Ramadhan Special Thread
UJUMBE WA LEO:

Hakika wamefuzu Waislamu ambao katika Swala zao huwa wanyenyekevu
 
Husnul Khuluq (Tabia Njema)
Tabia Njema




Husnul Khuluq (Tabia Njema)



Imekusanywa na: Ummu Faraj





Alhidaaya.com





Sifa njema zote Anastahiki Allaah Rabb wa viumbe wote na rehma na amani zimfikie Nabiy wetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), Jamaa na Swahaba zake wote.





Hivi unajua ndugu yangu Muislam, Allaah Akulinde na Akuhifadhi, kwamba 'amali iliyo bora zaidi na inayopendwa na Allaah Mtukufu na Rasuli wake ni tabia njema?



Katika Hadiyth sahihi: Kutoka kwa Sa'ad bin Abiy Waqqaas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Hakika Allaah Anapenda tabia njema na Anachukia tabia mbaya"





Na tabia njema tumefahamishwa kuwa ni ukunjufu wa uso kutenda wema na kujizuia na maovu."





Hakika sisi Waislam wa zama hizi tumo katika tatizo kubwa la tabia, tabia za Kiislam ambazo watu wengi wa kheri wamezikosa, na zimekua kwa baadhi yao ni kama mazungumzo ya kawaida na wala hazihitaji kutekelezwa.





Tabia njema zinauweka Uislam kwenye daraja ya juu kabisa. Je, Hujui kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kwa hakika nimeletwa ili nikamilishe tabia njema" kulingana na maneno haya inaonyesha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekusanya umuhimu wote alIokuja nao kwa jambo la tabia njema na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akamsifu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Qur-aan Tukufu: Amesema:

وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٍ﴿٤﴾

Na hakika wewe uko juu ya kiwango adhimu cha tabia njema. [Qur-aaan Al-Qalaam:4]





Kwa hakika yamethibiti mambo matukufu makubwa kutokana na tabia njema, baadhi ya mambo hayo ni:





1- Wema haupatikani ila kwa tabia njema, kasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika hadithi ilyopokelewa na Nawwaas bin Sam'aan (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Wema ni tabia njema na dhambi "uovu" Ni ile iliyojificha kwenye moyo (inakutia wahka) ukachukia watu wajue. [Imepokelewa na Muslim]





2- Na tabia njema ni 'amali itakayo mpelekea mtu kuingia peponi kwa wingi kama aliyvosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth iliyopokewa na Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) Amesema: Na aliulizwa ni kitu gani kitakachowaingiza watu kwa wingi peponi? Akasema: "Kumcha Allaah na tabia njema" Na akaulizwa tena ni kitu gani kitakachowaingiza watu wengi kwa wingi motoni? Akasema "kinywa (mdomo) na utupu. [Imepokelewa na At-Tirmidhiy na akasema Hadiyth nzuri na sahihi]





3- Tabia njema ni katika 'amali nzito atakayoikuta Muislam katika miradi ya matendo yake siku ya Qiyaama.





Katika Hadiyth iliyopokelewa na Abu Dardaa (Radhwiya Allaahu 'anhu), Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: "Hakuna kitu kizito katika mizani ya Muumin siku ya Qiyaama kuliko tabia njema. Hakika Allaah Humchukia mtu muovu mwenye tabia mbaya." [Imepokelewa na At-Tirmidhiy, na ni Hadiyth Hasan]





4- Mwenye kujipamba na kusifika na tabia njema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amemdhamini nyumba katika jannah ya juu kabisa. Kama ilivyopokewa kutoka kwa Abu Umaamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mimi ni mdhamini wa nyumba "iliyopo" katikati ya Jannah kwa yule mwenye kuacha mijadala (ubishani) japo akiwa ana haki, Na nitakua mdhamini wa nyumba katika Jannah ya juu kwa mwenye Tabia njema."





5- Imepokelewa kutoka kwa mama wa waumini 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) akisema, nimemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika Muumin hupata kwa tabia yake njema daraja za aliyefunga na anayesimama usiku kufanya ibada."





6- Katika Hadiyth waliyoafikiana ma-Imaam Al-Bukhaariy na Muslim kutoka kwa 'Abdullaah bin Amru bnil-'Aaswi (Radhwiya Allaahu 'anhuma) amesema, alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema "Hakika aliye bora kati yenu ni yule mwenye tabia njema"





Hakika mwenye tabia mbaya ni mwenye kuzungumza maneno mabaya na vilevile Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema: "Hakika Allaah Huwarehemu waja wake wenye huruma, basi wahurumieni walio katika ardhi na Atawahurumia aliye mbinguni"





Hivyo basi, tabia njema inafuatana na kuhurumiana na Iymaan iliyokamilika.





Mwenye kuangalia hali ya hivi sasa utakuta ni mtihani kwetu na mbele ya Allaah (Subhanahu wa Ta'aalaa), utaona mambo ya ajabu, utaona uongo badala ya ukweli, utaona nguvu zikitumika badala ya upole, utaona khiyana badala ya uaminifu, utaona ghadhabu badala ya subira na kuondosha ghadhabu na kusameheana baina ya watu, utaona maudhi badala ya hisani, utaona ubakhili badala ya ukarimu, utaona uchoyo katika kuchukua sehemu ya kukaa au kufanya ibada, au katika vinywaji au chakula, badala ya kuathirika na kuwatanguliza wengine kabla yake, utaona kiburi badala ya unyenyekevu, kisha mtu atajiuliza katika nafsi yake hivi hawa ni Waislam kweli? Uko wapi uchaji Allaah? Iko wapi Iymaan? Kuko wapi kuoneana hayaa? Iko wapi huruma kwa maskini, yako wapi mapenzi na huruma kati ya Waislam???





Je, tuwafanye nini watu hawa? Tuwalipe uovu kwa uovu tukawaadhibu hapo hapo? Tukifanya hivyo hatutowazuia kitu, bali tutakuwa tumeshirikiana nao katika kueneza tabia mbaya. Lililo wajibu kwetu mimi na wewe juu ya watu hawa ni kufuata muongozo wa Allaah Mtukufu, nao ni; kuwasamehe na kufuta kabisa nyoyoni mwetu yale wanayotufanyia, na kubadilisha baya kwa kutenda jema na Allaah Mtukufu Anasema:



الَّذِينَ يُنفِقُونَ فِي السَّرَّاءِ وَالضَّرَّاءِ وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٣٤﴾



Na wanazuia ghadhabu, na wenye kusamehe watu. Na Allaah Anapenda wafanyao ihsaan. [Al-'Imraan: 134]



Na Akasema tena Allaah Mtukufu kuwasifu waumini:



وَيَدْرَءُونَ بِالْحَسَنَةِ السَّيِّئَةَ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عُقْبَى الدَّارِ ﴿٢٢﴾



Na wanaepusha ovu kwa zuri, hao watapata khatima njema ya makazi ya Aakhirah. [Ar-Ra'd: 22]



Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):



وَلَا تَسْتَوِي الْحَسَنَةُ وَلَا السَّيِّئَةُ ۚ ادْفَعْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ فَإِذَا الَّذِي بَيْنَكَ وَبَيْنَهُ عَدَاوَةٌ كَأَنَّهُ وَلِيٌّ حَمِيمٌ﴿٣٤﴾

Na wala haulingani sawa wema na uovu. Lipiza (uovu) kwa ambalo ni zuri zaidi; tahamaki yule ambaye baina yako na baina yake kuna uadui, atakuwa kama ni rafiki mwandani.

[Fusw-swilat: 34]





Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: katika Hadiyth iliyopokewa na Abu Dharr Jundub bin Junaadah na Abu Abdur-Rahmaan Mu'aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu 'anhum) kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa kasema " Muogope Allaah popote ulipo, na lifutishe ovu (baya) kwa jema, na tangamana na watu kwa tabia zilizo njema





Na hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amesema:



إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ

"Hakika mema yanaondosha maovu". [Huwd: 114]





Pamoja na hayo yote Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakulipiza kisasi kwa maudhi aliyofanyiwa yeye binafsi, ila yatakapovunjwa maamrisho ya Allaah au makatazo (maharamisho) Basi huadhibu kwa ajili ya Allaah.





Allah Atuwafiqishe Kwa Anayoyapenda Na Kuyaridhia Na Ajaalie Tuwe Wenye Kuyafanya Yalio Mema. Aamiin.



Wa Allahu A'lam
 
Tabia Njema


Matani Na Masikhara Yanayoruhusiwa Katika Dini



Imekusanywa na Ukht Ruqayyah A. Baahasan





Alhidaaya.com





Kanuni Za Mzaha



1. Jiepusheni na mzaha kwenye mambo ya Dini ya Kiislam.



Hiki ni kitu kimoja kinachotengua Uislam wa binaadam. Allaah Anasema:



وَلَئِن سَأَلْتَهُمْ لَيَقُولُنَّ إِنَّمَا كُنَّا نَخُوضُ وَنَلْعَبُ ۚ قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ﴿٦٥﴾لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ ۚ



Na ukiwauliza, bila shaka watasema: Hakika tulikuwa tunaporoja na tunacheza. Sema: Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayaat Zake na Rasuli Wake? Msitoe udhuru. Mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu. [Tawbah: 65- 66]



Ibn Taymiyah (Rahimahu Allaah) kasema kuwa: “Kumfanyia masikhara Allaah au Ishara Zake na Rasuli Wake ni kufru. Na mtu anayefanya hivyo amekufuru baada ya kuamini.” Hali kadhalika wale wanaokejeli baadhi ya Sunnah, kama kuwacheka watu wanaofupisha kanzu au kufuga ndevu, au wanawake wanaovaa Hijaab, au Niqaab n.k.



Shaykh Muhammad ibn ‘Uthaymiyn amesema katika al-Majmu’u ath-Thamiyn, 16/3: “Mambo yanayohusu shari'ah za Uungu, Utume, Wahy na Dini ni vitu vitakatifu vinavyopaswa kutukuzwa na kuheshimiwa. Si mambo ya kuchekeshana, na hairuhusiwi kutoviheshimu au kuvicheka au kuvifanyia mzaha. Mtu anayefanya hivyo ni Kaafir na inaonesha kama mtu huyo hamuheshimu Allaah, na Rusuli Wake na Vitabu Vyake na Sheria za Kiislamu. Mtu huyo lazima atubu kwa Allaah, na aombe msamaha na asuluhishe vitendo vyake na kujenga khofu kwa Allaah. Vile vile lazima amtukuze Allaah na azidishe mapenzi yake kwa Allaah kwenye moyo wake.”





2. Matani Lazima Yawe Yanayosadikika Na Ya Ukweli Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa Salam) amesema:



"Ole wake yule anayesema uongo kwa ajili ya kuwafanya watu wacheke.” (Abu Daawuud)

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa salam) katuonya kuhusu tabia hii waliyozoea watu na akasema:



"Binaadam anaweza akasema kitu kuchekesha wenzake na akaingia katika Moto wa Jahanam umbali mkubwa kwa tendo hilo." [Ahmad]





3. Msiwatishe Na Mkawashituwa Wenzenu Wale watu walio hodari na watendaji hususan, au wale wanaokamata silaha au chuma, au wanaotumia nafasi kwenye kiza kwa kutumia udhaifu wa wenzao na kuwatisha na kuwashtua. Amesema Abu Layla, “Swahaba wa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa salam) walikua wanasafiri na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa salam) na mtu miongoni mwao alisinzia na akalala. Baadhi yao walimfunga na kamba na alipoamka Alishtuka sana na kuogopa. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa salam) akasema:



“Haifai kwa Muislam kumogopesha Muislam mwenzake. [Abu Daawuud]





4. Kumkejeli Mtu Kwa Kupwesa Jicho Nyuma Yake Au Kumtolea Maneno Ya Ujeuri Watu wanatofautiana kwa uwezo wao wa kufahamu na kwa tabia zao; watu wengine ni dhaifu, na waliozoea kudharau wenzao wanaweza kuwafanya watu kama hao wawe ni kitu cha matani. Allaah kakataza tabia hiyo kwenye aayah hii kutoka Suwrah Al-Hujuraat: 11]



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَسْخَرْ قَوْمٌ مِّن قَوْمٍ عَسَىٰ أَن يَكُونُوا خَيْرًا مِّنْهُمْ وَلَا نِسَاءٌ مِّن نِّسَاءٍ عَسَىٰ أَن يَكُنَّ خَيْرًا مِّنْهُنَّ ۖ وَلَا تَلْمِزُوا أَنفُسَكُمْ وَلَا تَنَابَزُوا بِالْأَلْقَابِ ۖ بِئْسَ الِاسْمُ الْفُسُوقُ بَعْدَ الْإِيمَانِ ۚ وَمَن لَّمْ يَتُبْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ﴿١١﴾

Enyi walioamini! Wanaume wasiwafanyie dhihaka na kudharau wanaume wengineo asaa wakawa bora kuliko wao, wala wanawake kwa wanawake wengineo, asaa wakawa bora kuliko wao. Na wala msifedheheshane kwa kutukanana na wala msiitane majina (mabaya) ya utani. Ubaya ulioje kuita jina la ufasiki baada ya iymaan. Na yeyote asiyetubu, basi hao ndio madhalimu. [Al-Hujuraat :11]



Ibn Kathiyr kasema kwenye Tafsiyr yake:



“Imekusudiwa kuwatukana na kuwakejeli. Hii ni haraam na inahesabika kama tabia za wanaafik.”



Watu wengine wanacheka umbo la mtu, au mwendo wao au gari ya mwenzao. Hofu ya Allaah inaweza kumfanya mtu huyo awafikirie wale anaowacheka. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa salam) amesema:



“Msije mkafurahia hali mbaya ya ndugu yenu wa Kiislam. Allaah Anaweza kufanya kikupate kile ulichokicheka au kukifanyia utani”. [at-Tirmidhiy]



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa salam) alitutahadharisha juu ya kuwadharau na kuwashutumu watu kwa sababu tabia hiyo inaweza kuleta chuki kwenye jamii ya Kiislam. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa salam) amesema:



“Muislam yeyote ni ndugu wa Muislam mwenzake. Asije akamdharau au kumshutumu. Taqwa ipo hapa (na akaonyesha kwenye kifua chake mara tatu) kila Muislam kaharamishiwa kwa mweziwe; damu yake, mali yake, na heshima yake.” (Muslim)





5. Mzaha Usivuke Mipaka Watu wengine wanafanya masikhara sana hadi inakuwa ni tabia yao. Hii ni kinyume na na tabia za Waislam ambao wanatakiwa wawe ni watu wa dhati na makini. Masikhara ni mapumziko kutokana na kazi na udhati na umakini wa muda mrefu, ni burudani ya moyo. 'Umar bin ‘Abdil ‘Aziyz alisema:



“Ogopeni masikhara kwa sababu inazalisha chuki.”





Imaam an-Nawawiy amesema kuwa:



“Aina za matani yaliyokatazwa ni matani yaliyovuka mipaka na yakawa ni kawaida na tabia. Aina hi ya matani husababisha kucheka sana na kuushupaza moyo wa Muislam. Pia husababisha mtu asahau kumkumbuka Allaah na inazidisha watu kuumizana na kuzalisha chuki baina yao”





6. Lazima Ujue Cheo Cha Mtu Baadhi ya watu wanaweza kufanya mzaha na kila mtu bila kutofautisha cheo cha mtu au hadhi yake. Wanachuoni wanasema kuwa wazee wana haki zao na lazima tujue tabia ya mtu tunayemkabili. Usifanye masikhara na wajinga na watu usiowajua.

Kuhusu maudhui hii, ‘Umar ibn ‘Abdil-‘Aziyz alisema:



“Ogopeni masikhara, kwa sababu yanapunguza uungwana na uanaume.” Sa’ad ibn Abi Waqqaas alisema kuwa:



“Wekeni mipaka kwa vichekesho vyenu, kwa sababu mkivuka mipaka mtapoteza heshima na mnaweza kuchochea ujinga dhidi yenu”





7. Kiasi Cha Mzaha Kinachokubalika Ni Lazima Kisizidi Kadiri Ya Chumvi Kwenye Chakula Chako Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa Swallam) alisema:



“Msicheke sana kwa sababu kucheka sana kunaua moyo wa mtu.” [Sahiyh al-jaami’, 7312]



‘Umar ibn Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alisema:



“Yeyote anayecheka kupita kiasi anapoteza heshima. Na yeyote anayeshikilia kufanya kitu atajulikana kwa hicho kitu anachokifanya.”



Lazima tutahadhari na masikhara, kwa sababu yanaweza kumfanya mtu apoteze heshima baada ya kusifika kuwa ni mwenye heshima, na anaweza kufedheheka baada ya kuheshimiwa.





8. Kusengenyana Hairuhusiwi Kusengenya ni maradhi machafu. Baadhi ya watu wanafikiri kama wanaweza kuwasema wenzao na kukubalika kama ni masikhara, lakini imetajwa kwenye Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa salam) kuwa, “Kumsengenya ndugu yako ni kutaja kitu anachokichukia.” [Muslim]





9. Chagueni Wakati Muwafaka Wa Kutaniana Kama kwenye safari ya kwenda mapumzikoni nje ya mji au kwenye hafla jioni au kama mmekutana na rafiki na mnataka kupumzika na kupeana mazungumzo mazuri na mzaha; mkataniana kwa ajili ya kuzidisha mapenzi, urafiki na furaha kwenye nyoyo zenu. Au kama matatizo ya kifamilia yamezidi au mmoja wenu amekasirika mnaweza kufanya masikhara kupunguza fadhaa na mazonge na kujifurahisha nafsi zenu.



Ee! Muislam, Mtu alimwambia Sufyaan ibn ‘Uyaynah (radhiya Allaahu ‘anhu), “Masikhara si kitu sahihi, lazima kikatazwe.”

Akamjibu, “Bali ni Sunnah, lakini kwa wale wanaojua vipi kuyafanya hayo masikhara na wanaofanya masikhara kwenye wakati wake unaotakikana.”



Siku hizi, Ummah wa Kiislamu wanatakiwa wazidishe mapenzi baina yao na kupunguza uchoshi, lakini wamepitisha kiasi kwenye kufanya matani, mzaha na vichekesho. Imekua ni kawaida kwenye mikusanyiko, na watu wanapoteza wakati mwingi. Wanapoteza maisha na wakati wao kwenye mzaha na hadi kwenye magezeti yao kumejaa vichekesho na michezo.



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa salam) alisema:



“Kama mlikua mnajua (mna elimu) kama navyojua mie basi mungecheka kidogo na kulia sana.” (Katika Fat-hul Baariy imeandikwa kuwa, “Elimu” hapa inamaanisha kuwa kwa nguvu za Allaah na kisasi Chake kwa wale wanaokufuru, na kwa khofu inayokuwa katika mauti, na kwenye makaburi na kwenye Siku ya Qiyaamah.)



Waislam wanaume na wanawake lazima wachague marafiki waadilifu na wa dhati (si wapenda utani na wapotezaji muda) katika maisha yao. Marafiki hao watawasaidia kutumia wakati wao vizuri na watawaelekeza katika njia sahihi na kujitahidi kwa ajili ya Allaah. Marafiki hao watawasaidia kuwa Waislam wema na thabiti.

Bilaal ibn Sa’ad alisema,

“Mimi niliwaona Maswahaba wanapigania vitu, kwa masikhara, wanacheka na wenzao lakini ukiingia usiku wanakuwa kama Maimaam.”

Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhuma) aliulizwa,

“Je, Swahaba wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walikuwa wanacheka?”

Akajibu, “Naam, na Imani ilikuwa ndani ya nyoyo zao kama milima.”



Lazima tufuate mifano ya watu kama hao, waliokua mashujaa mchana na Imaam (wafuasi wacha wa Allaah wa Dini yetu) usiku.



Allaah Atuhifadhi sisi na nyinyi na wazee wetu siku ya Qiyaamah. Na tuwe katika wale watakaoambiwa siku hiyo:



أَهَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَقْسَمْتُمْ لَا يَنَالُهُمُ اللَّـهُ بِرَحْمَةٍ ۚ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمْ وَلَا أَنتُمْ تَحْزَنُونَ ﴿٤٩﴾

Je, hawa si wale ambao mliapa kwamba Allaah hatowafikishia kwa rahmah yoyote ile? (Leo wanaambiwa) Ingieni Jannah! Hakuna khofu juu yenu na wala nyinyi hamtohuzunika. [Al-A’raaf: 49]





Wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa Ahlihi wa Asw-haabihi.
 
Tabia Njema


Simu Katika Shariy'ah Ya Kiislamu-1

Imekusanywa Na: Sulaymaan ‘Iysaa





Alhidaaya.com





BismiLLaahir Rahmaanir Rahiym





Simu katika lugha ya kiarabu inaitwa “HAATWIF” au “AL-JAWWAAL” au “TILFUUN” vyovyote iwavyo simu ni chombo kitumikacho kwa ajili ya kuwasiliana.



Uislamu upo pamoja na wakati (Yaani haujapitwa na wakati kama wanavyodhani wasioujua Uislamu au maadui wa Uislamu kadhalika. Wakati upo na Uislamu.) Tazama watu wakisema nani wa kwanza kufika mbinguni? (si kwenye sayari kama tunavyosikia na kuona katika vitabu). Basi jawabu si mwengine bali ni Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Vile vile wakisema ni nani wa kwanza kufanyiwa upasuwaji? Basi jibu si mwengine bali ni Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam); bali kafanyiwa upasuaji mara mbili. Al-Muhim, mambo ya utumaji wa barua toka sehemu kwenda sehemu nyengine, mawasiliyano haya ya simu au mfano wake japo si katika sura iliyo sasa duniani ya mtandao huu wa simu ni vitu ambavyo Uislamu umetangulia zaidi – someni mkitaka historia ya Uislamu.



Mnamo mwaka 1865 liliasisiwa shirika la Nokia na mwaka 1972 ilitoa simu ya kwanza na ilikuwa simu hiyo ni kwa ajili ya matumizi ya askari tu. Na mnamo mwaka 1981 ikatoka simu nyengine tena, na mwaka 1992 ikatoka simu nyengine tena -hata nyakati zote hizi ilikuwa simu ikiuzwa bei ghali mno kwa kipindi hicho– hivyo ikapelekea kutomiliki chombo hichi muhimu katika mawasiliano baina ya mtu na mtu ila watu wenye uwezo kama vile wafanya biashara na watu wenye vyeo au nyadhi fulani. Kisha baada ya hapo ikawa simu inapatikana katika baadhi ya miji na nchi lakini bado ni kwa bei ya juu vile vile.





Hata hivyo kuna maswali ya kujiuliza kama Mwafrika wa Afrika Ya Mashariki lini iliingia simu kwako? Runinga (Television) ilivumbuliwa mwaka 1944, kwako iliingia lini?



Al-Muhim, yakupasa uelewe kuwa Uislamu upo na zama na zama, hali kadhalika upo na Uislamu -kuna baadhi ya simu zina mambo makubwa na ajabu na bei yake ni kubwa, hata hivyo hilo si lengo, lengo ni kuielezea simu na adabu zake katika shari’ah ya Kiislamu nianze kwa kusema.





Kila sifa njema anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na Swalah na salamu zimuendee Rasuli wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na Swahaba zake na wote walioongoka kwa uongofu wake mpaka siku ya Qiyaamah.



Ama baada ya utangulizi huo, hakika adabu ya simu kwa mujibu wa shari’ah tukufu ya Kiislamu haiepukiki kabisa na kuchukuliwa kifiqh katika adabu za ziara (yaani kutembeleana), na adabu za katika idhini (yaani kubisha hodi), na adabu za kuzugumza baina ya mtu na mtu kwa kulingana na hadhi na nafasi yake, kwa kulingana kadhalika na wakati na sehemu yenyewe. Vyote hivi vimeelekezwa na Uislamu kinaga ubaga (wazi wazi) kwa ajili ya kuyajenga maisha ya Muislamu chini ya tabiya zilizojaa upole na ulaini, na hakika pamethibiti katika Sahihi Muslim kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



“Hakika hauwi upole (ulaini) katika kitu ila hukipamba kitu hicho, na hauondolewi upole (ulaini) katika kitu ila hukiaribu.”



Na katika Hadiyth nyingine:



“Aliyenyimwa upole amenyimwa kheri zote” [Imepokelewa na Muslim.]



Adabu za simu ni adabu zitakikanazo kujulikana baina ya pande mbili:

1. Mpigaji simu

2. Mpokea simu japokuwa mpiga simu kwake ni muhimu zaidi kujipamba na adabu hizo kuliko mpokea simu.



Ndugu msomaji, bila shaka ni jambo lisilojificha kwako na mwengine kuwa simu ni chombo kinachosimamia mambo mengi na makubwa katika maisha ya kila siku yahusiyanayo na dini na pamoja na dunia. Sehemu ambayo ingeligharimu gharama ya muda wa kwenda na kurudi, mali nyingi, nguvu nyingi, kwa kupitia simu yamekuwa mambo hayo sasa yawezekana kufanyika kwa gharama chache bila kutumia nguvu nyingi katika hilo.



Hakika si mwengine anayestahiki kushukuriwa kwa neema hii ila Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa kumpa mwana Aadam akili iliyomuwezesha kuvumbua na hatimaye kutengeneza chombo hichi.





Tuanze basi kutaja adabu moja baada ya nyengine:





1. Kuhakikisha namba ya unayempigia

Hakikisha namba ya unayempigia kwanza kabla ya kuruhusu simu iite upande wa pili (kwa mwenzio) ili usje kufanya makosa kumwamsha aliyelala na asiyekuwa yule unayemuhitaji, au kumsumbua mgonjwa na kadhalika. Hivyo, hakikisha namba kwanza au tazama vyema simu yako katika sehemu ya majina na namba.



Na kwa upande wa mpokeaji ni vizuri pindi atakapogundua kuwa mpiga simu huyo hakuwa anakukusudia wewe, ni kumsamehe kwa usumbufu ambao utakua umeupata na kumfahamisha kuwa namba si hiyo umekosea, kama alikusudia kukuudhi basi utakua umepenyesha mshale katika moyo wake nawe una malipo na madhambi ni kwake.





2. Wakati wa kufanya mawasiliano

Pindi unapofanya mawasiliano -kumbuka kuwa- kama ilivyo kwako kuwa ni mwenye shughuli nyingine basi kadhalika wenzio mambo ni hivyo hivyo, wanahitajia muda wa mapumziko kwa sababu ya mihangaiko yao ya kimaisha, wanahitaji kulala, kula na kadhalika.

Kwa kuzingatia hayo, shari’ah ya Kiislamu tukufu ikampa fursa mwenye kutembelewa na mfano wake -katika hili mpigiwa simu-, ikampa haki ya udhuru (huwenda amelala, huenda ana jambo analisimamia, huenda… huenda… huwenda…) pasi na kusababisha aingie katika kusema uongo ambao umeharamishwa na shari’ah ya Kiislamu. Ndio utakuta mtu yupo ndani lakini kwa kuwa amelala amepumzika au ana mgonjwa anamhudumia –anajilazimisha kusema uongo “mwambie baba hayupo”, hali ya kuwa yupo mtu hajui kama anamfundisha mwanae uongo!! Mwanae huyu pengine naye aseme uongo au ashindwe na aseme kama alivyoambiwa “baba anasema hayupo”!!

Hivyo shariy’ah ya Kiislamu ili haya yasitokee ikasema,

وَإِن قِيلَ لَكُمُ ارْجِعُوا فَارْجِعُوا ۖ هُوَ أَزْكَىٰ لَكُمْ ۚ



Na mkiambiwa: Rejeeni! Basi rejeeni. Huo ni utakaso zaidi kwenu. [An-Nuwr: 28]



Ni juu yako kutafuta wakati muafaka ukichunga nyakati za kazi, nyakati za kula na mapumzko ya mchana (Qayluulah). Tazama tu kwa mfano vile shari’ah tukufu ya Kiislamu ilivyowaamrisha watumwa na wajakazi pamoja na watoto wadogo chini ya umri wa baleghe katika idhini katika nyakati tatu:

Kabla ya Swalah ya Alfajiri
Wakati wa Dhwahira (wakati wa Qayluulah)
Wakati baada ya Swalah ya ’Ishaa.
Ama ambao si watumwa wala wajakazi na ambao ni baleghe mfano wangu mimi na wewe, ikatutaka shari’ah ya Kiislamu kutaka idhini (kubisha hodi) kila wakati – kama Alivyoeleza Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa mapana na marefu kuanzia Aayah ya 58 mpaka Aayah ya 59 Suwrah-Nuwr. Na kama haitoshi, akakataza Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mtu kuja usiku wa manane nyumbani kwake pasina kutoa taarifa. Yote haya ni ili asije akakutana na yatakayomkera na kumuudhi kama vile kutokuwepo na usafi wa kuridisha upande wa nyumba yake, wanawe na kadhalika. Hali kadhalika kwa upande wake yeye asije akawakera kwa kuwakatiza usingizi wao na kadhalika.



Kwa ufupi ni kwamba chunga mnaasaba na muafaka wa kufanya mawasiliano na kama akakutaka udhuru mpaka wakati mwengine basi kubali kwa moyo mkunjufu. Na kama akakuambia subiri, basi subiri bila kuchukia juu ya hilo.



Hata hivyo hili la kuchunga wakata muafaka wa kufanya mawasiliyano si kwa kila mtu na kila ofisi na mashirika na makampuni _ kwani maeneo ya huduma ya jamii ambapo huwa wazi kwa ajili ya kuihudumia jamii usiku na mchana hawaingii katika hukumu hii – hili limechukuliwa Qiyaas (kipimo) katika faida ya Aayah ya kutaka ya kutaka idini “si vibaya kwenu mkaingia (bila ya kutaka idhini) katika nyumba ambazo hazikaliwi na watu ndani yake mna mahitajio yenu – na Allaah anajua mnayo ya dhihirisha na mnayo yaficha” 29 Suwrah An-Nuwr hapo inaingia kufanya mawasiliano wakati wowote ule na maeneo yatoayo huduma ya jamii kama vile – vituo vya afya vituo vya usalama (polisi, zima moto) vituo vya usafiri, mahoteli na kadhalika.





3 Muda wa miito ya simu

Yatakikana kulazimiana na sifa ya kati na kati; kuwa na dhana ya juu kabisa kuwa unayewasiliana naye kwa muda wote wa uitaji simu yake itakua amejua na kupata taarifa kuwa una haja ya kuzungumza naye, na wala haizingatiwi idadi ya miito ya simu kuwa iite mara tatu au uwasiliane naye mara tatu kama inavyoelekeza Hadiyth sahihi katika [Sahihi Al-Bukhaariy na Sahihi Muslim kuwa amesema Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



“Atakapobisha hodi (kutaka idhini) mmoja wenu mara tatu kisha hakukaribishwa basi na aondoke.”

kwani Hadiyth hii imebainishwa hekma ya kubisha hodi, nayo ni kwa ajili ya kuyahifadhi macho yasije yakaona yale ambayo mwenye nyumba au aliye ndani hakupenda yaonwe na mwengine. Akasema Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



“Hakika si vinginevyo kubisha hodi (kutaka idhini ya kuingia) ni kwa ajili ya kuyahifadhi macho.” Imepokewa na Al-Bukhaariy



Na hili la kuifadhi macho halipo katika simu, hata hivyo jiepushe na kukariri na kurudia rudia kumpigia simu “eti mpaka apokee”. Huenda akawa anaswali hivyo ukamuudhi yeye pamoja na kumtia tashwishi na wasiwasi katika Swalah yake na hata wenzake -kama ni Swala ya jamaa-. Au yupo katika kikao au mkutano pamoja na wenzake, kwani tunaona alikuja mwanamke mmoja kwa Imaam Ahmad (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akagonga mlango kwa nguvu na kwa muda mrefu, akatoka Imaam naye akiwa anasema “ugongaji gani huu? huu ni ugongaji wa kiaskari, naye akiwa amechukizwa na kitendo hicho.



Bali angalia wema waliotangulia, swahaba (Radhwiya Allaahu ’anhum) katika ukubwa wa ajabu zao pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) “walikua wakibisha hodi na kutaka idhini katika milango ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ncha za vidole ya mikono yao” ameipokea Hadiyth hii Imaam Al-Bukhaariy katika ktabu chake “Al-Adabul-Mufrad ” na Al-Qurtwubiy katika tafsiri yake (12/218).



Mfano wa hili la kupiga mlango kwa nguvu katika zama zetu hizi, ni kengele zilizowekwa katika milango na mageti yetu.





(inaendelea.../2)
 
Tabia Njema


Simu Katika Shariy'ah Ya Kiislamu-2

Imekusanywa Na: Sulaymaan ‘Iysaa





Alhidaaya.com







4-Dakika na muda wa maongezi



Kipimo chake ni maneno ya kiusuli yasemayo:

Kila sehemu pana mazungumzo husika.
Na kila mazungumzo yana kipimo husika.
Katika kipindi cha nyuma kidogo na mpaka sasa baadhi ya mitandao ya simu imekuwa ikitoa ofa ya kuongea muda mrefu kwa gharama ndogo, na mtu bila kujali kuwa huu ni wakati wa kazi au usiku watu wamelala na kadhalika, anarefusha mazungumzo kisa na mkasa ni kwamba leo ana ofa ya kuongea bure masaa 24 au 12 kwa thamani ndogo ya vocha alizoingiza katika simu yake.


5-Maamkizi ya Kiislamu kwa mwenye kufanya mawasiliano mwanzo na mwisho



Mpigaji simu ni kama vile mjaji katika adabu za ziara, hivyo, atakaporuhusu au kupokea simu nduguyo fanya haraka kumtolea salamu ya Kiislamu “Assalaamu ‘Alaykum” kwani maamkizi haya ni nembo kuu za Uislamu na ni ufunguo wa amani na salama si hivyo tu bali ni sharaf ya Ummat Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika mambo yanayowauma sana wasiokuwa Waislamu na haswa Mayahudi ni kuwaona Waislamu na kuwasikia wakitoleana salaam hii “Assalamu ‘Alaykum wa RahmatuLlaahi wa Barakaatuh” na ni lazima kujibu kwa kusema “Wa ‘Alaykumus Salam wa RamatuLlaahi wa Barakaatuh” kwa atakayesikia salaam hii.



Pamepokelewa katika Sunan Abiy Daawuud kutoka kwa Rabiu (Radhwiya Allaahu ‘anhu) anasema, alitueleza mtu mmoja katika kabila la bani Aamir kwamba yeye alitaka idhini kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa ndani kwake – akasema yule mtu wakati anabisha hodi, “niingie?” Akasema Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kumwambia mfanyakazi wake: “Toka na umfundishe mtu huyu kubisha hodi – mwambie aseme – Assalaamu ‘Alaykum – Je. niingie? Akasikia yule mtu akasema, “Assalaamu ‘Alaykum, je, ningie?” Akakaribiswa na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaingia.

Inafahamisha Hadiyth hii juu ya kutanguliza salamu kwa mwenye kufanya ziara – hiyo pia kwa mwenye kufanya mawasiliano na atangulize salaam ya kishari’ah – si kunyamaza au kuanza kwa kusema ‘hallo’ au ‘khabari’, ‘mambo’, n.k. Hata hivyo baadhi ya salaam ni vizuri.



Amepokea Imaam Muslim katika sahihi yake na Abuu Daawuud katika Sunnan yake kuwa Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema:

“Nilitaka idhini ya kuingia kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema ni nani huyu anayebisha hodi? Nikasema, “mimi”. Akasema Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), “mimi”, “mimi” – kama kwamba neno hilo lilimkera.”



Ikiwa itatokea mpokea simu hatakufahamu, akataka kujua nani anawasiliana naye, basi taja jina au sifa ya ujumla mfano ‘jina lako’ au ‘kun-yah yako’ na mfano wa hayo.


Kadhalika kujifahamisha kwa jina lako la Kun-yah kama kusema, “mimi Abuu Hannaan” au “mimi Abuu Hasan” au “Abuu Maryam” na kadhalika ikiwa jina kama hilo wewe si maarufu nalo si vyema, bali wema waliotangulia hawakuwa wakijitambulisha hivyo – hili ni kwa wale hayakua majina yao ni maarufu –, lakini waliojulikana sana kwa Kun-yah zao si vibaya kuyatumia kama ambayo alivyokuwa Abuu Bakr na Abuu Dharr na Ummu Haaniy (Radhwiya Allaahu ‘anhum) ambao walikuwa wakijulikana zaidi kwa majina hayo ya Al-kunaa kuliko majina yao ya asili.



Kisha kama ulivyoanza mazungumzo kwa salaam, kamilisha au funga mazungumzo yako kwa salaam. Ansema Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



“Pindi atakapofika mmoja wenu katika kikao chochote basi atoe salaam na atakapo kuamka ili aondoke basi atoe salaam tena, kwani salaam ya mwanzo si kwenye haki (si bora zaidi) kuliko ya mwisho.” [Amepokea Abuu Daawuud.]





6-Simu na mwanamke



Pindi awapo mmoja kati ya wenye kufanya mawasiliano ni mwanamke, basi na achukue tahadhari yake ya Kiislamu kutolainisha na kuiremba sauti yake, kwani Allaah (Subhanahu wa Ta’aalaa) Aliwakataza wake wa Nabiy Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mama wa Waumini (Radhwiya Allaahu ’anhunna) ambao hakuna yeyote awezae kuwatamani! (kwani kuna yeyote awezae kumtamani mama yake? Ila aliye punguwani) na walikatazwa kulainisha na kuremba sauti zao pindi waongeapo na Swahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum) katika zama tukufu na bora, zama za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum). Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):



فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا ﴿٣٢﴾

Basi msilegeze kauli asije akaingiwa tamaa ambaye moyoni mwake mna maradhi na semeni kauli inayokubalika. [Al-Ahzaab: 32]



Vipi kwa wanawake wa zama zetu? Uongeavyo na mumeo; mumeo mrembee na umpambie sauti na maneno pia. Zama zisizo bora, zama zilizojaa uovu na uchafu wa kila aina? Hakika kulainisha na kuremba sauti zao kunakatazwa zaidi. Hivyo mcheni Rabb wenu enyi wanawake wa Kiislamu msilainishe wala kuziremba sauti zenu pindi muongeapo na watu wasi Mahrim zenu (ajnabiy) iwe ndani ya simu au laa; kwa ufupi usiongee na mwanaume yeyote kama



Kadhalika si vizuri kuchukua muda mrefu kuongea na kutoa sauti kubwa isiyokuwa na haja ya kunyanyuliwa isipokuwa kiasi cha kusikilizana wao wawili tu. Na itakapokuwa hali ni kama hivi tulivyoeleza (yaani mwanamke anaongea kwa sauti laini iliyojaa kila aina za kurembwa, inakuwa ni haramu mwanaume kwa kuhofia fitna kuendelea kumsikiliza na kuongea nae hata kama mwanamke huyo anasoma Qur-aan kwa sauti iliyo jaa mahaba na kadhalika).



Na hapa tunajifunza pia, kwa mwanaume mwenye wivu na mwenye kuijua dini yake vizuri mchunga wa familia yake kimaadili na kitabia, kama anavyojihifadhi kiafya – basi na aijifadhi na yaliyo haramu, asiwe mwanamke ni wa kwanza kupokea simu, kuitikia, na kukaribisha mbisha hodi pindi awapo mwaname nyumbani.



Tumeona katika sehemu ya (5) Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ndiye aliyekuwa akiuliza nani mbisha hodi? Na si wake zake au watoto wake wa kike.



Imetukuka kimaadili nyumba ile ambayo ipo chini ya msimamizi, mchunga, mwenye akili na mwenye elimu, si mkali wala mwenye hasira, ila mwenye kumuudhi Allaah. Na imepata hasara nyumba ile ambayo haina msimamizi, mchunga mwenye akili, wala elimu. Simu ya baba mwenye nyumba kila mtu ni yake; ikiita tu mara mtoto kapokea, au mke wake, au mfanyakazi wake wa ndani, na kila mmoja kati ya wao aigombea si mdogo wala mkubwa!! Maskini aliyepiga hajulikani au ajulikana basi akiipokea mke ataongea kama vile anamjua, au kama ni baba yake mzazi aliyepotezana nae muda mrefu – Ya Allaah Rabb wetu – ni mara ngapi matatizo hutokea katika majumba yetu kwa sababu hizi? Ee Rabb wetu kwa upole Wako na sitara Yako tusitiri wewe ni Mwingi wa rahma na huruma tuhurumie, Aamiyn, Aamiyn.





7-Simu na miito (kengele) au miziki



Watu (watumia simu) katika hili wamegawanyika pande mbili zenye kupingana:

(1) Kuna watu ambao simu zao zikiita au ukiwapigia patasikika zikiita kwa kutoa sauti za pumbao miongoni mwa nyimbo na muziki na kadhalika, hili ni haramu.



(2) Na kuna watu ambao simu zao zikiita au ukiwasiliana nao patasikika katika simu zao sauti za Qur-aan ikisomwa au dhikri na kadhalika na pindi iitapo simu hapawezekani kabisa kusubiri mpaka msomaji afike mwisho wa Aayah wala dhikri au Hadiyth iishe. Hivyo, panatokeya kusimamisha au kupokea simu katika Aayah kabla ya jumla (sentensi) haijakamilika; kwani ni vigumu mno kusubiri kwa kuzingatia yafuatayo:



(a) Ikiwa aliyepiga simu mtu anayemdai muda mrefu na aliahidi kuwa leo saa fulani atawasiliana nawe ili mkutane sehemu apate kukulipa deni lako, kwa tamaa na hamu ya kulipwa deni lako, hutoweza kusubiri mpaka Aayah imalizwe!



(b) Ikiwa aliyepiga simu mathalani ni mmoja kati ya jamaa zako aliyekuwa amebaki na mgonjwa wenu hospitalini au nyumbani na hali yake haikuwa nzuri bali yu hoi taabani kadhalika katika hali kama hii pia hapawezekani kusubiri mpaka msomaji afike mwishoni mwa Aayah au jumla au pia Hadiyth iishe.



Hivyo kutampelekea kusimama au kupokea simu sehemu isiyoridhiwa kishariy’ah mfano Suwratul Anfaal Aayah 1:

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنفَالِ

“Wanakuuliza kuhusu ngawira…”

Akipokea simu kabla jumla haijaisha: يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنف

Maana inakua: “Wanakuuliza kuhusu pua”, na si “wanakuuliza kuhusu ngawira” (mali igawiwayo baada ya vita), hili nalo halifai (yaani kujaalia Qur-aan ndiyo mwito wa kukuita ili upokee simu au dhikri au mawaidha au du'aa na kadhalika).



Bali Qur-aan haikuletwa ila iwe ni mawaidha na kuwaonya na kuwaelekeza watu wazuri na kuwakataza watu mabaya tazama Suwrah Yaasiyn (69–70) haikuwa Qur-aan ila ni ukumbusho na Kitabu kibainishacho kila yanayohitajiwa ili imwonye aliye hai hai na ihakikike kauli (ya kuadhibiwa) juu ya Makafiri.



Hivyo kuifanya Qur-aan ndio mwito wa wewe kupokelea simu ni jambo baya kabisa mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) ni madharau ya Kitabu Chake na ni kejeli na maneno Yake.



Watu wema walikuwa wakiheshimu mno maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) bali hata ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mfano mmoja tu katika hilo kisa cha Imaam Daarul Hijrah, Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) alipokuwa akidarisisha (akifundisha) Hadiyth za bwana Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika kitabu chake “Al-Muwatwaa” katika Msikiti wa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) huko Madiynah, ghafla akang’atwa na nge (mdudu mkali mwenye sumu kali mno – baadhi ya watu wakiumwa na mdudu huyu hupoteza fahamu, wengine hutokwa na povu jingi mdomoni, wengine hubaki na maumivu muda wa masaa 12 na wakati mwengine masaa 24) nge huyo alimng’ata Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) mara tatu! Na kila mara Imaam anashtuka kidogo lakini hakatishi Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kumaliza akawaambia wanafunzi wake, angalieni hapa chini kuna nini? Wakafungua na kunyanyua tandiko alilokalia tahamaki wanamuona nge. (Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) akawaonyesha sehemu alizomuuma mara wanazikuta ni tatu!

Wakasema wanafunzi kwanini Imaam usikatize Hadiyth mara alipokuuma tu, tukamuua kisha ukaendelea na Hadiyth? Akawajibu Imaam maneno yenye maana: “Haikuwa kwangu ni rahisi kukatisha maneno ya bwana Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa sababu ya nge aliyening’ata!



Ona hiyo heshima waliyokuwa nayo, kisha tazama hali tulizo nazo sisi na maneno ya Allaah!! Tazama hali tulizonazo sisi na Hadiyth za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)!! Kwetu ni miito ya kutujulisha kwa kuna mtu kakupigia simu!! Yaa Allaah ya Kariym, Kwake pekee twashtakia unyonge wetu – tutengeneze Yaa Allaah hali zetu.





8-Kutorekodi maneno ya mwenzio



Adabu ya nane na ya mwisho, ni kutorekodi maneno ya mwenzio vyovyote yatakayokuwa maneno – ya kidini au kidunia ila kwa idhini yake au kwa kumjuilisha kabla –, hakika pamethibiti Hadiyth sahihi kama ilivyokuja katika Sunnan At-Tirmidhiy au Abuu Daawuud na Musnad Ahmad bin Hanbal (Rahimahum Allaah) kutoka kwa Jaabir bin Abdillaah Al-Answaariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



“Pindi atakapozungumza mtu na mtu kabla ya kuzungumza akatazama huku na huku basi hiyo ni dalili tosha kuwa hiyo ni amana.”



Imamu Raaghib (Rahimahu Allaah) anasema, siri zipo aina mbili:



(1) Ni ili aisemayo mwana mwana Aadam akataka ifichwe kwa kusema kwake mwishoni mwa mazungumzo: “Hii ni siri baina yangu mimi na wewe” au “ficha siri hii” au “usimwambie mtu haya.”



(2) Siri ijulikanayo bila kuambiwa bali mazingira yanatosha kukufahamisha hii ni siri usiitoe kama kujitahidi mzungumzaji maneno yenu yawe yenu tu – kwa kutoka pembeni au kukunong’oneza au kwa kuangalia huku na huku… na kadhalika.



Na simu inaingia katika hali zote hizi mbili, hivyo kusajili au kurekodi bila idhini yake ni khadaa na makosa, bali kosa kubwa kabisa ni kule kurekodi bila idhini yake na kumjuilisha kisha ukayaeneza yale mliyoongea naye kwa watu wengine, Hilo ni baya mno na ni kubomoa amana.



Allaah Atuhifadhi na yote mabaya Allaahumma Aamiyn.





Mwisho





Nimekusanya Adabu hizi toka sehemu tofauti, lakini kubwa zaidi nimerejea sana katika risala ya Shaykh Bakr bin 'Abdillaah Abuu Zayd (Rahimahu Allaah) aliyoiita “Aadabul-Haatwif.”
 
Tabia Njema




Tabia Za Mwenendo Wa Kiislamu

Imetarjumiwa Na: Naaswir Haamid

Imechukuliwa Kutoka Kitabu:
“Ujumbe Wa Uislamu.”





Alhidaaya.com





Shari’ah ya Kiislamu imeasisi na kulingania ustaarabu mbali mbali wa jamii. Wakati huo huo, imetahadharisha kuwepo adhabu siku ya Qiyaamah pindipo mtu atakaposhindwa kushikamana na Shari’ah hizo. Imaam Muslim amepokea kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Je munamjua nani muflisi?" Walijibu: ((Muflisi miongoni mwetu ni yule ambaye hana pesa wala mali.)) Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Muflisi ndani ya ummah wangu ni yule anayekuja siku ya Qiyaamah akiwa na Swalaah, Zakaah na Swawm, hata hivyo alikuwa akivunjia heshima, kusengenya, kutukana na kuwapiga wengine. Hivyo wenye kumdai wanalipwa kutokana na matendo yake mazuri. Iwapo mema yake yamemalizika, anaadhibiwa kwa matendo yao maovu hadi pale anapotupwa Motoni."





1. Adabu za Kula:



a. Anza kula kwa jina la Allaah (BismiLlaahir Rahmaanir Rahiym) na malizia kwa kumhimidi na kumshukuru Allaah (Al-Hamdul Lillaahi Rabbil-‘Aalamiyn). Kula kile kilichopo mbele yako kwenye chombo chako na tumia mkono wako wa kulia, kwa sababu mkono wa kushoto kawaida yake unatumika kwa kusafishia uchafu. [Al-Bukhaariy na Musim] wamepokea kutokana na simulizi ya ‘Umar Abi Salaam (Radhwiya Allaahu ‘anhu), kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amemwambia: "Litaje jina la Allaah, kula kwa mkono wako wa kulia na kula kile kilichopo mbele yako kwenye chombo."



b. Katu usilalamike au kukataa chakula kwa namna yoyote. [Al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kutokana na simulizi ya Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu)], kwamba: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), hakupatapo kuona kasoro kwenye chakula chochote. Iwapo amekipenda, atakila, iwapo hakukipenda atakiacha tu."



c. Jiepushe na kula au kunywa kupita mpaka kwa mujibu wa muongozo wa maneno ya Qur-aan:



يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ ﴿٣١﴾


Enyi wana wa Aadam! Chukueni mapambo yenu (ya mavazi ya sitara na twahara) katika kila mahala pa ‘Ibaadah. Na kuleni na kunyweni na wala msifanye israfu. Hakika Yeye (Allaah) Hapendi wanaofanya israfu. [Al-Aaraaf: 31]


Na kwa maneno ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): "Mtoto wa Aadam (mwanaadamu) hakupatapo kujaza chombo zaidi ya tumbo lake. Iwapo hakuna njia yoyote, basi iwepo thuluthi kwa chakula, nyengine kwa kinywaji na nyengine kwa pumzi zake." [Imesimuliwa na Ahmad].



d. Usishushie pumzi wala usipulizie ndani ya vyombo. Kutokana na Ibn ‘Abbaas Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Jihadharini na kurudushia pumzi au kupulizia ndani ya chombo." [Imepokewa na At-Tirmidhidy].



e. Kula pamoja na wengine, usiwe peke yako, kwani Mjumbe wa Allaah amesema: "Kusanyikeni kwenye chakula chenu ili kibarikiwe." [Imepokewa na Abu Daawuud na Tirmidhiy].



f. Iwapo umealikwa kwenye chakula na umemchukua mtu pamoja na wewe, ni lazima uombe ruhusa kutoka kwa mwalikaji. Kutokana na Abu Mas’uud Al-Badriy (Radhwiya Allaahu ‘anhu), mtu mmoja alimualika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwenye chakula pamoja na watu wengine wanne. Kuna mtu mmoja alimfuata Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Alipofika mlangoni, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia mwalikaji (mwenyeji):



"Mtu huyu amekuja pamoja nasi: Iwapo utaruhusu ataingia ndani, na iwapo hutamruhusu atarudi zake." Mwalikaji akasema: Ninampa ruhusa, Ee Rasuli wa Allaah. [Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim].





2. Adabu za Kuomba Ruhusa:



Kuna aina mbili za ustaarabu:



a. Zile ambazo zipo nje ya mlango wa nyumba:



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَدْخُلُوا بُيُوتًا غَيْرَ بُيُوتِكُمْ حَتَّىٰ تَسْتَأْنِسُوا وَتُسَلِّمُوا عَلَىٰ أَهْلِهَا ۚ

Enyi walioamini! Msiingie nyumba zisizokuwa nyumba zenu mpaka muombe ruhusa na muwatolee salamu wenyewe. [An-Nuwr: 24-27].



b. Zile ambazo zimo ndani ya nyumba:

وَإِذَا بَلَغَ الْأَطْفَالُ مِنكُمُ الْحُلُمَ فَلْيَسْتَأْذِنُوا كَمَا اسْتَأْذَنَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ

Na watoto miongoni mwenu watakapofikia baleghe, basi waombe idhini (wakati wote) kama walivyoomba idhini wale wa kabla yao. [An-Nuwr: 59].



Haya yote yanaazimia kuzilinda siri za nyumba na kuzipa nyumba faragha, kama ilivyooneshwa na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Kuomba idhini kunakusudia kulinda stara." [Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim].

Inashauriwa kutong’ang’ania kuomba ruhusa ya kuingia kwa mtu (kupiga hodi): "Ni lazima uombe ruhusa (kuingia kwa mtu) mara tatu. Iwapo hujaruhusiwa kuingia ndani, rudi zako." [Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim].





3. Adabu za Kuamkia (Salaam):



Uislamu umehimiza sana mila ya kusalimiana miongoni mwa wana jamii kwa sababu inapelekea kwenye mahabba na urafiki. Hili linaenda sambamba na Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): "Hautaingia Jannah hadi muwe Waumini, na wala hautakuwa Waumini hadi mpendane. Je, nikuelekezeni kwenye jambo ambalo linawafanya mpendane mmoja kwa mwengine? Kithirisheni maamkizi kwa amani miongoni mwenu." [Imepokewa na Muslim] – Kuitikia maamkizi ni lazima:



وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا ۗ

Na mtapoamkiwa kwa maamkizi yoyote, basi itikieni kwa yaliyo mazuri zaidi kuliko hayo.[An-Nisaa: 86].



Uislamu pia umetoa maelezo ya daraja kuhusu mwenye kuwajibika kutoa salamu juu ya mwengine. Kwa mujibu wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mpandaji amsalimie mwenye kwenda kwa miguu, mwenye kwenda kwa miguu amsalimie aliyeketi, na kikundi kidogo cha watu kwa idadi kiwasalimie kikundi kilicho kikubwa kwa idadi." [Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim]. Kwenye mapokezi moja kutoka Al-Bukhaariy, imeongezwa: "Mtoto au kijana amsalimie mtu mzima."





4. Adabu za Kikao:



a. Toa salamu juu ya waliohudhuria kwenye kikao au mjumuiko. Imesimuliwa kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Iwapo atakuja mmoja kwenye kikao basi na aseme: Assalaamu ‘Alaykum (yaani Amani Iwe Juu Yenu) Na anapoondoka afanye hivyo hivyo, kwani maamkizi ya mwanzo hayana umuhimu sana kuliko ya mwisho." [Imepokewa na Abu Daawuud na At-Tirmidhiy].



b. Haifai kumtaka mtu mmoja kuondoka (kumpisha) kwenye kikao chake kwa ajili ya mtu mwengine: "Wala asimfanye (asimtake) yeyote kati yenu mmoja wenu kunyanyuka kwenye sehemu yake na (yeye) kukalia sehemu yake; isipokuwa, tengenezeni nafasi (toeni nafasi, zitanue) zaidi kwa ajili ya wengine kuweza kukaa." [Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim].



c. "Iwapo mtu ataondoka kwenye sehemu yake kisha akarejea, atakuwa na haki zaidi na ile sehemu aliyoiacha." kama ilivyosimuliwa na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). [Imepokewa na Muslim].



d. Wala usiwatenganishe watu wawili waliokaa: "Hairuhusiwi kwa mtu kuwatenganisha watu wawili (kwa kujiingiza kukaa kati baina yao) isipokuwa watakapompa ruhusa." [Abu Daawuud na At-Tirmidhiy].



e. Usizungumze faragha na rafiki mbele ya mtu wa tatu: "Kama mupo watu watatu, haipasi watu wawili peke yao kuzungumza bila ya kumshirikisha wa tatu hadi mutakapojumuika pamoja na watu wengine, kwani hili litamsikitisha wa tatu." [Imepokewa na Al-Bukhaariy].



f. Wala usikae katikati ya duara au kundi la watu: "Amelaanika yule mwenye kukaa katikati ya watu waliokaa kikundi." [Imepokewa na Abu Daawuud].



g. Acha nafasi kwa wengine kuweza kukaa:



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قِيلَ لَكُمْ تَفَسَّحُوا فِي الْمَجَالِسِ فَافْسَحُوا يَفْسَحِ اللَّـهُ لَكُمْ ۖ وَإِذَا قِيلَ انشُزُوا فَانشُزُوا يَرْفَعِ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَالَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ دَرَجَاتٍ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ﴿١١﴾

Enyi walioamini! Mnapoambiwa: Fanyeni nafasi katika mabaraza, basi fanyeni nafasi; Allaah Atakufanyieni nafasi. Na mnapoambiwa: Inukeni, basi inukeni; Allaah Atawainua wale walioamini miongoni mwenu na waliopewa elimu daraja za juu. Na Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Al-Mujaadalah: 11].



h. Inapendekezwa kuzuia miayo kwa kadiri itakavyowezekana kwani ni alama ya uvivu: "Miayo unatokana na Shaytwaan, hivyo pale mmoja wenu anapokwenda miayo basi na ajitahidi kuuzuia kwa kadiri atakavyoweza, kwani iwapo mtu atalalama ‘Aaah!’ (pale anapokwenda miayo) Shaytwaan atamcheka." [Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim].



i. Ama kuhusu kwenda chafya, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Pindipo mmoja wenu anapokwenda chafya, basi na aseme: Shukrani zote ni za Allaah! Na ndugu yake Muislamu amwambie: Allaah Akurehemu! Ambapo naye atajibu: Allaah Akuongoze na Akutengenezee mambo yako vizuri." [Imepokewa na Al-Bukhaariy]. Pia inahimizwa kwa mtu, kama vile ilivyosimuliwa na Rasuli wa Allaah kutokana na simulizi ya Abu Hurayrah: "pale anapokwenda chafya, kufunika mdomo wake kwa mkono wake au guo na kuizuia sauti yake." [Imepokewa na Abu Daawuud na At-Tirmidhiy].



j. Acha kwenda mbweu pale unapokaa mbele ya wengine. Kutokana na Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhuma), mtu mmoja alienda mbweu mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ambapo Nabiy alimwambia: "Acha kwenda mbweu, walaji wakuu humu duniani ndio watakuwa wenye njaa kali zaidi siku ya Qiyaamah." [Imepokewa na At-Tirmidhiy na Ibn Maajah].



k. Mkusanyiko wa watu usiwe na mashughuliko ya mambo yasiyo na maana au yaliyo batili katika kumkumbuka Allaah na kufanya mazungumzo yenye manufaa duniani na katika Diyn. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kuhusiana na hili: "Mtu yeyote anayeinuka kutoka kwenye mkusanyiko ambapo jina la Allaah halitajwi ni sawaswa na wale wanaoinuka kutoka katika mzoga wa punda, na mkusanyiko huo (ambao ndani yake hatajwi Allaah) utakuwa ni chanzo cha huzuni kwao." [Imepokewa na Abu Daawuud].



l. Mtu asiwaelekee wale wanaokaa pamoja naye kwa kile kinachowachukiza.





5. Adabu Za Mikusanyiko:



Uislamu unaheshimu hisia za watu wanaokusanyika kwenye sehemu kufanya mikusanyiko yenye kupendeza na kupiga marufuku mikusanyiko yote yenye kusababisha watu kuchukiana. Hivyo, Uislamu unatoa muongozo kwa wafuasi wake kuwa ni wenye mwili msafi, usio na harufu mbaya, na nguo zilizovaliwa ziwe safi, zisizo na muonekano wa kuchukiza. Pia Uislamu unawaelekeza kumsikiliza mzungumzaji bila ya kumkatisha na pia kukaa pale ambapo watakuta nafasi bila ya kukanyaga shingo (unapopita na kuwapangua watu waliokaa kwenye Swafu Msikitini) za watu au kuwasababibishia usumbufu kwa kuwabana bana. Hili linaenda sambamba na maneno ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pale alipowahutubia Waislamu khutbah ya Ijumaa: "Yeyote anayeoga siku ya Ijumaa, akavaa nguo yake iliyo bora kuliko zengine, akaitia manukato, kisha akahudhuria Swalaah ya Ijumaa bila ya kuwapita pita (kuwapangua waliokaa) watu na akaswali rakaa anazoweza kuswali, kisha akakaa kimya pale Imaam anapowahutubia watu hadi akahitimisha Swalaah yake, basi Swalaah yake itakuwa ni malipo kwa wiki nzima hadi wiki nyengine." [Imepokewa na Abu Daawuud].





6. Adabu Za Majadiliano:



a. Msikilize mzungumzaji bila ya kumkatisha hadi amalize kuzungumza. Katika khutbah yake ya kuaga wakati wa Hajj, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: "Waombe watu wakae kimya." [Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim].



b. Zungumza kwa ufasaha ili kwamba wasililizaji waweze kukuelewa. Bibi ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha), mke wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Maneno ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yalikuwa ni yenye ufasaha hadi kwamba watu wote wakiweza kuyafahamu." [Imepokewa na Abu Daawuud].



c. Kuwa mchangamfu na zungumza kwa furaha. Hii ni kwa mujibu wa Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): "Usidogoshe aina yoyote ya matendo, hata kumpokea ndugu yako kwa uchangamfu." [Imepokewa na Muslim], na Hadiyth yake nyengine: "Neno zuri ni tendo jema." [Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim]. Al-Hussayn (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alisema: "Nilimuuliza Baba yangu kuhusu adabu za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) miongoni mwa wafuasi wake." ambapo alijibu: "Daima alikuwa mchangamfu, mwenye tabia nzuri na laini. Alikuwa sio mbughudhi, mwenye kelele, mtukanaji, mvunjaji heshima wala mdhurifu. Alikuwa ni mwenye kuliangalia kwa matarajio ya juu jambo asilolipenda bila ya kuwazuia watu wengine matumaini au kuwajibu kwa mtindo wa kuwakatisha tamaa. Alijizuia katika mijadala, kung’ang’ania hoja na kufanya makelele. Alijihadharisha na mambo matatu: Alikuwa sio mwenye kufanya fujo, kuona kosa au kuwafuatilia. Alizungumza pale tu anapotarajia kuwepo malipo. Pale anapozungumza, wasikilizaji wake waliinamisha vichwa vyao kimya kabisa na pale anapokuwa kimya wao wanazungumza. Walikuwa hawazungumzi kwa fujo mbele yake. Iwapo mmoja wao atazungumza mbele yake, watamsikiliza hadi amalize. Alikuwa akicheka na kushangaa pale wanapocheka au kushangaa. Alikuwa ni mwenye subira kwa watu wasioeleweka ambao walikuwa ni wabughudhi kwenye mazungumzo na maombi yao."





7. Adabu Za Mzaha:



a. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema kwa Swahaabah wake aitwaye Hanzalah, ambaye alidhani kwamba maisha yapo mbali na michezo na starehe ambaye alicheza na kupumbazana kwa unafiki pamoja na mkewe na watoto wake: "Lakini, Hanzalah, ufanye upya moyo wako muda hadi muda." [Imepokewa na Muslim]. Hapa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuelezea mtu huyo kwamba furaha zilizoruhusiwa na kujiliwaza mwenyewe ni yenye kukubalika kwa roho ya mwanaadamu ili kurudisha tena uhai na mishughuliko yake tena. Yeye, (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), pia aliwafunza kanuni za tabia njema kwa mnasaba wa mzaha, pale alipoulizwa kuhusiana na mzaha wake pamoja nao, kwa kusema: "Ndio, lakini ninazungumza ukweli." [Imepokewa na At-Tirmidhiy].



b. Mara moja alikuja bibi mzee na kusema: Ee Rasuli wa Allaah, niombee du’aa juu yangu ili niingie Jannah. Alimwambia: "Hakuna bibi kizee atakayeingia Jannah". Aliposikia hivi (bibi yule), alikwenda zake huku akilia. Akasema (Nabiy): Mwambie kwamba hatokuwa bibi kizee pale atakapoingia Jannah. Allaah, Mtukufu Anasema:



إِنَّا أَنشَأْنَاهُنَّ إِنشَاءً ﴿٣٥﴾فَجَعَلْنَاهُنَّ أَبْكَارًا ﴿٣٦﴾

Hakika Sisi Tunawaanzisha (huwrun-’iyn) uanzishaji. Tunawafanya mabikra. [Al-Waaqi’ah: 35-37]



c. Mizaha ya Rasuli wa Allaah haikuwa tu kwenye maneno, bali pia yalikuwa kwenye matendo. Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu), amesema: Bedui mmoja akiitwa Zaahir alikuwa akileta zawadi kutoka jangwani kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa pia akimpatia vitu anapoondoka. Alisema kuhusiana naye: "Zaahir ni ‘jangwa’ letu na sisi ni ‘mji’ wake." Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akimpenda, ingawa alikuwa na sura ambayo kwa wanaadam inaonekana haivutii. Siku moja, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimjia akiwa anauza bidhaa fulani, alimkumbatia kwa nyuma bila ya (Zaahir) kutambua. Zaahir akasema: “Niachie” Kisha akaangalia kwa nyuma na kumgundua Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), hivyo akaegemeza mgongo wake dhidi ya kifua cha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatangazia: "Nani atamnunua huyu mtumwa?" Zaahir akasema: “Ee Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), utatambua kwamba mimi siuziki”. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamjibu: "Lakini mbele ya Allaah, wewe sio mwenye kutouzika", ama alisema: "Mbele ya Allaah, wewe ni mpenzi mno." [Imepokewa na At-Tirmidhiy].



d. Mzaha usiwe ni wenye kunasibiana na kumuumiza au kumtusi Muislamu yeyote. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hapana ruhusa kwa Muislamu kumtisha Muislamu mwengine." [Imepokewa na Abu Daawuud]. Pia amesema: "Asichukue (Muislamu) yeyote mali za ndugu yake." [Imepokewa na Abu Daawuud na At-Tirmidhiy].



e. Mzaha usiwe ni wenye kumpelekea Muislamu kusema uongo kwa ajili ya kuwafanya wengine wacheke; hili linafahamika kutokana na maneno ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): "Ole wake yule anayesema uongo pale anapozungumza ili kuwafanya watu wacheke. Ole wake! Ole wake!"





8. Adabu za Kuomboleza:



a. Kitendo cha kuomboleza kinaelezwa kwamba kina lengo la kuifariji familia ya mfiwa, kuwapatia afueni na kupunguza majonzi. Rasuli wa Allaah amesema: "Muumini ambaye anamuomboleza ndugu yake kwa kufariki kwake atavishwa na Allaah nguo bora kabisa kwa heshima na hadhi ya juu Siku ya Qiyaamah."



b. Hakuna mfumo maalumu wa kuomboleza. Hata hivyo, Imaam Ash-Shafi’iy amependekeza kauli ya: "Allaah Akujaalie kuongezeka malipo yako, Akupatie faraja na kumsamehe maiti wako."



c. Inapendekezwa kutayarisha chakula kwa familia ya mfiwa kama inavyooneshwa wazi kutokana na Hadiyth ifuatayo: "Tayarisheni chakula kwa familia ya Ja’afar kwani wamepatwa na [jambo kubwa] lisilotegemewa."

9. Adabu Za Kulala:



a. Litaje neno la Allaah: “BismiLlaahir Rahmaanir Rahiym” na lalia ubavu wako wa kulia kwa mujibu wa maneno ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yaliyosimuliwa na Al-Baraa bin ‘Aazib: "Unapokwenda kitandani, chukua Wudhuu kama wa Swalah, kisha lalia ubavu wako wa kulia, na sema: Ee Allaah! Ninajisalimisha Kwako, na kuelekeza uso wangu Kwako, na nina matumaini ya jambo lolote juu Yako, na kimbilio langu ni Kwako, kwa mapenzi na khofu Kwako. Hakuna hifadhi wala kimbilio kutoka Kwako isipokuwa Kwako. Ninaamini Kitabu Chako, ambacho Umekiteremsha kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ambaye Umemtuma kama ni Mjumbe." [Imepokewa na Bukhariy na Muslim].



b. Usichelewe kulala hadi usiku (wa manane) na jitahidi kadiri uwezavyo kulala mapema isipokuwa pale panapo na udhuru au haja maalumu. Imesimuliwa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akichukizwa kulala kabla ya Swalah ya ‘Isha (jioni) na (kukaa na) kuzungumza baada yake. [Imesimuliwa na Al-Bukhaariy na Muslim].



c. Usilalie tumbo lako, kwani hili limekatazwa na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): "Mtindo huo wa ulalaji unachukizwa na Allaah." [Imesimuliwa na Abu Daawud].



d. Hakikisha kwamba hakuna chochote ambacho kinakuumiza kitandani mwako, kama ilivyopendekezwa na Rasuli wetu Mtukufu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): "Pindipo mmoja wenu anapokwenda kitandani, asafishe kitanda chake kwa pande la kitambaa chake kwani hajui nini kimelala ndani yake baada ya yeye kuondoka, na aseme: “Allaahumma bika wadhwa’tu janbiy, wabika afra’uh. Allahumma in amsakta nafsiy faghfir laha, wa in arsaltaha fahfadh-ha bima tahfadhu bihi ‘ibaadas-Swaalihiyn.” – “Ee Allaah! Kwa jina Lako nimejilaza ubavu, na kwa jina Lako ninainuka. Ee Allaah! Iwapo utaikamata roho yangu (yaani kuchukua maisha yangu), basi [nakuomba] unifanyie huruma, na iwapo utairudisha, basi ilinde kwa kile Unachowalindia waja wako Wacha wa Allaah." [Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim].



e. Kuwa muangalifu na ondosha kitu chochote kinachoweza kusababisha hatari. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Moto huu ni adui kwenu, hivyo munapotaka kulala uzimeni." [Imepokewa na Al-Bukhaariy].





10. Adabu Za Tendo La Ndoa:



a. Inapendekezwa, kabla ya kuingiliana na mkewe au mumewe kulitaja jina la Allaah. "Pale mmoja wenu anapomuingilia mkewe, iwapo atasema: “Kwa jina la Allaah! Tuepushe mbali kutokana na Shaytwaan, na muweke mbali Shaytwaan na (mtoto) utakayeturuzuku.” na iwapo mtoto atazaliwa kutokana na mjumuiko huu, Shaytwaan hatakuwa na mlango wa kumuumiza mtoto huyo." [Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim].



b. Mahusiano ya kifaragha baina ya mume na mke ni lazima yawekwe siri, kama ilivyosimuliwa katika Hadiyth ifuatayo: "Ambaye atakuwa na hadhi mbovu kulizo za watu wote mbele ya hesabu ya Allaah Siku ya Qiyaamah atakuwa ni mtu ambaye anaingiliana na mkewe au mwanamke ambaye anaingiliana na mumewe, kisha aidha yeyote kati ya hao anatoboa siri za (kitandani) za mwenza wake." [Imesimuliwa na Muslim].



c. Allaah wa Allaah amehimiza kuchezeana kimapenzi, ubembe wa mazungumzo na kubusiana kabla ya tendo la ndoa kama ilivyothibitishwa na maneno yake kwa Swahaba wake: "Usifanye tendo la ndoa na yeye isipokuwa pale anapokuwa na hamu/hali sawa sawa ya kufanya tendo la ndoa ili usimalize kabla yake yeye." Akauliza: Je nifanye hivi? Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Ndio, mbusu, mkumbatie na mtomase hadi uone kwamba ana hali ya shauku na hamu kama ulivyo wewe, kisha fanya naye tendo la ndoa pamoja naye." [Imepokewa na Imaam Ahmad].



d. Mume asiichopoe dhakari yake kutoka kwenye utupu wake hadi pale (mke) anapomaliza.





11. Adabu Za Kusafiri:



a. Rejesha amana kwa wenyewe, sawazisha malalamiko na madeni, na iache familia yako ikiwa na mahitaji ya kutosha. Usisafiri peke yako isipokuwa kwa haja ya dharura ambapo hujapata Swahiba. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Abiria mmoja ni Shaytwaan, abiria wawili ni Mashaytwaan wawili, lakini abiria watatu wanafanya kuwa ni msafara." [Imesimuliwa na Abu Daawuud, An-Nasaaiy na At-Tirmidhiy].



b. Unaposafiri, chagua Swahiba mwema na teuni mmoja wenu kuwa ni kiongozi. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Pindipo watu wawili wanapokwenda safarini, ni lazima wateue mmoja wao kama ni kiongozi." [Imesimuliwa na Abu Daawuud].



c. Ni lazima uwaarifu familia yako wakati unaporudi kwao. Usirejee nyumbani kwako usiku kwani hili halipendezi ili kwamba usione vitu ambavyo utavichukia. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Iwapo mmoja wenu hayupo nyumbani kwa muda mrefu, asirejee kwa familia yake usiku." Katika tamko jengine la Hadiyth, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimzuia mtu kurejea nyumbani usiku. [Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim].



d. Awaage kwa heri familia yake, marafiki na watu wake wa karibu kwani Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Iwapo mmoja wenu anadhamiria kwenda safarini, basi na aseme kwaheri kwa ndugu zake, kwani Allaah Mtukufu Atafanya ndani ya du’aa zao baraka kwake."



e. Arejee nyumbani kwake haraka baada ya kufanikisha lengo la safari yake. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Safari ni kipande cha masumbuko kwani inazuia kila msafiri (kwako wewe) kwenye huduma za kula, kunywa na kulala. Hivyo, pindipo mmoja wenu anapotimiza lengo la safari yake arejee nyumbani kwake haraka." [Al-Bukhaariy na Muslim].





12. Adabu Za Sokoni



a. Miongoni mwa sharti za adabu (njema) sokoni ni zile ambazo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Acheni kukaa mitaani [mabarazani]". Swahaba wakasema: ((Ee Rasuli wa Allaah, hatuna (njia) mbadala, hakuna sehemu nyengine yoyote ambapo tutakaa na kujadili masuala.)) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Iwapo ni hivyo, basi kwa suala hilo, tekelezeni majukumu yenu (kwa haki) ya njia [mabarazani]."



b. Swahaba waliuliza ni jambo gani linalohitajika kutelekezwa mtaani [majiani, mabarazani]. Alisema: "Kuangusha macho chini, kuondosha vikwazo mitaani, kuitikia maamkizi ya salaam, kuamrishana mema na kukatazama maovu." [Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim]. Katika simulizi nyengine, aliongezea: "Kuwasaidia wenye matatizo na kuwaongoza walemavu." [Imepokewa na Abu Daawuud]. Pia amesema: ((Jihadharini na matendo mawili yaliyolaaniwa" Swahaba wake wakasema: ((Ni yepi hayo matendo mawili yaliyolaaniwa?)) Yeye, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akajibu: "Mtu kwenda haja mbele za watu anapoonekana au kwenye sehemu za vivuli (sehemu ambazo watu wanapumzika)." [Imepokewa na Muslim].



c. Mpitaji njia aache kubeba zana au vyombo vya hatari kama ilivyoamrishwa na Nabiy Mtukufu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye amesema: "Pindipo mmoja wenu yeyote atatokezea kuingia Misikitini mwetu au sokoni (madukani) akiwa na mshale (mkononi) ni lazima aukamate ncha yake mkononi mwake, ili kwamba hakuna yeyote miongoni mwa Waislamu atakayepata jeraha kutokana nao." [Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim].





13. Adabu Za Kununua Na Kuuza



a. Kishari’ah, kuuza ni halali ndani ya Uislamu kwa sababu kumeegemezwa kutokana na kubadilishana manufaa baina ya muuzaji na mnunuzi. Hata hivyo, iwapo kuna dhara yoyote iliyojitokeza kwa upande wowote, makubaliano hayo yanakuwa ni haramu kwa mujibu wa Aayah ifuatayo:



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُم بَيْنَكُم بِالْبَاطِلِ

Enyi walioamini! Msiliane mali zenu kwa ubatilifu, [Al-Nisaa: 29].



b. Pia kwa mujibu wa Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), pale alipotokezea kupita rundi la kinacholiwa (mahindi). Alipenyeza mkono wake ndani ya rundi hilo na mikono yake ikatokeza kuwa na majimaji. Alisema kumwambia mmiliki wa rundi lile: "Ni nini hichi" Akajibu: “Ee Rasuli wa Allaah, hizi zimeharibika kutokana na kuanguka kwa mvua”. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatanabahisha: "Kwanini usiliweke hili (rundi la mahindi zilizorowana) juu ili kwamba watu waone? Yeyote anayetudanganya sisi sio miongoni mwangu (yaani mfuasi wangu)." [Imepokewa na Muslim].



c. Ukweli na maelezo yaliyo wazi (ya kasoro, kama ipo) inahitajika kwa mujibu wa maneno ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliyesema: "Pande zote mbili ndani ya mauziano ya biashara ina haki ya kubatilisha alimuradi hawajatawanyika. Hivyo, iwapo watazungumza ukweli na kufanya kila kitu dhahiri watabarikiwa ndani ya mauziano yao; lakini iwapo wataambizana uongo na kuficha chochote, baraka za mauziano yao zitazuiliwa." [Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim].



d. Huruma na makubaliano yaliyo haki yanahimizwa ndani ya biashara, kwani inamaanisha kujenga mahusiano mazuri ya muuzaji-mnunuzi kama ilivyotanabahishwa na Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): "Allaah Amjaalie rahma juu ya mtu ambaye ni mwepesi na makini anapouza, kununua au kuulizia malipo ya haki zake." [Imepokewa na Al-Bukhariy]. Hii ni kwa sababu Uislamu unahitaji huu wepesi wa makubaliano na kuvumiliana ndani ya masuala ya kuuza na kununua kuwaokoa watu kutokana na kuweka mbele maslahi ya dunia ambayo yanaharibu udugu na mahusiano ya kibinaadamu.



e. Jiepushe na kula kiapo unapouza, kwa mujibu wa maelekezo ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): "Jiepushe na kula kiapo sana pindipo unapouza (bidhaa zako), kwani mwanzoni inashajiisha biashara na baadaye inaleta hasara zote." [Imepokewa na Muslim].



Hizo juu ni baadhi ya tabia za mwenendo wa Kiislamu na adabu zake, na zipo nyengine zaidi ambazo zitahitaji muda zaidi wa kuzielezea. Juu ya hivyo, inatosheleza hapa kukumbushia kwamba hakuna tendo la binaadamu, la faragha au dhahiri, lisiloendana na maelezo na muongozo wa Qur-aan au Hadiyth za Nabiy ambazo zinatafsiri na kushurutisha.
 
Tabia Njema


Tabia Njema: Uadilifu





Alhidaaya.com





Alhamdu Lillaahi Rabil'aalamiyn) Allaahumma Swalli 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Swallayta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym wa Baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa Baarakta 'alaa Ibraahiym wa 'alaa aali Ibraahiym fil'aalamyna Innaka Hamiydun Majiyd.



Ndugu zangu Waislam Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema katika Qur-aan.



إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚ يَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ﴿٩٠﴾

Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini ili huenda mkapata kukumbuka. [An - Nahl: 90]





I. Nini Maana Ya Uadilifu?



Kilugha:

a. Hali ya kitu kuwa sawa kama inavyopasa kiwe.

b. Kuhukumu kwa haki bila ya upendeleo.



Kisharia:

a. Kukipa kila kitu haki yake inayostahiki.

b. Kuipa nafsi yako yale yaliyo ya haki tu.

c. Ni hali ya kuwa katikati baina ya kuchupa mipaka katika kufanya jambo au kujizuia kufanya jambo hilo bila ya kumdhulumu mwengine.





II. Hukumu Ya Uadilifu



Hukumu yake ni wajibu na ni fardhi kwa kila mtu - Muislamu au asiye Muislamu.

Kama Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anavyosema katika Suwrah An –Nahl: 90 iliyotajwa hapo juu.



Uadilifu ikiwa wa kauli, vitendo, ikiwa katika mahusiano ya mtu wa karibu au wa mbali ikiwa kwa rafiki au kwa adui ikiwa kwa kiongozi au waongozwaji n.k ni WAJIBU kwa kila muislamu.



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



وَإِن طَائِفَتَانِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ اقْتَتَلُوا فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا ۖ فَإِن بَغَتْ إِحْدَاهُمَا عَلَى الْأُخْرَىٰ فَقَاتِلُوا الَّتِي تَبْغِي حَتَّىٰ تَفِيءَ إِلَىٰ أَمْرِ اللَّـهِ ۚ فَإِن فَاءَتْ فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا بِالْعَدْلِ وَأَقْسِطُوا ۖ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ﴿٩﴾

Na ikiwa makundi mawili ya Waumini yakipigana, basi suluhisheni baina yao. Lakini mojawapo likikandamiza jengine, basi piganeni na ambalo linakandamiza mpaka lielemee kwenye amri ya Allaah. Likishaelemea, basi suluhisheni baina yao kwa uadilifu, na timizeni haki. Hakika Allaah Anapenda wanaotimiza haki. [Al-Hujuraat: 9]





III. Hadiyth Za Nabiy Zenye Kuhimiza Uadilifu.



Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (Watu saba watakuwa katika kivuli cha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) siku ambayo itakuwa haina kivuli isipokuwa cha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) 1. Imamu Muadilifu. 2. Kijana aliyekulia katika Ibada, 3. Mtu ambaye moyo wake umefungamana na miskiti…) [Imewafikiwa na Al-Bukhaariy na Muslim]

Kutokana na Abdillaah ibn ’Amr Ibnil ‘Aas (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (Hakika waadilifu mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) watakuwa katika Minbar za nuru: Ambao wanafanya uadilifu katika hukumu zao na watu wao na mambo mengine) [Imepokelewa na Muslim].



Kutoka kwa Iyaadhw Ibn Haamir (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: nimemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (Watu wa Jannah ni watatu: Mwenye ufalme ambaye muadilifu aliyeridhiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), na mtu ambaye ana huruma mpole kwa jamaa wa karibu na Waislamu, na anayejizuilia kuomba na aliyefika mbali katika kujizuilia) [Imepokelewa na Muslim]





IV. Fadhila Za Uadilifu



Malipo mema kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



1. Waadilifu watapewa viriri/minbari za nuru na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

2. Watakuwa chini ya kivuli cha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) siku ambayo hapatakuwa na kivuli chochote isipokuwa Chake Yeye Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).





Fadhila za Uadilifu ndani ya Jamii

1. Kuondoka kwa aina zote za dhulma.

2. Kuenea utulivu wa nafsi na Jamii.

3. Kuwa na heshima upendo na kuaminiana mfano:

a. Baina ya mke na mume

b. Baina ya mtoto au mzee

c. Katika uchaguzi n.k

4. Kuondoa rushwa katika Jamii

5. Kuondosha choyo, uhasidi, wivu na ujambazi





V. Nyanja Za Uadilifu Ndani Ya Jamii



Uislamu ndio uliokuja na uadilifu na umetilia hima utekelezwe katika nyanja zote za maisha ya mwanaadamu kama vile:



1 Nyanja za maneno na vitendo

2 Nyanja zote za mahusiano: Jamaa au si jamaa, rafiki au adui.

3 Katika kuhukumu (Jaji, Qaadhi, Sheha, Polisi n.k)

4 Uadilifu katika vipimo.



1. Uadilifu katika maneno



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema katika Qur-aan



وَإِذَا قُلْتُمْ فَاعْدِلُوا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۖ وَبِعَهْدِ اللَّـهِ أَوْفُوا ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ ﴿١٥٢﴾

Na mnaposema basi fanyeni uadilifu japokuwa ni jamaa wa karibu. Na timizeni ahadi ya Allaah. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni (Allaah) kwayo mpate kukumbuka. [Al- An'aam: 152]



2. Uadilifu katika kuandika

وَلْيَكْتُب بَّيْنَكُمْ كَاتِبٌ بِالْعَدْلِ ۚ

Na aandike baina yenu mwandishi kwa uadilifu. [Al-Baqarah: 282]



3. Uadilifu katika Vipimo; Mizani, ujazo, mita

وَأَوْفُوا الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِ ۖ

Na timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu. [Al-An'aam :152]



4. Malipo siku ya kiama yatakua ya uadilifu (Hakuna dhulma)



وَنَضَعُ الْمَوَازِينَ الْقِسْطَ لِيَوْمِ الْقِيَامَةِ فَلَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْئًا ۖ وَإِن كَانَ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ أَتَيْنَا بِهَا ۗ وَكَفَىٰ بِنَا حَاسِبِينَ ﴿٤٧﴾

Na Tutaweka mizani za uadilifu Siku ya Qiyaamah; basi nafsi haitodhulumiwa kitu chochote. Na japo ikiwa uzito wa mbegu ya haradali, Tutaileta. Na inatosheleza Kwetu kuwa Wenye kuhesabu. [Al-Anbiyaa: 47]





VI. Faida Za Uadilifu




a. Muadilifu atakuwa katika amani duniani na akhera (atapendwa)




b. Daima atakua anajimilki na hamilikiwi na wengine




c. Ataridhiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na viumbe pia




d. Viumbe wataepukana na shari zake




e. Ni sababu ya kupata cheo, mafanikio na maendeleo ya mtu




f. Ni njia ya kufanikiwa kimaisha




g. Sababu ya kupata utulivu na amani katika Jamii ya Waislamu




h.

Inaondosha fitna katika jamii





VII. Hasara Za Kuacha Uadilifu Katika Jamii




a)

Ni jambo rahisi sana kubomoa mfumo na uongozi




b)

Ni mbolea ya kukuza udikteta na ukandamizaji katika Jamii




c) Ni ufisadi mwepesi wa kufisidi dhamira na nafasi za wana Jamii




d) Ni chanzo kikubwa cha machafuko ya Jamii (hasa pale dhuluma inapogeuka na kuwa ubaguzi wa wazi




e)

Kutakuwepo matabaka na uadui katika Jamii




f)

Chanzo cha maovu.





VIII. Aina Za Uadilifu



1. Uadilifu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

Kutomshirikisha na yeyote katika ibada na sifa zake kwa:



a. Kumtii bila kumuasi kwa lolote.

b. Kumtaja na kumdhiriki katika hali zote

c. Kumshukuru bila kukosa



2. Uadilifu wa Mtu Katika Nafsi Yake



a. Ni kuilazimisha nafsi kufanya mema na kuacha mabaya kwake na kwa Jamii.

b. Aifanye nafsi iwe na uwiano katika matendo yake. Asichupe mipaka katika kufanya jambo wala asizembee. Akifanya hayo atakuwa anaidhulumu nafsi. Na anayeidhulumu nafsi yake atakuwa anadhulumu wenzake.



3. Uadilifu Wa Mtu Kwa Binaadamu Wenzake



a. Kuwapendelea kheri anazozipendelea nafsi yake

b. Kuthamini utu wao mali na heshima zao

c. Kujiepusha na kuwaudhi na kuwafanyia maovu.



4. Uadilifu Kwa Walio Sawa Na Yeye



a. Kutowatendea wasiyoyataka.

b. Kuwaepusha na maudhi

c. Mambo yote hayo yanapelekea mapenzi baina yao.

d. Yasipotekelezwa patatokea ufisadi ambao hautokei isipokuwa pahala pasipokuwa na uadilifu



5. Uadilifu Kwa Walio Chini Yake.

Kiongozi kwa wanaoongozwa.



a. Kuwepesisha mambo

b. Kuondosha shida

c. Kutotumia maguvu

d. Kutetea haki na usawa, kutodhulumu na kuwa muadilifu.



6. Uadilifu Kwa Walio Juu Yake. Raia kwa viongozi



a. Kutii viongozi utiifu wa kweli

b. Kuulinda uongozi

c. Ufuasi wa uhakika wa kutumia akili.



7. Uadilifu Kwa Viumbe Wengine Wa Mazingira




1.

Kuwaonea huruma wanyama na viumbe wengine.


2.

Kuwatumia kwa mujibu ya maamrisho ya Allaah


3.

Kuwapa wanyama haki zao na yeye kunufaika na wanyama kwa mujibu wa sharia.





IX. Misingi Muhimu Inayojenga Na Kudumisha Uadilifu Katika Jamii




1.

Uadilifu wa viongozi



Kiongozi ni mtu mwanzo anayepaswa kuwa muadilifu kwani yeye ni kigezo, na atakapotengenea kiongozi katika kuondoa maovu mfano. (dhulma, rushwa, zinaa, n.k) basi Jamii yote itatengenea.



Mfano wa viongozi waliofanikiwa katika kutekeleza uadilifu ni Sayyidna ‘Umar Ibnu-Khatwaab na ‘Umar Ibn ‘Abdul-‘Aziyz.



2. Msingi wa usawa kwa wote

Usawa ndiyo lengo linalokusudiwa na Uadilifu



Suwraah/Aina za Usawa katika Uislamu:



- Usawa wa mwanamke na mwanamume katika kutekeleza wajibu wa kisharia na malipo

- Usawa baina ya binaadamu wote katika Jamii

- Usawa baina ya watoto (kama katika kuwapa zawadi n.k).

- Usawa wa wanaoshitakiana katika mahkama/korti.

- Usawa katika kulindwa damu, mali na familia za kila Mmoja.

- Usawa katika utekelezwaji wa hukumu na kuhukumiwa.

- Usawa katika kupata malipo ya duniani na thawabu za Akhiraah kwa kila afanyae wema.



3. Uadilifu kwa wana Jamii wote.



Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (Muogopeni Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na fanyeni uadilifu baina ya watoto wenu)



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۚ

Lakini mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi mmoja tu au ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. [An-Nisaa: 3].



4. Kupinga aina zote za dhulma.

Dhulma ndiyo kinyume cha uadilifu malipo yake ni mabaya mno

Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِن نَّصِيرٍ ﴿٧١﴾

Na madhalimu hawana yeyote mwenye kunusuru. [Al-Hajj: 71]



Na Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

أَلَا لَعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الظَّالِمِينَ﴿١٨﴾

Tanabahi! Laana ya Allaah iko juu ya waliodhulumu. [Huwd: 18]



Na mwisho ndugu zangu Waislamu naiusia nafsi yangu pamoja na nyinyi kufanya uadilifu na kuepukana na dhulma kwani:



Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Iogope du’aa ya mwenye kudhulumiwa, hakika hiyo (du’aa ya mwenye kudhulumiwa) haina baina yake na baina ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kizuizi).”



Na pia akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) “Iogopeni dhulma, hakika dhulma ni giza siku ya Qiyaama.”





Wa BiLLaahi At-Tawfiyq
 
Tabia Njema


Umuhimu Wa Kuwa Na Rafiki Mwema



Imekusanywa na: Ummu ‘Aliy



Alhidaaya.com







Bismillahir-Rrahmaanir-Rahiym. Alhamdulillaahi Rabbil Aalamin, waswalatu wassalam alaa RasuliLLaahi (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).



Ningependa kuwahusia enyi ndugu zangu kuhusu umuhimu wa kuwa na marafiki wema, kwa vile ni kawaida kwa sisi binaadamu kuhitaji marafiki.



Kuchagua rafiki mzuri ni lazima kwa ajili ya kuhifadhi dini yetu. Waislamu wakiwa na tabia nzuri na wenye kufuata njia ya Allaah, basi uislamu utakuwa na nguvu, ni hivyo ndivyo inavyotakikana. Kufanya urafiki na watu wema wenye tabia nzuri, ni mojawapo ya njia ya kutufanya sisi kuwa kwenye njia iliyonyooka.



Nabiy Muhammad ((Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)) amesema: “Mtu yamkini kufuata dini ya rafiki yake, kwa hivyo muangalie unaemfanya rafiki.” [Abu Dawuud na At-Tirmidhiy].



Lazima tuchague marafiki ambao wako radhi na dini yetu na tuepukane na wale ambao hawako radhi na dini yetu. Na tukiona marafiki zetu matendo yao sio mazuri, ni lazima tuepukane nao kwasababu tunaweza tukaiga tabia zao ambazo zinakwenda kinyume na dini yetu. Kutangamana na marafiki ambao wanakwenda kinyume na njia ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), inaweza ikatubadilisha tabia, fikra na mwenendo wetu. Lakini vile vile inatupasa kuwatendea wema.



Katika Hadiyth, Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema: "Mfano wa rafiki mwema na rafiki mbaya ni kama ule wa muuzaji wa misk na mhunzi. Basi kwa muuzaji wa misk, imma atakunusisha, au utanunua kwake ama angalau utafurahia harufu nzuri kwake. Na kwa yule mhunzi, imma atakuchomea nguo au utapata harufu mbaya kutoka kwake.” [Al-Bukhaariy na Muslim].





Katika tafsiri ya Hadiyth hii, Imam An-Nawawiy alisema: Nabiy ((Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)) alilinganisha rafiki mzuri na muuzaji misk kwasababu, kwa rafiki mzuri mwenye tabia ya upole, na elimu, utapata faida kwake. Na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitukataza kukaa na wale wenye kufanya maovu.



Mwanachuoni mmoja amesema: “Kuweka uhusiano mzuri na watu wema, matokeo yake ni kupata elimu iliyo na faida, tabia nzuri, na matendo mema, ambapo kuweka uhusiano na waliopotoka, huzuia hayo mema yote.”



Allaah Anasema katika Qur-aan:



وَيَوْمَ يَعَضُّ الظَّالِمُ عَلَىٰ يَدَيْهِ يَقُولُ يَا لَيْتَنِي اتَّخَذْتُ مَعَ الرَّسُولِ سَبِيلًا ﴿٢٧﴾

Na siku dhalimu atakapotafuna mikono yake akisema: “Laiti ningeshika njia pamoja na Rasuli.



يَا وَيْلَتَىٰ لَيْتَنِي لَمْ أَتَّخِذْ فُلَانًا خَلِيلًا ﴿٢٨﴾

Ee ole wangu! Laiti nisingelimfanya fulani kuwa rafiki mwandani.





لَّقَدْ أَضَلَّنِي عَنِ الذِّكْرِ بَعْدَ إِذْ جَاءَنِي ۗ وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِلْإِنسَانِ خَذُولًا ﴿٢٩﴾

Kwa yakini amenipoteza mbali na Ukumbusho baada ya kunijia.” Na shaytwaan kwa insani daima ni mwenye kutelekeza. [Al-Furqaan 25: 27-29].





Allaah (‘Azza wa Jalla) Anasema pia:

الْأَخِلَّاءُ يَوْمَئِذٍ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ إِلَّا الْمُتَّقِينَ﴿٦٧﴾

Rafiki wapenzi Siku hiyo watakuwa maadui wao kwa wao isipokuwa wenye taqwa. [Az-Zukhruf 43: 67].





Ibn Kathiyr ameeleza kuhusu Aayah hii, kisa ambacho kimepokewa na ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa, urafiki wowote ambao si kwa ajili ya Allaah, hugeuzwa ukawa wa uadui isipokuwa chochote kilichokuwemo kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).



Watu wawili ambao ni marafiki kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa); mmoja wao akifariki, hupewa bishara nzuri kuwa amejaaliwa kuingi Jannah (Peponi), basi humkumbuka rafiki yake na kumuombea dua akisema: “Ee Rabb wangu, rafiki yangu alikuwa akiniamrisha kukutii na kumtii Rasuli Wako Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na alikuwa akiniamrisha kufanya mema na alikuwa akinikataza kufanya maovu. Na aliniambia kuwa nitakutana na Wewe. Ee Rabb wangu, basi usimuache kupotea baada ya mimi kuondoka, na muoneshe haya ulionionesha mimi, Na Uwe Radhi naye kama Ulivyoridhika na mimi.” Basi ataambiwa: “Laiti ungelijua aliyoandaliwa rafiki yako, basi ungefurahi sana na ungelia kidogo.” Kisha rafiki yake akifariki, roho zao zinakusanywa, na wote wanaambiwa watoe maoni kuhusu kila mmoja. Basi kila mmoja anamwambia mwenzake: “Ulikuwa ndugu mzuri kabisa, mwenzangu mzuri kabisa, na rafiki mzuri kabisa.” Na mmoja wa wale marafiki wawili wasioamini anapokufa na kupewa bishara za moto wa Jahannam, humkumbuka rafiki yake na kusema: “Ee Rabb wangu, rafiki yangu alikuwa akiniamrisha nikuasi na nimuasi Rasuli Wako Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), na alikuwa akiniamrisha kufanya maovu na kunikataza kufanya mema, na akaniambia sitokutana na wewe. Ee Rabb wangu, usimuongoze baada ya mimi kufa, na Muoneshe haya ulonionesha mimi, na Usiwe Radhi nae kama ambavyo Huko Radhi na mimi.” Kisha yule rafiki mwengine akifa na nyoyo zao zikikusanywa, wote wawili wanaambiwa watoe maoni kuhusu kila mmoja. Basi kila mmoja anamwambia mwenzake: “Ulikuwa ndugu mbaya kabisa, mwenzangu mbaya kabisa, na rafiki mbaya kabisa.”



Kwa hivyo, ni katika urafiki mwema ndio Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Humuokoa aliyepotea na kumuongoza aliyekosa. Faida ya kutangamana na marafiki wema ni kubwa kupita kiasi na In Shaa Allaah itakuwa wazi zaidi kwetu siku ya Qiyaamah, kama tulivyoona kwenye Aayah na visa tulivyotaja.



Na katika Hadiyth nyengine pia, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuamrisha kutangamana na Muumin peke yake. [Abu Dawuud na At-Tirmidhiy] Na pia, mtu atakuwa na wale awapendao. [Al-Bukhaariy na Muslim].



Kwa hivyo, tukiwapenda na kuwaandama waliopotoka, lazima tujiogopee mwisho wetu.



‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alisema: "Tangamana na watu wema wapole, utakuwa mmoja wao; na epukana na watu waovu usalimike na maovu yao."



Muumin ni kioo cha ndugu yake, akiona makosa ya Muumin mwenzake inampasa amueleze kwa uzuri na kumsaidia kurekebisha kosa hilo.



Ibn Hazm amesema: “Yeyote anayekukosoa, anajali urafiki wako. Na yeyote ambae anachukulia wepesi makosa yako, basi hajali urafiki wako.”



Kwa hivyo ikiwa tunafikiria kuhusu mwisho wetu, lazima tutambue kuwa,wale ambao wanatuepusha na Kumkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na kumfuata Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), wale ambao hawatukumbushi Swalaah zetu na wala hawatupi mawaidha mazuri kuhusu Dini yetu, basi wao kweli ni maadui si marafiki zetu.



Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa ) Anasema:



وَمَن يَتَوَلَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا فَإِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْغَالِبُونَ ﴿٥٦﴾

Na atakayemfanya Allaah kuwa ni Mlinzi na Rasuli Wake na wale walioamini, basi hakika kundi la Allaah ndio washindi. [Al-Maaidah: 56].





Hitimisho



Namuomba Allaah Atujaaliye tuwe miongoni mwa waja Wake wema na Atupe katika marafiki ambao watatuepusha na ghadhabu Yake, na watakaotuelekeza kwenye njia ya Allaah na Radhi Zake Namuomba Allaah Atujaaliye tuwe miongoni mwa waja Wake wema ambao watakutana kwa furaha na kusifiana kama kile kisa tulichokisikia. Na Atujaaliye tuingie katika Jannah Yake ya Firdaus kwa Rahmah Zake. Aamiyn
 
Amekopeshwa Kwa Pesa Za Kigeni, Je, Anaweza Kulipa Kwa Pesa Za Kwao?
Maswali: Uchumi (Biashara-Kazi)
SWALI:


ASSALLAM ALAIKUM



suala langu liko hivi:Mimi nilitumiwa (U.A.E Dirham 20,000) sawa sawa na (TZ shiling millioni 3 na nusu) mwaka 1996 , lakini huyu sasa hivi anataka mimi lazima nimlipe dirham , lakini mimi nimepokea tanzania shillingi million 3 na laki 5 kwa wakati huo ,yeye anataka mimi nimlipe dirham wakati mimi nimepokea tanzania shilingi.Je nafaa mimi kulipa dirham


wabillah tawfiq






JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.


Kuhusu hilo deni kwanza inatakiwa umshukuru sana huyo aliyekukopesha au kukupatia kwa sababu nyingine hizo pesa kutokana na sababu zifuatazo:


Amekufadhili na amekufanyia ihsani kwa muda wote huo wa miaka 14 hadi leo bila ya kukulazimisha ulipe.



Juu ya hivyo yeye anataka umlipe kama alivyotoa yaani Dhs 20,000/- na hali wakati huo ilikuwa thamani yake kama unavyosema kuwa ni hizo Shilingi za Tanzania 3.5 milioni. Huwezi kuona mangapi uliweza kufanyia hizo pesa hadi sasa? Na kama ni biashara, labda ungekuwa umetajirika na kupata zaidi na zaidi ya hizo!


Tambua kwamba kwa hivi sasa hizo Dhs 20,000 kwa hivi sasa, thamani yake ni ndogo sana kuliko ilivyokuwa hapo alipokupa mwaka 1996 na kwa hiyo angeliweza kufaidika nazo kwa kufanya mengi kuliko sasa. Kadhalika ana haki hiyo kwani yeye alitoa Dirhamu na hakutoa Shilingi wakati alipokutumia, na hivyo ni haki yake kupewa kilekile alichotoa.

Isitoshe mtu huyo hakutaka faida au Ribaa au kudai kiwango cha hizo Dirhamu kwa thamani ya hivi sasa ambayo bila shaka ingekuwa kubwa zaidi na maradufu ya alivyotoa! Je, bado huoni kama ni uungwana mkubwa aliokutendea?


Hivyo ni wajib wako hivi sasa kukumbuka ihsani yake na umrudishe kama anavyotaka kwa Dhirhams, na tena tunakshauri umrudishie haraka iwezekanayo na umshukuru kwa ihsani yake na hasa kwa vile hakutaka umlipe thamani ile ile na umuombee Allaah (Subhanaahu wa Ta’ala) Ambariki.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Amepatiwa Kazi Na Aliye Na Mahusiano Yasiyo Halaal Na Dada Yake- Je Kazi Hiyo Ni Halaal Kwake?
Maswali: Uchumi (Biashara-Kazi)
SWALI:




Asalam alaikum warahmatullahi wabarakatu sheikh nauliza mnisaidie naomba mnijibu haraka kwa kuwa kazi yenyewe nimeambiwa kuanza baada ya wiki ni hivi dada yangu alikuwa na mpenzi wake ambae ni kinyume na dini yetu tukufu sasa dada yangu alishasafiri siku nyingi takriban miaka mitatu sasa nimekutana na yule mpenzi wake nimemuomba anitafutie kazi amekubali na ameshanipatia kazi je? Kazi hiyo itakuwa halali kwangu? Au haram naomba nijibiwe upesi ili nisijekuanza







JIBU:




Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.




Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kutafuta na kupata kazi.

Kazi ni njia nzuri ya Muislamu kutafuta na kufanya. Na sharti ya kazi ambayo Muislamu anafaa afanye ni ile ambayo ni halali kisheria.




Mapenzi ambayo huyo bwana anafanya na dada yako ni makosa na madhambi watapata wao. Lako ni kujaribu kuzungumza na dada yako aache dhambi hilo kwani zinaa ni miongoni mwa madhambi makubwa katika Uislamu. Kwa hivyo, ikiwa kazi ambayo utamfanyia ni ya halali hakuna ubaya wowote wako kufanya ili upate ajira.




Makosa aliyofanya dada yako na huyu bwana ni tofauti na kazi ya halali utakayomfanyia upate chumo la halali. Lakini pia kumbuka kuwa kumfuata mtu kama huyo mwenye kushiriki haraam na dada yako, ni kumpa nguvu ya kuendeleza maasi yake na pia wewe kujiduniza zaidi kwake na kuonesha kuridhia kwako na mahusiano yao ya haraam hadi kumfuata yeye akusaidie ilihali ndiye anayemuharibu dada yako. Lazima wewe uwe ni mtu mwenye msimamo, na suala hilo hata asiyeshikamana na Dini hatoweza kulikubali kuona mtu anacheza na dada yake. Na ikiwa ushaanza kazi kwake au kwa njia yake, basi unaloweza kufanya ni kumpa nasaha huyo bwana aache maasi yao na mfahamishe madhara yake na madhambi makubwa yanayopatikana katika mahusiano hayo yao na mtake arejee kwa Mola wake na afanye toba. Na hilo laweza kufanikiwa zaidi ikiwa wewe ni mtu wa msimamo na unatekeleza mafundisho ya Dini yako, lakini ikiwa wewe mwenyewe huna mwelekeo na ni mtu ovyo ovyo kama wao, basi ujue hakuna taathira yoyote itakayopatikana.







Na Allaah Anajua zaidi
 
Amepokea Bidhaa Si Zake, Kuzifungua Ni Pombe, Afanyeje?
Maswali: Uchumi (Biashara-Kazi)
SWALI:




Mmi ni mfanyabiashara ya vitabu vya kiislamu. Siku moja nilinunua bidhaa, ikabidi nitangulie mzigo ufuatie baadae. Nilipofika ofisi ya gari nikakuta boksi lenye sura kama la kwangu, nikalichukua mpaka dukani. SubhanaLlaah nilipofungua ni makopo ya bia, nifanyeje?

Nilisita kuurudisha mpaka mwenyewe akaufuata. Mzigo wangu uliletwa kabla huyo jamaa hajaja. Jee ilikuwa niurudishe, niutupe au nifanyeje?




JIBU:




Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu upokeaji wa bidhaa ambazo si zako.




Ifahamike kuwa Muislamu ni mtu ambaye yuko makini sana katika kufanya mambo katika maisha yake hapa duniani. Uliwajibika mwanzo kabisa kuutazama mzigo kabla ya kwenda nao dukani kwako kwani kufanya hivyo kungekupunguzia mengi katika taabu hizo ulizozieleza. Na kila wakati unatakiwa uwe hivyo kuhakikisha mambo na vitu kabla ya kujiingiza, kwani usipofanya hivyo huenda ukapata shida ambayo hukuitarajia kabisa.




Mbali na hayo, Muislamu anakuwa ni muaminifu na uaminifu unakuja hapa ni kuwa ulichukua mzigo wa watu kimakosa na hivyo unatakiwa umjulishe mwenye mzigo huo aufuate kuuchukua haraka kwani wewe kukaa nao pia haifai kwani ni katika mambo yaliyokatazwa kuyahifadhi Muislamu.




Tanbihi: Inatakiwa kama Waislamu tusaidianeni katika uchaji Mungu na wema wala tusisaidiane katika uadui na madhambi. Kwa minajili hiyo inatakiwa tuwe waangalifu sana katika utumaji wa bidhaa kupitia usafiri wowote. Kwa hiyo, ni wajibu wako kwa kuwa gari hilo linapakia pombe na vitu vingine vya haramu nawe umejua utafute usafiri wa gari jingine ambalo halitakuwa kama hilo. Ikiwa mwenye gari ni Muislamu ni wajibu wako kumueleza kuwa hilo linalofanyika ni makosa. Ikiwa atajirekebisha endelea kutuma kupitia kwa gari lake na lau ataendelea basi tafuta usafiri mwengine wa Muislamu na ikiwa hakuna Muislamu basi tuma kupitia kwa mwengine ambaye si Muislamu lakini habebi pombe au vitu vya haramu.




Na Allaah Anajua zaidi
 
Anafanya Kazi Inayohusu Ubebaji Wa Maboksi Yenye Ulevi
Maswali: Uchumi (Biashara-Kazi)
SWALI:

Asalam aleikum warahmatulahi. kuna rafiki yangu twafanya kazi kiwanja kimoja {EUROPE} sehemu ambayo niko mimi, ni sehemu ya mboga. lakini huyu rafiki yangu hufanya sehemu ya kulord makeji ya supermarket, sasa swali langu katika keji hizo kuna maboksi mengine yana tembo. nilazimu kwake kufanya hivyo. niliwahiyi kumwambiya lakini. akaniambiya kuwa yeye, hufanya kila siku. nainapotokeya basi lazima afanye hivyo. kwa sababu yeye hufanya sehemu ya goods in, inapotokeya upungufu wa watu ndiyo yeye hupelekwa huko.

kufanya hivyo, sasa nauliza kwa hayo niliyoyaeleza kwake ni haramu kufanya hivyo. shukran. Mungu awazidishieni ilimu na awape subra amen amen.









JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.


Shukrani kwa swali lako zuri. Hakika hilo ni tatizo linalowapata watu wengi wenye kwenda Bara Ulaya kwa sababu moja au nyingine lakini sababu kubwa ikiwa ni kupata ajira yoyote ile.


Uislamu umehimiza sana Muislamu awe ni mwenye kutafuta na kufanya kazi ili aweze kujikimu kimaisha na kuweza kusaidia jamaa zake. Dini yetu tukufu imefanya ufanyaji wa kazi kuwa ni Ibadah na hivyo mwenye kuchuma chumo la halali kupata thawabu. Ufanyaji wa kazi ulikuwa ndio mfumo wa Manabii wote akiwemo wa mwisho, Nabii Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hata hivyo Uislamu umeweka misingi na kanuni za kutekeleza shughuli hizo. Msingi mkubwa ukiwa ni wajibu wa Muislamu kufanya kazi ya halali tu kinyume chake ni haramu kwa Muislamu.


Msingi mkubwa katika Uislamu wa kukataza kitu kilicho haramu ni kuwa bidhaa ikiwa haramu basi vyote vinavyosaidia vinakuwa haramu. Ndio Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Hakukataza zinaa tu bali vyote vinavyomkaribisha mtu kutekeleza kitendo hicho kibaya. Amesema Aliyetukuka:

”Wala msikaribie zinaa. Hakika hiyo (zinaa) ni uchafu mkubwa na ni njia mbaya kabisa” (17: 32).


Kwa ajili hiyo, ndio Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakukataza pombe tu bali pia mbebaji, mtengenezaji, mpandaji mimea au matunda kwa ajili hiyo, mnywaji, na wengineo kama tunavyoona katika Hadiyth ifuatayo:

Kutoka kwa Anas kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amelaani mambo kumi yanayohusiana na ulevi; mwenye kuukamua (kuutengeneza), Mwenye kutengenezewa, mnywaji, mbebaji, anayebebewa, anayeendesha (kuupeleka ulevi), muuzaji, anayekula thamani yake, anayenunua na anayeuza. [At-Tirmidhiy na Ibn Maajah)

Na Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Anatueleza kuwa haifai kwetu sisi kusaidiana katika uovu: Na saidianeni katika wema na ucha Mungu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni Mkali wa kuadhibu” (5: 2).


Hivyo, haifai kwake kufanya kazi ya kubeba masanduku ya pombe kwa hali yoyote ile. Inafaa kwake afanye juhudi sana ili asiwe ni mwenye kufanya hivyo. Na jambo hilo litafanikiwa tu pale atakapozungumza na mkubwa ili asiwe ni mwenye kufanyishwa kwa sababu za kidini.




Na Allaah Anajua zaidi
 
Anafanya Kazi Ya Kuchunga Watu Wasizame – Kuna Wanawake Wako Uchi Je, Halali Au Haramu?
Maswali: Uchumi (Biashara-Kazi)
SWALI:

Assalam aleikum awrahmatullah wabarakaatuh?

Ama baada ya salam, mim ni kijana ambae nafanya kazi hotelini, kazi yangu ni kuchunza wageni wasizame katika mahali pa kuogelea. Na wageni hao huvaa uchi (sidiria na chupi) wanawake. Jee yafaa kufanya kazi hiyo? Na pato langu ni halali ama haramu? Shukran



JIBU:

AlhamduliLLaah - Sifa njema zote Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.


Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuchunga wanawake walio uchi wasizame.



Kazi hiyo si sawa kufanywa na kijana Muislamu kwa kuwa kazi hiyo ni kuokoa wanawake walio uchi pindi wanapokuwa wanazama. Mpango ulio mzuri katika kazi hiyo ni mwanaume kuwaokoa wanaume, na mwanamke awepo wa kufanya kazi hiyo ya kuwaokoa wanawake wenzake.



Uharamu wa mwanaume kufanya kazi hiyo ni kule kuwepo katika eneo lililo na wanawake wasiojistiri vizuri. Linalotakiwa ni wewe uzunguze na wenye hoteli ikiwa ni Waislamu inaweza kuwa rahisi lakini hata ikiwa si Waislamu uwaelezee hilo na huenda wakakufahamu na kukupatia kazi mbadala.



Ikiwa mwenye hoteli hakukubali itabidi ufanye juhudi ya kutafuta kazi nyingine. Na uache hiyo pindi tu unapofanikiwa katika hilo lakini ni lazima ujiwekee muda na ufanye bidii. Ukifanya hivyo basi Allaah Aliyetukuka Atakusaidia inshaAllaah.



Tunakuombea kila la kheri katika suala hilo.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Anapata Matatizo Na Meneja Wake Kazini Nchi Za Kigeni Afanyeje?

www.alhidaaya.com







SWALI:



Assalamu aleikum swala langu leo, ilikuwa naomba kupata maoni kutoka kwenu, maoni yenyewe ni kuhusu kazi ninayofanya, mimi niko Uingereza na ndiko nnako fanya kazi, sasa basi huko kazini yuko mzungu mmoja ambae yeye ndio manager lakini ananichukia sana mimi sijui kwa nini ananifanyia madharau sana hanifanyi usawa kama anavyo wafanyia wengine, na mengineo baya, sasa naomba maoni yenu nifanye nini ahsantum.









JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Hakika ni kuwa kazi nyingi hapa duniani zina matatizo na mitihani. Wewe si wa kwanza kupata matatizo hayo wala hutokuwa wa mwisho. Na ni hakika wapo Wazungu ambao ni wazuri kwa muamala wao na wafanyakazi walio chini yao na wengine ni waovu na wabaguzi.



Nasaha ambazo tunaweza kukupatia ni kama zifuatazo:



1-Huenda Mzungu huyo ana nadhariya zake kukuhusu wewe. Ima hajakuelewa vyema au anaona hutekelezi kazi yako inavyohitajika, au unazembea au sababu nyingine yoyote. Hivyo, unatakiwa uwe na ujasiri wa kuweka miadi naye ili umueleze unayohisi akilini mwako. Kwa kumuelezea kinaganaga huenda yakajitokeza mengi katika hayo mazungumzo. Huenda akakuelezea anayoona ni makosa kwa upande wako au kukiri kuwa kweli amefanya makosa hivyo ajirekebishe.



2-Mripoti kwa Meneja mkuu, au waone Jumuiya ya Wafanyakazi kama mnayo hapo kazini waweze kuzungumza naye ili akupe haki zako kama wafanyakazi wengine.





3-Kuomba Du’aa katika kila nyakati ambazo du’aa inakubaliwa kama unapoamka usiku kwa ajili ya Tahajjud, unapokuwa umefunga, baina ya Adhaan na Iqaamah na nyakati nyingine. Muombe Allaah ('Azza wa Jalla) Akutengenezee mambo yako na Akuepushe na shari hizo.





4-Huenda kazi hiyo ikawa haina kheri nawe, kwako binafsi au kwa Dini yako kwa zote mbili. Hivyo, kitu ambacho unaweza au unatakiwa kufanya ni kutafuta kazi sehemu nyingine. Pindi tu utakapopata, basi aacha hiyo uende kufanya huko kwengine, lakini kabla ya hapo Swali Swalaah ya Istikhaarah utake ushauri kutoka kwa Allaah ('Azza wa Jalla) kwa jambo ambalo linafaa wewe ufanye katika tatizo hilo ulilo nalo.



Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo yake:



Swalaah Ya Istikhaarah Iswaliwe Kwa Ajili Ya Nini Na Ipi Du'aa Yake?


Na timiza fadhi zako ipasavyo kisha mdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa Istighfaar (kuomba maghfirah), kuswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Adhkaar nyenginezo zilizothibiti.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Anapewa Pesa Na Serikali, Je, Mume Hapasi Kumhudumia Ikiwa Ni Hivyo?
Maswali: Uchumi (Biashara-Kazi)
SWALI:



Asalam alekum. Naomba kuuliza suali ni sawa kama tuko ulaya waume zetu kuwa wasema tuna pesa zetu twapawa na sirkali kwa hivo mume hana haki yakukutizama kukupa masrufu hatakama unashida pesa haikotoshi ni sawa kweli naomba munijibu kwa sababa sio mimi peke yangu kuna wenzangu wengi wana shida hio hapa ulaya shukran.




JIBU

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kupewa masrufu na mumeo. Mara nyingi katika jamii yetu ya Waislamu wanawake hunyanyasika na kunyanyaswa kwa sababu moja au nyengine. Mbali na kuwa Dini ya Kiislamu imemlinda sana mwanamke ili asiwe ni mwenye kunyanyaswa.

Wanaume huwa wanachukua fursa kwa kuwa wanawake wetu hawana maalumati ya Kidini huwa ni rahisi sana kupoteza haki zao. Inatakiwa ieleweke kuwa wanawake wana haki sawa na wanaume kwa nyanja kadhaa. Ni jukumu la mume kumpatia mkewe malazi, chakula, nguo, matibabu na mengineo, ikiwa mke ni tajiri au masikini. Jukumu hilo haliondoki kwa mume hata kama mke anapata kipato kikubwa zaidi. Anachopata mke ni chake na cha mume ni cha wote, lakini mke kwa ridhaa yake bila kulazimishwa akitaka kumsaidia mumewe hakatazwi na Dini kufanya hivyo na atapata thawabu kwa hilo.



Hata hivyo tuelewe kuwa, kwanza, ni vipi mwanamke ana pesa zake? Vipi serikali impatie mwanamke pesa na hali ana mume na mume anafanya kazi? Bila shaka hapo ima kuna njia zisizo halali zimetumika za kupata chumo hilo, au kuna udanganyifu wa kudanganya serikali hiyo na kutoa madai kama ambayo tunayasikia ya kuwa mwanamke anakwenda kudai serikalini kuwa hana mume na hali anaye, au kujiita 'single mother' na serikali kumpatia masurufu yake kila wiki, na ikamlipia na nyumba, na bado ikampa na pesa za kumhudumia mtoto/ watoto wake.

Hakika njia hizo ni mbaya, za dhuluma na chafu. Mbaya kwa sababu kunatumika uongo kupata maslahi hayo, Dhuluma kwa sababu unapokea usichostahiki na hivyo kuchukua kwa dhuluma. Chafu kwa sababu ya kuikataa ndoa yako na kudai uko peke yako na hali una mume, na isitoshe Uchafu zaidi waja kwa sababu kila mara mwanamke huyo huyo wa Kiislam, tena labda na Hijaab yake, anaonekana na akiwa na mimba na kisha kuzaa na hali kasema yeye ni 'single mother' au hana mume! Hakika huko ni kuutukanisha Uislam, na kuchafua jina la Dini yetu safi. Inaleta picha kwa makafiri kuwa wanawake wengi wa Kiislam ni Malaya pamoja na mahijaab yao wanayovaa.

Kosa hilo kwanza kabla ya yote linamwendea mume, mume kwa kuruhusu mkewe kuchukua pesa hizo serikalini kwa udanganyifu na madai ya kuwa si mkewe, na utakuta hata mume anaogopa kukaa au kulala kwenye nyumba hiyo ya mke wake kwa sababu serikali inatambua kuwa hiyo ni nyumba ya mwanamke 'single mother' na wakimkuta mwanaume humo, huenda wakapata mashaka na hata kumkatia huyo mwanamke pesa wanazompa na malipo ya kodi ya nyumba wanayomlipia kila wiki. Mwanaume wa namna hiyo, ni mwanaume mchafu, asiye na ghera, asiye na Iymaan, na hata asiye na maadili wala khofu kwa Mola wake.

Hali kadhalika, wanawake wengine waliokwenda kwenye nchi hizo za Ulaya na kuweza kupata nyumba na kipato cha bure serikalini, na wakawa wanaendelea kupata chumo hilo la haraam hata baada ya kupata waume wa kuwaoa, bado wanaendelea kuchukua pato hilo ilihali waume zao wanaweza kuwahudumia kwa kila kitu. Hao ni wenye makosa makubwa kwa tamaa zao hizo ambazo huenda zikawapeleka kwenye adhabu kali ya Mola wao. Na waume hao dhaifu wenye kupenda maslahi na kubana matumizi na kukwepa kulipa kodi za nyumba, ndio wamekuwa wakiyafurahia maisha hayo wakiona kuwa wanaweza kubana matumizi na kutogharamika sana. Matokeo yake tumesikia wanaume wengi wamefukuzwa na wake zao kwenye hizo nyumba kwa sababu mwanamke ndiye mwenye kumiliki nyumba na kulipiwa na serikali. Ndio kumekuwa na mtindo wa kutimuliwa waume kwenye nyumba na wake zao kwa sababu wake ndio wenye kujulikana na serikali kuwa ndio wenye hizo nyumba. Hii ni fedheha kubwa na aibu na udhalilishwaji kwa waume hao wasiomuogopa Allaah.

Tunawasisitiza nyote, mke, na mume, mubadilishe maisha yenu haraka, na muachane na hizo tamaa za kidunia zitakazowapeleka pabaya hapa duniani na kesho Akhera.

Mwanaume arejee kwenye Uislam wake na atekeleze maamrisho ya Dini yake ambayo yanamtaka awe ni msimamizi kamili wa nyumba yake, kuanzia kulipa kodi ya nyumba, kuilisha na kuivisha na kuitibu familia yake, pamoja na majukumu mengineyo yanayompasa yeye. Na awe na uchungu kuona mkewe analishwa na makafiri, na kuhifadhiwa na makafiri. Pia aone vibaya na achukizwe zaidi kuona mkewe anajulikana kama Malaya kwa kuzaa watoto bila mume. Hilo tu hakika latosha kumfanya mume mwenye chembe cha Iymaan na Uislam, kupinga kwa nguvu jambo hilo la mkewe kulishwa na kuhifadhiwa na serikali.

Na mke aone vibaya kuendeleza uongo na kujidhalilisha na kujitukanisha kwa makafiri na kuutukanisha Uislam wake.

Rejeeni kwa Mola wenu na mumche Yeye. Kwani Yeye ni Mwenye Kuona na ni Mwenye Kusikia Yote na Mjuzi wa yote muyafanyayo.

Na Allaah Anajua zaidi
 
Anasomea Uundaji Wa Kompyuta Je Halaal Kazi Hii Ikiwa Watu Wanatumia Kwa Maasi?
Maswali: Uchumi (Biashara-Kazi)
SWALI:



"ASSALAAMU ALEYKUM WARAHMATUL LAHI WABARAKATUH"



Sheikh nawashukuru sana kwa nasaha yenu mliotunasihi kuhusu vijana kusomea kazi zinazo kubaliwa na dini.



Mimi huu ndio mwaka wangu wa kwanza college na ninasomea kazi ya kutengeneza/ kujenga upya computer {technology} na kama unavyojua sheikh hichi chombo kina maasi mengi na faida nyingi pia. Je sheikh watu wakija kuitupia kutafutia maasi na balaa nyenginezo na mimi huwa nipo ndani au?



NAWATAKIA KILLA LA KHERI. ASSALAAMU ALEIKUM



JIBU:







Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.







Shukrani zetu za dhati kwa swali lako zuri kuhusu uundaji wa Kompyuta. Hakika hili ni somo zuri katika wakati wetu wa sasa na tunahitaji Waislamu wema wajifunze na wafikie daraja ya umahiri katika ufundi huo. Hakuna tatizo lolote kwako kusomea somo hilo na baadaye kufanya kazi kwani kazi yenyewe ni halali katika Uislamu.



Pia ufahamu kuwa si lazima umuulize mwenye kutaka kutengeneza kompyuta yake atataka kuitumia vipi. Hiyo ni yake na Mola wake Mlezi, hata hivyo ikiwa unamjua mtu yule si mwema na ataitumia vibaya kwa ushahidi wa wazi basi hapo unatakiwa ukatae kumtengenezea chombo chake hicho.



Mfano huu ni kama wa muuzaji kisu. Kisu kina manufaa na madhara lakini wewe hulazimiki kumuuliza mnunuaji atatumia vipi kisu hicho. Hata hivyo, ukimjua kuwa mtu mwenyewe ni jambazi na anatumia silaha kuua watu hutomuuzia kisu hicho.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Anataka Kujiajiri Mwenyewe Lakini Hana Mtaji
Maswali: Uchumi (Biashara-Kazi)
SWALI:



assalam aleykum



Asante kwa alhidaya kutuwekea website nzuri yenye mafundisho.



naomba muniambie kama nahitaji kujiajiri mwenyewe lakini sina mtaji nifanye nini? Mimi nimeajiriwa lakini mshahara una isha wote sina hata akiba. Naomba ushauri. wabillahi tawfiq





JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.





Shukrani kwa swali lako kuhusu mashauri ya kutaka kujiajiri.

Kama ulivyosema kujiajiri kunatakwia mtaji ambao utakusaidia kuweza kufanya shughuli au kazi unayoona itakukimu kimaisha. Zipo njia nyingi za kufuatwa ili kufikia hilo kutegemea na nchi unayoishi. Nazo ni kama zifuatazo:



1. Kupata mkopo kutoka kwa jamaa, marafiki au rafiki, taasisi za Kiislamu, benki ya Kiislamu au njia nyengine yoyote ambayo haina ribaa.



2. Kushirikiana na mtu mwengine au taasisi ambaye/ ambaye inaweza kukupatia mtaji na faida mnayopata mgawane kulingana na mlivyoafikiana. Kumaanisha wewe utatumia wakati wako na nguvu na mwengine atatoa pesa za shughuli hiyo.



3. Kutafuta kazi nyengine ambayo mshahara wake haujambo ili uweze kuweka akiba ambayo itakuwa mtaji wa kuanza shughuli yako mwenyewe.



Katika kutafuta mtaji, jiweke karibu na Allaah Aliyetukuka kwa kufanya ‘Ibaadah na kumuomba aufanye mtaji huo kuwa wa kheri.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Anayefanya Kazi Benki Anahesabiwa Kuwa Ni Mpokea Rushwa? Nini Hukumu Ya Kufanya Kazi Benki?
Maswali: Uchumi (Biashara-Kazi)
SWALI:

Assalam aleykum Warahmatollah wabaratoh.

Kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi mzima wa Al-hidaaya kwa ushirikiano mzuri wanaotoa kwa waislam wote duniani.

Swali langu ni nini hukumu ya mtu afanyae kazi Bank. Je anahisabika kama mtoa na mpokea rushwa? Natanguliza shukrani kwa ushirikiano wenu katika hili.



JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Kwanza tunakushukuru kwa shukurani zako na tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Atupe tawfiyq tuweze kuendelea kutoa ushirikiano na mafundisho yenye kuwanufaisha Waislam inshaAllaah.

Asli miongoni mwa mambo yanayosababisha watu kukosa haki zao au wengine kudhulumu haki za wengine kwa kujichotea haki zisizo zao au kupewa nyadhifa wasizostahiki kwa njia isiyo ya haki ambayo hueleweka kama ni Rushwa.

Uislamu umepiga vita kila lenye kusababisha na kupelekea watu kufikia kuwadhulumu wengine kwa jina la aina yo yote ikiwemo rushwa, Uislamu umeipiga vita rushwa kwa nguvu zake zote na kutahadharisha kuwa wahusika wake ni watu wa motoni, hivyo Waislamu hawatakiwi kujishughulisha na jambo hilo kwani ni katika mambo yaliyo haramu na wenye kushiriki rushwa huwa ni watu wa motoni kama ilivyothibiti kati Hadiyth:

“Laana ya Allaah iwe juu ya ar-Raashiy (mtoa rushwa) na (mpokea rushwa).” At-Tirmidhiy.

Hiyo ndio hukumu ya mtoa rushwa na mpokea rushwa.



Hukumu ya mtu afanyae kazi benki.

Mabenki karibu yote huwa yanafanya kazi kwa kutumia riba (interest) katika mu’aamalat wake, na riba ni katika Aliyoyaharamisha Allaah na Mtumewe (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) , hivyo mwenye kuamini Allaah na Siku ya Mwisho hatarajiwi kuchepa katika fukwe za makatazo yake wachilia mbali kuogelea katika Aliloharamisha Allaah; kwa kufanya kazi katika mabenki haya tunayoyaelewa kuwa ni ya kuvutia na kushajiisha riba, pia hatakiwi kuchukuwa mikopo kutoka katika mabenki hayo vile vile kwani ndani yake huwa kuna riba isipokuwa ikiwa mkopo huo hauna riba (interest free), Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema:

“Enyi mlioamini! Mcheni Allaah, na acheni riba zilizobakia, ikiwa nyinyi ni Waumini. Basi mkitofanya jitangazieni vita na Allaah na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilmali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe.” Al-Baqarah: 278-279.

Kufanya kazi katika pahala ambapo yanayoshughulikiwa ni kila lenye kueleweka na kufahamika katika Uislamu kuwa ni vita na Allaah na Mtumewe ni haramu kwa mwenye imani ya Kiislamu, bali benki si pahala pa kujipachika na kuwepo mwenye kuamini Allaah na Siku ya Mwisho. Na mfanyakazi wa benki huwa anashughulika na uandishi na utayarishaji na ushughulikiaji wa mambo ya riba na tunajua kuwa imethibiti kuwa Muandishi (katika makubaliano na ushughulikiaji wa mambo ya mapatano ya riba, na hapa tunamzungumzia Muandishi (mfanyakazi) wa benki), na Mashahidi wawili, na Wakala kama ilivyo katika Hadiyth za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni watu waliolaaniwa:

“Allaah Amemlaani mla riba, wakala (muwakilishi) wake, mwandishi wake na mashahidi wake wawili; wote in sawa” Muslim.

Je anahisabika mfanya kazi benki kama mtoa na mpokea rushwa? Huenda ndugu yetu muulizaji anakusudia riba kwani mabenki hakuna rushwa labda iwe rushwa katika kuchaguliwa nani wa kupewa mkopo na kadhalika; hata hivyo tumejaribu kwa uwezo wake Allaah kugusia mambo yote mawili Riba na Rushwa na mfanya kazi benki huwa anahisabika bila ya shaka yoyote ile katika waandishi au mashahidi wa riba na hukumu yake pamoja na mtoa rushwa na mpokea rushwa ndio kama ilivyokuja na kuthibiti katika Hadiyth.

Na Allaah Anajua zaidi
 
NASAHA ZA IJUMAA


Assalaam alaykum warahmatullah wabarakatuh

Alhamdulillah tunashukuru kwa kutufikia siku ya Ijumaa ambayo ni siku bora kabisa,humo aliumbwa Adam alyhi salaam,akawekwa peponi,na siku kama hii akatolewa humo,na Kiama inshaallah kitasimama siku Ijumaa

Naihusia nafsi kwanza juu ya kumcha Allah azza wa jallah,pamoja na kuwahusia juu ya swala zima la kumcha Allah. Kwani hakika mwisho mwema ni kwa ambao wanamcha Allah,hili likae akilini mwetu,ni Ucha Mungu tu ndio salama yetu

Naam leo nasaha zangu ni kupitia maneno ya Nabii swalla aallahu alayhi wa aalih wassallam,katika mfumo wa hadith amesema:

"Ole wake yule atakaye kuwa funguo ya Shari na kuwa komeo la kheri"

Hapa ni wale watu ambao kwanza wao ndio huwa chanzo cha shari zote,wao ndio huwapa watu hamasa ya kufanya maovu na mabaya,yani wahamasishaji wazuri linapokuja swala la kufanya shari

Hawa ndio wachochezi wa ugomvi baina ya watu,hutoa maneno hapa na kuyapeleka kule lengo ni kufitinisha,husambaza picha chafu za ngono na za namna hiyo ili uovu upate kuenea,yaani anashindwa kuwa muovu yeye binafsi lakini mpaka awashirikishe na wengine

Atafungua group kama ni la whatsapp basi awaunganishe watu wayaone machafu humo,kifupi yeye huwa ndio chanzo cha ufisadi na maovu kuenea katika jamii,basi ole wake

Upande wa pili kuna watu ambao wao ndio huwa komeo la kheri,yaani wao hawataki mambo ya kheri yafanyike au yawepo,uta msikia ndio chanzo cha kuhamasisha watu kwa mfano wasitoe sadaka,kwa kusema hela zenu zinaliwa na masheikh,au sadaka zenu hazifiki kwa walengwa,na mambo kama hayo

Wala hana uhakika na hayo anayoyasema isipokuwa ni dhana tu,na ndio maana Allah Subhaanahu wa Taala amesema enyi mlioamini jiepusheni na dhana kwani hakika baadhi ya dhana ni dhambi

Mtu wa namna hii hapendi mambo ya kheri yaenee katika ardhi,huwa katisha watu tamaa wasiyaendee mambo ya kheri,iwe ama ni kuswali,kutoa sadaka,kusaidia mayatima na maskini,ili mradi atajitahidi awe kikwazo,ole wake

Naam ndugu zangu katika imani basi ebu tujikague katika nafsi zetu,je sisi tupo miongoni mwao? Na kama tupo basi tutubu kwa Allah na tuache mara moja tabia hizi,kwani hakika mwisho wake sio mzuri

Nawakumbusha tena nyinyi na mimi juu ya swala zima la kumcha Allah azza wa jallah,kwani hakika mwisho mwema ni kwa wamchao Allah

Subhaanaka allahuma wabihamdik ashahadu anlaa ilaah ila anta astaghfiruka waatubu ilaik


Ijumaa Mubarak!
 
Baadhi ya post zangu za zamani...


Kukufuru Kwa lugha isiyo rasmi ni Hali ya kumlaumu Mola wetu Kwa kutotutimizia au kutufanyia jambo letu Fulani.

Na

Kushukuru ni kufurahia au kuikubali neema mbali mbali ambazo ametujalia au ametupa Mola wetu.

Kwa bahati mbaya Sana watu wengi Tunapenda kumkufuru Mungu na Kusahau neema mbali mbali ambazo ametujalia kama wanadamu,huwa tuna angalia vitu vinavyopendwa na nafsi zetu kama magari,majumba na anasa nyingine mbali mbali,tukivikosa hivyo basi hapo kufuru inaanza,kwanini Mimi Mungu hajanipa nyumba? Au hajanipa kazi nzuri? Na mambo kama hayo.

Lakini

Tunasahau neema ya afya,Uhai,macho,masikio na viungo vilio kamilika,je ni wangapi ni vipofu,viziwi na walemavu?

Hakika Allah hawapendi watu ambao wanakufuru neema mbali mbali walizopewa,na hayo ni makosa makubwa Sana.

Tunatakiwa kushukuru Kwa kila Jambo ambalo tumepewa na Allah,huna gari lakini Una afya njema,Una uwakika wa Kula Milo mitatu Kwa siku hakika hiyo ni neema,kwasababu kuna watu Kula Yao ni shida Sana.

Kwa kila ulichonacho kiwe Kikubwa au kidogo basi mshukuru Mola wako hakika yeye huwapend Sana watu wanaoshukuru,na wanao shukuru huongezewa kila siku.

Hapa namkumbuka Malcom ambaye sasa ni marehemu ambaye allikuwa mtoto wa Masudi Kipanya hakika Allah amrehemu, pamoja na kuwa mlemavu na WA kitandani Mda wote lakini alikuwa mtu WA kushukuru na siku zote alitufundisha namna ya kumshukuru Mungu Kwa kila Jambo,binafsi nilikuwa namkubali Sana Katu hakutetereka katika Imani yake Kwa Mola wake.

Hivyo ndivyo tunavyotakiwa tuishi na kushukuru Kwa kila Jambo. Mwenyezi Mungu anasema:

Mkinikumbuka Nitawakumbuka, Mnishukuru na wala Msinikufuru
 
Back
Top Bottom