Ramadhan Special Thread
Naogopa Kudai Urithi
Baba Aliyeoa Wake Wanne Amefariki – Naogopa Kudai Urithi
Maswali: Mirathi
SWALI:



Assalam alykum warahmatullahi wabarakatuhu.

Swali langu ni hili.

Baba yangu kafaa mwaka 2000 na kaacha nyumba na alikuwa kaowa wake 4 sasa mimi na mama yangu hatueshi hapo tunaeshi kwao na mama na wao hawajifikirii kuhusu kugawa urithi na hata kunisaidiya mimi hawajifikirii, na hapo kwenye iyo nyumba alioacha baba anaeshi mama mkubwa na wanae na mimi ndio wa mwisho ninahofia kuomba urithi juu niko mdogo sasa nifanyeje na mnanishauri nini?





JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu hofu ya kudai urithi.



Hakika ni kuwa pindi mtu wa karibu anapokufa kama baba, mama, mke, mume inakuwa ni haki kwa warithi kupata urithi wao. Inapasa kwa wazee wanaobaki kuhakikisha kuwa kila mmoja amepata haki yake, na ikitokea kuwa mwenye haki kwa mfano kama wewe hujapatiwa mgao wako, basi sheria inakutaka uombe haki yako kwa njia nzuri.



Kwa ajili hiyo inafaa wewe na mama yako kuzungumza na jamaa kuhusu kupatiwa haki zenu nyinyi na wote ambao hawakupewa. Katika hali hiyo wake 4 watagawanya thumuni (1/8). Na ikiwa aliyefariki aliacha baba na mama wao pia watapata haki yao kwa alichoacha mtoto wao.

Tunakuombea kila la kheri katika kutafuta haki yako.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Baba Amefariki Ameacha Mjane, Ndugu, Watoto Na Anamiliki Nyumba



Alhidaaya.com







SWALI:



Asalaam aleykum, mzee amefariki kaacha nyumba 1, ndugu wa kike 2, wa kiume 1, watoto wa kike 2 na mjane 1, nyumba itagawanywaje?







JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.







Awali ya yote ni kuwa lazima mwanzo ikiwa mzee ana madeni basi alipiwe na ikiwa aliacha wasiya basi pia utekelezwe lakini kiwango cha kutolewa kisizidi thuluthi (1/3).



Kwa hakika, inakuwa shida kuigawa nyumba kwa warithi hivyo wanaweza kuitia thamani hiyo nyumba kisha wakagawa kulingana na kiwango cha kila mmoja. Ikiwa si hivyo basi inatakiwa igawanywe vyumba na jambo hilo linakuwa ni vigumu ila tu iwe na vyumba vingi ambapo kila mmoja atapata sehemu yake. Kwa kuwa warithi ni wengi kiasi mara nyingi hutokea mtafaruku na hubidi nyumba ima kutiwa bei na kuuzwa au kununuliwa na mrithi mmoja kisha kila mmoja akapata sehemu yake.



Ama mjane kiwango chake kinafahamika vilivyo nacho ni thumuni kama Alivyobainisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَلَكُمْ نِصْفُ مَا تَرَكَ أَزْوَاجُكُمْ إِن لَّمْ يَكُن لَّهُنَّ وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَ لَهُنَّ وَلَدٌ فَلَكُمُ الرُّبُعُ مِمَّا تَرَكْنَ ۚ مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصِينَ بِهَا أَوْ دَيْنٍ ۚ وَلَهُنَّ الرُّبُعُ مِمَّا تَرَكْتُمْ إِن لَّمْ يَكُن لَّكُمْ وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَ لَكُمْ وَلَدٌ فَلَهُنَّ الثُّمُنُ مِمَّا تَرَكْتُم ۚ مِّن بَعْدِ وَصِيَّةٍ تُوصُونَ بِهَا أَوْ دَيْنٍ ۗ وَإِن كَانَ رَجُلٌ يُورَثُ كَلَالَةً أَوِ امْرَأَةٌ وَلَهُ أَخٌ أَوْ أُخْتٌ فَلِكُلِّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا السُّدُسُ ۚ فَإِن كَانُوا أَكْثَرَ مِن ذَٰلِكَ فَهُمْ شُرَكَاءُ فِي الثُّلُثِ ۚ مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصَىٰ بِهَا أَوْ دَيْنٍ غَيْرَ مُضَارٍّ ۚ وَصِيَّةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَلِيمٌ ﴿١٢﴾

Nanyi mtastahiki nusu katika walichoacha wake zenu ikiwa hawakuwa na mtoto. Na ikiwa wana mtoto, basi mtastahiki robo katika walichoacha, baada ya kutoa wasia waliyousia au kulipa deni. Nao wake zenu watastahiki robo katika mlichoacha ikiwa hamna mtoto. Na ikiwa mna mtoto basi watastahiki thumni katika mlichoacha, baada ya kutoa wasia mliousia au kulipa deni. Na ikiwa mwanamume au mwanamke anayerithiwa hana mtoto wala wazazi, lakini anaye kaka au dada, basi kila mmoja kati yao atastahiki sudusi. Na wakiwa ni wengi ya hivyo basi watashirikiana katika theluthi, baada ya kutoa wasia uliousiwa na kulipwa deni pasipo kuleta dhara. Huu ni wasia kutoka kwa Allaah, na Allaah ni Mjuzi wa yote, Mvumilivu. [An-Nisa: 12]





Ndugu wa kiume na wa kike wa aliyefariki watarithi pia kwa kuwa aliyefariki hakuacha mtoto wa kiume. Kwa hiyo, binti 2 wa aliyefariki watapata kila mmoja thuluthi.



Jadwali ya wirathi itakuwa kama ifuatavyo:





Namba



Uhusiano na Aliyefariki



Kiwango



Asilimia

1

Mjane

Thumuni (1/8)

12.5



2

Binti 1

Thuluthi (1/3)

33.33



3

Binti 2

Thuluthi (1/3)

33.33



4

Kaka


10.42



5

Dada 1


5.21



6

Dada 2


5.21




Jumla


100.00













Na Allaah Anajua zaidi
 
Baba Amempa Mkewe Wa Pili Dhahabu Za Mama Yetu - Naye Baba Kafariki Je Tunayo Haki Kumdai Mama Wa Kambo Hizo Dhahabu?
Maswali: Mirathi
SWALI:



Salaam alaykum! Mimi nina swali, wakati marehem mama yangu amefariki aliacha vitu vya dhahabu na sisi kipindi hicho tulikuwa wadogo sana, baada ya muda baba akaja akapata mwanamke mwingine akachukuwa dhahabu za mama yetu akampa yule mwanamke sasa hivi na baba nae kashafariki pia, na pia kwa sasa tunaakili zetu je tunaweza kumdai yule mwanamke hizo dhahabu? Shukrani









JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mirathi za dhahabu za mama yenu.

Kabla hatujaingia katika kujibu lako tungependa kumnasihi kila mmoja na sisi wenyewe pia tuwe na adabu tunapowaita mama zetu. Haifai kwetu sisi kuwaita mama wa kambo kuwa ni mwanamke badala ya mama. Kwa hali yoyote ile mwanamke yeyote anayeolewa na baba ya mmoja wetu anakuwa ni mama, kwani huwezi kumuoa hata baba akiaga dunia. Hivyo, inatakiwa tuwape heshima wanayostahiki.



Swali lililo juu halieleweki vyema kwani hukutueleza kama vitu hivyo vya dhahabu vilikuwa ni vya mama au alikuwa amepewa na baba kwa matumizi tu.

Tuchukue ni vyake miliki yake kwa hivyo itakuwa nanyi mpate haki yenu kulingana na idadi yenu mlivyo. Ikiwa ni hivyo baba yenu pia atakuwa ana haki ya dhahabu hizo, naye atapata robo ya mali ya mama yenu. Kwa jinsi hiyo nanyi mtakuwa na haki ya dhahabu hizo.



Ikiwa ni hivyo mlivyosema basi baba yenu atakuwa na makosa nanyi mnatakiwa mumsamehe baba yenu kwa kosa hilo. Ikiwa mmeshamsamehe baba yenu kwa kosa hilo mnaweza kufanya moja kati ya mawili:



1. Kumsamehe na kumuachia mama yenu hizo dhahabu na kutomdai.

2. Kumdai haki yenu lakini kwa njia iliyo nzuri ya hekima si kwa ujeuri wala matusi.



Ikiwa mmechukua njia ya pili itabidi mwende nyinyi wenyewe kwa mama yenu, au mumtumie watu wazima wenye busara au kwenda kwa Qaadhi ili mpate haki yenu hiyo. Hata hivyo, njia ya mwisho si nzuri kwani mtakuwa mumekiuka nidhamu iliyopo.



Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Awape ilhamu ya kufuata njia iliyo bora.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Baadhi ya post zangu za zamani.....

HEKIMA ZA MALKIA BALKIS


Tunarudi nyuma kidogo enzi za Nabii Suleiman.

Suleimani alipata habar kuwa kuna inchi inaitwa Sabaa Chini ya Malkia Balkis,hawa walikuwa wanaliabudu Jua. Hivyo Suleimani akamtumia Barua aripoti kwakwe Hali ya kuwa Amesilimu.

Basi Malkia aliwaita mawaziri wake na kusema kapata Barua toka Kwa Mfalme Suleimani ikimtaka aende kwake Hali ya kuwa Amesilimu,kwahiyo akawaomba ushauri juu ya barua Ile.

Mawaziri wakwambia Sisi ni watu wenye nguvu na tuna jeshi Mahiri hivyo tupo tayar kwa Vita,tunasubir uamuzi wako Tu.

Malkia Balkis akasema kwa kawaida Wafalme huwa wana kawaida ya kuvamia inchi za wenyeji na kuwafanya hao wenyeji wanyonge na dhalili na kufanya uharibifu mkubwa,hivyo naona ngoja tuwapelekee zawadi na kuona wajumbe watakuja na habari gani?

Balkis aliona hatar mapema sana kabla ya haijatokea na hivyo akaamua atumie hekima ili kujiepusha inchi yake na umwagaji damu na uharibifu ambao ungeweza kutokea kama angejaribu kupambana na Suleiman.

Watu wengi sana tunajiingiza katika mambo ambayo huja kutugharimu baadae kwasababu ima tunapuuza kuona viashiria vya kushindwa huko mbeleni au kutochukua tahadhari mapema kuepuka madhara ambayo huja kutupata baadae.

Tunadaharau mambo katika biashara zetu,katika mahusiano yetu na katika nyanja mbali mbali katika Maisha yetu, tujifunze kuyaangalia mambo katika angle zote na kuchukua tahadhari zote ili tuepuke madhara ambayo yangeweza kuja kutupata baadae.

Ngoja tutoe mfano kidogo ili hili somo lieleweke vizuri zaidi. Chukulia wewe ni mkali WA kutembea na wake za watu,je umeshawahi kuwaza kuwa IPO siku utakuja kujulikana Tu, je umeshawahi kufikiria madhara au aibu ambayo unaweza kuipata baada ya kujulikana uchafu wako.

Wewe ni Mwalimu kwa mamlaka yako unaweza kumshawishi mwanafunzi yeyote hapo shuleni kwako na kutembea nae,je umeshawahi kufikiria aibu ambayo unaweza kuipata baada ya uchafu wako kujulikana?

Nadhani Kwa mifano hiyo unaweza ona ni muhimu sana kuona mwisho wa kitu au Jambo kabla ya kuamua kuliendea.

Kuwa kama Malkia Balkis ili uepuke aibu ndogo ndogo.
 
Baadhi ya post zangu za zamani....

Tuelekee moja Kwa moja mpaka Misri, hapa tunakutana na marafiki na majirani wawili ambao walikuwa wanapendana Sana na kuheshimiana Sana.

Bwana mmoja alikuwa na mtoto WA kike na mwingine WA kiume,basi Maisha yanasonga mbele,kwakuwa walikuwa majirani Wazuri na marafiki pia,wakataka urafiki wao uende mbali zaidi Kwa kuunganisha undugu WA ndoa.

Hivyo bwana mwenye mtoto wa kijana wa kiume akatoa mahari kabisa ili baada ya miaka kadhaa baada ya vijana kumaliza masomo Yao basi wafunge ndoa. Sasa kadri binti alivyokuwa anakuwa alikuwa ananoga Sana yaani/ anavutia na kuwa mrembo Sana.

Basi wazazi wa binti wakaingia tamaa na kupokea posa toka Kwa watu wengine huku wakisahau au kupuuza makubaliano Yao ya awali na jirani Yao. Basi bwana mwenye kijana wa kiume baada ya kupata habari Akaona isiwe tabu wala haina haja ya kuvunja urafiki na ujirani Kwa mambo kama hayo.

Ila alichotaka ni kurudishiwa Tu mahari yake, lahaula! Bwana mwenye binti Kwa USO mkavu kabisa akasema Mimi sina mahari yako au Kwa maana nyingine hukunipa mahari yoyote Ile,basi malumbano yakaendelea mpaka kifikishana mahakamani.

Kama unavyojua mwenye Kisu kikali ndio hula nyama, upande wa binti walikuwa vizuri kwahiyo swala la kuhonga mahakama na kupindisha sheria yani sio ishu kabisa,nadhani haya mambo tunayafahamu Sana Tu na sio mageni kwenu unless uwe umekuja kutoka sayari ya mars.

Baada ya kesi mwenye binti kashinda na kibaya zaidi baada ya kutoka nje ya ukumbi WA mahakama akaanza kujidai kwamba yeye ndio jembe na hakuna ambaye anaweza kumtetemesha.

Bwana aliyeshindwa kesi yeye akanyanyua mikono juu na kumwambia Allah " ewe Mola wangu huyu amenidhulumu naomba umuonyeshe nguvu zako"

Kama wanavyosema waswahili Mungu si Ertugrul bey, basi bwana hakika dua ya mtu anaye dhulumiwa haina pazia hiyo hujibiwa chap Tu ni swala la Mda Tu, yaani hata wewe ebu jitathimini sometime unalalamika mambo magumu lkn huenda ulidhulumu huko nyuma na ukasahau hivyo unalipia dhuluma zako,rejesha haki za wenyewe halafu trust me utaona mambo yanaenda Sawa.

Anyways tuendelee na ishu yetu,basi bwana Yule binti akapata ugonjwa usio eleweka,bwana akiwa viwanja vya mahakama akapata news mara chap home,kwenda hospital binti kafariki, ndani ya siku mbili tatu Baba mtu naye kapata ugonjwa kama WA binti yake naye siku mbili tatu chap kafariki,wakiwa Makaburini wanazika huku home ukuta WA nyumba umekatika nusu,yaani ni varangati mwanzo mwisho.

Kamwe hata siku moja usidhulumu haki za watu,kwani hakika dua ya mtu ambaye amedhulumiwa huwa majibu yake huwa chap Sana.
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com









51-Tufanye nini pale tunapokhitilafiana?



Pale tunapokhitilafiana, inatupasa turejee katika Qur-aan na Sunnah Sahihi?



فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ

Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli [An-Nisaa: 59]



((تَرَكْتُ فِيكُمْ أَمْرَيْنِ لَنْ تَضِلُّوا مَا تَمَسَّكْتُمْ بِهِمَا: كِتَابَ اللهِ وَسُنَّةَ نَبِيِّهِ)) صحيح لغيره رواه مالك

((Nimekuachieni viwili ambavyo mkikamatana navyo hamtopotea abadan baada yangu; Kitabu cha Allaah na Sunnah zangu)) [Swahiyh lighayrihi – ameipokea Maalik]
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com









52-Nini Bid'ah katika Dini?



Bid’ah katika Dini ni kila kilichokuwa hakina dalili katika Shariy’ah ya Dini.



أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّـهُ ۚ

Je, wanao washirika waliowaamuru Dini yale ambayo Allaah Hakuyatolea idhini? [Ash-Shuwraa: 21]



((مَنْ أَحْدَثَ فِيْ أَمْرِنَا هَذَا مَا لَيْسَ مِنْهُ فَهُوَ رَدٌّ)) متّفق عَلَيهِ

Atakayezusha katika mambo yetu haya (Dini yetu) yasiyokuwemo basi kitarudishwa)) [Al-Bukhaariy, Muslim]



Yaani: Hakitokubaliwa kitendo chake
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com









53-Je, Ipo bid'ah inayoitwa bid-‘atun-hasanah’ katika Dini?



Hapana! Hakuna bid’atun-hasanah (uzushi mzuri) katika Dini.





الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ

Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni neema Yangu, na Nimekuridhieni Uislaam uwe Dini yenu. [Al-Maaidah: 3]





((إِيَّاكُمْ وَمُحْدَثَاتِ الْأُمُورِ، فَإِنَّ كُلَّ مُحْدَثَةٍ بِدْعَةٌ، وَكُلَّ بِدْعَةٍ ضَلَالَةٌ)) صحيح رواه أبو داود

((Jitahadharini na uzushi wa mambo, kwani kila uzushi ni bid'ah na kila bid'ah ni upotofu)) [Swahiyh - Abuu Daawuwd]
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com









54-Je, Ipo Sunnatun-hasanah katika Uislamu?



Naam, ipo Sunnatun-hasanah (Sunnah nzuri) katika Uislamuu kama vile anayeanza kufanya kitendo chema cha kheri akafuatwa.



وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا ﴿٧٤﴾

Na Tujaalie kuwa waongozi kwa wenye taqwa. [Al-Furqaan: 74]



((مَنْ سَنَّ فِي الإِسْلامِ سُنَّةً حَسَنَةً فَلَهُ أَجْرُهَا وَأَجْرُ مَنْ عَمِلَ بِهَا مِنْ بَعْدِه )) مسلم

"Atakayeanzisha mwenendo mwema " سُنَّةً حَسَنَةً katika Uislamu atapata ujira wake na ujira wa atakayetenda wema huo." [Muslim]
 
55-Je, inamtosheleza mtu kuwa ajichunge na kujilinda dhidi ya maasi peke yake tu?



Hapana! Bali inamapsa ajichunge na ajilinde nafsi yake na pia familia yake.



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَاراً

Enyi walioamini! Jikingeni nafsi zenu na ahli zenu na moto)) [At-Tahriym: 6]



((إِنَّ اللهَ سَائِلٌ كُلَّ رَاعٍ عَمَّا اسْتَرْعَاهُ، أَحَفِظَ أَمْ ضَيَّعَه)) حسن رواه النسائي

((Hakika Allaah Atamuuliza kila mchungaji kile alichokichunga kama alikilinda au alikiacha kikapotea)) [Hadiyth Hasan –
 
56-Lini watapata nusra Waumini?



Waumini watapata nusura pale watakapofuata Kitabu cha Rabb wao na Sunnah za Nabiy wao.



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّـهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ﴿٧﴾

Enyi mloamini! Mkisaidia kunusuru Dini ya Allaah, (Allaah) Atakunusuruni na Ataithibitisha miguu yenu. [Muhammad: 7]



((لَا تَزَالُ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِي مَنْصُورِينَ)) صحيح رواه ابن ماجه

((Litabakie kundi miongoni mwa Umma wangu kuwa ni lenye kunusuriwa)) [Hadiyth Swahiyh Ibn
 
57-Nani watu bora kabisa baada ya Rusuli?





Watu bora kabisa baada ya Rusuli, ni Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).





وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿١٠٠﴾

Na wale waliotangulia awali (katika Uislamu) miongoni mwa Muhajirina na Answaar na wale waliowafuata kwa ihsaan; Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye)) [At-Tawbah: 110]



((خَيْرُ النَّاسِ قَرْنِي، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ)) متَّفق عليه

((Watu bora kabisa ni karne yangu, kisha wanaowafuatia kisha wanawafuatia)) [Al-Bukhaariy, Muslim]
 
58-Wepi ni Maswahaba bora kabisa?



Maswahaba bora kabisa ni Makhulafaa Ar-Raashiduwn nao ni: Abuu Bakr, kisha ‘Umar, kisha ‘Uthmaan, kisha ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhum)



إِلَّا تَنصُرُوهُ فَقَدْ نَصَرَهُ اللَّـهُ إِذْ أَخْرَجَهُ الَّذِينَ كَفَرُوا ثَانِيَ اثْنَيْنِ إِذْ هُمَا فِي الْغَارِ إِذْ يَقُولُ لِصَاحِبِهِ لَا تَحْزَنْ إِنَّ اللَّـهَ مَعَنَا ۖ

Msipomnusuru (Rasuli), basi Allaah Amekwishamnusuru, pale walipomtoa (Makkah) wale waliokufuru akiwa wa pili katika wawili; walipokuwa katika pango, alipomwambia swahibu yake: ““Usihuzunike, hakika Allaah Yu Pamoja nasi.”[At-Tawbah: 40]



((فَعَلَيْكُمْ بِسُنَّتِي وَسُنَّةِ الْخُلَفَاءِ الْمَهْدِيِّينَ الرَّاشِدِينَ، تَمَسَّكُوا بِهَا وَعَضُّوا عَلَيْهَا بِالنَّوَاجِذِ)) رواه أبو داوود والترمذي وقال حديث حسن صحيح

((Kwa hiyo, shikamaneni na mwenendo wangu na mwenendo wa Makhalifa waongofu, yashikilieni na yakamateni barabara kwa magego)) [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, na amesema: Hadiyth Hasan Swahiyh]
 
59-Nini hukmu ya anayesema kuwa Qur-aan imepotoshwa?



Anayesema kuwa Qur-aan impotoshwa ni kafiri.



إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ ﴿٩﴾

Hakika Sisi Tumeteremsha Adh-Dhikra (Qur-aan) na hakika Sisi bila shaka ndio Wenye kuihifadhi. [Al-Hijr: 9]



((وَأَنْزَلْتُ عَلَيْكَ كِتَابًا لاَ يَغْسِلُهُ الْمَاءُ تَقْرَؤُهُ نَائِمًا وَيَقْظَانَ)) مسلم - كتاب الجنة وصفة نعيمها وأهلها

((Na Nimekuturemshia Kitabu ambacho hakioshelewi mbali na maji ili ukisome katika hali ya kulala na kuwa macho)) [Muslim – Kitabu cha Jannah, wasifu wake, neema zake na watu wake]
 
60-Je, Nabiy ‘Iysaa atateremka duniani kuwa ni miongoni mwa alama kubwa za Qiyaamah?



Naam! Nabiy ‘Iysaa ('Alayhis-Salaam) atateremka kutoka mbinguni kuja duniani kama ni miongoni mwa alama kubwa za Qiyaamah.



وَإِن مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلَّا لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا﴿١٥٩﴾

Na hakuna yeyote katika Ahlil-Kitaabi ila atamwamini kabla ya kufa kwake. Na Siku ya Qiyaamah atakuwa shahidi juu yao [An-Nisaa: 159]



((وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَيُوشِكَنَّ أَنْ يَنْزِلَ فِيكُمْ ابْنُ مَرْيَمَ حَكَمًا مُقْسِطًا))

((Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu iko Mikononi Mwake, hivi karibuni atateremka kwenu mwana wa Maryam ('Iysaa) akiwa ni kiongozi muadilifu)) [Al-Bukhaariy, Muslim]
 
Alhamdulillah tumemaliza kusoma au kujifunza Mukhtasari wa Aqiydah ya Muislamu


................................................................................................
 
UJUMBE WA LEO :

Katika mfumo wa hadith, Nabii swalla aallahu alayh wasallam anasema, yule ambaye wasi wasi wake ni maisha ya dunia tu na sio akhera yake


Basi ataendelea kuwa na hofu na wasi wasi katika maisha yake yote hapa duniani
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب تحريم العقوق وقطيعة الرحم

041-Mlango Wa Uharamu wa Kuwaasi Wazazi na Kukata Kizazi



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:



فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِن تَوَلَّيْتُمْ أَن تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ﴿٢٢﴾ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَىٰ أَبْصَارَهُمْ﴿٢٣﴾

Basi huenda nyinyi mkigeuka ndio mfanye ufisadi katika ardhi na kukata jamaa zenu wa uhusiano wa damu? Hao ndio ambao Allaah Amewalaani; Akawafanya viziwi na Akawapofua macho yao. [Muhammad: 22-23]



وَالَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ ۙ أُولَـٰئِكَ لَهُمُ اللَّعْنَةُ وَلَهُمْ سُوءُ الدَّارِ ﴿٢٥﴾

Na wale wanaovunja ahadi ya Allaah baada ya kufungamana kwake na wanakata yale Aliyoyaamrisha Allaah kuwa yaungwe na wanafanya ufisadi katika ardhi, hao watapata laana na watapata makazi mabaya (motoni). [Ar-Ra'd: 25]



وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۚ إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا ﴿٢٣﴾ وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا ﴿٢٤﴾

Na Rabb wako Amehukumu kwamba: Msiabudu isipokuwa Yeye Pekee na (Ameamrisha) kuwafanyia ihsaan wazazi wawili. Kama mmoja wao akifikia uzee naye yuko pamoja nawe, au wote wawili basi usiwaambie, Uff! Na wala usiwakemee; na waambie maneno ya heshima. Na wainamishie bawa la unyenyekevu kwa huruma, na useme: Rabb wangu! Warehemu kama walivyonilea udogoni. [Al-Israa: 23-24]







Hadiyth – 1

وعن أَبي بكرة نُفَيع بن الحارث رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( ألا أُنَبِّئُكُمْ بأكْبَرِ الكَبَائِرِ ؟ )) – ثلاثاً – قُلْنَا : بَلَى ، يَا رَسُول الله ، قَالَ : (( الإشْرَاكُ بالله ، وَعُقُوقُ الوَالِدَيْنِ )) ، وكان مُتَّكِئاً فَجَلَسَ ، فَقَالَ : (( ألاَ وَقَوْلُ الزُّورِ وَشَهَادَةُ الزُّورِ )) فَمَا زَالَ يُكَرِّرُهَا حَتَّى قُلْنَا : لَيْتَهُ سَكَتَ . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Imepokewa kwa Bakrah Nufay' bin Al-Haarith Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Je, hamtaki niwaambieni dhambi kubwa katika madhambi makubwa?"- mara tatu. Tukasema: "Ndio (tuambie), Ee Rasuli wa Allaah." Akawaambia: "Ni kumshirikisha Allaah na kuwaasi wazazi." Na alikuwa ameegemea, akakaa na kusema: "Eleweni pia kusema urongo na kutoa ushahidi wa urongo." Aliendelea kukariri hilo mpaka tukasema: "Laiti angenyamaza." [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 2

وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( الكَبَائِرُ : الإشْرَاكُ بالله ، وَعُقُوقُ الوَالِدَيْنِ ، وَقَتْلُ النَّفْس ، وَاليَمِينُ الغَمُوسُ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaahi bin 'Amru bin Al-'Aasw (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Madhambi makubwa ni kumshirikisha Allaah, kuwaasi wazazi, kuua nafsi na kiapo (yamini) cha urongo wa kusudi." [Al-Bukhaariy]







Hadiyth – 3

وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ: (( مِنَ الكَبَائِر شَتْمُ الرَّجُل وَالِدَيهِ ! ))، قالوا : يَا رَسُول الله ، وَهَلْ يَشْتُمُ الرَّجُلُ وَالِدَيْهِ ؟! قَالَ : (( نَعَمْ ، يَسُبُّ أَبَا الرَّجُلِ ، فَيَسُبُّ أبَاه ، وَيَسُبُّ أُمَّهُ ، فَيَسُبُّ أُمَّهُ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية : (( إنَّ مِنْ أكْبَرِ الكَبَائِرِ أنْ يَلْعَنَ الرَّجُلُ وَالِدَيْهِ ! )) ، قِيلَ : يَا رَسُول الله ، كَيْفَ يَلْعَنُ الرَّجُلُ وَالِدَيهِ ؟! قَالَ: (( يَسُبُّ أَبَا الرَّجُلِ ، فَيَسُبُّ أباهُ ، وَيَسُبُّ أُمَّهُ ، فَيَسُبُّ أُمَّهُ )) .

Kutoka kwa 'Abdillaahi bin 'Amru bin Al-'Aasw (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Miongoni mwa madhambi makubwa ni mtu kuwatusi wazazi wake ." Wakauliza (yaani Maswahaba): "Ee Rasuli wa Allaah! Na je, mtu, anaweza kuwatusi wazazi wake?" Akasema: "Ndio, atamtusi baba ya mtu, naye amtusi babake, na atamtusi mama ya mtu, naye amtusi mamake." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]

Katika riwaayah nyingine: "Hakika miongoni mwa madhambi makubwa ni mtu kuwalaani wazazi ake." Pakasemwa: "Ee Rasuli wa Allaah! Vipi mtu atawalaani wazazi wake?" Akasema: "Atamtusi baba ya mtu, naye amtusi babake, na atamtusi mama ya mtu, naye amtusi mamake."







Hadiyth – 4

وعن أَبي محمد جبيرِ بن مطعم رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( لاَ يَدْخُلُ الجَنَّةَ قَاطِعٌ )) قَالَ سفيان في روايته : يَعْنِي : قَاطِع رَحِم . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Muhammad Jubayr bin Mutw'im (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hataingia Peponi mwenye kukata." Amesema Sufyaan katika riwaayah yake: "Yaani mwenye kukata kizazi." [Al- Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 5

وعن أَبي عيسى المغيرة بن شعبة رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( إنَّ اللهَ تَعَالَى حَرَّمَ عَلَيْكُمْ : عُقُوقَ الأمَّهَاتِ ، وَمَنْعاً وهاتِ ، وَوَأْد البَنَاتِ ، وكَرِهَ لَكُمْ : قِيلَ وَقالَ ، وَكَثْرَةَ السُّؤَالِ ، وَإضَاعَةَ المَالِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu 'Iysa Mughyrah bin Shu'bah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ameharamisha kuwaasi mama zenu; na kuzuia na lete (kuzuia kilicho wajibu kutoa na kutaka kisicho chake); na kuzika wasichana wakiwa hai; na Amechukia kwenu kusema ovyo; kuomba sana; na kufuja mali." [Al-Bukhaariy na Muslim]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب فضل بر أصدقاء الأب والأم والأقارب والزوجة وسائر من يندب إكرامه

042-Mlango Wa Kuwafanyia Wema Marafiki wa Baba na Mama, Jamaa, Mkw na Wote Wanaopendekezwa Kuwafanyia Ukarimu



Alhidaaya.com







Hadiyth – 1

عن ابن عمر رضي الله عنهما : أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( إنّ أبَرَّ البرِّ أنْ يَصِلَ الرَّجُلُ وُدَّ أبيهِ )) .رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika wema mkubwa kabisa ni mtu kuwaunga vipenzi wa baba yake." [Muslim]







Hadiyth – 2

وعن عبد الله بن دينار ، عن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رَجُلاً مِنَ الأعْرَابِ لَقِيَهُ بطَريق مَكَّةَ ، فَسَلَّمَ عَلَيهِ عبدُ الله بْنُ عُمَرَ ، وَحَمَلَهُ عَلَى حِمَارٍ كَانَ يَرْكَبُهُ ، وَأعْطَاهُ عِمَامَةً كَانَتْ عَلَى رَأسِهِ ، قَالَ ابنُ دِينَار : فَقُلْنَا لَهُ : أصْلَحَكَ الله ، إنَّهُمُ الأعرَابُ وَهُمْ يَرْضَوْنَ باليَسير ، فَقَالَ عبد الله بن عمر : إن أَبَا هَذَا كَانَ وُدّاً لِعُمَرَ بنِ الخطاب رضي الله عنه، وإنِّي سَمِعتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( إنَّ أبرَّ البِرِّ صِلَةُ الرَّجُلِ أهْلَ وُدِّ أبِيهِ )) .

وفي رواية عن ابن دينار ، عن ابن عمر : أنَّهُ كَانَ إِذَا خَرَجَ إِلَى مَكّةَ كَانَ لَهُ حِمَارٌ يَتَرَوَّحُ عَلَيهِ إِذَا مَلَّ رُكُوبَ الرَّاحِلةِ ، وَعِمَامَةٌ يَشُدُّ بِهَا رَأسَهُ ، فَبيْنَا هُوَ يَوماً عَلَى ذلِكَ الحِمَارِ إِذْ مَرَّ بِهِ أعْرابيٌّ ، فَقَالَ : ألَسْتَ فُلاَنَ بْنَ فُلاَن ؟ قَالَ : بَلَى . فَأعْطَاهُ الحِمَارَ ، فَقَالَ : ارْكَبْ هَذَا ، وَأعْطَاهُ العِمَامَةَ وَقالَ : اشْدُدْ بِهَا رَأسَكَ ، فَقَالَ لَهُ بعضُ أصْحَابِهِ : غَفَرَ الله لَكَ أعْطَيْتَ هَذَا الأعْرَابيَّ حِمَاراً كُنْتَ تَرَوَّحُ عَلَيهِ ، وعِمَامةً كُنْتَ تَشُدُّ بِهَا رَأسَكَ ؟ فَقَالَ : إنِّي سَمِعتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، يَقُولُ : (( إنَّ مِنْ أبَرِّ البِرِّ أنْ يَصِلَ الرَّجُلُ أهْلَ وُدِّ أبيهِ بَعْدَ أنْ يُولِّيَ )) وَإنَّ أبَاهُ كَانَ صَديقاً لعُمَرَرضي الله عنه.

رَوَى هذِهِ الرواياتِ كُلَّهَا مسلم .

Imepokewa kutoka kwake 'Abdillaahi bin Diynaar (Radhwiyah Allaahu 'anhu) Kuwa 'Abdillaahi bin 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) alikutana na Bedui katika njia ya Makkah. 'Abdillaahi bin 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu) akamsalimia akampandisha kwenya punda wake aliye mpaka, akampatia kilemba kilicho kichwani mwake. Ibn Diynaar (Radhwiyah Allaahu 'anhu) akasema: Tukamwambia: "Allaah Akutengeneza, Wao ni Mabedui wanaridhika na mepesi." Akasema 'Abdillaahi bin 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu): "Babake huyu alikuwa rafiki mkubwa wa 'Umar bin Al-Khatw'aab (Radhwiyah Allaahu 'anhu), nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika wema mkubwa ni kwa mtu kuunga vipenzi vya baba yake."

Katika riwaayah ya Ibn Diynaar, Ibn 'Umar (Radhiwyah Allaahu 'anhu) alikuwa anapotoka kwenda Makkah alipochoka kupanda ngamia anapumzika, kilemba anakazia kichwa chake. Alipokuwa hivyo siku moja juu ya punda, akapita bedui, akamuuliza: "Je, wewe ndiye mtoto wa fulani?" Akajibu: "Ndio." Akamtunikia punda, na kumwambia: "Mpande huyu." Na pia akampatia kilemba, kamwambia: "Kifunge kichwani mwako." Baadhi ya maswahibu zake wakamwambia: "Allaah Akughufirie, umempatia huyu bedui punda uliyekuwa ukimtumia kwa safari zako na kilemba ulichokuwa ukifunikia kichwa chako." Akasema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika wema mkubwa kabisa ni mtu kuunga vipenzi wa baba yake baada ya kufa kwake", na babake alikuwa ni rafiki wa 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu). [Zimepokewa hizi riwaayah zote na Muslim]









Hadiyth – 3

وعن أَبي أُسَيد - بضم الهمزة وفتح السين - مالك بن ربيعة الساعدي رضي الله عنه، قَالَ : بَيْنَا نَحْنُ جُلُوسٌ عِنْدَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم إذ جَاءهُ رَجُلٌ مِنْ بَنِي سَلَمَةَ ، فَقَالَ : يَا رسولَ اللهِ ، هَلْ بَقِيَ مِنْ برِّ أَبَوَيَّ شَيء أبرُّهُما بِهِ بَعْدَ مَوتِهمَا ؟ فَقَالَ : (( نَعَمْ ، الصَّلاةُ عَلَيْهِمَا ، والاسْتغْفَارُ لَهُمَا ، وَإنْفَاذُ عَهْدِهِمَا مِنْ بَعْدِهِما ، وَصِلَةُ الرَّحِمِ الَّتي لا تُوصَلُ إلاَّ بِهِمَا ، وَإكرامُ صَدِيقهمَا )) رواه أَبُو داود .

Amesema Abu Usayd Maalik bin Rabi'ah As-Saa'idiy (Radhwiyah Allaahu 'anhu): "Tulipokuwa tumekaa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaja mtu kutoka katika ukoo wa Salimah akasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Je, kumebakia wema wa kuwatendea wazazi wangu baada ya kufa kwao?" Akasema: "Ndio, kuwaombea du'aa, kuwatakia maghfira, kutekeleza ahadi zao baada ya kufa kwao, kuunga kizazi ambacho hakiungiki ila kwa sababu yao na kuwakirimu marafiki zao." [Abu Daawuud]





Hadiyth – 4

وعن عائشة رضي الله عنها ، قَالَتْ : مَا غِرْتُ عَلَى أحَدٍ مِنْ نِسَاءِ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم مَا غِرْتُ عَلَى خَدِيجَة رضي الله عنها ، وَمَا رَأيْتُهَا قَطُّ ، وَلَكِنْ كَانَ يُكْثِرُ ذِكْرَهَا ، وَرُبَّمَا ذَبَحَ الشَّاةَ ، ثُمَّ يقَطِّعُهَا أعْضَاء ، ثُمَّ يَبْعثُهَا في صَدَائِقِ خَديجَةَ ، فَرُبَّمَا قُلْتُ لَهُ : كَأنْ لَمْ يَكُنْ في الدُّنْيَا إلاَّ خَديجَةَ ‍! فَيَقُولُ : (( إنَّهَا كَانَتْ وَكَانَتْ وَكَانَ لي مِنْهَا وَلَدٌ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية : وإنْ كَانَ لَيَذْبَحُ الشَّاءَ ، فَيُهْدِي في خَلاَئِلِهَا مِنْهَا مَا يَسَعُهُنَّ .

وفي رواية:كَانَ إِذَا ذبح الشاة، يقولُ : (( أَرْسِلُوا بِهَا إِلَى أصْدِقَاءِ خَديجَةَ )) .

وفي رواية : قَالَت : اسْتَأذَنتْ هَالَةُ بِنْتُ خُوَيْلِد أُخْتُ خَدِيجَةَ عَلَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، فَعرَفَ اسْتِئذَانَ خَديجَةَ ، فَارتَاحَ لِذَلِكَ ، فَقَالَ : (( اللَّهُمَّ هَالةُ بِنْتُ خُوَيْلِدٍ )) .

Amesema 'Aa'ishah (Radhwiyah Allaahu 'anhaa): "Sijamuonea wivu yeyote miongoni mwa wake wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kama nilivyomuonea wivu Khadijah ilhali sijawahi kumuona kabisa Khadijah (Radhwiyah Allahu 'anhaa), lakini Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akimtaja sana. Mara nyengine alikuwa akichinja mbuzi, akimkata vipande kisha akiwapelekea marafiki za Khadijah. Mara nyengine nilimwambia: "Kama kwamba hakuna duniani ila Khadijah." Akasema: "Alikuwa kadha wa kadha, amenizalia watoto." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Katika riwaayah nyengine: "Alikuwa anachinja mbuzi na kuwazawadia rafikize Khadijah kinachowatosha.

Katika riwaayah nyengine: "Alikuwa anapochinja mbuzi husema: "Wapelekeeni rafiki za Khadijah."

Katika riwaayah nyengine: "Haalah bint Khuwaylid, dadake Khadijah, alibisha hodi kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Akamtambua hodi ya Khadijah (kwa ile sauti), akafurahi kuja kwake, akasema: "Ee Allaah! Huyu ni Haalah bint Khuwaylid."





Hadiyth – 5

وعن أنس بن مالك رضي الله عنه، قَالَ : خرجت مَعَ جرير بن عبد الله البَجَليّ رضي الله عنه في سَفَرٍ ، فَكَانَ يَخْدُمُني ، فَقُلْتُ لَهُ : لاَ تَفْعَل ، فَقَالَ : إِنِّي قَدْ رَأيْتُ الأنْصَارَ تَصْنَعُ برسول الله صلى الله عليه وسلم شيئاً آلَيْتُ عَلَى نَفسِي أنْ لا أصْحَبَ أحَداً مِنْهُمْ إلاَّ خَدَمْتُهُ . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Amesema Anas bin Maalik (Radhwiyah Allaahu 'anhu): "Nilisafiri na Jariyr bin 'Abdillaahi Al-Bajaliyy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) safarini, alikuwa ananitumikia, nikamwambia: "Usifanye hivyo." Akasema: "Mimi nimewaona Answari wakimfanyia hilo Rasuli Wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), hivyo nikala kiapo kuwa kila nitakapofuatana na mmoja nitamhudumia." [Al-Bukhaariy na Muslim]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn





باب إكرام أهل بيت رَسُول الله صلى الله عليه وسلم وبيان فضلهم

043-Mlango Wa Kuwakirimu Watu wa Nyumba ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Kubainisha Fadhila Zao



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:



إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُذْهِبَ عَنكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا ﴿٣٣﴾

Hakika Allaah Anataka Akuondosheeni maovu enyi ahli wa nyumba (ya Nabiy) na Akutakaseni mtakaso barabara. [Al-Ahzaab: 33]





وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّـهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى الْقُلُوبِ ﴿٣٢﴾

Na yeyote anayeadhimisha Ishara za Allaah, basi hayo ni katika taqwa ya nyoyo. [Al-Hajj: 22]









Hadiyth – 1

وعن يزيد بن حَيَّانَ ، قَالَ : انْطَلَقْتُ أنَا وحُصَيْنُ بْنُ سَبْرَة ، وَعَمْرُو ابن مُسْلِم إِلَى زَيْد بْنِ أرقَمَ رضي الله عنه، فَلَمَّا جَلسْنَا إِلَيْهِ قَالَ لَهُ حُصَيْن : لَقَدْ لقِيتَ يَا زَيْدُ خَيْراً كَثِيراً ، رَأيْتَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، وسمعتَ حديثَهُ ، وغَزوْتَ مَعَهُ ، وَصَلَّيْتَ خَلْفَهُ : لَقَدْ لَقِيتَ يَا زَيْدُ خَيْراً كَثيراً ، حَدِّثْنَا يَا زَيْدُ مَا سَمِعْتَ مِنْ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم قَالَ : يَا ابْنَ أخِي ، وَاللهِ لقد كَبِرَتْ سِنِّي ، وَقَدُمَ عَهدِي ، وَنَسيتُ بَعْضَ الَّذِي كُنْتُ أعِي مِنْ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ، فما حَدَّثْتُكُمْ ، فَاقْبَلُوا ، ومَا لا فَلاَ تُكَلِّفُونيهِ . ثُمَّ قَالَ : قام رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يَوماً فينا خَطِيباً بمَاء يُدْعَى خُمَّاً بَيْنَ مَكَّةَ وَالمَدِينَةِ ، فَحَمِدَ الله ، وَأثْنَى عَلَيهِ ، وَوعظَ وَذَكَّرَ ، ثُمَّ قَالَ : (( أمَّا بَعدُ ، ألاَ أَيُّهَا النَّاسُ ، فَإنَّمَا أنَا بَشَرٌ يُوشِكَ أنْ يَأتِي رسولُ ربِّي فَأُجِيبَ ، وَأنَا تارك فيكم ثَقَلَيْنِ : أوَّلُهُمَا كِتَابُ اللهِ ، فِيهِ الهُدَى وَالنُّورُ ، فَخُذُوا بِكتابِ الله ، وَاسْتَمْسِكُوا بِهِ )) ، فَحَثَّ عَلَى كِتَابِ الله ، وَرَغَّبَ فِيهِ ، ثُمَّ قَالَ : (( وَأهْلُ بَيْتِي أُذكِّرُكُمُ الله في أهلِ بَيْتي ، أذكرُكُمُ الله في أهل بيتي )) فَقَالَ لَهُ حُصَيْنٌ : وَمَنْ أهْلُ بَيتهِ يَا زَيْدُ ، أَلَيْسَ نِسَاؤُهُ مِنْ أهْلِ بَيْتِهِ ؟ قَالَ : نِسَاؤُهُ مِنْ أهْلِ بَيتهِ ، وَلكِنْ أهْلُ بَيتِهِ مَنْ حُرِمَ الصَّدَقَةَ بَعدَهُ ، قَالَ : وَمَنْ هُمْ ؟ قَالَ : هُمْ آلُ عَلِيٍّ وَآلُ عقيل وَآلُ جَعفَرَ وآلُ عَبَّاسٍ . قَالَ : كُلُّ هؤلاء حُرِمَ الصَّدَقَةَ ؟ قَالَ : نَعَمْ . رواه مسلم .

وفي رواية : (( ألاَ وَإنّي تَارِكٌ فِيكُمْ ثَقَليْنِ : أحَدُهُما كِتَابُ الله وَهُوَ حَبْلُ الله ، مَنِ اتَّبَعَهُ كَانَ عَلَى الهُدَى ، وَمَنْ تَرَكَهُ كَانَ عَلَى ضَلالَة )) .

Amesema Yaziyd bin Hayyaan: Mimi, Huswayn bin Sabrah na 'Amru bin Muslim tulimtembelea Zayd bin Muslim (Radhwiyah Allaahu 'anhu). Tulipokaa naye, Huswayn akamwambia: "Hakika ee Zayd, umepata kheri nyingi, umemuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), ukasikia mazungumzo yake, ukapigana pamoja naye, na ukaswali nyuma yake. Hakika umepata kheri nyingi,ee Zayd! Tuhadithie Zayd uliyosikia kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Akamwambia: "Ee mpwa wangu! Wa- Allaahi, Nimezeeka, zama zangu zimepita na nimesahau baadhi ya niliyohifadhi kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Nitakacho wahadithia kipokeeni, na ambacho sikuwahadithia musinilazimishe kukizungumza." Kisha akasema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisimama siku moja mahali panapoitwa Khum baina ya Makkah na Madiynah; kutuhutubia, Akamuhimidi Allaah, akamsifu, akaedhea; kisha akasema: "Ama baada ya haya: Fahamuni enyi watu! Hakika mimi ni mwanadamu, anakaribia kunijia Mjumbe wa Mola wangu nami niitikie wito huo, nami nimewaachia vizito viwili: cha kwanza ni Kitabu cha Allaah, ambacho kina uongofu na nuru ndani yake, kichukueni Kitabu cha Allaah ns mshikamane nacho barabara." Akasisitiza mno juu ya kushikamana na Kitabu cha Allaah, kisha akasema: "Na watu wangu wa nyumbani, mkumbukeni Allaah kwa watu wa nyumbani kwangu." Huswayn akamwambia: "Ee Yaziyd, ni nani hao watu wa nyumbani kwake? Wake zake si ni watu wa nyumba yake?" Akasema: "Wake zake ni katika watu wa nyumbani kwake, lakini watu wa nyumba yake haswa ni wale waliokatazwa kula sadaqah baada yake." Akaulizwa: "Na ni kina nani hao?" Akasema: "Hao ni familia ya 'Aliy, familia ya 'Aqiyl, familia ya Ja'far na familia ya 'Abbaas." Akasema: "Wote hao wamekatazwa na kuharamishwa sadaqah?" Akasema: "Ndio." [Muslim]

Katika riwaayah: "Fahamuni kuwa nimewaachieni vizito na vitukufu viwili: Ya kwanza Kitabu cha Allaah, nayo ni kamba ya Allaah. Mwenye kukifuata atakuwa juu ya uongofu na mwenye kukiacha atakuwa juu ya upotevu."





Hadiyth – 2

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، عن أَبي بكر الصديق رضي الله عنه - مَوقُوفاً عَلَيهِ - أنَّهُ قَالَ : ارْقَبُوا مُحَمداً صلى الله عليه وسلم في أهْلِ بَيْتِهِ . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) kuwa Abu Bakr Asw-Swiddiq (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: "Mheshimmuni na mkirimuni Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika familia yake." [Al-Bukhaariy]
 
Back
Top Bottom