Ramadhan Special Thread
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn





باب توقير العلماء والكبار وأهل الفضل وتقديمهم عَلَى غيرهم ورفع مجالسهم وإظهار مرتبتهم

044-Mlango Wa Kuwaheshimu Wanazuoni, Wakubwa na Watu Watukufu na Kuwatanguliza Juu ya Wengine, Kutukuza Vikao Vyao na Kudhihirisha Utukufu Wao



Alhidaaya.com





قَالَ الله تَعَالَى:

قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ۗ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٩﴾

Sema: Je, wanalingana sawa wale wanaouja na wale wasiojua? Hakika wanakumbuka wenye akili tu.[Az-Zumar: 9]







Hadiyth – 1

وعن أَبي مسعودٍ عقبةَ بن عمرو البدري الأنصاري رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( يَؤُمُّ القَوْمَ أقْرَؤُهُمْ لِكِتَابِ الله ، فَإنْ كَانُوا في القِراءةِ سَوَاءً ، فأَعْلَمُهُمْ بِالسُّنَّةِ ، فَإنْ كَانُوا في السُّنَّةِ سَوَاءً ، فَأَقْدَمُهُمْ هِجْرَةً ، فَإنْ كَانُوا في الهِجْرَةِ سَوَاءً ، فَأقْدَمُهُمْ سِنّاً ، وَلاَ يُؤمّنَّ الرَّجُلُ الرَّجُلَ في سُلْطَانِهِ ، وَلاَ يَقْعُدْ في بَيْتِهِ عَلَى تَكْرِمَتِهِ إلاَّ بِإذْنهِ )) رواه مسلم .

وفي رواية لَهُ : (( فَأقْدَمُهُمْ سِلْماً )) بَدَلَ (( سِنّاً )) : أيْ إسْلاماً . وفي رواية : (( يَؤُمُّ القَومَ أقْرَؤُهُمْ لِكِتَابِ اللهِ ، وَأقْدَمُهُمْ قِراءةً ، فَإنْ كَانَتْ قِرَاءتُهُمْ سَوَاءً فَيَؤُمُّهُمْ أقْدَمُهُمْ هِجْرَةً ، فَإنْ كَانُوا في الهِجْرَةِ سَواء ، فَليَؤُمُّهُمْ أكْبَرُهُمْ سِنّاً )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Mas'uud 'Uqbah bin 'Amru Al-Badriy Al-Answaarriyy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Aswalishe msomi wao wa Kitabu cha Allaah. Ikiwa wako sawa katika kisomo, basi mjuzi zaidi katika Sunnah. Ikiwa wako sawa katika Sunnah, wa mwanzo wao kuhama. Wakiwa sawa katika kuhama, basi mkubwa wao wa umri, Wala mtu hamswalishi mwingine katika mamlaka yake ila kwa idhini yake, wala asikae katika utukufu wake ila kwa ruhusa yake." [Muslim]

Katika riwaayah yake: "Wa mwanzo kusilimu" badala ya "umri mkubwa."

Katika riwaayah nyengine: "Aswalisha watu msomi wao kwa Kitabu cha Allaah , na wa mwanzo wao kusoma,. Ikiwa kisomo chao ni sawa, basi aswalishe wa mwanzo wao kuhama. Ikiwa wapo sawa katika kuhama, basi mkubwa wao."







Hadiyth – 2

وعن أَبي مسعودٍ عقبةَ بن عمرو البدري الأنصاري رضي الله عنه، قَالَ : كَانَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يَمْسَحُ مَنَاكِبَنَا في الصَّلاةِ ، ويَقُولُ : (( اسْتَوُوا وَلاَ تَخْتَلِفُوا ، فَتَخْتَلِفَ قُلُوبُكُمْ ، لِيَلِني مِنْكُمْ أُولُوا الأحْلاَمِ وَالنُّهَى ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Mas'uud 'Uqbah bin 'Amru Al-Badriy Al-Answaarriyy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa akifuta mabega yetu katika swalaah na kusema: "Nyookeni wala msikhitilafiane zikatofautiana nyoyo zenu. Wanikaribie wenye utambuzi na akili miongoni mwenu, kisha wanaowafuatia wao, kisha wanaowafuatia wao." [Muslim]







Hadiyth – 3

وعن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( لِيَلِني مِنْكُمْ أُولُوا الأحْلام وَالنُّهَى ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ )) ثَلاثاً (( وَإيَّاكُمْ وَهَيْشَاتِ الأسْوَاق )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwake 'Abdillaahi bin Mas'uud (Radhwiyah Allaahu 'anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Wanikaribie wenye akili na utambuzi miongoni mwenu, kisha wanaowafuatia wao (mara tatu) na nawatahadharisheni sana na vurumai na tangamano la watu wa masokoni." [Muslim]







Hadiyth – 4

وعن أَبي يَحيَى ، وقيل : أَبي محمد سهلِ بن أَبي حَثْمة - بفتح الحاءِ المهملة وإسكان الثاءِ المثلثةِ - الأنصاري رضي الله عنه، قَالَ : انطَلَقَ عَبدُ اللهِ بنُ سهْلٍ وَمُحَيِّصَة بن مَسْعُود إِلَى خَيْبَرَ وَهِيَ يَومَئذٍ صُلْحٌ ، فَتَفَرَّقَا ، فَأتَى مُحَيِّصَةُ إِلَى عبدِ اللهِ ابنِ سهل وَهُوَ يَتشَحَّطُ في دَمِهِ قَتِيلاً ، فَدَفَنَهُ ، ثُمَّ قَدِمَ المَدِينَةَ فَانْطَلَقَ عَبدُ الرحمان ابنُ سهل وَمُحَيِّصَةُ وحوَيِّصَةُ ابْنَا مَسْعُودٍ إِلَى النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، فَذَهَبَ عَبدُ الرحمان يَتَكَلَّمُ ، فَقَالَ : (( كَبِّرْ كَبِّرْ )) وَهُوَ أحْدَثُ القَوم ، فَسَكَتَ ، فَتَكَلَّمَا ، فَقَالَ : (( أتَحْلِفُونَ وتَسْتَحِقُّونَ قَاتِلَكُمْ ؟ … )) وذكر تمام الحديث . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Amesema Abu Yahyaa au Abu Muhammad Sahl bin Abi Hathmah: 'Abdillaahi bin Sahl, Muhayyiswah bin Mas'uud waliekea Khaybar wakati wa sulhu. Wakaachana. Muhayyiswah akamjia 'Abdillaahi bin Sahl akiwa ameolewa damu ameuwawa, Akamzika akarudi Madiynah. Wakaenda kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), 'Abdur-Rahman bin Sahl, Muhayyiswah na Huwayyiswah watoto wa Mas'uud. 'Abdur-Rahman akazungumza. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: Azungumze mkubwa wenu" Nae alikuwa mdogo wao, akanyamaza. Wakazungumza wawili wao. Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Je, mtaapa ili mstahiki fidia kwa muuaji wenu?" Akataja ukamilifu wa Hadiyth. [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 5

وعن جابر رضي الله عنه: أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَجْمَعُ بَيْنَ الرَّجُلَيْنِ مِنْ قَتْلَى أُحُد يَعْنِي في القَبْرِ ، ثُمَّ يَقُولُ : (( أيُّهُما أكْثَرُ أخذاً للقُرآنِ ؟ )) فَإذَا أُشيرَ لَهُ إِلَى أحَدِهِمَا قَدَّمَهُ في اللَّحْدِ . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akijumuisha watu wawili katika waliouliwa Uhud, yaani katika kaburi; kisha hutuuliza: "Ni yupi kati yao amehifadhi Qur-aan?" Anapoashiriwa mmoja wao anamtanguliza katika mwana ndani." [Al-Bukhaariy]







Hadiyth – 6

وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( أرَانِي فِي المَنَامِ أتَسَوَّكُ بِسِوَاكٍ ، فَجَاءنِي رَجُلانِ ، أحَدُهُما أكبر مِنَ الآخرِ ، فَنَاوَلْتُ السِّوَاكَ الأصْغَرَ ، فَقِيلَ لِي : كَبِّرْ ، فَدَفَعْتهُ إِلَى الأكْبَرِ مِنْهُمَا )) رواه مسلم مسنداً والبخاري تعليقاً .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nilijiona usingizini nikipiga msuwaki. Wakanijia watu wawili, mmoja wao ni mkubwa kuliko mwenziwe. Nikataka kumpa msuwaki yule mdogo, hapo nikaambiwa: "Mtangulize mkubwa". Nikampatia huyo mkubwa." [Muslim na Al-Bukhaariy]







Hadiyth – 7

وعن أَبي موسى رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( إنَّ مِنْ إجْلالِ اللهِ تَعَالَى : إكْرَامَ ذِي الشَّيْبَةِ المُسْلِمِ ، وَحَامِلِ القُرآنِ غَيْرِ الغَالِي فِيهِ ، وَالجَافِي عَنْهُ ، وَإكْرَامَ ذِي السُّلْطَانِ المُقْسِط )) حديث حسن رواه أَبُو داود .

Imepokewa kutoka kwa Abu Muusa kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika katika Kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aala) ni kumkirimu mzee Muislamu, na kuiacha mbali bila kuitumia, na kumkirimu kiongozi muadilifu". Hadiyth Hassan. [Abu Daawuud]







Hadiyth – 8

وعن عمرو بن شعيب ، عن أبيه ، عن جده رضي الله عنهم، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( لَيْسَ مِنَّا مَنْ لَمْ يَرْحَمْ صَغِيرنَا ، وَيَعْرِفْ شَرَفَ كَبيرِنَا )) حديث صحيح رواه أَبُو داود والترمذي ، وَقالَ الترمذي : (( حديث حسن صحيح )) .

وفي رواية أبي داود : (( حَقَّ كَبيرِنَا )) .

Na imepokewa kutoka kwa 'Amru bin Shu'ayb kutoka kwa babake kutoka kwa babu yake (Radhwiyah Allaahu 'anhuma) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Si katika sisi asiye warehemu wadogo wetu na kutambua heshima (utukufu) wa wakubwa wetu." Hadiyth Swahiyh iliyonukuliwa na Abu-Daawuud na At-Tirmidhiy, ambaye amesema: Hadiyth Hassan Swahiyh.







Hadiyth – 9

وعن ميمون بن أَبي شَبيب رحمه الله : أنَّ عائشة رَضي الله عنها مَرَّ بِهَا سَائِلٌ ، فَأعْطَتْهُ كِسْرَةً ، وَمَرَّ بِهَا رَجُلٌ عَلَيهِ ثِيَابٌ وَهَيْئَةٌ ، فَأقْعَدَتهُ ، فَأكَلَ ، فقِيلَ لَهَا في ذلِكَ ؟ فقَالتْ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( أنْزِلُوا النَّاسَ مَنَازِلَهُمْ )) رواه أبو داود . لكن قال : ميمون لم يدرك عائشة . وقد ذكره مسلم في أول صحيحه تعليقاً فقال : وذكر عن عائشة رضي الله عنها قالت : أمرنا رسول الله صلى الله عليه وسلم أن ننـزل الناس منازلهم ، وَذَكَرَهُ الحَاكِمُ أَبُو عبد الله في كتابه (( مَعرِفَة عُلُومِ الحَديث )) وَقالَ : (( هُوَ حديث صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwake 'Maymuuna bin Abu Shabiyb (Rahimmahu Allaah) kuwa 'Aa'ishah (Radhwiyah Allaahu 'anhaa) alipitiwa na mwombaji, naye akampatia kisra (mkate). Baadaye, akapita mtu aliyevaa vizuri, akamuomba, naye ('Aa'ishah) akamkalisha chini na akampatia chakula ili ale. Akaulizwa kuhusu hilo, naye akasema: "Rasuli wa Allaah amesema: Wawekeni watu katika vyeo vyao." [Abu Daawuud,aliyesema Maymuun hakukutana na 'Aa'ishah] Na imetajwa na Muslim mwanzo wa Sahihi yake, akasema: Na imetajwa kuwa 'Aa'ishah (Radhwiyah Allaahu 'anhaa) amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuamuru kuweka watu katika vyeo vyao. Na Allaah ametuamuru kuwaweka watu kwa vyeo vyao." Ameitaja hiyo Al-Haakim Abu 'Abdillaahi katika kitabu chake (Ma'rifatu 'Uluumil Hadiyth) Akasema ni Hadiyth Swahiyh.







Hadiyth – 10

وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، قَالَ : قَدِمَ عُيَيْنَةُ بنُ حِصْن ، فَنَزَلَ عَلَى ابْنِ أخِيهِ الحُرِّ بنِ قَيسٍ ، وَكَانَ مِنَ النَّفَرِ الَّذِينَ يُدْنِيهِمْ عُمرُ رضي الله عنه، وَكَانَ القُرَّاءُ أصْحَاب مَجْلِس عُمَرَ وَمُشاوَرَتِهِ ، كُهُولاً كاَنُوا أَوْ شُبَّاناً ، فَقَالَ عُيَيْنَةُ لابْنِ أخيهِ : يَا ابْنَ أخِي ، لَكَ وَجْهٌ عِنْدَ هَذَا الأمِيرِ ، فَاسْتَأذِنْ لِي عَلَيهِ ، فاسْتَأذَن له ، فَإذِنَ لَهُ عُمَرُ رضي الله عنه، فَلَمَّا دَخَلَ قَالَ : هِي يَا ابنَ الخَطَّابِ ، فَواللهِ مَا تُعْطِينَا الْجَزْلَ ، وَلا تَحْكُمُ فِينَا بالعَدْلِ ، فَغَضِبَ عُمَرُ رضي الله عنه حَتَّى هَمَّ أنْ يُوقِعَ بِهِ ، فَقَالَ لَهُ الحُرُّ : يَا أميرَ المُؤْمِنينَ ، إنَّ الله تَعَالَى قَالَ لِنَبيِّهِ صلى الله عليه وسلم: ( خُذِ الْعَفْوَ وَأْمُرْ بِالْعُرْفِ وَأَعْرِضْ عَنِ الْجَاهِلِينَ ) وَإنَّ هَذَا مِنَ الجَاهِلِينَ . واللهِ مَا جَاوَزَهاَ عُمَرُ حِينَ تَلاَهَا عليه ، وكَانَ وَقَّافاً عِنْدَ كِتَابِ اللهِ تَعَالَى . رواه البخاري .

Amesema Ibn 'Abbaas (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) Alikuja 'Uyaynah bin Hiswnakashukia kwa mtoto wa nduguye, Al-Hurr bin Qays, mtu wa karibu kwa 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwa ubora wake. Kamati ya shuura ya majlis ya 'Umar walikuwa wasomi, wazee na vijana. 'Uyaynah akamwambia mtoto wa nduguye: "Eemtoto wa ndugu yangu! Wewe una hadhi kwa huyu Amiri, niombee ruhusa nimuone." Akamuombea idhini, na 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu) akamruhusu Alipoingia alisema: "Hiy (kutishia), ee Ibn Al-Khatwtwaab: Wa-Allaahi hutupi zawadi wala hutuhukumu kwa uadilifu." Akakasirika 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu) akakaribia kumwadhibu, Al'Hurr akamwambia: "Ee Amiri wa Waumini! "Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aala) Alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Shikamana na usamehevu, na amrisha mema na jiepushe na majahili." [Al-A'raaf: 199] na huyu ni miongoni mwa wajinga." Wa-Allaahi, aliposikia maneno hayo alitulia tuli, kwani yeye ni mtu mwenye kufuata kabisa Kitabu cha Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aala). [Al-Bukhaariy]







Hadiyth – 11

وعن أَبي سعيد سَمُرة بنِ جُندب رضي الله عنه، قَالَ : لقد كنت عَلَى عَهْدِ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم غُلاماً ، فَكُنْتُ أحْفَظُ عَنْهُ ، فَمَا يَمْنَعُنِي مِنَ القَوْلِ إلاَّ أنَّ هاهُنَا رِجَالاً هُمْ أسَنُّ مِنِّي . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

AmesemaAbu Sa'iyd Samurah bin Jundub (Radhwiyah Allaahu 'anhu): Hakika nilikuwa kijana katika zama za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na nilikuwa ni mwenye kuhifadhi kutoka kwake. Hakunikataza mimi kuzungumza ila kulikuwepo na watu wakubwa (kiumri) kuniliko." [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 12

وعن أنس رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( مَا أكْرَمَ شَابٌّ شَيْخاً لِسِنِّهِ إلاَّ قَيَّضَ الله لَهُ مَنْ يُكْرِمُهُ عِنْدَ سِنِّه )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث غريب )) .

Na imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hatomkirimu kijana mzee kwa ajili ya umri wake isipokuwa Allaah Atamtolea atakaye mkirimu katika uzee wake." [At-Tirmidhiy, na akasema Hadiyth Ghariyb
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn





باب زيارة أهل الخير ومجالستهم وصحبتهم ومحبتهم وطلب زيارتهم والدعاء منهم وزيارة المواضع الفاضلة

045-Mlango Wa Kuwazuru Watu wa Kheri, Kukaa Nao, Kuhusubiana Nao na Kuwapenda



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:

وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِفَتَاهُ لَا أَبْرَحُ حَتَّىٰ أَبْلُغَ مَجْمَعَ الْبَحْرَيْنِ أَوْ أَمْضِيَ حُقُبًا ﴿٦٠﴾ إِلَى قوله تَعَالَى : قَالَ لَهُ مُوسَىٰ هَلْ أَتَّبِعُكَ عَلَىٰ أَن تُعَلِّمَنِ مِمَّا عُلِّمْتَ رُشْدًا ﴿٦٦﴾

Na pindi Muwsaa alipomwambia kijana wake: Sitoacha kuendelea mpaka nifikie zinapokutana bahari mbili, na nitaendelea muda mrefu. Hadi Kauli Yake T'aalaa: ...Basi walipofika zinapoungana bahari mbili, walimsahau samaki wao; naye akachukua njia yake baharini akiponyoka chini kwa chini. [Al-Kahf: 60-66]



وَاصْبِرْ نَفْسَكَ مَعَ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ ﴿٢٨﴾

Na isubirishe nafsi yako pamoja na wale wanaomuomba Rabb wao asubuhi kabla jua kucha na jioni, wanataka Wajihi Wake. [Al-Kahf: 28]







Hadiyth – 1

وعن أنس رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ أَبُو بكر لِعُمَرَ رضي الله عنهما بَعْدَ وَفَاةِ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم: انْطَلِقْ بِنَا إِلَى أُمِّ أيْمَنَ رضي الله عنها نَزُورُهَا كَمَا كَانَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يَزُورُهَا ، فَلَمَّا انْتَهَيَا إِلَيْهَا ، بَكَتْ ، فَقَالاَ لَهَا : مَا يُبْكِيكِ ؟ أمَا تَعْلَمِينَ أنَّ مَا عِنْدَ اللهِ خَيْرٌ لرَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم، فَقَالَتْ : مَا أبْكِي أَنْ لاَ أَكُونَ أَعْلَم أنَّ مَا عِنْدَ الله تَعَالَى خَيْرٌ لرسول الله صلى الله عليه وسلم، ولَكِنْ أبكي أنَّ الوَحْيَ قدِ انْقَطَعَ مِنَ السَّماءِ ، فَهَيَّجَتْهُمَا عَلَى البُكَاءِ ، فَجَعَلا يَبْكِيَانِ مَعَهَا . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Abu Bakr (Radhwiyah Allaahu 'anhu) alimwambia 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu) baada ya kuanga dunia kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Twende tukamzuru Ummu Ayman (Radhwiyah Allaahu 'anhaa) kama alivyokuwa akimzuru Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)." Walipofika kwake akalia. Wakamwambia: "Nini kinachokuliza? "Kwani hujui Allaah Aliyomwandalia Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni bora?" Akasema: "Mimi nami silii kwa kuwa sijui yalio kwa Allaah ni bora kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), bali nalia kwa sababu wahyi umekatika toka mbinguni." Wakawa wanalia pamoja naye." [Muslim]









Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم: (( أنَّ رَجُلاً زَارَ أَخَاً لَهُ في قَريَة أُخْرَى ، فَأرْصَدَ الله تَعَالَى عَلَى مَدْرَجَتِهِ مَلَكاً ، فَلَمَّا أتَى عَلَيهِ ، قَالَ : أيْنَ تُريدُ ؟ قَالَ : أُريدُ أخاً لي في هذِهِ القَريَةِ . قَالَ : هَلْ لَكَ عَلَيهِ مِنْ نِعْمَة تَرُبُّهَا عَلَيهِ ؟ قَالَ : لا ، غَيْرَ أنِّي أحْبَبْتُهُ في الله تَعَالَى ، قَالَ : فإنِّي رَسُول الله إلَيْكَ بَأنَّ الله قَدْ أَحَبَّكَ كَمَا أحْبَبْتَهُ فِيهِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: " Mtu mmoja alimzuru nduguye katika kijiji kingine. Allaah akamwakilishia Malaika njiani. Alipomfikia alisema: "Unaelekea wapi?" Akasema: "Namtaka ndugu yangu katika kijiji hiki." Akasema: "Una neema yeyote unaipata kwake?" Akasema: "La, isipokuwa mimi nampenda kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa)." Akasema: "Mimi ni mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwako; kuwa Allaah anakupenda kama ulivyompenda ndugu yako kwa ajili Yake." [Muslim]









Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( مَنْ عَادَ مَرِيضاً أَوْ زَارَ أخاً لَهُ في الله ، نَادَاهُ مُنَادٍ : بِأنْ طِبْتَ ، وَطَابَ مَمْشَاكَ ، وَتَبَوَّأتَ مِنَ الجَنَّةِ مَنْزِلاً )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن )) ، وفي بعض النسخ : (( غريب )) .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote mwenye kumtembelea mgonjwa au akamzuru ndugu yake kwa ajili ya Allaah, anaita mwenye kuita: Uwe na furaha, na kwenda kwako kubarikiwe na utunukiwe cheo Peponi." [At-Tirmidhy], ambaye amesema hii ni Hadiyth Hassan, na katika baadhi ya nuskha ni Hadiyth Ghariib (Ngeni)









Hadiyth – 4

وعن أَبي موسى الأشعري رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِنَّمَا مَثلُ الجَلِيسِ الصَّالِحِ وَجَلِيسِ السُّوءِ ، كَحَامِلِ المِسْكِ ، وَنَافِخِ الْكِيرِ ، فَحَامِلُ الْمِسْكِ : إمَّا أنْ يُحْذِيَكَ ، وَإمَّا أنْ تَبْتَاعَ مِنْهُ ، وَإمَّا أنْ تَجِدَ مِنْهُ ريحاً طَيِّبَةً ، وَنَافِخُ الكِيرِ : إمَّا أنْ يُحْرِقَ ثِيَابَكَ ، وَإمَّا أنْ تَجِدَ مِنْهُ رِيحاً مُنْتِنَةً )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika mfano wa kikao kizuri na kikao kiovu ni kama mfano wa mchukuaji (mwuzaji) manukato na mfuaji vyuma. Ama mbebaji manukato ima atakupatia (hidaya) au utanunua kutoka kwake au utapata harufu nzuri. Na kwa mfuaji chuma, ima atakuunguzia nguo yako au utapata harufu mbaya kutoka kwake." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]







Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( تُنْكَحُ المَرْأَةُ لأَرْبَعٍ : لِمَالِهَا ، وَلِحَسَبِهَا ، وَلِجَمَالِهَا ، وَلِدِينِهَا ، فَاظْفَرْ بِذاتِ الدِّينِ تَربَتْ يَدَاك )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwanamke huolewa kwa sababu nne: Mali yake, nasaba yake, uzuri wake na Dini yake. Tafuta yule mwenye Dini, isije ikafukarika mikono yako (yaani ili upate kubarikiwa)." [Al-Bukhaariy na Muslim]









Hadiyth – 6

وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم لِجبريل : (( مَا يَمْنَعُكَ أنْ تَزُورنَا أكثَر مِمَّا تَزُورَنَا ؟ )) فَنَزَلَتْ : ( وَمَا نَتَنَزَّلُ إِلاَّ بِأَمْرِ رَبِّكَ لَهُ مَا بَيْنَ أَيْدِينَا وَمَا خَلْفَنَا وَمَا بَيْنَ ذَلِكَ ) [ مريم : 64 ] رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) kuwa amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia Jibriyl: "Ni kitu gani kinachokuzuilia kutuzuru kwa wingi zaidi kuliko unavyoturuzuku sasa." Hapo ikateremka ayah inayosema: (Na (sisi Malaika) hatuteremki ila kwa amri ya Rabb wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Ni Yake Yeye yaliyoko mbele yetu, na yaliyoko nyuma yetu, na yaliyoko baina ya hayo). [Maryam: 64] [Al-Bukhaariy]









Hadiyth – 7

وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( لا تُصَاحِبْ إلاَّ مُؤْمِناً ، وَلاَ يَأْكُلْ طَعَامَكَ إلاَّ تَقِيٌّ )) . رواه أَبُو داود والترمذي بإسناد لا بأس بِهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Msiwe pamoja isipokuwa na Muumini na wala asile chakula chako isipokuwa mcha Mungu." [Abu Daawuud na At-Tirmidhy, kwa Isnaad ambayo si mbaya]







Hadiyth – 8

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( الرَّجُلُ عَلَى دِينِ خَلِيلِهِ ، فَليَنْظُرْ أَحَدُكُمْ مَنْ يُخَالِلُ )) رواه أَبُو داود والترمذي بإسناد صحيح ، وَقالَ الترمذي : (( حديث حسن )) .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtu anakuwa katika Dini ya rafiki yake, basi atizame mmoja wenu anayefanya urafiki naye." [Abu Daawuud na At-Tirmidhy na amesema kuwa hii ni Hadiyth Hasan]







Hadiyth – 9

وعن أَبي موسى الأشعري رضي الله عنه: أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( المَرْءُ مَعَ مَنْ أَحَبَّ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية : قيل للنبي صلى الله عليه وسلم: الرَّجُلُ يُحبُّ القَومَ وَلَمَّا يَلْحَقْ بِهِمْ ؟ قَالَ : (( المَرْءُ مَعَ مَنْ أَحَبَّ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtu anakuwa pamoja na wale anaowapenda." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na katika riwaayah nyengine amesema: aliambiwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Mtu anawapenda watu lakini hatangamani nao?" Akasema: "Mtu anakuwa pamoja na wale aanowapenda."







Hadiyth – 10

وعن أنس رضي الله عنه: أنَّ أعرابياً قَالَ لرسول الله صلى الله عليه وسلم: مَتَى السَّاعَةُ ؟ قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( مَا أعْدَدْتَ لَهَا ؟ )) قَالَ : حُبَّ الله ورسولهِ ، قَالَ : (( أنْتَ مَعَ مَنْ أحْبَبْتَ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ ، وهذا لفظ مسلم .

وفي رواية لهما : مَا أعْدَدْتُ لَهَا مِنْ كَثيرِ صَوْمٍ ، وَلاَ صَلاَةٍ ، وَلاَ صَدَقَةٍ ، وَلَكِنِّي أُحِبُّ الله وَرَسُولَهُ .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) ya kwamba Mbedui mmoja alimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Lini Qiyaamah?" Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: "Je, umejiandalia nini?" Akasema: "Mapenzi ya Allaah na Rasuli Wake." Akasema: "Wewe uko pamoja na unaowapenda." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud na At-Tirmidhiy]. Na hii ni lafdhi ya Muslim.

Na katika riwaayah ya Al-Bukhaariy na Muslim: "Sijajiandaa kwa kwa hicho Qiyaamah kwa funga nyingi wala Swalaah na Swadaqah nyingi lakini mimi nampenda Allaah na Rasuli Wake."







Hadiyth – 11

وعن ابن مسعود رضي الله عنه، قَالَ : جاء رجلٌ إلى رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ: يَا رَسُول الله ، كَيْفَ تَقُولُ في رَجُلٍ أَحَبَّ قَوْماً وَلَمْ يَلْحَقْ بِهِمْ ؟ فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( المَرْءُ مَعَ مَنْ أحَبَّ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uud (Radhwiyah Allaahu 'anhu) ambaye amesema: "Alikuja mtu kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia: "Ee Rasuli wa Allaah unasemaje kuhusu mtu ambaye anawapenda watu lakini hajatangamana nao? Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Mtu anakuwa pamoja na wale anaowapenda." [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 12

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( النَّاسُ مَعَادِنٌ كَمَعَادِنِ الذَّهَبِ وَالفِضَّةِ ، خِيَارُهُمْ في الجَاهِلِيَّةِ خِيَارُهُمْ في الإسْلاَمِ إِذَا فَقهُوا ، وَالأرْوَاحُ جُنُودٌ مُجَنَّدَةٌ ، فَمَا تَعَارَفَ مِنْهَا ائْتَلَفَ ، ومَا تَنَاكَرَ مِنْهَا اخْتَلَفَ )) رواه مسلم .

وروى البخاري قوله: (( الأَرْوَاحُ … )) إلخ مِنْ رواية عائشة رضي الله عنها .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Watu ni kama madini ya dhahabu na fedha, mbora wao katika ujahiliya (zama za ujinga) anakuwa mbora katika Uislamu anapokuwa na ufahamu (wa Dini). Na roho zao zinakuwa kama kundi la jeshi, miongoni mwao ni wale wenye sifa zilizosawa, hivyo kuchanganyika na kuwa pamoja na wale wenye sifa tofauti wanatengana na wenziwao." [Muslim] .

Al-Bukhaariy amepokea kauli: "Roho" mpaka mwisho kuwa hii ni riwaayah ya 'Aaishah (Radhwiyah Allaahu 'anhaa).







Hadiyth – 13

وعن أُسَيْر بن عمرو ، ويقال : ابن جابر وَهُوَ - بضم الهمزة وفتح السين المهملة - قَالَ : كَانَ عُمَرُ بْنُ الخَطَّابِ رضي الله عنه إِذَا أتَى عَلَيهِ أمْدَادُ أهْلِ اليَمَنِ سَألَهُمْ : أفِيكُمْ أُوَيْسُ بْنُ عَامِرٍ ؟ حَتَّى أتَى عَلَى أُوَيْسٍ رضي الله عنه ، فَقَالَ لَهُ : أنْتَ أُوَيْسُ ابْنُ عَامِر ؟ قَالَ : نَعَمْ ، قَالَ : مِنْ مُرَادٍ ثُمَّ مِنْ قَرَنٍ ؟ قَالَ : نَعَمْ . قَالَ : فَكَانَ بِكَ بَرَصٌ ، فَبَرَأْتَ مِنْهُ إلاَّ مَوْضِعَ دِرْهَمٍ ؟ قَالَ : نَعَمْ . قَالَ : لَكَ وَالِدةٌ ؟ قَالَ : نَعَمْ . قَالَ : سَمِعْتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( يَأتِي عَلَيْكُمْ أُويْسُ بْنُ عَامِرٍ مَعَ أمْدَادِ أهْلِ اليَمَنِ مِنْ مُرَادٍ ، ثُمَّ مِنْ قَرَنٍ كَانَ بِهِ بَرَصٌ ، فَبَرَأَ مِنْهُ إلاَّ موْضِعَ دِرْهَمٍ ، لَهُ وَالدةٌ هُوَ بِهَا بَرٌّ لَوْ أقْسَمَ عَلَى الله لأَبَرَّهُ ، فإنِ اسْتَطَعْتَ أنْ يَسْتَغْفِرَ لَكَ فَافْعَل )) فَاسْتَغْفِرْ لي فَاسْتَغْفَرَ لَهُ ، فَقَالَ لَهُ عُمَرُ : أيْنَ تُريدُ ؟ قَالَ : الكُوفَةَ ، قَالَ : ألاَ أكْتُبُ لَكَ إِلَى عَامِلِهَا ؟ قَالَ : أكُونُ في غَبْرَاءِ النَّاسِ أَحَبُّ إِلَيَّ ، فَلَمَّا كَانَ مِنَ العَامِ المُقْبِلِ حَجَّ رَجُلٌ مِنْ أشْرَافِهِمْ ، فَوافَقَ عُمَرَ ، فَسَألَهُ عَنْ أُوَيْسٍ ، فَقَالَ : تَرَكْتُهُ رَثَّ البَيْتِ قَليلَ المَتَاع ، قَالَ : سَمِعْتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، يقولُ : (( يَأتِي عَلَيْكُمْ أُوَيْسُ بْنُ عَامِرٍ مَعَ أمْدَادٍ مِنْ أهْلِ اليَمَنِ مِنْ مُرَادٍ ، ثُمَّ مِنْ قَرَنٍ ، كَانَ بِهِ بَرَصٌ فَبَرَأَ مِنْهُ إلاَّ مَوضِعَ دِرْهَمٍ ، لَهُ وَالِدَةٌ هُوَ بِهَا بَرٌّ لَوْ أقْسَمَ عَلَى اللهِ لأَبَرَّهُ ، فَإنِ اسْتَطْعتَ أنْ يَسْتَغْفِرَ لَكَ ، فَافْعَلْ )) فَأتَى أُوَيْساً ، فَقَالَ : اسْتَغْفِرْ لِي . قَالَ : أنْتَ أحْدَثُ عَهْداً بسَفَرٍ صَالِحٍ ، فَاسْتَغْفِرْ لي . قَالَ : لَقِيتَ عُمَرَ ؟ قَالَ : نَعَمْ ، فاسْتَغْفَرَ لَهُ ، فَفَطِنَ لَهُ النَّاسُ ، فَانْطَلَقَ عَلَى وَجْهِهِ . رواه مسلم .

وفي رواية لمسلم أيضاً عن أُسَيْر بن جابر رضي الله عنه: أنَّ أهْلَ الكُوفَةِ وَفَدُوا عَلَى عُمَرَ رضي الله عنه، وَفِيهمْ رَجُلٌ مِمَّنْ كَانَ يَسْخَرُ بِأُوَيْسٍ ، فَقَالَ عُمَرُ : هَلْ هاهُنَا أَحَدٌ مِنَ القَرَنِيِّينَ ؟ فَجَاءَ ذلِكَ الرَّجُلُ ، فَقَالَ عمرُ : إنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَدْ قَالَ : (( إنَّ رَجُلاً يَأتِيكُمْ مِنَ اليَمَنِ يُقَالُ لَهُ : أُوَيْسٌ ، لاَ يَدَعُ باليَمَنِ غَيْرَ أُمٍّ لَهُ ، قَدْ كَانَ بِهِ بَيَاضٌ فَدَعَا الله تَعَالَى ، فَأذْهَبَهُ إلاَّ مَوضِعَ الدِّينَارِ أَو الدِّرْهَمِ ، فَمَنْ لَقِيَهُ مِنْكُمْ ، فَلْيَسْتَغْفِرْ لَكُمْ )) .

وفي رواية لَهُ : عن عمر رضي الله عنه، قَالَ : إنِّي سَمِعْتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، يقول 🙁( إنَّ خَيْرَ التَّابِعِينَ رَجُلٌ يُقَالُ لَهُ : أُوَيْسٌ ، وَلَهُ وَالِدَةٌ وَكَانَ بِهِ بَيَاضٌ ، فَمُرُوهُ ، فَلْيَسْتَغْفِرْ لَكُمْ )) .

Imepokewa kutoka kwa Usayr bin 'Amru (Radhwiyah Allaahu 'anhu), Imesemwa ni Ibn Jaabir (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: "'Umar bin Al-Khataab (Radhwiyah Allaahu 'anhu) anapojiwa na kundi kutoka Yemen huwauliza: "Ndani yenu yupo Uways bin 'Aamir?" Mpaka siku hiyo akamkuta Uways, akamwambia: "Wewe ni Uways bin 'Aamir?" Akasema: "Ndio." Akasema: "Kutoka kabila la Muraad, kutoka ukoo wa Qaran?" akasema: "Ndio." Akasema: "Ulikuwa na mbalanga ukapona isipokuwa sehemu kiasi cha dirhamu?" Akasema: "Ndio'" Akasema: "Una mama?" Akasema: "Ndio." Akasema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akisema: "Atakujieni Uways pamoja na kundi la watu wa Yemen kabila la Muraad, kisha kwa Qaran. Alikuwa na mbalanga akapona isipokuwa sehemu ndogo mfano wa dirhamu. Ana mama anayemtendea wema, lau ataapa kwa Allaah atamtimizia. Ukiweza kumpata ili akuombee maghfira fanya." Hivyo niombee msamaha kwa Allaah, naye akamuombea. 'Umar akamwambia: "Unakwenda wapi?" Akasema; "Kufah." Akasema: "Je, nikuandikie kwa gavana wake? Akasema; "Kuwa katika watu maskini ni bora kwangu. Ulipofika mwaka uliofuata walihiji watu watukufu kutoka Kufah nao walikutana na 'Umar, akawauliza kuhusu Uways. Akasema: "Nimemuacha katika nyumba mbaya, samani chache." Akasema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akisema: "Atakujieni Uways pamoja na kundi la watu wa Yemen kabila la Muraad, kisha kwa Qaran. Alikuwa na mbalanga akapona isipokuwa sehemu ndogo mfano wa dirhamu. Ana mama anayemtendea wema, lau ataapa kwa Allaah atamtimizia. Ukiweza kumpata ili akuombee maghfira fanya." Akamjia Uways akamwambia: "Niombee msamaha kwa Allaah." Akasema: 'Wewe umerudi punde safarini niombee msamaha."Akamuuliza: "Je, umekutana na 'Umar?" Akasema: "Ndio." Akamuombea maghfira, watu wakamgundua." [Muslim]

Na riwaayah ya Muslim toka kwa Usayr bin Jaabir (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa watu wa Kufah walipeleka wawakilishi wao kwa 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu), Miongoni mwao alikuwepo mtu aliyekuwa akimdhihaki Uways. Akasema 'Umar: "Hapa yupo yeyote kutoka ukoo wa Qaran?" Yule mtu akaja mbele. Akasema 'Umar: "Hakika Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika atakujieni mtu kutoka Yemen anaitwa Uways. Amemuacha mamake peke yake, ana weupe (mbalanga) akamuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa). Allaah akauondoa isipokuwa sehemu ndogo mfano wa dinari au dirhamu. Atakayekutana naye miongoni mwenu amtake amuombee maghfira kwa Allaah."

Katika riwaayah yake kutoka kwa 'Umar amesema: "Hakika nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mbora wa Tabi'in ni mtu anayeitwa Uways. Ana mama yake na weupe katika mwili wake. Nendeni kwake na mumuombe awaombee maghfira."







Hadiyth – 14

وعن عمر بن الخطاب رضي الله عنه، قَالَ : اسْتَأذَنْتُ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم في العُمْرَةِ ، فَأذِنَ لِي ، وَقالَ : (( لاَ تَنْسَنا يَا أُخَيَّ مِنْ دُعَائِكَ )) فَقَالَ كَلِمَةً مَا يَسُرُّنِي أنَّ لِي بِهَا الدُّنْيَا

وفي رواية : وَقالَ : (( أشْرِكْنَا يَا أُخَيَّ في دُعَائِكَ )) .

حديث صحيح رواه أَبُو داود والترمذي، وَقالَ: (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa 'Umar bin Al-Khattaab (Radhwiyah Allaahu 'anhu) ambaye alisema: "Nilimuomba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)ruhusa ya kwenda kufanya Umrah, naye alinipatia idhini. Na akasema: "Ee ndugu yangu! Usitusahau katika dua'a zako." Akasema (Radhwiyah Allaahu 'anhu):"Hili ni neno ambalo sitataka kubadilishana hata na dunia yote."

Na katika riwaayah nyingine, alisema: "Ee ndugu yangu! Tushirikishe katika dua yako."

Hadiyth Swahiyh iliyonukuliwa na Abu Daawuud na At-Tirmidhiy, ambaye amesema kuwa hii ni Hadiyth Swahiyh.







Hadiyth – 15

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : كَانَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم يزور قُبَاءَ رَاكِباً وَمَاشِياً ، فَيُصَلِّي فِيهِ رَكْعَتَيْنِ . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية : كَانَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم يَأتي مَسْجِد قُبَاءَ كُلَّ سَبْتٍ رَاكباً ، وَمَاشِياً وَكَانَ ابْنُ عُمَرَ يَفْعَلُهُ .

Imepokewa kwa Ibn 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) ambaye amesema: "Alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akizuru Qubaa (Msikiti wa sehemu hiyo) akiwa amepanda (mnyama) na kwa miguu. Na alikuwa akiswali katika Msikiti huo rakaa mbili." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad].

Katika riwaayah nyingine: "Alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiuzuru Msikiti wa Qubaa kila siku ya Jumamosi kwa kupanda mnyama na kwa miguu (wakatika mwengine). Na Ibn 'Umar alikuwa akifanya hivyo."
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب فضل الحب في الله والحث عَلَيهِ وإعلام الرجل من يحبه ، أنه يحبه ، وماذا يقول لَهُ إِذَا أعلمه

046-Mlango Wa Fadhila za Kupenda kwa Ajili ya Allaah na Kuhimiza hilo



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:

مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖ ﴿٢٩﴾

Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Rasuli wa Allaah. Na wale walio pamoja naye ni wakali zaidi dhidi ya makafiri; wanahurumiana baina yao. [Al-Fat-h: 29] Hadi mwisho wa Surah.



وَالَّذِينَ تَبَوَّءُوا الدَّارَ وَالْإِيمَانَ مِن قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ ﴿٩﴾

Na wale waliokuwa na masikani (Madiynah) na wakawa na iymaan kabla yao, wanawapenda wale waliohajiri kwao. [Al-Hashr: 9]









Hadiyth – 1

وعن أنسٍ رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( ثَلاثٌ مَنْ كُنَّ فِيهِ وَجَدَ بِهِنَّ حَلاوَةَ الإيمانِ : أنْ يَكُونَ اللهُ وَرَسُولُهُ أحَبَّ إِلَيْهِ مِمَّا سَوَاهُمَا ، وَأنْ يُحِبّ المَرْءَ لاَ يُحِبُّهُ إلاَّ للهِ ، وَأَنْ يَكْرَهَ أنْ يَعُودَ في الكُفْرِ بَعْدَ أنْ أنْقَذَهُ الله مِنْهُ ، كَمَا يَكْرَهُ أنْ يُقْذَفَ في النَّارِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Sifa tatu yeyote mwenye kuwa nazo atapata ladha (utamu) wa Imani: Kuwa Allaah na Rasuli Wake ndiyo awapendao zaidi kuliko wasiokuwa wao; (la pili) kumpenda mtu kwa ajili ya Allaah Peke Yake, (la tatu) kuchukia kurudi katika ukafiri kama anavyochukia kutupwa motoni. [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( سَبْعَةٌ يُظِلُّهُمُ اللهُ في ظِلِّهِ يَوْمَ لاَ ظِلَّ إلاَّ ظِلُّهُ : إمَامٌ عَادِلٌ ، وَشَابٌّ نَشَأ في عِبَادَةِ الله (عزّ وجلّ)، وَرَجُلٌ قَلْبُهُ مُعَلَّقٌ بِالمَسَاجِدِ ، وَرَجُلاَنِ تَحَابّا في اللهِ اجْتَمَعَا عَلَيهِ وتَفَرَّقَا عَلَيهِ ، وَرَجُلٌ دَعَتْهُ امْرَأةٌ ذَاتُ حُسْنٍ وَجَمَالٍ ، فَقَالَ : إنِّي أخَافُ الله ، وَرَجُلٌ تَصَدَّقَ بِصَدَقَةٍ ، فَأخْفَاهَا حَتَّى لاَ تَعْلَمَ شِمَالُهُ مَا تُنْفِقُ يَمِينُهُ ، وَرَجُلٌ ذَكَرَ الله خَالِياً فَفَاضَتْ عَيْنَاهُ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Watu saba atawafunika chini ya kivuli Chake siku hakuna kivuli isipokuwa kivuli Chake: Imamu (kiongozi) muadilifu, kijana aliyeinukia katika kumuabudu Allaah ('Azza wa Jall), na mtu moyo wake umetundikwa Msikitini, na watu wawili wamependana kwa ajili ya Allaah, wakajumuika juu yake, na kufarikiana kwa ajili Yake, na mtu ameitwa na mwanamke mzuri mwenye kuvutia, akasema: 'Mimi namwogoa Allaah,' na mtu aliyetoa sadaka akaificha hadi kushoto kwake kusijue ulichotoa kulia kwake, na mtu amemtaja Allaah faraghani macho yake yakabubujika machozi." [Al-Bukhaariy na Muslim].







Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم : (( إنّ الله تَعَالَى يقول يَوْمَ القِيَامَةِ : أيْنَ المُتَحَابُّونَ بِجَلالِي ؟ اليَوْمَ أُظِلُّهُمْ فِي ظِلِّي يَوْمَ لاَ ظِلَّ إلاَّ ظِلِّي )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah Ta'aalaa atasema Siku ya Qiyaamah: "Wawapi waliopendana kwa Utukufu Wangu?, Leo nitawafunika katika kivuli Changu siku hakuna kivuli isipokuwa kivuli Changu." [Muslim]







Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( والَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ ، لا تَدْخُلُوا الجَنَّةَ حَتَّى تُؤْمِنُوا ، وَلا تُؤْمِنُوا حَتَّى تَحَابُّوا ، أوَلاَ أدُلُّكُمْ عَلَى شَيْءٍ إِذَا فَعَلْتُمُوهُ تَحَابَبْتُمْ ؟ أفْشُوا السَّلامَ بينكم )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Naapa kwa ambaye nafsi yangu iko mkononi Mwake! Hamtaingia Peponi hadi Muamini, wala hamtaamini mpaka mpendane. Je niwaonyeshe kitu mkikifanya mtapendana? Enezeni salamu baina yenu." [Muslim].







Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم: (( أنَّ رَجُلاً زَارَ أخاً لَهُ في قَرْيَةٍ أخْرَى ، فَأرصَدَ اللهُ لَهُ عَلَى مَدْرَجَتِهِ مَلَكاً … )) وذكر الحديث إِلَى قوله : (( إنَّ الله قَدْ أحبَّكَ كَمَا أحْبَبْتَهُ فِيهِ )) رواه مسلم ، وقد سبق بالباب قبله .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtu mmoja alimzuru nduguye katika Kijiji chengine. Allaah alimwakilisha Malaika njiani...." Akataja hadiyth hadi kauli yake: "Hakika Allaah amekupenda kama ulivyompenda ndugu yako kwa ajili Yake." [Muslim]. Imetanguliwa kutajwa katika mlango uliofuata.







Hadiyth – 6

وعن البرَاءِ بن عازب رضي الله عنهما ، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم أنَّهُ قَالَ في الأنصار : (( لاَ يُحِبُّهُمْ إلاَّ مُؤمِنٌ ، وَلاَ يُبْغِضُهُمْ إلاَّ مُنَافِقٌ ، مَنْ أحَبَّهُمْ أَحَبَّهُ الله ، وَمَنْ أبْغَضَهُمْ أبْغَضَهُ الله )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Al-Baraa'i bin 'Aazib (Radhwiyah Allaahu 'anhu) ya kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema yafuatayo kuhusu Ansari: "Hawapendi wao isipokuwa Muumini na hawachukii isipokuwa mnafiki. Kwa hiyo Allaah Atampenda anayewapenda na Atamchukia anayewachukia." [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 7

وعن معاذ رضي الله عنه، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( قَالَ الله (عزّ وجلّ) : المُتَحَابُّونَ في جَلالِي ، لَهُمْ مَنَابِرُ مِنْ نُورٍ يَغْبِطُهُمُ النَّبِيُّونَ وَالشُّهَدَاءُ )) . رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن صحيح )) .

Na imepokewa kutoka kwake Mu'aadh (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: "Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Amesema Allaah ('Azza wa Jall): Wanaopendana kwa ajili ya Utukufu Wangu, watakaa katika minbari za nuru huku Manabii na mashahidi wakitamani hadhi na kheri hiyo." [At-Tirmidhiy, ambaye amesema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]







Hadiyth – 8

وعن أَبي إدريس الخولاني رحمه الله ، قَالَ :دخَلْتُ مَسْجِدَ دِمَشْقَ ، فَإذَا فَتَىً بَرَّاق الثَّنَايَا وَإِذَا النَّاسُ مَعَهُ ، فَإِذَا اخْتَلَفُوا في شَيْءٍ ، أَسْنَدُوهُ إِلَيْه ، وَصَدَرُوا عَنْ رَأيِهِ ، فَسَأَلْتُ عَنْهُ ، فَقيلَ : هَذَا مُعَاذُ بْنُ جَبَل رضي الله عنه. فَلَمَّا كَانَ مِنَ الغَدِ ، هَجَّرْتُ ، فَوَجَدْتُهُ قَدْ سَبَقَنِي بالتَّهْجِيرِ ، ووَجَدْتُهُ يُصَلِّي ، فانْتَظَرتُهُ حَتَّى قَضَى صَلاتَهُ ، ثُمَّ جِئْتُهُ مِنْ قِبَلِ وَجْهِهِ ، فَسَلَّمْتُ عَلَيهِ ، ثُمَّ قُلْتُ : وَاللهِ إنّي لأَحِبُّكَ لِله ، فَقَالَ : آلله ؟ فَقُلْتُ : اللهِ ، فَقَالَ : آللهِ ؟ فَقُلْتُ : اللهِ ، فَأخَذَنِي بِحَبْوَةِ رِدَائِي ، فجبذني إِلَيْهِ ، فَقَالَ : أبْشِرْ ! فإنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( قَالَ الله تَعَالَى : وَجَبَتْ مَحَبَّتي لِلْمُتَحابين فيَّ ، وَالمُتَجَالِسينَ فيَّ ، وَالمُتَزَاوِرِينَ فيَّ ، وَالمُتَبَاذِلِينَفِيَّ )) حديث صحيح رواه مالك في الموطأ بإسناده الصحيح .

Imepokewa kutoka kwa Abu Idris Al-Khawlaani (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: "Niliingia Msikiti wa Damascus, nikamuona kijana ana meno meupe masafi (mwenye kutabasamu sana), watu wako pamoja naye. Watu wanapotofautiana katika jambo walikuwa wakitaka na kuichukua rai yake. Nikauliza kuhusu yeye na nikaambiwa: 'Huyu ni Mu'aadh bin Jabal (Radhwiyah Allaahu 'anhu). Siku ya pili nilifika mapema Msikitini lakini nikapata kuwa ameshafika kabla yangu. Nilimpata yeye anaswali hivyo nilingojea mpaka akamaliza Swalah yake. Hapo nilikwenda mbele yake na kumsalimia, kisha nikamwambia: 'Naapa kwa Allaah kuwa mimi nakupenda kwa ajili ya Allaah.' Akasema: 'je, ni kwa ajili ya Allaah?' Nikasema: 'Ndio, kwa ajili ya Allaah.' Akasema: 'Je, ni kwa ajili ya Allaah?' Nikasema: 'Ndio kwa ajili ya Allaah.' Hapo akanishika kwa mkunjo wa shuka yangu na kunileta karibu naye, akasema: 'Hakika nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: Amesema Allaah Ta'aalaa! Ni wajibu kuwapenda wale wanaopendana kwa ajili Yangu, na wenye kukaa pamoja kwa ajili Yangu na wenye kutembeleana kwa ajili Yangu na wenye kusaidiana kwa ajili Yangu." [Hadiyth Swahiyh iliyonukuliwa na Imam Malik katika al-Muwatta' kwa Isnaad iliyo Swahiyh]







Hadiyth – 9

وعن أَبي كَرِيمَةَ المقداد بن معد يكرب رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( إِذَا أَحَبَّ الرَّجُلُ أخَاهُ ، فَليُخْبِرْهُ أَنَّهُ يُحِبُّهُ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وَقالَ 🙁( حديث صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Kariimah al-Miqdaad bin Ma'diyakrib (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ndugu mmoja anapompenda mwenziwe, ampashe habari ya kuwa anampenda." [Abu Daawuud na At-Tirmidhiy, ambaye amesema kuwa ni Hadiyth Hasan]







Hadiyth – 10

وعن معاذ رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم أخذ بيدهِ ، وَقالَ : (( يَا مُعَاذُ ، وَاللهِ ، إنِّي لأُحِبُّكَ ، ثُمَّ أُوصِيكَ يَا مُعَاذُ لاَ تَدَعَنَّ في دُبُرِ كُلِّ صَلاَةٍ تَقُولُ : اللَّهُمَّ أعِنِّي عَلَى ذِكْرِكَ ، وَشُكْرِكَ ، وَحُسْنِ عِبَادَتِكَ )) حديث صحيح ، رواه أَبُو داود والنسائي بإسناد صحيح .

Imepokewa kutoka kwa Mu'aadh (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimshika mkono wake na kumwambia: "Ee Mu'aadh! Naapa kwa Allaah kuwa nakupenda, kisha nakuusia ee Mu'aadh; Usiache kusema kila baada ya Swalah ya faradhi maneno yafuatayo: 'Ee Mola Wangu! Nisaidie katika kukutaja na kukushukuru na kukuabudu katika njia bora kabisa." [Hadiyth Swahiyh iliyonukuliwa na Abu Daawuud na An-Nasai kwa isnaad swahiyh]







Hadiyth – 11

وعن أنس رضي الله عنه: أنَّ رَجُلاً كَانَ عِنْدَ النَّبيِّ ، صلى الله عليه وسلم، فَمَرَّ رَجُلٌ بِهِ ، فَقَالَ : يَا رَسُول الله ، أنِّي لأُحِبُّ هَذَا ، فَقَالَ لَهُ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم: (( أأعْلَمْتَهُ ؟ )) قَالَ : لا . قَالَ : (( أعْلِمْهُ )) فَلَحِقَهُ ، فَقَالَ : إنِّي أُحِبُّكَ في الله ، فَقَالَ : أَحَبَّكَ الَّذِي أحْبَبْتَنِي لَهُ . رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .

Na imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) ya kwamba: "Kwa hakika kulikuwa na mtu pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na akapita mbele yao mtu mwingine. Akasema: 'Ee Rasuli wa Allaah! Hakika mimi nampenda huyu mtu.' Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: 'Je, umemjulisha hili?' Akasema: 'La! Akamwambia: 'Basi kamjulishe hilo.' Aliondoka huyu mtu na kukutana naye na hapo akamwambia: 'Hakika mimi nakupenda kwa ajili ya Allaah.' Akasema: 'Akupende Allaah ambaye kwa ajili Yake umenipenda mimi'." [Abu Daawuud kwa isnaad iliyo swahiyh]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn





باب علامات حب الله تَعَالَى للعبد والحث عَلَى التخلق بِهَا والسعي في تحصيلها

047-Mlango Wa Alama za Upendo wa Allaah kwa Waja Wake na Kuhimizwa Kujipamba Nayo na Kuitafuta



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:



قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣١﴾

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Aal-'Imraan: 31]



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ ۚ ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٥٤﴾

Enyi walioamini! Yeyote atakayeritadi miongoni mwenu kutoka Dini yake, basi Allaah Ataleta watu (badala yao) Atakaowapenda nao watampenda; wanyenyekevu kwa Waumini, washupavu juu ya makafiri; wanafanya jihaad katika njia ya Allaah na wala hawakhofu lawama za mwenye kulaumu. Hiyo ni fadhila ya Allaah Humpa Amtakaye. Na Allaah ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote. [Al-Maaidah: 54]







Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( إنَّ الله تَعَالَى قَالَ : مَنْ عَادَى ليَ وَلِيّاً ، فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالحَرْبِ ، وَمَا تَقَرَّبَ إِلَيَّ عَبْدِي بِشَيءٍ أَحَبَّ إِلَيَّ مِمَّا افْتَرَضْتُ عَلَيهِ ، وَمَا يَزالُ عَبْدِي يَتَقَرَّبُ إِلَيَّ بِالنَّوَافِلِ حَتَّى أُحِبَّهُ ، فَإِذَا أحْبَبْتُهُ ، كُنْتُ سَمْعَهُ الَّذِي يَسْمَعُ بِهِ ، وَبَصَرَهُ الَّذِي يُبْصِرُ بِهِ ، ويَدَهُ الَّتي يَبْطِشُ بِهَا ، وَرجْلَهُ الَّتِي يَمْشِي بِهَا وَإنْ سَألَنِي أعْطَيْتُهُ ، وَلَئِن اسْتَعَاذَنِي لأعِيذَنَّهُ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah Ta'aalaa amesema: "Mwenye kumfanyia uadui rafiki yangu basi Nimemtangazia vita. Hajikurubishi Kwangu mja Wangu kwa kitu ninachokipenda zaidi kuliko nilichomfaradhishia, Na mja haachi kujikurubishi kwangu kwa Sunnah mpaka Nimpende. Ninapompenda, Ninakuwa sikio lake analosikilizia, na jicho lake analoonea, na mkono wake anaoshikia, na mguu wake anayotembelea, Akiniomba Nitampa, na akijilinda kwangu Nitamlinda." [Al-Bukhaariy]







Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( إِذَا أَحَبَّ اللهُ تَعَالَى العَبْدَ ، نَادَى جِبْريلَ : إنَّ الله تَعَالَى يُحِبُّ فُلاناً ، فَأَحْبِبْهُ ، فَيُحِبُّهُ جِبريلُ ، فَيُنَادِي في أَهْلِ السَّمَاءِ : إنَّ اللهَ يُحِبُّ فُلاناً ، فَأحِبُّوهُ ، فَيُحِبُّهُ أهْلُ السَّمَاءِ ، ثُمَّ يُوضَعُ لَهُ القَبُولُ في الأرْضِ )) متفق عليه . وفي رواية لمسلم : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( إنَّ الله تعالى إذا أحب عبداً دعا جبريلَ ، فقال : إنّي أُحِبُّ فلاناً فأحببهُ ، فيحبُّهُ جبريلُ ، ثمَّ ينادي في السماءِ ، فيقول : إنَّ اللهَ يحبُّ فلاناً فأحبوهُ ، فيحبُّهُ أهلُ السماءِ ، ثمَّ يوضعُ لهُ القبولُ في الأرضِ ، وَإِذَا أبْغَضَ عَبْداً دَعَا جِبْريلَ ، فَيَقُولُ : إنّي أُبْغِضُ فُلاناً فَأبْغِضْهُ . فَيُبغِضُهُ جِبريلُ ثُمَّ يُنَادِي في أَهْلِ السَّماءِ : إنَّ الله يُبْغِضُ فُلاناً فَأبْغِضُوهُ ، ثُمَّ تُوضَعُ لَهُ البَغْضَاءُ في الأَرْضِ )) .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah Ta'aalaa anapompenda mja anamuita Jibriyl na kumwambia: "Hakika Allaah Ta'aalaa anampenda Fulani, hivyo nawe mpende." Hivyo Jibriyl anampenda mtu huyo na baada ya hapo anatangaza kwa watu wa mbinguni kwamba: 'Hakika Allaah anampenda fulani, kwa hivyo nanyi nyote mpendeni.' Hapo watu wa mbinguni wanampenda mtu huyo. Kisha anawekewa kukubaliwa na watu wa ardhini. [Al-Bukhaariy na Muslim]. Na katika riwaayah ya Muslim: Amesema Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Hakika Allaah Ta'aalaa anapompenda mja, anamuita Jibriyl, na kumwambia: "Hakika Mimi nampenda fulani, nawe mpende." Hivyo Jibriyl anampenda mtu huyo na baada ya hapo anatangaza mbinguni kwa kusema: 'Hakika Allaah anampenda fulani, kwa hivyo nanyi nyote mpendeni.' Hapo watu wa mbinguni nao pia wanampenda mtu huyo. Kisha anawekewa kabuli (kukubaliwa) na watu wa ardhini. Na Allaah anapomchukia mtu yeyote anamuita Jibriyl na kumwambia: "Hakika Mimi namchukia fulani, nawe mchukie." Hivyo Jibriyl ('Alayhi salaam) anamchukia mtu huyo na baada ya hapo anatangaza kwa watu wa mbinguni kwamba: "Hakika Allaah anamchukia fulani, kwa hivyo nanyi nyote mchukieni." Hapo watu wa mbinguni nao pia wanamchukia mtu huyo. Kisha anawekewa chuki na watu wa ardhini."







Hadiyth – 3

وعن عائشة رضي الله عنها : أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم بعث رجلاً عَلَى سَريَّة فَكَانَ يَقْرَأُ لأَصْحَابِهِ في صَلاَتِهِمْ فَيَخْتِمُ بـ ( قُل هُوَ الله أَحَدٌ ) ، فَلَمَّا رَجَعُوا ذَكَرُوا ذلِكَ لرسول الله صلى الله عليه وسلم، فَقَالَ : (( سَلُوهُ لأَيِّ شَيْءٍ يَصْنَعُ ذلِكَ )) ؟ فَسَألُوهُ فَقَالَ : لأَنَّهَا صِفَةُ الرَّحْمانِ فَأَنَا أُحِبُّ أنْ أقْرَأ بِهَا . فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( أخْبِرُوهُ أنَّ اللهَ تَعَالَى يُحِبُّهُ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiyah Allaahu 'anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah alimchagua mtu kuongoza kikosi cha Sarriyah kuwaongoza wenzake katika vita. Akawa katika Swalaah zake zote alizokuwa akiswalisha wenzake akimalizia na (قُل هُوَ الله أَحَدٌ). Waliporudi (Madinah), Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alielezwa hilo, naye akawaambia: "Muulizeni ni kwa sababu gani anafanya hivyo?" Wakamuuliza, naye akasema: "Kwa sababu humo ndani zipo sifa za Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma), nami napenda kuzisoma." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Mpeni habari ya kwamba Allaah Ta'aalaa anampenda." [Al-Bukhaariy na
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn





باب التحذير من إيذاء الصالحين والضعفة والمساكين

048-Mlango Wa Onyo kwa Wenye Kuwaudhi Watu Wema, Wanyonge na Masikini



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:

وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا ﴿٥٨﴾

Na wale wanaowaudhi Waumini wa kiume na Waumini wa kike bila ya kuwa wamechuma kosa, basi kwa yakini wamejibebea usingiziaji mkuu wa dhulma na dhambi bayana. [Al-Ahzaab: 58]



فَأَمَّا الْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ ﴿٩﴾وَأَمَّا السَّائِلَ فَلَا تَنْهَرْ ﴿١٠﴾

Kwa hivyo basi yatima usimuonee.Na mwombaji usimkaripie. [Adhw-Dhwuhaa: 9-10]



وأما الأحاديث ، فكثيرة مِنْهَا :

حديث أَبي هريرة رضي الله عنه في الباب قبل هَذَا : (( مَنْ عَادَى لِي وَليّاً فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالحَرْبِ )) .

ومنها حديث سعد بن أَبي وقاص رضي الله عنه السابق في باب ملاطفة اليتيم ، وقوله صلى الله عليه وسلم: (( يَا أَبَا بَكْرٍ ، لَئِنْ كُنْتَ أغْضَبْتَهُمْ لَقَدْ أغْضَبْتَ رَبَّكَ )) .

Ama Hadiyth ni nyingi, miongoni mwa hizo ni zifuatazo: Toka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu): "Yeyote atakayefanya uadui na rafiki yangu basi Nimetangaza vita naye."

Na Hadiyth ya sa'ad bin Abi Waqqaas (Radhwiyah Allaahu 'anhu): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ee Abu Bakr! Ikiwa umewakasirisha, hakika utakuwa umemkasirisha Rabb wako."





Hadiyth – 1

وعن جندب بن عبد الله رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( مَنْ صَلَّى صَلاةَ الصُّبْحِ ، فَهُوَ في ذِمَّةِ الله ، فَلاَ يَطْلُبَنَّكُمُ الله مِنْ ذِمَّتِهِ بِشَيْءٍ ، فَإنَّهُ مَنْ يَطْلُبُهُ مِنْ ذِمَّتِهِ بِشَيْءٍ يُدْرِكْهُ ، ثُمَّ يَكُبُّهُ عَلَى وَجْهِهِ في نَارِ جَهَنَّمَ )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Jundub bin 'Abdillaah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuswali Swalaah ya Asubuhi yupo katika dhima (himaya) ya Allaah. Hivyo jihadharini Allaah Kuwadai katika dhimma yake chochote, Kwani Anayemtaka dhimmayake atamdiriki, kisha Kumtupa katika Moto wa Jahanam." [Muslim]

Na katika Riwaayah: "Atakayeswali Swalaah ta asubuhi katika Jamaa."
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn





باب إجراء أحكام الناس عَلَى الظاهر وسرائرهم إِلَى الله تَعَالَى

049-Mlango Wa Kuwahukumu Watu kwa Dhahiri ya Mambo na Kumwachia Allaah Siri Zao



Alhidaaya.com





قَالَ الله تَعَالَى:

فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ ۚ ﴿٥﴾

Lakini wakitubu, na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah, basi iacheni njia yao (huru). [At-Tawbah: 5]





Hadiyth – 1

وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( أُمِرْتُ أنْ أُقَاتِلَ النَّاسَ حَتَّى يَشْهَدُوا أنْ لاَ إلهَ إلاَّ الله ، وَأنَّ مُحَمَّداً رَسُول الله ، وَيُقيمُوا الصَّلاةَ ، وَيُؤتُوا الزَّكَاةَ ، فَإِذَا فَعَلُوا ذلِكَ عَصَمُوا مِنِّي دِمَاءهُمْ وَأمْوَالَهُمْ إلاَّ بحَقِّ الإسْلاَمِ ، وَحِسَابُهُمْ عَلَى الله تَعَالَى )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nimeamrishwa kupigana na watu mpaka wakubali kuwa hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah, kusimamisha Swalaah, na kutoa Zakaah.Wakifanya hivyo zitahifadhika damu zao na mali yao isipokuwa kwa haki ya Uislamu, na hesabu yao iko kwa Allaah Ta'aalaa." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 2

وعن أَبي عبدِ الله طارِق بن أشَيْم رضي الله عنه، قَالَ : سَمِعْتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( مَنْ قالَ لاَ إلهَ إلاَّ الله ، وَكَفَرَ بما يُعْبَدُ مِنْ دُونِ اللهِ ، حَرُمَ مَالُهُ وَدَمُهُ ، وَحِسَابُهُ عَلَى الله تَعَالَى )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Abu 'Abdillaah Twaariq bin Ushaym amesema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mwenye kusema Laa ilaaha illa-Allaah, na akakufuru vyote vinavyoabudiwa kinyume na Allaah, atahifadhiwa mali na damu yake, na hesabu yake itakuwa kwa Allaah Ta'aalaa." [Muslim]





Hadiyth – 3

وعن أَبي معبد المقداد بن الأسْود رضي الله عنه ، قَالَ : قُلْتُ لرسول الله صلى الله عليه وسلم: أرَأيْتَ إنْ لَقِيتُ رَجُلاً مِنَ الكُفَّارِ ، فَاقْتتَلْنَا ، فَضَرَبَ إحْدَى يَدَيَّ بِالسَّيْفِ ، فَقَطَعَها ، ثُمَّ لاذَ مِنِّي بِشَجَرَةٍ ، فَقَالَ : أسْلَمْتُ لِلهِ ، أأقْتُلُهُ يَا رَسُول الله بَعْدَ أنْ قَالَهَا ؟ فَقَالَ : (( لا تَقْتُلهُ )) فَقُلْتُ : يَا رَسُول الله ، قَطَعَ إحْدَى يَدَيَّ ، ثُمَّ قَالَ ذلِكَ بَعْدَ مَا قَطَعَهَا ؟! فَقَالَ : (( لا تَقتُلْهُ ، فإنْ قَتَلْتَهُ فَإنَّهُ بِمَنْزِلَتِكَ قَبْلَ أنْ تَقْتُلَهُ ، وَإنَّكَ بِمَنْزِلَتِهِ قَبْلَ أنْ يَقُولَ كَلِمَتَهُ التي قَالَ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Ma'bad Al-Miqdaad bin Al-Aswad (Radhwiyah Allaahu 'anhu) ya kwamba, nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Waonaje nikikutana na mtu miongoni mwa makafiri. Tukapigana, naye akanikata mkono wangu kwa upanga, kisha akajificha kutoka kwangu nyuma ya mti, akasema: 'Nimesilimu kwa ajili ya Allaah.' Je, naweza kumuua Ee Rasuli wa Allaah baada ya kusema maneno hayo? Akasema: 'Usimuue.'Nikasema: 'Ee Rasuli wa Allaah! Ameukata mkono wangu mmoja, kisha akasema maneno hayo baada ya kuukata?' Akasema: 'Usimuue, kwani utakapofanya hivyo atakuwa katika nafasi yako kabla ya kumuua. Na hakika wewe utakuwa katika nafasi yake kabla ya yeye kutamka kauli yake hiyo." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 4

وعن أُسَامة بن زيدٍ رضي الله عنهما ، قَالَ : بعثنا رَسُول الله صلى الله عليه وسلم إِلَى الْحُرَقَةِ مِنْ جُهَيْنَةَ فَصَبَّحْنَا القَوْمَ عَلَى مِيَاهِهِمْ ، وَلَحقْتُ أنَا وَرَجُلٌ مِنَ الأَنْصَارِ رَجُلاً مِنْهُمْ ، فَلَمَّا غَشَيْنَاهُ ، قَالَ : لاَ إلهَ إلاَّ الله ، فَكفَّ عَنْهُ الأَنْصَاري ، وطَعَنْتُهُ برُمْحِي حَتَّى قَتَلْتُهُ ، فَلَمَّا قَدِمْنَا المَدِينَةَ ، بَلَغَ ذلِكَ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ لِي : (( يَا أُسَامَة ، أقَتَلْتَهُ بَعْدَ مَا قَالَ لا إلهَ إلاَّ اللهُ ؟! )) قُلْتُ : يَا رَسُول الله ، إِنَّمَا كَانَ متعوِّذاً ، فَقَالَ : (( أقَتَلْتَهُ بَعْدَ مَا قَالَ لا إلهَ إلاَّ اللهُ ؟! )) فما زَالَ يُكَرِّرُهَا عَلَيَّ حَتَّى تَمنْيَّتُ أنِّي لَمْ أكُنْ أسْلَمْتُ قَبْلَ ذلِكَ اليَوْمِ . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية : فَقَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( أقالَ : لا إلهَ إلاَّ اللهُ وقَتَلْتَهُ ؟! )) قُلْتُ : يَا رَسُول الله ، إِنَّمَا قَالَهَا خَوْفاً مِن السِّلاحِ ، قَالَ : (( أَفَلاَ شَقَقْتَ عَنْ قَلْبِهِ حَتَّى تَعْلَمَ أَقَالَهَا أمْ لا ؟! )) فمَا زَالَ يُكَرِّرُهَا حَتَّى تَمَنَّيْتُ أنِّي أسْلَمْتُ يَوْمَئذٍ .

Na imepokewa kutoka kwa Usamah bin Zayd (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) amesema, alitutuma Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwenda al-Huraqah, tuliwaamkia asubuhi, tukawashambulia tukawashinda. Mimi na mtu mmoja miongoni mwao, tulipompata akasema: 'Laa ilaaha illa Allaah,' Ansari akamwacha, mimi nikamchoma kwa mkuki wangu nikammuua . Tuliporudi taarifa zikamfikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), naya akaniambia, "Ee Usamah! Umemuua baada ya kuwa amesema, "Laa ilaaha illa Allaah." Nikasema: "Alikuwa akijisalimisha tu." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliendelea kulirudia hilo mpaka nikatamani heri nisingekuwa Muislamu kabla ya siku ile." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Katika riwaayah nyingine: Alisema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Amesema Laa ilaaha illa Allaah, nawe ukamuua?" Nikasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika amesema hilo akihofia silaha." Akasema: "Je, uliupasua moyo wake mpaka ukajua kuwa amesema hilo kweli au la." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliendelea kulirudia hilo mpaka nikatamani nisingekuwa nimesilimu wakati ule.





Hadiyth – 5

وعن جندب بن عبد الله رضي الله عنه: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم بَعَثَ بَعْثاً مِنَ المُسْلِمينَ إِلَى قَومٍ مِنَ المُشرِكينَ ، وَأنَّهُمْ التَقَوْا ، فَكَانَ رَجُلٌ مِنَ المُشْركينَ إِذَا شَاءَ أنْ يَقْصِدَ إِلَى رَجُل مِنَ المُسْلِمينَ قَصَدَ لَهُ فَقَتَلَهُ ، وَأنَّ رَجُلاً مِنَ المُسْلِمِينَ قَصَدَ غَفْلَتَهُ . وَكُنَّا نتحَدَّثُ أنَّهُ أُسَامَةُ بْنُ زَيْدٍ ، فَلَمَّا رَفَعَ عَلَيهِ السَّيفَ ، قَالَ : لا إلهَ إلاَّ اللهُ ، فَقَتَلهُ ، فَجَاءَ البَشيرُ إِلَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم فَسَألَهُ وَأخبَرَهُ ، حَتَّى أخْبَرَهُ خَبَرَ الرَّجُلِ كَيْفَ صَنَعَ ، فَدَعَاهُ فَسَألَهُ ، فَقَالَ : (( لِمَ قَتَلْتَهُ ؟ )) فَقَالَ : يَا رَسُول اللهِ ، أوْجَعَ في المُسلِمِينَ ، وَقَتَلَ فُلاناً وفلاناً ، وسمى لَهُ نَفراً ، وَإنِّي حَمَلْتُ عَلَيهِ ، فَلَمَّا رَأى السَّيفَ ، قَالَ : لا إلهَ إلاَّ اللهُ . قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( أقَتَلْتَهُ ؟ )) قَالَ : نَعَمْ . قَالَ : (( فَكَيفَ تَصْنَعُ بلاَ إلهَ إلاَّ اللهُ ، إِذَا جَاءتْ يَوْمَ القِيَامَةِ ؟ )) قَالَ : يَا رَسُول الله ، اسْتَغْفِرْ لِي . قَالَ : (( وكَيفَ تَصْنَعُ بِلا إلهَ إلاَّ الله إِذَا جَاءتْ يَوْمَ القِيَامَةِ ؟ )) فَجَعَلَ لاَ يَزِيدُ عَلَى أنْ يَقُولَ : (( كَيفَ تَصْنَعُ بِلا إلهَ إلاَّ الله إِذَا جَاءتْ يَوْمَ القِيَامَةِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Jundub bin 'Abdillaah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alituma Waisilamu kwa watu wa washirikina. Nao wakakautana, ikawa mtu katika washirikina akimkusudia mtu katika Waislamu anamkusudia na anamuua, Nakuwa mtu miongoni mwa Waislamu anakusudia kutaka kumuua, Tulikuwa tunahadithia kuwa huyo Usamah bin Zayd. Aliponyanyua upanga wake, yule mtu alisema: 'Laa ilaaha illa Allaah,' naye akamuua. Akaja mwenye kuleta bishara kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), akamuuliza akampa habari hadi akampa ya mtu yule alichofanya, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimuita Usaamah akamuuliza, akasema: "Kwa nini umemuua?" Akasema: "Ee Rasuli wa Allaah!, Ameumiza Waislamu, amemuua fulani na fulani akataja watu, Hivyo, nilimwendea na alipouona upanga ndipo alipotamka, 'Laa ilaaha illa Allaah'." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Je, umemuua?" Akasema: "Ndio." Akasema: "Siku ya Qiyaamah utasema kitu gani kwa kutamka kwake Laa ilaaha illa Allaah?" Akasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Niombee maghfirah." Akasema: "Siku ya Qiyaamah utasema kitu gani kwa kutamka kwake Laa ilaaha illa Allaah?" Na akawa hazidishi kauli yake: ""Siku ya Qiyaamah utasema kitu gani kwa kutamka kwake Laa ilaaha illa Allaah?" [Muslim]





Hadiyth – 6

وعن عبد الله بن عتبة بن مسعود ، قَالَ : سَمِعْتُ عمر بن الخطاب رضي الله عنه، يقولُ : إنَّ نَاساً كَانُوا يُؤْخَذُونَ بِالوَحْيِ في عَهْدِ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، وَإنَّ الوَحْيَ قَدِ انْقَطَعَ ، وإِنَّمَا نَأخُذُكُمُ الآن بما ظَهَرَ لَنَا مِنْ أعمَالِكُمْ ، فَمَنْ أظْهَرَ لَنَا خَيْراً أمَّنَّاهُ وَقَرَّبْنَاهُ ، وَلَيْسَ لَنَا مِنْ سَرِيرَتِهِ شَيْء ، اللهُ يُحَاسِبُهُ فِي سَرِيرَتِهِ ، وَمَنْ أظْهَرَ لَنَا سُوءاً لَمْ نَأمَنْهُ وَلَمْ نُصَدِّقْهُ وَإنْ قَالَ : إنَّ سَرِيرَتَهُ حَسَنَةٌ . رواه البخاري .

Toka kwa 'Abdillaah bin Mas'uwd amesema: "Nimemsikia 'Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiyah Allaahu 'anhu) anasema: "Watu walikuwa wakihukumiwa kwa Wahyi wakati wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), Wahyi umekatika, sasa tunawahukumu kwa amali zenu zilizotudhihirikia, Hivyo mwenye kutudhihirishia kheri tutamuamini na kumkaribisha, na si juu yetu kuchunguza chochote katika siri zake, Allaah atamhesabu katika siri zake, Na anayotudhihirishia uovu hatutomuamini wala hatumsadiki japo atasema: Hakika niya yangu ni nzuri." [Al-Bukhaariy]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب الخوف

050-Mlango Wa Hofu (Ya Allaah)



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:

وَإِيَّايَ فَارْهَبُونِ ﴿٤٠﴾

Na Mimi Pekee niogopeni. [Al-Baqarah: 40]



إِنَّ بَطْشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ ﴿١٢﴾

Hakika mkamato wa kuadhibu wa Rabb wako bila shaka ni mkali. [Al-Buruj: 12]



وَكَذَٰلِكَ أَخْذُ رَبِّكَ إِذَا أَخَذَ الْقُرَىٰ وَهِيَ ظَالِمَةٌ ۚ إِنَّ أَخْذَهُ أَلِيمٌ شَدِيدٌ﴿١٠٢﴾

Na hivyo ndivyo mkamato wa Rabb wako unavyokuwa Anapokamata miji na huku ikifanya dhulma. Hakika mkamato Wake unaumiza vikali.



إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّمَنْ خَافَ عَذَابَ الْآخِرَةِ ۚ ذَٰلِكَ يَوْمٌ مَّجْمُوعٌ لَّهُ النَّاسُ وَذَٰلِكَ يَوْمٌ مَّشْهُودٌ﴿١٠٣﴾

Hakika katika hayo mna Aayah (funzo, zingatio, dalili) kwa anayekhofu adhabu ya Aakhirah. Hiyo ni Siku ya kujumuishwa watu, na hiyo ni Siku ya kushuhudiwa.



وَمَا نُؤَخِّرُهُ إِلَّا لِأَجَلٍ مَّعْدُودٍ﴿١٠٤﴾

Na hatuiakhirishi isipokuwa kwa muda maalumu unaohesabiwa.



يَوْمَ يَأْتِ لَا تَكَلَّمُ نَفْسٌ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ فَمِنْهُمْ شَقِيٌّ وَسَعِيدٌ﴿١٠٥﴾

Siku itakapofika; haitosema nafsi yeyote isipokuwa kwa idhini Yake (Allaah). Basi miongoni mwao ni wenye mashaka wanaostahiki adhabu, na wenye furaha na neema.



فَأَمَّا الَّذِينَ شَقُوا فَفِي النَّارِ لَهُمْ فِيهَا زَفِيرٌ وَشَهِيقٌ﴿١٠٦﴾

Basi ama wale walio mashakani, basi watakuwa motoni, lao humo ni upumuaji pumzi kwa mngurumo na uvutaji pumzi kwa mkoromo. [Huwd: 102-106]



وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّـهُ نَفْسَهُ ۗ ﴿٢٨﴾

Na Allaah Anakutahadharisheni na Nafsi yake. [Aal-'Imraan: 28]





يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ ﴿٣٤﴾ وَأُمِّهِ وَأَبِيهِ ﴿٣٥﴾ وَصَاحِبَتِهِ وَبَنِيهِ ﴿٣٦﴾ لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِ ﴿٣٧﴾

Siku mtu atakapomkimbia ndugu yake. Na mama yake na baba yake. Na mkewe na wanawe.

Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na hali ya kumtosheleza. ['Abasa: 34-37]





يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ ۚ إِنَّ زَلْزَلَةَ السَّاعَةِ شَيْءٌ عَظِيمٌ ﴿١﴾

Enyi watu! Mcheni Rabb wenu. Hakika zilizala la Saa (Qiyaamah) ni jambo kuu.



يَوْمَ تَرَوْنَهَا تَذْهَلُ كُلُّ مُرْضِعَةٍ عَمَّا أَرْضَعَتْ وَتَضَعُ كُلُّ ذَاتِ حَمْلٍ حَمْلَهَا وَتَرَى النَّاسَ سُكَارَىٰ وَمَا هُم بِسُكَارَىٰ وَلَـٰكِنَّ عَذَابَ اللَّـهِ شَدِيدٌ ﴿٢﴾

Siku mtakapoiona kila mnyonyeshaji atamsahau anayemnyonyesha, na kila mwenye mimba ataizaa mimba yake, na utawaona watu wamelewa, kumbe hawakulewa lakini ni adhabu ya Allaah kali. [Al-Hajj: 1-2]



وَلِمَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ جَنَّتَانِ ﴿٤٦﴾

Na kwa mwenye kukhofu kisimamo mbele ya Rabb wake atapata bustani mbili. [Ar-Rahmaan: 46]



وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ ﴿٢٥﴾

Na watakabiliana baadhi yao kwa wengineo wakiulizana.



قَالُوا إِنَّا كُنَّا قَبْلُ فِي أَهْلِنَا مُشْفِقِينَ ﴿٢٦﴾

Watasema: Hakika sisi tulikuwa kabla kwenye ahli zetu wenye kuogopa



فَمَنَّ اللَّـهُ عَلَيْنَا وَوَقَانَا عَذَابَ السَّمُومِ ﴿٢٧﴾

Basi Allaah Akatufadhilisha, na Akatuokoa na adhabu ya moto unaobabua.



إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلُ نَدْعُوهُ ۖ إِنَّهُ هُوَ الْبَرُّ الرَّحِيمُ ﴿٢٨﴾

Hakika sisi tulikuwa kabla Tunamuomba Yeye Pekee, hakika yeye Ndiye Mwingi huruma na fadhila, Mwenye kurehemu. [Atw-Twuwr: 25-28]







Hadiyth – 1

عن ابن مسعود رضي الله عنه، قَالَ : حدثنا رَسُول الله صلى الله عليه وسلم وَهُوَ الصادق المصدوق : (( إنَّ أحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ في بَطْنِ أُمِّهِ أربَعِينَ يَوماً نُطْفَةً ، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذلِكَ ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذلِكَ ، ثُمَّ يُرْسَلُ المَلَكُ ، فَيَنْفُخُ فِيهِ الرُّوحَ ، وَيُؤْمَرُ بِأرْبَعِ كَلِمَاتٍ : بِكَتْبِ رِزْقِهِ وَأجَلِهِ وَعَمَلِهِ وَشَقِيٌّ أَوْ سَعِيدٌ . فَوَالَّذِي لا إلهَ غَيْرُهُ إنَّ أحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أهْلِ الجَنَّةِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وبيْنَهَا إلاَّ ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيهِ الكِتَابُ ، فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أهْلِ النَّارِ فَيدْخُلُهَا ، وَإنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أهْلِ النَّارِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلاَّ ذراعٌ ، فَيَسْبِقُ عَلَيهِ الكِتَابُ فَيعْمَلُ بِعَمَلِ أهْلِ الجَنَّةِ فَيَدْخُلُهَا )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa na Ibn Mas'uud (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa: "Ametuhadithia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na yeye ni mkweli mswadikishwa: Hakika mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mamake siku arobaini; kisha kuwa pande la damu muda kama huo; kisha pande la nyama muda kama huo. Kisha hutumwa Malaika anapuliza roho ndani yake, na anaamrishwa maneno manne: Kuandika riziki yake, ajali yake, amali yake, mwema au muovu. Wa-Allaahi hakuna Rabb asiyekuwa Yeye, hakika mmoja wenu hufanya amali ya watu wa Peponi, mpaka haiwi baina yake na Pepo ila dhiraa, Basi kitabu kimtangulie akafanya amali ya watu wa Motoni. Na mmoja wenu hufanya amali ya watu wa Motoni mpaka haiwi baina yake na Moto ila dhiraa, kitabu kikamtangulia na hivyo akafanya amali za watu wa Pepono na kisha akaingia humo." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 2

عن ابن مسعود رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( يُؤتَى بِجَهَنَّمَ يَومَئذٍ لَهَا سَبْعُونَ ألفَ زِمَامٍ ، مَعَ كُلِّ زِمَامٍ سَبعُونَ ألْفَ مَلَكٍ يَجُرُّونَهَا )) رواه مسلم .

Imepokewa na Ibn Mas'uud (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Siku ya Qiyaamah Jahanam italetwa ikiwa na hatamu elfu sabiini pamoja na kila hatamu kutakuwa na Malaika elfu sabiini wanaoikokota." [Muslim]





Hadiyth – 3

وعن النعمان بن بشير رضي الله عنهما ، قَالَ : سَمِعْتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( إنَّ أهْوَنَ أهْلِ النَّارِ عَذَاباً يَوْمَ القِيَامَةِ لَرَجُلٌ يوضعُ في أخْمَصِ قَدَمَيْهِ جَمْرَتَانِ يَغْلِي مِنْهُمَا دِمَاغُهُ . مَا يَرَى أنَّ أَحَداً أشَدُّ مِنْهُ عَذَاباً ، وَأنَّهُ لأَهْوَنُهُمْ عَذَاباً )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa an-Nu'maan bin Bashiir (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) ambaye amesema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika watu wa Motoni watakaokuwa na adhabu duni kabisa Siku ya Qiyaamah ni mtu atakaye wekewa makaa mawili ya Moto chini ya miguu yake yatakayo lifanya bongo lake lichemke. Mtu huyo atajihisi kuwa yeye anapata adhabu kali zaidi kuliko wote, kumbe ndio amepewa adhabu ya chini kabisa." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]







Hadiyth – 4

وعن سمرة بن جندب رضي الله عنه: أنَّ نبيَّ الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( مِنْهُمْ مَنْ تَأخُذُهُ النَّارُ إِلَى كَعْبَيهِ ، وَمنْهُمْ مَنْ تَأخُذُهُ إِلَى رُكْبَتَيهِ ، وَمنْهُمْ مَنْ تَأخُذُهُ إِلَى حُجزَتِهِ ، وَمِنْهُمْ مَنْ تَأخُذُهُ إِلَى تَرْقُوَتِهِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Samurah bin Jundub (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Miongoni mwa watu wa Motoni ni wale ambao moto kwa ukali wake utawafika kwenye tindi za miguu, na wengine kwenye magoti, na wengine mpaka kiunoni, na madhambi yao." [Muslim]





Hadiyth – 5

وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( يَقُومُ النَّاس لِرَبِّ العَالَمينَ حَتَّى يَغِيبَ أحَدُهُمْ في رَشْحِهِ إِلَى أنْصَافِ أُذُنَيهِ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Watasimama watu mbele ya Rabb wa walimwengu, (kwa amri Yake na kupatiwa malipo) hadi baadhi yao wapotee katika jasho lao hadi katika ya masikio yao." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]





Hadiyth – 6

وعن أنس رضي الله عنه، قَالَ : خطبنا رَسُول الله صلى الله عليه وسلمخطبة مَا سَمِعْتُ مِثلها قطّ ، فَقَالَ : (( لَوْ تَعْلَمُونَ مَا أعْلَمُ ، لَضحِكْتُمْ قَلِيلاً وَلَبَكَيتُمْ كَثِيراً )) فَغَطَّى أصْحَابُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم وَجُوهَهُمْ ، وَلَهُمْ خَنَينٌ . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

وفي رواية : بَلَغَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم عَنْ أَصْحَابِهِ شَيْءٌ فَخَطَبَ ، فَقَالَ : (( عُرِضَتْ عَلَيَّ الجَنَّةُ وَالنَّارُ ، فَلَمْ أرَ كَاليَومِ في الخَيرِ وَالشَّرِّ ، وَلَوْ تَعْلَمونَ مَا أعلَمُ لَضَحِكْتُمْ قَلِيلاً وَلَبَكَيْتُمْ كَثِيراً )) فَمَا أتَى عَلَى أصْحَابِ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يَوْمٌ أَشَدُّ مِنْهُ ، غَطَّوْا رُؤُسَهُمْ وَلَهُمْ خَنِينٌ .

Na imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: "Alituhutubia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), hotuba sijasikia mfano wake katu, akasema: 'Lau mngejua ninayoyajua, mngecheka kidogo na kulia sana.' Swahaaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakafunika nyuso zao na kulia kwa mayowe." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Katika riwaayah: "Habari zilimfikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) toka kwa Swahaaba zake, basi akahutubia, akasema: 'Nime onyeshwa Pepo na Moto sijaona kama leo katika mazuri na shari. Lau mngejua ninayoyajua basi mngecheka kidogo na kulia sana.' Hii ilikuwa siku nzito zaidi kwa Swahaaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Walifunika nyuso zao wakaanza kulia kwa nguvu.





Hadiyth – 7

وعن المقداد رضي الله عنه، قَالَ : سمِعْتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( تُدْنَى الشَّمْسُ يَوْمَ القِيَامَةِ مِنَ الخَلْقِ حَتَّى تَكُونَ مِنْهُمْ كَمِقْدَارِ مِيلٍ )) قَالَ سُلَيْم بنُ عامِر الراوي عن المقداد : فَوَاللهِ مَا أدْرِي مَا يعني بالمِيلِ ، أمَسَافَةَ الأرضِ أَمِ المِيلَ الَّذِي تُكْتَحَلُ بِهِ العَيْنُ ؟ قَالَ : (( فَيكُونُ النَّاسُ عَلَى قَدْرِ أعْمَالِهِمْ في العَرَقِ ، فَمِنْهُمْ مَنْ يَكُونُ إِلَى كَعْبَيْهِ ، ومنهم من يكون إِلَى ركبتيه ، ومنهم مَنْ يَكُونُ إِلَى حِقْوَيْهِ ، وَمِنْهُمْ مَنْ يُلْجِمُهُ العَرَقُ إلْجَاماً )) . قَالَ : وَأَشَارَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم بيدهِ إِلَى فِيهِ . رواه مسلم.

Toka kwa Al-Miqdaad (Radhwiyah Allahu 'anhu) Nilimsikia Rasuli wa Allaahu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Siku ya Qiyaamah jua litasongezwa kwa viumbe, litakuwa kiasi cha maili." Sulaym bin 'Aamir mpokezi kutoka kwa Al-Maqdaad alisema: "Naapa kwa Allaah! Sikujua alichokusudia kwa Maili - je, ni masafa ya ardhi au ni kijiti kinachopaka jicho wanja?, Watu watatokwa jasho kadiri ya matendo yao, kuna ambao jasho itawafika katika tindi mbili za miguu, na wengine magotini, na wengine kiunoni na wengine kufunikwa kabisa kwa mkono kwenye mdomo wake." [Muslim]





Hadiyth – 8

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( يَعْرَقُ النَّاسُ يَومَ القِيَامَةِ حَتَّى يَذْهَبَ عَرَقُهُمْ في الأرضِ سَبْعِينَ ذِراعاً ، وَيُلْجِمُهُمْ حَتَّى يَبْلُغَ آذَانَهُمْ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaah 'anhu) amesema kuwa: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: Watu watatoa jasho Siku ya Qiyaamah mpaka jasho yao ifike ardhini dhiraa sabini, naiwafunike, hadi ifike masikioni mwao." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 9

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : كُنَّا مَعَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم إذْ سمع وجبة، فَقَالَ : (( هَلْ تَدْرُونَ مَا هَذَا ؟ )) قُلْنَا : الله وَرَسُولُهُ أعْلَمُ . قَالَ : (( هذَا حَجَرٌ رُمِيَ بِهِ في النَّارِ مُنْذُ سَبْعينَ خَريفاً ، فَهُوَ يَهْوِي في النَّارِ الآنَ حَتَّى انْتَهَى إِلَى قَعْرِها فَسَمِعْتُمْ وَجْبَتَهَا )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) ambaye alisilimu: "Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na mara tukasikia sauti ya kitu kilichoanguka chini. Hapo akasema: "Je, mnajua hicho ni kitu gani?" Tukasema: "Allaah na Rasuli Wake wajua zaidi." Akasema: "Hilo ni jiwe liliorushwa Motoni miaka sabini iliyopita; lilikuwa likizunguka kwa kipindi mpaka leo ndilo limefika chini na ndio mmesikia kugusa chini." [Muslim]





Hadiyth – 10

وعن عدي بن حاتم رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( مَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ إلاَّ سَيُكَلِّمُهُ رَبُّهُ لَيْسَ بَيْنَهُ وبَيْنَهُ تَرْجُمَانٌ ، فَيَنْظُرُ أيْمَنَ مِنْهُ فَلاَ يَرَى إلاَّ مَا قَدَّمَ ، وَيَنْظُرُ أشْأَمَ مِنْهُ فَلاَ يَرَى إلاَّ مَا قَدَّمَ ، وَيَنْظُرُ بَيْنَ يَدَيْهِ فَلاَ يَرَى إلاَّ النَّارَ تِلْقَاءَ وَجْهِهِ ، فَاتَّقُوا النَّارَ وَلَوْ بِشِقِّ تَمْرَةٍ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Na imepokewa kutoka kwa 'Adiy bin Haatim (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna yeyote miongoni mwenu isipokuwa Allaah Atazungumza naye Siku ya Qiyaamah, kutakuwa hakuna mkalimani kati yake na Allaah. Kisha ataangalia kuliani mwake na wala hatoona kitu alichokitanguliza, kisha ataagalia mbele yake ataona Moto unampokea, kwa hiyo awezaye kutoa kipande cha tende moja kama sadaqa, na afanye hivyo." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 11

وعن أَبي ذر رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( إنِّي أَرَى مَا لا تَرَوْنَ ، أطَّتِ السَّمَاءُ وَحُقَّ لَهَا أنْ تَئِطَّ ، مَا فِيهَا مَوضِعُ أرْبَع أصَابعَ إلاَّ وَمَلَكٌ وَاضِعٌ جَبْهَتَهُ سَاجِداً للهِ تَعَالَى . والله لَوْ تَعْلَمُونَ مَا أعْلَمُ ، لَضَحِكْتُمْ قَلِيلاً وَلَبَكَيْتُمْ كَثِيراً ، وَمَا تَلَذَّذْتُمْ بالنِّساءِ عَلَى الفُرُشِ ، وَلَخَرَجْتُمْ إِلَى الصُّعُدَاتِ تَجْأرُونَ إِلَى اللهِ تَعَالَى )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika mimi naona msiyoyaona, na ninasikia msiyosikia. Mbingu zinalia na ina haki kufanya hivyo (kulia). Hakuna nafasi yeyote hata ya vidole vinne isipokuwa yupo Malaaika ametandaza mbawa yake akimsujudia Allaah Ta'aalaa. Naapa kwa Allaah! Lau mngekuwa mnajua ninayoyajua basi mngecheka kidogo na kulia sana; hamngekuwa ni wenye kustarehe na wake zenu katika vitanda. Mngefanya haraka kutoka barabarani na njiani ili kutaka ulinzi wa Allaah." [At-Tirmidhiy, ambaye amesema hii ni Hadiyth Hasan]





Hadiyth – 12

وعن أَبي برزة نَضْلَة بن عبيد الأسلمي رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( لا تَزُولُ قَدَمَا عَبْدٍ يَومَ القِيَامَةِ حَتَّى يُسْأَلَ عَنْ عُمُرِهِ فِيمَ أفنَاهُ ؟ وَعَنْ عِلمِهِ فِيمَ فَعَلَ فِيهِ ؟ وَعَنْ مَالِهِ مِنْ أيْنَ اكْتَسَبَهُ ؟ وَفيمَ أنْفَقَهُ ؟ وَعَنْ جِسمِهِ فِيمَ أبلاهُ ؟ )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Barzah Nadhlah bin 'Ubayd al-Aslamiy (Radhwiyah Allaah 'anhu) kuwa: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Haitaondoka miguu ya mja Siku ya Qiyaamah mpaka aulizwe kuhusu Umri wake ameumaliza vipi; na kuhusu elimu yake ametumia vipi; na kuhusu mali yake ameichuma vipi na ameitumia vipi; na kuhusu mwili wake ameuzeesha vipi? [At-Tirmidhiy, ambaye amesema ni Hadiyth Hasan]







Hadiyth – 13

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قرأ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ( يَوْمَئِذٍ تُحَدِّثُ أَخْبَارَهَا ) [ الزلزلة : 4 ] ثُمَّ قَالَ : (( أتَدْرونَ مَا أخْبَارهَا )) ؟ قالوا : الله وَرَسُولُهُ أعْلَمُ . قَالَ : (( فإنَّ أخْبَارَهَا أنْ تَشْهَدَ عَلَى كُلّ عَبْدٍ أَوْ أمَةٍ بما عَمِلَ عَلَى ظَهْرِهَا تَقُولُ : عَملْتَ كَذَا وكَذَا في يَومِ كَذَا وكَذَا فَهذِهِ أخْبَارُهَا )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Alisoma Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Kauli ya Allaah: (Siku hiyo itahadithia khabari zake) [Al-Zalzalah: 4]. Kisha akasema: "Je, mnajua khabari yake?" Wakasema: "Allaah na Rasuli Wake Wajua zaidi." Akasema: Hakika khabari yake ni kumshuhudia kila mja mwanamume au mwanamke kwa aliyoyafanya juu ya mgongo wake. Itasema: 'Ulifanya kadha na kadha siku kadha na kadha, hii ndiyo hiyo khabari yake.' [At-Tirmidhiy, ambaye amesema kuwa hii ni Hadiyth Hasan Swahiyh]





Hadiyth – 14

وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( كَيْفَ أنْعَمُ ! وَصَاحِبُ القَرْنِ قَدِ التَقَمَ القَرْنَ ، وَاسْتَمَعَ الإذْنَ مَتَى يُؤمَرُ بالنَّفْخِ فَيَنْفُخُ )) فَكَأنَّ ذلِكَ ثَقُلَ عَلَى أصْحَابِ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم فَقَالَ لَهُمْ : (( قُولُوا : حَسْبُنَا الله وَنِعْمَ الوَكِيلُ )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسنٌ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iid Al-Khudriy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Vipi nitakuwa na furaha na mwenye baragumu (Malaika Israfil) ametia mdomoni mwake hilo baragumu huku akisubiri idhini ni lini atapatiwa ili apulize." Kama kwamba hilo lilikuwa zito kwa Masahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), hivyo akawaambia semeni: "Hasbuna Allaahu wa Ni'mal Wakiil yaani Allaah anatutosha, naye ni mbora wa kutegemewa." [At-Tirmidhiy, ambaye amesema ni Hadiyth Hasan]





Hadiyth – 15

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( مَنْ خَافَ أدْلَجَ ، وَمَنْ أدْلَجَ بَلَغَ المَنْزِلَ . ألا إنَّ سِلْعَةَ اللهِ غَالِيَةٌ ، ألاَ إنَّ سِلْعَةَ الله الجَنَّةُ )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن )) .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kumuogopa adui hutoks wakati wa mwanzo wa usiku; na mwenye kutoka mapema (usiku), hufika sehemu ya usalama (kutokana na adui). Jueni ya kwamba bidhaa za Allaah zina thamani kubwa. Jueni ya kwamba bidhaa za Allaah ni Pepo Yake." [At-Tirmidhiy, ambaye amesema ni Hadiyth Hasan]





Hadiyth – 16

وعن عائشة رضي الله عنها ، قَالَتْ : سَمِعْتُ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( يُحْشَرُ النَّاسُ يَوْمَ القِيَامَةِ حُفَاةً عُرَاةً غُرْلاً )) قُلْتُ : يَا رَسُول الله ، الرِّجَالُ وَالنِّساءُ جَمِيعاً يَنْظُرُ بَعضُهُمْ إِلَى بَعْض ؟! قَالَ : (( يَا عائِشَةُ ، الأمرُ أشَدُّ مِنْ أنْ يُهِمَّهُمْ ذلِكَ )) .

وفي رواية : (( الأَمْرُ أهمُّ مِنْ أنْ يَنْظُرَ بَعضُهُمْ إِلَى بَعض )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .

Imepokewa kutoka kwake 'Aaishah (Radhwiyah Allaahu 'anhaa) ambaye amesema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Watu watafufuliwa Siku ya Qiyaamah wakiwa hawana viatu, uchi na wenye magovi." Nikasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Wanaume na wanawake wote wakiwa pamoja, si wataangaliana wao kwa wao?" Akasema: "Ee 'Aaishah! Jambo hilo litakuwa zito (lenye kutisha) zaidi ya wao kutaka kuangaliana." Na katika riwaayah nyengine: "Jambo hilo litakuwa muhimu zaidi kuliko kuangaliana wao kwa wao (hawatakuwa na nafasi hiyo)." [Al-Bukhaariy na Muslim]
 
Amefiwa Na Ndugu Yake Akiwa Mbali, Anaweza Kumswalia Swalaatul-Ghayb?
Maswali: Fiqhi



Amefiwa Na Ndugu Yake Akiwa Mbali, Anaweza Kumswalia Swalaatul-Ghayb?



Alhidaaya.com





Swali:



Ndugu yangu kafa lakini mimi sinipo naweza kumsaliya mahali nilipo?





Jibu:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Hakika ni kuwa mtu hafai kumswalia yeyote yule aliyekufa mbali ikiwa maiti ataswaliwa na Waislamu waliopo huko. Itafaa kwako kumswalia hapo ulipo ikiwa huko alikofia nduguyo hakuna Waislamu na hivyo hakuswaliwa.



Kwa sasa ni vigumu kupata sehemu ambayo hakuna Waislamu. Kitu ambacho unaweza kufanya ni kumuombea du’aa kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amghufurie na Amrehemu.



Soma jibu kuhusiana na swali kama lako katika kiungo kifuatacho:



Swalaah Ya Ghayb (Kumswalia Swalaah Maiti Aliye Mbali)





Na Allaah Anajua zaidi
 
Idadi Ngapi Ya Watu Wanaotakiwa Kuwa Mashahidi Wa Jambo Ki Shariy’ah?



Alhidaaya.com





Swali:



Assalaam Alaykum warahmatullaahi wabarakaatu. Mimi ni muislamu, Je ni idadi gani ya mashahidi wanaohitajika kutoa ushahidi juu ya jambo/tukio lolote?





Jibu:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Hakika mashahidi wanatofautiana kulingana na tukio au jambo lenyewe. Tunakuwekea hapa chini baadhi ya mifano:



1. Ikiwa ni suala la uzinzi kunahitajika mashahidi wanne (4) waadilifu.



2. Katika kukopeshana kunahitajika mashahidi wawili wanaume, wakikosekana wanaume wawili, basi mwanaume mmoja na wanawake wawili.



3. Katika ndoa vilevile kunahitajika mashahidi wawili.



4. Kuanza mwezi mpya katika kalenda ya Kiislamu kunahitajika shahidi mmoja na katika kutoka Ramadhwaan mashahidi wawili kuwa wameuona mwezi.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Imaam Asiyesoma Vizuri Qur-aan Anafaa Kuswalisha?
Maswali: Fiqhi


Imaam Asiyesoma Vizuri Qur-aan Anafaa Kuswalisha?



Alhidaaya.com







Swali:



Assalamu Alaykum,



Imamu ambaye hasomi vizuri Qur-an kiasi ambacho hawezi kusalisha Swala za Jahra (Magharibi, Isha na Asubhi), jee anaweza kutusalisha katika Swala za siri kama vile Adhuhuri na Alasiri?





Jibu:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuusia kuwa Imaam anatakiwa awe ni mjuzi juu ya wengine kwa kisomo cha Qur-aan. Ikiwa wapo wawili walio sawa kwa ujuzi na elimu ya somo hilo, basi atazamwe aliye mjuzi wa Sunnah za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na ikiwa kwa kipengele hicho pia wapo sawa basi atatizamwa yule ambaye ni mkubwa zaidi kwa umri awe Imaam kama ilivyothibiti katika Hadiyth:



عَنْ أَبِي مَسْعُودٍ الْأَنْصَارِيِّ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((يَؤُمُّ الْقَوْمَ أَقْرَؤُهُمْ لِكِتَابِ اللَّهِ فَإِنْ كَانُوا فِي الْقِرَاءَةِ سَوَاءً فَأَعْلَمُهُمْ بِالسُّنَّةِ فَإِنْ كَانُوا فِي السُّنَّةِ سَوَاءً فَأَقْدَمُهُمْ هِجْرَةً فَإِنْ كَانُوا فِي الْهِجْرَةِ سَوَاءً فَأَقْدَمُهُمْ سِلْمًا وَلَا يَؤُمَّنَّ الرَّجُلُ الرَّجُلَ فِي سُلْطَانِهِ وَلَا يَقْعُدْ فِي بَيْتِهِ عَلَى تَكْرِمَتِهِ إِلَّا بِإِذْنِهِ))

Kutoka kwa Abuu Mas’uwd Al-Answaariyy (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Awaswalishe watu yule mwenye kujua kusoma zaidi Kitabu cha Allaah na wakiwa katika kusoma wako sawa, basi mwenye ujuzi zaidi wa Sunnah, na wakiwa kwenye Sunnah wako sawa, basi aliyetangulia Hijrah, na wakiwa katika hijrah wako sawa, basi mkubwa wao kwa umri, wala asiswalishe mtu (mwengine) katika nyumba yake wala katika mamlaka yake wala asikae mahali pake pa heshima isipokuwa kwa idhini yake)) [Muslim]



Ikiwa Imaam ni hivyo ulivyosema itabidi mjaribu kutazama aliye mzuri zaidi au ikiwa amechaguliwa na wasimamizi wa Msikiti basi mzungumze na wasimamizi wa Msikiti ili aangaliwe mwengine wa kuongoza Swalaah. Na lau atakuwa hasomi vizuri Qur-aan lakini yeye ndiye bora katika mtaa au eneo hilo, basi huyo ndiye atakayeendelea kuwa Imaam hadi apatikane mwengine.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Kufuata Rai Katika Mas-ala Ya Dini
Maswali: Fiqhi



Kufuata Rai Katika Mas-ala Ya Dini



Alhidaaya.com





Swali:



Ndugu zangu, Assalaam alaykum,



Katika kujibu swali linalohusu "Mas-hul-khufayn" Mlijibu kama kuna tafauti ya Rai miongoni mwa ‘Ulamaa. Katika kuendelea kujibu swali hilohilo mlielezea kama katika masaala ya ibada Dini yetu hii haiendi na Rai zetu bali ni juu yetu kufuata alivyofanya mtume Muhammad (swalla allahu alayhi wa sallam).



Naomba ufafanuzi zaidi kuhusu masaala haya ya kufuata rai. Natumai nimefahamika. Ahsanteni sana.





Jibu:


AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Tulipokusudia kuwa Dini yetu haifuati rai ni pale rai zinapokosa ushahidi uliothibiti kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Hivyo, panapokuwa na maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) au maneno ya Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), basi rai yoyote ile haichukuliwi, kwani kuna watu wanataonguliza akili zao pale ambapo tayari Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wameshatoa hukmu, kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:




وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا ﴿٣٦﴾

Na haiwi kwa Muumini mwanamume na wala kwa Muumini mwanamke, Anapohukumu Allaah na Rasuli Wake jambo lolote, iwe wana hiari katika jambo lao. Na anayemuasi Allaah na Rasuli Wake, basi kwa yakini amepotoka upotofu bayana. [Al-Ahzaab: 36]



Na ndipo ukaona maneno ya 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) aliposema:



"لو كان الدين بالرأي لكان أسفل الخف أولى بالمسح من أعلاه لقد رأيت رسول الله صلى الله عليه وسلم يمسح على ظاهر خفيه" رواه أبو داود والدارقطني

Ingelikuwa Dini inakwenda kwa rai ingelikuwa kupangusa chini ya khuff (soksi za ngozi) ni bora zaidi kuliko juu. Hakika nimemuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa alihi wa sallam) anapangusa juu ya khuff (soksi za ngozi)” [Imepokelwa na Abu Daawuwd na ad-Daaraqutwniy]



Japokuwa inaweza isiingie kwenye akili za hao wenye kutumia rai zao wakaona kuwa kwa nini kusipanguswe chini yaani nyayoni penye kukanyagiwa ambapo ndipo panapokusanya uchafu? Na akamalizia 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwa kusema kuwa hivyo ndivyo alivyofanya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), kwa maana hata kama haingii akilini kwa baadhi ya watu, lakini maadam ndivyo alivyofanya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), basi hakuna tena rai hapo.



Ama rai katika Dini inakubalika pale ambapo hakuna dalili iliyo wazi katika masuala fulani. Na kwa upande mwengine hujulikana hizo rai kama ni Ijtihaad na pia kama Qiyaas katika upande wa Uswuwl. Na hivyo ni kama ilivyo katika Hadiyth ifuatayo:



عَنْ مُعَاذٍ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم حِينَ بَعَثَهُ إِلَى الْيَمَنِ ، فَقَالَ (( كَيْفَ تَصْنَعُ إِنْ عَرَضَ لَكَ قَضَاءٌ؟)) قَالَ : أَقْضِي بِمَا فِي كِتَابِ اللهِ ، قَالَ (( فَإِنْ لَمْ يَكُنْ فِي كِتَابِ اللهِ؟)) قَالَ : فَسُنَّةُ رَسُولِ الله ، قَالَ : ((فَإِنْ لَمْ يَكُنْ فِي سُنَّةِ رَسُولِ الله؟)) قَالَ : أَجْتَهِدُ رَأْيِي لاَ آلُو ، قَالَ : فَضَرَبَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم صَدْرِي ، ثُمَّ قَالَ : ((الْحَمْدُ ِللهِ الَّذِي وَفَّقَ رَسُولَ رَسُولِ اللهِ لِمَا يُرْضِي رَسُولَ الله)) سنن أبي داود

Kutoka kwa Mu’aadh kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa alihi wa sallam) alipomtuma Yemen alimuuliza: ((Utafanyaje yatakapokufikia mas-ala?)) Akasema: “Nitahukumu kwa Kitabu cha Allaah”. Akauliza: ((Ikiwa hutopata katika Kitabu cha Allaah?)). Akasema: “Kwa Sunnah ya Rasuli wa Allaah.” Akauliza: ((Ikiwa hukupata katika Sunnah ya Rasuli wa Allaah?)) Akasema: “Basi nitajitahidi rai yangu na sitovuka mipaka, Akasema: “Rasuli wa Allaah (Swallah Allaahu ‘alayhi wa sallam) akanipiga katika kifua changu akasema: ((AlhamduliLLaah Ambaye Amemuwafikia mjumbe wa Rasuli wa Allaah katika yale aliyoyaridhia Rasuli wa Allaah)) [Sunan Abi Daawuwd]



Ingawa Hadiyth hii wamekhitilafiana ‘Ulamaa kuhusu usahihi wake, ila baadhi yao wamesema ni Swahiyh kwa njia zake nyingi zenye kuitilia nguvu. Na wakasema kuwa inaungwa mkono na kauli za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuhusiana kutii kiongozi wa Dini:



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا ﴿٥٩﴾

Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Rasuli na wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli mkiwa mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri zaidi. [An-Nisaa: 59]



Na pia,



وَإِذَا جَاءَهُمْ أَمْرٌ مِّنَ الْأَمْنِ أَوِ الْخَوْفِ أَذَاعُوا بِهِ ۖ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى الرَّسُولِ وَإِلَىٰ أُولِي الْأَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنبِطُونَهُ مِنْهُمْ ۗ وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَاتَّبَعْتُمُ الشَّيْطَانَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٨٣﴾

Na linapowafikia jambo lolote la amani au la khofu hulitangaza. Na lau wangelirudisha kwa Rasuli na kwa wenye madaraka kati yao, wangelijua wale wanaotafiti wakabainisha ya sahihi miongoni mwao. Na lau si fadhila ya Allaah juu yenu na rahmah Yake kwa yakini mngelimfuata shaytwaan ila wachache tu.[An-Nisaa: 83]


Hivyo masuala ya rai yanakubalika pale ambapo hiyo rai haitapingana na Qur-aan au Sunnah. Na ndio maana Imaam wakubwa wa Madhehebu manne wakawa wanatofautiana katika mas-ala mbalimbali ya ki-Fiqhi. Lakini Imaam hao wote wanaheshimiwa kwa elimu zao na Ijtihaad zao, kwa kuwa vilevile Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) keshaeleza kuwa atakayejitahidi miongoni mwa Imaam au 'Aalim, akapatia katika ijtihad yake, atapata ujira mara mbili, na atakayekosa atapata ujira mmoja [al-Bukhaariy na Muslim].



Yote hayo ni katika kuonyesha kuwa rai ambayo inawafikiana na Qur-aan na Sunnah inakubalika katika Dini.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Kuhudhuria Shughuli Za Mazishi Za Wasio Waislamu Inafaa?



Alhidaaya.com



Swali:



Assalaamu alaikum warah matullahi wa barakaatuh.



Shukurani kwa juhudi mnayoifanya kutuelimisha kuhusu dini yetu. Allaah awalipe wema na awahifadhi. Swali langu ni hili: Je sheria ya dini yetu ya uislamu inaturuhusu kuweza kuhudhuria shughuli za kuzika asiyekuwa muislamu? Wengine wanasema eti unaweza kuhudhuria shughuli nyingine lakini usiende tu na jeneza makaburini, wengine wasema unaeza kwenda hata makaburini. Naomba muniweke wazi In shaa Allaah. Asanteni.





Jibu



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Uislamu hautaki kabisa kuvunja na kuharibu mahusiano na jamaa hata wakiwa si Waislamu. Uislamu umeweka umuhimu mkubwa kuwa na uhusiano bora na wazazi na jamaa. Na kwa hiyo, ukamuamrisha Muislamu awafanyie wema wazazi na jamaa hata wakiwa si Waislamu. Hivyo, Muislamu anaruhusiwa kuhudhuria mazishi ya wazazi na jamaa wasio Waislamu ila haruhusiwi kushiriki katika ‘amali za kidini au zinazo kwenda kinyume na Uislamu.



Uislamu unataka wazazi waheshimiwe kwa kiasi kikubwa. Hivyo, Allaah Aliyetukuka Amesema:



وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۚ إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا ﴿٢٣﴾

Na Rabb wako Amehukumu kwamba: Msiabudu isipokuwa Yeye Pekee na (Ameamrisha) kuwafanyia ihsaan wazazi wawili. Kama mmoja wao akifikia uzee naye yuko pamoja nawe, au wote wawili basi usiwaambie, Uff! Na wala usiwakemee; na waambie maneno ya heshima. [Al-Israa: 23].



Pia Amesema Aliyetukuka:



وَإِن جَاهَدَاكَ عَلَىٰ أَن تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۖ وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا ۖ وَاتَّبِعْ سَبِيلَ مَنْ أَنَابَ إِلَيَّ ۚ ثُمَّ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٥﴾

Lakini wakikushikilia kuwa Unishirikishe na ambayo huna elimu nayo, basi usiwatii. Na suhubiana nao kwa wema duniani, na fuata njia ya anayerudi kutubia Kwangu. Kisha Kwangu ndio marejeo yenu, na Nitakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda. [Luqmaan : 15].



Jukumu la ukarimu na mahusiano mema huhimizwa nyakati za furaha, shida na majanga, kubwa ikiwa ni kifo. Kifo ambacho kinawaleta jamaa pamoja wanapohuzunika kwa kuondokewa na mmoja wao. Mwanadamu anakuwa ni mwenye kuonyesha hisia zake kwa aliyekufa sawa akiwa ni jamaa au rafiki wa karibu. Kwa ajili ya hiyo, tunasoma katika Hadiyth iliyo sahihi kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) aliyesema: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alizuru kaburi la mama yake na kulia na kuwafanya waliokuwa naye pia kulia, akasema:



"Nilimuomba Rabb wangu Mlezi Aniruhusu kumuombea msamaha mama yangu, lakini Alikataa kunipatia idhini kwa hilo. Kisha nikamuomba ruhusa kulizuru kaburi lake, naye Akanipatia ruhusa. Hivyo, zuruni makaburi kwani yatamkumbusha mmoja wenu kifo" [Muslim, Ahmad, Abu Daawuud, an-Nasaa’iy na Ibn Maajah].



Ziada ya hayo, Uislamu unaita na kusisitiza katika kumheshimu mwanaadamu yeyote, ikiwa ni Muumini au asiyekuwa Muislamu, katika uhai wao na baada ya kuaga dunia.



[Imenukuliwa na Al-Bukhaariy na Muslim] katika Hadiyth kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisimama pindi jeneza ya Myahudi ilipokuwa ikipita mbele yake. Mtu mmoja akamuarifu kuwa aliyekufa ni Myahudi tu. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Je, hiyo si nafsi?"



Hivyo, nafsi ya baba, mama au jamaa wa karibu anahitaji kuheshimiwa. Kwa hiyo, Muislamu anaweza kuhudhuria mazishi ya wazazi ambao si Waislamu, au jamaa zake, maadamu hatoshiriki katika maombi, ‘amali za kidini na nashati nyingine za kidini. Pia anaweza kushiriki katika mazishi, na katika yote hayo ni lazima nia yake iwe ni kutekeleza wema kwa wazazi na kuweka mahusiano mazuri na jamaa na marafiki kwa msiba uliowakumba na kudumisha mahusiano mema. Lile ambalo linakatazwa ni kuwaombea wasiokuwa Waislamu hata kama ni wazazi.



Kadhalika imepokewa kuwa ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alisema, "Alipofariki Abu Twaalib, nilimjia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na nikamwambia, "’Ami yako, mzee aliyepotoka, amefariki." Akasema, "Nenda kamzike." [Abu Daawuud, An-Nasaaiy].





Na Allaah Anajua zaidi
 
Kulisha Masikini Sitini



Alhidaaya.com





Swali:



Asalamu Alaykum,



Ikiwa mtu analisha masikini 60 jee mtu huyo anakuwa kafanya nini mbele ya Allaah? Naomba ufafanuzi wako





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Amma ba'ad,



Kulisha masikini kwa idadi yoyote ni amali njema na Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa Amesisitiza sana katika Qur-aan kulisha masikini na atakayefanya hivyo basi atapata thawaabu zake.



Ama idadi ya kulisha masikini 60 haikutajwa kuwa khaswa ina fadhila fulani ila tu imekuja hukumu ya Kafara ya 'Adh-Dhwihaar' ambayo inatoka katika neno la 'Adh-Dhwahr' yaani mgongo. Ilikuwa katika zama za Jaahiliyyah (zama za ujinga, kabla ya Uislamu) mume humuambia mkewe "Umekuwa kwangu kama mgongo wa mama yangu". Na ilikuwa ndio njia mojawapo ya kutoa Talaka wakati huo.Na Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa Ameruhusu Ummah huu wa Kiisalmu kulipa Kafara kwa kauli hii na haihesabiki kama ni talaka kinyume na ilivyo katika Ujaahiliyyah.



Kafara hii imetajwa katika aayah zifautazo ambazo ziliteremshwa baada ya Bibi Khuwaylah bint Tha'alabah kumshtakia Nabiy( Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kwamba mumewe 'Aws bin As-Swaamit amemwambia kauli hiyo ya Adh-Dhwihaar :



قَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّتِي تُجَادِلُكَ فِي زَوْجِهَا وَتَشْتَكِي إِلَى اللَّـهِ وَاللَّـهُ يَسْمَعُ تَحَاوُرَكُمَا ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ﴿١﴾الَّذِينَ يُظَاهِرُونَ مِنكُم مِّن نِّسَائِهِم مَّا هُنَّ أُمَّهَاتِهِمْ ۖ إِنْ أُمَّهَاتُهُمْ إِلَّا اللَّائِي وَلَدْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَيَقُولُونَ مُنكَرًا مِّنَ الْقَوْلِ وَزُورًا ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ لَعَفُوٌّ غَفُورٌ﴿٢﴾وَالَّذِينَ يُظَاهِرُونَ مِن نِّسَائِهِمْ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا قَالُوا فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مِّن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا ۚ ذَٰلِكُمْ تُوعَظُونَ بِهِ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ﴿٣﴾فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ مِن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا ۖ فَمَن لَّمْ يَسْتَطِعْ فَإِطْعَامُ سِتِّينَ مِسْكِينًا ۚ ذَٰلِكَ لِتُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۚ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ ۗ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٤﴾

Allaah Amekwishasikia kauli ya yule mwanamke anayejadiliana nawe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mumewe, na anamshitakia Allaah; na Allaah Anayasikia majibizano yenu. Hakika Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote. Wale miongoni mwenu wanaowatamkia wake zao dhwihaar: Nyinyi kwetu kama migongo ya mama zetu. Hao wake zao si mama zao. Hawakuwa mama zao isipokuwa wale waliowazaa. Na hakika wao bila shaka wanasema yasiyokubalika na kauli ya kuchukiza na uongo. Na hakika Allaah bila shaka ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kughufuria. Na wale wanaowatamkia wake zao dhwihaar, kisha wakarudi katika waliyoyasema (kuitengua dhwihaar), basi ni kuacha huru mtumwa kabla ya kugusana. Hayo mnawaidhiwa kwayo. Na Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. Na yule asiyepata uwezo, basi afunge Swiyaam miezi miwili mfululuzo kabla ya kugusana. Na yule asiyeweza, basi alishe chakula masikini sitini. Hivyo ili mumuamini Allaah na Rasuli Wake. Na hiyo ni mipaka ya Allaah. Na makafiri watapata adhabu iumizayo. [Al-Mujaadalah :1-4]





Na Allaah Anajua Zaidi
 
Maswali: Fiqhi


Kumuadhinia Maiti Anapozikwa Inajuzu?



Alhidaaya.com





Swali:



Wakati wa kuzika maiti watu wengine wanawa adhiniya maiti inafaa.



Jibu:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Haifai Muislamu kuadhiniwa kaburini au nje yake anapoaga dunia. Haikupatikana kabisa dalili ya kufanya hivyo katika mafunzo ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).



Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida zaidi:



Dalili Za Kheri Katika Mambo Yamfaayo Maiti



Yampasayo Maiti





Na Allaah Anajua zaidi
 
Kusafirisha Maiti Japo Kuna Waislamu, Kuipeleka Alipotoka Inajuzu?



Alhidaaya.com



Swali:



Assalam Alykum wa -Rahmatu Allaahi wa barakatuh. ALLAAH akujaliyeni kila la kheri na afya njema. Nina shukuru kwa msaada wenu na kwakujitolea kutu elimisha.



Swali langu nikuomba kuelimishwa mimi na wenzangu kuhusu maisha tunao kwa wakazi wa europa. Je, ni halali kusafirisha maiti, ikiwa kuna waislam hapo?





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Haijapatikana kabisa katika historia na maisha ya Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu ‘anhum) kuwa walisafirisha maiti ili kwenda kuzikwa sehemu nyingine.



Hivyo, haijuzu kwa Muislamu kusafirisha maiti ya Muislamu kuipeleka sehemu nyingine ili ipate kuzikwa. Ni jukumu la Waislamu wa sehemu hiyo kumfanyia mambo manne maiti huyo, nayo ni:



1. Kumuosha.



2. Kumkafini.



3. Kumswalia.



4. Kumzika.



Wale ambao si katika jamaa zake wafanye bidii kumuombea maghfira kwa Allaah Aliyetukuka.



Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:



Inafaa Kusafirisha Maiti Kutoka Mji Hadi Mji Mwengine?





Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Fiqhi


Kusafirisha Maiti Kutoka Mji Hadi Mji Mwengine Inajuzu?



Alhidaaya.com



Swali:



As-salaam Aleykum.



Nawashukuru sana nyote mnaotupa elimu kupitia mtandao, na sifa zote njema ni za ALLAAH (SW).



In shaa Allaah nategemea kupata elima kuhusu kusafarisha Maiti kwa wale wanaokutwa na umauti mjini kisha kwenda kuzikiwa vijijini (nyumbani) kwao.

Na ni ipi hukumu ya wanaokwenda kwenye misafara hiyo.





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Nabiy, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.) kama ilivyozoelekea na wengi, bali andika kwa kirefu maneno hayo bila ya kuyafupisha. Andika (Subhaanahu wa Ta’aalaa) baada ya kumtaja Allaah, na andika Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) au (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kumtaja Nabiy. Hivyo ndivyo inavyopaswa, na ndio heshima zaidi na utukufu na ndivyo inavyotamkwa na si kama inavyofupishwa na wengi kimazoea na kivivu.



Hakika ni kuwa mas-ala haya hayana utata kwani haijapatikana katika maisha ya watangu wema waliopita kwamba walifanya shughuli hiyo ya kusafirisha maiti. Swahaba (Radhwiya Allaahu 'anhum) walikufa miji ya mbali – wapo wale waliokufa sehemu ya Shaam, Misri, Ethiopia, Iraq, Yemen, Morocco, Uturuki na sehemu nyingine za mbali. Ilikuwa ni aula kwao kusafirishwa katika sehemu walizotoka ambazo pia zilikuwa tukufu kama Makkah na Madiynah lakini hakuna hata mmoja aliyesafirishwa kuzikwa sehemu hizo.



Yapo makaburi ya Swahaba (Radhwiya Allaahu 'anhum) takriban 18,000 katika sehemu ya Shaam pekee.



Hili la kusafirisha maiti ni uzushi mpya ambao umejitokeza katika sehemu zetu tukiwaiga wasiokuwa Waislamu katika hilo au kufuata ada na desturi zetu ambazo sio nzuri. Mazishi ya Uislamu ni kuwa yanatakiwa yafanywe haraka iwezekanavyo ili akiwa maiti ni mwema afike kwa Allaah Aliyetukuka mapema na akiwa ni muovu basi muondoshe uovu huo nyumbani kwa haraka.



Anasema Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



"Harakisheni jeneza, akiwa ni mtu mwema, basi ni kheri mnayoitanguliza kwake, na akiwa ni kinyume chake (muovu) basi hiyo ni shari (mliyoibeba ambayo mnatakiwe haraka) muishushe kutoka katika shingo zenu". [Al-Bukhaariy na Muslim na wengneo].



Maamrisho hayo ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) si tu kuharakisha kulipeleka jeneza kaburini, bali ni kuharakisha kuzifanya taratibu zote za kumuandaa maiti kwa ajili ya kumswalia na kumzika.



Kadhalika Hadiyth hiyo inajulisha umuhimu wa kumzika pale pale alipofariki maiti na si kumchelewesha kwa kumsafirisha eneo jingine au mji au nchi nyingine, kwani kufanya hivyo kutachelewesha kuzikwa maiti na hivyo kutagongana na maamrisho hayo ya kipenzi chetu.



Jaabir bin ‘Abdillaah (Radhwiya Allaahu ‘anhuma) anasimulia:



"Katika vita vya Uhud Waislamu waliokufa walikuwa wakibebwa kupelekwa (katika makaburi ya) al-Baqiy’i. Lakini baadaye ikatangazwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kaamrisha nyinyi kuzika waliokufa pale walipofia/walipouliwa. Hapo ni wakati ambao mama yangu alikuwa tayari keshaweka maiti ya baba yangu na mjomba wangu juu ya ngamia. Na hapo wakachukuliwa na kurudishwa kwenda kuzikwa kule walipouliza." [Ahmad, Abu Daawuud na wengineo. Imethibitishwa usahihi wake na Shaykh al-Albaaniy katika Ahkaamul Janaaiz uk.25]



Pia tunapata kuwa ‘Abdur-Rahmaan bin Abi Bakr (Radhwiya Allaahu ‘anhuma) alifariki katika sehemu iitwayo Waadul Habasha kiasi cha maili 12 kutoka Makkah na akasafirishwa kuzikwa Makkah. Na mama wa waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) ambaye ni ndugu na ‘Abdur-Rahmaan alipokwenda Makkah alizuru kaburi lake na akasema:



"Nimehuzunishwa kwa kuwa hakuzikwa kule alipofia" [Kainukulu al-Bayhaqiy, na Shaykh al-Albaaniy kaeleza usahihi wake kwenye Ahkaamul Janaaiz uk. 25]

Na kwa hili akasema Imaam an-Nawawiy:



"Ikiwa mtu kaacha katika wasia wake kuwa atakapokufa asafirishwe kuzikwa mahala pengine, wasia kama huo unapaswa kutofanyiwa kazi kwani unapingana na mafunzo ya kukatazwa kusafirishwa maiti. Na huu ndio msimamo sahihi na uliokubalika, ambao unawafikiwa na Wanachuoni wengi." [Imaam an-Nawawiy Al-Adhkaar]



Muislamu anafaa azikwe anapokufa kwani hakuna fadhila ya kupelekwa nyumbani au kijiji mlichotoka. Utapata kuwa warithi ambao wanafaa wabakishiwe mali huwa hawapati kwani mali nyingi inafujwa kwa ajili ya kusafirishwa au inatumika kwa wingi ambapo mazishi ya Kiislamu yanatakiwa yawe ni mepesi na yenye kutumia pesa ndogo. Hakika ni kuwa ikiwa kusafirisha kunakatazwa na wenye kulifuata pia kwenda nalo kijijini watakuwa na sehemu yako ya madhambi. Inatakiwa watu wasifanye hivyo ili hii ada mbaya iondoke.



Maiti inaweza kusafirishwa ikiwa pale alipokufa Muislamu hakuna Waislamu ambao wanaweza kumuosha, kumvisha sanda, kumswalia na baadaye kumzika. Ikiwa ipo shida hiyo basi maiti hiyo itasafirishwa sio kijijini kwao bali kijiji kilicho karibu na hapo alipokufa ili aweze kutimiziwa mambo hayo manne.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Kuzikwa Asiye Muislamu Ndani Ya Kaburi Alilozikwa Mtoto Muislamu



Alhidaaya.com





Swali:



Bismillahi Rahamani Raheem



Asaalam Alykum Waramathullahi Wabarakatu.



Swali langu ni juu ya mazishi hapa Ujerumani hasa kwa sisi ndugu zenu waaislamu tunaoishi huku.



Awali nitaelezezea kisa chenyewe kwa ufupu ambacho kitaelezea swali halisi.

Mimi nimzawa wa Mombasa nimejuana na ndugu waislamu wengi sana hapa wengi wao usafirisha maiti zao makwao mfano ya ndugu wengi wanaotoka (North Africa) au Uturuki.



Sasa kunaeye kaka yetu mmoja MMerikani mweusi alisilimu zaidi miaka kumi na mbili sasa kaoa mke wakazaa mtoto wao wa kwanza bahati mbaya huyu mtoto alifariki hapa Ujerumani wakapewa sehemu ya kumzika imamu wa msikiti tunaoswali aliwongoza kwa kila jema la kisheria kwa kumzika mtoto huyo. Hapa zipo sehemu zilizotengwa kwa waislamu lakini mitaa maalumu sasa yeye kwa ujiandikishaji wa ukaaji wa hapa mtaa wao hawakuwa na sehemu ya waislamu hakaomba kumzika mtoto wake kwa sehemu ya waislamu lakini walimkatalia kisheria lazima hamzike sehemu ya mji wao. Basi walifanya hivyo walimzika sehemu ya kuzikana hapo kwao mjini sehemu wanaozikwa wakristo, lakini alizikwa kiislamu.



Sasa mda mrefu sasa zaidi ya miaka minanae serikali imemletea bili ya kulipia kaburi sehemu aliyozikiwa aliyefariki huyo ya 500€ hii wanasema ni sheria hapa aliyefariki kulipiwa kaburi kwa umri wote litakapojulikana hili ni kaburi la fulani bin fulani. Au kama hataki kulipa basi hiyo sehemu atazikwa mtu mwengine yeyote ambaye atafuatia ili hii sehemu ipate kulipiwa kodi. Huyu ndugu yetu kanielezea kuwa yeye alikuwa anataka kuchimba na kutoa sehemu iliyobakia ya aliyefariki mtoto wake na kuisafirisha nchi yeyote ya kiislamu iliyoko karibu hawa watu wa serikali wanamshauri yakuwa huyo alikuwa mtoto mdogo na kufikia sasa sahau hapatapatikana lolote na pia patazikwa yeyote atakayejaliwa tena. kama hatalipia hiyo kaburi au kwa desturi mtu yeyote atakaye shindwa kulipia kaburi basi mabaki ya aliyefariki yatatolewa na kuchomwa kisha jivu litupwe hili papatikane sehemu ya mtu mwingine.



Subuhana Allaah hii ni huzuni sana yeye kanieleza kisa hichi jana baada ya kupokea hii bili ya kulipia kaburi na mawazo duni ya makafiri waliyompa.



Ndugu zetu waaislamu wa alhidaaya naomba msaada wenu kwa kutufafanulia usawa wa kisa hichi kufuatia kurani tukufu na pia katika hadiyth za Nabiy wetu Muhammad (s.a.w).



Hapa huyu ndugu yetu kataka ushauri kutoka kwangu nami nikamuambia nitawauliza mashekhe wetu wa ukumbi wa alhidaaya kwani hata sisi hatujui lini mauti yatatufikia.



Baraka lahu fik.



Barua Ya Pili:



Bismillahi Rahamani Raheem.



Asalaam Alykum Waramathullahi Wabarakatu.



Ndugu zangu waislamu mimi tena nimerudia mara ya pili kuwaletea maombi yangu juu ya swali langu la jana nililolileta kwenu juu ya kulipia kaburi ama wazazi wanahitajika kutoa mabaki ya aliyefariki au pahala papo hapo mazikwe mtu mwengine.



Tafadhali tupeni jawabu wasaa utakavyowezekana kwani huyu ndugu yetu ameletewa barua kwa mda wa wiki mbili sehemu hiyo akishindwa kulipia au kutoa kilochobakia basi serikali washadhaminiwa na watu wengine tayari kuzika maiti ya jamma yao kwani mahala kama nilivyotangulia kueleza kuwa ni pa wakristo na hata huko kwa waaislamu lazima pia kulipia kaburi kisheria ya serikali umri wote wa kaburini.



Je huyu ndugu yetu ashike wapi pa sawa kufuatia kurani tukufu na sunnah za Nabiy wetu Muhammad (s.a.w). Ninaomba msaada kutoka kwa Mashekhe wetu wa alihidaaya kwani hata yeye mwenyewe amenituma kuulizia kwani hafahamu kiswahili.



Masaalam.





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Tunasikitika sana kupata Swali hili la ndugu yetu aliyefikwa na janga hilo la maiti ya mwanawe, tunaanza na kumuombea Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amfanyie wepesi jambo gumu hili na Ampe subira kwa hali yoyote itakavyomfika.



Kwanza tunapenda kuwatambulisha ndugu zetu popote walipo kwamba mtu anapofariki haipasi kuhamishwa maiti kupelekewa nchi nyingine ila ikiwa kuna sababu maalumu. Hakuna mwenye kujua wapi atafariki, ardhi yote ni ardhi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ambaye Ametueleza kuwa:



وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ ﴿٣٤﴾

Na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani, hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Luqmaan: 34]



Sunnah ilivyokuwa wakati wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake ni kumzika aliyefariki katika makaburi ya mji huo aliofariki. Mashuhadaa walizikwa sehemu ile ile waliyofariki. Hakuna dalili yoyote au usimulizi kwamba Swahaba au Salafus Swaalih (Wema Waliotangulia) waliwahamisha watu wao waliofariki kuwazika miji mingine au nchi zingine.



Kwa sababu hii 'Ulamaa wengi wamekataza jambo hili ila tu ikiwa kuna sababu au dharura maalumu mfano; kama kuna khofu ya kuwa kaburi litatendwa vibaya hapo itakuwa ni bora kumzika sehemu ambako atasalimika na uovu wowote.



Vilevile zikiwa gharama za kuzikia maeneo hayo kama ilivyo huko Ulaya, Marekani na Japan, na akawa mtu huyo hana gharama hizo au hakuweza kupata msaada wowote kutoka kwa Waislam walio sehemu hizo, na kukawa kuisafirisha maiti ile ni nafuu mno kuliko kuizikia pale na hali hana uwezo, basi kwa hali hiyo Maulamaa wamejuzisha hali hiyo kwa dharura hiyo.



Kwa hivyo, ndugu zetu wanaosafirisha maiti zao watambue hili. Ni bora wajiepushe na kwenda kinyume na sheria bali wakimbilie kumzika maiti wao mji huo huo aliofariki, jambo ambalo linapendekezeka zaidi katika sheria. Hivi ni kumhifadhi maiti kutokana na mateso na usumbufu wakati anatayarishwa na kufanyiwa maandalizi maiti kwa ajili ya kumsafirisha, na pia kujiepusha na taklifu kubwa za kifedha zinazowakabili watu kwa jambo ambalo halikuwekwa katika sheria.



Kuzikwa mtu mji wake hakutamsaidia maiti lolote katika kumzidishia mema kwenye kitabu chake wala haitomsaidia lolote kaburini, bali ni amali zake ndizo zitakazomfaa.



Ama kuhusu hali ya mtoto huyo aliyezikwa miaka minane nyuma katika makaburi ya wasio Waislamu na hivi sasa hali imefika kama hivyo ya kutaka kuzikwa asiye Muislamu juu yake, tunakuwekea hapa maelekezo ambayo anapaswa kufuata na kukubali kuyakabili kutokana na mafunzo ya sheria ya dini yetu:



1. Kwanza ajaribu kuuliza na kutafuta msaada wa hali na mali katika Jumuiya za Kiislamu zilioko huko Ujerumani wampatie njia ya kumfukua maiti na kumzika katika makaburi ya Kiislamu.



2. Pindi akishindwa kupata msaada huo, lililo bora kukabili ni kuwaacha Serikali wazike mtu mwingine juu yake, japo kama sio Muislamu kama ulivyoelezea, kwani baina ya kuchagua kufukuliwa kisha akachomwe na baina ya kumzika mtu juu yake, ni bora kumzika mtu juu yake kuliko kuchomwa kwa sababu kuchomwa maiti sio jambo lililo na asasi katika dini yetu, hayo ni mambo ya washirikina kama Mabaniani (Hindus). Ama kuzikwa watu wengi katika kaburi moja limepatikana dalili mfano katika vita vya Uhud. Japo katika suala hili azikwaye si Muislam, lakini kwa dharura hiyo hakuna budi.



3. Ikiwa Serikali imegoma kufanya hivyo na imeshikilia kuwa lazima mabaki ya maiti yatolewe na yachomwe na kutupiliwa mbali, basi pia ndugu yetu asitaharuki na kukhofu kuwa atakuwa ameruhusu jambo ambalo haliko katika sheria, kwani hapa atakuwa yeye hana makosa kabisa na ataangukia katika 'Mudhwtwarr' (asiye na budi) kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika hali ya kula visivyo vya halali :



إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةَ وَالدَّمَ وَلَحْمَ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ بِهِ لِغَيْرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٧٣﴾

Hakika Allaah Amekuharamishieni mzoga na damu na nyama ya nguruwe na kilichotajiwa katika kuchinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Allaah. Lakini aliyefikwa na dharura bila ya kutamani wala kupindukia mipaka; basi si dhambi juu yake. Hakika Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-Baqarah: 173]



Vile vile kwa Rahma Yake Rabb wetu Mtukufu Hatukalifishi jambo tusiloliweza kwa uwezo wetu au lililo nje ya uwezo wetu:

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ

Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake. [Al-Baqarah: 286]



Juu ya hivyo mwanawe aliyezikwa hapo ni mtoto mdogo hana dhambi yeyote hivyo hata akizikwa asiye Muislamu juu yake hatoathirika kitu bali yeye ni wa kwenda Peponi moja kwa moja In shaa Allaah.



Kwa hivyo hali yoyote itakayomkabili hata ikiwa ni ya ubaya vipi hatohesabiwa kuwa amefanya makosa.



Hayo juu ya kwamba mtoto mwenyewe amezikwa miaka minane nyuma, kwa hivyo bila shaka hivi sasa hatakuwa amebakia kitu bali labda ni mafupa tu kwa hiyo kumchimbua na kuyakusanya hayo mabaki yake haitokuwa jambo la busara kulingana na taklifu itakayopatikana; kwanza kujitia huzuni zaidi ya kumfufua mwanawe, pili taklifu ya gharama kubwa itakayomgharimu.



Tunamuomba ndugu yetu akinai na Qadhwaa na Qadar: (Yaliyohukumiwa na Yaliyokadiriwa) na Allaah na atambue kuwa kukubali makadirio na mtihani na kusubiri ni kupata thawabu kwake na ahli yake. Tunazidi kumuombea Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amuondoshee huzuni ya jambo hili na abakie katika kuridhika na haya majaaliwa.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Fiqhi


Kwa Nini Watoto Waliokufa Wanaombewa Du’aa Katika Swalaah Ya Jenaza Na Hali Hawana Madhambi?



Alhidaaya.com



Swali:



Assalaam Alaykum,



Tunavyoambiwa katika dini kuwa, watoto wadogo na wasiofikia baleigh akil, wakifariki huwa hawana hesabu yaani ni moja kwa moja peponi. Jee nini asili au mantiki ya kuwaombea dua kuepushwa na moto wakati ya sala ya maiti??





Jibu:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Hilo ambalo ndugu yetu aliloandika si sawa kwani zipo Hadiyth nyingi kuhusu hukumu ya watoto wachanga watakaohukumiwa na Allaah Aliyetukuka.



Ama suala la watoto wachanga wanachuoni waliotangulia na wa sasa wametofautiana, Allaah Awarehemu wote. Mas-ala yenyewe ni kuhusu watoto waliokufa wakiwa wachanga, ilhali wazazi wao ni makafiri: Je, hukumu yao ni gani? Na hivyo hivyo, wendawazimu, viziwi, vikongwe na wanaokufa katika Fitwrah (maumbile ya mwanaadam ya asili –Tawhiyd-), wakiwa hawajafikiwa na ujumbe, hukumu yao itakuwa ipi? Hadiyth nyingi zimepokewa katika mas-ala haya, lakini tuchukue mojawapo tu:



Imepokewa na Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kila kinachozaliwa kinazaliwa katika Fitwrah (maumbile ya mwanaadamu ya asli –Tawhiyd-), ni wazazi wake ndio wanaomfanya awe Myahudi, Mkristo au Majusi kama hayawani wanavyozaa hayawani – je waona yeyote anayezaliwa akiwa ameatilika (akiwa hana kiungo kimoja au kingine)?"



Katika riwaya moja, walisema: "Ee Rasuli wa Allaah! Waonaje kuhusu wale wanaozaliwa wakiwa wachanga?" Akasema: "Allaah Anajua zaidi kwa kile ambacho wangekifanya" [al-Bukhaariy na Muslim].



Mantiki hiyo ni kuwa Allaah Aliyetukuka Anajua zaidi kuwahusu wao hivyo inakuwa vyema kuwaombea kama tulivyofunzwa na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ili waingie katika rehema ya Rabb wao.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Naam ndugu zangu katika imani naamini kabisa tunaendelea kupata masomo na mafunzo juu ya uislamu wetu

Na hii inatufanya tuijue dini yetu na kuyaendea mambo kwa namna ambayo dini inatutaka tuwe hivyo

Uislamu sio kwa ajili ya watu wanao bahatisha Uislamu wao bali kwa wanao soma na kuufahamu Uislamu wao

Endelea kufuatilia uzi......
 
Baadhi ya post zangu za zamani.....

UNAWEZA KUMUOMBA ALLAH KWA AMALI ZAKO NJEMA

Matendo mema ambayo ninayazungumzia hapa ni Matendo ambayo mja ameyafanya Kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu Tu.

Je namaanisha nini Kwa kusema hivi?
Namaanisha Yale matendo mema ambayo uliyafanya Kwa kumkusudia yeye Peke yake pasina kutaka kuonekana na watu au kujionyesha Kwa watu kuwa umefanya Jambo Fulani ili upate sifa au utambulike umefanya Jambo Fulani.

Kwa mfano, kuna watu hutoa sadaka ili watu wamuone kuwa Ni mtoaji sadaka mzuri au anasaidia yatima na matangazo na Waandishi WA habari juu au picha,huyu atakuwa amefanya kujionyesha ili jamii imtambue kuwa Leo ETUGRUL BEY amesaidia kituo Fulani cha watoto yatima,hapa nitakuwa nimefanya Jambo hili Kwa AJILI ya watu na si Kwa AJILI ya Mungu.

Na matendo kama haya haijalishi ni mazuri kiasi gani lakini mbele ya Mwenyezi Mungu hayana malipo yoyote Yale,malipo yake ushapata Kwa kujulikana na watu kuwa umefanya Jambo Fulani.

Kwahiyo siku zote jichunge Sana pale unapo fanya ibada mbali mbali na jiulize je hili nalifanya Kwa AJILI ya Mungu au wanadamu?

Sasa kama unafanya matendo mema Kwa AJILI ya kutaka radhi za Mungu basi kwakutumia matendo hayo hayo unaweza kuyatumia kama sababu ya Allah kukutimizia au kujibu maombi yako.

Tupate kisa Fulani toka Kwa vijana watatu katika jamii ya Israel, hawa vijana walikuwa wanaenda katika msafara wao Fulani lakini njiani wakakutana na mvua hivyo wakaamua kuingia katika pango moja Kwa AJILI ya kujistiri. Mara paap kuna Jiwe kubwa likaziba njia au mlango WA pango Lao.

Wakafanya mashauriano pale mwisho wakaja na wazo moja,kuwa kila mtu amuombe Mola wao Kwa Yale matendo mazuri ambayo waliyafanya Kwa kutaka radhi za Allah.

Basi WA Kwanza akasema "Ewe Mwenyezi Mungu Mimi nilikuwa na mfanyakazi wangu ananifanyia kazi na kumlipa lakini siku moja hakuchuku malipo yake na kuondoka zake,basi Mimi Ile hela nikanunua wanyama na kuwafuga na wakazaliana na kuwa wengi Sana, na siku ya siku akaja na kutaka ujira wake.

Nikamwambia ujira wako nimenunua mifugo na hii yote ni yako, basi Yule bwana akachukua mifugo yake yote na kuondoka, Ewe Mwenyezi Mungu kama kweli nilifanya Jambo lile Kwa kutaka radhi zako naomba utuondolee hili Jiwe ili tuweze kutoka" basi like Jiwe likasogea kidogo ingawa walikuwa hawawezi kutoka bado.

WA pili akasema " Ewe Mwenyezi Mungu Mimi nilikuwa na kawaida ya kuja na maziwa nyumbani na kabla sijawapa watoto wangu Kwanza huanza kuwapa wazazi wangu na baadae ndio familia yangu, lakini siku ya masiku nikachelewa kurudi na nikawakuta wamelala hivyo nikasimama na jagi mlangoni nikiwasubiri waamke ndio niwape na huku watoto wangu wanalia njaa.

Kama kweli nilifanya Jambo hili Kwa AJILI yako basi naomba utuondolee hili Jiwe tupate kutoka humu" basi Jiwe likasogea kidogo ingawa bado walikuwa hawawezi kutoka ingawa nje wanapaona.

Kijana wa tatu na wa mwisho akasema "Ewe Allah Mimi nilikuwa na Ami yangu/ mtoto wa Baba yangu mdogo,nilikuwa nampenda Sana na mara nyingi Sana nilikuwa namuitaita lakini alikuwa alikataa, siku ya siku alikuwa na shida sana akataka nimtatulie shida yake basi nami nikamwambia nitafanya hivyo kama nae atakubali ombi langu.

Nikiwa nae kitandani tayar Kwa kufanya Jambo langu akaniambia Ewe mja WA Allah usiivae Pete hii Bila ya haki yake na muogope Allah,akasema mara baada ya kuniambia vile nikaacha nilichotaka kufanya Kwa kukuogopa wewe kama kweli nilifanya Kwa AJILI yako naomba ututolee hili Jiwe tupate kutoka"

Basi Mashallah Jiwe likatoka na hao wakasalimika na mtihani ule,naam ndugu yangu msomaji hayo ni mambo ambayo yalitokea huko zamani na kutuonyesha ni jinsi gani tunaweza kutumia matendo yetu mema kama sababu ya kumtaka Mwenyezi Mungu atujibu maombi yetu, kwahiyo kumbuka Yale ambayo uliyafanya Kwa dhati kabisa ya kumridhisha Allah ndo yatakuwa sababu ya kukuokoa na mitihani yako.
 
Back
Top Bottom