Ramadhan Special Thread
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب فضل الزهد في الدنيا والحث عَلَى التقلل منها وفضل الفقر

055-Mlango Wa Fadhila na Ubora wa Kuupa Nyongo Ulimwengu wa Kukinai Kwa Kichache na Ubora wa Ufakiri



Alhidaaya.com





قَالَ الله تَعَالَى:

إِنَّمَا مَثَلُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ مِمَّا يَأْكُلُ النَّاسُ وَالْأَنْعَامُ حَتَّىٰ إِذَا أَخَذَتِ الْأَرْضُ زُخْرُفَهَا وَازَّيَّنَتْ وَظَنَّ أَهْلُهَا أَنَّهُمْ قَادِرُونَ عَلَيْهَا أَتَاهَا أَمْرُنَا لَيْلًا أَوْ نَهَارًا فَجَعَلْنَاهَا حَصِيدًا كَأَن لَّمْ تَغْنَ بِالْأَمْسِ ۚ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴿٢٤﴾

Hakika mfano wa uhai wa dunia ni kama maji Tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, kisha yakachanganyika nayo mimea ya ardhi katika wanayoila watu na wanyama, mpaka ardhi ilipokamilisha uzuri wake na ikapambika na wakayakinisha watu wake kwamba wanao uwezo juu yake (kuivuna); tahamaki amri Yetu ikaijia usiku au mchana, Tukaifanya kama iliyofekwa kama kwamba haikusitawi jana. Hivyo ndivyo Tunavyofasili waziwazi Aayaat (ishara, hoja) kwa watu wanaotafakari. [Yuwnus: 24]





وَاضْرِبْ لَهُم مَّثَلَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ فَأَصْبَحَ هَشِيمًا تَذْرُوهُ الرِّيَاحُ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ مُّقْتَدِرًا ﴿٤٥﴾ الْمَالُ وَالْبَنُونَ زِينَةُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ أَمَلًا ﴿٤٦﴾

Na wapigie mfano wa uhai wa dunia kama maji Tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, yakachanganyika kwayo mimea ya ardhi (ikasitawi), kisha yakawa makavu yaliyovurugika yanapeperushwa na upepo. Na Allaah daima ni Mwenye Uwezo wa juu kabisa kwa kila kitu. Mali na watoto ni pambo la uhai wa dunia. Na mema yanayobakia ni bora mbele ya Rabb wako, kwa thawabu na matumaini. [Al-Kahf: 45-46]



اعْلَمُوا أَنَّمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا لَعِبٌ وَلَهْوٌ وَزِينَةٌ وَتَفَاخُرٌ بَيْنَكُمْ وَتَكَاثُرٌ فِي الْأَمْوَالِ وَالْأَوْلَادِ ۖ كَمَثَلِ غَيْثٍ أَعْجَبَ الْكُفَّارَ نَبَاتُهُ ثُمَّ يَهِيجُ فَتَرَاهُ مُصْفَرًّا ثُمَّ يَكُونُ حُطَامًا ۖ وَفِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ شَدِيدٌ وَمَغْفِرَةٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانٌ ۚ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ ﴿٢٠﴾

Jueni kwamba uhai wa dunia ni mchezo na pumbao na mapambo, na kufakharishana baina yenu na kushindana kukithiri katika mali na watoto; ni kama mfano wa mvua inayowafurahisha wakulima mimea yake, kisha yananyweya, basi utayaona yamepiga manjano, kisha yanakuwa mabua yaliyonyauka na kupondekapondeka. Na Aakhirah kuna adhabu kali, na maghfirah kutoka kwa Allaah na radhi. Na uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni sterehe fupi za kughuri. [Al-Hadiyd: 29]





زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ الشَّهَوَاتِ مِنَ النِّسَاءِ وَالْبَنِينَ وَالْقَنَاطِيرِ الْمُقَنطَرَةِ مِنَ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ وَالْخَيْلِ الْمُسَوَّمَةِ وَالْأَنْعَامِ وَالْحَرْثِ ۗ ذَٰلِكَ مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَاللَّـهُ عِندَهُ حُسْنُ الْمَآبِ ﴿١٤﴾

Watu wamepambiwa huba ya matamanio miongoni mwa wanawake, na watoto, na mirundi ya mali iliyorundikwa ya dhahabu na fedha na farasi wenye chapa ya aina bora na wanyama wa mifugo na mashamba. Hayo ni starehe za uhai wa dunia, na Allaah Kwake kuna marejeo mazuri. [Aal-'Imraan: 14]





يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ ۖ فَلَا تَغُرَّنَّكُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا ۖ وَلَا يَغُرَّنَّكُم بِاللَّـهِ الْغَرُورُ ﴿٥﴾

Enyi watu! Hakika ahadi ya Allaah ni haki; basi usikughururini uhai wa dunia, na wala (shaytwaan) mwenye kughuri asikughururini kuhusu Allaah. [Faatwir: 5]



أَلْهَاكُمُ التَّكَاثُرُ ﴿١﴾ حَتَّىٰ زُرْتُمُ الْمَقَابِرَ ﴿٢﴾ كَلَّا سَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٣﴾ ثُمَّ كَلَّا سَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٤﴾ كَلَّا لَوْ تَعْلَمُونَ عِلْمَ الْيَقِينِ ﴿٥﴾

Kumekughafilisheni kutafuta wingi. Mpaka muingie makaburini. Laa hasha! Mtakuja kujua. Kisha laa hasha! Mtakuja kujua. Laa hasha! Lau mngelijua ujuzi wa yakini. [At-Takaathur: 1-5]





وَمَا هَـٰذِهِ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا لَهْوٌ وَلَعِبٌ ۚ وَإِنَّ الدَّارَ الْآخِرَةَ لَهِيَ الْحَيَوَانُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿٦٤﴾

Na huu uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni pumbao na mchezo; na hakika Nyumba ya Aakhirah bila shaka hiyo ndiyo yenye uhai wa kweli hasa (wa milele), lau wangelikuwa wanajua! [Al-'Ankabuwt: 64]







والآيات في الباب كثيرة مشهورة . وأما الأحاديث فأكثر مِنْ أن تحصر فننبِّهُ بطرف منها عَلَى مَا سواه .

Na ayah katika mlango huu ni nyingi na mashuhuri. Ama Hadiyth ni nyingi zaidi hata hazihesabiki na hapa tuataja baadhi yake.









Hadiyth – 1

عن عمرو بن عوف الأنصاري رضي الله عنه: أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم بَعَثَ أَبَا عبيدة بنَ الجَرَّاح رضي الله عنه إِلَى الْبَحْرَيْنِ يَأتِي بِجِزْيَتِهَا ، فَقَدِمَ بمَالٍ مِنَ الْبَحْرَيْنِ ، فَسَمِعَتِ الأَنْصَارُ بقُدُومِ أَبي عُبيْدَةَ ، فَوَافَوْا صَلاَةَ الفَجْرِ مَعَ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم، فَلَمَّا صَلَّى رسولُ الله صلى الله عليه وسلم ، انْصَرفَ ، فَتَعَرَّضُوا لَهُ ، فَتَبَسَّمَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم حِيْنَ رَآهُمْ ، ثُمَّ قَالَ: (( أظُنُّكُمْ سَمعتُمْ أنَّ أَبَا عُبَيْدَةَ قَدِمَ بِشَيْءٍ مِنَ الْبَحْرَيْنِ ؟ )) فقالوا : أجل ، يَا رسول الله، فقال : (( أبْشِرُوا وَأَمِّلْوا مَا يَسُرُّكُمْ، فَوالله مَا الفَقْرَ أخْشَى عَلَيْكُمْ ، وَلكِنِّي أخْشَى أنْ تُبْسَط الدُّنْيَا عَلَيْكُمْ كَمَا بُسِطَتْ عَلَى مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ ، فَتَنَافَسُوهَا كَمَا تَنَافَسُوهَا ، فَتُهْلِكَكُمْ كَمَا أهْلَكَتْهُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Amru bin Al 'Awfy Al Answaary (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimpeleka Abu 'Ubaydah 'Amir bin al-Jarraah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) Bahrayn kukusanya Jizyah yao. Akarudi na mali kutoka Bahrayn. Ma-Ansaar walipata habari ya kurudi kwa Abu 'Ubaydah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) hivyo wakaswali Swalaah ya Alfajiri pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Alipomaliza kuswali Rasuli wa Allaah, walikuja kwake. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitabasamu alipowaona, kisha akasema: "Nadhania mumesikia ya kwamba Abu 'Ubaydah amerudi na kitu kutoka Bahrayn?" Wakasema: "Ndio, ee Rasuli wa Allaah!" Akasema: "Furahini, na tarajieni vitu vitakavyo wafurahisha. Wa-Allaahi! Siwaogopeeni ufukara, lakini naogopa kukunjuliwa dunia juu yenu, kama walivyo kunjuliwa waliokuwa kabla yenu, mkaishindania kama walivyoishindania, ikakuangamizeni nyinyi kama ilivyowangamiza wao." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 2

وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه ، قَالَ : جلس رسولُ الله صلى الله عليه وسلم عَلَى الْمِنْبَرِ ، وَجَلَسْنَا حَوْلَهُ ، فقال : (( إنَّ ممَّا أخَافُ عَلَيْكُمْ مِنْ بَعْدِي مَا يُفْتَحُ عَلَيْكُمْ مِنْ زَهْرَةِ الدُّنْيَا وَزِينَتِهَا )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd al-Khudriy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: Alikaa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwenye mimbar nasi tukakaa duara (tukiwa tumemzunguka), akasema: "Kwa hakika yale ninayowaogopea nyinyi baada yangu ni kufunguliwa kwenu utajiri na kuvutiwa na dunia na mapambo yake." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 3

وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه : أن رسول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ: (( إنَّ الدُّنْيَا حُلْوَةٌ خَضِرَةٌ وَإنَّ الله تَعَالَى مُسْتَخْلِفُكُمْ فِيهَا، فَيَنْظُرُ كَيْفَ تَعْمَلُونَ، فَاتَّقُوا الدُّنْيَا وَاتَّقُوا النِّسَاءَ )) رواه مسلم.

Impokewa kutoka kwa Abu Saiyd Al-Khudriy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika dunia ni tamu na kijani (imejaa utajiri) na Allaah Ta'aalaa atawafanya nyinyi kuwa makhalifa humo na atawaangalia kwa yale mnayofanya. Hivyo tahadharini na dunia na wanawake." [Muslim]





Hadiyth – 4

وعن أنس رضي الله عنه : أن النبي صلى الله عليه وسلم، قَالَ: (( اللَّهُمَّ لاَ عَيْشَ إِلاَّ عَيْشَ الآخِرَةِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ee Allaah! Hakuna starehe isipokuwa starehe ya Aakherah." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 5

وعن أنس رضي الله عنه ، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( يَتْبَعُ الْمَيِّتَ ثَلاَثَةٌ : أهْلُهُ وَمَالُهُ وَعَمَلُهُ : فَيَرْجِعُ اثْنَانِ ، وَيَبْقَى وَاحِدٌ : يَرْجِعُ أهْلُهُ وَمَالُهُ وَيبْقَى عَمَلُهُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hufuata maiti mambo matatu: Watu wake, mali yake na amali yake. Viwili hurudi na kubakia jambo moja tu: Hurudi watu wake na mali yake na kubakia amali yake." [Ahmad, Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 6

وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( يُؤْتَى بِأنْعَمِ أهْلِ الدُّنْيَا مِنْ أهْلِ النَّارِ يَوْمَ القِيَامَةِ ، فَيُصْبَغُ في النَّارِ صَبْغَةً، ثُمَّ يُقَالُ : يَا ابْنَ آدَمَ ، هَلْ رَأيْتَ خَيْراً قَطُّ ؟ هَلْ مَرَّ بِكَ نَعِيمٌ قَطُّ ؟ فَيَقُولُ : لاَ وَاللهِ يَا رَبِّ ، وَيُؤْتَى بِأشَدِّ النَّاسِ بُؤسَاً في الدُّنْيَا مِنْ أهْلِ الجَنَّةِ ، فَيُصْبَغُ صَبْغَةً في الجَنَّةِ ، فَيُقَالُ لَهُ : يَا ابْنَ آدَمَ ، هَلْ رَأيْتَ بُؤساً قَطُّ ؟ هَلْ مَرَّ بِكَ شِدَّةٌ قَطُّ ؟ فيَقُولُ : لاَ وَاللهِ ، مَا مَرَّ بِي بُؤْسٌ قَطُّ ، وَلاَ رَأيْتُ شِدَّةً قَطُّ )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Anas kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ataletwa mtu mwenye neema zaidi katika watu duniani Siku ya Qiyaamah na kuchovya Motoni mara moja. Kisha kutasemwa: 'Ee binadamu! Je, umeona kheri yeyote? Je, ulipata neema yeyote?' Atasema: 'La! Wa-Allaahi! Sijapata, ee Rabb wangu.' Ataletwa maskini zaidi duniani katika watu wa Peponi, Atatiwa mara moja Peponi, Kutasemwa: 'Ee binadamu! Je, ulipata shida yeyeote?, Atasema: 'Wa-Allaahi! Sijapata tabu, sikupata shida yeyeote." [Muslim]





Hadiyth – 7

وعن المُسْتَوْرِد بن شَدَّاد رضي الله عنه، قَالَ: قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( مَا الدُّنْيَا في الآخِرَةِ إِلاَّ مِثْلُ مَا يَجْعَلُ أَحَدُكُمْ أُصْبُعَهُ في اليَمِّ، فَلْيَنْظُرْ بِمَ يَرْجِعُ ! )) رواه مسلم.

Imepokewa kutoka kwa Al-Mustawrid bin Shaddaad (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Dunia si chochote katika Aakherah isipokuwa ni kama mfano wa mtu anayetia kidole chake katika bahari. Naangalie kiasi gani cha maji kinachukua." [Muslim]





Hadiyth – 8

وعن جابر رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم مَرَّ بالسُّوقِ وَالنَّاسُ كَنَفَتَيْهِ ، فَمَرَّ بِجَدْيٍ أَسَكَّ مَيِّتٍ ، فَتَنَاوَلَهُ فَأَخَذَ بِأُذُنِهِ ، ثُمَّ قَالَ : (( أَيُّكُم يُحِبُّ أنْ يَكُونَ هَذَا لَهُ بِدرْهَم ؟ )) فقالوا : مَا نُحِبُّ أنَّهُ لَنَا بِشَيْءٍ وَمَا نَصْنَعُ بِهِ ؟ ثُمَّ قَالَ : (( أَتُحِبُّونَ أَنَّهُ لَكُمْ ؟ )) قَالُوا : وَاللهِ لَوْ كَانَ حَيّاً كَانَ عَيْباً ، إنَّهُ أسَكُّ فَكَيْفَ وَهُوَ ميِّتٌ ! فقال : (( فوَاللهِ للدُّنْيَا أهْوَنُ عَلَى اللهِ مِنْ هَذَا عَلَيْكُمْ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiyah Allaah 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipita sokoni pamoja na Swahaaba zake alimuona mbuzi mdogo amekufa na masikio yake yamekatwa. Alikishika katika masikio na kuuliza: "Nani anayemtaka (huyu mbuzi aliyekufa) kwa dirhamu moja?" Wakasema: "Hatutaki huyo awe ni wetu kwa chochote (hata bure). Na je, tutamfanya nini? " Kisha akasema: "Je, mngependa awe wenu bure?" Wakasema: "Wa-Allaahi! Hata kama angekuwa hai angekuwa na kasoro, vipi akiwa maiti?" Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Wa-Allaahu! dunia ni duni zaidi mbele ya Allaah kuliko juu yenu." [Muslim]







Hadiyth – 9

وعن أَبي ذر رضي الله عنه ، قَالَ : كُنْتُ أَمْشِي مَعَ النَّبي صلى الله عليه وسلم في حَرَّةٍ بِالمَدِينَةِ ، فَاسْتَقْبَلَنَا أُحُدٌ ، فقال : (( يَا أَبَا ذَرٍّ )) قلت : لَبَّيْكَ يَا رسولَ الله . فقال : (( مَا يَسُرُّنِي أنَّ عِنْدِي مِثْلَ أُحُدٍ هَذَا ذَهَباً تَمْضي عَلَيَّ ثَلاَثَةُ أيّامٍ وَعِنْدِي مِنْهُ دِينَارٌ ، إِلاَّ شَيْءٌ أرْصُدُهُ لِدَيْنٍ ، إِلاَّ أنْ أقُولَ بِهِ في عِبَادِ الله هكذا وَهَكَذَا وَهكَذَا )) عن يَمِينِهِ وعن شِمَالِهِ وَمِنْ خَلْفِهِ ، ثُمَّ سَارَ ، فقال : (( إنَّ الأَكْثَرينَ هُمُ الأَقَلُّونَ يَوْمَ القِيَامَةِ إِلاَّ مَنْ قَالَ بالمَالِ هكَذَا وَهكَذَا وَهكَذَا )) عن يمينِهِ وعن شِمَالِهِ وِمنْ خَلْفِهِ (( وَقَلِيلٌ مَاهُمُ )) . ثُمَّ قَالَ لي : (( مَكَانَكَ لاَ تَبْرَحْ حَتَّى آتِيكَ )) ثُمَّ انْطَلَقَ في سَوادِ اللَّيْلِ حَتَّى تَوَارَى ، فَسَمِعْتُ صَوتاً ، قَدِ ارْتَفَع ، فَتَخَوَّفْتُ أنْ يَكُونَ أحَدٌ عَرَضَ للنَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، فَأرَدْتُ أنْ آتِيهِ فَذَكَرتُ قَوْله : (( لا تَبْرَحْ حَتَّى آتِيَكَ )) فلم أبْرَحْ حَتَّى أتَاني ، فَقُلْتُ : لَقَدْ سَمِعْتُ صَوتاً تَخَوَّفْتُ مِنْهُ ، فَذَكَرْتُ لَهُ ، فقال : (( وَهَلْ سَمِعْتَهُ ؟ )) قلت : نَعَمْ ، قَالَ : (( ذَاكَ جِبريلُ أتَانِي . فقال : مَنْ مَاتَ مِنْ أُمَّتِكَ لاَ يُشْرِكُ بِاللهِ شَيْئاً دَخَلَ الْجَنَّةَ )) ، قلت : وَإنْ زَنَى وَإنْ سَرَقَ ؟ قَالَ : (( وَإنْ زَنَى وَإنْ سَرَقَ )) متفقٌ عَلَيْهِ ، وهذا لفظ البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: Nilikuwa natembea na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika majabali Madiynah tukatokea Uhud. Akaniita: "Ee Abu Dharr." Nikasema: "Labbayka ee Rasuli wa Allaah." Akasema: "Lau ningekuwa na dhahabu mfano wa Uhud hii, Ipite kwangu suku tatu nibaki nayo hata dinari moja, isipokuwa kuiweka kwa ajili ya deni. Ila Ningeigawa kwa waja wa Allaah hivi na hivi na hivi', kulia, kushoto na nyuma." Kisha akatembea akasema: "Hakika wenye vingi duniani ndio wenye kidogo zaidi Siku ya Qiyaamah, isipokuwa wanaotumia mali hivi na hivi na hivi', kulia na kushoto na nyuma, "Nao wao ni wachache." Baada ya hapo akaniambia: "Hapo hapo usiondoke hadi nikujie." Kisha alitembea katika giza nene hadi akapotea. Nilisikia sauti kubwa, nikahofia mtu kumtokea Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), isiwe amepatikana na jambo baya. Nilitaka kumuendea nikakumbuka kauli yake: "Usiondoke hadi nikujie." Sikuondoka mpaka aliporudi, nikasema: "Nilisikia sauti kubwa sana nikaihofia, nikamkumbusha." Akasema: "Uliisikia?" Nikasema: "Ndio." Akasema: "Huyu alikuwa ni Jibriyl alinijia, akaniambia: 'Atakayekufa katika Ummah wako hamshirikishi Allaah na chochote ataingia Peponi." Nikauliza: "Hata akizini na kuiba?" Akasema: "Hata kama atazini na ataiba." [Al-Bukhaariy na Muslim, na hii ni lafdhi ya Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 10

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لَوْ كَانَ لِي مِثْلُ أُحُدٍ ذَهَباً ، لَسَرَّنِي أنْ لاَ تَمُرَّ عَلَيَّ ثَلاَثُ لَيالٍ وَعِنْدِي مِنْهُ شَيْءٌ إِلاَّ شَيْءٌ أرْصُدُهُ لِدَيْنٍ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Lau ningekuwa na dhahabu mfano wa Mlima Uhud, ingenifurahisha kutopita siku tatu nami nimebakia na chochote isipokuwa kitu nakiweka kwa ajili ya kulipa madeni." [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 11

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( انْظُرُوا إِلَى مَنْ هُوَ أسْفَلَ مِنْكُمْ وَلاَ تَنْظُرُوا إِلَى مَنْ هُوَ فَوْقَكُمْ ؛ فَهُوَ أجْدَرُ أنْ لاَ تَزْدَرُوا نِعْمَةَ الله عَلَيْكُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ ، وهذا لفظ مسلم .

وفي رواية البخاري : (( إِذَا نَظَرَ أَحَدُكُمْ إِلَى مَنْ فُضِّلَ عَلَيْهِ في المَالِ وَالخَلْقِ ، فَلْيَنْظُرْ إِلَى مَنْ هُوَ أسْفَل مِنْهُ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwangalie wa chini yako, wala usiangalie wa juu yako, hilo ni hakika hutopuuza neema za Allaah juu yako." [Al-Bukhaariy na Muslim, na hii ni lafdhi ya Muslim]

Na katika riwaayah ya Al-Bukhaariy: "Anapoangalia mmoja wenu aliyefadhilishwa juu yake kwa mali na sura nzuri, basi amtizame aliye chini yake."





Hadiyth – 12

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( تَعِسَ عَبْدُ الدِّينَارِ ، وَالدِّرْهَمِ ، وَالقَطِيفَةِ ، وَالخَمِيصَةِ ، إنْ أُعْطِيَ رَضِيَ ، وَإنْ لَمْ يُعْطَ لَمْ يَرْضَ )) رواه البخاري .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ameangamia mwenye kutafuta dinari na dirhamu na nguo zenye manyoa na mavazi ya thamani. Wanapopatiwa huridhia na wasipopatiwa basi hawaridhiki." [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 13

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : لَقَدْ رَأيْتُ سَبعِينَ مِنْ أهْلِ الصُّفَّةِ ، مَا منهُمْ رَجُلٌ عَلَيْهِ رِدَاءٌ : إمَّا إزارٌ ، وَإمَّا كِسَاءٌ ، قَدْ رَبَطُوا في أعنَاقِهِمْ ، فَمِنْهَا مَا يَبْلُغُ نِصْفَ السَّاقَيْن ، وَمِنْهَا مَا يَبْلُغُ الكَعْبَيْنِ ، فَيَجْمَعُهُ بِيَدِهِ كَراهِيَةَ أنْ تُرَى عَوْرَتُهُ . رواه البخاري .

Na imepokewa kutoka kwake Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: "Hakika nimeona Swahaaba sabiini katika watu wa Swuffah hakuna hata mmoja miongoni mwao mwenye kikoi: Ima ni shuka wamezifunga katika shingo zao, katika hizo kuna zinazofika katikati ya miguu, katika hizo kuna zinazofika kongo mbili, kwa hiyo wakazikusanya kiunoni kwa kuchukia kuonekana uchi wao." [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 14

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( الدُّنْيَا سِجْنُ الْمُؤْمِنِ ، وَجَنَّةُ الكَافِرِ )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: "Dunia ni jela ya Muumini na Pepo ya kafiri." [Muslim]





Hadiyth – 15

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : أخذ رسول الله صلى الله عليه وسلم بِمَنْكِبَيَّ ، فقال : (( كُنْ في الدُّنْيَا كَأنَّكَ غَرِيبٌ ، أَو عَابِرُ سَبيلٍ )) .

وَكَانَ ابن عُمَرَ رضي الله عنهما ، يقول : إِذَا أمْسَيتَ فَلاَ تَنْتَظِرِ الصَّبَاحَ ، وَإِذَا أَصْبَحْتَ فَلاَ تَنْتَظِرِ المَسَاءَ ، وَخُذْ مِنْ صِحَّتِكَ لِمَرَضِكَ ، وَمِنْ حَيَاتِكَ لِمَوْتِكَ . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) akisema kwamba: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alishika mabega yangu akisema: 'Kuwa duniani kama kwamba wewe ni mgeni au mpita njia.' Na Ibn 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) alikuwa akisema: 'Na ufikiwapo na usiku usitaraji kuwa uatafika hadi asubuhi, na ukipambazukiwa usitaraji kuwa utafika hadi jioni. Na faidika na (wakati wa) siha yako kabla ya (wakati wa) uhai wako kabla ya kufa kwako." [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 16

وعن أَبي العباس سهل بن سعد الساعدي رضي الله عنه ، قَالَ : جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النبي صلى الله عليه وسلم ، فقال : يَا رسولَ الله ، دُلَّنِي عَلَى عَمَلٍ إِذَا عَمِلْتُهُ أحَبَّنِي اللهُ وَأحَبَّنِي النَّاسُ ، فقال : (( ازْهَدْ في الدُّنْيَا يُحِبّك اللهُ ، وَازْهَدْ فِيمَا عِنْدَ النَّاسِ يُحِبّك النَّاسُ )) حديث حسن رواه ابن ماجه وغيره بأسانيد حسنة .

Imepokewa kutoka kwa Abui 'Abbaas Sahl bin Sa'd As-Sa'idiy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa: Alikuja mtu kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Ee Rasuli wa Allaah, nijulishe mimi amali ambayo nikiifanya Allaah atanipenda na watu watanipenda." Akasema: "Upe nyongo ulimwengu atakupenda Allaah, na vipe nyongo viliomo mikononi mwa watu watakupenda watu." Hadiyth Hasan [Ibn Maajah na wengineo kwa isnad nzuri]





Hadiyth – 17

وعن النعمان بن بشير رضي الله عنهما ، قَالَ : ذَكَرَ عُمَرُ بْنُ الخَطَّابِ رضي الله عنه ، مَا أَصَابَ النَّاسُ مِنَ الدُّنْيَا ، فَقَالَ : لَقَدْ رَأيْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم يَظَلُّ الْيَوْمَ يَلْتَوِي مَا يَجِدُ مِنَ الدَّقَلِ مَا يَمْلأ بِهِ بَطْنَهُ . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa An-Nu'maan bin Bashiyr (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) ambaye amesema: Alitaja 'Umar bin Al-Khattaab (Radhwiyah Allaahu 'anhu) yale yaliyowafikia watu katika hii dunia, akasema: "Hakika nilimuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akipitisha siku zake akiwa na njaa hana hata tende mbaya ya kuondoa njaa yake." [Muslim]





Hadiyth – 18

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : تُوفي رسول الله صلى الله عليه وسلم، وَمَا في بَيْتِي مِنْ شَيْءٍ يَأكُلُهُ ذُو كَبِدٍ إِلاَّ شَطْرُ شَعِيرٍ في رَفٍّ لي ، فَأكَلْتُ مِنْهُ حَتَّى طَالَ عَلَيَّ ، فَكِلْتُهُ فَفَنِيَ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiyah Allaahu 'anhaa) amesema: "Aliaga dunia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na hakukuwa katika nyumba chakula cha sawa (kwa watu kula) isipokuwa mtama kidogo katika stoo yangu ambao nilikuwa nikiutumia kwa muda. Baadae nilitaka kuupima lakini ukawa umemalizika." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 19

وعن عمرو بن الحارث أخي جُوَيْرِيّة بنتِ الحارِث أُمِّ المُؤْمِنِينَ ، رضي الله عنهما ، قَالَ : مَا تَرَكَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم عِنْدَ مَوْتِهِ دِيناراً ، وَلاَ دِرْهَماً ، وَلاَ عَبْداً ، وَلاَ أَمَةً ، وَلاَ شَيْئاً إِلاَّ بَغْلَتَهُ الْبَيضَاءَ الَّتي كَانَ يَرْكَبُهَا ، وَسِلاَحَهُ ، وَأرْضاً جَعَلَهَا لاِبْنِ السَّبِيلِ صَدَقَةً . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa 'Amri bin Al-Haarith, kakake Juwayriyyah bint Al-Haarith, Mama wa Waumini ambaye amesema: "Hakuacha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakati wa kufariki hata dinari moja wala dirhamu wala mjakazi wala kijakazi wala kitu kingine chochote isipokuwa nyumbu wake mweupe aliyekuwa akipanda na silaha zake na ardhi aliyoiacha kama swadaqah kwa wasafiri." [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 20

وعن خَبابِ بن الأَرَتِّ رضي الله عنه، قَالَ : هَاجَرْنَا مَعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم نَلْتَمِسُ وَجْهَ اللهِ تَعَالَى ، فَوَقَعَ أجْرُنَا عَلَى اللهِ ، فَمِنَّا مَنْ مَاتَ وَلَمْ يَأكُل منْ أجْرِهِ شَيْئاً ، مِنْهُمْ : مُصْعَبُ بن عُمَيْرٍ رضي الله عنه ، قُتِلَ يَوْمَ أُحُد ، وَتَرَكَ نَمِرَةً ، فَكُنَّا إِذَا غَطَّيْنَا بِهَا رَأْسَهُ ، بَدَتْ رِجْلاَهُ ، وَإِذَا غَطَّيْنَا بِهَا رِجْلَيْهِ ، بَدَا رَأسُهُ ، فَأمَرَنَا رسول الله صلى الله عليه وسلم ، أنْ نُغَطِّي رَأسَهُ ، وَنَجْعَل عَلَى رِجْلَيْهِ شَيْئاً مِنَ الإذْخِرِ ، وَمِنَّا مَنْ أيْنَعَتْ لَهُ ثَمَرَتُهُ ، فَهُوَ يَهْدِبُهَا . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Khabbaab bin Al-Aratt (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa amesema: "Tulihama pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ajili ya radhi za Allaah Ta'aalaa, ujira wetu ukatoka kwa Allaah, Miongoni mwetu kuna waliokufa kabla ya kula ujira wao, Miongoni mwao ni Mus'ab bin 'Umayr (Radhwiyah Allaah 'anhu) ameuwawa siku ya Uhud, ameacha shuka tukimfunika nayo uso wake miguu yake inakuwa wazi, na tulipomfunika miguu, uso wake umakuwa wazi. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alituamuru tumfunike uso wake na kumfunika miguu yake na Idhkhir (aina ya mmea ambao ni maarufu na wenye harufu nzuri). Na miongoni mwetu kuna waliopata neema kwa wingi (hapa duniani) nao wakafurahia hilo." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 21

وعن سهلِ بن سعد الساعدي رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( لَوْ كَانَت الدُّنْيَا تَعْدِلُ عِنْدَ الله جَنَاحَ بَعُوضَةٍ ، مَا سَقَى كَافِراً مِنْهَا شَرْبَةَ مَاءٍ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Sahl bin Sa'ad As-Saa'idiy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Lau kama uliwengu ungekuwa na thamani sawa na bawa la mbu mbele ya Allaah, hangempatia kafiri maji ya kunywa hata kiasi cha mkono mmoja." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]





Hadiyth – 22

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( أَلاَ إنَّ الدُّنْيَا مَلْعُونَةٌ ، مَلْعُونٌ مَا فِيهَا ، إِلاَّ ذِكْرَ اللهِ تَعَالَى ، وَمَا وَالاهُ ، وَعالِماً وَمُتَعَلِّماً )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسنٌ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Jueni ya kuwa hii dunia imelaaniwa, na vimelaaniwa vilivyo ndani yake ispokuwa kumtaja Allaah Ta'aalaa na vile Anavyovipenda na wanavyuoni na wanafunzi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hasan]





Hadiyth – 23

وعن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( لاَ تَتَّخِذُوا الضَّيْعَةَ فَتَرْغَبُوا في الدُّنْيَا )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديثٌ حسنٌ )) .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uud (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Msiwe ni wenye kupapia raslimali (zisizohamishika) na hivyo kupendelea dunia." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hasan]





Hadiyth – 24

وعن عبدِ الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قَالَ : مَرَّ عَلَيْنَا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم وَنَحْنُ نعالِجُ خُصّاً لَنَا ، فَقَالَ : (( مَا هَذَا ؟ )) فَقُلْنَا : قَدْ وَهَى ، فَنَحَنُ نُصْلِحُهُ ، فَقَالَ : (( مَا أرَى الأَمْرَ إِلاَّ أعْجَلَ مِنْ ذَلِكَ )) . رواه أَبو داود والترمذي بإسناد البخاري ومسلم ، وقال الترمذي : (( حديثٌ حسنٌ صحيحٌ )) .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amru bin Al-'Aas kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipita tukiwa tunatengeneza paa (la nyumba ya mbao), akasema: "Munafanya nini?" Tukasema: "Paa limekuwa dhaifu nasi tunalitengeneza." Akasema: " Ninaona amri hiyo (Siku ya Qiyaamah) inafika kwa haraka zaidi kuliko jambo lenu hili." [Abu Dawuud na At-Tirmidhiy kwa Isnaad ya Al-Bukhaariy na Muslim, na akasema At-Tirmidhiy kuwa hii ni Hadiyth Hassan Swahiyh]







Hadiyth – 25

وعن كعب بن عياض رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( إنَّ لِكُلِّ أُمَّةٍ فِتْنَةً ، وفِتْنَةُ أُمَّتِي : المَالُ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديثٌ حسنٌ صحيحٌ )) .

Na imepokewa kutoka kwa Ka'b bin 'Iyaadh (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika kila Ummah una fitnah (mtihani) na fitnah ya Ummah wangu ni mali." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]





Hadiyth – 26

وعن أَبي عمرو ، ويقالُ : أَبو عبدِ الله ، ويقالُ : أَبو ليلى عثمان بن عفان رضي الله عنه : أنَّ النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لَيْسَ لاِبْنِ آدَمَ حَقٌّ في سِوَى هذِهِ الخِصَالِ : بَيْتٌ يَسْكُنُهُ ، وَثَوْبٌ يُوارِي عَوْرَتَهُ ، وَجِلْفُ الخُبز وَالماء )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu 'Amri (Radhwiyah Allaahu 'anhu), Inasemwa ni Abu 'Abdillaah, na inasemwa Abu Laylaa 'Uthmaan bin 'Affaan kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwanadamu hana haki ya kuwa na zaidi ya vitu aina tatu: nyumba atakayoishi, na mavazi ya kusitiri uchi wake na kipande cha mkate na maji." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Swahiyh]





Hadiyth – 27

وعن عبدِ الله بن الشِّخِّيرِ - بكسر الشينِ والخاء المعجمتين - رضي الله عنه، أنه قَالَ : أتَيْتُ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، وَهُوَ يَقْرَأُ : ( أَلْهَاكُمُ التَّكَاثُرُ ) قَالَ : (( يَقُولُ ابْنُ آدَمَ : مَالِي ، مالي ، وَهَلْ لَكَ يَا ابْنَ آدَمَ مِنْ مَالِكَ إِلاَّ مَا أكَلْتَ فَأفْنَيْتَ ، أَو لَبِسْتَ فَأَبْلَيْتَ ، أَوْ تَصَدَّقْتَ فَأَمْضَيْتَ ؟! )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin Ash-Shikhiyr (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Nilikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa anasoma: "Al-Haakumut Takaathur." Akasema: "Mwanadamu anasema: Mali yangu, mali yangu. Kwani wewe mwanadamu una mali isipokuwa kile ulichokula kikapotea au ulichovaa kikamalizika au ukatoa swadaqah na ukatanguliza mbele yako?" [Muslim]





Hadiyth – 28

وعن عبدِ الله بن مُغَفَّل رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رجل للنبي صلى الله عليه وسلم :
يَا رسولَ الله ، وَاللهِ إنِّي لأُحِبُّكَ ، فَقَالَ : (( انْظُرْ مَاذَا تَقُولُ ؟ )) قَالَ : وَاللهِ إنِّي لأُحِبُّكَ ، ثَلاَثَ مَرَّات ، فَقَالَ : (( إنْ كُنْتَ تُحِبُّنِي فَأَعِدَّ لِلْفَقْرِ تِجْفَافاً ، فإنَّ الفَقْرَ أسْرَعُ إِلَى مَنْ يُحِبُّني مِنَ السَّيْلِ إِلَى مُنْتَهَاهُ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Na imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin Mughaffal (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: Mtu alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ee Rasuli wa Allaah! Wa-Allaahi mimi nakupenda." Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Angalia usemalo." Akasema: "Wa-Allaahi mimi nakupenda." Mara tatu. Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ikiwa unanipenda jitayarishe kwa ufukara, kwani ufukara ni haraka zaidi kwa menye kunipenda, kuliko mafuriko na mwisho wake." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]





Hadiyth – 29

وعن كعب بن مالك رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَا ذِئْبَانِ جَائِعَانِ أُرْسِلا في غَنَمٍ بِأفْسَدَ لَهَا مِنْ حِرْصِ المَرْءِ عَلَى المَالِ وَالشَّرَفِ لِدِينهِ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Ka'abbin Maalik (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mbwa mwitu wawili wenye njaa watakao pelekwa kwenye mkao (kundi) kwa kondoo hawatatia hasara zaidi kuliko pupa ya mtu kwa mali na utukufu kwa Dini yake." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]





Hadiyth – 30

وعن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه، قَالَ : نَامَ رسول الله صلى الله عليه وسلم عَلَى حَصيرٍ ، فَقَامَ وَقَدْ أثَّرَ في جَنْبِهِ ، قُلْنَا : يَا رَسُولَ اللهِ ، لَوْ اتَّخَذْنَا لَكَ وِطَاءً . فَقَالَ : (( مَا لِي وَلِلدُّنْيَا ؟ مَا أَنَا في الدُّنْيَا إِلاَّ كَرَاكِبٍ اسْتَظَلَّ تَحْتَ شَجَرَةٍ ثُمَّ رَاحَ وَتَرَكَهَا )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uud (Radhwiyah Allaah 'anhu) kuwa Rasuli wa sallam (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alilala mara moja juu ya majani ya mtende na alipoamka alama za majani hayo yalikuwa yanaonekana kwenye mwili wake. Tukamwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Je, tukutayarishie godoro laini kwa ajili yako?" Akasema: "Sina haja na mambo ya dunia. Mfano wangu hapa duniani ni kama mpandaji anapumzika chini ya kivuli cha mti, kisha akaanza tena safari na kuuacha mti." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]





Hadiyth – 31

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( يدْخُلُ الفُقَرَاءُ الْجَنَّةَ قَبْلَ الأَغْنِيَاءِ بِخَمْسِمئَةِ عَامٍ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mafakiri wataingia Peponi miaka mia tano kabla ya matajiri." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Swahiyh]





Hadiyth – 32

وعن ابن عباس وعِمْرَانَ بن الحُصَيْنِ رضي الله عنهما ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ: (( اطَّلَعْتُ في الجَنَّةِ فَرَأيْتُ أكْثَرَ أهْلِهَا الفُقَرَاءَ ، وَاطَّلَعْتُ في النَّارِ فَرَأيْتُ أكْثَرَ أهْلِهَا النِّسَاءَ )) متفقٌ عَلَيْهِ من رواية ابن عباس ، ورواه البخاري أيضاً من رواية عِمْرَان بن الحُصَيْن .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas na 'Imraan Ibn Al-Huswayn (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nilichungulia Peponi nikaona watu wake wengi ni mafakiri. Na nikatizama Motoni nikaona watu wake wengi ni wanawake." [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]







Hadiyth – 33

وعن أسامة بن زيد رضي الله عنه ، عن النبي صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( قُمْتُ عَلَى بَابِ الجَنَّةِ ، فَكَانَ عَامَّةُ مَنْ دَخَلَهَا المَسَاكِينُ ، وَأصْحَابُ الجَدِّ مَحبُوسُونَ ، غَيْرَ أنَّ أصْحَابِ النَّارِ قَدْ أُمِرَ بِهِم إِلَى النَّارِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Usaamah bin Zayd (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nilisimama kwenye mlango wa Pepo, ikawa wengi wanaoingia ni masikini, na wenye utajiri wamezuiwa, isipokuwa watu wa Motoni wameamriwa kuingizwa motoni." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 34

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( أصْدَقُ كَلِمَةٍ قَالَهَا شَاعِرٌ كَلِمَةُ لَبِيدٍ : ألاَ كُلُّ شَيْءٍ مَا خَلاَ اللهَ بَاطِلُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Neno la kweli alilosema mshairi ni neno la Labiyd: "Tanabahi kwamba kila kitu mbali na Allaah ni batili." [Al-Bukhaariy na Muslim]
 
Baadhi ya post za zamani....

MAISHA YA NDOA YA BINTI WA MTUME


Mtume rehma na amani ziwe juu yake alikuwa na mabinti wanne ambao ni Zainab, Ummu kuluthum, Ruqaiya na Faatwimatu (Fatuma) . Wote waliolewa, isipokuwa hao watatu yaani Zainab, Ummu Kuluthum na Ruqaiya walifariki kabla ya mtume.

Fatuma Peke yake alifariki baada ya Mtume (s.a.w) miezi sita baada ya Mtume kufariki naye ndio akafuata.

Kwahiyo hapa binti ambaye tunaangalia maisha yake ya ndoa ni Fatuma.

MAISHA YA NDOA

kuoa ni mfungamano wenye nguvu unaowakusanya mwanaume na mwanamke katika kivuli cha maisha ya ndoa kisheria. Mtume rehma na amani ziwe juu yake amesema "kuoa ni sunna yangu na asiyetumia sunna yangu huyo hana shirika nami (yani hajashirikiana na mtume kwa jambo lolote).

Allah anasema Katika Quran 30:21

"Na katika ishara zake za kuonyesha ihsani zake juu yenu ni kuwa amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mpate utulivu Kwao. Na amejaalia mapenzi na huruma baina yenu, bilashaka katika haya zimo ishara kwa wanao fikiri "

Kwahiyo kwa maana hiyo kuoa ni njia ya uchamungu na usafi na ni hifadhi ya afya na ni hifadhi ya tabia njema katika jamii, na ni kinga ya shari na magonjwa.

KUPEWA HABARI YA UCHUMBA

sheria ya kiislamu haikumnyima mwanamke rai yake ya kumchagua mchumba anaye mtaka, mwanamke amepewa haki ya kufanya hivyo na si kuchaguliwa mchumba na watu wengine bali yeye mwenyewe atafanya uamuzi wake.

Kipindi cha Mtume rehma na amani ziwe juu yake, alijiwa na binti mmoja bikra, akilalamika kuwa baba yake amemuoza kwa mwanaume ambaye yeye anamchukia kwa maana nyingine hamtaki huyo mumewe. Basi Mtume akampa uhuru wa kuchagua ama aondoke au abakie katika ndoa yake.

Na mfano mzuri wa uhuru wa mwanamke kuchagua tunauona kwa Bi khadija alipomchagua Mtume pamoja na kwamba walikuwepo watu wenye fedha na wafanyabiashara na wenye vyeo katika jamii ya makuraishi lkn aliamua kumchagua Mtume (s. a. w).

Je bibi Fatuma katika Uchumba wake na Sayidina Ally ilikuwaje?


Ifahamike hawa wawili waliishi nyumba moja, ulipo fika wakati wa kuolewa bibi Fatuma,baada ya sayidina Ally kuomba posa kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake. Mtume aliingia chumbani kwa bibi Fatuma akamwambia "Ewe binti yangu hakika mtoto wa baba yako mdogo Ally amekuchumbia sasa unasemaje?

Bibi Fatuma akalia kisha akasema "Ni kama kwamba ewe baba yangu umeniweka akiba kwa malofa wa kikuraishi" Mtume akamwambia binti yake kuwa "Namuapa Allah aliyenituma kudhihirisha haki sikuzungumza chochote katika habar hii, mpaka alipo nipa idhini Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni juu jambo hili " Bibi Fatuma akasema kuwa "Nimeridhika na yale aliyoyaridhia kwangu Mwenyezi Mungu
na Mtume (s. a. w).

Kwahiyo hapa tunaona bibi Fatuma katendewa haki ya kusikilizwa rai yake na uamuzi wake. Na kigezo alichotumia Mtume kuchagua mchumba sio mali wala hadhi au cheo cha mtu bali aliangalia dini na tabia njema. Na mwanamke vile vile anatakiwa amchague mtu mwenye dini na tabia njema.


KUMTAZAMA MCHUMBA

Swala la kumtazama mchumba katika uislamu limeruhusiwa ila sharti lazima awepo ndugu wa karibu wa huyo mchumba, hakuna kizuizi cha kukaa nae na kuzungumza nae iwapo atakuwepo maharimu wake,yaani ndugu yake, kaka au mwingine katika familia.

Mtume rehma na amani ziwe juu yake alimwambia Mughira wakati alipokuwa amemchumbia mwanamke, je umemtazama? Mughira akasema hapana. Mtume akasema nenda na umtazame hakika kumtazama kutapelekea kukubaliana na kutengemaa maisha ya ndoa. Hapo mwenye kuchumbia atajua mchumba wake yukoje, kiakili na mtazamo wake kimaisha, si uzuri wa mwili tu bali uzuri wa fikra na ukunjufu wa moyo.

BIBI FATUMA NA SAYYIDINA ALLY WACHUNGUZANA

Sayyidina Ally alipofikia umri wa miaka ishirini na moja alikuwa hajaoa. Naye bibi Fatuma alikuwa amefikia umri wa miaka kumi na nane. Siku moja bibi Fatuma alimuambia Sayyidina Ally kuwa mimi nakushinda mimi ni mkubwa kuliko wewe. Wakati huo huo alifika Sayyidina Abbas akasema "ewe fatuma hakika umezaliwa wakati maquraishi wanajenga kaaba na Mtume akiwa na umri wa miaka 35 ama wewe Ally ulizaliwa kabla ya hapo kwa miaka mingi.

Lakini yote hayo yanaonyesha jinsi walivyotaka kufahamiana vizur kabla ya kuoana. Hivyo usikubali kuoa au kuolewa bila kujua unaolewa na nani.


MAHARI YA FATUMA

Sheria ya kiislamu haikuweka mipaka juu ya mahari ambayo anatoa mume kumpa mkewe. Bali sheria imeliacha jambo hilo kuwa ni maridhiano ya pande mbili.

Mtume rehma na amani ziwe juu yake amesema "hakika wanawake wenye baraka zaidi ni wale wenye mahari nyepesi "

Basi wakati sayyidina Ally alipotaka kumuoa bibi Fatuma, Mtume alimuuliza sayyidina Ally, je una chochote cha kutoa ambacho kitakua ndiyo uhalali wako wa kumuoa Fatuma? Ally akasema hapana. Mtume akamkumbusha vazi la kivita alilompa zawadi ambalo thamani yake haizidi dirhamu nne. Ally akasema lipo , Mtume akasema basi Fatuma iwe ndiyo mahari yake.

NASAHA KWA MAWALII NA WENYE KUOA

Mtume rehma na amani ziwe juu yake ni kiigizo chema kwa wazazi na wenye kuoa katika jambo hili la mahari. Sayyidina Umar al Faaaruq anasema "eleweni kama jambo la kuzidisha mahari lingekuwa ni jambo la kuheshimika katika dunia au la uchamungu mbele ya Allah, mbora wenu juu ya hilo angekuwa nabii Muhammad, hakutoa mahari kumpa mwanamke katika wake zake, wala hakupewa mahari mwanamke katika binti zake zaidi ya waqia kumi na mbili. Hivyo eleweni kwamba mahari sio thamani ya mwanamke mpaka iwe sababu ya wazazi kufanya ghali"

Uislamu umefanya njia kuwa nyepesi, na Mtume kaonyesha njia kwa maneno na vitendo.

Hali ilivyo hivi sasa wazazi wengi wameshikamana na desturi za kijahili na mila zilizo mbali na uislamu, wanazidisha mahari na kukataa kuwaoza mabinti zao mpaka mume atoe maelfu ya fedha. Wamegeuza kana kwamba mwanamke ni bidhaa inayouzwa na kufanyiwa biashara. Kutokana na hayo wanawake wanakuwa hawaolewi na hivyo kufanya mambo machafu kwasababu vijana wanashindwa kuoa na wanabaki kufanya zinaa.

NDOA YA BIBI FATUMA

Baada ya masuala ya uchumba kukamilika na mahari kulipwa, kilicho fuata ilikuwa ni ndoa. Mwaka wa pili baada ya Mtume rehma na amani ziwe juu yake kuhamia madina, na baada ya Mtume kurejea kutoka katika Vita vya badri, ilifanyika ndoa ya bibi Fatuma na sayyidina Ally.

Baada ya ndoa kufungwa, ukoo wa mutwalibu walifurahi upeo wa kufurahi, wakalisha watu Chakula cha harusi (walimatul-ars). Sayyidina Hamza akachinja baadhi ya ngamia wake na Saad r. a akachinja kondoo wake, na masahaba wa kiansar wakaleta vibaba vya mahindi wakawalisha watu. Kisha baada ya sherehe watu wakaondoka hali ni wenye furaha.

Hapa tunajifunza kuwa kusaidiana katika sherehe kama hii ya ndoa ni jambo zuri, utaona ni namna gani walichangia masahaba, mitwalib na wengineo kuhakikisha harusi ya binti wa Mtume inakuwa ya kupendeza.


MTUME AWAOMBEA DUA FATUMA NA ALLY

bibi Fatuma alipokwenda nyumbani kwa Ally r. a hakukuta nyumbani isipokuwa changarawe zilizotandikwa na mto wa ngozi uliojazwa majani, pamoja na glass moja na jagi moja.

Mtume rehma na amani ziwe juu yake akaomba apewe chombo chenye Maji, akaomba yale aliyokadiriwa kusema, akatemea mate ndani ya Maji hayo kisha akampaka Ally kifuani mwake na usoni mwake. Kisha akamwita Bibi Fatuma akamnyunyuzia maji yale na akamuombea kiasi alichojaliwa. Dua aliyowaombea ni hii :

"ewe Mwenyezi Mungu wabarikie ndani yao na nje yao na uwabarikie kizazi chao"

MATUMIZI KATIKA NDOA

mwanamke anatakiwa apate matumizi yake kutokana na uwezo na ni juu ya mwanaume kuishi na mkewe kutokana na uwezo wake. Ajiepushe na kila chenye kuharibu maisha ya mkewe. Na ni juu yake kumletea chakula anachokihitaji, na amuondolee taabu ya kwenda huku na huko nje ya nyumba yake, ili aweze kutekeleza wajibu wake kwa namna iliyo nzuri. Basi matumizi ya mume kwa mkewe yasiwe ya fujo wala kwa ubakhili.

Anasema Allah:

"Mwenye wasaa agharimu kadri ya wasaa wake na yule ambaye amepungukiwa riziki yake, atoe katika alichojaaliwa na Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu yoyote kwa kadri ya alichompa, atajaalia Mwenyezi Mungu baada ya dhiki faraja"

Na amesema Mtume:

"Mwogopeni Allah muwatendee wema wanawake, hakika nyie mmewachukua kwa amana ya Mwenyezi Mungu na mmehalalishiwa tupu zao kwa maneno ya Allah, basi wanayo haki kwenu kuwalisha na kuwavika kwa wema"

Huu ndio uislamu. Tugeuke nyumbani kwa Sayyidina Ally hali ilikuwaje?

Kama tulivyoona huko nyuma hali ya sayidina Ally kiuchumi haikuwa nzuri, wanandoa hawa waliishi maisha magumu na ya dhiki, siku ile ya kwanza hapakuwa na kitanda cha sita kwa sita wala tandiko la sita kwa sita tofauti na tulivyozoea sisi,lakini bibi Fatuma hakuona tabu.

Kitanda alicholalia ilikuwa ni ngozi ya kondoo na mto ni ngozi ambayo imejazwa majani,shuka la kujifunika ni dogo haliwatoshi. Wakijifunika juu kichwa miguu inabaki wazi na wakijifunika miguu vichwa vinabaki wazi, je wewe binti wa leo ungeweza kuvumilia maisha haya?

BIBI FATUMA AOMBA MSAADA KWA BABA YAKE

kama tulivyoona maisha sayyidina Ally hayakuwa mazuri kiuchumi hivyo alishindwa kumuajiri mfanyakazi wa kumsaidia mkewe shughuli mbali mbali kama kuchota maji, kutwanga, kupika mikate na mengineyo. Mume huyu alipata sana tabu kuona mkewe kipenzi anachoshwa na kazi za nyumbani,akadhoofika na kukonda kwa mawazo. Lakini hana namna ya kuiondoa hali hiyo ili apate kumfariji mkewe kwa kumletea mtumishi.

Basi akamgeukia mkewe Fatuma akamwambia " nimebeba maji ya kuwanywesha ngamia toka kisimani ewe Fatuma mpaka kifua kinauma, na Kwa hakika Allah amemletea baba yako (mtume s. a. w) mateka, basi nenda umuombe akupe mtumishi "

Bibi Fatuma naye akasema "na mimi namuapa Allah nimetwanga mpaka mikono yangu imevimba na inalengalenga damu "

Basi Fatuma alipoenda kwa baba yake aliona haya kusema shida, kisha akarudi, mumewe akamuuliza vipi imekuwaje? Akajibu nimeona haya kumuomba.

Basi Ally Akamwambi mkewe basi twende wote kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake, walipofika na baada ya kusalimia, bwana Ally alisema

"Ewe Mtume wa Allah, namuapa Allah nimechota maji ya kuwanywesha ngamia mpaka kifua kinauma " Bibi Fatuma naye akasema "Nimetwanga mpaka mikono imevimba na kulengalenga damu, na kwa hakika Allah amewaleta mateka kwako na wepesi basi tupe mtumishi "

Mtume rehma na amani ziwe juu yake akasema

"Namuapa Allah sitakupeni mtumishi halafu niwaache masufi wakifunga matumbo yao kwa njaa kwani sina cha kuwalisha, nitawauza hao mateka kisha niwalishe hao masufi kutokana na thamani ya hao mateka. "

Basi sayidina Ally na mkewe wakarudi bure nyumbani,mpaka hapa tunapata mafunzo mengi, kwanza mke na mume wanatakiwa kusaidiana katika maisha pale inapobidi, kama dereva na utingo pale gari linapo kwama husaidiana kulisukuma ili safari iendelee.

Pia kushauriana ili kupata mbinu mbadala ,kama kwa wazazi wa mmoja wao kuna hali nzuri, basi si vibaya kuomba msaada, na ni juu ya wazazi kuwasaidia watoto wao ili wajikwamue kimaisha.

Tatu kama hali inaruhusu mume amtafutie mke Mtumishi ili aweze kutimiza majukumu yake mengine barabara. Mwisho akija kwa wazazi, kwanza aulizwe kilichomleta kisha ndio afanyiwe mambo mengine.


MTUME AWAELEKEZA NJIA BORA ZAIDI YA KUFANYA BADALA YA MTUMISHI

Mtume rehma na amani ziwe juu yake hakuwaacha hivi hivi baada ya kuwaambia kuwa mateka wale atawatumia kwa kuwasaidia masufi, alitafuta njia mbadala. Alikwenda nyumbani kwao na akakuta kweli wana hali mbaya, shuka wajifunikayo haiwatoshi, ukifunika kichwa miguu inabaki wazi na ukifunika miguu basi kichwa kinabaki wazi.

Akawaambia "Tulieni hapo, je nikupeni habari iliyo bora kuliko mtumishi mliyemuomba?" wakasema ndio ewe Mtume wa Allah. Mtume rehma na amani ziwe juu yake akasema: Ni maneno aliyonifundisha Jibril (huyu ni yule malaika mkuu ambaye hushusha ufunuo kwa manabii na mitume)
Semeni subhanallah mara kumi kila baada ya swala, alhamdulillah mara kumi na allahu Akbaru mara kumi, na mtakapotaka kulala semeni subhanallah mara 33,alhamdulillah 33 na Allahu Akbaru mara 34.

Sayyidina Ally r. a anasema kulwa, namuapa Allah sikuacha kuyatumia maneno hayo aliyonifundisha Mtume. Hapa tunajifunza kuwa wazazi wajitahidi kwa kila namna iwezekanavyo kuwasaidia watoto wao waliomo katika ndoa. Mfano kama Baba wa binti ana uwezo asione vibaya kumsaidia mkwe wake, kwani kumsaidia mkwewe ni kumsaidia binti yake.


KUISHI NA MUME KWA WEMA

Msingi wa maisha ya ndoa ni upole na uvumilivu na kuyafumbia macho matatizo madogo madogo ambayo yanatokea kwa mmoja wa wanandoa kuteleza. Na katika mambo yanayo dhihirisha wanandoa kuishi kwa wema ni mume kuingiza furaha kwa mkewe na hivyo hivyo mke kwa mumewe. Mume aheshimu utu wa mkewe na awe awe mkunjufu wa Sura usoni kwa mkewe (aonyeshe tabasamu). Wakeze Mtume rehma na amani iwe juu yake walikuwa wakimfanyia maneno yenye kumuudhi, wanakaa mpaka usiku bila kumsemesha, lakini Mtume alivumilia kwasababu ya kuwafanyi upole na ukarimu.

Allah anasema:

"Na kaeni nao kwa wema, na kama mkiwachukia basi (msiwaache) kwani huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake "4:39

Kwa mujibu huu tunaona maisha ya bibi Fatuma na mumewe yalivyokuwa mazuri wakipendana, wakishirikiana katika taabu na raha na hivi ndivyo wanavyotakiwa kuishi wanandoa. Lakini je waliishi tu bila mikwaruzano?

UGOMVI WAZUKA BAINA YA BIBI FATUMA NA MUMEWE

Maisha yalikwenda vizuri katika nyumba hii tukufu na kuishi kwa furaha na amani, huku wakizungukwa na mapenzi na huruma. Lakini mambo hayaendi siku zote katika mpango wa namna moja.

Tabia ya Ally r. a ilikuwa ya ukali na udhibiti wa mambo, na bibi Fatuma alikuwa mwepesi, mpole anayeweza kuvumilia tabu na anayehitaji upole toka kwa mumewe.

Siku moja sayyidina Ally alidhihirisha ukali kwa mkewe, bibi Fatuma akasema "Namuapa Allah nitakushitaki kwa Mtume " Fatuma akaenda kwa Mtume na kushitaki ukali wa mumewe, huku mumewe nae alimfuata nyuma, baada ya Mtume rehma na amani ziwe juu yake kusikia mashtaka yale, akakaa kimya kitambo kidogo kisha akasema

"Ewe binti yangu, sikia na upende kusikia (ukiambiwa) hakika hawi mwanamke wa maana,mwanamke ambaye hatekelezi matakwa ya mumewe,na mume akabakia kimya (lazima acharuke).

Basi Mtume aliwasuluhisha hao wanandoa na mambo yakerejea katika hali yake ya awali.


BIBI FATUMA AJIFUNGUA WATOTO

Siku ile ya ndoa Mtume rehma na amani ziwe juu yake aliwaombea dua hii "Ewe Mwenyezi Mungu wabarikie ndani yao na nje yao na uwabarikie kizazi chao"

Basi akawarudhuku watoto wanne, wawili wa kiume na wawili wa kike, wa kwanza Hussein, wa pili Hassan, Zainab na wa mwisho ummu kulthumu.
 
Afanye Ibada Zipi Ili Aombe Kuondoa Matatizo?
Maswali: familia-Jamii


Afanye Ibada Zipi Ili Aombe Kuondoa Matatizo?



Alhidaaya.com



Swali:



Aslaam aleykum



Mimi ni kijana ambaye kwa hakika Allah [S.A] amenijali afya njema pamoja na familia yangu na namshukuru Allah [S.A] kwahilo na hakika hakuna mwanadamu ambaye hana matatizo sasa swali langu ni kwamba kuna tatizo kubwa sana linanisumbua katika maisha yangu na nimeshafanya ibada nyingi za sunna katika kuomba hili kwa Allah [S.A] kama kufunga siku saba pamoja na kuswahili swalatul hajj kwa rakaa nne na ya kwanza kusoma Suwraah Fatiha na Qulhulwahu 10 na rakaa ya pili Suwrah Fatiha na Qulhulwahu 20 na rakaa ya tatu Suwrah Fatiha na Qulhulwahu 30 na rakaa ya nne Suwrah Fatiha na Qulhulwahu 40. Je naweza kufanya kisimamo gani cha Sunna ili Allah [S.A] anajalie ninachoomba kwa wepesi na haraka zaidi



Wabillah tawfiq



Jibu:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Ulimwenguni tumeletwa na Allaah Aliyetukuka ili kujaribiwa na kupatiwa mitihani. Kila mmoja miongoni mwetu anapata mtihani aina yake ulio tofauti na mwengine. Hiyo ndio ada ya Allaah Aliyetukuka kwa viumbe vyake.



Kuondoa matatizo na kujibiwa du’aa zetu kuna masharti yake bila kuyatimiza hatutakuwa ni wenye kujibiwa. Miongoni mwa masharti ni:



1. Kula, kunywa na kuvaa vya halali.

2. Kutofanya haraka kujibiwa kama kusema nataka Ee Allaah unijibu leo leo.

3. Kufanya ‘Ibaadah inavyotakiwa.

4. Kuacha ada na desturi mbaya na maasiya.



Allaah Aliyetukuka Ameahidi kila anayemuomba Atamjibu. Hata hivyo, du’aa zetu zinajibiwa kwa njia gani? Mwanachuoni mkubwa Ibn al-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema kuwa tunajibiwa du’aa zetu kwa njia zifuatazo:



1. Kujibiwa uliloomba.

2. Kubadilishiwa jambo lenye kheri zaidi nawe.

3. Kucheleweshewa na kupatiwa Pepo Siku ya Qiyaamah.



Kisha katika kuomba huhitajiki kufunga siku saba au kuswali Swalatul Haajah na kusoma suwraah ulizoziandika. Njia hizo hazikupatikana kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye tunahitajika kumfuata.



Swalaah Ya Haja haikuthibiti usahihi wake kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na maelezo yake yanapatikana katika kiungo kifuatacho:



Je, Swalatul-Haajah Ni Sahiyh Na Ipi Duaa Yake?



Unachotakiwa kufanya ni pindi unapofunga Sunnah kama Jumatatu au Alkhamiys au siku nyeupe uwe ni mwenye kumuomba Allaah Aliyetukuka kwa utakacho. Na pia uinuke usiku kuswali Swalaah za usiku wa manane na hapo umuombe Allaah Aliyetukuka. Au uwe ni mwenye kuswali Swalaah ya Istikhaarah. Na hapo bila shaka utajibiwa kwa jinsi ambayo anataka Yeye mwenyewe Allaah Aliyetukuka.



Tafadhali bonyeza viungo vifautavyo upate maelezo zaidi:





Nisome Duaa Gani Ili Nipate Kibali Cha Kuishi Nchi Ya Kigeni?





Na Allaah Anajua zaidi
 
Afanye Nini Kwa Aliyemdhulumu? Ni Bora Kumlipa Kisasi Au Kumwachia Allaah?



Alhidaaya.com



Swali:



Swali langu ni hili, ikiwa mtu amekudhulumu kwa aina yoyote wewe haki yako nikumfanya nini au muachiye Allaah.





Jibu:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Mwanzo inahitajika ieleweke kuwa Muislamu hafai kukubali kudhulumiwa kwa njia yoyote ile na pia haifai kwake kudhulumu.



Hivyo, ikiwa mtu amekudhulumu inafaa uitafute haki yako kwa njia zote zile za kishariy'ah ili urudishiwe haki yako. Wala usichoke kufanya hivyo kwani kuachilia haki yako itamfanya mtu huyo awe na ujasiri wa kukudhulumu kwa mara nyingine tena.



Katika Hadiyth al-Qudsiy Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema: Allaah Aliyetukuka Amesema: "Enyi waja Wangu! Mimi Nimejiharamishia dhuluma juu ya Nafsi Yangu na Nikaifanya ni haramu baina yenu basi msidhulumiane" (Muslim).


Unapodhuliwa kwa namna yoyote ile Uislamu umekupatia njia tatu ya kuliendea suala hilo: Kulipiza kisasi au kumsamehe na kufanya subra au kumuachia Allaah. Hakika ni kuwa kusamehe ni bora, kwani kufanya hivyo kuna faida nyingi tunazitaja chache zifuatazo:



1- Kuwa pamoja na Allaah, na kulipwa ujira wa kusubiri.



وَإِنْ عَاقَبْتُمْ فَعَاقِبُوا بِمِثْلِ مَا عُوقِبْتُم بِهِ ۖ وَلَئِن صَبَرْتُمْ لَهُوَ خَيْرٌ لِّلصَّابِرِينَ﴿١٢٦﴾وَاصْبِرْ وَمَا صَبْرُكَ إِلَّا بِاللَّـهِ ۚ وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَلَا تَكُ فِي ضَيْقٍ مِّمَّا يَمْكُرُونَ﴿١٢٧﴾إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوا وَّالَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ﴿١٢٨﴾

Na mkilipiza, basi lipizeni kulingana na vile mlivyoadhibiwa. Na mkisubiri, basi bila shaka hivyo ni bora kwa wenye kusubiri. Na subiri (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), na haiwi subira yako isipokuwa kupitia kwa Allaah. Na wala usiwahuzunukie, na wala usiwe katika dhiki kutokana na njama wanazozifanya. Hakika Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa, na wale ambao wao ni wenye kufanya ihsaan. [An-Nahl: 126 – 128]



2- Kusamehewa madhambi ya mja



Vile vile kumsamehe aliyekudhulumu au aliyekukosea ni kupata maghfirah kutoka kwa Mola wako ambayo hakuna mmoja wetu asiyetaka kusamehewa madhambi yake. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
وَلْيَعْفُوا وَلْيَصْفَحُوا ۗ أَلَا تُحِبُّونَ أَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٢﴾

Na wasamehe na waachilie mbali. Je, hampendi Allaah Akughufurieni? Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [An-Nuwr: 22]



3- Kupandishwa daraja na kuwa miongoni mwa Muhsiniyn



Pia ni kupandishwa daraja ya kuwa Muhsiniyn kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

الَّذِينَ يُنفِقُونَ فِي السَّرَّاء وَالضَّرَّاء وَالْكَاظِمِينَالْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ وَاللّهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ

Ambao hutoa wanapokuwa na wasaa na wanapokuwa na dhiki, na wanajizuia ghadhabu, na wasamehevu kwa watu; na Allaah Huwapenda wafanyao wema. [Al-'Imraan: 133]



4- Kulipwa ujira kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَجَزَاءُ سَيِّئَةٍ سَيِّئَةٌ مِّثْلُهَا ۖ فَمَنْ عَفَا وَأَصْلَحَ فَأَجْرُهُ عَلَى اللَّـهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الظَّالِمِينَ﴿٤٠﴾

Na jazaa ya uovu ni uovu mfano wake. Lakini atakayesamehe na akasuluhisha, basi ujira wake uko kwa Allaah, hakika Yeye Hapendi madhalimu. [Ash-Shuwraa: 40]




Na Allaah Anajua zaidi
 
Ajiepushe Na Rafiki Asiyeswali Au Aendelee Kumnasihi?
Maswali: familia-Jamii


SWALI:

A.Alaykum WarahmatuAllaahi Wabarakatuh,

Namshukuru Mwenyeezi Mungu kwa kunipa uwezo wakuisoma hii website yenu na kuwaezesha nyinyi kutuelimisha sisi. Hii website yenu inatufundisha mingi sana, Alhamdullillaahi. InshaAllaah jaza yenu iko kwa Allaah (S.W). Kila nikisoma ninapata faida nyingi sana.

Swali langu hili? Nina rafiki yangu ambaye anaswali akitaka na saa ingine haswali kabisa. Mume wake haswali kabisa. Nimejaribu kumnasihi mara nyingi. Mara ingine ananisikia mara ingine hanisikii. Sasa mimi nimekuwa confused kidogo. Nifanye nini? Nijiepushe naye ama niendelee kumnasihii. Na jee kama nimejiepusha naye nitakuwa nimefanya makosa?







JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa dada yetu kwa swali lako hilo nyeti. Hakika tatizo hilo linatokana na uchaguzi mbaya wa mume kwa huyo rafiki yako wa kike. Pindi mwanamke anapokubali kuolewa na mume ambaye haswali moja kati ya mambo mawili hutokea. Ama huyo mwanamke ataweza kumgeuza mumewe awe ni wa kufanya Ibadah au atabadilishwa yeye awe asi. Mara nyingi wanawake hugeuzwa kuwa waovu na maasi kwa sababu ya kuzidiwa na waume zao na hivyo kufuata mkumbo.



Kwa hali zote kila mmoja wetu ana wajibu na jukumu la kuwalingania wenzetu kwa uwezo wetu kwa kuwa Allaah Aliyetukuka Anasema: “Allaah Haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake” (2: 286).



Mwanadamu ni dhaifu sana na hukosea kila wakati hivyo kufaa kukumbushwa. Allaah Aliyetukuka Anasema: “Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini” (51: 55).



Ushauri wetu kwako ni kuwa ni lazima uendelee kumnasihi kwani hujui ni wakati gani Allaah Aliyetukuka Atakutilia kabuli. Ni sifa ya Muislamu kuwa hafi moyo kabisa katika shughuli kama hii ya Da‘wah na nyinginezo.



Allaah Aliyetukuka Anaelezea Imani kabambe ya Nabii Ya‘quub (‘Alayhis Salaam): “Enyi wanangu! Nendeni mkamtafute Yuusuf na nduguye, wala msikate tamaa na faraji ya Allaah. Hakika hawakati tamaa na faraji ya Allaah isipokuwa watu makafiri” (12: 87).



Zidi kumlingania kwa mawaidha mazuri kisha natija ya kubadilika ipo mikononi mwa Allaah Aliyetukuka, lakini ujira wako uko pale pale. Mchapishie makala muhimu kuhusu Swalah zilioko katika kiungo kifuatacho:



Swalaah - Kuwajibika Na Fadhila Zake



Kwa sababu yake huyo rafiki yako kuendelea na maasiya mbali na kumnasihi inatakiwa umkate kidogo. Hii ni kumaanisha usiwe na urafiki naye kama zamani kwani ukiwa na urafiki wa karibu zaidi huenda akakuathiri kidogo kidogo. Hii ni kuwa ukaribu na umbali baina ya waja umewekewa mipaka na Allaah Aliyetukuka na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mja yuko katika Dini ya rafiki yake, hivyo achague mmoja wenu yule anayefanya usuhuba naye” (at-Tirmidhiy).



Kupendana na usuhuba unafaywa kwa ajili ya Allaah na kuchukiana hivyo hivyo kwa sababu Yake. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Anayependa kwa ajili ya Allaah na akachukia kwa ajili ya Allaah, na akatoa kwa ajili ya Allaah, na akazuia kwa ajili ya Allaah basi amekamilika Imani” (Abu Daawuud).

Pia miongoni mwa watu saba watakaokuwa chini ya kivuli cha Allaah Siku ya Kiyama siku ambayo hakutakuwa na kivuli ila kivuli Chake, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anasema: “… Watu wawili waliopendana kwa ajili ya Allaah wakawa pamoja kwa hilo, na wakatengana kwa hilo …” (al-Bukhaariy na Muslim).



Kwa muhtasari ni kuwa usiwe na urafiki kama zamani lakini endelea kumpatia nasaha. Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Akupatie tawfiki katika hilo.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Amekhasimikiana Na Ndugu, Naye Anakhofu Hatari Zake Na Kupata Madhara Yake Na Kukosa Fadhila Za Kupatana
Maswali: familia-Jamii


SWALI:




ASSALAMA ALAEKUM WA RAHMATU LLAHI WA BARAKATU SHEKH TUNASHUKURU SANA KWA JUHUDI ZENU MNAZO ZICHUKUA KATKA KUTUELIMISHA DINI YETU YA ISLAM MADDA MULIO ITOA HIVI KARIBUNI YA KUSULUHISHA WALIO GOMBANA MIMI BINAFSI YANGU YAMENIPATA HAYA BAADA YA KUDAI HAKI YANGU BAADA YA BABA YETU MUNGU AMREHEMU WALINIFUKUZA KWA MUDA MREFU SASA NIMEPATA KHOFU BAADA YA KUSOMA MAKALA HII YA WALIOGOMBANA NIMEFIKIRIA KWENDA KWA SHEKH AHMED AL KHALILI ILI AWAITE NA

KUWAPA MAWAIDHA NAOMBA USHAURI WENU














JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.




Shukurani kwa kujua kwamba unafaidika na mafunzo ya Alhidaaya na unafuata nasaha zetu. Hii ni neema kwako kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Kutaka Kukuongoza na Kukuepusha na shari hii, inapasa umshukuru kwa Hidaaya Yake.




Kutokana na umuhimu wake jambo hili na hatari zake, tumefanya juhudi haraka mno kukujibu kabla ya wengine ambao maswali yao yameingia zamani sana kabla yako. Hii kwa sababu tunamkhofia kila Muislamu mwenye kukhasimikiana na nduguye, ikiwa undugu wa Kiislamu au undugu wa uhusiano wa damu, kupoteza ‘amali zake na kupata madhara yake kama zilivyotajwa katika makala ya 'Nasiha Ya Ijumaa' na humu kwenye jibu hili.




Bila shaka ikiwa umekhasimikiana na ndugu zako, jambo ambalo linachukiza sana kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), bali Analaani wenye kukata uhusiano wa damu. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):



((فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِن تَوَلَّيْتُمْ أَن تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ )) (( أُوْلَئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَى أَبْصَارَهُمْ))



((Basi yanayotarajiwa kwenu mkitawala ndio mfisidi katika nchi na muwatupe jamaa zenu)) ((Hao ndio Allaah Aliowalaani, na Akawatia uziwi, na Akawapofoa macho yao)) [Muhammad: 22-23]






Pia Anasema:




((الَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ اللَّهِ مِن بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الأَرْضِ أُولَئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ))

((Wanaovunja ahadi ya Allaah baada ya kwishaifunga, na wakayakata Aliyoamrisha Allaah kuungwa, na wakafanya uharibifu katika nchi; hao ndio wenye khasara)) [Al-Baqarah: 27]

Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameonya kwamba mwenye kukata uhusiano wa damu hatoingia Peponi! Hali kadhaalika mwenye kukata uhusiano wa ndugu Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Hukmata, na ni sababu mojawapo wa kupunguziwa rizki, umri na mali. Maonyo mbali mbali kama haya tunapata katika kauli za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) zifuatazo:




Hadiyth ya kwanza:

قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( لا يدخل الجنة قاطع رحم)) رواه الترمذي.

Amesema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Haingii Peponi mwenye kukata udugu)) [At-Trimidhiy]






Hadiyth ya pili:

عن عائشة رضي الله عنه قالت: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((الرحم معلقة بالعرش تقول: من وصلني وصله الله ومن قطعني قطعه الله)) رواه البخاري ومسلم

Kutoka kwa Mama wa Waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anhaa) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Uteresi [Fuko la uzazi] limetundikwa na 'Arsh [Kiti cha Enzi cha Allaah] linasema: Atakayeniunga, Allaah Atamuunga, na atakayenikata, Atakatwa na Allaah)) [Al-Bukhaariy na Muslimu]



Hadiyth ya tatu:



((إن الله خلق الخلق حتى إذا فرغ من خلقه قالت الرحم: : هذا مقام العائذ بك من القطيعة. قال: نعم. أما ترضين أن أصل من وصلك واقطع من قطعك؟ قالت: بلى يا رب قال فهو لك )) رواه البخاري ومسلم.



((Hakika Allaah Ameumba viumbe mpaka Alipomaliza likasema uteresi [fuko la uzazi) Huyu amesimama anajikinga Kwako na anayemkata, Akasema ndio hivi huridhii Nikimuunga anayekuunga na Ninamkata anayekukata? Akasema sawa. Akasema hilo lako [umekubaliwa ombi lako])) [Al-Bukhaariy]




Hadiyth ya nne:



فعن أنس بن مالك رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((من أحب أن يبسط له في رزقه وينسأ له في أثره فليصل رحمه)) رواه البخاري ومسلم.

Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kupenda kutanuliwa rizki yake, na azidishiwe baraka katika umri wake, basi aunge undugu wake)) [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth ya tano:

عن أبي أيوب الأنصاري رضي الله عنه أن رجلا قال: يا رسول الله: أخبرني بعمل يدخلني الجنة . فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((تعبد الله لا تشرك به شيئا وتقيم الصلاة وتؤتي الزكاة وتصل الرحم)) رواه البخاري ومسلم.


Kutoka kwa Abu Ayyuub Al-Answaariyy (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba mtu alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Ewe Mtume wa Allaah, nifahamishe tendo litakaloniingiza Peponi na litakaloniepusha na moto. Akasema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam): ((Umuabudu Allaah wala Usimshirikishe na chochote, usimamishe Swalaah utoe Zakaah na uunge undugu)) [Al-Bukhaariy na Muslim].




Kwa hiyo nasaha zetu za dhati kama ulivyotaka kwetu, ni kwamba fanya haraka kabisa upatane na ndugu zako kwa ili ubakie salama na ‘amali zako, na upate fadhila na kujepusha na madhara yaliyotajwa katika Qur-aan na Sunnah, na upate Radhi za Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala).




Pia tambua kwamba mwenye kuanza kupatana na nduguye ni bora mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwani daraja yake hupandishwa kwa kunyenyekea kwake na kuwa yeye wa kwanza kumlaani Shaytwaan ambaye anawashawishi watu wakhasimikiane. Na pindi ukifanya juhudi ya kuwasiliana na ndugu zako kwa kutaka kupatana nao, kisha wao wawe wakaidi, basi wewe utakuwa huru na umeshajitoa hatiani katika kupata madhara ya kukata uhusiano wa ndugu; watabaki wao kubeba dhambi. Lakini tunaomba kuwa isiwe hivyo bali wote warudie kwa Mola wao kuunga undugu inshaAllaah.




Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi kuhusu maudhui hii muhimu mno kwa kila Muislamu:




Kukata Undugu




Amezuiliwa Kuonana Na Mama Yake Afanyeje?




Baba Ametukataza Tusiwasiliane Na Dada Yetu – Je Tumtii?







Na Allaah Anajua zaidi
 
Amezuiliwa Kuonana Na Mama Yake Afanyeje?
Maswali: familia-Jamii





SWALI:

SWALI LANGU NI SOMA KWA MAKINI HALAFU NAOMBA MINIJIBU.

Mimi wazazi wangu upandewa baba hawataki niende wa mama(upande wa mama) ati kwa sababu mama alipoachwa na baba mimi nilikuwa ni mdogo sana mtoto wa mienzi 8 halafu mama akaolwa na mume mwengine halafu akawa hapiti kuja kunitembela. sasamimi nilikuwa najiuliza mimi mama ninae au amekufa.kuna siku moja nilikutana na mjomba kaka ake mama mimi nilikuwa simjui lakini yeye ananijuwa mimi aliniambia kuwa tupange siku tuende kumuona mama kwa vile mimi nilikuwa simjui mama nikamuambia hamna shida mimi nyumbani siku hiyo nikatoroka na nikarnda kumuona mama akiwa shamba fujoni.niliporudi nyumbani wakanipiga hapo nilikuwa kama miaka12 hawakujuwa lakini kama nilikuwa nimeenda kwa mama lakini kuna mtu mimi simjui nani alikuja kusema kuwa mimekweda kwa mama na walipojuwa kuwa nimekwnda kwa mama walinipiga pia na kunisimanga. toka siku hiyo nika siendi tena kwa mama sasa mimi ninamiaka 20 nishakuwa naakili sio kama ile ya zamani kila siku ya jumaapili ninakwenda kwa mama lakini natoroka sitaki wajue kwani wakijuwa itakuwa matatizo sana kwangu.na hata nikiwambia sasa hivi itakuwa kama ninampigia mbizi gitaa.sasa.

SASA NILIKUWA NATAKA USHAURI AU KAMA KUNA DUWA YA KUSOMA NIPENI NIPATE KUSOMA ILI WANIPERUHUSA NIPATE NIIJUWE FAMILA YA UPANDE WA MAMA.KWANI NI HAMU SANA YA KUIJUWA FAMILA YA UPANDE WA MAMA.NA KIWA SUBIRI WAO WANIPE RUHUSA NAONA NITACHELEWA SANA KUWASUBIRI.

NAOMBA MINIJIBU HARAKA KWANI NINA KAA KILA SIKU NA MAJOZI LINI NITAKAA NA MAMA NARUDIA TENA KAMA KUNA DUWA YA KUSOMA NAOMBA MUNIPE.

RAMAHDANI NJEMA.

Muulizaji amerudia kutuma tena Swali:




MIMI NILIKUWA NATAKA USHAURI KWANI MIMI KILA SIKU NAKUWA NAKAA KWA KUMUWAZA MAMA. SASA KAMA KUNA DAWA AU DUA YA KUSOMA NILIKUWA NATAKA MUNIPE KWANI MIMI WAZAZI WANGU WA UPANDE WA BABA HAWATAKI MIMI NIENDE UPANDE WA MAMA SASA MIMI NIFANYE NINI ILI WAWEZE KUNIPA RUHUSA NIENDE KWA MAMA.

SASA NILIKUWA NATA MUNIPE IYO DUA AU DAWA YA ILI NIPATE MIMI KUKAA NA MAMA

NAOM,BA MUNIJIBU HARAKA








JIBU:




Sifa zote njema anastahiki Allah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Kwanza tuwe

Hapana dawa ya shughuli hiyo na anayekwambia ipo basi kakudanganya. Iliyopo ni Da‘wah (kulingania) kwa wazazi wako wa upande wa baba. Unatakiwa ukae nao na uwaeleze namna Uislamu unavyomhimiza Muislamu kuwatendea wema wazazi wake na hasa mama yake. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipoulizwa:

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: جاء رجل إلى رسول الله صلى الله عليه وسلم فقال: يا رسول الله من أحق الناس بحسن صحابتي؟ قال: (( أمك)) قال: ثم من؟ قال : (( أمك))


قال: ثم من؟ قال : (( أمك)) قال: ثم من؟ قال : ((أبوك)) رواه البخاري ومسلم




Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allahu 'anhu) kwamba alikuja mtu kwa Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamuuliza: "Ewe Mjume wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), nani mwenye haki zaidi mimi kumfanyia wema?". Akasema: ((Mama yako)) Kisha kasema: "Nani baada yake?" Akasema ((Mama yako)) Kisha kasema: "Nani baada yake?" Akasema ((Mama yako)). Kisha kasema: "Nani baada yake?" Akasema: ((Baba yako)) [Al-Bukhaariy na Muslim]






Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amekemea sana jambo hili la kukatisha mawasiliano ya wazazi na waliohusiana kwa damu hadi kufika kumlaani mwenye kufanya hivyo:

فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِن تَوَلَّيْتُمْ أَن تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ


أُوْلَئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَى أَبْصَارَهُمْ



((Basi yanayotarajiwa kwenu mkitawala ndio mfisidi katika nchi na muwatupe jamaa zenu))

((Hao ndio Allah Aliowalaani, na akawatia uziwi, na akawapofoa macho yao)) [Muhammad: 22-23]

((الَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ اللَّهِ مِن بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الأَرْضِ أُولَئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ))



((Wanaovunja ahadi ya Allah baada ya kwishaifunga, na wakayakata Aliyoamrisha Allah kuungwa, na wakafanya uharibifu katika nchi; hao ndio wenye khasara)) [Al-Baqarah:27]



Amesema Ibn Kathiry: Hii ina maana kukata uhusiano na jamaa na udugu kama alivyokiri Qataadah

Vile vile Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametukataza jambo hili katika Hadiyth nyingi, moja ifuatayo:




عن أبي هريرة رضي الله عنه ان النبي صلى الله عليه وسلم قال : ((من كان يؤمن بالله واليوم الأخر فليصل رحمه )) رواه البخاري

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwenye kumuamini Allah na siku ya Akhera, basi aungane na jamaa (udugu wa damu) zake)) [Al-Bukhaariy]




Kisha naye kakemea kuwa kukata udugu kutamharimisha mtu Pepo:

قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( لا يدخل الجنة قاطع رحم)) رواه الترمذي.

Amesema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Haingii Peponi mwenye kukata udugu)) [At-Trimidhiy]




Ikiwa umeshindwa kuwakinaisha wazazi wako wa upande wa baba kukuruhusu kumtembelea mama yako, basi watumie Mashaykh ambao wanaweza kuzungumza nao na kuwafahamisha umuhimu wa kuunga kizazi. Hii ni njia moja ambayo tunatarajia inaweza kuleta natija nzuri.




Njia nyengine ni kuinuka usiku na uswali Swalah ya usiku. Baada ya Swalah umuombe Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) Awalainishe nyoyo za wazazi wako hao. Bila shaka yoyote Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atakutolea njia katika hiyo shida na tatizo lako.




Hili lililokupata ni janga au balaa ya kutoweza kumuona au kumtembelea mama yako, hivyo Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) anatutaka tuwe ni wenye kuomba dua hii hapa ili atuepushie na balaa hiyo.


لا إلَهَ إلاَّ اللَّهُ الْعَظـيمُ الْحَلِـيمْ، لا إلَهَ إلاَّ اللَّهُ رَبُّ العَـرْشِ العَظِيـمِ، لا إلَهَ إلاَّ اللَّهُ رَبُّ السَّمَـوّاتِ ورّبُّ الأَرْضِ ورَبُّ العَرْشِ الكَـريم



“Laa ilaha illaa Llahul ‘Adhiimul Haliim. Laa ilaha illaa Llaahu Rabbul ‘Arshil ‘Adhiim. Laa ilaha illaa Llahu Rabbus samawaati wa Rabbul ardhi wa Rabbul ‘Arshil Kariym”

“Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu aliye Mtukufu Mpole, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu Mola wa ‘Arshi tukufu, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu Mola wa mbingu na Mola wa ardhi na Mola wa ‘Arshi tukufu" (Al-Bukhaariy na Muslim).



Tunakuombea kwa Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) Akusahilishie na akuondolee tatizo hilo ili uweze kwenda na kumtazama mama yako na mwish muweze kukaa na kuishi pamoja naye inshaAllah.

Na Allah Anajua zaidi
 
Baba Ametukataza Tusiwasiliane Na Dada Yetu – Je Tumtii?
Maswali: familia-Jamii




SWALI:



Mimi nina dadangu ambaye anaishi na mwanaume bila kuolewa na mbaya zaidi akapata ujauzito. Na wakati wote anakaa na mwanaume babangu hakuwa anajua hilo alikuwa anajua kuwa anaishi peke yake kwani ndiyo ilikuwa ahadi kuwa angeishi kwa misingi ya dini.

Sasa babangu alivyosikia kuwa ni mjazito alitoa maneno makali sana juu ya dadangu na kumtaka kama anataka msamaha arudi nyumbani na kadi la kliniki lifutwe jina la huyo mwanaume. Licha ya upenyo huo dada yangu akakataa kurudi nyumbani hivyo mpaka sasa amejifungua bado anakaa na huyo mwanaume wake ambaye ni mgalatia.

Sasa basi babangu amesema mtu yeyote atakayempa msaada dadangu iwe kwenda kumuona au kumpelekea zawadi yeye hayuko pamoja naye. Hivyo mpaka sasa mimi sijaenda kumuona dada yangu huyo. Je kisheria babangu yuko sawa









JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa dada yetu muulizaji swali. Hakika ukweli wa mambo ni ule msingi ambao ametuekea sisi kipenzi Mtume wetu, Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliyesema: " Hakuna utiifu kwa kiumbe ikiwa itakwenda katika kumuasi Muumba". Lakini ikiwa mwenye kutoa amri ni katika wale walioelezwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) na Mtume Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) basi kutiiwa inakuwa ni lazima.

Miongoni mwa wale ambao tunafaa tuwatii ni wazazi wawili wakiamrisha jambo linalokwenda sambamba na sheria. Mas-ala ya kupigwa vita na kususiwa watu wa maasi ni jambo ambalo limehimizwa na sheria. Katika hilo ndio tunaona kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliamrisha Maswahaba watatu waliokosa kwenda katika Vita vya Taabuuk kupigwa vita na kusususiwa hata katika salamu. Maswahaba wenyewe walikuwa ni Ka'b bin Maalik, Muraarah bin ar-Rabii' al-'Amriy na Hilaal bin Umayyah al-Waaqifiy (Radhiya Allaahu 'anhum). Hawa watatu walianza kusemeshwa tu baada ya kupatiwa msamaha na Allaah Aliyetukuka (al-Bukhaariy na Muslim, waweza kuipata Hadiyth hiyo kwa urefu katika kitabu Riyaadh asw-Swaalihiyn, Hadiyth namba 21).

Ama Qur-aan imetuelezea yafuatayo kuhusu twaa kwa wazazi: "Na pindi wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna elimu nayo, basi usiwatii, lakini kaa nao kwa wema duniani" (31: 15).



Kwa mujibu wa swali lako, fuata na tekeleza yafuatayo:

1. Kwanza wasiliana na dada yako ukiweza na lengo lako la kufanya hivyo ni kumpatia nasaha kwamba maisha anayoishi hayo sio sawa, na dini yetu hairuhusu hivyo bali ni haraam.



2. Jaribu kwa kila njia kumpatia makala, mawaidha atambue uharamu wa maisha anayoishi na matokeo yake kupata ghadhabu za Mola wake.



3. Mjulishe kuwa unawasiliana naye kwa kuvunja amri ya mzazi wenu, na sababu ni kwamba unamtakia kheri ya maisha yake ya kidunia na Akhera. Kwani pindi atakapokatana na wazazi wake na ndugu zake ni hatari kubwa mno na jambo la kulaaniwa na Mola na pia ataharamishwa na Pepo. Mchapishie Swali katika kiungo kifuatacho:



Amezuiliwa Kuonana Na Mama Yake Afanyeje?

4. Mtahadhirishe kuwa hayo ni maisha ya dunia ambayo yatakwisha – na pindi watakapoondoka mmoja wa mzazi wenu akiwa ameghadhibika naye basi atambue kuwa amekosa Pepo bali atapata ghadhabu za Mola wake na hatokuwa na kheri na Baraka katika maisha yake kwa kukosa radhi za wazazi wake, bali huenda akadhurika! Hivyo faida gani atakayopata au atafaidika vipi na huyo mume na watoto wake?



5. Aachane na huyo mwanaume mara moja, na ikiwa huyo mwanaume anataka kuendelea kuishi naye, basi amjulishe kuwa anatakiwa kusilimu kwanza kwa khiyari yake na si kuitikia tu ili apate kukaa naye kama wanavyofanya wengi wenye kufuata mapenzi na si Dini! Mwambie afanye toba kwa yote hayo na Allaah Atamsamehe inshaAllaah na Kumpa bora kuliko huyo mwanaume aliyenaye hivi sasa.




6. Atakapokupa jibu la kuwa na matumaini ya kukubali nasaha basi endelea kuwasiliana naye. Lakini pindi utakapoona kuwa kashikilia kuishi hivyo hivyo bila ya kutaka kujaribu kusawazisha maisha yake basi hapo ndipo itakapokubidi umjulishe kuwa hutoweza kuendelea kuwasiliana naye na kwamba itabidi ukate mawasiliano naye



Tunakuombea kila la kheri katika jitihada yako na nia yako njema ya kutaka kumuokoa dada yako kwenye haraam na madhara ya maisha yake.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Anaishi Katika Nyumba Isiyokuwa Na Masikilizano Aombe Du’aa Gani Naye Apate Mume Atoke Katika Nyumba
Maswali: familia-Jamii
SWALI:



Asalaam Alaikum Warahmatullahi Wabarakaatu



Tuna ndugu yetu anaomba msaada yeye anaishi na kaka yake na wifi yake, ndani ya nyumba hiyo hamna masikilizano mazuri na yeye hana mume. Suala lake iko dua ambayo ataweza kuomba ili Mola Subhana Wataala amjaalie apate mume na yeye awe na kwake.



JIBU:





Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.





Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuwa ndani ya nyumba iliyo na matatizo

.

Tufahamu kuwa tatizo moja au jengine ni katika mitihani ambayo mwanaadamu anakumbana nayo kwa njia moja au nyingine. Katika hali hiyo inafaa mtu asubiri sana kwani Allaah Aliyetukuka Amesema:

“Hakika Allaah yu pamoja na wanaosubiri”.



Na hakika subira huvuta kheri.



Pia tufahamu kuwa hakuna dhiki juu ya dhiki; baada ya dhiki ni faraji. Na minajili hiyo, Anasema Aliyetukuka: “Hakika pamoja na dhiki huja faraji” (94: 6). Na faraji kwako huenda ikawa ipo karibu.



Ama kuhusu du’aa hakuna du’aa maalumu kuhusu hilo. Unachohitajika kufanya ni kumuomba Allaah Aliyetukuka katika nyakati ambazo du’aa hukubaliwa. Nyakati hizo ni kama zifuatazo:



1. Baina ya Adhana na Swalah ya faradhi.

2. Wakati umefunga.

3. Wakati wa kufungua mwadhini siku unayofunga.

4. Ukiwa katika sijdah.

5. Baada ya kumaliza Tahiyyaatu kabla ya kutoa Salaam ndani ya Swalah.

6. Wakati wa usiku unapoinuka kwa ajili ya Swalah ya Tahajjud.

7. Wakati uko katika safari, na kadhalika.



Tunakuombea kila la kheri utoke katika balaa na mtihani huo.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Anaishi Nje Ya Nchi, Wakwe Zake Wanamzuia Mtoto Wake Asiende Kwa Wazazi Wake



Alhidaaya.com





Swali:



Assalamu Aleikum Warahmatullahi Wabaratu.



Mimi niko na mtoto wakiume yuko na miaka sita,mimi niko safari na mumewangu lakini mtoto tumemuwacha kwa watu wa mume wangu,shida ni kwamba watu wake hawataki mtoto aende kwetu,nikumwambia mume wangu asema yeye hayaingilii watu wakwao wafanye vile wanavyotaka,mamake na babake wakiamuwa huyo mtoto pia asiende kwetu kabisa basi ndio hivyo kwani yeye ataka radhi za wazee wake,je hiyo ni sawa?na mwenye kuamuwa yote haya ni dadake mkubwa ndiye anayetaka kutupangia sisi mambo anavyotaka yeye sio waume zetu,je ni sawa?atakalo sema yeye ndilo litakalo fuatwa,mimi huuliza je nimeolewa na mume au na family nzima?kwasababu ni mambo yakushangaza,kila mtu ataka kukucontrol wewe mke mmoja.



Waiting for reply



Shukran





Swali Jingine:



Assalamu Aleikum Warahmatullahi Wabarakatuh.



ningependa munitatulie tatizo hili.mimi niko safari na niko na mtoto wangu mwenye miaka sita ambaye hatukusafiri nayeye tumemuacha na nyanyake mzaa baba,lakini hataki kukaa huko ataka kwenda kwetu lakini babake na watu wake hawataki aende akakae kwetu,hivi anamwezi na siku kadhaa hajakwenda kwetu akisema ataka kwenda kwetu aambiwa angojee mpaka school zifungwe na school zikifungwa yeye yuwasafiri kuja huku kutuangalia kwa sababu ya viza isiharibike,school niliyomtia ni karibu na nyumbani kwetu pia ametolewa bila ya mimi na babake kujuulishwa,dadangu akienda school kumjulia aambiwa haendi school, nikamwambiya babake ajulie ndipo alipoambiwa ametolewa na kutiwa school nyingine ili asipate nafasi ya kwenda kwetu. na kila akienda kwetu huambiwa hakuna kulala huko na hutishiwa atachapwa, hivi mimi nimeamuwa nirudi nikakae na mwanangu.Je nifanyeje?





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho





Mtoto ni wenu nyote na wazazi wa baba wana haki kama walivyo na haki hiyo hiyo wazee wa mama; hivyo basi kumzuia mtoto wakati wowote ule kwenda kwa mama yake au baba yake au kumzuia kwenda kwa wazee wa mama yake au wazee wa baba yake ni moja kati ya yenye kueleweka kama ni kuvunja udugu, na hilo ni katika madhambi makubwa; kwani mtoto au mtu yeyote kuwatembelea jamaa zake wawe wa upande wowote ule ni katika jambo la wajibu na huko ndio kuunga na kuimarisha udugu/ujamaa. Na kumkataza au kumzuilia huyo mtoto kutekeleza jambo hilo ni lililo wajibu ni haramu, Allaah Anasema:

وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ ۚ

Na mcheni Allaah Ambaye Kwake mnaombana (haki zenu kwa kuunga) undugu. [An-Nisaa: 1].





Hivyo wewe na huyo mumeo munahitaji muelewe haya na mujaribu kadiri ya uwezo wenu bila ya kuvutana wala kugombana kuwaelewesha wengine ili wasiingie katika makosa kwa kukataza jambo lilioamrishwa na Uislamu; na huko ndio kutafuta radhi za wazee wenu kwani mutakuwa mumewasaidia kuachana na yaliyokatazwa na Uislamu na kuwapelekea kutekeleza yaliyohimizwa na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama ilivyothibiti katika Hadiyth aliyoulizwa Nabiy Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam kuhusu kitu kitachomuingiza mtu peponi, alijibu kwa kusema:





"Haingii peponi mwenye kukata udugu" [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] Kitabu cha Aadabu, mlango dhambi za asiyeunga udugu.





Ama maamuzi yako ya kwenda kuishi na mwanao, hayo ni maamuzi ya busara, na ni jambo linalohitajika haswa wazazi kuishi na mwana wao kwani kunaimarisha mapenzi, kujenge mahusiano ya karibu, malezi kuwa mepesi na kufuatilia nyendo zake kwa karibu. Na haipendezi kukaa mbali na mtoto wenu kwa sababu tu ya maslahi ya kidunia, bila dharura zozote zile za msingi.





Bonyeza kiungo kiufatacho upate manufaa zaidi:



Kukata Undugu





Na Allaah Anajua zaidi
 
Baba Amemkana Binti Yake Kwa Ajili Amekataa Kuolewa
Maswali: familia-Jamii
SWALI:





Assalaamu aleykum, sheikh mimi nina sister yangu ambaye yuwaendelea na kisomo ilhali asha baleghe kitambo, so hivi majuzi mzee wetu alimwita dada na kumwambia ya kwamba ashapanga yeye mzee na rafiki ya kuwa ili wawaozeshe watoto wao (yaani sister yangu na mtoto wa swahiba yake buda) kwa hiyo sister na huyo kijana hawajuani kichwa wala miguu na dada yangu hayuko tayari kuolewa, hapo dada yangu alikataa katakata hiyo harusi! Sasa balaa yenyewe ilitoka kwa mzee alipomwambia bintiye kuanzia saa hii hatujuani kwa la kheri wala la shari kama umekataa hii amri yangu! Sasa sheikh sijui ndio akhir zamani ama kiyama hichi? Nimeshindwa kuelewa. Inshaallah nataraji jibu ambalo litawanufaisha waislamu wote. Sheikh Mungu akupe umri ili upate kutujibia maswali yetu tutakapopata family na cc "amiin".













JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu baba mzazi kumkana bintiye kwa kukataa kuolewa.



Hakika ni kuwa hicho si Qiyaamah na wala si akhiri zamani japokuwa zipo ishara nyingi ndogo ndogo kuonyesha hayo. Hata hivyo, kukataa kwa dada yako kuolewa na kijana aliyemchagua baba yako si miongoni mwa alama za Qiyaamah. Kwa mujibu wa dini ya Kiislamu zipo alama nyingi za Qiyaamah ambazo tumeelezewa kinaganaga bila utata wa aina yoyote.



Katika Uislamu, binti amepatiwa haki ya kuikubali posa au kuikataa kwa sababu moja au nyingine. Baba amekosea kidogo kwa kumletea binti yake mchumba na bila kumjulisha na kumlazimishia. Kipo kisa ambacho kinapatikana katika Swahiyh al-Bukhaariy pale baba alipomchagulia mume binti yake kabla ya kumjulisha. Binti huyo alikuja kushitaki kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), naye Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamchaguza baina ya kukubali wito wa baba au kukataa. Yule binti akamwambia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa amekubali uchaguzi wa baba yake lakini alikuwa anataka kuwafundisha wanawake wengine kuhusu haki yao ya uchaguzi katika suala zima la ndoa.



Pia yalikuwa makosa kwa baba badala ya kuzungumza na binti yake baada ya hapo kwa njia nzuri ili amkinaishe aolewe akatumia mabavu kwa kumkana binti. Haifai kisheria kwa baba kumkana binti au kijana wake baada ya kuwa amemkubali muda wote huo. Na pia haifai kwa baba kukataa jukumu la bintiye kwa ajili tu amekataa bali ilikuwa azungumze naye kwa makini na upole na pengine ingekuwa ni busara zaidi kumshirikisha mkewe ili azungumze na bintiye kwa hali ya ulaini na urafiki. Ikiwa binti ameshikilia hilo itabidi wazazi wakubali haki hiyo ya binti.



Inabidi kwa wakati huu wazee waingilie kati suala hilo ili kurudisha hali ya awali.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Baba Yetu Alitutupa Sasa Amefariki Nataka Kumsamehe, Mnashaurije?



www.alhidaaya.com





SWALI:



assalam alaykum warahmatuh-llah wabarakatuh.

swala langu ni kuhusu babayangu, Aliyefariki kwanzia afariki sijawahi kumuombea mungu kwa sababu nilikuwa na uchungu sana wa kuwa hakuweza kutuangalia kwa lolote kwanzia kuzaliwa kwangu, na hata ndugu zangu. Yaani ametutupa kwa kila kitu,kwahivyo hatukuwa na uhusiano hata kidogo twajua tu yule ndio baba yetu, kila nikikaa najiuliza kwa nini ametufanya hivi na alikuwa akijiweza hata kututazama alikuwa hakutaka tu! Mpaka sasa ndio naona nimeanza kurudi nyuma manake nisingelipenda kumchukia mpaka ikafika hali ya zaidi ningelipenda kumuombea dua anisamehe na vile ashafariki mungu amsamehe. tafadha kwa kila shukrani munisaidie manake yananisumbua sana.ahsante.





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Hapana shaka kutokana na hisia zako ulizokuwa nazo kuhusu aliyefariki mzazi wako kuwa zimetokana na hali ilivyokuwa baina yenu na aliyefariki mzazi wenu ambaye hakuwa akikutazameni. Lakini tunapenda kukumbusha kwamba vyovyote itakavyokuwa yeye ni mzazi wako, na pia hamuwezi kujua sababu gani alifanya hivyo. Kwa hiyo mpeni udhuru kwa kumdhania vizuri badala ya kumwekea dhana mbaya kama inavyopasa baina wa Waislamu. Juu ya hivyo kwa vile ni mzazi wako hakuna budi kumuombea kwani ni maamrisho kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala).



Kumsamehe makosa yake na kumuombe du’aa mzazi wenu kutapatikana faida kubwa kuliko kuzidi kuweka chuki. Kwani kwa vyovyote imeshatokea la kutokea na ima uchague kumuombea du’aa na kumfanyia wema ambao utaendelea kumfikia na kumnufaisha, au umwache aendelee kuteseka mzazi wako huko katika maisha yake ya Barzakh nawe huku ubakie na dukuduku, huzuni na dhiki? Ipi mojawapo itakayokupa wewe furaha? Bila ya shaka kumsamehe na kumfanyia wema! Faida zenyewe ni zifuatazo:



1. Utakuwa umetekeleza amri za Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) za kuwaombea du’aa mzazi au wazazi wako.



2. Kila utakapomuombea Maghfirah atakuwa anapandishwa daraja moja juu, na hali itakuwa kama ilivyo katika usimulizi ufuatao:





عن أبي هريرة رضي الله عنه ، قال : قال رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْه ِ وَ سَلَّمَ : إِنَّ الرَّجُلَ لَتُرْفَعُ دَرَجَتُهُ فِي الْجَنَّةِ فَيَقُولُ : أَنَّى هَذَا ؟ فَيُقَالُ :باسْتِغْفَارِ وَلَدِكَ لَكَ)) لإمام أحمد و في سنن ابن ماجة أيضاً بإسنادٍ صحيح



Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika mtu hupandishwa daraja yake Peponi. Kisha huuliza: Kwa ajili ya nini? [huku kupandishwa kwangu daraja?] Huambiwa: Kwa ajili ya kuombewa Maghfirah na mtoto wako)) [Ahmad, na katika Sunan Ibn Maajah ikiwa na isnaad Swahiyh]



3. Kumsamehe mtu ni sawa na kusamehewa wewe madhambi yako. Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) alipotaka kumgomea kuendelea kumsadiia jamaa yake ambaye alikuwa mmojawapo aliyechangia katika uzushi wa kumzulia mwanawe Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anhaa), Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Akateremsha Aayah ifautayo:



((وَلاَ يَأْتَلِ أُوْلُوا الْفَضْلِ مِنْكُمْ وَالسَّعَةِ أَنْ يُؤْتُوا أُوْلِي الْقُرْبَى وَالْمَسَاكِينَ وَالْمُهَاجِرِينَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَلْيَعْفُوا وَلْيَصْفَحُوا أَلاَ تُحِبُّونَ أَنْ يَغْفِرَ اللَّهُ لَكُمْ وَاللَّهُ غَفُور ٌ رَحِيم))

((Na wala wasiape wale wenye fadhila miongoni mwenu na wenye wasaa wa mali kuwa hawatowapa (swadaqah) jamaa wa karibu, na masikini, na Muhaajiriyn katika njia ya Allaah. Na wasamehe na waachilie mbali. Je, hampendi Allaah Akughufurieni? Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu)) [An-Nuwr: 22]



Hisia zako tayari zinaonyesha kuwa unakaribia kumsamehe na hii ni alama ya iymaan na mapenzi ya kimaumbile baina ya mtoto na mzazi. Kwa hiyo usiache Shaytwaan akakughilibu na kukubakisha katika hali isiyomridhisha Mola wako Mtukufu wala kukuridhisha wewe nafsi yako. Muombee mzazi wako Maghfirah, muombee du’aa na mfanyie wema kama kwamba yuhai duniani.



Na la muhimu zaidi ni kuwa uwape nasaha ndugu zako wote nao wapate ujumbe huu na nyote mtapata malipo mema kutoka kwa Mola wenu.



Bonyeza kiungo kifuatacho kwa faida zaidi:



‘Amali Za Kuwatendea Wazazi Waliofariki Waendelee Kupokea Thawabu





Na Allaah Anajua zaidi
 
Amali Za Kuwatendea Wazazi Waliofariki Waendelee Kupokea Thawabu
Jamii


‘Amali Za Kuwatendea Wazazi Waliofariki Waendelee Kupokea Thawabu



Alhidaaya.com





‘Amali za mwana Aadam zinakatika baada ya kufariki kwake isipokuwa matatu kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



((إذا مات إبن آدم إنقطع عمله إلا من ثلاث: صدقة جارية أو علم ينتفع به أو ولدٌ صالح يدعوا له)) مسلم

((Anapokufa mja, hukatika amali zake zote isipokuwa mambo matatu, swadaqah inayoendelea, au elimu yenye kunufaikiwa, au mtoto mwema anayemuombea)) [Muslim]



Lakini Muislamu anaweza kuendelea kuwatendea wema wazazi wake wawili kwa ‘amali nyenginezo ambazo zimethibiti kuwa thawabu zake zinawafikia kama ifuatavyo:





1-Kuwaombea du’aa na kuwaombea maghfirah:



عن أبي أسيد مالك بن ربيعة رضي الله عنه قال: بينا نحن جلوس عند رسول الله صلى الله عليه وسلم إذا جاءه رجل من بني سلمة فقال يا رسول الله هل بقي من بر أبوي شيء أبرهما به بعد موتهما ؟ قال: ((نعم! الصلاة عليهما والاستغفار لهما وإنفاذ عهدهما من بعدهما وصلة الرحم التي لا توصل إلا بهما وإكرام صديقهما)) رواه ابن حبان في صحيحه أبو داود وابن ماجه

Kutoka kwa Abuu Asyad Maalik bin Rabiy’ah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Tulipokuwa tumekaa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja mtu kutoka [kabila la] Bani Salamah akasema: Ee Rasuli Allaah, je, kuna kilichobakia katika wema ninaoweza kuwafanyia wazazi wangu baada ya kifo chao? Akasema: ((Naam! Kuwaombea du’aa, kuwaombea maghfirah, kuwalipa deni zao, na kuunga ukoo ambao hauungiki ila kutokana nao, na kuwakirimu rafiki zao)) [Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake, Abu Daawuwd na Ibn Maajah]





Kuwaombea Maghfirah Ni Kupandishwa Kwao Daraja Ya Jannah (Peponi):



عن أبي هريرة رضي الله عنه ، قال : قال رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْه ِ وَ سَلَّمَ: ((إِنَّ الرَّجُلَ لَتُرْفَعُ دَرَجَتُهُ فِي الْجَنَّةِ فَيَقُولُ : أَنَّى هَذَا ؟ فَيُقَالُ :باسْتِغْفَارِ وَلَدِكَ لَكَ)) لإمام أحمد و في سنن ابن ماجة أيضاً بإسنادٍ صحيح

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika mtu hupandishwa daraja yake Jannah (Peponi). Kisha huuliza: Kwa ajili ya nini? [huku kupandishwa kwangu daraja?] Huambiwa: Kwa ajili ya kuombewa maghfirah na mtoto wako)) [Ahmad, na katika Sunan Ibn Maajah ikiwa na isnaad Swahiyh]



Miongoni mwa du’aa za kuwaombea ni zilizotajwa katika kauli za Allaah ('Azza wa Jalla)



رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا ﴿٢٤﴾

Rabb wangu! Warehemu kama walivyonilea udogoni. [Al-Israa: 24]





رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ الْحِسَابُ ﴿٤١﴾

Rabb wetu! Nighufurie na wazazi wangu wawili na Waumini Siku itakayosimama hesabu. [Ibraahiym: 41]



Katika Sunnah wanaposaliwa Swalaah ya Janaazah:



Maiti mwanamume:



اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُ وَارْحَمْـه، وَعافِهِ وَاعْفُ عَنْـه، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـه، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَه، وَاغْسِلْـهُ بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِ مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقَّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُ داراً خَـيْراً مِنْ دارِه، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـه، وَزَوْجَـاً خَـيْراً مِنْ زَوْجِه، وَأَدْخِـلْهُ الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُ مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار

Eee Allaah, Mghufurie na Mrehemu, na Muafu na Msamehe na Mtukuze kushuka kwake (kaburini) na Mpanulie kuingia kwake, na Muoshe na maji na kwa theluji na barafu na Mtakase na makosa kama inavyotakaswa nguo nyeupe kutokana na uchafu, na Mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba yake na jamaa bora kuliko jamaa zake, na mke bora kuliko mke wake, na Muingize Jannah (Peponi) na Mkinge na adhabu ya kaburi na adhabu ya moto.



Maiti mwanamke:



اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُا وَارْحَمْـها، وَعافِهاِ وَاعْفُ عَنْـها، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـها، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَها، وَاغْسِلْـهُا بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِا مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقَّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُا داراً خَـيْراً مِنْ دارِها، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـها، وَزَوْجَـاً خَـيْراً مِنْ زَوْجِها، وَأَدْخِـلْهُا الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُا مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار



Kuwaombea Wazazi Wawili:



اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُما وَارْحَمْـهما، وَعافِهِما وَاعْفُ عَنْـهما، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـهما، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَهما، وَاغْسِلْـهُما بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِما مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقَّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُما داراً خَـيْراً مِنْ دارِهما، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـهما، وأَزَوْاجَـاً خَـيْراً مِنْ اَزْوَاجِهِما وَأَدْخِـلْهُما الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُما مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار







2. Kuwalipia Deni La Swawm:



Kuwalipia deni la Swawm ikiwa ni la fardhi (Ramadhwaan) au Swawm ya nadhiri au ya kafara. Ama ikiwa amefariki kabla ya kumalizika Ramadhwaan na amewahi kufunga siku za nyuma, hakuna haja kumlipia:



عن ابن عباس رضي الله عنهما ، قال :جاء رجل إلى النبي صلى الله عليه و سلم فقال : يا رسول الله إن أمي ماتت، و عليها صوم شهر أفأقضيه عنها ؟ قال : (( لو كان على أمك دين أكنت قاضيه عنها ؟)) قال : نعم. قال: (( فدين الله أحق أن يُقضى)) البخاري و مسلم

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: Alikuja mtu kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Ee Rasuli wa Allaah, Mama yangu amefariki naye ameacha deni la mwezi la Swawm, je nimlipie? Akasema: ((Je angelikuwa mama yako ana deni [la fedha] ungelimlipia?)) Akajibu: Ndio. Akasema ((Basi deni la Allaah lina haki zaidi ya kulipwa)) [Al-Bukhaariy na Muslim]



Na pia:



عن عائشة رضي الله عنها ، قالت : قال رسول الله صلى الله عليه و سلّم: ((من مات و عليه صيامٌ صام عنه وليُّه)) البخاري و مسلم

Kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Aliyefariki akiwa na [deni la] Swawm, walii wake amfungie)) [Al-Bukhaariy na Muslim]





3-Kuwafanyia Hajj Ikiwa Hawakufanya Au Kuwafanyia ‘Umrah:



عن ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما أَنَّ امْرَأَةً جَاءَتْ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ ، فَقَالَتْ : إِنَّ أُمِّي نَذَرَتْ أَنْ تَحُجَّ ، فَمَاتَتْ قَبْلَ أَنْ تَحُجَّ ، أَفَأَحُجُّ عَنْهَا ؟ قَالَ: ((نَعَمْ ، حُجِّي عَنْهَا أَرَأَيْتِ لَوْ كَانَ عَلَى أُمِّكِ دَيْنٌ أَكُنْتِ قَاضِيَتَهُ ؟ )) قَالَتْ : نَعَمْ . فَقَالَ : ((اقْضُوا اللَّهَ الَّذِي لَهُ ، فَإِنَّ اللَّهَ أَحَقُّ بِالْوَفَاءِ )) رواه البخاري

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: Alikuja mwanamke kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Nina mama ambaye aliweka nadhiri kuwa atahiji, akafariki kabla ya kuhiji, je nimhijie? Akasema: ((Ndio, mhijie je ingelikuwa mama yako ana deni ungelimlipia?)) Akasema: Ndio. Akasema: ((Mkidhieni Allaah (deni) Lake, kwani Allaah Ana Haki zaidi kutimiziwa)) [Al-Bukhaariy]



Pia:



عن عَبْد اللَّهِ بْن بُرَيْدَةَ عَنْ أَبِيهِ رَضِي اللَّه عَنْهما ، قَالَ : بَيْنَما أَنَا جَالِسٌ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ ، إِذْ أَتَتْهُ امْرَأَةٌ ، فَقَالَتْ: إِنِّي تَصَدَّقْتُ عَلَى أُمِّي بِجَارِيَةٍ ، وَ إِنَّهَا مَاتَتْ . فَقَالَ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ : (( وَجَبَ أَجْرُكِ وَ رَدَّهَا عَلَيْكِ الْمِيرَاثُ)) قَالَتْ : يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّهُ كَانَ عَلَيْهَا صَوْمُ شَهْرٍ أفأصُومُ عَنْهَا ؟ قَالَ: ((صُومِي عَنْهَا)) قَالَتْ : إِنَّهَا لَمْ تَحُجَّ قَطُّ ، أَفَأَحُجُّ عَنْهَا؟ قَالَ: ((حُجِّي عَنْهَا)) مسلم

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Buraydah kutoka kwa baba yake (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: Nilipokuwa nimekaa kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja mwanamke akasema: Nimemtolea mama yangu swadaqah ya kijakazi. Naye amefariki. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Umewajibika kupata ujira na mirathi itakurudia)). Akasema: “Ee Rasuli wa Allaah, alikuwa ana deni la mwezi la Swawm, je nimfungie?” Akasema: ((Mfungie)). Akasema: “Yeye hakuwahi kuhiji, je nimhijie?” Akasema: ((Mhijie)) [Muslim]





4-Kuwatolea Swadaqah:



عن أمّ المؤمنين عَائِشَةَ رَضِي اللَّه عَنْهَا ، أَنَّ رَجُلاً قَالَ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ : إِنَّ أُمِّي افْتُلِتَتْ نَفْسُهَا ( أي ماتت فجأةً ) وَ أَظُنُّهَا لَوْ تَكَلَّمَتْ تَصَدَّقَتْ ، فَهَلْ لَهَا أَجْرٌ إِنْ تَصَدَّقْتُ عَنْهَا ؟ قَالَ: ((نَعَمْ)) البخاري

Kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) ambaye amesema: Mtu mmoja alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) “Mama yangu imesokoteka nafsi yake [kwa maana amefariki ghafla] na nadhani kama alizungumza kutaka kutoa swadaqah. Je, atapata ujira nikimtolea swadaqah?” Akasema: ((Ndio)) [Al-Bukhaariy]



Pia



عن ابْنُ عَبَّاسٍ رَضِي اللَّه عَنْهمَا ، أَنَّ سَعدَ بْنَ عُبَادَةَ رَضِي اللَّه عَنْهما تُوُفِّيَتْ أُمُّهُ وَ هُوَ غَائِبٌ عَنْهَا فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّ أُمِّي تُوُفِّيَتْ وَ أَنَا غَائِبٌ عَنْهَا أَيَنْفَعُهَا شَيْءٌ إِنْ تَصَدَّقْتُ بِهِ عَنْهَا ؟ قَالَ: ((نَعَمْ )) قَالَ: فَإِنِّي أُشْهِدُكَ أَنَّ حَائِطِيَ الْمِخْرَافَ ( اسم لبستان كان له) صَدَقَة ٌ عَلَيْهَا .- البخاري

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: Sa’ad bin ‘Ubaadah (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) alifiwa na mama yake naye alikuwa hayupo akasema: “Ee Rasuli wa Allaah, Mama yangu amefariki nami sikuweko. Je, itamfaa lolote nikimtolea swadaqah?” Akasema: ((Ndio)) Akasema: “Basi nashuhudia kwako kwamba ukuta wangu wa al-Mikhraaf [jina la bustani yake] ni swadaqah kwa ajili yake.” [Al-Bukhaariy]



Pia,



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَجُلاً قَالَ لِلنَّبِيّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ : إِنَّ أَبِي مَاتَ ، وَ تَرَكَ مَالاً وَ لَمْ يُوصِ ، فَهَلْ يُكَفِّرُ عَنْهُ أَنْ أَتَصَدَّقَ عَنْهُ ؟ قَالَ : (( نَعَمْ)) روى مسلم و ابن ماجة و النسائي

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Mtu mmoja alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Baba yangu amefariki na ameacha mali wala hakuiusia. Je, itakuwa kafara yake (atapata ujira na malipo) nikimtolea swadaqah kwayo?” Akasema: ((Ndio)) [Muslim, Ibn Maajah na an-Nasaaiy





5-Kuunga Ukoo Ambao Hauungiki Ila Kutokana Na Wao:



Dalili ni Hadiyth iliyotangulia katika nukta ya kwanza ambayo imetaja:

((na kuunga ukoo ambao hauungiki ila kutokana nao))



Ni kuwasiliana na ndugu, jamaa wenye uhusiano wa damu, wa karibu na wa mbali, mfano ‘ammu (kaka wa baba) ‘ammat (shangazi), khaal (kaka wa mama), khaalat (mama mdogo au mkubwa), watoto wao wote, bibi wa baba, bibi wa mama na wanaouhusiana wote kwa damu kwa kila upande.



Tutamube kwamba kuunga undugu wa uhusiano wa damu ni kitendo ambacho kimesisitizwa sana. Dalili zake zinapatikana katika Qur-aan na Sunnah kwamba mwenye kukataa kuunga undugu amelaaniwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), rizki yake itadhikika, umri wake utapunguka, Allaah ('Azza wa Jalla) Atamkatilia mbali na hatoingia Jannah (Peponi).







6-Kuwakirimu Rafiki Zao



عن عبد الله بن دينار عن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما أن رجلا من الأعراب لقيه بطريق مكة فسلم عليه عبد الله بن عمر وحمله على حمار كان يركبه وأعطاه عمامة كانت على رأسه . قال ابن دينار : فقلنا أصلحك الله إنهم الأعراب وهم يرضون باليسير , فقال عبد الله بن عمر إن أبا هذا كان ودا لعمر بن الخطاب وإني سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: (( وإن أبر البر صلة الولد أهل ود أبيه )) مسلم

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Diynaar na kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba bedui mmoja alikutana naye njiani akielekea Makkah, akamsalimia ‘Abdullaah bin ‘Umar kisha akampakia juu ya punda aliyekuwa amempanda akavua kilemba chake na kumpa. Akasema Ibn Diynaar: Tukasema: “Allaah Akuwekee vizuri. Hao ni mabedui nao wanaridhika na kichache.” ‘Abdullaah bin ‘Umar akasema: “Baba yake huyu alikuwa mpenzi wa ‘Umar ibnul Khattwwaab [Baba yangu] nami nimesikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Kitendo chema kabisa ni mtoto kumpenda (kuungana na) rafiki wa baba)) [Muslim]



Na pia:



عن أبي بردة قال: قدمت المدينة فأتاني عبد الله بن عمر فقال أتدري لم أتيتك ؟ قال قلت لا . قال سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((من أحب أن يصل أباه في قبره فليصل إخوان أبيه)) وأنه كان بين أبي عمر وبين أبيك إخاء وود فأحببت أن أصل ذاك - ابن حبان في صحيحه

Pia kutoka kwa Abuu Bardah ambaye amesema: Nilikuwa naelekea Madiynah akanijia ‘Abdullaah bin ‘Umar akasema: “Je, unajua kwa nini nimekujia?” Akasema: Nikasema: “Hapana!” Akasema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Anayependa kuungana na baba yake katika kaburi lake basi awasiliane na ndugu zake (rafiki zake) baba yake)) Na baina ya baba yangu ‘Umar na baba yako walikuwa na undugu wa mapenzi, basi nimependa kuwaunga.” [Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake]
 
UMRI WA UMMA HUU NI BAINA YA MIAKA 60 NA 70

Mtume swalla aallahu alahyi wa aalih wasallamu amesema umri wa umma wangu ni baina ya 60 mpaka 70

Na yeye mwenyewe amekufa akiwa na miaka 63,umri wa umma wetu ni mdogo ukilinganisha na kaumu zilizo pita,kwahiyo tusijisahau sana,na huyo ni kwa aliepewa umri huo maana wengine wameondoka kabla hawajafika,na wengine huenda tusifike pia

Sasa ebu jaribu kuangalia umri wako binafsi je una miaka mingapi,na umebakisha mingapi kwa mfano ndio unapewa umri wa miaka 60 au 70,je una mpango gani kwa umri uliobakia urekebishe pale ulipokosea huko nyuma

Mfano Etugrul bey juzi juzi tarehe 11/05/25 ametimiza miaka 46,ina maana kama atabahatika kupewa umri wa miaka 60 kwa mfano,amebakiwa na miaka 14 ya kuondoka hapa duniani,na anajua mwenyewe katanguliza nini huko nyuma,kwani kila nafsi inajijua yenyewe

Na Allah anasema watu wanapo kumbushwa ishara za Allah wanazipuuza na huku wamesahau waliyo yatanguliza huko nyuma,kwa maana huko nyuma tumetanguliza mabaya na maovu mengi,tunaambiwa tumche Allah ili turekebishe makosa yetu ya nyuma lakini tunapuuza

Allah anachukizwa na mzee ambaye amefikisha miaka 60 na bado anaendelea kuzini,haimaanishi kwamba chini ya miaka hiyo ndio hachukizwi laa!, ingawa mtu anapofikia uzee halafu bado anaendekeza uchafu huyo amepita mipaka

Maana mtu huyu anaishi kwa miaka ya extra time/mda wa ziada lakini bado anasahau kwamba mda wowote anarudi kwa Mola wake

Kwahiyo ndugu zangu hapana shaka yoyote wengi wetu huko nyuma hatukuishi katika ucha mungu,ukiacha ule wa mwezi wa Ramadhani,na baada ya Ramadhani tulirejea katika kuchanganya haki na batili,kama ambavyo baadhi yetu wengine wamerejea tena katika business as usual,wanaendelea na batili

Allah atuzindue,wallah huu uzima na maisha haya ya starehe fupi hapa duniani yana tudanganya sana,lakini tujue hakika sisi tupo safarini na mda wowote ule ni wenye kurejea kwa Allah azza wa jalla

Tumche Allah
 
UJUMBE WA SHUKRANI KWENU

Wallahi muitikio wenu wa kusoma uzi huu ni mkubwa sana,toka mwishoni mwa Ramadhani mpaka sasa kuna wasomaji kama 9000 wameutembelea uzi huu,toka 236k mpaka 245k

Hii inanipa hamasa kubwa sana ya kuendelea kufanya kazi hii kwa hamu kubwa,kwani najiona nina deni kubwa kwa wasomaji wangu

Allah azidi kutuongoza sote na kikubwa tuyafanyie kazi yale ambayo tunajifunza humu,kwani hakuna pepo ya msomaji au ya msikilizaji bali ipo pepo kwa ajili ya wanaofanya mambo kwa vitendo

Endelea kufuatilia uzi.....
 
Baadhi ya post zangu za zamani...

ASILI YA NENO INSHAALLAH

Wakazi wa makkah ambao ni maquraish walikuwa na mashaka juu ya Utume wa Muhammad rehma na amani ziwe juu yake, hivyo walitaka kujiridhisha je huyu kweli ni Mtume wa Mungu au laa!

Basi kwakuwa wanajua kule Madina kuna wanazuoni wa Kiyahudi au watawa wa kiyahudi na wanaijua vizuri Taurati pamoja na manabii, basi wakawatuma watu ambao ni An nadr na Uqba, waende kule wawaeleze wasifu wa Muhammad na wawaeleze yale ambayo Muhammad anawahubiria,lengo ni kutaka kujua ukweli?

Basi wakaenda kwa hao mabwana wakubwa na kuwaeleza wajihi wa Muhammad rehma na amani ziwe juu yake na yale ambayo huwa anayahubiri.

Wanachuoni wa Kiyahudi wakasema muulizeni maswali matatu ambayo tutawaambia, kama akijibu basi huyo ni Mtume na mumfuate na kama akishindwa basi huyo sio mtume anasema uwongo na mtajua namna ya kudili naye.

Basi wakaenda kwa jamaa zao na kuwapa mrejesho kisha wote wakaenda kwa Muhammad kumuuliza hayo maswali.

Swali la kwanza, huko zamani kabisa kulikuwa na vijana ambao habari zao zilikuwa zenye kuajabisha na kushtua, je hao ni vijana gani?

Swali la pili, kuna mtu ambaye alikuwa mtembezi, alitembea mashariki ya dunia na magharibi, je ni mtu gani huyo?

Swali la tatu, tueleze kuhusu roho,je roho ni nini?


Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake, kwakuwa anajua Malaika Jibril / Gabriel mara nyingi humjia na kuumpa ufunuo basi AKAWAAMBIA KUWA NITAWAJIBU KESHO.

kwa faida kidogo Malaika huyu ndio mkuu wa Malaika na ndiye ambaye tangu zama na zama kazi yake pamoja na mambo mengine ni kufikisha ufunuo kwa mitume wote tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

Haya tuendelee, zikapita siku kumi na tano hajaletewa ufunuo kutoka mbinguni, huku nako watu wamelianzisha zengwe, huyu Muhammad alisema atatupa jibu kesho lkn sasa zimepita siku kumi na tano hana majibu, watu wakaanza kuwa na mashaka na Utume wake, na yeye huku anajisikia vibaya kwakuto wajibu na kusikia maneno yao ya Shombo.

Ndio baadae akaja Malaika Jibril na kushusha suratul Kahf ambayo pamoja na mambo mengine ikajibu yale maswali.

Kwanza Mtume aliambiwa katu usiseme jambo lolote lile kuwa ntalifanya kesho ila kuongeza na kusema INSHAALLAH /MUNGU AKIPENDA, hapa tunafundishwa kuwa hakika hakuna ajuaye kesho yake isipokuwa Mwenyezi Mungu tu.

Swali kuhusu wale vijana, jibu walikuwa vijana wa pangoni ambao walikimbilia huko pangoni kuepuka jamii yao ambayo inamshirikisha Mungu, wao walikuwa wanamwamini Mungu mmoja tu, wakalazwa usingizini kwa miaka 309 kisha wakafufuliwa, habar yao ni ndefu ngoja niishie hapa.

Swali la pili, mmtembeaje aliyetembea mashariki na magharibi ya dunia ni Dhul Qarnain nae ana habar nzito, ngoja niishie hapa.

Swali la tatu, kuhusu roho ni nini, jibu ni kuwa roho elimu yake ipo kwa Mungu mwenyewe, wanadamu wamepewa sehemu ndogo sana ya elimu hiyo.
 
Baadhi ya post zangu za zamani...

ISLAMIC PHOBIA

Phobia kwa tafsir isiyo rasmi ni ile hali ya kuwa na hofu au wasiwasi juu ya jambo fulani au kitu fulani, na kumfanya huyo mwenye hofu hiyo mara akutanapo na hali hiyo basi kuwa na hofu kwakuwa tu ameamini katika akili yake kuwa jambo fulani au kitu fulani ni hatar kwake.

Bahati mbaya sana Uislamu unahusishwa moja Kwa moja na Ugaidi kwakuwa watuhumiwa namba moja wanaojihusisha na mambo hayo ni watu wenye imani ya kiislamu au majina ya kiislamu.

Kwahiyo hata pale wahalifu hawa wanapofanya uhalifu wao basi hapo moja kwa moja Uislamu unahusishwa na kibaya zaidi wahuni hawa wenye majina ya kiislamu wanapofanya uhuni wao huku wakisema Allahu Akbar (mungu mkubwa) hapo tena ndio kama wamepiga mhuri wa moto kudhibitisha hii ni agenda ya Uislamu.

Uislamu hau husiani na ugaidi kwa namna yoyote ile kwani katika uislamu ustawi ,maisha na uhai wa mwanadamu ni mambo ambayo yamepewa kipaumbele Sana, na hata zile vita halali za kupigana na madhalimu, kuna kanuni zake ni kupigana na wale tu ambao wameshika silaha katika uwanja wa vita, lakini wale ambao hawapo katika uwanja wa vita katu hawata pata madhila yoyote yale.

Na kanuni nyingine inasema hakuna kuwapiga watoto, wanawake wala wazee kwasababu makundi hayo hayawezi kushiriki katika Vita sana sana watalazimishwa na jamaa zao lkn kiuhalisia huwa ni madhaifu.

Kanuni nyingine hakuna kukata mimea kwa ujumla wake wala kuharibu majumba ya ibada ya imani za watu wengine kwa namna yoyote ile.

Swali linakuja je, hawa magaidi huwa wanafuata kanuni hizo? Kama hawafuati kanuni hizo basi hao wako mbali na Uislamu na kamwe wasihusishwe na Uislamu kwa namna yoyote ile hata kama watamtaja Allah na hata wakiwa na majina ya kiislamu.

Nakumbuka siku moja Niko bank moja sitaki kuitaja nisije nikawapa promo, nilikuwa nafungua account, na wakati huo habari kwenye vyombo vya habari ni ugaidi kwa kwenda mbele,tukiwa pale bank ikaonywesha picha moja ya mlipuko wa bomu,kuna dada mmoja akasema "siwapendi waislamu" lkn Mimi nilimuelewa kwakuwa alikula matango pori kwa kuamini waislamu ndio wenye kuua watu hovyo.

Hofu na imani ya huyu dada ndio hofu ambazo wanazo watu wengi sana juu ya uislamu, na kuwafanya watu mara pale wanapo sikia sintofahamu yoyote ikihusishwa na uislamu mara moja hupagawa na kuripuka na kusema hovyo juu ya uislamu.

Mfano mzuri ni hii ishu ya vijana kukutwa wamekusanywa sehemu na kufundishwa karate au judo, hapo moja kwa moja itahusishwa na ugaidi kwakuwa tu tayar watu wana Islamic phobia na vichwani mwao kuna kengere zinapiga na kuwakosesha amani.

Swali linakuja, je kuna ubaya wowote wa kuwa na skills za self defence? Jibu hapana na wakati mwingine itasemwa mazoezi ni afya, je kwanini linapokuja swala la vijana wa kiislamu kujifunza ujuzi huo inakuwa ni ishu? Jibu ni moja tu watu wameingia hofu na uislamu.

Mwandishi wa makala hii anasema hivi, kama kuna waislamu wanakusanyika sehemu kwa kujifunza hizo skills kwa lengo baya basi sheria ichukue mkondo wake kwakuwa Tanzania ni yetu sote na tungependa amani iendelee kutawala, lakini kama wapo kwa lengo zuri basi wasihusishwe na ugaidi kwa namna yoyote,kama itabidi wajisajili na ijulikane wanafundisha utaalamu fulani.

Tusiwe wepesi wa kujaji mamba kabla hatujajua undani wake au ukweli wake hii hupelekea sintofahamu katika jamii na kuhatarisha amani ya inchi.

Mwisho kabisa kwa Waislamu wenzangu, tuwe makini sana na baadhi ya madhehebu ambayo yanafundisha na kuleta itikadi ambazo hazi husiani na dini ya Mwenyezi Mungu, hao ni wapotoshaji na hawafai kabisa kuwa nao karibu, na ikijulikana sio watu sahihi basi mara moja waripotiwe katika vyombo vya Usalama.
 
Baadhi ya post zangu za zamani...

NDOA HUUMPA HADHI NA HESHIMA MWANADAMU


Kumekuwa na Maandiko kadhaa na mijadala kadhaaa kuhusiana na umuhimu wa ndoa na wengine wakisimamia katika kampeni Yao ya Kataa ndoa,ndoa ni utapeli na kadhalika.

ETUGRUL BEY nae ameona achangie kidogo katika Jambo hili, nianze Kwa kusema Kwanza wale ambao wanakataa ndoa hawakatai Bila sababu,Ila kuna mambo ambayo wanayaona hayako Sawa katika ndoa ndio mpaka yanawapelekea kuamini kuwa ndoa ni gareza,maumivu,mateso,usaliti na ndio chanzo cha mabalaa mbali mbali ikiwemo kutoana Uhai.

Lakini kila Jambo lina changamoto zake hapa duniani,na wakati mwingine changamoto hizo ndio sehemu ya kutufanya kukua na kukomaa zaidi.

Ndoa ndiyo ambayo inampa mwanadamu hadhi na heshima hapa duniani tofauti na viumbe wengine,viumbe wote wanasex au wanaingiliana, lakini Mwenyezi Mungu amemtofautisha mwanadamu na viumbe wengine Kwa kujaaliwa kuwepo Kwa ndoa. Kwani ndoa ndio takaso Bora na linafanya kitendo kile cha kuingiliana kiwe tofauti na viumbe wengine.

Kama hatufungamani na ndoa na kuendelea kuingiliana nje ya mpango wa Mungu basi hakika hatuna tofauti yoyote na wanyama,ingawa kimwonekano sio kama wanyama Ila kitabia ni kama wanyama.

Pamoja na changamoto mbali mbali ambazo zipo katika ndoa,lakini bado ndoa itabakia kuwa taasisi imara ya kuendeleza kizazi cha mwanadamu katika njia halali kabisa ambayo inampendeza Mungu,kwahiyo vyovyote itakavyokuwa bado ndoa ina umuhimu mkubwa Sana.

Wakataa ndoa Kwa mtazamo wangu ni watu ambao hawana Imani na Mungu kabisa,kwasababu kama ndoa ndio mpango ambao amewatayarishia wanadamu waufuate na njia salama Kwa Maisha Yao hapa duniani na kesho siku ya hesabu je wewe ni nani usie na hofu ya Mungu wako mpaka ukatae kuwepo Kwa ndoa?

Mtu yoyote ambaye ana Imani juu ya Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi anajua na kuamini kabisa njia pekee ya kukwepa dhambi ya zinaa ni kuoa au kuolewa Tu. Sasa ukiona mtu anatumia nguvu kubwa kukataa ndoa ujue huyo hamjui Mungu na hajui hatima yake itakuwaje baada ya kumaliza Mda wake hapa duniani.

Hawa ni WA kuwahurumia Sana na bahati mbaya zaidi kuna watu wengine ambao nao kichwa kichwa wanaingia katika mtego huo huo ima Kwa ushabiki Tu au kwakujua au kutokujua,naomba niwazindue Kwa kuwaambia akili za kuambiwa changanya na zako,mwisho wa siku kila mtu atavuna anacho panda,hapo hakutakuwa na Sisi bali utakuwa wewe Tu na Mola wako.

Hoja inaweza kuja mbona kuna watu wameoa na bado wanazini? Hayo ni makosa mengine ambayo bado mwanadamu anaendelea kumkosea Mola wake. Tunapo kusudia kuoa INA maana sasa tunaachana na zinaa na kuwa katika ibada ya ndoa takatifu,tunakuwa katika njia ambayo inampendeza Mola wetu.

Na ndoa ni ibada, kwasababu ibada ni Matendo mazuri au maneno mazuri ambayo yanampendeza Allah, na unapata thawabu Kwa Jambo lolote la ibada. Kwa mfano unaposex na mumeo au mkeo ujue unapata thawabu,kwasababu unafanya kitendo ambacho kinampendeza Mungu,Maswahaba walipo sikia hili Kwa Mtume (s.a.w) walistaajabu Sana,wakamuuliza Nabii "yaani tunastarehe wenyewe na wake zetu na bado tunapata thawabu"?

Nabii akawajibu " vipi kama mngezini je msingeandikiwa madhambi"? Wakajibu ndio tungeandikiwa madhambi basi akawaambia na anayemwingilia mkewe WA halali basi anapata thawabu. Naam mpaka hapo naona umepata picha ni Kwa kiasi gani ndoa ni Jambo la muhimu na la kiibada.

Kwa mfano Kwa Sisi Waislamu, ndoa ni nusu ya Dini,Kwa maana ambaye ameoa basi ana asilimia 50 ya Dini na 50 iliyobaki ni kufanya ibada nyingine mbali mbali,kwasababu kwenye ndoa kunapatikana familia ambayo inatakiwa iishi katika misingi ya Dini na kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu,kifupi ndoa ni taasisi ambayo ina mambo mengi ndani yake ambayo mume na mke watakuja kuulizwa je walisimamia vipi malezi ya watoto wao na mambo kadhaa WA kadhaa.

Je tufanye nini ili taasisi ya ndoa iwe imara na hatimaye ifikie malengo yake.

Kwanza nianze na vigezo vinne ambavyo ndio sababu ya kuoa au kuolewa.

1) Tunaoa kutokana na uzuri WA mhusika - uzuri unao zungumziwa hapa ni uzur ambao wewe mhusika unakupendeza Kwa mwanamke wako au mwanaume wako,kwamba Oa mwanamke ambaye hata ukimtazama basi nafsi yako inafurahi/na mwanamke vile vile.

2) Tunaoa kutokana na Nasabu/Ukoo husika - nenda kaoe kwenye nasabu au ukoo ambao unafahamika Tabia zake na mwenendo wake,kwani kuna koo nyingine ni mtihani Sana,huko maugomvi na mabalaa ni sehemu ya Maisha Yao,na Tabia huwa inafuata mkondo.

3) Tunaoa kutokana na Mali - wakati mwingine tunaenda kuoa kutokana na Mali au kuolewa kutokana na Mali za mhusika,sasa hapa ndio Pana mitihani Sana,unajua kabisa Fulani humpendi lkn unafuata Mali zake au hela zake,ndio baadae hela au Mali zikikata balaa linaanza.

4) Na mwisho Tunaoa kutokana na Dini ya mhusika - hapa ndio penye Jambo la muhimu Sana,Yani cheza kote lakini hapa usikosee, hakika mwenye hofu na Imani ya Mungu mara nyingi ni mtu Bora Sana katika kuanzisha nae Maisha ya ndoa. Kwani huyu atakulindia Mali yako,atajihifadhi na machafu Kwa maana hata zini au kuchepuka hata ukiwa mbali nae,na hata malezi ya watoto wako yatakuwa katika mikono salama kabisa.

Watu wengi hapa ndio tunafeli na ndio maana ndoa zimekuwa mitihani kila kukicha,tunakutana huko vyuoni,makazini na mabarabarani bila hata kuangalia vigezo muhimu ambavyo vingeweza kutusaidia kuwa na ndoa imara huko mbeleni.

Mifano tunayo huko zamani wazazi walikuwa Makini Sana katika kuangalia wachumba sahihi Kwa watoto wao na hata ndoa zao zilidumu Sana kwakuwa zilifuata mifumo sahihi ya kutambua mtu sahihi na kufunga ndoa sahihi.

Nashauri kabla ya kueneza kampeni yako ya Kataa ndoa,sijui ndoa ni utapeli sijui ndoa ni batili ebu tafakari hayo niliyoandika hapo na fanya tathimini na uone tatizo liko wapi.
 
UJUMBE WA LEO:

Hakika Swala ikiswaliwa vizuri humkinga mswaliji kutokana na maovu na machafu
 
Back
Top Bottom