Ramadhan Special Thread
Baadhi ya post za zamani...

JE, UNAJUA KUWA ROHO HUWA INATOKA?

Hivi umeshawahi lala usiku halafu ukajikuta kama unaota hivi lakini fahamu zako zinakuonyesha kabisa upo macho na unajiona mwepesi Sana pasipo kawaida na saa nyingine huenda ukahisi kama upo hewani hivi

Au

Unaweza kwenda sehemu Fulani ambayo hujawahi fika lakini kuna kumbukumbu Fulani inakujia kana kwamba hiyo sehemu unaijua au ushawahi fika hivi.

Kifupi ni kwamba roho zetu huwa zinatoka katika viwili viwili vyetu na kwenda kupiga misele sehemu mbali mbali na mara nyingine hukutana na roho nyingine za ndugu zetu,ndio maana utasikia mtu atakwambia Jana nilimuota babu ananiambia moja mbili tatu na mara nyingi watu hao walikuwa Wacha Mungu.

Anyways sasa ni hivi, Kwa kawaida tunapo lala basi roho zetu huenda Kwa Mwenyezi Mungu kila siku ya Maisha yetu hapa duniani,sasa huenda zinaporudi ndio hukutana na roho nyingine na kukutana na matukio mbali mbali.

Kwa mujibu wa Qur'an inasema hivi Mwenyezi Mungu huzipokea roho zinazo kufa Kwa maana roho ambazo watu wameaga dunia,na roho ambazo watu wanakuwa wamelala,zile roho ambazo Mda wa kufa umefika huzizua na kubaki nazo,ndio hapa utasikia Fulani bwana kafa usingizini ujue roho yake haikurudi tena usiku huo na wale ambao mdao WA kufa bado basi Mwenyezi Mungu huziachia zile na kurudi katika miili yetu.

"MWENYEZI MUNGU huzipokea roho zinapo kufa. Na zile zisio kufa wakati wa kulala kwake, huzishika zilizo hukumiwa kufa, na huzirudisha nyengine mpaka ufike wakati uliowekwa. Hakika katika hayo bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri."
Azzumar : 42

Hayo ndio mambo ya Mwenyezi Mungu hakika mambo yake hakuna ayajuaye na hufanya katika namna atakavyo.

Ndio maana inatakiwa usiku Tulalapo basi tuombe msamaha na kuomba toba Kwa makosa yetu tuliyo fanya kutwa nzima kwani hatujui kama kesho tutaamka salama au laa!
 
Baadhi ya post zangu za zamani....

KWA TABIA HII,UNATOFAUTI GANI NA IBILISI

Tabia iliyomponza Ibilisi ni KIBURI. Baada ya kuambiwa na Mwenyezi Mungu amsujudie Adam sijida ya heshima basi yeye alikataa Kwa kujawa na Kiburi kwasababu yeye alijiona Bora sana.

Na alipoambiwa kwanini ulikataa kumsujudia Adam akasema;

Mimi ni Bora nimeumbwa Kwa Moto na yeye ameumbwa na Udongo

Kwahiyo Ibilisi akajiona yeye ni Bora zaidi ndio maana akakataa amri ya ya Mola wake.

Na Mwenyezi Mungu anasema hakika Kiburi ndio vazi lake kwahiyo yeyote ambaye analeta kiburi basi anafanya kosa kubwa Sana.

Na ili ujue Kibri ni kosa kubwa Sana mpaka Mwenyezi Mungu akamhukumu Ibilisi aende Motoni ,ebu tuangalie Ibilisi alikuwa wa namna gani.

Inasemwa Ibilisi alikuwa anafanya ibada Sana kiasi ambacho hakuna sehemu yoyote katika ardhi hakuacha Kusujudu,alisujudu kila sehemu Kwa AJILI ya kumwabudu Mola wake

Lakini

Pamoja na yote hayo basi Kiburi kikamuweka mbali na Mola wake na kuhukumiwa adhabu mbaya kabisa

Sasa baadhi yetu nasi tuna Uibilisi Fulani hivi ingawa ukitutazama machoni tunaonekana kama watu vile lakini tumejawa na Kiburi kupindukia katika Maisha yetu.

Kisa wewe ni CEO sehemu Fulani basi unajiona wewe ndio wewe, unajiona mpanaaa na wengine wote unawaona hawana maana kabisa,husikilizi shida za wafanyakazi wako,hujali mahitaji Yao kwasababu wewe ndio kila kitu hapo,usichojua ni kwamba kila kitu kina mwisho na IPO siku hiyo nafasi utaiacha, kwahiyo usitumie cheo kunyanyasa watu.

Malecture mpo? Nyie nanyi huwa mnajiona mko juu Sana kwasababu Maisha ya taaluma ya mwanachuo yapo mikononi mwenu basi mmejawa na Kiburi kuwa angamiza wanafunzi wenu tena saa nyingine kwasababu za kipuuzi Sana,machoni mnaonekana kama watu lkn mna Uibilisi Fulani hivi.

Madaktari na Manesi mpo? Nyie nanyi kwakuwa afya za binadamu wenzenu zipo mikononi mwenu basi Kiburi ni sehemu ya Maisha yenu. Mko radhi wagonjwa wafe au waendelee kupata maumivu kwasababu tu ya kiburi chenu,tena hawa manesi ndio balaa kabisa, mnayowafanyia wanawake wenzenu huko sehemu za kujifungua yaani Mungu Tu ndio anajua kwakweli, acheni Kiburi mwisho wenu utakuwa mbaya Sana.

Wana usalama kwanza nawapa Salute Kwa heshima yenu! Lakini nanyi pia huwa mnazingua Sana mnapokuwa katika majukumu yenu,kwa nafasi yenu huwa mna Kiburi Sana kwakuwa mna nguvu ambayo mmepewa na Katiba,niwakumbushe Tu ubinadamu ndio kila kitu katika Maisha IPO siku utaacha hayo majukumu na utarudi mtaani na huenda karma itafanya kazi yake.

Hiyo ni mifano michache Tu ambayo nimeitumia lkn watu viburi ambao Wana Uibilisi ndani yake wapo wengi Sana na wanakiburi Sana Kwa nafasi zao hadhi zao walizo kuwa nazo.

Niwakumbushe Tu kwamba Kiburi ni vazi la Mwenyezi Mungu kwahiyo unapokuwa Kiburi ni kana kwamba unataka kuchukua vazi lake nadhani mwisho wake unaujua utakuwaje.

Niwakumbushe nyie ni viumbe wa Allah hamna mnachokimiliki hapa duniani, kwahiyo muishi vizuri na watu na muwatendee wema daima dawamu ili muwe na mwisho mwema.
 
Ni hapo baadae kwenye kipengele chetu pendwa cha Maswali na Majibu

Hukujia kila siku jioni/usiku

Assalaam alaikum warahmatullah wabarakatu...
 
Akiokota Kitu Cha Thamani Njiani Je Ni Miliki Yake?
Maswali: Mchanganyiko
SWALI:



Assalam aleykum wa rahmatullah wa barakatuh,



Suala langu ni hili lifuatalo:-



Ikiwa mtu kaokota kitu njiani, madukani, ikiwa pesa, dhahabu, camera au kitu chochote kile, jee inaweza achukue au aulize kwanza?



JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kiokotwa. Katika istilahi ya kisheria inaitwa Luqtwah (Kuokota). Hii ina maana ya kukuta kitu kilichoachwa katika sehemu isiyokuwa na mmiliki na hali hiyo ni kama kukuta mtu Muislamu kwenye njia yoyote pesa au nguo na akaogopea kupotea kitu hicho itabidi akiokote.



Sheria ya Kiislamu inaruhusu kuokota kilichoachwa kama alivyoulizwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), naye akajibu:



"Taja mfuko wake na kifuniko chake halafu ukitangaze mwaka mzima, akija mwenyewe atakichukuwa na kama hakutokea kitakuwa ni chako" (al-Bukhaariy na Muslim).




Na aliulizwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ikiwa kitu kilichookotwa ni mbuzi/ kondoo, akasema:




"Mchukue kwani huyo ni wako au ni wa nduguyo au ni wa mbwa mwitu" (al-Bukhaariy, at-Tirmidhiy na Ibn Maajah).



Zipo kanuni Fulani za suala hili, nazo ni kama zifuatazo:

Kikiwa kitu kinachookotwa ni kitu duni ambacho hakina umuhimu wowote kwa watu kama vile tumba moja la tende, zabibu au kitambaa au bakora itakuwa si vibaya kukiokota na muokotaji atafaidika nacho wakati ule ule anapokiokota wala halazimiki kukitangaza na kukihifadhi. Na hilo ni kwa kauli ya Jaabir (Radhiya Allaahu 'anhuma): "Alituruhusu Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika fimbo, bakora na kamba na mfano wa vitu hivyo mtu akiviokota afaidike navyo" (Abu Daawuud).
Kikiwa kitu kilichookotwa ni chenye thamani katika jamii itampasa aliyeokota akitangaze mwaka mzima. Akitangaze kwenye milango ya Msikiti, sehemu za mkusanyiko wa watu au kupitia kwenye magazeti na Radio au vyombo vingine vya habari. Akija mwenyewe akakitaja kwa sifa zake, itabidi apewe na kama hakuja baada ya mwaka kamili atakitumia au atakitoa sadaka akitaka.
Kiokotwa cha Makkah hakifai kuokotwa ila kitakapohofiwa kupotea. Na mwenye kukiokota itampasa akitangaze muda wa kuwa bado yuko Makkah na akitoka Makkah atakipeleka alichokiokota kwa kiongozi na wala si haki yake kukimiliki. Kwa kauli yake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), mji wa Makkah ni haramu (mtukufu) hakiokotwi kitu.
Kiokotwa aina ya mnyama kinaitwa mnyama aliyepotea akiwa porini inafaa kumuokota na kunufaika naye kuanzia wakati huo kwa kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) iliyo hapo juu. Na mfano wa ngamia aliyepotea, punda, nyumbu na farasi waliopotea huitwa 'wapuuzwa' kwani hairuhusiwi kuwaokota.
Tumejibu kwa kina kidogo ili ikusanye mambo mengi kuhusu kiokotwa. Ama kuhusu swali lako jawabu lake lipo wazi katika kipengele cha pili hapo juu.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Alama Ya Mwezi Katika Misikiti
Maswali: Mchanganyiko


SWALI:

Nimefurahi sana kuona namna website hii nzuri kwa waislamu inavyotoa nafasi ya kuuliza maswali.

Swali: KWA NINI MISIKITI MINGI IMEWEKEWA ALAMA YA MWEZI? KAMA ALAMA HII NDO INATUMIKA KUASHIRIA MSIKITI,VP ISITUMIKE ALAMA NYINGINE KM JUA, MBINGU, MILIMA N.K. KWA SABABU VYOTE HIVI NI VIUMBE VYA M MUNGU NA NI ISHARA YA KUWEPO KWA ALLAH. SWALI HILI LINANICHANGANYA SANA WAISLAM WENZANGU. NAOMBA MSAADA NA NI JUZI TU MNASWARA ALINIULIZA NIKAMWAMBIA KUWA SIJUI NA TUKAELEWANA NAE KUWA NIFUATILIE









JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.




Kwa hakika alama na ishara hizo hazina umuhimu wala maana yoyote katika kuwekwa katika Misikiti au sehemu nyingine zozote. Kwani wakati wa Mtume (Swalla-Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake (Radhiya-Allaahu 'anhum) alama kama hizo zilikuwa hazipo.

Baada ya hapo huenda Waislamu wakaamua kuwa wawe na ishara kama vile Mayahudi na Manaswara, kwani Mayahudi wana ile ishara ya nyota ya Daudi ambayo ina pembe sita na Manaswara wana ishara ya kuwa na msalaba. Kwa kuwa sisi huwa tarehe zetu za siku na miezi yetu hufuata mwezi, basi baadhi ya Waislam wakaona kuwa waweke hiyo alama ya mwezi kama nembo, lakini kiuhakika haina maana yoyote ya kisheria.

Na Allah Anajua zaidi.
 
Amepoteza Pesa Je, Inapasa Kumshuku Mtu Yeyote?
Maswali: Mchanganyiko



SWALI:




Asalamu alaykum,




Natumai kwa nguvu za Allah nyote hamjambo.




Mimi kwangu naishi na mwanangu wenye miaka kumi (mtoto wa mdogo wangu) na mchumba wangu uwa anakuja kutembea. Miezi miwili iliyopita rafiki yangu alikuja kutembea hapa katika mji wetu, lakini akapata matatizo kidogo na mwenyeji wake, hivyo akaomba hifadhi kwangu. Nimekaa miaka mingi na watu lakini sijawahi kukutwa na jambo hili.




Jumatatu 02/11/2009 nimegundua kama dola mia tatu nilizokuwa nimeziweka chumbani kwangu katika wallet, hazimo nimetafuta mpaka leo hii sijazipata. Mgeni wangu huyu amesafiri siku ya Jumanne 03/11/2009 kwenda kwao kusalimia. Nimepanga akirudi niwaulize watu wote ambao wanaingia kwangu na wanaweza kuingia chumbani kwangu. Pia nimepanga wote niwaapishe kwamba wayasemayo ni kweli mbele za Mola, na baada ya hapa basi nitashukuru na kutafuta pesa za watu sasa nizilipe.




Imekuwa ngumu kwangu kuamini kama pesa zinaweza kupotea ndani ya nyumba? Haijawahi kutokea miaka yote na nimeishi na watu wengi tu ambao si ndugu zangu lakini sijawahi kuona mambo haya. Mwanangu DOLA MIA 3 (US$ 300) atazipeleka wapi? Mchumba wangu nimemuuliza kasema hajachukua, Mgeni wangu sikupata kumuuliza kwani ile siku ya mwanzo nilisema nisiulize labda mimi binadamu nimesahau hivyo niangalie kwanza, kwani mtu mwingine ukimuuliza ndiyo ingekuwa uhasama. Lakini kwa sasa sina jinsi lazima nimuulize!!!!!




JE NINAYOTAKA KUFANYA NI SAHIHI? JE NINYI MNAUSHAURI WOWOTE KWANGU? WABILAHI TAWFIQ.




JIBU:




Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.




Shukrani kwa swali lako kuhusu kupotea pesa chumbani kwako.

Hakika ni kuwa mwanaadamu ameumbwa katika maumbile ya sahau, papatiko na pia uharaka wa kuamua mambo – mema na mabaya. Kuhusu hilo lililotokea yumkinika pia kuwa umepoteza nje na hukufika nazo nyumbani kwako au umezipoteza nje.

‘Alaa kulli haal, ikiwa pesa zimechukuliwa kweli chumbani kwako wale ambao unatakiwa kuwauliza ni wale wenye kuingia kwenye chumba hicho. Wala huwezi kusema mtoto wangu wa miaka kumi hawezi kuchukua. Pia naye anaweza kuchukua bila ya wasiwasi. Hilo ni kuwa mara ngapi tumepata kusikia jinsi gani mtoto alichukua pesa za baba yake zilizo nyingi akaenda akazitumia pamoja na marafiki na huku anajificha. Unaweza kuchunguza hilo kwa kuwauliza marafiki zake walio watoto kama yeye kama walikuwa wakipewa vitu na mtoto wako. Hiyo pia inategemea na tabia za mtoto wako zikoje.




Kabla ya kumuuliza huyo mgeni wako unatakiwa ujibu swali hili: Je, mgeni wako alikuwa amepewa ruhusa nawe kuingia chumbani mwako? Na je, alikuwa akiingia ukiwa upo? Ikiwa jawabu ndio basi una haki ya kumuuliza lakini kwa njia iliyo njema na nzuri ili msiharibu uhusiano kwa kitu ambacho huenda hata hakufanya.




Hayo ambayo umeamua kuyafanya hayana neno isipokuwa ni vyema kuwauliza bila ya kuwaapisha na ukaswadiki wanayoyasema. Ikiwa hakupatikana mtu basi fanya subira na Allaah Aliyetukuka Atakulipia yaliyo mema na mazuri kuliko hizo pesa.




La mwisho ni nasaha kwako ndugu yetu kwani katika suala lako umesema kuwa una mchumba ambaye anakutembelea. Ikiwa kama tulivyoolewa mchumba, ni kuwa yule uliyemposa na una maandalizi ya kumuoa. Na kama ni hivyo, basi fahamu kuwa hairuhusiwi wewe kuwa na ukaribu au kutembeleana na mchumba wako. Hilo ni jambo lisilofaa na ikiwa tena anakuja na kukaa chumba kimoja na wewe hilo ni haraam na pia unatoa picha mbaya kwa mwanao huyo wa miaka 10 pindi akijua kuwa hilo haliruhusiwi litamfanya apoteze heshima na wewe na pia utakuwa unamfundisha kuwa na mahsiano na mwanamke ambaye hajamuoa.

Unaruhusiwa kumtembelea huyo mchumba akiwa kwa wazazi wake na ukiwa pamoja nao na si faragha wewe na yeye. Kumbuka mnapokuwa wawili faragha basi watatu wenu ni Shaytwaan ambaye kazi yake ni kuwashawishi mfanye maovu na maasi.




Na ikiwa huyo mchumba si yule uliyemposa bali ni yule anayejulikana kikafri ‘girl friend’, basi hiyo ni haraam kabisa na maovu yasiyofaa kufanywa na Muislamu. Kwa hiyo kumbuka kuwa usije ukawa unalalamika na pesa zilizoibiwa na hali wewe unamuibia Allaah haki Zake za utiifu na kwenda kinyume na maamrisho Yake.




Na Allaah Anajua zaidi
 
Asiyejulikana Yuko Wapi
Deni La Mtu Asiyejulikana Yuko Wapi
Maswali: Mchanganyiko








SWALI:

ASSALAM ALAIKUM

NATEGEMEA MWENYEZI MUNGU ANAENDELEA KUKUPENI NGUVU ZA KUWEZA KUTUJIBU MASWALI YETU

MIMI SWALA LANGU. ZAMANI NILIKWENDA DUKANI NA KUNUNUA KITU NA IKAWA BADO PESA KIDOGO HAZIJATIMIA NA MWENYE KUUZA ALINAMBIA KUA NIPE ULICHONACHO KILICHOBAKI UKIPATA UTANILETEA SASA NILIPOKIPATA NIMEMTAFUTA PAHALI NILIPOKUA NIMENUNUA KILE KITU KWAKE SIKUMPATA NA NIMEJARIBU TENA KUMTAFUTA SIKUMUONA SASA VIPI HIZI PESA NAWEZA NIKAZITOA SADAKA AU NIFANYE NINI MAANA NINA WASIWASI NA ZINANIKERA NA SASA HATA NIKIMUONA NITAKUA SIMJUI. VIPI NAOMBA MNISAIDIE.

NA SWALI JENGINE KUNA MTU ALIKWENDA DUKANI NA MTOTO NA PIA PESA ILIOBAKI KWA YULE MTU MWENYE DUKA ALIMWAMBIA KUA UKIZIPATA NILETEE SASA ALIPOFIKA KWAO ALISEMA MWENYE DUKA AMESEMA ZILIZOBAKI ZIPELEKWE NA HUYU MTOTO ANAPAJUA NI WAPI LAKINI ZILIPOPATIKANA ZINATAKA KUPELEKWA HUYO MTOTO MDOGO ANAULIZWA NI WAPI ANASEMA KUWA HAPAJUI TENA NA HUYO MTU ALIEACHA HAYO MAAGIZO KESHAKUFA NA HIZI PESA BADO ZINAWAKERA SASA WAFANYE NINI SHEIKH




JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.







Tunamshukuru Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa neema chungu mzima ambazo Ametupatia sisi kama wanaadamu na hasa kama Waislamu. Tunashukuru kwa swali hili kuhusu mkopo. Kwa hakika tunampongeza dada yetu kwa kuwa na Imani ya kutaka kuona kuwa amelipa deni analodaiwa kabla ya kufariki. Kwa hakika deni halisamehewi mpaka lilipwe au anayekudai akusamehe. Na ilikuwa ada ya Mtume wa Allah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kutomswalia mtu yeyote mpaka ahakikishe kuwa hana deni au akiwa nalo basi jamaa yake achukue ahadi ya kulilipa.

Na juhudi zako zinaonyesha kuwa una hamu kubwa ya kukamilisha madeni ya wanaadamu hapa hapa duniani. La kutambua ni kuwa Allah Haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri iwezavyo.

((Mwenyezi Mungu Haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo))

(2: 286)

Nawe umejaribu njia zote kuweza kumpata lakini bila ya mafanikio.

Inavyokupasa kufanya sasa ni moja katika yafuatayo:

1) Kuziweka hizo hela na lau atakuja mtu kukwambia kuwa anakudai basi umwamini na umpe ikiwa atataja kiwango ambacho ni sawa na kile unachodaiwa. Na ni vyema katika wasiya wako uandike na uwaachie warithi wako wajue kuwa unadaiwa na mtu hela kadhaa, na atakapotokea wakati ushafariki basi apatiwe. Ikiwa hajapatikana kabisa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) atakusamehe kwa kuwa umefanya juhudi zako zote za kulipa deni hilo kwa mwenyewe.

2) Ukipenda utoe hizo pesa sadaka kwa nia ya huyo mtu kwa sharti kwamba pindi atakapotokea umuelezee ulivyofanya, na ikiwa ataridhika sawa, na kama hakuridhika basi uwe tayari kumlipa wewe pesa zake na muombe Allaah Akutaqabalie zile ulizotoa mwanzo kuwa ziwe ni sadaka yako.

Kuhusu deni la mwenye duka inawapasa kwanza wazazi wa huyo mtoto wafanye juhudi zote za kumtafuta mwenye duka kwa kuuliza wenye maduka yaliokaribu yao kama yupo mwenye kudai kwa kuelezewa kuhusu mtoto huyo aliyefariki, na kama hakupatikana basi wazazi wafanye hivyo hivyo kama tulivyoeleza hapo juu.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Fulana Zenye Nembo Ya Klabu Za Mpira
Maswali: Mchanganyiko


SWALI:

Asalam aleykum


ni nini hukumu ya kuvaa fulana zenye nembo ya klabu za mpira kama Manchester au Arsenal?






JIBU

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.




Jazakallahu khayran kwa swali hili kutoka kwa kikundi chenye jina hapo juu.



Ikiwa fulana zina nembo ambazo zinaruhusiwa kisheria basi hazina neno wala hakuna tatizo lolote kuhusu hilo. Lakini zikiwa ni kinyume na hivyo itakuwa haifai kwa Muislamu kuzivaa. Fulana ili kuruhusiwa hazitakiwi ziwe na:

1) Tangazo la kitu au vitu haramu mbele au nyuma yake.

2) Maandishi nyuma ya fulana kwani humshughulisha mtu anayeswali nyuma yake na kumwondolea khushui (unyenyekevu). Na katika hili Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam ) amekataza kuswali na nguo yenye picha au marembo mbali mbali (Al-Bukhari na Muslim kutoka kwa Mama ‘Aishah [Radhiya Allaahu 'anhaa]). Na mara nyingi huwa tunavaa fulana hizi kwa kuwa sisi ni mashabiki wa timu hizo na zikiwa zinacheza basi huwa tunaswali na huku tumezivaa.

3) Mavazi hayo hayatakiwi yafanane na mavazi ya kikafiri kwani hilo amelikataza Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) au kuivaa kwa sababu ya kumpenda yule mchezaji kupita watu wengine wowote. Na katika hili Allah (Subhaanah wa Ta'ala) amekataza katika Surat At-Tawbah.

((Enyi mlio amini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu kuwa vipenzi vyenu ikiwa wanastahabu ukafiri kuliko Imani. Na katika nyinyi atakaye wafanya hao ndio vipenzi vyake, basi hao ndio madhaalimu))

((Sema: Ikiwa baba zenu, na wenenu, na ndugu zenu, na wake zenu, na jamaa zenu, na mali mliyo yachuma, na biashara mnazo ogopa kuharibika, na majumba mnayo yapenda, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Allaah na Mtume wake na Jihadi katika Njia yake, basi ngojeni mpaka Allaah Alete amri Yake. Na Allaah Hawaongoi watu wapotovu)) (At-Tawbah: 23 -24)



Hivyo, ni bora tujiepushe kuvaa fulana hizo ili tusije tukaingia katika matatizo tuliyoyataja.

Na Allah Anajua zaidi.
 
Inafaa Kununua Kitu Kilichoibiwa?
Maswali: Mchanganyiko



SWALI:

Je yafaa kununua kitu ambayo imeibiwa? na ni kama waihitaji hiyo kitu sana na huna uwezo wa kununua pia haifai??









JIBU:

Sifa zote njema anastahiki Allah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho




Haifai kununua kitu ambacho unajua kuwa kimeibiwa kwa sababu zifuatazo:

1) Kwanza utakuwa unampa nguvu mwenye kuiba aendelee kuiba na kuuza vitu vya wizi na kupata chumo lisilo halali, hivyo kuacha kununua kwake itakuwa ni fundisho kwake. Na pia inakupasa kumnasihi aache kufanya hivyo maadam umejua kuwa amefanya makosa hayo.

2) Kitu cha haramu huwa hakifai kutumika kwa vyovyote, ikiwa ni chakula au nguo au kitu chochote cha matumizi ya kila siku kwani Allaah سبحانه وتعالى Hapokei kitu chochote kibaya. Na pia huwa hapokelewi mtu du'aa zake kama anachuma chumo la haram au kula, kutumia na kufanyia kwa kile cha haram alivyosema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم :

( يا أيها الناس إن الله طيب لا يقبل إلا طيبا ، و إن الله أمر المتقين بما أمر به المرسلين فقال : ((يَا أَيُّهَا الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ)) (المؤمنون 51) و قال : ((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ كُلُواْ مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ )) (البقرة 172) ثم ذكر الرجل يطيل السفر أشعث أغبر يمد يديه إلى السماء يا رب يا رب و مطعمه حرام و مشربه حرام و غذي بالحرام فأنى يستجاب لذلك)) رواه مسلم .

Allah ni Mzuri na Hapokei ila kilicho kizuri. Na Allah Amewaamrisha wenye kumcha Mungu kama Alivyowaamrisha Mitume Aliposema: ((Enyi Mitume! Kuleni vyakula vizuri na tendeni mema. Hakika Mimi ni Mjuzi wa mnayoyatenda)) [Al-Muuminuun 51] Na Akasema: ((Enyi mlioamini! Kuleni vizuri Tulivyokuruzukuni )) [Al-Baqarah: 172] Kisha (Mtume صلى الله عليه وآله وسلم) akataja kisa cha mtu aliyekuwa safarini akiwa katika hali ya uchafu na mavumbi akiinua mikono yake mbinguni akiomba ((Ee Allaah, Ee Allaah, na hali chakula chake ni haram, kinywaji chake ni haram na kurutubika kwake Ni haram vipi atakubaliwa du'aa yake?)) [Muslim]

Na tuchukue mifano mema ya kutoka kwa waja wema wa zamani ambayo ina mafundisho makubwa yenye kuzidisha iymaan na taqwa.

Inasemekana kuwa Imaam Abu Haniyfah alijizuia kula mbuzi kwa muda wa miaka ya kukisia umri anaoishi mbuzi tokea kuzaliwa hadi kufa, kwa sababu tu wakati huo aliibiwa mbuzi mjini na hakujulikana nani aliyemuiba au kujulikana huyo mbuzi ni yupi.

Wa Allaahu A'alam
 
Inafaa Kushirikiana Na Makafiri Kuwachangisha Pesa Waislamu Wenzao Kuzitumia Kwa Siri?
Maswali: Mchanganyiko


SWALI:


Asalam Aleikum, Natarajia U mzima na Allah s.a.w, Apate kukuhifadhi na kukupa afya. Sheke nilikuwa na swali au ombezi moja na natarajia utanifafanulia au kunijibu hili hoja ambalo linalo ni kera sana

kuna watu ambao wanaowahubiria wasio kuwa waislamu (wakristo) kupitia kitabu chao, na kupata kuwasilimisha wengi sana, kwangu mimi nimefurahia jambo hili. Lakini kitu kinacho ni kera ni kuwa kuna baadhi yao wanaoshirikiana na wasiokuwa waislamu kuandaa mikutano hayo halafu kuchangisha na kugawanana nao hela. je uislamu unaruhusu jambo hili la baadhi ya wahubiri kushirikia na makafiri yaani kupanga kama game hivi halafu kula pesa za wailsamu kwa siri je yafaa ? naomba kama unaweza kunisaidia na aya au hadithi au kauli ya mwanachuoni yeyote yule abainishaye uchafu huu kupitia kitabu na sunnah. natarajia kama unaweza uniandikie kama nakala hivi


wasalam aleikum



JIBU:


Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu kushirikiana kwa Waislamu na Wakristo katika ukusanyaji wa pesa katika mihadhara.

Uislamu umeweka misingi ya ukweli na uaminifu na mlinganiaji Muislamu anatakiwa awe aifanye kazi ya ulinganiaji kwa kufuata maadili bora katika ulinganizi kama yalivyofundishwa na Uislamu. Muislamu haifai kumdanganya hata asiyekuwa Muislamu kwa njia yoyote ile.


Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitutahadharisha kwa kutuambia: “Mwenye kutudanganya si katika sisi” (Muslim).

Na haifai kwa Muislamu kushirikiana na hata Muislamu mwenziwe licha ya Mkristo katika kuwalaghai na kuwatapeli wanaadamu pesa au kitu chochote kingine. Hivyo, jambo hilo ambalo linafanywa halifai na pesa hizo zinakuwa ni za haramu kwao kutumia.




Na Allaah Anajua zaidi
 
Kuhusu Ndoto na Tafsiri Yake
Maswali: Mchanganyiko
SWALI:



Asala alaikum warahmatullah wabarakatu,

Swali langu ni hili: mimi nikiswali swala ya haja huwa mara nyingi naota kama nimefanikiwa kwenye mambo yangu lakini najikuta ni opposit, na sijuwi ni sababu gani.



Swala la pili napenda sana kuota ninasoma souratil fatha nawomba nipewe tafsiri ya ndoto hiyo pamoja na kuwota sana kama nawogota dhahabu.


Asalama alaikum warahmatullah wabarakatu



JIBU:


Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.


Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuota ndoto na tafsiri yake.

Kabla hatujaingia katika lako tungependa kukufahamisha kuwa hakuna Swalah inayoitwa Swalaatul Haajah (au Swalaah ya Haja) kwani Maulamaa wamesema Hadiyth inayoeleza Swalah hiyo ni dhaifu na isiyokubalika, bali ile ambayo ipo ni Istikhaarah. Nayo inaswaliwa ikiwa Muislamu anataka kufanya jambo na hajui lipi ndilo la kheri.

Bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:



Je, Swalatul-Haajah Ni Sahiyh Na Ipi Duaa Yake?


Ama kuhusu maswali ya ndoto, hatuna elimu nayo, na hakuna wengi wanaoweza kutafsiri ndoto kwa wakati huu na wachache wanaojiingiza huko ni wale wasio wakweli. Hivyo tunakushauri usiwe unaendekeza sana ndoto na kuzifanyia kazi au kuzitafutia majibu yake, bali shughulika sana na mafundisho sahihi ya Diyn na yafanyie kazi yale uliyoamrishwa na Qur-aan an Sunnah na yaache yale uliyokatazwa nayo, utasalimika.

Hata hivyo, kuja kupata kitu kinyume na ulivyoota ni mtihani kutoka kwa Muumba wetu kukupima kama tutabaki katika Dini yake au utakwenda kinyume. Ikiwa utabaki na msimamo wako wa Diyn itakuwa kheri kwako hapa duniani na kesho Akhera. Ukienda kinyume na hivyo hasara itakuwa kwako.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Kujiangalia Katika Kioo Usiku Haifai?
Maswali: Mchanganyiko


SWALI:


Allah awalipe ndugu zangu katika Imani kwa kazi nzito mnayoifanya na awafanyie sahali ndani ya kazi hii, awafanyie sahali ndani ya maisha ya dunia na Akhera.

Swali: Nimepata kumsikia mmoja wa wahadhiri wa Kiislamu, akisema haifai kwa muislamu kujiangalia kwenye kioo wakati wa usiku. Naomba ufafanuzi juu ya kauli hii. Asante










JIBU:


Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa ndugu yetu aliyeuliza swali hilo. Ingekuwa ni bora kwa ndugu aliyesikia muhadhara huo kutuandikia nasw ya Hadiyth ili tupate kuiangalia. Mas-ala ya kujitazama kwenye kioo yamekuja kwa ujumla bila kuainisha wakati wenyewe.


Miongoni mwa Hadiyth ni kile kitendo cha ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhuma) aliyejitazama mara moja kwenye kioo kwa kitu kilichokuwa kikimsumbua akiwa katika hali ya Ihraam (Maalik). ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) ameHadiythia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa akijitazama kwenye kioo alikuwa akisema:

“Sifa zote njema anastahiki Allaah, Ee Allaah! Nijaalie niwe na tabia nzuri kama Ulivyolifanya umbile langu kuwa zuri” (Ibn As-Sinniy).




Hizi Hadiyth ni za jumla kumaanisha wakati wowote. Kwa hiyo, kutofaa jambo lolote ni lazima kuwe na dalili. Twatumai utakuwa umepata picha sahihi ya suala hilo.




Na Allaah Anajua zaidi.
 
Skip to main content

Ukurasa Wa Kwanza
Search form
Tafuta
Submit
Ukurasa Wa Kwanza /Kulinganisha Vitu Viwili kwa Ubora
Kulinganisha Vitu Viwili kwa Ubora
Maswali: Mchanganyiko
SWALI:



assalam alaykum,

nayaleta masuali yangu nikitaraji mafanikio kwanza nihakki kwa muislamu kuuliza mfano wasuali hili? Ni nani ama ipi bora Qur-an ama mtume alayhi swalat was salam? Pili ni nani bora jibril alayhi salam ama mtume alayhi swalat was salam? Tafadhali mutakapo nipa jawabu nipeni kwa dalili ambayo itakua nisilaha yangu kama muumin itokamane na Qur-an na hadith mola awazidishie kheir aijaalie saay yenu iwe mashkura. Shukran



JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu kulinganisha baina ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Qur-aan au Jibriyl (‘Alayhis Salaam).

Mwanzo tungependa kuelezea kuwa yapo maswali mengine ambayo hayatufaidishi chochote katika Uislamu wetu, Imani yetu na mustakbali wetu Kesho Akhera.

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuonya kuhusu kuuliza maswali mengi kwani kufanya hivyo kunatupeleka pabaya. Amesema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

“Hakika waliangamia waliokuwa kabla yenu kwa wingi wa maswali yao, na kukhitalifiana kwao na Mitume yao” (al-Bukhaariy na Muslim).

Maswali mengi ambayo hayana msingi wala faida si vyema katika Dini kwani huenda yakaleta natija mbaya kwa muulizaji. Ndio Allaah Aliyetukuka Akasema:

“Enyi Mlioamini! Msiulize maswali ambayo lau mtafunuliwa, yatawaletea matatizo” (al-Maa’idah [5]: 101).

Hata hivyo, yapo maswali ambayo ni muhimu kwa Muislamu kupata majibu ikiwa kweli anataka kujua ili moyo wake utulie kama alivyotaka hivyo Nabii Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) {al-Baqarah [2]: 260}.

Ama kuhusiana na maswali yako mawili ni wazi kabisa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni bora kuliko Qur-aan na pia Jibriyl (‘Alayhis Salaam). Hiyo ni kuwa yeye ndiye aliyeteremshiwa Qur-aan na Allaah Aliyetukuka kupitia kwa Malaika Jibriyl ili kuifundisha. Yeye ndiye kiumbe bora kuliko viumbe vyote, ambaye atawaombea watu wahukumiwe na Allaah Aliyetukuka Siku ya Qiyaamah. Na kuonyosha ubora wake wakati wa safari ya Mi‘raaj, ilifika sehemu ambayo Jibriyl alimuambia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa hapo ndio mwisho wake hawezi kwenda zaidi. Kuanzia hapo Nabii Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikwenda peke yake kukutana na Allaah Aliyetukuka. Na yapo mengi mengine matukufu ya Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yanayoonyesha na kuashiria ubora wake ukirejea katika Qur-aan na Siyrah yake utayajua.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Baadhi ya post za zamani...

MPAKA TUNAINGIA MAKABURINI HATUJA TANGULIZA CHOCHOTE


Hakika binadamu ameshughulishwa Sana na wingi WA kutafuta Mali mpaka amesahau kesho itakuwaje,amesahau hakika hapa duniani yeye ni Msafiri na Mda wowote ataondoka.

Mwenyezi Mungu anatutaka tutafute dunia yetu na Akhera yetu pia,Kwa maana tupambane tupate ridhiki ya halali tupate Kula vya halali na kuvaa vya halali na kuwa na Maisha Bora kabisa.

Lakini

Wakati huo huo anatutaka tujiwekee hazina Bora ambayo itakuja kutufaa huko mbele ya safari baada ya kuondoka hapa duniani,kwani mwisho wa siku tutaenda katika maisha mengine nje ya dunia hii.

Kuna ujumbe mmoja wa utani unasemwa na watu lakini umebeba ujumbe mkubwa Sana Kwa mtu mwenye kufikiri hatima yake unasema hivi;

Je kama sadaka ndio hela ya Matumizi yako huko Akhera unadhani ingekuwezesha kuishi kwa mda gani?

Ni utani lakini kuna ujumbe Fulani, ebu jitafakari wewe binafsi unafikir kwa sadaka yako uliyotoa ungetoboa miaka mingapi au miezi mingapi?

Hakika wengi wetu kama tungekufa Leo basi tungekuja kuwa ombamba huko mbinguni kwani naamini kabisa hizo sadaka tulizo toa ni hafifu mno kutuwezesha kufikisha miezi mitatu.

Tuwekeze katika maisha yajayo ambayo wengi wetu tunaamini yapo kwa mujibu wa imani zetu na Dini zetu.

Mwenyezi Mungu anasema hakika mwanadamu amekula hasara mpaka anaingia Makaburini hakuna kheri yoyote aliyoitanguliza ambayo itakuja kumfaa huko Akhera.

Kwahiyo ndugu zangu fanya utakavyo fanya na tafuta Maisha utakavyo lakini mwisho wa siku Sisi ni mavumbi na tutarudi mavumbini Tu kwahiyo hatuna budi kujitayarishia hazina ambayo itakuja kutufaa huko mbele ya safari.

Walio tangulia wameshajua hatima Yao na laiti wangeweza kutupenyezea ujumbe basi wangetuambia:

Jamani Yale tulivyo ambiwa katika vitabu ni kweli na tumeyakuta huku msimdharau hata jambo moja!

Bahati mbaya wanashindwa kuwasiliana na Sisi na wanabakia kusema laiti walio bakia duniani wangejua hakika wangefanya Yale yanayo mpendeza Mwenyezi Mungu.

Kazi kwetu kufanya yale ambayo yatakuja kutufaa huko mbele ya safari.
 
UJUMBE WA LEO:

Ni haki na wajibu wa Mume kumhudumia mkewe kwa malazi,mavazi,chakula na matibabu yake hata kama huyo mke ni tajiri au maskini

Hata kama mke anakipato chake kikubwa kuliko wewe,kwa mujibu wa Uislamu,hicho kipato ni chake,na kipato chako ni chenu wote

Labda aamue mwenyewe kwa mapenzi yake kukusaidia majukumu
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب الرجاء

051-Mlango Wa Kuwa na Matumaini



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:

قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا ۚ إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿٥٣﴾

Sema: Enyi waja Wangu ambao wamepindukia mipaka juu ya nafsi zao: Msikate tamaa na rahmah ya Allaah; hakika Allaah Anaghufuria dhambi zote; hakika Yeye Ndiye Mwenye kughufuria, Mwenye kurehemu. [Az-Zumar: 53]



وَهَلْ نُجَازِي إِلَّا الْكَفُورَ ﴿١٧﴾

Na Hatuadhibu isipokuwa anayekufuru. [Sabaa: 17]



إِنَّا قَدْ أُوحِيَ إِلَيْنَا أَنَّ الْعَذَابَ عَلَىٰ مَن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ﴿٤٨﴾

Hakika tumefunuliwa Wahy ya kwamba adhabu itakuwa kwa yule atakayekadhibisha na akakengeuka. [Twaahaa: 48]



وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ ۚ ﴿١٥٦﴾

Na rahmah Yangu imeenea kila kitu. [At-A'raaf: 106]







Hadiyth – 1

وعن عبادة بن الصامتِ رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ شَهِدَ أنَّ لا إلهَ إلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ ، وَأنَّ مُحَمداً عَبْدهُ ورَسُولُهُ ، وَأنَّ عِيسى عَبْدُ اللهِ وَرَسُولُهُ وَكَلِمَتُهُ ألْقَاهَا إِلَى مَرْيَمَ ورُوحٌ مِنْهُ ، وَأنَّ الجَنَّةَ حَقٌّ ، وَالنَّارَ حَقٌّ ، أدْخَلَهُ اللهُ الجَنَّةَ عَلَى مَا كَانَ مِنَ العَمَلِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية لمسلم : (( مَنْ شَهِدَ أنْ لا إلَهَ إلاَّ اللهُ وَأنَّ مُحَمَّداً رَسُولُ اللهِ ، حَرَّمَ اللهُ عَلَيهِ النَّارَ )) .

Imepokewa kutoka kwake 'Ubaadah bin Saamit (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kushuhudia kuwa hapana apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allaah Peke Yake hana mshirika, kuwa Muhammad ni mja na Rasuli Wake, na kuwa 'Iysa ni mja wa Allaah na Rasuli Wake, na ni Neno Lake Alilotia kwa Maryam na roho toka kwake, na kuwa Pepo ni kweli, na Moto ni kweli, Allaah atamwingiza Peponi kwa amali alizokuwa akifanya." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Katika riwaayah ya Muslim: "Mwenye kushuhudia kuwa hapana Mola isipokuwa Allaah, na kuwa Muhammad ni Rasuli wa Allaah, Allaah atamharamishia Moto."







Hadiyth – 2

وعن أَبي ذررضي الله عنه، قَالَ : قَالَ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم : (( يقول الله (عزّ وجلّ) : مَنْ جَاء بالحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أمْثَالِهَا أَوْ أزْيَد ، وَمَنْ جَاءَ بالسَيِّئَةِ فَجَزاءُ سَيِّئَةٍ سَيِّئَةٌ مِثْلُهَا أَوْ أغْفِرُ . وَمَنْ تَقَرَّبَ مِنِّي شِبْراً تَقَرَّبْتُ مِنْهُ ذِرَاعاً ، وَمَنْ تَقَرَّبَ مِنِّي ذِرَاعاً تَقَرَّبْتُ مِنْهُ بَاعاً ، وَمَنْ أتَانِي يَمْشِي أتَيْتُهُ هَرْوَلَةً ، وَمَنْ لَقِيني بِقُرَابِ الأرْض خَطِيئةً لا يُشْرِكُ بِي شَيئاً ، لَقِيتُهُ بِمِثْلِهَا مَغفِرَةً )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: Amesema Allaah Ta'aalaa: "Mwenye kuleta jema atapata mara kumi mfano wake au zaidi, na Mwenye kuleta ovu, malipo yake ni uovu mfano wake au Namsamehe. Na Mwenye kunikaribia kwa shubiri, Nitamkaribia kwa dhiraa. Na mwenye kunikaribia kwa kutembelea, Nitamjia kwa kukimbia, Mwenye kukutana nami kwa madhambi ujazo wa ardhi, na asinishirikishe na chochote, Nitakutana naye kwa msamaha kama huo." [Muslim]





Hadiyth – 3

وعن جابر رضي الله عنه، قَالَ : جاء أعرابي إِلَى النَّبيّ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ: يَا رَسُول الله ، مَا الموجِبَتَانِ؟ قَالَ : (( مَنْ مَاتَ لاَ يُشْرِكُ بالله شَيئاً دَخَلَ الجَنَّةَ ، وَمَنْ مَاتَ يُشْرِكُ بِهِ شَيْئاً دَخَلَ النَّار )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiyah Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Alikuja Bedui kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alahi wa aalihi wa sallam) na kuuliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Ni vitu gani viwili vinavyomfanya mtu aingie Peponi au Motoni?" Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Yeyote anayekufa hakumshirikisha Allaah na chochote ataingia Peponi na mwenye kuaga dunia huku anamshirikisha Allaah basi ataingia Motoni." [Muslim]





Hadiyth – 4

وعن أنس رضي الله عنه : أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم ومعاذ رديفه عَلَى الرَّحْل ، قَالَ : (( يَا مُعَاذُ )) قَالَ : لَبِّيْكَ يَا رَسُول الله وَسَعْدَيْكَ ، قَالَ : (( يَا مُعَاذُ )) قَالَ : لَبَّيْكَ يَا رَسُول الله وَسَعْدَيْكَ ، قَالَ : (( يَا مُعَاذُ )) قَالَ : لَبِّيْكَ يَا رَسُول الله وسَعْدَيْكَ ، ثَلاثاً ، قَالَ : (( مَا مِنْ عَبْدٍ يَشْهَدُ أن لا إلهَ إلاَّ الله ، وَأنَّ مُحَمَّداً عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ صِدْقاً مِنْ قَلْبِهِ إلاَّ حَرَّمَهُ الله عَلَى النَّار )) قَالَ : يَا رَسُول الله ، أفَلاَ أخْبِرُ بِهَا النَّاس فَيَسْتَبْشِروا ؟ قَالَ : (( إِذاً يَتَّكِلُوا )) فأخبر بِهَا مُعاذٌ عِنْدَ موتِه تَأثُّماً . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Mu'aadh akiwa nyuma yake, wakiwa juu ya kipndo, aliita: "Ee Mu'aadh!" Naye akajibu: "Labbaika Ee Rasuli wa Allaah wa Sa'dayka." Aliita (tena): "Ee Mu'aadh!" Naye akajibu: "Labbaika Ee Rasuli wa Allaah wa Sa'dayka." (Aliita hivi) mara tatu, kisha akasema: "Hakuna yeyote anayekiri kwa moyo na akatamka kwa ulimi kuwa hakuna Mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allaah na Muhammad ni mja na Rasuli wa Allaah kwa ukweli wa moyo wake isipokuwa Allaah Atamharamishia moto." Akasema: "Ee Rasuli wa Allaah niwaeleze watu kwa hilo wakafurahi?" Akanijibu: "Kama utawaambia watabweteka!" Na hilo Mu'aadh alilieleza wakati wa kufa kwake kwa kuhofia kupata dhambi (ya kuficha mafundisho)." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه- أَوْ أَبي سعيد الخدري رضي الله عنهما - شك الراوي - ولا يَضُرُّ الشَّكُّ في عَين الصَّحَابيّ ؛ لأنَّهُمْ كُلُّهُمْ عُدُولٌ – قَالَ : لَمَّا كَانَ غَزوَةُ تَبُوكَ ، أصَابَ النَّاسَ مَجَاعَةٌ ، فقالوا : يَا رَسُول الله ، لَوْ أذِنْتَ لَنَا فَنَحرْنَا نَواضِحَنَا فَأكَلْنَا وَادَّهَنَّا ؟ فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( افْعَلُوا )) فَجاء عُمَرُ رضي الله عنه ، فَقَالَ : يَا رَسُول الله ، إنْ فَعَلْتَ قَلَّ الظَّهْرُ ، وَلَكِن ادعُهُمْ بفَضلِ أزْوَادِهِمْ ، ثُمَّ ادعُ الله لَهُمْ عَلَيْهَا بِالبَرَكَةِ ، لَعَلَّ الله أنْ يَجْعَلَ في ذلِكَ البَرَكَةَ . فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم : (( نَعَمْ )) فَدَعَا بِنَطْع فَبَسَطَهُ ، ثُمَّ دَعَا بِفضلِ أزْوَادِهِمْ ، فَجَعَلَ الرَّجُلُ يَجيءُ بكَفّ ذُرَة وَيَجيءُ بِكَفّ تمر وَيجيءُ الآخرُ بِكِسرَة حَتَّى اجْتَمَعَ عَلَى النّطعِ مِنْ ذلِكَ شَيء يَسيرٌ ، فَدَعَا رَسُول الله صلى الله عليه وسلم بِالبَرَكَةِ ، ثُمَّ قَالَ : (( خُذُوا في أوعِيَتِكُمْ )) فَأَخَذُوا في أوْعِيَتهم حَتَّى مَا تَرَكُوا في العَسْكَرِ وِعَاء إلاَّ مَلأوهُ وَأَكَلُوا حَتَّى شَبعُوا وَفَضَلَ فَضْلَةٌ فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم : (( أشْهَدُ أنْ لا إلهَ إلاَّ اللهُ وَأنّي رَسُولُ الله ، لا يَلْقَى الله بِهِما عَبْدٌ غَيْرَ شَاكٍّ فَيُحْجَبَ عَنِ الجَنَّةِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) au Abu Sa'iid Al-Khudriy (Radhwiyah Allaahu 'anhu), mpokezi ana shaka na wala shaka haidhuru katika Swahaba yoyote, kwani wote ni waadilifu: "Ilipokuwa Vita vya Taabuk, watu walipatwa na njaa, wakasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Lau ungeruhusu kuchinja ngamia wetu, tule na kutumia mafuta yake." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Fanyeni hivyo." Akaja 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu) na kusema: "Ee Rasuli wa Allaah! Ikiwa tutafanya hivyo vipando vitapungua, lakini waitishe chakula chao cha ziada, Kisha muombe Allaah awabarikie hicho. Huenda Allaah akawatilia baraka." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ndio." Akaitisha busati la ngozi akalitandika, kisha akaomba watu walete vyakula vilivyozidi. Watu wakaleta vyakula, mtu analeta kifumba cha mahindi, mwingine analeta tende, mwingine analeta kipande cha mkate, Vyakula hivyo vikakusanywa katika busati hilo. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akakiombea baraka, kisha akasema: "Chukueni katika vyombo vyenu." Wakachukua katika vyombo vyao, hadi hakukubakia chombo katika kambi isipokuwa wakajaza vyombo vyao vyote katika kambi. Hapo wakala mpaka wakashiba, kingine kikabaki. Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Nashuhudia ya kwamba hapana Mola isipokuwa Allaah, na mimi ni Rasuli wa Allaah. Hatokutana mja na Allaah akiwa na kauli hizi mbili na hana shaka yoyote, kisha akazuiwa kuingia Peponi." [Muslim]







Hadiyth – 6

وعن عِتْبَانَ بن مالك رضي الله عنه وَهُوَ مِمَّن شَهِدَ بَدراً ، قَالَ : كنت أُصَلِّي لِقَوْمِي بَني سَالِم ، وَكَانَ يَحُولُ بَيْنِي وبَيْنَهُمْ وَادٍ إِذَا جَاءتِ الأَمْطَار ، فَيَشُقُّ عَلَيَّ اجْتِيَازُهُ قِبَلَ مسْجِدِهم ، فَجِئتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم فقلت لَهُ : إنّي أنْكَرْتُ بَصَرِي وَإنَّ الوَادِي الَّذِي بَيْنِي وبَيْنَ قَومِي يَسيلُ إِذَا جَاءتِ الأمْطَارُ فَيَشُقُّ عَلَيَّ اجْتِيَازُهُ فَوَدِدْتُ أنَّكَ تَأتِي فَتُصَلِّي في بَيْتِي مَكَاناً أتَّخِذُهُ مُصَلّى ، فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم : (( سَأفْعَلُ )) فَغَدَا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم وَأَبُو بكر رضي الله عنه بَعْدَ مَا اشْتَدَّ النَّهَارُ ، وَاسْتَأذَنَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم فَأذِنْتُ لَهُ ، فَلَمْ يَجْلِسْ حَتَّى قَالَ : (( أيْنَ تُحِبُّ أنْ أُصَلِّيَ مِنْ بَيْتِكَ ؟ )) فَأشَرْتُ لَهُ إِلَى المَكَانِ الَّذِي أُحبُّ أنْ يُصَلِّيَ فِيهِ ، فَقَامَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم فَكَبَّرَ وَصَفَفْنَا وَرَاءَهُ فَصَلَّى رَكعَتَينِ ثُمَّ سَلَّمَ وَسَلَّمْنَا حِينَ سَلَّمَ فَحَبَسْتُهُ عَلَى خَزيرَةٍ تُصْنَعُ لَهُ ، فَسَمِعَ أهلُ الدَّارِ أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم في بَيْتِي فَثَابَ رِجالٌ مِنْهُمْ حَتَّى كَثُرَ الرِّجَالُ في البَيْتِ ، فَقَالَ رَجُلٌ : مَا فَعَلَ مَالِكٌ لا أرَاهُ ! فَقَالَ رَجُلٌ : ذلِكَ مُنَافِقٌ لا يُحِبُّ الله ورسولَهُ ، فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم : (( لا تَقُلْ ذلِكَ ، ألاَ تَرَاهُ قَالَ : لا إلهَ إلاَّ الله يَبْتَغي بذَلِكَ وَجهَ الله تَعَالَى )) فَقَالَ : اللهُ ورسُولُهُ أعْلَمُ أمَّا نَحْنُ فَوَاللهِ مَا نَرَى وُدَّهُ وَلاَ حَدِيثَهُ إلاَّ إِلَى المُنَافِقينَ ! فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم : (( فإنَّ الله قَدْ حَرَّمَ عَلَى النَّارِ مَنْ قَالَ : لا إلهَ إلاَّ الله يَبْتَغِي بذَلِكَ وَجْهَ الله )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Itbaan bin Maalik (Radhwiyah Allaahu 'anhu) miongoni mwa waliohudhuria Badr, amesema: Nilikuwa nikiswali na watu wangu Bani Saalim baina yangu na wao kuna bonde, mvua ikinyesha linafurika na huwa tabu kwangu kwenda msikitini. Nikaenda kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nikasema: "Macho yangu ni dhaifu na bonde lililopo baina yangu na watu wangu linafurika ikinyesha mvua hivyo nashindwa kulivuka, Hivyo Napenda uje uswali nyumbani sehemu ninayotumia kuswalia." Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akasema: "Nitafanya." Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaja na Abu Bakr (Radhwiyah Allaahu 'anhu) baada jua kuwa juu. Rasuli wa Allaah (Swallah Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akabisha nikamkaribisha, Hakukaa hadi akasema: "Ni wapi unapopenda niswali nyumbani kwako?" Nikamuashiria sehemu nilipenda aswali. Akasimama Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akapiga takbira tukasimama nyuma yake, Akaswali rakaa mbili kisha akatoa salamu, nasi tukatoa salamu baada yake. Nikamzuia kwa sababu ya chakula anachoandaliwa. Watu wa mji wakasikia kuwa Rasuli wa Allaah yupo nyumbani kwangu wakaja watu wengi hadi wakajaa nyumbani, Akasema mtu mmoja: "Maalik amefanya nini simuoni?" Akasema mwingine: "Yule ni mnafiki hampendi Allaah na Rasuli Wake." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Usiseme hivyo, kwani humuoni amesema Laa Ilaaha Illa Allaah akitaka radhi za Allaah Ta'aalaa?", Akasema: "Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi. Ama sisi hatuwaoni marafiki zake wala mazungumzo yake isipokuwa ya wanafiki." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Hakika amemharamishia moto mwenye kusema Laa Ilaaha Illa Allaah hatafuti kwa hilo isipokuwa radhi ya Allaah." [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 7

وعن عمر بن الخطاب رضي الله عنه ، قَالَ : قدِم رَسُول الله صلى الله عليه وسلم بسَبْيٍ فَإِذَا امْرَأةٌ مِنَ السَّبْيِ تَسْعَى ، إِذْ وَجَدَتْ صَبياً في السَّبْيِ أخَذَتْهُ فَألْزَقَتهُ بِبَطْنِهَا فَأَرضَعَتْهُ ، فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( أتَرَوْنَ هذِهِ المَرْأةَ طَارِحَةً وَلَدَها في النَّارِ ؟ )) قُلْنَا : لاَ وَاللهِ . فَقَالَ : (( للهُ أرْحَمُ بِعِبَادِهِ مِنْ هذِهِ بِوَلَدِهَا )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Imepokewa kutoka kwa 'Umar bin Al-Khattaab (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: "Waliletwa mateka wa vita kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Kulikuwa na mwanamke akizunguka kutafuta mwanae. Akampata katika mateka akamchukua akamuweka tumboni mwake, akamnyonyesha. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Je, munamuona huyu mwanamke anaweza kumtia mtoto wake motoni?" Tukasema: "La! Wa-Allaahi." Akasema: "Allaah ana huruma zaidi kwa waja wake kuliko huyu kwa mtoto wake." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 8

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( لَمَّا خَلَقَ الله الخَلْقَ كَتَبَ في كِتَابٍ ، فَهُوَ عِنْدَهُ فَوقَ العَرْشِ : إنَّ رَحْمَتِي تَغْلِبُ غَضَبي )) .

وفي رواية : (( غَلَبَتْ غَضَبي )) وفي رواية : (( سَبَقَتْ غَضَبي )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Pindi Allaah Alipoviumba viumbe, Aliandika katika kitabu, ambacho kipo Kwake juu ya 'Arshi Yake: Hakika rehema Yangu inashinda ghadhabu Yangu."

Na katika riwaayah nyingine: "Imeshinda ghadhabu Yangu."

Na katika riwaayah nyengine: "Imepita ghadhabu Yangu." [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhy]





Hadiyth – 9

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( جَعَلَ الله الرَّحْمَةَ مِئَةَ جُزْءٍ، فَأمْسَكَ عِنْدَهُ تِسْعَةً وَتِسْعِينَ، وَأنْزَلَ في الأرْضِ جُزْءاً وَاحِداً، فَمِنْ ذلِكَ الجُزءِ يَتَرَاحَمُ الخَلائِقُ، حَتَّى تَرْفَعَ الدَّابّةُ حَافِرهَا عَنْ وَلَدِهَا خَشْيَةَ أنْ تُصِيبَهُ )) .

وفي رواية : (( إنّ للهِ تَعَالَى مئَةَ رَحمَةٍ ، أنْزَلَ مِنْهَا رَحْمَةً وَاحِدَةً بَيْنَ الجنِّ وَالإنس وَالبهائِمِ وَالهَوامّ ، فبها يَتَعاطَفُونَ ، وبِهَا يَتَرَاحَمُونَ ، وبِهَا تَعْطِفُ الوَحْشُ عَلَى وَلَدِهَا ، وَأخَّرَ اللهُ تَعَالَى تِسْعاً وَتِسْعينَ رَحْمَةً يرْحَمُ بِهَا عِبَادَهُ يَوْمَ القِيَامَة )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

ورواه مسلم أيضاً مِنْ رواية سَلْمَانَ الفارِسيِّ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( إنَّ للهِ تَعَالَى مِئَة رَحْمَةٍ فَمِنْهَا رَحْمَةٌ يَتَرَاحمُ بِهَا الخَلْقُ بَيْنَهُمْ ، وَتِسْعٌ وَتِسعُونَ لِيَومِ القِيَامَةِ )) .

وفي رواية : (( إنَّ الله تَعَالَى خَلَقَ يَوْمَ خَلَقَ السَّمَاواتِ وَالأَرْضَ مَئَةَ رَحْمَةٍ كُلُّ رَحْمَةٍ طِبَاقُ مَا بَيْنَ السَّماءِ إِلَى الأرْضِ ، فَجَعَلَ مِنْهَا في الأرضِ رَحْمَةً فَبِهَا تَعْطفُ الوَالِدَةُ عَلَى وَلَدِهَا ، وَالوَحْشُ وَالطَّيْرُ بَعْضُهَا عَلَى بَعْض ، فَإذا كَانَ يَوْمُ القِيَامَةِ أكملَهَا بِهذِهِ الرَّحمَةِ ))

Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: Allaah Amefanya rehema kuwa sehemu mia moja, Akabakia na sehemu tisini na tisa, Akateremsha ardhini sehemu moja, katika sehemu hiyo viumbe wanahurumiana, mpaka mnyama anainua kwato zake akihofia kumdhuru mwanae."

Katika riwaayah nyengine: "Hakika Allaah Ta'aalaa ana rehma mia moja, katika hizo ameteremsha rehma moja baina ya majini na wanadamu, wanyama na wadudu. Katika hiyo rehma wanasikitiana, wanahurumiana, mnyama pori anamhurumia mwanae. Allaah Amebakisha rehema tisini na tisa Arawarahamu nazo waja Wake Siku ya Qiyaamah." [Al-Bukhaary, Muslim na At-Tirmidhy]

Amepokea Muslim Hadiyth kutoka kwa Salmaan Al-Faarisy; Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah Ta'aalaa ana rehema mia moja, miongoni mwa hizo ni rehema moja, wanahurumiana viumbe baina yao, tisini na tisa ni kwa ajili ya Siku ya Qiyaamah."

Katika riwaayah nyingine: "Hakika Allaah Ta'aalaa ameumba siku Aliyoumba mbingu na ardhi rehema mia moja; kila moja ni baina ya mbingu na ardhi. Akajalia katika ardhi rehema Mama anamhurumia mwanae, na wanyama na ndege wanahurumiana wao kwa wao, Ikifika Siku ya Qiyaamah, Allaah ataikamilisha kwa rehema hii."





Hadiyth – 10

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم فيما يحكِي عن ربهِ تبارك وتعالى ، قَالَ: (( أذْنَبَ عَبْدٌ ذَنْباً ، فَقَالَ : اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي ذَنْبِي ، فَقَالَ الله تَبَاركَ وَتَعَالَى : أذنَبَ عبدي ذَنباً ، فَعَلِمَ أنَّ لَهُ رَبّاً يَغْفِرُ الذَّنْبَ ، وَيَأْخُذُ بالذَّنْبِ ، ثُمَّ عَادَ فَأذْنَبَ ، فَقَالَ : أيْ رَبِّ اغْفِرْ لِي ذَنْبي ، فَقَالَ تبارك وتعالى : أذنَبَ عبدِي ذَنباً ، فَعَلِمَ أنَّ لَهُ رَبّاً ، يَغْفِرُ الذَّنْبَ ، وَيَأْخُذُ بالذَّنْبِ ، قَدْ غَفَرْتُ لِعَبْدِي فَلْيَفْعَلْ مَا شَاءَ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anayohadithia kutoka kwa Mola wake (Tabaaraka wa Ta'aalaa) kuwa Amesema: "Mja amefanya dhambi, akasema: "Ee Mola wangu nisamehe dhambi yangu." Akasema Allaah (Tabaaraka wa Ta'aalaa): "Mja Wangu amefanya dhambi, akajua kuwa anaye Mola anayesamehe dhambi, na anayehesabu dhambi." Kisha akarudi akafanya dhambi, akasema: "Ee Mola Wangu nisamehe dhambi yangu." Akasema Allaah (Tabaaraka wa Ta'aalaa): "Mja Wangu amefanya dhambi, akajua kuwa anaye Mola anayesamehe dhambi, na anayehesabu dhambi." Kisha akarudi akafanya dhambi, akasema: "Ee Mola Wangu nisamehe dhambi yangu."Akasema Allaah (Tabaaraka wa Ta'aalaa): "Mja Wangu amefanya dhambi, akajua kuwa anaye Mola anayesamehe dhambi, na mwenye kuhesabu dhambi. Nimemsamehe mja Wangu dhambi zake, hivyo afanye anavyotaka." [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 11

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( والَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ ، لَوْ لَمْ تُذْنِبُوا ، لَذَهَبَ الله بِكُمْ ، وَجَاءَ بِقَومٍ يُذْنِبُونَ ، فَيَسْتَغْفِرُونَ الله تَعَالَى ، فَيَغْفِرُ لَهُمْ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi Mwake kwamba lau hamngekuwa mkifanya dhambi Allaah angewaondosha na Akawaleta watu ambao watafanya dhambi na kisha wataomba msamaha kwa Allaah (Ta'aalaa) Naye atawasamehe." [Muslim]





Hadiyth – 12

وعن أَبي أيوب خالد بن زيد رضي الله عنه، قَالَ : سَمِعْتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( لَوْلاَ أنَّكُمْ تُذْنِبُونَ ، لَخَلَقَ الله خَلْقاً يُذْنِبُونَ ، فَيَسْتَغْفِرونَ ، فَيَغْفِرُ لَهُمْ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Ayub Khalid bin Zaiyd (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Msingekuwa mnafanya dhambi basi Allaah angewaumba viumbe wenye kufanya madhambi kisha wataomba toba na Allaah atawasamehe." [Muslim]





Hadiyth – 13

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : كُنَّا قُعُوداً مَعَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، مَعَنَا أَبُو بَكْرٍ وَعُمْرُ رضي الله عنهما ، في نَفَرٍ فَقَامَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم مِنْ بَيْنِ أظْهُرِنَا ، فَأبْطَأَ عَلَيْنَا فَخَشِينَا أنْ يُقتطَعَ دُونَنَا ، فَفَزِعْنَا فَقُمْنَا فَكُنْتُ أوَّلَ مَنْ فَزِعَ فَخَرَجْتُ أبْتَغِي رسولَ الله صلى الله عليه وسلم، حَتَّى أتَيْتُ حَائِطاً للأنْصَارِ ... وَذَكَرَ الحَدِيثَ بِطُولِهِ إِلَى قوله : فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( اذهَبْ فَمَن لَقِيتَ وَرَاءَ هَذَا الحَائِطِ يَشْهَدُ أنْ لا إله إلاَّ الله ، مُسْتَيقِناً بِهَا قَلبُهُ فَبَشِّرْهُ بِالجَنَّةِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah(Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: Tulikuwa tumekaa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na pamoja nasi kulikuwa na Abu Bakr na 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhummaa) miongoni mwa Swahaaba wengine Alisimama Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baina ya migongo yetu na akakawia sana, hivyo tukawa na hofu kubwa sana kuhusu usalama wake. Hapo tulisimama ili kumtafuta, nami ndiye niliyekuwa wa mwanzo kuwa na hamu hiyo. Niliinuka ili kumtafuta Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), mpaka nikafika kwenye ukuta wa Ansaar. Hapa aliitaja Hadiyth kwa urefu na ukamilifu wake mpaka katika kauli yake: Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Nenda nyuma ya ukuta huu umbashirie Pepo kila utakayekutana naye huku anashuhudia ya kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah." [Muslim]







Hadiyth – 14

وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما : أنَّ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم تَلاَ قَولَ الله (عزّ وجلّ) في إبراهيم صلى الله عليه وسلم: ( رَبِّ إِنَّهُنَّ أَضْلَلْنَ كَثِيراً مِنَ النَّاسِ فَمَنْ تَبِعَنِي فَإِنَّهُ مِنِّي ) [ إبراهيم : 36 ] الآية ، وقَولَ عِيسَى صلى الله عليه وسلم: ( إِنْ تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ وَإِنْ تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنْتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ) [ المائدة : 118 ] فَرَفَعَ يَدَيهِ وَقالَ : (( اللَّهُمَّ أُمّتي أُمّتي )) وبَكَى ، فَقَالَ الله (عزّ وجلّ) : (( يَا جِبْريلُ ، اذْهَبْ إِلَى مُحَمَّدٍ -وَرَبُّكَ أعْلَمُ - فَسَلْهُ مَا يُبْكِيهِ ؟ )) فَأتَاهُ جبريلُ ، فَأخْبَرَهُ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم، بِمَا قَالَ - وَهُوَ أعْلَمُ - فَقَالَ اللهُ تَعَالَى : (( يَا جِبريلُ ، اذْهَبْ إِلَى مُحَمّدٍ ، فَقُلْ : إنَّا سَنُرْضِيكَ في أُمّتِكَ وَلاَ نَسُوءكَ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwake 'Abdillaahi bin 'Amru bin al-'Aasw (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisoma kauli ya Allaah ('Azza wa Jalla) kuhusu Ibraahiym (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Rabb wangu! Hakika hao (masanamu) wamepoteza wengi kati ya watu. Basi atakayenifuata, huyo ni katika mimi." [Ibraahiym: 36] Na kauli ya 'Iyssaa (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ukiwaadhibu, basi bila shaka hao ni waja Wako; na Ukiwaghufuria basi hakika Wewe Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote." [Al-Maaidah: 118] Nabiy alinyanyua mikono yake na kusema: "Ee Mola wangu! Ummah wangu, Ummah wangu", na akaanza kulia. Akasema Allaah ('Azza wa Jalla): "Ee Jibriyl! Nenda kwa Muhammad na Rabb wako ni mjuzi zaidi na umuulize ni kipi kinachomliza (yaani analia kwa nini)?" Jibriyl ('Alayhi sallaam) alikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), naye akamwambia alichokisema na Allaah anajua zaidi. Akasema Allaah Ta'aalaa: "Ee Jibriyl! Nenda kwa Muhammad na umwambie: 'Hakika tutakufanya uridhike kwa Ummah wako na hatutakufanya uhuzunike'." [Muslim]







Hadiyth – 15

وعن معاذ بن جبل رضي الله عنه، قَالَ : كُنْتُ رِدْفَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم عَلَى حِمَارٍ ، فَقَالَ : (( يَا مُعَاذُ ، هَلْ تَدْرِي مَا حَقُّ الله عَلَى عِبَادِهِ ؟ وَمَا حَقُّ العِبَادِ عَلَى الله ؟ )) قُلْتُ : اللهُ وَرَسُولُهُ أعْلَمُ . قَالَ : (( فإنَّ حَقَّ اللهِ عَلَى العِبَادِ أنْ يَعْبُدُوهُ ، وَلاَ يُشْرِكُوا بِهِ شَيئاً ، وَحَقَّ العِبَادِ عَلَى اللهِ أنْ لاَ يُعَذِّبَ مَنْ لا يُشْرِكُ بِهِ شَيئاً )) فقلتُ : يَا رَسُول الله ، أفَلا أُبَشِّرُ النَّاسَ ؟ قَالَ : (( لاَ تُبَشِّرْهُمْ فَيَتَّكِلُوا )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Mu'aadh bin Jabal (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: Nilikuwa nimepanda nyuma ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya punda, akaniambia: "Ee Mu'aadh! Unajua haki ya Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi." Akasema: "Hakika haki ya Allaah juu ya waja Wake wamuabudu wala wasimshirikishe na chochote. Na haki ya waja kwa Allaah, ni kumuadhibu asiyemshirikisha na chochote." Nikasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Je nisiwabashirie wakabweteka." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 16

وعن البراءِ بن عازب رضي الله عنهما ، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( المُسْلِمُ إِذَا سُئِلَ في القَبْرِ يَشْهَدُ أنْ لاَ إلَهَ إلاَّ الله ، وَأنّ مُحَمّداً رَسُول الله ، فذلك قوله تَعَالَى: ( يُثَبِّتُ اللهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الآخِرَة ) [ إبراهيم : 27 ] )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.

Imepokewa kutoka kwa Al-Baraa'a bin 'Aazib (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Muislamu atakapoulizwa kaburini, anashuhudia kuwa hapana Mola isipokuwa Allaah, na kuwa Muhammad ni Rasuli Wake, hiyo ni kauli Yake Ta'aalaa: "Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah." [Ibraahiym: 27]





Hadiyth – 17

وعن أنس رضي الله عنه ، عن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إنّ الكَافِرَ إِذَا عَمِلَ حَسَنَةً ، أُطعِمَ بِهَا طُعْمَةً مِنَ الدُّنْيَا ، وَأَمَّا المُؤْمِنُ فَإنَّ الله تَعَالَى يَدَّخِرُ لَهُ حَسَنَاتِهِ في الآخِرَةِ ، وَيُعْقِبُهُ رِزْقاً في الدُّنْيَا عَلَى طَاعَتِهِ )) .

وفي رواية : (( إنَّ الله لاَ يَظْلِمُ مُؤْمِناً حَسنَةً يُعْطَى بِهَا في الدُّنْيَا ، وَيُجْزَى بِهَا في الآخِرَةِ . وَأَمَّا الكَافِرُ فَيُطْعَمُ بِحَسَنَاتِ مَا عَمِلَ للهِ تَعَالَى في الدُّنْيَا ، حَتَّى إِذَا أفْضَى إِلَى الآخرَةِ ، لَمْ يَكُنْ لَهُ حَسَنَةٌ يُجْزَى بِهَا )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika kafiri akifanya jema, hulishwa chakula duniani, Ama Muumini Allaah Ta'aalaa anamuwekea amali yake njema Aakhirah, na anampa riziki hapa duniani kwa sababu ya utiifu wake."

Na katika riwaayah nyengine: "Hakika Allaah hamdhulumu Muumini aliyefanya mambo mema anampa duniani, na kumlipa nayo nayo Aakhirah. Ama kafiri analishwa kwa mema aliyoyafanya kwa ajili ya Allaah duniani; hadi akifika Aakhirah, hawi na mema yoyote ya kulipwa huko." [Muslim]





Hadiyth – 18

وعن جابر رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( مَثَلُ الصَّلَوَاتِ الخَمْسِ كَمَثَلِ نَهْرٍ جَارٍ غَمْرٍ عَلَى بَابِ أحَدِكُمْ يَغْتَسِلُ مِنْهُ كُلَّ يَوْم خَمْسَ مَرَّات )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: "Mfano wa Swalaah tano ni kama mfano wa mto mkubwa unaopita mbele ya mlango wa mmoja wenu, ambaye atakuwa anajiosha kila siku mara tano." [Muslim].





Hadiyth – 19

وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، قَالَ : سَمِعْتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( مَا مِنْ رَجُلٍ مُسْلِمٍ يَمُوتُ ، فَيقُومُ عَلَى جَنَازَتهِ أرْبَعونَ رَجُلاً لاَ يُشْرِكُونَ بِاللهِ شَيئاً ، إلاَّ شَفَّعَهُمُ اللهُ فِيهِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakuna Muislamu yeyote ambaye anaaga dunia, wakasimama watu arobaini kumswalia (Swalaah ya Jeneza) wasiomshirikisha Allaah na chochote isipokuwa Allaah anakubali maombi yao." [Muslim]





Hadiyth – 20

وعن ابن مسعود رضي الله عنه، قَالَ : كُنَّا مَعَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم في قُبَّة نَحْوَاً مِنْ أربَعِينَ ، فَقَالَ : (( أتَرْضَونَ أنْ تَكُونُوا رُبُعَ أهْلِ الجَنَّةِ ؟ )) قُلْنَا : نَعَمْ . قَالَ : (( أتَرْضَوْنَ أنْ تَكُونُوا ثُلُثَ أهلِ الجَنَّةِ ؟ )) قُلْنَا : نَعَمْ ، قَالَ : (( وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمّدٍ بيَدِهِ ، إنِّي لأَرْجُو أنْ تَكُونُوا نِصْفَ أهْلِ الجَنَّةِ وذلك أنَّ الجنَّةَ لاَ يَدْخُلُهَا إلاَّ نَفْسٌ مُسْلِمَةٌ ، ومَا أنْتُم في أهْلِ الشِّركِ إلاَّ كَالشَّعْرَةِ البَيْضَاءِ في جلدِ الثَّورِ الأَسْوَدِ ، أَوْ كَالشَّعْرَةِ السَّودَاءِ في جلدِ الثَّورِ الأحْمَر )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uud (Radhwiyah Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Tulikuwa takriban watu arobaini katika nyumba ndogo pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Je, mtaridhia kuwa robo ya watu wa Peponi?" Tulisema: "Ndio." Akasema: "Je, mtaridhia kuwa thulithi ya watu wa Peponi?" Tulisema: "Ndio." Akasema: "Naapa kwa ambaye nafsi ya Muhammad ipo mkononi Mwake, hakika nina matarajio kuwa nyinyi mtakuwa nusu ya watu wa Peponi. Na hiyo kwa sababu ya kuwa hataingia Peponi ila nafsi ya Muislamu. Na idadi yenu kulinganishwa na watu wa shirki ni kama nywele nyeupe katika ngozi ya fahali mweusi, au nywele nyeusi katika ngozi ya fahali mwekundu." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 21

وعن أَبي موسى الأشعري رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا كَانَ يَوْمُ القِيَامَةِ دَفَعَ اللهُ إِلَى كُلِّ مُسْلِم يَهُودياً أَوْ نَصْرانِياً ، فَيَقُولُ : هَذَا فِكَاكُكَ مِنَ النَّارِ )) .

وفي رواية عَنْهُ ، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( يَجِيءُ يَوْمَ القِيَامَةِ نَاسٌ مِنَ المُسْلِمينَ بِذُنُوبٍ أَمْثَال الجِبَالِ يَغْفِرُهَا الله لَهُمْ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Itakapokuwa siku ya Qiyaamah Allaah atampa kila Muislamu Yahudi au Mnasara, Atasema: 'Hii ni fidiya yako na Moto'."

Katika riwaayah yake nyingine: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Watakuja watu Siku ya Qiyaamah miongoni mwa Waislamu na madhambi mfano wa mlima, Allaah atawasamehe (madhambi yao hayo)." [Muslim]





Hadiyth – 22

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( يُدْنَى المُؤْمِنُ يَوْمَ القِيَامَة مِنْ رَبِّهِ حَتَّى يَضَعَ كَنَفَهُ عَلَيهِ ، فَيُقَرِّرُهُ بذُنُوبِهِ ، فيقولُ : أتعرِفُ ذَنْبَ كَذَا ؟ أتَعرفُ ذَنْبَ كَذَا ؟ فيقول : رَبِّ أعْرِفُ ، قَالَ : فَإنِّي قَدْ سَتَرْتُهَا عَلَيْكَ في الدُّنْيا ، وَأنَا أغْفِرُهَا لَكَ اليَومَ ، فَيُعْطَى صَحيفَةَ حَسَنَاتِهِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Muumini atasogezwa karibu na Mola wake Siku ya Qiyaamah na kumfunika kwa sitara Yake. Atamuulizia dhambi zake, Atasema:, 'Unajua dhambi kadhaa? Unajua dhambi kadhaa?' Atasema: 'Mola wangu najua, Atasema: Mimi nimekusitiri duniani, Nami ninaisamehe kwako leo. Atapewa sahifa ya mema yake." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 23

وعن ابن مسعود رضي الله عنه: أنَّ رَجُلاً أصَابَ مِن امْرَأة قُبْلَةً ، فَأتَى النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم فَأخْبَرَهُ ، فَأنْزَلَ الله تَعَالَى : ( وَأَقِمِ الصَّلاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفاً مِنَ اللَّيْلِ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَات ) [ هود : 114] فَقَالَ الرجل: أَليَ هَذَا يَا رَسُول الله ؟ قَالَ : (( لجميعِ أُمَّتِي كُلِّهِمْ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uud (Radhwiyah Allaah 'anhu) kuwa : Mtu mmoja alimbusu mwanamke ajnabi, akaja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kumwelezea hilo. Allaah Ta'aalaa akateremsha: "Na simamisha Swalaah katika ncha mbili za mchana na sehemu ya kwanza ya usiku; hakika mema yanaondosha maovu." [Huwd: 114]. Akasema yule mtu: "Ee Rasuli wa Allaah! Je, hili ni langu?" Akasema: "Ni kwa Ummah wangu wote." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 24

وعن أنس رضي الله عنه، قَالَ: جاء رجل إِلَى النَّبيّ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : يَا رَسُول الله، أَصَبْتُ حَدّاً ، فَأَقِمْهُ عَلَيَّ ، وَحَضَرَتِ الصَّلاةُ ، فَصَلَّى مَعَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، فَلَمَّا قَضَى الصَّلاةَ ، قَالَ : يَا رَسُول الله ، إنِّي أصَبْتُ حَدّاً فَأقِمْ فيَّ كِتَابَ الله . قَالَ : (( هَلْ حَضَرْتَ مَعَنَا الصَّلاةَ )) ؟ قَالَ : نَعَمْ . قَالَ : (( قَدْ غُفِرَ لَكَ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Alikuja mtu kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kuuliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Nimefanya kosa la kusimamishiwa hadd, kwa hivyo isimamishe." Wakati wa Swalaah ulifika, naye (huyo mtu) akaswali pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Baada ya swalaah alisema tena: "EeRasuli wa Allaah! Nimefanya kosa la kusimamishiwa hadd kwa hivyo isimamishe kulingana na Kitabu cha Allaah." Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Je, umeswali na sisi?" Akasema: "Ndio." Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Hakika umesamehe (kosa lako hilo)." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 25

وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ الله لَيرْضَى عَنِ العَبْدِ أنْ يَأكُلَ الأَكْلَةَ ، فَيَحْمَدُهُ عَلَيْهَا ، أَوْ يَشْرَبَ الشَّرْبَةَ ، فَيَحْمَدُهُ عَلَيْهَا )) رواه مسلم

Na imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah anamridhia mja anayekula chakula na baadae akamuhimidi (akamshukuru Allaah) au akanywa kinywaji kisha akamuhimidi kwa ajili ya kupata kinywaji hicho." [Muslim]





Hadiyth – 26

وعن أَبي موسى رضي الله عنه ، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إنَّ الله تَعَالَى يَبْسُطُ يَدَهُ باللَّيلِ ليَتُوبَ مُسِيءُ النَّهَارِ ، وَيَبْسُطُ يَدَهُ بالنَّهَارِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ اللَّيلِ ، حَتَّى تَطلُعَ الشَّمْسُ مِنْ مَغْرِبِهَا )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Muuwsaa 'Abdillahi bin Qays al-Ash'ariy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah Ta'aalaa hunyoosha mkono Wake usiku wapate kutubia mpaka jua lichomoza upande wa magharibi." [Muslim]





Hadiyth – 27

وعن أَبي نجيح عمرو بن عَبَسَة - بفتح العين والباءِ - السُّلَمِيِّ رضي الله عنه، قَالَ : كُنْتُ وأنَا في الجاهِلِيَّةِ أظُنُّ أنَّ النَّاسَ عَلَى ضَلاَلَةٍ ، وَأَنَّهُمْ لَيْسُوا عَلَى شَيْءٍ ، وَهُمْ يَعْبُدُونَ الأَوْثَانَ ، فَسَمِعْتُ بِرَجُلٍ بِمَكَّةَ يُخْبِرُ أخْبَاراً ، فَقَعَدْتُ عَلَى رَاحِلَتِي ، فَقَدِمْتُ عَلَيهِ ، فإِذَا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم مُسْتَخْفِياً ، جرَءاءُ عَلَيهِ قَومُهُ ، فَتَلَطَّفَتُ حَتَّى دَخَلْتُ عَلَيهِ بِمَكَّةَ ، فَقُلْتُ لَهُ : مَا أنْتَ ؟ قَالَ : (( أنا نَبيٌّ )) قُلْتُ : وما نبيٌّ ؟ قَالَ : (( أرْسَلَنِي الله )) قُلْتُ : وبأيِّ شَيْء أرْسَلَكَ ؟ قَالَ : (( أَرْسَلَنِي بِصِلَةِ الأرْحَامِ ، وَكَسْرِ الأَوْثَانِ ، وَأنْ يُوَحَّدَ اللهُ لاَ يُشْرَكُ بِهِ شَيْء )) قُلْتُ : فَمَنْ مَعَكَ عَلَى هَذَا ؟ قَالَ : (( حُرٌّ وَعَبْدٌ )) ومعه يَوْمَئذٍ أَبُو بكرٍ وبلالٌ رضي الله عنهما ، قُلْتُ : إنّي مُتَّبِعُكَ ، قَالَ : (( إنَّكَ لَنْ تَسْتَطيعَ ذلِكَ يَومَكَ هَذَا ، ألا تَرَى حَالي وحالَ النَّاسِ ؟ وَلَكِنِ ارْجعْ إِلَى أهْلِكَ فَإِذَا سَمِعْتَ بي قَدْ ظَهرْتُ فَأتِنِي )) قَالَ : فَذَهَبْتُ إِلَى أهْلِي وقَدِمَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم المَدِينَةَ حَتَّى قَدِمَ نَفَرٌ مِنْ أهْلِي المَدِينَةَ ، فقلتُ : مَا فَعَلَ هَذَا الرَّجُلُ الَّذِي قَدِمَ المَدِينَةَ ؟ فقالوا : النَّاس إلَيهِ سِرَاعٌ ، وَقَدْ أرادَ قَومُهُ قَتْلَهُ ، فلَمْ يَسْتَطِيعُوا ذلِكَ ، فقَدِمْتُ المدينَةَ ، فَدَخَلْتُ عَلَيهِ ، فقلتُ : يَا رَسُول الله أَتَعْرِفُني ؟ قَالَ : (( نَعَمْ ، أنْتَ الَّذِي لَقَيْتَنِي بمكّةَ )) قَالَ : فقلتُ : يَا رَسُول الله ، أخْبِرنِي عَمَّا عَلَّمَكَ الله وأَجْهَلُهُ ، أخْبِرْنِي عَنِ الصَّلاَةِ ؟ قَالَ : (( صَلِّ صَلاَةَ الصُّبْحِ ، ثُمَّ اقْصُرْ عَنِ الصَّلاَةِ حَتَّى تَرْتَفِعَ الشَّمْسُ قِيدَ رُمْحٍ ، فَإنَّهَا تَطْلُعُ حِينَ تَطلُعُ بَيْنَ قَرْنَيْ شَيطَان ، وَحينَئذٍ يَسجُدُ لَهَا الكُفَّارُ ، ثُمَّ صَلِّ فَإنَّ الصَلاَةَ مَشْهُودَةٌ مَحْضُورةٌ حَتَّى يَسْتَقِلَّ الظِّلُّ بالرُّمْحِ ، ثُمَّ اقْصُرْ عَنِ الصَّلاةِ ، فَإنَّهُ حينئذ تُسْجَرُ جَهَنَّمُ ، فإذَا أقْبَلَ الفَيْءُ فَصَلِّ ، فَإنَّ الصَّلاةَ مَشْهُودَةٌ مَحضُورَةٌ حَتَّى تُصَلِّي العصرَ ، ثُمَّ اقْصرْ عَنِ الصَّلاةِ حَتَّى تَغْرُبَ الشَّمْسُ ، فإنَّهَا تَغْرُبُ بينَ قَرْنَيْ شَيطانٍ ، وَحِينَئذٍ يَسْجُدُ لَهَا الكُفّارُ )) قَالَ : فقلتُ : يَا نَبيَّ الله ، فالوضوءُ حدثني عَنْهُ ؟ فَقَالَ : (( مَا مِنْكُمْ رَجُلٌ يُقَرِّبُ وَضُوءهُ ، فَيَتَمَضْمَضُ وَيسْتَنْشِقُ فَيَسْتَنْثِرُ ، إلاَّ خَرَّتْ خَطَايَا وَجْهِهِ مِنْ أطْرَافِ لِحْيَتِهِ مَعَ المَاءِ ، ثُمَّ يَغْسِلُ يديهِ إِلَى المِرفقَيْن ، إلاَّ خَرَّتْ خَطَايَا يَدَيْهِ مِنْ أنَامِلِهِ مَعَ الماءِ ، ثُمَّ يَمْسَحُ رَأسَهُ ، إلاَّ خرّتْ خطايا رأسِهِ من أطْرَافِ شَعْرِهِ مَعَ الماءِ ، ثُمَّ يغسل قدميه إِلَى الكعْبَيْنِ ، إلاَّ خَرَّتْ خَطَايَا رِجلَيْهِ مِنْ أنَاملِهِ مَعَ الماءِ ، فَإنْ هُوَ قَامَ فَصَلَّى ، فَحَمِدَ الله تَعَالَى ، وأثنى عَلَيهِ ومَجَّدَهُ بالَّذي هُوَ لَهُ أهْلٌ ، وَفَرَّغَ قلبه للهِ تَعَالَى ، إلاَّ انْصَرفَ مِنْ خَطِيئَتِهِ كهيئته يَومَ وَلَدتهُ أُمُّهُ )) .

فحدث عَمرُو بن عَبسَة بهذا الحديث أَبَا أُمَامَة صاحِب رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ لَهُ أَبُو أُمَامَة : يَا عَمْرُو بنُ عَبسَة ، انْظُر مَا تقولُ ‍! في مقامٍ واحدٍ يُعْطَى هَذَا الرَّجُلُ ؟ فَقَالَ عَمْرٌو : يَا أَبَا أُمَامَة ، لقد كَبرَتْ سِنّي ، وَرَقَّ عَظمِي ، وَاقْتَرَبَ أجَلِي ، وَمَا بِي حَاجَةٌ أنْ أكْذِبَ عَلَى اللهِ تَعَالَى ، وَلا عَلَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، لَوْ لَمْ أسمعه مِنْ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، إلاَّ مَرَّةً أَوْ مَرَّتَينِ أَوْ ثَلاثاً – حَتَّى عَدَّ سَبْعَ مَرَّات – مَا حَدَّثْتُ أبداً بِهِ ، وَلكنِّي سمعتُهُ أكثَر من ذلِكَ . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Najiih 'Amru bin 'Asabah As-Sulamiy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Katika siku zangu za Ujahiliyyah nilikuwa nadhani kuwa watu wapo katika upotevu na wao hawakuwa katika kitu chochote (katika kufuata Dini ya haki). Watu wakati huo walikuwa wakiabudu masanamu. Nilisikia habari ya kwamba yupo mtu Makkah aliyekuwa akieleza kuhusu jambo jipya. Nilipanda kipandio changu na nikaelekea Makkah na nilipofika nilikutana na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye alikuwa akifanya mambo yake kwa siri kwa sababu ya mateso kutoka kwa watu wake. Nilijificha mpaka nikapata nafasi ya kukutana naye hapo Makkah, na hapo nikamuuliza: "Wewe ni nani?" Akasema: "Mimi ni Nabiy" Nikasema: "Na Nabiy ni nini?" Akasema: "Nimetumwa na Allaah." Nikasema: "Amekutuma na kitu gani?" Akasema: "Amenituma kuunganisha kizazi, na kuvunja masanamu, na kumpwekesha Allaah wala asishirikishwe na chochote." Nikamuuliza: "Na ni akina nani ambao wako nawe juu ya hili?" Akasema: "Watu walio huru pamoja na watumwa." Na wakati huo alikuwa pamoja na Abu Bakr na Bilaal. Nikasema: "Mimi nakufuata wewe." Akasema: "Hakika wewe huwezi kufanya hivyo sasa, je huoni hali yangu na watu? Lakini nenda zako kwa familia yako na pindi utakaposikia ya kuwa nimefaulu katika jukumu basi wakati huo njoo kwangu." Kwa hali hiyo nilirudi kwa familia na watu wangu na Rasuli wa Allaah alihama Madinah. Nilibaki pamoja na familia yangu na huku ninafuatilia habari na nikawa nawauliza watu kuhusu Rasuli wa Allaah mpaka baadhi ya watu wangu walipozuru Madinah. Nikawauliza (waliporudi): "Huyu mtu aliyehamia Madinah amefanya nini?" Wakasema: "Watu wanakwenda kwake kukubali ujumbe wake (kusilimu) japokuwa watu wake walikuwa wanataka kumuua lakini wakashindwa." Niliwasili Madinah na nikafika kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), na kumuuliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Je, unanifahamu?" Akasema: "Ndio, wewe ni yule uliyenikuta Makkah." Nikasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Nijulishe yale aliyokuelimisha Allaah ambayo siyajui na unipe habari ya Swalaah?" Akasema: "Swali Swalaah ya Asubuhi (Swalatul Fajr), kisha jiweke kando (usiswali) mpaka jua liwe limepanda juu ya mbingu kiasi cha mkuki, kwani linapochomoza linachomoza baina ya pembe mbili za Shetani na wakati huo ndio makafiri wanalisujudia. Baada ya hapo unaweza kuswali, kwani Swalaah inashuhudiwa na inahudhuriwa na Malaika mpaka kivuli cha mkuki kiwe sawa (kwa kupotea) na urefu wa mkuki. Baada ya hapo usiswali, kwani wakati huo Moto uantiwa kuni (za kuuwakisha). Kivuli kitakaporefuka basi Swali, kwani Swalaah inashuhudiwa na ianhudhuriwa na Malaika mpaka wakati wa Alasiri. Baada ya hapo jiepushe kuswali mpaka machweo, kwani jua linakuchwa (linazama) baina ya pembe mbili za Shetani na wakati huo makafiri wanalisujudia." Hapo nikasema: "Ee Nabiy wa Allaah! Wudhu', nihadithie kuhusu hilo." Akasema: "Hakuna mtu yeyote ambaye atachukua maji ya kutawadhia, akasukutua na kusafisha pua yake isipokuwa madhambi ya pua na modomo wake yanaoshwa na kutolewa nje. Kisha anapoosha uso wake kama alivyoamrisha Allaah isipokuwa madhambi yake ya uso yanadondoka pembezoni mwa ndevu zake pamoja na maji. Kisha anaosha mikono yake mpaka vifundoni, isipokuwa hudondoka madhambi ya mikono yake kwenye vidole pamoja na maji. Kisha anapaka kichwa chake, isipokuwa hutoka madhambi yote ya kichwa kutoka katika mwisho wa nywele pamoja na maji hayo. Kisha anaosha miguu yake mpaka vifundoni isipokuwa makosa yote ya miguu hufutwa pamoja na maji yanapotoka. Na hapo anaposimama kuswali, akamuhimidi Allaah Ta'aalaa, akamsifu na kumtukuza kwa lile ambalo Yeye ndiye Mwenyewe (anastahiki zaidi) na akaufanya moyo wake unyenyekee kikamilifu kwa ajili ya Allaah Ta'aalaa isipokuwa makosa yake yote hufutwa akawa yuko katika hali kama ile siku aliyezaliwa na mamake. Pale 'Amru bin 'Abasah alipomuhadithia Hadiyth hii Abu Umamah, Swahaaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), Abu Umamah alimwambia: "Ee 'Amru: "Ee Abu Umamah! Hakika nimekuwa mzee na mifupa yangu imekauka na ajali yangu imekaribia (kufa kwangu) na wala sina haja yeyote ya kusema uwongo juu ya Allaah Ta'aalaa wala juu ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Lau kama sikumsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mara moja au mbili au tatu na akahesabu mpaka kufika mara saba nisingekuwa ni mwenye kumhadithia yeyeote milele lakini nimesikia zaidi ya hivyo." [Muslim]





Hadiyth – 28

وعن أَبي موسى الأشعري رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( إِذَا أرادَ الله تَعَالَى رَحمةَ أُمَّةٍ ، قَبَضَ نَبيَّهَا قَبْلَها ، فَجعلهُ لَهَا فَرطاً وسلَفاً بَيْنَ يَديْهَا ، وإذَا أرادَ هَلَكَةَ أُمَّةٍ ، عَذَّبَهَا وَنَبِيُّهَا حَيٌّ ، فَأهلكَها وَهُوَ حيٌّ يَنظُرُ ، فَأقرّ عَينَهُ بهلاكِها حِينَ كَذَّبُوهُ وَعَصَوا أمْرَهُ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Muuwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapotaka Allaah Mtukufu rahma kwa watu, Humfisha Nabiy wao kabla yao, na kufanya ishara, na mtangulizi siku ya mwisho; na Anapotaka Kuangamiza watu, Huwaadhibu na Nabiy wao yu hai, na Huwaangamiza Nabiy wao akiwatazama, Hutuliza jicho lake kwa kuangamia kwao, kwa kumkadhibisha kwao na kuasi amri yake." [Muslim]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب فضل الرجاء

052-Mlango Wa Ubora wa Matarajio Mema



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:

وَأُفَوِّضُ أَمْرِي إِلَى اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ﴿٤٤﴾

Na naaminisha mambo yangu kwa Allaah. Hakika Allaah ni Mwenye kuona waja Wake. [Ghaafir: 44]





فَوَقَاهُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِ مَا مَكَرُوا ۖ ﴿٤٥﴾

Basi Allaah Akamlinda na maovu ya yale waliyoyapangia njama. [Ghaafir: 45]







Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم، أَنَّهُ قَالَ : (( قَالَ الله (عزّ وجلّ) : أَنَا عِنْدَ ظَنِّ عَبْدِي بِي ، وَأَنا معه حَيْثُ يَذْكُرنِي ، وَاللهِ ، للهُ أفْرَحُ بِتَوبَةِ عَبْدِهِ مِنْ أحَدِكُمْ يَجِدُ ضَالَّتَهُ بالفَلاَةِ ، وَمَنْ تَقَرَّبَ إلَيَّ شِبْراً ، تَقَرَّبْتُ إِلَيْهِ ذِرَاعاً ، وَمَنْ تَقَرَّبَ إِلَيَّ ذِرَاعاً ، تَقَرَّبْتُ إِلَيْهِ بَاعاً ، وَإِذَا أقْبَلَ إِلَيَّ يَمْشِي أقْبَلْتُ إِلَيْهِ أُهَرْوِلُ )) متفقٌ عليه ، وهذا لفظ إحدى روايات مسلم . وتقدم شرحه في الباب قبله.

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema kuwa: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: Amesema Allaah ('Azza wa Jalla): "Hakika Mimi namchukulia mja kwa anavyonichukulia, Nami nipo pamoja naye pale anaponitaja. Naapa kwa Allaah! Allaah ana furaha zaidi kwa toba ya mja Wake kuliko mmoja wenu anayempata ngamia wake aliyepotea jangwani. Na yeyote anayekuja karibu Nami kwa shibiri, Mimi nakuja karibu yake kwa dhiraa. Yule anayekuja karibu Nami kwa dhiraa, Mimi nakuja kwake kwa kiasi cha pima moja. Na anayekuja Kwangu kwa kutembea, Mimi nakuja kwake kwa kukimbia." [Al-Bukhaariy na Muslim]. Na hii ni lafdhi moja wapo ya riwaayah ya Muslim. Na imepokewa katika Swahiyh mbili: "Nami niko pamoja naye anaponikumbuka na kunitaja."







Hadiyth – 2

وعن جابر بن عبد الله رضي الله عنهما : أنه سمع رسول الله صلى الله عليه وسلم قبلَ مَوْتِه بثَلاثَةِ أيّام ، يقولُ : (( لاَ يَمُوتَنّ أحَدُكُمْ إِلاَّ وَهُوَ يُحْسِنُ الظَّنَّ بالله (عزّ وجلّ) )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Jaabir bin 'Abdillaah (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) kuwa yeye amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kabla ya mauti yake kwa siku tatu akisema: "Asife mmoja wenu isipokuwa atarajie mema na mazuri kutoka kwa Allaah ('Azza wa Jalla)." [Muslim]





Hadiyth – 3

وعن أنس رضي الله عنه، قَالَ : سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( قَالَ الله تَعَالَى : يَا ابْنَ آدَمَ ، إنَّكَ ما دَعَوْتَنِي وَرَجَوْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ عَلَى مَا كَانَ مِنْكَ وَلاَ أُبَالِي . يَا ابْنَ آدَمَ ، لَوْ بَلَغت ذُنُوبُك عَنَانَ السماءِ ، ثُمَّ اسْتَغْفَرْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ وَلاَ أُبَالِي . يَا ابْنَ آدَمَ ، إِنَّكَ لَوْ أتَيْتَنِي بِقُرَابِ الأَرْضِ خَطَايا ، ثُمَّ لَقَيْتَنِي لاَ تُشْرِكُ بِي شَيْئاً ، لأَتَيْتُكَ بقُرَابِها مَغْفِرَةً )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa amemsikia Rasuli wa Allaahu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema kwamba Allaah Ta'aalaa amesema: "Ee binadamu, hakika wewe kila unapoendelea kuniomba na kunitarajia, basi Nitakusamehe dhambi ulizonazo wala sijali. Ee binadamu, hata kama dhambi zako zikifika mpaka mawinguni, kisha ukaniomba msamaha, Nitakughufiria. Ee binadamu, hakika wewe lau wanijia na makosa yenye kujaa ardhi kisha ukanikabili Mimi na hali hunishirikishi na kitu chochote, basi Nitakupa mfano wake maghfira." [At-Tirmidhiy, na alisema ni Hadiyth Hasan.
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب الجمع بين الخوف والرجاء

053-Mlango Wa Kujumuisha Baina ya Hofu na Matarajio



Alhidaaya.com



اعْلَمْ أنَّ المُخْتَارَ لِلْعَبْدِ في حَالِ صِحَّتِهِ أنْ يَكُونَ خَائفاً رَاجِياً ، وَيَكُونَ خَوْفُهُ وَرَجَاؤُهُ سَواءً ، وفي حَالِ المَرَضِ يُمحَّضُ الرَّجاءُ ، وقواعِدُ الشَّرْع مِنْ نصُوصِ الكِتَابِ والسُّنَةِ وغَيْرِ ذَلِكَ مُتظاهِرَةٌ عَلَى ذلك .

Imam An-Nawawiy anasema: "Mja wa Allaah anatakiwa ajue ya kwamba inapendeza kwake akiwa katika hali ya siha nzuri awe ni mwenye kuwa na hofu kwa Allaah Ta'aalaa na matarajio. Na hofu yake na matumaini yake yawe sawa sawa. Na anapokuwa mgonjwa anatakiwa awe na Imani thabiti pamoja na matarajio yaliyo makubwa zaidi. Katika hili kanuni za sheria ya Kiislamu zipo wazi kabisa kwa naswi (maandiko) katika Kitabu (Qur-aan) na Sunnah na nyinginezo."





قَالَ الله تَعَالَى:

فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٩٩﴾

Basi hawaaminishi mipango ya Allaah isipokuwa watu wenye kukhasirika. [Al-A'raaf: 99]



إِنَّهُ لَا يَيْأَسُ مِن رَّوْحِ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْكَافِرُونَ ﴿٨٧﴾

Hakika hawakati tamaa na faraja ya Allaah isipokuwa watu makafiri. [Yuwsuf: 87]



يَوْمَ تَبْيَضُّ وُجُوهٌ وَتَسْوَدُّ وُجُوهٌ ۚ ﴿١٠٦﴾

Siku nyuso zitakuwa nyeupe na nyuso (nyingine) zitakuwa nyeusi. [Aal-'Imraan: 106]



إِنَّ رَبَّكَ سَرِيعُ الْعِقَابِ وَإِنَّهُ لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٦٥﴾

Hakika Rabb wako ni Mwepesi wa kuakibu, na hakika Yeye bila shaka ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-An'aam: 165]



إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ ﴿١٣﴾ وَإِنَّ الْفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٍ ﴿١٤﴾

Hakika Waumini watendao mema kwa wingi bila shaka watakuwa katika neema (taanasa, furaha n.k). Na hakika watendao dhambi bila shaka watakuwa katika moto uwakao vikali mno. [Al-Infitwaar: 13-14]



فَأَمَّا مَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ ﴿٦﴾ فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ ﴿٧﴾ وَأَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ ﴿٨﴾ فَأُمُّهُ هَاوِيَةٌ ﴿٩﴾

Basi yule itakayekuwa mizani yake nzito. Huyo atakuwa katika maisha ya kuridhisha. Na yule itakayekuwa mizani yake khafifu.Basi makazi yake ni Haawiyah. [Al-Qaari-'ah: 6-9]







Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( لَوْ يَعْلَمُ الْمُؤمِنُ مَا عِنْدَ الله مِنَ العُقُوبَةِ ، مَا طَمِعَ بِجَنَّتِهِ أَحَدٌ ، وَلَوْ يَعْلَمُ الكَافِرُ مَا عِنْدَ الله مِنَ الرَّحْمَةِ ، مَا قَنَطَ مِنْ جَنَّتِهِ أحَدٌ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Lau kama Muumini atajua ile adhabu kamili ya Allaah, hangetamani yeyote Pepo Yake. Na lau kafiri angejua kwa ukamilifu wake rehema aliyonayo Allaah, asingekata tamaa yeyote na Pepo Yake." [Muslim]





Hadiyth – 2

وعن أَبي سعيد الخدرِيِّ رضي الله عنه: أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( إِذَا وُضِعَتِ الجنازةُ واحْتَمَلَهَا النَّاسُ أَوِ الرِّجَالُ عَلَى أعناقِهِمْ ، فَإنْ كَانَتْ صَالِحَةً ، قالتْ: قَدِّمُونِي قَدِّمُونِي ، وَإنْ كَانَتْ غَيْرَ صَالِحَةٍ ، قالتْ : يَا وَيْلَهَا ! أَيْنَ تَذْهَبُونَ بها ؟ يَسْمَعُ صَوْتَها كُلُّ شَيْءٍ إِلاَّ الإنْسانُ ، وَلَوْ سَمِعَهُ صَعِقَ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Itakapokuwa tayari jeneza na ikabebwa na watu juu ya mabega yao, akiwa ni mtu mwema atasema: 'Nipelekeni mbele, nipelekeni mbele. Na ikiwa si mwema, atasema: 'Ole wake! Mnanipeleka wapi?' Sauti yake inasikika na kila kitu isipokuwa mwanadamu na lau angesikia (mwanadamu) basi angezimia." [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 3

وعن ابن مسعود رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( الجَنَّةُ أقْرَبُ إِلى أحَدِكُمْ مِنْ شِرَاكِ نَعْلِهِ ، وَالنَّارُ مِثْلُ ذلك )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uud (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (SWalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Pepo ipo karibu sana na mmoja wenu kuliko kamba zake za viatu na Moto ni mfano wa hivyo." [Al-Bukhaariy]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب فضل البكاء من خشية الله تَعَالَى وشوقاً إِليه

054-Mlango Wa Fadhila ya Kulia Kutokana na Kumuogopa Allaah na Shauku Kwake



Alhidaaya.com





قَالَ الله تَعَالَى:

وَيَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ يَبْكُونَ وَيَزِيدُهُمْ خُشُوعًا ۩﴿١٠٩﴾

Na wanaporomoka kifudifudi huku wanalia na inawazidishia unyenyekevu. [Al-Israa: 109]



أَفَمِنْ هَـٰذَا الْحَدِيثِ تَعْجَبُونَ ﴿٥٩﴾ وَتَضْحَكُونَ وَلَا تَبْكُونَ ﴿٦٠﴾

Je, mnastaajabu kwa Al-Hadiyth hii (ya Qur-aan)? Na mnacheka na wala hamlii? [An-Najm: 59-60]







Hadiyth – 1

وعن ابن مسعود رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ لِي النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم: (( اقْرَأْ عليَّ القُرْآنَ )) قلت : يَا رسول اللهِ ، أقرأُ عَلَيْكَ ، وَعَلَيْكَ أُنْزِلَ ؟! قَالَ : (( إِنِّي أُحِبُّ أنْ أسْمَعَهُ مِنْ غَيرِي )) فَقَرَأْتُ عَلَيْهِ سورةَ النِّسَاءِ ، حَتَّى جِئْتُ إِلى هذِهِ الآية 🙁 فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِنْ كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَى هؤُلاءِ شَهيداً) [ النساء : 41 ] قَالَ : (( حَسْبُكَ الآنَ )) فَالَتَفَتُّ إِلَيْهِ فإذا عَيْنَاهُ تَذْرِفَان . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uud (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: "Nisomee Qur-aan." Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! nikusomee Qur-aan na juu yako imeteremshwa?" Akasema: "Mimi napenda niisikie kwa mwingine Hivyo nikamsomea Suwrah an-Nisaa' mpaka nikafika katika ayah hii: "Basi itakuwaje Tutakapoleta kutoka kila Ummah shahidi, na Tukakuleta (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa shahidi juu ya hawa?" [An-Nisaa: 41]. Akasema: "Inatosha sasa." Tahamaki macho yake yanabubujika machozi." [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 2

وعن أنس رضي الله عنه، قَالَ : خطب رسول الله صلى الله عليه وسلم خُطْبَةً مَا سَمِعْتُ مِثْلَهَا قَطُّ ، فقال : (( لَوْ تَعْلَمُونَ مَا أعْلَمُ ، لَضَحِكْتُمْ قَليلاً وَلَبَكَيْتُمْ كَثِيراً )) قَالَ : فَغَطَّى أصْحَابُ رسول الله صلى الله عليه وسلم وُجُوهَهُمْ ، وَلَهُمْ خَنِينٌ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Anas ambaye amesema: "Alituhutubia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hotuba ambayo sijawahi kusikia mfano wake kabisa, akasema: 'Lau nyinyi mgejua ninayoyajua basi mgecheka kidogo na kulia sana.' Hapo Swahaaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) waliokuwepo walifunika nyuso zao na kuanza kumamia (kulia) kwa kwikwi." [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( لا يَلِجُ النَّارَ رَجُلٌ بَكَى مِنْ خَشْيَةِ اللهِ حَتَّى يَعُودَ اللَّبَنُ في الضَّرْعِ ، وَلاَ يَجْتَمِعُ غُبَارٌ في سبيلِ اللهِ وَدُخَانُ جَهَنَّمَ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديثٌ حَسنٌ صحيحٌ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hataingia Motoni mtu ambaye Amelia kwa kumuogopa Allaah mpaka maziwa yarudi katika matiti yake na pia vumbi liliopatikana kwa mtu kufanya Jihadi katika njia ya Allaah na moshi wa Jahanam haziungani pamoja." [At-Tirmidhiy, na alisema ni Hadiyth Hasan Swahiyh].





Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( سَبْعَةٌ يُظِلُّهُمُ اللهُ في ظِلِّهِ يَوْمَ لا ظِلَّ إِلاَّ ظِلُّهُ : إمَامٌ عَادِلٌ ، وَشَابٌ نَشَأَ فِي عِبَادَةِ اللهِ تَعَالَى ، وَرَجُلٌ قَلْبُهُ مُعَلَّقٌ بِالمَسَاجِدِ ، وَرَجُلاَنِ تَحَابّا في الله اجْتَمَعَا عَلَيْهِ وتَفَرَّقَا عَلَيْهِ ، وَرَجُلٌ دَعَتْهُ امْرَأَةٌ ذَاتُ مَنْصِبٍ وَجَمَالٍ، فَقال: إنِّي أَخَافُ الله، وَرَجُلٌ تَصَدَّقَ بِصَدَقَةٍ فَأخْفَاهَا حَتَّى لاَ تَعْلَمَ شِمَالُه مَا تُنْفِقُ يَمِينُهُ ، وَرَجُلٌ ذَكَرَ الله خَالِياً ففاضت عَيْنَاهُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Na imepokewa kwa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Saba, Allaah atawafunika chini ya kivuli Chake Siku ambayo hakuna kivuli isipokuwa kivuli Chake: Imamu (kiongozi) muadilifu, na kijana aliyeinukia katika kumuabudu Allaah Ta'aalaa, na mtu ambaye moyo wake umetundikwa katika Msikiti, na watu wawili wanaopendana kwa ajili ya Allaah, wanakuwa pamoja na kufarikiana kwa ajili Yake, na mtu ambaye ameitwa na mwanamke mzuri na mwenye kuvutia (kuzini naye), akasema: 'Mimi namwogopa Allaah.' na mtu aliyetoa swadaqah kwa kuificha sana mpaka mkono wake wa kushoto usijue kilichotolewa na mkono wa kuume, na mtu ambaye amemkumbuka Allaah peke yake na macho yake yakabubujika na machozi." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 5

وعن عبد الله بن الشِّخِّير رضي الله عنه ، قَالَ : أتيتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم وَهُوَ يُصَلِّي ولِجَوْفِهِ أَزِيزٌ كَأَزِيزِ المِرْجَلِ مِنَ البُكَاءِ . حديث صحيح رواه أَبو داود والترمذي في الشمائل بإسناد صحيح .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillah bin Ash-Shikhayr (Radhwiyah Allaah 'anhu) ambaye amesema: Nilikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) naye alikuwa anaswali. Nilisikia sauti ya kilio kutoka katika kifua chake ambacho kilikua kama sauti ya chungu kinacho chemka." [Abu Daawuud na At-Tirmidhiy katika "Shamaa'il" na Isnaad yake ni Swahiyh]





Hadiyth – 6

وعن أنس رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم لأُبَي بن كعب رضي الله عنه: (( إنَّ الله (عزّ وجلّ) أَمَرَنِي أنْ أقْرَأَ عَلَيْكَ 🙁 لَمْ يَكُنِ الَّذِينَ كَفَروا ... )قَالَ : وَسَمَّانِي ؟ قَالَ : (( نَعَمْ )) فَبَكَى أُبَيٌّ . متفقٌ عَلَيْهِ .وفي رواية : فَجَعَلَ أُبَيٌّ يَبْكِي .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia Ubayy bin Ka'b: "Hakika Allaah ('Azza wa Jalla), ameniamuru nikusomee: "Lam Yakunil Ladhiina Kafaruu..." [Al-Bayyinah]." Ubayy akauliza: "Allaah amenitaja mimi kwa jina?" Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ndio." Ubayy akawa alilia." [Al-Bukhaariy na Muslim]. Na katika riwaayah: "Ubayy akawa analia."





Hadiyth – 7

وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ أَبو بكر لِعُمَرَ ، رَضِيَ اللهُ عنهما ، بعد وفاة رسول الله صلى الله عليه وسلم: انْطَلِقْ بِنَا إِلى أُمِّ أيْمَنَ رضي الله عنها نَزورُهَا ، كَمَا كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم يَزُورُها ، فَلَمَّا انْتَهَيَا إِلَيْهَا بَكَتْ ، فقالا لها : مَا يُبْكِيكِ ؟ أمَا تَعْلَمِينَ أنَّ مَا عِنْدَ الله تَعَالَى خَيرٌ لرسولِ الله صلى الله عليه وسلم! قالت : مَا أبْكِي أَنْ لاَ أَكُونَ أَعْلَمُ أنَّ مَا عِنْدَ اللهِ خَيْرٌ لرسولِ الله صلى الله عليه وسلم، وَلكِنِّي أبكِي أَنَّ الْوَحْيَ قَد انْقَطَعَ مِنَ السَّمَاءِ ؛ فَهَيَّجَتْهُما عَلَى البُكَاءِ ، فَجَعَلا يَبْكِيَانِ مَعَهَا . رواه مسلم.

Kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: Abu Bakr alimwambia 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) baada ya kufa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Twende kumzuru Ummu Ayman (Radhwiyah Allaahu 'anhaa), kama alivyokuwa Rasuli wa Allaah anamzuru." Tulipofika kwake akalia. Wakamwambia: "Nini kinachokuliza?, kwani hujui yalio kwa Allaah ni bora kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)?" Akasema: "Mimi najua nami silii kwa sababu hiyo bali nalia kukatika wahyi toka mbinguni." Hili liliwafanya Swahaaba wawili watukufu (Abu Bakr na 'Umar Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) walie pamoja naye." [Muslim]







Hadiyth – 8

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : لَمَّا اشْتَدَّ برسول الله صلى الله عليه وسلم وَجَعُهُ ، قِيلَ له في الصَّلاَةِ ، فقال : (( مُرُوا أَبَا بَكْرٍ فَلْيُصَلِّ بِالنَّاسِ )) فقالت عائشة رضي الله عنها : إنَّ أَبَا بَكْرٍ رَجُلٌ رَقِيقٌ ، إِذَا قَرَأَ القُرْآنَ غَلَبَهُ البُكَاءُ ، فقال : (( مُرُوهُ فَليُصَلِّ )) .

وفي رواية عن عائشة ، رضي الله عنها ، قالت : قلت : إنَّ أَبَا بَكْرٍ إِذَا قَامَ مَقَامَكَ لَمْ يُسْمِعِ النَّاسَ مِنَ البُكَاءِ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) amesema: "ugonjwa wa Rasuli wa Allaahu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ulipozidi aliulizwa nani aswalishe watu. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: "Muamrisheni Abu Bakr aswalishe watu." 'Aaisha (Radhwiyah Allaahu 'anhaa) alisema: "Hakika Abu Bakr (Radhwiyah Allaahu 'anhu) moyo wake ni mwema (laini) na hivyo anaposoma Quraan huanguka kilio (hulia)." Akasema: "Muamuruni (yeye Abu Bakr) aswalishe."

Na katika riwaayah kutoka kwa 'Aisha (Radhwiyah Allaahu 'anhaa) ambaye amesema, nikasema: "Hakika Abu Bakr anaposimama (Imamu) watu hawatamsikia kwa sababu ya kulia." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 9

وعن إبراهيم بن عبد الرحمان بن عوف : أنَّ عبد الرحمان بن عوف رضي الله عنه أُتِيَ بطعام وكان صائِماً ، فقال : قُتِلَ مُصْعَبُ بن عُمَيْر رضي الله عنه، وَهُوَ خَيْرٌ مِنِّي ، فَلَمْ يوجَدْ له مَا يُكَفَّنُ فيهِ إِلاَّ بُرْدَةٌ إنْ غُطِّيَ بِهَا رَأسُهُ بَدَتْ رِجْلاهُ ؛ وَإنْ غُطِّيَ بِهَا رِجْلاَهُ بَدَا رَأسُهُ ، ثُمَّ بُسِطَ لَنَا مِنَ الدُّنْيَا مَا بُسِطَ – أَو قَالَ : أُعْطِينَا مِنَ الدُّنْيَا مَا أُعْطِينَا – قَدْ خَشِينا أنْ تَكُونَ حَسَنَاتُنَا عُجِّلَتْ لَنَا ، ثُمَّ جَعَلَ يَبكِي حَتَّى تَرَكَ الطعَام . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwake Ibraahiym bin 'Abdir-Rahmaan bin 'Awf kwamba 'Abdir-Rahmaan bin 'Awf (Radhwiyah Allaahu 'anhu) aliletewa chakula akiwa ameamefunga, akasema: "Mus'ab bin 'Umayr (Radhwiyah Allaahu 'anhu) aliuliwa naye ni bora kuliko mimi na hakukupatikana kitu cha kumkafini isipokuwa kitambara kilichokuwa kifupi sana. Akifinikwa kichwa miguu kichwa hubaki wazi. Baada ya hapo tukafunguliwa dunia au alisema: 'Tukapatiwa katika dunia kile tulichopatiwa (tukapatiwa mali nyingi).' Tunaogopa isiwe malipo yetu tumepatiwa mapema (yaani katika hii dunia). Kisha akaanza kulia mpaka akaacha chakula." [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 10

وعن أَبي أُمَامَة صُدَيِّ بن عجلان الباهلي رضي الله عنه، عن النبي صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( لَيْسَ شَيْءٌ أحَبَّ إِلى اللهِ تَعَالَى مِنْ قطْرَتَيْنِ وَأثَرَيْنِ : قَطَرَةُ دُمُوع مِنْ خَشْيَةِ اللهِ ، وَقَطَرَةُ دَمٍ تُهَرَاقُ في سَبيلِ اللهِ. وَأَمَّا الأَثَرَانِ : فَأَثَرٌ في سَبيلِ اللهِ تَعَالَى، وَأَثَرٌ في فَريضةٍ مِنْ فَرائِضِ الله تَعَالَى )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديثٌ حسنٌ )) .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Umamah Swudayyi bin 'Ajlaan Al-Baahiliy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna kitu kinachompendeza Allaah Ta'aalaa kama matone mawili na alambili. Ama matone ni machozi yanayobubujika kwa kumuogopa Allaah na damu inayotoka katika njia ya Allaah. Na alama mbili, alama katika njia ya Allaah Ta'aalaa na alama inayopatikana katika kutekeleza faradhi miongoni mwa faradhi miongoni mwa faradhi alizoamrisha Allaah Ta'aalaa." [At-Tirmidhiy, na alisema ni Hadiyth Hasan]



Hadiyth – 11

حديث العرباض بن سارية رضي الله عنه، قَالَ : وعظنا رسول الله صلى الله عليه وسلم مَوعظةً وَجلَتْ منها القُلُوبُ ، وذرِفت منها الْعُيُونُ . وقد سبق في باب النهي عن البدع.

Amehadithia al-'Irbaadh bin Saariyah kwamba: "Alituaidhia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mawaidha yaliyozifanya nyoyo zikaingia hofu na macho yakatokwa na machozi." Hii ni sehemu tu ya Hadiyth ndefu iliyotangulia kutajwa katika Mlango wa Amri ya kuhifadhi Sunnah na Adabu Zake.
 
Back
Top Bottom