu ya njia wanazotumia wachawi na jinsi ya kumtambua mchawi:





Huwakamata wale wenye ugonjwa wa ngozi (zeruzeru) na kuwaua na kutumia viungo vyao katika uchawi wao. Hii ni dhulma kubwa mno wanayowafanyia bin Aadamu wenzao! Allaah Awahifadhi bin Aadam hao waliosibiwa na maradhi hayo, jambo ambalo limekuwa ni mtihani kwao kudhulumiwa na wachawi!


Hutamka kauli au maneno ya kufru.


Huandika maneno katika vijikaratasi na kumtaka mtu avivae kama hirizi, au avifukize apate moshi wake, au kutundika vitu mahali fulani kama vile katika miti, au kumtaka mtu atupe vitu baharini, au avifukie ardhini.


Humtaka mtu alete wanyama wenye sifa fulani, au wanyama wenye rangi fulani awachinje bila ya kutaja Jina la Allaah!


Husoma Qur-aan kinyumenyume, au kuikhini Qur-aan kwa kuiweka sehemu zisizopasa.


Huandika maneno ya Qur-aan na mengine ya kufru na kumtaka achemshe vikaratasi hivyo na kunywa maji yake, au hutia zaafarani au rangi kisha humfanyia kombe anywe kwa muda fulani.


Humuuliza mtu jina la mama yake.


Humtaka mtu nguo zake za ndani kwa ajili ya kupata jasho lake.


Humtaka mtu ajitenge na watu abakie katika chumba cha kiza na aepukane na jua kwa muda wa masiku.


Humtaka mtu asioge kwa masiku na aghalabu hutumia idadi ya arobaini (40).


Humpa mtu kinywaji kisha humtapisha kwa njia mbali mbali na kumzuga macho aone kuwa ametokwa na vidudu tumboni!


Humzuga macho na mwili kwa njia zake na kumchoma visu mwilini bila ya mtu kuhisi maumivu.


Humpa mtu miiko asile vyakula fulani.


Aghlabu hutumia vitambaa vyekundu katika kazi zao za uchawi.


Na mengine mengineyo.

Rejea Makala: Jini, Shaytwaan Na Mchawi



2- Kufanya Au Kuhudhuruia Michezo Ya Sihri (Mazingaombwe)





Ama pia njia nyengine ya sihri ni watu kufanya michezo yake (mazingaombwe) na watu kugharamika kununua tiketi za kuingia michezoni kutazama uchawi. Hapo hufanya mazingaombwe ya kuwafanya watu watekwe akili zao na waone miujiza isiyokuwa ya kweli kama vile wachawi wa Fir’awn kabla ya kuamini kwao walipowahudhurisha halaiki ya watu uwandani wakayazuga macho yao:



قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِمَّا أَن تُلْقِيَ وَإِمَّا أَن نَّكُونَ نَحْنُ الْمُلْقِينَ﴿١١٥﴾

(Wachawi) Wakasema: “Ee Muwsaa, ima utupe wewe au tuwe sisi wa (kwanza) kutupa.”





قَالَ أَلْقُوا ۖ فَلَمَّا أَلْقَوْا سَحَرُوا أَعْيُنَ النَّاسِ وَاسْتَرْهَبُوهُمْ وَجَاءُوا بِسِحْرٍ عَظِيمٍ﴿١١٦﴾

(Muwsaa) Akasema: “Tupeni!” Basi walipotupa, waliyasihiri macho ya watu na wakawatia woga, na wakaja na sihiri kuu. [Al-A’raaf: 115-116]





Ee ndugu Muislamu! Jiepushe na sihri na wachawi ubakie salama katika maasi, kufru na shirki kubwa kama hii!



Kwa aliyetendewa Sihri (uchawi) basi atafute Tiba ya Sunnah, maelezo yanapatikana katika kiungo kifuatacho:



10-Ruqya: Kutafuta Shifaa: Poza Ya Maradhi, Sihri (Uchawi) Katika Baadhi Ya Vyakula
 
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم



Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!



24-Vipi Kujiepusha Na Shirki



Alhidaaya.com









Ndugu Muislamu! Hakika shirki ni dhulma kubwa mno! Kwa kumfanyia shirki Rabb wako Aliyekuumba, Ambaye unaishi katika ardhi Yake, Ambaye Anakuruzuku na Akakujaalia neema nyingi mno zisizohesabika, Ambaye Anakurehemu na Akakujaalia fadhila na neema za kila aina.





Miongoni mwa neema Zake Allaah ('Azza wa Jalla) ni kukujaalia uhai mpaka hii leo uweze kutambua yanayomshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ili urudie kutubia Kwake kabla ya kufariki kwako. Basi hii ni fursa adhimu kwa kila aliyekuwa akimshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) atekeleze yafuatayo ambayo yatasaidia kumuepusha na shirki In Shaa Allaah:



1. Tawbah ya kweli:



Rudi kwa Rabb wako kwa kutubia tawbah ya nasuha (kwelikweli) kama Anavyoamrisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّـهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يُكَفِّرَ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيُدْخِلَكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ يَوْمَ لَا يُخْزِي اللَّـهُ النَّبِيَّ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ ۖ نُورُهُمْ يَسْعَىٰ بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَانِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَاغْفِرْ لَنَا ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٨﴾

Enyi walioamini! Tubieni kwa Allaah tawbah ya nasuha (kwelikweli); asaa Rabb wenu Akakufutieni maovu yenu, na Akakuingizeni Jannaat zipitazo chini yake mito. Siku ambayo Allaah Hatomfedhehesha Nabiy (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na wale walioamini pamoja naye. Nuru yao itatembea mbele yao na kuliani mwao, watasema: “Rabb wetu! Tutimizie Nuru yetu, na Tughufurie, hakika Wewe juu ya kila kitu ni Muweza. [At-Tahriym: 8]



Twabah ya nasuha ina masharti yafuatayo:



a. Kuomba maghfirah

b. Kuacha hayo maasi

c. Kujuta

d. Kuweka niyyah (azma) kuwa hatorudia tena

e. Kama kaidhulumu haki ya mtu basi ni kuirudisha hiyo haki.



Na kutubia shirki ni kujisalimisha katika Uislamu pekee kama alivyosema Imaam As-Sa’dy (Rahimahu Allaah) kuhusu Aayah:



قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوا إِن يَنتَهُوا يُغْفَرْ لَهُم مَّا قَدْ سَلَفَ وَإِن يَعُودُوا فَقَدْ مَضَتْ سُنَّتُ الْأَوَّلِينَ﴿٣٨﴾

Waambie waliokufuru kwamba wakikoma wataghufuriwa yaliyopita, lakini wakirudia, basi imekwishapita desturi ya watu wa awali. [Al-Anfaal: 38]



Akasema: “Wakikoma; inamaanisha kufru zao, nako ni kujisilimisha kwa Allaah Pekee bila ya kumshirikisha.”



Adhkaar mbalimbali zimethibiti katika Sunnah jinsi ya kuomba maghfirah, na Sayyidul-Istighfaar (du’aa kuu kabisa ya kuomba maghfirah) ni:



اللّهـمَّ أَنْتَ رَبِّـي لا إلهَ إلاّ أَنْتَ، خَلَقْتَنـي وَأَنا عَبْـدُك، وَأَنا عَلـى عَهْـدِكَ وَوَعْـدِكَ ما اسْتَـطَعْـت، أَعـوذُبِكَ مِنْ شَـرِّ ما صَنَـعْت، أَبـوءُ لَـكَ بِنِعْـمَتِـكَ عَلَـيَّ وَأَبـوءُ بِذَنْـبي فَاغْفـِرْ لي فَإِنَّـهُ لا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْتَ .

Allaahumma Anta Rabbiy laa ilaaha illaa Anta Khalaqtaniy wa ana ‘abduka wa anaa ‘alaa ‘ah-dika wawa’-dika mastatwa’-tu, a’uwdhu bika min sharri maa swana’-tu, abuw-u Laka bini’-matika ‘alayya wa abuw-u bidhanbiy, faghfirliy fainnahu laa yaghfirudh- dhunuwba illaa Anta.



Ee Allaah, Wewe ni Rabb wangu, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, umeniumba mimi na mimi ni mja Wako, nami niko juu ya ahadi Yako, na agano Lako, kiasi cha uwezo wangu, najikinga Kwako kutokana na shari ya nilichokifanya, nakiri Kwako kwa kunineemesha, na nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba unighufurie kwani hakuna wa kughufuria madhambi ila Wewe. [Al-Bukhaariy (7/150) [2306] kutoka kwa Shaddaad bin Aws Radhwiya Allaahu ’anhu]





Na Nabiy (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akistaghfiru mara 70 kila siku na katika riwaayah nyingine mara 100 kwa siku:



الْأَغَرِّ الْمُزَنِيِّ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: (إِنِّي لَأَسْتَغْفِرُ اللَّهَ فِي الْيَوْمِ مِائَةَ مَرَّةٍ) رواه مسلم (2702

Al-Agharr Al-Muzaniyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amepokea kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba: ((Hakika mimi nastaghfiru kwa Allaah mara mia katika siku moja)). [Muslim (2702)]



Na vilevile:



وقَالَ أَبُو هُرَيْرَةَ رضي الله عنه : سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ : ( وَاللَّهِ إِنِّي لاَسْتَغْفِرُ اللَّهَ وَأَتُوبُ إِلَيْهِ فِي الْيَوْمِ أَكْثَرَ مِنْ سَبْعِينَ مَرَّةً ) رواه البخاري (6307).

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ’anhu) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Wa-Allaahi mimi nastaghfiru kwa Allaah na natubia Kwake zaidi ya mara sabini katika siku moja)). [Al-Bukhaariy (6307)]



Hivyo ni kusema: ”Astaghfiru Allaah wa atuwubu Ilayhi.”



Juu ya hayo, faida kadhaa za kuomba maghfirah zinamrudia bin-Aadam anayemuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) maghfirah.





2. Kuomba Isti’aanah (msaada) kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



Zidisha kuswali Swalaah za Sunnah na kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) humo Akuepushe na shirki. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَاسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلَّا عَلَى الْخَاشِعِينَ ﴿٤٥﴾

Na tafuteni msaada kupitia subira na Swalaah; na hakika hilo ni kubwa isipokuwa kwa wanyenyekevu. [Al-Baqarah: 45]





Pia, du’aa muhimu kabisa ya kujiepusha na shirki kama ilivyothibti katika Sunnah:



اللّهُـمَّ إِنّـي أَعـوذُبِكَ أَنْ أُشْـرِكَ بِكَ وَأَنا أَعْـلَمْ، وَأَسْتَـغْفِرُكَ لِما لا أَعْـلَم

Allaahumma inniy a’uwdhu Bika an ushrika Bika wa anaa a’-alamu wa astaghfiruka limaa laa a’-lam

Ee Allaah hakika mimi Najikinga Kwako kutokana na kukushirikisha hali ya kuwa najua na ninakuomba maghfirah kwa nisiyoyajua. [Ahmad (4/403) na wengineo; Taz. Swahiyh Al-Jaami’(3/233) [3731] na Swahiyh At-Targhiyb wat-Tarhiyb ya Al-Albaaniy (1/122) [36]







3. Kumdhukuru Allaah Kwa Wingi:



Mdhukuru mno Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) khaswa kwa kusoma Qur-aan kwa kuwa ni poza ya nyoyo kwa kila aina ya maradhi; kufru, shirki na kadhaalika. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَتْكُم مَّوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَشِفَاءٌ لِّمَا فِي الصُّدُورِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ﴿٥٧﴾

Enyi watu! Kwa yakini yamekujieni mawaidha kutoka kwa Rabb wenu, na shifaa ya yale yaliyomo vifuani, na mwongozo na rahmah kwa Waumini. [Yuwnus: 57]



Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



اتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِنَ الْكِتَابِ وَأَقِمِ الصَّلَاةَ ۖ إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ ۗ وَلَذِكْرُ اللَّـهِ أَكْبَرُ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تَصْنَعُونَ ﴿٤٥﴾

Soma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uliyoletewa Wahy katika Kitabu na simamisha Swalaah, hakika Swalaah inazuia machafu na munkari. Na bila shaka kumdhukuru Allaah ni kubwa zaidi. Na Allaah Anajua yale mnayoyatenda. [Al-‘Ankabuwt: 45]





4. Kutafuta Na Kuongeza ‘Ilmu:



Mojawapo ya kinga ya shirki ni kuongeza ‘ilmu sahihi ya Dini hii tukufu ili kutambua yanayothibitisha Tawhiyd (Kumwpekesha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na yaliyo kinyume chake (yanayomshirikisha). Bila ya kuwa na ‘ilmu hutoweza kutambua. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ۗ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٩﴾

Sema: “Je, wanalingana sawa wale wanaouja na wale wasiojua?” Hakika wanakumbuka wenye akili tu. [Az-Zumar: 9]



Na pia:



فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مُتَقَلَّبَكُمْ وَمَثْوَاكُمْ﴿١٩﴾

Basi jua kwamba laa ilaaha illa-Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah na omba maghfirah kwa dhambi zako na kwa ajili ya Waumini wa kiume na Waumini wa kike. Na Allaah Anajua harakati zenu huku na kule na pahala penu pa kupumzikia. [Muhammad: 19]



5. Kuwa Na Taqwa:



Kumcha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kila wakati, kila mahali. Jibriyl ('Alayhis-Salaam) alipomwendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza maswali mojawapo lilikuwa kuhusu ihsaan akajibu:

أنْ تَعْبُدَ الله كَأَنَّكَ تَرَاهُ فإنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فإنَّهُ يَرَاك

((Umwabudu Allaah kama kwamba unamuona, na ikiwa humuoni, basi Yeye hakika Anakuona)) [Muslim]





6. Kuwaza Adhabu Za Allaah Duniani Na Aakhirah:



Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



حُنَفَاءَ لِلَّـهِ غَيْرَ مُشْرِكِينَ بِهِ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَكَأَنَّمَا خَرَّ مِنَ السَّمَاءِ فَتَخْطَفُهُ الطَّيْرُ أَوْ تَهْوِي بِهِ الرِّيحُ فِي مَكَانٍ سَحِيقٍ ﴿٣١﴾

Muelemee haki kwa kumwabudu Allaah Pekee bila ya kumshirikisha. Na yeyote anayemshirikisha Allaah basi kama kwamba ameporomoka kutoka mbinguni, wakamnyakua ndege au upepo ukamtupa mahali mbali mno. [Al-Hajj: 31]



Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

لَّا تَجْعَلْ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ فَتَقْعُدَ مَذْمُومًا مَّخْذُولًا ﴿٢٢﴾

Usifanye pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine, ukaja kushutumiwa na mwenye kutelekezwa mbali (motoni). [Al-Israa: 22]



Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَلَا تَجْعَلْ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ فَتُلْقَىٰ فِي جَهَنَّمَ مَلُومًا مَّدْحُورًا ﴿٣٩﴾

Na wala usifanye pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine ukaja kutupwa katika Jahannam hali ya kuwa mwenye kulaumiwa na kufukuziliwa mbali. [Al-Israa: 39]



Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuhusu sifa za ‘Ibaadur-Rahmaan (Waja wa Mwingi wa Rahmah):



وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ يَلْقَ أَثَامًا ﴿٦٨﴾

Na wale ambao hawaombi pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine na wala hawaui nafsi ambayo Allaah Ameiharamisha isipokuwa kwa haki, na wala hawazini. Na atakayefanya hivyo atakutana na adhabu.

يُضَاعَفْ لَهُ الْعَذَابُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَيَخْلُدْ فِيهِ مُهَانًا ﴿٦٩﴾

Ataongezewa adhabu maradufu Siku ya Qiyaamah, na mwenye kudumu humo akiwa amedhalilika.



إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يُبَدِّلُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٧٠﴾

Isipokuwa yule aliyetubu na akaamini na akatenda ‘amali njema; basi hao Allaah Atawabadilishia maovu yao kuwa mema. Na Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.



وَمَن تَابَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَإِنَّهُ يَتُوبُ إِلَى اللَّـهِ مَتَابًا ﴿٧١﴾

Na atakayetubu na akatenda mema, basi hakika yeye anatubia kwa Allaah tawbah ya kweli. [Al-Furqaan: 68-71]



Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَاۚ أُولَـٰئِكَ هُمْ شَرُّ الْبَرِيَّةِ ﴿٦﴾

Hakika wale waliokufuru miongoni mwa watu wa kitabu na washirikina watakuwa katika moto wa Jahannam, ni wenye kudumu humo; hao ndio waovu kabisa wa viumbe. [Al-Bayyinah: 6]





Na dalili nyingi nyenginezo zimetajwa katika Qur-aan na Sunnah kuhusu adhabu za mwenye kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) zikiwemo ambazo zimetajwa katika milango iliyotangulia ya somo hili la ‘Hakika Shirki ni Dhulma Kubwa Mno’, basi rudia ee ndugu Muislamu upate kujikumbusha na kuwaidhika zaidi.



Wa biLLaahi At-Tawfiyq.
 
Alhamdulillah tumemaliza hizi Makala za Hakika shirki ni dhuluma kubwa mno

................................................................................................
 
Visa vya wachamungu ni simulizi za kweli au za kujifunza kuhusu watu waliomcha Allah kwa dhati. Hivi ni baadhi ya visa vya wachamungu vilivyojaa hekima na mafunzo:

1. Mtoto Mcha Mungu na Dada Yake
Mtoto mmoja mdogo alikuwa akiswali kila wakati nyumbani, hata ndugu zake walipokuwa wakimcheka. Siku moja dada yake alipata ajali na akaanguka, akavunjika. Mtoto huyo alimkumbatia dada yake na kusema, "Allah ndiye mwenye kurekebisha, tusimwache."
Wote walilia na kuomba dua — na baada ya matibabu, dada yake alipona haraka ajabu. Tangu siku hiyo, familia ilianza kuswali pamoja kila siku.

Somo: Kumcha Allah huleta baraka hata kwa wengine walio karibu nawe.

---

2. Mchungaji na Toba ya Kweli
Mchungaji mmoja wa kondoo alikuwa akiishi peke yake milimani. Alikuwa na moyo wa kumuogopa Allah sana. Alipomsikia mtu akitukana dini, alilia na akaenda msikitini kumuomba Allah awaongoze watu wake.
Siku moja kijana aliyekuwa akimtukana Mungu alikuja kwake, akavutiwa na upole wake, na hatimaye akasilimu.

Somo: Kumcha Allah kwa vitendo hubadilisha hata mioyo migumu.

---

3. Imam na Dirham Haramu
Imamu mmoja alipata dirham moja ya ziada kwenye biashara yake. Badala ya kuitumia, aliirudisha kwa mteja aliyelipa zaidi kwa bahati mbaya.

"Mlo wangu hautachanganywa na pesa yenye shaka."
Tabia hiyo iliwavutia watu wengi na wengi wakarudi katika njia ya haki.

Somo: Kumcha Allah ni pamoja na kuwa mwadilifu hata pasipo kushuhudiwa.
 
UJUMBE WA LEO
Screenshot_20250603_141050_Quran Swahili.jpg
 
Umuhimu wa Ikhlaas (Ukweli wa Nia kwa Allah):

Ikhlaas ni kufanya kila jambo kwa ajili ya Allah tu, bila kutaka sifa, umaarufu au malipo kutoka kwa watu. Ni msingi wa kukubaliwa kwa ibada na matendo mema.

📖 Qur’an inasema:
"Wameamrishwa kumuabudu Allah kwa ikhlaas..." (Qur'an 98:5)

🌟 Umuhimu wake:
1. Matendo hukubaliwa tu kwa ikhlaas.
2. Huleta utulivu wa moyo – hufanyi kwa watu, bali kwa Mola.
3. Hulinda mtu dhidi ya riyaa (unafiki).
4. Hubarikiwa hata kazi ndogo – kwa sababu nia ni safi.
5. Ikhlaas ni silaha dhidi ya wasiwasi na lawama.

🕊️ Maneno ya hekima:
“Amali bila ikhlaas ni kama mwili bila roho – linaonekana, lakini halina uhai.”

Dua fupi:
“Allahumma ja’al a’malanaa kullahaa ikhlaasan li wajhika.”
(Ya Allah, yafanye matendo yetu yote yawe kwa ajili yako tu.)
 
Kuchinja - Fadhila, Hikmah Na Hukmu Zake




www.alhidaaya.com





Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa):



فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ ﴿٢﴾

Basi swali kwa ajili ya Rabb wako na chinja kwa ajili Yake. [Al-Kawthar: 2]



Kuchinja ni moja ya ‘ibaadah za Kiislam ambayo inatukumbusha Tawhiyd ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) na Baraka Zake kwetu, pamoja na kutupa mafunzo ya utiifu wa baba yetu Ibraahiym kwa Rabb wake na kumpwekesha Allaah. Hivyo ‘ibaadah hii ya kuchinja ni muhimu sana kwa Muislamu, na inatupasa tuizingatie kwa makini na kuitekeleza.





Ubainifu Wake:



Ni kuchinja kondoo, ngamia au ng'ombe au mbuzi siku ya 'Iydul-Adhwhaa na siku za Tashriyq (siku ya 11, 12, 13 Dhul-Hijjah) ili kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa).





Hukmu Yake:



Wanavyuoni wamekhitilafiana kuhusu hukmu yake, hivyo kuna kauli mbili:



Ya Kwanza: Kuchinja ni Sunnah Muakkadah (Sunnah iliyosisitizwa) na hii ndio rai iliyotiliwa nguvu kabisa na Ma-Imaam Maalik, Shaafi'iyy, Ahmad bin Hanbal na wengineo.





Ya Pili: Kuchinja ni waajib kwa kila mwenye uwezo. Rai hii ni ya Abuu Haniyfah na wengineo. Inawajibika katika familia ya kila nyumba ya Muislamu, ambayo watu wake wanao uwezo wa kuchinja. Wakanukuu kauli za Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa):



فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ ﴿٢﴾

2. Basi swali kwa ajili ya Rabb wako na chinja kwa ajili Yake. [Al-Kawthar: 2]



وَالْبُدْنَ جَعَلْنَاهَا لَكُم مِّن شَعَائِرِ اللَّـهِ لَكُمْ فِيهَا خَيْرٌ ۖ

36. Na ngamia na ng’ombe Tumekufanyieni kuwa ni miongoni mwa Ishara za Allaah; kwa hao mnapata khayr nyingi. [Al-Hajj: 36]



Pia wakanukuu Hadiyth kadhaa za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Athaar.



Aliulizwa Imaam Muhammad bin 'Uthaymiyn kama masikini inampasa achinje. Akajibu "Ikiwa anao uwezo wa kuchinja basi achinje ili apate khayr hizi na kama hana uwezo basi haimpasi".



Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam),



(( ضحى بكبشين أملحين أقرنين ذبحهما بيده وسمى وكبر)) رواه البخاري ومسلم

alichinja kondoo wawili walionona, walio na pembe, aliwachinja kwa mikono yake akataja jina la Allaah, Akamtukuza kwa kusema BimiLLaahi Allaahu Akbar [Al-Bukhaariy na Muslim]



Maoni ya Wanachuoni wengi kuhusu fadhila, hukmu na hekima ni kama yafuatayo:





Fadhila Zake:



Kuna ushahidi kwamba ‘ibaadah ya kuchinja ina fadhila kubwa kwa sababu ya kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



عن عائشة رضي الله عنها أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((ما عمل ابن آدم يوم النحر عملاً أحبُّ إلى الله من إراقة الدم، وإنه ليؤتى يوم القيامة بقرونها، وأظلافها، وأشعارها، وإن الدم ليقع من الله عز وجل بمكان قبل أن يقع على الأرض، فطيبوا بها نفساً))

Kutoka kwa mama wa Waumini 'Aaishah (Radhwiya Allaahu anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna kitendo cha mwana Aadam kilichokuwa ni kipenzi kabisa kwa Allaah siku ya kuchinja kama kumwaga damu (kuchinja). Atakuja (huyo mnyama) siku ya Qiyaamah na pembe zake, kucha zake na nywele zake. Damu yake itamwagika mahali fulani Allaah Anapajua kabla ya kumwagika katika ardhi. Hivyo zipendezesheni nafsi kwayo)) [At-Tirmidhiy]





Hikmah Yake:



1. Kujikurubisha Kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) kama Anavyosema katika kauli Yake:



فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ ﴿٢﴾

2. Basi swali kwa ajili ya Rabb wako na chinja kwa ajili Yake. [Al-Kawthar: 2]



Anasema pia:



قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦٢﴾

162. Sema: “Hakika Swalaah yangu, na kuchinja kafara na ‘ibaadah zangu na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah Pekee Rabb wa walimwengu.”



لَا شَرِيكَ لَهُ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ ﴿١٦٣﴾

163. Hana mshirika, na kwa hayo ndio nimeamrishwa, nami ni Muislamu wa kwanza. [Al-An'aam: 162-163].



لَن يَنَالَ اللَّـهَ لُحُومُهَا وَلَا دِمَاؤُهَا وَلَـٰكِن يَنَالُهُ التَّقْوَىٰ مِنكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ سَخَّرَهَا لَكُمْ لِتُكَبِّرُوا اللَّـهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ ۗ وَبَشِّرِ الْمُحْسِنِينَ ﴿٣٧﴾

37. Haimfikii Allaah nyama zake wala damu yake, lakini inamfikia taqwa kutoka kwenu. Hivyo ndivyo Tulivyowatiisha kwenu ili mpate kumtukuza Allaah; Allaahu Akbar, kwa yale Aliyokuongozeni; na wabashirie wafanyao ihsaan. [Al-Hajj: 37]



Na kafara ni kuchinja kwa kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa)





2. Kuihuisha Sunnah Mojawapo Ya Tawhiyd, wakati Allaah Alipompa wahyi Ibraahiym (alayhis-salaam) amchinje mwanawe Ismaa'iyl. Kisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) Akampa fidia ya kondoo, akamchinja badala yake. Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) Anasema:



وَفَدَيْنَاهُ بِذِبْحٍ عَظِيمٍ ﴿١٠٧﴾

107. Na Tukamfidia kwa dhabihu adhimu. [Aswaaffaat: 107]





3. Muislam kuweza kuwalisha nyama familia yake pamoja na jamaa zake siku ya 'Iyd na kueneza Rahmah miongoni mwa masikini na mafakiri.





4. Kutoa shukurani kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) kutujaalia kuwa na wanyama wafugwao kama Anavyosema:



وَالْبُدْنَ جَعَلْنَاهَا لَكُم مِّن شَعَائِرِ اللَّـهِ لَكُمْ فِيهَا خَيْرٌ ۖ فَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ عَلَيْهَا صَوَافَّ ۖ فَإِذَا وَجَبَتْ جُنُوبُهَا فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْقَانِعَ وَالْمُعْتَرَّ ۚ كَذَٰلِكَ سَخَّرْنَاهَا لَكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٣٦﴾

36. Na ngamia na ng’ombe Tumekufanyieni kuwa ni miongoni mwa Ishara za Allaah; kwa hao mnapata khayr nyingi. Basi tajeni Jina la Allaah juu yao wanapopangwa safu (kuchinjwa). Na waangukapo ubavu, basi kuleni kutoka humo, na lisheni waliokinai na wanaolazimika kuomba. Hivyo ndivyo Tulivyowatiisha kwa ajili yenu ili mpate kushukuru.



لَن يَنَالَ اللَّـهَ لُحُومُهَا وَلَا دِمَاؤُهَا وَلَـٰكِن يَنَالُهُ التَّقْوَىٰ مِنكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ سَخَّرَهَا لَكُمْ لِتُكَبِّرُوا اللَّـهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ ۗ وَبَشِّرِ الْمُحْسِنِينَ ﴿٣٧﴾

37. Haimfikii Allaah nyama zake wala damu yake, lakini inamfikia taqwa kutoka kwenu. Hivyo ndivyo Tulivyowatiisha kwenu ili mpate kumtukuza Allaah; Allaahu Akbar, kwa yale Aliyokuongozeni; na wabashirie wafanyao ihsaan.

[Al-Hajj: 36-37]





Hukmu Za Hali Ya Mnyama



Umri Wake:



Kondoo wawe ni kondoo ambao wamekamilisha umri wa mwaka mmoja takriban. Mbuzi wawe wamekamilisha umri wa mwaka mmoja na kuingia mwaka wa pili. Ngamia wawe wamekamilisha umri wa miaka minne na kuingia wa tano. Ng'ombe wawe wamekamilisha miaka miwili na kuingia mwaka wa tatu, kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

((لا تذبحوا إلا مسنة إلا أن تعسر عليكم فتذبحوا جذعة من الضأن)) رواه مسلم

((Msichinjie ila mnyama mwenye makamo isipokuwa ikiwa ni shida kwenu, hivyo mchinje kondoo (japo wa chini ya umri wa mwaka lakini awe zaidi ya umri wa miezi sita)) [Muslim]



Usalama Wake:



Asiwe na kasoro yoyote kwani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



((أربع لا تجوز في الأضاحي: العوراء البيّن عورها، والمريضة البيّن مرضها، والعرجاء البيّن ظلعها، والعجفاء التي لا تنقي))

((Mambo manne (kasoro nne) hayapasi katika kuchinja; mwenye jicho chongo lenye kudhihirika, mnyama mgonjwa mwenye kudhihirika ugonjwa wake, kilema mwenye kudhihirika kuchechemea kwake na aliyedhoofika ambaye hana nyama katika mifupa yake)) [Swahiyh Al-Jaami']





Wakati Wa Kuchinja:



Kuchinja asubuhi ya siku ya 'Iyd baada ya Swalaah. Hairuhusiwi kuchinja kabla ya Swalaah kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



حديث أنس رضي الله عنه- قال: قال رسول الله -صلى الله عليه وسلم: ((من ذبح قبل الصلاة فإنما ذبح لنفسه، ومن ذبح بعد الصلاة فقد تم نسكه وأصاب سنة المسلمين)) البخاري ومسلم

Kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayechinja kabla ya Swalaah atakuwa amejichinjia kwa ajili yake mwenyewe. Na Atakayechinja baada ya Swalaah atakamilisha kafara (kichinjo) yake na atapata (atatekeleza) Sunnah ya Waislam)) [Al-Bukhaariy na Muslim]



Anaweza kuchinja siku ya pili ya 'Iyd au kuchelewesha hadi siku ya mwisho ya Ayyaamut-Tashriyq (siku za Tashriyq) ambayo ni siku ya kumi na tatu Dhul-Hijjah.



(... وفي كل أيام التشريق ذبح))

((...siku zote za Tashriyq ni siku za kuchinja)) [Ahmad]





Yanayopendekezeka Katika Kuchinja:



Kumpwekesha Allaah:



Inapendekezeka kumuelekeza mnyama Qiblah wakati wa kumchinja na kusema:



((بسم الله والله اكبر، اللهم هذا منك ولك))

((BismiLLaah, wa Allaahu Akbar, Ee Allaah hii ni kutoka Kwako na kwa ajili Yako))





Kuchinja mwenyewe ni bora zaidi:



Inapendekezeka Muislamu achinje mwenyewe na akimuwakilisha mtu kumchinjia pia inaruhusiwa hakuna ikhtilaaf katika jambo hili baina ya 'Ulamaa.





Kugawa Nyama:



Inapendekeza kuigawa nyama kwanza kwa familia yake, na pia kuwagawia swadaqah masikini, majirani, marafiki, n.k. kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa):



لِّيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ وَيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ فِي أَيَّامٍ مَّعْلُومَاتٍ عَلَىٰ مَا رَزَقَهُم مِّن بَهِيمَةِ الْأَنْعَامِ ۖ فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْبَائِسَ الْفَقِيرَ ﴿٢٨﴾

28. Ili washuhudie manufaa yao; na walitaje Jina la Allaah katika siku maalumu kwa yale Aliyowaruzuku kati ya wanyama wenye miguu minne wa mifugo. Basi kuleni humo, na lisheni mwenye shida fakiri. [Al-Hajj: 28]



وَالْبُدْنَ جَعَلْنَاهَا لَكُم مِّن شَعَائِرِ اللَّـهِ لَكُمْ فِيهَا خَيْرٌ ۖ فَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ عَلَيْهَا صَوَافَّ ۖ فَإِذَا وَجَبَتْ جُنُوبُهَا فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْقَانِعَ وَالْمُعْتَرَّ ۚ

36. Na ngamia na ng’ombe Tumekufanyieni kuwa ni miongoni mwa Ishara za Allaah; kwa hao mnapata khayr nyingi. Basi tajeni Jina la Allaah juu yao wanapopangwa safu (kuchinjwa). Na waangukapo ubavu, basi kuleni kutoka humo, na lisheni waliokinai na wanaolazimika kuomba. [Al-Hajj: 36]



Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

((كلوا وأطعموا وادخروا)). رواه البخاري

((Kuleni, lisheni na mbakishe [akiba])) [Al-Bukhaariy]



Na usemi mwengine kutoka kwa Muslim kutoka kwa mama wa Waumini 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa):



عن عائشة رضي الله عنها أن النبي صلى الله عليه وسلّم قال: ((كلوا وادخروا وتصدقوا)) رواه مسلم.

((Kuleni, bakisheni na mtoe swadaqah)) [Muslim]



Inaruhusiwa pia kuigawa nyama yote swadaqah na Inaruhusiwa kubakisha sehemu.





Haifai Kumpa Chochote Katika Nyama Mchinjaji Kama Ni Ujira:



Hairuhusiwi kumlipa mchinjaji aliyewakilishwa kuchinja baadhi ya nyama kama ujira wake kutokana na Hadiyth ifuatayo:



عن علي قال‏:‏ أمرني رسول الله صلى الله عليه وسلم أن أقوم على بدنه وأن أتصدق بلحومها وجلدها وأجلتها ‏(‏وأجلتها‏:‏ أي لباسها الذي يقيها البرد‏) وأن لا أعطي الجزار منها شيئا، وقال‏:‏ نعطيه من عندنا‏.

Kutoka kwa 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Rasuli wa Alllaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliniamrisha kuchinja? Na kutoa nyama, ngozi na kile kinachomfunika kumhifadhi na baridi kuvitolea swadaqah na nisimpe chochote katika nyama hiyo. ((Tutampa kitu tulichonacho)) [Al-Bukhaariy na Muslim]





Ufafanuzi Zaidi:



Ukichinja AL-HADYI, mchinjaji hapewi katika nyama alioichinja lakini anapewa ujira wake. AL-HADYI ni kuchinja na wewe upo katika Hajj.



Ukichinja UDHWHIYAH, mchinjaji anaweza akapewa katika nyama hiyo aliyoichinja kama swadaqah ikiwa ni masikini. UDHWHIYAH ni kichinjo kwa wale wasiokuwa katika Hajj. Walio katika Hajj kichinjo kinaitwa AL-HADYI.





Mnyama Mmoja Anatosheleza Familia Nzima:



Kuchinja mnyama mmoja anatosheleza katika kila familia japo kama kuna watu wengi katika familia kutokana na kauli ya:

أبي أيوب -رضي الله عنه- لما سئل: كيف كانت الضحايا على عهد رسول الله؟ فقال: "كان الرجل يضحي بالشاة عنه وعن أهل بيته" (الترمذي)

Abuu Ayyuwb (Radhwiya Allaahu 'anhu) alipoulizwa: "Uchinjaji ulikuwa vipi zama za Rasuli wa Allaah?" Akajibu: "Mtu alikuwa anachinja kondoo mmoja kwa ajili yake na familia yake" [At-Trimidhiy]



Yanayompasa Kufanya Mwenye Kutaka Kuchinja:



Baada ya kutia Niyyah ya kuchinja, asikate mtu nywele wala kucha mpaka amalize kuchinja kama tulivyoamrishwa katika

Hadiyth ifuatayo:



عن أم سلمة رضي الله عنها، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((إذا رأيتم هلال ذي الحجة وأراد أحدكـم أن يضحّي فليمسك عــن شعره وأظفاره)) ، وفي راوية (( فلا يأخذ من شعره ولا من أظفـاره حتى يضحّي )) مسلم

Imetoka kwa Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ukiandama mwezi wa Dhul-Hijjah na ikiwa yuko anayetaka kuchinja basi azuie (asikate) nywele zake na kucha zake)).



Na katika riwaya nyingine ((Asikate nywele wala kucha mpaka atakapomaliza kuchinja)) [Muslim na wengineo]





Mwenye Uwezo Wa Kuchinja Zaidi Ya Mmoja:



Mwenye uwezo wa kuchinja zaidi ya mmoja na akipenda achinje kama alivyochinja Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ajili ya Ummah wa Kiislam wote. Hivyo Muislam asiye na uwezo wa kuchinja naye atapata fadhila hizi za kuchinja, naye mchinjaji atachuma thawabu za Waislam wote wasio na uwezo. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifanya hivyo:

وعن أبي رافع رضي الله عنه «أن النبي صلى لله عليه وسلّم كان يضحي بكبشين أحدهما عنه وعن آله، والاخر عن أمته جميعاً»، رواه أحمد

Kutoka ka Abuu Raafi' (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akichinja kondoo wawili; mmoja kwa ajili yake na familia yake na wa mwengine kwa ajili ya Ummah wake wote)) [Ahmad]



Kutoka kwa Jaabir kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa akichinja kwa ajili ya Ummah akisema:

(( بسم الله والله أكبر. اللهم هذا عني وعمن لم يضح من أمتي)) رواه أحمد وأبو داود والترمذي.

((BismiLLaah, wa Allaahu Akbar, Ee Allaah hii kwa ajili yangu na kwa ajili ya wasio na uwezo katika Ummah wangu)) [Ahmad, Abu Daawuud na At-Tirmidhiy]



Wa BiLLaahi at-Tawfiyq
 
Kwa kuongezea inafaa pia kwa ndugu au waislamu wakachanga hela na kuchinja kwa pamoja

Kwahiyo mnaweza mkachanga hela zenu na kuchinja na kupata fadhila za kuchinja nyie wote
 
Nguzo Ya Hajj Itekelezwe Mara Ngapi Kishari'ah?



Alhidaaya.com



Swali:



As.kum



Hijja mafrudh ni faradhi kwa mwenye uwezo jee hajj hasa ni mara ngapi mbona watu wanakwenda zaidi ya mara 1inakuaje?





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Nguzo ya Hijjah imefaridhiwa kwa Waislamu katika Qur-aan kuitekeleza mara moja tu katika umri wao na hivyo atakapofanya mtu mara moja tu, atakuwa ameshakamilisha nguzo yake na kupata fadhila zake zote. Na juu ya hivyo nguzo hii haikufaridhiswa ila kwa mwenye uwezo tu. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ

Na kwa ajili ya Allaah imewajibika watu watekeleze Hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo. [Al-'Imraan: 97]



Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَأَتِمُّوا الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ لِلَّـهِ ۚ

Na timizeni Hajj na ‘Umrah kwa ajili ya Allaah. [Al-Baqarah: 196]



Ikiwa Hajj si lazima kwa asiye na uwezo ni dhahiri kuwa mwenye uwezo inamtosha kuitekeleza mara moja na kuhesabika kuwa katimiza fardhi yake kama tulivyoona katika Aayah juu.



Hata Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametekeleza nguzo hii mara moja katika maisha yake. Na alipofaridhisha nguzo hii katika Sunnah alikuja mtu kumuuliza kama inapasa kufanya Hajj kila mwaka, maelezo katika usimulizi ufuatao yanatupa majibu:



عن أبي هريرة قال : خطبنا رسول الله صلى الله عليه وسلم فقال: ((أيها الناس قد فرض الله عليكم الحج فحجوا)) ، فقال رجل : "أكلَّ عام يا رسول الله ؟" فسكت حتى قالها ثلاثا ، فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم(( : لو قلت نعم لوجبت ولما استطعتم)) ، ثم قال : ((ذروني ما تركتكم فإنما هلك من كان قبلكم بكثرة سؤالهم واختلافهم على أنبيائهم فإذا أمرتكم بشيء فأتوا منه ما استطعتم وإذا نهيتكم عن شيء فدعو)) رواه مسلم

Kutoka kwa Abu Hurayrah ambaye amesema: “Alitukhutubia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Enyi watu Allaah Amekufaridhisheni Hajj hivyo mhiji)). Mtu mmoja akasema: Kila mwaka ee Rasuli wa Allaah? Akanyamaza kimya (Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hadi yule mtu aliporudia mara tatu [swali lake] akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Ningelisema ndio, ingeliwajibika, na wala msingeliweza)). Kisha akasema ((Niacheni kwa yale niliyokuachieni kwani watu wa kabla yenu waliangamia kwa maswali yao mengi na ikhitilaaf zao [kujadiliana sana kwao] na Rusuli yao. Hivyo nnapokuamrisheni jambo lifanyeni muwezavyo na nnapokukatazeni jambo jiepusheni)) [Muslim]



Vile vile:



عن ابْنِ عَبَّاسٍ أَنَّ الأَقْرَعَ بْنَ حَابِسٍ سَأَلَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ : يَا رَسُولَ اللَّهِ الْحَجُّ فِي كُلِّ سَنَةٍ أَوْ مَرَّةً وَاحِدَةً ؟ قَالَ : ((بَلْ مَرَّةً وَاحِدَةً ، فَمَنْ زَادَ فَهُوَ تَطَوُّعٌ)) رواه أَبُو دَاوُد وصححه الألباني

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas kwamba Al-Aqra’ bin Haabis alimuuliza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Ee Rasuli wa Allaah, je, Hijjah ni kila mwaka au mara moja tu? Akasema: ((Ni mara moja lakini mwenye kupenda kuzidisha ni tatwawwu’ [kujitolea na anapata ujira wake])) [Abu Daawuud na imepewa daraja ya Swahiyh na Shaykh al-Albaaniy]



Tunafahamu katika usimulizi huo ulio Swahiyh kwamba mwenye uwezo wa kufanya zaidi ya mara moja (Hajj au ‘Umrah) anaweza kufanya, kwani ni katika kutafuta fadhila zake nyingi na tukufu kama tulivyopata mafunzo katika simulizi mbali mbali, tunazinukuu baadhi yake:



Kufanya ‘Umrah katika Ramadhwaan ni sawa na Hajj:



(( عمرة في رمضان تعدل حجة )) أخرجه البخاري و مسلم

(('Umrah katika Ramadhwaan ni sawa [kwa thawabu] na Hijjah)) [Al-Bukhaariy na Muslim]



Baina ya Hajj na Umra ni kufutiwa madhambi:



((العمرة إلى العمرة كفارة لما بينهما، والحج المبرور ليس له جزاء إلا الجنة)) البخاري

((‘Umrah hadi ‘Umrah [nyingine] ni kafara [kutufiwa dhambi] baina yake, na Hajjum-Mabruur haina jazaa ((isipokuwa ni Pepo)) [Al-Bukhaariy]



Vile vile:

عن إبن مسعود قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((تابعوا بين الحج والعمرة فإنهما ينفيان الفقر والذنوب كما ينفى الكير خبث الحديد والذهب والفضة وليس للحج المبرور ثواب دون الجنة)) سنن النسائي و أحمد والترمذي بإسناد حسن

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Fuatilieni Hajj na ‘Umrah kwani hizo (mbili) zinaondosha ufakiri na madhambi kama kinavyoondosha chombo cha kupulizia moto uchafu wa chuma na dhahabu na fedha, na Hajj Mabruur (Hajj iliyotakabaliwa) jazaa ya thawabu yake hakuna zaidi ya Pepo)) [Sunan An-Nasaaiy, Ahmad na At-Tirmidhiy ikiwa na isnaad Swahiyh]



Miongoni mwa vitendo bora kabisa:



عن أبي هريرة أن رسول الله صلى الله عليه وسلم سئل أي العمل أفضل ؟ فقال : ((إيمان بالله ورسوله)) قيل : ثم ماذا ؟ قال : ((الجهاد في سبيل الله)) قيل : ثم ماذا ؟ قال : ((حج مبرور)) رواه البخاري ومسلم

Kutoka kwa Abu Hurayrah kwamba aliulizwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Kitendo gani bora kabisa? Akasema: ((Kumuamini Allaah na Rasuli Wake)) Akulizwa: Kisha nini? Akasema: ((Jihaad katika njia ya Allaah)) Akaulizwa: Kisha nini? Akasema: ((Hajjum-mabruur [Hajj iliyotakabaliwa])) [Al-Bukhaariy na Muslim]



Kufutiwa dhambi zote



عن أبي هريرة رضي الله عنه قال : سمعت النبي صلى الله عليه وسلم يقول : ((من حج لله فلم يرفث ولم يفسق رجع كيوم ولدته أمه)). رواه البخاري ومسلم

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Nimemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Atakayefanya Hajj asitoe maneno machafu wala asitende vitendo vichafu atarejea kama siku aliyozaliwa na mama yake)) [Al-Bukhaariy na Muslim]



Lakini ni vizuri Muislamu aliyekwishatimiza Hajj kuwafikiria ndugu zake waliokuwa bado hawakujaaliwa kutekeleza nguzo hii na badala ya kwenda yeye zaidi ya mara moja amsaidie ndugu yake ili aweze kutekeleza naye nguzo hii. Walio muhimu zaidi kusaidiwa kutekeleza nguzo hii na wazazi wawili kwani itakuwa ni katika kuwafanyia wema wazazi, ambayo ni moja ya amri tuliyoamrishwa na kusisitizwa sana. Juu ya hivyo itakuwa ni kupata radhi zao.



Pia kutokana na zahma zinazozidi kila mwaka ya mamilioni ya watu kwenda Hijjah, kutokurudia Hijjah itapunguza zahma hizo na kuwapa fursa ndugu wengine ambao hawakutekeleza bado nguzo hii kwani kama tunavyojua kuwa Serikali na wasimamizi wa Hijjah wanatoa idadi fulani tu ya watu kila nchi kwenda kutekeleza nguzo hii na sasa hivi kwa miaka kadhaa wameanzisha utaratibu wa kutoruhusu aliyefanya Hajj asiende tena hadi baada ya miaka kadhaa ili wengine wapate nafasi. Hatuna uhakika kama utaratibu huo unafuatwa vizuri na nchi wanazotoka mahujaji au na hao watoaji visa.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Nywele Zikitoka Na Kucha Zikikatika Je, Ihraam Inavunjika?



Alhidaaya.com





Swali:



If I put the intention to slaughter , how does that work with the ihram that is, cutting the nails n hair. Because when I have to jitwahirisha (after haydh) i have to wash my hair and hair will come out. How will that work??. will my ihraam be invalidated? Please advice...





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.IBU:





Hali ya kuwa katika ihraam kwa wenye kutia nia ya kuchinja ni Rahma ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa waja Wake ili wajihisi kuwa wako katika hali ya taqwa na wajihisi kuwa wanashiriki katika 'ibaadah za Mahujaji. Inapasa basi kuitumia neema hiyo kwa kujitahidi kubakia katika hali hiyo ya ihraam kwa kadiri mtu awezavyo.





Ikiwa umeosha nywele na zikang'oka wakati wa kuosha au wakati wa kuchana au ikiwa mtu kakata kucha kwa kusahau, yote hayo hayavunji Ihraam ya mtu. Lakini walioko Hajj wazingate sana kutokufanya makosa hayo kwani matendo mengineyo yaliyoharamishwa hupasa mtu kulipa fidia. Ama kwa hali ya muulizaji kuhusu Ihraam ndogo ya nje ya Hajj kwa ajili ya kuchinja hakuna fidia na kuchinja kwako kutakuwa kumekamilika In Shaa Allaah.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Tofauti Baina Ya Wanawake Na Wanaume Kukimbia Katika Twawaaf Na Sa’y



Alhidaaya.com





Swali:



Je kuna tofuati baina ya wanaume na wanawake katika kutekeleza tawafu na saiy? Katika kuharakiza mwendo?





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Ipo tofauti baina ya wanawake na wanaume katika kutekeleza Twawaaf na Sa’y. Katika Twawaaf inajulikana kuna kitu kinaitwa ‘Ar-Raml’ nayo maana yake ni kuchepuka (kukimbia kidogo kidogo) katika mizunguko mitatu ya mwanzo. Ar-Raml ina maana kwamba kuzunguka kwa mwendo wa haraka kwa hatua ndogo ndogo. Kisha anatakiwa atembee mwendo wa kawaida katika Twawwaaf zake nne za mwisho.





Katika Sa’y ambayo ni baina ya Asw-Swafaa na kuelekea Al-Marwaa mwanamume anatakiwa atembee kwa mwendo wa kawaida mpaka anapofika katika alama ya kijani, hapo atakimbia mpaka alama ya kijani nyingine. Ataendelea kuelekea Al-Marwaa kwa mwendo wa kawaida. Atakapofikia ataupanda (mlima) na kuelekea Qiblah, atanyanyua mikono na kurudia kusema kama alivyosema alipokuwa Asw-Swafaa. Atateremka Al-Marwah kuelekea As-Swafaa, akihakikisha anatembea sehemu zinazohusika na kukimbia katika sehemu zinazohusika.





Hikma hiyo ya kuwataka wanaume watembee kwa mwendo wa kukimbia ni kuonyesha nguvu zao na ukakamavu na wanawake hawakujumuika katika kitendo hiki kwani ni maumbile yao kuwa tofauti na wanaume katika nguvu. Hivyo, wanawake watatembea kawaida bila kuwa na haja ya kukimbia mchaka mchaka kama wanaume.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Uzushi Wa Unoadaiwa Ni Fadhila Za Siku Kumi Za Dhul-Hijjah



Alhidaaya.com







Swali:

Nimepokea e-mail iliyotumwa yenye kutaja fadhila za siku kumi kila siku kuwa ni jambo fulani limetokea na kadha kama inavyoeleza hapa chini. Je hii ipo dalili au ni katika uzushi?




Siku Kumi Bora

Allaah subhanahu wataala ameapa kwa masiku bora katika quraan takatifu sura 89 aya 1-2 isemayo : Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametusimulia vilivyotendeka na umuhimu wa siku hizi kumi bora za mfungo tatu (DhulHijja); Rasula-Allah atueleza sisi ummati wake kuwa, mwenye kufunga siku hizo hupata fadhla kubwa mno,kwani kila siku ina fadhila na kheri zake:





Siku Ya Kwanza Ya Mfungo Tatu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asema kuwa - "Ni siku ambayo Allah alimsamehe Nabiy Adam ('Alayhis-Salaam) kwa makosa yake".Mwenye kufunga siku hiyo, Allah humsamehe madhambi yake.




Siku Ya Pili Ya Mfungo Tatu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asema kuwa:-"Ni siku ambayo Allaah alikubali maombi ya Nabiy Yunus ('Alayhis-Salaam) ya kumtoa katika matumbo ya samaki".Mwenye kufunga siku hiyo, ni kama aliyefanya ibada ya mwaka mzima pasi na kufanya makosa.





Siku Ya TaTa Mfungo Tatu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asema kuwa:- "Ni siku ambayo Allaah aliitikia Dua ya Nabii Zakariya ('Alayhis-salaam) yakumpata mtoto". Mwenye kufunga siku hiyo, Allah huitikia dua yake.





Siku Ya Nne Ya Mfungo Tatu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asema kuwa:-"Ni siku ambayo alizaliwa Nabiy 'Issa ('Alayhis-Salaam) .Mwenye kufunga siku hiyo, Allah humuondolea matatizo na umasikini.





Siku Ya Tano Mfungo Tatu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asema kuwa:- "Ni siku alizaliwa Nabiy Muwsaa ('Alayhis-Salaam) "Mwenye kufunga siku hiyo, Allaah humtakasa na unafiki na humuondolea adhabu za kabori.





Siku Ya Sita Mfungo Tatu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asema kuwa:- Ni siku ambayo Allah alimfungulia Nabiy wake Muhammad(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kheri". Mwenye kufunga siko hiyo, Allah humuangalia kwa jicho la huruma wala hapati adhabu siku ya kiyama.





Siku Ya Saba Ya Mfungo Tatu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asema kuwa:- "Ni siku ambayo Milango ya Jahannam (Moto) hufungwa na hayafunguliwi hadi masiku kumi yatimie". Mwenye kufunga Allah humfungia Milango thelathini ya mambo mazito na humfungulia Milango thelathini ya mambo mepesi.





Siku Ya Nane Ya Mfungo Tatu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asema kuwa:- "Ni siku iitwayo Tar-wiya". Mwenye kufunga hupewa malipo ambayo hakuna ayajuwaye isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)





Siku Ya Tisa Ya Mfungo Tatu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asema kuwa:- "Ni siku iitwayo Arafat". Mwenye kufunga siku hiyo, hufutiwa makosa ya mwaka uliopita, na utakao kuja.





Siku Ya Kumi Ya Mfungo Tatu:- Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asema kuwa:-"Ni siku ya kuchinja Mnyama (itakuwa Iddi Kubwa), tone la kwanza la damu litakapo tona Allah humsamehe dhambi zake na za jamaa zake. Na mwenye kumpa chakula Masikini au akatowa sadaka siku hiyo, Allah atamfufua siku ya Kiyama kwa amali na mizani ya uzito, thawabu zake zitashinda uzito wa Mlima Uhud".



Please Do Not Forget To Enlighten Other Muslims By Forwarding This Mail


Jibu:

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Kwanza kabisa haifai kufupisha kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Manabii wote kwa kuandikwa hivyo kifupi (S.A.W) au (A.S) na pia haifai kufupisha kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) au kuwaombea radhi Swahaba na kadhaalika. Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo bayana. (Tumeondosha na kurekebisha vifupisho hivyo).





Hukmu Ya Kufupisha Thanaa (Kumtukuza Allaah) Na Kumswalia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Na Maamkizi Ya Kiislam





Tunasikitika kwamba siku hizi fitna za kusambaza uzushi zimezidi kutokana na wepesi wa mawasiliano kupitia mitandao ya jamii. Jambo linaloshangaza ni kwamba Hadiyth zilizo Sahihi zimejaa tele lakini hizo hazisambazwi kama zinavyosambazwa za uzushi. Ni dhahiri kwamba wanaofanya hivyo ima hawajui tofauti ya mafunzo sahihi na yale potofu ima kwa uchache wa elimu, au kwa pupa tu za kutafuta thawabu kwa njia za mkato ndiko kunakowasababisha wao kueneza haya mambo yasiyo na dalili wala asili. Lakini wanaghafilika ndugu hao kutambua madhara yanayopatikana kutokana na hayo wanayoyaeneza kila mara.





Moja ya dhara kubwa ni kupoteza mafundisho sahihi ya Dini yetu, na kueneza ya uongo na hivyo kutawala upotofu katika jamii ya Kiislam, Kwani kama wanavyosema wema waliotangulia, kuwa, bid’ah inavyoenea, ndio Sunnah hupotea.



Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate faida:



Hatari Ya Kueneza Hadiyth Dhaifu Na Visa Vya Uongo


Tumepekuwa vitabu mbalimbali vya Hadiyth vikubwa na mashuhuri na hakuna hata sehemu moja tuliyokuta kuna Hadiyth inayotaja Fadhila za masiku kumi ya Dhul-Hijjah kwa mtindo huo na kwa maelezo hayo! Vilevile ‘Ulamaa waliowahi kukumbana na maelezo hayo, wamesema kuwa ni ‘Mawdhuw’ – yaani ya kutungwa na si ya kweli.





Kuna hatari vilevile ya watu kutumbukia katika maonyo na makemeo aliyoyatoa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



((من كذب علي متعمدا فليتبوأ مقعده من النار)) متفق عليه

((Atakayeniongopea makusudi basi ajitayarishie makazi yake motoni)) [Al-Bukhaariy Na Muslim]



Ukiwa umeeneza mambo hayo na hali unajua kuwa si sahihi, basi tambua kuwa ushaingia katika walioelezwa ndani ya Hadiyth hiyo.





Na ikiwa una mazoea ya kueneza au kutuma kila unachopata ukidhani utapata thawabu kwa kufanya hivyo na hali huna uhakika nacho, au huna elimu ya jambo hilo kama ni sahihi au la, basi utakuwa pia una majukumu kwa kuwa Uislam umesisitiza sana elimu na umuhimu wa kuitafuta; hivyo kwanini ubakie katika ujinga na kutokufahamu unayotuma? Pia ikiwa hujui, ushaelezwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa), uulize wenye elimu na upambuzi, je, ulijaribu kufanya hayo kabla hujasambaza mambo hayo ya kutunga yenye kupotezea Waislam muda, juhudi, na hata ‘amali zao kwa kufanya yasiyo sahihi na yasiyo katika mafundisho ya Dini?





Na madhara mengine ni kwamba dhambi za mwenye kueneza uzushi huzidi kila uzushi unapozidi kusambaa na mwenye kuanza kueneza uzushi hubeba dhambi za kila mtu anayepokea na kujifunza uzushi huo:



عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال : ( من دعا إلى هدى كان له من الأجر من أجور من تبعه لا ينقص من أجورهم شيئاً ومن دعا إلى ضلالة كان عليه من الإثم مثل آثام من تبعه لا ينقص ذلك من آثامهم شيئاً) رواه مسلم

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: ((Atakayelingania kwenye uongofu atapata thawabu (ujira) wa yule atakayemfuata bila ya kupungukiwa chochote katika thawabu zao. Na atakayeelekeza katika upotofu atapata dhambi mfano wa dhambi za yule atakayefuata bila ya kupungukiwa chochote katika dhambi zao)) [Muslim]



Tumefanya utafiti mkubwa kutafuta kauli kama hizo kuhakikisha kama ipo kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inayotaja fadhila za siku hizo kama zilivyotajwa humu lakini hatukupata. Mojawapo ya matokeo ya utafiti ni kupata fatwa kutoka kwa ‘Ulamaa kutoka Markaz ya Fataawa walioulizwa kuhusu ujumbe huo nao pia wamehakikisha kuwa ni uzushi usio na dalili yoyote [Markaz al-Fataawa 24 Dhul-Hijjah 1424/16-02-2004].



Tunawanasihi ndugu zetu Waislamu wasome mada muhimu katika kiungo kifuatacho ili watambue hatari ya kueneza uzushi:




Hatari Ya Kueneza Hadiyth Dhaifu Na Visa Vya Uongo



Vilevile mtu anatakiwa asome mada hii hapa chini yenye kuhusu uzushi wenye kufanana na huo:





Uzushi Unaodaiwa Kuhusu Mambo Yaliyotokea Siku Ya Ashuraa Tarehe 10



Pia tunawaomba ndugu zetu kwamba wanapopata jambo lenye shaka kwanza wawe wanahakikisha kabla ya kutuma kwa wenzao kwani tutambue kuwa Muislamu inapomfikia kauli inayodaiwa kuwa ni ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) basi imeshakuwa ni waajib kwake kuhakikisha. Na ikiwa hakupata dalili yake ni bora kuacha kutuma kuliko kuleta madhara ya uzushi na kuzidisha ufisadi katika dini na jamii kwa ujumla kwa kupoteza mafunzo sahihi na kueneza mafunzo ya uzushi.





Kidokezo Cha Kuweza Kutambua Hadiyth Zisizo Sahihi Au Ujumbe Wa Uongo:



Ndugu Muislam, ukitaka kugundua haraka ujumbe ulioupata kwenye mitandao ya jamii, kwanza kitakachokujulisha kuwa ujumbe huo una utata na sio sahihi, ni kuwa, mara nyingi maelezo yaliyomo ndani ya ujumbe huo zikiwemo zinazosemwa ni Hadiyth, utakuta hazitajwi zilipotolewa, kama ni Hadiyth utaona haisemwi nani kasimulia, nani kapokea, kitabu gani, hakuna hata Imaam wa Hadiyth (Muhaddith) aliyetajwa kwenye Hadiyth hiyo n.k. Hayo yote yanatosha kumtia mashaka mtu kuhusiana na alichokipokea. Hivyo, endapo utapokea ujumbe au Hadiyth ambayo imekuja tu na kudaiwa kasema Mtume bila kutajwa zaidi ya hivyo… basi mrudishie aliyekutumia na muombe akueleze Hadiyth hiyo iko kwenye kitabu kipi, na nani kaisimulia na kama ni sahihi au dhaifu. Usiwe na pupa ya kueneza au kusambaza kwa wengine hadi kwanza upate uhakika 100%. Vilevile unaweza kutuandikia maswali@alhidaaya.com kuulizia masuala kama hayo na tukiweza In Shaa Allaah tutakusaidia haraka katika masuala hayo.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Vipi Kutekeleza Umrah



Alhidaaya.com



Swali:



Asalam Alaykum.



Tafadhali Naomba Mnijulishe Yanayopasa Kufanya Ktk Umra Toka Kukusudia Kwenda Makka Dua Za Kusoma Na Mahali Panapohusu Kusoma Na Yote Yanayo Mhusu Kufanywa Ktk Safari Hii. Nimekusudia Kwenda Ktk Kumi La Mwanzo La Mwezi Wa Ramadhwaan In Shaa Allaah Mwaka Huu.



Shukuran





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Kwanza tunatambua kutokana na barua yako kuwa wewe ni mwanamke hivyo haikupasi kwenda ‘Umrah peke yako bila ya kuwa na Mahram (mumeo au kaka zako au baba au ‘ami au yeyote mwenye undugu wa damu na wewe ambaye kisheria hawezi kukuoa). ‘Umrah kawaida unaweza kuikamilisha kwa siku moja tu, bali ni masaa machache tu utakuwa umemaliza ‘Umrah yako na sio kama Hajj ambayo inahitaji masiku kadhaa na taratibu ndefu.



Yafutayo ni ya kufanya kwa mpangilio:





Nia:



Nia ya ‘Umrah au ya ibada yoyote inakuwa moyoni na haitamkwi kwa ulimi. Kwa hiyo unapofika Miyqaat (sehemu ya kuanzia ibada yako hiyo, ambapo atakoga na kuvaa ihraam) utakapomaliza ndio utakuwa umetia nia yako moyoni kisha utaleta talbiyah ifuatayo:



لبيك عمرة، لبيك اللهم لبيك، لبيك لا شريك لك لبيك، إن الحمد والنعمة لك والملك لا شريك لك.

Labbayka '‘Umrah, Labbayka-Llaahumma Labbayk. Labbayka Laa Shariyka Laka Labbayk. Innal-Hamda Wan-Ni'imata Laka Wal-Mulk Laa Shariyka Lak.



"Nimekuitikia Ee Allaah '‘Umrah, Nimekuitika Ee Allaah nimekuitika, nimekuitika Huna mshirika Wako nimekuitika, hakika Sifa njema na Neema na Ufalme ni Vyako Huna mshrika"



Sehemu hiyo ya Miyqaat inategemea usafiri wako, kama ni wa gari basi ndio itabidi ufikie hapo kutia tohara. Na kama ni usafiri wa ndege basi tohara na nia hiyo itabidi utie tokea nyumbani.





Twawwaaf:



Ni kuzunguka mara saba kuanzia Hajarul-Aswad (jiwe jeusi) na kuanza kwa kusema:

بسم الله والله أكبر

Bismillahi Wa-Allaahu Akbar



Unapozunguza Twawwaaf, unaweza kusoma Qur-aan au kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) yaani Subhaana Allaah, au Kumshukuru, yaani Alhmadulillah, au Tahliyl yaani Laa Ilaah Illa Allah, au kuleta takbiyr yaani Allaahu Akbar, au kumswalia Nabiy (Swallah Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), au kusoma duaa zozote unazotaka. Lakini sio kusoma vile vitabu ambavyo vinauzwa na vimeandikwa duaa za kila Twawwaaf na du’aa yake, vitabu hivyo vimeandikwa na watu na havina ushahidi kutoka katika Hadiyth za Nabiy kuwa alifundisha du’aa hizo zilizopangiliwa kwenye hivyo vitabu, bali ni mambo ya uzushi na juu ya hivyo yanasababisha zahma za watu kwa kutembea pole pole huku wakisoma vitabu kwa sauti. Ni bora kusoma du’aa zako mwenyewe unazohitajia kwa matatizo yako na shida zako, kwani hiyo ni fursa ya kuomba kila unachokitaka na kutamani kuliko kusoma vitabu hivyo ambavyo wengi hawajui hata maana ya yaliyoandikwa ndani yake.



Na kila unapofika katika Rukn (nguzo) ya Yamani hadi katika jiwe jeusi unasema:



رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الاَخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ

((Rabbanaa Aatinaa Fid-Duniyaa Hasanataw-Wafil-Aakhirati Hasanataw-Waqinaa 'Adhaaban-Naar)).



"Rabb wetu Mlezi, Tupe duniani mema, na Aakhirah mema, na Utulinde na adhabu ya Moto"



Ukifika katika Hajarul-Aswad (jiwe jeusi) utaashiria kwa mkono wako kuelekea jiwe hilo na kusema

بسم الله والله أكبر

Bismillahi Wa-Allaahu Akbar



Utakuwa umemaliza Twawwaaf moja. Utaendelea hivyo hadi umalize Twawwaaf (mizunguko) zote saba.



Haifai kujilazimisha kwenda kuligusa au kulibusu Hajarul-Aswad na kusababaisha zahma na kusongamana zaidi na watu kwani inatosheleza kuashiria kwa mkono na thawabu ni zile zile, bali pengine ni zaidi kuliko mwenye kusababisha kusukumana na wenzake kwa ajili ya kutaka kuligusa jiwe.





Rakaa Mbili Katika Maqaamu Ibrahiym



Ukimaliza Twawwaaf ya saba utasogea upande wa Maqaamu Ibraahiym na utaswali Rakaa mbili, Rakaa ya kwanza utasoma Suwrah Al-Kaafiruun (Qul Yaa Ayyuhal-Kaafiruun) na ya pili utasoma Suwral Al-Ikhlaasw (Qul-Huwa Allahu Ahad).



Kwa hali ilivyo hivi sasa sehemu hiyo imekuwa ni zahma sana, hivyo haikupasi kujilizamisha kuswali karibu kabisa na Maqaamu Ibraahiym, bali unaweza kusogea mbali kabisa almuradi umeelekea hiyo Maqaam ya Ibraahiym. Ni makosa kusababisha zahma zaidi na msongamano na kuswali sehemu ambazo zina zahma kuzidi kuleta mashaka kwa Waislamu wengine.





Sa'y



Utakwenda Swafaa na kuanza Sa’y kwa kupanda juu ya kilima cha Swafaa na utaelekea Kaaba na kusema:



لا إِلهَ إلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ وهُوَ عَلى كُلِّ شَيءٍ قَديرٌ، لا إِلَهَ إلا اللهُ وَحْدَهُ أَنْجَزَ وَعْدَهُ، وَنَصَرَ عَبْدَهُ وَهَزَمَ الأَحْزَابَ وَحْدَهُ

Laa Ilaaha Illa-Allaah Wahdahu Laa Shariyka Lah, Lahul-Mulku Walahul-Hamd Wa Huwa 'Alaa Kulli Shay-in Qadiyr. Laa Ilaaha Illa-Allaah Wahdahu, Anjaza Wa'dahu Wanaswara 'Abdahu Wahazamal-Ahzaaba Wahdahu))



"Hapana Rabb Apasae kuabudiwa kwa haki ila Allaah, hali ya kuwa peke Yake, wala Hana mshirika Wake, ni Wake Ufalme na ni Zake sifa njema. Naye juu ya kila kitu ni Muweza. Hapana Rabb apasae kuabudiwa kwa haki ila Allaah hali ya kuwa peke Yake, Ametekeleza ahadi Yake, na Amemnusuru mja Wake, na Amevishinda vikosi peke Yake"



Utaomba du’aa zako unazotaka kisha utaanza Sa’y ukifika Marwa utakuwa umemaliza Sa’y moja, utapanda kilima na kusema hivyo hivyo na kuomba kwa kuelekea vile vile Ka’abah. Kuanzia Swafaa na kufika Marwa unahesabu kuwa ni moja, na kutoka Marwa na kufika tena Swafaa ni mbili hivyo hivyo hadi utamalizia Sa’y yako ya saba katika kilima cha Marwa.



Kama ni mwanamme atanyoa au kukata nywele, na wewe utakata tu kidogo nywele zako kama inchi moja hivi au chini yake.





Kunywa Maji Ya Zamzam



Utakunywa maji ya zamzam na kuomba du’aa unayotaka na hapa utakuwa umemaliza ‘Umrah yako.





Ya Kuzingatia:



Du’aa hizo ni kuzisoma kwa Kiarabu tu.



Unaweza kunywa maji ya Zamzam kabla ya Sa’y au baada yake upendavyo.

Kwa maelezo zaidi tafadhali soma mada hii ifuatayo ambayo iko www.alhidaaya.com katika kiungo kifuatacho:



Bonyeza hapa:



TARATIBU ZA HAJJ NA ‘UMRAH





Na Allaah Anajua zaidi
 
Back
Top Bottom